Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA FINLAND WAZIDI KUIMARIKA

$
0
0
 Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yuko nchini Finland kwa ziara ya kikazi ya siku mbili tarehe 25 hadi 26 Februari. Ziara hiyo imefanyika kufuatia mwaliko kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Mhe. Timo Soini. 

Mheshimiwa Waziri ameanza ziara hiyo kwa kukutana na mwenyeji wake, Mheshimiwa Waziri Timo Soini. Kwenye mazungumzo yao, Mawaziri hao wamekubaliana kuboresha ushirikiano kwenye sekta biashara, uwekezaji, mafunzo ya ufundi, kuongeza ajira kupitia sekta ya misitu, kuendeleza ushirikiano katika majukwaa ya kimataifa kwa kuzingatia usawa, pamoja na kuwajengea uwezo wanawake na watoto. 

Wakati wa mazungumzo, Waziri Soini wa Finland alipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kupambana na rushwa na kusimamia uwajibikaji. Pia, aliipongeza Tanzania kwa kuendelea kuhifadhi wakimbizi na mchango wake katika usuluhishi wa migogoro inayozikabili baadhi ya nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu. Mawaziri hao walikubaliana kuendelea kushirikiana katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiusalama ikiwa ni pamoja na biashara ya madawa ya kulevya, biashara haramu ya kusafirisha watu, na matishio ya ugaidi. 

Kabla ya mazungumzo hayo, Mheshimiwa Balozi Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na Bw. Sampo Suihko, Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha OMNIA Espoo ambaye alieleza utayari wa Taasisi yake kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kubadilishana uzoefu wa kutoa mafunzo ya elimu ya ufundi yanayoendana na soko la ajira. 

Pia, Mheshimiwa Mahiga alifanya mazungumzo na Mheshimiwa Matti Ahtisaari, Rais Mstaafu wa Finland na Mwanzilishi wa Taasisi ya Utatuzi wa Migogoro. Mheshimiwa Ahtisaari aliipongeza Tanzania kwa kazi nzuri inayofanya katika utatuzi wa migogoro kwenye nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu na kusihi kusihi kuendeleza jitihada hizo kwa ustawi wa Dunia nzima. 

Vilevile, Balozi Mahiga alifanya mazungumzo na Bw. Jukka Kallio, Makamu wa Rais wa ya Helsinki. Katika mazungumzo hayo, uongozi wa Bandari ya Vuosaari uko tayari kushirikiana na uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania katika kuboresha mifumo (Digitalization) itakayoongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es salaam. 

Kadhalika, Mheshimiwa Waziri Mahiga alifanya mazungumzo na Jumuiya ya Wafanyabiashara (Business Finland) na Makampuni makubwa ya kibiashara nchini Finland. Wafanyabiasha hao walipongeza jitihada zinazoendelea kufanyika nchini Tanzania katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji. Waliahidi kuwekeza nchini na kushawishi makampuni mbalimbali kuona umuhimu wa kuwekeza nchini Tanzania. 
Leo Mheshimiwa Waziri amehitimisha ziara hiyo kwa kufanya mazungumzo na Bi. Anne-Mari Virolainen, Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland; Bw. Mauri Pekkarinen, Naibu Spika wa Bunge la Finland na baadaye kuzungumza na Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge hilo; na Bw. Juhan Damski, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya nchini Finland. 



WIZARA YA MAMBO YA NJE NA 

USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI 



26 Februari 2019 


USIKU WA WANANDOA NDANI YA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI DAR ES SALAAM MARCH 8, 2019

Hii ndio Nafasi ya pekee kwa timu hizi kushinda Kombe Coppa Italia

$
0
0
Kwa timu zilizosalia kwenye Coppa Italia, shindano hili ndio nafasi ya wazi au nafasi pekee kwa timu hizo kushinda Kombe msimu huu. Baada ya kutolewa kwa Juventus ambao wameshinda kombe hilo kwa miaka minne mfululizo timu za AC Milan, Fiorentina, Lazio na Atalanta iliyowafunga Juventus katika robo fainali watategemea kushinda Kombe hilo.

Bahati nzuri hatua ya nusu fainali huwa na mechi za marudiano. Hii inatoa fursa kwa timu zote kutumia vizuri viwanja vya nyumbani.  Lazio dhidi ya AC Milan ndiyo mechi ya kwanza, mchezo huo utapigwa katika dimba la Stadio Olimpico. Lazio maarufu kama I Biancocelesti, wao wanatafuta kushinda Kombe la Coppa Italia kwa mara ya saba, mzunguko uliopita walihitaji mikwaju ya penati ili kufuzu sasa wanakutana na mtihani mwingine dhidi ya wenzao wa jiji la Milan.

Kwa upande wa Rossoneri (AC Milan) watategemea magoli ya straika wao mpya Krzysztof Piatek aliyejiunga nao akitokea Genoa baada ya Gonzalo Higuain kujiunga na Chelsea. Mshambuliaji huyo raia wa Poland amekuwa katika kiwango kizuri tangu ajiunge na AC Milan, amefunga magoli sita katika mechi tano, huku magoli yake mawili yakiwaondoa Napoli katika michuano hiyo. Mchezo wa Lazio vs AC Milan utapigwa Jumanne saa 5:00 Usiku na utarushwa LIVE kupitia ST World Football pekee.

Siku ya Jumatano Fiorentina watacheza dhidi ya Atalanta. Licha ya kuwahi kufika fainali mara tatu pekee, timu ya Atalanta wanaamini wana kila sababu ya kushinda Kombe hasa baada ya kuwang’oa mabingwa Juventus kwa ushindi wa kuvutia 3-0 mashabiki wao wana kila sababu ya kuamini huu ni mwaka wao. Mcolombia Duvan Zapata ndio kinara wao katika ufungaji huku akifunga mabao mawili dhidi ya Juve ya Ronaldo. Mshambuliaji huyo amekuwa na kiwango kizuri mbele ya goli baada ya kutua Atalanta kwa mkopo akitokea Sampdoria.

