Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

Hakimu wa wilaya amwagiwa sifa

$
0
0
Picha ya kwanza ni Diwani mpya Kassimu Gunda kata ya Likuyuseka wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma akiapa mbele ya Hakimu wa wilaya ya Namtumbo Gloria Lwomile.
picha ya pili ni Waheshimiwa madiwani wakiwa na diwani mpya wa kata ya Likuyuseka bwana Kassimu Gunda


NA YEREMIAS NGERANGERA …NAMTUMBO

Hakimu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Gloria Lwomile amemwagiwa sifa kutoka kwa wananchi wilayani hapa pamoja na waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kwa kutenda haki kizalendo katika kazi zake za kimahakama.

Wakiongeza mara baada ya kikao cha baraza la madiwani hivi karibuni katika ukumbi wa Hamashauri hiyo diwani wa kata ya Limamu Isdori Nyati na diwani wa kata ya Mgombasi Mrisho Mbawala walisema kuwa hakimu huyo ni msaada mkubwa kwa jamii hasa kwa kutoa miongozo ya kisheria kwa jamii hasa kwa kutumia muda wake mwingi katika kusaidia jamii .

Madiwani hao walisema wapo mahakimu wananchi wanawaogopa hata kwa kuongea nao na namna wanavyojiweka lakini hakimu huyo ni kimbilio la wananchi wilayani hapo hasa kwa kukubali kuongea na mwananchi wa kima cha chini mwenye tatizo na kumsaidia kisheria bila masharti yoyote walisema madiwani hao.

Madiwani walimwagia sifa hizo wakati hakimu huyo alipoombwa kumwapisha diwani mpya wa kata ya Likuyuseka bwana Kassimu Buruhani Gunda (CCM) aliyechaguliwa kuziba nafasi ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo marehemu Ally Kombo.

Aidha Rashidi Kumbikila mwananchi wa mjini Namtumbo alidai kuwa hakimu huyo wa wilaya amekuwa kimbilio la wanyonge kwenda kupata ushauri wa kisheria hasa kwa kusaidia jamii ya watu maskini bure alisema mwananchi huyo.

Bwana kumbikila alidai amewaona mahakimu wengi katika wilaya ya Namtumbo lakini hakimu huyo hana makuu na hutoa ushauri kwa mtu yoyote anayehitaji msaada wa kisheria hasa kwa watu wengi maskini wasiona uwezo.

Mwandishi wa gazeti hili alimfuata hakimu huyo ili kuweza kuhojiana naye lakini alikataa kuongea chochote na badala yake aliingia kwenye gari na kurudi ofisini mara baada ya kumaliza kumwapisha diwani huyo mpya.

MKUTANO WA 23 WA TAASISI ZA MAWASILIANO AFRIKA MASHARIKI (EACO) WAANZA JIJINI MWANZA

$
0
0
NA MWANDISHI WETU, MWANZA

MKUTANO wa 23 wa Taasisi zinazosimamia Mawasiliano kwa Nchi za Afrika Mashariki, (EACO) umeanza leo Julai 1, 2019 jijini Mwanza.

Sambamba na mkutamno huo pia wajumbe watashiriki Mkutano Mkuu wa 26 wa EACO ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kuiweka Afrika Mashariki katika eneo la Uchumi wa Kidijitali".Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Atashasta Nditiye (Mb), ndiye aliyefungua mkutano huo utakaodumu hadi Julai 5, wenyeji ni Tanzania, pamoja na mataifa mengine ya EAC, ambayo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini. 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (Mb), (wapili kushoto), akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasilkiano Tanzania (TCRA), Mhandisi James M. Kilaba (watatu kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya (TCRA), Dkt. Jones Killimbe (wanne kushoto) Afisa Mtendaji Mkuu wa EACO Dtk. Ally Yahya Simba (wakwanza kulia) na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Mawasiliano Bw.Mulembwa Munaku. (wakwanza kushoto), baada ya kufungua Mkutano wa 23 wa Taasisi zinazosimamia Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO), utakaofuatiwa na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 26 wa EACO jijini Mwanza Julai 1, 2019
Muwakilishi wa Umoja wa Shirika la Posta Duniani (upu), Kusini mwa Afrika na Asia, Bi. Gladys Mutyavaviri ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa upu, akizungumza kwenye mkutano huo wakati wa ufunguzi.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James M. Kilaba, akizungumza na waandishi wa habari kufafanua baadhi ya mambo kuhusu mkutano huo.
Wajumbe kutoka Burundi, wakisikilzia hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
Wajumbe kutoka Kenya, wakisikilzia hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
Wajumbe kutoka Rwanda, wakisikilzia hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
Wajumbe wenyeji Tanzania, wakimsikiliza Mhe. Naibu Waziri Mhandisi Nditiye wakati akifungua mkutano huo.
Wajumbe kutoka Uganda, wakisikilzia hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
Mhe. Naibu Waziri Mhandisi Nditiye na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka mataifa wanachama wa EACO. 

