Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

HIVI NDIVYO MKUU WA MKOA WA DAR PAUL MAKONDA ALIVYOMTEMBELEA KIJANA MWENYE TATIZO LA UVIMBE USONI


Mambosasa Sasa Awape Fursa Walemavu Kwenye Sadc

$
0
0
Uchambuzi Wa Habari: 

Mambosasa Sasa Awape Fursa Walemavu Kwenye Sadc

Ndugu , 

Marufuku ya bodaboda kuingia mjini wakati huu wa mkutano wa Sadc ni sahihi. Hoja za Kamanda Mambosasa ni za msingi. 

Hata hivyo, leo nilipata nafasi ya kufika pale ukumbi wa Mwalimu Nyerere kwenye maonyesho ya Sadc. 

Ushauri wangu:

Ili kuvutia watembeleaji wengi zaidi wa maonyesho ya Sadc yanayoendelea sasa kunahitajika usafiri wa haraka na wa gharama nafuu kufika na kutoka eneo la tukio pale Mwalimu Nyerere Conference Centre.

Marufuku ya bodaboda sawa, lakini, Kamanda Mambosasa na waandaaji wa tukio wangetoa fursa ya ajira kwa walemavu waendesha bajaj ili kuwasaidia watembeleaji kwenda na kutoka eneo la tukio.

Ingewezekana kabisa, kukaandaliwa utaratibu wa kuwepo kwa bajaji  50 za walemavu. 25 zikawapo nje ya eneo la tukio zikiwa na stika za usajili za Sadc zenye namba na jina la dereva, na 25 nyingine zikawepo pale Posta Mpya kwa utaratibu huo huo . 

Waendesha bajaj hao walemavu wapewe na waandaaji hata elfu 20 kwa siku kila mmoja na wawatoze kila abiria shilingi mia tano kwa safari moja ya kwenda kwenye eneo la tukio na kurudi Posta Mpya. Bajaj moja inabeba abiria watatu mpaka wanne.

Kwa kufanya hivi tutakuwa tumeongeza idadi ya watembeleaji na wakati huo huo kutoa fursa kwa walemavu wetu waendesha bajaj kujiongezea kipato kipindi hiki cha maonyesho ya Sadc na mkutano wa Sadc hapa nchini mwetu.

Ni ushauri tu.

Maggid Mjengwa.

HASUNGA AKAGUA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU KUHUSU UNUNUZI WA PAMBA WILAYA YA BARIADI, ITILIMA NA MASWA

$
0
0


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu kukagua utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu aliyoyatoa hivi karibuni kwa wafanyabiashara kununua Pamba ya wakulima, tarehe 6 Agosti 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu kukagua utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu aliyoyatoa hivi karibuni kwa wafanyabiashara kununua Pamba ya wakulima, tarehe 6 Agosti 2019.


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu kukagua utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu aliyoyatoa hivi karibuni kwa wafanyabiashara kununua Pamba ya wakulima, tarehe 6 Agosti 2019.


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) tarehe 6 Agosti 2019 amefanya ziara ya kikazi mkoani Simiyu kukagua utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu aliyoyatoa hivi karibuni kwa wafanyabiashara kununua Pamba ya wakulima.

Mhe Hasunga ametembelea na kukagua Kituo cha ununuzi wa Pamba cha Itemelo kilichopo kata ya Dutwa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Kituo cha ununuzi cha Lugulu katika kata ya Lugulu Wilaya ya Itilima na Kituo cha Kumalija kilichopo katika kata ya Shanwa wilayani Maswa.

Katika ziara hiyo Mhe Waziri amejionea hali ya ununuzi wa Pamba ya wakulima ukiwa unaendelea kutokana na serikali hivi karibuni kupata muarobaini wa mustakabali wa zao hilo.

Waziri huyo wa Kilimo amepiga marufuku Pamba ya wakulima kupimwa katika mizani zisizofahamika badala yake lazima ipimwe katika mizani iliyothibitishwa na wakala wa vipimo.

Katika hatua nyingine pia Mhe Hasunga ametoa kalipio Kali kwa wanunuzi wa Pamba kadhalika vyama vya ushirika vinavyowakata kilo moja wakulima kwa madai ya mifuko ya kupimia badala yake ameagiza mkulima akatwe kutokana na uzito wa mfuko sio kukadiria kilo moja.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imekusudia kuwanufaisha wakulima kupitia mazao wanayozalisha kwa kuwaongezea elimu ya Kilimo bora na chenye tija.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga yupo mkoani Simiyu kwa ajili ya sherehe za wakulima (Nanenane) ambazo kilele chake ni tarehe 8 Agosti 2019 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga maadhimisho hayo akimuwakilisha Rais wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.

JESHI LA POLISI LATOA ONYO KALI KWA MADEREVA

$
0
0

Jeshi la Polisi nchini limetoa ufafanuzi na kuweka msisitizo kwenye katazo alilotoa  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum  Dar es salaam tarehe 05/08/2019 kuhusu kupiga marufuku magari kufunga taa za vimulimuli au za rangi rangi, taa zenye mwanga mkali (spot light) na kufunga ving’ora kwenye magari ya kiraia au watu binafsi na pikipiki za kiraia.
Akitoa tamkoa hilo Msemaji wa Jeshi hilo SACP David Misime amesema kuwa, katazo hilo ni kwa nchi nzima, kutokana na kujitokeza  kwa baadhi ya watu walioamua kufunga vimulimuli na ving’ora  na kuvitumia wawapo barabarani na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara.  Wamefunga vifaa hivyo kutaka kupewa kipaumbele wawapo barabarani kwa kujua au kwa kutofahamu kuwa ni kinyume  na sheria, kanuni na taratibu zilizopo.


Na Kwa mujibu wa sheria ya usalama barabarani sura ya 168 ya mwaka 1973 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002 kifungu cha 39 B (I) na (2) kinafafanua juu ya matumizi ya ishara ikiwepo ving’ora na vimulimuli.


SERIKALI KUPIGWA TAFU UJENZI WA MRADI WA MAJI WA MUGANGO-KIABAKARI MKOANI MARA

$
0
0

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiwa kwenye chanzo cha maji cha Bukanga kinachotumiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA), mkoani Mara. 
Magari mawili ya majitaka ya Mradi wa Majitaka wa Manispaa ya Musoma Mjini unaotekelezwa na Kampuni ya Lahmeyer GKW Consult, mkoani Mara 

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akikagua moja ya magari mawili ya majitaka ya Mradi wa Majitaka wa Manispaa ya Musoma Mjini unaotekelezwa na Kampuni ya Lahmeyer GKW Consult, mkoani Mara. 
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza na viongozi na wataalam wa mkoa wa Mara, pamoja na wataalam wa Kampuni ya Lahmeyer GKW wanaotekeleza ujenzi wa Mradi wa Majitaka Musoma mjini, mkoani Mara. 
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiangalia ujazo wa maji kwenye tenki la maji la Nyamiongo lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 5, katika Manispaa ya Mji wa Musoma, mkoani Mara. 
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akipokea maelekezo ya ujenzi wa Mradi wa Majitaka katika Manispaa ya Mji wa Musoma kutoka kwa Mhandisi Mshauri Mkuu, Rweyemamu Kassimbi, mkoani Mara. 
………………… 
Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (BADEA) na Mfuko wa Maendeleo wa Saudia (SFD) zipo katika hatua za mwisho za kusaini mkataba wa ujenzi wa Mradi wa Maji wa Mugango-Kiabakari katika mkoa wa Mara. 

