Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

DKT. MPANGO AAGIZA KUTOTUMIA FUNGU LA LISHE KWA MATUMIZI MENGINE

$
0
0
Serikali imeziagiza Wizara, Mikoa na Halmashauri zote nchini kutumia fungu lililotengwa kwa ajili ya lishe  kwa matumizi yaliyopangwa  ili kuhakikisha watanzania wanaimarika kiafya na kushiriki kikamilifu katika Shughuli za Maendeleo.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wa Mkutano kati yake na Mwana wa Mfalme wa Jordan ambaye ni balozi wa masuala ya Lishe Dunia, Sarah Zeid na Mwakilishi wa Shirika  la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) nchini Tanzania, Michael Dunford, Jijini Dodoma.
Dkt. Mpango alisema kuwa iwapo eneo la lishe halitasimamiwa kikamilifu Taifa litazalisha watoto wenye udumavu wa ubongo na kusababisha kupungua kwa uwezo wa kufikiri na utendaji hafifu wakiwa katika shughuli mbalimbali.
Alisema ipo mikoa ambayo inazalisha mazao mengi  kama Mbeya na Njombe lakini inaidadi kubwa ya watoto wenye utapimulo, hivyo ni jukumu la kila mtanzania kuhakikisha anaangalia ni chakula gani kinahitajika kwa ajili ya watoto na wakinamama wajawazito ili kupunguza suala la ukosefu wa lishe.
Aidha amempongeza Mwana wa Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid, kwa kupambana na vifo vya wakina mama wajawazito na watoto kote Duniani, kwa kuwa mchango wa wanawake ni mkubwa sana katika Sekta za maendeleo kama Kilimo ikizingatiwa kuwa, kwa upande wa Tanzania wanawake ni takribani asilimia 51 ya watanzania wote hivyo kuwa na umuhimu wa kutunza raslimali hiyo kwa manufaa ya kizazi hiki na kijacho.
Kwa upande wake Mwana wa Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada zake katika kupambana na utapiamlo unaosababishwa na ukosefu wa lishe na amewataka watanzania kuhakikisha suala la Lishe linapewa kipaumbele  na kila mmoja kwa manufaa ya Taifa na Dunia kwa ujumla.
Naye Mwakilishi wa WFP nchini Tanzania Michael Dunford, amesema dhumuni la Mwana wa Mfalme kuitembelea Tanzania ni kujifunza na kuhakikisha WFP inafanya kazi kwa Karibu na Serikali kwa lengo la kuwasaidia wananchi kupata Lishe bora kwa kuwa Shirika hilo lina uwezo na lipo tayari  kutoa misaada hiyo kwa Tanzania. 
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akieleza jitihada za Serikali katika kupambana na utapiamlo ikiwa ni pamoja na  kila Mkoa kuandaa bajeti ya Lishe  wakati wa Mkutano kati yake na Mwana wa Mfalme wa Jordan ambaye ni balozi wa masuala ya Lishe Dunia, Sarah Zeid (hayupo pichani), Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Khatib Kazungu na kulia ni Kamishana msaidizi wa Bajeti wa Wizara hiyo Charles Mwamwaja. 
 Mwana wa Mfalme wa Jordan ambaye ni balozi wa masuala ya Lishe Dunia, Sarah Zeid, akieleza anavyofurahishwa na Serikali ya Tanzania inavyosimamia suala la Lishe, wakati wa Mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani- WFP nchini Tanzania, Michael Dunford.
 Mwakilishi wa Shirika  la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) Michael Dunford, akieleza utayari wa Shirika hilo kuisaidia Tanzania katika masuala ya Lishe, wakati wa Mkutano kati ya Mwana wa Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid (kushoto) na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
 Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia), na Ujumbe wa Shirika  la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP), ukiongozwa na Mwana wa Mfalme wa Jordan ambaye ni balozi wa masuala ya Lishe Dunia, Sarah Zeid (wa pili kulia) katika mkutano kuhusu Lishe uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango  Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akipeana mkono na Mwana wa Mfalme wa Jordan ambaye ni balozi wa masuala ya Lishe Dunia, Sarah Zeid (kushoto), baada ya kumalizika mkutano kuhusu Lishe uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Mwana wa Mfalme wa Jordan ambaye ni balozi wa masuala ya Lishe Dunia, Sarah Zeid (kushoto), wakifurahia jambo katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Tanzania na Shirika la Chakula Duniani- WFP, baada ya kumalizika mkutano kuhusu Lishe uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
(Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango)

PROF KABUDI AKUTANA BARONESS LYNDA CHALKER

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba John Kabudi (kulia) akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Taasisi ya Afrika Matters Limited Lyinda Chalker (kulia) jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi amesema mabadiliko yote ya sheria yaliyofanyika hivi karibuni katika sekta za madini,maliasili na uwekezaji yana lengo la kuweka mazingira bora zaidi yatakayoleta tija kwa Taifa na wawekezaji kutokana na sheria mpya kuondoa utaifishaji (nationalization) na upokonyaji mali (confiscation).

Profesa Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo wakati wa mazungumzo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited Mhe. Lynda Chalker na kuongeza kuwa hatua zilizochukuliwa na serikali ya awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli ni kuweka uwanda sawa kwa kuondoa rushwa na urasimu na kumtaka Mhe Chalker kuhamasisha wawekezaji kutoka Uingereza kuja kuwekeza hapa nchini.

Katika mazungumzo hayo Profesa Palamagamba John Kabudi amemuahakikishia Mwenyekiti huyo wa Taasisi ya Africa Matters limited kuwa mazingira ya uwekezaji nchini ni salama na yameboreshwa zaidi na hakuna masuala ya utaifishaji (nationalisation) wala upokonyaji mali (confiscation) kama inavyopotoshwa na baadhi ya watu wasioitakia mema Tanzania.

“Katika kutekeleza diplomasia ya Uchumi Tanzania inatoa kipaumbele kwa uwekezaji wenye tija kwa Taifa na unaozingatia maslahi ya pande zote (Win – win situation) kwa kuwa sasa kupitia sheria mpya tuna mfumo wa kodi unaofahamika, misamaha ya kodi isiyo na upendeleo na si kweli kuwa mazingira yamebadilika na kusema kweli kilichbadilika ni usimamizi madhubuti,kupambana na rushwa na kuhakikisha kodi stahiki inalipwa”

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited Mhe. Lynda Chalker amempongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kuongeza kuwa atakaporejea Uingereza msafara wa wafanyabiashara na wawekezaji kuja Tanzania na kwamba kuna uwezekano mkubwa wa uwepo wa mabadiliko ya kisiasa nchini Uingereza na marafiki wa Jumuia ya madola kama Tanzania wanapewa kipaumbele katika uwekezaji na ujenzi wa viwanda.

