Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

BENKI YA CRDB YAELEZEA UMUHIMU WA AKAUNTI YA TANZANITE KWA WANADIASPORA KATIKA MKUTANO WA SADC

$
0
0

Meneja Uhusiano wa benki ya CRDB , Godwin Semunyu na Nuru Kilasa Afisa Uhusiano Mwandamizi Benki ya CRDB wakitoa maelezo kwa baadhi ya wateja waliotembelea katika banda la benki hiyo kwenye Maonesho ya 4 Wiki ya Viwanda kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa benki ya CRDB , Godwin Semunyu , Lucy Kimei Meneja wa Benki ya CRDB Diaspora na Nuru Kilasa Afisa Uhusiano Mwandamizi Benki ya CRDB wakitoa maelezo kwa baadhi ya wateja waliotembelea katika banda la benki hiyo kwenye Maonesho ya 4  ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC, yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Maafisa ardhi 183 wasimamishwa kazi,Majina yao kupelekwa Takukuru kwa uchunguzi

ZINGATIENI SHERIA YA MAZINGIRA - SIMA

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akiangalia namna dhahabu inavyochenjuliwa kwa kutumia zebaki katika eneo la wachimbaji wadogo Mugusu Mkoani Geita. Serikali imeazimia kupunguza matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo kutokana na athari kwa binadamu na mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akikagua chanzo cha maji cha Mto Mabubi kilichopo katika Kata ya Mugusu Mkoani Geita. Naibu Waziri Sima amewaagiza wakazi wa eneo hilo kulinda chanzo hicho kwa kutofanya shughuli za kibinadamu kandokando, sambamba na kupunguza matumizi ya zebaki ili kulinda afya za wanachi.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akizungumza na wakazi wa Kata ya Mugusu Mkoa wa Geita ambao wanajishughulisha na shughuli za uchimbaji madini na kuchenjua dhahabu kwa kutumia zebaki. Naibu Waziri amewaeleza athari za matumizi ya zebaki na kuwataka kujiunga na vikundi rasmi ili waweze kunufaika na mikopo itolewayo na Serikali.
Afisa Madini Mkoa wa Geita Bw. Ernest Maganga (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima mara baada ya kutembelea mtambo maalumu wa kuchenjua dhahabu wa Jambo Africa – Geita. 


Na Lulu Mussa,GEITA 

Wachimbaji wadogo wa dhahabu katika Kata ya Mugusu Mkoani Geita wametakiwa kufuata taratibu za hifadhi ya mazingira ili kunusuru afya zao na kuchukua tahadhari ya kukabiliana na uwezekano wa milipuko ya magonjwa. 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima mara baada ya kufanya ziara ya kikazi kutembelea eneo la Mgusu, kuona uzingatiaji na utekelezaji wa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004. 

Akiwa katika eneo la Mugusu Naibu Waziri Sima amesema bado kuna tatizo la usafi wa mazingira katika maeneo wanayoyatumia kuchenjua dhahabu kwa kutumia zebaki, na kuna haja wachimbaji hao kukaa na halmashauri ya Geita Vijijini ili kuhakikisha wanakuwa na vyoo bora. 

Akitoa kauli ya Serikali kuhusu mpango kazi wa Taifa wa kupunguza matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu katika shughuli za uchenjuaji, Sima amewataka wakazi wa Mgusu kuendelea na shughuli za uzalishaji wa dhahabu bila kuathiri sekta ya mazingira kwa kupunguza matumizi ya zebaki inayoharibu mazingira na afya za binadamu. 

“Nimeona namna vijana wanavyojishughulisha kwa ajili ya kujipatia kipato, hili ni jambo jema kwenye Taifa letu, lakini nimetembea hadi chini kwenye ule mto wa Nyamasenge hakuna vyoo, watu wanatumia pori na mto kwa ajili ya haja ndogo na kubwa. 

“Kwa mazingira yetu ni hatari sana, tunaweza kufanya kazi nzuri lakini ugonjwa utasitisha shughuli zetu. Nawasisitiza kuwa Usafi ni jambo la kwanza katika kufanya kazi, huwezi kuwa na nguvu isiyojali usafi,” alisema Sima. 

Awali, Naibu Waziri Sima alitembelea chanzo cha maji cha maji cha Mto Mabubi na kujionea hali mbaya inayotishia kutoweka kwa chanzo hicho kutokana na shughuli za kibinadamu zinazoendelea kandokando ya eneo hilo. 

“Chanzo cha maji cha mto Mabubi, hakitadumu na maji hayatakuwa salama kwa matumizi ya binadamu endapo kitaendelea kuingia kemikali ya zebaki nanyi wachimbaji kujisaidia katika eneo hilo” Sima alisisitiza. 

Diwani wa Kata ya Mgusu Bw. Pastory Ruhusa amesema kuwa ataitisha mkutano wa wananchi mapema iwezekanavyo ili kuweka mikakati ya haraka kutokomeza hali hiyo ikiwa ni pamoja na usafi wa mazingira na kupunguza matumizi ya zebaki. 

Naibu Waziri Sima yuko katika ziara ya kikazi Kanda ya Ziwa kukagua uzingatiaji na usimamizi wa Sheria ya Mazingira pamoja na uwaelimisha wananchi mpango wa Serikali wa kupunguza matumizi ya zebaki nchini. 

WAKURUGENZI WAKUTANA KUBORESHA MWONGOZO WA UKOPAJI NA UPOKEAJI MISAADA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (katikati), akisikiliza kwa makini maelezo ya wajumbe wakati wa warsha ya kupitia na kuboresha mwongozo wa ukopaji, utoaji wa dhamana na upokeaji misaada iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu Msaafu, Bw. Peniel Lyimo na kulia ni Mwenyekiti wea warsha hiyo Bi. Mameltha Mutagwaba.
Mwenyekiti Msaidizi wa Kamati ya kuandaa Mwongozo wa ukopaji, utoaji wa dhamana na upokeaji misaada, Bi. Mameltha Mutagwaba, akifafanua jambo wakati wa warsha yakupitia na kuboresha mwongozo wa ukopaji, utoaji wa dhamana na upokeaji misaada iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Doto James (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya wakurugenzi wa sera kutoka wizara mbalimbali, wakati wa warsha ya kujadili mwongozo wa ukopaji, utoaji wa dhamana na upokeaji misaada, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, akizungumza jambo na Katibu Mkuu Msaafu, Bw. Peniel Lyimo, katika viwanja vya Benki Kuu, wakati wa warsha yakupitia na kuboresha mwongozo wa ukopaji, utoaji wa dhamana na upokeaji misaada, uliofanyika katika ukumbi BOT, Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki warsha ya kupitia na kuboresha mwongozo wa ukopaji, utoaji wa dhamana na upokeaji misaada wakisikiliza mjadala, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.(Picha na Scola Malinga, WFM, Dar es Salaam)

Na. Scola Malinga, WFM, Dar es Salaam

Serikali imejipanga upya kuongeza ufanisi wa kiutendaji kwa kupitia na kuboresha mwongozo wa ukopaji, utoaji wa dhamana na upokeaji misaada nchini.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Saalam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na mipango, Bw. Doto James,wakati wa ufunguzi wa warsha ya wakurugenzi wa Sera na Mipango wa wizara mbalimbali iliyoangazia kujadili na kuweka mkakati wa mwongozo huo.

Bw. James alisema kuwa, chimbuko la Mwongozo huo ni changamoto ambazo Serikali imekuwa ikikabiliana nazo wakati wa kutekeleza miradi ya maendeleo hususan miradi inayotekelezwa kwa fedha za mikopo na misaada kutoka kwa wadau wa maendeleo.

“Kama Wizara ya Fedha na Mipango, tumeshuhudia uwepo wa maandalizi duni ya miradi,na pia miradi kuchukua muda mrefu kuanza kutekelezwa na hivyo kuigharimu Serikali muda na fedha", alieleza Bw. James.

Aidha, Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Fedha, alieleza kuwa eneo lingine ambalo limekuwa na changamoto katika utekelezaji wa miradi ni misamaha ya kodi. Katika kulifanyia kazi jambo hilo, Wizara ya Fedha na Mipango imeandaa taarifa na mapendekezo kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto za masuala ya kodi ili miradi yote yenye changamoto za kodi itekelezwe ipasavyo kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi.

Bw. James, aliwasisitiza wakurugenzi hao kufanya majadiliano ya rasimu ya Mwongozo na kutoa mapendekezo ambayo yatatumika katika kukamilisha Mwongozo huo ili uje kusaidia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Aidha, Mwenyekiti wa Warsha hiyo ambaye ni Katibu Mkuu Msaafu, Bw. Peniel Lyimo, aliwasisitiza wajumbe wa kamati hiyo kuendelea kusaidia usimamizi wa miradi ya serikali kwenye maeneo yao.

