Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

HALOTEL YAKABIDHI MSAADA KWA NAIBU WAZIRI WA MIPANGO NA FEDHA DKT. ASHATU KIJAJI KONDOA.

$
0
0


Kampuni ya simu za mikononi ya Halotel imetoa msaada wa madawati 55 kwa ajili ya shule za Sekondari za wilaya ya Kondoa ikiwa ni malengo yake ya kuunga mkono juhudi za wilaya hiyo na Serikali katika kuboresha elimu.

Akipokea msaada huo wilayani humo juzi, Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaji mbali na kuipongeza Halotel kwa msaada huo alisema madawati hayo ni msaada mkubwa kwa wilaya hiyo iliyojipambanua katika mkakati wa kipekee wa kukuza elimu.

Alisema Halmshauri hiyo na wanakondoa wote kwa ujumla wanatambua juhudi mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ya simu katika kuboresha maisha ya wananchi hayo ikiwemo ya kuwaunganisha na nchi nzima kupitia njia ya mawasiliano ya simu za mkononi.

Dkt Kijaji alisema kupokelewa kwa madawati hayo kwa kiasi kikubwa kutasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa madawati uliomo katika wilaya hiyo na hivyo kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kutokana na uhitaji uliopo kwa sasa.

“Naomba nichukue nafasi hii kuwapongeza Halotel kwa msaada huu ikiwa kama mdau mkubwa wa maendeleo ya elimu ndani ya wilaya hii na Tanzania kwa ujumla, nitoe wito kwa taasisi na kampuni zingine kuiga mfano huu kwa ajili ya maendeleo ya elimu katika Taifa letu” alisema Dk Kijaji.

Aidha aliiomba Kampuni hiyo kuisaidia wilaya hiyo kuboresha elimu kwa kuwajengea maabara itakayokuwa imeunganishwa na mfumo wa mtandao wa intaneti kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo masomo mbalimbali hususani ya sayansi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Nguyen van Son, alisema kampuni hiyo kama mdau mkubwa maendeleo inayo mikakati mbalimbali katika kuboresha ya sekta ya elimu na afya nchini ikiwa ni mipango yake ya kushirikiana na Serikali kutatua changamoto mbalimbali zilizopo nchini.

Alisema kwa kutambua changamoto za kielimu zilizopo katika wilaya hiyo, Halotel iliona ina kila sababu ya kutoa msaada wa c madawati hayo kwa lengo la kumuunga mkono juhuzi za wilaya hiyo za kuboresha elimu zinazofanywa na Naibu Waziri wa Wizara ya fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo hilo la Kondoa Dk Ashatu Kijaji.

Alisema Halotel imekuwa ikiunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali kuboresha maisha ya wananchi wake kwa kushiriki katika mambo mbalimbali hususani katika sekta za afya na elimu, na hivyo kupunguza changamoto hizo zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini.

Akitolea mfano katika sekta ya afya, Van Son alisema katika siku za hivi karibuni Halotel imenzisha mpango maalumu utakaowawezesha watu wenye matatizo ya kiafya kukutana na kupata ushauri wa tiba na matibabu kwa kuwaunganisha na madaktari bingwa chini ya mpango maalumu ulioanzishwa na kampuni hiyo.

Alisema Halotel inatambua changamoto zilizopo katika eneo hilo hivyo wao kama wadau wakubwa wa maendeleo wanaona wana kila sababu kushirikiana na Serikali katika kuzitatua na hivyo kuongeza kasi ya maendeleo nchini inayofanywa chini ya uongozi wa awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli.

Naye Afisa elimu wa Wilaya ya Kondoa Hildegard Segunda alisema wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu wa madawati 906 uliotokana na ongezeko la wanafunzi katika shule za Sekondari zilizopo katika wilaya hiyo.Alisema hatua hiyo imetokana na muitiko wa wanafunzi kuingia shuleni kwa wingi na hususani baada ya kuondolewa gharama za malipo chini ya mpango bure wa elimu uliotolewa na Rais Magufuli. 
Naibu Waziri wa wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel Nguyen Van Son,wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla fupi ya kukabidhi madawati kwa ajili ya shule za Sekondari za wilaya ya Kondoa ikiwa ni moja ya malengo yake ya kuunga  mkono juhudi za wilaya hiyo .Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kondoa na baadhi wa maofisa na watendaji katika wilaya hiyo.

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akikabidhiwa madawati 55 na Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel Nguyen Van Son, kwa ajili ya shule za Sekondari za wilaya ya Kondoa ikiwa ni moja ya malengo yake ya kuunga  mkono juhudi za wilaya hiyo na Serikali  katika kuboresha elimu katika wilaya hiyo.

STARTIMES YAJA NA CHANELI YENYE MAUDHUI YA WATOTO KWA KISWAHILI

$
0
0
KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes imetangaza ujio wa chaneli ya watoto kwa lugha ya Kiswahili kupitia king’amuzi chake. Chaneli ya StarTimes Kids itakuwa na chaguo la lugha ya Kiswahili kuanzia tarehe 10 Aprili mwaka huu.

Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja maudhui   wa Startimes Zamaradi Nzowa amesema kuwa chaneli hiyo ya ST Kids ni mahususi kwa ajili ya watoto wadogo wenye umri kati ya 5 hadi 9, na maudhui yake yanalenga kuwajengea watoto uwezo wa kuwa wabunifu na kuhusiana vizuri na wazazi wao.

Pia amesema kuwa,  "Kwa kuonesha tunajali ukuaji wa mtoto pamoja na utamaduni wa kitanzania, kwa sababu lugha ni sehemu ya utamaduni basi kuwa na vipindi vya watoto katika lugha ya Kiswahili itawasaidia kuwajengea kujiamini na kujifunza kwa urahisi zaidi kwa sababu ni lugha ambayo wanaielewa” Ameeleza Zamaradi.

 Aidha amesema kuwa ST Kids  ni chaneli ya kwanza ya watoto nchini ambayo vipindi vyake vitakuwa katika lugha ya Kiswahili hivyo ni nafasi ya kipekee kwa wazazi kuwapatia watoto wao kilicho bora kwa ajili ya ukuaji bora na amesema kuwa
Katuni ambazo zitakuwa katika lugha ya Kiswahili ni pamoja  na ile inayopendwa zaidi ya paka wa Opera na  vipindi hivyo vitaanza kuoneka saa 12 jioni hadi saa 2 Usiku na vitakuwa vikirudiwa. 

Amesema kuwa mbali na katuni hizo pia kutakuwa na vipindi vingine vitakavyokuwa vikifundisha watoto mambo mbali mbali kama michezo, kuchora, kutengeneza maumbo pamoja na nyimbo.


Katuni na vipindi vingine vya Kiswahili vitaanza kuonekana saa 12 jioni siku ya tarehe 10 Aprili kwenye chaneli ya ST Kids ambayo inapatika katika kifurushi cha MAMBO kwa watumiaji wa dikoda za Antenna na kifurushi cha SMART kwa watumiaji wa dikoda za Dish nchi nzima.
Muhamasishaji wa Mtandaoni Wema Sepetu akikikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Mapambano kwa niaba ya StarTimes Tanzania wakati wa uzinduzi wa Chaneli ya StarTimes Kids kwa lugha ya Kiswahili leo katika Shule ya Msingi Mapambano jijini Dar es Salaam.
Muhamasishaji wa Mtandaoni Dinah Marious akikikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Mapambano kwa niaba ya StarTimes Tanzania wakati wa uzinduzi wa Chaneli ya StarTimes Kids kwa lugha ya Kiswahili leo katika Shule ya Msingi Mapambano jijini Dar es Salaam.
Timu ya Idara ya Masoko StarTimes Tanzania na Wahamashaji wa Mtandaoni Dina Marious na Wema Sepetu wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano mara baada ya uzinduzi wa Chaneli ya StarTimes Kids kwa lugha ya Kiswahili  leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa StarTimes Tanzania, David Malisa akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa uzinduzi wa Chaneli ya StarTimes Kids kwa lugha ya Kiswahili leo katika Shule ya Msingi Mapambano jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais afungua Warsha ya 24 ya Utafiti (REPOA)

