Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

DKT. MABODI AWAONYA WANACCM WANAOTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi,amewataka Viongozi wa CCM kutumia Vikao halali vya Kikatiba na Wazee wa Taasisi hiyo kutafuta ufumbuzi wa changamoto hasa tuhuma za kisiasa badala ya kutumia Mitandao ya Kijamii.

Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Dimani,uliofanyika katika Ofisi ya CCM iliyopo Mbweni Unguja.

Dk.Mabodi alisema kila Mwanachama ndani ya CCM ana Haki na Wajibu wa kutumia miongozo na kanuni ya kikatiba kutafuta ufumbuzi wa changamoto yoyote inayomkabili kisiasa na sio kutumia majukwaa mengine yasiyokuwa rasmi.

Alieleza kwamba ni kosa kimaadili jambo lolote linalogusa maslahi ya Chama Cha Mapinduzi kulijadili na kulitolea maamuzi kinyume na utaratibu uliowekwa na miongozo ya Chama.

Kupitia Kikao hicho Naibu Katibu Mkuu huyo, alisema kiongozi,Mtendaji na Mwanachama yeyote mwenye malalamiko juu ya mwenzake anatakiwa kufuata tararibu zilizowekwa kuanzia ngazi za Mashina hadi Taifa.

“Nakemea tabia ya baadhi ya Wanachama na Viongozi kutumia Mitandao ya Kijamii kuchafuana kisiasa sio utaratibu wa CCM, na yeyote tutakayembaini kufanya hivyo basi tutamchukulia hatua za Kimaadili kwa mujibu wa Miongozo yetu.”, alisema Dk.Mabodi.

Pamoja na hayo aliwakumbusha Wajumbe wa Mkutano huo kuwa ni marufuku kwa Mwanachama yeyote kufanya kazi ya udalali wa kisiasa wa kuwapigia kampeni za kuwania Uongozi wa ngazi yeyote baadhi ya Makada mwaka 2020 kabla ya kampeni hizo kuruhusiwa kikatiba.

Aliwapongeza Viongozi wa Wilaya hiyo kwa kufanya kikao hicho kinachowaunganisha Wanachama na Utendaji wao katika kuandaa mazingira ya Ushindi wa CCM kwa mujibu wa Ibara ya Tano ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977.

Aliwataka Wabunge,Wawakilishi na Madiwani kuendelea kutekeleza Ilani ya CCM katika maeneo yao ili Wananchi wanufaike na huduma bora za maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Ndugu Mohamed Rajab Soud, aliwataka Wanachama wa CCM kuungana pamoja katika kuandaa ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao na kubadilika kitabia kwa kutofanya kazi kwa mazoea.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Dk.Abdulla Juma Mabodi akizungumza katika Kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Dimani huko Mbweni Unguja.
WAJUMBE wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Dimani wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi.

MKUU WA MKOA WA SIMIYU APOKEA MSAADA WA BAISKELI ZA WALEMAVU 48

$
0
0
Mmoja wa watoto wenye ulemavu akisaidiwa kuwekwa kwenye moja ya baiskeli 48 zilizotolewa kwa pamoja kati ya kampuni ya Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL) na taasisi ya Wheelchair Foundation ya Marekani zenye thamani ya Sh 20 milioni katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu. 

Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Anthony Mtaka akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa baiskeli 48 za watu wenye ulemavu zilizotolewa kwa pamoja kati ya kampuni ya Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL) na taasisi ya Wheelchair Foundation ya Marekani zenye thamani ya Sh 20 milioni katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu. 
Mkurugenzi wa taasisi Wheelchair Foundation,Charli Butterfield akimpa zawadi mmoja wa washindi wa mashindano ya baiskeli kwa watu wenye ulemavu katika kusherekea Jambo Festival kwenye uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu. 

Mkurugenzi wa kampuni ya kitalii ya Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL)akimpa zawadi mmoja wa washindi wa mashindano ya baiskeli kwa watu wenye ulemavu katika kusherekea Jambo Festival kwenye uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu. 
Ngoma za utamaduni wa jamii ya wasukuma huwa ni moja ya kivutio kikubwa wakati wa sherehe za kila mwaka zaJambo Festival wilayani Bariadi. 
Katibu Tawala mkoa wa Simiyu,Jumanne Sagini(kulia) akiwaongoza viongozi kuondoka mara baada ya sherehe zilizoambana na zawadi mbalimbali kwa washiriki kwenye uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi.



Mwandishi Wetu,Bariadi 

Watu wenye ulemavu wa miguu mkoani Simiyu wamenufaika kwa kupata msaada wa baiskeli zitakazowawezesha kutoka sehemu moja kwenda nyingine bila vikwazo baada ya shirika la Wheelchair Foundation la nchini Marekani na Friedkin Conservation Fund (FCF) kutoa baiskeli 48 zenye thamani ya Sh 20 milioni.

Mkurugenzi wa taasisi ya Wheelchair Foundation ,Charli Butterfield alimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Anthony Mtaka baiskeli hizo alisema zitawasaidia watu wenye ulemavu kujishughulisha na shughuli za maendeleo na kuona wapo watu wanaowajali katika hali waliyonayo.

Alisema taasisi hiyo imekua ikiwajali watu wenye uhitaji wa baiskeli duniani kote kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita na hapa nchini wameshatoa jumla ya baiskeli 2,240 katika mikoa tofauti na wataendelea kufanya hivyo kadiri wasamaria wema wanavyochangia taasisi yao.

Akipokea baiskeli hizo Mkuu wa mkoa huo alisema ni muhimu sana kuwepo na ushirikiano wa kuwafikia wenye ulemavu ambao hawawezi kumudu gharama za kununua baiskeli hizo na kuiomba taasisi hiyo iendelee kusaidia zaidi katika eneo la kuwawezesha watu wenye ulemavu na sekta ya afya na elimu.

Aliongeza kuwa wakati wote serikali ya mkoa inatambua ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya nchi mbili za Marekani na Tanzania na mkoa utaendeleza mahusiano hayo kwa faida ya wananchi wa pande zote mbili katika kuhamasisha maendeleo ya mshikamano.

TAKUKURU Dodoma yabaini vitendo vya rushwa Chemba

$
0
0
Na Charles James, Michuzi TV
TAASISI ya kizuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma imeingilia kati ujenzi wa mradi wa maji wa Kijiji cha Kelema Kuu wilayani Chemba baada ya kubaini thamani ya fedha iliyotumika kutoendana na kazi halisi iliyofanyika.