Bw. Lyimo aliwapongeza wajumbe wa mkutano kwa michango yao itakayowezesha kufanikisha kukamilika kwa mwongozo huo, ambapo utakapokamilia utasaidia katika kutekeleza na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo na hivyo kuleta tija kwa wananchi.

Aidha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi Amina Shaaban, alieleza kuwa, nchi ya Tanzania imeshuhudia kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani katika miaka ya karibuni, hususan kuanzia mwaka 2016. Pamoja na kuongezeka kwa mapato, bado nakisi ya bajeti imekuwa ikiongezeka kutokana na Serikali kujikita katika kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, ukiwemo mradi wa Umeme wa Maporomoko ya mto Rufiji, Reli ya Kisasa kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), ujenzi na ukarabati wa madaraja na miundombinu mbalimbali.

Alisema ili kuziba pengo la nakisi, Serikali imekuwa ikiingia katika michakato mbalimbali ya madeni, dhamana na misaada kwa kutumia sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Suraya 134.

Bi. Amina Shaaban alibainisha kuwa, changamoto iliyojitokeza miaka ya hivi karibuni, ni kupungua kwa mikopo yenye masharti nafuu (concessional loans), hivyo Serikali imelazimika kuingia katika mikopo ya kibiashara (commercial loans).

Aidha, mikopo hiyo huambatana na masharti magumu na hivyo huhitaji umakini mkubwa (responsible borrowing) ili kuepuka kuingiza Taifa katika mikopo isiyolipika.Alisema kuwa pamoja na michango wajumbe wa warsha hiyo katika kupitia na kuboresha rasimu ya mwongozo huo, Serikali imejipanga kuutekeleza mara utakapokamilika.

MKUTANO WA KIKANDA WA KUPAMBANA NA MARADHI YA VIKOPE (TRACHOMA) WAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
Mkurugenzi mradi wa kupambana na maradhi ya vikope Duniani , Paul Emerson, akielezea juu ya juhudidi zinazochukuliwa kuhakikisha maradhi ya vikope yanaondoka duniani kote.
Msaidizi Meneja Kitengo cha Maradhi yasiyopewa kipaumbele Salum Abubakar (alieshika maiki) akijibu maswali ya wajumbe wa mkutano huo mara baada ya kuwasilisha mada ya uzoefu wa Zanzibar kama kisiwa katika kupambana na maradhi ya vikope.
NAIBU Waziri wa Afya Zanzibar Harusi Said Suleiman akifungua Mkutano wa siku mbili wa kupambana na maradhi ya vikope (Trachoma) Duniani kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, mkutano huo umefanyika Hoteli Sea Cliff Mangapwani Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa kumbambana na maradhi ya vikope Duniani wakisikiliza hutubaya ya Naibu Waziri wa Afya (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mkutano huo.
Mkurugenzi kinga na elimu ya afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed Abdalla(kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi mradi wa kupambana na maradhi ya vikope Duniani, Paul Emerson.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Harusi Said (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa kupambana na maradhi ya vikope (Trachoma) uliofanyika Hoteli ya Sea Cliff Mangapwani. 
Picha na Makame Mshenga.

Dkt Kalemani awekea mkazo agizo la wananchi vijijini kutolipia nguzo

$
0
0
Teresia Mhagama na Hafsa Omar, Geita

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ameendelea kusisitiza utekelezaji wa agizo alilolitoa la wananchi vijijini kutotozwa gharama ya nguzo pale wanahitaji kuunganishiwa umeme.

Dkt. Kalemani alisema hayo tarehe 7 Agosti, 2019, wakati akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Mwelani, Kata ya Mganza wilayani Chato mkoani Geita kabla ya kuwasha umeme rasmi katika Kijiji hicho.

“ Kuna baadhi ya wananchi wanalalamika kuwa wakienda kulipia huduma ya umeme ofisi za TANESCO au kwa Wakandarasi, wanaambiwa kuwa walipie nguzo, hili suala nimeshalikataza nchi nzima,” alisema Dkt Kalemani.

Vilevile Dkt. Kalemani aliagiza kuwa, wananchi wasikataliwe kutoa malipo pale wanapotaka huduma ya umeme kwa kisingizio cha kutokuwepo kwa vifaa kwani suala hilo limekuwa kama kigezo cha kuwacheleweshea huduma wananchi.

Akizungumza na wananchi katika Kijiji hicho aliwahakikishia kuwa, vitongoji vyote vinne vilivyopo kwenye Kata hiyo vitapata umeme.

Aidha, alitoa agizo kwa Meneja wa TANESCO Wilaya ya Chato kufungua ofisi ndogo ya TANESCO kwenye Kata ya Mganza ili shughuli zote za kuhudumia wananchi zifanyike kwenye Kata hiyo na hivyo kuwapunguzia umbali wa kufuata huduma.

Pia alitoa wito kwa wananchi, kulipia umeme kwa wingi kwani itasadia kuenea haraka kwa umeme nchini na hivyo kuchochea maendeleo ya wananchi.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uwashaji rasmi wa umeme katika Kijiji cha Mwelani, Kata ya Mganza wilayani Chato, Mkoa wa Geita. Wengine katika picha ni viongozi katika Kata hiyo.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia) akigawa vifaa vya UMETA kwa wananchi wa Kijiji cha Mwelani wilayani Chato ambacho kitawawezesha kuunganishwa na umeme bila kuingia gharama za wiring.
Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakiwa katika Mkutano wa Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani na wananchi wa Kijiji cha Mwelani wilayani Chato.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia) akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Mwelani wilayani Chato kabla ya kuwasha umeme kwenye Kijiji hicho.

MAHAKAMA KUU KANDA MPYA YA KIGOMA YAJIPANGA KUDHIBITI MLUNDIKANO WA MASHAURI

$
0
0
Naibu msajili wa Mahakama Kuu Kanda Kigoma, Mhe. Hussein Mushi (Aliyesimama) akimkaribisha Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Kigom, Mhe. Jaji Ilvin Mugeta(katikati) kwa ajili ya kufungua kikao cha kusukuma mashauri.
Wadau wa kikao cha kusukuma mashauri Wakipitia kwa umakini moja ya mashauri ya jinai yaliyowasilisha katika kikao hicho kilichoketi mapema tarehe Agosti 6, 2019.


Naibu msajili wa Mahakama Kuu Kanda Kigoma, Mhe. Hussein Mushi (Aliyesimama) akimkaribisha Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Kigom, Mhe. Jaji Ilvin Mugeta(katikati) kwa ajili ya kufungua kikao cha kusukuma mashauri.
Mandhari ya Jengo jipya la Mahakama Kuu, Kanda ya Kigoma lililopo katika hatua za mwisho ya ukamilishwaji ‘finishing’
Picha ya pamoja ya wajumbe wa kikao cha kusukuma mashauri mara tu walipotembelea Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma kujua matumizi ya vyumba na mifumo mbalimbali iliyopo katika Jengo.


Na Festo Sanga, Mahakama ya Hakimu Mkazi- Kigoma 

Mahakama kuu Kanda ya Kigoma imeendesha kikao chake cha kwanza cha mashauriano na wadau (caseflow management) tangu kuanzishwa kwake rasmi na Mheshimiwa Jaji Mkuu wa Tanzania kwa tangazo la Serikali namba 112 la Februari 1, 2019. 

Akifungua kikao hicho mapema Agosti 6, 2019 kilichofanyika katika Jengo la Hakimu Mkazi Kigoma, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, Mhe. Jaji Ilvin Mugeta aliwasilisha maeneo makuu matatu katika kuhakikisha Kanda ya Kigoma inakuwa ya mfano kwa kumaliza mashauri kwa wakati ili kuondokana na mrundikano na kupunguza Idadi ya Mahabusu katika Magereza. 

“Baadhi ya maeneo yenye changamoto ni pamoja na baadhi ya Wadau wetu kutotimiza wajibu ipasavyo, mawasiliano yasiyoridhisha baina ya mtu na mtu, Taasisi kwa Taasisi pamoja na uwezo mdogo wa wadau wetu katika upelelezi imekuwa ni changamoto inayokwamisha adhima yetu ya upatikanaji wa haki kwa wakati” alieleza Mhe. Jaji Mugeta 

Mhe Jaji huyo Mfawidhi alitoa maelekezo juu ya kuwa na mwelekeo sahihi wa kanda na namna bora itakayoleta matokeo chanya kwa kuwaeleza wajumbe kuhahakikisha wanaweka mfumo wa uwajibikaji wa pamoja na kuweka maazimio ya pamoja ikiwa sambamba na kuweka viwango vya kupimika katika utendaji kazi wa kila siku. 

Aidha aliwasisitiza wajumbe kufungua milango ya mawasiliano ili kuhakikisha wanafikiana kwa wakati na kupeana taarifa stahiki ikiwa ni pamoja na kila mjumbe kutambua wajibu wake na kuongeza kuwa upelelezi unapochukua muda mrefu hupelekea kupotea kwa haki za watu. 