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi na washiriki wakati wa warsha ya 24 ya Utafiti iliyoandaliwa na Taasisi yaUtafiti wa Masuala ya Umaskini (REPOA) jijini Dar es Salaam leo April 10,2019.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Baadhi ya washiriki wa Warsha ya 24 ya Utafiti wa masuala mbalimbali, wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua Warsha ya 24 ya Utafiti wa masuala mbalimbali iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa masuala ya Umaskini (REPOA) Warsha hiyo imefunguliwa leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa Warsha ya 24 ya Utafiti iliyoandaliwa na Taasisi yaUtafiti wa Masuala ya Umaskini (REPOA) jijini Dar Es Salaam leo April 10,2019.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Taasisi ya Utafiti ya REPOA, wakati alipowasili kwenye ufunguzi wa Warsha ya 24 ya Utafiti  (REPOA) inayofanyika leo Aprili 10, 2019 jijini Dar es Salaam.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Warsha ya 24 ya Utafiti wa masuala mbalimbali iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa masuala ya Umaskini (REPOA) Warsha hiyo imefunguliwa leo April 10,2019 jijini Dar es Salaam.

RC MAKONDA ATIMIZA AHADI YA KUWAPATIA WAJANE MILIONI 10 NA KUWAJENGEA JENGO LA MAKAO MAKUU YA CHAMA CHA WAJANE NCHINI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MKUU  wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo April 10 ametimiza ahadi yake aliyoitoa  ya kuwapatia wajane kiasi cha Shillingi milioni 10 za kusaidia kutatua changamoto za kiofisi zilizokuwa zikiwasumbua wajane na hiyo ni pamoja na malimbikizo ya madeni ya kodi kwenye nyumba wanayoitumia kama ofisi.

Inakumbukwa kuwa Aprili 4 wakati wa kongamano la wajane Makonda alitoa ahadi ya kuwapatia wajane hao kiasi cha shilingi milioni 10 na kuwatafutia eneo la kujenga jengo la ofisi za makao makuu ya chama cha wajane nchini na tayari eneo hilo limepatikana tayari kwa kuanza ujenzi.

Mapema leo Afisa elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam Hamis Lissu amewakabidhi wajane hoa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa niaba ya RC Makonda ambaye yupo katika majukumu mengine ya kitaifa.

Kwa upande wao wajane hao wamemshukuru RC Makonda kwa kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili na wanaamini kupitia uongozi thabiti wa RC huyo ujenzi wa jengo la makao makuu ya chama hicho utakamilika kwa uharaka.
 Afisa elimu na katibu tawala msaidizi wa Mkoa wa Dar es Salaam Hamis Lissu (kulia) akikabidhi fedha takribani ya shilingi milioni 10 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kwa mwenyekiti wa wajane Rose Sarwatt leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti na Mkurugenzi wa chama cha wajane nchini Rose Sarwatt akionesha fedha walizopewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Mokonda kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi, leo jijini Dar es Salaam.

WABUNGE WA UGANDA WAFANYA ZIARA BUNGENI DODOMA

$
0
0
 Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akizungumza jambo na Mkuu wa Msafara wa Wabunge na Watumishi wa Bunge la Uganda na Mnadhimu Mkuu wa Upinzani wa Bunge hilo Ssemujju Ibrahim Ofisini kwake Jijini Dodoma hii leo. 
 Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akizungumza jambo na Ujumbe wa Wabunge na Watumishi wa Bunge la Uganda waliopo ziarani hapa nchini Ofisini kwake Jijini Dodoma hii leo. 
Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wabunge na Watumishi wa Bunge la Uganda waliomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)

SERIKALI YAFAFANUA KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI

$
0
0
Na Lulu Mussa,Dodoma 

Serikali imejipanga kuhakisha kuwa mifuko mbadala wa plastiki inapatikana kwa wingi ili kukidhi mahitaji. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika hii leo Jijini Dodoma na kusisitiza kuwa katazo la Mifuko ya Plastiki lililotolewa jana na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa linakuwa na nguvu kisheria kwa kuandika kanuni za katazo ya mifuko ya plastiki zitakazotangazwa katika gazeti la Serikali chini ya Sheria ya Mazingira na kutoa adhabu kwa kila mtu atakaekiuka utaratibu uliowekwa. 

“Kabla ya Serikali kutangaza hatua ya kupiga marufuku mifuko ya plastiki, ulifanyika utafiti na maandalizi ya mifuko mbadala. Uwezo wa kuzalisha upo na mifuko ya karatasi inayotumika Kenya na Rwanda inatumia malighafi inayozalishwa Mgololo-Iringa,Tanzania.” Makamba alisistiza 

Waziri Makamba ameainisha kuwa kuna vifungashio ambavyo havitapigwa marufuku ambavyo ni pamoja na vifungashio vya dawa za hospitalini, vifungashio katika sekta ya kilimo na ujenzi pia vile vya kuhifadhi maziwa na kutolea mfano wa vifungashio vya maziwa ya ASAS na Tanga Fresh, hata hivyo utaratibu maalumu utawekwa kwa wamiliki wa kukusanya vifungashio hivyo mara baada ya matumizi yake. 

Akizungumzia juu ya ushirikishwaji, Waziri Makamba amesema kuwa zoezi hili limekuwa ni shirikishi na hatua iliyotangazwa na Waziri Mkuu sio ya kushtukiza kwa kuwa Ofisi yake iliratibu mikutano katika maeneo kadhaa nchini kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu zuio la mifuko ya plastiki. 

Katika kukamilisha utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Waziri Makamba amesema Ofisi yake imeunda kikosi kazi cha kusimamia katazo hilo kikihusisha wajumbe kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, Mamlaka ya Mapato Tanzania, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Shirika la Viwango Tanzania, Mamlaka ya Chakula na Dawa, Jeshi la Polisi na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Wengine ni Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Katika hatua nyingine Waziri Makamba amesema kuwa mapema wiki ijayo ataitisha mkutano wa wawekezaji wa mifuko mbadala kote nchini na kujadili kwa kina namna bora ya kuwekeza katika uzalishaji wa mifuko mbadala rafiki wa mazingira. 

Serikali imetangaza kuanzia Juni Mosi 2019 kuwa ni marufuku kutengeneza, kuingiza, kuuza na kutumia mifuko ya plastiki kwa ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote na matumizi yake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea na waandishi wa Habari kufafanua tamko la Serikali la kupiga marufuku uzalishaji, usambazaji na matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchini. Mkutano huo umefanyika hii leo katika jengo la PSSSF jijjini Dodoma.

WANANCHI IRINGA WAPO HATARINI KUPATA MAGONJWA YA MLIPUKO

$
0
0
Diwani wa Kata ya Mshindo Ibrahimu Ngwada akifanya mahojiano na mwandishi wa habari Fredy Mgunda wa kituo cha Radio Nuru FM Iringa ambaye amepata mafunzo kutoka Mradi wa Boresha Habari na kukiri kuwepo kwa kero hiyo inayotokana na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuwa na uhaba wa magari ya kuondolea taka katika mitaa mbalimbali.
Mmoja ya wanafunzi akipita katika kontena la kuhifadhia taka taka lilopo manispaa ya Iringa ambalo wananchi wanalilamikia pia
Diwani wa Kata ya Mshindo Ibrahimu Ngwada akifanya mahojiano na mwandishi wa habari Fredy Mgunda wa kituo cha Radio Nuru FM Iringaambaye amepata mafunzo kutoka Mradi wa Boresha Habari akimuoneshea umbali wanakotoka wananchi kuja kutupa taka kwenye kontena hilo

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

WANANCHI wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa wapo hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na serikali kushindwa kuzoa taka kwa wakati katika makontena ya kuhifadhia taka taka mbalimbali zilizopo katika halmashauri hiyo.