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ametoa kauli hiyo akiwa kwenye ziara ya kikazi katika kufuatilia na kukagua miradi ya maji inayotekelezwa mkoani Mara. 

Amesema mkataba huo utakaogharimu Dola za Marekani milioni 30.69 unatarajiwa kusainiwa tarehe 15 Agosti, 2019 unalenga kuboresha huduma ya maji katika maeneo ya Mugango, Kiabakari na Butiama, na kwa sasa hatua ya usanifu wa kina na uandaaji wa makabrasha ya zabuni umekamilika na taratibu za kumpata Mkandarasi zinaendelea. 

Kazi ya uboreshaji ya mradi huo mkongwe ulioanza mwaka 1974 itakapokamilika utanufaisha wananchi wapatao 80,000 waliopo katika eneo la mradi pamoja na vijiji 13 vilivyopo ndani ya kilomita 12 kutoka bomba kuu. Serikali imetenga Shilingi bilioni 8.5 kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo. 

Wakati huo huo, Naibu Waziri Aweso amesema Mtaalam Mshauri kutoka Kampuni ya WAPCOS Ltd ya India tayari ameanza kazi ya upembuzi yakinifu kwa miradi ya maji katika miji ya Rorya, Tarime na Mugumu mkoani Mara tangu tarehe 1 Juni, 2019 na atakamilisha kazi hiyo ifikapo tarehe 31 Agosti, 2019. 

Akisisitiza kuwa lengo la Serikali ni kumaliza tatizo la maji katika maeneo yote yaliyo pembezoni mwa Ziwa Victoria. 

Miji ya Rorya, Tarime na Mugumu ni miongoni miji itakayonufaika na Mradi wa Maji wa Miji Mikuu ya Wilaya 29 inayotekelezwa na Serikali kwa kutumia mkopo wa Dola za Marekani milioni 500 kupitia Benki ya Exim ya India.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI KIWANDA CHA KUCHAKATA MPUNGA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa Meneja Ufundi  wa Kiwanda cha kuchakata Mpunga na kuzalisha Mchele cha Murza Wilmer East Africa Miller Ltd Mkoani Morogoro  Bw. Vaidya  Subramaniam wakati wa hafla ya Uwekaji  Jiwe la Msingi wa Kiwanda hicho leo Agost 07,2019. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa Ziara ya kikazi ya siku Tatu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Kiwanda Cha kuchakata Mpunga na kuzalisha Mchele cha Murza Wilmer East Africa Miller Ltd kiliopo Mkoani Morogoro leo Agost 07,2019. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa Ziara ya kikazi ya siku Tatu.

WAZIRI KIGWANGALLA AFUTA UMILIKI WA KITALU CHA UWINDAJI CHA GREEN MILES

SAVE THE CHILDREN YAADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI DUNIANI MKOA WA DODOMA

$
0
0
Shirika la Kimataifa la Kuhudumia watoto la Save The Children kupitia mradi wake wa Lishe Endelevu unaolenga kuimarisha hali ya lishe kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa, wajawazito na wanaonyonyesha, vijana wa rika la balehe na watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano limeadhimisha wiki ya Unyonyeshaji duniani mkoani Dodoma.

Kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani yaliyoandaliwa na shirika la Save The Children yamefanyika leo Agosti 7,2019 katika kijiji cha Kingale wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa Msoleni Dakawa kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma. 

Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Dodoma Benety Malima alisema maadhimisho hayo ya wiki ya unyonyeshaji ni sehemu ya utekelezaji wa mradi Lishe Endelevu unaofadhiliwa na Mfuko wa Watu wa Marekani 'USAID'.

Malima alitumia fursa hiyo kuwahimiza waajiri kwenye mashirika na taasisi mbalimbali kutenga chumba maalumu kwa ajili ya akina mama kuwanyonyesha watoto wao. Alisema siku 1000 za lishe ya mtoto zinaanzia tumboni na na kuwasisitiza akina mama wajawazito kula vyakula vyenye lishe kabla na baada ya kujifungua. Malima alisema kwa mujibu wa takwimu za hali ya lishe kutoka taasisi ya chakula na lishe kuwa katika mikoa minne ya Dodoma, Rukwa, Iringa na Morogoro ambako shirika lao linafanya nao kazi hali ya lishe hairidhishi. Malima aliwasisitiza wanaume kushirikiana na akina mama katika suala zima la kunyonyesha na kuongeza kuwa wakati mwingine wa baba ni chanzo wa mama kutopata maziwa kutokana na ugomvi hivyo ni vyema wanaume wakawapenda wake wao. 

Aidha alisema lishe kwa wanawake wajawazito inachochea hatari ya kujifungua watoto njiti , waliodumaa au kuharibu mimba. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa Msoleni Dakawa alisema takwimu za hali ya ulishaji watoto wachanga na wadogo katika mkoa wa Dodoma takribani asilimia 97 ya watoto wenye umri wa miaka miwili,wananyonyeshwa maziwa ya mama, idadi ya watoto wanaoanzishiwa maziwa ya mama kwa wakati sahihi katika kipindi sahihi kisichozidi saa moja baada ya kuzaliwa ni asilimia 57. 

"Idadi ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kupewa maji, vinywaji na vyakula vingine katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa ni asilimia 47.7, idadi ya watoto wenye umri wa miezi 6-23 wanaolishwa chakula kinachokidhi vigezo cha ubora kiliishe ni asilimia 35.9 na idadi ta watoto wanaoanzishiwa vyakula cha nyongeza kwa wakati sahihi katika umri wa miezi 6 hadi 8 ni asilimia 85.7,'' alieleza. 

Alibanisha kuwa changamoto ya matumizi ya chumvi yenye madini joto, ni asilimia 81 ndio wanatumia chumvi yenye madini joto la kutosha, mama mjamzito anatumia chumvi siyo na madini joto, hivyo afya ya mtoto inaathiriwa sana kwani anaweza kuzaliwa akiwa na udumavu wa ubongo au ulemavu wa viungo. 

