Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

Serikali Yaahidi Kukarabati Karakana za Uhandisi SUA

$
0
0

Na Mariam Mwayela, SUA 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeahidi kutoajumla ya Tsh. 750 milioni kupitia mradi wa kukuza ujuzi na stadi za kazi (ESPJ) ili kukarabati karakana mbalimbali hasa zile za uhandisi kilimo. 

Akizungumza wakati akifungua rasmijjuma la Kumbukizi ya Sokoine Dkt. Leonard Akwilapo amesema kuwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kina mchango mkubwa katika azma ya kuleta mapinduzi katika Kilimo hivyo ukarabati wa karakana hizo una dhumuni la kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine. 

“Katika siku hii ya kihistoria Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itakiunga mkono Chuo kwa kufanya ukarabati mkubwa wa Karakana ili karakana hizi ziwe bora na ziendane na mwenye jina la Chuo, Hayati Sokoine” alisema Dkt. Akwilapo. 

Aidha aliongeza kuwa mada ya kumbukizi hili imejikita vyema katika mipangoya sasa ya serikali ya Awamu ya tano hususani dhana kuu tatu ambazo ni uzalishaji katika kilimo, mageuzi ya viwanda na maendeleo ya Tanzania na hivyo kuwataka wanataaluma kufanya uwasilishaji na mijadala mizuri ya maandiko katika mkutano wa kisayansi ili kuwa na mipango mizuri kwa mustakabali wa baadaye kwa kuangalia matokeo ya maadhimisho ya mwaka huu ya kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine. 

Naye Makamu wa Mkuu wa Chuo, Prof. Raphael Chibunda alisema kuwa kumbukizi hili limekuwa ni chachu ya kuendeleza mambo mazuri aliyoyafanya Sokoine na kuhakikisha maono yake yanakuwa hai. 

“SUA imekuwa ikifanya kumbukizi hili ikiwa ni kama sehemu ya kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine kwa kuendeleza mambo aliyoyafanya na kufanya maono yake kuwa hai kwa ajili ya maendeleo ya Taifa”, alisema Prof. Chibunda. 

Prof. Chibunda alisema pamoja na maonesho ya kazi za SUA pamoja na teknolojia pia kutakuwa na mdahalo wa kitaifa ambapo maarifa yatakayopatikana yatahaririwa kwa umahiri na umakini mkubwa na kuchapishwa kwenye toleo maalumu la Jarida la Kisayansi. 

Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 7 Mei, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli alitembelea Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo na kutoa matrekta 10 kwaajili ya mafunzo kwa vitendo ya wanafunzi na wananchi kwa ujumla. Hivyo basi ujio huu wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na ahadi aliyoitoa inaonyesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kutekeleza Sera ya Taifa ya Kilimo ya mwaka 2013 yenye lengo la kuifanya sekta ya kilimo kuwa yenye ufanisi, ushindani na yenye kuleta faida ambayo itachangia kuboresha maisha ya Watanzania na hivyo kufikia uchumi mkubwa na kupunguza umasikini

OSHA yawa Taasisi ya wstu wengine kujifunza

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Wakala wa Afya wa Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) imesema kuwa OSHA imekuwa sehemu ya watu wengine kujifunza kutokana na utoaji wa huduma sehemu za kazi.

Akizungumza na waandishi habari Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa OSHA Joshua Matiko  wakati wa ugeni wa Wizara ya Kazi ,Uwezeshaji ,Wazee,Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walipotembelea  OSHA kwa ajili ya kujifunza utoaji wa usalama wa afya mahala Pa Kazi.
Matiko amesema kuwa nia ya OSHA ni kuwa Taasisi kubwa ya watu kujifunza masuala ya utendaji mahala pakazi na kuweza kupata tija.

Amesema kuwa serikali ya mapinduzi kuja kujifunza licha ya kubadilishana mawazo inaunganisha udugu uliopo kati ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani. Matiko amesema kuwa Zanzibar kwenda kujifunza sio peke yao bali hadi taasisi za nje zimefika kujifunza na kwenda kwao kuunda chombo kama OSHA.Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kutokana na kutoa elimu kwa ajili kumepungua kwa magonjwa na majanga mahala pakazi kutokana na elimu wanayoitoa.

Nae Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shadia Mohamed Suleiman amesema kuwa OSHA wana vitu vizuri ambapo tukienda  kufanyia kazi tutaweza kupata mabadiliko katika mahala pakazi. Shadia amesema kuwa licha ya kujifunza ni pamoja na kuishauri serikali kuanzisha wakala inayojitegemea ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo, Wanawake ,Habari ,Utalii na Vijana Mwantatu Mbaraka Khamis amesema OSHA imezatiti katika kulinda usalama wa afya mahala pakazi kutokana na utendaji wake pamoja na kuwa  wataalam wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Afya wa Usalama Mahala Pakazi (OSHA) Joshua Matiko akizungumza kuhusiana na ugeni kutoka Zanzibar kujifunza katika wakala huyo.
 Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji,Wazee ,Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shadia Mohamed Suleiman akizungumza kuhusiana na ujio wao katika Wakala wa Afya wa Usalama Pahala Pakazi (OSHA) jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji,Wazee ,Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shadia Mohamed Suleiman akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya Bunge na Kaimu Mkurugenzi OSHA.

WAZIRI WA UJENZI, MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI WA SMZ DK. UBWA MAMBOYA AIPONGEZA TTCL

$
0
0

Mhandisi wa Mitambo ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Aman Kichere (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mhe. Dk. Sira Ubwa Mamboya (katikati) namna mitambo ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano inavyofanya kazi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba akishuhudia.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mhe. Dk. Sira Ubwa Mamboya (kushoto) akizungumza mara baada ya ziara yake kutembelea Miundombinu na Mitambo ya Mawasiliano inayosimamiwa na TTCL Corporation. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba akiwa na mgeni wake.

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation Bw. Waziri Kindamba (mwenye kipaza sauti) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mhe. Dk. Sira Ubwa Mamboya (kushoto) alipotembelea miundombinu na Mitambo ya Mawasiliano inayosimamiwa na TTCL Corporation.

Waziri, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation Bw. Waziri Kindamba (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mhe. Dk. Sira Ubwa Mamboya (kulia mbele) alipotembelea miundombinu na mitambo ya mawasiliano inayosimamiwa na TTCL Corporation. Wengine ni maofisa kutoka TTCL Corporation, na Wizara ya Mawasiliano Zanzibar.







Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mhe. Dk. Sira Ubwa Mamboya (mbele) akitembelea miundombinu na mitambo ya mawasiliano inayosimamiwa na TTCL Corporation. Wengine ni maofisa kutoka TTCL Corporation, na Wizara ya Mawasiliano Zanzibar.



WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Sira Ubwa Mamboya, amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Shirika lsa Mawasiliano Tanzania( TTCL Corporation) katika kutoa huduma bora za Mawasiliano na usimamizi wa Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano Nchini.

Mhe Waziri Dkt. Sira Ubwa Mamboya,ametoa pongezi hizo Jijini Dar Es Salaam mara baada ya ziara yake katika Shirika la Mawasiliano Tanzania, kutembelea Miundombinu na Mitambo ya Mawasiliano inayosimamiwa na TTCL Corporation.

Katika salamu zake, Mhe Waziri amepongeza utendaji wa TTCL mpya ambayo inafanya juhudi kubwa za kuliimarisha Shirika na huduma zake na kuonesha kufurahishwa na utaratibu wa Shirika hilo kutoa ajira kwa kuzingatia pande zote za Muungano hali inayoimarisha udugu na uhusiano mwema.

Akizungumza katika salamu za kumkaribisha Mhe. Waziri, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation Bw Waziri Kindamba amewashukuru viongozi Wakuu wa SMZ kwa uongozi wao thabiti unaodumisha Muungano na kustawisha ushirikiano unaoiwezesha TTCL Corporation kutimiza vyema majukumu yake katika Ofisi zake zote Tanzania Visiwani ambapo inaihudumia Serikali, Taasisi za Umma na Sekta binafsi.

“Tunapopata ugeni kama huu, tunafarijika sana kwani kupitia tukio hili, uhusiano mwema wa kindugu baina ya pande mbili za Muungano unaimarishwa, Aidha, tunabadilishana ujuzi na uzoefu pamoja na kujenga mtazamo wa pamoja wa namna bora zaidi ya kuwahudumia Wananchi wetu” amesema Kindamba.

Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation lilizaliwa tarehe 01 Februari 2018, kwa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2017. Kuundwa upya kwa Shirika hili la TTCL Corporation ni matokeo ya kukamilika kwa mchakato wa kutunga sheria uliopitia katika hatua zake zote ikiwemo kuridhiwa na Bunge na hatimaye kupata idhini ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 28 Novemba, 2017.

Huduma za mkongo wa Taifa wa Mawasiliano zinazosimamiwa na kuendeshwa na TTCL zimeiwezesha Tanzania kuwa Nchi ya kupigiwa mfano katika Ukanda wa kiuchumi wa Nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara kutokana na kuwa na mfumo mzuri zaidi kukusanya kodi kwa kutumia mfumo maalumu wa kielektroniki wa Serikali ujulikanao kama GePG.

AKWILAPO ATAKA SUA KUSAIDIA ONGEZEKO LA UZALISHAJI KILIMO

$
0
0
katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na teknolojia Dokta Leonard Akwilapo amesema hali ya uzalishaji wa chakula nchini inaelezwa kuwa ndogo,ambapo takwimu za uzalishaji za mwaka 2015 zinaonesha kuwa ni asilimia tatu nukta tatu kwa mujibu wa mpango wa Taifa ya maendeleo ya awamu ya pili 2016/ 2017, 2020/ 2021 ambapo mpango wa serikali unatajwa kupandisha kiwango hicho kufikia asilimia nne nukta sifuri ifikapo kabla ya mwaka 2025…

Katika kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa,Katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo anatumia kumbukizi ya miaka kumi na sita ya kifo cha hayati Edward Moringe Sokoine kukiagiza chuo kikuu cha Sokoine (SUA ) kuhakikisha kinatumia wataalamu wake katika kufanikisha dhana hiyo.

“kwa pamoja tunakazi kubwa ya kufanya ili kufikia lengo hili kilimo chetu kinapaswa kukuzwa na kuwa cha kisasa Zaidi” alisema dkt akwilapo. Pia katibu mkuu amehaidi kutoa million 750 kutoka mradi wa kukuza ujuzi na stadi za kazi kwa ajili ya kuboresha kalakala ya idara uhandisi kilimo katika chuo hicho cha kilimo SUA..

Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Profesa Raphael Chibunda amesema chuo kimeaandaa mdahalo kwa kuwakutanisha wanasanyansi na watu ambao wamefanya kazi pamoja na Sokoine ili kupata kwa kiina yale aliyofanya Marehemu huyo ambapo mada kuu ni Uzalishaji wa kilimo na Viwanda na Maendeleo ya Tanzania mabo ya kujifunza kutoka kwa sokoine na na siku zijazo..

“Tumewaalika wazee waliofanya kazi na hayati sokoine enzi za uhai wake na wametukubalia ambao watatupatia uzoefu wa namna ya utendaji wake enzi za uhai wake jambo litakalokuwa na tija kwetu” alisema Prof chibunda.. mwakilishi wa familia ya aliyekuwa waziri mkuu wa serikali ya awamu ya kwanza hayati Edward Moringe Sokoine Bw. Ole Edward amesema kama familia wameanda wakfu ili kuendelea kuyaenzi yale aliyofanya marehemu Sokoine…

Hayati Edward Moringe Sokoine alifariki aprili 12 mwaka 1984 katika eneo la Wami sokoine wilayani Mvomero akitokae Bungeni katika majukumu ya kikazi na wiki ya kumbukikizi hiyo imeanza aprili 9 mwaka huu na inatarajiwa kufikia kilele aprili 12 mwaka huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Raisi mama samia Suluhu Hassani.
 Katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na teknolojia Dokta Leonard Akwilapo kulia akiwa na makamu mkuu wa chuo kikuu cha Sokoine cha  Kilimo SUA Profesa  Raphael Chibunda wakitazama moja ya njia rafiki ya kkilimo ch

 Katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na teknolojia Dokta Leonard Akwilapo, wa pili kutoka kushoto akiambatana na katibu tawala mkoa wa morogoro cliford tandari katika ukaguzi wa miradi mbalimbali ya kilimo chuo cha Sokoine.

