Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

MEJA JENERALI KINGU AKASIRIKA SPIDI UJENZI JENGO JIPYA LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KATIKA MJI WA SERIKALI IHUMWA JIJINI DODOMA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akilikagua jengo jipya la Wizara yake linalojengwa katika Mji wa Serikali, Ihumwa, jijini Dodoma, wakati alipofanya ziara katika eneo hilo leo, kwa lengo la kukagua ujenzi unavyoendelea. Meja Jenerali Kingu amemtaka Mkandarasi afanye kazi usiku na mchana ili ndani ya mwezi huu wa Februari awe amemkabidhi jengo hilo.

Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akizungumza na Wakandarasi wa Ujenzi wa Jengo jipya la Wizara yake, Mshauri Mwelekezi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), pamoja na wawakilishi wa Wizara yake wanaosimamia ujenzi unaoendelea wa jengo hilo katika Mji wa Serikali, Ihumwa, jijini Dodoma. Kingu amemtaka Mkandarasi afanye kazi usiku na mchana ili ndani ya mwezi huu wa Februari awe amemkabidhi jengo hilo.

Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Aron Lunyungu, akionyesha madirisha ambayo yapo tayari kwa ajili ya kufungwa katika jengo hilo la Wizara. Lunyungu ambaye pia ndiyo Mkandarasi wa Ujezni huo ameagizwa awe amemaliza ujenzi wa jengo hilo na kumkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mwezi huu wa Februari.

……………………

Na Felix Mwagara, MOHA.

KATIBU Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, amemtaka Mkandarasi anaejenga Jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma, afanye kazi usiku na mchana ili ndani ya mwezi huu wa Februari awe amemkabidhi jengo hilo.

Meja Jenerali Kingu amesema kasi ya ujenzi huo umenza kusuasua kwasababu Wizara yake ilifikia hatua kubwa lakini sasa imepitwa na baadhi ya Wizara kutokana na Mkandarasi anayejenga jengo hilo kupunguza kasi ikiwa ni tofauti na ile walioanza nayo awali.

Katibu Mkuu aliyazungumza hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika eneo hilo la ujenzi, jijini humo, leo, na alifanya ukaguzi na baadaye alizungumza na wadau kutoka pande tatu zinazoshirikiana katika kufanikisha ujenzi huo ambao ulianza mwezi Desemba mwaka jana.

Wadau wa pande tatu wanaofanikisha ujenzi huo ni Mmiliki wa Jengo hilo ambaye ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mshauri Mwelekezi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) pamoja na Mkandarasi ambaye ni Jeshi la Magereza.

“Nimepokea taarifa ya ujenzi unaoendelea, lakini sijaridhishwa nayo kutokana na asilimia ya ujenzi huu ulipofikia mpaka sasa, mmenipa ratiba mpya ya kukamilika kwa jengo hili, kasi yenu imekua ndogo mpaka tumeanza kupitwa na baadhi ya Wizara ambazo sisi tulikua tunaongoza, sasa nataka mfanye kazi hii usiku na mchana ili ndani ya mwezi huu wa Februari ujenzi huu uwe umekamilika na mnikabidhi jengo hili,” alisema Meja Jenerali Kingu.

Kwa upande wake Mshauri Mwelekezi wa ujenzi wa jengo hilo kutoka TBA, Arch. Hassan Mnandala alimwambia Katibu Mkuu huyo kuwa, ataendelea kusimamia na kushauri ili Mkandarasi awe amemaliza kazi hiyo kwa wakati kama ratiba ilivyopangwa.

Naye Mkandarasi wa ujenzi huo, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP) Aron Lunyungu, kwa upande wake amesema ujenzi huo unaendelea na tayari ujenzi wa kuta umefanyika, na imefikia usawa wa kupaua na tayari upigaji wa ripu ndani ya jengo hilo umefanyika.

“Tunamshukuru Katibu Mkuu Meja Jenerali Kingu, leo katutembelea na ametuagiza tujipange ili tuweze kukamilisha kwa wakati ujenzi wa jengo hili, nasi tumejipanga kazi tutaifanya usiku na mchana kuhakikisha jengo hili tunalikamilisha na tunalikabidhi kwa wakati,” alisema ACP Lunyungu.