''Nitoe rai kwa wazazi na walezi kutafuta taarifa sahihi kuhusu unyonyeshaji unaofaa kutoka kwa mtoa huduma ya kiafya katika jamii, mtaalam wa afya kipindi cha ujauzito hili likienda sambamba na kuhudhuria kliniki mapema pindi tu mama anapojigundua ni mjamzito,'' alisema Mkurugenzi huyo. 

Aliwataka akina baba kuwasindikiza wenza wao kliniki ili kuhakikisha kwamba mume/mwenza na familia wana taarifa kuhusu malengo ya unyonyshaji ili waweze kutoa msaada , pia aliwasisitiza kina mama wanaonyonyesha kuainisha msaada wa vitendo unaohitajika na kuomba msaada kutoka kwa mume/mwenza, familia na ndugu wengine ili kupata msaada. 

Nao baadhi ya akina mama waliohudhuria katika maadhimisho hayo akiwemo Sikitu Damian Lyimo aliwataka akina mama wote nchini kula vyakula vyenye lishe ili kuweza kuzaa watoto wenye afya njema na akili timamu. Aliongeza kuwa wamepata elimu ya kutosha Shirika la Save the Children hivyo watahakikisha wanaitumia ipasavyo kwa kuwa vyakula vyote vyenye lishe bora vinapatikana kijijini hapo. 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa Msoleni Dakawa akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani leo Agosti 7,2019 katika kijiji cha Kingale wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma. 
Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Dodoma Benety Malima (mwenye tisheti nyekundu kulia) akiwa kwenye Kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani yaliyoandaliwa na shirika la Save The Children leo Agosti 7,2019 katika kijiji cha Kingale wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma. 
Zoezi la upimaji wa hali ya lishe kwa watoto wa miezi 6 hadi 59 likiendelea. 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa Msoleni Dakawa akishuhudia mafunzo ya upishi wa chakula cha watoto kwa wanajamii hususani akina mama. 
Kulia ni Mtaalamu wa afya akionesha aina mbalimbali za za vyakula lishe vinavyopatikana katika mkoa wa Dodoma.

WAZIRI MKUU AONGOZA MAZISHI YA MKE WA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi katika mazishi yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, katika mazishi yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Serikali, Profesa Adelardus Kilangi (wa pili kushoto) na familia yake wakishiriki katika Ibada ya mazishi ya Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanaza Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Profesa Kilangi, Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
Waziri Mkuui, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Renatus Nkwande na Askofu wa Jimbo la Geita, Flavian Kassala katika mazishi ya Natalia Bahati Kilangi, Mke wa mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi wakati alipoiwakilisha serikali katika mazishi ya Mke wa mwanasheria Mkuu wa Serikali, Natalia Bahati Kilangi yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza katika mazishi ya Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia kwa Waziri Mkuu) wakishiriki katika ibada ya mazishi ya Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi yaliyoanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira, na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Waziri wa Madini, Doto Biteko. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo, Agosti 7, 2019 ameongoza mazishi ya mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, Bibi Natalia Bahati Kilangi.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali katika mazishi hayo yaliyofanyika nyumbani kwa Profesa Kilangi eneo la Luchelele jijini Mwanza, Waziri Mkuu amemuomba Profesa Kilangi na familia yake kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu ambapo wamempoteza mama ambaye ni nguzo muhimu ya familia.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasilisha salamu za pole kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa Profesa Kilangi na familia yake kutokana na msiba mzito walioupata.

Katika salamu zake Rais Dkt. Magufuli amesema Serikali inathamini sana mchango mkubwa na mahili unaotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na anamini kwamba kwa vyovyote vile wakati wa uhai wake, marehemu Natalia alishiriki kwa kiwango kikubwa kuhakikisha kwamba mumewe anaifanya kazi yake vizuri.

Awali, Spika wa Bunge, Job Ndugai aliwasihi waombolezaji wote wamkumbuke katika sala zao, Mwanasheria Mkuu wa Seriakali Profesa Kilangi ambaye ana kazi nzito ya kuishauri Serikali na alimtaja kuwa ni kiungo muhimu cha mihimili yote mitatu.

Naye, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Renatus Nkwande alimuomba Profesa Kilangi na familia yake wajipe moyo kwa sababu binadamu anapokuwa hai au anapokufa bado anabaki kuwa mali ya Mwenyezi Mungu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Mabenki nchini, Abdulmajid Msekela ambaye pia ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB alisema wanachama wote wa umoja huo wanatoa pole kwa familia na wanamwombea Mwanasheria Mkuu wa Serikali na familia nzima, Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki cha majonzi.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria katika mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga, Waziri wa Madini, Doto Biteko, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga.

Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally, Manaibu Mawazi, Wakuu wa Mikoa na wilaya na viomgozi mbalimbali wa Serikali.Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na Askofu wa Jimbo la Geita na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania(TEC), Flavian Kassala, Mapadri na Masheikh kutoka maeneo mbalimbali nchini.

WANAFUNZI WA LINDI SEKONDARI WAASWA KUSOMA KWA BIDII.

$
0
0


Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma kwa Umma Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam Dr. Arnold Towo akizungumza na Wanafunzi wa kidato cha Tano na Sita wakati wa ziara fupi katika Shule ya Lindi Sekondari. 

Mkuu wa Kitengo cha Udahili Kurugenzi ya Shahada za Awali kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Victoria Lyimo akiwapa maelezo wanafunzi wa Lindi Sekondari wakati wa Ziara fupi iliyofanywa shuleni hapo. 


Wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa wataalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa ziara fupi iliyofanywa na Chuo hicho Agosti 7,2019. 

************* 

Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kimetembelea na kufanya mazungumzo na Wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari ya Mkoa wa Lindi. 

Akizungumza na wanafunzi hao, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma kwa Umma Dr. Arnold Towo aliwasihi wanafunzi kusoma kwa bidii na kuwataka wawe wabunifu na wenye kujituma katika masoma yao. 

Jambo la msingi sana kwenu ni kujitambua na kuchagua masomo yale ambayo yatawasaidia katika maisha yenu ya baadae. 

“Nawaomba sana mjitume na kutumia nafasi mnazopata ikiwa ni pamoja kufanya midahalo itakayo wasaidia kuwajengea uwezo wa kujieleza, hii itawasaidia pale mtakapomaliza masomo na kujiandaa na ajira”, alisisitiza Dr. Towo. 

Aidha Mkuu wa Kitengo cha Udahili, Kurugenzi ya Shahada za Awali Victoria Lyimo aliwasisitiza wanafunzi hao kuwa Wachamungu, kuwa na nidhamu na kusoma kwa bidii kwa kuzingatia haya hata kwenye Masomo yenu mtaweza kufanya vizuri sana. 

Shule ya Lindi Sekondari kidato cha Tano na Sita inamichepuo ya HKL, HGL, EGM, PGM na HGK katika masomo haya wanafunzi wameaswa kusoma kwa bidii ili waweze kuwa nanufaulu mkubwa utakao wasaidia pindi wanapotaka kujiunga na Chuo Kikuu. 