“Ninadhani wawekezaji hasa wa nje ya Tanzania wanahitaji kufanya utafiti kidogo kuhusu kile Tanzania inachokihitaji na namna watakavyonufaika kwa kuwekeza Tanzania,nimuahidi waziri hapa kuwa nitakaporejea London, nitakutana na mjumbe maalum wa Uingereza wa mambo ya biashara kwa Tanzania pia nitaonana na mawaziri wa mambo ya nje wa Uingereza na Jumuia ya Madola kuona uwezekano wa kuwa na mkutano mkubwa ambao utazungumzia zaidi masuala ya uwekezaji na biashara kwa Tanzania”

Wafanyakazi wa JKCI wamuaga Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hiyo (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie Mullaney (kulia) baada ya kukamilisha muda wake wa kubadilishana uzoefu na wauguzi wa taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Bi. Mollie amefanya kazi katika chumba cha ICU katika taasisi ya JKCI kwa miezi 8
 Mkuu wa Kitengo cha ubora wa huduma za afya ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tulizo Shemu akimpongeza Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie Mullaney (kulia) kwa kushirikishana uzoefu na wauguzi wa JKCI wakati wa hafla fupi ya kumuaga. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi na wapili kulia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi ya JKCI Robert Mallya
 Baadhi ya wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie Mullaney (hayupo pichani) baada ya kubadilishana uzoefu na wauguzi wa taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi 8 na kuagwa  leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akimkabidhi zawadi ya fremu ya kuweka picha Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie Mullaney wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam baada ya kubadilishana uzoefu na wauguzi wa JKCI kwa kipindi cha miezi 8. Kulia ni afisa uuguzi mwandamizi wa taasisi hiyo Mary Haule
 Afisa Uuguzi Mwandamizi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mary Haule akimwekea zawadi ya gauni juu ya mwili wake Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie Mullaney wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam baada ya kubadilishana uzoefu na wauguzi wa JKCI kwa kipindi cha miezi 8.
 Afisa Uuguzi Mwandamizi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mary Haule akimfunga zawadi ya kikoi Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie Mullaney wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam baada ya kubadilishana uzoefu na wauguzi wa JKCI kwa kipindi cha miezi 8.
Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie Mullaney katika picha ya pamoja na baadhi ya madaktari na wauguzi wa JKCI baada ya hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Bi Mollie Mullaney amefanya kazi katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum katika taasisi ya JKCI kwa kipindi cha miezi 8 na kubadilishana ujuzi na uzoefu na wauguzi wa ICI wa taasisi hiyo.
Picha na: Genofeva Matemu - JKCI

WATU 62 WAFANYIWA VIPIMO KUBAINI MOYO UNAVYOFANYA KAZI

$
0
0
Na Mwandishi Maalum – JKCI

 Jumla ya watu 62 wamefanywa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo Cardiogram) na umeme wa moyo (ECG) wakati wa punguzo la gharama za matibabu kwa wagonjwa wa kulipia lililotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Punguzo hilo lilitolewa hivi karibuni na Taasisi hiyo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea ushindi wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu kwa kuifunga timu ya Uganda mabao 3-0 na kuweza kushiriki katika mashindano ya Taifa Bingwa Barani Afrika AFCON. 2019.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Dkt. Delila Kimambo alisema kati ya wagonjwa 62 waliopima afya zao nane walikuwa ni watoto.

Dkt. Delila alisema katika kusherehekea ushindi wa timu ya Taifa Taasisi hiyo imeona ni vyema kufungua milango na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kupima afya ya moyo.

“Kati ya watu 62 tuliowapima 19 tuliwakuta na matatizo ya moyo ambapo wa nne wanatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo, mmoja kati yao ameshafanyiwa na kukutwa na tatizo la kuziba kwa mishipa miwili ya damu ameshazibuliwa mshipa mmoja na anaendelea vizuri”,.

“Wengine wanne walikutwa na tatizo la valvu ambapo wawili wanatakiwa kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha valve. Wengine tumewakuta na shinikizo la juu la damu”,.

“Zoezi hili limefanyika vizuri, tunafahamu kuwa kuna wananchi ambao huwa wanahitaji vipimo vya moyo kwa dharula na hawawezi kufika kwetu kutokana na shida mbalimbali za maisha, hivyo tulitoa punguzo hili la bei ili kuwafungulia milango ya kupata matibabu ya vipimo vinavyoweza kugundua kama mtu ana magonjwa ya moyo”, alisema Dkt. Delila.

Dkt. Delila alimalizia kwa kuwaomba watanzania kuwa na utamaduni wa kupenda kupima afya zao mara kwa mara ,kupata matibabu na majibu ya magonjwa yanayowasumbua kutoka kwa wataalamu wa magonjwa husika.

Kwa upande wake Frank Karia ambaye ni makazi wa Mwanza alisema alipewa Rufaa kutoka hospitali ya rufaa ya Bugando na kufika JKCI siku ya Jumatatu ambapo kulikuwa na punguzo la bei na kubahatika kufanyiwa vipimo vya ECHO na ECG baada ya kufanyiwa vipimo aligundulika kuziba kwa mishipa miwili inayopeleka damu kwenye moyo.

“Baada ya kukutwa na tatizo ndani ya wiki moja tayari nimeshazibuliwa mshipa mmoja wa damu na hali yangu inaendelea vizuri kama unavyoniona, baada ya wiki mbili nitarudi kliniki . Leo tarehe 29/03/2019nimeruhusiwa kwenda nyumbani, kwa kweli sikutegemea kama ningepata huduma hii kwa kipindi cha wiki moja” alisema Karia.

Alisema huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo ni za kimataifa na kuwaomba waendelee kutoa elimu kwa umma ili wananchi wafahamu zaidi huduma zinazotolewa.

MRADI WA MAJI MLANDIZI MBOGA KUANZA KATIKATI YA MWEZI WA NNE

$
0
0

MBUNGE wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ametembelea kiwanda cha mabomba cha Tanzania Steel Pipes kinachotengeneza mabomba ya kusafirishia maji kwenye mradi wa maji wa Mlandizi- Chalinze- Mboga.

Akitembelea kiwanda hicho, Ridhiwani amefurahishwa na maendeleo ya utengenezaji wa mabomba hayo ambapo takribani mabomba 321 yameanza kusafirishwa kwa ajili ujenzi wa meadi huo unaotarajiwa kuanza katikati ya mwezi April.

Akizungumza baada ya kumaliza kukagua mabomba hayo, Ridhiwani amesema kuwa imechukua miaka 16 kwa wananchi wa Chalinze kupata majisafi na salama na imani yake kubwa ipo kwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA wafanikishe mradi huo.

Amesema, kukamilika kwa mradi huo ambao wameahidi utakuwa umekamilika katika kipindi cha miezi mitano hadi sita utaweza kulinda kiti chake cha Ubungo kwani wananchi wamekuwa wanamsumbua kwa kipindi kirefu.

“Sikuwahi kuona namna wananchi wanatumia maji pamoja na wanyama kama ng’ombe ila kukamilika kwa mradi huu kutawezesha watu wangu kupata majisafi na salama ila na wao kwa upande wao nitawaomba walipie huduma ili kuweza kuendesha miradi hii maji yaweze kupatikana,”amesema Ridhiwani.


Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Arone Joseph amesema mradi huo utawanufaisha wakazi wa maeneo hayo ikiwa pamoja na wananchi wanaoishi kwenye eneo la mradi.

Joseph amesema Mradi wa maji wa Mlandizi -Mboga unatarajiwa kusafirisha maji lita milioni 9.3  (mita za ujazo 9300) kwa siku kiasi kianchokisiwa kuweza kutosheleza mahitaji ya walengwa kwa sasa na ongezeko la matumizi kwa siku za usoni.

“Hadi sasa, kiasi cha mabomba ya umbali wa km 3.7 yameshazalishwa katika kiwanda cha TSP na yameanza kupelekwa kwenye maeneo ya mradi ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza katika Vijiji vya Mboga na Msoga,” amesema Joseph.

“Katika usanifu wa mradi huo, umetilia maanani ongezeko la watu na mahitaji ya miaka 20 ijayo na kutosheleza idadi ya watu hadi kufikia 120,912 ndani ya eneo la mradi na utakuwa kwa umbali wa Kilomita 58 ujenzi wa vituo viwili vya kusukumia maji na utagharimu bilion 14 hadi kukamilika kwake,”amesema Joseph.

Afisa Utawala wa Kiwanda cha Mabomba cha TSP, Elly Bohela amesema anashukuru sana kwa Mbunge Ridhiwani Kikwete kufika kwenye Kiwanda chao kuona namna wanavyotengeneza mabomba hayo ambayo yanaenda kuwekwa kwenye mradi uliopo katika jimbo lake.

