Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

TAARIFA KWA UMMA: TANGAZO LA MAFUNZO YA KILIMO NCHINI ISRAEL

$
0
0

28 Machi 2019



UTANGULIZI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inatangaza mafunzo katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini Israel. Mafunzo hayo ni ya miezi 11 kuanzia mwezi Septemba, 2019 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Serikali ya Israel kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mafunzo hayo yatahusisha pia vitendo (field attachment) kwenye mashamba makubwa ya mazao mbali mbali yakiwemo ya matunda, mbogamboga, ufugaji, uvuvi na mazao mengine ya biashara kwa ujira maalum.

SIFA NA VIGEZO VYA MWOMBAJI

      i.     Awe ni raia wa Tanzania mwenye umri wa kati ya miaka 20-35 pamoja na cheti cha            kuzaliwa na Kitambulisho cha Uraia.  
 ii.        Awe amehitimu mafunzo ya Kilimo katika ngazi ya shahada ya Chuo Kikuu,                         Stashahada au Astashahada ya Vyuo vya kilimo vinavyotambulika nchini. 
iii.        Awe na afya njema.  
iv.        Awe na ujuzi wa kuandika na kuongea lugha ya Kiingereza.   
 v.        Awe na uwezo wa kufanya kazi na watu wa tamaduni mbalimbali.  
vi.        Awe tayari kurejea nchini baada ya mafunzo yake.        

                                                                                                                                                
UTARATIBU WA KUFANYA MAOMBI

Maombi yote yatumwe kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yakiwa yameambatishwa na nakala za nyaraka zifuatazo:

     i.               i.    Cheti cha kuzaliwa na uraia.  
   ii.        Vyeti vya kitaaluma.
 iii.        Hati ya Kusafiria au uthibitisho wa maombi ya pasipoti.
  iv.        Cheti cha kuthibitisha afya kutoka hospitali inayotambulika.
    v.        Barua ya kuonesha sababu za kushiriki mafunzo hayo  (Motivation letter) kwa lugha           ya Kiingereza.
  vi.        Wasifu (Curriculum Vitae).
 vii.        Picha mbili ndogo (Passport size).
viii.        Majina na anwani za wadhamini watatu wanaoishi nchini akiwemo mwalimu wa                 Chuo ulichohitimu.

Maombi yote yatumwe kupitia anwani ifuatayo: -

Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Jengo la LAPF
Ghorofa ya 6,
Barabara ya Makole,
S.L.P   2933,
DODOMA.

Au kwa baruapepe; mafunzo.israel@nje.go.tz

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 12 Aprili, 2019

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.


NAFASI ZA AJIRA KATIKA SEKRETARIETI YA JUMUIYA YA MADOLA, LONDON, UINGEREZA.

$
0
0


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, inawahimiza Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za ajira katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola, London, Uingereza.

Ajira hizo ni kama ifuatavyo:-

1.           Mshauri wa masuala ya Miundombinu na Usanifu wa Majengo        (Advisor Infrustructure and Architecture);
2.           Mkurugenzi wa masuala ya Uchumi, Vijana na Maendeleo      Endelevu (Senior Director, Economic, Youth and Sustainable         Development) na
3.           Mshauri  na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Ushindani (Advisor and Head,   Trade and Competitiveness section).

Watanzania wenye sifa wanahamasishwa kuomba nafasi hizo hasa ikizingatiwa kuwa, nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola ambazo hazina watumishi wengi katika ngazi ya maafisa waandamzi watapewa  kipaumbele ili kuimarisha uwiano wa kikanda katika nafasi hizo za ajira.
Kwa kuzingatia sera ya Jumuiya ya Madola ya usawa wa kijinsia, Sekretarieti ya taasisi  inawahimiza wanawake wengi zaidi wenye vigezo kuomba nafasi hizo.
Taarifa zote muhimu kuhusu fursa hizo za ajira zinapatikana kwa kupitia tovuti http://thecommonwealth.org.jobs.
Mwisho wa kutuma maombi kwa nafasi hizo ni tarehe 10 Aprili, 2019; tarehe 16 Aprili, 2019 na tarehe 17 Aprili, 2019, mtawalia.

 Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma
28 Machi, 2019.

Balozi Seif Ali Iddi akutana na Waziri wa Kilimo na Rais wa Bunge la Cuba, ahudhuria maonesho ya kilimo nchini humo

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, amekutana na kufanya mkutano na Naibu Waziri wa Kilimo wa Cuba, Mhe. Guastavo Rodriguez Roller. Mkutano huo ulijikita katika kuwajengea uwezo wakulima kwenye mazao ya kimkakati, ikiwemo kilimo cha pamba, miwa na maembe.


Mkutano ukiendelea kati ya ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na ujumbe wa Cuba ukioongozwa na Mhe. Guastavo Rodriguez Roller.
Mhe. Balozi  Iddi, akimkabidhi Waziri wa Kilimo wa Cuba, Mhe. Guastavo Rodriguez Roller, zawadi ya mlango wa mji Mkongwe ikiashiria ukaribisho wa ushirikiano mpya wa sekta ya kilimo kati ya Tanzania na Cuba.

==================================


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, ameipongeza Serikali ya Cuba kupitia Wizara ya  Kilimo na Mifugo kwa mtazamo wake wa  kuanzisha ushirikiano mpana zaidi baina ya  Zanzibar na Tanzania katika sekta hiyo muhimu.

Akizungumza na Waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Guastavo Rodriguez Roller, katika makao makuu ya wizara hiyo mjini Havana, Balozi Seif  alieleza kuwa, Zanzibar na Cuba zimekuwa na ushirikiano ya karibu katika sekta za afya na elimu kwa kipindi kirefu sasa suala ambalo limeleta mafanikio makubwa.

Balozi Seif alibainisha kuwa, kwa kuwa maonyesho ni moja ya njia ya kubadilishana mawazo kitaaluma alimuomba Waziri wa Kilimo wa Cuba kutenga muda wa kushiriki katika Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Tanzania yanayofanyika  mwezi  Agosti wa kila mwaka nchini.

Kwa upande wake,  Mhe. Roller alibainisha kwamba, Cuba imebarikiwa kuwa na hekta milioni 10,000,000 ambazo zinatoa ajira kwa wakulima zaidi ya  5,000.Alifafanua kuwa, asilimia 70% ya ardhi hiyo ina maliasili, asilimia 3.5 inatumika kufuga na zaidi ya asilimia 60 inatumika katika uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na kilimo pekee.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Rais wa Bunge la Cuba, Mhe. Esteban Lazo Harnandez, mjini Havana, Cuba.
Mhe. Harnandez kulia akipokea zawadi ya mlango wa mji Mkongwe kutoka kwa Balozi Seif kama ishara ya kufunguliwa milango ya kuitembelea Zanzibar.

 Mhe. Harnandez akimtembeza Mhe. Balozi Iddi katika sehemu mbalimbali za jengo la Bunge ya Cuba lenye historia ya muda mrefu ambazo zimewekwa kama kumbukumbu ya taifa hilo.
Mhe. Balozi  Iddi wa pili kutoka kulia na ujumbe wake akifanya mazungumzo na uongozi wa Wizara ya Afya mjini Havana, Cuba.

