Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

SIMBA, LIPULI NANI KUVUNJA REKODI YA KUMFUNGA MWENZAKE

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Simba SC kesho watashuka dimbani wakiwa ni wageni kumenyana na Wanapaluhengo Lipuli FC katika mchezo wa marudiano wa raundi ya pili msimu huu 2018/2019.

Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na shauku kubwa utapigwa katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa majira ya saa kumi za jioni huku kiingilio kikiwa  VIP kwa bei 10000, Mzunguko 5000 na Watoto kwa 2500.

Sio Simba wala Lipuli wanaitaji matokeo mazuri ya alama tatu dhidi ya mwenzake  kujiweka sehemu nzuri katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo msimu uliopita 2017-18 hakuna timu iliyomfunga mwenzake baada ya timu zote kushindwa kufungana kwa kutoka sare ya bao 1-1 katika Mchezo wa nyumbani na ugenini, Msimu huu 2018-19 wameendeleza rekodi ya kutofungana kwa kutoka 0-0 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Simba walipowakaribisha Lipuli FC.

Katika Msimamo wa Ligi Kuu Simba ikiwa nafasi ya 3 ikiwa na alama 45 na michezo 18, Yanga wao wakiwa Vinara wa Ligi hiyo wakiwa na alama 61 michezo 25, wakifuatiwa na Azam FC wenye alama 50 akiwa ameshacheza  michezo 25 pia, Lipuli FC ambao wanakibarua kizito cha kufuana na Simba kesho wao wapo nafasi ya 5 wakiwa na pointi 38 na michezo 27.

Nani atavunja mwiko Simba au Lipuli kwa kumfunga mwenzake mara hii?ukizingatia Wekundu hao wa Msimbazi wapo kwenye kasi na Safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Emmanuel Okwi pamoja na  Middie Kagere ambaye amekuwa hatari zaidi kwa kufumania nyavu za wapinzani.

Huku Wanapaluhengo wakionekana kupoteza mchezo  wake wa mwisho aliocheza Stand United ambapo alikula kichapo cha bao 3-2 akiwa ugenini,

Simba SC wao waliendeleza rekodi yake ya kufanya vizuri baada ya kumfunga Yanga hivyo kupata morali zaidi ya kuendelea kufanya vema ambapo pia katika michezo wake wa mwisho uliopigwa februari 22 Mwaka huu katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam alishinda bao 3-1 dhidi ya wana lamba lamba  wa Chamazi Azam FC.

SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA WATU TISA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA GARI KUTUMBUKIA MTONI

$
0
0

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angela Mabula aongoza uagaji wa miili tisa (9) ya watumishi wa serikali pamoja na mfanya mfanyakazi mmoja wa Shirika la Plan International Morogoro.

Miili hiyo ya watumishi wa serikali kutoka wizara ya ardhi sambamba na mfanyakazi mmoja wa Shirika la Plan International imeagwa katika eneo la uwanja wa Tangani maarufu uwanja waTaifa Ifakara na kushuhudiwa na wananchi mbalimbali sambamba na viongozi wa Kitaifa ikiwemo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Wakuu wa Wilaya za kilombero, Malinyi pamoja na Ulanga ambapo katika msiba huo mratibu wa mradi wa Land Ternual Supporting Program (LTSP)Godfrey Machabe akasoma wosia wa watumishi hao na kubainisha umuhimu wa kazi waliokua wakifanya. Naibu Waziri wa Ardhi akibainisha serikali kugharamia shughuli zote za mazishi ambapo mpaka sasa serikali imeshatumia shilingi milioni 96 katika kuratibu.

Naibu Waziri Mabula amesema serikali itagharamia shughuli zote za mazishi ambapo mpaka sasa na kudai kuwa hadi kufikia hatua ya kuaga wametumia shilingi milioni 96 katika kuratibu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt.Kebwe Steven kebwe amewaomba wananchi kuwa watulivu na kuvitaka vyombo husika kufuatilia kwa makini na kujua chanzo cha ajali na kutenda haki inayohitajika.

 Naibu Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angela Mabula akiwa na kamati ya Ulinzi ya Mkoa wa Morogoro wakati ya uagaji wa Miili Tisa ya watumishi wa Wizara ya Ardhi waliofariki katika ajali ya gari kutumbukia katika mto Ifakara.

 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angela Mabula akizungumza katika uagaji wa Miili Tisa ya wafanyakazi waliopata ajali ya gari kutumbukia Mtoni
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Steven Kebwe akizungumza katika uagaji wa Miili Tisa ya wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi waliotumbukia  Mtoni.


 
 
 Waombolezaji katika uagaji wa Miili Tisa ya wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi.

MADAKTARI MOI NA CHINA WAENDESHA KAMBI YA UPASUAJI UBONGO, MGONGO NA MISHIPA YA FAHAMU

$
0
0
 Daktari bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu MOI Dkt Nicephorus Rutabasibwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika kambi ya upasuaji iliyofanywa kwa ushirikiano kati ya MOI na Hospitali ya Peking ya China
 Kiongozi wa jopo la madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Peking ya China Profesa Yuanli Zhao akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika kambi ya upasuaji iliyoendeshwa kwa ushirikiano kati ya MOI na hospitali ya Peking
Madaktari bingwa wa MOI pamoja na Peking ya China wakishiriki katika moja ya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye ubongo kwa kutumia darubini ya kisasa. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)



NA KHAMISI MUSSA.

Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu leo wameshirikiana na madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha nchini China kufanya upasuaji mkubwa wa kuondoa uvimbe kwenye Ubongo, upasuaji wa kuviba mishipa ya damu iliyopasuka kwenye ubongo pamoja na upasuaji wa mgongo

Upasuaji huu umefuatia ujio wa jopo la madaktari bingwa watatu wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu kutoka Hospitali ya chuo Kikuu cha Peking cha china ambao walipokelewa MOI tarehe 23/02/2019.

Akizungumza katika chumba cha Upasuaji MOI, Dkt Nicephorus Rutabansibwa amesema ushirikiano kati ya MOI na Peking utakuwa wenye manufaa makubwa kwani huduma za MOI zitaendelea kuwa bora na watanzania wataendelea kupata huduma hizo hapa nchini billa ya kwenda nje ya nchi.

“huu ni muendelezo wa ushirikiano tulioingia na wenzetu hawa wa Peking mwaka jana, tunaamini tutabadilishana uzoefu na wenzetu hawa ambao wamepiga hatua kubwa kwenye teknolojia ya matibabu, kupitaia ushirikiano huu mbinu tunazopata zitatusaidia kuendelea kutoa tiba bora na kwa wakati kwa wagonjwa wetu” alisema Dkt Rutabansibwa

Dkt Rutabansibwa amesema leo watawafanyia upasuaji wagonjwa 3 mmoja atafanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye ubongo kwa kutumia darubini ya kisasa, mwingine upasuaji wa mgongo na mwingine atafanyiwa upasuaji wa kuziba mishipa ya damu iliyopasuka kwenye kichwa.

Pia amesema ujio huu wa wataalamu kutoka peking umelenga kuweka mazingira bora ya ushirikiano na MOI ili watakapo kuja tena wajue ni maeneo gani yanahitaji kuwa kipaumbele kwenye ushirikiano.