Fiorentina nao wako katika morali ya hali ya juu baada ya kuwatoa Roma. Fiorentina waliwaadhibu Roma kwa mabao 7-1 katika mchezo ambao mtoto wa Kocha Diego Simeone, Giovanni Simeone alifunga mabao mawili. Mchezo wa Fiorentina vs Atalanta utapigwa Jumatano saa 5:00 Usiku na utarushwa LIVE kupitia ST World Football pekee. Mechi za marudiano zinatarajiwa kupigwa katika wiki ya mwisho ya mwezi April.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA DAKTARI BINGWA WA UPASUAJI WA UBONGO NA MISHIPA YA FAHAMU

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Profesa Zhao Yuanil kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing nchini China mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Mazungumzo na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Profesa Zhao Yuanil kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing nchini China aliyeambatana na ujumbe wake pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Maseru na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Respicious Boniface Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Profesa Zhao Yuanil kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing nchini China wanne kutoka kulia, Balozi wa China hapa nchini Wang Ke watatu kutoka kulia pamoja Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Respicious Boniface. Wengine katika picha ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Balozi Zuhura Bundala pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Maseru.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Profesa Zhao Yuanil kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing China wanne kutoka kulia mara baada ya kumaliza kupiga picha ya kumbukumbu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya Kinyago Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo  na Mishipa ya Fahamu Profesa Zhao Yuanil kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing China mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Balozi wa China hapa nchini Wang Ke akishuhudia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke mara baada ya kumaliza mazungumzo na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo  na Mishipa ya Fahamu Profesa Zhao Yuanil kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha Beijing China. PICHA NA IKULU

NAIBU WAZIRI NISHATI ATAKA BUSARA ITUMIKE KUUNGANISHA UMEME VIJIJINI

$
0
0
Na Veronica Simba – Nachingwea
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini kutumia busara katika kazi hiyo ili iwaongoze kufanya maamuzi sahihi hususan uunganishaji umeme katika taasisi na miradi ya umma. Alitoa wito huo kwa nyakati tofauti jana, Februari 25 mwaka huu, akiwa katika ziara ya kazi wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi.

Akizungumza ofisini kwa Mkuu wa Mkoa na baadaye katika vijiji vya Kihuwe, Muungano na Mapochero, ambavyo aliviwashia umeme rasmi; Naibu Waziri alisisitiza kuwa pamoja na kila mkandarasi kuwa na wigo wa eneo analopaswa kuunganisha umeme, lakini siyo busara kwake kuruka taasisi za umma na miradi muhimu kama vile ya maji, afya na mingineyo kwa sababu tu iko nje ya wigo.

“Unafika eneo, unaona Zahanati ile pale, akina mama wanajifungua gizani; Shule ile pale, kuna hosteli, unaziachaje bila umeme sababu tu hazipo ndani ya wigo! Mkandarasi unapaswa kutumia busara, ikibidi tuandikie sisi Serikali, tuone namna gani gharama husika zitalipwa ili maeneo kama hayo yasikose umeme,” alisema.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri alisema kuwa serikali inaendelea kujivunia kugundulika kwa gesi katika mikoa ya kusini na kwamba watanzania wanapaswa kufahamu kwamba serikali imedhamiria kuitumia ipasavyo.

Akifafanua, alisema gesi inapaswa itumike katika viwanda vya mbolea, majumbani na katika kuzalisha umeme. Hivyo, aliwataka wananchi kupuuza maneno yanayosemwa na baadhi ya watu kuwa serikali haitoi tena kipaumbele kwa gesi iliyogunduliwa mikoa ya kusini.

Naibu Waziri alifafanua zaidi kuwa, ili kupata umeme mwingi, wenye bei nafuu na wa uhakika; ni lazima serikali ihakikishe inatumia vyanzo mbalimbali vya kuzalisha umeme ikiwemo maji, upepo, jua, gesi, tungamotaka na vinginevyo.

“Ndiyo maana tunaanzisha miradi mbalimbali ya kuzalisha umeme ambayo inatumia vyanzo mbalimbali, siyo gesi peke yake. Ni muhimu mkalitambua hilo kwamba, kama nchi, hatuwezi kutumia gesi peke yake katika kuzalisha umeme, tukaacha vyanzo vingine. Inabidi tutumie vyanzo vyetu vyote tulivyojaaliwa na Mungu.”

Akizungumzia utekelezaji wa miradi ya kupeleka umeme maeneo mbalimbali ya nchi hususan vijijini, Naibu Waziri alisema kazi hiyo inaendelea kufanyika  kwa ufanisi ambapo sasa serikali imewaelekeza wakandarasi wa miradi hiyo kuhakikisha wanawasha umeme katika vijiji vitatu kila wiki kwa kila mkandarasi.

Hata hivyo, aliwataka wananchi kuwa na subirá kwani kazi ya kuunganisha umeme inatekelezwa hatua kwa hatua.

Naibu Waziri anaendelea na ziara yake mkoani Lindi ambapo amefuatana na wataalamu mbalimbali kutoka wizarani, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kihuwe, Wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Februari 25, 2019, akiwa katika ziara ya kazi, ambapo pia aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kinasa sauti) akifurahi pamoja na wananchi wa kijiji cha Kihuwe, Wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Februari 25, 2019, mara baada ya kuwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.
 Sehemu ya umati wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Namatula, iliyopo wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza nao, kabla ya kuwasha rasmi umeme katika shule hiyo, Februari 25, 2019.
 Baadhi ya wataalamu kutoka Wizara ya Nishati, TANESCO na REA wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Muungano, wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Februari 25, alipokuwa katika ziara ya kazi ambapo aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.
 Mkazi wa Kijiji cha Kihuwe, wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Samwel Ndungo akiuliza swali na kueleza changamoto kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipofika katika kijiji hicho kuwasha rasmi umeme na kuzungumza na wananchi, akiwa katika ziara ya kazi, Februari 25, 2019.
 Mkazi wa Kijiji cha Kihuwe, wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi, William Hassan akiuliza swali na kueleza changamoto kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipofika katika kijiji hicho kuwasha rasmi umeme na kuzungumza na wananchi, akiwa katika ziara ya kazi, Februari 25, 2019.
Mkazi wa Kijiji cha Kihuwe, wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi, Matthew Ntunga akiuliza swali na kueleza changamoto kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipofika katika kijiji hicho kuwasha rasmi umeme na kuzungumza na wananchi, akiwa katika ziara ya kazi, Februari 25, 2019.
Sehemu ya umati wa wananchi wa kijiji cha Mapochelo, Wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, Februari 25, 2019 alipokuwa katika ziara ya kazi ambapo pia aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.