=====================================


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amelitembelea Bunge la Cuba na kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa bunge la nchi hiyo, Mhe. Esteban Lazo Harnandez.  
Katika mazungumzo baina ya viongozi hao wawili, Mhe. Harnandez ameahidi kuwa, Cuba itaendelea kudumisha ushirikiano wake wa kidiplomasia na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kuendeleza wananchi wake licha ya taifa hilo la Caribean kupita katika mabadiliko ya kisiasa, uchumi na utamaduni. 
Mhe. Harnandez alieleza kuwa, kutokana na mabadiliko yaliyopo sasa katika mfumo wa dunia  katika masuala ya uchumi, siasa na utamaduni Jamhuri ya Cuba imelazimika kufanya mabadiliko ya katiba yake ili yalingane na mfumo huo wa dunia inayoizunguka.
Alifafanua kuwa, tayari Bunge la Cuba limeshafanya marekebisho katika katiba yake kutoa nafasi kwa wananchi wake kuwa na uwezo na uhuru wa kumiliki nyumba, ardhi pamoja na uwepo wa waziri mkuu atakayekuwa na mamlaka ya kusimamia utendaji wa serikali.
Mhe. Harnandez alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, kwamba katika vikao vya bunge hilo vinavyotarajiwa kuanza wiki ijayo baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa wabunge, serikali ya nchi hiyo itakuwa imepiga hatua kubwa zaidi ya maendeleo kutokana na mabadiliko hayo.
Rais huyo wa Bunge la Cuba alisisitiza kwamba taasisi za kifedha zitalazimika kuzingatia ukusanyaji bora zaidi wa mapato katika maeneo yote ya uchumi ili kuimarisha ushiriki wa wananchi waliowengi katika mfumo huo.
Mhe. Harnandez alihitimisha kwa kumuhakikishia Balozi Seif kwamba,  uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya pande hizo mbili utaendelea kuimarishwa na kukuzwa katika muda wote.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Iddi alimpongeza Mhe. Harnandez kwa kuchaguliwa tena kuliongoza bunge hilo na kueleza kuwa, hatua hiyo inaonesha wazi ishara halisi ya kukubalika vyema na wananchi wa nchi hiyo kupitia viongozi wake.
Halikadhalika, Mhe. Balozi Iddi alieleza kuwa, kwa ujumla Zanzibar itaendelea kufuatilia mabadiliko ya Cuba na kuangalia endapo inaweza kuiga mabadiliko hayo ili kuimarisha uchumi na ustawi wa wananchi walio wengi.
Mhe. Balozi Iddi na ujumbe wake ulihitimisha ziara yake  nchini humo kwa kufanya mazungumzo na uongozi wa Wizara ya Afya ya Cuba uliokuwa ukiongozwa na Naibu Waziri, Mhe. Bibi Marcia Cobas,  katika makao makuu ya wizara hiyo yaliyopo Havana, Cuba.
Katika mazungumzo hayo ya ushirikiano wa kindugu, Balozi Iddi alisema matunda ya darasa la madaktari wazalendo waliosimamiwa na wataalamu pamoja na wahadhiri wa nchi ya Cuba yameanza kutoa matumaini.Alifafanua kuwa, kitendo cha Serikali ya Cuba kukubali kupunguza gharama kubwa ya kuwaendeleza madaktari hao wazalendo wapatao 15 katika shahada ya juu ya udaktari wa uzamili nchini humo kinaendelea kuleta faraja kubwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na watu wake.
Alisema wakati Zanzibar ikiendelea kutekeleza sera ya afya ya kuwa na miuondombinu ya huduma za afya katika umbali usiozidi kilomita tano kundi hilo na madaktari linaloendelea kuongezeka kila mwaka litakuwa mkombozi wa utekelezaji wa sera hiyo muhimu.
Naye Kaibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Bibi Asha Ali Abdullah, aliueleza uongozi huo wa Wizara ya Afya Cuba kwamba, hivi sasa Zanzibar  inapita katika kipindi cha kujiimarisha kwenye mapambano yake dhidi ya maradhi yasiyoambukiza.
Bibi Abdullah alisema maradhi yasiyoambukiza kama Kisukari pamoja na Shindikizo la Damu hivi sasa yamekuwa yakiathiri wananchi walio wengi na kuleta vifo vingi. Hata hivyo, jitihada zinachukuliwa ili kupunguza kasi  ya athari za maradhi hayo na kuimaliza kabisa kadhia hiyo kabisa.
Alibainisha kuwa, maradhi ya Malaria hivi  sasa yamepungua kutokana na kampeni kubwa iliyofanywa na serikali kwa kushirikiana na taasisi na mataifa wahisani katika kuangamiza vilui lui vya maradhi hayo.
Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Afya Zanzibar alimuhakikishia Naibu Waziri wa Afya wa Cuba kwamba ushauri wote walioupata katika ziara yao kwenye taasisi za Afya nchini Cuba likiwemo suala la upatikanaji wa dawa litazingatiwa na iwapo linaweza kuleta afueni ya gharama kwa Zanzibar litachukuliwa hatua mara moja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi,  na Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Dkt. Makame Ali Ussi, wakikaribishwa na Naibu Waziri wa Kilimo wa Cuba Mhe. Jose Miguel Rodriquez De Armas, kwenye Maonesho ya Kimataifa ya 22 ya Kilimo yaliyofanyika jijini Havana, Cuba.  Mhe. Balozi Seif Ali Iddi alialikwa kama mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo yaliyofanyika mnamo tarehe18 Machi, 2019. Maonesho hayo yalihudhuriwa na wananchi zaidi ya  3000. 

Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, akitizama kikundi cha wakulima waliokuwa wameandaliwa kutoa burudani kwenye maonyesho hayo.
Burudani zikiendelea kutolewa na vikundi mbalimbali vya wakulima.

Naibu Waziri wa Kilimo wa Cuba Mhe. Jose Miguel Rodriquez De Armas, akihutubia kwenye ufunguzi wa maonyesho hayo.
Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, akitembelea na kujionea mazao mbalimbali yanayolimwa nchini Cuba kwenye mabanda ya makampuni mbalimbali ya wafanyabiashara na yawakulima.

Posted: 28 Mar 2019 05:48 AM PDT
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, amekutana na kufanya mkutano na Naibu Waziri wa Kilimo wa Cuba, Mhe. Guastavo Rodriguez Roller. Mkutano huo ulijikita katika kuwajengea uwezo wakulima kwenye mazao ya kimkakati, ikiwemo kilimo cha pamba, miwa na maembe.

Mkutano ukiendelea kati ya ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na ujumbe wa Cuba ukioongozwa na Mhe. Guastavo Rodriguez Roller.
Mhe. Balozi  Iddi, akimkabidhi Waziri wa Kilimo wa Cuba, Mhe. Guastavo Rodriguez Roller, zawadi ya mlango wa mji Mkongwe ikiashiria ukaribisho wa ushirikiano mpya wa sekta ya kilimo kati ya Tanzania na Cuba.

==================================

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, ameipongeza Serikali ya Cuba kupitia Wizara ya  Kilimo na Mifugo kwa mtazamo wake wa  kuanzisha ushirikiano mpana zaidi baina ya  Zanzibar na Tanzania katika sekta hiyo muhimu.

