Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

MANCHESTER CITY YATWAA UBINGWA WA LIGI KUU YA UINGEREZA

0
0

Klabu ya Manchester City imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Soka nchini humo baada ya leo kuifunga klabu ya Brighton goli 4-1 na kufikisha alama 98.
-
Man City inachukua ubingwa huo huku Liverpool iliyokuwa inaipa ushindani mkubwa inamaliza nafasi ya pili baada ya leo kuifunga klabu ya Wolves goli 2-0 na kufikisha alama 97

Man City imetetea kombe hilo baada ya msimu uliopita kuwa mabingwa na hili ni kombe lao la nne ndani ya kipindi cha misimu 8 iliyopita

Nafasi ya 3 imechukuliwa na Chelsea yenye alama 72, nafasi ya 4 imechukuliwa na Tottenham yenye alama 71, Arsenal imechukua nafasi ya 5 baada ya kupata alama 70 huku Manchester United ikiwa nafasi ya 6 na alama 66

Kwa msimamo huo, vilabu vya Manchester City, Liverpool, Chelsea na Tottenham vimekata tiketi ya kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Ulaya kwa msimu wa 2019/2020

MRADI WA MAJI WA BILIONI 1.8 WASAINIWA BUSEGA

0
0
Serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) imesaini mkataba na Mkandarasi Kampuni ya BENNET Contractors Ltd ya Mkoani Mwanza kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo, Wilayani Busega Mkoani Simiyu utakaonufaisha wananchi wapatao 12,000 wa vitongoji vya Bukabile, Bulima na Mwagulanja.

Hafla ya utiaji saini ilifanyikia hivi karibuni Wilayani Busega na kushuhudiwa na wananchi, watendaji wa Serikali na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambaye alibainisha kwamba zaidi ya asilimia 74 ya wananchi wa Busega watakua na uhakika wa maji safi na salama mara baada ya kukamilika kwa mradi.

Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga akielezea utekelezaji wa mradi huo alibainisha kuwa ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli baada ya ahadi aliyoitoa kwa wananchi wa Nyashimo ya kuwapelekea maji safi na salama.

“Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli alivyopita hapa Nyashimo wakati wa ziara zake aliwaahidi wananchi wa hapa kuwatatulia kero ya maji na aliiagiza Wizara ya Maji kuhakikisha inatekeleza mradi haraka iwezekanavyo,” alisema Mhandisi Sanga.

Mhandisi Sanga alisema mradi utatekelezwa kwa Miezi 15 na utagharimu jumla ya Shilingi Bilioni 1.8 na kwamba unafadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa upande wake Mhe Mtaka alisisitiza mradi ukamilike kabla ya muda uliopangwa wa miezi 15 na alimtaka Mkandarasi kuhakikisha analifanyia kazi suala hilo na alisema endapo kama Mkandarasi atabaini urasimu katika utekelezaji wa mradi amfahamishe haraka ili kuondoa hali hiyo.

Aliongeza kuwa utekelezwaji wa mradi ni neema kwa wananchi wa Busega na aliwasihi kuchangamkia fursa zitokanazo na ujenzi wake kuanzia hatua za awali za utekelezaji na alimuagiza Mkandarasi kuhakikisha anatekeleza mradi kwa ufanisi mkubwa na kutoa kipaumbele kwa jamii inayozunguka kuwa ya kwanza kunufaika. 

Mtaka alimpongeza Mhandisi Sanga kwa jitihada zake na umahiri wa kusimamia miradi anayokabidhiwa kwa niaba ya Wizara ya Maji na alimsisitiza aendelee na moyo huo wa kizalendo na aliipongeza Bodi ya Wakurugenzi na wafanyakazi wa MWAUWASA.

Naye Mbunge wa Jimbo la Busega Mkoani Simiyu, Dkt. Raphael Chegeni ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi walioshuhudia tukio hilo alisema kero kubwa waliyokuwa nayo wananchi wa jimbo lake ni ukosefu wa maji safi na salama na tayari mwarobaini wake umepatikana. 

Dkt. Chegeni alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kutimiza ahadi alizotoa kwa wananchi wakiwemo wa jimbo lake na alibainisha kuwa utekelezaji wa miradi ni maelekezo ya Rais na kwamba kwa Wilaya ya Busega ipo miradi mingi inatekelezwa na aliitaja baadhi ambayo ni ya Kiloleli na Lamadi.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkandarasi, Sabato Boas aliahidi kutekeleza mradi kwa muda mfupi kadri itavyowezekana na kwa utaalam unaotakiwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa kwenye mkataba. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) na Mwakilishi wa Kampuni ya BENNET Contractors Ltd, Sabato Boaz (kulia) wakisaini mkataba wa ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nyashimo-Busega, Mkoani Simyu. Wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Busega.
 Mkuu wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka (katikati), akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga mara baada ya kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji Nyashimo. Kulia kwa Mkuu wa Mkoa ni Mbunge wa Jimbo la Busega Mkoani Simiyu, Dkt. Raphael Chegeni.
 Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu na Wajumbe wa Bodi ya MWAUWASA wakishuhudia tukio la utiaji saini mradi wa maji Nyashimo.
 Baadhi ya wananchi waliyofika kwenye hafla ya utiaji saini ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo-Busega, Mkoani Simiyu wakifuatilia tukio hilo.
 Mbunge wa Jimbo la Busega Mkoani Simiyu, Dkt. Raphael Chegeni akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo- Busega.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi MWAUWASA wakijadiliana jambo wakati wa halfa ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya MWAUWASA, Edith Mudogo na Mjumbe wa Bodi, Hellen Bogohe.


Mkurugenzi wa Uchaguzi aridhishwa na utendaji kazi wa watumishi wa NEC

0
0
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia ameeleza kuridhishwa na utendaji kazi wa watumishi wa tume hiyo kutokana na kufanya kazi kwa bidii, ushirikiano, weledi na uzalendo.

Dkt. Kihamia ameeleza hayo wakati alipokutana na wafanyakazi wa  NEC kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya Tume.

Alisema katika kipindi alichokaa Tume amegundua kuwa sasa utendaji kazi wa mazeoa umepungua na watumishi wengi wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kwa wakati, kwa uaminifu, kutunza siri na kuepuka matumizi ya fedha yasiyo ya lazima.

Mkurugenzi huyo wa NEC alifafanua kuwa katika kikao chake cha kwanza na watumishi wa Tume cha Agosti 7 mwaka 2018, alijadili changamoto zinazowakabili watumishi hao ambazo zilikuwa kikwazo cha utekelezaji wa majukumu yao kwa njia moja au nyingine.

“Tuligundua kuwa changamoto nyingi zilitokana na tabia binafsi za baadhi ya watumishi, na baadhi yao kufanya kazi kwa kuigiza yaani kwa mazoea kwa kisingizio cha mchakato”, alisema Dkt. Kihamia na kufafanua kuwa:

“Lakini sasa hivi jambo la kufurahisha asilimia kubwa ya watumishi wanafanya kazi sio kwa mazoea, lakini pia ufanisi wa kazi zao umeongezeka kwa kiwango kikubwa”.

Alibainisha kuwa kwa sasa Tume imeimarika vya kutosha kwa kuwa wakati alipofika wastani wa utendaji kazi ulikuwa asilimia 52, ikimaanisha kuwa zaidi ya asilimia 48 ya watumishi walikuwa hawawajibiki ipasavyo, lakini sasa uwajibikaji umefikia wastani wa asilimia 65 baada ya kuwekeana malengo.

“Kwa hiyo tulipo sasa tupo juu ila ni lazima tuendelee kuwa kitu kimoja,  ingawa katika kuimarika huko wapo wenzetu wachache sana wenye matatizo madogo madogo, hivyo wanatakiwa warekebishwe” alisisitiza Dkt. Kihamia

Alifafanua kuwa kuimarika kwa utendaji kazi ni jambo kubwa kwa maendeleo ya nchi kwa kuwa kutowajibika ipasavyo kwa watumishi wa umma katika nchi nyingi za Afrika kumesababisha udumavu wa maendeleo ya nchi hizo.

Hivyo aliwataka watumishi wa NEC kuendeleza tabia ya uwajibikaji kwa mustakbali wa maendeleo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tanzania kwa ujumla kwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuwa chachu ya maendeleo ya nchi.

Ili kuboresha zaidi utendaji kazi wa Tume, Dkt. Kihamia aliziagiza kila idara ziainishe vipaumbele (priorities) vitakavyotekelezwa na idara husika kwa kipindi chote kuanzia Julai 1 mwaka huu.