WAZIRI MKUCHIKA ATOA SIKU 34 KWA AFISA UTUMISHI HALMASHAURI YA WILAYA YA KILWA KUWEKA TAARIFA SAHIHI ZA WATUMISHI KWENYE MFUMO WA HCMIS

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) ametoa siku 34 kwa Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Jovita Buyobe kuhakikisha anaweka taarifa sahihi za watumishi wa halmashauri yake katika Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS).
Agizo hilo amelitoa wakati wa mkutano kati yake na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, wilayani Kilwa.
Mkuchika amemtaka Afisa Utumishi huyo kuhitimisha zoezi la kuweka taarifa sahihi za watumishi wa halmashauri yake kwenye mfumo wa HCMIS ndani ya siku 34 kuanzia sasa mpaka mwishoni mwa mwezi wa tatu.
 Mkuchika amesema, ripoti zinaonyesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa inaongoza kwa kuwa na taarifa zisizo sahihi za watumishi kwenye mfumo wa HCMIS, hivyo amemtaka Afisa Utumishi huyo kutimiza wajibu wake.
Awali, akizungumzia taarifa za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa zilizomo kwenye mfumo wa HCMIS, Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Bi. Jovita Buyobe amekiri kuwepo kwa taarifa zisizo sahihi za watumishi kwenye mfumo wa HCMIS na kutoa sababu ya uhaba wa watumishi.
Bi. Buyobe amefafanua kuwa, amekuwa akijitahidi kuweka taarifa sahihi za watumishi kwenye mfumo wa HCMIS bila mafanikio kwa kuwa anafanya kazi zote za kiutumishi na kiutawala peke yake, lakini amemhakikishia Waziri kumaliza suala hilo kwa kushirikiana na Afisa Utumishi mpya aliyeajiriwa hivi karibuni.
Mkuchika amehitimisha ziara ya kikazi mkoani Lindi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma pamoja na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani humo ambapo ametembelea Wilaya ya Liwale, Nachingwea, Ruangwa, Manispaa ya Lindi na Kilwa.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi (hawapo pichani) katika kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, wilayani Kilwa. Kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Dkt. Bora Haule na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai (kulia kwake).
 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Dkt. Bora Haule akitoa utambulisho wa makundi ya watumishi waliohudhuria kikao kazi kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, wilayani Kilwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) kuzungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa katika kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, wilayani Kilwa.
 Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, wilayani Kilwa.
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Bi. Jovita Buyobe akijibu hoja wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, wilayani Kilwa.

SIMBA, LIPULI NANI KUVUNJA REKODI YA KUMFUNGA MWENZAKE

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Simba SC kesho watashuka dimbani wakiwa ni wageni kumenyana na Wanapaluhengo Lipuli FC katika mchezo wa marudiano wa raundi ya pili msimu huu 2018/2019.

Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na shauku kubwa utapigwa katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa majira ya saa kumi za jioni huku kiingilio kikiwa  VIP kwa bei 10000, Mzunguko 5000 na Watoto kwa 2500.

Sio Simba wala Lipuli wanaitaji matokeo mazuri ya alama tatu dhidi ya mwenzake  kujiweka sehemu nzuri katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo msimu uliopita 2017-18 hakuna timu iliyomfunga mwenzake baada ya timu zote kushindwa kufungana kwa kutoka sare ya bao 1-1 katika Mchezo wa nyumbani na ugenini, Msimu huu 2018-19 wameendeleza rekodi ya kutofungana kwa kutoka 0-0 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Simba walipowakaribisha Lipuli FC.

Katika Msimamo wa Ligi Kuu Simba ikiwa nafasi ya 3 ikiwa na alama 45 na michezo 18, Yanga wao wakiwa Vinara wa Ligi hiyo wakiwa na alama 61 michezo 25, wakifuatiwa na Azam FC wenye alama 50 akiwa ameshacheza  michezo 25 pia, Lipuli FC ambao wanakibarua kizito cha kufuana na Simba kesho wao wapo nafasi ya 5 wakiwa na pointi 38 na michezo 27.

Nani atavunja mwiko Simba au Lipuli kwa kumfunga mwenzake mara hii?ukizingatia Wekundu hao wa Msimbazi wapo kwenye kasi na Safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Emmanuel Okwi pamoja na  Middie Kagere ambaye amekuwa hatari zaidi kwa kufumania nyavu za wapinzani.

Huku Wanapaluhengo wakionekana kupoteza mchezo  wake wa mwisho aliocheza Stand United ambapo alikula kichapo cha bao 3-2 akiwa ugenini,

Simba SC wao waliendeleza rekodi yake ya kufanya vizuri baada ya kumfunga Yanga hivyo kupata morali zaidi ya kuendelea kufanya vema ambapo pia katika michezo wake wa mwisho uliopigwa februari 22 Mwaka huu katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam alishinda bao 3-1 dhidi ya wana lamba lamba  wa Chamazi Azam FC.