MAMA WA MITINDO KUNOGESHA DMV LADIES NITE WASHINGTON DC USA

$
0
0
Mama wa mitindo Asya Khamsin kunogesha DMV LADIES NITE ITAKAYOFANYIKA WASHINGTON DC USA SIKU YA TAREHE  9 FEBRUARY 2019  KATIKA UKUMBI ULIOPO KATIKA FLYER KUANZIA SAA 11 jioni hadi saa 5 usiku wahi tiket yako mapema

RAIS MAGUFULI AMJULIA HALI MBUNGE KITWANGA ALIYELAZWA HOSPITALI MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Charles Kitwanga 8-min
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Mbunge wa Misungwi,Charles Kitwanga ambaye amelazwa katika Hospitali  ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa matibabu.Picha na IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Februari, 2019 amemjulia hali Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe. Charles Kitwanga ambaye amelazwa katika wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam kwa matibabu.

Mhe. Kitwanga alilazwa hospitalini hapo tangu tarehe 31 Januari, 2019.


Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Dkt. Juma Mfinanga amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa hali ya Mhe. Kitwanga inaendelea vizuri ikilinganishwa na wakati alipofika hospitalini hapo.


Akiwa wodini hapo Mhe. Rais Magufuli ameshiriki sala ya kumuombea Mhe. Kitwanga ilia pone haraka na amewashukuru Madaktari na Wauguzi kwa juhudi kubwa wanazozifanya kuwahudumia wagonjwa.



UFAFANUZI WA KODI YA MABANGO

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE ATEMBELEA MABANDA YA MAADHIMISHO WIKI YA SHERIA, LEO JIJINI DODOMA

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Msemaji wa Jeshi la Magereza, SP. Amina Kavirondo(kulia katikati) alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza leo Februari 2, 2019 katika Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea jijini Dodoma. 

 Mtendaji wa Mahakama Kuu, Bw. Leonard Magacha akimtembeza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto) katika mabanda ya Mahakama ya Tanzania alipotembelea leo Februari 2, 2019 katika Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea jijini Dodoma. 

 Maafisa washiriki katika Banda la Tume ya Utumishi wa Mahakama(kushoto) wakitoa maelezo namna Tume hiyo inavyotenda kazi zake mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) katika mabanda ya Mahakama ya Tanzania alipotembelea leo Februari 2, 2019 katika Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea jijini Dodoma. 


Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiteta jambo na Bregedia Jenerali Mkande walipokutana leo Februari 2, 2019 jijini Arusha(Picha na Jeshi la Magereza).

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kushoto) akisaini kitabu cha wageni katika Banda la Jeshi la Polisi alipotembelea leo Februari 2, 2019 katika Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea jijini Dodoma.                                            

Kijana wa miaka 18 akabidhiwa milioni 10 za Biko Ukerewe Mwanza

$
0
0
Na Ripota Wetu, Mwanza.

Kijana mdogo mwenye umri wa miaka 18 tu kutokea kisiwani Ukerewe, mkoani Mwanza, anayejihusisha na ujasiriamali, Cathbert Masanal, amekabidhiwa fedha sake alizoshinda kutoka kwenye Bahati nasibu ya Watanzania ya Biko, akitokea kwenye droo ya 177 ijulikanayo kama Jumatamu Jenga.

Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Mwanza kwa kumpatia mamilioni yake mshindi huyo aliyeanza rasmi harakati zake za kimaisha kwasababu ya kuingia kwenye umri wa ujana wa miaka 18, hivyo ni wazi ameanza vizuri kwenye mbio hizo za kimaisha.

Akizungumzia ushindi wake huo, Manasal alisema kushinda fedha za biko kutarahisisha maisha yake kwa kuhakikisha kwamba anafanyia kitu cha maana ili ushindi huo uweze kumnufaisha kwa namna moja ama nyingine.