Akizungumza na Waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Guastavo Rodriguez Roller, katika makao makuu ya wizara hiyo mjini Havana, Balozi Seif  alieleza kuwa, Zanzibar na Cuba zimekuwa na ushirikiano ya karibu katika sekta za afya na elimu kwa kipindi kirefu sasa suala ambalo limeleta mafanikio makubwa.

Balozi Seif alibainisha kuwa, kwa kuwa maonyesho ni moja ya njia ya kubadilishana mawazo kitaaluma alimuomba Waziri wa Kilimo wa Cuba kutenga muda wa kushiriki katika Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Tanzania yanayofanyika  mwezi  Agosti wa kila mwaka nchini.

Kwa upande wake,  Mhe. Roller alibainisha kwamba, Cuba imebarikiwa kuwa na hekta milioni 10,000,000 ambazo zinatoa ajira kwa wakulima zaidi ya  5,000.Alifafanua kuwa, asilimia 70% ya ardhi hiyo ina maliasili, asilimia 3.5 inatumika kufuga na zaidi ya asilimia 60 inatumika katika uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na kilimo pekee.

Sekretarieti ya Baraza La Usalama wa Taifa Limeutembelea MRADI WA SGR, Yaridhishwa na kasi ya Ujenzi

RAIS MAGUFULI AMWAPISHA KAMISHNA MLOWOLA KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI CUBA, APOKEA RIPOTI YA UTENDAJI YA TAKUKURU

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Valentino Longino Mlowola kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi Machi 28, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi baada ya kumuapisha Kamishna Valentino Longino Mlowola kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi Machi 28, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna Diwani Athumani na akiwa na Naibu wake Brigedia Jenerali John Mbungo pamoja na  Kamishna Valentino Longino Mlowola  baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kupokea Ripoti ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi Machi 28, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna Diwani Athumani Ripoti ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi Machi 28, 2019. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya  kupokea vitabu vya Ripoti ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam  Alhamisi Machi 28, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza baada ya kumuapisha Kamishna Valentino Longino Mlowola kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi Machi 28, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kumuapisha Kamishna Valentino Longino Mlowola kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kupokea Ripoti ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam  Alhamisi Machi 28, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna Diwani Athumani na Naibu wake Brigedia Jenerali John baada ya kumuapisha Kamishna Valentino Longino Mlowola kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kupokea Ripoti ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi Machi 28, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Kamishna Valentino Longino Mlowola baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kupokea Ripoti ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi Machi 28, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya kumbukumbu na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna Diwani Athumani na Naibu wake Brigedia Jenerali John Mbungo pamoja na  Kamishna Valentino Longino Mlowola  baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kupokea Ripoti ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU pamoja na Makamanda wa Mikoa Yote na Maafisa Waandamizi wa TAKUKURU kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi Machi 28, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna Diwani Athumani na Naibu wake Brigedia Jenerali John Mbungo pamoja na  Kamishna Valentino Longino Mlowola  baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kupokea Ripoti ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi Machi 28, 2019.
PICHA NA IKULU 

RC MGHWILA ATEMBELEA KAMBI YA TIMU YA NEW GENERATION MPWAPWA DODOMA .

$
0
0
Anaandika Dixon Busagaga.
MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira ametembelea kambi ya mabingwa wa soka mkoa wa Kilimanjaro,timu ya New Generation na kuanikiza ushindi katika mchezo wao wa Kwanza wa Ligi ya mabingwa wa mkoa utakaopigwa leo katika uwanja wa Mgambo ,Mpwapwa mkoani Dodoma.

Dkt. Mgwira amefika katika kambi ya timu hiyo akiwa na wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya ya Mwanga,Moshi DC,Siha na Manispaa ya Moshi na kutoa motisha ya fedha kwa wachezaji .

Wakurugenzi walioambatana na Dkt Mghwira ni pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi,Michael Mwandezi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi ,Castory Msigala, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mwanga,Zefrin Lubuva na Valerian Juwal, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Siha.

Katika mazungumzo yake na wachezaji wa New Generation,Mkuu wa Mkoa Dkt Mghwira aliwataka kuhakikisha wanashinda michezo yao katika kituo hicho ili kuwapa nguvu wadau ya kuendelea kuisadia timu hiyo huku akitoa wito watu mbalimbali kujitokeza kusaidia timu hiyo.

Timu ya New Generation FC  Leo inacheza m hezo wake wa Kwanza  dhidi ya timu ya Timberland kutoka mkoani Lindi. Kwa upande wake ,Meneja wa timu Laurant kinabo ameshukuru ujio wa ugeni huo kufika Mpwapwa kuwatia moyo  wachezaji huku wakiaahidi kufanya vyema katika michezo yao yote ili kuibeba heshima ya mkoa wa Kilimanjaro.






Introducing "TUNAFANANA" by JohVenturetz.com

NEWS ALERT: TAKUKURU KUMFIKISHA MAHAKAMANI MKURUGENZI WAKE WA MIPANGO, UFUATILIAJI NA TATHMINI KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI NA KUJIPATIA FEDHA

$
0
0

*Ni yule aliyezungumzwa na Rais Magufuli jana 
Ikulu kuwa amechukua fedha za wenzake bilioni 1.4 

*Aliwaambia anavyoviwanja...wakampa fedha 
akawaliza na kisha kuanza kuwazugusha 

 Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imetangaza kuwa itamfikisha  Mahakamani leo Mkurugenzi wa Mipango ,Ufuatiliaji na Tathimini wa taasisi hiyo Kulthum Ahmed Mansoor kwa kosa la kughushi na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu Sh.Bilioni 1.6.

Inaelezwa kuwa Kulthum anadaiwa kughushi nyaraka mbalimbali na kujipatia fedha taslimu Sh.bilioni 1.4 kutoka kwa watumishi wa TAKUKURU kwa ahadi  ya kuwauzia viwanja vilivyoko katika eneo alilodai alikuwa analimiki kihalali huko maeneo ya Nzole -Ukuni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Machi 29,2019 jijini Dar es Salaam Naibu Mkurugenzi a TAKUKURU Brigedia Generali John Mbungo amesema mtumishi huo alijiunga na taasisi hiyo kama Mkurugenzi wa Mipango,Ufuatiliaji na Tathmini Oktoba 2009 akiwa amehamishiwa kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria.

Kuhusu tuhuma zinazomkabili Naibu Mkurugenzi wa TAKUKURU amesema mwaka 2012 mtuhumiwa huyo akiwa mwajiri wa taasisi hiyo kwa cheo chake aliwajulisha watumishi wa wenzake kwamba analo eneo kubwa la ardhi analolimiliki kihalali katika eneo la Bagamoyo na anataka kuwauzia viwanja watumishi kwa utaratibu wa kulipa fedha taslimu au kidogo kidogo.

Amesema viwanja hivyo ambavyo vilikuwa vya ukubwa tofauti vilikuwa vikiuzwa kwa thamani ya kati ya Sh.5000,000 na Sh.7000,000 kwa mtumishi binafsi kwa utaratibu wa kulipia fedha kidogokidogo au zote.

"Watumishu walikubali na utaratibu huo na walijiorodhesha kununua viwanja hivyo, wao pamoja na ndugu zao na kumlipa Kulthum fedha taslimu au kwa awamu kwa utaratibu waliokubaliana.