Alisema baada ya kupata vipaumbele hivyo kutoka kila idara vitaunganishwa kupata vipaumbele vya Tume na aliwataka watumishi kutambua kuwa majukumu ya kila idara ni majukumu ya Tume hivyo ni muhimu kuwa kitu kimoja katika kuyatekeleza.

“‘Checklist’ ni jambo kubwa sana kwa sababu kuna mtu ukienda kwenye idara yake ukimuuliza amefanya mambo gani, anaweza akawa amefanya mambo mazuri tu lakini hayakumbuki mpaka ayafikirie ndio akwambie” alisema Dkt. Kihamia na kufafanua kuwa:

Alisema checklist ni mpango kazi ambao hata watafiti wanaofanya tafiti za kisasa wamegundua kwamba kampuni nyingi za kibiashara zinazofilisika ni zile ambazo hazina checklist za kisasa.

“Kwa hiyo checklist ni moja ya agenda ambayo nimekuja kuizungumzia leo kwa sababu tunafanya kazi kwa mipangokazi na unapokuwa na checklist unajua hili nimelifanya hili sijafanya” alisema Dkt. Kihamia.

Alisema mtumishi asipokuwa na checklist ya kazi zake hawezi kuwa na muendelezo (consistency) mzuri wa majukumu ambayo mtumishi anataka kuyatekeleza na ukamilifu wa kazi zake hautakuwepo.

Alisema wataalamu wanasema kwamba checklist ndio njia pekee kwa sasa inayoaminika katika kutekeleza majukumu kwa ufasaha.

“Mtafiti mmoja aliwahi kusema checklist ni aina ya mpangilio wa majukumu ambao unapunguza kushindwa (failure)katika kazi, ina maana usipokuwa na checklist uwezekano wa kushindwa ni mkubwa” aliongeza Dkt. Kihamia.

Kwa upande mwingine Dkt. Kihamia alimtaka kila mtumishi wa Tume atambue majukumu ya msingi ya NEC na ikiwemo kufahamu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ni nini na kufahamu taratibu zote za uchaguzi.

“Watu wajifunze kuwepo kwa nafasi wazi ni nini maana watu wanalalamika kwamba Serikali inatumia fedha nyingi kufanya chaguzi ndogo za mara kwa mara lakini wanasahau kwamba suala hilo lipo kwenye katiba na ni utarabu.” alisema Dkt. Kihamia.

Dkt. Kihamia tangu alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi amejiwekea utaratibu wa kukutana na watumishi wa tume hiyo huku hiki kikiwa ni kikao chake cha tatu.

Katika kikao cha kwanza cha tarehe 7 Agosti mwaka 2018, Dkt. Kihamia aliainisha vipaumbele vyake 30 vya kuzingatia katika utekelezaji wa majukumu ya Tume na kuvifanyia tathmini kwenye kikao cha pili kilichofanyika mwezi Desemba mwaka 2018.

Baadhi ya vipaumbele alivyosisitiza ni kuweka mpango kazi wa kila idara, kitengo na mtumishi na utekelezaji wake kwa kile mwezi,  kuandaa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya kila idara, kutambua madeni ya kila idara na kitengo na kuonesha kama yamehakikiwa au la, sababu ya madeni hayo na kuwepo rejesta na mpango kazi wa malipo.

Katika vikao hivyo wakuu wa Idara wamepewana nafasi ya kufafanua mambo mbalimbali katika idara zao na watumishi kuwepo nafasi ya kueleza mambo mbalimbali kuhusu utekelezaji wa majukumu yao.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia akizungumza an wafanyakazi wa NEC (hawapo pichani).
 Mkurugenzi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu wa NEC, Gerald Mwanilwa akifafanua jambo.

  Baadhi ya wafanyakazi wa NEC wakimsikiliza  Dkt. Kihamia
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (wa mbele katikati) akizungumza na wafanyakazi wa NEC 

Serikali yatekeleza ahadi ya kupeleka umeme kwa wachimbaji wadogo Nyakafuru

0
0
Na Teresia Mhagama, Geita
Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imetekeleza ahadi ya kupeleka umeme kwenye migodi ya wachimbaji wadogo katika Kijiji cha Nyakafuru wilayani Mbogwe hivyo kuwawezesha wachimbaji hao kutumia umeme badala ya mafuta katika kuendesha mitambo mbalimbali ikiwemo ya kuchenjulia madini.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani aliwasha umeme katika katika eneo hilo la wachimbaji wadogo tarehe 12 Mei, 2019 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa mwezi Februari  mwaka huu wakati alipotembelea machimbo hayo na wachimbaji wadogo wa eneo hilo kumlalamikia kuhusu gharama kubwa wanazotumia katika ununuzi wa mafuta ambazo zinafikia hadi shilingi milioni Tatu kwa mwezi.

" Serikali inatekeleza ahadi zake badala ya kupiga maneno, hivyo tumeleta umeme hapa si kwa ajili ya kuwasha taa tu, bali umeme huu utawawezesha kuchimba kwa tija, Serikali inataka mchimbe kwa faida ili nanyi muweze kulipa kodi stahiki serikalini itakayotumika kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo." alisema Dkt. Kalemani.

Alisema kuwa, katika eneo hilo tayari imeshafungwa transfoma moja kubwa yenye uwezo wa kVA 315 na kwamba zitafungwa transfoma nyingine Tatu zenye uwezo wa kVA 315 ili kuwezesha eneo hilo kupata umeme wa uhakika utakaotosheleza mahitaji.

Pamoja na kuipongeza TANESCO kwa utekelezaji wa agizo hilo, Dkt. Kalemani alitoa agizo kwa watendaji wa TANESCO kuhakikisha kuwa hadi ifikapo mwisho wa mwezi wa Tano wawe tayari wameshafunga transfoma tatu na moja iliyosalia ifungwe mwezi Juni.

Aidha, Dkt Kalemani aliwaasa wachimbaji hao kuchangamkia fursa ya uuganishaji umeme  kwa bei ya REA inayoanzia 27,000 na  pia aliagiza TANESCO kupeleka umeme huo katika vitongoji vyote vya Kijiji hicho.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wachimbaji wa Nyakafuru, Walwa Katemi Walwa aliishukuru Serikali kwa kupeleka umeme katika eneo hilo ambalo lina wachimbaji zaidi ya 3000 na kuahidi kulipa kodi stahiki serikali.

Alisema kuwa wakati wakitumia mafuta kuendeshea mitambo katika eneo hilo walikuwa wakilipa kodi zaidi ya shilingi milioni 400 hivyo sasa wanaamini kuwa kodi hiyo itaongezeka maradufu kwani gharama za uendeshaji zitapungua na pia wataongeza uzalishaji kwa kuwa kuna uhakika wa nishati ya kuendeshea mitambo yao. 
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akizungumza na wachimbaji wadogo katika Kijiji cha Nyakafuru wilayani Mbogwe mkoani Geita wakati alipofika kuwasha umeme katika eneo la wachimbaji wadogo kijijini hapo.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akiwasha rasmi umeme katika migodi ya wachimbaji wadogo iliyo katika Kijiji cha Nyakafuru wilayani Mbogwe mkoani Geita. Wengine katika picha ni watendaji kutoka Wizara ya Nishati, TANESCO na viongozi wa wachimbaji wadogo katika eneo hilo.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akikata utepe kuashiria kuwasha rasmi umeme katika migodi ya wachimbaji wadogo iliyo katika Kijiji cha Nyakafuru wilayani Mbogwe mkoa wa Geita. Wengine katika picha ni watendaji kutoka Wizara ya Nishati, TANESCO na viongozi wa wachimbaji wadogo katika eneo hilo.
 Wachimbaji wadogo katika Kijiji cha Nyakafuru wilayani Mbogwe wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati alipofika kuwasha umeme kwenye eneo la wachimbaji wadogo kijijini hapo.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa kwanza kushoto) akifurahi na wachimbaji wadogo mara baada ya kuwasha rasmi umeme katika migodi ya wachimbaji wadogo katika Kijiji cha Nyakafuru wilayani Mbogwe mkoani Geita.

KONGAMANO LA KISWAHILI JIJINI DAR ES SALAAM

JENERALI MSTAAFU GEORGE WAITARA AWAVISHA VYEO VIPYA VIONGOZI WAPYA TANAPA

0
0

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii.

Mweyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa ,Jenerali (Mstaafu) George Waitara amezindua mfumo mpya wa utendaji kazi ndani ya Hifadhi za Taifa unaopeleka madaraka zaidi katika ngazi ya Kanda nne kuu zilizoundwa ili kuboresha utendaji kazi unaoendana na mfumo mpya wa jeshi -usu.

Uzinduzi huo ulienda sambamba na zoezi la utoaji vyeo vipya vilivyoidhinishwa na bodi ya wadhamini kwa viongozi wa shirika ambao ni Naibu Kamishna wa Uhifadhi wawili,Makamishna wa Uhifadhi wa kanda wanne,Makamishna Wasaidizi Waandamizi 14,Makamishna wasaidizi 22 pamoja na Maafisa Wakuu na Waandamizi saba.

Muundo mpya unahusisha Kanda ya Kaskazini yenye Hifadhi za Arusha,Tarangire ,Ziwa Manyara,Kilimanjaro na Mkomazi ,Kanda ya mashariki inayojumuisha Hifadhi za Saadan,Mikumi na Udzungwa ,Hifadhi za Ruaha na Kitulo na Katavi zitakuwa chini ya usimamizi wa  kanda ya Kusini ,

Kanda ya Magharibi itasimamia Hifadhi za Taifa za Gombe,Mahale ,kisiwa cha Saanane ,Kisiwa cha Rubondo ,Serengeti pamoja na Hifadhi mpya za Burigi,Kimisi,Biharamulo,Ibanda na Rumanyika.

Hafla hiyo pia imeendana na zoezi la kuwatunuku vyeti wahitimu 217 wa mafunzo yaliyochukua miezi sita kwa awamu mbili yakihusisha Maafisa wa Uhifadhi pamoja na waajiriwa wapya.

Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwawezesha wahitimu kufanya kazi  kwa mfumo wa kijeshi -usu katika kuboresha utendaji kazi na majukumu ya usimamizi thabiti wa maliasili zilizopo hifadhini kwa kuwajengea wahitimu uwezo wa kimwili ,kisaikolojia,kimaadili na uzalendo

Dkt Gwajima ataka Wagonjwa kutoandikiwa kununua dawa nje ya hospitali za halmashauri

0
0
Na Mathew Kwembe, Babati
Serikali imezitaka Halmashauri za Wilaya kuhakikisha kuwa zinatekeleza agizo lake la kuhakikisha wanaimarisha upatikanaji wa dawa katika vituo vya huduma za afya na kuepuka tabia ya kuwaandikia wagonjwa kwenda kununua dawa nje ya kituo.

Agizo hilo limetolewa jana mjini Babati na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt Dorothy Gwajima mara baada ya kuitembelea  hospitali ya Mrara ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kukagua huduma za afya na uwezo wa timu za usimamizi huduma za afya mikoa na halmashauri.

 Amesema, kila halmashauri haina budi kutenga fedha toka vyanzo vya ndani kwa ajili ya kuhakikisha dawa zilizokosekana bohari kuu ya dawa zinanunuliwa na stoo za dawa katika hospitali zinakuwa na dawa aina zote muda wote ili kuepuka kuwaandikia wateja kwenda kununua dawa hizo nje ya maduka ya hospitali.

“Hivi halmashauri zinashindwa nini kutenga fedha toka vyanzo vya ndani kwa ajili ya kuandaa chumba maalumu cha kutunza dawa kisha kununua dawa aina zote kufidia zilizokosekana bohari kuu ya dawa ili, wateja wanaoelekezwa kununua nje ya hospitali wapate dawa hizo ndani ya hospitali husika, mbona maelekezo haya kwingine yamewezekana nyie mnagonja nini?” amehoji Dkt. Gwajima.

 Kauli hiyo ya Dkt Gwajima inafuatia maelezo ya Mfamasia wa Hospitali ya mji bwana Elly John Bomani kwamba baadhi ya dawa muhimu katika hospitali hiyo zinakosekana ambapo juhudi za kuagiza dawa nyingine bohari kuu ya dawa zimekwishafanyika.

Akizungumzia kuhusu hali ya utoaji wa huduma aliyoikuta kwenye hospitali hiyo, Dkt Gwajima ameelezea kutofurahishwa na hali ya usafi wa mazingira na kuelekeza mganga mkuu wa mkoa asimamie usafi wa kina ufanyike vilevile, waganga wakuu wa mikoa na halmashauri zote waelekeze macho yao kwenye usafi wa mazingira kila eneo la huduma na asikute tena popote hali ya usafi wenye mashaka.

“Sitarajii nikute haya mambo madogo kabisa hayaridhishi, natarajia nikute hoja kubwa za kimkakati ili, tujadiliane hizo. Hii habari ya kukutana na magodoro yaliyochoka hayana mipara stahiki ya kufunika, viti vimechoka, vyoo na bafu zisizofanyiwa usafi, vumbi, mara milango na madirisha yako wazi hapana kabisa. Naagiza mapungufu haya yafanyiwe kazi mara moja na magodoro yaliyochoka yachambuliwe yatolewe na mganga mkuu wa mkoa uniletee taarifa,” amesema.



Hivyo Dkt Gwajima amemwagiza Katibu wa Afya wa Mkoa Bwana Thomas Malle kuhakikisha kuwa anatekeleza wajibu wake wa kusimamia kikamilifu wataalamu wa afya ya mazingira wa halmashauri wahakikishe kuwa usafi unafanyika katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya katika mkoa wa Manyara ama la sivyo naye ajipime maana yuko karibu kabisa na hospitali hiyo.

“Mimi nashangazwa inakuwaje timu ya usimamizi huduma za afya halmashauri ofisi zake ziko humu humu hospitalini lakini hali ya kituo ni hivi, na mwaka mzima hawajafanya ukaguzi, huu ni utendaji wa mazoea, naenda kutakafari juu yenu,” amesema Dkt Gwajima.

Ameongeza “Sitaki mazoea wala wasaidizi ambao inabidi nitumie nguvu kubwa kuwafanya watekeleze majukumu yao ya msingi bali kila mmoja ajitume mwenyewe vinginevyo ama akabidhi kwa hiari madaraka aliyopewa ama kwa lazima.”

Pia Naibu Katibu Mkuu ametembelea jengo la Maabara na kukuta kuwa hospitali hiyo haitoi baadhi ya huduma za vipimo muhimu huku, mashine kwa ajili ya vipimo hivyo zipo na wataalamu wapo.

Dkt Gwajima ametaja vipimo hivyo kuwa ni culture and sensitivity ambapo, sababu iliyotolewa ni kuwa, wako kwenye mchakato wa kukarabati jengo huku makadirio ya gharama yakiwa ni madogo na yapo ndani ya uwezo wa hospitali.

Naibu Katibu Mkuu amemuagiza Mganga mkuu wa mkoa aifuatilie timu ya usimamizi huduma za afya ya halmashauri ya mji wa Babati ili iachane na  habari ya neno mchakato na badala yake watumie utaratibu wa force account kununua vifaa na kutumia mafundi wa kutoka jamii wafanye kazi hiyo na ndani ya siku 30 watoe taarifa ya kuwa zoezi limekamilika.

“Maeneo mengi nilikopita naona baadhi ya wasaidizi wangu hawajaielewa kasi tunayotakiwa kwenda nayo kwa kuwa naendelea kushuhudia mambo madogo madogo yakiwa hayajatekelezwa kinyume na maelekezo na makubaliano  tuliyojiwekea na mambo haya wala hayahitaji fedha wala si kwamba, wasaidizi wangu wamezidiwa na majukumu, ni mazoea tu,” amesema

Dkt Gwajima amehoji: “Hivi huwa mnakuwa mnafanya nini kila siku hadi kunakuwa na mapungufu kama haya na wengine mnalalamikiwa kwa tuhuma za wizi, rushwa, ubadhirifu na lugha chafu kwa wagonjwa?”

Katika ziara hiyo Dkt Gwajima aliambatana na kamati ya usimamizi huduma za afya ya halmashauri ya mji wa Babati pamoja na ile ya Mkoa wa Manyara ambapo amemtaka Mganga mkuu wa mkoa kuongeza kasi ya kusimamia timu za halmashauri na kujiridhisha kama wasaidizi wake wanamsadia au nao ni sehemu ya wanaohitaji kutazamwa upya.