Wakizungumza na blog hii wananchi hao walisema kuwa makontena ya kuhifadhia taka taka yamekuwa ni hatari kubwa hasa kwa watoto ambao wanacheza karibu na mazingira ya maeneo hiyo hali inayopelekea kuhofia kupata magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu

“makontena ya kuhifadhia taka taka haya ya kubebea taka taka yanatuathiri sana kutoka na uchafu ulipo,unakuta wametupa Mbwa waliokufa,taka taka zilizooza ambazo ndio zimekuwa zikisababisha magonjwa ya milipiko,hivyo tunaomba serikali iwe makini na haya makontena ya taka taka” walisema Wananchi

Wananchi hao walisema kuwa uongozi wa halmashauri umekuwa ukiwajibu wananchi kuwa tatizo ni kukosekana kwa mafuta kwenye gari ambazo zimekuwa zikitumika kubebea makontena ya kuhifadhia taka taka jambo ambalo limekuwa likiwakera wananchi kutokana na kauli hiyo.

“Mwandishi ukiwaambia viongozi kuhusu tatizo hili la kujazana kwa taka taka kwenye maeneo haya ni kutokana na uongozi wetu wa halmashuri ya manispaa ya Iringa kusema kuwa hawana mafuta,sasa sisi wananchi tunaoteseka tunakuwa hatuna cha kufanya” walisema Wananchi 

Aidha wananchi hao walisema kuwa maeneo mengi ya kutupa taka taka hizo yanapakana na shule za misingi zilizopo katika halmashauri ya manispaa ya Iringa hivyo inapelekea kuhatarisha afya za wanafunzi wetu ambao bado ni watoto wadogo.

Hiki kipindi cha vua na taka zinatupwa karibu kabisa na maeneo ambayo yanashule zetu za msingi na watoto wetu wanapita katika maeneo hayo na wengine wapenda kucheza katika maeneo hivyo ni hatari sana kwa watoto kupata magonjwa ya mlipuko” walisema Wananchi

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mshindo Ibrahimu Ngwada amekiri kuwepo kwa kero kwani inatokana na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuwa na uhaba wa magari ya kuondolea taka katika mitaa mbalimbali.

“Niwaambie ukweli hata mimi ni mmoja ya waathirika wa taka taka hizi ambapo naona hali hii ikiendelea kuwa hivi basi yawezekana kukalipuka kwa magonjwa ya milipuko kutokana nauchafu ulipo na sio kata hii hata kata zingine hali hii ipo kama hapa” alisema Ngwada

Ngwada alisema kuwa mikakati ni kuhakikisha anaibana halmashauri kuchukua uchafu huo uliopo kwenye makontena ya kuhifadhia taka taka yanatolewa kwa wakati maana hakuna namna nyingine zaidi ya hiyo.
“Sisi hatuna uwezo wa kutoa hapa hizi taka taka kuzipeleka Kihesa Kilolo ambao ndio kuna eneo la kutupa taka taka zote za halmashauri ya mji ,hivyo ni lazima halmashuri iwajibike kwa jukumu la kutoa hizi taka taka kwa wakati ili kuwaondolea kero wananchi wetu” alisema Ngwada

Ngwada aliupongeza Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kwa kuwapa mafunzo waandishi wa habari na kusababisha kuibua kero za wananchi na kucha kuandika habari za viongozi tu.

“Kwa kweli mradi huu umenifurahi maana sijawahi kupata waandishi wengi wakija katika kata yangu na kuibua kero za wananchi kama hivi bari hii ndio mara ya kwanza na naomba waandishi wa radio Nuru fm endeleeni hivi hivi kwa kuwa mtatukumbusha viongozi kuwatumika wananchi vilivyo” alisema Ngwada

Katika mafunzo hayo Mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo aliichagua habari hii kutoka group na moja kuwa ndio habari iliyoandikwa kwa kiwango kinachotakiwa kutokana na mafunzo.

Naye afisa afya wa halmashauri ya manispaa ya iringa christian ndenga amesema kuwa changamamoto inayopelekea takataka kukaa muda mrefu kwenye makontena ya kuhifadhia taka taka ya mitaa ni kutokana na mji kukua pamoja na kuharibika kwa magari ya kuzolea taka.

Changamoto kubwa ni kuharibika kwa magari yetu na magari mengine kwenda kufanyiwa matengenezo ya kawaida hivyo kukosekana kwa gari moja tu kwa siku lazima tutazidiwa tu kutoa taka taka hizo.

Licha ya wananchi kulalamikia kuwepo kwa mrundikano wa taka kwa muda mrefu manispaa ya Iringa hivi karibuni imeshika nafasi ya kwanza kati ya manispaa zote hapa nchini kwa usafi.

Prof. Kabudi azungumza na Uongozi wa Airtel jijini Dodoma.

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa kampuni ya Simu ya Airtel, mazungumzo hayo yamefanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma Tarehe 10 Aprili,2019. 
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Kampuni ya Simu za Mkononi Airtel nchini, wapili kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Bharti Airtel Bw. Mukesh Bhavnani, wa kwanza kulia Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw. Sunil Colaso na wakwanza kilia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) leo tarehe 10 Aprili,2019 Jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Simu za Mkononi Airtel ukiongozwa na Bw. Mukesh Bhavnani, Mwanasheria wa Bharti Airtel, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw. Sunil Colaso na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano.

Katika mazungumzo hayo, Uongozi wa Airtel umemuhakikishia Mheshimiwa Kabudi kuwa Kampuni ya Bharti Airtel itaendelea kuwa Mbia mzuri na Serikali na kwamba wataendelea kupanua wigo wa huduma zao katika maeneo yote nchini na kuhakikisha hudua hizo zinakuwa za viwango na nafuu kwa watumiaji. Na kwamba mpango wao wa uwekezaji na kupanua wigo wa huduma zao hususan maeneo ya vijijini utakuwa moja ya chachu ya maendeleo ya kiuchumi nchini.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Kabudi pamoja na kuwashukuru kwa kumtembelea ameihakikishia Bharti Airtel kuwa Serikali iko tayari kuendelea na ubia walionao na iko tayari kuendelea kushauriana na kushirikiana namna bora ya kuimarisha ubia huo ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa na viwango na zinafika katika maeneo mengi nchini kwa gharama nafuu.

TAKUKURU TANGA YAMTAKA MTUMISHI ALIYECHUKUA MSHAHARA HEWA MILIONI 30 MUHEZA KUREJESHA

$
0
0
 MKUU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru Mkoani Tanga Christopher Mariba akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakati akitoa taarifa yao ya miezi mitatu ya utendaji wao ambapo katika kipindi hicho walifungua shauri moja ambalo lilifikia mwisho na kutolewa maamuzi.
Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mkoani Tanga wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Takukuru mkoa wa Tanga Christopher Mariba wakati akitoa taarifa yao ya miezi mitatu ya utendaji wao

TAASISI ya kuzuia na Kupamba na Rushwa Mkoani Tanga imemtaka aliyekuwa mtumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Idara ya Elimu Aneth Makame kurejesha kiasi cha milioni 30 alizichukua wakati akijua tayari amekwisha kustaafu na kuisababishia serikali hasara.

Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa Takukuru Mkoani Tanga Christopher Mariba wakati akitoa taarifa yao ya miezi mitatu ya utendaji wao ambapo katika kipindi hicho walifungua shauri moja ambalo lilifikia mwisho na kutolewa maamuzi.

Alisema mtumishi huyo aliomba kustaafu kwa hiyari akiwa na miaka 55 lakini akaendelea kuchukua mshahara kwa miaka mitano iliyofuatia na hivyo kuisababishia hasara kiasi hicho.