PROMOSHENI SHINDA MCHONGO MWANASPOTI YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Mwananchi Communications Limited (MCL), Frank Sanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai, Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo na Meneja Masoko wa MCL, Sarah Munema wakiwa katika  waliazindua promosheni ya Shinda Mchongo wa Mwanaspoti ilifanyika  leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai, akionesha gazeti la Mwanaspoti  katika uzinduzi wa  promosheni ya Shinda Mchongo wa Mwanaspoti leo jijini Dar es Salaam.

Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo kushoto akizungumza mara baada ya kuzinduzi  promosheni ya Shinda Mchongo wa Mwanaspoti ilifanyika  leo jijini Dar es Salaam.

AZMA YA SERIKALI AWAMU YA TANO NI KUIMARISHA VIWANDA,NA KUTEKELEZWA KWA VITENDO.

$
0
0
Azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuimarisha Viwanda imeonekana kutekelezwa kwa vitendo katika vyuo vya Elimu vya Juu nchini ambapo Chuo Kikuu Mzumbe kwa mwaka huu 2019 kimeshiriki maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba, ambapo mbali na kutangaza programu zake imeshirikisha wanafunzi wabunifu ambao kupitia mafunzo ya Biashara wanayoyapata chuoni hapo wamekubuni biashara na kufungua makampuni mbalimbali wakitekelezs kauli mbiu ya mwaka huu ya " usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda"

Mbali na bidhaa kupitia kitivo cha sayansi na teknolojia wanafunzi kwa kushirikiana na wakufunzi wao wamefanikiwa kubuni mfumo unaojulikana kama TraSMS-Cargo ambao utahusika kurahisisha uchukuzi wa mazao na bidhaa za kilimo kutoka kwa wakulima kwenda kwa walaji. TraSMS-Cargo ni mfumo wa kielektroniki unaowakutanisha wa wachukuzi na wasafirishaji kwa Lengo la kurahisha na kupunguza gharama za usafirishaji. 
Morice Daudi Mhadhiri wa Kitivo cha Sayansi naTeknolojia chuo kikuu Mzumbe akionesha  picha ya mchoro unaoonyesha mfumo wa TraSMS-Cargo uliobuniwa na wanafunzi na wakufunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe leo katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wananchi akipata maelezo ya bidhaa kutoka kwa Jasinta Msamula mhadhiri wa Shule ya Biashara Chuo Kikuu Mzumbe leo katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Bi. Fatna Mfalingundi Afisa Habari wa Chuo Kikuu Mzumbe akitoa maelezo kuhusu shughuli za Chuo Kikuu Mzumbe kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la hilo leo katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Chuo kikuu Mzumbe wakiwa wamejipanga kwenye banda Lao tayari kuwahudumia wananchi wanaofika kupata huduma.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

A TO Z YAIPAISHA TANZANIA,AFRIKA TUZO ZA KAIZEN

$
0
0

NA SEIF MANGWANGI ARUSHA

TANZANIA imeibuka mshindi wa kwanza katika bara la Afrika wa tuzo ya Kimataifa ya KAIZEN katika viwanda bora na vinavyofanyakazi kwa ufanisi kupitia kiwanda cha A TO Z Textile Mills kilichopo Kisongo Jijini Arusha.

Tuzo hiyo ya Kimataifa ambayo hushirikisha sekta mbalimbali ikiwemo viwanda vya kati na vikubwa zilizofanyika katika mji wa Tunis nchini Tunisia, hutolewa na shirika la kimataifa la misaada la JAPAN (JICA), kwa taasisi hizo kutekeleza majukumu yao kwa kufuata dhana ya KAIZEN ambayo ni kuzalisha kwa tija, ubora, kupunguza gharama.