Wakati huo huo Dkt Gwajima amewataka Makatibu wa Afya wa Mikoa, Wilaya na Vituo vya kutolea huduma za afya kuandaa kanuni na taratibu za taasisi (organizational culture) zitakazowaongoza watoa huduma kufikia uwajibikaji bora zaidi.

Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu alimpongeza Dkt Pastory Mahendeka ambaye ni daktari wa meno wa hospitali ya mji wa Babati kwa kufanya majukumu yote ya ujumbe wa timu ya usimamizi wa huduma za afya halmashauri na pia kumudu kufanya majukumu ya kitabibu na kuandaa takwimu zake vizuri  bila kusimamiwa wala kufuatiliwa.

Amemuelekeza kuwa, kwa kuwa yuko peke yake, vema aweke kwenye mpango utaratibu wa kuomba kibali cha watumishi wengine kupelekwa masomoni.

Vilevile, Naibu Katibu Mkuu amepongeza daktari wa wodi ya watoto kaika hospitali ya mji wa Babati Dkt. Moses Mollel kwa uwajibikaji wake makini katika kutoa huduma za kitabibu katika wodi hiyo kila siku na kwa kumbukumbu zisizotia shaka.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt Damas Kayera amesema wamepokea maagizo ya Naibu Katibu Mkuu na akaahidi kuyatekeleza kikamilifu na kuendeleza ufuatiliaji kama huu katika halamshauri zingine.

Naye Mratibu wa Malaria kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi Stellah Kajange ameutaka uongozi wa hospitali ya mji wa Babati kuhakikisha kuwa inajenga kichomea taka cha kisasa kwani  kilichopo sasa hakifai.

Naibu Katibu Mkuu pia ametembelea kituo cha afya Magugu kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Babati, ambapo ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Babati kwa kusimamia vema ujenzi wa jengo la huduma za uzazi na upasuaji na kuwataka huduma zianze kutolewa kwenye jengo hilo ifikapo tarehe 10 Juni, 2019.

Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya siku mbili kutembelea vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Manyara.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt Dorothy Gwajima akipata maelezo kutoka kwa Mfamasia wa stoo ya dawa ya Hospitali ya mji wa Babati bwana Elly John Bomani  jana kuhusu  dawa muhimu  zinakosekana hospitalini hapo
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt Dorothy Gwajima akipata maelezo ya idadi ya wagonjwa wa nje wanaohudumiwa na hospitali ya mji Babati kutoka kwa Muuguzi Msaidizi wa hospitali hiyo bibi Rose Mwakanosya
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt Dorothy Gwajima akitembelea majengo mbalimbali ya hospitali ya mji Babati jana ambapo alitembelea jengo linalotumika kuhudumia wagonjwa wa nje, maabara, wodi ya wazazi, wanaume na jengo la kliniki ya meno.

Tigo yaendesha zoezi la usajili wa laini za simu Bungeni

0
0
 Afisa Huduma kwa wateja kutoka Kampuni ya Tigo Regani Emmanuel, akimsajili Mbunge wa jimbo la Chwaka, Bhagwanji Meisuria (kulia), kupitia utaratibu mpya wa  usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole katika viwanja vya bunge mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. 
 Afisa anayehusika na usajili wa laini za simu kutoka kampuni ya Tigo Tanzania, Atupiani Makweta, akimsajilia mbunge Tunduma Frank Mwakajoka kwa kutumia mfumo mpya wa usajili kwa kutumia alama za vidole mwishoni katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
 Afisa anayehusika na usajili wa laini za simu kutoka kampuni ya Tigo Tanzania, Atupiani Makweta, akimsajilia mbunge Tunduma Frank Mwakajoka kwa kutumia mfumo mpya wa usajili kwa kutumia alama za vidole mwishoni katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.




MDAHALO WAWANAWAKE VIJANA WAFANYIKA JIINI ARUSHA

0
0
Na.Vero Ignatus,Arusha.

 Mdahalo wa wanawake vijana umefanyika Jiiini Arusha ukiwa na lengo la kukuza sauti na ushiriki wa wanawake vijana kwenye sera zinazohusu Afya zao.

Odero Charles Odero ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Uraia na msaada kisheria amesema wanafanya kazi na makundi mbalimbali ya wanawake haswa katika maeneo ya Demokrasia,haki za binadamu,utawala bora kwa jamii zile ambazo haziwezi kujiwakilisha kupata haki zao.

Amesema lengo la mradi huo wa miezi 3 ni kukuza sauti za wanawake vijana ambao wapo kwenye rika  balehe katika sera zinazohusu maisha na afya zao,kuwatia vijana hamasa ili waweze kushiriki katika sera zinazohusu maisha yao  kwani asilimia kubwa ya wanawake hawashiriki maamuzi yanayowahusu

Uzoefu wetu kama shirika ndani ya miaka 5 sasa ukienda kwenye mikutano mbalimbali ya vijiji wanawake hawashiriki kutoa maamuzi.

Dkt.Eliamani Laltaika ni mkufunzi kutoka chuo cha Nelson na muwezeshaji wa mdahalo huo, ameainisha kuwa 75% ni Vijana na wanahitaji Sera ya maeneo maalumu  ili waweze kutambuliwa ambapo inakwenda sambamba na Elimu ya Ufundi Sayansi na Teknolojia ili aweze kujitegemea mahusiano,Elimu ya Afya ya uzazi.

Amesema vijana wanatakiwa kupaza sauti kwani wanayo matamanio katika maisha kwasababu vyombo vya maamuzi vinatakiwa vielewe mahitaji ya vijana ili waweze kupata msaada na kutambua nguvu kazi.

Amesema kuwa njia ambazo zinatumika kupaza sauti kijana anatakiwa ajitambue yeye ni nani,ajielewe,ajiheshimu,aseme asikike,ajiunge pamoja ili kubadilishana uzoefu,kwakutumia vyombo vya serikali,Mashirika yasiyo ya kiserikali na mitandao ya kijamii.

Dkt.Laltaika amewataka vijana kutumia mitandao ya kijamii vizuri kwa faida ili  sauti kwani shughuli zote za kijamii ikiwemo Biashara  zinapatikana humo,ila pia lazima watambue zipo changamoto,athari pamoja na faida katika mitandao ya kijamii katika kuleta haki za vijana.

Mwenyekiti wa Maendeleo ya Jamii Jiji la Arusha na Diwani wa Kata ya Ngarenaro Isaya Doita amesema Kumpiga mwanamke ni kosa ,ni udhakikishaji wa kijinsia hivyo amewataka wanawake pale wanapoona vitendo vya udhalikishaji watoe taarifa katika vyombo vya sheria na watapatiwa msaada mara moja.

Mradi huo umewezeshwa na shirika la SAT,eannaso,Hervoice kuweza kupaza sauti Mradi unaitwa kukuza sauti za vijana ambapo ni mradi wa miezi mitatu.zaidi ya vijana wanawake 40 wameshiriki mjadala huo ambao umeshirikisha watunga sera,kamati ya Afya na Elimu
Mkufunzi kutoka chuo cha Nelson Mandela Dkt.Eliamani Laltaika,na muwezeshaji wa  Mdahalo wa siku moja kuhusiana na kukuza sauti kwa wanawake vijana kuhusiana na Sera zinazohusiana na Afya zao
Odero Charles Odero ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Uraia na msaada kisheria (CiLAO)akizungumza na wanawake katika mdahao wa siku moja uoiofanyika Jiiiji Arusha.
Mwenyekiti wa Maendeleo ya Jamii Jiji la Arusha na Diwani wa Kata ya Ngarenaro Isaya Doita :Kumpiga mwanamke ni kosa ,ni udhakikishaji wa kijinsia.
Baadhi ya washiriki wa msahalo wa msahalo wa siku moja wa wananawake vijana ,pia waliweza kuzungumzia matumizi ya mitandao ya kijamii kwa vijana ,athari,changamoto,faida zake katika kupaza sauti za vijana.
Muwezeshaji wa Mdahalo huo Dkt. Eliamani Laltaika,akiwa anampatia kitabu alichokiandika ,Mkurugenzi wa Taasisi ya Uraia na msaada kisheria (CiLAO)Odero Charles Odero.
Washiriki wa mdahalo wakifuatilia mada zilizokuwa zinaendelea ikiwemo ya mikakati ya utekelezaji wa sera za vijana,Ushiriki wa wanawake na uongozi wa serikali za mitaa,vitongoji,vijiji na mitaa.
Mmoja wawaandishi akichangia mada katika msahalo huo wawanawake vijana uliofanyika jijini Arusha.
 Emma Ally Kimambo akijibu swali aliloulizwa na Mkugunzi wa Chuo Kikuu ca Nelson Mandela Dkt .Laltaika.
Baadhi ya Wanawake vijana wakifurahia jambo katika Mdahalo wa kukuza sauti kwa wanawake vijana kuhusiana na Seea zinaazohusiana na Afya zao.
Washiriki pia wakiwa darasani katika msahalo huo wa siku mojankama inavyoonekana pichani.
Mijadala katika makundi yalioundwa katika mdahalo huo.
Mkufunzi kutoka chuo cha Nelson Mandela Dkt.Laltaika akiwaonyesha wanawake vijana namna ya kutumia mtandao wa kijamii wa Twita kama #tag inavyoonekana hapo.
Mazoezi yalikuwa moja ya somo katika mdahalo huo kana inavyoonekana pichani.
Picha ya pamoja baada ya Mdahalo kumalizika.

