Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

BancABC yatoa msaada wa mabati 200 kwa wilaya ya Kilindi.

$
0
0
BancABC kupitia Huduma yetu ya Mkopo Rahisi imejidhatiti kuweza kuhakikisha kwamba tunainua kuendeleza mazingira ya elimu katika wilaya ambazo benki hii inafanya shughuli zake kupitia miradi yetu ya kusaidia jamii inayotuzunguka. 

Sisi BancABC tunaamini kwenye umuhimu wa elimu bora katika jamii zetu hapa Tanzania na kwa hivyo tunaunga mkono Serikali ya Awamu ya 5 na hususani Rais wetu Mhe. John Pombe Mafuguli Katika miradi mbali mbali ya elimu kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu na kuweza kuwafikia kila jamii na hasa maeneo ya vijijini kwa wale ambao wako kwenye hali duni. 

Akizungumza katika hafla hiyo fupi Bw. Emmanuel Nzutu ambaye ni mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi alisema; “Kwa kuunga mkono juhudi za serikali za kutoa elimu bure kwa kila Mtanzania kuanzia chekechekea hadi kidato cha nne, Leo Bancabc tunatoa msaada wa mabati 200 kwa wilaya ya Kilindi, na msaada huu tunaukabidhi hapa kwa Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Sauda Salum Mtondoo.” 

Napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha Bancabc na pia kuwajulisha kuwa benki yetu tunatoa huduma ya Mkopo ambao ni mahususi kwa wafanyakazi wa serikali, Easy loans ambapo inakupa nafasi ya kulipa Mkopo kwa muda wa miaka sita na vile vile una uwezo wa kuweza kuongeza Mkopo hata kabla ya kumaliza kulipa ule wa awali. 

Uzuri wa mkopo huu tofauti na mikopo mingine ni kwamba, mwenye kuomba Mkopo anaweza kuchagua ni mradi gani wa kuwekeza fedha zake kwa mfano kulipa karo ya shule, kununua gari, kufanya marekebisho ya nyumba, kulipa kodi ya nyumba au kumalizia ujenzi. 

Vile vile tunaweza kununua Mkopo wako wa awali ukabaki na Mkopo mpya. 

‘Mkopo huu utakuwa na bima ya maisha pale ambapo mwenye Mkopo anapofariki, familia yake inapewa pesa taslimu Tzs500, 000 kwa ajili ya kugharamia mazishi.’ 

Tunatoa wito kwa wateja wetu na wale ambao pia sio wateja wetu kujiunga na Bancabc na kuchangamkia Mkopo huu kwani sisi tunakuweka karibu na ndoto zako.

Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akikabidhi msaada wa mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo


Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja na Asmah Abubakar(kushoto) kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi msaada wa mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo (kulia)


Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja na Asmah Abubakar(kushoto) kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi msaada wa mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo (kulia)


.Mheshimiwa Sauda Salum Mtondoo, mkuu wa Wilaya ya Kilindi akikabidhi mabati yaliyotolewa na BancAbc kwa walimu wa shule ambazo zimenufaika na msaada huo.

Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja na Asmah Abubakar kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi msaada wa mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo


Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akipeana mkono na mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo baada ya kukabidhi msaada wa mabati 200. Wengine katika picha ni Asmah Abubakar na Raphael Kalinga wa BancAbc.

SPIKA NDUGAI AWEKA JIWE LA MSINGI TAWI LA UBAGO WILAYA YA KATI MKOA WA KUSINI UNGUJA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mjumbe wa Kamati Kuu CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Kaskazini na Kusini Unguja Mhe. Job Ndugai akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Ofisi ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja leo tarehe 28 Machi, 2019 Mjini Zanzibar.
 Spika wa Bunge, Mjumbe wa Kamati Kuu CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Kaskaizni na Kusini Unguja Mhe. Job Ndugai akiweka jiwe la msingi Tawi la Ubago Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo tarehe 28 Machi, 2019 Mjini Zanzibar.
 Spika wa Bunge, Mjumbe wa Kamati Kuu CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Kaskazini na Kusini Unguja Mhe. Job Ndugai (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Ndg. Ali Abdu Ali (kushoto) wakati wa utandazaji wa mabomba ya maji safi na salama, kutoka kisima cha Bambi kuelekea Kijiji cha Uroa Jimbo la Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja leo tarehe 28 Machi, 2019 Mjini Zanzibar.
 Spika wa Bunge, Mjumbe wa Kamati Kuu CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Kaskazini na Kusini Unguja Mhe. Job Ndugai akiongoza Waheshimiwa Wabunge kufukia bomba la maji wakati wa utandazaji wa mabomba ya maji safi na salama, kutoka kisima cha Bambi kuelekea Kijiji cha Uroa Jimbo la Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja leo tarehe 28 Machi, 2019 Mjini Zanzibar.

Spika wa Bunge, Mjumbe wa Kamati Kuu CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Kaskazini na Kusini Unguja Mhe. Job Ndugai akizungumza na Wajumbe wa Kamati za Siasa za Halmashauri Kuu za CCM, pamoja na Kamati za utekelezaji Jumuiya za CCM ngazi ya Mkoa na Wilaya katika kikao kilichofanyika leo tarehe 28 Machi, 2019 Mkoa wa Kusini Unguja Mjini Zanzibar.
 Wajumbe wa Kamati za Siasa za Halmashauri Kuu za CCM Mkoa wa Kusini Unguja, pamoja na Kamati za utekelezaji Jumuiya za CCM ngazi ya Mkoa na Wilaya wakimsikiliza Spika wa Bunge, Mjumbe wa Kamati Kuu CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Kaskazini na Kusini Unguja Mhe. Job Ndugai (hayupo kwenye picha) katika kikao kilichofanyika leo tarehe 28 Machi, 2019 Mkoa wa Kusini Unguja Mjini Zanzibar.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

WEZI WA MILIONI 33 ZA WAKULIMA WA KOROSHO WAKAMATWA, WASILIMULIA WALIVOWAIBIA

$
0
0
Jeshi la Polisi Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma linawashikilia viongozi kumi na moja wa Chama cha msingi MJI MWEMA kwa kuwaibia wakulima tani 10 za korosho zenye Thamani ya Shilingi milioni 33. Watuhumiwa hao wamekili mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kuhusika na wizi wa fedha hizo.

