Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Sera ya Ugatuaji wa Madaraka Imekwama Wapi- Waziri Jafo

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Kutokuwepo kwa Sera ya Ugatuaji Madaraka iliyojengwa kwenye mfumo wa Sheria ni moja ya changamoto iliyofanya Serikali kufanya mapitio ya sera hiyo.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo(Mb) wakati wa kufungua kikoa kazi kilichokutanisha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kutoka Mikoa yote 26 kwa ajili ya kutoa maoni na mapendekezo kwenye Rasimu ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji Madaraka ya 2019.
Alisema kuwa changamoto moja wapo ni kutokuwepo kwa sera ya ugatuaji iliyojengwa kwenye mfumo wa kisheria inayoelekeza mipaka, majukumu na utaratibu wa utekelezaji wake, jambo ambalo linafanya ionekane kama ni hiari na utashi (Voluntary and Willingness).
Jafo alisema changamoto nyingine ni kuwepo kwa mitazamo inayokinzana kati ya watendaji na viongozi wa kisiasa katika ngazi ya vijiji, kata na halmashauri katika kuweka vipaumbele na kutekeleza miradi ya maendeleo
Aliongeza kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zimekuwa zikitegemea fedha kwa kiasi kikubwa kutoka Serikali kuu na kutolea mfano kwa mwaka 2018 zilitegemea zaidi ya asilimia 88 ya mapato.
“ Wizara za Kisekta kuandaa sera na sheria na kupeleka halmashauri kwa ajili ya utekelezaji bila kuambatanisha rasilimali fedha, vifaa na watu.”
Waziri Jafo alibainisha kuwa uelewa mdogo wa dhana ya Ugatuaji wa Madaraka (D by D)  kwa baadhi ya Wizara za Kisekta na hivyo Sera hii kuonekana kama ni suala ya OR-TAMISEMI  kwa kiasi kikubwa imechangia kufanya Sera hii kutotekelezeka kwa kiwango kilichotegemewa.
Jafo aliongeza: “Kwa ujumla hatujafikia kiwango cha mafanikio kilichotarajiwa kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeaza na ndio maana Serikali imeamua kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji ili kupata suluhisho la changamoto zilizojitokea.
Aidha, Jafo amewataka wakuu wa mikoa na makatibu tawala kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kutoa maoni na mapendekezo hayo ili kuboresha rasimu hiyo kwa maslahi mapana ya wananchi, wadau na taifa kwa ujumla.
Aidha  Jafo alitumia fursa hiyo kuwahimiza wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa kuhakikisha wanasimamia kwa ukabilifu fedha na utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwamo ujenzi wa vituo vya afya, ujenzi wa hospitali za wilata, ujenzi wa mabweni, madarasa, vyoo katika shule za msingi na sekondari ambayo tayari fedha zake zimeshatolewa na serikali.
Naye Mwenyekiti wa wakuu wa mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng. Evarist Ndikilo aliahidi kushiriki mzuri wa wawakuu hao kwa kuwa wao ndio wanaotoka kwa wananchi.
Pia alimhakikishia Waziri Jafo kuwa watasimamia kwa umakini  utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuwa itakamilika katika muda uliopangwa na kwa ubora unaotakiwa.
Naye Mwakilishi wa UNICEF, Pius Chaya alisema agenda ya mapitio ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji Madaraka imekuja wakati muafaka, kwasababu Serikali inatakiwa kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma wanazostahili na ambazo zinawafikia kwa wakati.
Aidha, Chaya alisema wadau wa maendeo ambao pia wameshiriki katika machakto wa mapitio ya sera hiyo wameahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya awamu ya tano katika kuwaletea wananchi wake maendeleo
Sera ya Ugatuaji wa Madaraka  ni dhana ya Kupeleka Madaraka, Majukumu na Rasilimali kutoka Serikali Kuu kwenda kwa Wananchi kupitia vyombo vya kidemokrasia na Kisiasa ambavyo, wajumbe wake huchaguliwa na kuwajibika kwa Wananchi na vimepewa Mamlaka ya kutoa Maamuzi na kusimamia rasilimali (yaani vina uhuru, vinajitawala, na vina hadhi ya kisheria).
Sera hii ilianza kutekelezwa mwaka 1998 kupitia mpango wa maboresho ya Serikali za Mitaa ikiwa na lengo la kuwawezesha wananchi kushiriki shughuli za Maendeleo katika maeneo yao na kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa shughuli za Serikali.
 Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI  Selemani Jafo akifungua  kikao cha  Wakuu wa Mikoa  na Makatibu Tawala wa Mikoa  cha kupitia rasimu ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga akitoa taarifa ya utangulizi kwenye ufunguzi wa kikao cha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa cha kupitia rasimu ya Sera ya Taifa ya ugatuaji wa madaraka kilichofanyika katika ukumbi wa St. Gasper Jijini Dodoma.
 Baadhi wa Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI  Seleman Jafo wakati akifungua  kikao cha kupitia rasimu ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.
 Baadhi wa Makatibu Tawala wa Mikoa  wakimsikiliza Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI  Seleman Jafo wakati akifungua  kikao cha kupitia rasimu ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (watatu kutoka kushoto aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa mara baada ya kufungua Kikao cha kupitia Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  Selemani Jafo (watatu kutoka kushoto aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala mara baada ya kufungua Kikao cha kupitia Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.


Jumuiya ya Wazazi CCM yaita kikao cha dharura

$
0
0
Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imekutana na kwa dharura katika kikao cha Kamati ya Utekelezaji chini ya Mwenyekiti wake, Dk. Edmund Mndolwa.

Kikao hicho kimefanyika leo Ofisi Ndogo za CCM Lumumba, jijini Dar es Salaa, ambapo kitajadili masuala mbalimbali ya chama.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Siasa na Oganizesheni ya Jumuiya ya Wazazi, Chollaje Mohamed, alisema kuwa kikao hicho kipo chini ya uenyekiti wa Dk. Mndolwa.

"Bado tunaendelea na kikao, ni kako cha dharura cha kamati ya utekelezaji ya Taifa. Pindi kitakapokamilika tutatoa taarifa kamili," alisema Chollaje
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Edmund Mndolwa akizungumza kwenye Kikao cha dharura cha kamati ya utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Taifa kilichofanyika leo katika ukumbi wa ofisi Ndogo ya  CCM Lumumba jijini Dar es Salam.
Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho

UWT IRINGA, DC WAUNGA MKONO KAZI INAYOFANYWA NA RAIS DKT MAGUFULI

$
0
0
Hii ndio ya pongezi iliyotolewa na UWT Iringa Dc kwa Rais Dkt John Joseph Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa.

Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Iringa Lena Hongole akiongea kwenye kongamano hilo lilofanyika katika kijiji cha Kisinga' kata ya Kising'a lakini pia viongozi mbalimbali walishiriki kongamano hilo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Daktari Abery Nyamahanga akitoa neno kwa UWT wakati wa kongamano la kumpongeza Rais Daktari John Joseph Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa.
Baadhi ya madiwani wa chama cha mapinduzi wakiwa wameshiriki katika kongamano hilo la UWT la kupongeza Rais Daktari John Joseph Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa





NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Umoja wa wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Iringa wamefanya kongamano la kuunga mkono juhudi na kazi zinazofanywa na Rais Daktari John Joseph Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa.

Akizungumzia malengo ya kongamano hilo Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Iringa Lena Hongole amesema kuwa Rais amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo kwa wananchi waliomchagua 2015.

“Sisi wanawake wa wilaya ya Iringa tunampongeza sana Rais Daktari John Joseph Magufuli kwa kazi kubwa ya kuleta maendeleo wananchi waliomchagua kwa kipindi hiki kifupi tangu aingie madarakani”alisema HongoleHongole alisema kuwa Tanzania inakuwa kimaendeleo kwa kasi kubwa kutokana na uongozi wa Rais ambapo amefanikiwa kuwajenga watanzania kuwa wazalendo kwa kufanya kazi na kujituma kuhakikisha wanapata maendeleo.

“Mafanikio yenye tija tunayaona hivi sasa hivyo sisi kama wanawake hatuna haja ya kushindwa kumpongeza Rais wetu ambaye amekuwa kiungo muhimu cha maendeleo ya nchi hii hivi sasa” alisema Hongole

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Daktari Abery Nyamahanga amewapongeza wanawake hao kwa kuunga mkono juhudi za Rais.

“Nyinyi akina mama mmekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi hizi ambazo zinazaa matunda ya kuleta maendeleo ndio maana tunaiona hata iringa inazidi kupata maendeleo kila kukicha tunaona sura mpya ya maendeleo ya nchi” alisema Nyamahanga

Nyamahanga alisema kuwa Rais Daktari John Joseph Magufuli amefanya mambo makubwa kwa kipindi kifupi kwa kuboresha sekta ya afya ,sekta ya elimu,uchumi,miundombinu na utalii na kufanikisha maendeleo haya tunayoyaona hivi sasa.

“Hakuna mtanzania ambaye haoni nini kinafanyika katika nchi hii kwa kila mtu mwenye macho na masikio anajionea na kusikia maana hakuna ubishi kuwa Rais huyu amekuwa mzalendo kweli kweli katika nchi yetu hii” alisema Nyamahanga

Nyamahanga aliwataka wanawake hao UWT kukumbuka juu ya chaguzi zinazokuja hivi karibuni kuhakikisha wanakuwa na Wagombea ambao wanakubarika katika jamii ili kuhakikisha CCM wanashinda kwa kishindo.

“Wakina mama hakikisheni kama mnasifa ahakikisheni mnajitokeza kwa wingi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye chaguzi hizi zinazokuja na kuhakikisha tunamuunga mkono mgombea wa CCM na sio kutoka nje ya chama chetu” alisema Nyamahanga

Naye Diwani wa kata ya Kising’a Bi Ritta Mlagala amesema toka mwaka 2015 hadi sasa wamefakiwa kuboresha sekta ya afya na elimu kwa kutekeleza ilani ya CCM ya 2015 hadi 2020.

“Tumefanikiwa kujenga kituo cha afya,kuendelea kujenga majengo mapya ya shule ya sekondari ya Ilambilole iliyopo kata ya Kising’a na tumejenga madarasa manne na ofisi mbili katika shule msingi kising’a hivyo hayo ndio maendeleo yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano” alisema Mlagala

Aidha Mlagala alisema kuwa wameanza kujenga zahanati ya kijiji cha Mkungugu na nyumba ya waaguzi ambazo zote zinatarajia kukamilika hizi karibuni licha ya kuwa na changamoto kadhaa ambazo zinatusukuma kuhakikisha tunatafuta wadau watuunge mkono kumalizia.

KAYA 200 ZENYE MAISHA DUNI HUKO KATA YA VIGWAZA ZAPATIWA MSAADA WA BAADHI YA VYAKULA-MEESAM

$
0
0
 NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO
SHIRIKA linalosaidia watu wenye maisha duni na kuleta mabadiliko chanya katika jamii (WHO IS HUSSAIN?), tawi la Dar es salaam kwa kushirikiana na diwani wa kata ya Vigwaza Mohsin Bharwani ,limetoa msaada wa vyakula kwa kaya 200 zilizopo kwenye kata hiyo,uliogharimu sh.milioni kumi.

Kila kaya kati ya hizo imepatiwa box lenye vitu vilivyogharimu sh. 50,000 ,ikiwemo mchele kilo 3, maharage kilo tatu, sukari kilo 3, majani ya chai, tende na tambi ili kuwasaidia katika mwezi mtukufu wa Ramadan.

Akikabidhi msaada huo, mratibu msaidizi wa shirika la Who is Hussain?, tawi la Dar es salaam Meesam Bandali amesema,walengwa ni watu wasio na uwezo wakiwemo wenye ulemavu,wazee katika kaya 200 kata ya Vigwaza.
Awali diwani wa kata ya Vigwaza, Mohsin Bharwani, amelishukuru shirika hilo kwa kumfuata kumuomba kupeleka msaada kwa kaya zinazoishi kwenye mazingira magumu.

Nae msemaji mkuu wa who is Hussain? Iffet Thawer ameeleza Hussain ni mjukuu wa mtume Mohammad S.W.A. ambae alipinga dhuluma hivyo kuwa chanzo cha wao kuhamasika kufanya shughuli za kusaidia jamii ikiwa sasa ni miaka kumi .

WAKALA WA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR NA WADAU WA AFYA WAJADILI MUONGOZO WA DAWA WA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Na Miza Kona Maelezo Zanzibar
Wakala Chakula na Dawa imeanza kujadili muongozo maalum uliotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki wenye lengo la kuinusuru jamii na athari zitakanazo na matumizi ya dawa ambayo hatimae husababisha madhara mbalimbali kwa wananchi.

Hayo yameelezwa na Afisa kutoka Wakala wa Dawa na Chakula Mohammed Omar kwenye Ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe katika kikao cha wadau kinachojadili hatua zinazofaa kuepukana na madhara ya dawa na vifaa tiba.