Akisoma taarifa ya Kanda hiyo, naye Naibu Msajili wa Kanda hiyo, Mhe. Hussein Mushi aliwaeleza wajumbe kuwa tangu kuanzishwa kwake mapema mwezi February, 2019 hadi mwezi Julai, 2019 masjala ya Mahakama kuu kanda ya Kigoma imesajili jumla ya mashauri 59 ya jinai pekee, mashauri 12 yaliamuliwa na mashauri 47 yamebaki. 

Kamati ya kusukuma mashauri kanda ya Kigoma kwa pamoja walikubaliana kushirikiana katika kuhakikisha wanaondokana na mlundikano wa mashauri na Mahabusu kwa kila mjumbe kutimiza wajibu wake kikamilifu. 

Aidha baada ya kikao wajumbe walipata fursa ya kutembelea Jengo la Mahakama Kuu lililopo katika eneo la Bangwe mkabala na shule ya Sekondari Kigoma ambako liko katika hatua za mwisho za ujenzi wake. 

Wajumbe waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Jaji Mfawidhi wa Kanda, Naibu Msajili, Mtendaji wa Mahakama-Kigoma, Hakimu Mkazi Mfawidhi(M), Mkuu wa Mashtaka Kigoma (M), Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma, Wawakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Polisi, Mkuu wa Upelelezi, Mkuu wa Gereza la Bangwe. na Katibu wa Jukwaa la Mawakili wa kujitegemea Kigoma (M). 



MAELEZO KATIKA PICHA

PROFESA MANYA AONGOZA MDAHALO KUHUSU USHIRIKISHWAJI WA WAZAWA KWENYE UTOAJI WA HUDUMA (LOCAL CONTENT) KATIKA MKUTANO WA SADC

$
0
0
 Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya akifafanua jambo kwenye mdahalo kuhusu ushirikishwaji wa wazawa katika utoaji wa huduma kwenye sekta mbalimbali nchini (local content) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika (SADC) yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 08 Agosti, 2019.

 Sehemu ya wajumbe wa mdahalo huo wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya (hayupo pichani).

 Kutoka kushoto Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya, Mkurugenzi wa Tafiti za Kimkakati kutoka Taasisi ya REPOA, Dk. Jamal Msami na Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe –Tawi la Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’l Issa. (hayupo pichani)

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’l Issa akifafanua jambo katika kikao hicho.



Leo tarehe 08 Agosti, 2019 Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya ameongoza mdahalo kuhusu ushirikishwaji wa wazawa katika utoaji wa huduma kwenye sekta mbalimbali nchini (local content) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika (SADC) yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


Mdahalo huo ulishirikisha pia Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’l Issa, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe –Tawi la Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi na Mkurugenzi wa Tafiti za Kimkakati kutoka Taasisi ya REPOA, Dk. Jamal Msami


Waliohudhuria katika mdahalo huo walikuwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Madini, Augustine Ollal, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira wa Tume ya Madini, Dk. Abdulrahman Mwanga, watendaji kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini pamoja na wadau kutoka taasisi za fedha na  wajasiriamali.


Awali akielezea manufaa ya ushirikishwaji wa wazawa katika utoaji wa huduma kwenye shughuli za madini na sekta nyingine, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’l Issa alisema kuwa ni pamoja na kuinua uchumi kuanzia katika ngazi ya chini na Taifa kwa ujumla.


Akielezea mafanikio ya utekelezaji wa mpango wa ushirikishwaji wa wazawa katika utoaji wa huduma kwenye shughuli zinazofanywa na wawekezaji nchini, Beng’l alisema wawekezaji kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo wameanza kutumia huduma zinazotolewa na watanzania hivyo kuongeza kipato.Alitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ule wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, miundombinu, sekta ya madini na gesi.

Mapendekezo yaliyowasilishwa na wachangiaji mbalimbali kupitia mdahalo huo yalikuwa ni pamoja na utoaji wa elimu kwa watoaji huduma wa ndani kuhusu namna bora ya kutoa huduma na bidhaa bora, wazalishaji na watoa huduma wa ndani kuingia ubia na kampuni nyingine kubwa kutoka nje ya nchi lengo likiwa ni kuongeza ufanisi na kupata uzoefu zaidi.

Akihitimisha mdahalo huo, Profesa Manya aliwataka wadau kutumia changamoto mbalimbali kwenye sekta mbalimbali kama fursa hususan kwenye utoaji wa huduma na kujipatia kipato.



SERIKALI YAWATAKA WANUNUZI WA PAMBA WAONGEZE KASI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua pamba wakati alipotembelea Chama cha Ushirika cha msingi cha Itemelo, eneo la Dutwa mkoani Simiyu, Agosti 8, 2019. Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally, Wa nne kulia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na wa tano kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Japhet Hasunga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisaidiana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (kulia) na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wa nne kulia) kupandisha pamba kwenye mzani wa kielektroniki wakati alipokaguaununuzi wa pamba kwenye Chama cha Ushirika cha Msingi cha Itemelo, eneo la Dutwa mkoani Simiyu, Agosti 8, 2019. Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia kazi ya kupima pamba kwa njia ya kielektroniki wakati alipokagua ununuzi wa pamba katika Chama cha Ushirika cha Msingi cha Itemelo kilichopo eneo la Dutwa mkoani Simiyu, Agosti 8, 2019 Kulia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na wa tatu Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipotembelea maonyesho ya Nanenane yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu, Agosti 8, 2019. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellak na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanunuzi wa zao la pamba katika maeneo mbalimbali nchini wahakikishe wanaongeza kasi ya ununuzi wa zao hilo ili wakulima waweze kupata fedha zao kwa wakati.

Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga pamoja na Manaibu Waziri wake kubaki katika mikoa yote inayolima zao la pamba hadi wakulima wote watakapolipwa fedha zao na kuhakikisha pamba yote iliyomo mikononi mwa wakulima inauzwa.

Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Agosti 8, 2019) wakati alipotembelea Chama cha Msingi cha Itemelo kilichoko eneo la Dutwa wilayani Bariadi, Simiyu kwa ajili ya kujionea mauzo ya zao la pamba.

Waziri Mkuu amesema ataendelea kusimamia mwenendo wa zao hilo kwa ukaribu lengo likiwa kuona wakulima wananufaika kwa kupata tija. “Ilani ya CCM ya 2015/2020 inasisitiza kilimo na inataka wakulima wapate masoko ya uhakika na tunalitekeleza jambo hilo na pamba yote itanunuliwa.”

Amesema Serikali inataka kuona pamba yote iliyoko kwa wakulima inatoka ili wakulima waweze kulipwa fedha ambazo zitawawezesha kujikimu kimaisha pamoja na kununua pembejeo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka viongozi wa AMCOS wahakikishe wanawatambua wakulima kwa majina, maeneo wanayoishi pamoja na ukubwa wa mashamba yao ili waweze kuagiza pembejeo kulingana na mahitaji halisi.Hata hivyo, Waziri Mkuu amewasihi wakulima kufungua akaunti katika taasisi mbalimbali za kifedha lengo likiwa ni kuhifadhi vizuri fedha wanazozipata kutokana na mauzo ya pamba ili ziweze kuwasaidia baadaye.

Pia, Waziri Mkuu amewasisitiza wakulima hao waendelee kutunza vizuri pamba yao na kuipeleka ghalani ikiwa katika hali nzuri ya usafi na ubora wa hali ya juu, kwani kwa sasa pamba ya Tanzania inasifika kwa ubora katika soko la dunia. 

Kwa upande wa masoko hususan ya pamba, Waziri Mkuu aliwasisitizia wananchi wa Dutwa na Watanzania kwa ujumla kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. Magufuli inaendelea kuhakikisha uwepo wa masoko ya uhakika wa mazao yote hususan yale ya kimkakati. 

Pia, Waziri Mkuu ameongeza kuwa moja ya agenda muhimu ya ziara yake ya Kiserikali aliyoifanya nchini Misri mwezi Julai 2019 ilikuwa ni kutafuta masoko ya uhakika ya mazao ya Tanzania likiwemo na zao la pamba.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally alipokaribishwa kuwasalimu wananchi alimshukuru Waziri Mkuu kwa kutoa msukumo katika ununuzi zao la pamba. Aidha alimuomba Waziri Mkuu aongeze msukumo zaidi ili wakulima walipwe fedha zao kwa wakati.

Naye,Waziri wa Kilimo Hasunga amesema kuwa hali ya malipo kwa wakulima wa zao la pamba kwa sasa ni ya kuridhisha kwa kuwa wakulima katika maeneo mbalimbali wameanza kulipwa.Pia Waziri huyo amemuahidi Waziri Mkuu kwamba wataendelea kubakia katika mikoa inayolima pamba kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa mauzo ya pamba ili kuhakikisha wakulima wote wanalipwa fedha zao kwa wakati. 