Kucheza Biko sasa ni kuanzia sh 500 na sh 1000 na kuendelea, huku ushindi wake ukianzia sh 1000 hadi sh 100000 kwa watakaocheza sh 500 hadi sh 9500 wakati watakaocheza kwa sh 1000 na kuendelea, mchezaji anaweza kujishindia zawadi ya papo kwa hapo kuanzia sh 5000 hadi sh milioni moja bila kusahau wote kuingia kwenye droo kubwa ya Jumatano na Jumapili.

Bahati nasibu ya Biko inachezwa kwa mitandao ya simu minne ambayo ni Tigo Pesa, M-Pesa, Artel Money na HaloPesa, ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu namba 2456, huku Watanzania wakiweza kujishindia zawadi kubwa katika droo ya Jumatano na Jumapili.
 Kijana mwenye miaka 18 tu kutoka Kazilankanda, wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza, Cathbert Marco Masanal, akionyesha pozi baada ya kukabidhiwa fedha zake sh milioni 10 alizoshinda katika bahati nasibu ya Watanzania ya Biko droo ya 177 maarufu kama Jumatamu Jenga iliyotoa washindi sita wa mamilioni na bodaboda. Picha na Mpigapicha Wetu.
 

MITAA MITATU KATA YA PANGANI WANUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA VIKAWE

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

KERO kubwa ya maji safi na salama iliyokuwa ikiwakabili kipindi kirefu ,wakazi wa mitaa mitatu ya miwale, vikawe shule na vikawe Bondeni, kata ya Pangani ,Kibaha, mkoani Pwani imepata mkombozi baada ya kukamilika kwa mradi wa maji ambao utapunguza kero hiyo. 

Wakizungumza wakati mbunge wa jimbo la Kibaha Mji, Silvestey Koka alipokwenda kukagua miradi ya maendeleo kata ya Pangani, walieleza kipindi cha nyuma walikuwa wakitumia maji ya visimani yasiyo salama kiafya. 
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amkitwisha ndoo ya maji mmoja wa akina  mama


Grace Sinzuki na Maua Mussa walisema walitumia muda mwingi nyakati za usiku na mchana kwa ajili ya kutafuta huduma hiyo. "Visima vilikuwa mbali kufikika ,tulikuwa tunaacha kulala waume zetu kitandani kwenda kusaka maji hivyo mradi huu utakuwa ni mkombozi mkubwa "alifafanua Grace. 

Maua alisema, hivi karibuni Koka alifanya ziara Vikawe na kupata malalamiko juu ya kusuasua kwa mradi huo ,na alilazimika kuunda kamati ndogo ili kufuatilia DAWASA Bagamoyo ambayo sasa imeuchukua mradi na kuanza kazi. 

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka aliahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya awamu ya tano na mamlaka zinazohusika kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika baadhi ya maeneo. 

Koka alieleza lengo la serikali ni kumtua ndoo mama kichwani, hivyo ni wajibu wake kusimamia kero iliyopo ili wananchi wasambaziwe maji majumbani. Nae mhandisi wa miradi ya DAWASA wilayani Bagamoyo ,Hamad Omary alisema kwamba lengo lao ni kuhakikisha wanaboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi .

Alifafanua juhudi zinaendelea kufanyika ili wananchi waweze kuondokana na changamoto ya kutembea umbali mrefu ikiwa ni pamoja na kufufua vizimba ambavyo vilikuwa vimekufa.

DC KITETO AWATAKA WAFUGAJI NA WAKULIMA KUTOVAMIA MAENEO YA HIFADHI

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, mhandisi Tumaini Magessa akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Lairumbe Mollel akifungua kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Diwani wa kata ya Makame Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, Jacob Nini (CCM) akiapishwa baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, awali alijiuzulu kwa kuondoka Chadema kwa kumuunga mkono Rais John Magufuli na Mkuu wa mkoa huo Alexander Mnyeti.
 
…………………….
MKUU wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, mhandisi Tumaini Magessa amewataka wakulima na wafugaji kutovamia maeneo ya hifadhi kwa kupotosha kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa hivi karibuni juu ya vijiji 366 vinavyopakana na hifadhi. 