MISS TANZANIA QUEEN ELIZABETH ASAINI MKATABA NA TTB KUTANGAZA UTALII

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Miss Tanzania 2018/2019 Queen Elizabeth Mukune amesaini mkataba 
wa kuwa Balozi wa Bodi ya Utalii Tanzania leo March28 2019 kwa kutangaza Utalii wa ndani na kutoa hamasa kwa watanzania. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam  wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba huo wa mwaka mmoja Queen Elizabeth anasema kuwa yeye anaona fahari kubwa kupata nafasi ya kuwa balozi wa kutangaza vivutio vyetu hivyo amefurahi kupata nafasi hiyo.

"nimefurahi kupata nafasi ya kutangaza vivutio vyetu ndani na nje ya nchi na naahidi kuitumia nafasi hii vizuri kabisa  kwa kutumia nafasi na umaharufu wangu nilionao kwa sasa kwa kuwa mfano wa Mrembo ambaye nitafanya ziara ya utalii wa ndani kama taji langu linavyojieleza kwani nitatoa hamasa kupitia mitandao yangu ya kijamii na makundi yote yanayoniunga mkono hili waweze kutembelea vivutio vyetu vilivyopo hapa nchini"anasema 

Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa bodi ya Utalii nchini Devotha Mdachi anasema katika kuendelea kutangaza utalii wa nchi wamehamua kutumia vijana wenye ushawishi ili kuzidi kuitangaza  utalii wetu kwa watanzania na wageni wanaotuzunguka. 

"Tumeamua kumtumia Miss Tanzania kwanza ni kijana pia anaushawishi mkubwa kwa jamii kwa watu wengi kwani ameweza kutuwakilisha kimataifa hivyo kupitia yeye tutaweza kutangaza vivutio vyetu vikafika mbali na kuwafikia vijana wengi hapa nchini ambao wamekuwa wakifatilia masuala ya burudani na urembo"anasema.

anasema wataendelea kuwatumia vijana maarufu kuzidi kutangaza utalii wa nchi na wameshaanza mazungumzo na baadhi yao. 
 Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini,Devotha Mdachi akizungumza na Waandishi wa habari Kabla ya kutiliana Saini na Miss Tanzania 2018/2019, Queen Elizabeth Mukune katika Ofisi za TTB Zilizopo Jijini Dar es Salaam.
 Miss Tanzania 2018/2019, Queen Elizabeth Mukune akizungumza na Waandishi wa habari kabla ya kutiliana Saini Mkataba wa kuwa Balozi wa Bodi ya Utalii Nchini.
 Miss Tanzania 2018/2019, Queen Elizabeth Mukune pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini,Devotha Mdachi wakitiliana saini Mkataba wa mrebo huyo kuwa balozi wa utalii nchini
  Miss Tanzania 2018/2019, Queen Elizabeth Mukune pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini,Devotha Mdachi, Wakibadilishana Mkataba mara baada ya kuliana Saini
Sehemu ya Waandishi wa habari waliofika kushuhudia utiliaji saini Mkataba wa  Miss Tanzania 2018/2019, Queen Elizabeth Mukune pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini,Devotha Mdachi

Balozi Seif ahudhuria maonesho ya kilimo Cuba.

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, na Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Dkt. Makame Ali Ussi, wakikaribishwa na Naibu Waziri wa Kilimo wa Cuba Mhe. Jose Miguel Rodriquez De Armas, kwenye Maonesho ya Kimataifa ya 22 ya Kilimo yaliyofanyika jijini Havana, Cuba. Mhe. Balozi Seif Ali Iddi alialikwa kama mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo yaliyofanyika mnamo tarehe18 Machi, 2019. Maonesho hayo yalihudhuriwa na wananchi zaidi ya 3000. 
Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, akitizama kikundi cha wakulima waliokuwa wameandaliwa kutoa burudani kwenye maonyesho hayo. 
Burudani zikiendelea kutolewa na vikundi mbalimbali vya wakulima. 
Naibu Waziri wa Kilimo wa Cuba Mhe. Jose Miguel Rodriquez De Armas, akihutubia kwenye ufunguzi wa maonyesho hayo. 
Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, akitembelea na kujionea mazao mbalimbali yanayolimwa nchini Cuba kwenye mabanda ya makampuni mbalimbali ya wafanyabiashara na yawakulima. 

Dkt. Ussi atembelea Shamba Asilia nchini Cuba

$
0
0
Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Dkt. Makame Ali Ussi, ametembelea shamba la mimea asilia ( organic farm ) nchini Cuba, ambapo alipata maelezo juu ya uzalishaji wa mazao mbalimbali bila kutumia kemikali ambapo mradi huo umeweza kuajiri wafanyakazi takribani 200 wakiwemo wazee na vijana. Wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shamba hilo, wa pili kutoka kulia ni mkalimani Bi. Beatriz Soto na wa kwanza kushoto ni Afisa kilimo, Bw. Jose Antonio. 
Mhe. Dkt. Ussi akiendelea kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa shamba hilo, Bw.Miguel Angel Lopez, wa kwanza kulia ni Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Mohamed Kamal Mohamed, akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa. 

Mhe. Dkt. Ussi akiendelea kupata maelezo juu ya kilimo cha miwa. 
Juu na chini Mhe. Dkt. Ussi akipata maelezo namna ya utengenezaji wa mbolea isiyokuwa na kemikali yeyote. 
Bw. Lopezi akimwonyesha Mhe.Dkt. Ussi teknolojia ya kifaa cha kupandia mazao. 
Mhe. Dkt. Ussi akizungumza na mmoja wa wakulima kwenye shamba hilo, aliyeonekana kufurahishwa na ujio wa Watanzania.
Sehemu ya mazao yanayopatikana kwenye shamba hilo. 