JK Aongoza Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola kwenye Uchaguzi Mkuu wa Nigeria

$
0
0
 Kufuatia kukamilika kwa hatua ya kupiga kura na kuanza kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Nigeria, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Tanzania na Kiongozi wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola kwenye Uchaguzi Mkuu wa Nigeria ametoa taarifa yake ya awali ya uchaguzi huo inayopatikana kupitia link hapa chini: http://www.thecommonwealth.org/sites/default/files/inline/Interim%20Statement%20of%20the%20Commonwealth%20Observer%20Group%20Draft%20-%2025%20Feb%20Final%20Interim%20Statement%20PDF.pdf

 Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Tanzania na Kiongozi wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola kwenye Uchaguzi Mkuu wa Nigeria akitoa ripoti ya awali ya jumuiya hiyo

 Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Tanzania na Kiongozi wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola kwenye Uchaguzi Mkuu wa Nigeria akiangalia makarani kabla ya zoezi la upigaji kura kuanza mjini Abuja Februari 23, 2019
 Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Tanzania na Kiongozi wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola kwenye Uchaguzi Mkuu wa Nigeria akiangalia wasimamizi wa  upigaji kura kuanza mjini Abuja Februari 23, 2019
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Tanzania na Kiongozi wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola kwenye Uchaguzi Mkuu wa Nigeria akiongea na wapiga kura wenye ulemavu wa majo wakati wa upigaji kura mjini Abuja Februari 23, 2019

BENKI YA CRDB YAJIPAMBANUA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI YA KUTOA ELIMU BURE NA BORA

$
0
0
Benki ya CRDB imeendelea kujipambanua kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufili ya kutoa elimu bure na bora kwa wanafunzi wote nchini. Hilo limedhihilika leo Februari 26, 2019 kwa kukabidhi madarasa mawili pamoja na madawati 40 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 60 kwa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls).

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (kulia), Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dkt. Neema Mori (wa pili kushoto) pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Iringa, Ritha Kabati wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls Secondary School), hafla iliyofanyika mapema leo asubuhi shuleni hapo, Mkoani Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakingukua kitambaa cha jiwe la msingi wakati wa ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls Secondary School), hafla iliyofanyika mapema leo asubuhi shuleni hapo, Mkoani Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kwa msaada wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls Secondary School), hafla iliyofanyika mapema leo asubuhi shuleni hapo, Mkoani Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls Secondary School), hafla iliyofanyika mapema leo asubuhi shuleni hapo, Mkoani Iringa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla ya ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls Secondary School), hafla iliyofanyika mapema leo asubuhi shuleni hapo, Mkoani Iringa.
Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dkt. Neema Mori akizungumza machache katika ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls Secondary School), hafla iliyofanyika mapema leo asubuhi shuleni hapo, Mkoani Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akifurahi jambo wakati wa ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls Secondary School), hafla iliyofanyika mapema leo asubuhi shuleni hapo, Mkoani Iringa.
Mbunge wa Viti Maalum Iringa, Ritha Kabati akisalimia wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB kwa shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa (Iringa Girls Secondary School), hafla iliyofanyika mapema leo asubuhi shuleni hapo, Mkoani Iringa.

























MEYA MANISPAA YA TEMEKE ABDALLAH CHAUREMBO ATOA OMBI KWA BENKI YA DUNIA

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MEYA wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Abdallah Chaurembo ametoa ombi kwa Benki ya Dunia kuendelea kuisaidia fedha Serikali ya Tanzania na hasa ndani ya manispaa hiyo ili kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi.

Chaurembo ametoa ombi hilo wakati maofisa wa Benki ya Dunia walipofanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Jijii la Dar es Salaam (DMDP).

Maofisa hao wa benki ya dunia wametembelea miradi hiyo wakiongozwa na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Sulemani Jafo.

Akifafanua zaidi kuhusu utekelezaji wa miradi ya DMDP ,Chaurembo amesema katika kufanikisha miradi hiyo wao Temeke waliamua kukopa fedha Benki ya CRDB Sh.Bilioni 20 ambazo zilitumika kulipa fidia wananchi katika baadhi ya maeneo ili kupisha mradi huo.

Ameongeza kwa kumwambia Waziri Jafo kuwa pamoja na kukopa fedha hizo wameendelea kulipa deni bila tatizo na manispaa ya Temeke iko salama kwani utekelezaji wa miradi ya maendeleo unakwenda vizuri.

" Pamoja na kukopa fedha Sh Bilioni 20 kutoka Benki ya CRDB ,tunalipa deni bila tatizo.Pia tunaendelea na kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya manispaa yetu.Hivyo Temeke tuko salama sana,"amesema Chaurembo.

Pia amesema wanatoa ombi kwa Serikali ili kupata fedha hizo za fidia kama ambavyo imefanyika kwa manispaa ya Kinondoni na Ilala,hivyo ni vema Serikali Kuu ikawapa fedha hizo.

Wakati huo huo ametumia fursa hiyo kutoa ombi kwa Benki ya Dunia iwapo bajeti yao itaruhusu waendelee kuisaidia fedha Manispaa ya Temeke na kufafanua kuwa mrado wa DMDP unatekelezwa katika kata 12 na hivyo bado kuna kata nyingine ambazo nazo zinahitaji kuendelezwa.

"Tunashukuru Serikali yetu ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli ambaye amedhamiria kuboresha maisha ya wananchi kupitia miradi ya maendeleo.

"Kwetu Temeke pamoja na kutambua juhudi hizo tunaomba ombi kwa Benki ya Dunia kuendelea kutusaidia fedha kwa kushirikiana na Serikali yetu ili tuendelee kuboresha maeneo yetu," amefafanua Chaurembo.

Kuhusu namna ambavyo miradi inavyotekelezwa,Chaurembo amesema viongozi wa Manispaa ya Temeke wakiwamo madiwani wamekuwa makini kuhakikisha thamani ya fedha inayotolewa kwa ajili ya miradi hiyo inakwenda sambamba na ubora wa mradi.

"Tumekuwa makini kufuatilia miradi hii ili iandane na fedha inayotolewa.Ndio maana miradi hii kwa Temeke inavutia sana na inatekelezwa kwa kiwango cha hali ya juu," amesema Chaurembo huku akisisitiza kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo ndio maana wanapata ujasiri wa kuomba fedha kwa ajili ya kuendelea kuboresha miundombinu.