Kabla ya kuibuka na ushindi huo, A to Z iliibuka kidedea dhidi ya viwanda vyote vya Tanzania katika mashindano ya Tanzania Kaizen Award, yaliyoandaliwa na wizara ya Viwanda na Biashara kupitia kitengo cha Kaizen Tanzania (TKU), yaliyofanyika Machi 1, 2019 Jijini Dar es salaam na kuchaguliwa kwenda kuiwakilisha Tanzania katika ngazi ya Afrika.

Mkurugenzi wa uzalishaji wa kiwanda cha A to Z Textile Mills, Binesh Haria alisema Kampuni 16 kutoka katika nchi za Kenya, Ghana, Ethiopia, Afrika Kusini, Zambia, Cameroon na DRC Congo na Tanzania zilishiriki kwenye tuzo hizo na A to Z kuibuka mshindi wa kwanza kwa kuwa kiwanda bora Afrika.

Mmoja wa wasimamizi wa kitengo cha Kaizen katika kiwanda cha A to Z, na ambaye ndiye aliyewasilisha utekelezaji wa dhana ya KAIZEN katika mkutano huo nchini Tunisia alisema katika uwasilishaji huo ambao hutokana na taarifa ya waangalizi wa tuzo hizo ambazo huzichukua awali baada ya kutembelea viwanda hivyo, Tanzania ilionekana kufanya vizuri zaidi kuliko nchi zingine.

Lyanga alisema baada ya tuzo hiyo, Agosti mwaka huu A TO Z itashiriki kwenye mkutano wa Kimataifa unaojulikana kama TICAD7 utakaoshirikisha wakuu mbalimbali wa nchi kwa lengo la kuzungumzia maendeleo ya Afrika katika sekta tofauti ikiwemo sekta ya viwanda ambapo pia katika mkutano huo, washindi  wa tuzo ya KAIZEN watapata fursa ya kueleza utekelezaji wake na mafanikio waliyopata.

Akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa A TO Z, Kalpesh Shah, Meneja wa biashara za nje, Sylvester Kazi alisema tuzo hiyo ya kwanza kutolewa Afrika ni zawadi ya watanzania hasa kupitia Serikali ya wamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli.Alisema ni kweli kiwanda cha A to  Z kimeibuka mshindi lakini anayestahili kupewa hongera na pongezi nyingi ni Rais Dkt Magufuli kwa  kuwa amekuwa akihamasisha uanzishwaji wa viwanda mbalimbali tangu alipoingia madarakani.

Kazi alimuomba Rais Magufuli kuipokea Tuzo hiyo yeye mwenyewe au kupitia kwa kiongozi wa chini yake ambaye ataagiza apatiwe ili kuonyesha ishara ya uwajibikaji na utekelezaji wa malengo ya Serikali ya awamu ya tano ya kuanzishwa kwa viwanda  na kutoa ajira nyingi kwa watanzania.

“Sisi kama kiwanda tumefurahi sana na tunafanya utaratibu wa kumfikishia Tuzo hii, Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli ili aiweke Ikulu na kuonyesha jitihada zake zinapelekea za kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda, tutajitahidi kuwasiliana nae kama itampendeza tutamfikishia Ikulu,”alisema Kazi.

“Pia kiwanda kinapenda kutoa shukrani zake kwa shirika la viwanda vidogo SIDO Mkoa wa Arusha, kitengo cha Kaizen nchini (TKU), shirika la Kimataifa la Ushirikiano wa kimaendeleo la  watu wa Japan (JICA) na wizara ya viwanda kwa mchango wao mkubwa wa kufanikisha mafanikio iliyofikia hivi sasa A to Z.
 Wawakilishi wa kiwanda cha A to Z, Reuben Lyanga pamoja na Marco Alphay wakiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa tuzo ya Kimataifa ya KAIZEN mara baada ya Tanzania kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo katika hafla iliyofanyika katika mji wa Tunis nchini Tunisia
 Mwenyekiti wa taasisi ya Lean Institute na mmoja wa majaji wa tuzo ya KAIZEN,  Profesa Norman Faull akishuhudiwa mwakilishi wa kiwanda cha A TO Z Reuben Lyanga akivishwa bendera ya Tanzania baada ya kumtangaza kuwa mshindi wa kwanza wa tuzo za KAIZEN 2019.
 Tuzo walizokabidhiwa kiwanda cha A to Z baada ya kuiwakilisha vyema Tanzania