Hii ni sehemu mojawapo ya jukumu la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Kitengo cha Huduma kwa Umma kurudi kwa jamii kuzungumza na kutoa hamasa kwa wanafunzi mbalimbali nchini katika Masuala ya Elimu,Tafiti na Ushauri. 

Chuo kikuu cha Dar es Salaam, kupitia ndaki ya Sayansi ya Kilimo na Ufugaji wa Samaki wa Kisasa kimeshiriki katika Maonesho ya Wakulima Nane Nane yenye kauli mbiu isemayo “Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Nchi” kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti, 2019 katika Viwanjanvya Ngongo Kanda ya Kusini Mkoani Lindi ambapo kilele cha maonesho hayo ni kesho Tarehe 8 Agosti, 2019.

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK SHEIN AKIIPOKEA MELI MPYA YA MAFUTA YA MT. MAPINDUZI 2 IKIWASILI ZANZIBAR

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiangalia Meli Mpya ya Mafuta ya MT.UKOMBO II,Ikiwasili kuelekea katika bandari ya Malindi Zanzibar ikitokea Shanghai Nchini China, iliyotengenezwa na Kampuni ya Damen Shipyard ya Uholanzi.(Picha na Ikulu) 
……………. 

HATIMAE ahadi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein aliyowaahidi wananachi wa Zanzibar kuwa Serikali anayoiongoza itanunua meli mpya ya mafuta MT MKOMBOZI II leo imetimia baada ya meli hiyo kuwasili katika Bandari ya Zanzibar ikitokea Shanghai nchini China. 

Rais Dk. Shein akiwa Ofisini kwake Ikulu mjini Zanzibar alipata fursa ya kuiona meli ya MT MKOMBOZI II ikiwasili kutoka ukingoni mwa pwani ya Zanzibar ikitokea usawa wa kisiwa cha Chumbe na kuelekea katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja ilipokwenda kutia nanga. 

Akiwa katika varanda ya jengo la Ikulu mjini Zanzibar Rais Dk. Shein alionekana akiwa na furaha kubwa wakati akiiangalia meli hiyo ikiwasili ikiwa ni kutokana na ahadi aliyoitoa na azma yake juu ya ujio wa meli hiyo mpya ya mafuta. 

Meli hiyo iliyotengenezwa na Kampuni ya Damen Shipyard ya nchini Uholanzi iliwasili rasmi katika Bandari ya Malindi Zanzibar majira ya saa saa tano za asubuhi na kupata mapokezi ya aina yake.

MZEE JENGUA AWAOMBA WASANII KUBORESHA SOKO LA FILAMU ,AKANA KUSHUKA KWA SOKO

$
0
0

Na.Khadija seif, Michuzi tv

MKONGWE wa Tasnia ya filamu Mohammed Fungafunga a.k.a Jengua aamrekana wazi wazi kushuka kwa soko la filamu nchini..

Jengua amesema soko bado lipo ila linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo swala la filamu kubeba dhima moja inajirudia mara kwa mara ya Mapenzi na kutoleta utofauti katika utunzi wa kazi za Sanaa.

" Wasanii wazuri wapo na kazi za sanaa zipo zinafanya vizuri kutokana na kupata wadau wapya wanaipeleka tasnia hi kimataifa Kama kuwepo kwa tuzo za sinema zetu pamoja na tuzo mbalimbali zinazotambua mchango wa tasnia ya filamu,"

Aidha, ameeleza kuwa ili tufike mbali ni lazima soko liboreshwe kuanzia kuboreshwa kwa uvaaji wa uhusika (acting) pamoja na utungaji wa miongozo (script) pamoja kuhariri picha jongefu.

Pia amesema ni wakati wa wasanii kujitambua na kuiheshimu tasnia ya filamu kwani walikuepo waasisi ambao ndio waliofanya baadhi ya wasanii wasasa kufata nyayo zao.

"Mama Ambiliki,Mzee pwagu,kipara wametangulia mbele ya haki lakini ni baadhi ya watu ambao waliheshimu Sanaa hii na kutupa hamasa wakina sisi kuingia kwenye kazi hiyo,"

Jengua amewataka wasanii chipukizi na waliobobea kuacha kujiona kwani imekua ngumu kwao wakongwe wa tasnia hi hasa wazee kutoa maarifa au kutoa ushauri katika kutengeneza kitu kizuri kutokana na kuonekana hawana jipya kwa sasa.

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI APATA KITABU KINACHOONESHA MADINI YAPATIKANAYO NCHINI.

$
0
0

Leo tarehe Augusti 7, 2019 , Dr Hassan Abbas ambaye ni msemaji Mkuu wa serikali ya Jamhuri wa Muungano Tanzania atembelea Banda la *GST* katika wiki ya Maonesho ya Mkutano Mkuu wa 39 wa  *SADC* kwa lengo la kupata taarifa mbalimbali za kitaalam juu ya Madini na Miamba iliyopo nchini.

Kitabu hicho ambacho ni toleo jipya  kinachoonesha Madini kuanzia ngazi ya Wilaya , kata na Kijiji kimeainisha Zaidi ya madini 220.

Akiambatana na jopo la waandishi wa Habari , Dr.Hassan alipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Mtaalam Mhandisi Priscuss Kaspana hususani katika sekta ya Madini ya viwanda yaani Industrial Minerals.

Sambamba na taarifa hizo Dr.Hassan kwa niaba ya serikali alipata zawadi ya kitabu Cha Madini Yapatikanayo Tanzania toleo jipya.

WAZIRI MPINA ASHANGAZWA NA UWEPO WA CHAMA CHA WAVUVI NGAZI YA TAIFA BILA WIZARA YAKE KUWA NA TAARIFA

$
0
0
Na. Edward Kondela.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina ameitaka Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini kukaa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kupitia kwa pamoja taratibu za usajili wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Wavuvi nchini (CHAKUWATA) ambao hautambuliki katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilhali kinafanya kazi na wavuvi.

Waziri Mpina amesema hayo leo (07.08.2019) katika Maonesho ya wakulima, wafugaji na wavuvi nchini (Nanenane) kwenye viwanja vya Nyakabindi katika Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo na kukuta uwepo wa chama hicho CHAKUWATA na kushangazwa kwa kuwa kinajishughulisha na wavuvi bila Wizara ya Mifugo na Uvuvi yenye dhamana na wavuvi kufahamu uwepo wake ambapo hakuridhishwa na sababu zilizotolewa na Naibu Mrajis Uhamasishaji kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini Bw. Charles Malunde juu ya uhalali wa CHAKUWATA.