" Baada ya makubaliano hayo watumishi waliokamilisha malipo yao walianza kuona dalili za kudanganywa baada ya kutokabidhiwa hati ya kiwanja wala nyaraka yoyote inayoonesha umiliki halali wa kiwanja alichonunua na walipomuuliza alisema viwanja hivyo vina mgogoro anvao uko mahakamani,"amesema.

Ameongeza baada ya kupokea malalamiko ya watumishi dhidi ya Kulthum uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU pamoja na mambo mengine umebaini viwanja vilivyoahidiwa kuuzwa vilikuwa ni zaidi ya 300, fedha alizokwishachukua mtuhumiwa kutoka kwa watumishi kulipia viwanja hivyo zaidi ya Sh.bilioni 1.4

Uchunguzi pia umebaini mtuhumiwa alijipatia fedha nyingine zaidi ya Sh.milioni 200 ambazo alilipwa na watumishi kama gharama kwa ajili ya kulipia hati na nyaraka nyingine za umiliki."Uchunguzi umebaini fedha hizo hazikuwahi kuwasilishwa wizara ya ardhi.Viwanja vilivyokuwa vikizungumzwa kama vinauzwa uchunguzi umebaini Kulthum hakuwa na umiliki wowote zaidi ya kuwa na nyaraka za kughushi.
yafuatayo chunguzi."

Kutokana na uchunguzi huo TAKUKURU iliamua kuchukua hatua ya kumsimamisha kazi mtuhumiwa tangu Machi 8,2018 na kwamba tasisi hiyo inatarajia kumfikisha mahakamani leo kwa makosa ya kughushi ,kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu pamoja na utakatishaji fedha.

NAIBU WAZIRI NISHATI AWAONYA WAKANDARASI WA MIRADI YA UMEME VIJIJINI

$
0
0
Na Veronica Simba – Lushoto
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewaonya wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini kuzingatia masharti yaliyowekwa na serikali hususani kutumia vifaa vya ndani ya nchi, na kwamba atakayeona hawezi kutekeleza masharti hayo, arudishe kazi hiyo kwa Serikali ili apewe mkandarasi mwingine.
Alitoa onyo hilo jana, Machi 28, 2019 katika kijiji cha Ngazi, wilayani Lushoto, Mkoa wa Tanga, wakati akizungumza na wananchi, kabla ya kuwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.
“Kwanini muagize vifaa kama nguzo nje ya nchi wakati sisi bado miti tunayo na mingine imepandwa kwa makusudio hayo?”
Alisisitiza kwamba wakandarasi wanaochelewesha kazi kwa visingizio vya namna hiyo waache mara moja kwani sababu hizo hazina mashiko.
Naibu Waziri alilazimika kutoa onyo hilo kufuatia kazi duni ya mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza (REA III – I) wilayani Lushoto, ambao ni muunganiko wa kampuni za Njarita, Aguila na Radi.
Alipohojiwa kuhusu suala hilo, Mkandarasi husika alitoa utetezi kwamba mojawapo ya sababu zilizofanya acheleweshe kazi ni agizo la serikali linalowataka wakandarasi kutoagiza vifaa nje ya nchi, badala yake watumie vifaa vya ndani ya nchi.
Akijibu utetezi wa mkandarasi husika, Naibu Waziri alimtaka kujitathmini kuona kama anakidhi vigezo kwani wenzake wanaotekeleza miradi ya aina hiyo sehemu mbalimbali za nchi wanafanya vizuri.
“Tumewasha vijiji zaidi ya 1,900 katika Mradi wa REA III na karibu kila Mkoa na Wilaya, vijiji vimewashwa. Wewe uliomba kazi hii na unashindwa. Inakuwaje wenzako wanaweza?
Akifafanua zaidi, Naibu Waziri alisema kuwa kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais John Magufuli, matarajio ni kuwa, ifikapo Juni 2021, vijiji vyote vilivyokuwa havina umeme tangu serikali husika iingie madarakani, ambavyo vilikuwa takribani 7,873; viwe vimepata umeme.
Alisema, wakati mwingine baadhi ya wakandarasi wanarudisha nyuma jitihada hizo ndiyo maana Serikali ikaunda kamati mbalimbali za usimamizi. Aliwataja wasimamizi wa miradi ya REA kuwa wanatoka ngazi ya Wizara, REA, Meneja Tathmini wa Mkoa, mafundi mchundo wa Wilaya pamoja na wasimamizi wa Kanda.
“Hata hivyo, mwisho wa siku, msimamizi mkuu ni Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya wakishirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama za maeneo yao,” alibainisha.
Katika hatua nyingine, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ngazi wilayani Lushoto, kabla ya kuwasha rasmi umeme katika kijiji hicho, Naibu Waziri alisisitiza kuwa gharama ya kuunganishiwa umeme kwa wananchi wa vijijini ni shilingi 27,000 tu.
Aidha, alitoa rai kwa walimu wa Shule ya Sekondari Ngazi iliyopo wilayani humo, ambayo ndiyo aliyoiwashia umeme; kuhakikisha wanautumia umeme waliounganishiwa kuboresha kiwango cha elimu shuleni hapo.
Awali, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini wilayani Lushoto, Meneja wa TANESCO wilayani humo, Mhandisi Kasim Rajabu alimweleza Naibu Waziri kuwa, mradi ulianza kutekelezwa Julai 2018 na mkataba wake ni wa miaka miwili, ambapo hadi sasa umekamilika kwa kiwango cha asilimia 30.
Alisema, mradi unahusisha ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovoti 33, yenye urefu wa kilomita 33.6, usimikaji wa mashine umba 61 na ujenzi wa njia ndogo za umeme zenye jumla ya urefu wa kilomita 112.
Nyingine ni uunganishaji wa wateja wapya wa awali 1,338 ambapo wateja wa matumizi ya kawaida ni 1,300 na wale wa viwanda vidogo vidogo ni 38.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kilemba) akikata utepe kuashiria uwashaji rasmi wa umeme katika kijiji cha Ngazi, wilayani Lushoto, Machi 28, 2019 akiwa katika ziara ya kazi. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, January Lugangika.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ngazi wilayani Lushoto, wakati wa hafla ya kuwasha rasmi umeme kijijini hapo, Machi 28, 2019 akiwa katika ziara ya kazi.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kilemba cha njano – katikati) pamoja na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Lushoto na wa kijiji cha Ngazi wakishuhudia taa ya umeme inayowaka, baada ya uwashaji rasmi wa umeme katika Shule ya Sekondari Ngazi kijijini humo, Machi 28, 2019. Naibu Waziri aliwasha rasmi umeme kijijini hapo akiwa katika ziara ya kazi.
 Sehemu ya umati wa wanafunzi wa Shule ya Msingi na wa Sekondari Ngazi, wilayani Lushoto, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza katika hafla ya uwashaji rasmi wa umeme kijijini Ngazi, Machi 28, 2019. Naibu Waziri aliwasha umeme katika Shule ya Sekondari Ngazi akiwa katika ziara ya kazi na kuwasisitiza wanafunzi wautumie umeme kuboresha kiwango chao cha elimu.
 Mkazi wa Kijiji cha Ngazi, Wilaya ya Lushoto, Hassan Rajabu, akiwasilisha maoni yake kuhusu umeme vijijini, mbele ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), wakati wa hafla ya uwashaji rasmi wa umeme kijijini hapo, Machi 28, 2019.
 Msimamizi wa Miradi ya Umeme Vijijini, Kanda ya Kaskazini, kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi John Kitonga (wa pili kutoka kushoto) na baadhi ya viongozi na maafisa kutoka TANESCO na REA, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza wakati wa hafla ya uwashaji rasmi umeme katika kijiji cha Ngazi, Wilaya ya Lushoto, Machi 28, 2019.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kilemba cha njano – kulia) akiwa amefuatana na uongozi wa Wilaya, Kijiji, wataalamu kutoka wizarani, REA, TANESCO na wananchi; kwenda kuwasha rasmi umeme katika Shule ya Sekondari Ngazi iliyopo wilayani Lushoto, Machi 28, 2019.