 Wawakilishi wa A TO Z Reuben Lyanga wa pili kushoto na Marko Aphayo wakiwa wameshikilia tuzo bora ya Afrika ya kaizen 2019 katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa taasisi ya kimataifa ya Grips na waandaaji wa tuzo hiyo, Professa Tetsushi Sonobe.


TAFITI ZAIDI KUFANYIKA KUKUZA SEKTA YA UVUVI NA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

$
0
0

Baadhi ya vifaa vyenye thamani ya Tshs Milioni 70 vilivyotolewa kwa Taasisi ya Uvuvi nchini (TAFIRI) kwa ajili ya kuendeleza tafiti za sekta ya uvuvi nchini
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (mstari wa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo.
Washiriki wa mafunzo wakiwa katika hatua za mwisho za mafunzo kabla ya mafunzo hayo kuhitimishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah.
****************

Na. Edward Kondela
Katibu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah amesema wizara hiyo kupitia Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) imeweka mikakati ya kufanya tafiti ikiwa ni moja ya vipaumbele katika kukuza sekta ya uvuvi nchini katika mwaka wa fedha 2019/2020.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyokuwa yakiendeshwa kwenye makao makuu ya TAFIRI, Dkt. Tamatamah amesema mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Serikali ya Watu wa China kupitia Sino-Africa Joint Research Centre (SAJOREC) na East African Great Lakes Urban Ecology (EAGLU) kwa kushirikiana na TAFIRI yana lenga kuhakikisha washiriki wa mafunzo hayo ya siku sita ya uelewa wa ufuatiliaji wa ubora na unadhifu wa maji na mazingira, wanafanya tafiti ili kuleta matokeo chanya katika ukanda wa Bahari ya Hindi, maziwa na mito iliyopo nchini.

Dkt. Tamatamah amesema pia washiriki wamepata mafunzo kupitia mihadhara iliyotolewa na wakufunzi wabobezi kutoka China na Tanzania pamoja na kukusanya takwimu kutoka katika mito iliyopo Mkoani Dar es Salaam na kuchakata takwimu hizo katika maabara ya TAFIRI. 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu TAFIRI Dkt. Semvua Mzighani amesema kupitia mafunzo hayo Serikali ya Watu wa China, SAJOREC na EAGLU wametoa vifaa vya utafiti vyenye thamani ya Tshs Milioni 70 ambavyo vitatumika kwa tafiti za kuangalia ubora na unadhifu wa maji na mazingira kwa ujumla.

Amesema mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kuwafundisha wenzao katika sekta ya uvuvi ili kuhakikisha viumbe vinavyotegemea maji katika maisha yao ya kila siku, vinapata maji safi na salama kutokana na tafiti zitakazokuwa zikifanywa na kutafuta njia mbadala za kuhakikisha maji yanaendelea kuwa salama na kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi kuathiri usalama wa maji.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema mafunzo yatawezesha taasisi mbalimbali zinazohusika na usalama wa maji kufanya tafiti zenye matokeo chanya ili maji ya Bahari ya Hindi, maziwa na mito katika Ukanda wa Afrika kuwa salama na kupata suluhu namna ya kukabiliana na mabadiliko yoyote ya tabia nchi ambayo yanaweza kusababisha athari katika maji hayo.

Mafunzo hayo yameshirikisha washiriki kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Ethiopia pia walikuwepo waendesha mafunzo hayo kutoka China.