Aidha mradi huo wenye thamani ya shilingi 222,978,680 ulipaswa kukamilika tangu mwaka 2015.

Hatua hiyo imefanyika ikiwa ni utekelezaji wa moja ya majukumu yake chini ya kifungu cha 7 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ya mwaka 2007.

Hayo yamebainishwa Julai mosi mwaka huu  jijini Dodoma na Mkuu wa TAKUKURU Dodoma Sosthenes Kibwengo wakati akitoa taarifa kwa umma juu ya vitendo vya rushwa katika robo ya mwezi April hadi Juni.

Aidha Kibwengo amesema ,katika uchunguzi huo ilibainika kuwa thamani ya fedha haikupatikana kutokana na uwepo wa malipo zidifu ya kazi halisi zilizofanyika na kutandikwa kwa aina ya mabomba kinyume na mkataba hivyo kusababisha mradi huo kutokutoa maji.

"Baada ya TAKUKURU kuingilia kati ,mkandarasi wa mradi huo JUIN COMPANY LIMITED ameridhia kurekebisha mapungufu yaliyobainika na leo hulali mosi anaanza kazi ya kubadili mabomba na kuweka yanayostahili,"alisema.

Pamoja na hayo amesema Mkandarasi huyu atarejesha malipo zidifu yaliyolipwa bila kustahili .

"Jumla ya shilingi 67,542,600/= zimeokolewa na tunatarajia wananchi watapata huduma ya maji ,"alisema Kibwengo.

Katika hatua nyingine taasisi hiyo imemkamata Be.Gaston Meltus Francis ambaye ni mkurugenzi wa Global Space East Afrika Limited iliyopewa kazi ya ujenzi wa kituo cha afya Mima wilayani Mpwapwa ambapo kampuni yake ililipwa kiasi cha shilingi 86,405,205 isivyo halali kwa kazi ambazo hazikufanyika katika mradi huo.

Kwa mujibu wa mkuu wa TAKUKURU Dodoma ,uchunguzi huo umeokoa na kurejesha Serikalini jumla ya shilingi 11,877,353 /=zilizolipwa kinyume na taratibu Kama mshahara kwenye akaunti ya benki ya mwalimu aliyefariki.

Aidha kufuatia matukio hayo , TAKUKURU mkoa wa Dodoma inawataka wananchi wote kuendelea kutoa ushirikiano na kuwaomba wasiwe watazaji bali washiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa.

"Tunawataka wanajamii kuwa waangalifu na kamwe wasikubali kurubuniwa na matapeli wanaojifanya maofisa wa TAKUKURU wanaowapigia simu na kuwatisha bali watoe taarifa kupitia namba 113 au kufika katika Ofisi zetu,"alisema Kibwengo.
Kamanda wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo, akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma.

TTCL YASAMBAZA HUDUMA YA MAWASILIANO KWA VIONGOZI

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Akabidhiwa Simu ya TTCL na Mkurugenzi Mkuu wa Shrika la Simu Tanzania (TTCL), Bwana Waziri Kindamba.leo Julai /1/2019 Jijini Dar es salaam ,wanao shuhudia kushoto kwa Waziri Mkuu. ni Meneja wa TTCL Mkoa wa Kinondoni Bibi Janeth Maeda. na kulia mwisho ni Meneja Huduma wa TTCL Kinondoni Bwana Salim Msalilwa. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

BALOZI SEIF AONGOZA DUA YA HITMA YA DKT. BADRIYA

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, ameongoza Kisomo cha Hitma ya Mke wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi Marehemu Dk.Badriya Abubakar Gurnah kilichofanyika katika Msikiti wa Mwushawal uliopo Mwembe Shauri Unguja.

Kisomo hicho kimeudhuriwa na Waumini wa Dini ya Kiislamu,Viongozi wa Dini,Kiserikali na Chama Cha Mapinduzi pamoja na Wananchi kwa ujumla.

Akitoa Mawaidha Sheikh Norman Jongo, amewasihi Waumini hao kuendelea kumuombea dua mara kwa mara Marehemu Dk.Badriya ili awe miongoni mwa Waja Wema katika Pepo ya Mwenyezi Mungu.

Akitoa shukrani Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi, amewashukru Wananchi walioshiriki katika kisomo hicho na harakati zingine za kumsaidia Dk.Badriya Enzi za Uhai wake.

Sambamba na hayo pia amewashukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Joseph Magufuli kwa mchango walioutoa kabla na baada ya Kifo cha Dk.Badriya.

Wakati huo huo Wananchi,Viongozi wa Dini ya kiislamu, Kiserikali na Chama cha Mapinduzi kwa upande wa Wanawake nao wameshiriki kisomo hicho cha Hitma ya Dk.Badriya Abubakar hapo Nyumbani kwa Dk.Mabodi  Mtaa wa Raha leo Unguja.

Mwenyezi Mungu amlaze mahala Pema Peponi Amin.

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd,akiongoza Kisomo cha Hitma ya Marehemu Dk.Badriya Abubakar Gurnah aliyekuwa Mke wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi, kilichofanyika katika Msikiti wa Mwushawal Mwembe Shauri Unguja.
WAUMINI mbali mbali wa Dini ya Kiislamu wakishiriki Kisomo cha Hitma ya Marehemu Dk.Badriya Abubakar Gurnah, kilichofanyika katika Msikiti wa Mwushawal Mwembe Shauri Unguja.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi, akiwashukru Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwemo Viongozi wa Dini,Serikali,Chama Cha Mapinduzi na Wananchi wote walioshiriki Kisomo cha Hitma ya Mkewe Marehemu Dk.Badriya Abubakar kilichofanyika Msikiti wa Mwushawal Mwembe Shauri Unguja.
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Idd, akijumuika na Wananchi katika kisomo cha Hitma ya Marehemu Badriya Abubakar kilichofanyika kwa upande wa Wanawake Nyumbani kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi, Rahaleo Unguja.

KAIMU MKURUGENZI WA HUDUMA ZA TUME AFANYA ZIARA KWENYE BANDA LA TUME YA MADINI KATIKA MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tume amefanya ziara kwenye Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba kwa mwaka 2019 yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Taasisi za Serikali zinazoshiriki katika banda la Tume ya Madini ni pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Masuala ya Madini na Gesi Asilia (TEITI).
 Kampuni za madini zinazoshiriki katika Banda la Tume ya Madini ni pamoja na Williamson Diamonds Limited, Shanta Mining  Co. Limited, Geita Gold Mining Limited, TANSHEQ, Marmo & Granito Mines (T) Limited na Afro Gems Limited

NSSF NA PSSSF WASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA SABASABA KWA PAMOJA

$
0
0
Maonesho hayo yameanza tarehe 28/06/2019 na yatamalizika tarehe 13/06/2019. Wanachama wa mifuko yote miwili wanaalikwa kuja kupata huduma mbalimbali katika banda namba 13.