Alisema suala hilo linahusiana na mishahara hewa kutokana na kwamba baada ya kustaafu kwa hiari mtumishi huyo aliendelea kula mshahara na kusababisha hasara ya kiasi hicho kwa serikali huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Aidha alisema bado mtumishi huyo hajaanza kurejesha fedha hizo huku taasisi hiyo ikimtaka kufika ofisini kwao yeye na familia yake ili waweze kuweka utaratibu wa kuzirejesha fedha hizo haraka iwezekanavyo.

“Endapo atashindwa kufanya hivyo basi itabidi tutafute utaratibu mwengine kupata fedha hiyo nah ii itakuwa ni pamoja na kuuza nyumba au mali yoyote anayomiliki…kabla ya maamuzi hayo mshtakiwa alikuwa amekwisha kukaa mahabusu takribani mwaka mmoja na nusu bila dhamana”Alisema.

Mkuu huyo wa Takukuru Mkoa alisema pia katika kipindi hicho mkoa huu umeokoa kiasi cha sh.milioni 2,190,500 kilicho kuwa kimechukuliwa kinyume cha sheria na taratibu za fedha .

“Pamoja na kiasi hicho kurejeshwa tumewaandikia barua waajiri wa wahusika kwa lengo la kuweza kuchukua hatua za kinidhamu /kiutawala dhidi ya watumishi waliohusika na matendo hayo “Alisema.

MAMA SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA 24 WA REPOA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na Watafiti na Viongozi wa Kiserikali, wasomi pamoja na Wadau wa Maendeleo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Watafiti la 24 Lililoandaliwa na Repoa lenye Ujumbe usemao Maendelo ya Uchumi wa ndani kwa kuanzia katika ngazi ya Serikali za Mitaa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Repoa Dr. Donald Mmari akizungumza na Washiriki kabl ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Repoa aweze kumkaribisha mgeni ramsi hili azungumze na Washiriki wa Kongamano hilo.
Mtoa Mada juu ya Maendeleo ya kiuchumi kutoka Erasmus Univesity nchini Uholanzi,Prof .Peter Knoriga akiwa silisha Mada yake mbele ya Mgeni Rasmi wakati wa Kongamano la 24 la Watafiti lililoandaliwa na Repoa 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu akisalimiana na Mmoja ya Wafanyakazi wa Tasisi ya Utafiti Nchini Repoa, Khadija Omari wakati akiwasili katika Mkutano mkuu wa 24 wa mwaka.
 Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wakisikiliza kwa Makini Hotuba ya Mgeni Rasmi Mama Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali wakifatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya Pamoja na Viongozi wa Repoa pamoja na Washiriki wa Kongamano la 24 la Tasisi hiyo.

WAISLAMU WAOMBA KUJITOKEZA KUSHIRIKI RAMADHANI MARATHON

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Tasisi ya Pink Hijab Initiatives imeandaa mbio na Matembezi ya Kilometa kumi kuanzia Viwanja vya Green Ground Osterbay na kuishia katika Viwanja hivyo kwa kupitia barabara ya  Kenyata, Chole Road,Karume Road , Haile Salasi Road kupitia Coco Beach na kurudi katika Viwanjani hapo.

akizungumza na Globu ya Jamii Mratibu wa Mbio hizo kutoka Pink Hijab Initiative, Alhaj Jamal Mwarab Khalfan amesema kuwa lengo la mbio hizo ni kusaidia watoto waliopo katika Mazingira hatarishi katika Mkoa wa Tanga Wilaya ya Pangani.

"Sisi kama Tasisi ya Kislamu tumeona vyema kuitumia Ramdhani hii kama sehemu ya kurudisha tunachokipata kwa jamii kwa kuandaa mbio hizi na matembezi hili tuweze kuwasaidia watoto wetu waliopo katika Wilaya ya Pangani hivyo tunawaomba wote wenye mapenzi mema na watoto wetu kuja kujumuika na sisi April 21 Mwaka huu"amesema Alhaj Jamal.

Amesema mtu anayependa kushiriki mbio hizi anaweza kuchangia kiasi cha shilingi 20,000/-pia naweza kuwasiliana nasi kupitia namba 0713433407 au 0655445105 hili aweze kushiriki na kuchangia zaidi.

--

DC KISHAPU AZINDUA MRADI WA SAUTI YA MWANAMKE NA MTOTO

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga bi. Nyabaganga Talaba akipokea nyaraka za mradi wa 'Sauti ya Mwanamke na Mtoto' kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape ACP, John Myola (kulia) wakati wa uzinduzi wa mradi huo leo Aprili 9,2019 


Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga Nyabaganga Talaba amezindua rasmi Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Mtoto unaotekelezwa na Shirika la Agape ACP kwa lengo la kumwezesha mwanamke na mtoto kupata haki na usawa kwa wakati katika jamii.

Mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la United Nation Development Programme (UNDP) utatekelezwa kwa kipindi cha miezi sita katika kata tatu za wilaya ya Kishapu ambazo ni Itilima,Bunambiyu na Kishapu.

Akizungumza leo Jumanne Aprili 9,2019 wakati akizindua Mradi huo katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu,Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba alisema mradi huo unalenga kumuinua,kumtetea mwanamke na mtoto.

“Sauti ya mwanamke na mtoto siyo sauti ya kawaida,ni sauti ambayo ikisikika jamii hushtuka, mradi huu uwe chachu ya kuleta mabadiliko kwa wanawake na watoto, wajihisi kuwa wao ni watu wa muhimu sana katika taifa hili,tubadilike pale tulipojisahau na kusahau sauti za makundi haya,sauti, wale waliofanya wanawake na watoto wakose upendo na furaha waache sasa”,alisema Talaba.

“Nawashukuru UNDP kwa kuwezesha mradi huu kufanyika katika wilaya yetu,naomba wasichoke na sisi kama serikali tutahakikisha kuwa tupo bega kwa bega na Agape kuhakikisha malengo ya mradi yaliyokusudiwa yanafikia mwisho”,alisema Talaba.

Alisema hatutaweza kufikia malengo ya serikali ya kufikia uchumi wa kati kama mwanamke bado hajitambui huku akibainisha kuwa mwanamke akijitambua na taifa litajitambua lakini pia maendeleo hayaji kwa kumuacha mwanamke nyuma.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape ACP, John Myola alisema mradi huo unalenga kuboresha na kuimarisha upatikanaji wa huduma bora ya haki na kwa wakati muafaka miongoni mwa wanawake na watoto pamoja na kuimarisha mfumo mzima wa haki za jinai kwa upatikanaji wa haki za jinai kwa watuhumiwa na wahanga/waathirika wa makosa ya jinai.

“Shirika la Agape ACP litashirikiana na wadau mbalimbali ngazi ya mkoa na halmashauri ya wilaya ya Kishapu kupitia idara zake za ustawi wa jamii, maendeleo ya jamii, sheria, viongozi ngazi ya kata na vijiji, polisi kitengo cha dawati la jinsia na watoto, mahakama na ofisi ya mwendesha mashitaka wa serikali, pamoja na Baraza la Watoto la Wilaya ya Kishapu”,alisema Myola.

Aidha alieleza kuwa mradi huo utatelekezwa kwa kipindi cha miezi sita kwa majaribio katika kata ya Kishapu,Itilima na Bunambiyu na kama mafanikio yataonekana maeneo ya utekelezaji wa mradi yanaweza kuongezwa hivyo kuwataka viongozi wa serikali na jamii kwa ujumla kushirikiana na Agape ili kufanikisha mradi huo.

Naye Msimamizi wa mradi wa Sauti ya Mwanamke na Mtoto, Felix Ngaiza aliyataja matarajio ya mradi kuwa ni kuongezeka uelewa na ufahamu kuhusu sheria na haki miongoni mwa wanajamii ikiwemo ongezeko la taarifa za kesi za ukatili na uvunjifu wa haki za jinai kwa wanawake na watoto.