Kuhusu suala la makato ya fedha za pembejeo ambazo wakulima wanalalamikia kukatwa kiasi kikubwa kuliko kiwango halisi wanachostahili, Waziri huyo wa Kilimo amesema atalishughulikia.

Aidha,Mbunge wa jimbo la Bariadi, Andrew Chenge amesema amefanya ziara katika kata 20 kati ya 30 kwenye jimbo hilo na changamoto kubwa ya wananchi ni mauzo ya pamba. “Ujio wa Waziri Mkuu umeleta manufaa kwani wanunuzi wameanza kuja kwa kasi”.

Mbunge huyo amemuomba Waziri Kuu awafikishie salamu zao kwa Rais Dkt. John Magufuli kwamba wanamshukuru kwa namna anavyowajali wakulima mbalimbali nchini wakiwemo na wa zao la pamba. 

Kwa upande wake, Mbunge wa jimbo la Itilima, Njalu Silanga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Nsangali ambayo inanunua pamba amemuahidi Waziri Mkuu kwamba ifikapo kesho (Ijumaa, Agosti 9, 2019) saa nane mchana atakuwa amelipa sh. milioni 135 zinazohitajika na amcos ya Itemelo ili kulipia deni la pamba iliyoko ghalani.



Awali, Katibu wa Amcos ya Itemelo, Lucas Ephraim alimuomba Waziri Mkuu awasaidie kuyahimiza makampuni mbalimbali yanayonunua yapeleke fedha kwa wakati ili kukidhi makisio tarajiwa.



Katibu huyo alisema chama chao kinahudumia vijiji vitano vikiwa na jumla ya wakulima 2,665 wa pamba wenye jumla ya ekari 9,675. Pia chama chao kinahitaji sh. milioni 135.139 ili kulipia deni la pamba ambayo iko ghalani.

TPDC YAZIHAKIKISHIA NCHI ZA SADC TANZANIA KUNA GESI YA KUTOSHA, WAJIVUNIA UZOEFU WA MIAKA 50

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

SHIRIKA la Maendeleo la Petroli Tanzania(TPDC) limezihakikisha nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC) kuwa wana gesi ya kutosha na wanajivunia kuwa na uzoefu wa miaka 50 katika ujenzi wa miundombinu ya gesi na mafuta.

Pia limesema kwa sasa mahitaji ya gesi yanaongezeka na tayari wameanza kufanya mazungumzo na nchi tano za Kenya, Zambia, Uganda , Malawi na DRC ili wapelekewe gesi kwenye nchi zao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TPDC James Mataragio wakati anazungumza na waandishi waliokuwa kwenye mjadala ambao mada yake ilijikita kuzungumzia mafuta na ujenzi wa miundombinu katika kuondoa umasikini.

Hivyo wametumia nafasi hiyo kueleza kuwa mahitaji ya gesi kwa nchi mbalimbali za SADC ni makubwa na ndio maana kuna nchi wanaendelea kuzungumza nazo ili kuhakikisha nishati ya gesi inawafikia.

“Kuhusu nafasi ya soko ya gesi, mahitaji ni makubwa na yanaongezeka kila siku .Nchi za Kenya, Zambia, Uganda , Malawi na DRC wameomba kusambaziwa gesi.

“Hivyo kuna uwezekano wa kujenga bomba la gesi kutoka Dar es Salaam kwenda Mombasa, kujenga bomba la gesi kutoka Tanga kwenda Uganda na tayari kuna uwezekano wa kutumia mkuza wa kupitisha mafuta mazito kwenda Ndola Zambia ambalo litatumika kupitisha gesi,”amesema Mataragio.

Alipoulizwa kuhusu nafasi ya TPDC ,Mataragio amejibu wao wamekuwa na uzoefu mkuwa katika eneo la mafuta na gesi na wamekuwa wakifanya tafiti nyingi katika eneo hilo ikiwemo kugundua mafuta na gesi.

“Tanzania tunao uzoefu kwa miaka 50 katika ujenzi wa miundombinu na hasa kwenye gesi na mafuta. Kuna mabonda kama nne ambayo tumewahi kujenga.Tumejenga bomba kutoka Tanzania kwenda Zambia ambalo linasafarisha mafuta mazito.

“Tumejenga bomba kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam kwa ajili kusafirisha gesi, bomba la Msimbati hadi Mtwara na bomba la kutoka Songo songo kwenda Dar es Salaam,”amesema.

Hivyo amesema wao wametumia majadiliano hayo kuelezea uzoefu wao katika kujenga miundombinu hiyo pamoja na kuisimamia na kwa sasa kuna ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda kuja Tanzania.

Pia amesema ujumbe ambao washiriki wa majadiliano hayo wameupata kutoka kwao ni kwamba wataondoka na ujumbe Tanzania imejiimarisha kwenye miundombinu ya gesi na mafuta pamoja na uwekezaji wa uhakika katika sekta hiyo.

Kuhusu hali ya mafuta nchini amesema ni nzuri na kuna tafiti zinaendelea kwenye maeneo mbalimbali nchini ambako kunaonekana kuna dalili za uwepo wa mafuta.Kuhusu mahitaji ya gesi nchini amesema ni kama futi za ujazo milioni 200 na sehemu kubwa ya gesi inatumika kuzalisha umeme na mchukuaji mkubwa ni TANESCO kwa zaidi ya asilimia 50.

“Pia matumizi ya gesi yanaongezeka kila siku na ndio maana kwa sasa tunaendelea kufanya utafiti wa gesi na mafuta endelevu ili kuhakikisha tunakuwa na nishati hiyo kwa miaka mingi ijayo na kazi hiyo tunaifanya sisi wenyewe,”amesema.

Pia amesema wanaendelea kujenga miundombinu ili kusambaza gesi majumbani na viwandani huku akisisitiza TPDC wamejipanga kuhakikisha na gesi inakuwa endelevu.
Baadhi ya washiriki wa majadiliano yaliyojikita kuzungumzia umuhimu wa mafuta na ujenzi wa miundombinu katika kuondoa umasikini kwa nchi za Jumuiya za maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC) ambapo Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania(TPDC),wametumia nafasi hiyo kutoa uzoefu wao
Washiriki wakiendelea kufuatilia mjadala kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC James Mataragio wakati anatoa uzoefuwashirika hilo katika eneo la mafuta ,gesi na ujenzi wa miundombinu
Mmoja wa washiriki akifutulia mjadala kuhusu gesi na mafuta katika kuondoa umasikini kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)

HOSPITALI YENYE HADHI YA KUWA HOSPITALI YA RUFAA YAFUNGULIWA KIJIJI CHA MARUA -KILIMANJARO

$
0
0
Hospitali mpya ya St Monica iliyojengwa na Taasisi ya Kirua Children Care Foundation katika kijiji cha Marua ,kata ya Kirua Vunjo Magharibi katika wilaya ya Moshi. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kirua Children Care Foundation ,Padri Amedeus Macha wakielekea katika ufunguzi rasmi wa Hosptali hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akitia saini katika kitabu cha wageni alipofika katika Hosptali hiyo kwa ajili ya ufunguzi. 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kirua Children Care Foundation ,Padri Amedeus Macha akimueleza jambo mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira wakati akitembelea vyumba vya kulaza wagonjwa katika Hosptali hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akitizama baadhi ya mashine zilizoko katika Hospitali hiyo. 
Chumba cha kulaza wagonjwa. 
Padri Amedeus Macha akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira chumba maalumu kwa ajili ya wanawake kujifungulia. 
Baadhi ya Vifa vilivyopo maabara ya Hospotli hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa Hospitali hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akitoa kitambaa kufungua jengo hilo la Hosptali ya St Monica. 
Padri Amedeus Macha akifanya Ibada mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa Hospitali hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akizungumza wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya St Monica iliyopo jimbo la Vunjo wilaya ya Moshi.

Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Mkuu huyo wa mkoa. 

Mbunge wa Jimbo la Vunjo,James Mbatia akizungumza katika hafla ya ufunguzi rasmi wa Hospitali ya St Monica. 

Baadhi ya wananchi waliofika katika ufunguzi wa Hospitali hiyo.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Kirua Children Care Foundation ,Padri ,Amedeus Macha akizungumza katika ufunguzi wa Hosptli hiyo. 

Mkuu wa mkoa wa Kiliamanjaro Dkt Anna Mghwira akiwa katika picha ya pamoja na wageni waliofika kwa ajili ya kushuhudia ufunguzi rasmi wa Hospitali ya St Monica iliyopo kijiji cha Marua ,wilaya ya Moshi .



Na Dixon Busagaga wa Michuzi TV .