NSSF na PSSSF wanashiriki kwa pamoja katika maonesho hayo ili kuweza kutoa huduma ya Hifadhi ya jamii ambapo NSSF inawahudumia wananchi kutoka sekta binafsi na sekta isiyokuwa rasmi na kwa upande wa PSSSF wanawahudumia wanawahudumia watumishi wa umma.

Wanachama pamoja na wadau wa Mifuko hiyo wanatakiwa kutumia fursa hiyo kutembelea banda katika viwanja vya sabasaba

Mabadiliko ya mwaka 2018 katika sekta ya Hifadhi ya jamii yalifuta ushindani katika sekta hiyo. Hivyo wananchi wanaandikishwa kwenye mifuko hiyo kulingana na sekta waliopo.
Meneja KIongozi wa Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF Bi Lulu Mengele akitoa elimu kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na NSSF katika banda la NSSF na PSSSF katika maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.
Afisa Uhusuano wa NSSF Bi Aisha Sango akitoa ufafanuzi kwa mgeni alietembelea banda la NSSF na PSSSF katika maonesho yanayoendelea ya kimataifa ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.
Meneja KIongozi wa Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF Bi Lulu Mengele akitoa elimu kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na NSSF katika banda la NSSF na PSSSF katika maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.
Afisa matekelezo wa NSSF Ndugu Abdulaziz Abeid akitoa ufafanuzi kwa mgeni alietembelea banda la NSSF na PSSSF katika maonesho yanayoendelea ya kimataifa ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.
Maafisa Uhusiano wa NSSF (Aisha Sango, Kushoto na Amani Marcel, Katikati) na wa PSSSF (Coleta Mnyamani) wakitoa elimu kwa wageni mbalimbali kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mifuko hiyo katika maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.
Afisa Uhusuano wa PSSSF ndugu Abdul Njaidi akitoa ufafanuzi kwa mgeni alietembelea banda la NSSF na PSSSF katika maonesho yanayoendelea ya kimataifa ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa

WATU WAWILI WAMEUAWA KATIKA MATUKIO TOFAUTI YA MAUAJI MKOANI PWANI-WANKYO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
WATU wawili wamefariki dunia mkoani Pwani, kutokana na matukio tofauti ya mauaji yaliyotokea wilaya ya kipolisi Chalinze, ikiwa ni pamoja na Damian Kimiti (70) ambae ameuawa kwa kupigwa shoka. Kufuatia mauaji hayo watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapo.

Akielezea kuhusiana na matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani hapo, kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa alisema Kimiti aliuawa huko Malivundo, Talawanda, Chalinze, ambapo mtiliwa shaka Said Ngosha amekubali kuuwa na tayari amekamatwa .

Alisema, baada ya mauaji muaji alipora simu tatu aina ya tecno ,solar panel moja,shuka na baiskeli. "Pia alikubali kuonyesha simu tecno mbili ,solar panel moja na shoka moja"alifafanua Wankyo.

Katika tukio jingine ,Wankyo alieleza Ngurai Waziri (33) mfugaji huko Msolwa kijiji cha Lukenge aliuawa kwa kukatwa na visu.

Kamanda huyo alibainisha, mtiliwa shaka David Mwanje (28) , Thomas Gau (25) na Magoma Ramadhani Mbwiga (32) wamekamatwa na katika mahojiano ya awali watuhumiwa hao wamedai marehemu alikuwa mwizi wa mifugo na alikuwa kero katika wizi wa mifugo.

Wakati huo huo Wankyo alisema, juni 30 eneo la Sweat Corner Vigwaza katika barabara kuu ya Morogoro -Dar es salaam ,gari lenye namba za usajili T.182 DGH/T .182 DGM aina ya scania ,lililokuwa likitokea Iringa kuelekea Dar es salaam likiendeshwa na dereva Samwel Emanuel mkazi wa Makambako Iringa.

"Gari hilo liligongana uso kwa uso na gari lenye namba za usajili T.420 CGK/T.909 BZU scania lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Chalinze likiendeshwa na Iddi Rashid mkazi wa Tegeta ikiwa imebeba malighafi zitumikazo kutengeneza juice na kusababisha moto mkubwa na magari yote yaliteketea."aliongeza Wankyo.

Wankyo alitaja chanzo cha ajali ni gari lenye namba T.420 CGK aina ya scania kuhama upande wake na kuhamia upande wa kulia mwa barabara.

UCHUNGUZI WA AWAMU YA PILI YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WANAWAKE WAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
Na Kijakazi Abdalla Maelezo 
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed amesema kuwa kuwepo kwa zoezi la uchunguzi wa saratani ya kishingo ya kizazi ni kuweza kupata takwimu sahihi ya kujua wanaosumbuliwa na maradhi hayo hapa Zanzibar.

Hayo ameyasema huko katika Hospitali ya Mnazi mmoja wakati akiangalia zoezi zima la uchunguzi wa saratani wa shingo ya kizazi kwa wanawake.

Amesema kuwa kwa hivi sasa idadi kamili bado haijulikani kwa wanaousumbuliwa na maradhi hayo jambo linaifanya kuweza kutoa takwimu sahihi na hata maeneo gani yaliaathirika na maradhi hayo.

Aidha alisema kuwa kupata takwimu sahihi pia kutawezesha Wizara ya Afya kuengeza bajeti ya tiba ili kuweza kurahisisha na kupambana na maradhi hayo.

Aidha alisema kuwa maradhi ya saratani ya shingo ya kizazi yanatibika bila ya hata kwenda kwa waganga kwani tiba sahihi ya maradhi hayo yanapatikana katika hospitalini.

Alisema kuwa kinamama walio wengi wamekuwa wanaamini kuwa ugonjwa huo unatokana na kurogwa jambo ambalo sio sahihi hali ambayo inaweza kutowafanya kutofika hospitali kwa ajili ya uchunguzi.

“Kinamama wengi mnaamini maradhi haya yanatokana na kurogwa na hasa wale wanawake wenye wakewenza kumbe sio sahihi”, alisema Waziri Rashid.