Alisema mradi huo pia utachangia katika kufikia lengo la Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) la kufikia 50% ifikapo mwaka 2022.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga bi. Nyabaganga Talaba akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa mradi wa 'Sauti ya Mwanamke na Mtoto' unaotekelezwa na shirika la Agape ACP katika kata ya Kishapu,Itilima na Bunambiyu wilayani Kishapu.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape ACP, John Myola. - Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga bi. Nyabaganga Talaba akijiandaa kukata utepe ishara ya uzinduzi wa mradi wa 'Sauti ya Mwanamke na Mtoto' unaotekelezwa na shirika la Agape ACP. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape ACP, John Myola. 
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga bi. Nyabaganga Talaba akikata utepe wakati wa uzinduzi wa mradi wa 'Sauti ya Mwanamke na Mtoto' .
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga bi. Nyabaganga Talaba akipokea nyaraka za mradi wa 'Sauti ya Mwanamke na Mtoto' kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape ACP, John Myola.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape ACP, John Myola akimonesha Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba Andiko la Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Mtoto.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape ACP, John Myola akielezea lengo la mradi wa Sauti ya Mwanamke na Mtoto na kueleza kuwa walengwa ni wanawake wenye umri wa miaka18-55 na watoto wenye umri wa miaka 7- 17. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Underson Mandia akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba.
Msimamizi wa mradi wa Sauti ya Mwanamke na Mtoto, Felix Ngaiza akitambulisha mradi wa Sauti ya Mwanamke na Mtoto.
Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala akiwataka Maafisa watendaji wa kata na vijiji kutoa ushirikiano katika kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake kwani baadhi yao wamekuwa wakituhumiwa kukwamisha kesi kwa kuendekeza vitendo vya rushwa na kukwepesha ukweli.
Wadau wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Wadau wakiwa ukumbini.
Wadau mbalimbali wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa mradi wa Sauti ya Mwanamke na Mtoto.
Wadau wakiwa ukumbini.
Uzinduzi wa mradi unaendelea.
Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Sauti ya Mwanamke na mtoto.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Agape ACP, John Myola akiwaomba wadau katika mradi huo kushirikiana na Agape na serikali kwa kutoa taarifa za matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto badala ya kuwa na tamaa ya pesa.
Afisa Ufuatiliaji,Tathmini na Kujifunza wa Mradi wa Sauti ya Mwanamke na mtoto,Lucy Maganga akisisitiza wadau katika mradi huo kufanya kazi kwa weledi na kutokuwa waoga ili kumkomboa mwanamke na mtoto.
Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Anderson Mandia akisisitiza kuwa madiwani watakuwa mstari wa mbele katika kufanikisha mradi wa Sauti ya Mwanamke na mtoto na kwamba halmashauri ya wilaya ya Kishapu itaendelea kushirikiana na shirika la Agape ili kuhakikisha kuwa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinakomeshwa wilayani Kishapu.

Picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa mradi wa Sauti ya Mwanamke na mtoto.

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA NJOMBE PIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA NJOMBE-MAKETE KM 107.4 MKOANI NJOMBE

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu pamoja na viongozi wengine  akivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo mbalimbali ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ambayo ujenzi wake upo katika hatua za mwisho kukamilika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyakazi mbalimbali, pamoja na wakandarasi wanaojenga majengo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe mara baada ya kuweka jiwe la msingi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu pamoja na viongozi wengine mara baada ya ya kuweka jiwe la msingi katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Njombe-Makete km 107.4
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiimba pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ramadhani wakati alipokwenda kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Njombe-Makete km 107.4.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ramadhani walipokuwa wakimuonesha Shule yao ilipo pembezoni mwa barabara ya Njombe-Makete. Mkandarasi wa barabara hiyo amewaahidi watoto hao kuwajengea vyumba vya madarasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi waishio pembezoni mwa barabara ya Njombe-Makete mara baada ya kuiwekea jiwe la msingi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Njombe katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya sabasaba mkoani Njombe. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu  akisikiliza maelezo yaliokuwa yakitolewa na Dkt. Mkoni kuhusu ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe kabla ya kuweka jiwe la msingi hospitalini hapo. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono pamoja na kuwasukuru wanachi wa Njombe waliojitokeza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Sabasaba mkoani humo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia jengo hilo la hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe.
Baadhi ya wakazi wa Njombe wakiwa katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya sabasaba.
Sehemu ya jengo la la hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe. PICHA NA IKULU

RIPOTI ZA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA ULIOISHIA TAREHE 30 JUNI, 2018

$
0
0
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Juma Assad.

WAZIRI MKUCHIKA AWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2019/20

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst)  George H. Mkuchika (Mb) amewasilisha Bungeni Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na kuwataka Waajiri katika Taasisi za Umma nchini kuwawezesha Watumishi wa Umma wanaoajiriwa kwa mara ya kwanza kupata mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji katika Chuo cha Utumishi wa Umma ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Mhe. Mkuchika amesema kuwa, watumishi wengi hawajui taratibu za kiutumishi hivyo kukosa uwezo wa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Mhe. Mkuchika amesisitiza kuwa, pamoja na majukumu mengine, Chuo cha Utumishi wa Umma kina jukumu la kuwajengea uwezo Watumishi wa Umma ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma iliyopo, hivyo ni vema watumishi hao wakapata mafunzo katika chuo hicho. 

Ameongeza kuwa, kuanzia sasa atafanya ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha waajiri wote wanawapeleka watumishi wa umma wote wanaoajiriwa kwa mara ya kwanza katika Chuo hicho kupata mafunzo stahiki.

Mhe. Mkuchika ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha jumla ya kiasi cha shilingi 683, 529,221,617 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na Taasisi zilizo chini yake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst)  George H. Mkuchika (Mb) akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na Taasisi zilizo chini yake.

RIPOTI YA CAG PROFESA ASSAD YAANIKA MADUDU KILA KONA

$
0
0

*Abaini malipo hewa ya mabilioni ya fedha, mashirika mengine hoi kwa madeni

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Asaad ametoa ropoti ya ofisi yake kuhusu ripoti ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ambapo imebaini uwepo wa ubadhirifu wa fedha katika maeno mbalimbali.

Ripoti hiyo ya CAG ni ile inayoishia kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2018 ambapo Profesa Assad anasoma ripoti hiyo leo kwa waandishi wa habari Mjini Dodoma ripoti hiyo inaonesha mashirika ya umma 14 yenye yana matatizo makubwa ya kifedha na kwamba baadhi ya mashirika yamepata hasara kiasi cha kusababisha  madeni zaidi ya mitaji yao kwa zaidi ya asilimia 100. 

"Ukiangalia ripoti hii inaonesha kati ya mashirika hayo 14,  mashirika 11 yanajiendesha kwa hasara kwa zaidi ya miaka miwili.Ni dhahiri mashirika hayo hayawezi kujiendesha bila kutegemea msaada kutoka Serikali Kuu. Kwa mazingira ya aina hiyo mashirika hayo hayaweza kujiendesha na kutoa huduma kwa jamii,"amesema.

Profesa Assad ameyataja baadhi ya mashirika hayo ni Kampuni ya Maendeleo ya Nishati ya Joto Tanzania (TGDC), Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira  Dar es Salaam (DAWASA), Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Baraza la Taifa la Bishara, Baraza la Michezo la Taifa, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira, Mtwara, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira, Lindi na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira, Mwanza, Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Kampuni ya Usafirishaji na Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usambazaji wa Umeme, Bodi ya Utalii Tanzania, Kampuni ya Simu (TTCL – Pesa), Shirika la Maji Safi na Usafi wa Mazingira, Dar es Salaam (DAWASCO) na Bodi ya Maziwa Tanzania.