TUHUMA ZA KUKUTWA NA GRAMU 232.70 ZA HEROINE ZAWAFIKISHA KORTNI SHAMIM NA MUMEWE

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

MMILIKI wa Blog ya 8020 Fashion, Shamim Omary Mwasha (41) na mume wake, Abdul Nsembo(45) wamefikishwa katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa wakikabiliwa na tuhuma za kusafrisha dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride zenye uzito wa gramu 232.70.

Akisoma hati ya mashtaka leo Mei 13, 2019  Wakili wa Serikali, Costastine Kakula amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi, Steven Mhina kuwa washtakiwa wametenda kosa hilo Mei 1,2019 wakiwa huko Mbezi beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini  Dar es Salaam.

Imedaiwa kuwa siku ya tukio washtakiwa hao walikutwa na gramu 232.70. za Dawa za kulevya kinyume na sheria ya uhujumu uchumi. 
 Hata hivyo,  washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa  kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi  mpaka Mahakama Kuu ama kwa kupata Kibali kutoka kwa DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Wakili wa utetezi, Hajra Mungula ameuomba upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi haraka ili hatua nyingine iweze kuendelea licha ya kwamba Leo  ndiyo siku ya kwanza kwa kesi hiyo kusomwa Mahakama hapo.

Kesi imeahirishwa hadi Mei 27, 2019 kwa kutajwa na kuangalia kama upelelezi umekamilika au la.

WAZIRI HASUNGA APIGILIA MSUMARI MARUFUKU AJIRA KWA WATOTO KWENYE SEKTA YA TUMBAKU Inbox x

0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) sambamba na viongozi wengine wakikagua madaraja ya kwenye zao la Tumbaku mara baada ya mkutano wa wadau wa wa sekta ya Tumbaku katika hafla ya ufunguzi wa msimu wa masoko ya Tumbaku mwaka 2019 iliyofanyika katika maghala ya kampuni ya Alliance One Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, leo Tarehe 13 Mei 2019.


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa wa sekta ya Tumbaku katika hafla ya ufunguzi wa msimu wa masoko ya Tumbaku mwaka 2019 iliyofanyika katika maghala ya kampuni ya Alliance One Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, leo Tarehe 13 Mei 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa wa sekta ya Tumbaku katika hafla ya ufunguzi wa msimu wa masoko ya Tumbaku mwaka 2019 iliyofanyika katika maghala ya kampuni ya Alliance One Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, leo Tarehe 13 Mei 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Baadhi ya wakulima wa zao la Tumbaku wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa wa sekta ya Tumbaku katika hafla ya ufunguzi wa msimu wa masoko ya Tumbaku mwaka 2019 iliyofanyika katika maghala ya kampuni ya Alliance One Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, leo Tarehe 13 Mei 2019.
Baadhi ya wakulima wa zao la Tumbaku wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa wa sekta ya Tumbaku katika hafla ya ufunguzi wa msimu wa masoko ya Tumbaku mwaka 2019 iliyofanyika katika maghala ya kampuni ya Alliance One Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, leo Tarehe 13 Mei 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua ubora wa Tumabku wakati wa mkutano wa wadau wa wa sekta ya Tumbaku katika hafla ya ufunguzi wa msimu wa masoko ya Tumbaku mwaka 2019 iliyofanyika katika maghala ya kampuni ya Alliance One Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, leo Tarehe 13 Mei 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Katikati) akizungumza na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa kampuni ya Alliance One Ndg David Mayunga (Kulia) sambamba na Mwenyekiti wa umoja wa Vyama vikuu vya wakulima wa Tumbaku Tanzania (TCJE) Ndg Emmanuel Cherehani mara baada ya mkutano wa wadau wa wa sekta ya Tumbaku katika hafla ya ufunguzi wa msimu wa masoko ya Tumbaku mwaka 2019 iliyofanyika katika maghala ya kampuni ya Alliance One Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, leo Tarehe 13 Mei 2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Tabora


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesisitiza marufuku yake aliyoitoa hivi karibuni kuhusu ajira kwa watoto ambao wapo chini ya miaka 18.


Mhe Hasunga amepiga marufuku hiyo leo tarehe 13 Mei 2019 wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa wa sekta ya Tumbaku katika hafla ya ufunguzi wa msimu wa masoko ya Tumbaku mwaka 2019 iliyofanyika katika maghala ya kampuni ya Alliance One Wilaya ya Urambo mkoani Tabora.


Alisema kuwa suala la ajira kwa watoto ni miongoni mwa mambo yanazuiliwa kwenye Sheria za kimataifa kupitia Shirika la Kazi Duniani (International Labour Organization) na Sheria za Ajira hapa nchini hivyo mdau yeyote atakayebainika kukiukwa maelekezo hayo atashtakiwa.


“Nawasihi wadau wote tuendelee kupiga vita ajira kwa watoto katika tasnia ya tumbaku kwa kuwa ni eneo ambalo limeendelea kulalamikiwa na wadau” Alikaririwa Mhe Hasunga


Kadhalika, Mhe Hasunga alisema kuwa katika kuhakikisha zao la tumbaku linaendelea kutoa mchango mkubwa katika pato la mkulima na Taifa, Wizara imejiwekea malengo ya haraka yanayopaswa kutekelezwa ambayo ni pamoja na kukamilisha usajili wa wakulima wote wa tumbaku ifikapo tarehe 30 Juni 2019, kuwapatia vitambulisho na kuwaingiza kwenye kanzidata ili kupata takwimu za uhakika za maeneo wanayolima na kuiwezesha serikali kusimamia upatikanaji wa pembejeo kulingana na mahitaji yao.


Malengo mengine ni Tumbaku yote inayovunwa na wakulima sasa inauzwa ifikapo mwisho wa masoko tarehe 31 Julai, 2019 huku akiiagiza Bodi ya Tumbaku kushirikiana na wakulima wote kusimamia kwa makini masoko ili tuweze kuanza mapema maandalizi ya zao la msimu wa 2019/2020.


Aidha, mipango mingine ni kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo kwa wakati kwa kuweka utaratibu wa kumwezesha mkulima kujitegemea kwa pembejeo ili aache kuwa tegemezi wa mikopo ya mabenki yenye riba kubwa.


Mhe Hasunga ameiagiza Bodi na Tume ya Maendeleo Ushirika kuhakikisha wanavishirikisha wakulima kupitia vyama vyao kuweka akiba ya fedha kununua pembejeo kwa kukatwa kiasi watakachokubaliana wakati wa mauzo ya tumbaku.


Pamoja na malengo hayo ya haraka, Wizara ya Kilimo inasimamia utekelezaji wa malengo ya muda mrefu yakiwemo Upatikanaji wa wanunuzi wapya wa tumbaku kwa sasa na kwa miaka ijayo kabla ya Juni, 2020, Kuongeza ubora wa zao la tumbaku kutoka asilimia 87 ya sasa hadi asilimia 92 ifikapo Juni 2022 na Kuongeza mbegu mpya na bora za tumbaku ili tuweze kupata masoko katika nchi nyingine kama vile China.


Alisema ili kufikia malengo hayo wadau wote wa tasnia ya tumbaku wanapaswa kushirikiana ili kufikia malengo hayo na wakulima kunufaika na jasho lao.


“Viongozi ngazi ya Mkoa na Wilaya wakiwemo Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Waheshimiwa Wabunge, Wenyeviti wa Halmashauri na Wakurugenzi wa Halmashauri wanaowajibu na mchango mkubwa kuendeleza zao hili kwa kusimamia Sheria zinazosimamia zao hili, kusimamia huduma za ugani na kutenga fedha kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri” Alisisitiza Mhe Hasunga


Tumbaku ni miongoni mwa mazao makuu ya kimkakati ya yaliyopewa kipaumbele na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mazao mengine ni pamoja na Tumbaku,  Kahawa, Pamba, Korosho, Chai, michikichi na alizeti.  