Hata hivyo amewataka kinamama kujitokeza kwa wengi katika vituo vya afya kuchunguza afya zao ili kuweza kujua hali zao mapema jambo ambapo litaweza kuondokana na usumbufu mara wanapobainika wanasumbuliwa na maradhi mbalimbali.

Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikijitahidi kupambana na maradhi mbalimbali hali kwa wananchi wake ili kuweza kupata taifa lenye afya.

Nae Mratibu wa Mradi wa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi kutokana Serikali ya Jamuhuri ya watu wa China QI Xiaomin amesema kuwa zoezi la kufanyia uchunguzi kinamama linafanyika kitaalamu kwa hali ya juu kabisa.

Nae Meneja wa Kitengo cha maradhi yasiyoambikiza Zanzibar Omar Mwalimu Omar amewataka kinamama kuitumia fursa iliyowepo ili kuweza kupatiwa vipimo kwa uhakika.

Hata hivyo alisema uzuri wa kupatiwa vipimo kwa uhakika kutawezesha kinamama kuondokana na kutumia gharama nyingi za matibabu pale wanapobainika na maradhi kama hayo.

Nae Mwakilishi wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Kaskazini Panya Ali Abdalla ambae alishiriki katika zoezi la uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa kuazisha zoezi hili .

Aidha aliwataka kinamama kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili kwani halina malipo wala halina usumbufu kwa wale wanasumbuliwa na ugonjwa huo na tiba yake inapatikana.
 Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika Uchunguzi na Utibabu wa Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake inayofanywa na madaktari Kutoka China Ikiwa ni muendelezo wa awamu ya Pili ya Mradi wa miaka Mitano uliofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kulia ni Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman.
 Mmoja kati ya madaktari kutoka China Hupaohai akifanya uchunguzi wa maradhi ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake Ikiwa ni muendelezo wa awamu ya Pili ya Mradi wa miaka Mitano uliofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
 Baadhi ya Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika Uchunguzi na Utibabu wa Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake inayofanywa na madaktari Kutoka China Ikiwa ni muendelezo wa awamu ya Pili ya Mradi wa miaka Mitano uliofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
 Muakilishi Nafasi za Wanawake Panya Ali Abdalla akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufanyiwa Uchunguzi wa maradhi ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake Ikiwa ni muendelezo wa awamu ya Pili ya Mradi wa miaka Mitano uliofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar. 
 Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed(katikati) na Naibu Waziri wa Afya kushoto yake wakiwa katika Picha ya pamoja na Madaktari Kutoka China waliofika Nchini kwa ajili ya kufanya Uchunguzi na Utibabu wa Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake uliofanyika Hospitali Mnazi Mmoja Zanzibar.
Mmoja kati ya madaktari wanaoshirikiana na Madaktari kutoka China Faiza Habibu (kushoto)akimfanyia mahojiano Mwananchi Zuhura Bazi Mkaazi wa Chukwani katika uchunguzi wa maradhi ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake Ikiwa ni muendelezo wa awamu ya Pili ya Mradi wa miaka Mitano uliofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

UTENDAJI KAZI BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI WAMKOSHA WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA

$
0
0

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amesema amefurahishwa na utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ( NEEC) huku akishauri baraza hilo kuona namna kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara katika kueleta maendeleo kwa Watanzania.

Bashungwa ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea mabanda mbalimbali katika maonyesho ya 43 ya biashara,Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.

"Nimefurashwa na kazi ambazo baraza hili linafanya , hata hivyo nataka kuona mnashirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kukaa pamoja kuangalia namna gani mnaweza kuwasaidia watanzania,"amesema Waziri Bashungwa

Kwa upande wake Ofisa Mwezeshaji Mawasiliano wa mawasiliano kwa Umma Kutoka Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi Edward Kessy amefafanua kuwa baraza hilo ni taasisi ya Serikali iliyoko chini ya ofisi ta Waziri Mkuu na moja ya majukumu yake nikuratibu masuala ya uwezeshaji kiuchumi wananchi na sekta binafsi.

Pia amesema ni baraza ambalo linaratibu mifuko mbalimbali ya uwezeshaji wananchi kiuchumi zaidi ya 30 na wanaofika kwenye banda lao wanasikilizwa na kuelezwa mifuko hiyo iliko na iwapo wanakero zinapatiwa ufumbuzi.

Amefafanua zaidi kuhusu baraza hilo amesema pia linasimamia miradi mikubwa ya kimkakati iliyopo nchini ikiwemo ya mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa na mradi wa bwawa la kufumua umeme mto rufiji ambapo wanaangalia ni kwa namna ganikanchi wanweza kunufaika na uwepo wa miradi mikubwa iliyopo nchini.

Kessy ametoa mwito kwa wananchi kutembelea Banda lao ili kujua wanafanya nini na nafasi yao.katika kushiriki kwenye uwezeshaji kiuchumi.
Akizungumzia kuhusu maonyesho hayo Kessy alisema wamefurahishwa na ushiriki wa wajasiliamali wadogo na wakati na hasa wanavyojitahidi kuboresha bidhaa zao

Amesema anatamani kuona wasiliamali wanajifunza nakuboresha zaidi bidhaa zao kupitia maonyesho hayo ili watakaporudi kwenye maeneo yao wakatatue changamoto walizoziona .
 Ofisa Mwezeshaji - Mawasiliano kwa Umma wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Edward Kessy akifafanua jambo kwa baadhi ya wananchi waliofika kwenye banda la baraza hilo lililopo kwenye maonesho ya 43 ya biashara yanayoendelea Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Ofisa Mwandamizi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Nyakahu Mahemba (wa pili kulia) akieleza jambo kwa moja ya wananchi waliofika kwenye banda hilo kupata maelezo kuhusu Baraza unavyofanya kazi.Kushoto ni Ofisa Mwezeshaji Mawasiliano kwa Umma kutoka baraza hilo
Ofisa Mwandamizi Mifuko ya Uwezeshaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyakahu Mahembe akifafanua jambo kwa moja ya wananchi waliofika kwenye banda la baraza hilo lililopo kwenye maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam

HOSPITALI ZA RUFAA ZA MIKOA ZATAKIWA KUWA NA VIFAA MUHIMU VYA KUTOLEA HUDUMA

$
0
0
NA WAMJW-DOM
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa nchini kuhakikisha wanakua na vifaa vya muhimu vya kutolea huduma za afya kwa wagonjwa wanaofika Hospitalini kupata matibabu.