Akizungumzia zaidi ripoti hiyo, Profesa Assad amesema kuwa ripoti imebaini katika ununuzi wa Mashine za Mfumo wa Kidigitali wa Usajili wa Wapiga kura (BVR) uliofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) ilinunua mashine za BVR, 8,000 ili kusajili wapiga kura na kati ya mashine hizo 5,000 hazikukidhi vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba.

Amesema kuwa hivyo imesababisha kutolandana kimatumizi na vile vilivyonunuliwa hapo awali na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wakala wa Taifa wa Usajili, Ufilisi, na Udhamini (RITA). "Hivyo kutolandana huko kumeisababishia hasara kwa Serikali Sh. milioni 862.08 zilizotumiwa na NIDA kununulia leseni mpya za “Windows” na “Biometric Algorithms” ili kubadilisha mashine 5,000 zilizopokelewa kutoka NEC ziweze kufanya kazi na mfumo wa BVR wa NIDA,"amesema.

Pia amesema ndani ya ripoti hiyo imebaini mzabuni alilipwa dola milioni 72.3 badala ya dola milioni 72.1 na kwamba kiasi hicho kilikuwa bei ya mkataba."Ukifuatilia eneo hilo utaona kuna ongezeko la dola 148,243.73. Wakati mafunzo kwa maofisa 15 wa TEHAMA wa NEC hayakufanyika licha ya mzabuni kulipwa dola 358,650 kwa ajili ya mafunzo hayo".

Wakati huo huo Profesa Assad amesema ripoti hiyo imebaini ndani ya
Jeshi la Polisi katika ununuzi wa sare za askari ambapo ukaguzi maalumu uliofanywa ndani ya jeshi hilo,umeonesha Polisi wamelipa Sh.bilioni 16.66 bila ya kuwepo ushahidi wa uagizaji na upokeaji wa sare za askari kwa Boharia Mkuu katika jeshi hilo.

Profesa Assad amesema ukaguzi huo umebaini kuna maoni ya kisheria ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yanayohusu uwasilishaji wa kiapo cha nguvu ya kisheria na leseni halali ya biashara hayakuzingatiwa wakati wa kusaini Mkataba Namba. ME.014/PF/2015/2016/G/30 Lot 2, uliohusu ununuzi wa sare za askari polisi.

Amefafanua zaidi ripoti imebaini katika ukaguzi maalumu wa Mfumo wa Utambuzi wa Alama za Vidole (AFIS)kuna mambo yameonekana ambayo ni mahitaji ya kitaalamu kutoka idara inayotumia mfumo huo ambayo hayakuzingatiwa wakati wa kutathmini na kutoa zabuni.

Pia amesema kuna malipo ya Sh. bilioni 3.30 yalifanyika kwa mzabuni kwa ajili ya huduma ya matengenezo na msaada wa kitaalamu wa Mfumo wa Utambuzi wa Alama za Vidole kwenye mikoa nane ya Kipolisi ya Temeke, Simiyu, Mwanza, Tabora, Rukwa, Kigoma, na Kinondoni Geita  lakini Polisi ilishindwa kuthibitisha kuwa matengenezo hayo na msaada wa kitaalamu ulifanyika. 


Profesa Assad amesema kwamba vifaa vya Utambuzi wa Alama za Vidole vyenye thamani ya Sh. bilioni 1.73 havikufungwa kwenye magereza 35 yaliyoainishwa badala yake vilihifadhiwa katika Ofisi ya Upelelezi, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kuongeza malipo ya Sh. milioni 604.3 kwa ajili ya mafunzo kwa wataalamu 30 hayakufanyika kwani Jeshi la Polisi lilishindwa kuwaonesha maofisi ya CAG monita 58 za kompyuta aina ya Dell zenye thamani ya Sh. milioni 159.1 zilizopelekwa kwenye Kitengo cha Uchunguzi wa Kisayansi cha Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

"Ripoti inaonesha kuwa monita 213 za kompyuta aina ya Dell zililipiwa Sh.milioni 195.22 kwa mzabuni Lugumi Enterprises Limited lakini mzabuni hakuzileta,"amesema Profesa Assad.

Kuhusu malipo hewa ,Profesa Assad amesema ripoti imebaini katika uchunguzi wa vitabu vya fedha, taarifa za benki na hati za malipo za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kuna malipo ya Sh. bilioni 3, kati ya malipo hayo sh. bilioni 2.61 yalikuwa malipo hewa, sh. milioni 350.8 ni malipo ambayo walipwaji walishindwa kubainika na sh. milioni 42.6 hazikuweza kuthibitika kupokelewa na walipwaji. 


"Malipo hayo yalitakiwa kulipwa watoa huduma za afya kwa kutumia hundi zilizofungwa lakini yalifanywa kwa fedha taslimu kinyume na Kanuni za Fedha za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.Makusanyo ya mwaka yanaendelea kuwa makubwa zaidi ya malipo ya huduma za bima ya afya, ambapo kwa sasa malipo ya huduma za afya yanakua kwa uwiano mkubwa mwaka hadi mwaka zaidi ya uwiano wa kukua kwa mapato,"amesema wakati anasoma ripoti hiyo.

Ameongeza kutokana na hali hiyo makisio ya madai ya huduma za bima ya afya pekee ifikapo mwaka wa fedha utakaoishia Juni 2024 yatakuwa ni asilimia 99.2 ya jumla ya makusanyo yote ambapo uwiano huu unakisiwa kuongezeka zaidi hadi kufikia asilimia 104.8 katika mwaka unaofuata. Profesa Assad amesema uchunguzi wa vitabu vya fedha, taarifa za benki na hati za malipoza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umebaini uwepo wa Sh.bilioni tatu.

"Kati ya malipo hayo Sh.bilioni 2.61 yalikuwamalipo hewa, Sh. milioni 350.8 ni malipo ambayo walipwaji walishindwa kubainika na Sh. milioni 42.6 hazikuthibitika kupokelewa na walipwaji. 

Kwa upande wa udanganyifu katika halmashauri, Profesa Assad amesema kuna udanganyifu katika malipo ya Sh. milioni 267.89 kwenye akaunti ya matumizi mengine katika Halmashauri ya Wilaya ya Rombo ambapo alikagua malipo mbalimbali katika akaunti ya matumizi mengine na kubaini kuwa kwa nyakati tofauti kuna watumishi walianzisha, kupitisha, na kufanya malipo ya ya Sh. milioni 267.89 ambayo hayakuwa na viambatisho husika.

"Na mengine yalikuwa na viambatisho vyenye shaka.Upotevu wa mapato ya zaidi ya Sh. bilioni 3.4 katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’  ambapo mapitio ya mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani umebaini upungufu ukiwemo wa halmashauri hiyo kushindwa kuwasilisha vitabu 425 vya kukusanyia mapato. 

"Mambo mengine yaliyobainika ni upotevu wa mapato ya ndani ya Halmashauri ya sh. bilioni 1.04 yaliyokuwa yanakusanywa na mawakala, kutopatikana kwa nyaraka muhimu za makampuni ya mawakala wa ukusanyaji wa mapato kwa mikataba yenye thamani ya sh. bilioni 2.36 na malipo hewa ya sh. milioni 73.45 katika kandarasi za Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’.


"Pia ukaguzi maalumu umebaini kuwa fedha Sh. milioni 73.45 za Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji zililipwa kwa wakandarasi kama dharura bila kuwepo kazi za dharura. Ukaguzi umebaini kutokuwepo kwa ushahidi wowote wa kufanyika kwa kazi hiyo na hivyo kudhihirika kuwa matumizi hayo ni hewa," amesema Profesa Assad.