Amesema, kiwanda cha TSP ni cha wazawa na wamejizatiti kwenye kutengeneza mabomba yenye ubora aidha ameishukuru dawasa kwa kuweza kuwaamini na kuwapatia kazi hiyo muhimu.

Maeneo yatakayohudumiwa na mradi huo ni pamoja na Ruvu darajani, Vigwaza,Ranchi ya Taifa Ruvu (NARCO), Chahua -Lukenge, Visenzi, Buyuni na Mdaula -Unebazomozi.

Kwingine ni Chamakweza, Pingi, Pera, Chalinze, Chalinze Mzee, Msoga na Mboga aidha, viwanda vitakavyofaidika ni pamoja na Twyford, kiwanda cha ngozi, kiwanda cha Matunda cha Sayona pamoja na watumiaji wengine wakubwa ikiwemo kampuni Yapi Merkezi wajenzireli ya kisasa (SGR).

 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa ndani ya gari lililobeba mabomba yanayoelekea kwenye jimbo lake kwa ajili ya mradi wa maji wa Mlandizi Mboga baada ya kutembelea kiwanda cha Mabomba cha Tanzania Steel Pipes leo Jijini Dar es Salaam.
 Gari iloyobeba mabomba kwa ajili ha ujenzi wa mradi wa maji wa Mlandizi Mboga likiwa tayari kwa ajili ya safari ya kuelekea Chalinze.
 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Mhandisi Arone Joseph akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa ziara ya Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete (kushoto) kwenye kiwanda cha Mabomba cha Tanzania Steel Pipes leo Jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa anakagua eneo lilalotengenezwa mabomba ya kusambazia maji yatakayotumika kwenye mradi wa maji Mlandizi Mboga leo Jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa anakagua eneo lilalotengenezwa mabomba ya kusambazia maji yatakayotumika kwenye mradi wa maji Mlandizi Mboga leo Jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Chalinze akielezea kwa umakini ramani ya mradi wa Mlandizi Mboga unaotarajiwa kuanza kujengwa Katikati ya mwezi April mwaka huu utakaohudumia wakazi wa jimboni kwake akiwa sambamba na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Mhandisi Arone Joseph na Mkurugenzi wa Miradi DAWASA Mhandisi Lydia Ndibalema.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAPONGEZWA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA

$
0
0
Na Lulu Mussa, Dodoma
Serikali imesema itaendelea na juhudi za kushawishi wadau wa maendeleo na Jumuiya za Kimataifa ili kupata fedha za kusimamia uratibu wa shughuli za mazingira na kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba ameyasema hayo hii leo Jijini Dodoma wakati wa kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji  wa Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2019/2020 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira. 

Amesema Tanzania ni Mwanachama kwenye Mifuko na Mikataba mbalimbali duniani hivyo kuna fursa za kunufaika na fedha zitolewazo na mifuko hiyo akitoa mfano wa Green Climate Fund.
Aidha Waziri Makamba ameainisha mafanikio yaliyopatikana katika Ofisi yake kwa kipindi cha mwaka 2018/2019, kuwa ni pamoja na kufanya Mapitio ya Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 1997 na Mkakati wa Utekelezaji wake,  kuandaa rasimu ya Mpango wa Taifa wa Mazingira wa mwaka 2019 - 2023, na Maandalizi ya Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti Viumbe Vamizi (Invasive Alien Species). 

Pia, katika kipindi cha mwaka 2018/19, Ofisi ya Makamu wa Rais imekamilisha rasimu ya mwisho ya Ripoti ya Tatu ya Hali ya Mazingira Nchini baada ya kupata maoni ya wadau kabla ya kuwasilishwa Bungeni kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004.

Waziri Makamba amesema katika kuhakikisha usimamizi na utekelezaji wa Sheria ya Mazingira unazingatiwa jumla ya miradi 1,254 ya maendeleo imefanyiwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) na Ukaguzi wa Mazingira na katika kuharakisha uwekezaji katika sekta ya viwanda nchini, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira linatoa Kibali cha Awali cha Mazingira (Provisional Environmental Clearance) ili kuwawezesha wawekezaji kuendelea na maandalizi ya awali ya mradi wakati mchakato wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira unaendelea. 

Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira Suleiman Sadick amepongeza uongozi wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa jitihada za kuhifadhi mazingira nchini. " Kamati inatambua jitihada za Ofisi yenu katika kuhifadhi mazingira, sisi tunawaunga mkono" alisisitiza Sadick.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba (katikati) akiongea na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge wa Viwanda, Biashara na Mazingira Suleiman Murad Sadick katika moja ya ziara za kikazi za Kamati hiyo hivi karibuni.  

MAMLAKA HALI YA HEWA YATOA TAHADHARI MVUA KUBWA KUNYESHA MIKOA HII

$
0
0

Taarifa hii inatoa muhtasari wa mwelekeo wa hali ya hewa wa muda mfupi na muda wa kati kwa lengo la kuwapatia wananchi taarifa sahihi na za ziada kuhusu utabiri wa mvua iliokwishatolewa. Mwenendo wa mvua katika kipindi hicho hautarajiwi kubadili matarajio ya jumla ya mvua za Masika. Hivyo, msimu unatarajiwa kuwa mfupi na vipindi vya upungufu wa mvua za Masika vikijitokeza katika maeneo mengi.

Mvua zinatarajiwa kunyesha katika maeneo mengi yanayopata mvua za Masika baada ya athari ya upungufu wa mvua uliotokana na vimbunga vilivyojitokeza mfululizo katika bahari ya Hindi ikiwemo kimbunga Idai, Savannah na Joaninha katika mifumo ya hali ya hewa kuanza kupungua. Vipindi vya mvua vinatarajiwa kuongezeka katika baadhi ya maeneo katika wiki mbili zijazo za mwezi Aprili, 2019.

Aidha, maeneo ya mikoa ya Dodoma, Singida, Manyara na Kilimanjaro ambayo yalikumbwa na upungufu wa mvua kutokana na vimbunga hivyo, yanatarajiwa kuanza kupata mvua katika kipindi hiki cha mwishoni mwa mwezi Machi na wiki ya kwanza ya mwezi Aprili, 2019. Ongezeko la mvua linatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara hususan katika wiki ya pili ya mwezi Aprili, 2019 kwa siku chache.

ANGALIZO
 Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa kujitokeza katika maeneo yafuatayo katika muda uliotajwa.

i. Vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya nyanda za juu kusini magharibi (mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Rukwa na Morogoro-Mahenge) na mikoa ya Lindi na Mtwara katika kipindi cha mwisho wa wiki kuanzia tarehe 30 Machi hadi 3 Aprili, 2019.

ii. Mwanzoni mwa mwezi Aprili, 2019 vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa kujitokeza katika mkoa wa Morogoro na kusambaa katika maeneo machache ya mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.

HALI YA JOTO
Wimbi la joto lililojitokeza katika kipindi cha upungufu wa mvua katika maeneo ya pwani ya kaskazini na nyanda za juu kaskazini mashariki linatarajiwa kupungua kiasi katika kipindi cha uwepo wa mvua.

USHAURI: Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na kuzingatia tahadhari zilizotolewa na mirejeo yake pamoja na kupata na kuzingatia ushauri na miongozo ya wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

Imetolewa tarehe 29 Machi 2019 na:
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

COCA COLA KWANZA BOTTLERS YAKABIDHI ZAWADI ZA PROMOSHENI YA ‘KUNYWAAH NA USHINDE'

$
0
0

Mtaalamu wa Masuala ya masoko wa Kampuni ya Coca-Cola Kwanza, Maureen Stambuli (kushoto) akikabidhi zawadi ya fedha taslimu kiasi cha shilingi laki moja 100,000/= kwa Mkazi wa Mbagala, Furaha Suleiman Mwinyimvua (42) wakati wa hafla ya kuwakabidhi washindi wa Promosheni inayoendelea ya ‘Kunywaaah na Ushinde’ ambayo ilifanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Promosheni hiyo ya miezi mitatu inaenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambapo imedhamiria kuwatunuku wateja wake pendwa ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola.