FAIDA YA MAZOEZI YA YOGA KATIKA KUJENGA MWILI NA FIKRA

$
0
0


 Na Sensei Rumadha Fundi
 Uchambuzi Madhubuti katika kuielewa Sanaa ya Yoga na mafunzo yake, haina budi pia kuzielewa na kutambua faida zake kimifano kupitia wahusuka na mchezo huo wa Sanaa isiyo ya kawaida kwa wengi. Ipo mifano mingi sana katika sehemu tofauti ambako mafunzo haya ya Yoga yametumika kama utafiti kuwezalinganisha tabia na stahimili za kujenga uvumilivu na kuwa na upeo wa kuyaona mengi kifikra na kuyatafakari kabla ya maamuzi yoyote ili kuepuka maamuzi yasio stahili na kuleta madhara.

Mfano wa kwanza, Canada, ni nchi iliyoendelea na imefanya utafiti mkubwa katika jeshi lake la polisi kwa kuwahusisha baadhi ya maofisa wake katika kozi ya Yoga na kutafakari kabla ya kuanza kazi kila siku ili kutuliza mawazo na kuwa na utulivu wa kuwamuda raia wake wakati wa shughuli zao za dolia ( https://www​.reddit.com/.../canadian_polic..       ), (https://www​.canadaamindfulnation.ca/.../). Kwani, nchi ya jirani na Canada, Marekani, hivi karibuni mnamo miaka michache iliyopita, imebainika kwamba maafisa wa jeshi la Marekani hutumia nguvu nyingi sana zisizohitajika katika kuwa kabili wa harifu au watuhumiwa kutokana na kile kiitwacho hasira au chuki za ubaguzi nchini humo. Hiyo ndio moja ya sababu kuu nchini Canada polisi hawana lawama kama zile za wenzao wa Marekani. Na sababu kubwa ni kile kiitwacho amani na ustamilivu wa fikra na utumiaji wa nguvu au unyanyasaji wa haki za raia.

 Mfano wa pili ni wafungwa huko nchini New Zealand  (https://www​.yogainprisonstrust.org/),   na  mwisho ulifanyika nchini Afrika Kusini ( South Africa) 2016 (https://www​.pressreader.com/south-africa..). Kutokana na vurugu na ukatili wa wafungwa wa jela za ulinzi wa usalama wa hali ya juu wa huko Afrika ya Kusini, utafiti huo wenye lengo la kujaribu kama kweli mafunzo ya Yoga yatawasaidia wafungwa hao kuwa wapole na utulivu wa mawazo na fikra ilikupunguza ghasia na fujo ndani ya jela hizo. Matokea yake ni kwamba ilibainika kuwa asilimia 90 za washiriki na hali ya jela ilikuwa shwari na fujo zilitulia n ahata wengi wa wafungwa hao walibadilika na kuwa na tabia njema na kuwa na utulivu sababu mafunzo hayo yamewezesha kuilekez mihimili ya mawazo yao katika njia sahihi kimawazo kupitia mafunzo haya ya Yoga.

Faida kuu za mafunzo haya kwa mifano na ushahidi toka kwa washiriki mbalimbali wa mafunzo haya ni : kulainisha viungo, kupunguza shinikizo la damu, utulivu wa fikra na mawazo, kupunguza “stress”; maumivu ya  kichwa, mgongo, na  viungo au mifupa. Zipo faida na vyakula muhimu katika kulifanikisha zoezi hili la afya ya mwili na fikra liwe na faida bora katika Maisha ya mtu wa kawaida. Leo hii, katika nchi za viwanda na zilizoendelea, watu wengi wana badilisha mfumo mzima wa maisha yao baada ya kuwa na mambo yanayochangia  hatarisha afya zao, ikiwemo vyakula, ulevi kupita kiasi  na uvutaji sigara.


Mtaalam wa somo hili la Yoga bwana Rumadha Fundi, alisoma kozi hii chini ya tawi la chama cha Yoga cha mjini Tiljala, Kolkata, India, katika tawi la chuo hicho (European Bracnh) College of Neo Humanist Studies, Gullringen, Vimmaby, Sweden 1985 hadi 1987 na kupata  Diploma ya Yoga. Hatimae kwenda India kwa mafunzo ya mwisho baada ya miaka miwili ya mafunzo ya awali huko Sweden.


MAKAMU WA RAIS AWASILI MKOANI SHINYANGA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Shinyanga tayari kwa ziara ya kikazi ya siku 5. Makamu wa Rais ambaye amesafiri kwa njia ya barabara akitokea mkoani Tabora ambapo napo alikuwa na ziara yenye lengo la kuhamasisha na kukagua shughuli za kimaendeleo.

Mara baada ya kuwasili mkoani Shinyanga Makamu wa Rais alitembelea kituo cha Afya cha Samuye na kupata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa eneo hilo. “Serikali ina kila nia ya kusogeza huduma za afya bora kwa wananchi”alisema Makamu wa Rais.

Aidha aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali inakuja na sheria ya mpango wa bima za afya kwa wote ambayo itamuhitaji kila mtanzania kuwa na bima ya afya. Makamu wa Rais amewataka wakazi wa kata ya Samuye kushirikiana katika kuzuia mimba za utotoni kwani kwa kiasi kikubwa zinahatarisha maisha ya watoto wa kike.

Kwa upande wake Naibu Waziri TAMISEMI Mwita Waitara amesisitiza Halmashuri kutenga asilimia 40 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kuzitaka halmashauri zote kumalizia maboma ya zahanati wakati serikali kuu inaleta pesa za kumalizia maboma ya shule na madawati.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa kata ya Tinde waliojitokeza kumlaki wakati akiwasili mkoani Shinyanga akitokea mkoani Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (kulia) mara baada ya kuwasili katika kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kulia) mara baada ya kuwasili katika kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Kata ya Samuye mara baada ya kutembelea na kukagua  kituo cha afya Samuye mkoani Shinyanga, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI Mwita Waitara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WAZIRI MHAGAMA- VIJANA TUMIENI FURSA ZILIZOPO NCHINI KUANZISHA VIJIWE VYA KIUCHUMI

$
0
0
Na OWM (KVAU) - SONGWE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewataka vijana nchini kuchangamkia fursa zilizopo kwenye maeneo yao kwa kuanzisha vijiwe vya kiuchumi.