NSSF NA PSSSF WASHIRIKIANA KUHUDUMIA WANANCHI MAONESHO YA SABASABA

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA DKT MAKAKALA JIJINI DODOMA

$
0
0

 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala alipomtembelea  Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) akiagana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA YAPONGEZWA KWA KUUNDA BARAZA LA WAFANYAKAZI

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula akikata utepe kuashiria rasmi uzinduzi rasmi wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa jana jijini Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula akimkabidhi Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Bw. Maudhi Mayunga Mkataba wa Utendaji Kazi alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo jana jijini Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula akimkabidhi Mwakilishi wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Mkataba wa Utendaji Kazi katika hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo jana jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo jana jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo jana jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo jana jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (TUGHE) mkoa wa Dodoma Mchenya John mara baada ya kuzindua Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa mapema hivi karibuni jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo jana jijini Dodoma.
Picha ya pamoja. (PICHA NA FRANK SHIJA-MAELEZO)

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEO

VOA SWAHILI: HABARI MBALIMBALI ZA MICHEZO

TASWIRA ZA TERMINAL lll UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE KATIKA MAJARIBIO

WANANCHI WA WAJITOKEZA KWA WINGI BANDA LA RITA KUPATA HUDUMA YA VYETI VYA KUZALIWA

$
0
0
 Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye misururu mirefu wakipata huduma ya vyeti vya kuzaliwa katika banda la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) leo katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wananchi kama wanavyo onekana pichani wakijaza fomu katika banda la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) leo katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
 Watumishi wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), wakiwaelekeza wananchi namna ya kujaza fom za cheti cha kuzaliwa  leo katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.

 
Waanachi mbalimbali wakionekana kujitokeza kununua bidhaaa zilizotengenezwa kwa mikono ya wajasiriamali kutoka ndani ya Tanzania  leo katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.















MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 2,2019

WAZIRI KAIRUKI AUTAKA UONGOZI KIWANDA CHA GOOD WILL KUZINGATIA USTAWI WA WAFANYAKAZI WAKE

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiangalia na kupata ufafanuzi kutoka kwa Meneja Mwajiri wa kiwanda cha Good Will Bw. Figa Msaphiry juu ya marumaru zinazotengenezwa kiwandani hapo alipotembelea kukagua na kuzungumza na wawekezaji hao Juni 29, 2019 Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiangalia namna vifungashio vya marumaru vinavyotengenezwa katika kiwanda cha kutengeneza marumaru cha Good Will kilichopo Mkuranga Mkoa wa Pwani wakati wa ziara yake kiwandani hapo.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) pamoja na viongozi wa Halmashauri alioongozana nao katika ziara yake kujionea namna marumaru zinavyotengenezwa katika kiwanda cha Good Will Limited kilichopo Mkuranga Pwani.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho mara baada ya ziara yake kiwandani hapo.Meneja Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza marumaru cha Good Will akizungumza jambo wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki alipotembelea kiwanda hicho Mkoani Pwani.Afisa Ufuatiliaji Idara ya Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Moureen Guveti akichangia chambo wakati wa kikao hicho.Baadhi ya wajumbe wa kikao walioshiriki ziara hiyo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati wa kikao cha pamoja cha majumuisho mara baada ya kumaliza ziara yake kiwandani hapo.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

…………………..

NA.MWANDISHI WETU – OWM

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchi Mhe. Angellah Kairuki ameutaka uongozi wa Kiwanda cha kutengeneza marumaru cha GoodWill Tanzania ceramic ltd kuzingatia ustawi wa wafanyakazi wake kwa kuzingatia kanuni na sheria mbalimbali za ajira nchini ili kuendelea kuwa mazingira mazuri ya wafanyakazi wake.
Ametoa kauli hiyo alipofanya ziara yake mwishoni mwa wiki katika kiwanda hicho kilichopo katika Kijiji cha Mkiu kata ya Nyamato Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.

Waziri Kairuki alieleza kuwa, upo umuhimu wa kujali wafanyakazi katika maeneo yao ya kazi kwa kuzingatia usalama na afya mahala pa kazi ili kuondokana na mazingira mabaya yanayoweza kukwamisha uzalishaji unaotarajiwa.

“Ikiwa kiwanda kimeweza kutoa ajira zipatazo 3000 ni idadi kubwa hivyo lazima myatazame mahitaji yao na kuendelea kuzingatia sheria na haki za wafanyakazi wawapo kazini,”Alisema Waziri Kairuki.

Aliongeze kuwa miongoni mwa maeneo muhimu kwa wafanyakazi wenu ni kuhakikisha mnawapa mafunzo kazini ili kuongeza ujuzi katika fani mbalimbali zinazoendana na uzalishaji kiwandani hapo.Aidha aliwataka kuendelea kuwapa motisha na kuwa na njia za ubunifu katika kuhakikisha kila mfanyakazi anakuwa mwenye ustawi na kufurahia mafanikio ya uwepo wa kiwanda hicho.