Meneja Mauzo wa Coca-Cola Kwanza, Alex Ishengoma (kushoto) akikabidhi zawadi ya fedha taslimu kiasi cha shilingi laki moja 100,000/= kwa Mkazi wa Kawe, Bi. Martha Mushi wakati wa hafla ya kuwakabidhi washindi wa Promosheni inayoendelea ya ‘Kunywaaah na Ushinde’ ambayo ilifanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Promosheni hiyo ya miezi mitatu inaenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambapo imedhamiria kuwatunuku wateja wake pendwa ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola.

Meneja Usambazaji wa Coca-Cola Kwanza, Jacqueline Kimoy (kushoto) akikabidhi zawadi ya fedha taslimu kiasi cha shilingi laki moja 100,000/= kwa Mkazi wa Ubungo Msewe, Bi. Esther Luca Machanja wakati wa hafla ya kuwakabidhi washindi wa Promosheni inayoendelea ya ‘Kunywaaah na Ushinde’ ambayo ilifanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Promosheni hiyo ya miezi mitatu inaenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambapo imedhamiria kuwatunuku wateja wake pendwa ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola.

Meneja Mauzo wa Coca-Cola Kwanza, Beatrice Nchimbi (kushoto) akikabidhi zawadi ya Runinga kwa Mkazi wa Kinondoni, Daniel Mollel wakati wa hafla ya kuwakabidhi washindi wa Promosheni inayoendelea ya ‘Kunywaaah na Ushinde’ ambayo ilifanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Promosheni hiyo ya miezi mitatu inaenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambapo imedhamiria kuwatunuku wateja wake pendwa ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola.

Meneja Mauzo wa Coca-Cola Kwanza, Beatrice Nchimbi (kushoto) akikabidhi zawadi ya Runinga kwa Mkazi wa Ukonga, Nassib Suleiman wakati wa hafla ya kuwakabidhi washindi wa Promosheni inayoendelea ya ‘Kunywaaah na Ushinde’ ambayo ilifanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Promosheni hiyo ya miezi mitatu inaenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambapo imedhamiria kuwatunuku wateja wake pendwa ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola.

Afisa wa Coca-Cola Kwanza kutoka kitengo cha Masoko, Arthur Kiara (kushoto) akikabidhi zawadi ya Runinga kwa Mkazi wa Mbezi Beach, Augustino Paulo wakati wa hafla ya kuwakabidhi washindi wa Promosheni inayoendelea ya ‘Kunywaaah na Ushinde’ ambayo ilifanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Promosheni hiyo ya miezi mitatu inaenda sambamba na msimu huu wa Coke Studio ambapo imedhamiria kuwatunuku wateja wake pendwa ambapo watu mbalimbali wanajinyakulia fedha taslimu, runinga na bidhaa nyingine nyingi kutoka Coca Cola.

MVUA ILIYONYESHA MOSHI KWA MUDA MFUPI YALETA ATHARI.

$
0
0

Anaadika Dixon Busagaga,Moshi

MVUA kubwa iliyoambatana na upepo imesababisha adha kwa watumiaji wa BARABARA kadhaa katika mji wa Moshi baada ya miti kukatika na kufunga barabara.

Globu ya Jamii  imepita maeneo kadhaa ya mji wa Moshi na kujionea kadhia hiyo huku maeneo mengine wananchi wakijitolea kuondosha miti iloyoanguka barabarani kwa kuikata huku watumiaji wa vyombo vya moto wakilazimika kunadili njia za kupita .

Maeneo ambayo watumiaji wa vyombo vya moto wameathirika ni pamoja  barabara ya Shanty town,barabara ya International school pamoja na barabara ya Shule ya sekondari Mawenzi.

Maeneo mengine imeshuhudiwa miundombinu ya umeme ikiwa imeharibika baada ya nguzo kukatika na nyaya kuangakua katikati ya barabara.










WAZIRI MKUCHIKA AMTEMBELEA MAMA MARIA NYERERE NA RAIS MSTAAFU ALHAJ MWINYI

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiagana na Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akimsikiliza Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), wa pili kushoto ni Mama Siti Mwinyi na wa kwanza kushoto ni Afisa anayesimamia Dawati la Viongozi Wastaafu wa Kitaifa, Bi. Nyasinde Mukono.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiteta jambo na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akifafanua jambo kwa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akizungumza na watoto wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alipomtembelea Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Wa kwanza kulia ni Andrew Nyerere na wa kwanza kushoto ni Magige Nyerere. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akimsikiliza Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb).
 Afisa anayesimamia Dawati la Viongozi Wastaafu wa Kitaifa, Bi. Nyasinde Mukono, akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Mkuchika ya kuwatembelea Viongozi Wastaafu wa Kitaifa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

BARAZA LA FAMASI NCHINI LAJIZATITI KUSIMAMIA TAALUMA YA FAMASI NA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA DAWA NCHINI

$
0
0
* Yawashauri wananchi kuhusu matumizi sahihi ya dawa

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

BARAZA la Famasi nchini lililopo chini ya Wizara ya afya, maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto limejipanga katika kuendelea kutekeleza majukumu yao hasa kwa kuendelea kuboresha mifumo hasa ya ukaguzi, usajili pamoja na kujenga uwezo kwa wataalamu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam katika kikao kazi kilichowakutanisha, Msajili kutoka Baraza la Famasi nchini Elizabeth Shekalage amesema kuwa dira ya baraza hilo ni kuzidi kuwa taasisi bora zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kukidhi mahitaji ya jamii.

Amesema kuwa baraza hilo lina majukumu mbalimbali ikiwemo kusajili, kutambua na kutunza kumbukumbu za wanataaluma wa fani ya famasi ambao hadi sasa wataalamu wa kada hiyo waliosajiliwa imefikia 1863.

Pia amesema kuwa baraza hilo lina jukumu la kuhamasisha wananchi juu ya matumizi sahihi ya dawa na kuwataka wananchi kutotumia dawa bila ushauri wa daktari kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yao.

Imeelezwa kuwa  baraza hilo hufuatilia malalamiko yote  yanayohusiana na usimamizi wa taaluma ya famasi yanayotolewa na wananchi na kusema kuwa wananchi wapo huru kupiga simu bure 0800110015 na malalamiko yao kutoka katika famasi na maduka ya dawa muhimu na yatafanyiwa kazi punde.

Akieleza mafanikio yaliyopatikana hadi sasa Shekalage amesema kuwa baraza limefikia malengo mengi ikiwa ni pamoja na kuwa moja ya taasisi ya mfano katika kutekeleza mpango wa kuboresha upatikanaji wa dawa (mpango wa maduka ya dawa muhimu) ambapo baadhi ya nchi zimekuja kupata ujuzi na kutekeleza mpango huo ambapo nchi za Uganda, Liberia, Zambia, Nigeria, Ghana, Burundi na Bangladesh zimejifunza namna ya utekelezaji wa mpango huo.

Pia Baraza hilo limefanikiwa katika masuala ya kusajili wafamasia, na hadi sasa baraza hilo limesajili fundi dawa sanifu 1863 na fundi dawa wasaidizi 625 huku wakijivunia uanzishwaji wa kozi ya mmoja ya utoaji wa dawa ambayi inethibitishwa na Baraza la Elimu ya Ufundi la Taifa (NACTE.)