KAMPUNI YA COCA-COLA YAPONGEZWA KWA UBUNIFU KUPITIA MICHEZO YA COPA COCA-COLA

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mheshimiwa Mwita Waitara leo ameshiriki uzinduzi wa semina shirikishi ya maofisa michezo kutoka mikoa 26 nchini katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa hafla Mhe. Mwita Waitara alipongeza uamuzi wa Coca Cola kutambulisha Kampeni ya ‘COPA Coca Cola Kusanya na Ushinde’, ambayo imenuia kutoa hamasa kwa vijana kuyatunza mazingira kwa kuwajibika kukusanya chupa za plastiki mashuleni katika kipindi ambacho michezo ya Copa Coca-Cola UMISSETA itakapokuwa inaendelea kuwa ni muelekeo sahihi.

“Ninafahamu kuwa kwa mwaka huu, lengo la COPA Coca-Cola (UMISSETA) ni kujenga uelewa juu ya umuhimu wa utunzaji mazingira kupitia ukusanyaji wa chupa za plastiki. Ninapenda kuwahakikishia kuwa, nipo tayari kuwaunga mkono ili kufanikisha hamasa hii ya kuhifadhi mazingira ya shule zetu hapa nchini,"alisema.

“Mwaka jana, niliwaombeni muendelee kufadhili mashindano ya UMISSETA na mchukue umiliki wa michezo hii. Ninafarijika kuona ili mmelifanyia kazi kwa wakati. Wakati akizindua michezo ya mwaka 2019 COPA Coca-Cola, Waziri amebainisha kimkoa yataanza Manyara Aprili 5, mwaka huu.

Mhe. Waitara pia alibainisha kuwa, Serikali inatambua mchango mkubwa wa Coca Cola katika kuendeleza vipaji vya vijana. Amesema, Wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha katika kampuni hiyo ya vinywaji. Waitara alitoa wito kwa makampuni mengine na wadau wa michezo kuipa michezo shuleni kipaumbele kama Coca Cola inavyofanya kwa miaka mingi na dhamira ya Serikali ni kuinua michezo shuleni.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma na Mawasiliano wa Coca-Cola Kwanza, Haji Mzee amesema, michezo ni chaguo la vijana wengi na mizizi ya maendeleo ya soka nchini huanzia kwao. Mfumo huu wa Coca-Cola umejikita katika kutoa hamasa ya michezo kwa kuibua vipaji mbalimbali katika michezo.

Ameongeza kuwa, mashindano ya COPA huwa yanawawezesha vijana kuonyesha vipaji vyao katika umri mdogo, pia huwapa fursa ya kuviendeleza vipaji vyao. “Mwaka huu COPA Coca-Cola dhumuni lake ni Kukusanya na Ushinde, mradi uliobuniwa kuhakikisha plastiki zote zinakusanywa katika shule shiriki wakati wa michezo.Kupitia kampeni hii tumelenga wanafunzi wawe wawajibikaji katika jamii kwa kuyahifadhi vema mazingira,"alisema.

Aidha, ameishukuru Serikali na wadau mbalimbali wa michezo kwa kuunga mkono juhudi hizo za Coca Cola. Semina hiyo imehudhuriwa na maofisa michezo wa mikoa yote, walimu wa michezo wa shule za sekondari, Maafisa elimu wa mikoa, Shule za Sekondari na Msingi, Wizara ya habari, Tamaduni, Sanaa na michezo, Maafisa kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI.
1056724
Meneja bidhaa wa Kampuni ya vinywaji Kampuni ya Coca-Cola Pamela Lugenge akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mheshimiwa Mwita Waitara wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Copa Coca-Cola kwa shule za Msingi na Sekondari kwa mwaka huu jijini Dodoma.
1056726
Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma na Mawasiliano-Coca Cola Kwanza akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mwita Waitara katika hafla ya uzinduzi rasmi wa semina elekezi ya mashinadano ya Copa Coca-Cola kwa shule za Msingi na Sekondari Tanzania 2019 jana Jijini Dodoma. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza hivi karibuni.
1056733
Pamela Lugenge akitoa hotuba yake.
1056734
Mheshimiwa Waziri akihutubia wageni waalikwa.

Shabiki wa Simba atetema na Sh84.8 milioni za M-BET

$
0
0

 Shabiki wa timu ya Simba, Chelsea, Juventus na Real Madrid , Semistocles Mkiza (41) ameshinda kiasi cha Sh 84,814,160 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 za ligi mbalimbali katika droo ya Perfect 12 inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet.

Mkiza ambaye ni mkazi wa Muleba Mkoa wa Kagera liibuka kidedea katika droo iliyofanyika Machi 24 na anakuwa mshindi nne kushinda mamilioni ya fedha ya M-Bet tokea kuanza kwa mwaka huu.

Msemaji wa kampuni ya M-Bet, David Malley alisema kampuni yao imedhihirisha kuwa ni nyumba ya mabingwa kutokana na kutoa mamilioninya fedha kwa Watanzania kadhaa na kuweza kubadili maisha yao.

Malley alisema kuwa kwa kuwa kampuni yao inafuata sheria za michezo ya kubahatisha nchini, Mkiza amekatwa Sh16, 962,632 kama kodi ya ushindi na kupelekwa serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Mkiz anaungana na washindi wengine wanne ambapo tokea Januari mwaka huu wameshinda mamilioni ya fedha na kuweza kubadili maisha yao. Tunaomba watanzania wenye umri kuanzia miaka 18, kujiunga na bidhaa zetu mbalimbali za kubahatisha ili kuweza kushinda,” alisema Malley.

Kwa upande wake, Mkiza alisema kuwa amefurahi sana kushinda kiasi hicho cha fedha ambacho atakitumia kwa masuala ya maendeleo.

Alisema kuwa hajaamini alipoambiwa kuwa ameshinda kiasi hicho cha fedha na kusubiri kwa hamu sana siku ya kakabidhiano. Alisema kuwa kushinda zaidi ya Sh milioni 84 kwa kutimia sh1,000 tu ni bahati ya hali ya juu.

“Mimi ni mjasiliamari, sikuwahi kupata kiasi hiki cha fedha pamoja na kubeti mara kadhaa, nitatumia kuhimarisha biashara zangu, kujenga nyuma na vile vile kusomesha watoto wangu,” alisema Mkiza.


Msemaji wa kampuni ya M-Bet, David Malley (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh 84,814,160 mshindi wa droo ya Perfect 12, Semistocles Mkiza (41) kutoka Muleba, mkoa wa Kagera. Mkiza amebashiri kwa usahihi matokeo ya mechi 12 tofauti katika ligi mbalimbali duniani. 