NMB ‘kusomesha’ wafanyabiashara 10 China

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Albert Jonkergouw akiangalia moja ya bidhaa za Mkurugenzi wa Malaika Home Essentials, Rachael Moyo wakati wa Kongamano la wafanyabiashara Business Club Ilala lililofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha biashara, Donatus Richard.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Albert Jonkergouw wakati wa Kongamano la wafanyabiashara Business Club Ilala lililofanyika jijini Dar es Salaam jana.Picha ya kuchora.



KATIKA kuwaongeza uelewa, maarifa na elimu ya kujenga nidhamu ya fedha kwenye biashara zao, Benki ya NMB imeahidi kuwapeleka China kwa masomo na warsha wafanyabiashara 10 kutoka katika Klabu za Biashara za benki hiyo ‘NMB Business Club,’ baadaye mwaka huu.

Ahadi hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB, Donatus Richard, wakati wa kongamano la Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati (MSE), wanaounda Klabu za Biashara za NMB, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Kardinali Rugambwa, Oysterbay.

Richard alibainisha kuwa, lengo la ziara hiyo ya mafunzo ni kuimarisha uelewa wa masuala ya fedha miongoni mwa wafanyabiashara wanaounda klabu hizo, lengo likiwa ni kuwaongezea elimu ya kuhakikisha mtiririko wa fedha kwenye biashara zao, unakuwa mnyoofu.

Akisisitiza ahadi hiyo, mbele ya wafanyabiashara zaidi ya 300 walioshiriki kongamano hilo, Richard alisema kuwa mchakato wa namna ya kuwapata wateule wa ziara hiyo utatangazwa miongoni mwao,ili kwenda kupata fursa za kimataifa, safari ikitarajiwa kufanywa Oktoba mwaka huu.

“Ushindani kibiashara nchini umekuwa mkubwa, nasi ndio maana tunatumia klabu hizi kufundisha mifumo, njia na mipango rafiki ya kuimarisha biashara za wateja wetu hawa ambao pia ni mabalozi wetu kwa jamii. Tutawapeleka China kujiongezea maarifa juu ya hilo,” alisema Richard.

Awali akifungua kongamano hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Albert Jonkergouw, alisema watayafanyia kazi mapendekezo yote yatakayotolewa na wafanyabiashara wanaohudhuria makongamano yao kutoka klabu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na punguzo la gharama za uendeshaji wa akaunti ya biashara.

Jonkergouw alibainisha ya kwamba, Klabu za Wafanyabiashara ni nzuri na muhimu sio tu kwa wanachama wake na Benki ya NMB, bali pia kwa ustawi na ukuaji wa uchumi wa Taifa na kwamba wafanyabiashara hao ni kati ya mabalozi wema wa benki hiyo.

“Kongamano hili ni kati ya fursa tunazozitumia kusikiliza changamoto zenu, kujadiliana namna ya kuzitatua na mwisho wa mwezi kwenda pamoja katika kasi ya uchumi wa mteja mmoja mmoja, benki kama taasisi na taifa kwa ujumla wake,” alisisitiza Jonkergouw.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara waliohudhuria, aliishukuru NMB kwa kuwakabidhi baadhi yao vyeti vya ubalozi mwema wa benki kwa wafanyabiashara wa kupigiwa mfano, Award Mpandila, aliitaka Serikali kuwasaidia ujenga mazingira rafiki ya kibiashara.

Mpandila alifafanua kwamba, moja ya changamoto zinazokwaza biashara zao ni tozo zisizo wazi hususani bandarini, ambazo zinawakwamisha na kusababisha kutorejesha mikopo yao kwa wakati, kutokana na kuchelewesha kwa uondoshaji mizigo bandarini.

MBARAKA YUSUPH KUKAA BENCHI MIEZI TISA

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii. 

MSHAMBULIAJI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC Mbaraka Yusuph anatarajia kukaa nje ya dimba kwa muda wa miezi tisa ijayo baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti jana jijini Cape Town huko nchini  Afrika kisini. 

Uongozi wa klabu hiyo umesema kuwa nyota huyo amekutwa na tatizo la kuchanika mtulinga wa kati wa goti lake la mguu wa kulia (Anterior Cruciate Ligament Tear), hali iliyomlazimu  afanyiwe upasuaji huo Katika Hospitali ya Vincent Pallotti iliyopo nchini Afrika kisini.

Yusuph amepata majeraha hayo wakati akiwa kwenye kikosi cha Namungo kinachoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL), iliyomchukua mchezaji hiyo kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. 

Aidha Daktari wa Azam FC, Dr. Mwanandi Mwankemwa, aliyeongozana na mshambuliaji huyo nchini humo kushughulikia matibabu yake ametoa ripoti ya mchezaji huyo

Mwankema  amesema kuwa " Yusuph anatarajia kurejea tena dimbani kwa ajili ya ushindani Desemba 8 mwaka huu"

Kunako Ligi soka Tanzania bara Azam anatarajia kushuka dimbani April 14  mwaka huu wakiwa wageni dhidi ya Mbeya City Katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya majira ya Saa kumi jioni. 

Ambapo Katika mchezo uliopita kikosi cha Azam kilionekana kufanya vibaya  akilazimika sare ya bila kufungana dhidi ya Mbao FC  mechi iliyochezwa Jijini Mwanza CCM Kirumba. 

Wana lambalamba hao bado wanashikilia nafasi ya 2  kwa alama 63 wakiwa wameshacheza michezo 30 sawa na Yanga Sc mwenye alama 71 ambao ni Vinara wa  Ligi hiyo Tanzania bara, huku wekundu wa msimbazi Simba SC akiwa nafasi ya Tatu kwa pointi 57 ambaye Mpaka sasa anamichezo 22.

MKE WA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA UDART KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUUZA MAFUTA BILA KIBALI

$
0
0
 Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MKE waliyekuwa Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART) Robert Kisena (46), Florencia Mashauri amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashitaka sita likiwemo shtaka la kuuza mafuta bila kibali na kusababisha hasara ya Sh bilioni 2.4.

Florence ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Zenon, na mkazi wa mtaa wa Isevya Upanga, amefikishwa mahakamani hapo April  10, 2019 na kusomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi, Augustino Rwizile.

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali, Ester Martin akisaidiana na Fatuma Waziri, amedai, kati ya Januari Mosi, 2011 na Mei 31,2018 katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa  Florence akiwa na watu ambao hawapo mahakamani, waliratibu genge la uhalifu.
Imeendelea kudaiwa kuwa, kati ya Januari Mosi, 2015 na Desemba 31, 2017 huko katika maeneo ya Jangwani wilayani Ilala mshtakiwa akiwa Mkurugenzi wa Zenon Oil & Gas Limited, alijenga Kituo cha mafuta cha Petroli kilichopo yadi ya Kituo cha Mabasi ya Mwendokasi bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Imedaiwa, mshitakiwa huyo ambaye anajulikana pia kwa jina la Florencia Membe, akiwa Mkurugenzi wa kampuni hiyo, alianzisha biashara ya kuuza mafuta katika eneo lisiloruhusiwa.

Katika shtaka la nne,  imedaiwa kati ya Mei 25, 2015 na Desemba 31, 2016 maeneo ya Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDA-PLC), aliiba mafuta ya Sh 1,216,145,375.10 mali ya UDA

Aidha imedaiwa,  kwa lengo la kuhalalisha au kuficha uhalisi alibadili mafuta ya Sh 1,216,145,375.10 kwa kuyauza wakati akijua kwamba mafuta hayo ni zao la uhalifu. Pia mshtakiwa Florence anadaiwa kumiliki Sh bilioni 1.2 huku akijua kwamba fedha hizo ni zao la kosa la wizi.

Katika mashitaka ya kuisababishia serikali hasara inadaiwa kuwa kati ya tarehe hizo, Florence  aliisababishia UDART hasara ya Sh 2,414,326,260.

Hata hivyo, mshitakiwa hukuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi  ambazo kwa kawaida husikilizwa Mahakama Kuu au kwa kupata kibali kutoka kwa DPP.

Kwa Mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.  

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 23, kesi hiyo itakapokuja tena mahakamani hapo kwa kutajwa, mshitakiwa amerudishwa rumande

Agizo la Waziri halijadiliwi, ni kutekeleza – Prof. Kikula

$
0
0
Na Issa Mtuwa- Ulanga Morogoro
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amewataka  Watumishi wa tume hiyo ofisi ya Morogoro na Ulanga kutambua kwamba agizo la Waziri linalowataka kufuta leseni zisizofuata utaratibu wa kisheria sio la kujadili bali ni kutekeleza. Prof. Kikula ameyasema hayo Aprili 10, 2019 wilayani Ulanga wakati akizungumza na watumishi wa tume hiyo wakati wa ziara yake. 

Taarifa iliyosomwa kwake na Afisa Migodi Mkazi ofisi ya Mahenge Ulanga, Tandu Jilabi inaonyesha kuwa wilaya ya Ulanga ina leseni za wachimbaji wadogo 221 kati ya hizo ni leseni 9 tu ndio zinazofanya kazi huku leseni za uchimbaji wa kati zikiwa 5 na leseni za utafiti wa madini 13.
 Kufuatia hali hiyo, Afisa Migodi Mkazi ofisi ya Mahenge ameiomba tume ya madini kufuta leseni zisizofanya kazi ili wapewe wenye uhitaji ili waweze kuziendeleza. Kufuatia ombi hilo, Mwenyekiti wa tume amesema jukumu la kuzifuta leseni hizo ni la kwake pamoja na Afisa Madini Mkazi Morogoro na halina mjadala kwakuwa muongozo wa utekeleza wa suala hilo ulishatolewa na waziri wa Madini.

“Suala la leseni zisizofanya kazi sio la kujadili, hili ni agizo la Waziri na kazi yetu ni kutekeleza na wenye kuzifuta ni ninyi, fuateni taratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria katika kuzifuta na sio kuzifuta lazima wote waliozishikilia leseni hizo kwa muda wote walipe fidia na wasipo fanya hivyo taratibu za kisheria zifuatwe kwani katika kipindi hicho chote serikali imekosa mapato yake. Kuanzia leo pitieni leseni zote na ifikapo Juni 30 mwaka huu leseni zote zisizo hai ziwe zimefutwa”, amesema Prof. Kikula. 

Wakati huo huo, mwenyekiti wa tume amekutana na kuzungumza mwakilishi wa mwekezaji wa kampuni ya TanzGraphite (T) Ltd ambae ni Meneja Uhusiano wa Jamii na kuzungumzia kuhusu mgogoro uliopo baina ya mwekezaji huyo na baadhi ya wananchi wanaotakiwa kufanyiwa tathimini ili kupisha shuguli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo. Prof. Kikula ameonyesha kusikitishwa na mgogoro huo ambao amesema ni wa muda mrefu sasa na unachelewesha maendeleo ya watu na kuikosesha serikali mapato. 