Waziri Ummy amesema hayo wakati akifungua mkutano wa viongozi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Mipango Jijini Dodoma.

Waziri Ummy amewataka Waganga Wafawidhi hao kubainisha aina ya vifaa vya matibabu vinavyotakiwa kupelekwa katika Hospitali zao ili kuhakikisha mgonjwa anapofika Hospitalini hakosi huduma wakati anapoenda kupata matibabu.

“Mganga Mfawidhi unatakiwa useme vifaa gani ukivipata utaboresha huduma, hatutaki mgonjwa afike Hospitali halafu akose huduma, boresha kwanza kupata vifaa vya msingi kabla ya vile vikubwa kama CT-Scan”. Amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amesema lengo la Wizara ya Afya chini ya Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha huduma bora za afya zinatolewa ili mwananchi akifika katika Hospitali za Rufaa aseme kweli huduma zimeboreshwa.

“Lengo la Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kila Hospitali ya Rufaa inakua na huduma za kipaumbele 13 zikiwepo huduma za mama na mtoto ili kusaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na magonjwa mengine ambayo yanaweza kutibiwa bila kumpa rufaa mgonjwa”. Ameongeza Waziri Ummy.

Kwa upande wake, Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewataka Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za mikoa kuhakikisha wanasimamia vizuri ukusanyaji wa mapato kwa kufunga mfumo utakaotumika kukusanya mapato na kuachana na makaratasi.

“Tuendelee kuboresha huduma za afya na kusimamia ubora wa huduma tunazozitoa na kuboresha upatikanaji wa vifaa na kuwa wabunifu japokuwa tuna changamoto za rasilimali watu ila huduma za kibingwa ziboreshwe ili kupunguza rufaa za nje”. Amesema Dkt. Ndugulile.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Zainab Chaula amewataka Waganga Wafawidhi hao kuhakikisha wanaripoti taarifa za maendeleo ya Hospitali na atakayeshindwa kufanya hivyo hataendelea na uongozi. Pia amewataka Waganga Wafawidhi hao kuwa na ushirikiano ili kufanya sekta ya afya kuwa ya mfano.

“Tuhakikishe tunaweka mifumo vizuri ya kutoa huduma kwa wahitaji kuanzia ngazi ya chini kwa kufuata miongozo na mikataba iliyotolewa, na tufanye kazi kwa ushirikiano bila kujali cheo au nafasi ya mtu”. Amesema Dkt. Chaula.

Pamoja na hayo katika Mkutano huo Waziri Ummy alizindua muongozo wa uendeshaji wa Hospitali za Rufaa za Mikoa pamoja na jarida la afya ya jamii toleo la kwanza.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (katikati) akizndua muongozo wa uendeshaji wa Hospitali za Rufaa za mikoa wakati wa uzinduzi wa mkutano wa Waganga Wafawidhi wa Mikoa unaoendelea jijini Dodoma. Kushoto Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Grace Maghembe na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Muhammad Kambi.
 Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu alifurahia muongozo wa uendeshaji wa Hospitali za Rufaa aliouzindua mapema leo, kulia ni Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Grace Maghembe, akipokea muongozo huo kutoka kwa katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula na katikati ni Naibu waziri Dkt. Faustine Ndugulile akishuhudia.
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akionesha jarida la afya ya jamii toleo la kwanza alilozindua wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa unaoendelea jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile na Kulia ni Katibu wa Afya Dkt. Zainab Chaula.
 Viongozi mbalimbali wa Wizara ya Afya na TAMISEMI wakiongozwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakionesha jarida la afya ya jamii toleo la kwanza lililozinduliwa leo na Waziri Ummy.
Waziri wa Afya, Mhe Ummy Mwalimu akihutubia Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa waliofika katika Mkutano unaoanza leo jijini Dodoma

WAZIRI WA KILIMO AKUTANA NA MKURUGENZI MKAAZI WA USAID TANZANIA NDG ANDY KARAS, AMUELEZA MAMBO MAKUBWA MATANO

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Tanzania Ndg Andy Karas katika Ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam, leo Tarehe 1 Julai 2019. (Picha Zote Na Mathias Cnal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa na picha ya pamoja na mratibu wa mradi wa maboresho ya sera (ASPIRES) Prof David Nyange katika Ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam, leo Tarehe 1 Julai 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Tanzania Ndg Andy Karas katika Ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam, leo Tarehe 1 Julai 2019. Wengine pichani ni Naibu Mkurugenzi wa ofisi ya ukuaji wa uchumi (USAID) Tanzania Bi Michelle Corzine, na Mtaalamu wa sera katika usimamizi wa miradi Ndg Semaly kisamo




Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo - Dar es salaam


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo Tarehe 1 Julai 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Ndg Andy Karas katika Ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam.

Katika mazungumzo hayo Mhe Hasunga amemueleza Mkurugenzi huyo kuwa Wizara ya Kilimo imejipanga kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo ili kuondokana na dhana ya kilimo cha kujikimu na kuhamia katika kilimo cha kibiashara. Waziri Hasunga alisema kuwa ili kuongeza tija katika Kilimo, Wizara yake imejipanga kuimarisha utafiti.

Alisema kuwa maendeleo ya kilimo yanategemea zaidi utafiti hususani wa udongo vilevile kubaini teknolojia bora itakayo pelekea kukisogeza kilimo katika hatua kubwa ya mafanikio na kimageuzi.

Amesema kuwa pamoja na mambo mengine wizara ya kilimo pia imejipanga katika kuongeza thamani ya mazao ya kilimo kuliko kusafirisha pasina kuongeza thamani.“Tukiongeza thamani ni wazi kuwa uchumi utapanda, lakini zaidi ajira ziataongezeka kwa wananchi, tutakuwa na Pato zuri la kigeni sambamba na utambulisho wa nchi” Alikaririwa Mhe Hasunga

Kuhusu sekta ya umwagiliaji Mhe Hasunga alisema kuwa Tanzania ina jumla ya Hekta zaidi ya Milioni 29 zinazofaa katika umwagiliaji lakini ni hekta 475,000 ndizo ambazo zimefanyiwa kazi.