ALIYEKUWA BOSI TAKUKURU AFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA SHILINGI BILIONI 1.4 KWA NJIA YA UDANGANYIFU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Mipango, Ufutuatiliaji na Tathmini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kulthumu Mansoor amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na kesi ya uhujumu ambapo anadaiwa kujipatia zaidi ya sh. bilioni 1.4 kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kujipatia fedha hizo kutoka kwa wafanyakazi wenzake. Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali Wankyo Simon amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Kelvin Mhina kuwa katika tarehe tofauti za Januari 2013 na Mei 2018, mshtakiwa alighushi barua ya ofa ya tarehe 13 Agosti 2003 kwa madhumuni ya kuonesha kuwa, barua hiyo imetolewa na Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo huku akijua kuwa si kweli.

Katika shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu imedaiwa, kati ya Januari 2012 na Mei 2017 huko Upanga ndani ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Saalam mshtakiwa kwa kudanganya alijipatia jumla ya sh. milioni 32.2 kutoka kwa watu sita tofauti tofauti kama malipo ya viwanja tofauti vilivyoko Wilaya ya Bagamoyo katika kijiji cha Ukuni kwa kujifanya kuwa yeye ni mmliki wa kiwanja viwanja hivyo huku akijua kuwa sio kweli.

Mshtakiwa anadaiwa kujipatia fedha hizo kutoka kwa Alex Mavika ( milioni Sh.5.2), Wakati Katondo, (milioni 3), Gogo James, (milioni Sh.5), Ekwabi Majungu, (Sh.milioni 7) John Amos (Sh.milioni 7) na Rose Anatory, (Sh.milioni 5), ambao wote ni wafanyakazi wa taasisi hiyo.

Katika shtaka la mwisho imedaiwa kati ya Januari 2013 na Mei 2018 huko Upanga, mshtakiwa Kulthumu alijipatia fedha Sh.1,477,243,000 wakati akijua kuwa fedha hizo ni haramu na ni zao la kosa Tangulizi la kughushi.

Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina Mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 12, 2019
 ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kulthumu Mansoor akiwa kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam  akikabiliwa na kesi ya uhujumu ambapo anadaiwa kujipatia zaidi ya sh. bilioni 1.4 kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha 
 ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kulthumu Mansoor akifikishwa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na kesi ya uhujumu ambapo anadaiwa kujipatia zaidi ya sh. bilioni 1.4 kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha 

BAMIZA MISIC CHART 30TH MARCH 2019

$
0
0

92.9 Dar & Mtwara, 93.3Dodoma, 98.5Arusha,

 101.7 Mwanza & Tanga, 98.7 Morogoro.

MAGIC FM BAMIZA TOP 20 COUNT DOWN March 30th 2019

SONG

ARTIST

PRODUCER

PEAK/POS

20. Incase you don’t know

Jux ft Nyashinski

Bob MAnecke / Ellipiano

NEW

19. Tetema

Rayvanny Ft Diamond

S2kizzy

NEW

18. Niuwe

Lava Lava

Abidad


17. KAINAMA

Harmonise ft Diamond & Burna Boy

Master Grazy


16. Hazipo

Nandy

Ema the boy


15. Kadogo

Ali Kiba

Abidad

3 WEEKS NO 1.

14. Funga Geti

Billnass ft Roma

Mr T Touchez


13. Noma kweli

Young Dee

Tonny dreezy / Mr T Touchez


12. NI WEWE

Ommy Dimpoz

Yogo Beats


11. Maselebration

Fid Q ft Chin Bees

Mudy/Goncha


10. Wapoloo

Weusi

Ammy Waves


9. Wezele

Rich Mavoko

Abidad


8. Blue

Mr Blue ft Nandy

Producer Mbezi


7. Too late

Linex ft Lady Jay Dee

Triss


6.  Safari

AY & King Kikii

Makochali

2ND  WEEK NO 1.

5. Bambino

Vannesa Mdee ft Reekado Banks

E kelly


4. Mbele kwa mbele

Nay wa Mitego

Gachi B


3. Achia njia

Darassa

Mr vs/Abba


2. Masozy

Kings Music (Cheed ft, K2Ga, Ali Kiba)

Man Water


1. Washa

Barnaba Boy Classic

Abba

2nd  WEEK NO 1.

@magicfmtanzania INSTAGRAM

@magicfmtanzania TWITTER &

@magicfmtanzania FACEBOOK

Mobile App kwenye Playstore tafuta MAGIC FM TANZANIA



MAKAMU WA RAIS AZINDUA JENGO NA MASHINE ZA TIBA ZA LINAC KATIKA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema tatizo la saratani kwa Watanzania linaweza kupungua ama kuondokana nalo endapo kutakuwa na tabia ya kupima afya zetu mara kwa mara.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo kwenye uzinduzi wa jengo na mashine mpya za tiba ya mionzi LINAC ambazo ni za kisasa kabisa na kwa Afrika, Tanzania inakuwa nchi ya kwanza kuwa nazo.

“tunaweza kujikinga kwa kufuata kanuni za afya zinavyotuelekeza kula chakula bora, kufanya mazoezi mara kwa mara, na kuepuka kunywa pombe kupita kiasi na kuepuka matumizi ya tumbaku”alisema Makamu wa Rais.

Mradi wa ununuzi na ufungaji wa mashine mpya za kisasa za tiba ya mionzi umegharamiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo shilingi bilioni 9.5 zimetumika.

Aidha, Serikali itaendelea kuimarisha huduma za saratani hasa huduma za Kinga, Uchunguzi na Matibabu ya awali ikiwemo kuongeza vituo vya upimaji wa dalili za awali za Saratani ya mlango wa kizazi na matiti ambapo jumla ya vituo 650 vinatoa huduma hii kwa wakati.

Makamu wa Rais amewataka  wananchi wote hasa wanawake kufika katika vituo ili kufanyiwa uchunguzi  kwani zikigundulika dalili za awali mgonjwa atatibiwa na kupona.

Pia Makamu wa Rais amesisitiza wanaume waanze kuchukua mwamko wa kupima afya  zao hasa kupima saratani ya tezi dume.

“Nashukuru Wizara kwa kuanzisha kampeni ya upimaji wa virusi vya ukimwi kwa wanaume, kwa kauli mbiu ya Furaha Yangu na ingefaa suala hili liende pia kwa upimaji wa Saratani ya Tezi Dume” alisisitiza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais ameupongeza mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuingiza matibabu ya Saratani katika huduma ambazo wanagharimia“Ningependa kuwaagiza mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuhakikisha wanagharimia huduma hii ya tiba ya mionzi kwa LINAC.”

Wakati huohuo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema katika kipindi kifupi cha miaka mitatu sekta ya Afya imepata mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo  chanjo kwa watoto zimefikia asilimia 98%, upatikanaji wa dawa muhimu ni asilimia 95%, vifaa na vifaa tiba, huduma za mama na mtoto ikiwemo ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya.