Ameongeza kimsingi wananchi wanapaswa kuelewa kuwa “right surface” (haki ya kumiliki vitu vilivyo juu ya ardhi) inampa mwananchi haki  ya kulipwa fidia ya mali zilizo juu ya ardhi anayo miliki lakini watambue kuwa kuna “resource right” (haki ya kumiliki raslimali zilizo chini ya ardhi) ikiwemo madini ambayo mmiliki wake ni serikali, ndio maana inapohitaji raslimali hizo humuondoa na kumfidia mliliki wa mali za juu ya ardhi, hivyo wananchi wanapo ng’ang’ania wanatakiwa walitambue hilo.

Pia, amesema kuwa, kwa mpango ulioanishwa na mwekezaji huyo unaonyesha manufaa kwa wananchi kupitia miradi ya maendeleo (CSR) ambapo amebainisha kuwa mwekezaji ameahidi kuwalipa fidia, kuwajengea nyumba za kisasa wale wote walio ndani ya eneo. Mambo mengine ni pamoja na kuwapatia chakula kwa muda wa miaka miwili wakiwa kwenye makazi mapya watakayo jengewa na kila kaya kusomesha mtoto mmoja kwenye vyuo vya veta na wakihitimu wataajiriwa na mgodi ili waweze kupata kipato cha kusaidia na kuendeleza kaya zao. 

Pamoja na hayo, mwekezaji huyo amemweleza mwenyekiti wa tume kuwa tayari wameshakubaliana kujengaa kituo cha afya, matundu ya vyoo kwa baadhi ya shule, kujenga shule na ukarabati wa vyumba vya madarasa katika shule mbalimbali. Hata hivyo hakusita kuonyesha kusikitishwa kwake na watu wachache wanaogoma kuondoka kupisha shuguli za uchimbaji huku kila kitu ikiwemo mtaji wa shuguli hizo ukiwa tayari.

Katika mgogoro huo, kaya 347 zinatakiwa kuondoka kupisha mwekezaji huyo na kati ya hizo kaya 62 ndio zinazo goma kuondoka ili mwekezaji aanze kazi ya uchimbaji. Mwenyekiti amesikitishwa na hali hiyo na na kuuomba uongozi wa mkoa na wilaya kuzungumza na kaya hizo sambamba na Baba Askofu aliyeko ndani ya eneo hilo ili mradi huo uanze kwani ni wa muda mrefu na serikali inakosa mapato. 

Amesema kwa sasa anaziachia juhudi za serikali ya mkoa na wilaya katika kuupatia ufumbuzi mgogoro huo. Mapema mwenyekiti alikutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya ambapo amemshukuru kwa ushirikiano anao utoa kwa viongozi na wafanyakazi wa tume ya madini wilaya ya Ulanga.

Amesisitiza suala la uadilifu kwa wafanyakazi wa tume na amesema hilo litakuwa jambo la kwanza kulisema kila aendapo sambamba na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali.  Aidha, amesema kipimo kikubwa cha kila mkuu wa kituo cha tume ya madini kitakuwa ni ukusanyaji wa maduhuli ambapo katika Mwaka wa Fedha 2018/2019 tume ilipangiwa kukusanya Bilioni 310 na mwaka wa fedha ujao tume imepangiwa kukusanya Bilioni 467.

Upande wake, Kamishna wa tume hiyo Dkt. Athanas Macheyeki amewakumbusha na kuwasisitiza watumishi wa tume na wachimbaji wa madini kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji na ulipaji wa tozo na stahiki zote za serikali kwa wakati. Amesema kwa kufanya hivyo raslimali za madini zitakuwa na tija kwa taifa kama anavyo sisitiza Rais John Pombe Magufuli kuwa anataka raslimali za madini ziwanufaishe watanzania wote na namna za kuwanufaisha ni kulipa stahiki za serikali zinazo tokana na madini ili zikatumike kujenga uchumi wa taifa.

Prof. Kikula na Dkt. Macheyeki wanaendelea na ziara yao mkoani Morogoro kukagua shuguli za Tume katika Wilaya mbalimbali ambapo leo walitembelea eneo la wachimbaaji wadogo ipanko wilayani ulanga.
 Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula wa pili kushoto akiwa katika eneo la wachimbaji wadogo Ipanko wilayani Ulanga akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Madini Mkazi Morogoro Mhandisi Emmanuel Shija alipotembelea kujionea namna shuguli za uchimbaji zinavyofanyika. Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Tume hiyo Dkt. Athanas Macheyeki.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari kwenye eneo la mgodi wa wachimbaji wadogo Ipanko.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula akionyesha jambo kwenye ramani ya mwekezaji wa Madini ya Graphite; TanzGraphite (T) Ltd. Wa tatu kushoto ni Meneja Uhusiano wa Jamii Bernad Mihayo, wa pili kushoto ni Kamishna wa Tume hiyo Dkt. Athanas Macheyeki.
 Kamishna wa Tume ya Madini  Dkt. Athanas Macheyeki kushoto akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula mara baada ya kuzunguka na kukagua eneo la wachimbaji lililopo Iponka eneo ambalo awali lilifungiwa kufanya shuguli za uchimbaji. 
 Wachimbaji wadogo wakiwa chini ya mgodi katika shimo lenye urefu wa zaidi ya mita hamsini wakiwa wanaendelea na shuguli za uchimbaji katika eneo la Ipanko. 

TUNATAKA KURAHISISHA MAZINGIRA BIASHARA YA MADINI - BITEKO

$
0
0

*Naibu Waziri Nyongo ataka Soko la Madini Arusha kuanzishwa haraka
Waziri wa Madini Doto Biteko amesema Serikali kupitia Wizara yake inalenga kurahisisha Mazingira ya Biashara ya Madini ikiwemo kuwalea wachimbaji na kuwataka wafanyabiashara na wachimbaji kuhakikisha wanajisimamia wenyewe kwa manufaa yao na Taifa.

Waziri Biteko ameyasema hayo alipokutana na viongozi wa Chama Cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA), wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Sam Mollel ofisini kwake jijini Dodoma Aprili 10, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu biashara ya madini nchini.
Amekitaka chama hicho kuendelea kushirikiana na wizara kwa lengo la kusukuma mbele Sekta ya Madini ikiwemo kuhakikisha biashara ya madini inafanyika katika mazingira yenye kuzinufaisha pande zote na kuwasisitiza viongozi hao kuhakikisha wanachama wao wanafuata taratibu wanapofanya biashara ya madini.

Awali, kabla ya kujibu hoja zilizowasilishwa na chama hicho, Waziri Biteko amekipongeza  chama  hicho kwa kuwa kimekuwa kikitoa njia mbadala pindi kinapowasilisha changamoto na kero  zake badala ya kuishia kulalamika na kuongeza, “wizara inaona fahari kwa hilo na tunayachukulia kwa umuhimu maoni yenu,”.

Akizungumzia suala la kodi ya ongezeko la thamani na kodi ya zuio ambayo imeondolewa kwenye uchimbaji mdogo, Waziri Biteko amekitaka Chama hicho kutoa nafasi kwa serikali kufuatilia suala hilo. Waziri Biteko ameleeza hilo kufuatia hoja iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa TAMIDA Sam Mollel ambaye ameeleza kuwa, katika mkoa wa Arusha, kodi hiyo bado inatozwa licha ya serikali kuiondoa.

Aidha, Waziri Biteko ametolea ufafanuzi wa changamoto kadhaa zilizowasilishwa na Mwenyekiti Sam Mollel kwa niaba ya chama hicho ikiwemo. Kuhusu bei elekezi, Waziri Biteko  amesema wizara itaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha suala hilo linakuwa shirikishi. Waziri Biteko amesema hilo baada ya TAMIDA kutoa pongezi kwa serikali kwa kutoa nafasi kwa wadau kukaa pamoja na serikali kujadili suala la bei elekezi ambapo Mwenyekiti huyo amemweleza Waziri Biteko kuwa, katika hilo, serikali na wadau wameanza vizuri.'

Akitolea ufafanuzi kuhusu suala la kurejesha maonesho ya madini jijini Arusha, Waziri Biteko amesema suala la maonesho ya madini kufanyika arusha inawezekana lakini si kwa madini ya Tanzanite, na kuongeza kuwa, serikali imedhamiria kufanya shughuli zote zinazohusu madini hayo ndani ya ukuta unaozunguka machimbo ya mirerani lakini pia ikilenga kuubadilisha  mji wa  mirerani ufanane na madini hayo.

Aidha, Waziri Biteko amezungumzia suala la kuongeza wataalam wa kuthamini madini ya Tanzanite Mirerani na kueleza kuwa, kutokana na unyeti na umuhimu wa suala hilo, tayari serikali imeanza kulifanyia kazi ili kuhakikisha inaongeza idadi ya wataalam kuwezesha shughuli za uthamini Mirerani, kufanyika kwa wakati. Ufafanuzi huo umetolewa baada ya Mwenyekiti wa TAMIDA Sam Mollel kuwasilisha changamoto ya kuwepo na  upungufu wa wataalam hao.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza katika kikao hicho, ametaka kuanzishwa haraka kwa soko la Madini jijini Arusha na kueleza kuwa, kwa upande wa wizara itahakikisha inashirikiana na serikali ya mkoa kuhakikisha soko hilo linaanzishwa haraka. Naibu Waziri Nyongo amesema hayo akijibu hoja ya Mwenyekiti wa TAMIDA Sam Mollel ambaye ameleeza katika kikao hicho kuwa, Chama hicho kinaunga mkono Serikali kuhusu uanzishwaji wa masoko ya madini na kuitaka serikali ione umuhimu wa kuanzisha soko La madini la madini mkoani arusha kuwezesha biashara ya madini ya vito kufanyika kwa urahisi.

Kuhusu vibali vya Wataalam wa masuala ya ukataji na unga’rishaji wa madini kutoka nje ya nchi, Naibu Waziri Nyongo amesema kuwa, ni kweli kwamba serikali inawahitaji wataalam hao kwa kuwa pia watawezesha kutoa ujuzi huo kwa wataalam wa ndani ili kuhamasisha viwanda vya ukataji madini na kuongeza, “ serikali inaangalia namna ya kulipatia ufumbuzi suala hilo kwa kushirikiana na mamlaka zinazohusika kwa sababu pia tunataka watu wetu wanufaike na utaalam huo”,. 

Pia, ameongeza kuwa, kutokana na kulichukulia suala la uongezaji thamani madini kwa umuhimu, inakitegemea kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kwa ajili ya kuzalisha wataalam na kukitaka chama hicho kusaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa katika kituo hicho kwa kuwa hivi sasa idadi bado ni ndogo.

Kikao hicho cha Waziri na TAMIDA ni cha kwanza tangu kuteuliwa kwa Waziri wa Madini Doto Biteko kuiongoza wizara husika. Wengine waliohudhuria kikao hicho ni Viongozi Waandamizi kutoka wizara ya Madini na Tume ya Madini.
 Waziri wa Madini Doto Biteko  (wa kwanza kulia) akizungumza jambo wakati wa kikao baina yake na Chama Cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA). Wengine wanaofuatilia ni Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mulabwa (kulia kwa Waziri) na   Ujumbe wa Chama hicho.
  Waziri wa Madini Doto Biteko na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakimsikiliza Mwenyekiti wa TAMIDA Sam Mollel wakati akizungumza jambo katika kikao hicho. Wengine wanaofuatilia ni Kamishna wa Madini David Mulabwa na mmoja wa wajumbe wa chama hicho, Abe Latif.
 Baadhi ya Viongozi wa Chama Cha Wafanyabiashara ya Madini Tanzania  (Tamida) wakifuatilia mkutano wao baina ya Waziri wa Madini Doto Biteko , Naibu Waziri na Viongozi wa Wizara.
Baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini wakifuatilia kikao baina ya Waziri wa Madini na Ujumbe wa Chama Cha Wafanyabiashara ya Madini Tanzania (TAMIDA).
Waziri wa Madini Doto Biteko katika picha ya pamoja na Viongozi wa (TAMIDA) pamoja na  Viongozi Waandamizi wa Wizara baada ya kikao.  