Mhe Hasunga alisema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa malengo ya uzalishaji yanafikiwa kwa kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa pembejeo kwa wakati, kuboresha huduma za ugani na kutafuta masoko mapya ya tumbaku.


Serikali inatumia mfumo wa uagizaji wa mbolea kwa pamoja ili kuhakikisha mbolea inafika kwa wakati, kwa bei nafuu na kudhibiti upandishaji holea wa bei. “Nichukue nafasi hii kuigiza Bodi ya Tumbaku na viongozi wa vyama vya ushirika kuhakikisha kuwa wakamilisha kwa wakati kuweka malengo ya uzalishaji na mahitaji ya mbolea ili uagizaji wa mbolea ufanyike mapema” Alisema Mhe Hasunga


Takwimu zinaonesha kwamba kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 hadi kufikia mwaka 2016 tumbaku imekuwa na mchango mkubwa wa kuliingizia Taifa fedha za kigeni.  Kwa mfano katika mwaka 2017, tumbaku iliingiza fedha za kigeni kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 195.8 ikishika nafasi ya pili baada ya zao la korosho. Licha ya faida kwa taifa, pia, uzalishaji wa tumbaku unawanufaisha wakulima, wanunuzi, viwanda vya kusindika tumbaku, mabenki, wasambazaji wa pembejeo, Halmashauri za wilaya na wadau wengine katika mnyororo wa thamani.

WAZIRI MKUU AJUMUIKA NA WATALII 330 TOKA CHINA KATIKA CHAKULA CHA USIKU

0
0
 Waziri  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii na Utamaduni katika jumbo la Zhejiang, Bw. Xu Peng, wakati alipowapokea Watalii 330 tokea nchini China, katika uwanja wa KIA mkoani Kilimanjaro, Mei 12.2019. Tokea kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni  ya Touchroad Group ya China, Bw. He Liehui  na kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangala. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii na Utamaduni katika jumbo la Zhejiang, Bw. Xu Peng, wakati alipowapokea Watalii 330 tokea nchini China, katika uwanja wa KIA mkoani Kilimanjaro, Mei 12.2019. Tokea kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni  ya Touchroad Group ya China, Bw. He Liehui  na kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kigwangala.  
  Waziri  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii na Utamaduni katika jumbo la Zhejiang, Bw. Xu Peng, kwenye chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa Watalii 330 tokea nchini China, katika Hoteli ya Mount Meru mkoani Arusha, Mei 12.2019. 
 Waziri  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watalii waliotoka China wakati alipowapokea Watalii 330 tokea nchini China, katika uwanja wa KIA mkoani Kilimanjaro, Mei 12.2019. 




Watalii tokea nchini China, wakiwa wameshika bendera ya Tanzania, kwenye chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa ajili yao, baada ya kuwasili katika uwanja wa KIA mkoani Kilimanjaro, Mei 12.2019. kushoto ni He Xiao Ping na Hu Baohua. 

 Waziri  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa zawadi ya picha ya tingatinga, Mwenyekiti wa Kampuni  ya Touchroad Group ya China, Bw. He Liehui, kwenye chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa ajili ya watalii tokea nchini China, Mei 12.2019.
 Msanii wa musiki tokea China  Di Na , akiwa amejichanganya na wasanii wa ngoma za asili nchini, kwenye chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa ajili ya watalii tokea China, Mei 12.2019.



WAKULIMA WA MPUNGA 69 WAPATIWA MAFUNZO NAMTUMBO

0
0
NA YEREMIAS NGERANGERA, NAMTUMBO
Wakulima 69 wa kijiji cha ligera wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma wamepatiwa mafunzo ya siku tatu ya Kupanda mpunga kwa njia ya Mfereji, kutawanya ,kwa njia ya ibaraki na kwa njia ya shimo ili kuwewezesha kupata mavuno ya kutosha.

Mafunzo hayo yalitolewa kwa vitendo na kwa nadharia na wataalamu wa kilimo kutoka chuo cha kilimo MATI Mtwara waliowafundisha wakulima njia za upandaji mpunga wa mabondeni na unaotegemea mvua.

Aidha wataalamu hao ni Doroth Mushi, Daudi Kasabuku na Kenedy Siame wote ni wakufunzi kutoka chuo cha kilimo MATI Mtwara ambao walifundisha namna ya kupanda mpunga aina ya Saro tano,Mtalimawangu na supermbeya.

Hata hivyo waliwafundisha wakulima hao namna sahihi ya kuvuna mpunga uliotayari kuvunwa na namna sahihi ya kuuhifadhi mpunga huo na kisha namna sahihi ya kukoboa mpunga tayari kwa kupelekwa sokoni.

Mwenyekiti wa kikundi cha wakulima wa mpunga kijiji cha ligera Lukanus Luena alisema watayatumia mafunzo hayo waliyoyapata kuongeza uzalishaji wa mpunga na kujipatia kipato kwa mwanakikundi mmoja mmoja na kikundi pia.

Bwana Luena alidai mafunzo hayo yamewaongezea morali ya kulima zaidi kwa kutumia njia sahihi za kilimo cha kisasa na kuahidi kuongeza wanachama wengine katika kikundi hicho kutokana na hitaji la wakulima wengine ambao wameonesha nia ya kujiunga na kikundi hicho cha wakulima wa mpunga.

Ofisa kilimo anayeshughulikia umwagiliaji Bwana Eleuter Mndendemi aliwataka wakulima wa kijiji cha Ligera kuyatumia mafunzo hayo vyema kwa kuonesha matokeo chanya y a mapato yanayoshabahiana na wakulima wanaolima kwa kitaalamu na kuonesha utofauti na awali kabla ya kupatiwa mafunzo hayo.

Mafunzo ya kilimo cha mpunga wa Mabondeni ( kutegemea maji ya Mvua) unafadhiliwa na JICA(Japan International Cooperation Agency) kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo pamoja na chuo cha Kilimo MATI-Mtwara.

Kikundi cha wakulima wa Mpunga wa kijiji cha Ligera kilianzishwa mwaka 2017 kikiwa na wanachama 30 na mwaka huu 2019 kikundi kina wanakikundi 80 na kati ya hao waliopatiwa mafunzo ni 69 ikiwa wanawake 29 na wanaume 40.
 Mtaalamu wa kilimo Kenedy Siame (mwenye kofia nyekundu) akiwaelekeza wakulima umuhimu wa kuzingatia vipimo wakati wa upandaji wa mpunga,Picha ya pili wakulima wakiwa katika mafunzo kwa vitendo namna ya kukata mpunga na kuuhifadhi.

VIWANJA VYA MPIRA VIKUBWA ZAIDI DUNIANI

0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
Ni ukweli usiopingika kuwa mpira wa miguu ndio mchezo wenye mashabiki wengi zaidi ukilinganisha na michezo mingine,  na hiyo imepelekea uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo ambayo vijana wanapata ajira kwa kiasi kikubwa.

Katika sekta hiyo ya mpira wa miguu kwa mujibu wa jarida la Daily Mail viwanja vikubwa vitatu vilivyotajwa ni pamoja na;

1. Uwanja Rungrado May 

Huu ni uwanja wa mpira wa miguu mkubwa zaidi duniani, unapatikana Pyongyang Korea Kaskazini, na una uwezo wa kubeba watazamaji 114,000 na ujenzi wake ulikamilika mwaka 1989 na mathalani hutumika kwa kucheza mechi kubwa za watu wengi pamoja na matukio makubwa, paa ya uwanja huo una mita 197 kutoka ardhini.

2. Uwanja wa Camp Nou

Uwanja huu unapatikana Barcelona Spain ukiwa ni uwanja wa pili kwa ukubwa duniani, tangu mwaka 1957 uwanja huo umekuwa umekuwa ukitumika kama uwanja wa nyumbani kwa timu ya Barcelona, uwanja huo unauwezo wa kubeba watazamaji 99,354 huku ukiwa uwanja mkubwa zaidi katika bara la Ulaya. Unatumika katika michezo mbalimbali ikiwemo mashindano ya Olympiki ya mwaka 1992 pamoja na fainali za UEFA, uwanja huu ulichukua takribani miaka mitatu katika ujenzi wake huku ikieleza kuwa umegharimu zaidi ya shilingi milioni 288.