“Mpaka chama kinasajiliwa wizara haijui, lazima wizara ihusishwe katika hatua zote sasa kama katibu anayehusika na uvuvi hajui, mimi waziri sijui yaani hapa ndiyo tunashangaa kuna Chama Kikuu cha Ushirika wa Wavuvi Tanzania (CHAKUWATA). Sasa kwa sababu mmeshalifikisha hapa nia ya kuanzisha ushirika ni nzuri ibaki palepale lakini nyinyi (Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini) mkae muone namna bora kama kuna vitu havikufuatwa vikamilishwe kwa ukamilifu kwa sababu kuanzishwa huko bado hautuzuii kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza huko nyuma.” Amesema Waziri Mpina

Akitembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho hayo Waziri Mpina amesema ameridhishwa na umati wa watu unaofika katika banda hilo ili kupata elimu na kusema nia ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ni kuwafikia wadau ili kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika sekta za mifugo na uvuvi.

“Tunataka tuwahakikishie zile changamoto ambazo wametuwasilishia hapa tunaenda kuzifanyia kazi ili kuhakikisha tunapokutana mwaka mwingine wa Maonesho ya Nanenane zitakuwa zimesharekebishwa ili mwaka unaofuata wawe mashahidi kwa kushuhudia mageuzi makubwa ambayo yatakuwa yamefanyika.” Amefafanunua Waziri Mpina

Amefafanua kuwa baadhi ya changamoto kubwa ambazo amekutana nazo ni upungufu mkubwa wa chakula cha samaki na mifugo ambapo amesema anawahakikishia wadau katika sekta za mifugo na uvuvi katika kipindi kinachofuata Wizara ya Mifugo na Uvuvi itapanga mikakati madhubuti kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa.

Kuhusu masoko ya bidhaa mbalimbali zinazotokana na mifugo ambazo amezishuhudia kwenye Maonesho ya Nanenane Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amesema wizara itahakikisha wadau wake wanatafutiwa soko la uhakika ili waweze kuuza mazao yao pamoja na bidhaa zinazotokana na mazao ya mifugo.

Akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na watendaji wa taasisi zilizo chini ya wizara ambao wanashiriki katika Maonesho ya Nanenane kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu, Waziri Mpina amesema ameridhishwa na namna wananchi wanavyohudumiwa kwa kupatiwa elimu na ufahamu juu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kesho (08.08.2019) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha maadhimisho ya Maonesho ya Nanenane kitaifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi vilivyopo katika Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.

Mloganzila Kufungua Benki za Maziwa ya Mama kwa Ajili ya Watoto Wachanga

$
0
0
Mtaalam wa lishe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Bi. Theresia Thomas akiwafundisha wazazi umuhimu wa unyonyeshaji na uandaaji wa chakula cha watoto kuanzia miezi sita mpaka miaka miwili katika maadhimisho ya siku ya unyonyeshaji duniani ambayo huadhimishwa tarehe 1 hadi 7 Agosti, kila mwaka. 
Mtaalam wa lishe Bi. Prisca Emmanuel (kulia) akimpima hali ya lishe mtoto Brightness Temba, aliyembeba mtoto ni Bw. Emily Temba. 
Mtaalam wa lishe Bi. Arafa Mkumbo akimpima uzito na urefu mtoto Aria Madari ili kujua hali yake ya lishe ikiwa ni maadhimisho ya siku ya unyonyeshaji duniani ambapo Hospitali ya Mloganzila imetoa bure huduma ya upimaji wa hali ya lishe kwa watoto chini ya miaka mitano, ushauri wa lishe, miongozo ya uandaaji wa chakula cha watoto pamoja na elimu ya umuhimu wa unyonyeshaji kwa watu wote. 
Baadhi ya wazazi ambao wamejitokeza leo kwa ajili ya kupata huduma ya upimaji wa hali ya lishe kwa watoto chini ya miaka mitano, ushauri wa lishe, miongozo ya uandaaji wa chakula cha watoto pamoja na elimu ya umuhimu wa unyonyeshaji. 

……………………….. 
Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mloganzila inatarajia kufungua benki za maziwa ya mama kwa lengo la kusisitiza umuhimu wa kuwapatia watoto wachanga maziwa ya mama ambayo ni chakula bora na salama. 
Hivyo kina mama watakojifungua katika Hospitali ya Muhimbili watahimizwa kutoa maziwa yao ambayo yatatunzwa na kutumiwa na watoto wachanga wote waliozaliwa kwa wakati huo wakiwemo watoto ambao mama zao wamefariki au mama hatoi maziwa. 

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru wakati akizungumzia kuhusu maadhimisho ya siku ya unyonyeshaji duniani ambapo Hospitali ya Mloganzila imetoa bure huduma ya upimaji wa hali ya lishe kwa watoto chini ya miaka mitano, ushauri wa lishe, miongozo ya uandaaji wa chakula cha watoto pamoja na elimu ya umuhimu wa unyonyeshaji kwa watu wote. 

Amesema nia ya serikali ni kwamba zitakapofunguliwa benki za maziwa Muhimbili baadaye huduma hiyo itaenea nchi nzima ambapo hospitali mbambali nazo zitatakiwa zifungue benki hizo kwa ajili ya kuwapatia maziwa ya mama watoto wachanga waliopo hospitalini. 

“Tunaamini katika hili pia mama aliyeko nyumbani endapo anashughuli zake anaweza kutoa maziwa yake akayaweka muda ukifika wa kunyonyesha mtoto atanyonyeshwa na yule aliyepo huku mama akiendelea na shughuli nyingine” amesema Prof. Museru. 

Baadhi ya faida za unyonyeshaji ni, maziwa ya mama yana maji na virutubisho vyote muhimu hivyo husaidia mtoto kukua vizuri mwili na akili, huimarisha kinga ya mwili wa mtoto na kumkinga dhidi ya magonjwa pia maziwa ya mama ni safi, salama na yana joo linalofaa. 

Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yalianza mwaka 1992 mpaka sasa takribani nchi 120 ni wafuasi wa siku hii duniani ambapo, huadhimishwa kwa lengo la kuhamasisha, kulinda na kuwezesha unyonyeshaji wa watoto ndani ya saa moja anapozaliwa mpaka miaka miwili ili kufanya ukuaji bora na wenye tija.

VIONGOZI WA SADC TANZANIA NI NYUMBANI KWAO- DKT ABBASI

$
0
0



Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi akifafanua jambo kuhusu
Mkutano Mkuu wa SADC katika kipindi cha 360 cha Clouds TV kilichofanyika
kwenye banda la maonesho ya wiki ya viwanda yanayoendelea katika Kituo cha Mkutano cha Kimataifa Julius Nyere, Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Watangazaji kutoka Clouds TV, Sam Sasari na Baby Kabaye. 
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi(kulia) akifafanua jambo
kuhusu Mkutano Mkuu wa SADC katika kipindi cha 360 cha Clouds TV
kilichofanyika kwenye banda la maonesho ya wiki ya viwanda yanayoendelea  katika Kituo cha Mkutano cha Kimataifa Julius Nyere, Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam kushoto kwake ni mtangazaji kutoka Clouds TV, Sam Sasari. (Picha na Idara ya Habari-MAELEZO) 

************* 



Na Pascal Dotto-Maelezo

Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Hassan Abbasi amesema kuwa Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika- SADC kwa viongozi Tanzania ni nyumbani. 