TATIZO LA USIKIVU WA MAWASILIANO MAFIA KUKAMILIKA NDANI YA MIEZI 7

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye (Mb.) amewaahidi wakazi wa Kisiwa cha Mafia kuwa Serikali imejipanga kuboresha mawasiliano katika vijiji vitatu vyenye usikivu hafifu wa mawasiliano ya simu za mkononi.

Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Miburani, Chunguruma na Banja kisiwani Mafia wakati wa ziara ya kukagua usikivu wa mawasiliano ya simu za mkononi, alisema anatambua na amethibitisha kuwa wananchi wa vijiji hivyo wanapata usikivu hafifu na kuahidi kuwa kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Serikali itaboresha mawasiliano hayo katika kipindi cha miezi saba kuanzia mwezi huu wa Aprili.

Nditiye amesema hayo katika ziara ya kukagua usikivu wa mawasiliano na masuala ya Uchukuzi akiwa ameongozana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mwenye dhamana ya Sekta ya Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi, Mbunge wa Mafia Mbaraka Dau (Mb.) pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Injinia Peter Ulanga.

“Nawaomba muwe na subira, serikali inalitambua hili na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote utahakikisha kuwa mawasiliano yanakuwa bora na yenye usikivu wa kutosha,” aliahidi Nditiye.
Pamoja na kukagua usikivu wa Mawasiliano katika kisiwa cha Mafia, Nditiye pia alikagua uwanja wa ndege wa Mafia na kumuagiza Meneja wa Uwanja huo kupeleka mara moja makao makuu mahitaji ya kuboresha uwanja huo ili kuhakikisha unafanya kazi kwa viwango vinavyohitajika kwa ajili ya usalama wa usafiri wa anga kisiwani humo.

Vilevile Nditiye alifanya ukaguzi katika gati ya Kilindoni na kuagiza matengenezo ya mbao za gati hiyo zifanyiwe ukarabati na matengenezo mengine muhimu mara moja kuanzia wiki hii na taarifa za kukamilika kwa marekebisho hayo zipelekwe Wizarani mara matengenezo yatakapokamilika.

Pia  Nditiye alizungumza nawananchi wa Mafia na kupokea kero za wananchi kuhusu masuala ya usafiri hususani barabara na vivuko. Akizungumzia suala la kivuko, alisema kivuko kipya kimeanza kutengenezwa na kinategemewa kukamilika hivi karibuni. Hali kadhalika aliwaambia wananchi kuwa wakati kivuko kipya kinatengenezwa, kivuko kilichopo Chuo cha Mabaharia Tanzania kitaanza kuhudumia wananchi katika kipindi cha mwezi mmoja kwa ajili ya usafiri kati ya Jiji la Dar es Salaam, Kilindoni, Mafuya na Nyamisati Kibiti.

Nditiye alimshukuru sana Mbunge wa Mafia Dau kwa kuwa mstari wa mbele kusimamia maendeleo ya Mafia katika maeneo yote ya Uchukuzi na Mawasiliano na aliahidi Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na  Rais Dkt. John Pombe Magufuli inafanya kila linalowezekana kuhakikisha maeneo yote ya Tanzania yanafikika kwa usafiri na mawasiliano. 

Aidha aliwaeleza wananchi wa Mafia kuwa ujenzi wa gati la Nyamisati limefikia asilimia 88 na inatarajiwa litakamilika hivi karibuni na kuondoa kero za wananchi wa eneo hilo ambao wamekuwa wakipata shida ya usafiri katika Kisiwa cha Mafia.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye (wa 4 kutoka kulia) akikagua mbao za Gati la Kilindoni Wilayani Mafia. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi akisalimia wananchi wa Mafia wakati wa mkutano wa Naibu Waziri Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye kusikiliza kero za wananchi wa Wilaya hiyo kuhusu masuala ya usafiri na mawasiliano.

ZAIKO LANGA ‘CHUO’ CHA MUZIKI WA DRC KONGO

$
0
0
Na Moshy Kiyungi

Huwezi kuzungumzia historia ya muziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pasi kuitaja bendi ya Zaiko Langa Langa. Bendi hiyo ilianzishwa rasmi mwaka 1970 wakati huo ikijulikana kama Orchestra Zaiko.

Baadae kidogo mashabiki wakaanza kuwaita Langa Langa wakimaanisha “Kulewa” kwa kuwa nyimbo zao zilikuwa zikipigwa sana kwenye vilabu vya pombe.

Kama siyo kutoka ubavuni mwake, basi bendi nyingi, kama si zote ambazo zinazotamba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa sasa, zimeasisiwa na wanamuziki ama waliotoka ndani ya bendi hii au katika bendi zilizoanzishwa na wakali waliopata kuipigia.

Hiyo ndiyo Zaiko Langa Langa, bendi kongwe nchini humo kwa sasa ambayo bado inaendelea kudunda licha ya wimbi kubwa la kuhamwa na wanamuziki mahiri pamoja na ushindani uliopo hivi sasa. Zaiko Langa Langa ni chuo cha muziki katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kwa sababu bendi nyingi zinazotamba hivi sasa, ambazo zilianzishwa kuanzia miaka ya 1970, ni matunda yake.

Zaiko inaweza kulinganishwa na bendi ya Msondo Ngoma ya hapa nchini kwa historia zao zinavyokaribiana. Msondo Ngoma na Zaiko Langa Langa, zimetoa wanamuziki wengi wenye majina makubwa kimuziki.

Ukitaja wanamuziki nyota wa nchini humo akina Papa Wemba, Bozi Boziana, Dindo Yogo, Evoloko Ley Ley ‘Joker’, Defao Matumona, Koffi Olomide, na wengine wengi, chimbuko lao limetoka kwenye shina la Zaiko Langa Langa.

Bendi nyingi kama Isifi Lokole, Yoka Lokole, Viva la Musica, Langa Langa Stars, Zaiko Familia Dei, Choc Stars, Le Anti Choc, Le Grand Zaiko Wawa, Quartie Latin na nyinginezo nyingi zimetoka kwenye chimbuko la Zaiko ambayo sasa inajulikana kama Zaiko Langa Langa Nkolo Mboka, yaani ‘Wakuu wa Mji’.

Idadi kubwa ya bendi zilizotokea ubavuni mwa Zaiko Langa Langa zimekuwa zikijiita ‘Ukoo wa Langa Langa’ (Clan Langa Langa).

Bendi hizo ni Isifi Lokole iliyoanzishwa na Papa Wemba, Bozi Boziana, Evoloko Jocker na Mavuela Somo, Yoka Lokole iliyoanzishwa na Papa Wemba, Bozi Boziana na Mavuela Somo. Bendi ya Grand Zaïko Wa Wa iliyoanzishwa na Felix ‘Pepe’ Manuaku Waku aliyeungana na Shimita El Diego na Djo Poster. Bendi ya Viva La Musica iliyoanzishwa na Papa Wemba akiwa na Emeneya Mubiala na Theodore Djangi Dindo Yogo.

Bendi ya Choc Stars iliyoanzishwa na wanamuziki akina Bozi Boziana, Tshimpaka Roxy na kuungana na akina Ben Nyamabo, Carlito Lassa, na Defao Matumona.

Bozi Boziana akiungana na Deyesse Mukangi, Jolie Detta, Dodoli, Walingonda, Fifi Mofude, na wengineo waliungana na kuanzisha bendi ya L'Orchestre Anti-Choc.

Langa Langa Stars iliyoanzishwa na Waze la Mbongo Kiamuangana Mateta ’Verckys’, Evoloko Jocker, Tshimpaka Roxy, Emeneya Mabiala na Djo Mali.

Zaiko Langa Langa Familia Dei, ilianzishwa na akina Lengi Lenga, Ilo Pablo, Bimi Ombale, Beniko Popolipo, Petit Poisson, na Djimi Yaba.

Zaïko Langa Langa Nkolo Mboka yenyewe chini ya N'Yoka Longo, Meridjo, Oncle Bapius, Zamuangana, Nono Atalaku, Mbuta Matima, Malage de Lugendo, Adamo Ekula, Baroza, na Shiro Shiro. Ikaanzishwa bendi zingine za Zaiko Universel chini ya wanamuziki Meridjo na Oncle Bapius Muaka wakati bendi ya Langa Langa Rénove ikiongozwa na mwanamzuiki Evoloko Jocker.

Histori ya bendi ya Zaiko Langa Langa imekuwa ikikosewa na baadhi ya watu wakataja ilianzishwa mwaka 1970. Yasadikika kuwa bendi hii ilianzishwa rasmi Desemba 24, 1969 jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati huo ikijulikana kama Orchestra Zaiko.

Wakati huo muziki wa Kongo ulitawaliwa zaidi na bendi za African Jazz ya Joseph Athanase Tchamala Kabaselleh ‘Le Grand Kalle’, African Fiesta ya Nicolas Kassanda wa Mikalay maarufu kama Dk. Nico, Tout Puisant Orchestre Kinnie Jazz (TP OK Jazz) ya L’Okanga La Ndju Pene Luambo Luanzo Makiadi Franco na hata African Fiesta National ya Pascal-Emmanuel Sinamoyi Tabu, almaarufu Tabu-Rey Rochereau, aliyoianzisha baada ya kutengana na Dk. Nico na mwaka 1970 akaibadili jina na kuiita Orchestre Afrisa Intanatinale.

Waanzilishi wa Zaiko Langa Langa walikuwa wanamuziki ambao baadhi walikuwa wanapigia bendi ndogo ndogo za mitaani na wengine walikuwa wanafunzi.

Baadhi yao ni mpiga Konga maarufu D.V. Moanda, ambaye jina lake halisi ni Vital Moanda-di Veta Marcelin Delo, Henry Mongombe, Olemi Eshar-Eshar dem'belina, Andre Bita, Mavuela ‘Somo’ Simeon, Evoloko Lay Lay ‘Joker’, Teddy Sukami, Oncle Bapius aliyekuwa akipiga bass, Zamuangana Enock le Meilleur, baba ya wapiga solo wa kizazi kipya Kongo Felix Manuaku Waku na N'Yoka Longo Mvula, anayelikana kama Jossart, ama Vieux Mbombas ambaye asili yake ni kutoka nchini Angola.

Hawa walikuwa wakipiga muziki wa Soukous. Katika upande wa Pop waliokuwa wakifungua pazia katika shoo zote za bendi hiyo, kulikuwa akina Bimi Ombale, Mbuta Matima Zephirin na Mashakado Mbuta.

Historia inaonesha kuwa wanamuziki akina Moanda, Mongombe, Marcelin, Waku, N’Yoka Longo na Andre Bita walitokea kwenye bendi ya mtaani iliyojulikana kama Bel Guide National. Wote hawa walikuwa wanafunzi wakitokea katika familia za matajiri jijini Kinshasa.

Baadaye Zaiko ikamchukua bwana mdogo aliyekuwa na umri wa miaka 19 wakati huo, ambaye alikuwa anaimba kwaya kanisani, Jules Shungu Wembadia Pene Kikumba, maarufu kama Papa Wemba. Bendi hiyo hivi sasa ipo ikiongozwa na mkongwe N’Yoka Longo Mvula.

FALLY IPUPA ANATAMBA KWA MUZIKI WA KONGO

$
0
0
Na Moshy Kiyungi

Muziki wa Kongo hivi sasa ‘umekamatwa’ na wanamuziki wa kizazi kipya, akiwemo Fally Ipupa. Sifa za mwanamuziki huyu zimeenea kila pembe Afrika, Ulaya hadi Marekani kuliko na wapenzi wa muziki wa dansi. Ipupa pamoja na mwenzake Ferre Golla, wanatajwa kuelekea kuchukua nafasi za wanamuziki wakubwa waliowatangulia. 