Kwa upande wake kiongozi wa jopo la madaktari bingwa kutoka Peking Peking amesema ushirikiano kati ya MOI na Peking utakuwa wenye mafanikio makubwa na utawanufaisha wagonjwa pamoja na madaktari vijana ambao watapata fursa ya kusoma kenye chuo chao

“Tumefarijika kuja Tanzania, tumewaeleza hali halisi ya hospitali yet una vifaa tulivyonavyo, tunaamini kupitia ushirikiano huu wataalamu wa hapa watajifunza na pia tutatoa fursa kwa wataalamu 2- 3 kuja kujifunza kwetu” Alisema Profesa Zhao.

Kambi hii ni sehemu ya muendelezo wa mkataba wa ushirikiano uliosainiwa kati ya MOI, Chuo Kikuu cha MUHAS na Hospitali ya Peking ya China ambao umejikita katika ,Mafunzo ya muda mrefu na Mfupi, utafiti,tiba pamoja na uboreshaji wa miundombinu.

SERIKALI KUANZISHA MACHINJIO YA KUKU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii 
SERIKALI  imesema iko kwenye mikakati ya kisera ya kuanzisha sera ya kuwepo kwa machinjio ya kisasa ya ndege wafugwao hasa katika miji  mikubwa ili kuboresha sekta hiyo. 

Hayo yameelezwa leo na Mtafiti Mkuu wa Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. John Kaijage katika warsha ya siku moja ya kuangalia changamoto zinazoipata sekta ndogo ya ndege wafugwao iliyoandaliwa na taasisi inayotoa mikopo kwa Wajasiriliamali ya Victoria Finance iliyowakutanisha Wadau mbalimbali wa sekta hiyo ya mnyororo wa thamani kwenye ufugaji. 

Amesema kuwa, sekta ya ufugaji wa kuku inakua kwa kasi sana, sasa hivi kuna vituo vya kutotolesha vifaranga ,huku uzalishaji wa vifaranga ukiwa umeongezeka kwa kasi kubwa

"Katika harakati za kuboresha sekta hii,  serikali inataraji kuanzisha machinjio ya kuku na kila mtu anayefanya biashara za kuku akitaka kuchinja basi atalazimika kwenda kwenye machinjio na siyo kuchinjia nyumbani labda tu Kama mtu anachinja kale ka kula nyumbani Kwake". Amesema Dkt. Kaijage. 

Dkt Kaijage Amesema, lengo la Taifa kwa sasa hi kuzalisha Tani Za  nyama kwa wingi na mayai kuanzia BIL. 3 hadi BIL. 3.4 hadi ifikapo mwaka 2020.21.22.

Aidha ameongeza kuwa, lengo kubwa la kufanya hayo yote ni kuongeza ubora wa wanyama wafugwao ili kuweza kuyapeleka mazao hayo nje ya nchi, amesema Serikali pia inatarajia kuanzisha sheria nyingi ikiwemo  kuboresha kanuni za kuzuia magonjwa kwa mtu yeyote anayeanzisha shamba La kuzalisha kuku wazazi na vituo vya kutotoresha vifaranga na mawakala lazima wasajiliwe. 

Ameongeza kuwa, mikakati iliyopo sasa hivi ni kutengeneza chanjo za kideli ambapo kuanzia mwakani kuku wote wataanza kuchanjwa  na wameiomba Serikali ipunguze bei ya chanjo hiyo ili kutokomeza ugonjwa huo kabisa. 

"Pia tunafanya tafiti  ya kubaini kuku wanaoweza kumudu mazingira ya nchi yetu kwa vijijini na mijini na pia kuweza kusaidia au kuimarisha teknolojia ya kuwabaini kuku wetu wa asili ili tuweze kubaini kuku bora na baadae kutengeneza Kuku chotara," amesema.

Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Victoria Finance, Julius Mcharo amesema lengo la kukutana na Wadau hao ni kuzungumzia fursa na Changamoto mbalimbali za upatikanaji wa Mikopo, Mitaji katika kuendeleza Biashara ya ufugaji kuku.
Amesema sekta hiyo imekuwa ikikimbiwa sana na  watoaji mikopo, lakini wao Kama Taasisi ya kusaidia wafanyabiashara ndogo ndogo wameona umuhimu wa kusaidia hilo ili kuwakomboa wadau wa sekta hiyo katika nyonya mbali mbali kuanzia vifaa,  mitaji na mahitaji mengine mengi. 

 Amesema kuwa uzalishaji wa Kuku ni mkubwa Katika mkoa wa Dar es salaam huku Changamoto kubwa inayoikumba sekta hiyo ni  kwamba sekta hiyo ni  kukimbiwa sana na watoaji wa mikopo licha ya kuwepo kwa  uitikio  mkubwa. 

Amesema kuwa,  "naamini yale ambayo yatazungumzwa hapa yatasaidia sana kuendeleza. Tunataka kuwasaidia hawa wafugaji kwa kuwa  mazingira ya  ufugaji yanaridhika na Mkopo huu hautakuwa wa kutoa hela halafu zikaenda kutumika ndivyo sivyo, sasa hivi tutaangalia mahitaji ya mtu kutokana na mradi wake"
Ameongeza.

 Pia amesema kuwa wataalamu wa mifugo kwa kushirikiana na wakulima au wafugaji pamoja na wale watoa huduma watakuwa wakitembelea miradi hiyo ili kujua mahitaji na maendeleo yao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Victoria Finance, Julius Mcharo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua warsha ya siku moja na wadau wa sekta ndogo ya wanyama wafugwao. Amesema dhumuni kubwa la Wash hiyo ni fursa na Changamoto mbalimbali za upatikanaji wa Mikopo, Mitaji katika kuendeleza Biashara ya ufugaji kuku inayotolewa na Victoria Microfinace.

Tanzania moja ya nchi yenye mifumo imara ya udhibiti wa dawa ,vyakula pamoja na vipodozi

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Tanzania  imekuwa ni  miongoni mwa nchi 50 kati ya 194 duniani zenye mifumo imara na madhubuti ya udhibiti wa ubora wa bidhaa za vyakula, dawa na vipodozi kutokana na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kudhibiti bidhaa hizo.

Hayo ameyasema  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula leo wakati akifungua mafunzo ya siku Tano kwa wataalam wa udhibiti ubora wa Mamlaka ya Chakula na Dawa  Tanzania (TFDA), Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi (ZDFA)  pamoja na nchi ya  Malawi.

Dkt.Chaula amesema serikali ilianzisha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)  kwa ajili ya kudhibiti dawa ,vipodozi,vifaa tiba ,Chakula pamoja vitendanishi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za  afya.

Amesema mafunzo hayo maalum yameandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO-Tanzania) kwa lengo la kuwaongezea mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kuimarisha nchi hizo kuongeza nguvu ya udhibiti wa bidhaa hizo.Amesema kuwa usambazaji wa dawa katika soko umeendelea  na  viwango ya  ubora na salama mpaka katika hatua ya usajili.

Dkt.Chaula amesema serikali ilianzisha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)  kwa ajili ya kudhibiti dawa ,vipodozi,vifaa tiba ,Chakula pamoja vitendanishi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za  afya.