MBUNGE WA Jimbo la Vunjo ,James Mbatia ameshauri kuanzishwa kwa Utalii wa Tiba (Medical Tourism) katika eneo linalozunguka Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) ili kurahisha utoaji wa huduma kwa wageni wanaopata matatizo wakati wa kupanda mlima Kilimanjaro.

Mbatia aliyasema hayo jana wakati wa ufunguzi rasmi wa Hospitali ya St Monica iliyopo jirani na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro katika kijiji cha Marua ,kata ya Kirua Vunjo Magharibi,katika wilaya ya Moshi huku akiiomba serikali kusaidia katika uboreshaji wa Miundombinu ya barabara.

Akizungumza mara baada ya kufungua na kutembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali Hospitali iliyojengwa na Taasisi ya Kirua Children Care Foundation Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira ameipongeza taasisi hiyo kwa kujenga Hosptali hiyo ambayo itasaidia kupunguza changamoto za kiafya kwa wakazi wa maeneo hayo na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Kirua Children Care Foundation Padri Amedeus Macha amesema Hospitali hiyo itakayo kuwa na uwezo wa vitanda zaidi ya 100 imelenga kutoa huduma za matibabu kwa wazee na watoto ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za Afya.

Dkt.Bogias Mwamgunda ni mwakilishi wa mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro hapa akaeleza namna ambavyo Hosptali hiyo itasaidia Wazee na watoto katika kupambana na magonjwa yatokanayo na Baridi .

Taasisi za Dini katika jimbo la Vunjo zimekuwa mstari wa mbele katika uwekezaji wa masuala ya huduma za afya ,hali inayochangia urahishaji wa upatikanaji wa matibabu tofauti na ilivyokuwa kwa kutembea umbali mrefu hasa nyakati za mvua na usiku .

MAKAMU WA RAIS AFUNGA MAONESHO YA NANENANE MOROGORO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Bidhaa za aina mbalimbali wakati alipotembelea  mabanda ya Maonesho katika kilele cha Maadhimisho ya  Ufungaji wa Sikukuu ya Wakulima Nanenane Mkoani Morogoro leo Agost 08,2019.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa Shamba la Miwa Kilombero Mohamed Salum  wakati alipotembelea  mabanda ya Maonesho katika kilele cha Maadhimisho ya  Ufungaji wa Sikukuu ya Wakulima Nanenane Mkoani Morogoro leo Agost 08,2019.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Kombe Mshindi wa Ushiriki Bora katika Maadhimishi ya sikukuu ya wakulima Nanenane kwa Mwaka 2019 Kanali Aisha Matanzi wa JKT  wakati  wa Maadhimisho ya  Ufungaji wa Sikukuu ya Wakulima Nanenane Mkoani Morogoro leo Agost 08,2019.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WAZIRI MKUU ATOA MAAGIZO MAZITO KWA WIZARA TANO

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameziagiza Wizara za Kilimo, Viwanda na Biashara, Uvuvi na Mifugo kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji kutengeneza mkakati wa kuanzisha viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi nchini.

Amevitaja viwanda kuwa ni pamoja na vya nyuzi, nguo, ngozi, maziwa, minofu, nyama, kubangua korosho, kutengeneza unga, mafuta ya kula, sabuni, usindikaji wa matunda na mbogamboga, “Kwani ndiyo msingi wa kauli mbiu yetu ya kufikia uchumi wa viwanda 2025”. 

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Agosti 8, 2019) katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima nane nane Kitaifa kwenye viwanja vya maonesho Nyakabindi mkoani Simiyu kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.

Waziri Mkuu amsema sambamba na mkakati huo, pia ameagiza kuimarishwa kwa vyama vya ushirika ili kumwezesha mkulima kuendelea kumiliki zao lake mpaka hatua ya kuuza sokoni. “Vyama vya ushirika vikiweza kuchakata mazao na kuyaongeza thamani vitamuwezesha mkulima kuwa na umiliki na kufaidika na bei ya soko”. 

Amesema mfano uliooneshwa katika zao la Kahawa kupitia Chama Kikuu cha Ushirika Kagera (KCU) ni mzuri ambapo wanamiliki asilimia 100 ya Kiwanda cha Kukoboa Kahawa (BUCOP), pamoja na asilimia 54 ya Kiwanda cha Kuzalisha Kahawa – Tanganyika Instant Coffee (TANICA). 

“Kwa upande wa Pamba, Nyanza Cooperative Union (NCU) walianza vizuri kwa kumiliki viwanda vinane vya kuchambulia pamba. Tunataka jitihada za namna hii zianzishwe katika shughuli za wakulima wetu na zilizopo ziimarishwe”. 

Hivyo, ameitaka Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa kushirikiana na wadau, ifanye tathmini kwenye vyama vya ushirika vinavyomiliki viwanda ili kubaini hali ilivyo kwa sasa na kuweka mikakati ya kuvifufua na kuviongezea uwezo.

Amesema safari ya kujenga uchumi wa viwanda itaiwezesha Tanzania kuwa nchi yenye kipato cha kati imeanza na inaendelea vizuri na  matarajio yake ni kuona wananchi wote bila kujali tofauti za kiitikadi, wataendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa kuwa maendeleo wanayoyapigania ni kwa manufaa ya wote waliopo leo na vizazi vijavyo.

Waziri Mkuu amesema kwa mantiki hiyo, kila Mtanzania hanabudi kuongeza bidii katika kufanya kazi, kupiga vita rushwa, kulipa kodi ya Serikali na kulinda rasilimali za Taifa ili ziweze kutumika sasa na kwa faida ya vizazi vyetu vijavyo. 

“Niwaombe muendelee kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano kwa namna ambavyo imeamua kwa makusudi kuanzisha miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi inayoendelea kujengwa nchini ikiwemo reli ya kisasa ya mwendokasi, mradi mkubwa wa umeme wa Mto Rufiji, upanuzi wa viwanja vya ndege, bandari na ununuzi wa ndege kubwa”. 

Amesema kuboreshwa kwa miundombinu hiyo, pamoja na mambo mengine kutachochea uwekezaji mkubwa katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi, kurahisisha usafirishaji wa mazao, mifugo, samaki, na kupunguza gharama za uzalishaji na hivyo kuwezesha viwanda vya ndani kushindana kibiashara na bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya nje ya nchi. 

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoawito kwa viongozi wa Mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga kuendelea kushirikiana na Wizara za Sekta ya Kilimo kuhakikisha viwanja hivyo vya Nyakabindi, vinakuwa kituo cha mafunzo ya wakulima, wafugaji na wavuvi.  

“Kumbukeni kuwa kila mmoja wetu akitimiza wajibu wake ipasavyo, maendeleo ya viwanda yanawezekana, ajira zitapatikana, uhakika wa chakula na lishe bora itakuwepo na sote kwa pamoja tutasonga mbele kufikia nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025”. 

Kauli mbiu ya maadhimisho ya Nane Nane ya mwaka huu inasema: - “Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Nchi”.Kaulimbiu hiyo inakwenda sambamba na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kukuza uchumi wa viwanda na biashara, ikilenga kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa na wakati huo huo kupunguza umaskini.

 Awali, Waziri Mkuu alitembelea na kukagua mabanda mbalimbali katika maoneosho hayo. Miongoni mwa mabanda aliyoyatembelea ni pamoja na banda la EPZA, NMB, CRDB, NBC, BOT kitengo cha mifumo ya malipo ya Kielektroniki ya Serikali, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na JKT. 

 Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally, Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, Naibu Waziri Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Josephat Kandege, Naibu Waziri wa Madini, Stansalaus Nyongo pamoja na maafisa wengine wa Serikali.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua pamba wakati alipotembelea Chama cha Ushirika cha msingi cha Itemelo, eneo la Dutwa mkoani Simiyu, Agosti 8, 2019. Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally, Wa nne kulia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na wa tano kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Japhet Hasunga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisaidiana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (kulia) na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka  wa nne kulia) kupandisha pamba kwenye mzani wa kielektroniki wakati alipokaguaununuzi wa pamba kwenye Chama cha Ushirika cha Msingi cha Itemelo, eneo la Dutwa mkoani Simiyu, Agosti 8, 2019. Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia kazi ya kupima pamba kwa njia ya kielektroniki wakati alipokagua ununuzi wa pamba  katika Chama cha Ushirika  cha Msingi cha Itemelo  kilichopo eneo la Dutwa mkoani Simiyu, Agosti 8, 2019   Kulia ni  Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na wa tatu Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipotembelea maonyesho ya Nanenane  yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi  mkoani Simiyu, Agosti 8, 2019. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellak na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Ummy azikaribisha nchi za SADC kutibiwa Muhimbili, MOI na JKCI

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu  amezikaribisha nchi wanachama wa SADC kutumia huduma za ubingwa wa juu zinazopatika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Ummy ameyasema hayo leo alipotembelea  mabanda ya MNH, MOI na JKCI yanayoshiriki maonesho ya viwanda yanayofanyika katika viwanja vya ukumbi  wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) kuelekea mkutano mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi zilizopo Kusini mwa Afrika (SADC) ambao utaanza mapema wiki hii.