 Vijana hao hivi sasa waatamba katika anga ya muziki Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakipishana kwa mwaka mmoja kwa kuzaliwa. Ferre Gola alizaliwa Machi 03, 1976 wakati Fally Ipupa alizaliwa Desemba 14, 1977 wote katika jiji la Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Majina yake kamili anaitwa Fally Ipupa Nsimba, alizaliwa na ndugu zake watatu akikwemo kaka yake ajulikanae kwa majina ya Bony Listton pamoja na dada zake wawili Tyna na Niclette. Baba yake mzazi anaitwa Faustin Ebamba na mama yake anajulikana kwa majina ya Monique Bolutuli Mbo.

Fally alianza kuvutiwa zaidi katika muziki kati miaka ya 1992 na 1993. Akishirikiana na wenzake akina Sankara Dekunta, Atele Kunianga, Pitshou Luzolo kwa pamoja wakaunda kundi lao la muziki walilolipa majina ya Flash success. Kundi hilo lilikuwa limejikita katika mitaa yao iliyopo kwenye Manispaa ya Bandalungwa aka Bandal, jijini Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kundi hilo likaungana na la Fraternité Musica. Wazazi wa Fally Ipupa hawakupenda awe mwanamuziki, walikuwa wakimhimiza na kushinikiza kuendelea na shule. Wao walitaka kijana wao asomee fani ya Udaktari badala ya muziki. Kati ya mwaka 1995 na 1996, Fally Ipupa alikwenda kujiunga na kundi la Kibinda Nkoy, kwenye Manispaa ya Kintambo. Alipoingia kundini humo, aliwakuta wanamuziki wengine kama Seguin Mignon.

Wakati anaendelea kupiga muziki katika bendi hiyo, ukatokea mgawanyiko kwenye katika kundi hilo. Yeye Fally Ipupa, Seguin Mignon na wengine wakajiengua na kwenda kuunda kundi jingine walilolipa majina ya Nouvelle Alliance. Katika kundi hilo ndiko Fally Ipupa umaarufu wake wa kuimba na unenguaji uliimarika zaidi.

Mwaka 1997, Fally alijiunga na bendi ya Talents Latent’s, akawa kama Kiongozi wa bendi. Kwenye bendi hiyo pia walikuwepo marafiki zake akina Atele Kunianga, Pitsho Uluzolo bila kuwasahau ma rapa akina Gentamicine Lissimo, na Cellulaire Yankobo.

Mwaka 1999, Fally Ipupa akajiunga katika bendi ya Quartier Latin, inayomilikiwa na Koffi Olomide Le Grand Mopao Mokonzi. Akiwa na bendi hiyo Ipupa akatokea kupendwa sana na kiongozi huyo, kwa kipindi kifupi akatafutiwa hati yake ya kusafiria. (Passport). Baada ya kupata hati hiyo aliungana na wanamuziki wenzake kwenda hadi jijini Paris, nchini Ufaransa kufanya onesho la Bercy.

Kwenye album ya Attentat ingawa Fally Ipupa alikuwa bado mpya kwenye bendi, alichangia kwa kiasi kikubwa sana. Koffi Olomide aliweka matumaini makubwa sana kwa Fally Ipupa, hata pale album ya Force De Frappe ilipotolewa, alipewa fursa ya kuimba na Mopao kwenye wimbo wake wa Éternellement.

Wakati anatunga wimbo huo, Fally alikuwa na umri mdogo wa miaka 15. Albuma ya Effrakata wakati inatolewa mwaka 2001, Koffi Olomide akampendelea zaidi Fally Ipupa ukilinganisha na wenzake. Ipipa licha ya kuweka sauti yake kwenye nyimbo takriban zote, pia aliweka rap kwenye wimbo wa Generation Bercy. Fally Ipupa aliimba kwa Pamoja na Koffi Olomide kwenye wimbo wa Effervescent.

Kama hiyo haitoshi, Koffi Olomide akampa cheo cha kuwa kiongozi wa bendi badala ya Felly Tyson ambaye ndiye ilitakiwa apewe wadhifa huo. Mwaka 2003, ikatolewa album Affaire D’etat, Fally Ipupa akawa mwanamuziki pekee ambae wimbo wake wa Ko Ko Ko Ko, uliwekwa kwenye CD zote mbili za album. Album ya Monde Arabe iliyotolewa mwaka 2004, Fally Ipupa akapewa kipaumbele tena.

Sauti yake yasikika kwenye nyimbo zote zilizopendwa, nyimbo za Esili na Eputsha, ni mfano tosha. Ipupa aliimba kwa weledi mkubwa wimbo wa Pharmacie, ambapo sifa zake ziliendelea kusambaa.

Nguli huyu ana talanta nyingi zikiwemo za kutunga na kuimba nyimbo, unenguaji, pia anao uwezo mkubwa wa kurap. Baada ya kujiona kuwa ameiva katika muziki majina yake si ya kutambulishwa tena, wazo la kutaka kujitegemea likajengeka kichwani mwake. Fikra zake za mwanzoni zilikuwa apewe fursa ya kufanya muziki kivyake vyake ‘Solo artist’, ndipo akaanza kununua nyimbo toka kwa watunzi mbalimbali.

Ipupa akijiweka mwenyewe katika kazi ya kutunga akisaidiwa na marafiki zake. Akawa anasubiria wakati muafaka ambao atatangaza hadharani nia yake ya kufanya ‘Solo Album’, wakati huohuo akiendelea kufanyakazi katika bendi ya Quartier Latin. Mwaka 2005 ikatolewa Maxi-Single ya Boma Nga N’elengi, ambapo Fally Ipupa alichangia pia kwenye matayarisho ya album ya Danger De Mort. Hapo ndipo kaamua kuifichua siri yake, akamwendea bosi wake Koffi OLomide, akamwambia nia ya kutaka kutoa Solo Album yake.

Kwa makusudi mazima jambo hilo lilipingwa vikali na Koffi Olomide. Fally Ipupa hakuridhishwa na maamuzi ya bosi wake huyo, mapungufu ya kutokuelewana kati yao yakaanza. Mvutano huo ulijitokeza huku wapambe wa pande zote mbili wakiingilia kati kujaribu kupata suluhisho. Wapambe wa Fally Ipupa wakamshauri aweke tishio la kujiondoa kwenye bendi yake ya Quartier Latin, ikiwa ni njia mojawapo ya Koffi Olomide kukubali kufanya Solo album yake.

Muafaka ukapatikana, ombi lake likakubaliwa, baada ya kuzungumzwa kwenye jopo la uongozi, japo wengi wa Wanamuziki wakawa hawaridhishwi na jambo hilo hasa pande ya Waimbaji. Baadhi ya wanamuziki waliokubali na kumpa kampani, Fally Ipupa ni Modogo Abarambwa na Montana Kamenga, ambao kwa kiasi kikubwa walichangia kwenye album ya Danger de Mort.

Fally Ipupa akatangaza kwenye luninga kwamba wimbo wa Associe, ndio utakao uweka kwenye album hiyo. Baadae akabadili mawazo hayo, akaamua kuweka wimbo wa Pharmacien, huku wa Associe akiuweka kwenye album yake. Mwaka 2006, Fally kajiunga na Lebo ya Obouo Music, iliyokuwa ikiongozwa na David Monsoh ambae ni raia kutoka nchi ya Cote D’Ivoire. (Ivory Coast)

Pasipo kuchelewa David akamtolea Ipupa album yake ya kwanza ya Droit Chemin. Album hiyo ilikubalika mno na kundi la walio wengi, ikafanikiwa kupewa tuzo la Dhahabu baada ya mwaka mmoja tangu itolewe. Ipupa ilipotimu mwaka 2009, ikatolewa album ya Arsenal Des Belles Melodies. Aidha mwaka 2013 wakatoa album ya Power Kosa Leka.

Fally Ipupa ni kiongozi na mmiliki wa Lebo ya F’Victeam), jina ambalo amelipa bendi yake muziki ya Fally na F’Victeam. Walifanikiwa kutoa Album ya Libre Parcours. Baadhi nyimbo za Fally Ipupa ni pamoja na Eloko Oyo, Kiname, Bad Boy, Jeudi Soir, Nidja, Mannequin na Liputa. Nyingine ni Just une danse, Na Lingui Ye, Travelling Love, Mon Amour, Double Clinc, Esengo Sexy dance, Sopeka na Bakandja. Ipupa na kundi lake waliachia vibao vya Associe, Siamois, Cadenas, Orgas na Ndoki.

Walitoka na Video za Origina na Sweet Life na Love don’t care. Video ya Original aliyoitoa Mei 05, 2014, wimbo huo umefuatiliwa na kutizamwa watu takribani million 10 kwenye You Tube. Mwanamuziki Fally Ipupa alifunga ndoa ya asili na bi Nana Ketchup Bafana, mwaka 2000. Kwa kipindi chote cha ndoa hiyo, wamebahatika kupata watoto watatu ambao ni Marcosins, Vincenzo na Jayden.

Mwanawe mwengine ni Keyna, alimpata toka kwa mama mwengine Nicky Menga. Fally ni msanii mwenye moyo wa kusaidia jamii kupitia shirika lake la Fally Ipupa Foundation (FIF) Shirika hilo hutoa misaada mingi kwa makundi ya watu walio na hali duni kimaisha, Watoto, pia hupenda kuwajulia hali wagonjwa.

Fally Ipupa amekwisha nyakua tuzo nyingi za Kimataifa. Mwaka 2008 alipokea tuzo ya msanii bora wa Kiume Afrika kwenye KORA Awards Mwaka 2013, alipewa tuzo la msanii bora wa Afrika kwenye Trace Urban Music Awards. Aidha mwaka huohuo wa 2013, alipata tuzo mbili kwenye Ndule Awards, album bora ya Power Kosa Leka na video bora Eke. Julai 2014, alichukua Tuzo la Afrimma kama mwanamuziki bora wa kiume Afrika ya Kati, jijini Dallas nchini Marekani.

Fally Ipupa amewahi kushiriki kwenye MTV all stars, akiambatana na wanamuziki wenye majina makubwa, akina Snoop Dogg, 2Face Idibia, Flavour na wengineo wengi Wakati wa uongozi wa rais Barack Obama wa Marekani, Fally Ipupa aliwahi kuwa mmoja wa Wasanii wengine walipokea mwaliko kutoka kwa rais huyo, ili wapate fursa ya kushiriki kwenye kikao cha Ushirikiano na Maendeleo kati ya Marekani na nchi za Afrika.

Fally Ipupa ni mmoja kati ya wanamuziki waliotumbuiza mara mbili na kuujaza ukumbi wa kifahari wa Zenith, uliopo katika jiji la Paris nchini Ufaransa. Hiyo ilikuwa kati ya Januari 02, 2010, kwa mara ya pili Ilikuwa Machi 12, 2011. Ikumbukwe kwamba mwanamuziki huyo kijana Fally Ipupa, aliwahi kufika nchini Tanzania, akafanya maonesho kadhaa katika jiji la Dar es Salaam mwaka 2009.

“Bravo Fally Ipupa”

KAMPUNI YA CLOUDS MEDIA GROUP YAMKOSHA WAZIRI DKT.MWAKYEMBE

$
0
0
*Ni baada ya Kampuni hiyo kupata leseni ya kuonesha mashindano makubwa ya kukuza vipaji

*Amwambia Joseph Kusaga ubunifu, uthubutu wao ni fahari kubwa kwa nchi ya Tanzania

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAMPUNI ya Clouds Media Group wameandika tena historia! Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya kampuni hiyo kupewa leseni kamili ya kuendesha mashindano makubwa ya vipaji kwa Ukanda wa Africa Mashariki (East Africa’s Got Talent).