SOLSKJAER ALAMBA MKATABA WA KUDUMU MAN UNITED

$
0
0



Klabu ya Manchester United imeweza kumpatia Mkataba wa miaka Mitatu Veterani wa Timu Hiyo Ole Gunnar Solskjaer mara baada ya kufanya Vizuri mara baada ya kupewa jukumu la kuwa kocha wa muda wa timu hiyo akirithi mikoba ya kocha Machachari Joseph Mourinho ambaye akuweza kufanya vyema na kikosi hicho na kuwafanya mashabiki wa klabu hiyo kuwa na gazabu kubwa mno.



Ole Gunnar Solskjær (alizaliwa Kristiansund 26 Februari 1973) ni mchezaji wa soka wa zamani wa Norway. Alicheza mara nyingi kama mshambuliaji katika timu ya Manchester United iliyopo nchini Uingereza katika jiji la Manchester,. Pia alichezea timu ya taifa ya Norway

Solskjær alijiunga na Manchester United mwaka 1996 kwa ada ya uhamisho wa £ 1.5 milioni. Alicheza mechi 366 kwa klabu hiyo na akafunga mabao 126 wakati wa mafanikio kwa klabu hiyo. Mwaka 1999, alifunga mabao manne kwa dakika kumi na mbili dhidi ya Nottingham Forest.
Pamoja na Manchester United, Solskjær alishinda Ligi Kuu mara sita na Kombe la FA mara mbili. Alifunga bao la ushindi katika mechi ya fainali ya UEFA mwaka 1999.
Mnamo 2007, Solskjær alitangaza kustaafu soka baada ya kushindwa kupona majeraha makubwa ya magoti. Hata hivyo, alibakia Manchester United katika jukumu la kufundisha na pia katika uwezo wa balozi. Mwaka 2008Solskjær akawa meneja wa timu ya hifadhi ya klabu.

RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KUKAGUA KAZI YA UPAKAJI WA RANGI NDEGE YA FOKER 50 ILIYOKUWA IKITUMIWA KUBEBA VIONGOZI

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Mhandisi Julius Ndyamukama wakwanza (kushoto) pamoja na Richard Mayongela watatu kutoka (kushoto) ambaye uteuzi wake ulitenguliwa hivi karibuni wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kukagua kazi ya upakaji wa rangi katika ndege aina ya Foker 50 iliyokuwa ikitumika kubeba Viongozi wa Serikali ambayo sasa itatumika kubeba abiria wa kawaida katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ndege aina ya Foker 50 iliyokuwa ikitumika kubeba Viongozi wa Serikali na sasa itatumika kubeba abiria wa kawaida katika mikoa mbalimbali hapa nchini. Rais Dkt. Magufuli alizuia ndege hiyo kusafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya kazi hiyo ambapo ingegharimu zaidi ya Shilingi milioni 160 wakati kazi hiyo imefanywa na mafundi wa ndani kwa gharama ya shilingi miloni 7.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua sehemu ya ndani ya ndege hiyo ambapo ufungaji wa viti vipya umekamilika.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuka katika ndege hiyo aina ya Foker 50 iliyokuwa ikitumika kubeba Viongozi wa Serikali na sasa itatumika kubeba abiria wa kawaida katika mikoa mbalimbali hapa nchini. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wafanyakazi mbalimbali wa Shirika la ndege la Air Tanzania hawapo pichani wakati akitoka kufanya ukaguzi wa kazi ya upakaji rangi pamoja na uwekaji wa viti vipya katika ndege hiyo aina ya Foker 50.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkurugenzi wa ATCL Ladislaus Matindi wakati wa Ukaguzi wa ndege hiyo aina ya Foker 50

Sehemu ya Ndani na nje ya  Ndege hiyo ya Foker 50 ambayo kazi ya ufungaji wa viti vipya kutoka 32-48 umekamilika na kazi ya upakaji wa rangi ikielekea ukingoni. Hapo  awali ndege hiyo ilikuwa iende nje ya nchi kwa ajili ya kupaka rangi na kuchora ndembo ya twiga kwa gharama zaidi ya Shilingi milioni 160 kabla ya Rais Dkt. Magufuli kutoa maagizo kazi hiyo ifanyike nchini na mafundi wa ATCL ambapo gharama yake ni Shilingi miloni 7. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mafundi wazalendo ambao wamefanya kazi ya kuandika na kuchora nembo ya Twiga pamoja na kupaka rangi ndege hiyo ya Foker 50 kwa gharama ya  Shilingi milioni 7. Pia Rais Dkt. Magufuli amewazawadia mafundi hao kiasi cha Shilingi milioni 10 kutokana na kazi yao nzuri ya kizalendo walioifanya.  PICHA NA IKULU

SAMATTA KUUTANGAZA UTALII WA TANZANIA KIMATAIFA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Bodi ya Utalii Tanzania(TTB), Ipo katika hatua za mwisho za Mazungumzo na Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Klabu ya Genk iliyopo nchini Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta kuwa Balozi wa kutangaza Utalii wetu Kimataifa.

akziungumza na Waandishi wa habari Mapema leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Muendeshaji wa Bodi hiyo, Devotha Mdachi amesema kuwa katika hatua ya kutangaza utalii kimataifa wameona wamtumie Mbwana Samatta.

"wote tunajua umaharufu wa Mchezaji wetu katika ligi ya ubegiji na soka la barani ulaya kwa sasa hivyo katika Malengo yetu ya kutumia watu maharufu ambao ni Vijana wa kitanzania tumezungumza na Mbwana Samatta na ametuambia kuwa ifikapo mwezi May atakapokuja katika mapumziko yake kila kitu kitakamilika"anasema Mdachi.

ametaja kuwa mbali ya Mbwana Samatta wapo wasanii wengi na Vijana Maharufu ambao wanataraji kuwafikia hili wawe mabalozi wa utalii wetu nchini lakini kwa kuanzia wameanza na Samatta pamoja na Miss Tanzania .

Samatta atakuwa Kijana wa Pili wa Kitanzania Mwenye Mafanikio ambaye atapata nafasi ya kuwa balozi wa TTB ambapo ametanguliwa na Miss Tanzania 2018/2019 Queen Elizabeth Mukune ambaye amesaini Mkataba leo.

--

OSHA YAPONGEZWA KWA UTENDAJI

$
0
0
Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi umepongezwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi ili kusaidia nguvu kazi iliyopo kutumika kuchochea maendeleo.