Kauli hiyo ameitoa na Waziri Mhagama wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua maendeleo na miradi ya vijana iliyopo katika Kituo cha Maendeleo ya Vijana, Sasanda kilichopo Kata ya Nyimbili, Mkoani Songwe.

Akiwa katika ziara hiyo Mhe. Mhagama alieleza kuwa, Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imeendelea kutimiza azima yake ya ujenzi wa uchumi wa viwanda, hivyo vijana watumie fursa hiyo kujifunza mambo muhimu na kuanzisha viwanda vidogo vidogo ambavyo vitawafanya wabadilishe vijiwe wanavyokaa kuwa vya kiuchumi.

“Tunataka kuona vijana watakapo jifunza kilimo bora, ufugaji wa ng’ombe au nyuki wataweza kuboresha thamani mazao na bidhaa kwa kuanzisha viwanda vidogo ndani ya Mkoa wa Songwe, mkakati wetu katika kituo hiki ni kutoa mafunzo yatakayowawezesha vijana kuongeza thamani ya mazao na bidhaa watakazozalisha ambazo zitakuwa ni kichocheo muhimu katika kufikia maendeleo yao” alisema Mhagama

Aliongeza kuwa, Takribani vijana 500 kwenye kituo hicho wamejifunza stadi za maisha, ufundi na elimu mbalimbali zinazotolewa kwenye kituo ambazo zitawawezesha kujipatia kipato.

Sambamba na hilo, Mhe. Mhagama aliwahimiza Viongozi wa Mkoa kushirikiana na Ofisi yake ili waweze kuwasaidia vijana ambao wamekwisha anzisha viwanda vidogo vidogo ndani ya mkoa huo kwa kuwawezesha kuzalisha bidhaa zenye ubora na kuwatafutia soko la uhakika ndani na nje ya nchi.

Aidha, Waziri Mhagama alitoa rai kwa vijana kujiunga kwenye vikundi ambavyo ni endelevu na vyenye muelekeo wa kuanzisha viwanda vidogo vitakavyowawezesha kujiajiri na kuajiri wenzao na pelekea kufikia uchumi wa kati kama mpango wa maendeleo wa taifa unavyoelekeza.

Pia, aliwaelezea juu ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru ambazo zitafanyika katika Mkoa huo na kuwataka vijana na wanawake kutumia fursa hiyo kuutangaza vyema mkoa wa Songwe.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Bw. James Kajugusi alieleza kuwa kituo cha Maendeleo ya Vijana cha Sasanda kimewawezesha vijana kujitambua na kujiwekea malengo ya maisha na kuyatekeleza kwa faida yao, jamii na taifa kwa ujumla.

“Tunatarajia kuanzisha mafunzo na programu zitakazowaelekeza vijana masuala ya kilimo biashara ambacho kitasaidia upatikanaji wa malighafi zitakazokuwa zinahitajika kwenye viwanda vilivyopo nchini,” alisema Kajugusi

Naye Bw. Silia Kibona ambaye ni mnufaika kupitia kituo hicho, aliishukuru Serikali kwa kuwajengea mazingira ya kujifunzia ambayo yamewasaidia kupata mafunzo muhimu na aliwahamasisha vijana wenzie kuhudhuria mafunzo yanayotolewa kwenye kituo hicho.

Kituo cha Maendeleo ya Vijana – Sasanda kilianzishwa mwaka 1979 kwa ushirikiano wa Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni wa Taifa, Vijana na Michezo iliyopo wakati huo pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Uanzishaji wa Kituo hicho ulifuatia kuanzishwa kwa mpango wa kuunda vikundi vya vijana vya uzalishaji mali, uliolenga kuwawezesha vijana wasio na ajira kuweza kujiunga na kufanya kazi za kujitegemea hasa katika sekta ya kilimo. 
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akioneshwa na kupata maelezo ya vifaa vinavyotumiwa na vijana wa kituo cha Sasanda katika shughuli ya kuvua samaki.
 Bw. Lusekelo Mbukwa akimueleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama kuhusu majani wanayotumia kwa ajili ya malisho ya ng’ombe yanayosaidia ukuaji bora wa mifugo hiyo na upatikanaji wa maziwa mengi.
 Bi. Oliveta Mwashilindi akimueleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama kuhusu bidhaa ya asali inayotengenezwa na kikundi cha vijana cha Maisha Daily kilichopata mafunzo ya ufugaji nyuki katika kituo cha Sasanda.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanakikundi cha Rasupashoma Group, Bw. Ibrahim Malabela jinsi wanavyotengeneza viatu bora na vyenye kudumu kwa muda mrefu. (Mwenye miwani ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela na (Kulia) ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na vijana walionufaika kupitia kituo cha maendelo ya vijana, Sasanda alipotembelea kuona mradi walioanzisha katika Kata ya Nyimbili. (Wenye miwani) ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela mara baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua maendeleo na miradi ya vijana katika kituo cha Sasanda.
 Muonekano wa shamba darasa moja wapo lililopo katika Kituo cha Maendeleo ya Vijana cha Sasanda Mkoani Songwe.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na vijana wanaopata mafunzo ya kilimo bora na ufugaji wa kisasa katika kituo cha Maendeleo ya Vijana – Sasanda kilichopo Kata ya Nyimbili, Mkoani Songwe alipofanya ziara kukagua maendeleo na miradi ya vijana katika kituo hicho.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akimwagilia maji mti alioupanda katika kituo hiko cha Sasanda alipofanya ziara katika kituo hicho kukagua maendeleo na miradi ya vijana. (Kushoto) ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Bi.  Tusubileghe Benjamin na (Kulia) ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.
 Bw. Zawadi Mdolo akimueleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama kuhusu mafunzo wanayopatiwa katika shamba darasa juu ya kulima bora na upatikanaji mazao mengi. (Mwenye miwani) ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAZIRI WA AFYA, UMMY MWALIMU

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kabla ya mazungumzo, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Februari 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Februari 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MKAZI WA MBULU ASHINDA MILIONI TANO ZA BIKO

$
0
0
Mshindi wa sh milioni tano wa Biko kutoka Mbulu, mkoani Manyara, Felista Fabian amekabidhiwa fedha zake baada ya kushinda kutoka Biko.