Mashindano hayo yatakuwa yanaonekana katika mabara mbalimbali na takribani nchi zaidi ya 58 duniani zitakuwa zikifuatilia hatua kwa hatua namna ya vipaji vinavyoibuliwa kupitia mashindano hayo.

Akizungumza Aprili 10 , 2019 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe amesema anawapongeza Clouds Media Group kwa kufanikiwa kupata leseni ya kuonesha mashindano hayo makubwa kwani wameletea heshima nchi yetu ya Tanzania.

Dk.Mwakyembe amesema " Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Joseph Kusaga na Clouds Media kwa ujumla mnafanya kazi kubwa sana katika nchi yetu na mmeendelea kuwa mstari wa mbele katika ubunifu na kuthubutu .Kwa kitendo hiki cha kupata leseni ya kuonesha mashindano haya makubwa ya kukuza vipaji , tukiri mmetutoa tena kimaso maso na sina maneno ya kusema.Leo hii naweza kutamba na kesho nikiwa bungeni nitatamba sana.

"Hongereni sana Clouds Media Group na kama ambavyo Joseph Kusaga ameeleza mashindano haya yataangaliwa na mamilioni ya watu duniani, kwetu sisi kama nchi hii ni fursa kwetu ya kujitangaza, kama mnavyofahamu tuna vivutio vingi vya utalii lakini bado havijatangazwa vya kutosha lakini kupitia mashindano haya kwetu ni sehemu ya kujitangaza na tutaitumia vema,"amesema Dk.Mwakyembe.

Amefafanua kuwa kama kipindi kitaangaliwa na mamilioni ya watu duniani maana yake ni fursa kwa nchi kutumia show hiyo kujitangaza kadri inavyoweza na tayari Wizara yake imejipanga kutumia fursa hiyo.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga wakati anazungumzia kupata leseni ya kuonesha mashindano hayo makubwa ya kukuza vipaji amesema kwa zaidi ya miaka 30 kampuni yao imejikita katika kutengeza fursa za kuhakikisha watanzania wenye vipaji wanapata nafasi ya kuonekana kufanikiwa kimaisha.

"Habari kubwa ya kiburudani ni kuzinduliwa rasmi kwa mashindano makubwa ya vipaji kwa ukanda wa Africa Mashariki (East Africa’s Got Talent). Mashindano haya yanaendeshwa kwenye mabara mbalimbali takribani nchi 58. Kwa mara ya kwanza katika historia Clouds Media Group tumepewa kamili (Franchised) ya kuendesha EAGT.

"Kwetu hili ni jambo kubwa na tunaamini tunakwenda kufungua fursa ya vijana wengi wenye vipaji mbalimbali, na kwa zaidi ya miaka 30 ya uwepo wetu tumekuwa tukiangalia namna ya kufungua fursa na maelfu ya vijana wa Tanzania wamefanikiwa,hivyo kama una kipaji chochote jiandae kwani tunakufungulia Dunia kuwa unachotaka,"amesema Kusaga.

Amefafanua zaidi pamoja na mambo mengine Clouds Media Group malengo yake ni kufungua milango kwa vijana wengi kwa kutengeneza Platfom ya kufungua fursa."Katika kuona hilo tuliona tunajaribu kila linalowezekana kufungua milango mingi zaidi na kubwa zaidi ni kupata International Brands na kisha kuzirudisha Tanzania ili kuinua vipaji vya vijana wetu."
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza mbele ya Wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa shindano hilo,Dkt Mwakyembe alisema "Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Joseph Kusaga na Clouds Media kwa ujumla mnafanya kazi kubwa sana katika nchi yetu na mmeendelea kuwa mstari wa mbele katika ubunifu na kuthubutu .Kwa kitendo hiki cha kupata leseni ya kuonesha mashindano haya makubwa ya kukuza vipaji , tukiri mmetutoa tena kimaso maso na sina maneno ya kusema.Leo hii naweza kutamba na kesho nikiwa bungeni nitatamba sana.

"Hongereni sana Clouds Media Group na kama ambavyo Joseph Kusaga ameeleza mashindano haya yataangaliwa na mamilioni ya watu duniani, kwetu sisi kama nchi hii ni fursa kwetu ya kujitangaza, kama mnavyofahamu tuna vivutio vingi vya utalii lakini bado havijatangazwa vya kutosha lakini kupitia mashindano haya kwetu ni sehemu ya kujitangaza na tutaitumia vema,"amesema Dk.Mwakyembe. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akifafanua jambo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi,Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe kuzindua rasmi shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akipiga makofi mara baada ya kumkaribisha mgeni rasmi,Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe kuzindua rasmi shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akipeana mkono na Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe mara baada ya kumkaribisha kuzungumza na Wageni waalikwa kabla ya uzinduzi wa shindano hilo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe na Mkurugenzi wa Clouds Media Bw. Joseph Kusaga wakiwa na waratibu wengine wa tamasha hilo kutoka kushoto ni Mmoja wa waratibu Godfrey Mkama, Mchekeshaji kutoka Uganda Anne Kansiime na Lee Ndayisaba Mtayarishaji wa maudhui ya tamasha la , East Africa’s Got Talent.


Mkurugenzi Mkuu wa Cluds Medai Group Joseph Kusaga akiwa ameambatana na Mgeni rasmi Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe walipokuwa wakiwasili ukumbini kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar


Baadhi ya Wadau wakijadiliana jambo kabla ya uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar

Baadhi ya Wadau wakijadiliana jambo kabla ya uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar
Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwa tayari kushuhudia uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar
Baadhi ya Wageni waalikwa wakijadiliana jambo kabla ya kushuhudia uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar
Mmoja wa Wadau akisubiri kushuhudia uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar
Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwa tayari kushuhudia uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi,Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe kuzindua rasmi shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar.

Baadhi ya Watangazaji Mahiri wa Clouds FM wakisubiri kushuhudia uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar



Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Fancy Nkuhi wa pili kutoka kushoto ni miongoni mwa wageni waliohudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi.
Muongozaji wa shughuli nzima (MC),ambaye pia ni mmoja wa Watangazaji mahiri wa Clouds FM,Masoud Kipanya akitoa muongozo wa namna ya shughili nzima ya uzinduzi eleza taratibu mbalimbali na ufafanuzi



Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Uganda Anne Kansiime akifafanua jambo


Baadhi ya Wageni waalikwa wakiwa tayari kushuhudia uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar.

Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa tayari kushuhudia uzinduzi rasmi wa shindano la East Africa’s Got Talent,jijini Dar.

HII NDIO HISTORIA YA BENDI YA TABORA JAZZ

$
0
0
Na Moshy Kiyungi
Bendi ya Tabora Jazz ilikuwa na makazi yake mjini Tabora ikipiga muziki wake katika ukumbi wa nyumbani wa Lumumba. Ilikuwa na sifa ya kutoka na nyimbo mpya kila baada ya kipindi fulani, ambazo zotezilikuwa zikiwagusa baadhi ya watu. Wakati huo nyimbo za bendi hiyo zilipigwa mno kwenye kumbi za starehe pamoja na kituo cha Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na vituo vingine vya Radio vya Afrika ya mashariki.

Bendi hiyo ilitamba kwa mitindo yake ya za Segere Matata, Segua Segua na Mambo mileka. Mji wa Tabora unaelezwa kwamba ulianza kupata burudani za muziki wa dansi hata kabla ya chama cha TANU hakijaanzishwa.

Mwandishi wa makala hii alimtembelea mzee Hassan Athumani, aliyewahi kuwa mwanamuziki akipiga gitaa la solo katika bendi za Tabora Jazz, Kiko Kids, Nyanyembe Jazz na Milambo Jazz ‘Sona Sona’ kwa nyakati tofauti. Hassan alisimulia kuwa mnamo mwaka 1953, ilianzishwa bendi ya muziki wa dansi iliyopewa majina ya Staff Jazz, ikiongozwa na Hamisi Wampa.
Vyombo vya muziki vya bendi hiyo vilinunuliwa na mfadhili mmoja wa kabila la Kimmanda’ toka nchini Malawi, wakati huo akiwa ni mfanyakazi wa Bomani.

Staff Jazz ilikuwa na mdhamini akiitwa mwalimu Hasanari. Waanzilishi wa bendi hiyo kati ya miaka ya 1953 hadi 1958, walikuwa akina Hamisi Ali Songo aliyekuwa akipiga ngoma kubwa, Hamisi Ngege alikuwa mpiga ngoma ndogo, Dani Kafumu na Nzige aliyekuwa akipulizaji tarumbeta.

Wengine ni Akbaru Hasanari Dremsi alikuwa akipiga ngoma kubwa, Joseph Kayombo ‘Bambo’ alikuwa mwimbaji, Moshi akichanganya marakasi, Saidi akizidunda ngoma ndogo, Haji Sungura mlinda mlango, Swedi Mandanda na Hamisi Issa wakipuliza tarumbeta na rhythm.

Wanamuziki wengine walikuwa akina Abdi Fundi upande wa saxophone, Athuman Tembo aliyekuwa mwimbaji na kucharaza gitaa la solo, Zakaria Tendawema na Sylvester Chifunda walikuwa waimbaji. Wengine ni Juma Athumani ‘Juma Lumango’ aliyekuwa akichanganya drums na Mlekwa Suleimani mmoja wa viongozi na Rajabu Risasi upande wa gita la besi.

Bendi ya Staff Jazz ilikuwa ikipiga muziki kwenye ukumbi wa baa ya Rufita, ambao baadae ukabadilishwa jina kuwa Lumumba, uliokuwa katika kona ya barabara za Rufita na Kapembe, katikati ya mji wa Tabora. Kwa sababu ambazo hazikuainishwa bendi hiyo kwa mwaka 1954 ilisambaratika.

Busara na hekima za Hamis Alli Songo zilimfanya aifufue bendi hiyo mwaka 1956 kwa jina lingine la Tabora Jazz. Yaelezwa kuwa Mlekwa Selemani aliyekuwa shabiki mkubwa wa bendi ya Kiko Kids, alijiunga na Tabora Jazz na kuwa mmoja wa viongozi wa bendi hiyo. Mwaka 1958 bendi hiyo ilichukuliwa kwenda mikoa ya Kanda ya Ziwa, kwa ajili ya kuhamashisha nguvu ya chama cha TANU.
Katika msafara huo waliongozana na viongozi wake Rashid Mfaume Kawawa, Mzee Herman Pacha, Mama Mosi Tambwe na mumuwe Abdallah Selemani Tambwe. Bendi iliporudi Rashidi Hazuruni aliondoka kwenda Dar es Salaam akajiunga na Cuban Branch iliyokuwa ikiongozwa na Mzee Mwaipungu mwaka 1959. Kati ya mwaka 1960 na 1961 bendi ilikuwa na wapigaji gitaa la solo wawili akina Abdi Fundi na Matata. Mwaka uliofuatia Athumani Tembo akaongezeka katika ukung’utaji wa gitaa hilo.

‘Maisha ni kuhangaika’ usemi huu ulijionesha wakati Rashidi Hazuruni aliporejea tena kupiga muziki na Tabora Jazz mwaka 1963. Tabora Jazz ilisheheni wanamuziki wengi wakiwemo akina Hamisi Wampa aliyekuwa Kiongozi, Hamisi Alli Songo na Akbaru Hasanari Dremsi walikuwa wadunda ngoma kubwa, Mambosasa alikuwa akipiga ukulele (gitaa la kizamani).

Mzee Mambosasa ndiye aliyekuwa baba mzazi wa Athumani Mambosasa, aliyewahi kuwa mlinda mlango wa Klabu ya Simba. Said na Hamis Ngege walikuwa wakipiga ngoma ndogo, Dani Kafundu na Nzige walikuwa wapulizaji wa tarumbeta wakati Joseph Kayombo ‘Bambo’ alikuwa mwimbaji.