Amesema TFDA iko nafasi ya tatu katika udhibiti wa dawa na kufanya ni mamlaka ambayo imekuwa na mfumo wa udhibiti wa dawa hadi inamfikia mlaji. “WHO imetutambua na imetupa level (daraja) la tatu, hii ni hatua nzuri, TFDA imefanya kazi kubwa, hii inamaanisha mifumo ya udhibiti tanzania inatambulika duniani kote na kwamba misingi ya udhibiti ya mamlaka yetu imefikia ngazi ya kimataifa". Amesema Dkt. Chaula na kuongeza “Lakini pamoja na hatua hiyo lazima iendelee kujiimarisha ili ikiwezekana tupande daraja tufikie level 4 ambayo ndiyo kiwango cha juu zaidi".

 “Ili tuweze kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi, mamlaka yetu inapaswa kutengeneza mifumo ya ufuatiliaji ubora na usalama wa bidhaa kuanzia viwandani hadi kwa mtumiaji, ili kuhakikisha hakuna dawa bandia zinaingia nchini mwetu”.

 Akiwasilisha mada Dkt. Alireza Khadem Broojerdi kutoka WHO amesema ili kuongeza nguvu ya udhibiti nchi zinapaswa kushirikiana kwa ukaribu.

“Tunayo malengo 17 ya kidunia (SDGs), lengo namba tatu linasisitiza juu ya afya bora kwa wote, tunayo pia malengo ya mwaka 2019- 2030, mpaka sasa nchi 50 ikiwamo Tanzania sawa na asilimia 26 zimefikia daraja la tatu na nne. Nchi 45 sawa na asilimia 23 zipo daraja la pili, nchi 96 zimefikia daraja la kwanza na zingine zilizobaki bado hazijafikia viwango hivyo,” amesema Dkt. Khademu.

Amesema TFDA iko nafasi ya tatu katika udhibiti wa dawa na kufanya ni mamlaka ambayo imekuwa na mfumo wa udhibiti wa dawa hadi inamfikia mlaji.Nae Kaimu Mkurugenzi wa  TFDA, Dkt. Candida Shirima amesema kupitia semina hiyo iliyoandaliwa na WHO watajifunza mbinu mbalimbali  zitakazowasaidia kuweza kufikia malengo waliyojiwekea katika kuendelea kuimarisha mifumo ya udhibiti wa bidhaa hizo.

Amesema kuna mwanya wa utekelezaji baadhi ya changamoto katika nchi zinazoendelea  katika masuala ya usambazaji wa dawa.Dkt.Shirima amesema kuwa mafunzo hayo yatawaongezea uwezo wa kufanya vizuri na kufanya wananchi wapate huduma bora ya dawa katika usambazaji

Amesema kuwa TFDA inasajili bidhaa za dawa na kuangalia masoko ikiwa ni pamoja kulinda mipaka kwa dawa ambazo hajachunguzwa na Maabara kwa kuhakikisha haziingii katika soko.
 Viongozi wakisikiliza maada za wataalam katika mkutano wadau wa udhibiti.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Dkt Candida Shirima akizungumza katika mkutano wa wataalam wa udhibiti uliofanyika jijini Dar es salaam.
 Picha ya pamoja ya wataalam wa udhibiti na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto
 Dkt.Alireza Broojerd wa Shirika la Afya Duniani (WHO) akizungumza katika warsha wataalam wa udhibiti wa ubora wa dawa na Chakula kutoka Mamlaka za TFDA,ZFDA na Zambia ukifanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa wataalam wa udhibiti  uliofanyika jijini Dar es salaam.

Maafisa Utamaduni Jitokezeni kwa Wingi Kushiriki kikao Kazi - Katibu Mkuu Susan Mlawi

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Susan Mlawi (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma kuhusu Kikao Kazi cha Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote Nchini kitakachofanyika tarehe 27-28 Februari 2019 Jijini hapo.Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara hiyo Bw.Bonoface Kadili, na Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kikao hicho Bw.Francis Songoro.

Na Shamimu Nyaki –WHUSM.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Susan Mlawi ametoa wito kwa Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri nchini kushiriki kwa wingi katika kikao kazi cha sekta hiyo kitakachofanyika kuanzi tarehe 27 na 28 Februari 2019 Jijini Dodoma.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma, Mlawi ameeleza kuwa kikao hicho ni cha 11 kufanyika ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Umoja Upendo na Kazi :Asili ya Utamaduni Wetu” lengo ikiwa ni kuendeleza Sekta ya Utamaduni hapa nchini.

“Lengo la kikao kazi hichi ni kuweka mikakati ya pamoja katika kutekeleza Sera ya Utamaduni kwa ngazi ya Mikoa na Halmashauri pamoja na kuhamasisha ukuzaji na matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili ambayo ndio lugha inayotambulisha nchi yetu”. Alisema.

Ameongeza kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kikao kazi hicho anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe huku kikifungwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jaffo.

Aidha Mlawi amezitaja mada zitakazowasilishwa katika kikao kazi hicho ambazo ni Ubidhaishaji wa Lugha ya Kiswahili,Utendaji kazi Kimuundo baina ya Maafisa Utamaduni wa Wizara Mikoa na Halmashauri,Uhuishaji wa Sera ya Taifa ya Utamaduni,Fursa za Utalii wa Kiutamaduni nchini.

Mada nyingine ni Ufahamu Kuhusu Haki Miliki na Hakishiriki za Wasanii,Fursa ya Soko kwa Bidhaa za Utamaduni pamoja na Mada itakayohusu Umuhimu wa Sekta ya Filamu katika kuimarisha Asili na Utamaduni wetu.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Susan Mlawi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma kuhusu Kikao Kazi cha Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote Nchini kitakachofanyika tarehe 27-28 Februari 2019 Jijini hapo. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara hiyo Bonoface Kadili, na Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kikao hicho Bw.Francis Songoro.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Bonoface Kadili akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi.Susan Mlawi (Katikati) azungumze na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma kuhusu Kikao Kazi cha Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote Nchini kitakachofanyika tarehe 27-28 Februari 2019 Jijini hapo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kikao hicho Bw.Francis Songoro.