Waziri Ummy amesema Wizara yake imeweka wataalam wa afya ili kutoa huduma kwa wajumbe wa mkutano wa SADC watakaohitaji huduma za matibabu pamoja na wananchi wengine watakaokuwapo katika viwanja hivyo.

Aidha ameziomba nchi za SADC kupata huduma za ubingwa wa juu zinazopatikana MNH kama upandikizaji figo (kidney transplant), upandikizaji watoto vifaa vya kusaidia kusikia (cochlear implant), tiba kwa njia ya radiolojia (interventional radiology).

Kwa upande wa MOI, Waziri Ummy amezitaka nchi za SADC kuja kupata huduma za upasuaji wa mivunjiko ya kikombe cha mfupa wa nyonga, upasuaji wa kuweka nyonga na magoti bandia na upasuaji wa magoti, ubongo na mgongo kupitia matundu madogo.

Kwa upande wa JKCI amezitaka nchi za SADC kupata huduma za tiba ya umeme wa moyo, kuzibua mishipa ya damu na upasuaji wa kufungua kifua kwa ajili ya kurekebisha valvu au matundu kwenye moyo.

 “Kama Wizara tumeweka wataalam wa afya hapa eneo la mkutano  ili kutoa huduma kwa wajumbe wa nchi za SADC. Wataalam wetu wa Muhimbili, MOI, JKCI na pamoja  Hospitali ya Lugalo wako tayari kuhudumia wageni wetu ambao watapata changamoto yoyote ya kiafya,” amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy ametembelea kliniki maalumu zilizoandaliwa kwa ajili ya kuhudumia wageni na wananchi mbalimbali wanaotembelea maonesho ya viwanda na maandalizi ya mkutano wa 39 wa SADC.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari katika banda la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alipotembelea leo. Kushoto ni Dkt. Juma Mfinanga akiwa na Waziri Ummy Mwalimu baada ya kumweleza jinsi MNH ilivyojiandaa kuwahudumia wajumbe wa mkutano wa SADC pamoja na wananchi wengine.
 Daktari Bingwa wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dkt. William Mugisha (kulia) akimweleza Waziri Ummy Mwalimu kuhusu huduma ya upasuaji wa mivunjiko ya kikombe cha mfupa wa nyonga alipotembelea banda la MOI leo.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mkuu wa Idara ya Utafiti na Mafunzo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Pedro Pallangyo akimweleza Waziri Ummy Mwalimu huduma zinazopatika JKCI zikiwamo huduma za tiba ya umeme wa moyo na  kuzibua mishipa ya damu.
 Daktari wa Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, Dkt. Andrew Laiser akieleza jinsi walivyojiandaa kuhudumia wajumbe wa mkutano wa SADC na wananchi wengine.
 Waziri Ummy Mwalimu akisoma jarida la Muhimbili linaloeleza huduma mbalimbali za afya zinazopatikana MNH. Kulia ni Dkt. Juma Mfinanga akimweleza jambo Waziri.
  Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, wataalam wa afya pamoja na wataalam wengine wakiwa katika viwanja vya ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) kukagua mabanda na kliniki zitakazotumika kuhudumia wajumbe wa mkutano wa SADC.
Wataalam wa afya wa Muhimbili, MOI, JKCI na Hospitali ya Lugalo wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Ummy Mwalimu leo katika viwanja vya ukumbi  wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC).

SERIKALI YAWATAKA WANUNUZI WA PAMBA WAONGEZE KASI

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanunuzi wa zao la pamba katika maeneo mbalimbali nchini wahakikishe wanaongeza kasi ya ununuzi wa zao hilo ili wakulima waweze kupata fedha zao kwa wakati.

Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga pamoja na Manaibu Waziri wake kubaki katika mikoa yote inayolima zao la pamba hadi wakulima wote watakapolipwa fedha zao na kuhakikisha pamba yote iliyomo mikononi mwa wakulima inauzwa.

Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Agosti 8, 2019) wakati alipotembelea Chama cha Msingi cha Itemelo kilichoko eneo la Dutwa wilayani Bariadi, Simiyu kwa ajili ya kujionea mauzo ya zao la pamba.

Waziri Mkuu amesema ataendelea kusimamia mwenendo wa zao hilo kwa ukaribu lengo likiwa kuona wakulima wananufaika kwa kupata tija. “Ilani ya CCM ya 2015/2020 inasisitiza kilimo na inataka wakulima wapate masoko ya uhakika na tunalitekeleza jambo hilo na pamba yote itanunuliwa.”

Amesema Serikali inataka kuona pamba yote iliyoko kwa wakulima inatoka ili wakulima waweze kulipwa fedha ambazo zitawawezesha kujikimu kimaisha pamoja na kununua pembejeo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka viongozi wa AMCOS wahakikishe wanawatambua wakulima kwa majina, maeneo wanayoishi pamoja na ukubwa wa mashamba yao ili waweze kuagiza pembejeo kulingana na mahitaji halisi.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewasihi wakulima kufungua akaunti katika taasisi mbalimbali za kifedha lengo likiwa ni kuhifadhi vizuri fedha wanazozipata kutokana na mauzo ya pamba ili ziweze kuwasaidia baadaye.

Pia, Waziri Mkuu amewasisitiza wakulima hao waendelee kutunza vizuri pamba yao na kuipeleka ghalani ikiwa katika hali nzuri ya usafi na ubora wa hali ya juu, kwani kwa sasa pamba ya Tanzania inasifika kwa ubora katika soko la dunia.

Kwa upande wa masoko hususan ya pamba, Waziri Mkuu aliwasisitizia wananchi wa Dutwa na Watanzania kwa ujumla kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. Magufuli inaendelea kuhakikisha uwepo wa masoko ya uhakika wa mazao yote hususan yale ya kimkakati.

Pia, Waziri Mkuu ameongeza kuwa moja ya agenda muhimu ya ziara yake ya Kiserikali aliyoifanya nchini Misri mwezi Julai 2019 ilikuwa ni kutafuta masoko ya uhakika ya mazao ya Tanzania likiwemo na zao la pamba.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally alipokaribishwa kuwasalimu wananchi alimshukuru Waziri Mkuu kwa kutoa msukumo katika ununuzi zao la pamba. Aidha alimuomba Waziri Mkuu aongeze msukumo zaidi ili wakulima walipwe fedha zao kwa wakati.

Naye,Waziri wa Kilimo Hasunga amesema kuwa hali ya malipo kwa wakulima wa zao la pamba kwa sasa ni ya kuridhisha kwa kuwa wakulima katika maeneo mbalimbali wameanza kulipwa.

Pia Waziri huyo amemuahidi Waziri Mkuu kwamba wataendelea kubakia katika mikoa inayolima pamba kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa mauzo ya pamba ili kuhakikisha wakulima wote wanalipwa fedha zao kwa wakati.

Kuhusu suala la makato ya fedha za pembejeo ambazo wakulima wanalalamikia kukatwa kiasi kikubwa kuliko kiwango halisi wanachostahili, Waziri huyo wa Kilimo amesema atalishughulikia.

Aidha,Mbunge wa jimbo la Bariadi, Andrew Chenge amesema amefanya ziara katika kata 20 kati ya 30 kwenye jimbo hilo na changamoto kubwa ya wananchi ni mauzo ya pamba. “Ujio wa Waziri Mkuu umeleta manufaa kwani wanunuzi wameanza kuja kwa kasi”.

Mbunge huyo amemuomba Waziri Kuu awafikishie salamu zao kwa Rais Dkt. John Magufuli kwamba wanamshukuru kwa namna anavyowajali wakulima mbalimbali nchini wakiwemo na wa zao la pamba.

Kwa upande wake, Mbunge wa jimbo la Itilima, Njalu Silanga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Nsangali ambayo inanunua pamba amemuahidi Waziri Mkuu kwamba ifikapo kesho (Ijumaa, Agosti 9, 2019) saa nane mchana atakuwa amelipa sh. milioni 135 zinazohitajika na amcos ya Itemelo ili kulipia deni la pamba iliyoko ghalani.

Awali, Katibu wa Amcos ya Itemelo, Lucas Ephraim alimuomba Waziri Mkuu awasaidie kuyahimiza makampuni mbalimbali yanayonunua yapeleke fedha kwa wakati ili kukidhi makisio tarajiwa.