“Ni lazima kujali masuala ya usalama wa afya zao wawapo kazini, kujali stahiki zao, kuwapa kazi zenye staha kwa kulingana na kanuni na sheria za kazi zilizopo,”alisisitiza Waziri Kairuki Naye Meneja Mwajiri wa kiwanda hicho Bw. Figa Msaphiry alimpongeza Waziri kwa Ziara yake kiwandani hapo na kuahidi kuendelea kuyatekeleza maagizo hayo ikiwemo la kuhakikisha wanaendelea kujali masuala ya Afya na Usalama Mahala Pa Kazi kwa kuzingatia mchango unaotolewa na wafanyakazi hao katika kiwanda hapo.

Alifafanua kuwa, kiwanda kimefanikiwa kutengeneza ajira za moja kwa moja kwa watanzania 936 kati ya hao wanaume 887 na wanawake 49, lakini pia kiwanda kimetengeneza ajira zisizo rasmi Zaidi ya 1,500 na kwa siku wanapokea vibarua ambao wapatao 40 hadi 50 na hii kupeleekea kuongeza fursa za ajira nchini.

Aliongeze kuwa wafanyakazi wamechangia matokeo chanya katika uzalishaji ambapo kiwanda kinazalisha marumaru mita za eneo 40,000 mpaka 50,000 kwa siku kuwa ambapo soko la ndani ni kwa asilimia 30 hadi 40 na soko la nje ni kwa asilimia 60 hadi 70.“Kiwanda chetu kimeweza kupanua soko la marumaru kwa kuuza katika nchi za nje, kwani kwasasa kiwanda kinauza marumaru katika nchi za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Congo kwa kuzingatia ubora wa bidhaa zetu,”alieleza Figa .


kiwanda cha Good Will Company Limited kilijengwa mwezi Machi, 2016 na kuwekwa jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda hiki na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kasimu Majaliwa, na kuanza uzalishaji wake mnamo Mwezi Aprili Mwaka 2017.Kiwanda kinazalisha marumaru za sakafuni (floor tiles) na marumaru za ukutani (wall tiles) kwa saizi zote na “scating”, Katika uzalishaji wa marumaru kiwanda kinatumia malighafi tofauti tofauti ambapo 95% ni malighafi toka hapahapa Tanzania na 5% kutoka China ambazo ni kemikali.

Malighafi zinazotoka Tanzania ni felidisper ambayo inatoka Tanga – Handeni, Morogoro na Dodoma, nyingine ni Soap stone kutoka Dodoma na Morogoro, Magnesite kutoka Same Moshi, Udongo wa mfinyanzi (clay soil) na udongo mwekundu (red soil) kutoka Mkuranga – Pwani, Limestone kutoka Mavuji – Kilwa na Kaolin kutoka Kisarawe Pwani. Mradi huu wa ujenzi wa kiwanda umegharimu jumla ya fedha za kigeni dola milioni 50.

NSSF NA PSSSF WASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA SABASABA KWA PAMOJA

$
0
0
Maonesho hayo yameanza tarehe 28/06/2019 na yatamalizika tarehe 13/06/2019. Wanachama wa mifuko yote miwili wanaalikwa kuja kupata huduma mbalimbali katika banda namba 13.

NSSF na PSSSF wanashiriki kwa pamoja katika maonesho hayo ili kuweza kutoa huduma ya Hifadhi ya jamii ambapo NSSF inawahudumia wananchi kutoka sekta binafsi na sekta isiyokuwa rasmi na kwa upande wa PSSSF wanawahudumia wanawahudumia watumishi wa umma.