KIKAO CHA KAMATI YA ULINZI WA WANAWAKE NA WATOTO MKOA WA MARA KIICHOKUTANA KUPOKEA JUMBE MAALUM

SERIKALI YAKARABATI SHULE ZAKE KONGWE ZA SERIKALI ILI KUBORESHA ELIMU

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Kibaha
Serikali imetoa zaidi ya  sh. bilioni 42 kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya Sekondari 42 kati ya shule 88 kongwe zilizopo nchini kote ikiwemo shule ya Sekondari Ruvu iliyoko Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Akizungumza mara baada ya kukagua ukarabati wa shule hiyo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango. Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa shule zote Kongwe ambazo zinahistoria kubwa ya kutoa viongozi wengi na wataalam mbalimbali nchini, zinakuwa na hadhi na kuwa kimbilio la wananchi.
Ametoa wito kwa uongozi wa shule hiyo ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, kuhakikisha kuwa elimu bora inatolewa kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ili thamani ya uwekezaji mkubwa wa Serikali unaofikia zaidi ya shilingi milioni 990 uweze kuonekana
"Dhamira yetu ni kuona watoto wetu wanasoma kwenye mazingira sahihi na ufaulu wao unaongeeaka kwa sababu tunawaandaa wataalam wa kesho wa Taifa letu" Aliosisitiza Dkt. Kijaji
Alisema amejionea ukarabati uliofanyika shuleni hapo ambapo pamoja na shilingi milioni 992 kutumika katika ukarabati huo, bado nyumba 6 za walimu hazijakarabatiwa pamoja na kutonunuliwa kwa samani za shule vikiwemo vitanda na kuahidi kuifanyia kazi changamoto hiyo wakati wa huu wa mchakato wa bajeti mpya
Kwa upande wao, Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Juma na Mkuu wa Shule hiyo, Juliana Chimazi, wameishukuru Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha shule hiyo na kuomba wapatiwe fedha kwa ajili ya kununulia samani hasa vitanda kwa ajili ya wanafunzi ili kwenda sambamba na uboreshaji mkubwa wa majengo uliofanyika shuleni hapo.
Mkuu wa shule hiyo Mwl. Juliana Chimazi alimweleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji kwamba shule hiyo inahitaji vitanda vipya kwa kuwa vilivyopo vimedumu zaidi ya miaka 50 pamoja na kuomba fedha kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa nyumba sita za walimu.
Miongoni mwa miundombinu iliyoboreshwa katika shule hiyo ya Sekondari ya washichana Ruvu ni pamoja na mifumo ya maji taka, madarasa, vyoo, mabweni, nyumba za walimu na Ofisi.

Naibu Waziri Dkt. Kijaji anaendelea na ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali iliyopewa fedha na Serikali ikiwemo ya kimkakati inayolenga kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kujitekemea kwa mapato.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa viongozi wa Shule Kongwe ya Sekondari ya Wasichana Ruvu Mkoani Pwani, kuhakikisha maboresho ya shule hiyo yanakwenda sambamba na ufanisi katika utoaji taaluma, wakati alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua uboreshaji huo. Kulia ni Mbunge wa Kibaha Vijijini Mhe. Hamoud Juma na kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo Bi. Juliana Chimazi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kulia), akikagua maboresho ya Shule Kongwe ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani, wa pili kushoto ni Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Kibaha Bi. Fatuma Kisanazo, watatu kushoto ni Mbunge wa Kibaha Vijijini Mhe. Hamoud Juma na kulia ni Mkuu wa Shule hiyo Bi. Juliana Chimazi.
Muonekano wa Bweni la wanafunzi wa Shule Kongwe ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani, ambapo Mkuu wa Shule hiyo Bi. Juliana Chimazi, aliomba Serikali isaidie katika kuboresha miundombinu ya nyumba 6 za walimu ambayo haijakarabariwa baada ya fedha sh. milioni 990 kumalizika kabla ya kazi hiyo kukamilika.
Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Kibaha Bi. Fatuma Kisanazo, akitoa ufafanuzi wa namna walivyosimamia fedha za Serikali zilizotolewa kwa ajili ya kuboresha Shule Kongwe ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani, wakati wa ziara yua kikazi ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani Bw. Shaibu Mangalu, akielezea namna Shule hiyo ilivyotumia utaratibu wa shule hiyo kwa njia ya Force Account uliogharimu takribani Sh. milioni 992, wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipotembelea na kukagua maboresho hayo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa sita kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Viongozi na walimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani, ,baada ya kukagua uboreshaji wa miundombinu ya shule hiyo .Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango).

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 25.02.2019

MKOA WA LINDI WAAGIZWA KUSITISHA UMWAGAJI WA MAJI TAKA KATIKA DAMPO LA TAKA NGUMU

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bw. Shaibu Ndemanga mara baaya ya kufanya ziara ya kukagua dampo la Manispaa hiyo ili kujionea uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira. Katika dampo hilo lililopo eneo la Machole Manispaa ya Lindi Naibu Waziri Sima ameuagiza uongozi wa Mkoa kusitisha umwagaji wa maji taka katika eneo hilo.
Naibu Waziri Mussa Sima akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Mkoa wa Lindi mara baada ya kukamilika kwa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi. Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kimeweka mikakati ya kuhifadhi ikolojia ya vyanzo vya maji vinanvyochangia maji katika bonde la Rufiji
 
 
Na Lulu Mussa,LINDI .

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima ameuagiza Uongozi wa Mkoa wa Lindi kusitisha mara moja hatua ya kumwaga maji taka katika dampo la Halmashauri hiyo.Agizo hilo limetolewa hii leo Mkoani Lindi mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya kukagua uzingatiaji na Usimaimizi wa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004. 
 
Akiwa katika Halmashauri hiyo Mhe. Sima amejione uchafuzi mkubwa mazingira kwa Halmashauri ya Lindi kuchanganya taka ngumu na maji taka katika dampo moja na kuagiza uongozi wa Mkoa huo kusitisha mara moja utaratibu huo na kupiga marufuku wananchi kuingia kiholela katika dampo hilo.“Utaratibu wa kutofautisha taka uanzie nyumbani na katika sehemu za kukusanyia taka, taka zikiletwa hapa dampo ziwe zimeshachambuliwa, huu utaratibu wa watu kuingia hapa dampo kuokota chupa za plastiki usitishwe mara moja” Alisisitiza Naibu Waziri Sima.
 
Waziri Sima amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa taka hatarishi kutupwa dampo kwakuwa hakuna mkakati madhubuti wa kutenganisha taka hizo toka kwenye vyanzo vya uzalishaji.Ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake katika Mkoa wa Lindi Naibu Waziri Sima pia amepata fursa ya kuongea na Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wakiwemo madiwani na viongozi wa Serikali za Mitaa kuweka mikakati madhubuti ya kutunza Ikolojia ya Vyanzo vya Maji ambavyo ni mto Njenje na Parang’andu ambavyo hutirisha maji yake katika Mto Luwengu ambao humwaga maji yake kati katika Mto Rufiji.
 
“Ndugu zangu sote tunafahamu umuhimu wa hifadhi ya Mazingira na umuhimu wa Bonde la Mto Rufiji katika uzalishaji wa Umeme wa Uhakika, sisi watu wa Mazingira hii kwetu ni fursa, maana uzalishaji wa umeme utasaidia kuhifadhi mazingira kwa kupunguza matumizi ya kuni na mkaa. Nawasihi wote tuwe mstari wa mbele katika kuhakikisha sisi tunakuwa mfano wa kulinda vyanzo vya maji.” Sima alisisitiza.
 

Aidha, Naibu Waziri Sima pia amepata fursa ya kutembelea Hospitali ya Mkoa wa Lindi na kuridhishwa na Mtambo maalumu wa kuteketeza taka ulipo Hospitalini hapo na kuagiza majengo yayojengwa katika Sekta ya Afya kuweka miundombinu ya kuvuna maji.Naibu Waziri Sima yuko katika ziara ya kukagua changamoto za kimazingira pamoja na kuweka mikakati ya kuzipatia ufumbuzi na pia kuhimizi usimamizi endelevu wa Mazingira kwenye ikolojia ya vyanzo vya maji vinavyochangia maji katika Bonde la Rufiji.

RC MAKONDA ATAJA SILAHA 3 ATAKAZOTUMIA KUISAIDIA TAIFA STARS KUFUZU MICHUANO YA AFCON.