Amesema lengo la kikao hicho ni kutengeneza Muongozo ambao utawezesha kufuatilia madhara ya dawa, vifaatiba, tiba asili pamoja na chanjo ili kupata jamii yenye afya bora na kuepukana na maradhi yanayotokana na matumizi ya dawa.

Amesema muongozo huo pia utaweza kusaidia kuripoti, kuziwakilisha na kizitambua kuchunguza na kufuatilia dawa ambazo zinaleta madhara kwa jamii na kuzitafutia hatua za kuzipatia ufumbuzi kwa kutumia njia muafaka bila ya kubadilisha dhamira iliyowekwa na Jumuiya hiyo

Amefahamisha kuwa kumekuwa na matatizo makubwa ya madhara ya dawa ambazo husababisha kupata maradhi yasiyoambukiza kutokana na jamii kutotumia dawa bila ya kiwango kinachotakiwa.

“Dawa zina faida lakini pia madhara kadri unavyotumia dawa ndio madhara yanapoonekana hivyo tumeandaa muongozo wa kuweza kuzitambua dawa zenye kuleta madhara kwa jamii na kuzifanyia kazi kwa kuzifutia na kuzitambua ili kuweza kuisadia jamii”, alieleza Afisa huyo.

Alisema wameweka fomu kila kituo cha Afya na hospitali kuzitambua dawa ambazo zinaleta madhara kwa jamii kwa kila mtumiaji ambae atapata madhara baada ya kutumia ili kupata ufumbuzi na kuisadia muongozo huo kufanyakazi yake lakini changamoto kubwa iliopo urejeshaji wa fomu hizo ni mdogo.

Nae MratibuMsaidizi wa Kitengo Shirikishi Ukimwi, Homa ya Ini, Kifua Kikuu na Ukoma Issa Abeid Mussa amesema muongozo huo utaweza kujadi namna ya ufuatiliaji wa dawa na kuratibu athari zinazotokana na madhara utumiaji wa dawa

Ameitaka Wakala wa Dawa na Chakula kuangalia kwa kina na kuzifuatilia dawa zote zinazoingizwa nchini kabla ya kuzisambaza katika vituo na kuzitumia ili kuepuka madhara kwa jamii.
 MratibuMsaidizi wa Kitengo Shirikishi Ukimwi, Homa ya Ini, Kifua Kikuu na Ukoma Issa Abeid Mussa akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uangalizi wa Dawa zikiwa sokoni katika Mkutano wa siku sita wa kujadili athari zitokanazo na dawa uliofanyika Ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.
Wadau wa Dawa na Vifaa tiba wakijadili mwangozo uliotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki wenye lengo la kuhakikisha matumizi ya dawa na vifaa tiba havileti madhara kwa wananchi katika Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe. Picha na Makame Mshenga.

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA JESHI LA POLISI MKAONI MBEYA

$
0
0

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WANNE WA TUKIO LA MAUAJI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wanne waliofahamika kwa majina ya:-
1.      JAPHET YAHAYA NGUKU [37] Mkazi wa Msewe – Igurusi Wilaya ya Mbarali
2.      AGATHA FRANCIS [30] Mkazi wa Mbalizi.
      3. ANDREW ANGANILE MWAMBULUMA [43] Mkazi wa Mapinduzi - Mbalizi
      4. MEJA JOTAM SANGA @ MESIA [48] Mkazi wa Ikonda Mkoa wa Njombe kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wa miaka sita [06] aitwaye ROSE JAPHET Mkazi wa Kijiji cha Msewe, Wilayani Mbarali.

Ni kwamba mnamo tarehe 03.05.2019 majira ya saa 21:00 usiku huko Kijiji cha Msewe kilichopo Kata ya Igurusi, Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya katika msitu wa hifadhi wa Chimala Mtoto aitwaye ROSE JAPHET [06] alikutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na kukatwa kanyagio la mguu wa kushoto pamoja na kiganja cha mkono wa kushoto ambapo kanyagio la marehemu limekutwa limefukiwa huko Mbalizi, Wilaya ya Mbeya Vijijini.

Chanzo cha tukio hili ni tamaa ya kupata utajiri ambapo baba mzazi wa marehemu aitwaye JAPHET YAHAYA NGUKU alimtoa mwanae kwa ANDREW ANGANILE MWAMBULUMA ambaye ni mfanyabiashara kwa malipo ya Tshs 5,000,000/= ili auwawe na kisha kukatwa kanyagio la mguu wa kushoto na kiganja cha mkono wa kushoto na kupatiwa mfanyabiashara huyo ili apeleke kwa mganga aitwaye MEJA JOTAM SANGA @ MESIA [48] ili amtengenezee ndagu (dawa ya utajiri) ili afanikiwe katika  biashara zake za Shule anayoimiliki iitwayo Shule ya Sekondari Ushindi iliyopo Mbalizi.
  
KUPATIKANA NA MALI YA WIZI GARI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili waliofahamika kwa majina ya:-
1.      ABRAHAM NSAJIGWA [37] Mkazi wa Forest
2.      FESTO ZAKARIA [35] Mkazi wa Ilemi
Kwa tuhuma ya kupatikana mali ya wizi gari lenye namba ya usajili T.899 DCW aina ya Noah rangi nyeusi.
Watuhumiwa wamekamatwa mnamo tarehe 12.05.2019 saa 02:00 usiku huko maeneo ya Isanga, Kata ya Isanga, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya. Gari hiyo iliibwa huko Temeke Mkoani Dar es Salaam ambapo baada ya tukio hilo, taarifa zililifikia Jeshi la Polisi na kuanza msako na jana kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na gari hilo.

TAARIFA YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MKOA WA MBEYA.

Kutokana na mvua zilizoanza kunyesha tangu tarehe 29/04/2019 hadi sasa Mkoani Mbeya zimesababisha uharibifu wa nyumba na mali yakiwemo mazao mbalimbali hasa katika Wilaya ya Rungwe na Kyela.

Katika Wilaya ya Rungwe huko Mtaa wa Igamba, Kata ya Bulyaga, Tarafa ya Tukuyu Mjini mvua iliyonyesha usiku wa tarehe 12.05.2019 zimesababisha hatari ya kuweza kuleta majanga ikiwemo kubomoka kwa nyumba za wakazi wa maeneo hayo.

Katika Wilaya ya Kyela mvua hizo zimesababisha uharibifu wa makazi ya watu na majengo hasa Shule ya Msingi Mwaya iliyopo Kata ya Mwaya kwani imezingirwa na maji. Pia maeneo ya Kata ya Mwaya na Tenende mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha nyumba zilizopo maeneo hayo kuzingirwa na maji.