“Kwa maana hiyo kuna fursa kubwa katika umwagiliaji hivyo ninyi kama wadau kadhalika natoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuwekeza katika umwagiliaji” Alisema

Kuhusu Lishe Waziri Hasunga alisema kuwa wizara imeendelea kuweka hamasa kwa wakulima ili kuwa na lishe bora. Aliongeza kuwa watanzania wanapaswa kuwa na utamaduni wa kula vizuri ili kuondokana na magonjwa mbalimbali kama vile utapiamlo.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Ndg Andy Karas ameipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa mikakati madhubuti ya kuimarisha sekta ya kilimo nchini.

Aidha, Karas amemuomba Waziri wa Kilimo kuteua watu wawili kutoka wizarani watakaokuwa kiungo muhimu baina ya serikali na miradi ya USAID sambamba na mtu atakayeratibu mikutano ya wadau wa maendeleo.

TANESCO ARUSHA YAWATAHADHARISHA WANANCHI

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

SHIRIKA la umeme Tanzania (TANESCO)mkoani hapa limewatahadharisha
wananchi kuepuka kufanya shughuli za kibinadamu chini ya miundombinu
ya umeme ikiwemo transfoma,nguzo na nyaya,ikiwa ni pamoja na kukaa
mbali na maeneo ambayo matengenezo ya umeme yanafanyika.

Kadhalika Shirika hilo limewasihi wananchi kuhakikisha kuwa wanatumia wakandarasi wenye ujuzi na waliosajiliwa kufanya kazi za kuchora ramani na kutandaza nyaya za umeme pindi wanapohitaji huduma ya kuunganishiwa umeme.

Afisa uhusiano wa Tanesco,Mkoani hapa,saidy mremi aliyasema hayo jana
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake alipokuwa
akizungumzia tahadhari ya ajali za umeme kwa wananchi na mali zao.

Alisema kuwa wakati umefika kwa wananchi kutambua madhara makubwa
yanayoweza kujitokeza pindi wasipochukua tahadhari za ajali hizo za
umeme kwani licha ya kuharibu miundombinu ya umeme,pia hupelekea
wananchi kupoteza uhai pamoja na uharibifu wa mali.

“Nawasihi pia waendesha magari yanayobeba mizigo mikubwa na mirefu
wachukue tahadhari pindi wanapopita chini ya maeneo mbalimbali yenye
miundombinu ya umeme,pia wananchi wachukue taadhari kwa vitu
vilivyoguswa na nyaya za umeme zilizoanguka mfano miti,uzio na kamba
za kuanikia nguo”alisisitiza Mremi.

Afisa uhusiano huyo altumia fursa hiyo pia kuwasihi wananchi wanaotaka
kuunganishiwa umeme kufika moja kwa moja katika ofisi za Tanesco kwa
lengo la kuepukana na watu ambao wamekuwa wakijifanya maafisa wa
Tanesco(Vishoka)walioko huko mtaani ambao wamekuwa wakiwarubuni na
kuwatapeli.

Aliongeza kuwa fomu ya kuomba kuunganishiwa umeme hutolewa bure na
shirika hilo,na kwamba gharama za kuunganishiwa umeme zinajulikana
hivyo ni bora wananchi wakafika katika ofisi za shirika hilo zilizopo
katika Wilaya zote za mkoa wa Arusha.

Walimu wa Hisabati na Sayansi Watajwa Kuchochea Ongezeko la Ufaulu wa Masomo Hayo

New Event Cultivates Economic Growth of the Oil and Gas Industry in Tanzania

$
0
0
Hussein Boffu,  the Chief Giving Officer of the Oil and Gas Happy Hour talks about the upcoming oil and gas event in Tanzania and how they cultivate the economic growth of the industry in the region through education awareness and connecting businesses with opportunities.
Can you tell us a little bit about the oil and gas happy hour?

The Oil and Gas Happy Hour was established in 2018 to facilitate the economic growth of the oil, gas and energy industry through education, awareness and connecting businesses with opportunities. The event allows attendees to network with their peers in a casual environment whilst simultaneously setting their career and business strategies using exclusive industry insights from the industry professionals.

The Happy Hour remains committed to and prides itself on providing a platform that brings together professionals to socialize and network. Aside from this, guests are able to discuss prominent and relevant issues; learn about upcoming projects in the oil and gas industry and engage in meaningful dialogue with their peers. A portion of the sales from the tickets is donated to children in need.

Supporting the community we live and work in is important for the sustainable economic growth of the industry. How does the event make a positive impact on the community?

We are proud to support our community through a variety of ways:
Firstly, we provide money and resources; with each ticket purchased, we donate a portion of net proceeds to children in need on behalf of our attendees, partners, and sponsors. In 2018, the organisation donated school uniforms, shoes and learning materials to a charity, Children in need, in Mkuranga. The charity is selected by participants of each year’s event
The oil and gas happy hour also gives rise to opportunities via the raising of awareness;  during the happy hour we invite the local non-profit organisations to host a booth at our events. This is an opportunity for such organisations to be introduced to the wide array of guests, partners and sponsors. In doing so, we allow the organisations to raise awareness of the various volunteering opportunities available. Volunteering opportunities in which members of the local community will be benefitting from.

What was the main result of the past event on local content?

Although this is an up and coming platform, we have already started to see a positive impact. In terms of local content, we have a gentleman from India who is forming a partnership with a local company that will develop the local workforce. We also have some local service providers who have registered with EWURA’s supplier database so that they may capitalize on the opportunities in the proposed East African crude oil pipeline (EACOP) project.

What is “Empower The Future”?
Empower the future is more than a tagline. The oil and gas happy hour has always aimed to empower for a better tomorrow. We know of only one way: we plant the seeds of the industry and business today so that we can have a plentiful harvest tomorrow. 

Service providers and equipment providers must connect with people and get sight to the project opportunities today as they have desired growth tomorrow. If you are a safety officer, lawyer, accountant or an engineer you must connect with people in the present so that you grow your career in the future. The same holds true with our giving model, for each ticket purchased we give away a portion of the net proceeds to children in need. As previously mentioned we have already donated shoes and learning materials to 18 children. We planted the seeds to the children of today so that they may have a better tomorrow. This is a platform that empowers people, industries and communities alike for brighter prospects.

Any final words?
Come one; come all for the second annual oil and gas happy hour. Oil and gas professionals are encouraged to join us to not only network with their peers but to set their career and business strategies with confidence using exclusive insights from the industry speakers. I would like to invite everybody  to the second annual oil and gas happy hour which will be hosted at the Best Western CBD hotel, Dar es Salaam, Tanzania on Friday, August 23, 2019, from 18:00 to 22:00PM

Hussein@oilandgashappyhour.com
+255655376543

New Event Cultivates Economic Growth of the Oil and Gas Industry in Tanzania

$
0
0
Hussein Boffu,  the Chief Giving Officer of the Oil and Gas Happy Hour talks about the upcoming oil and gas event in Tanzania and how they cultivate the economic growth of the industry in the region through education awareness and connecting businesses with opportunities.
Can you tell us a little bit about the oil and gas happy hour?