TFF-FIKAPO MACHI 5 TUTANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI WA KLABU YA YANGA

$
0
0
Na Agness  Francis,blogu ya Jamii.

KAMATI ya uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania  (TFF)  imefunguka rasmi kuwa itatangaza tarehe ya uchaguzi wa klabu ya Yanga  ifikapo machi 5 mwaka huu,ni baada ya  kamati hiyo kukaa kimya kwa muda mrefu na kuleta sintofahamu kwa baadhi ya wanachama wa klabu hiyo iliyokita maskani yake Jangwani maeneo ya Kariakoo Jijini Dar Da Salaam. 

Amesema hayo  Mwenyekiti wa kamati  ya uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania  (TFF)  Ally Mchunguhela  kuwa tayari ameshakutana na viongozi wa klabu ya Yanga  na kukubaliana  kuwa sasa  kinachosuburiwa ni kutangazwa kwa tarehe rasmi ya uchaguzi huo unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa klabu hiyo.

Mchungahela amesema kuwa uchaguzi huo ulipaswa kufanyika januari 13 mwaka huu  lakini kutokana na  baadhi ya wanachama wa Yanga kufungua  kesi mahakamani kusimamisha mchakato huo  na kupelekea zoezi zima  la uchaguzi  kusimama.

;Uchaguzi wa Yanga  utafanyika na hakutakuwa tena na mchakato mwingine  mpya  bali utaendelea palepale  ulipokuwa umefikia ,na  ifikapo Tarehe 5 Machi tutatangaza rasmi tarehe  mpya ya uchaguzi wa  Yanga na naamini utafanyika;amesema mchungahela.

Aidha Mchungahela amesema kuwa  mpaka kufikia tarehe itakayotangazwa rasmi ya uchaguzi  huo kila kitu kitakwenda sawa na hakutakuwa tena na kizuizi kingine ambacho kitafanya mchakato mzima kusimama.

Finland yaipongeza Tanzania vita dhidi ya Rushwa.

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Mhe. Timo Soini (kulia) akimkaribisha ofisini kwake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga. Dkt. Mahiga yupo nchini Finland kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Waziri Mahiga na ujumbe wake (kushoto) ukiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland na ujumbe wake.


Finland yaipongeza Tanzania vita dhidi ya Rushwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Mhe. Timo Soini.amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kupambana na rushwa na kusimamia uwajibikaji.

Pongezi hizo alizitoa wakati alipofanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ambaye yupo nchini Finland kwa ziara ya kikazi ya siku mbili tarehe 25 na 26 Februari 2019.

Kwenye mazungumzo yao, Mawaziri hao wamesisitiza umuhimu wa Tanzania na Finland kuboresha ushirikiano kwenye sekta mbalimbali zikiwemo za biashara, uwekezaji, mafunzo ya ufundi, ajira kupitia sekta ya misitu, ushirikiano katika majukwaa ya kimataifa kwa kuzingatia usawa, pamoja na kuwajengea uwezo wanawake na watoto.

Aidha, Mhe. Soini alitoa shukrani zake za dhati kwa Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuhifadhi wakimbizi na mchango mkubwa katika usuluhishi wa migogoro inayozikabili baadhi ya nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu. Hivyo, walikubaliana kuendelea kushirikiana katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiusalama ikiwa ni pamoja na biashara ya madawa ya kulevya, biashara haramu ya kusafirisha binadamu, na matishio ya ugaidi.

Kabla ya mazungumzo hayo, Mhe. Balozi Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na Bw. Sampo Suihko, Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha OMNIA Espoo ambaye alieleza utayari wa Taasisi yake wa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kubadilishana uzoefu wa kutoa mafunzo ya elimu ya ufundi yanayoendana na soko la ajira.

Mhe. Mahiga pia alifanya mazungumzo na Mhe. Matti Ahtisaari, Rais Mstaafu wa Finland na Mwanzilishi wa Taasisi ya Utatuzi wa Migogoro. Mhe. Ahtisaari aliipongeza Tanzania kwa kazi nzuri inayofanya katika utatuzi wa migogoro kwenye nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu na kusihi kuendeleza jitihada hizo kwa ustawi wa Dunia nzima.

Vilevile, Dkt. Mahiga alifanya mazungumzo na Bw. Jukka Kallio, Makamu wa Rais wa Helsinki. Katika mazungumzo hayo, uongozi wa Bandari ya Vuosaari umeahidi kushirikiana na uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania katika kuboresha mifumo ya kidigitali (Digitalization) itakayoongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam.

Katika kuhamasisha uwekezaji wa viwanda nchini, Mhe. Waziri Mahiga alifanya mazungumzo na Jumuiya ya Wafanyabiashara (Business Finland) na Makampuni makubwa ya kibiashara nchini humo. Wafanyabiasha hao walipongeza jitihada zinazoendelea kufanyika nchini Tanzania katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na waliahidi kuwekeza na kushawishi makampuni mengine kuona umuhimu wa kuwekeza nchini Tanzania.

Mhe. Waziri anahitimisha ziara hiyo kwa kufanya mazungumzo na Bi. Anne-Mari Virolainen, Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland; Bw. Mauri Pekkarinen, Naibu Spika wa Bunge la Finland, Bw. Juhan Damski, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya nchini Finland na baadaye kuzungumza na Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Finland.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
26 Februari 2019

WATUMISHI SEKTA YA AFYA WAASWA KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA

$
0
0
Na WAMJW - MTWARA
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewaasa watumishi wa wekta ya afya nchini kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea, na wajikite katika kutoa huduma kulingana na sheria na taratibu za taaluma zao.

Ameyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya kwa wananchi katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara - Ligula.