“Tumekusudia  kuleta watalii wa matibabu”alisema Waziri Ummy.  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jengo na mashine za tiba ya saratani katika taasisi ya Saratani Ocean Road. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Kijana Rashid Juma Kapungu mwenye umri wa miaka 29, akitoa ushuhuda wa mafanikio baada ya kupata tiba ya mionzi katika Taasisi ya Saratani Ocean Road wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jengo na mashine za tiba ya saratani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jengo na mashine za tiba ya saratani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo na mashine za tiba ya saratani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya mashine ya kisasa ya tiba ya saratani kwa mionzi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Maiselage wakati hafla ya uzinduzi wa Jengo na mashine za tiba ya saratani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Mashine mpya za kisasa za tiba ya saratani za Linac ( Linear Accelerator) ambazo zimezinduliwa leo katika Taasisi ya Saratani Ocean Road. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


DKT. MWANJELWA ATEMBELEA TAGLA, AWAPONGEZA KWA KASI KAZI NZURI

$
0
0
* Awataka kujitangaza zaidi ili wananchi waweze kujua kazi wanazozifanya, azungumza na chuo cha serikali cha nchini Kenya na wafanyakazi wa utumishi jijini Dodoma kupitia daraja video (video conference)

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

NAIBU Waziri ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na utawala bora Dkt. Mary Mwanjelwa ametembelea ofisi za wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao nchini (TaGLA) huku akitoa pongezi kwa wafanyakazi kwa kazi hiyo wanayoifanya ambayo ni tofauti na yenye tija kwa jamii.

Akizungumza mara baada ya kutembelea vitengo vya wakala hiyo Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa kazi zinazofanywa na wakala hiyo zina tija kwa wananchi na Serikali na kuwataka kujitangaza zaidi ili wananchi waelewe majukumu yanayofanywa na wakala hiyo.

Aidha amewataka wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuzidi kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt.John Joseph Magufuli.

Amesema kuwa wizara anayoisamia ipo tayari kushirikiana nao  katika shughuli zao ambazo nyingi zimelenga kuokoa gharama za Serikali.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa wakala hiyo Charles Senkondo amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa wakala hiyo miaka 18 iliyopita wamekuwa na jukwaa la TEHAMA linalohusisha wanajamii mbalimbali.

Senkondo amesema kuwa majukumu ya wakala hiyo ni pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma na sekta binafsi kwa kutumia mifumo ya kiteknolojia ikiwemo video Conference ambayo huwakutanisha watu tofauti kwa wakati mmoja hali inayopelekea kupunguza gharama.

Senkondo amesema kuwa  wakala hiyo pia inatoa huduma za mikutano ya kazi na zile za daraja video, midahalo huduma za maabara ya kompyuta.

Amesema kuwa wamejipanga katika kuhakikisha huduma hiyo inafika katika Mikoa yote nchini na tayari wamewasiliana na wizara ya mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa katika kushirikiana na sekta mbalimbali zikiwemo TANTRADE, TIC na madaktari bingwa katika kuwajengea uwezo.

Aidha amesema kuwa wana malengo ya kutoa mafunzo ya matumizi ya TEHAMA na kuendesha vikao vya kazi kwa watumishi wa umma na taasisi binafsi ili kuwajengea uwezo na kuwafikia wafanyakazi hao kwa muda mfupi na kuokoa gharama.

Vilevile Senkondo amesema kuwa wamefanya midahalo mingi na nchi nyingine  zikiwemo Korea kusini na kenya na kujadili masuala mbalimbali ya kijamii kama vile mabadiliko ya hali ya hewa na ukuaji wa miji kupitia mfumo wa daraja video huku akimpongeza Naibu waziri wa Viwanda na biashara Mhandisi Stella Manyanya kuwa balozi bora wa wakala hiyo.
Mkurugenzi mkuu wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao nchini Charles Senkondo akieleza majukumu ya wakala hiyo mbele wa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa mara baada ya kukagua utendaji kazi unaofanywa na wakala hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza na watumishi mara baada ya Mkurugenzi mkuu wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao nchini Charles Senkondo kuwasilisha majukumu ya wakala hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Meneja mafunzo na habari kutoka wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao TaGLA Dickson Mwanyika akitoa mwongozo katika warsha hiyo iliyofanyika katika ofisi za wakala hiyo, leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza na watumishi wa ofisi yake jijini Dodoma leo alipotembelea ofisi za TaGla leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao TaGLA  wakiwa kwenye mkutano na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa alipotembelea ofisihizo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza na wafanyakazi wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao TaGLA mara baada ya kukagua utendaji kazi unaofanywa na wakala hiyo huku akieleza kufurahishwa na utendaji kazi wao, leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Mkurugenzi mkuu wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao nchini Charles Senkondo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa akionesha zawadi aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa wakala hiyo Charles Senkondo, leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa katika picha  ya pamoja na wafanyakazi wa TaGLA leo jijini Dar es Salaam.


NAMNA VYAKULA VILIVYOMPELEKEA MARTIN KUWA NA UZITO WA KILO 980

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
KEITH Martin raia wa Uingereza ni moja kati ya watu ambao wameweka historia ya kuwa na uzito usio wa kawaida na unene uliopitiliza.

Martini akiwa na miaka 42 alikuwa na kilo zisizopungua 980 na hakuweza kujigeuza alipolala alihudumiwa na watu wa fani tofautitofauti zaidi ya 7 wakiwemo manesi na watu waliomsaidia usafi.

Akizungumza na jarida la North Sky huko nyumbani kwake Kaskazini mwa Uingereza Martin alieleza kuwa, "Najilaumu mwenyewe, siwezi kumlaumu yeyote ni kosa langu nilikuwa nakula mwenyewe, hakuna aliyeniwekea bunduki kichwani nilifanya mwenyewe" alieleza Martin.

Vyanzo vinaeleza kuwa Martin alifiwa na mama yake akiwa na miaka 16 tu baada ya hapo akaanza kula vyakula vya mafuta na sukari (junk food) kwa lengo la kujifariji hali iliyompelekea kuwa na uzito na unene uliopitiliza.

Hata hivyo Martin alifariki dunia mwaka 2014 akiwa na miaka 44 huku chanzo cha kifo chake kikielezwa kilitokana na tatizo la pumu.

Wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2018 ruksa kubadilisha Tahsusi(Combination)

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Serikali imetoa fursa kwa wanafunzi waliofaulu kidato cha nne mwaka 2018 na wanaotegemea kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo kwa mwaka 2019 kubadilisha Tahsusi(Combination).
Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo Serikali ya Awamu ya Tano inawapa wahitimu hao fursa ya kufanya mabadiliko ya machaguo ya Tahasusi (Combination) na kozi mbalimbali walizozichagua kwenye fomu ya “F4-Selform.
Amesema Fursa hii itawawezesha wanafunzi kurekebisha machaguo yao kulingana na ufaulu waliopata kwenye matokeo ya Kidato cha Nne 2018 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania, NECTA.

“Kwa mara ya kwanza Wanafunzi watakuwa na uwezo wa kubadili machaguo au kuchagua kutoka Kidato cha Tano kwenda Chuo au Chuo kwenda Kidato cha Tano kwa kadiri ya mahitaji yake na jinsi alivyofaulu mitihani yake” alisema Jafo.
Unajua wanafunzi hujaza Fomu za F4-Selform kabla ya kufanya mitihani sasa matokeo huweza kuja tofauti na vile alivyojaza lakini mwanafunzi huyo amefaulu hivyo ni wakati sasa kwa kubadilisha machaguo kwa kadiri ya ufaulu wake na anavyopendelea mwenyewe alisisitiza Jafo.