Wanachama pamoja na wadau wa Mifuko hiyo wanatakiwa kutumia fursa hiyo kutembelea banda katika viwanja vya sabasaba

Mabadiliko ya mwaka 2018 katika sekta ya Hifadhi ya jamii yalifuta ushindani katika sekta hiyo. Hivyo wananchi wanaandikishwa kwenye mifuko hiyo kulingana na sekta waliopo.
Meneja Kiongozi wa Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF Bi Lulu Mengele akitoa elimu kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na NSSF katika banda la NSSF na PSSSF katika maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa. 
Afisa Uhusiano wa NSSF Bi Aisha Sango akitoa ufafanuzi kwa mgeni alietembelea banda la NSSF na PSSSF katika maonesho yanayoendelea ya kimataifa ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa. 
Meneja Kiongozi wa Uhusiano na Elimu kwa Umma wa PSSSF Bi Eunice Chiume akitoa elimu kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na PSSSF  katika banda la NSSF na PSSSF wakati wa  maonesho yanayoendelea  ya kimataifa ya  Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa. 
Afisa matekelezo wa NSSF Ndugu Abdulaziz Abeid akitoa ufafanuzi kwa mgeni alietembelea banda la NSSF na PSSSF katika maonesho yanayoendelea ya kimataifa ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.
Maafisa Uhusiano wa NSSF (Aisha Sango, Kushoto na Amani Marcel, Katikati) na wa PSSSF (Coleta Mnyamani) wakitoa elimu kwa wageni mbalimbali kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mifuko hiyo katika maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa. 
Afisa Uhusiano wa PSSSF ndugu Abdul Njaidi akitoa ufafanuzi kwa mgeni alietembelea banda la NSSF na PSSSF katika maonesho yanayoendelea ya kimataifa ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa

TIC YAHAMASISHA WAWEKEZAJI KUANZISHA MIRADI YA UWEKEZAJI INAYOLENGA KUONGEZA THAMANI YA MAZAO YA KILIMO

$
0
0
KITUO cha Uwekezaji Tanzania(TIC) kinawahamasisha wawekezaji wazawa na wageni kuanzisha miradi ya uwekezaji inayolenga kuongeza thamani  mazao ya kilimo ili kuzalisha bidhaa kama vile juice, mvinyo, mafuta ya kula, unga, dawa, maziwa, chakula cha mifugo, samaki na uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na mifugo.

Kimesema hayo leo kwenye Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) yanayofanyika  kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam yaliyoanza  Juni 28 Juni, 2019.

Maofisa wa TIC waliokuwa kwenye maonesho hayo wamesema kauli mbiu ya maonesho ni "usindikaji wa mazao ya biashara kwa maendeleo endelevu ya biashara" na kwamba  kauli mbiu hiyo imelenga kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Mhe. Dkt. John Magufuli inayohimiza uanzishaji wa viwanda vya usindikaji.

Wamefafanua kuwa lengo likiwa kuwezesha uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali  zilizoongezwa thamani badala ya kusafirisha malighafi.

 "Lengo ni kuhakikisha  wananchi na Taifa kwa ujumla linanufaika na faida zinazotokana na uwekezaji kwenye mnyororo mzima wa thamani katika sekta ya Kilimo unaohusisha kilimo, usindikaji na biashara kiujumla,"amesema mmoja wa maofisa hao.

Hivyo ili kuunga mkono miradi ya wawekezaji itakayoanzishwa, Serikali inatoa vivutio vya uwekezaji vya  kodi na visivyo vya kikodi kwenye mitambo, mashine na bidhaa nyingine za mtaji zinazohusiana na    mradi. Bidhaa hizo ni zile zinazoagozwa kutoka nje ya nchi.Hata hivyo Wadau  wazingatie kwamba vivutio vya uwekezaji  hutolewa tu kwa miradi iliyosajiliwa na TIC. Lengo ni kusaidia   miradi ya uwekezaji  katika hatua za awali za utekelezaji.

Kwa kujibu wa TIC ni kwamba inawakumbusha wadau  kwamba TIC wanasajili miradi ya uwekezaji inayomilikiwa na wazawa ikiwa na  thamani ya dola za Kimarekani laki moja (100,000) na dola za  Kimarekanilaki tano (500,000) kwa mradi utakaomilikiwa na mgeni au ubia.  Kiasi hicho  pia kinaweza kuwa fedha za Kitanzania zinazolingana na kiasi hicho.