MKUTANO WA TANO MABADILIKO YA TABIANCHI WAFANYIKA DODOMA

$
0
0
Waziri Nchi,Ofisi yaMakamu wa  Rais, Anayeshughulikia  Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba akizungumza katika mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika leo jijini Dodoma katika ukumbi wa hotel ya Morena

Na.Vero Ignatus ,Dodoma 

Mkutano mkuu wa Mabadiliko ya Tabianchi umefanyika leo Jijini Dodoma ukiwashirikisha wadau zaidi ya 100 wameshiriki katika mkutano huo ukiwa na lengo la kujadili mabadiliko ya Tabia nchi na kujikwamua katika taizo hilo kama Taifa

Akifungua mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa FORUMCC Eric Mugurusi amesema lengo kuu la mkutano huo ni kujadili Sera ambazo zitatilia maanani mabadiliko ya Tabia nchi na namna ambavyo wananchi watashirikishwa ili kupunguza athari za mabadiliko hayo.  

 Amesema kuwa mkutano huo ni maalum kwaajili ya kuona nam,na ambavyo sera zinavyoweza kuwaondoa kwenye tatizo hiolo na ushirikiswahwaji wa wananchi katika hayo yote.

Waziri Nchi,Ofisi yaMakamu wa  Rais, Anayeshughulikia  Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba akizungumza katika mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi amesema katika kuhakikisha tunaondoa tatizo la mabadiliko ya tabia nchi kuwajumuishe watu wote,  kujifunze katika nchi zilizofanikiwa na kuzitumie mbinu hizo, Kuaanda Sera nzuri,Kuwahimiza watunga Sera kuamuru uchukuliwaji wa hatua

Mhe.Makamba amesema kuwa kwenye baadhi ya nchi Mabadiliko ya tabia ya nchi yametangazwa kama usalama wa nchi ambapio nasi kama nchi ipo haja ya kuonesha kuwa changamoto zinaweza kuwa kubwa kwani Utalii wetu ni Fukwe ambazo zinalika na thamani yake inaondoka sababu ya mabadiliko ya tabia ya nchi,hivyo utalii unapotea.

"Mama  yangu alikuwa Nesi miaka ya 1980 anasema kipindi hiko hakukuwa kabisa na kesi za wagonjwa wa malaria, lakini angali miaka ya sasa,Wagonjwa wa malaria wamekuwa wengi na ndo ugonjwa mkubwa hii ni sababu ya ongezeko la Mbu kwa kasi kubwa na kutokutunza mazingira yetu”Alisema Makamba

  Amesema kati ya miaka 5-10 mabadiliko ya tabia nchi yalionekana kama nadharia au yanawahusu wanasayansi ila kadri siku zinavyozidi kwenda ndivbyo tatizo linavyozidi kuwa kubwa, hata kwenye kilimo sababu ya mabadiliko ya Majira kumesababisha kuchelewa kwa mvua hivyo Kilimo kinafanyika kwa shida  pia yanapelekea umasikini.

Mimi nilisomeshwa sana kwa kilimo cha Chai na Kahawa ambacho ndio kikubwa Tanga, lakini sasa hivi kilimo cha mazao haya kinapotea,hali hii ni ishara ya kuongezeka kwa umasikini''Alisema Makamba

Kwa upande wake Meneja Mradi kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Oxfam Jovita Mlay amesema kuwa Mabadiliko ya Tabianchi yanaongeza umasikini kwa wanawaume na wanawake lakini wahanga wakubwa zaidi ni wakina mama na watoto kwani inagusa maeneo ambayo wanawake wanajipoatia kipato napo no kwenye kilimo.


Amesema kuwa wakati wa kushughulikia majanga kama hayo ni muhimu kuhakikisha kuwa inawekwa mipango na usimamizi wa kisera unaoweza kupunguza na kumaliza madhara ya yatokanayo na mabadiliko ya Tabianchi kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali

Amesema Oxfam inaendelea kufanya kazi  ili kuhakikisha kuwa maswala yanayoingizwa katika mipango mikakati na kuendelea kusapoti juhudi zinazofanywa na wadau katika kupambana na mabadiliko ya Tabianchi.

Kwa upande wake mbunge wa Babati vijijini Mhe,Jitu Soni amesema kuwa jamii nyingi zinaishi katika mazingira magumu kutokana na mabadiliko ya Tabianchi amesema kuwa mabadiliko hayo siyo jambo la mazingira peke yake bali linahusisha maswaka ya uchumi,miundombinu,mifumo ya uzalishaji,rasilimali,na nishati.

Nae Mwenyekiti wa Bunge ya Bajeti na mbunge wa Kibakwe Mhe.George Simbachawene amesema kuwa mgawanyo wa shughuli za kibinadamu imekuwa sababu kubwa ya uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya Tabianchi,amesema bado elimu inahitajika zaidi katika jamii zetu haswa vijijini ili kujinasua katika tatizo hilo.

Aidha watu wengi wanaharibu mazingira kwasababu ya kutafuta maji na nishati,uwekezaji wa kutafuta maji unatumia gharama kubwa sana,amesema nchi inahitaji kutengeneza mfumo wa kitaalam katika uharibifu wa mazingira kwani hali ni mbaya sana 

Mshiriki kutoka Asasi za kiraia mkoa wa Kagera bi Zainabu Shakiru amewaomba Serikali pamoja na wadau kuwa mchakato wa utekelezaji wa sera ya mabadiliko ya tabianchi wananchi nao washirikishwe ipasavyo ili waweze na wao kuitambua sera hiyo
Akifungua mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa FORUMCC Eric Mugurusi amesema lengo kuu la mkutanowa tano wa mabadiliko ya tabianchi Jijini Dodoma leo
Meneja Mradi Jovitha Mlay kutoka Shirika la Oxfam akizungumza katika mkutano wa tano wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika leo Jijinj Dodoma katika hotel ya Morena
Washiriki wa mkutano wa tano wa mabadiliko ya Tabianchi Jijini Dodoma leo
Ndugu Jensen Shuma kutoka shirika la TaTEDO akichangia mada katika mkutano wa tano wa mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Jijini Dodoma
Dkt.Lucy Ssendi Mshauri wa Maswala ya Mabadiliko ya Tabianchi ,Mradi wa Decentralized Climate Finance -TAMISEMI akichangia mada katika mkutano wa Tano wa mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Jijini Dodoma
Makamu Balozi wa EU Nchini Tanzania Charles Stuart akizungumza na washiriki wa mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Jijini Dodoma leo.
Jovita Mlay Meneja wa Mradi kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Oxfam Tanzania akizungumza katika mkutano wa mwaka wa mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika leo Jijini Dodoma katika hoteli ya Morena
Washiriki kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini Tanzania waliohudhuria katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Jijini Dodoma katika Hotel ya Morena.
Mkurugenzi mtendaji wa Jumuiko la maliasili Tanzania( TNRF)Zakaria Faustin akizungumza katika mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Jijini Dodoma.

MAGAZETI YA LEO AL HAMISI APRIL 11,2019

Waziri Kabudi akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudi, akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo baina yake na Balozi wa Ufaransa nchini Mheshimiwa Frédéric Clavier. Katika mazungumzo hayo Tanzania na Ufaransa wamekubaliana kushirikiana katika kilimo cha zabibu, uzalishaji na uuzaji wa mvinyo katika nchi mbalimbali duniani na usafiri wa anga.

Mazungumzo yakiendelea.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Palamagamba John Kabudi akiagana na Balozi wa Ufaransa nchini Mheshimiwa Frédéric Clavier baada ya mazungumzo baina yao. 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudi, akimkaribisha Balozi wa Ufaransa nchini, Mheshimiwa Frédéric Clavier alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 10 Aprili 2019. 