Katika ziara hiyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa licha ya jitihada za kuboresha huduma za afya kwa wananchi, ni wajibu wa kila mtoa huduma za afya nchini kuhakikisha anatimiza wajibu wake bila shurti na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

"Nyinyi mnafanya kazi kwa mazoea, kwa nini hamjajaza taarifa wala kusaini katika fomu ya wagonjwa, na hili linaendana na maelekezo ambayo Serikali tunawapa, kwamba kila mtu aandike tarehe na muda ambao amefanya kazi, nyinyi maabara hamfanyi" alisema Dkt. Ndugulile

Pia, Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeboresha vituo vya afya zaidi ya 300, ambavyo vitatoa huduma za dharura za upasuaji wakumtoa mtoto tumboni, na hospitali za wilaya 67, katika Mkoa wa Mtwara hospitali za wilaya 3 zinaenda kujengwa, ili kupunguza mzigo katika hospitali za mikoa,

Aidha, DKt. Ndugulile amesema kuwa amesema kuwa kutokana na Hospitali hiyo kuwa na Changamoto za x-ray na gari la kubebea Wagonjwa, Serikali imeahidi kuzitatua changamoto hizo kwa muda mfupi ili wananchi wa Mtwara waanze kupata huduma hizo mara moja.

"Mmeongelea huduma za mionzi (x-ray), niwaahidi tutawaletea mashine mpya ya x-ray za kidigitali, lakini vile vile kama kuna changamoto ya gari la kubebea wagonjwa, zikija tutazigawa, tunataka hospitali za mikoa zianze kuonekana kwamba ni hospitali za mikoa kweli" alisema Dkt. Ndugulile

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali inatambua pengo la watumishi katika sekta ya afya,  hivyo mwaka uliopita iliweza kuajiri watumishi takribani 11,000, huku watumishi 3000 kuziba pengo la watumishi ambao hawakuwa na vigezo, na 8000 walikuwa ni ajira mpya.

"Tumeweza kuajiri Watumishi takribani 11,000, 3000 kuziba pengo la watumishi ambao hawakuwa na vigezo na vyeti, na ajira mpya ni 8000, kuwahiyo jumla watumishi 11, kadri tunavoendelea kupata uwezo tutaendelea kuongeza rasilimali watu kuhakikisha kwamba tunaziba mapengo yaliyopo" alisema DKt. Ndugulile.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Kadi inayoonesha Idadi ya Dawa katika Chumba cha dawa, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua  Idadi ya Wagonjwa waliosajiliwa kwenye mfumo, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipokea daftari la mama aliyemleta mwanae kupata huduma katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo. Wakatikati ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Lobikieki Kissambu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua mkoba wa Vifaa vya kujifungulia, wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.

JICA’S EXECUTIVE SENIOR VICE PRESIDENT ARRIVES IN TANZANIA FOR A THREE – DAY LANDMARK OFFICIAL VISIT

$
0
0
The Executive Senior Vice President of Japan International Cooperation Agency, JICA, Mr. Kazuhiko KOSHIKAWA is scheduled to make a three-day official visit to Tanzania from February 27 to March 1, 2019. 

Mr. Kazuhiko KOSHIKAWA will also observe some of the JICA-supported projects in Dar es salaam and in Kilimanjaro Regions. 

In Dar es salaam he is expected to witness the Contractor Signing Ceremony of the Project for the Widening of New Bagamoyo Road (Mwenge – Morocco Section) tentatively scheduled for February 28, 2019 and in Kilimanjaro, he is expected to observe activities of the Project for Supporting Rice Development Industry in Tanzania commonly known as TANRICE Project 2 at the Lower Moshi Irrigation area on March 1, 2019. 

JICA is the world’s largest bilateral aid agency which works in over 150 countries and regions and has some over 100 overseas offices including the one in Tanzania. 

JICA Tanzania Office was officially opened in 1980 although Japanese assistance to the country commenced in 1962 with the acceptance of participants for technical training in Japan. Working closely with the Government, JICA’s operations in the country have continued to grow and expand over the years and now include not only technical cooperation but also the provision of grant aid and concessionary loans. 

JICA’s cooperation activities are in line with Tanzania Government’s development agenda which gives priority to sectors such as agriculture, industry, infrastructure development as well as the improvement of public services. 

JICA’s flagship projects include such projects as: Selander Bridge (1980), Mfugale Flyover (2018) etc. 

Projects currently being implemented range from quality infrastructure projects, health, water and energy to agriculture and education projects etc.

Walioigiza kuwa rais wa Kenya wakamatwa

$
0
0
Polisi nchini Kenya wamewakamata watu saba wanaodaiwa kushirikiana kuigiza sauti ya rais Uhuru Kenyatta na maafisa wengine wa serikali katika kumuibia pesa nyingi mfanyabiashara tajiri nchini humo -Naushad Merali.

Mmoja wa watu hao alimpigia simu Bwana Merali, ambaye ni mwenyekiti wa Sameer Africa, akiigiiza sauti ya rais Uhuru kenyatta akimshawishi ampatie pesa za kusaidia mipango ya biashara, kulingana na polisi.

Fedha kamili zilizoibiwa bado hazijafahamika wazi - mtandao wa habari wa gazeti la Daily Nation news umeelezea kuwa zilikuwa ni shilingi milioni 10 ($100,000; £76,000) huku gazeti la Star likisema pesa hizo zilikuwa ni shilingi milioni 80.

Saba hao walifikishwa mhakamani Jumanne, lakini bado hawajashtakiwa.

Polisi wamesema wanahitaji musa zaidi wa kufanya uchunguzi.

"kutokana na ugumu wa uchunguzi na idadi ya washukiwa wanaohusika , wakiwemo wale ambao bado hawajapatikana , uchunguzi unatarajiwa kujumuisha nyaraka nyingi zikiwemo zile za benki pamoja na uchunguzi wa kina wa data za mawasiliano simu ," ilieleza ripoti ya polisi iliyonukuliwa na gazeti la Daily Nation.

KUSOMA ZAIDI BOFYA BBC Swahili.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images