           Imetolewa na:
 [ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Zanzibar kufanya Utafiti wa kugundua mmomonyoko unaopelekea kudidimia kwa Ardhi

$
0
0
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif Mohamed Kulia na Mhadhiri Muandamizi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar {SUZA} Dd. Zakia Mohamed Abubakar wakitia saini Mkataba wa kufanya Utafiti kugundua sababu zinazopelekea Zanzibar kuathiriwa na tatizo la mmongo’nyoko unaopelekea kudidimia kwa ardhi. Wa kwanza kulia aliyefika kushuhudia utiaji saini Mkataba huo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed.

Baadhi ya Wakurugenzi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nchi Ofisdi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed akizungumza mara baada ya kumalizika kwa utiaji saini Mkataba huo.
Mhadhiri Muandamizi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar {SUZA} Dd. Zakia Mohamed Abubakar akielezea faraja yake kutokana na Serikali Kuu kuwaamini kuwapa fursa ya kutumia ujuzi wao katika masuala ya utafiti. Picha na – OMPR – ZNZ.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana saini Mkataba na Wataalamu wa chuo kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) ili kufanya tafiti kugundua sababu zinazopelekea Zanzibar kuathiriwa na tatizo la mmongo’nyoko unaopelekea kudidimia kwa ardhi katika baadhi ya maeneo hasa wakati wa kipindi cha mvua kubwa zinaponyesha.

Utafifiti huo utakwenda sambamba na kuchunguza mbinu mbadala zinazoweza kutumika katika kuondosha takataka zitokanazo na mali ghafi za platiki ambazo zimekua chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira kwa muda mrefu ndani ya Zanzibar hali inayosababisha athari juu ya mripuko wa maradhi katika jamii.

Mkataba huo umetiwa Saini na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif Mohamed kwa upande wa Serikali na Uongozi wa Chuo Kikuu ca Taifa Zanzibar ukatiwa na Mhadhiri Muandamizi wake Dr. Zakia Mohamed Abubakar.

Akizungumza mara baada ya utiaji saini huo katika ukumbi wa Kamati ya Sheria Baraza la wawakilishi Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud Mohamed alisema kitendo hicho kinachofanywa na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kitakuwa cha kihistoria ambacho matokeo yake yatavinufaisha vizazi vya sasa na vile vijavyo.

Waziri Aboud alisema ni kipindi cha muda mrefu sasa Zanzibar imekuwa ikikumbwa na tatizo la kudidimia kwa Aridhi katika maeneo mbali mbali ya unguja hasa inapowadia kipindi cha mvua kubwa hali inayozusha hofu kwa jamii na wakaazi wanaoishi katika maeneo yanayokubwa na kadhia hiyo.

“Kumekuwepo na tatizo katika visiwa vyetu hivi kila mvua kubwa zinaponyesha basi baadhi ya maeneo hudidimia na kutoa taharuki kwa serikali pamoja na wakaazi wa maeneo hayo” Alisema Mhe. Aboud

Sambamba na hayo alisema kutiwa saini kwa mkataba wa kufanyika utafiti kumempa imani na furaha kubwa kwani kitendo hicho kinaashiria kulipatia ufumbuzi tatizo ambalo wananchi wamekua wakipatwa na wasi wasi yanapotokea akitolea mfano kutokea kwa kudidimia kwa aridhi katika eneo la Jango’ombe mshelishelini, Kwerekwe “C” Mombasa na Tukio la juzi pembezoni mwa Madrasa Ismailia na Msikiti wa Mwanakwerekwe.

Akilitolea ufafanuzi tatizo la takataka pamoja na pemapasi Waziri Aboud alisema watafiti hao wana kazi ya kulichunguza kwa kina jambo ili kuja na suluhisho la kudumu juu ya mbinu mbadala zinazoweza kutumika ili jamii iondokane na kadhia hiyo huku akiwa na imani kwamba watafiti hao wataifanya kazi yao kwa ufasaha wa hali ya juu.

Nae Muhadhiri muandamizi kutoka chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar {SUZA} Dk. Zakia Mohamed Abubakar alisema watafiti kutoka chuoni hapo wanaishukuru serikali ya mapInduzi Zanzibar kwa kuwapa imani kubwa Ya kuwapatia kazi ya kufanya tafiti mbili ile ya kudiDImia kwa ardhi na tatizo la taka za plastiki na Pempasi na kuahidi kuwa wataifanya kazi hiyo kwa uweledi mkubwa katika kutokomeza tatizo hilo.

Dk. Zakia alisema timu ya watalamu hao itafanya kazi kwa ustadi ili kubaini kiini halisi cha tatizo hilo ili iwe rahisi kutoa maelekezo kwa wananchi juu ya sababu zinazopelekea kutokea kwa matukio hayo.

Aidha alisema jamii inapaswa kuondosha hofu juu ya matukio hayo kwani baadhi ya wakati hali hiyo inaweza kusababishwa na aina ya udogo au kutembea kwa udongo chini ya ardhi.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Ndu. Abdalla Hassan Mitawi alisema serikali imeamua kufanya tafiti hizo kusudi kubaini chanzo cha tatizo na alieleza kuwa matukio ya utafiti huo yatakapowasilishwa itaisaidia serikali kufahamu hatua za kuchukua kwa lengo la kupunguza athari hizo kwa wananchi wake.

Naibu katibu Mitawi Alisema matukio ya tafiti kwa upande wa matumizi ya plastiki na pempasi yataiwezesha serikali kubuni njia mbadala za kutumia ili kuviepushia visiwa vya Zanzibar kukumbwa na athari zinazoweza kuepukika.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa utafifiti na shahada za juu Dk. Makame Omar Makame alifafanua kuwa timu ya watalamu hao itajitahidi kuzifanya tafiti hizo kwa umahiri ili ije maelezo sahihi ndani ya kipindi cha muda mfupi kutokana na tatizo la taka za plastiki na pempasi kuzagaa kwa wingi mitaani hali inayosababisha kipindi cha mvua kubwa maji kutuwana na kuleta athari katika sehemu za makaazi ya wananchi.

Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na China lafanyika Arusha Inbox x

$
0
0


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki akizungumza wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na wawekezaji kutoka Jimbo la Zhejiang la China lililofanyika jijini Arusha tarehe 13 Mei 2019. Katika hotuba yake Mhe. Kairuki alisisitiz akuwa Tanzania ni eneo salama zaidi kuwekeza barani Afrika kutokana na sababu za msingi kama amani, mazingira na sheria rafiki za uwekezaji pamoja na maeneo lukuki ya kuwekeza kama kilimo, madini, usindikaji, viwanda na utalii. Kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Serikalini na Sekta binafsi liliwahusisha sehemu ya watalii 300 waliowasili nchini kwa ziara ya kitalii ya siku nne.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Caesar Waitara kwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Jeri Muro wakifuatilia hotuba ya Mhe. Kairuki hayupo pichani
Wadau mbalimbali wakishiriki kongamano hilo
Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki naye akifuatilia matukio wakati wa kongamabo la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China lililofanyika Arusha
Mhe. Waziri Kairuki akiendelea na hotuba yake huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqarro wakisikiliza
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Bw. GodfreySimbeye akizungumza
Mdau kutoka China naye akiwasilisha mada
Sehemu ya wawekezaji kutoka China wakifuatilia kongamano lililoandaliwa na Tanzania kwa ajili yao
Sehemu ya wadau kutoka Tanzania nao wakifuatilia kongamano
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na Mhe, Daqarro wakati wa kongamano hilo
Wadau wakifuatilia kongamano
Kongamano likiendelea

Waziri Kigwangallah azindua mpango wa kuwafungaTembo mikanda ya GPS utakaogharimu sh milioni 800 Inbox x

$
0
0
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangallah leo  amezindua mpango wa kuwafunga mikanda ya mawasiliano ya kijiographia(GPS) Tembo ambao wanapatikana hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Makao na Pori la Akiba la Maswa
 Maandalizi ya kumfunga tembo GPS 

 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangallah (kushoto) na Mkuu wa Mmkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakiangalia tembo aliyefungwa GPS. 
Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund(FCF) Nicholas Negri akizungumza kuhusu mradi huo utasaidia sana uhifadhi nchini na kuvutia watalii zaidi.

Mwandishi wetu,Arusha.

Zaidi ya sh 800 milioni zinatarajiwa kutumika katika zoezi la kuwafunga mikanda ya mawasiliano ya kijiographia(GPS) Tembo ambao wanapatikana hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Makao na Pori la Akiba la Maswa.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangallah leo  amezindua mpango huo katika eneo la Makao WMA ambalo imewekeza kampuni ya Mwiba Holding moja ya kampuni zilizochini ya Taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF)

Waziri Kigwangala alisemaVifaa hivyo il vya GPS vitawezesha Tembo kufatiliwa mienendo yao na kudhibitiwa matukio ya Tembo kuvamia mashamba na masuala ya ujangili.

Alisema katika mpango huo pia kutakuwa na uzio wa technolojia ya kielekronik ambao utawezesha kuonekana Tembo ambao wanatoka maeneo ya hifadhi kabla ya kufanya madhara.

Waziri Dk Kigwangallah alipongeza taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF) kwa kufadhili mradi huo na kueleza wizara yake ilifanya utafiti na kubaini taasisi hiyo ni miongoni mwa taasisi safi zinazoendekeza uhifadhi.

Waziri Kigwangallah pia alipongeza watafiti kutoka taasisi ya utafiti wa wanyamapori(TAWIRI) kwa kuendesha zoezi hilo.Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund(FCF) Nicholas Negri alisema mradi huo utasaidia sana uhifadhi nchini na kuvutia watalii zaidi.

Alisema FCF itaendelea kishirikiana na serikali katika kuendeleza uhifadhi kwani pia tayari wamefadhili mradi wa kuwafunga vifaa vya mawasiliano Faru ili kuwalinda na ujangili.Mtafiti Mkuu wa TAWIRI, Dk Edward Kohi amesema mradi huo,unatarajia kugharimu dola 300,000 ambazo ni zaidi ya sh 800 milioni.

Amesema katika eneo la hifadhi ya jamii ya makao na pori la akiba la Maswa Tembo 18 watafungwa vifaa vya GPS na katika maeneo mengine tayari Tembo 95 wamefungwa GPS.Mtafiti wa Tawiri Dk Emmanuel Masenga amesema hadi sasa Tembo 95 wamefungwa mikanda ya GPS maeneo mbali mbali ya hifadhi nchini.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo ,Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Anthony Mtaka alisema mpango huo wa kuwafunga Tembo GPS utasaidia kuondoa migogoro baina ya wa hifadhi na jamii.Alisema wananchi wamekuwa wakipiga simu mara kadhaa kuomba msaada pale Tembo wanapovamia mashamba yao.

"Sasa Tembo kufungwa GPS ni faraja kwetu lakini pia tunapongeza mwekezaji wetu Mwiba Holdings kwa  mradi huo" alisema

Prof. Kabudi akutana na Bodii ya AICC

$
0
0

Mhe. Prof. Kabudi akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya AICC, Balozi mstaafu, Ladis Komba (kulia) alipokuwa akimpatia taarifa fupi kuhus bodi hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi, Balozi Brigedia Jenerali (mst.), Francis Mndolwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC, Bw. Elishilia Kaaya.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kwa ajili ya kukutana na Bodi ya Kituo hicho ikiwa ni mkutano wake wa kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo mwezi Machi 2019. Mkutano huo ulifanyika jijini Arusha tarehe 13 Mei 2019 

MKAZI WA MBAGALA,DAR AKABIDHIWA KITITA CHAKE CHA MILIONI 5 KUTOKA BIKO

Songas yachangia milioni 47 kuboresha miundombinu ya elimu shule ya msingi Ubungo kisiwani

$
0
0
Mkurugenzi mtendaji wa Songas, Nigel Whittaker akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya milioni 47 Mwenyekiti wa mtaa wa Kibangu, Bw Desidery Ishengoma katika shule ya msingi Ubungo Kisiwani mapema leo, Kampuni hiyo ya uzalishaji wa gesi nchini Tanzania imetoa msada huo kama mchango wao katika kuisaidia serikali kuboresha miundombinu ya elimu nchini.
 PIC 3&2: Mkurugenzi mtendaji wa Songas, Nigel Whittaker akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya TZS milioni 47 kwa wanafunzi wa Ubungo Kisiwani mapema leo, Kampuni hiyo ya uzalishaji wa gesi nchini Tanzania imetoa msada huo kama mchango wao katika kuisaidia serikali kuboresha miundombinu ya elimu nchini.

EALA SWEARS IN TANZANIA’S FOREIGN AFFAIRS & EAC MINISTER AS EX-OFFICIO MEMBER

$
0
0

…Hon Prof Kabudi pledges support for the integration process

East African Legislative Assembly, Arusha, Tanzania: May 13th, 2019: The Minister for Foreign Affairs and East African Co-operation, United Republic of Tanzania, Hon Prof Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi this afternoon took Oath of Allegiance as an Ex-Officio Member of the Assembly.