3. Uwanja wa FNB Soccer City

Uwanja huu unapatikana Johannesburgy nchini Afrika Kusini ukiwa ni uwanja mkubwa zaidi Afrika huku ukishika nafasi ya tatu kwa ukubwa duniani, uwanja huu una uwezo wa kubeba mashabiki 94,736 na unapatikana  jirani na makao makuu ya shirikisho la mpira wa mguu nchini humo.

Uwanja wa FBN ulitangazwa zaidi katika uzinduzi wa fainali za kombe la duniani mwaka 2010 ambapo timu za Netherlands na Spain zilicheza kubwa zaidi mwaka 1990 uwanja huo ulitumiwa na aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Nelson Mandela kuhutubia wananchi kwa mara ya kwanza mara tu alipoteka jela.

WALIMU KINGS KIZIMBANI KWA KUFANYA KAZI NCHINI BILA KIBALI

0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
WALIMU wanne, raia wa Kenya,  wanaofundisha shule ya msingi na Sekondari ya  Kings na Mtanzania mmoja, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kufanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali.

 Akisoma hati mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile, wakili wa serikali Faraji Nguka, amewataja washtakiwa hao kuwa ni.Esrom Maina, (45), Ruth Njuguna (30), Joseph Kuria (30), Charles Sakawa (32) na mtanzania Stella Bizulu (44).

Imedaiwa kati ya Septemba 2018 na Machi 18, 2019 huko katika shule  ya msingi na Sekondari ya Kings iliyoko eneo la Goba ndani ya Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam,  washtakiwa hao raia wa Kenya walikutwa wakifanya kazi ya ualimu katika shule hiyo bila ya kuwa na kibali kutoka idara ya Uhamiaji.

 Katika shtaka la pili  imedaiwa, siku na mahali hapo mshtakiwa Bizulu,  akiwa kama Meneja wa shule hiyo, aliwaajiri walimu hao bila ya kuwa na kibali cha kufanya kazi nchini kutoka Uhamiaji.

Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na wameachiwa kwa dhamana hadi Mei 15, ambapo upande wa mashtaka unatarajiwa kufanyia mabadiliko hati ya mashtaka.

Sera ya Ugatuaji wa Madaraka Imekwama Wapi

0
0




Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akifungua kikao cha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa cha kupitia rasimu ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga akitoa taarifa ya utangulizi kwenye ufunguzi wa kikao cha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa cha kupitia rasimu ya Sera ya Taifa ya ugatuaji wa madaraka kilichofanyika katika ukumbi wa St. Gasper Jijini Dodoma.
Baadhi wa Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo wakati akifungua kikao cha kupitia rasimu ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.
Baadhi wa Makatibu Tawala wa Mikoa wakimsikiliza Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo wakati akifungua kikao cha kupitia rasimu ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (watatu kutoka kushoto aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa mara baada ya kufungua Kikao cha kupitia Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (watatu kutoka kushoto aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala mara baada ya kufungua Kikao cha kupitia Sera ya Taifa ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.

……………………………………………………………………………………………………..

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI

Kutokuwepo kwa Sera ya Ugatuaji Madaraka iliyojengwa kwenye mfumo wa Sheria ni moja ya changamoto iliyofanya Serikali kufanya mapitio ya sera hiyo.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo(Mb) wakati wa kufungua kikoa kazi kilichokutanisha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kutoka Mikoa yote 26 kwa ajili ya kutoa maoni na mapendekezo kwenye Rasimu ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji Madaraka ya 2019.

Alisema kuwa changamoto moja wapo ni kutokuwepo kwa sera ya ugatuaji iliyojengwa kwenye mfumo wa kisheria inayoelekeza mipaka, majukumu na utaratibu wa utekelezaji wake, jambo ambalo linafanya ionekane kama ni hiari na utashi (Voluntary and Willingness).Jafo alisema changamoto nyingine ni kuwepo kwa mitazamo inayokinzana kati ya watendaji na viongozi wa kisiasa katika ngazi ya vijiji, kata na halmashauri katika kuweka vipaumbele na kutekeleza miradi ya maendeleo

Aliongeza kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zimekuwa zikitegemea fedha kwa kiasi kikubwa kutoka Serikali kuu na kutolea mfano kwa mwaka 2018 zilitegemea zaidi ya asilimia 88 ya mapato.“ Wizara za Kisekta kuandaa sera na sheria na kupeleka halmashauri kwa ajili ya utekelezaji bila kuambatanisha rasilimali fedha, vifaa na watu.”

Waziri Jafo alibainisha kuwa uelewa mdogo wa dhana ya Ugatuaji wa Madaraka (D by D) kwa baadhi ya Wizara za Kisekta na hivyo Sera hii kuonekana kama ni suala ya OR-TAMISEMI kwa kiasi kikubwa imechangia kufanya Sera hii kutotekelezeka kwa kiwango kilichotegemewa.Jafo aliongeza: “Kwa ujumla hatujafikia kiwango cha mafanikio kilichotarajiwa kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeaza na ndio maana Serikali imeamua kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji ili kupata suluhisho la changamoto zilizojitokea.

Aidha, Jafo amewataka wakuu wa mikoa na makatibu tawala kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kutoa maoni na mapendekezo hayo ili kuboresha rasimu hiyo kwa maslahi mapana ya wananchi, wadau na taifa kwa ujumla.

Aidha Mhe. Jafo alitumia fursa hiyo kuwahimiza wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa kuhakikisha wanasimamia kwa ukabilifu fedha na utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwamo ujenzi wa vituo vya afya, ujenzi wa hospitali za wilata, ujenzi wa mabweni, madarasa, vyoo katika shule za msingi na sekondari ambayo tayari fedha zake zimeshatolewa na serikali.

Naye Mwenyekiti wa wakuu wa mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng. Evarist Ndikilo aliahidi kushiriki mzuri wa wawakuu hao kwa kuwa wao ndio wanaotoka kwa wananchi.Pia alimhakikishia Waziri Jafo kuwa watasimamia kwa umakini utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuwa itakamilika katika muda uliopangwa na kwa ubora unaotakiwa.

Naye Mwakilishi wa UNICEF, Pius Chaya alisema agenda ya mapitio ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji Madaraka imekuja wakati muafaka, kwasababu Serikali inatakiwa kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma wanazostahili na ambazo zinawafikia kwa wakati.

Aidha, Chaya alisema wadau wa maendeo ambao pia wameshiriki katika machakto wa mapitio ya sera hiyo wameahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya awamu ya tano katika kuwaletea wananchi wake maendeleo

Sera ya Ugatuaji wa Madaraka ni dhana ya Kupeleka Madaraka, Majukumu na Rasilimali kutoka Serikali Kuu kwenda kwa Wananchi kupitia vyombo vya kidemokrasia na Kisiasa ambavyo, wajumbe wake huchaguliwa na kuwajibika kwa Wananchi na vimepewa Mamlaka ya kutoa Maamuzi na kusimamia rasilimali (yaani vina uhuru, vinajitawala, na vina hadhi ya kisheria).

Sera hii ilianza kutekelezwa mwaka 1998 kupitia mpango wa maboresho ya Serikali za Mitaa ikiwa na lengo la kuwawezesha wananchi kushiriki shughuli za Maendeleo katika maeneo yao na kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa shughuli za Serikali.

International Mother's Day

0
0
Mothers across the country have been encouraged to endlessly pursue their careers without giving up while taking care of their families.
 
Speaking during a mother’s day forum on Friday in Dar es Salaam organised by NMB to commemorate Mother’s day (celebrated internationally today) Head, Customer Experience at NMB Ms Abella Tarimo said that for people to achieve anything in life they need clarity on what they what to achieve, how to achieve and lastly a way to measure success.

“As long as one has a clear vision and support system juggling between a career & family is manageable. Most women believe caring for a family and establishing a career at the same time is an impossible task for a mother to achieve,” she said.

Themed ‘Glass Ceiling and Motherhood’, Ms Tarimo stressed that no one can accomplish things alone. “Working mothers should establish support systems no matter what they want to accomplish at home or work.”

She pointed out that, “Mothers need to be there for their children, especially those who are still breastfeeding. It does cause challenge to careers but this is where as mothers we need to use our resourcefulness to be able to balance home and work, and this is where the support system comes in.”