The Oil and Gas Happy Hour was established in 2018 to facilitate the economic growth of the oil, gas and energy industry through education, awareness and connecting businesses with opportunities. The event allows attendees to network with their peers in a casual environment whilst simultaneously setting their career and business strategies using exclusive industry insights from the industry professionals.

The Happy Hour remains committed to and prides itself on providing a platform that brings together professionals to socialize and network. Aside from this, guests are able to discuss prominent and relevant issues; learn about upcoming projects in the oil and gas industry and engage in meaningful dialogue with their peers. A portion of the sales from the tickets is donated to children in need.

Supporting the community we live and work in is important for the sustainable economic growth of the industry. How does the event make a positive impact on the community?

We are proud to support our community through a variety of ways:
Firstly, we provide money and resources; with each ticket purchased, we donate a portion of net proceeds to children in need on behalf of our attendees, partners, and sponsors. In 2018, the organisation donated school uniforms, shoes and learning materials to a charity, Children in need, in Mkuranga. The charity is selected by participants of each year’s event
The oil and gas happy hour also gives rise to opportunities via the raising of awareness;  during the happy hour we invite the local non-profit organisations to host a booth at our events. This is an opportunity for such organisations to be introduced to the wide array of guests, partners and sponsors. In doing so, we allow the organisations to raise awareness of the various volunteering opportunities available. Volunteering opportunities in which members of the local community will be benefitting from.

What was the main result of the past event on local content?

Although this is an up and coming platform, we have already started to see a positive impact. In terms of local content, we have a gentleman from India who is forming a partnership with a local company that will develop the local workforce. We also have some local service providers who have registered with EWURA’s supplier database so that they may capitalize on the opportunities in the proposed East African crude oil pipeline (EACOP) project.

What is “Empower The Future”?
Empower the future is more than a tagline. The oil and gas happy hour has always aimed to empower for a better tomorrow. We know of only one way: we plant the seeds of the industry and business today so that we can have a plentiful harvest tomorrow. 

Service providers and equipment providers must connect with people and get sight to the project opportunities today as they have desired growth tomorrow. If you are a safety officer, lawyer, accountant or an engineer you must connect with people in the present so that you grow your career in the future. The same holds true with our giving model, for each ticket purchased we give away a portion of the net proceeds to children in need. As previously mentioned we have already donated shoes and learning materials to 18 children. We planted the seeds to the children of today so that they may have a better tomorrow. This is a platform that empowers people, industries and communities alike for brighter prospects.

Any final words?
Come one; come all for the second annual oil and gas happy hour. Oil and gas professionals are encouraged to join us to not only network with their peers but to set their career and business strategies with confidence using exclusive insights from the industry speakers. I would like to invite everybody  to the second annual oil and gas happy hour which will be hosted at the Best Western CBD hotel, Dar es Salaam, Tanzania on Friday, August 23, 2019, from 18:00 to 22:00PM

Hussein@oilandgashappyhour.com
+255655376543

PSPTB YATANGAZA RASMI MATOKEO YA 18 YA BODI HIYO

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa Manunuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza matokeo ya mitihani ya Bodi ya 18, pamoja na kutangaza rasmi nafasi ya usajili kwa ajili ya mitihani ya 19 ya Bodi hiyo itakayofanyika mwezi Novemba.

BODI ya wataalamu wa ununuzi na ugavi iimetangaza matokeo ya 18, pamoja na kutangaza rasmi nafasi ya usajili kwa ajili ya mitihani ya 19 ya bodi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijiji Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amesema kuwa leo Julai mosi Bodi ya wakurugenziimeidhinisha matokeo ya bodi ya 18 na kuwa rasmi.

Ameongeza kuwa mitihani hiyo ilifanywa katika vituo vitano nchini na zaidi ya watahiniwa 1400 walifanya mitihani huyo na watahiniwa zaidi ya 50 hawakuweza kufanya mitihani hiyo.

Aidha amesema kuwa Kuna baadhi ya watahiniwa ambao watarudia mitihani hiyo na kueleza kuwa somo la hesabu  linahitaji kutiliwa mkazo kwa kuwa ufaulu bado ni hafifu .

Vilevile amesema kuwa watahiniwa wawe na mawazo chanya na wao Kama Bodi watasimamia  vigezo vya ufaulu na kueleza kuwa uhidhinishaji wa matokeo hayo yanafungua milango ya kujisajili kwa mitihani ya 19 ya bodi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari  Mbanyi  ameongeza kuwa kutakuwa na warsha maalumu pamoja kuwajengea uwezo katika kuandika tafiti na kujieleza kwa kuwa wanaandaliwa kuwa viongozi wa baadaye.

"kuwa ngazi zote za mafunzo zitazingatiwa na hiyo ni pamoja na kanuni na Sheria zote za mitihani " alisema Mbanyi.

Chama cha kusaidiana jijini Mwanza chatimiza mwaka mmoja kwa mafanikio

$
0
0
Kikundi/ Chama cha kusaidiana cha Familia Yenye Upendo (Family with Passion-FAWIPA) kilichopo Nyegezi jijini Mwanza, kimetimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake ambapo hafla ya kusherehekea mafanikio yake imefanyika jana jumapili Juni 30, 2019 ndani ya Passion Hotel.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa FAWIPA, Twalib Mafele akizungumza kwenye hafla ya chama hicho iliyofanyika jana ukumbi wa Passion Hotel ikiambatana na harambee kabambe ya kuimarisha chama.
Mgeni rasmi kwenye hafla hioyo alikuwa Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi ambaye aliwakilishwa na Afisa Mtendaji Kata ya Nyegezi, Shaaban Mpuya (katikati).
Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana akitoa salamu zake kwenye hafla hiyo.
Mmoja wa wageni waalikwa akitoa nasaha zake kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakitoa salamu zo kwenye hafla hiyo.
Mgeni rasmi akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wanachama wa FAWIPA ambaye alionesha ushiriki mzuri wa shughuli mbalimbali za chama.
FAWIPA ilitoa motisha kwa wanachama wanne walioonyesha ushiriki mzuri wa shughuli mbalimbali za chama.
Washiriki kutoka vyama vingine rafiki pia walialiwa kwenye hafla hiyo.
Wanachama wa FAWIPA pamoja na wageni waalikwa walisimama kwa dakika moja kama ishara ya kumkumbuka mmoja wa waasisi wa chama hiki, mwanahabari Cathbert Japhet ambaye pia ndiye aliyependekeza jina la chama kuitwa Familia yenye Upendo, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Mei 13, 2019.