Hon Prof Kabudi was sworn in by the Clerk to the Assembly at a brief ceremony witnessed by the Speaker and Members of EALA in line with the Rule 5 of the Rules and Procedures of the Assembly. The Rule 5(4) of the Rules of Procedure says in part that: “No Member can sit or participate in the proceedings of the House until the Oath or Affirmation of Allegiance to the Treaty is taken”.

Rule 5(5) specifically states that “when a Member first attends to take his or her seat other than at the first Sitting of a new House, he or she shall be brought to the table by two Members and presented by them to the Speaker who shall then administer the Oath or Affirmation of Allegiance”.

Hon Prof Kabudi was ushered in to the House by EALA Members, Hon Mohammed Habib Mnyaa, Hon Fancy Nkuhi, Hon Leontine Nzeyimana and Hon Kasamba Mathias. EALA Speaker, Rt Hon Ngoga Karoli Martin congratulated Hon Prof Kabudi upon his swearing in – as he assumes his ex-officio role in the regional August House.

Hon Dr Kabudi was appointed to the Ministry by H.E. John Pombe Joseph Magufuli in March 2019, replacing Hon Dr Augustine Mahiga who moved to the docket of the Constitutional and Legal Affairs Ministry. Professor Kabudi is deputized at the Ministry of Foreign Affairs and East African Co-operation by Hon Dr Damas Ndumbaro.

Prior to the appointment as Minister for Foreign Affairs and East African Co-operation, Hon. Prof. Kabudi was the Minister for Constitutional and Legal Affairs from March 2017 to March 3, 2019. Prior to joining cabinet, Hon Prof. Kabudi was a Professor of Law at the University of Dar es Salaam with a wide-ranging academic expertise and long experience in public service and consultancy.

At the University of Dar es Salaam, he served as Dean of the Faculty of Law after having served as Associate Dean and Head of Department of International Law. At different intervals during his academic career, Prof. Kabudi was seconded to the Government as National Coordinator in the Vice President’s Office for review of institutional framework for environmental management in Tanzania and the drafting of the Environmental Management Act and its regulations. 
 
Prof. Kabudi has been a consultant to the Government of Tanzania on review and drafting of laws in areas of natural resources and water resources financed by the World Bank and other donor agencies in Tanzania and East Africa. Prof. Kabudi is a renowned Public Law expert having also served as a member of the Constitutional Review Commission that was tasked to draft a new Constitution.

Hon Prof Kabudi holds a Bachelor of Laws Degree – First Class honors (LL.B. Hons) and Master of Laws (LL.M) from University of Dar es Salaam and a Doctorate Degree in Laws (Dr. Jur) from the Freie Universtaet Berlin (FU Berlin), Germany.

In his maiden statement on the floor today, Prof Kabudi assured the House of his commitment to ensure integration is realized. “Coming together as the EAC is not a matter of choice, but it is necessitated by geographical proximity, culture and the region’s geopolitics. Mr Speaker, I commit to do my best to spearhead the EAC Integration”, Hon Prof Kabudi said. Prof Hon Kabudi appreciated the work done by his predecessor, Dr Augustine Mahiga.

SERIKALI YAKATA RUFAA KUPINGA UAMUZI WA MAHAKAMA KUU

$
0
0
*Ni kuhusu unaokataza wakurugenzi kusimamia uchaguzi
*Yataka nakala halisi ya uamuzi, mwenendo wa shauri

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

OFISI ya Wakili Mkuu wa Serikali imewasilisha Mahakama ya Rufaa Tanzania notisi ya kukataa rufaa kupinga sehemu ya uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu kuhusu uamuzi wa mahakama hiyo katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Bob Chacha Wangwe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wenzake kupinga vifungu vya sheria ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu wasimamizi wa uchaguzi.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imesema pia pamoja na notisi hiyo Serikali imeomba kupatiwa nakala ya uamuzi na mwenendo wa shauri hiyo na kufafanua kutoka na taarifa hiyo ya Serikali uamuzi ambao umetolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania katika kesi hiyo hauna nguvu kisheria.

Akizungumza leo Mei 13,2019 jijini Dar es Salaam , kabla ya kutoa msimamo huo wa kukata rufaa kuhusu uamuzi huo wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Adelardus Kilangi ameeleza Mei 10 mwaka huu Mahakama hiyo Kanda ya Dar es Salaam ilitoa uamuzi kuhusu shauri la kikatiba Na 17 la mwaka 2018.

Ambalo lilifunguliwa na Bob Chacha Wangwe kupinga baadhi ya vifungu vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ,sura ya 343 kama ilivyorekebishwa vinavyohusu uteuzi wa wasimamizi wa uchaguzi vinakinzana na Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho.

Amesema uamuzi huo ulitolewa na jopo la majaji watatu ambao ni Jaji Dkt.Atuganile Ngwala, Jaji Dkt.Benhaji Masoud na Jaji Firimin Matogolo na kwamba shauri hilo lilifunguliwa chini ya Sheria ya utekelezaji wa haki za msingi na wajibu sura ya tatu ya sheria za Tanzania.

Ameongeza shauri hilo lilifunguliwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mkurugenzi wa Uchaguzi. "Bob Chacha Wangwe ambaye alijitambulisha kama mpiga kura, alitaka Mahakama Kuu kuvitamka na kuvifuta baadhi ya vifungu sheria ya taifa ya uchaguzi kwa madai kuwa vinakinzana na ibara za Katiba."

Amevitaja vifungu hivyo ni kifungu cha 6(1) cha sheria ya taifa ya uchaguzi sura 343 kinachomtambua mkurugenzi wa uchaguzi ambaye ameteuliwa na Rais wa Tanzania kutoka katika utumishi wa umma.

Ambapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali amefafanua mlalamikaji alitaka kifungu hicho kibatilishwe kwa madai kuwa kinakinzana na ibara ya 21(1), 21(2) na 26(1) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

Pia wasimamizi wa uchaguzi, wakurugenzi hao hubanwa na masharti yanayosimamia uchaguzi chini ya sheria za uchaguzi. Katika utekelezaji wa jukumu la usimamizi, wakurugenzi hao huwajibika chini ya sheria ya sheria ya uchaguzi na si vinginevyo.

Kuhusu kifungu cha 7(2) , kinachotaka tume ya taifa ya uchaguzi, kuteuwa watumishi wa umma kusimamia chaguzi zinazoratibiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Serikali inaeleza kuwa hakikinzani na ibara ya 21(1) , 21(2) na 26(1) ya Katiba ya Tanzania.

"Zipo taratibu mbalimbali zinazozingatiwa wakati wakurugenzi hao na watumishi wengine wa umma wanapotakiwa kuhusika kusimamia uchaguzi ikiwemo viapo vya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, umakini bila upendeleo,"amesema.