Aidha Waziri aliongeza kuwa Ofisi yangu imetoa fursa hii kwa wahitimu kubadili machaguo yao ili kutoa mwanya zaidi kwa mwanafunzi kusoma fani au Tahasusi itakayomwandaa kuwa na mtaalam fulani katika maisha yake ya baadaye kwa namna ambayo anatamani yeye mwenyewe au kwa kushauriwa na wazazi au walezi wake; Hii ni kutokana na ukweli kwamba baadhi ya wanafunzi hawakujaza kwa uhakika Tahasusi au Kozi zao kutokana na kutokuwa na uhakika wa ufaulu katika masomo yao.

Aliongeza kuwa zoezi la awali la kuingiza taarifa zilizo kwenye “Selform” za wanafunzi kwenye kanzidata ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI, kama zilivyojazwa wakiwa shuleni kabla ya kuhitimu limekamilika na sasa wanafunzi wataweza kufanya mabadiliko kwa njia ya mtandao, (online) na baada ya wanafunzi kufanya marekebisho yao, kanzidata hii ndiyo itakayotumika kuwachagua na kuwapangia kidato cha Tano na Kozi za Vyuo. 

Waziri Jafo aliwakumbusha wahitimu wote  kuwa, endapo wanapenda kurekebisha machaguo ya Tahasusi na Kozi au kuhama kutoka Chuo kwenda Kidato cha Tano kulingana na ufaulu wao katika masomo wanatakiwa kuingia kwenye mfumo wa Selform unaopatikana katika anuani ya www.selform.tamisemi.go.tz na   maelekezo ya jinsi ya kufanya mabadiliko watayapata kwenye video ya mafunzo  inayopatikana kwenye tovuti ya TAMISEMI www.tamisemi.go.tz.

Pia alifafanua kuwa Ili mhitimu aweze kuingia kwenye mfumo itabidi kutumia namba ya mtihani wa kuhitimu Kidato cha Nne mwaka 2018, jina lake la mwisho, mwaka wa kuzaliwa na alama ya ufaulu aliyopata kwenye somo atakaloulizwa na mfumo au swali lolote atakaloulizwa.  
Zoezi hili la kubadilisha Tahasusi litafanyika kuanzia tarehe 01/04/2019 hadi tarehe 15/04/2019.

UTOAJI WA ELIMU BORA NI KIPAUMBELE CHA NCHI-MAJALIWA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema utoaji wa elimu bora kwa Watanzania ni moja ya vipaumbele vya nchi katika kuleta maendeleo na kufikia malengo ya Milenia 2025, Elimu kwa wote (EFA) na Mkakati wa Kupambana na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA). 

Amesema ili kuweza kufanikisha malengo hayo wanahitaji sekta hiyo kuwa bora, imara, inayokidhi mahitaji ya jamii kwa kuwapa vijana maarifa na ujuzi wa kukabiliana na matatizo ya kijamii, kitaifa na kimataifa.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 29, 2019) wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Parokia ya Ikwiriri, mkoani Pwani. Ameipongeza Parokia hiyo kwa kubuni mradi wa ujenzi wa shule.

Amesema sekta ya elimu ni wakala wa mabadiliko katika jamii kiuchumi, kiteknolojia na kiutamaduni katika kuleta maendeleo ya nchi na wadau muhimu wa sekta hiyo ni pamoja na Serikali, washirika wa maendeleo, mashirika ya kiraia na ya kidini, sekta binafsi na jamii kwa ujumla. 

Waziri Mkuu amesema kuwa wadau wote hao wamekuwa wakichangia kwa njia mbalimbali katika kuboresha utendaji wa sekta hiyo na kusababisha Serikali kupata mafanikio makubwa sana katika upatikanaji wa huduma za Jamii zikiwemo za elimu, afya na maji. 

”Hivi sasa kila Kijiji nchini kina shule ya msingi na ongezeko limefikia idadi ya shule 17,659 zikiwemo zilizo chini ya Kanisa katoliki 204. Pia tumeweza kujenga shule za sekondari katika kila kata ambapo ongezeko limefikia shule za sekondari 4,883 nchi nzima zikiwemo zilizo chini ya kanisa katoliki 266”. 

Waziri Mkuu amesema idadi hiyo ya shule imesaidia kutoa fursa kwa wanafunzi wengi kupata elimu nchini katika ngazi mbalimbali.  ”Hivi sasa kwa kuzingatia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2015/2010 tunatekeleza mpango wa elimu bila ada kwa kutoa sh. Bilioni 24.4 kila mwezi”.

Amesema lengo la Serikali la kutoa kiasi hicho cha fedha kila mwezi ni kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anapata fursa bila vikwazo na  Wilaya ya Rufiji nayo inanufaika, ambapo imetengewa kiasi cha milioni 394.5 kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Lengo la Serikali kutoa Elimumsingi Bila Ada ni kuleta ujumuishi kwa kuhakikisha watoto wote hususan wale ambao wanatoka katika familia zisizo na uwezo wanapata haki ya msingi ya kupata elimu. 

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kuongezeka kwa ufaulu wa darasa la saba kumeleta changamoto ya uwepo wa miundombinu ya shule za sekondari hususan kwa kidato cha kwanza ambayo ni kielelezo cha mafanikio ya utekelezaji wa sera ya Elimumsingi Bila Ada. 

Awali, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengoalitumia fursa hiyo kuishikuru Serikalikwa kurejesha hali ya usalama na utulivu katika eneo la Rufiji na Kibiti.


Kardinali Pengoalisema kurejea kwa hali ya utulivu na usalama katika maeneo hayo kumemuondolea mzigo wa kiutendaji uliokuwa ukimuumiza kwa kuwa mapadri aliokuwa akiwapangia katika parokia za huko walikuwa wakisema ‘tumekosa nini’.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Askofu wa Jimbo la Ifakara, Salutaris Libena wakiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019. Wa pili kulia ni Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Fancis wa Asiz Ikwiriri, Padre Disma Kimboi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza wakati alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri  mkoani Pwani, Machi 29, 2019.  Wengine kutoka kulia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu wa Jimbo la Ifakara, Salutaris Libena na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Francis wa Asiz Ikwiriri, Padre Dismas Kimboi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya wasichana ya  Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa ambaye alipewa nafasi ya kusalimia wakati Waziri Mkuu alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri Mkoani Pwani Rufiji, Machi 29, 2019.  Kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na wa nne kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani na  Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na Askofu wa Jimbo la Ifakra,  Salutarisi Libena baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019. Katikati ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wananchi  baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri Mkoani Pwani, Machi 29, 2019. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)

KATIBU WA BUNGE AKUTANA NA WABUNGE WA PAP

$
0
0
 Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai akimsikiliza Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP)  Stephen Massele aliyemtembelea Ofisi kwake Bungeni Mjini Dodoma.
Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai akimsikiliza Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP) Stephen Massele aliyemtembelea Ofisi kwake Bungeni Mjini Dodoma.  Massele aliongozana na Rais wa Umoja wa Vijana wa Bunge la Afrika Mboni Mhita  pamoja na Mjumbe wa Bunge la Afrika David Silinde. 

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YA NASSARI

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images