Katibu huyo alisema chama chao kinahudumia vijiji vitano vikiwa na jumla ya wakulima 2,665 wa pamba wenye jumla ya ekari 9,675. Pia chama chao kinahitaji sh. milioni 135.139 ili kulipia deni la pamba ambayo iko ghalani.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia kazi ya kupima pamba kwa njia ya kielektroniki wakati alipokagua ununuzi wa pamba  katika Chama cha Ushirika  cha Msingi cha Itemelo  kilichopo eneo la Dutwa mkoani Simiyu, Agosti 8, 2019   Kulia ni  Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na wa tatu Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka. 

WAZIRI WA AFYA AELEZA NAMNA AMBAVYO SEKTA YA AFYA ITANUFAIKA KUPITIA MKUTANO WA SADC

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV 

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imetaja maeneo matatu ya kimkakati ambayo nchi ya Tanzania itanufaika nayo kupitia mikutano inayoendelea kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADC).

Akizungumza leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwlimu Nyerere jijini Dar es Salaam Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalim amesema Tanzania kupitia Mkutano wa SADC kuna mambo mengi tutanufaika nayo.

Waziri Mwalim ametaja baadhi ya maeneo ambayo nchi yetu itanufaika ni pamoja na MSD  kutoa huduma za dharura kwa washiriki wa mkutano wa SADC 

Akifafanua zaidi Waziri Mwalim baada ya kutembelea mabanda ya Afya  yakiwemo ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya  Moyo ya Jakaya Kikwete ma Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) amesema sekta ya afya imejipanga katika maeneo makubwa matatu.

"Maeneo hayo ni pamoja na kutoa huduma ya dharura na kusisitiza kuna vyumba vimetengwa kwa ya kutoa huduma ya matibabu kwa mtu atakayekuwa na tatizo ya kiafya,"amesema.

“Pia kwa kutumia maonesho hayo sekta ya afya nchini inaonesha uwezo, ubunifu na utashi wa kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya utalii wa kimatibabu na kupitia hospitali ya Taifa ya Muhimbili  wamepandikiza vifaa vya kusikia kwa watoto na kutibu kwa kutumia radioloji,"amesema.

Waziri Mwalim amesema  huduma hizo zilikuwa hazipatikani nchini wala kwa nchi za SADC huku akitoa mfano upandikizaji wa figo ambapo ukitoa nchi ya Afrika Kusini nchi nyingi hazijaanza  kutoa huduma za kupandikiza figo.

Wakati huo amesema mkutano wa SADC wataeleza na kuwaonesha washiriki wa mkutano huo ni kwa namna gani Tanzania ambavyo imepiga hatua kwa kutoa huduma za kibingwa.

"Kwa mazingira hayo nchi za SADC hazina haja ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi za jumuiya hiyo.Wagonjwa waletwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH).Kila mwezi inapokea wagonjwa 24 kutoka nchi za SADC  na hasa nchi za Comoro,Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) pamoja na Malawi.

Amesema Wizara ya Afya inaamini mkutano wa SADC utaongeza idadi ya wagonjwa kuja nchini Tanzania kwa ajili ya matibabu." Muhimbili kwa mwaka tunapokea wagonjwa  284 kwa nchi za SADC,"amesema.

Pia amesema eneo la tatu  ni utoaji wa zabuni na kufafanua Tanzania itanufaika na ununuzi wa dawa,kwani MSD imepata  mkataba wa kusambaza dawa kwa nchi za SADC.

Amesema mawaziri wa afya wa nchi za SADC kwa umoja wao waliamua kuipa mkataba MSD  wa kununua na kusambaza dawa."Kupitia maonesho haya ya SADC yamechochea utaratibu wa kusambaza dawa na zabuni za kununua imeshakamilika,"amesema  na kuongeza nchi za Mauritius , Botswana na Lesotho zimekubali kununua dawa kupitia utaratibu wa nchi za SADC. 
 Wataalam wa afya wa Muhimbili, MOI, JKCI na Hospitali ya Lugalo wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mh.Ummy  Mwalimu katika viwanja vya ukumbi  wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC). 
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto  Mh.Ummy Mwalimu akisoma jarida la Muhimbili linaloeleza huduma mbalimbali za afya zinazopatikana MNH. Kulia ni Dkt. Juma Mfinanga akimweleza jambo Waziri. 
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mh.Ummy Mwalimu akimuonesha jambo Dkt. Juma Mfinanga 
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mkuu wa Idara ya Utafiti na Mafunzo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Pedro Pallangyo akimweleza v huduma zinazopatikana JKCI zikiwamo huduma za tiba ya umeme wa moyo na  kuzibua mishipa ya damu.

TBS yawapa mbinu wafanyabiashara za kuingia soko la SADC

$
0
0
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa mwito kwa wafanyabiashara wanaotaka kufanya shughuli zao kwenye nchini za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kufika kwenye ofisi za shirika hilo ili kupata elimu kuhusiana na namna ya kufanya biashara na nchi hizo bila vikwazo vyovyote.

Ushauri huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Ofisa Mwandamizi Uhakiki Ubora wa TBS, Stella Mrosso, wakati akizungumza na kwenye Maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda SADC yaliyomalizika jana (ALHAMISI) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jana.

Akieleza faida za wafanyabiashara kupata elimu TBS kabla ya kupeleka biashara zao kwenye soko la nchi za SADC, Mrossa alisema hatua hiyo inawasaidia kujua taratibu za kufuata, ambazo zinawasaidia kuepukana na vikwazo mbalimbali.

"Hii inarahisishia biarasha kuliko wale wanaopita juu kwa juu, kwani wanaweza kufika mipakani wakazuiwa kupeleka bidhaa zao kwenye nchi walizokusudia na hivyo kujikuta wakipata hasara kubwa," alisema.

Alisema TBS ni mdau mkubwa kwenye nchi za SADC hasa katika suala zima la umahiri, hivyo kwa ajili ya kuwasaidia. "Sisi tupo kwa ajili yao, kwa hiyo wakipita kwetu na kupatiwa elimu watafanyabiashara vizuri na kukuza uchumi wao na wa nchi kwa ujumla,"alisema.

Pia, aliwataka wafabiashara kufika kwenye ofisi za shirika hilo kuthibitisha ubora wa bidhaa zao, kwani shirika hilo lina maabara zenye umahiri uliothibitishwa kimataifa.

Alifafanua kwamba bidhaa ikishapimwa kwenye maabara zenye umahiri, haiwezi kupimwa tena, kwani matokeo yake yanakuwa yanaaminika.

Alitaja baadhi ya maabara za shirika hilo zenye umahiri kuwa ni maabara ya nguo, maabara ya kemia, maabara ya ujenzi, maabara ya umeme. "Bidhaa zikishapimwa kwenye maabara hizi kwenye soko la SADC haziwezi kupimwa tena," alisema.

Alizidi kufafanua kwamba Tanzania ina maabara 31 zenye umahiri, hivyo kuwa miongoni mwa nchi tatu bora kwenye ukanda wa nchi za SADC zenye maabara nyingi zenye umahiri.

Mrosso, alitaja hatua nyingine ambazo zinachukuliwa na nchi za SADC kuondoa vikwazo vya kibiashara kwa nchi wanachama kuwa ni pamoja na kuoanishwa viwango.

"Sisi kama TBS tuna wajibu mkubwa wa kuoanisha viwango ambavyo vitasaidia wafanyabiashara kuondokana na vikwazo vya kibiashara,"alisema Mrosso na kuongeza kwamba kwenye kuoanisha viwango wanawezesha ufanyikaji biashara bila vikwazo.

Alisema kwenye nchi za SADC viwango ambavyo tayari vimeoanishwa vinafanyakazi kulingana na mahitaji ya wafanyabiashara wa Tanzania.

Alipoulizwa wametujiaje fursa ya kushiriki maonesho ya SADC, Mrosso, alisema wameweza kutoa elimu ya huduma zitolewazo na shirika hilo pamoja na kuwataka wajasiriamali kujitokeza kwa wingi kwenda kuthibitisha bidhaa zao kwani huduma hiyo inatolewa bure.

Mrosso, alisema lengo la hatua hiyo kuwawezesha kufanya biashara, kukuza uchumi wao na wa nchi kwa ujumla. "Pia tunatoa elimu ili kuwawezesha kuzalisha bishaa zenye ubora," alisema.
Ofisa Mwandamizi Uhakiki Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Stella Mrosso, akizungumza na baadhi wananchi waliotembelea banda la shirika hilo na kwenye Maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) yaliyomalizika jana kuhusiana na shirika hilo linavyowezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwenye nchi za SADC bila vikwazo vyovyote. Maonesho yalifanyika katika kwenye kituo cha Mikutano wa Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. 

ELIMU INAHITAJIKA KWENDA NA MIPANGO YA SERIKALI-DKT AKWILAPO

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Serikali imesema kuwa katika kwenda na mipango na mikakati mbalimbali kunahitaji kuangalia sekta ya elimu kwa ajili ya kuzalisha wataalam wa kufundisha wenye uwezo wa kufundisha wanafunzi.