AGIZO LA WAZIRI HALIJADILIWI,NI KUTEKELEZA-PROF.KIKULA

$
0
0
Wachimbaji wadogo wakiwa chini ya mgodi katika shimo lenye urefu wa zaidi ya mita hamsini wakiwa wanaendelea na shuguli za uchimbaji katika eneo la Ipanko.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula wa pili kushoto akiwa katika eneo la wachimbaji wadogo Ipanko wilayani Ulanga akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Madini Mkazi Morogoro Mhandisi Emmanuel Shija alipotembelea kujionea namna shuguli za uchimbaji zinavyofanyika. Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Tume hiyo Dkt. Athanas Macheyeki.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari kwenye eneo la mgodi wa wachimbaji wadogo Ipanko.


Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula akionyesha jambo kwenye ramani ya mwekezaji wa Madini ya Graphite; TanzGraphite (T) Ltd. Wa tatu kushoto ni Meneja Uhusiano wa Jamii Bernad Mihayo, wa pili kushoto ni Kamishna wa Tume hiyo Dkt. Athanas Macheyeki.
Kamishna wa Tume ya Madini Dkt. Athanas Macheyeki kushoto akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula mara baada ya kuzunguka na kukagua eneo la wachimbaji lililopo Iponka eneo ambalo awali lilifungiwa kufanya shuguli za uchimbaji. 

 …………………..

Na Issa Mtuwa- Ulanga Morogoro

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amewataka Watumishi wa tume hiyo ofisi ya Morogoro na Ulanga kutambua kwamba agizo la Waziri linalowataka kufuta leseni zisizofuata utaratibu wa kisheria sio la kujadili bali ni kutekeleza.

Prof. Kikula ameyasema hayo Aprili 10, 2019 wilayani Ulanga wakati akizungumza na watumishi wa tume hiyo wakati wa ziara yake.

Taarifa iliyosomwa kwake na Afisa Migodi Mkazi ofisi ya Mahenge Ulanga, Tandu Jilabi inaonyesha kuwa wilaya ya Ulanga ina leseni za wachimbaji wadogo 221 kati ya hizo ni leseni 9 tu ndio zinazofanya kazi huku leseni za uchimbaji wa kati zikiwa 5 na leseni za utafiti wa madini 13.

Kufuatia hali hiyo, Afisa Migodi Mkazi ofisi ya Mahenge ameiomba tume ya madini kufuta leseni zisizofanya kazi ili wapewe wenye uhitaji ili waweze kuziendeleza. Kufuatia ombi hilo, Mwenyekiti wa tume amesema jukumu la kuzifuta leseni hizo ni la kwake pamoja na Afisa Madini Mkazi Morogoro na halina mjadala kwakuwa muongozo wa utekeleza wa suala hilo ulishatolewa na waziri wa Madini.

“Suala la leseni zisizofanya kazi sio la kujadili, hili ni agizo la Waziri na kazi yetu ni kutekeleza na wenye kuzifuta ni ninyi, fuateni taratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria katika kuzifuta na sio kuzifuta lazima wote waliozishikilia leseni hizo kwa muda wote walipe fidia na wasipo fanya hivyo taratibu za kisheria zifuatwe kwani katika kipindi hicho chote serikali imekosa mapato yake. Kuanzia leo pitieni leseni zote na ifikapo Juni 30 mwaka huu leseni zote zisizo hai ziwe zimefutwa”, amesema Prof. Kikula.

Wakati huo huo, mwenyekiti wa tume amekutana na kuzungumza mwakilishi wa mwekezaji wa kampuni ya TanzGraphite (T) Ltd ambae ni Meneja Uhusiano wa Jamii na kuzungumzia kuhusu mgogoro uliopo baina ya mwekezaji huyo na baadhi ya wananchi wanaotakiwa kufanyiwa tathimini ili kupisha shuguli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo.

Prof. Kikula ameonyesha kusikitishwa na mgogoro huo ambao amesema ni wa muda mrefu sasa na unachelewesha maendeleo ya watu na kuikosesha serikali mapato.

Ameongeza kimsingi wananchi wanapaswa kuelewa kuwa “right surface” (haki ya kumiliki vitu vilivyo juu ya ardhi) inampa mwananchi haki ya kulipwa fidia ya mali zilizo juu ya ardhi anayo miliki lakini watambue kuwa kuna “resource right” (haki ya kumiliki raslimali zilizo chini ya ardhi) ikiwemo madini ambayo mmiliki wake ni serikali, ndio maana inapohitaji raslimali hizo humuondoa na kumfidia mliliki wa mali za juu ya ardhi, hivyo wananchi wanapo ng’ang’ania wanatakiwa walitambue hilo.

Pia, amesema kuwa, kwa mpango ulioanishwa na mwekezaji huyo unaonyesha manufaa kwa wananchi kupitia miradi ya maendeleo (CSR) ambapo amebainisha kuwa mwekezaji ameahidi kuwalipa fidia, kuwajengea nyumba za kisasa wale wote walio ndani ya eneo.

Mambo mengine ni pamoja na kuwapatia chakula kwa muda wa miaka miwili wakiwa kwenye makazi mapya watakayo jengewa na kila kaya kusomesha mtoto mmoja kwenye vyuo vya veta na wakihitimu wataajiriwa na mgodi ili waweze kupata kipato cha kusaidia na kuendeleza kaya zao.

Pamoja na hayo, mwekezaji huyo amemweleza mwenyekiti wa tume kuwa tayari wameshakubaliana kujengaa kituo cha afya, matundu ya vyoo kwa baadhi ya shule, kujenga shule na ukarabati wa vyumba vya madarasa katika shule mbalimbali. Hata hivyo hakusita kuonyesha kusikitishwa kwake na watu wachache wanaogoma kuondoka kupisha shuguli za uchimbaji huku kila kitu ikiwemo mtaji wa shuguli hizo ukiwa tayari.

Katika mgogoro huo, kaya 347 zinatakiwa kuondoka kupisha mwekezaji huyo na kati ya hizo kaya 62 ndio zinazo goma kuondoka ili mwekezaji aanze kazi ya uchimbaji. Mwenyekiti amesikitishwa na hali hiyo na na kuuomba uongozi wa mkoa na wilaya kuzungumza na kaya hizo sambamba na Baba Askofu aliyeko ndani ya eneo hilo ili mradi huo uanze kwani ni wa muda mrefu na serikali inakosa mapato.

Amesema kwa sasa anaziachia juhudi za serikali ya mkoa na wilaya katika kuupatia ufumbuzi mgogoro huo.

Mapema mwenyekiti alikutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya ambapo amemshukuru kwa ushirikiano anao utoa kwa viongozi na wafanyakazi wa tume ya madini wilaya ya Ulanga.

Amesisitiza suala la uadilifu kwa wafanyakazi wa tume na amesema hilo litakuwa jambo la kwanza kulisema kila aendapo sambamba na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali. Aidha, amesema kipimo kikubwa cha kila mkuu wa kituo cha tume ya madini kitakuwa ni ukusanyaji wa maduhuli ambapo katika Mwaka wa Fedha 2018/2019 tume ilipangiwa kukusanya Bilioni 310 na mwaka wa fedha ujao tume imepangiwa kukusanya Bilioni 467.

Upande wake, Kamishna wa tume hiyo Dkt. Athanas Macheyeki amewakumbusha na kuwasisitiza watumishi wa tume na wachimbaji wa madini kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji na ulipaji wa tozo na stahiki zote za serikali kwa wakati.

Amesema kwa kufanya hivyo raslimali za madini zitakuwa na tija kwa taifa kama anavyo sisitiza Rais John Pombe Magufuli kuwa anataka raslimali za madini ziwanufaishe watanzania wote na namna za kuwanufaisha ni kulipa stahiki za serikali zinazo tokana na madini ili zikatumike kujenga uchumi wa taifa.

Prof. Kikula na Dkt. Macheyeki wanaendelea na ziara yao mkoani Morogoro kukagua shuguli za Tume katika Wilaya mbalimbali ambapo leo walitembelea eneo la wachimbaaji wadogo ipanko wilayani ulanga.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images