"Kipekee kabisa TIC inawakaribisha wadau (mtu binafsi,kampuni, vyama vya maendeleo na taasisi mbalimbali) kutembelea banda letu ili kupata elimu ya uwekezaji na namna ambavyo wanaweza kunufaika na huduma zetu.  Banda lipo  kwenye hema  la  Jakaya Kikwete (JK),"imesema TIC.
 Ofisa wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Benson Nkini akiweka moja ya bango kwenye banda la kituo hicho lililopo kwenye maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wananchi wakiwa katika banda la TIC wakipata maelezo kuhusu majukumu ya kituo hicho na hasa katika uwekezaji 
Ofisa wa Huduma kwa Wawekezaji Privata Chiwalo akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea banda la TIC

MDAU WA BLOG ZA KIJAMII MABULA KUTOKA NHIF TANGA AACHANA NA UKAPERA

$
0
0

MDAU wa Blog za Kijamii Peter Mabula kutoka ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) kushoto akiwa na Mkewe Jenipher Peter wakiingia kwenye Ukumbi wa Regail Naivera mara baada ya kufunga harusi kwenye Kanisa Katoliki la St.Anthony Chumbageni Jijini Tanga
MDAU wa Blog za Kijamii Peter Mabula kutoka ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) wa pili kutoka kushoto akiwa na Mkewa Janipher Peter wakiwa na wasimamizi waao
MDAU wa Blog za Kijamii Peter Mabula kutoka ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) wa pili kutoka kushoto akiwa na Mkewa Janipher Peter wakiwa na wazazi na ndugu
AMDAU wa Blog za Kijamii Peter Mabula kutoka ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) wa pili kutoka kushoto akiwa na Mkewa Janipher Peter wakiwa na wanafamilia

Sehemu ya wageni waliokuwepo kwenye Sherehe hiyo ya harusi hiyo kulia ni Mhandisi Geofrey Hilly ambaye ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu katika aliyevaa suti akiwa na watumishi wa Mfuko huo wakati wa sherehe ya Harusi ya mtumishi mwenzao Peter Mabula
 ALAWI Kupaza wa NHIF Tanga akitoka kumpongeza Bwana Harusi
 WAFANYAKAZI wanzake na Peter Mabula wakimpongeza
 MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akitoa nasaha kwa Bwana Harusi Peter Mabula kushoto ni Mhasibu wa NHIF Mkoa wa Tanga Hellena Manyanda
 MSIMAMIZI wa NHIF Ofisi ya Tanga Dinna Mlwilo akizungumza wakati wa sherehe hiyo kulia ni Maneja wa NHIF Mkoa wa Tanga Ally Mwakababu 
 MHASIBU wa NHIF Hellena Manyanga akiwa na watumishi wenzake

TAARIFA YA MSIBA

$
0
0
Kerioth George Sanga. Kuzaliwa: 24/06/1950 - Kufariki: 30/06/2019


Tunasikitka kutangaza Msiba wa Baba Yetu Mpendwa Kerioth George Sanga alietutoka tarehe 30/06/2019 katika hospitali ya TMJ Mikocheni. 



Bwana ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

VIONGOZI NA WANANCHI WATEMBELEA BANDA LA BUNGE KATIKA MAONYESHO YA SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Afisa wa Bunge Bw. Patson Sobha akimuelezea jambo Waziri wa Viwanda na Biashara Bw. Innocent Bashungwa alipotembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika Maonyesho ya  43 Kimataifa ya Kibiashara ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
 Afisa wa Bunge Bw. Dickson Bisile akizungumza na Wananchi waliotembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika Maonyesho ya  43 Kimataifa ya Kibiashara ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
 Afisa wa Bunge Bw. Prosper Minja akitoa elimu kuhusu Bunge kwa Wananchi waliotembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika maonyesho ya  43 Kimataifa ya Kibiashara ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mwandamizi wa Bunge Bw. Peter Magati akiwaelekeza jambo Watoto waliotembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika maonyesho ya  43 Kimataifa ya Kibiashara ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa Bw. Daniel Eliufoo (wa kwanza  kulia ) na Afisa wa Bunge Bw. Dickson Bisile wakimsikiliza mwananchi aliyetembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika maonyesho ya  43 Kimataifa ya Kibiashara ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam kwa lengo lakupata ufahamu kuhusu masuala ya Bunge.
 Maofisa wa Ofisi ya  Bunge wakitoa elimu kuhusu Bunge kwa Wananchi waliotembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika maonyesho ya  43 Kimataifa ya Kibiashara ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images