Akizugumzia kifungu cha 7(3), kinachoipa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mamlaka pale inapoona inafaa, kuteuwa wasimamizi wa uchaguzi kutoka miongoni mwa watumishi wa umma kuwa wasimamizi wa uchaguzi, Serikali ilieleza kuwa kifungu hichi hakikinzani na ibara hiyo ya 21(1),21(2) na 26(1) ya Katiba ya Tanzania.

"Utaratibu wa uteuzi wa watumishi wa umma kwenye uchaguzi, utazingatia sheria na kanuni za uchaguzi, na watumishi hao wanapotekeleza wajibu, wanazingatia sheria husika za uchaguzi,"amesema.


UAMUZI WA MAHAKAMA KUU

Akizungumzia uamuzi wa Mahakama hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema baada ya kusikiliza hoja za pande mbili ,Mahakama Kuu imeamua kwamba imeridhia uhalali wa Katiba wa kifungu cha 6(1) , sheria ya Taifa ya uchaguzi kinachomtambua Mkurugenzi wa Taifa wa uchaguzi ambaye anateuliwa na Rais kuendelea kusimamia chaguzi.

Pia imeridhia uhalali wa Kikatiba wa kifungu cha 7(2) cha sheria ya uchaguzi kinachoipatia mamlaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuteuwa wasimamizi wa uchaguzi kutoka miongoni mwa watumishi wa umma.

"Mahakama imethibitisha kifungu cha 7(1) na 7(3) vinavyowataka wakurugenzi wa majiji, halmashauri, miji na wakurugenzi wa wilaya pamoja na wateuliwa wa Tume ya uchaguzi kutoka katika utumishi wa umma kusimamia uchaguzi kwa kuwa vinakinzana na ibara ya 3.

"Kifungu cha 7(1) cha sheria ya taifa ya uchaguzi kinachowataka wakuregenzi wa majiji ,manispaa, miji na halmashauri za wilaya kusimamia chaguzi kwa madai kuwa kifungu hicho kinakinzana na ibara ya 21(1), 21(2) na 26(1) ya Katiba.Kifungu cha 7(2) kinachoitaka tume ya taifa ya uchaguzi kueteua watumishi a umma kusimamia chaguzi zinazoratibiwa na tume hiyo kwa madai kuwa zinakinzana na kuvunja haki ya msingi ya uhuru na wajibu unaolindwa na ibara ya 21(2), 21(2) na 26(1) ya Katiba,"amesema.

Pia amesema kifungu cha 7(3) kinachoipa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mamlaka pale inapoona inafaa kuteua wasimamizi wa uchaguzi kutoka miongoni mwa watumishi wa umma kuwa wasimamizi wa uchaguzi.Badala ya wakurugenzi wanaotajwa na sheria kusimamia uchaguzi, na pale ambapo tume inawateua watumishi wa umma basi wakurugenzi tajwa wanakoma kuwa wasimamizi. "Mlalamikaji alipinga kifungu hiki kwa madai kuwa kinakinzana na ibara ya 21(1), 21(2) na 26(1) ya Katiba,"amesema.


KUHUSU UTETEZI WA SERIKALI

Amesema katika utetezi wake Serikali ilipinga madai hayo kwa kuwa hayakuwa na msingi.Kwenye maelezo ya utetezi, Serikali kupitia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ilitao hoja kadhaa.

Ametaja hoja hizo kuwa kuhusu kifungu cha 6(1) cha sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura 343 kinachompa mamlaka Rais aliye madarakani kuteua mkurugenzi wa uchaguzi kutoka katika utumishi wa umma, Serikali ilieleza kifungu hicho hakikinzani na ibara ya 21(1) 21(2) nq 26(1) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

Pia amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Sheria ya Taifa ya uchaguzi imeweka misingi na utaratibu wa uteuzi wa mkurugenzi wa uchaguzi na kuwa na mkurugenzi huyo atatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa masharti yaliyomo kwenye Katiba, sheria ya uchaguzi na kanuni zinazoongoza uchaguzi.

Kuhusu kifungu cha 7(1) cha sheria ya Taifa ya uchaguzi kinachowataka wakurugenzi wa majiji, manispaa, miji na halmashauri za wilaya kusimamia chaguzi kwa madai kifungu hicho kinakinzana na ibara ya 21(1), 21(2) na 26(1) ,Serikali ilienza kuwa Katiba kama sheria mama imetoa fursa kwa Bunge kutunga sheria mbalimbali na kwamba uteuzi wa mkurugenzi wa uchaguzi unaofanywa na Rais unazingatia sheria za nchi.

"Japokuwa wakurugenzi wanateuliwa na Rais aliyepo madarakani , wanapohusika kama 74(14) ya Katiba inayozuia anayehusika na uchaguzi kujiunga na Chama chochote cha siasa.

"Hivyo msimamo wa Serikali dhidi ya uamuzi ea Mahakama Kuu , ni kwamba baada ya uamuzi huo Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, imenza taratibu za kisheria za kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufani Tanzania ili sehemu ya uamuzi huo upitiwe upya,"amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Prof. Kabudi ala kiapo cha utii Bunge la Afrika

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.), akila kiapo cha utii mbele ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ili kuwezesha kushiriki kwenye Bunge hilo kama Waziri anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania. Tukio hilo ambalo limefanyika kwenye Makao Makuu ya Bunge la Afrika Mashariki jijiji Arusha leo, limeshuhudiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Spika wa Bunge hilo, Mhe. Martin Ngoga.
Sehemu ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakishuhudia tukio la kuapishwa kwa Mhe. Prof. Kabudi
Mhe. Prof. Kabudi akizungumza kwenye Bunge la Afrika Mashariki mara baada ya kula kiapo cha utii cha kushiriki Bunge hilo
Sehemu nyingine ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakifurahia hotuba ya Mhe. Prof. Kabudi ambaye haonekani pichani
Mhe. Prof. Kabudi akizungumza kwenye Bunge la Afrika Mashariki mara baada ya kula kiapo cha utii huku Spika wa Bunge hilo, Mhe. Martin Ngoga na wabunge wengine wakimsikiliza.