Shekalage amesema kuwa mipango yao ya baadae kuzidi kuendelea kuboresha mifumo na wamejipanga zaidi katika masuala ya ukaguzi, usajili pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa idara ya mafunzo na maendeleo ya taaluma Grace Mallange amesema kuwa idara hiyo ambayo ina majukumu ya kusimamia mafunzo ya Famasi vyuoni ambapo inasimamia vyema katika hilo ili kuhakikisha kuwa vyuo hivyo vinazalisha wataalamu wenye tija na hiyo ni kwa kuandaa mitaala inayoongoza vyuo vyote, kuandaa na kusimamia miongozo ya kufundishia  ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu wanaofundisha vyuo hivyo.

Mallange amesema kuwa kuwa idara hiyo pia husimamia mafunzo ya vitendo kwa wafamasia (Intership) kwa kuhakikisha wanafanya mafunzo hayo katika sehemu zinazotambuliwa  na baraza pamoja na kusimamiwa na wafamasia wanaotambuliwa na baadaye kupimwa na mitihani kabla ya kuanza kazi zao za kitaaluma.

Pia Mkuu wa Idara ya usajili na utambuzi wa viwango vya kufuzu Suma Jairo amesema kuwa wanaendelea kutumia mfumo wa kieletroniki katika usajili ili kuthibiti kughushi leseni na vibali kwa maduka ya dawa muhimu na dawa moto.

Jairo amesema kuwa mahitaji wa wafamasia bado hayatoshelezi kulingana na idadi ya wananchi waliopo huku ushauri ukitolewa kwa wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ili kuweza kuweza wataalamu katika sekta hiyo.

Baraza la famasi nchini ambalo limeendelea kuratibu, kuboresha mifumo ya ukaguzi ili jamii ipate huduma bora hadi sasa imesajili wafamasia 1863, fundi dawa sanifu 2302, fundi dawa wasaidizi 652, na majengo ya kuuzia na kutunzia dawa 1683.

Msajili kutoka Baraza la Famasi nchini,Bi. Elizabeth Shekalage  

MAHAKAMA YAAMURU FAMILIA YA WATU SABA KUREJESHEWA NYUMBA YAO

$
0
0
Na Woinde Shizza Globu ya jamii

Mahakama kuu kanda ya Arusha imeamuru familia ya watu zaidi ya saba wenye asili ya kiasia walioondolewa kimabavu kwenye nyumba yao na kukosa mahala pa kuishi, kurejea katika Nyumba hiyo bila masharti yoyote iliyopo eneo la Sabena katikati ya Jiji la Arusha.

Uamuzi huo umetolewa na jaji wa mahakama hiyo,Thadeo Mwenempazi baada ya kupitia maombi yaliyowasilishwa na upande wa familia hiyo kupitia Wakili wao ,Bariki Maeda na kuamuru familia hiyo kurejea katika nyumba yao wakati kesi ya msingi ikiendeleà kusikilizwa.

Jaji Mwenempazi alidai kuwa familia hiyo inapaswa kurejea katika nyumba hiyo na kuendelea na makazi wakati wakisubili maamuzi ya kesi ya msingi iliyopo mahakamani hapo.

Jaji katika maamuzi yake alidai kuwa mahakama hiyo imezingatia hoja zilizowakilishwa na upande wa mlalamikaji,ambaye ni familia hiyo kupitia Wakili Maeda na hivyo kuamuru kurejea katika Nyumba yao .

Familia hiyo iliondolewa kimabavu February 21 mwaka huu na kundi la watu zaidi ya 20 wakidai wanatekeleza amri ya mahakama na kusababisha usumbufu na uharibifu mkubwa wa Mali huku familia hiyo ikikosa mahala pa kuishi na kujikuta ikilala chini kwa wasamalia wema.

Akizungumza na vyombo vya habari mama wa familia hiyo,Chandni Hussein ameishukuru mahakama hiyo kwa kutenda haki na kumrejesha tena katika nyumba yake kwani taratibu zilizotumika kumtoa ndani yeye na watoto wake hazikufuatwa.

Ameongeza kuwa Nyumba hiyo iliyopo katikati ya jiji la Arusha yeye maduka ya kupanga huku familia hiyo ikiishi and a no ipo kwenye mgogoro na shemeji yake aitwaye Mortaza Hussein ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa jijini Dar es salaam

Akizungumza huku akibubujikwa machozi mahakamani hapo mama huyo amemshukuru rais John Magufuli kwa kuendeleà kuwa mtetezi wa wanyonge ambao wamekuwa wakionewa na watu wenye kipato kikubwa cha fedha.

Kesi hiyo ya Ardhi namba 6/2019 , wakili ,Maeda ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mawakili Tanganyika Mkoa wa Arusha, aliiomba Mahakama hiyo iwarejeshe kwenye Nyumba yao hadi kesi ya msingi itakapomalizika kwa kuwa taratibu zilizotumika kuwaondoa zilikuwa na mapungufu ya kisheria .
 Pichani mama wa familia hiyo Chandni Hussein akilia kwa furaha  mara baada ya mahakama kutoa maamuzi.
 

JK ATEMBELEA TAASISI YA SAYANSI ZA BAHARI PANGANI

$
0
0
NA KARIM JUMA - TANGA

RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete ameitaka Taasisi ya
Sayansi za Bahari wilayani Pangani Mkoani Tanga iliyopo chini ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuhakikisha wanawekeza zaidi kwenye
utafiti ili waweze kupata maendeleo makubwa.
.
Dkt Kikwete ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
aliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea Taasisi ya
Sayansi za Bahari kituo cha Utafiti na mafunzo ya ufugaji wa samaki
kilichopo wilayani Pangani mkoani Tanga.
.
Na kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainab Abdallah
alisema uwepo wa chuo hicho ni faraja kubwa sana kwao na kitakuwa
kichocheo cha maendeleo kwa wakazi wa wilaya hiyo.

Mh.DC Pangani amesema kuwa kwa sasa bado changamoto kubwa vijana na wananchi wa Pangani hawajanufaika na chuo hicho ambao wanategemea uwezekaji kwenye sekta ya uvuvi hivyo kuomba chuo hicho kuona namna ya kushirikiana na kuliona hilo na kujipanga kutoa mafunzo ya muda mfupi na kuwahusisha moja kwa moja wana Pangani kupata maarifa.
.
Taarifa njema ni kuwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam amelipokea na kulikubali na kusema wanajipanga kulianza mara moja na watajadili namna ya uendeshaji na ujenzi wa kuongeza miundombinu utaanza pia uandaaji wa mitaala ya namna hiyo kuwekwa tayari.

Hii ni faraja kubwa sana kwa wakazi wa Pangani na ni picha halisi kuwa ujio wa Chancellor Dk.Jakaya M.Kikwete umeacha alama Pangani.
 

DKT. MPANGO AAGIZA KUTOTUMIA FUNGU LA LISHE KWA MATUMIZI MENGINE

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akipeana mkono na Binti Mfalme wa Jordan ambaye ni balozi wa masuala ya Lishe Duniani, Sarah Zeid (kushoto), baada ya kumalizika mkutano kuhusu Lishe uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Binti Mfalme wa Jordan ambaye ni balozi wa masuala ya lishe Duniani, Sarah Zeid (kushoto), wakifurahia jambo katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Tanzania na Shirika la Chakula Duniani- WFP, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
(Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango)

…………………………..


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amekutana na kufanya mazungumzo na Binti wa Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid, ambaye ni Mwanaharakati wa masuala ya lishe, wanawake na watoto Duniani, jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao, Dkt. Mpango, alimweleza Princess Sarah Zeid kwamba Tanzania bado inakabiliwa na changamoto ya masuala ya lishe, utapiamlo na udumavu wa watoto licha ya nchi kuwa na chakula cha kutosha.

Dkt. Mpango alisema kuwa iwapo eneo la lishe halitasimamiwa kikamilifu Taifa litazalisha watoto wenye udumavu wa ubongo na kusababisha kupungua kwa uwezo wa kufikiri na utendaji hafifu wakiwa katika shughuli mbalimbali.