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ambae amepewa jukumu la kuwa Mwenyekiti wa kuongoza Kamati ya kuisaidia timu ya Taifa (Taifa Stars) kufuzu fainali za mataifa ya Africa (AFCON) leo amezindua rasmi kamati hiyo yenye wajumbe 14 ambapo amewaomba wananchi kuwa kitu kimoja katika kuisapoti timu hiyo.

RC Makonda amesema majukumu makubwa 3 watakayoanza nayo Kama kamati ni Kuirudisha timu kwa wananchi, kuweka maandalizi mazuri ya timu na uwezeshaji wa timu. 

Aidha RC Makonda amesema katika kikao cha Leo kamati imepanga kukutana na watu wa makundi mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Dini, Wasanii, Wanasiasa, Wamiliki wa Vyombo vya Habari na wadau mbalimbali ili kwa pamoja tuiunge mkono timu ya Taifa. 

Hata hivyo RC Makonda amesema kwa sasa timu ipo katika mikakati ya maandalizi ya Mechi ya mwisho dhidi ya Uganda itakayochezwa Machi 24.

Kamati hiyo inaongozwa na RC Makonda ambae ni Mwenyekiti, Katibu wake akiwa ni Mhandisi Hersi Said ambapo Wajumbe wa kamati hiyo ni Mohamed Dewji, Haji Manara, Jerry Muro, Farouk Barhoza, Salim Abdallah, Mohamed Nassor, Patrick Kahemele, Abdallah Bin Kleb, Tedy Mapunda, Philimon Ntaihaja, Farid Nahid na Faraji Asas.

TAIFA STARS TUNA KILA SABABU YA KUSHINDA.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu jukumu la kuwa Mwenyekiti wa kuongoza Kamati ya kuisaidia timu ya Taifa (Taifa Stars) kufuzu fainali za mataifa ya Africa (AFCON) ,ambapo leo amezindua rasmi kamati hiyo yenye wajumbe 14 ambapo amewaomba wananchi kuwa kitu kimoja katika kuisapoti timu hiyo.

KOROSHO ZA SERIKALI ZAANZA KUBANGULIWA WILAYANI TUNDURU

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kubangua korosho cha Korosho Africa Ltd wakiendelea na kazi kiwandani hapo ambapo hadi kufikia jana zaidi ya wananchi 200 wamepata ajira.
Mfanyakazi wa kiwanda cha kubangua Korosho cha Korosho Africa Ltd Tunduru Mkoani Ruvuma Issa Kahesa kulia akimueleza Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera kazi ya ubanguaji wa korosho za Serikali inavyoendelea katika kiwanda hicho.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera aliyeinama akiangalia ubora wa korosho za Serikali zinazobanguliwa katika kiwanda cha kubangua korosho cha Korosho Africa Ltd kilichopo Tunduru Mkoani Ruvuma.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera akiangalia korosho zilizobanguliwa katika kiwanda cha Korosho Africa Ltd ambacho kimeingia mkataba na Serikali kwa ajili ya kubangua korosho za Serikali zilizonunuliwa katika msimu wa 2018/2019 kutoka kwa wakulima wa wilaya ya Tunduru,kulia ni mfanyakazi wa kiwanda hicho Issa Kahesa. Picha na Amri Mmanja, Ruvuma.

NAIBU WAZIRI IKUPA ATOA WITO KWA WENYE ULEMAVU KUJIUNGA NA CHF ILIYOBORESHWA

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia  masuala ya watu wenye  ulemavu, Mhe.Stella Ikupa  ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya watu wenye  ulemavu, kuwahamasisha wanachama wao kujiunga na  mfuko  wa afya ya jamii (CHF )ulioboreshwa ili waweze kupata uhakika wa matibabu.

IKUPA ametoa wito huo  wilayani Itilima  katika ziara yake wakati akizungumza na viongozi wa Wilaya, Viongozi wa Vyama vya wenye ulemavu na  baadhi ya wenye ulemavu wenyewe wakati wa ziara yake wilayani humo Februari 25, 2019, ambayo ililenga kukagua utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ikiwa ni pamoja na mradi wa Kitalu nyumba na masuala mbalimbali yahusuyo wenye walemavu.

Amesema ni vema viongozi wa vyama na wenye ulemavu wakapena taarifa na kuhamasishani kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) ulioboreshwa, ili wapewe vitambulisho waweze kutibiwa kirahisi.

“Mkijiunga na CHF iliyoboreshwa mkapata kadi mtakuwa na uwezo wa kutibiwa muda wowote, kwa hiyo peaneni hizo taarifa mjiunge watu mnaofahamiana muweze kupewa hivyo vitambulisho mpate kutibiwa kirahisi wakati tukiwa tunasubiri ile bima ya afya kwa kila Mtanzania” alisema Mhe. Ikupa.

Katika hatua nyingine amewaagiza maafisa Ustawi wa jamii na maendeleo ya jamii kutoa elimu vijijini kwa  watu wenye  ulemavu kuhusiana na  uundwaji wa vikundi na namna ya kutekeleza miradi mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima,Mhe.  Benson Kilangi  akizungumzia utekelezaji wa mradi wa kitalu nyumba amesema katika awamu ya kwanza jumla ya vijana 20 wamepata mafunzo ya utengenezaji wa vitalu nyumba na kufundishwa stadi mbalimbali za kuendesha kilimo biashara na kuongeza mnyororo wa thamani.
Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Festo Kiswaga amesema  miradi ya vitalu katika Mkoa wa Simiyu itatekelezwa kwa viwango na kwa malengo yaliyokusudiwa, huku akibainisha kuwa vitasaidia kuongeza kipato kwa wananchi katika mkoa  na kuwa sehemu ya wananchi kujifunza kilimo bora.
Kwa upande wao viongozi pamoja na watu wenye ulemavu walioshiriki katika ziara hiyo wamemwomba Mhe. Naibu Waziri kushughulikia baadhi ya changamoto zinazowakabili katika maeneo yao.
“Ninaomba Serikali itusaidie tuweze kupata wakalimani wa lugha ya alama ili na sisi walemavu wa kusikia tuweze kupata ujumbe unaokuwa unawasilishwa na viongozi wetu kwenye mikutano na ziara kama hii ya leo hii itatusaidia sana” alisema Mhandi Ntobi Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wasiosikia Mkoa wa Simiyu.
“NaombaWataalam waje watutembelee kwenye vijiji vyetu na kwenye vyama vyetu watusaidie kutupa elimu ya namna ya kuunda vikundi na namna ya kufanya shughuli zinazoweza kutuongezea kipato” Bw. Seni Jitabo mlemavu wa viungo Mkazi wa Zagayu wilayani Itilima.
Naibu Waziri Ikupa, anaendelea na ziara yake Mkoani Simiyu ambayo itahitimishwa 27 Februari 2019, akiwa wilayani Itilima Naibu waziri ametembelea kitalu nyumba kilichopo Lagangabilili na kituo cha maarifa ya jamii Kanadi, ambako amejionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazofanywa na vijana.
  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa akizungumza jambo na Bw. Mhandi Ntobi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Watu wasiosikia Mkoa wa Simiyu, wakati akiwa katika ziara yake Wilayani Itilima Mkoani Simiyu, Februari 25, 2019.
 Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhe. Andrew Chenge akimweleza jambo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa( wa pili kulia) alipotembea Ofisi za CCM Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Februari 25, 2019.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa( katikati kwa walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watumishi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Mkoani Simiyu(NSSF na PSSSF) mara baada ya kutembelea ofisi za mifuko hiyo wakati wa ziara yake mkoani Simiyu , Februari 25, 2019.
 Bw. Seni Jitabo ambaye ni mlemavu wa Viungo akiwasilisha baadhi ya changamoto kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa(hayupo pichani) wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Februari 25, 2019
 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa akipokea zawadi ya sabuni kutoka kwa Afisa Vijana wa Wilaya ya Itilima ambaye alimkabidhi kwa niaba ya viongozi wa Wilaya hiyo wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Februari 25, 2019
Moja ya Kitalu nyumba(green house) ikatika kata ya Lagangabilili wilayani Itilima, kilichotembelewa na  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa wakati wa ziara yake.