Akizungumza wakati wa semina kwa wabunge wa Kamati hiyo iliyofanyika Machi 27, 2019 katika Bungeni Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Mohamed Mchengelwa amesema kuwa  Wakala huo umeonesha mfano bora katika kutekeleza majukumu yake na pia kwa kuwajengea uwezo wabunge  kuhusu masuala ya usalama mahala pa kazi na umuhimu wake katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

 “Elimu tuliyopata ni muhimu kwetu na kwa wananchi hivyo pamoja na kazi nzuri mnayofanya ni vyema sasa elimu hii ikatolewa kwa wananchi wote na wabunge kwa ujumla ili kusaidia kupunguza athari zinazotokana na kukosekana kwa elimu kuhusiana na masuala ya Usalama Mahali Pa Kazi ikiwemo namna ya kutoa huduma ya kwanza,” alisisitiza Mchengelwa

Akifafanua amesema kuwa katika masuala ambayo Kamati hiyo imetoa ni pamoja na kuongeza kiwango cha utoaji wa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wabunge wanapata uelewa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya OSHA.

Aliongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa wakuwajengea uwezo wabunge kama wawakilishi wa wananchi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

“Lengo letu kama Serikali ni kuhakikisha kuwa tunalinda nguvu kazi iliyopo ili iweze kusadia katika ujenzi wa uchumi wa viwanda na maendeleo ya Taifa kwa ujumla,” alisisitiza Mavunde

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi. Khadija Mwenda amesema kuwa wameandaa semina hiyo kwa wabunge ili kuwajengea uwezo wa kujikinga na athari za ajali au panapotokea mgonjwa anayehitaji kupata msaada wa huduma ya kwanza katika mazingira yao ya kazi na mengine yanayowazunguka.

Aliongezea kuwa OSHA itaendelea kutoa elimu kwa umma ili kujua namna bora za kujilinda na kujiepusha na madhara yanayoweza kuwapata wawapo kazini pamoja na mazingira yote yanayowazunguka kwa kuzingatia misingi ya elimu ya utoaji wa huduma ya kwanza endapo kunatokea dharula au majanga kazini.

“Tumejipanga kuwafikia watanzania kwa wingi wao ili kutoa elimu kwa umma juu ya masuala ya Usalama mahala Pa Kazi kwa kuzingatia unyeti wa masuala hayo kwani ni muhimu wananchi wakaelewa namna bora za kujilinda kuepuka madhara wawapo kazini,”alisema Bi.Mwenda

OSHA imekuwa ikiwajengea uwezo makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo wabunge na wananchi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuilinda nguvu kazi iliyopo kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi Bi. Khadija Mwenda akieleza umuhimu wa kuzingatia kanuni za kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa au mtu aliyepata ajali wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Machi 27, 2019 Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Mafunzo na Tafiti na Takwimu kutoka Wakala wa Afya na Usalama mahala pa Kazi (OSHA) Joshua Matiko akiwasilisha mada wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wabunge ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuongeza tija.
 Mkurugenzi wa Mafunzo na Tafiti na Takwimu kutoka Wakala wa Afya na Usalama mahala pa Kazi (OSHA) Joshua Matiko akiwasilisha mada wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wabunge ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuongeza tija.
 Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakifuatilia semina ya kuwajengea uwezo kuhusu majukumu ya OSHA leo jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. David Mathayo akichangia jambo wakati wa mafunzo hayo.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

TANGAZO LA MAFUNZO YA KILIMO NCHINI ISRAEL

$
0
0


UTANGULIZI



Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa TanzaniakupitiaWizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inatangaza mafunzo katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini Israel. Mafunzo hayo ni ya miezi 11 kuanzia mwezi Septemba, 2019 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Serikali ya Israel kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mafunzo hayo yatahusisha pia vitendo (field attachment) kwenye mashamba makubwa ya mazao mbali mbali yakiwemo ya matunda, mbogamboga, ufugaji, uvuvi na mazao mengine ya biashara kwa ujira maalum. 

SIFA NA VIGEZO VYA MWOMBAJI


 

     i.     Awe ni raia wa Tanzania mwenye umri wa kati ya miaka 20-35 pamoja na cheti cha            kuzaliwa na Kitambulisho cha Uraia.  
 ii.        Awe amehitimu mafunzo ya Kilimo katika ngazi ya shahada ya Chuo Kikuu,                         Stashahada au Astashahada ya Vyuo vya kilimo vinavyotambulika nchini. 
iii.        Awe na afya njema.  
iv.        Awe na ujuzi wa kuandika na kuongea lugha ya Kiingereza.   
 v.        Awe na uwezo wa kufanya kazi na watu wa tamaduni mbalimbali.  
vi.        Awe tayari kurejea nchini baada ya mafunzo yake.         

NAIBU SPIKA AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR)

$
0
0
 Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson akifungua kikao cha Tano cha Kamati ya Demokrasia na Utawala cha Baraza la Wabunge wa Mabunge ya Jumuiya ya nchi za Maziwa makuu (FP-ICGLR) kilichofanyika hii leo Jijini Arusha. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kikao cha Tano cha Kamati ya Demokrasia na Utawala bora cha Baraza la Wabunge wa Mabunge ya Jumuiya ya nchi za Maziwa makuu (FP-ICGLR) kilichofanyika hii leo Jijini Arusha. (Picha na Ofisi ya Bunge)

UPASUAJI WA ESTER BULAYA WAKWAMISHA KESI YA UCHOCHEZI INAYOWAKABILI VIGOGO TISA CHADEMA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya Jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuanza kusikiliza kesi ya uchochezi inayowakabili vigogo tisa wa Chadema), akiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe kutokana na kutokuwepo kwa mbunge Aster Bulaya kwani amefanyiwa upasuaji.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi ameeleza hayo leo Machi 28,2019, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo kesi hiyo ilikuwa inatakiwa kuanza kusikilizwa na kwamba wana mashahidi wawili na wako tayar lakini mshitakiwa Bulaya hayupo mahakamani.

Hata hivyo, Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala amedai mahakamani hapo kuwa Bulaya ana matatizo ya kiafya lakini ameridhia kesi hiyo kuendelea kusikilizwa bila ya yeye kuwepo.