Akizungumza katika Kipindi cha 360 cha Clouds TV, Dkt. Abbasi amesema kuwa Tanzania ina historia kubwa kwa nchi za kusini mwa Afrika tokea enzi za ukombozi wa nchi hizo, ambapo Tanzania ilitumika kama kitovu cha wapigania uhuru. 

“Viongozi hawa wengi wanarudi nyumbani, ikumbukwe kuwa Tanzania ndiyo ilikuwa moja kati ya mataifa matatu yaliyoasisi kamati ya Ukombozi ya Nchi za Kusini mwa Afrika, Tanzania ndiyo ilikuwa Makao Makuu ya ukombozi na Ofisi Kuu ya ukombozi ipo Jijini Dar es Salaam, kwa hiyo hii ni hitoria kubwa kwa nchi yetu”, Dkt.Abbasi. 

Dkt.Abbasi amesema kuwa Mkutano huu ambao ni fursa kwa watanzania maandalizi yake yamekamilika na sasa Tanzania ipo tayari kuwakaribisha wageni kutoka nchi wanachama wa SADC, huku baadhi ya mambo yakikamilishwa na kamati ya maandalizi kutoka SADC, Serikali ya Tanzania, wabia wa SADC pamoja na Sekta binafsi. 

Aidha, Dkt. Abbasi amesema kuwa nchi za SADC zimekuwa na ajenda kubwa ya
kutekeleza ujenzi na kuimarisha viwanda Jambo ambalo alisisitiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli wakati wa ufunguzi wa maonesho ya nne ya wiki ya viwanda ya Nchi wanachama wa SADC. 

“Mhe.Rais Magufuli anaamini kwenye Sera ya Viwanda kama Tanzania tunavyotekeleza Sera hii, siyo kwa Tanzania tu bali hata kwenye nchi wananchama wa SADC. Rais ata sukuma maendeleo ya viwanda kwani atakuwa Mwenyekiti wa SADC, na kama mnavyojua nchi wanachama wanatengeneza ajenda kuhusu ukuaji na uimarishaji wa viwanda”, Dkt.Abbasi. 

Amesema kuwa viwanda ndiyo nguzo ya Maendeleo kwa nchi wanachama na kama Rais Magufuli, alivyosisitiza kuwa Afrika lazima ifanye biashara yenyewe kwa yenyewe badala ya kutegemea kufanya biashara na Nchi za Ulaya. Hivyo, SADC ni fursa kwa nchi wanachama kununua na kuuza bidhaa kwenye jumuia, kama nchi inahitaji mahindi basi Tanzania iuze mahindi yake ndani ya Jumuiya ili kukuza soko. 

Dkt.Abbasi alisema kuwa Rais Magufuli amekuwa ni kiongozi ambaye anasimamia yale anayoyaamini ili kuwaletea Maendeleo wananchi wake kwa hiyo sasa atakwenda kusukuma utekelezaji wa ujenzi wa viwanda kwa nchi wanachama. 

“Kuna mwanahistoria mmoja anaitwa Walter Rodney ambaye aliandika kitabu kushusu namna gani mataifa ya Ulaya yanayadidimiza mataifa ya Afrika, lakini pia unaona siku ile Rais anaongea na kukubaliana na msomi mwingine aliyeandika kuwa namna gani Afrika inajididimiza kwa hiyo msimamo wake utaifanya Tanzania na SADC kutekeleza ujenzi wa viwanda akiwa kama mwenyeketi wa Jumuiya hiyo kwa mwaka mmoja”, Dkt.Abbasi. 

Dkt.Abbasi alisema kuwa nchi za SADC zinatakiwa kuwa na viwanda vya kuchaka malighafi na kuzalisha bidhaa ili kuongeza thamani, akitolea mfano wa mahindi ukiuza bila kuchakatwa hindi moja shilingi 200. Lakini kumbe likiwa limechatwa na kuzalisha unga unaweza ukauza kilo moja kwa shilingi 2,000, kwa hiyo ajenda ya kujenga viwanda vya kuchakata mazao itasimamiwa vema itakuza thamani ya bidhaa ndani na Nje ya Jumuiya. 

Dkt. Abbasi alisema kuwa watanzania wengi sasa wameamka na Serikali ambacho inafanya ni kuwawezesha waamke na kuchangamkia fursa za biashara ndani ya SADC. 

Alitolea mfano kwenye maonesho ya SADC ambayo yanaendelea Jijini Dar es Salaam kuwa wapo watanzania ambao wanaonesha bidhaa zao wanazopeleka SADC. 

“Takwimu zinaonesha watanzania tumeaka sana kwenye soko la SADC, tumepeleka bidhaa zinazofikia dola za kimarekani milioni 900 na tumengiza bidhaa zinazokadiriwa kufikia Dola milioni 600, kwa hiyo sisi bado kitakwimu tumechangamka zaidi kwenye soko la SADC. 

Dkt.Abbasi alisema kuwa Serikali imeweka mikakati kwa Taasisi zinazohusisha masula ya biashara ikiwemo Tantrade na Bodi ya Masoko ya Mazao Mchanganyiko, kuitafuta masoko na kufanya utafiti ili kuwasaidia wafanyabiashara.

OLE NASHA AAGIZA MKANDARASI WA UKARABATI WA SHULE YA SEKONDARI KULIPWA

$
0
0
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Morris Limbe kumlipa fedha Mkandarasi anayekarabati shule ya sekondari Bukoba ili aweze kuendelea na kazi na kukamilisha ukarabati huo kwa wakati

Naibu Waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo mkoani Kagera wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya sekta ya elimu inayotekelezwa mkoani humo, ambapo amesema Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilishapeleka fedha zote za ukarabati huo kiasi cha shilingi bilioni 1.4 lakini mpaka sasa mkandarasi huyu amelipwa kiasi cha shilingi milioni 32 tu.

“Fedha zilishaletwa zote na wizara shilingi bilioni 1.4 lakini mpaka sasa Mzinga wamelipwa shilingi milioni 32 tu kati ya milioni mia mbili na zaidi walizotakiwa kuwa wamelipwa mpaka sasa, hivyo Mkurugenzi wa manispaa dirisha likifunguliwa hakikisha Mzinga wanapata fedha ambazo wanadai” amesisitiza Ole Nasha.