WAZIRI KANYASU ATOA MBINU YA KUZIBANA HALMASHAURI KUPANDA MITI MILIONI 1.5

$
0
0
NA LUSUNGU HELELA-WMU


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameshauri itungwe sheria ya kuhakikisha kila Halmashauri nchini inapanda miti milioni 1.5 kila mwaka ili kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira nchini

Hatua hiyo inakuja baada ya agizo la Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati alipokuwa akizindua kampeni ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani mwezi Disemba 2018 kuwa kila Halmashauri ihakikishe inapanda miti milioni 1.5 kila mwaka.

Amesema hata hivyo tangu agizo hilo lilipotolewa hakuna Halmashauri hata moja iliyoweza kulitekeleza agizo hilo badala yake Halmashauri zilizo nyingi zimekuwa zikitaja takwimu za uongo.

Akizungumza mbele ya Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan kwenye kongamano la kulinda Mazingira lililofanyika kitaifa mkoani Tabora, Mhe.Kanyasu ameshauri itungwe sheria itakayowabana Wakurugenzi kutekeleza agizo hilo.

Amesema endapo agizo hilo likapitishwa na bunge na baadaye kuwa sheria Wakurugenzi watalazimika kupanda idadi hiyo ya miti badala ya ilivyo sasa kila Mkurugenzi kutekeleza agizo hilo kama hiyari.

Ameeleza kuwa Halmashauri zilizo nyingi zimekuwa zikitaja takwimu kubwa za miti iliyopandwa lakini anapokwenda kwa ajili ya kuiona wmiti hiyo imekuwa haionekani na huku wengine wamekuwa wakiibuka na visingizio kwa vile hakuna idadi hiyo ya miti waliyoipanda.

Amesema idadi ya miti ambayo imekuwa ikitajwa na Halmashauri kupandwa imekuwa ya vitabuni isiyo na uhalisia wa aina yoyote.Ameongeza kuwa hata zile Halmashauri ambazo zimekuwa zikijaribu kupanda zimekuwa hazifikishi idadi hiyo hata zikishapanda zimekuwa hazijishughulishi na kufuatia maendeleo ya miti hiyo.

Amesema hali hiyo imepelekea miti iliyo mingi kufa kwa kukosa uangalizi huku mengine kuliwa na mifugo wakati Halmashauri hizo zimekuwa zikibaki na takwimu zile zile za miti waliyoipanda.

Akizungumza Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassani amesema agizo lake lililenga kila Halmashauri ipande miti milioni 1.5 ikiwa ni lazima na sio hiyari kama Halmashauri zinavyotekeleza.

Hata hivyo, Mhe. Samia ameeleza kuwa katika agizo hilo lilikuwa wazi liikitaka kila Halmashauri ihakikishe inapanda miti ya aina yoyote ile akitolea mfano mizabibu, miti ya matunda ili mradi tu uwe mti bila kujali miti ya aina gani.

Ameongeza kuwa kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea nchini, Ofisi yake itahakikisha taratibu zinafuatwa za kulifanya agizo hilo liwe sheria.
Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan akimwagilia miti mara baada ya kuupanda mara baada ya kumalizika kwa kongamano la mazingira lililofanyika mkoani Tabora.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza mbele ya Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan kuhusu umuhimu wa kutunga sheria ya kuzibana Halmashauri kupanda miti 1.5 kila mwaka ili kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira
Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kongamano la mazingira lililofanyika mkoani Tabora.
Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja wananchi waliohudhuria kongamano la mazingira mkoani Tabora
Miongoni mwa wachangiaji katika kongamano la Mazingira, Juma Elias akitoa mchango wa mawazo wa namna ya kulinda mazingira kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na ukataji miti ovyo mkoani Tabora.( PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA- MNRT)

KATIBU MKUU NISHATI ATEMBELEA MIRADI YA UMEME KINYEREZI

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

KATIBU Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua ametembelea Kituo cha kufua umeme wa Gesi Asilia Kinyerezi I na Kinyerezi II jijini Dar es Salaam.

Lengo la ziara yake alisema ni kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya Kinyerezi II na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I (Kinyerezi I expansion)

Mradi wa Kinyerezi II ambao unazalisha kiasi cha Megawati 240 tayari umekamilika na umeme umekwishaingizwa kwenye Gridi ya Taifa, wakati ule.

“Tunashukuru kwamba tunaenda vizuri hasa Kinyerezi II ambayo kiukweli mradi umeshamalizika sasa hivi tunapata umeme kilichobaki ni masuala ya kuweka kila kitunsawa baina ya Mkandarasi na wataalamu wetu.” Alisema Dkt. Mwinyimvua baada ya kupokea taarifa ya miradi hiyo miwili toka kwa Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO, Mhandisi Stephene Manda.

Alisema kwa upande wa mradi wa upanuzi Kinyerezi I, (Kinyerezi I extension) kazi imeanza ingawa kulikuwepo na ucheleweshwaji wa vifaa bandarini na kuagiza uongozi wa TANESCO kukutana na taasisi zinazohusika na masuala ya kodi na utoaji mizigo bandarini ili kupanga utaratibu wa jinsi ya kulipa kodi mbalimbali bila ya kuathiri utoaji wa mizigo hiyo (vifaa na mitambo) bandarini.

“Nakumbuka mlipewa wito na Mheshimiwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwataka mjitahidi isifike mwezi wa nane, ikiwezekana hata mwezi wa tano muwe mmemaliza kazi.” Alisema.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu alifuatana na Kamishna wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga wakati kwa upande wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, waliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dkt. Tito Mwinuka.

Akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu na ujumbe wake, Meneja Miradi wa TANESCO, Mhandisi Stephene Manda, alisema wakati Mradi wa Kinyerezi II Megawati 240 ambao umekamilika tangu Desemba mwaka jana (2018), mradi wa Kinyerezi I ambao unafanya kazi una Megawati 150 na ule wa kufanya upanuzi (Kinyeerzi I extension) utakuwa na Megawati 185 na kazi tayari imefikia asilimia 76%

“Tunategemea mtambo wa kwanza wa mradi huu wa upanuzi tutakuwa tumeuwasha ifikapo mwezi Mei, 2019 na kukamilika kabisa kwa mradi mzima itakuwa Agosti 2019.” Alibainisha Mhandisi Manda na kuongeza Jumla ya umeme utakaokuwa unazalishwa hapa Kinyerezi kufikia Agosti mwaka huu itakuwa Megawati 575.” Alisema

Akifafanua zaidi alisema kutoka pale Kinyerezi I Extension tutakuwa na extension ndogo ya kutoa umeme kwa ajili ya mradi wa SGR.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (kulia), wakiongozwa na Meneja Miradi wa Shirika hilo. Mhandisi Stephene Manda (kushoto), wakati Katibu Mkuu akikagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme wa Gesi Kinyerezi I (Kinyerezi I expansion), jijini Dar es Salaam, Februari 25, 2019.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua (watatu kulia), Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, (watano kulia), na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (wapili kulia), wakiongozwa na Meneja Miradi wa Shirika hilo. Mhandisi Stephene Manda (aliyenyoosha mikono) wakati Katibu Mkuu akikagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme wa Gesi Kinyerezi I (Kinyerezi I expansion), jijini Dar es Salaam, Februari 25, 2019. 
Katibu Mkuu pia alijionea kituo cha kupokelea gesi kikiwa tayari kwenye eneo la mradi huo. 
KATIBU Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua, akipatiwa maelezo.
Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga(kushoto), akiwa na Mkandarasi eneo la mradi.
Katibu Mkuu Dkt. Mwinyimvua na ujumbe wake wakimsikiliza mkandarasi anayetekeleza mradi wa upanuzi Kinyerezi I, kuhusu mwenendo wa mradi huo.
Kiongozi wa zamu wa chumba cha udhibiti mitambo, kwenye mradi wa umeme wa gesi Kinyerezi II, Mhandisi Chidololo Enzi, (kulia) akitoa maelezo mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Hamisi Hassan Mwinyimvua (katikati), alipotembelea kujihakikishia kukamilika kwa mradi huo unaozalisha Megawati 240.
Kiongozi wa zamu wa chumba cha udhibiti mitambo, kwenye mradi wa umeme wa gesi Kinyerezi II, Mhandisi Chidololo Enzi, (kulia) akitoa maelezo mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Hamisi Hassan Mwinyimvua(kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (wapili kushoto).
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua (wapili kushoto), Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, (wakwanza kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (wapili kulia), wakiongozwa na Meneja Miradi wa Shirika hilo. Mhandisi Stephene Manda (aliyenyoosha mkono) wakati Katibu Mkuu akikagua maendeleo ya mradi wa Kinyerezi II jijini Dar es Salaam Februari 25, 2019 ambapo alielezwa kuwa tayari umekamilika.



Hii ndiyo Kinyerezi II kama inavyoonekana Februari 25, 2019 wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Nishati, Dkt. Mwinyimvua.














TCRA YAANZA ZIARA YA KUVITEMBELEA VITUO VYA UTANGAZAJI MKOANI KAGERA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Generali Marco Gaguti, akiongea na Wajumbe wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania  (TCRA) ofisini kwake, mjini Bukoba tarehe 25 Feb 2019.

Mkuu huyo wa mkoa ameipongeza kazi nzuri ya kudhibiti na kuhimiza ubora wa maudhui ya vyombo vya utangazaji inayofanywa na Kamati ya Maudhui kwa pamoja na Sekretarieti ya TCRA.

Mhe Brig. Gen. Gaguti amewaomba Wajumbe hao kuwahimiza wanahabari katika vyombo vya utangazaji watakavyovitembelea mkoani Kagera, kuongeza juhudi katika kusukuma mbele agenda ya maendeleo mkoani mwake. 

Alisisitiza, kuwa agenda ya maendeleo ndiyo itangulie mbele katika kuharakisha maendeleo ya Taifa letu.

Wajumbe wa Kamati ya Maudhui walimtembelea Mhe Brig. Gen. Gaguti kabla ya kuanza ziara ya kuvitembelea baadhi ya vituo vya utangazaji vilivyoko mkoani humo, katika kuhimiza uandaaji na urushaji wa maudhui bora ya vyombo vya utangazaji nchini, ikiwa ni pamoja na kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali inayoongoza sekta ya Utangazaji nchini ili kudumisha amani na kuchochea maendeleo ya sekta pamoja na Taifa kwa ujumla.

Wajumbe hao ni Valerie Msoka (Mwenyekiti), Joseph Mapunda (Makamu Mwenyekiti), Abdul Ngarawa, Jacob Tesha na Derek Murusuri.

Wajumbe hao waliambatana na ofisa wa TCRA kutoka Kanda ya Ziwa Abdul Hussein pamoja na Eunice Mabagala na Rolf Kibaja kutoka ofisi za TCRA makao makuu.

 Picha na Thomas Salala, ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera.

NMB YADHAMINI MKUTANO WA WADAU WAKUBWA SEKTA YA MAZIWA

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akifungua mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Maziwa uliofanyika jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena. Mkutano huo ulishirikisha wadau wakubwa wa sekta ya maziwa kutoka nje na ndani ya nchi. 
Meneja Mwandamizi Biashara ya Kilimo, Huduma ya Ushauri na Utafiti wa Benki ya NMB akizungumza kwenye mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Maziwa uliofanyika jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena. 
Baadhi ya viongozi wa Jukwaa la Kimataifa la Maziwa wakiwasilisha mada kwenye mkutano huo ulishirikisha wadau wakubwa wa sekta ya maziwa kutoka nje na ndani ya nchi. 
Baadhi ya viongozi wa Jukwaa la Kimataifa la Maziwa wakiwasilisha mada kwenye mkutano huo ulishirikisha wadau wakubwa wa sekta ya maziwa kutoka nje na ndani ya nchi. 


BENKI ya NMB kwa kushirikiana na Jukwaa la Kimataifa la Maziwa na wadau wengine wameungana kukutanisha wadau wa sekta ya maziwa ili kuangalia namna ya kukuza uzalishaji, uchakataji na matumizi maziwa hususani nchini Tanzania.

Wadau hao zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali na Tanzania wanakutana kwa siku mbili mfululizo kuangalia namna bora ya kuifanya sekta ya maziwa kufanya vizuri zaidi na kushiriki katika kupunguza umasikini kwa jamii zinazozalisha bidhaa hiyo.

Benki ya NMB imetumia zaidi ya shilingi bilioni 100 kwa ajili ya mikopo kwa wakulima mbalimbali ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali kuinua kilimo ikiwemo sekta ya maziwa nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akizindua mkutano huo leo jijini Dar es Salaam, aliishukuru NMB kwa kukutanisha wadau hao kujadili namna bora ya kuinua sekta hiyo nchini Tanzania.
Baadhi ya wadau wa sekta ya maziwa kutoka nchini Tanzania wakizungumza katika mkutano huo. 
Sehemu ya wadau wakubwa wa sekta ya maziwa kutoka nje na ndani ya nchi wakishiriki katika mkutano huo. 
Sehemu ya wadau wakubwa wa sekta ya maziwa kutoka nje na ndani ya nchi wakishiriki katika mkutano huo. 

NAIBU WAZIRI NISHATI ATAKA BUSARA ITUMIKE KUUNGANISHA UMEME VIJIJINI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kihuwe, Wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Februari 25, 2019, akiwa katika ziara ya kazi, ambapo pia aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.

 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kinasa sauti) akifurahi pamoja na wananchi wa kijiji cha Kihuwe, Wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Februari 25, 2019, mara baada ya kuwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.