Alisema ipo mikoa ambayo inazalisha mazao mengi kama Mbeya na Njombe lakini ina kiwango kikubwa cha watoto wenye utapiamlo, na kutoa wito kwa kila mtanzania kuhakikisha anaangalia ni chakula gani kinahitajika kwa ajili ya lishe ya watoto na wakinamama wajawazito ili kupunguza udumavu na vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga.

Aidha amempongeza Mwana wa Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid, kwa kampeni yake anayoifanya duniani kote kupambana na vifo vya wakinamama wajawazito na watoto kwa kuwa mchango wa wanawake ni mkubwa katika jamii ikiwemo uzalishaji mali.

Alisema idadi ya wanawake nchini Tanzania ni asilimia 51 ya idadi ya watu wote wanaokadiriwa kufikia milioni 55 ambapo mchango wako katika sekta mbalimbali za uchumi umekuwa mkubwa hivyo jitihada za kuwalinda zinahitajika.

Alimweleza Binti Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid kwamba kwa kutambua umuhimu wa lishe serikali imelivalia njuga suala la lishe kwa kutenga bajeti kila mwaka katika kila wizara na kwamba fedha hizo zimewekewa wigo zisitumike kwa matumizi mengine.

“Nimeziagiza Wizara, Mikoa na Halmashauri zote nchini kutumia fungu lililotengwa kwa ajili ya lishe kwa matumizi yaliyopangwa ili kuhakikisha watanzania wanaimarika kiafya na kushiriki kikamilifu katika Shughuli za Maendeleo” Alisema Dkt. Mpango.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wa Mkutano kati yake na Mwana wa Mfalme wa Jordan ambaye ni balozi wa masuala ya Lishe Dunia, Sarah Zeid na

Kwa upande wake Mwana wa Mfalme wa Jordan, Sarah Zeid, ambaye aliambatana na Mwakilishi wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) nchini Tanzania, Bw. Michael Dunford, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada zake katika kupambana na utapiamlo unaosababishwa na ukosefu wa lishe.

Amewataka watanzania kuhakikisha suala la Lishe linapewa kipaumbele na kila mmoja kwa manufaa ya Taifa na Dunia kwa ujumla na kwamba atahamasisha jumuiya ya kimataifa kuchangia jitihada za Serikali za kupambana na tatizo la lishe, na vifo vya wanawake wajawazito na watoto.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa-WFP nchini Tanzania Bw. Michael Dunford, amesema kuwa shirika lake linatambua mchango mkubwa wa Serikali katika kupambana na masuala ya lishe duni na shirika lake litaendelea kushirikiana na nayo ili kufikia malengo yanayotarajiwa.

WAZIRI WA MAJI PROF.MBARAWA AKAGUA MIRADI YENYE CHANGAMOTO MKOANI SONGWE

$
0
0


Moja ya miundombinu ya maji inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje ambapo Waziri Mbarawa alifika kukagua ujenzi huo.
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akiwasili ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Generali Mstaafu Nicodemus Mwangela katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe David Kafulila.

Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Generali Mstaafu Nicodemus Mwangela.
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akipata maelezo ya ujenzi wa tanki (halipo pichani) kutoka kwa Mhandisi wa Maji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya Mhandisi Ndele Mengo. Kushoto kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Momba Halmashauri ya Tunduma Bw. Juma Said Irando.

…………………………

Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) leo ameanza ziara ya kukagua miradi ya maji mkoani Songwe hususan miradi yenye changamoto ambayo imechukua muda mrefu kukamilika.

Waziri aliyasema hayo alipofika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Mwangela mara tu baada ya kuwasili ofisini kwa Mkuu wa mkoa huyo.

“Nimekuja kukagua miradi ambayo ina changamoto kubwa ambayo haijakamilika kwa muda mrefu na wananchi wanaisubiri kwa muda mrefu” alisema Profesa Makame Mbarawa.

Serikali kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi imeahidi kwamba ifikapo mwaka 2020 kwenye miji mikuu ya mikoa wananchi wawe wamepata maji asilimia 95 na miji ya wilaya asilimia 90 na vijijini asilimia 85.

Hata hivyo, Waziri alisisitiza kwamba tunapopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maji inabidi lazima tusimamie kwa uadilifu, ukaribu zaidi na kuhakikisha kwamba wakandarasi wanaolipwa pesa kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maji wanaanza kazi mara moja baada ya kulipwa, kwa sababu wakandarasi wengine wamekuwa na tabia ya kuchukua pesa za miradi ya maji na kupeleka kwenye miradi mingine.

Naye, Mhandisi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya, Mhandisi Ndele Mengo akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Itumba Isongole amesema Mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi Singilimo Enterprises Ltd. ya jijini Dar es Salaam ambapo gharama ya mradi ni Tsh. 804,162,330/= na hadi sasa ameshalipwa Tsh. 313,238,780/= ambazo zikihusisha uchimbaji wa mitaro kwenye bomba kuu chanzo cha umbali wa mita 4332 na ulazaji wa bomba za plastic wenye kipenyo cha nchi 8 umbali wa mita 3924 pamoja na tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita laki. Mradi huu amesema unasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya. Matazamio ya kukamilika kwa mradi huu ni 30/5/2019.

Aidha, Waziri Profesa Mbarawa ameagiza mradi wa Itumba Isongole uwe umekamilika ifikapo tarehe 30/5/2019 na mradi wa maji wa mji wa Tunduma uwe umekamilika ifikapo 13/4/2019 ili wananchi wapate majisafi na salama kwa sababu karibu wakandarasi wote wameshalipwa pesa zao walizokuwa wanaidai Serikali.

MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA SEKONDARI YA KARDINALI PENGO IKWIRIR

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Askofu wa Jimbo la Ifakara, Salutaris Libena wakiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019. Wa pili kulia ni Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Fancis wa Asiz Ikwiriri, Padre Disma Kimboi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Askofu wa Jimbo la Ifakra, Salutarisi Libena baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019. Katikati ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa ambaye alipewa nafasi ya kusalimia wakati Waziri Mkuu alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri Mkoani Pwani Rufiji, Machi 29, 2019. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na wa nne kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019. Wengine kutoka kulia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu wa Jimbo la Ifakara, Salutaris Libena na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Francis wa Asiz Ikwiriri, Padre Dismas Kimboi
Wananchi wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya wasichana ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri Mkoani Pwani, Machi 29, 2019
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Benki zashauriwa kuja na amana ndogo kwa ajili ya wakulima

$
0
0
Taasisi za kifedha nchini zimekiwo benki zimeshauriwa kuja na mbinu mbadala wa amana ndogo ndogo kwa ajili ya wakulima na watu wa kipato cha kati na chini ili kuweza kukuza mitaji yao na kupunguza umasikini kwa wananchi wa hasa wa vijijini.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Benki ya Mkombozi, Tawi la Iringa mjini hivi karibuni, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema kwamba amana ndogo kwa ajili ya wakulima na wafanyabiashara wa kati inakuza mitaji kwenye benki na kukuza uchumi na ustawi wa jamii nchini.

"Achana na amana kubwa kutoka kwa matajiri ni lazima benki za ndani ya nchini zije na mkakati mathubuti wa kuwa na amana ndogo ndogo ambazo ni endelevu ili kuweza kukuza mitaji yao na kuwainua wananchi masikini kwa kipato," aliongeza Lukuvi

"Nataka kuhakikisha wakulima wa iringa wako wengi sana sasa muanze kufanya mpango wa kuwatembelea na nina uhakika mtarudi na pesa nyingi sana," alifafanua Lukuvi

Aliongeza kwamba kuna tabia ya mabenki ya kuwanya'nywa wadaiwa bila kufuata sheria za nchini na ni baada ya kuwapokesha ovyo ovyo, alisema mnatumia mawakala makanjanja ambao wanatangaza matangazo siku ya Jumapili ambapo mahakama zimefungwa na kuendesha mnada kihuni na kuuza nyumba za masikini.