Hayo ameyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo wakati akifungua mkutano wa Elimu ya Ualimu katika kujadili Usimamizi wa Mafunzo ya Ualimu uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa mkutano huo ni kuangalia mambo mbalimbali ya kuandaa Walimu pamoja na kuangalia mitaala inayokwenda na wakati.Dkt. Akwilapo amesema kuwa serikali inakwenda na mipango mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu inayoendana na mwelekeo ya mipango hiyo.

Amesema kuwa katika mkutano watajadili na mitaala namna ya kuboresha kwenda na mazingira yaliyopo na mabadiliko ya mitaala ni kutokana na serikali inavyotaka katika uboreshaji wa elimu nchini.

Aidha amesema watalaam waliokuwepo katika mkutano huo ni wabobezi katika mafunzo ya Vyuo vya ualimu ambao wanaweza kushauri serikali katika kuandaa Walimu wataokwenda kufundisha wanafunzi wa Msingi na Sekondari.

Nae Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Mafunzo ya Elimu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Agustina Lupokela amesema mkakati wa malengo ya Seksheni kwa mwaka 2019/2020 inayoongozwa na Kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa Taifa la Uchumi wa kati ifikapo 2025 kupitia uchumi wa Viwanda.

Amesema mikakati yote imejikita katika kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa walimu wa masomo ya Sayansi,Hisabati na fani za Ufundi ili kufanikisha azima ya serikali.

Mratibu wa Kuendeleza Elimu ya Ualimu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Ignas Chonya amesema kuwa Mradi huo unatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Tanzania na Japan na unaendelea kufanya vizuri katika sekta ya Elimu.

Amesema kuwa mradi huo umeanza hadi sasa mwaka wa tatu na matokeo yake katika uboreshaji wa Shule pamoja na rasiliamali watu kuongezewa ujuzi.
katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo akifungua Mkutano wa Wadau wa Elimu ya Ualimu kujadili Usimamizi wa Mafunzo ya Ualimu iliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Mafunzo ya Elimu Agusta Lupokela akitoa maelezo katika mkutano wa kujadili sekta ya Elimu kwa Ualimu.
Mratibu wa Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Ualimu Ignas Chonya akizungumza na waandishi kuhusiana na mafanikio ya mradi huo.


Mwenyekiti wa Walimiki wa Vyuo vya Ualimu Binafsi Mahamood Mulingo akizungumza namna ya uendeshaji wa elimu kutokana na mahitaji yaliyopo kwa muda uliopo.
Sehemu ya wadau katika mkutano huo.
picha ya pamoja wakuu wa Vyuo vya elimu katika picha ya pamoja( picha zote na Chalila Kibuda ,Michuzi TV)

KUZINDULIWA KWA MFUMO RASMI WA MAUZO YA MAZAO YA KILIMO KUTAIMARISHA MAENDELEO YA KILIMO NA USHIRIKA NCHINI– MHE HASUNGA

$
0
0


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za wakulima (Nanenane) zilizofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu Tarehe 8 Agosti 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za wakulima (Nanenane) zilizofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu. tarehe 8 Agosti 2019. 
Sehemu ya wananchi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za wakulima (Nanenane) zilizofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu. tarehe 8 Agosti 2019. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwapungia mikono wananchi ishara ya kuwasalimu wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za wakulima (Nanenane) zilizofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu. tarehe 8 Agosti 2019. 


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo, Simiyu

Serikali imesema kuwa kuwa maendeleo ya Sekta ya Kilimo na Tasnia ya Ushirika nchini itaimarika baada ya kuzinduliwa mfumo rasmi wa mauzo ya mazao ya kilimo kupitia Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).

TMX ina lengo la kuongeza ufanisi katika juhudi za Serikali za kurasimisha mifumo ya masoko ambayo imekuwa na changamoto kwa muda mrefu; kwa kuwaunganisha Wauzaji na Wanunuzi wa bidhaa, kuleta ushindani kwenye bei, kupunguza gharama za uendeshaji biashara na kuweka uwazi.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema hayo tarehe 8 Agosti 2019 wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za wakulima (Nanenane) zinazofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi Katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Amesema kuwa mbali na soko la bidhaa pia kuzinduliwa kwa Mfumo wa Kielektoniki wa usajili wa wakulima na mfumo wa kielekroniki wa Kusimamia Biashara (Agricultural Trade Management Information System – ATMIS) utaimarisha makusanyo ya maduhuli na tozo kwa kuhakikisha huduma zote za utoaji vibali, leseni na vyeti unafanyika kielektroniki na pia kudhibiti udanganyifu katika hati na nyaraka za huduma hizo.

Alizitaja faida zingine kuwa ni pamoja na Kuhakikisha kuwa kazi ya kumhudumia mteja inafanyika kwa wakati mara tu baada ya hatua zote za maombi ya utoaji vibali, na vyeti kumalizika na kuimarisha upatikaji wa taarifa na takwimu muhimu za uingizaji na usafirishaji mazao ya kilimo nje ya nchi na Kuondoa tatizo la nyaraka bandia ambalo huchangiwa na matumizi ya mfumo

Mhe Hasunga ameyataja maeneo maalumu ya kimkakati katika sekta ya kilimo ambacho kinafanyiwa maboresho ili kuimarisha usimamizi wa kilimo na kuwapatia Wakulima huduma kwa urahisi zaidi ambayo ni Bima ya Mazao, Ambapo wizara ya Kilimo imeanzisha mwongozo wa Bima ya Mazao kwa Wakulima ambao ukielekeza jinsi ya kujiunga, kutekeleza na kuwasilisha madai ili kumwezesha kulipwa fidia pale anapopata hasara.

Mapitio ya Sera na Sheria, Mhe Hasunga amesema kuwa Wizara imeanza na itaendelea kuipitia Sera ya Taifa ya Kilimo ya mwaka 2013 na sheria mbalimbali kwa lengo la kubaini maeneo ambayo yatapaswa kuhuishwa ili kwenda na hali halisi ya sasa na mwelekeo wa Serikali wa kubadili kilimo kuwa kilimo cha kibiashara. 

“Mtazamo wa Wizara ni kuwa na Sheria moja itakayosimamia rasilimali watu, matumizi bora ya pembejeo, ardhi ya kilimo na maeneo mengine muhimu” Alikaririwa Mhe Hasunga

Zingine ni Mfumo wa upatikanaji wa Pembejeo za Kilimo, Wizara inaendelea na zoezi la kupitia kwa kina mifumo iliyopo ya uzalishaji, uagizaji na usambazaji wa mbegu, mbolea na viuatilifu. Aidha wizara inaendelea kutoa elimu kwa Wakulima ili wazalishe kulingana na mahitaji ya soko na kufanya kazi kwa karibu na Taasisi nyingine zinazohusika na masoko nchini ikiwemo TANTRADE na Soko la Bidhaa (TMX).

Sambamba na hayo amesema kuwa wizara ya Kilimo imejipanga kuhakikisha kuwa kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) Sekta ya Uvuvi inaongeza ufugaji wa samaki wenye tija na endelevu katika mabwawa ili kuwe na uwezekano wa kuzalisha samaki wengi zaidi na kuondoa kabisa uvuvi haramu.

“Ni imani yangu kuwa kama ASDP II itatekelezwa vizuri, Tanzania itakuwa nchi ya kipato cha kati kabla ya mwaka 2025” Alisisitiza

RAIS WA ZANZIBAR DK KSHEIN AFUNGA MAONESHO YA WIKI YA NNE YA VIWANDA YA SADC JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Mkurugenzi wa Bishara ya Shirika la Air Tanzania Ndg. Patrick .W.Ndekama, alipokuywac akitembelea banda la maonesho la Air Tanzania katika viwanja vya Ukumbi wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam wakati wa ufungaji wa maonesho hayo(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Afisa wa TRC Bi. Jamila Mbarouk alipotembelea banda la maonesho katika viwanja vya Kulius Nyerere Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Afisa wa ZSTC Ndg. Issa Hamad Ramadhani alipotembelea maonesho ya Wiki ya Nne ya Viwanda ya SADC Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ikulu)

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa Serikali na SADC WAakiwa wamesimama wakati ukipigwa Wimbo.(Picha na Ikulu)

 KATIBU Mkuu wa SADC Mhe. Dr.Stergomena Tax, wakati wa ufungajin wa Maonesho ya Nne ya Wiki ya Maonesho ya Viwanda ya SADC leo Jijini Dar es Salaam.yaliofanyika katika ukumbi wa Juluis Nyerere.(Picha na Ikulu)
KAIMU Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombe akizungumza wakati wa mkutano wa Ufungaji wa Wiki ya Nne ya Maonesho ya Viwanda ya SADC Jijini Dares Salaam.(Picha na Ikulu)
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images