 Sehemu ya umati wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Namatula, iliyopo wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza nao, kabla ya kuwasha rasmi umeme katika shule hiyo, Februari 25, 2019.

 Baadhi ya wataalamu kutoka Wizara ya Nishati, TANESCO na REA wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Muungano, wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Februari 25, alipokuwa katika ziara ya kazi ambapo aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.

 Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Kihuwe, wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Samwel Ndungo akiuliza swali na kueleza changamoto kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipofika katika kijiji hicho kuwasha rasmi umeme na kuzungumza na wananchi, akiwa katika ziara ya kazi, Februari 25, 2019.

 Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Kihuwe, wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi, William Hassan akiuliza swali na kueleza changamoto kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipofika katika kijiji hicho kuwasha rasmi umeme na kuzungumza na wananchi, akiwa katika ziara ya kazi, Februari 25, 2019.
 Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Kihuwe, wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Matthew Ntunga akiuliza swali na kueleza changamoto kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipofika katika kijiji hicho kuwasha rasmi umeme na kuzungumza na wananchi, akiwa katika ziara ya kazi, Februari 25, 2019.

 Sehemu ya umati wa wananchi wa kijiji cha Mapochelo, Wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, Februari 25, 2019 alipokuwa katika ziara ya kazi ambapo pia aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.



Na Veronica Simba – Nachingwea
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini kutumia busara katika kazi hiyo ili iwaongoze kufanya maamuzi sahihi hususan uunganishaji umeme katika taasisi na miradi ya umma.
Alitoa wito huo kwa nyakati tofauti jana, Februari 25 mwaka huu, akiwa katika ziara ya kazi wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi.
Akizungumza ofisini kwa Mkuu wa Mkoa na baadaye katika vijiji vya Kihuwe, Muungano na Mapochero, ambavyo aliviwashia umeme rasmi; Naibu Waziri alisisitiza kuwa pamoja na kila mkandarasi kuwa na wigo wa eneo analopaswa kuunganisha umeme, lakini siyo busara kwake kuruka taasisi za umma na miradi muhimu kama vile ya maji, afya na mingineyo kwa sababu tu iko nje ya wigo.
“Unafika eneo, unaona Zahanati ile pale, akina mama wanajifungua gizani; Shule ile pale, kuna hosteli, unaziachaje bila umeme sababu tu hazipo ndani ya wigo! Mkandarasi unapaswa kutumia busara, ikibidi tuandikie sisi Serikali, tuone namna gani gharama husika zitalipwa ili maeneo kama hayo yasikose umeme,” alisema.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri alisema kuwa serikali inaendelea kujivunia kugundulika kwa gesi katika mikoa ya kusini na kwamba watanzania wanapaswa kufahamu kwamba serikali imedhamiria kuitumia ipasavyo.
Akifafanua, alisema gesi inapaswa itumike katika viwanda vya mbolea, majumbani na katika kuzalisha umeme. Hivyo, aliwataka wananchi kupuuza maneno yanayosemwa na baadhi ya watu kuwa serikali haitoi tena kipaumbele kwa gesi iliyogunduliwa mikoa ya kusini.
Naibu Waziri alifafanua zaidi kuwa, ili kupata umeme mwingi, wenye bei nafuu na wa uhakika; ni lazima serikali ihakikishe inatumia vyanzo mbalimbali vya kuzalisha umeme ikiwemo maji, upepo, jua, gesi, tungamotaka na vinginevyo.
“Ndiyo maana tunaanzisha miradi mbalimbali ya kuzalisha umeme ambayo inatumia vyanzo mbalimbali, siyo gesi peke yake. Ni muhimu mkalitambua hilo kwamba, kama nchi, hatuwezi kutumia gesi peke yake katika kuzalisha umeme, tukaacha vyanzo vingine. Inabidi tutumie vyanzo vyetu vyote tulivyojaaliwa na Mungu.”
Akizungumzia utekelezaji wa miradi ya kupeleka umeme maeneo mbalimbali ya nchi hususan vijijini, Naibu Waziri alisema kazi hiyo inaendelea kufanyika  kwa ufanisi ambapo sasa serikali imewaelekeza wakandarasi wa miradi hiyo kuhakikisha wanawasha umeme katika vijiji vitatu kila wiki kwa kila mkandarasi.
Hata hivyo, aliwataka wananchi kuwa na subirá kwani kazi ya kuunganisha umeme inatekelezwa hatua kwa hatua.
Naibu Waziri anaendelea na ziara yake mkoani Lindi ambapo amefuatana na wataalamu mbalimbali kutoka wizarani, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

UWT IRINGA ILIVYOADHIMISHA MIAKA 42 YA KUZALIWA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

$
0
0
UWT mkoa wa Iringa imeadhimisha  miaka 42 ya kuzaliwa chama Cha Mapinduzi ccm kwa kushiriki shuguhuli  za kijamii pamoja na wananchi.

Katika maadhimisho yaliyofanyika katika Kijiji Cha Tanangozi  kata ya Msekeha halmashauri ya Iringa vijiji,UWT ilikabidhi mifuko 40 ya Saruji katika Shule ya sekondari Tanangozi kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa,walipanda  miti 30 ya Parachichi  katika shamba la shule na kufyatua tofari kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea.

Mgeni rasm katika maadhimisho hayo alikuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Dkt.Abel Nyamahanga.




















WANAFUNZI 52 KUTOKA CHUO CHA UALIMU MONDULI WATEMBELEA OFISI ZA TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI JIJINI ARUSHA

$
0
0


Jumla ya  wanafunzi 52  wa stashahada ya ualimu kutoka katika chuo cha ualimu cha Monduli wamefika   katika ofisi za  Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, Makao Makuu Njiro Arusha  kwa lengo la kujifunza kwa vitendo masuala mbali mbali ya kisayansi ambayo wamekuwa wakiyasoma katika nadharia.


Lengo la ziara hii ya siku moja kwa wanafunzi hawa ni kujifunza ili kufahamu dhana nzima ya juu ya matumizi salama ya mionzi na namna udhibiti unavyofanyika na wao kuwa mabalozi wazuri katika uhamasishaji wa matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia.


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Profesa Lazaro Busagala amewaeleza wanafunzi hao kuwa elimu waliyoipata katika ziara hii ya mafunzo itawawezesha kuelewa matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia na kujilinda na mionzi pindi watakapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kikazi hapo baadaye.


Kiongozi wa wanafunzi hao Mwalimu  Sikana Menard ameeleza kuwa ziara hiyo imewasaidia wanafunzi hao ambao ni walimu watarajiwa hapo baadae katika masomo ya sayansi kuwa wamepata  elimu kubwa kuhusiana na masuala ya mionzi.


Amesema wamekuwa wakiwafundisha wananfunzi kwa njia ya nadharia tu hivyo kwa kutembelea kwenye Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania kutawasaidia sana kujionea teknolojia mbali mbali katika maabara za TAEC zenye ubora wa hali ya juu kwa ajili ya mafunzo.


Aidha TAEC inaendelea kuwakaribisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali ili kujipatia elimu na kujifunza masuala tofauti tofauti yanayohusu udhibiti salama wa mionzi na  matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia  hapa nchini.


Imetolewa na;



Peter G. Ngamilo

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania.

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images