Kutokana na hayo, mdhamini wa Bulaya, Ndeshukurwa Tungaraze amedai mshitakiwa huyo amefanyiwa upasuaji Machi 26, mwaka huu hivyo kutokana na hali yake ameshindwa kufika mahakamani.

Wakili Nchimbi amedai kama mshitakiwa ameridhia kesi hiyo iendelee kusikilizwa anatakiwa awasilishe taarifa kwa maandishi kuonesha kuridhia kwake.

Hakimu Simba amekubaliana na hoja za upande wa mashtaka, hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 17, 2019 kwa ajili ya kusikilizwa.

Mbali ya Mbowe washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu Taifa Dk.Vincent Mashinji , Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa Zanzibar Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Katibu Mkuu Taifa Vicent Mashinji, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, John Heche na Mbunge wa Bunda Ester Bulaya.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama ambapo wote wanadaiwa kuwa February 1 na 16, 2018, Dar es Salaam walikula njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

MGUNDUZI WA VIDONDA VYA TUMBO HUYU HAPA, ALIMEZA BAKTERIA KUWEZA KUTAFUTA DAWA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

DAKTARI Barry Marshall  ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Nobel aliyoipata kutokana na kugundua chanzo cha vidonda vya tumbo kwa kufanya majaribio katika mwili wake.

Wataalamu wengi wa Afya miaka ya nyuma waliamini kuwa bacteria hawezi kuishi ndani ya tumbo la mwanadamu kutokana na joto pia tindikali na asidi iliyopo humo. Hivyo basi iliaminika kuwa ugonjwa wa vidonda vya tumbo unatokana na mawazo au kutokula kwa muda mrefu.

Dkt. Barry akiwa na miaka 32 aligundua kuwa vidonda vya tumbo husambazwa na bacteria anayeitwa Helicobacter pylori na alipojaribu kuwashirikisha wataalamu wengine alipingwa  na hakuna aliyeamini kuwa bacteria huyo anaweza kuishi katika tumbo la binadamu kutokana na mazingira ya tindikali.

Barry Hakukata tamaa aliendelea na majaribio ili kuweza kugundua dawa ya kutibu kabisa vidonda vya tumbo na alipokwama ni jinsi ya kufanya majaribio, kwani taratibu hazikumruhusu kujaribu nadharia zake za bacteria anayepelekea vidonda vya tumbo. 

Daktari huyo  alifanya maamuzi magumu ya kuwameza vimelea hao wajulikanao kama Helicobacter pylori, chini ya uangalizi wa rafiki yake aitwaye Robin Warren na
baada ya wiki kadhaa alikuwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Hii iliwahadaha walimwengu wa wataalamu wa afya, na alipojaribu kutumia dawa alizoziandaa mwanzo hazikufanya kazi. Akiwa mgonjwa sana hatimaye aligundua antibayotiki inayotibu vidonda vya tumbo. 

Ilipofika mwaka 2007 alitunukiwa tuzo ya ya Nobel kwa ujasiri huo uliohatarisha maisha yake.

RAIS MAGUFULI APOKEA RIPOTI YA TAKUKURU, AMWAPISHA BALOZI WA TANZANIA NCHINI CUBA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Valentino Longino Mlowola kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 28, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi baada ya kumuapisha Kamishna Valentino Longino Mlowola kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 28, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna Diwani Athumani na akiwa na Naibu wake Brigedia Jenerali John Mbungo pamoja na  Kamishna Valentino Longino Mlowola  baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kupokea Ripoti ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 28, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna Diwani Athumani Ripoti ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 28, 2019. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya  kupokea vitabu vya Ripoti ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 28, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza baada ya kumuapisha Kamishna Valentino Longino Mlowola kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 28, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kumuapisha Kamishna Valentino Longino Mlowola kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kupokea Ripoti ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 28, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna Diwani Athumani na Naibu wake Brigedia Jenerali John baada ya kumuapisha Kamishna Valentino Longino Mlowola kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kupokea Ripoti ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 28, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Kamishna Valentino Longino Mlowola baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kupokea Ripoti ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 28, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya kumbukumbu na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna Diwani Athumani na Naibu wake Brigedia Jenerali John Mbungo pamoja na  Kamishna Valentino Longino Mlowola  baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kupokea Ripoti ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU pamoja na Makamanda wa Mikoa Yote na Maafisa Waandamizi wa TAKUKURU kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 28, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna Diwani Athumani na Naibu wake Brigedia Jenerali John Mbungo pamoja na  Kamishna Valentino Longino Mlowola  baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kupokea Ripoti ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 28, 2019.
PICHA NA IKULU

TFS YATAJA HATUA ZA KUCHUKUA KUKABILI ATHARI ZA UHARIBIFU WA MAZINGIRA NCHINI

$
0
0





*Yazungumzia Maadhimisho ya Siku ya upandaji miti itakayofanyika Aprili Mosi

*Kitafaifa kufanyika Wilaya ya Same mkoani Kimanjaro.... yatoa mwito kwa jamii



Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umesema ili kukabiliana na athari za uharibifu wa misitu ipo haja ya kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na hali hiyo ikiwemo ya kila familia kuanzisha bustani ndogo yenye miche inayoweza kutoa kivuli na matunda ambayo inayolingana na idadi ya wanafamilia.

Ambapo hiyo itakuwa rahisi kuitunza miche hiyo kwa kutumia maji yanayopatikana nyumbani au kutumia umwagiliaji wa matone ya maji kwa kutumia chupa (drip irrigation).

Hayo yamesemwa kwenye taarifa ya TFS iliyotolewa leo Machi 28,2019, kuelea Maadhimisho ya Siku ya Upandaji Miti ambayo ni Aprili 1 na kitaifa maadhimisho ya siku hiyo yatafanyika wilayani Same mkoani Kilimanjaro ambayo yatakwenda ambamba kwa ngazi ya mikoa yote Tanzania Bara kupanda miti.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tulizo Kilaga amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu ni ya kipekee kwa kuwa ni mwaka ambao utaratibu wa kuadhimisha siku hiyo utafanyika kwa kupanda miti zaidi badala ya kutumia fedha nyingi katika sherehe ya maazimisho ya siku hiyo. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni 'Tanzania ya Viwanda inawezekana, panda miti kwa maendeleo ya Viwanda'.