Ole Nasha amesema ukarabati wa shule hiyo unaoendelea umechelewa kukamilika kwani licha ya fedha hizo kupelekwa mapema mkandarasi amechelewa kuanza kufanya ukarabati huo. Hata hivyo amesema kasi ya ujenzi huo si mbaya kutokana na kuanza mwezi wa tano.

Aidha, Ole Nasha amewataka watendaji wa manispaa hiyo kufuatilia kwa ukaribu matumizi ya fedha hizo kwani ni nyingi kutumika kwa ukarabati ukilinganisha na fedha zinazotumika katika miradi mingine, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa fedha kubaki na kutumika katika kufanya shughuli nyingine za kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

“Nikifananisha fedha ambazo tumetumia kwenye maeneo mengine na miradi mingine mfano miradi ya afya ambao wanatumia bilioni 1.5 kujenga hospitali kubwa kwa kujenga majengo mapya makubwa saba lakini sisi hiyo bilioni 1.4 ambayo inakaribiana na bilioni 1.5 ya afya tunakarabati majengo tu, kuna umuhimu wa kuzisimamia fedha hizi kwa ukaribu," alisema Ole Nasha.

Aidha, Naibu Waziri amesema shule hiyo ina nafasi finyu ikilinganishwa na idadi kubwa ya wanafunzi mia saba waliopo na amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo kuwasiliana na Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) ambao wana eneo karibu na shule hiyo washaurine juu ya uwezekano wa kutoa eneo hilo kwa ajili ya upanuzi wa shule hiyo.

Awali Mkuu wa shule ya Sekondari Bukoba, Raymond Mutakyawa, amemweleza Naibu Waziri kuwa ukarabati wa shule hiyo ulikuwa ufanyike kwa siku sabini tano na ulipaswa kuwa umekamilika mwishoni mwa mwezi wa saba lakini ulisimama kutokana na kukosa fedha za kununua vifaa kwa ajili ya kazi hiyo baada ya mfumo wa malipo kufungwa kabla ya fedha hizo kulipwa kwa mkandarasi.

Shule ya Sekondari ya Bukoba inafanyiwa ukarabati na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia baada ya kuharibiwa na tetemeko la ardhi la mwaka 2016 lililoikumba mkoa wa Kagera ambapo baadhi ya kuta za shule hiyo zilianguka na majengo mengine kupata nyufa na baadae paa kuezuliwa na upepo mkali.

Ditopile akabidhi vitendea kazi kwa UVCCM Dar

$
0
0

Charles James, Michuzi TV

Mbunge wa Viti maalum anayewakilisha vijana Mhe Mariam Ditopile amekabidhi vitendea kazi zikiwemo Kompyuta zenye thamani ya Shilingu Milioni mbili pamoja na fedha taslimu Shilingi Laki Sita kwa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar Es Salaam.

Mhe Ditopile amekabidhi vitu hivyo wakati wa ufunguzi was Baraza la Vijana ambapo pia aliwaasa UVCCM kujitokeza hadharani kujibu porojo ambazo zimekua zikielekezwa kwa Chama na Serikali.

Amewataka vijana wa CCM kuyaeneza mazuri ambayo yamekua yakifanywa na Serikali ya Rais Magufuli bila kuona aibu na kuwasihi kusimamia mstari katika kuijenga Tanzania ya viwanda kwa vitendo na siyo maneno.

" Niwasiihi vijana wenzangu kuwa mstari wa mbele kuyasema na kuyatangaza hadharani yale yote yanayofanywa na serikali ya CCM katika kutekeleza ilani yake ya mwaka 2015 ambao ndio msahafu unaotuongoza ndani ya miaka hii mitano.

Na tunaposema tuunge mkono juhudi za Mh Rais Magufuli katika hizi zama za kuchapa kazi kama kauli mbiu yake inavyosema ya hapa kazi tu wananchi nao wajue ni kazi kweli kwa sababu hata sisi vijana tutaonekana kweli tunaitekeleza Ilani kwa kufanya kazi," amesema Mhe Ditopile.

Aidha amewapongeza UVCCM Dar Es Salaam kwa kuwa waasisi wa KIJANI na kuongeza kuwa hivi sasa nchi nzima kampeni hiyo imekua kubwa na imezidi kukiimarisha Chama hicho kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

" Nawapongeza kwa kuwa waasisi wa kampeni ya Kijani ambayo imefanikiwa, ila niwanasihi juhudi hizi kubwa zisiishie kwenye matamasha tu bali ni lazima ziwe chachu ya kuhakikisha ushindi mnono kwa Chama chety katika chaguzi zilizo mbele yetu," amesema Mhe Ditopile.
Mbunge wa Viti Maalum Taifa anayewakilisha vijana, Mhe Mariam Ditopile (katikati) akikabidhi vitendea kazi zikiwemo Kompyuta kwa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam.

KANYASU AZIAGIZA TAASISI ZA UHIFADHI NCHINI KUUNDA VIKOSI MAALUM VYA KUDHIBITI WANYAMAPORI WAKALI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa na Mkuu wa wilaya ya Lindi, Mhe. Shaibu Mgenda akizungumza na baadhi ya watumishi wakati alipofika katika eneo la kupumzikia watalii katika Msitu wa mazingira asilia wa Rondo ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya kutembelea msitu huo kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili watumishi pamoja na wananchi wanaoishi karibu na Hifadhi hiyo iliyopo katika wilaya ya Lindi mkoani Lindi. Wa kwanza kushoto mbele ni Mkuu wa HIfadhi ya Rondo, Richard Tarimo
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye mti wa Mwl. Julius Nyerere ambapo miaka ya 1970 alipofika katika katika kijiji cha Rondo hilo aliomba apelekwe katika eneo unakopatikana mti huo ambapo baada ya kufika alichukua gome la mti huo uitwao Mkufi na kisha akaondoka na gome ;a mti huo licha ya kuwa haijulikani alikwenda kulifafanyia nini gome hilo la mti huo ambao umekuwa kivutio kikubwa cha utalii na watu wengi kutoka maeneo mbalimbali nchini wamekuwa wakienda katika mti huo na kubandua magome yake na kisha kuondoka nayo.
(PICHA NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)






Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya watumishi kabla ya kutembelea Hifadhi ya msitu wa Mazingira asilia wa Rondo pamoja na Shamba la miti la Rondo inayoosimamiwa na Wakala wa Hudum za Misitu Tanzania (TFS) ikiwa ni ziara ya kikazi katika wilaya ya Lindi mkoani Lindi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya watumishi mara baada ya kutembelea Hifadhi ya msitu asilia wa Rondo unaosimamiwa na Wakala wa Hudum za Misitu Tanzania (TFS) ambao mara baada ya kuhifadhiwa ambao umekuwa na wanyamapori wakali kama vile tembeo na simba ambao wamekuwa wakivamia mashamba na kujeruhi wananchi mkoani Lindi, Wa kwanza ni Mkuu wa HIfadhi ya Rondo, Richard Tarimo