Kwa upande wa marakasi alikuwemo Moshi, Haji Sungura aliyekuwa mlinzi ‘mlangoni’, Swedi Mandanda alikuwa mcharazaji wa gita la solo, Hamisi Issa alikuwa akipiga gita la kati ‘rhythm’ na Tarumbeta.

Wanamziki wengine walikuwa Athumani Tembo kwenye solo, upande wa gita la rhythm walikuwa Hamis Issa na Hassan Athumani.

Besi liliungurumishwa na Kassim Mponda aliyeondoka katika bendi hiyo mwaka 1965 mwishoni, akifuatana wanamuziki wengine akina Rashidi Hazuruni na Omari Kayanda wakaenda kujiunga na bendi ya Western Jazz ya jijini Dar es Salaam.

Mwaka 1966 Tabora Jazz ikapata mpiga solo mwingine aliyejulikana kwa jina la Stan, akaziba pengo la Rashidi Hanzuruni. Shaddie aliyekuwa Chotara wa Kihindi naye alikuwepo katika safu ya wapiga gita kati ya miaka 1966/1968. Upande wa safu ya waimbaji walikuwa Athumani Tembo, Omari Kayanda , Sylvester Chifundu, Athumani Ngozi na Joseph Kayombo ‘Bambo’ Mpigaji bongos (ngoma ndogo) alikuwa Juma Athumani ‘Kisegeju’ Abdi Fundi alikuwa akipuliza saxophone ‘mdomo wa bata’.

Kwa upande wa upigaji tumba alikuwepo John Kajos Komba ambaye baadae aliondoka nafasi yake ikazibwa na Ally Mbaruku ‘Ally Sanaless’. Kati ya mwaka 1964 na 1965 Tabora Jazz walirekodi nyimbo baadhi yake zikiwa za Ndugu sikilizeni, Tuambie, Dunia haina mwisho, Mwanawanyeje na nyinginezo.

Mwaka 1967 Kassimu Kaluwona alikwenda Kigoma na kuweza kuwaleta wanamuziki akina Wema Abdallah, Hamis Kitambi, Mabrushi Ramadhani Mgoligwa na Hamisi Mkongo. Mwaka 1968 Salumu Luzira akaijunga na Tabora Jazz akitokea Nzega.

Mwaka 1971 Wema Abdallah akaondoka Tabora Jazz akaenda Western Jazz, nafasi yake ikachukuliwa na mpiga solo mwingine aliyejulikana kwa jina la Kalii, alikitokea Kigoma Jazz. Shem Karenga aliletwa na Kassim Kaluwona toka Kigoma, kuja Tabora kujiunga na bendi hiyo Aprili 1972. Pia alikuwepo mpigaji wa gita la solo Issa Ramadhani ‘‘Baba Watoto’

Kwa kipindi kifupi Said Mabera na Hassan Rehani Bichuka nao walijiunga na Tabora Jazz wakitokea Rumonge Jazz. Aidha mwanamuziki Shaaban Dede, alichukuliwa kujiunga na Tabora Jazz, akitokea bendi ya Milambo Jazz ‘Sona Sona’ ya mjini Tabora.

Shem baada ya kutua, alishiriki vilivyo katika utengenezaji wa wimbo wa Dada Asha ambao baadae ukaibwa na bendi ya Sokous Stars, ulikuwa ni utunzi wake Shem Karenga. Wanamuziki wa Soukous Stara ya nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, waliuchakachua wimbo huo ppamoja na wa Vigeregere uliopigwa na Western Jazz.

Tabu Ley aliiona album yenye wimbo huo wa Dada Asha akiwa Nairobi na aliinunua akaenda kuiuza nchini Kongo, Poland na Ubelgiji. Bendi hiyo baadae akajipanga upya kwa kupata damu changa ili kuendeleza muziki wake. Iliongeza watunzi na waimbaji wengi akiwemo Msafiri Horoub, Madaraka Morris, Ismail Wangoko na wengine wengi. Kwa umoja wao wakafyatua nyimbo nyingi zilizoweza kuridhisha nyoyo za wapenzi na mashabiki wa Tabora Jazz.

Nyimbo hizo ni Ashura, Helena, Dada Remi, Mapenzi ulimi, Visa uache, Lucie umeniacha, Zabibu na Niambie leo Kaka. Zingine zilikuwa za Usijifanye Mwewe, Mariam mpenzi, Zabibu No.2, Sofia mpenzi, Tatu, Serafina, Tamaa yako na Asha No. 1. Nguli hao waliachia vibao vingine vilivyoweza kutamba mno wakati huo, Alhamdulilah na Nashukuru sana.

Nyingine ni pamoja na Dada Mwantumu, Ujana una mwisho, mwisho wake ni uzee. Zingine zilikuwa za Salima, Mapenzi Ulimi, Dada Remmy na Rukia wajidanganya.

Wengi wa wanamuziki wanaotajwa katika makala hii wamekwishafariki. Walio hai ni Hassan Athumani, Madaraka Morris, Ismail Wangoko, Ramadhani Mwanangwa waliokuwa wapiga gitaa la rhythm, Salumu Luzira kwa upande wa gitaa la besi, na wengine wengi.

Bendi ya Tabora Jazz haipo tena katika ulimwengu wa muziki, limebaki jengo bovu likionekana katika kona ya barabara za Rufita na Kapembe, katikati ya mji wa Tabora!

YOSSOU N’DOUR ALIUTAKA URAIS

$
0
0
Na Moshy Kiyungi 
Mwanamuziki Youssou N'dour alikuwa na ujasiri mkubwa wa kutaka kugombea urais nchini mwake Senegal.

Alitamka kuwa alikuwa akiitikia wito wa kumtaka agombee kiti hicho dhidi ya rais wao wakati huo Abdoulaye Wade, ambaye alikuwa akipania kuwania kiti hicho kwa muhula wa tatu.

Katika hotuba iliyorushwa kupitia kituo chake cha redio na televisheni, mwanamuziki huyo ambaye pia ni mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa, alisema kama angelichaguliwa kuwa rais wa Senegal, angelipunguza matumizi ya serikali na kuahidi kuzalisha chakula na umeme kwa wote. Youssou ana historia ndefu katika talanta za uimbaji, uandishi wa nyimbo, na utunzi, mchanganyiko wa tamaduni pia ni mwigizaji.

Licha ya shughuli za muziki na harakati za kisiasa, amekuwa akijihusisha na masuala ya kibinadamu kwa siku nyingi na pia yeye ni balozi wa shirika la umoja wa mataifa kuhusu masuala ya watoto (UNICEF).

Youssou N'Dour alikiri kuwa yeye sio msomi lakini alielezea wadhifa wa urais kuwa ni kazi na sio taaluma. Kabla ya hapo N'Dour alikuwa rafiki wa karibu wa rais Abdoulaye Wade, lakini baada ya Wade kutangaza nia ya kuwania kiti cha urais kwa muhula wa tatu, aligeuka na kuwa mpinzani wake mkuu.

Alikuwa akisema kwamba Wade anatakiwa kutogombea mhula mwingine wa tatu kwa sababu anavunja katiba. Kabla ya upigaji kura ilibainika kuwa isingelikuwa kazi rahisi kwa Youssou Ndour kuwabadili maelfu ya wafuasi wake wa muziki kumpigia kura. Mwaka 2004, Rolling Stone alimuelezea kuwa, katika Senegal na sehemu kubwa ya Afrika, "ndiye mwimbaji maarufu kati ya walio hai."

Ndour amesaidia sana kuutangaza na kuuendeleza mtindo wa muziki maarufu nchini Senegal, unaojulikana kwa lugha ya Serer kama Mbalax, aina ya muziki ambao huelezea mbinu na mitindo yake mingi kutoka mapokeo ya kihafidhina ya muziki wa Serer wa "Njuup".

Aidha amesaidia sana kuleta mafanikio makubwa na tuzo kwa filamu ya “Return to Goree” aliyoshiriki kuiongoza kwa kushirikiana na Pierre-Yves Borgeaud, na “I Bring What I Love” ilivyoongozwa na Elizabeth Chai Vasarhelyi, zilizotolewa na kuoneshwa katika majumba ya sinema duniani kote. Msomaji wa makala hii yawezekana ukawa unataka kufahamu wasifu wa Youssou N'Dour.

Wasifu wa Youssou N'Dour unaonesha kuwa alizaliwa Oktoba 1, 1959 mjini Dakar nchini Senegal, baba ambaye ni wa kabila la Serer, aliyeanza kuimba akiwa na umri wa miaka 12. Kwa miaka michache alikuwa akiimba mara kwa mara katika bendi ya Star, kundi lililokuwa maarufu zaidi mjini Dakar mnamo miaka ya 1970. Aliwahi kujiunga katika bendi ya Orchestra Baobab nyakati hizo.

Ingawa Youssou N'Dour ana uhusiano wa tamaduni za Griot kwa upande wa mama yake, yeye hakulelewa katika utamaduni huo, ila alijifunza kutoka kwa ndugu zake. Wazazi wake walimtia moyo wa kutazama mambo kwa njia za kisasa zaidi, wakiacha kuzizoea tamaduni zote mbili. Matokeo yake alijichukulia mwenyewe kama mtu wa kisasa katika jamii ya Griot.

Mwaka 1979, Yousou alianzisha kundi lake mwenyewe, Etoile de Dakar. Kazi yake ya mwanzo na Etoile de Dakar ilikuwa katika mtindo wa kawaida wa Kilatini maarufu kote Afrika wakati huo. Mnamo miaka ya 1980 alianzisha sauti ya kipekee wakati alipoanzisha kundi lake jingine la Super Etoile de Dakar akishirikiana na Jimi Mbaye, kwenye gitaa.

Wapigaji wengine walikuwa akina Habib Faye aliyekuwa akipiga gitaa zito la besi, Tama alikuwa akizidunda ngoma na mchezaji Assane Thiam. Yosou N’Dour ana mvuto wa upigaji ambapo muziki wake hauegemei upande wowote. Hupiga mitindo mingi kuanzia Samba ya Cuba hadi Hip hop, Jazz na Soul, zilizompatia mamilioni ya mashabiki Kimataifa.

Katika nchi za Magharibi, Youssou ameshirikiana na wanamuziki wengine akina Peter Gabriel, Red Axelle, Sting, Alan Stivell, Bran Van 3000, Neneh Cherry, Wyclef Jean, Paul Simon, Bruce Springsteen, Tracy Chapman, Branford Marsalis, Ryuichi Sakamoto, Dido na wengineo. Nchini Senegal, Youssou ni nyota mwenye nguvu ya utamaduni anayeshiriki kikamilifu katika masuala ya kijamii.

Amejaaliwa kuwa na vipaji mbalimbali vya ajabu, mtunzi wa nyimbo, kiongozi wa bendi, na mtayarishaji na mwenye uwezo mkubwa katika muziki. Gazeti la New York Times liliielezea sauti yake kama "Sauti nyembamba yenye kukamata, silaha nyumbufu iliyotumika kwenye mapambano na yenye mamlaka ya kinabii". Youssou N'Dour ameuteka wigo wa muziki wote wa Senegal katika kazi yake.

Mwezi Julai 1993, mchezo wa kuigiza wa Kiafrika uliotungwa na Youssou N'Dour ulioneshwa katika tamasha jijini Paris nchini Ufaransa. Aliandika na kutumbuiza wimbo rasmi wa Kombe la Dunia 1998, akiwa na Axelle Red "La Cour des Grands". Youssou N'Dour aliteuliwa kuwa Balozi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) tarehe 16 Oktoba 2000.