Lukuvi alisema kwamba ni lazima wafuate sheria za nchini katika kuchukua nyumba za watu masikini kwa kuwashirikisha wizara ya ardhi na msajili ili serikali iweze kujiridhisha kwamba sheria za nchini zilifuatwa.

"Pamoja ya kwamba kuna mikopo chechefu lakini ni lazima mabenki yafuate sheria katika kuchukua dhamana ya wateja wao walioshidwa kulipa mikopo waliyokopa serikali haitakubali kuwapa mali za wanachi bila kufuata sheria maana kuna sheria ya jinsi ya kuchukua dhaman za wateja walioshidwa kurejesha mikopo yao kwa wakatim," alisisitiza Waziri.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, George Shumbusho alisema kwamba taasisi za kifedha zinapitia katika kipindi chenye changamoto ikiwa pamoja na ukuaji wa kiwango cha mikopo chechefu (growth of non-performing loans).

"Nichukue fursa hii kutanabaisha mbele ya wateja wenu kwamba pamoja na mambo mengine kuporomoka kwa mitaji, kupungua kwa ukwasi ambazo zote kwa pamoja zimeongeza changamoto katika taasisi za kifedha nchini," alisema.

Alifafanua kwamba katika suala la mikopo benki yao kushirikiana na watendaji wa kata na wenyeviti wa serikali za mitaa katika mkoa wa Iringa na maeneo mengine ndani ya nchini.

Aliongeza kwamba benki hiyo imewaelimisha wananchi umuhimu wa kujumuika kuunda vikundi vya watu watano ambavyo hujumuika katika makundi kumi ambapo ni watu hamsini na kuwa ndio msingi wa dhamana yao.

Shumbusho alisema kwamba pamoja na mano mengine benki hiyo ina riba rafiki inayowezesha mkopaji kujikomboa kiuchumi ndani ya muda husika na lengo endelevu la benki hiyo kuwafikia wananchi wa kawaida wengi zaidi na tawi hilo ni la tisa.

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawaza Kulevya yatoa msaada wa piki piki kwa Karapina Foundation

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawaza Kulevya imetoa msaada wa pikipiki yenye thamani ya Sh.milioni tatu kwa Karapina Foundation ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika harakati za udhibiti wa dawa za kulevya ikiwa pamoja na utoaji wa elimu yatonayo na matumizi ya dawa hizo. 

Akizungumza jana Machi 29, 2019 jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhi pikipiki hiyo kwa Karama Foundation , Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogars Siyanga amesema mamlaka hiyo imekuwa ikishirikiana na na mashirika yasiyo ya kiserikali na vikundi mbalimbali vya kijamii katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini. 

Amesema mamlaka hiyo inatambua na kuthamini kazi zinazofanywa na mashirika hayo huku akifafanua Karapina Foundation ni shirika ambalo linafanya kazi za udhibiti wa dawa za kulevya kwa kutoa elimu kuhusu madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya, kutembelea vituo vya kuwasaidia waathirika na dawa na kutembelea vijiwe vyao na kuwashauri waende kwenye vituo vya matibabu. 

"Katika kufanya kazi hizo Karama Foundation kupitia Karama Masoud ambaye ndio mwenye kufanya harakati hizo amekuwa na tatizo kutoweza kuwafikia walengwa wengi na kwa wakati, hii ni kutokana na kutokuwa na usafiri .Mamlaka imeamua kumkabidhi pikipiki yenye thamani ya Sh.milioni tatu ili imsadie katika kazi hiyo. 

"Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inawataka Karapina Foundation kuitumia pikipiki hii kwa kazi iliyokusudiwa ili kufanikisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya .Aidha Karapina Foundation wanatakiwa kuitunza ili pikipikipi idumu muda mrefu,"amesema Kamishina Jenerali Siyanga. 

kuona  kwa lengo la kuwezesha kazi za udhibiti wa dawa za kulevya ikiwa pamoja na kutoa elimu kuhusu madhara ya dawa za kulevya na kutembelea vit ufanisi wa shughuli muwezesha katika harakati zake za kupambana na dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na kutoa elimu sema itaendelea kushirikana na taasisi mbalimbali zikiwemo za watu bi binafsi pamoja na makundi ya watu 

Amefafanua kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikifuatilia namna ambavyo Karapina Foundation imekuwa ikiifanya kazi hiyo kwa moyo wa uzalendo na hivyo imeona ni vema ikatambua mchango wake kwa kumpa pikipiki na kwamba itaendelea kumsaidia kadri inavyowezekana hasa kwa kutambua kazi ya kupambana na dawa za kulevya ni jukumu la kila mmoja wetu. 

Pia amesema mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, imekuwa ikishirikiana na makundi na taasisi za watu mbalimbali na hivyo wamekuwa wakisaidia makundi hayo kwa nyakati tofauti."Ni jukumu letu mamlaka kuzisaidia taasisi binafsi na makundi ya watu mbalimbali kwani tunaamini kwa umoja wetu tutafanikiwa kukomesha dawa za kulevya nchini. 

"Leo hii tumekabidhi pikipiki hii kama kitendea kazi kwa Karama Foundation na tumekuwa tukifanya hivyo kwa taasisi nyingine pia.Kikubwa tunachoweza kueleza kwa leo, tunatambua kazi nzuri inayofanywa na Karama na hivyo katika kuthibitisha kumtambua tumeona anastahili kuwepa pikipiki.Tumekuwa tukizungumza naye Karama mara nyingi na amekuwa akija ofisini kwetu na kufanya mazungumzo .Tumeona tunakila sababu ya kumsaidia ili atekeleza kile ambachoa amekuwa akikifanya kwa shida na hara,"amesema Kamishina Jenerali Siyanga. 

Kwa upande wake Karama Masoud ambaye ndio anayeisimamia Karama Foundation , amesema anashukuru kwa msaada wa kitendea kazi ambacho amekipata na kwamba mamlaka imethibitisha kuwa iko pamoja naye , hivyo ameahidi ataendelea kuifanya kazi hiyo kwa uzalendo mkuwa na wa hali ya juu. 

"Harakati za kupambana na dawa za kulevya nimeianza muda mrefu , ilifika mahali nikawa nakata tamaa kwani changamoto ni nyingi ikiwemo ya kifedha na usafiri, hatimaye leo hii Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya wameona ninastahili kupata pikipiki ili kurahisisha namna ya kuwafikia Watanzania wengi zaidi. 

"Kwangu sina cha kuwalipa zaidi ya kutambua , kazi ambayo naifanya inatathiminiwa.Naomba nitumie nafasi hii kueleza wazi, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli imesimama kidete kukomesha dawa za kulevya .Kwa mazingira yaliyopo na jitihada za mamlaka nina uhakika Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana,"amesema Masoud.

Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers Siyanga  (wa kwanza kushoto) akiwa ameshika pikipiki leo jijini Dar es Salaam baada ya kumkabidhi Karama Masoud ambaye amekuwa akishiriki katika udhibiti wa matumizi ya dawa za kulevya na kutoa elimu kuhusu madhara yatokanayo na matumizi ya dawa hizo kupitia Karama Foundation.
 Kamishina  Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers Siyanga (kushoto), akiwa ameshikana mkono na Karama Masoud kutoka Karama Foundation baada ya kumkabidhi pikipiki kwa ajili ya kumsaidia kwenye shughuli zake za kudhibiti dawa za kulevya na kutoa elimu kuhusu athari zitokanazo na matumizi ya dawa hizo.Kamishina Siyanga amekabidhi pikipiki hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Karama Masoud kutoka Karama Foundation (kushoto) akiwa ameshikana mkono na Kamishna wa Kitengo cha Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi baada ya tukio la mamlaka hiyo kukabidhi pikipiki kwa lengo la kumuwezesha Masoud kutekeleza majukumu yake.