Akifafanua zaidi kuhusu hatua nyingine za kuchukua kukabiliana na athari za uharibifu wa misitu ni kuongeza kiwango cha upandaji miti kwa kupanda mbegu moja kwa moja ardhini kwa baadhi ya miti hasa katika mikoa iliyo na maeneo yenye mvua nyingi ikiwqepo Mikoa ya Tanga, Iringa, Mbeya na Njombe.


Pia kustawisha miti kwa kutumia miche inayojiotea yenyewe ardhini kama maotea. Miche hiyo inapandwa katika sehemu zilizokusudiwa ikiwa bado midogo. Njia hii inatumika hasa kwenye sehemu zenye mvua nyingi na udongo tifutifu.

Kilaga amesema ni vema kustawisha misitu ya asili kwa kutenga na kulinda eneo kutokana na uharibifu wa kimazingira ili mbegu ziote zenyewe (natural regeneration).Njia hiyo imefanikisha shughuli za kustawisha misitu na malisho ya mifugo mkoani Shinyanga na kwamba wananchi wa Shinyanga wanatumia utaalam wao wa jadi unaojulikana kwa jina la Ngitili wa kutenga maeneo na kuyapumzisha ili mbegu zijiotee zenyewe, matokeo yake mkoa huo umeongeza zaidi ya hekta 500,000 za ardhi ambayo ilikuwa imeharibika kabisa hapo awali lakini sasa ina miti.

Pia kuanzisha mashamba makubwa ya miti kwa lengo la kutunza mazingira na kujiongezea kipato na kwmaba katika kuadhimisha siku hiyo TFS itapanda miti katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa kushirikiana na wadau ambapo katika jiji la Dar es Salaam upandaji huo utafanyika eneo la Kilongawima Mbezi Beach kwa kupanda mikoko na mivinje.

"Wadau na wananchi wote mnakaribishwa kushiriki zoezi hili muhimu kwa mstakabari wa nchi yetu. Maadhimisho ya Siku ya Taifa ya kupanda miti yalifanyika kwa mara ya kwanza Januari Mosi mwaka 2001 kutokana na Waraka wa Waziri Mkuu namba 1 wa mwaka 2000 na kuhuhishwa mwaka 2009 na kuifanya siku hiyo kufanyika Aprili Mosi kila mwaka ukimtaka kila mwananchi kupanda miti kwa manufaa yake.

"Mwaka jana Siku ya Taifa ya Kupanda Miti iliadhimishwa kitaifa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Aprili 3 hadi 5, 2018.Ni wajibu wa kila mmoja wetu kutathimini athari atakazopata kutokana na ufyekaji na uharibifu wa misitu ili aamue kwa dhati kuihifadhi misitu kwa ajili ya kuwanufaisha watu wa kizazi hiki na vizazi vijavyo,"amesema.

Kuhusu maadhimisho ya siku hiyo ya upandaji miti ,Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania unatoa mwito kwa kila Mtanzania kutathmini tulikotoka, tulipo na tunapokwenda kuhusiana na hali ya misitu.

DAWASA YATATUA ASILIAMIA 70 YA MALALAMIKO KATIKA WIKI YA JAMII

$
0
0
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam imetatua asilimia 70 ya malalamiko yaliyotolewa na wananchi kwenye maadhimisho ya wiki ya maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Maadhimisho ya wiki ya maji yalifanyika kuanzia Machi 16-22 mwaka huu kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DAWASA Bi Neli Msuya amesema kuwa jumla ya wakazi zaidi ya 400 waliweza kufika  kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja na kutoa maoni na malalamiko mbalimbali yaliyolenga kuboresha huduma za DAWASA.

Amesema,  kwenye maadhimisho ya mwaka huu waliweza kufungua dawati maalum la kupokea taarifa, kero, malalamiko na maoni ya wananchi juu ya huduma zinazotolewa na DAWASA na kwa asilimia kubwa hilo limefanikiwa.

Msuya amesema, kwenye dawati maalum kulikuwa na wataalamu wa DAWASA wa fani mbalimbali na kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwasikiliza wananchi waliojitokeza kwenye Maadhimisho hayo.

"Kwanza napenda kuwashukuru wateja wote na wananchi kwa ujumla waliojitokeza kuungana na Mamlaka katika maadhimisho ya wiki ya maji yaliyofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja kwa Mkoa wa Dar es Salaam na wameweza kutoa kero, maoni na ushauri mbalimbali ambapo asilimia 70 ya malalamiko tumeshafanyia kazi na zingine zipo kwenye hatua ya ufuatiliaji kwenye idara husika," amesema Msuya.

Ameeleza kuwa, DAWASA wamedhamiria kuboresha utaratibu wa kupokea maoni kwa wateja ikiwa ni pamoja na kuwa na dawati linalohama kutoka eneo moja hadi lingine litakalojulikana kama 'mobile customer care desk' ili kufikia wakazi wengi na kupokea maoni mengi zaidi kwa lengo la kuboresha huduma kwa wananchi wanaohudumiwa na DAWASA.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso alipotembelea maonyesho ya Mamlaka ya Majisafi na majitaka DAWASA akiwa pamoja na wananchi waliofika kwa ajili ya kupata maelezo mbalimbali kuhusiana na Mamlaka hiyo kwenye dawati la Afisa wa DAWASA.

KWA TANESCO HII MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU...

$
0
0


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MACHO yangu yanashuhudia kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Shirika la Umeme  Tanzania(TANESCO) chini ya Wizara ya Nishati kwa niaba ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli.

Kubwa zaidi masikio yangu kwa miaka miwili sasa yamekuwa yakisikia sifa zikitolewa kwa TANESCO kwasababu tu yale mambo ya kukatika katika kwa umeme yamepungua .Tulizoea kuita mgao.Mara umeme unatika...mara huooooo umerudi.Leo hii umeme ukikatika basi ni kwasababu maalumu na umma utakuwa umeshapata taarifa mapema.Mbona raha jamani.