Rasilimali kubwa ya Youssou N'Dour ni kwamba ana ufahamu mkubwa sana katika utamaduni wake. Hata kama aliamua kutafiti mahali pengine, mizizi yake ni imara. Baadhi wamekwenda mbali wakimuelezea kama Msanii wa Afrika wa Karne (jarida la Folk Roots). Ameshafanya ziara za kimataifa kwa miaka thelathini. Alishinda tuzo yake ya kwanza ya American Grammy Award (best contemporary world music album) kwa CD yake ya Egypt mwaka 2005.

Mwaka 1991 alifungua studio yake ya kurekodia, ya Xippi, na alitengeneza lebo yake mwenyewe ya Jololi mwaka 1995. N’Dour pia ni mmiliki wa L'Observateur, moja ya magazeti makubwa nchini Senegal, na kituo cha redio RFM (Radio Future Medias).

Youssou N'Doura amekuwa akijihusisha na masuala kadhaa ya kijamii na kisiasa. Mwaka 1985, aliandaa tamasha kwa ajili ya kutolewa kwa Nelson Mandela. Alishirikiswa kuimba katika matamasha ya Haki za Binadamu yalilojulikana kama ‘Amnesty International Human Rights Now’ mwaka 1988 duniani kote.

Ziara iliyomshirikisha Lou Reed kuchangia toleo la wimbo wa Peter Gabriel uliotolewa na Richard James Burgess na kushirikishwa kwenye albamu ya Amnesty International. Yousou amewahi kufanya kazi katika Umoja wa Mataifa na UNICEF na alianzisha mradi wa Joko kwa kufungua migahawa ya Intaneti katika Afrika na kuunganisha jamii ya Senegal duniani kote.

Amewahi kutumbuiza katika matamasha maarufu ya Live manane likiwemo la Live 8, London, t Live 8, Paris na katika tamasha la Live 8, Mradi wa Edeni katika Cornwall tarehe 2 Julai 2005, akiwa na Dido. Mwaka 2006, Youssou N'Dour alicheza katika filamu ya kustaajabisha ya Wafrika-Waingereza (African-British abolitionist Olaudah Equiano), iliyoelezea juhudi za William Wilberforce kumaliza utumwa katika Dola ya Uingereza.

Alishiriki katika "Jealous Guy" akiwa na John Lennon kaitka CD ya 2007, Karma Instant , kampeni ya Amnesty International Kuiokoa Darfur pia alishiriki katika kampeni ya pamoja ya Hispania na Senegal dhidi ya wahamiaji haramu. Aidha Youssou N'Dour alishiriki katika Soko la Hisa la mradi wa Visions mwaka 2007. Tangu mwaka 2007 amekuwa mwanachama wa baraza la World Future Council.

Mwaka 2008, Youssou N'Dour alitoa kama zawadi moja ya nyimbo zake za bebe, kwa mwimbaji wa Kifaransa, Cynthia Brown. Mwaka 2009, aliachia wimbo wake "Wake Up (It's Africa Calling)" chini ya leseni ya Creative Commons ili kusaidia afya kimataifa katika kampeni ya IntraHealth Open ili kuleta chanzo cha maombi ya wazi ya afya kwa Afrika.

Wimbo uliorudiwa ukichanganya wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Nas, Peter Buck wa R.E.M., na Duncan Sheik kusaidia kutafuta fedha kwa ajili ya kampeni. Mwaka 2011, N'Dour ilitunukiwa shahada ya udaktari wa heshima katika Muziki kutoka Chuo Kikuu cha Yale.

JESHI NCHINI SUDAN LASUBIRIWA KUTOA TAMKO

$
0
0

*Lazingira makazi ya Omar Al Bashir, Bint Alaa (22) azidi kuwa maarufu

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii 

JESHI la Sudan linasubiriwa kutoa Kauli Muhimu mara  baada ya kuzingira makazi ya Omar Al Bashir ambaye amekuwepo madarakani kwa muda wa miaka 30.

Katika Maandamano ya kumlazimisha kiongozi huyo kung'oka madarakani, Binti Alaa Salah amekuwa ni Ishara ya Mapinduzi na amehusika katika kuchochea vijana kuingia mtaani kuidai 
Nchi Yao. Alaa ana miaka 22 na ni mwanafunzi wa uhandisi chuo kikuu cha kimaifa cha Sudan.

Maandamano hayo ya kumshinikiza Omar Al Bashir kung'oka madarakani yalianza Disemba mwaka jana na hiyo ni baada ya kupanda kwa gharama za maisha na bei ya mkate.

Ikumbukwe kuwa Kuna hati ya kumkamata Bashir iliyotolewa na Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai (ICC.)

WAZIRI MKUU AFUNGUA KONGAMANO MAALUM LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA BABA WA TAIFA, MWALIMU NYERERE, KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, wakati alipo wasili kufungua kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Aprili 11, 2019, katika Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Stephen Wasira wakati alipo wasili kwenye ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Aprili 11, 2019, Kigamboni jijini Dar es Salaam. Tokea kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, kwenye ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Aprili 11, 2019, katika Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa akitoka kwenye jengo la Utawala la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam, kabla ya kufungua kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Aprili 11, 2019. Kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Stephen Wasira, kwenye ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere yaliyofanyika katika Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam Aprili 11, 2019.
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia, kwenye ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere lililofanyika katika Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam Aprili 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere yaliyofanyika katika Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam Aprili 11, 2019.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Stephen Wasira akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere yaliyofanyika katika Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam Aprili 11, 2019.


RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA MAFINGA-IGAWA (TANZAM HIGH WAY) MARA BAADA YA U UJENZI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wengine akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara kuu ya TANZAM sehemu ya Mafinga-Igawa km 138.7 katika sherehe zilizofanyika Wanging’ombe Makambako mkoani Njombe.
 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi mbalimbali akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa barabara kuu ya TANZAM sehemu ya Mafinga-Igawa km 138.7 katika sherehe zilizofanyika Wanging’ombe Makambako mkoani Njombe.
  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Makambako mara baada ya kuwasili katika eneo la viwanja vya Polisi Makambako mkoani Njombe.
 Barabara Kuu ya TANZAM sehemu ya Mafinga-Igawa km 138.7 ambayo ukarabati wake wa Ujenzi umekamilika kama inavyoonekana.

 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mtwango Makambako wakati akielekea kwenda kufungua mradi wa barabara.

 Ngoma ya mganda ikitoa burudani katika viwanja vya Polisi Makambako mkoani Njombe mara baada ya ufunguzi wa barabara hiyo. PICHA NA IKULU

HII NI KUBWA ZAIDI, WATEJA HALOTEL KUONGEA BURE

$
0
0


Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Halotel Mhina Semwenda akiongea na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Huduma mpya ya TOMATO PLUS katika ofisi za makao makuu ya Kampuni ya simu ya Halotel, ambapo mteja wa Halotel atapata uhuru wa kupiga simu na kuongea dakika 5 za kwanza kwenda mitandao yote bila kikomo. Kujiunga na huduma hii piga *148*66# Kisha chagua namba 8.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Halotel Mhina Semwenda akiongea na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Huduma mpya ya TOMATO PLUS katika ofisi za makao makuu ya Kampuni ya simu ya Halotel, ambapo mteja wa Halotel atapata uhuru wa kupiga simu na kuongea dakika 5 za kwanza kwenda mitandao yote bila kikomo. Kujiunga na huduma hii piga *148*66# Kisha chagua namba 8. Pamoja naye ni Afisa Uhusiano wa Kampuni hiyo Stella Pius.

…………………………………………………………………………..

Kampuni ya Mawasiliano ya simu ya Halotel, imeendelea kuongeza thamani na ubunifu katika mawasiliano kwa kuzindua huduma mpya iliyoboreshwa ili kuwawezesha wateja wake nchi nzima kufurahia mawasiliano wakiwa mtandao wa Halotel pekee.

Huduma hiyo mpya iendayo kwa jina la TOMATO PLUS itamuwezesha mteja wa Halotel kuongea kwa dakika 5 za mwanzo bure mitandao yote kwa kila simu atakayopiga pale atakapojiunga na huduma ya Tomato Plus.

Akiongea na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa kitengo cha Mawasiiano wa Halotel Mhina Semwenda,amesema huduma hii ni ya wateja wote wa Halotel na Mteja akijiunga na huduma ya Tomato Plus, anaweza kuongea kwa dakika tano za mwanzo bure mitandao yote kwa kila simu atakayopiga.

“Huduma hii imeboreshwa zaidi kwa kuzingatia mahitaji ya wateja wetu katika mawasiliano ili kuwawezesha kuwasiliana bila kikomo kwa kupiga simu mitandao yote na kuongea kwa dakika 5 za mwanzo bure kwa kila simu watakayopiga” alisema Semwenda.

“Mteja wa Halotel anaweza kujiunga na kufurahia huduma hii kwa kupitia menu yetu ya kwaida ya *148*66# na kasha atachagua namba namba 8 ambapo ataweza kujiunga kwa siku, wiki au mwezi na kufuraha huduma ya Tomao Plus wakati wowote na mahali popote.” Alisema na kuongeza Semwenda.

Huduma ya TOMATO PLUS imelenga katika kuongeza ufanisi, nafasi na uwezo wa mawasiliano kwa wateja wa Halotel na kwa watanzania wote, wakiwemo wafanya biashara, wafanyakazi wa sekta binafsi na serikali na wateja wengine walioko sekta zingine mijini na vijijini ambako maeneo haya kwa kiasi kikubwa hutegemea njia ya simu za mkononi kuweza kuwasiliana na kupata taarifa mbali mbali kwa uhakika.

SERIKALI YATOA TAHADHARI KUHUSU UGONJWA WA DENGUE NCHINI

$
0
0

Na WAJMW-DODOMA

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa tahadhari ya kuwepo kwa ugonjwa wa Dengue nchini ambao umebainika katika mikoa ya Dar Es Salaam na Tanga.

Akitoa tahadhari hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma leo, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema hadi kufikia April 2 2019 kati ya watu 470 waliopimwa, wagonjwa 307 wamethibitishhwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa Dengue, na kati ya hao 252 ni kutoka Dar Es Salaam na 55 ni kutoka Tanga.

Dkt. Ndugulile amesema ugonjwa wa homa ya Dengue unasababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu wa aina ya “Aedes” ambao ni weusi wenye madoadoa meupe yenye kung’aa.

Aidha, Dkt. Ndugulile  ametaja dalili za ugonjwa huu kuwa ni homa ya ghafla, kuumwa kichwa hususani sehemu za macho, maumivu ya viungo na uchovu. Dalili hizi huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi 14 tangu mtu alipoambikizwa  virusi vya ugonjwa huu.

Naibu Waziri huyo amewataka wananchi kuwa makini pindi wapatapo homa na wahakikishe wanakwenda kupata huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya ili waweze kupimwa na kupatiwa tiba sahihi.

Dkt. Ndugulile amewataka wananchi kusafisha mazingira na kufukia madimbwi ambayo mbu aina ya Aedes hupendelea kuzaliana kwenye maji yaliyotuama karibu na makazi ya watu au hata ndani ya nyumba, kuondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalia ya mbu kama vile vifuu vya nazi, makopo, magurudumu ya magari. Pia wanatakiwa kufyeka vichaka na kusafisha gata za mapaa ya nyumba ili kutoruhusu maji kutuama.

Pamoja na hayo, Dkt. Ndugulile amesema mbu hawa huwa na tabia ya kuuma Zaidi wakati wa mchana hasa wakati wa asubuhi jua linapochomoza na jioni jua linapozama na hivyo wananchi wanatakiwa kujihadhari.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa tahadhari kuhusu kuzuka kwa ugonjwa wa Dengue nchini. Kushoto ni Mganga mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images