Introducing "Dede" by Anitha Ft Beka Flavour (Official Music Video)

HABARI ZA UN KUTOKA NEW YORK LEO

TAASISI YA UTAFITI WA WANYAMAPORI(TAWIRI ) NA FRIEDKIN CONSERVATION FUND LIMITED(FCFL) WAWAWEKEA TEMBO 18 VIFAA MAALUMU

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangala(wa pili kushoto) akiwa pamoja na Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Anthony Mtaka ,Mkuu wa wilaya ya Meatu,Dk Joseph Chilongani(kulia) na Meneja wa shirika linalojihusisha na uhifadhi la Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL),Nana Grosse alipowasili kwenye uwanja mdogo wa ndege wa Mwiba Wildlife Ranch kushuhudia uwekaji mikanda maalumu ya ufatiliaji mienendo ya Tembo eneo la Maswa Game Reserve.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangala akizungumza   kabla ya kushudia  uwekaji wa mikanda maalumu ya ufatiliaji mienendo ya Tembo kwenye Pori  la Maswa Game Reserve uliofadhiliwa na shirika linalojihusisha na uhifadhi la Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL) katika eneo la  Mwiba Wildlife Ranch .

Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangala(kulia) akishuhudia uweka  uwekaji wa mikanda maalumu ya ufatiliaji mienendo ya Tembo kwenye Pori  la Maswa Game Reserve uliofadhiliwa na shirika linalojihusisha na uhifadhi la Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL) katika eneo la  Mwiba Wildlife Ranch .

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (Tawiri),Dk Janemary Ntalwila  akionesha mchoro wa namna kifaa  maalumu   cha  ufatiliaji mienendo ya Tembo kwenye Pori  la Maswa Game Reserve uliofadhiliwa na shirika linalojihusisha na uhifadhi la Friedkin Conservation Fund Limited(FCFL) katika eneo la  Mwiba Wildlife Ranch .


Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (Tawiri),Dk Edward Kohi akizungumza mienendo na tabia za Tembo huku Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangala akimsikiliza kwa makini.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamis Kigwangala akifurahia jambo baada ya zoezi la uwekaji kifaa hicho kukamilika,jumla ya Tembo 18 wamewekewa mikanda yenye vifaa maalumu ya kuwafatilia mienendo yao.

Wataalamu wakimfatilia mmoja wa Tembo ambaye alifungwa kifaa maalumu 
Wataalamu wa Wanyamapori wakimfatilia mmoja wa Tembo aliyefungwa kifaa hicho kinachowawezesha kufahamu mienendo yake katika ikolojia ya uhifadhi



KAYA 200 ZENYE MAISHA DUNI HUKO KATA YA VIGWAZA ZAPATIWA MSAADA WA BAADHI YA VYAKULA-MEESAM

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO

SHIRIKA linalosaidia watu wenye maisha duni na kuleta mabadiliko chanya katika jamii (WHO IS HUSSAIN?), tawi la Dar es salaam kwa kushirikiana na diwani wa kata ya Vigwaza Mohsin Bharwani ,limetoa msaada wa vyakula kwa kaya 200 zilizopo kwenye kata hiyo,uliogharimu sh.milioni kumi. 

Kila kaya kati ya hizo imepatiwa box lenye vitu vilivyogharimu sh. 50,000 ,ikiwemo mchele kilo 3, maharage kilo tatu, sukari kilo 3, majani ya chai, tende na tambi ili kuwasaidia katika mwezi mtukufu wa Ramadan.  

Akikabidhi msaada huo, mratibu msaidizi wa shirika la Who is Hussain?, tawi la Dar es salaam Meesam Bandali alisema,walengwa ni watu wasio na uwezo wakiwemo wenye ulemavu,wazee katika kaya 200 kata ya Vigwaza. 

Awali diwani wa kata ya Vigwaza, Mohsin Bharwani, alilishukuru shirika hilo kwa ujali na kujitoa kwao . 

"Sisi wanasiasa tunajua hali za wananchi waliopo katika maeneo yetu ambao wana hali duni kimaisha, ikitokea wafadhili kama hawa tunashukuru, nami waliponifuata niliona ni vyema kushirikiana kusaidia baadhi ya kaya ambazo zinaishi kwenye maisha duni"alisema Bharwani. 
Naye msemaji mkuu wa who is Hussain? Iffet Thawer 
alibainisha, mjukuu wa mtume Mohammad S.W.A. ambae ni Hussain alijitolea muhanga na aliuawa na familia yake kutokana na kusimama kidete dhidi ya mfalme aliyekuwa mdharimu. 

Iffet alisema ,Hussain alipinga dhuluma hivyo kuwa chanzo cha wao kuhamasika kufanya shughuli za kusaidia jamii ambapo lilianza miaka kumi iliyopita huko London.

Baadhi ya wakazi waliopata msaada huo,  akiwemo Said Imani, Maimuna Iddi  walielezea, vitu hivyo vinaweza kuwafikisha kimatumizi wiki mbili jambo ambalo litakuwa limezisogeza familia hizo kutokana na hali zao. 

MAENDELEO YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA UYUI, KUMALIZIKA MWEZI JUNI

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT

UJENZI wa Hospitali ya Wilaya ya Uyui unatarajia kukamilika mwishoni mwa Mwezi ujao tayari kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati akielezea maendeleo ya ujenzi wa majengo saba ya Hospitali hiyo.

Alisema kwa upande wa jengo la Utawala tayari yameezekwa na kuwekewe miundo ya umeme na maji na kwa jengo la kufulia limeshaezekwa.
Jengo la kufulia katika Hospitali ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora lilipofikia.

Msuya alisema kwenye jengo la wagonjwa wa nje(OPD) , jengo la uchunguzi wa mionzi, na , maabara iko kwenye lenta na jengo la stoo ya dawa liko katika hatua ya upauaji baada ya kumaliza hatua ya kufunga lenta.

Alisema kwa upande wa jengo la mama na mtoto liko katika hatua ya kuanza kufungwa lenta.

Mkuu huyo wa Wilaya alisema wanatarajia kumaliza ujenzi katika kipindi kilichopangwa.
Jengo la uchungui wa maabara katika Hospitali ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora lilipofikia.

Kaimu Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora Akwilin Mwachali alisema hivi wanakwenda kwa kasi baada ya kuvunja mkataba na baadhi ya mafundi wa awali na kukabidhi shughuli kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Alisema mafundi wa awali walikuwa wakifanyakazi pole pole na wakati mwingine wakishindwa kufika kazini kwa visingizio mbalimbali na ndio waliona wachukue hatua ya kusitisha mkataba ili waweze kumaliza kazi hiyo kwa wakati.

Mkazi wa Ilalansimba wilayani Uyui John Kulwa ameishukuru serikali kwa kuwajengea Hospitali ya Wilaya kwa kuwa imesaidia kutokwenda mbali kufuata huduma za ngazi ya Hospitali ya Wilaya.
Jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora lilipofikia.
Jengo la huduma ya uchunguzi wa mionzi katika Hospitali ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora lilipofikia.
Jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora lilipofikia.
Jengo la stoo ya Dawa katika Hospitali ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora lilipofikia.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images