Kwangu mimi najaribu kuiangalia TANESCO ya sasa na ile ya zamani.Kuna tofauti kubwa ya kiutendaji.TANESCO ya sasa chini ya Mkurugenzi Mtendaji wake Dk. Tito Mwinuka inajua umuhimu wa nishati ya umeme.Inajua kabisa uchumi wetu unahitaji uwepo wa umeme wa uhakika katika kufanya shughuli zao za kila siku.

TANESCO inayoongozwa na Dk.Mwinuka inajua umuhimu wa kutoa taarifa kwa wananchi hasa pale ambapo kutakuwa na matenengezo katika eneo fulani.TANESCO ya sasa inajua kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inataka kuelekea uchumi wa kati ambao utachagwiza na umeme wa uhakika.

Pia inatambua fika kama kuna eneo ambalo lilikuwa linalalamikiwa ni kukatika kwa umeme.Mgao wa umeme ulikuwa kero kwa watu wengi.Tena kero haswaa na najua sio kwangu tu hata kwako.Ndio mgao ilikuwa kero.Unabisha?

Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutambua nchi yoyote ili iendelee inahitahaji kuwa na nishati ya umeme wa kutosha na uhakika.Ndio maana leo hii TANESCO inaendelea na ujenzi wa miradi mikubwa na midogo ya umeme ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake.

Kutekelezwa kwa miradi hiyo na hasa kwenye maeneo ambayo awali yalikuwa na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara leo hii hakuna tena mgao.Wananchi wanafurahia nishati hiyo ya umeme wa uhakika.Ukitaka kuamini hili inaloeleza hapa nenda mikoa ya Kaskazini ikiwemo ya Arusha na Kilimanjaro.Hawana tena tatizo la kukatika kwa umeme kama zamani.

Sote tunafahamu kabla ya Awamu ya Tano kuingia madarakani kulikuwa na changamoto kubwa ya umeme.Leo hii imebaki historia.Umeme unaozalishwa Mkoa wa Arusha umekidhi mahitaji na kufanya kuwepo na umeme wa akiba.Hivyo ninaposema TANESCO inastahili pongezi sio kwamba natoa sifa sehemu ambayo haistahili.

Hongereni TANESCO kazi ambayo mnaifanya kwa niaba ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kubwa na tunaiona. Pamoja na mambo mengine , TANESCO kwa sasa wanaendelea na majukumu ya kuendelea kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya nishati ya umeme.

Na si tu kuondoa changamoto,pia imeendelea na wajibu wake mkubwa kusambaza umeme kwa wananchi.Nafahamu jitihada za kupeleka umeme kwa kila kijiji ndani ya nchi yetu kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Naomba niwe mkweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu.Hakika Wizara ya Nishati na TANECSO wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha umeme unafika kwa kila Mtanzania anayeuhitaji.Kwa siku mbili hizi nimekuwa nikishuhudia baadhi ya nyumba tena za matembe zikiwa zimewekwa umeme.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukisikia tu, umeme unawekwa vijijini ila kwa bahati mbaya tupo baadhi yetu ni kama Tomaso.Bila kuona hakuna kuamini.Sasa tunaamini kumbe kweli.Hivyo uwepo wa picha hizo ambazo zinaonesha nyumba za udongo zikiwa zimewekwa umeme inaleta maana halisi ya kile ambacho Wizara ya Nishati inafanya kwa wananchi wake.

Tunafahamu kauli mbiu ya TANESCO imekuwa ikisema "Tunaangaza maisha" .Nimeamini hata uwe kijijini bado utaangaziwa maisha.Hili ni jambo jema na la kupongezwa.Umeme wa uhakika vijijini ni jambo la msingi sana, na tunafahamu kwa muda mrefu vijiji vyetu vilikosa maendeleo kwasababu ya kutokuwa na umeme.Leo wanao.

Kwa waliobahatika kuishi maeneo ya vijijini wanafahamu mazingira ya kutokuwa na umeme.Wana vijiji wanalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta nishati ya umeme.Ameaniaka mahindi au mpunga wake lakini linapofika suala la kusaga au kukoboa anawaza umbali wa kwenda mashineni.Leo hii hakutakuwa na kuwaza tena.

Umeme unapatikana kila mahali.Shida iko wapi? Hata hivyo, kuna baadhi ya watu kwenye mitandao nimeona wakijadiliana na wengine kuhoji kwanini umeme unawekwa kwenye nyumba za tembe ambazo kuta zake zinatengenishwa na udongo.Kwangu naona wanaohiji hayo ni kama vile wamekosa hoja.

Watalaam wamejiridhisha na wanajua hakuna madhara yoyote kwani kuna vifaa maalum vinavyotumika katika kuunganisha umeme kwenye nyumba hizo.Nitoe rai kwa Wizara ya Nishati pamoja na TANESCO endeleeni na majukumu yenu ya kuweka umeme vijijini.Kwa maisha ya sasa nishati ya umeme ambayo ni ya uhakika inahitajika sana kuliko nyakati nyingine zozote.Huo ndio ukweli.

Kwanini bibi na baba yangu waendelee kuteseka? Eti washindwe kuwa na luninga pale sebuluni kisa tu wapo kijijini.Eti waendelee tu kutumia vibatari .Hapana bwana lazima ifike mwisho.Walioko vijijini ni Watanzania na wana haki ya kupata umeme kama wengine wanaoishi maeneo ya mijini.

Tunafahamu kuna baadhi ya familia ambazo ziko mjini na zilishindwa kutembelea ndugu , jamaa na marafiki walioko vijijini na sababu tu ni kwamba eti wakienda huko hakuna umeme na wanasema hawawezi kutumia vibari.Kufungwa kwa umeme katika nyumba zetu za vijijini ambako wengi ndiko tunatokea, kunakwenda kufanya mabadiliko makubwa.