She explained that the support system can be members of the family, husband, maids; people that will be a helping hand for a mother or any person who has focused in achieving a targeted goal. “A mother just needs to realize the type of support system she needs.”

On the other hand, Senior Relationship Manager; Business Liability, Business Banking Ms Beatrice Mwambije said that working mothers who are overwhelmed and think of quitting their career to take care of their children need to evaluate the situation first before doing so.

The rigorous daily schedule of caring for an infant may tempt mothers to stay at home and care for their children. However, if you are a career person, there are ways you can strike a balance and achieve both successfully. Establish plans on how you can balance both career and family,” she commented.

Adding that, “Mothers should think of the future in terms of financial security and their relevance as human beings after the children are grown up. Plan the future while putting all into consideration like sudden death or illness of a partner before deciding that quitting your job is the best option.”

 Pauline Mohele, (center) NMB’s Manager Recovery, Special Asset Management, speaking during a panel discussion organised by NMB Bank Plc to commemorate World’s Mother’s Day themed ‘Glass Ceiling and Motherhood’. Right is Beatrice Mwambije, Senior Relationship Manager; Business Liability, Business Banking and NMB’s Head, Customer Experience, Abella Tarimo (left).
Lillian Mwinula, (1ST right) NMB’s Senior Manager Special Projects, speaking during a panel discussion organized by NMB Bank Plc to commemorate World’s Mother’s Day themed ‘Glass Ceiling and Motherhood’. Left is NMB’s Head, Customer Experience, Abella Tarimo, Pauline Mohele, (centre ) NMB’s Manager Recovery, Special Asset Management and Right is Beatrice Mwambije, Senior Relationship Manager; Business Liability, Business Banking.

SERIKALI INAFANYA MAZUNGUMZO NA CYPRUS ILI KUWALIPA WATEJA WA BENKI YA FBME Inbox x

0
0
Na. Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Serikali ya Tanzania inafanya mazungumzo na Serikali ya Cyprus ili kuweza kutatua changamoto za malipo kwa wateja walioweka amana zao katika Benki ya FBME ambayo ilifutiwa leseni ya kufanya shughuli za kibenki hapa nchini na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Viti maalaum  Mhe. Asha Abdullah Juma, alieuliza kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali kuwasaidia wananchi walioweka amana zao katika Benki ya FBME.
Dkt. Kijaji alisema kuwa zoezi la kukusanya mali na fedha zilizokuwa za Benki ya FBME katika taasisi mbalimbali za fedha hasa zilizopo nje ya nchi, limekumbwa na changamoto za kisheria kati ya Tanzania na Cyprus ambako benki ya FBME ilikuwa ikiendesha sehemu kubwa ya biashara zake hivyo kusababisha ucheleweshaji wa ukusanyaji na ugawaji wa fedha na ufilisi.
“Hakuna tarehe rasmi ya kuanza kulipa fedha kwa sasa kutokana na uwepo wa kesi zinazokwamisha zoezi la ukusanyaji mali na madeni ya Benki ya FBME”, alieleza Dkt. Kijaji.
Alisema kuwa, Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 inaeleza kuwa amana au akiba za wateja katika Benki au Taasisi zina kinga ya Bima ya Amana ya kiasi kisichozidi Sh. milioni 1.5,  na iwapo mteja ana salio la amana la kiasi kisichozidi Sh. 1.5 atapata fidia ya asilimia 100.
Aidha wateja walio na zaidi ya Sh. milioni 1.5 wanalipwa Sh. milioni 1.5 kama fidia ya bima ya amana na kiasi kinachobakia kinalipwa kwa mujibu wa Sheria na taratibu za Ufilisi.
Hata hivyo malipo kwa mujibu wa Sheria na taratibu za ufilisi yanategemea makusanyo ya fedha kutoka kwenye mauzo ya mali pamoja na fedha zilizowekwa na benki katika taasisi mbalimbali za fedha za ndani na nje ya nchi.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).

RAIS DKT.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA AFYA ZANZIBAR

0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar , wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Afya Zanzibar kwa Kipindi cha Julai 2018 -Marchi 2019.(Picha na Ikulu)
 KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Ali Abdalla akiwasilisha Mpango Kazi wa Wizara ya Afya Zanzibar kuazi Julai 2019 hadi Marchi 2019, uliofanyika katika ukumbi wa mkutano Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.kulia Mshauri wa Wizara ya Afya Zanzibar Dr. Mohammed Jidawi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi.
 VIONGOZI wa Wizara ya Afya Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa Mkutano Ikulu Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Afya Zanzibar kwa kipindi cha Julai 2018 hadi Marchi 2019, uliofanyika katika Ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 MKURUGENZI Mkuu Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar Dr. Mayasa Salum Ally akichangia wakati wa mkutano huo wa Utekelezaji wa Mipango Kazi Wizara ya Afya uliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
 MKURUGENZI Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dr. Fadhil Mohammed akichangia wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Afya Zanzibar.wakati wa mkutano huo.
 MKURUGENZI wa Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar Dr. Zahrani Ali Hamad, akichangia wakati wa mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpongo Kazi wa Wizara ya Afya Zanzibar. uliofanyika katika ukumbi wa mkutano Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
 NAIBU Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar Mhe. Harusi Said Suleiman akizungumza wakati wa mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Afya Zanzibar

Wanawake washauriwa kuendeleza ujuzi wao huku wakizingatia majukumu ya familia zao

0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB, mkoani Mwanza wakitoa msaada kwenye Kituo cha Afya cha Buzuruga wodi ya Mama na Watoto-Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mama Duniani.


WANAWAKE nchini wameshauriwa kutokata tamaa kufanyia kazi taaluma walizonazo huku wakizihudumia familia zao kwa mujibu wa majukumu yao nyumbani.

Ushauri huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Abella Tarimo katika mjadaLa ulioandaliwa na benki hiyo kuadhimisha Siku ya Mama Duniani (Mother's Day).

Alisema ili wanawake waweze kufanikiwa katika jambo lolote juhudi na uwazi juu ya suala wanalolifanya zinahitajika."Ili mradi mtu uwe na nia na unaungwa mkono huku ukiweka jitihada za dhati bila kusahau familia yako, utafanikiwa. Wapo baadhi ya wanawake ambao wamekuwa wakijikwamisha kwa kudhani kuwa hawawezi kufanyia kazi ujuzi waliousomea na kufanikiwa huku wakizihudumia familia zao ipasavyo, jambo ambalo si sawa," alisema Bi. Tarimo.

Alisema kwa kuanzia mafanikio wanawake wafanyakazi hawana budi kujenga utamaduni wa kushirikiana pamoja na kuungana mkono bila kuathiri majukumu yao kifamilia.

Kwa upande wake Meneja Uhusiano Mwandamizi, Amana na Biashara wa NMB, Beatrice Mwambije akichangia mada katika mjadala huo, aliwataka akina mama ambao wako kazini na wamekata tamaa na hata kufikiria kuacha kazi ili wakalee familia zao kutathmini mara mbilimbili kabla ya kufanya maamuzi yao."Ni kweli ukiangalia majukumu ya mama mwenye mtoto mchanga anaweza kubanwa akashindwa kutekeleza kazi zake ofisini...lakini hiki kisiwe kikwazo kuna namna unaweza kujipanga na kukabiliana na yote hayo na ukaendelea na kazi pasipo kuathiri pande zote," alisema Bi. Mwambije.

Aidha aliwataka akinamama kuangalia usalama wa familia na watoto kwa maisha ya baadaye wanapokuwa wakubwa hivyo kuna kila sababu ya kuwajengea msingi imara.Mjadala huo ulioandaliwa na Benki ya NMB ulienda sambamba na maadhimisho ya 'Siku ya Mama Duniani’ huku ukisisitiza kutambuliwa kwa majukumu ya kinamama duniani kote kwani wanamchango mkubwa kimaendeleo.

Benki ya NMB imeadhimisha siku hii kwa kualika wadau mbalimbali kujadili mada ya mama katika matawi yake yote nchi nzima pamoja na baadhi yao kutoa misaada kwa watoto na akina mama.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB matawi mbalimbali, wakiwa katika picha za kumbukumbu mara baada ya maadhimisho ya Siku ya Mama Duniani. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB matawi mbalimbali, wakiwa katika picha za kumbukumbu mara baada ya maadhimisho ya Siku ya Mama Duniani. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB matawi mbalimbali, wakiwa katika picha za kumbukumbu mara baada ya maadhimisho ya Siku ya Mama Duniani.
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images