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya watumishi wakati alipofika katika eneo ambalo tembo wanaotokea katika Hifadhi ya Mazingira asilia ya Msitu wa Rondo ambao wamekuwa wakivunja miti iliyopandwa kwenye shamba Rondo ambao baadhi ya miti hiyo imeshindwa kukua ipasavyo baada miti hiyo kuvunjwa mara kwa mara
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akisalimiana baadhi ya watumishi wakati alipofika katika ofis za Hifadhi ya Mazingira asilia ya Msitu na Msitu wa Kupandwa wa Rondo ambapo amewaagiza watumishi wa Rondo wafanye kazi kwa maarifa na weledi wa hali ya juu.
………………….
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameagiza kila Taasisi ya Uhifadhi nchini ihakikishe inaunda kikosi maalum cha askari wanyamapori watakaokuwa wakitumika kudhibiti wanyama wakali na waharibifu pindi wanapovamia makazi ya wananchi badala ya kutegemea kikosi kimoja p cha Askari kutoka Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU)

Agizo hilo amelitoa jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa Shamba la miti la Rondo ikiwa ni ziara yake ya kikazi katika mkoa wa Lindi.

Akizungumza na watumishi hao, Mhe.Kanyasu amesema kutokana na Serikali kudhibiti ujangili kwa kiasi kikubwa wanyamapori kama vile tembo, chui na simba wamekuwa wakitembea kila mahali kwa sababu hawana hofu ya kuuliwa kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.

Amesema hali hiyo imepelekea mazao pamoja na maisha ya wananchi kuwa hatarini hasa kwa wananchi wanaoishi karibu na Hifadhi.

Amesema licha ya wanyamapori hao kuongezeka ikiwa moja ya sababu ni Serikali kuzuia kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi wanyama hao wamekuwa wakipita njia zao za asili ambazo tayari zimevamiwa na hivyo kusababisha matatizo makubwa kwa wananchi.

Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu ameitaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Hifadhi za Taifa( TANAPA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) ziwe na vikosi maalum vya askari watakaotumika kukabiliana na wanyamapori hao wakati wanapovamia vijiji.

” Kwa sasa kukutana na kundi la tembo zaidi ya 500 katika miji ya Butiama, Dodoma pamoja Morogoro ni jambo la kawaida, Hatuwezi kutegemea KDU pekee lazima nguvu iongezwe” alisema Mhe.Kanyasu.Amesema TFS ihakikishe inakuwa kikosi hicho cha Askari katika Hifadhi za Mazingira Asilia ambako kuna wanyamapori wakali ma waharibifu wakiwemo tembo na viboko, simba na chui.

Amesema kwa sasa Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa ikipokea maombi mengi kwa siku kutoka kwa wananchi walioathiriwa na wanyamapori wakali na waharibifu.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu ametoa pole kwa wananchi wa Kijiji cha Rondo kufuatia kifo cha kumpoteza Mwalimu wa shule ya msingi pekee katika kijiji hicho aliyekufa baada ya kuuliwa na tembo baada ya kumpiga picha tembo aliyekuwa akihangaika kumnasua mtoto wake aliyekuwa amenaswa kwenye kichaka.

Aidha, Mhe.Kanyasu amezitaka Halmashauri nchini zinazopakana na Hifadhi zihakikishe zinaajiri askari Wanyamapori watakaokuwa wakisaidia kutoa msaada wa haraka pindi wanyamapori hao wanapovamia vijiji

Pia, Amezitaka Halmashauri ziangalie uwezekano wa kuwatumia askari wanyamapori wa vijiji (VGS) kwa kuandaa utaratibu maalum wa kuwakabidhi silaha pindi wanyamapori wanapovamia mashamba na makazi ya wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Mgenda amesema kutokana na juhudi za uhifadhi unaofanywa na Mkoa huo umechangia wanyamapori kuongezeka na kuwa huru kutembea kila mahali

Kufuatia na hali hiyo, Mhe. amemuomba Naibu Waziri huyo ahakikishe Taasisi zake za Uhifadhi nchini zunatoa elimu kwa wananchi ili waweze kujihami wakati wanyamapori hao wanavamia mali na makazi yao.

Dkt.ABBASI ALIVYOTEMBELEA MAONESHO YA VIWANDA -SADC

$
0
0
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akipata maeleo kutoka kwa
Meneja Masoko na Uhusiano wa Benki ya Maendeleo (TIB), Saidi Mkabakuli
alipotembelea banda la Taasisi hiyo kwenye katika maonesho ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam, katika ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Konnectt Wire Sheila Mwapachu.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akisoma kipeperushi cha Benki ya TIB, alipotembelea banda la Taasisi hiyo kwenye katika maonesho ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam, wengine ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Konnectt Wire Sheila Mwapachu na Meneja Masoko na Uhusiano wa Benki ya Maendeleo (TIB), Saidi Mkabakuli.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akifafanua Jambo mbele ya
wafanyakazi wa Kampuni ya Tanzanitie Founder Foundation, kuhusu kuyatangaza madini ya Tanzanite alipotembelea kwenye Banda hilo katika Maonesho ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC, yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akisoma kipeperushi cha badhaa inayozalishwa nan a kampuni ya ushonaji Malika Designer alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Mmiliki wa Kampuni hiyo Malika Rashidi.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akipokea kitabu kinachohusu
utafiti na Uchenjuaji Madini kutoka kwa Mhandisi Mchenjuaji Madini Mwandamizi,Priscus Kaspana alipotembelea Banda la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini–Tanzania katika maonesho ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akiwa kwenye picha ya pamojana Wafanyakazi wa Wakala wa Vipimo, Ukaguzi wa Bidhaa Zilizofungashwaalipotembelea banda la Taasisi hiyo katika maonesho ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Ukanda wa Uzalishaji wa Mauzo ya Nje(EPZA),George Karumuna na Zubeda Elias, wakimsikiliza Msemaji Mkuu wa Serikali,Dkt.Hassan Abbasi, alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Wiki ya Viwandakutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC yanayoendelea katika Kituo chaMikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akiangalia moja ya bidhaa yakorosho inayozalishwa hapa nchini na Kampuni ya Tan Korosho alipotembelea Banda la Mkuu Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), katika maonesho ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bw.Edwin Rutegaruka.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akipata maelezo kutoka kwa
Ben Mwanantala wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kuhusu ujenzi na ufanyaji kazi wa reli ya kisasa(SGR) alipotembelea Banda la TRC katika maonesho ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akipeana mkono na Ben
Mwanantala wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), mara baada ya kupata maelezo kuhusu ujenzi na ufanyaji kazi wa reli ya kisasa(SGR) alipotembelea Banda la TRC katika maonesho ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam.(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images