Mjini umeme upo na kijiji nako upo.Ukiishi kwenye ghorofa utakuwa na umeme na ukiishi kwenye nyumba ya tembe utakuwa na umeme.Hongereni TANESCO. Kufungwa umeme kwenye nyumba za vijijini kunakwenda kuifanya Tanzania kuwa yenye maendeleo.Kokote Mtanzania alipo na anahitaji umeme kwa ajili ya ujenzi wa maendeleo ya nchi yetu.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameizindua nyumba ya Rose Kagoma iliyounganishiwa umeme wa REA katika Kijiji cha Ruganga Wilayani Kibondo.Katika hafla hiyo iliyofanyika Machi 24 mwaka huu, Waziri Kalemani amewataka Wandarasi kutokubagua Wananchi kwenye mradi huoKijiji cha Rugunga kimeunganishiwa umeme kupitia mradi wa umeme Vijijini wamu ya tatu sehemu ya kwanza(REA)

SELOU MARATHON KUFANYIKA KWA MARA YA KWANZA MKOANI MOROGORO AGOSTI 25 MWAKA HUU

$
0
0
Na Agness Francis, blogu ya jamii.

UZINDUZI wa maandalizi ya mbio za riadha Selou marathon umefanyika leo ambapo itakuwa ni mara ya kwanza kufanyika mkoani Morogoro agosti 25 mwaka huu, lengo likiwa ni kukuza utalii wetu wa ndani na nje ya nchi pamoja na kujenga afya.

Mgeni rasmi ambaye ni muaakilishi wa mkurugenzi wa baraza la michezo Taifa Neema Msitu, akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi huo leo Jijini Dar es Salaam ambapo ametoa wito kwa watanzania kujitokeza kushiriki mbio hizo za Selou marathon itakayofanyika mkoani Morogoro pamoja na kushiriki michezo yote kwa ujumla.

"Michezo inajenga mwili na afya na kutupa uhai hivyo basi watanzania tuweke utamaduni wa kufanya mazoezi,pia tukijumuika kwa pamoja kushiriki mbio hizo tutakuza utalii wetu na uchumi pia"amesema Neema Msitu.

Aidha mratibu wa Mratibu wa Selou Marathon Rehema Jonas amesema kuwa uzinduzi wa mbio hizo inahazina kubwa ya watu wanaopenda michezo na kwa kutambua hilo wameamua kuchukua jukumu la kuandaa mbio za riadha mwaka huu mkoani morogoro.

"Morogoro ni Mkoa unaofikika kiurahisi zaidi nataraji watu wengi kutoka sehemu mbali mbali watajitokeza kuja kujumuika nasi mbio ambazo zitaanzia kilimota 21,kilomita 10,kilomita 5 ambazo ni za furaha pamoja na mbiao za kilomita 2 na nusu kwa ajili ya watoto." amesema Mratibu huyo.

Hata hivyo mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Selou marathon Emmanuel Kajula pia ameongezea kuwa lengo la kuandaa mbio hizo ni kutaka kuchochea na kukuza maendeleo ya mbio za riadha nchini Tanzania, ambapo ameeleza kuwa maendeleo ya mchezo huo hautafika mbali kama hakutakuwepo na waandaaji wa uhakika.

Nao mabalozi wa Selou marathon Msanii wa kizazi kipya Barnaba boy pamoja na mchekeshaji Tabu mtindiga wametoa wito kwa wasanii na vijana wenzao kuunga mkono mandalizi ya mbio hizo mpaka zitakapofikia kilele chake agosti 25 mwaka huu.
Mgeni rasmi  ambaye ni  muaakilishi wa mkurugenzi wa baraza la michezo Taifa Neema Msitu,akikata utepe akiashiria maandalizi ya uzinduzi wa Selou Marathon yamezinduliwa rasmi leo Jijini Dar es Salaam
 Mgeni rasmi  ambaye ni  muakilishi wa mkurugenzi wa baraza la michezo Taifa Neema Msitu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Selou Marathon leo Jijini Dar es Salaam ambapo mbizo hizo zitafanyika Mkoani Morogoro agosti 25  mwaka huu.
 msanii wa kizazi kipya Barnaba boy, ambaye pia mi balozi wa mbio za Selou marathon  akizungumza na vyombo vya habari  wakati wa uzinduzi huo leo Jijini  Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA AKAUNTI YA TABASAMU

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Tano imefanya jitihada kubwa kuweka mazingira mazuri ya kisera na kimifumo ili kuchochea ukuaji wa sekta ya fedha hapa nchini.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Akaunti ya TABASASMU, iliyozinduliwa leo na Benki ya Posta jijini Dar es Salaam.

“Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania imeendelea kutoa miongozo mbalimbali ili kuhakikisha watanzania takribani asilimia 50 wanafikiwa na huduma za kibenki ifikapo Mwaka 2025”alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amependezwa na wazo la kuhakikisha kuwa kupitia akaunti ya TABASAMU wanawake watauziwa bima za kijamii.

Benki ya Posta ina matawi takriban 80, ATM 54, mtandao wa Umoja Switch takriban 200 na mawakala 150 kupitia Shirika la Posta ambapo Makamu wa Rais ameitaka benki hiyo kuwafikia wanawake wengi haswa vijijini na kuhakikisha wanapata huduma na elimu ya masuala ya kifedha.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa wanawake ni nguzo kuu ya uchumi wetu, kwani wao ndiyo wazalishaji wakuu kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa. Mbali ya kulea familia, huwezi kuwakosa wanawake kwenye sekta yoyote ya uzalishaji mali, na hivyo siyo upendeleo kuanzisha akaunti maalumu ya TABASAMkwa wanawake, bali ni haki yao ya msingi kama ilivyofanya benki ya TPB.

Makamu wa Rais amewataka Akaunti ya TABASAM inashirikiana na makampuni ya simu kuhakikisha kuwa wanawake hawa si tu wanapata taarifa za kibenki hata ikiwezekana kuweza kupata huduma za kibenki kama mikopo kupitia simu zao za mikononi. 


Wakati huo huo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amesema Tanzania ina rekodi nzuri Afrika na duniani kwa ujumla katika masuala ya huduma za kifedha 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Akaunti ya TABASAMU uliofanyika katika ukumbi wa Kisenga, jengo la LAPF jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua rasmi  Akaunti ya TABASAMU uliofanyika katika ukumbi wa Kisenga, jengo la LAPF jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Dkt. Edmund Mndolwa (kulia) wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Akaunti ya TABASAMU uliofanyika katika ukumbi wa Kisenga, jengo la LAPF jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Picha ya pamoja 
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images