Wanachama na wageni waalikwa wakiwa ukumbini.
Wanachama na waalikwa mbalimbali wakiwa ukumbini.
Wasaa wa maakuli pia ulikuwepo.
Wasaa wa kusakata rhumba pia ukawadia.
Katibu wa FAWIPA, Innocent Alloyce (kushoto) akiweka kumbukumbu na baadhi ya waalikwa kwenye hafla hiyo.
Tazama Video hapa chini

WATU WAWILI WADAIWA KUWAWA KWA KWA SHOKA NA VISU HUKO CHALINZE

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI


WATU wawili wamefariki dunia mkoani Pwani ,kutokana na matukio tofauti ya mauaji yaliyotokea wilaya ya kipolisi Chalinze, ikiwa ni pamoja na Damian Kimiti (70) ambae ameuawa kwa kupigwa shoka.

Kufuatia mauaji hayo watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapo. 

Akielezea kuhusiana na matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani hapo, kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani ,Wankyo Nyigesa alisema Kimiti aliuawa huko Malivundo ,Talawanda ,Chalinze, ambapo mtiliwa shaka Said Ngosha amekubali kuuwa na tayari amekamatwa .

Alisema ,baada ya mauaji muaji alipora simu tatu aina ya tecno ,solar panel moja,shuka na baiskeli."Pia alikubali kuonyesha simu tecno mbili ,solar panel moja na shoka moja"alifafanua Wankyo.

Katika tukio jingine ,Wankyo alieleza Ngurai Waziri (33) mfugaji huko Msolwa kijiji cha Lukenge aliuawa kwa kukatwa na visu.

Kamanda huyo alibainisha, mtiliwa shaka David Mwanje (28) , Thomas Gau (25) na Magoma Ramadhani Mbwiga (32) wamekamatwa na katika mahojiano ya awali watuhumiwa hao wamedai marehemu alikuwa mwizi wa mifugo na alikuwa kero katika wizi wa mifugo.

Wakati huo huo Wankyo alisema, juni 30 eneo la Sweat Corner Vigwaza katika barabara kuu ya Morogoro -Dar es salaam ,gari lenye namba za usajili T.182 DGH/T .182 DGM aina ya scania ,lililokuwa likitokea Iringa kuelekea Dar es salaam likiendeshwa na dereva Samwel Emanuel mkazi wa Makambako Iringa.

"Gari hilo liligongana uso kwa uso na gari lenye namba za usajili T.420 CGK/T.909 BZU scania lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Chalinze likiendeshwa na Iddi Rashid mkazi wa Tegeta ikiwa imebeba malighafi zitumikazo kutengeneza juice na kusababisha moto mkubwa na magari yote yaliteketea."aliongeza Wankyo.

Wankyo alitaja chanzo cha ajali ni gari lenye namba T.420 CGK aina ya scania kuhama upande wake na kuhamia upande wa kulia mwa barabara.

MATUKIO KATIKA PICHA: MAONESHO YA 43 YA BIASHARA SABASABA

$
0
0
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, Akiwa
kwenye viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam, Tayari kwa kuanza
kutembelea mabanda yaliyoko kwenye maonesho ya 43 ya biashara(sabasaba), Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bwana Edwin Rutegaruka
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa
akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Kuhusu
Maonesho ya 43 ya Biashara (sabasaba) ambayo yalianza Juni 28, 2019 na
yatazinduliwa Rasmi Hapo Kesho na Makamu wa Rais wa Tanzania, Suluhu
Hassan, huku kauli mbiu ikiwa ni “ Usindikaji wa mazoa ya kilimo kwa
maendeleo endelevu ya Viwanda”. 
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa akiwa
katika banda la kampuni ya kutengeneza Majani ya Chai (Chai Bora)
alipokua akitembelea mabanda yaliyoko kwenye maonesho ya 43 ya
biashara(sabasaba), wa pili Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bwana Edwin Rutegaruka.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa,
akipokea Maelezo kutoka kwa mjasiriamali wa asali ya asili katika
maonesho ya 43 ya biashara(sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya
sabasaba Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Maneja Msaidizi, Idara ya Uhusiano na
Itifaki kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Vicky Msina, kuhusu historia ya
Sarafu ya Tanzania, mara baada ya kutembelea katika Banda hilo, kwenye
maonesho ya 43 ya biashara(sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya
sabasaba Jijini Dar es Salaam, Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bwana Edwin Rutegaruka. 

Elizabeth Daudi kutoka Dodoma Akionesha vitu vya asili katika
kabila la Wagogo katika Maenesho ya 43 ya Biashara (sabasaba) ambayo
yalianza Juni 28, 2019 na yatazinduliwa Rasmi Hapo Kesho na Makamu wa
Rais wa Tanzania, Suluhu Hassan, huku kauli mbiu yake ikiwa “ Usindikaji
wa Mazoa ya Kilimo kwa Maendeleo Endelevu ya Viwanda”. 

Afisa Habari kutoka kituo cha Uwekezaji, Latifa Kigoda, akielezea
huduma ambazo Taasisi hiyo inazitoa kwa wawekezaji katika Maonesho ya 43 ya Biashara (sabasaba) ambayo yalianza Juni 28, 2019 na yatazinduliwa
Rasmi Hapo Kesho na Makamu wa Rais wa Tanzania, Suluhu Hassan, huku
kauli mbiu yake ikiwa “ Usindikaji wa Mazoa ya Kilimo kwa Maendeleo
Endelevu ya Viwanda”. 
Moja ya Bidhaa kutoka katika kampuni ya kuunganisha Matrecta ya
URSUS kama linavyonekana kwenye picha katika maenesho ya 43 ya
Biashara (sabasaba) ambayo yalianza Juni 28, 2019 na yatazinduliwa
Rasmi Hapo Kesho na Makamu wa Rais wa Tanzania, Suluhu Hassan, huku
kauli mbiu yake ikiwa “ Usindikaji wa Mazoa ya Kilimo kwa Maendeleo
Endelevu ya Viwanda”.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images