NAIBU WAZIRI FEDHA NA MIPANGO ATEMBELEA CHUO KIKUU MZUMBE NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MABWENI YA WANAFUNZI

$
0
0
 Bi. Amina Jumanne Mkazi wa kipera ambaye ni kibarua katika ujenzi unaoendelea eneo la Maekani akisalimiana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) wakati alipotembelea shughuli ya Ujenzi inayoendelea. 
 Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) akiwa na mwenyeji wake Makamu Mkuu wa Chuo sili Chuo Pro. Lughano Kusiluka; baada ya kuwasili Chuo Kikuu Mzumbe; alipofanya ziara hivi karibuni.

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) akiweka saini kwenye kitabu cha Wageni baada ya kuwasili Chuo Kikuu Mzumbe.

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango akiwasili eneo la Maekani ambako ujenzi wa mabweni ya wanafunzi unaendelea. Kushoto ni Prof. Ernest Kihanga Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha, akifuatiwa na Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB), mwenye kofia ni injinia na msimimizi ya mradi Injinia Focus Alex Odecho, na wa mwisho kulia ni Prof. Lughano Kusiluka Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe.

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) akielekeza jambo kwenye moja wapo ya majengo ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi unaoendelea eneo la Maekani. Kulia ni msimamizi wa mradi Injinia Focus Alex  Odecho.
 Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) afurahia zawadi yenye kumbukumbu ya Chuo Kikuu Mzumbe alichosoma na kufanya kazi kabla ya kuingia kwenye siasa.

Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (katikakati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe alipotembelea hivi karibuni.





Naibu Waziri Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) ametembelea Chuo Kikuu Mzumbe na kukagua ujenzi wa Mabweni ya Wanafunzi unaoendelea katika eneo la Maekani, Makao Makuu ya Chuo hicho, Morogoro.


Mhe. Naibu Waziri, amepongeza jitihada kubwa zilizofanywa na Uongozi wa Chuo kwa kushirikiana na Serikali katika kutatua kero ya malazi kwa wanafunzi na kusisitiza umuhimu wa kuanza mara moja awamu ya pili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na mihadhara katika eneo hilo ili kuwarahisishia wanafunzi kutotembea umbali mrefu wakati wa masomo.


“Serikali inategemea mchango mkubwa wa Vyuo Vikuu katika kutimiza malengo; hasa kwenye hili la ukuaji wa uchumi. Pamoja na kwamba tunajivunia uchumi wetu kukua lakini tusibweteke, badala yake tufanye tafiti na kuandaa vema vijana ambao watakuwa watumishi bora wa Umma wanaoendana na dhana ya sasa ya nidhamu ya kazi. Hivyo, nimefarijika sana kuona maendeleo na hatua kubwa ambayo mmepiga kitaaluma na katika miradi ya maendeleo mnayosimamia” alisema Mhe. Naibu Waziri.


Akikamkaribisha Naibu Waziri huyo, ambaye pia alipata fursa ya kuzungumza na Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe; Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka amemweleza Mheshimiwa Naibu Waziri kuwa, kwa sasa Chuo Kikuu Mzumbe kinatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya miundombinu katika Kampasi Kuu ya Morogoro, Kampasi ya Mbeya na Kampasi ya Dar-es-salaam na kwamba, lengo ni kuendelea kutumia ruzuku inayotolewa na Serikali na vyanzo vya mapato ya ndani kuendeleza ujenzi na kuboresha miundombinu ya Chuo ili kujenga mazingira bora ya utoaji wa Elimu ya Juu.


“Napenda kuipongeza sana Serikali yetu kwa kutambua mchango mkubwa wa Vyuo Vikuu nchini, na kwa upande wa Taaluma, Chuo chetu kitaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuendeleza Uchumi wa Viwanda; kwa kuendelea kufanya tafiti, kubuni miradi ya maendeleo na kutoa nguvu kazi itakayowezesha Tanzania kufikia malengo yake” alisema Prof. Kusiluka.


Ameahidi Chuo Kikuu Mzumbe kuendelea kuimarisha uhusiano na kufanya kazi kwa karibu zaidi na Taasisi na Mashirika mbalimbali ya Umma kwa kubadilishana ujuzi na uzoefu, pamoja na kutumia wanataaluma kuboresha utendaji Serikalini, kulinda nidhamu na kuinua kiwango cha elimu inayoendelea kutolewa na Chuo hicho.


Mradi wa Ujenzi wa Mabweni katika Kampasi Kuu ya Chuo Kikuu Mzumbe ambao unafadhiliwa na Serikali,unatekelezwa na SUMA JKT na unategemewa kukamilika ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu. Mradi unategemea kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.5 hadi utakapokamilika. Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha wanachuo wengi zaidi katika Kampasi Kuu kukaa kwenye hosteli za Chuo.


SERIKALI YAIAGIZA BMT KUHAKIKISHA UCHAGUZI WA KLABU YA YANGA UNAFANYIKA NDANI YA SIKU 30

$
0
0

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo (Kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 30, 2019 Jijini Dodoma kuhusu kuliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kusimamia Uchaguzi ndani ya Klabu ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) ufanyike ndani ya siku 30 kuanzia leo.Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Bw.Alex Nkenyenge.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw.Alex Nkenyenge (Kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 30, 2019 Jijini Dodoma kuhusu kutekeleza maagizo ya Serikali kwa Baraza hilo kusimamia Uchaguzi ndani ya Klabu ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) ndani ya siku 30 kuanzia leo.Kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo.

……………………

Na Shamimu nyaki –WHUSM

Serikali imeliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kushirikiana na Shirikisho la mpira wa Miguu (TFF) kuhakikisha uchaguzi ndani ya Klabu ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) unafanyika ndani ya siku 30 kuanzia leo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo katika mkutano na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma ambapo amesema kuwa migogoro iliyokuwepo huko nyuma imeshafika tamati hivyo uchaguzi ndani ya Klabu hiyo ni lazima ufanyike.

“Nailekeza BMT iwaelekeze TFF kuhakikisha taratibu zote za uchaguzi zinafuatwa na uchaguzi ndani ya Klabu ya Dar es Salaam Young Africans unafayika ndani ya siku 30 kuanzia sasa”.amesema Bw.Singo

Aidha Bw.Singo amewahisi Viongozi, wanachama na wapenzi wa Klabu ya Dar es Salaam Young Africans kutoanzisha migogoro wala vikwazo vingine bali kutumia siku 30 hizo kufanya uchaguzi ili kupata viongozi watakaoisimamia na kuiongoza Klabu hiyo kuendelea kufanya vizuri katika mpira wa miguu ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw.Alex Nkenyenge amesema amepokea maagizo na atayafanyia kazi mara moja ili kipindi kilichowekwa na Serikali cha siku 30 Klabu ya Yanga iwe tayari ina uongozi.

Bw.Nkenyenge ameongeza kuwa atahakikisha Kamati ya Uchaguzi ya TFF inapanga utaratibu unaotakiwa kufuatwa kulingana na Katiba ya Shirikisho hilo ili Uchaguzi huo ufanyike hatimaye migogoro iliyodumu kwa muda mrefu ndani ya Klabu hiyo ifikie mwisho na Klabu iendelee kufanya vizuri katika mpira wa miguu.

Klabu ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) ni miongoni mwa Klabu kubwa za mpira wa miguu hapa nchini ambayo kwa muda mrefu haijatekekeleza uchaguzi kwa mujibu wa Katiba yao
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images