Mhandisi Magessa aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo. Mhandisi Magessa alisema baadhi ya wafugaji na wakulima hawakuelewa ipasavyo taarifa ya hiyo hivyo kusababisha upotoshwaji. 

Alisema baada ya taarifa hiyo kutolewa baadhi ya wafugaji na wakulima walijiandaa kulima na kufugia mifugo ambayo itasababisha migogoro upya.
“Kwenye hivyo vijiji 366 vilivyotajwa na Rais Magufuli na kunufaika na tamko hilo sisi Kiteto tuna vitongoji viwili pekee sasa hao wengine wasiokuwepo wasijiingize huko,” alisema mhandisi Magessa. 

Alisema utaratibu ulishawekwa vizuri juu ya maeneo hayo na wao kama serikali ya wilaya hawatakubali kuona watu wachache wanawaingiza kwenye migogoro. Diwani wa Kata ya Partimbo, Paul Tunyoni alisema baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto linapaswa kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwajali wafugaji na wakulima. 

Tunyoni alisema kauli ya Rais Magufuli ya kuwajali wanyonge na kuhakikisha jamii ya wafugaji na wakulima wanafaidi rasilimali zilizopo ni jambo la kupongezwa. 
Hata hivyo, mbunge wa jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian alisema pori la akiba la Mkungunero linatambulika kisheria hivyo baadhi ya viongozi wasipotoshe hilo. Papian alisema kumekuwepo na wapotoshaji juu ya kauli ya Rais Magufuli juu ya sehemu zenye migogoro ya hifadhi na jamii inayowazunguka. 


Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Lairumbe Mollel alisema wananchi wanapaswa kuwa watulivu wakati huu ambapo serikali inaweka utaratibu vizuri. Mollel alisema wananchi wote wanapaswa kusubiri ili uhakiki ufanyike kwa ushirikishwaji wa uwazi kuliko kuingia sehemu zisizoruhusiwa na kuzua migogoro upya.

DKT. MWANJELWA ASHIRIKI KUPANDA MITI KUTEKELEZA KWA VITENDO KAMPENI YA MAKAMU WA RAIS YA KULIFANYA JIJI LA DODOMA KUWA KIJANI

$
0
0

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akipanda mti katika eneo la ofisi yake inayojengwa kwenye mji wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akitoa maelekezo kwa Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba wakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo la ofisi yake inayojengwa kwenye mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba akiandaa eneo kwa ajili ya kupanda mti wakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inayojengwa kwenye mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma.

…………………………..

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) mapema leo amewaongoza watumishi wa ofisi yake kupanda miti katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inayojengwa kwenye Mji wa Serikali, Ihumwa jijini Dodoma ili kutekeleza kwa vitendo kampeni ya Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa la kijani.

Mhe Dkt. Mwanjelwa (Mb) amesema, watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora kama kioo cha Utumishi wa Umma nchini, wamejitokeza kuunga mkono kwa vitendo kampeni hiyo ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani kwa kupanda miti ili kuwa mfano bora kwa taasisi nyingine za umma ambazo hazijatekeleza kampeni hiyo.

Akiongoza zoezi hilo, Mhe Dkt. Mwanjelwa (Mb) amesema, pamoja na kuunga mkono kampeni ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora inatambua kuwa mazingira ni uhai ndio maana Jumamosi hii, yeye pamoja na watumishi wa ofisi yake wamejitokeza kwa wingi kupanda miti.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa (Mb) amewataka watumishi wa ofisi yake kuendelea na moyo wa kujituma katika utekelezaji wa kampeni ya kulifanya jiji la Dodoma ambalo ni Makao Makuu ya Nchi kuwa la kijani.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa (Mb) amewataka watumishi hao kuhakikisha wanahudumia miti hiyo ili iweze kustawi na kulifikia lengo la kuwa na Dodoma ya kijani.

CCM BAGAMOYO YAPOKEA WAPINZANI WATANO KATA YA PERA

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE 

KATIKA kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 42 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kata ya Pera Chalinze, Bagamoyo, Shawali Ndembo amekihama chama hicho na kukimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Pia wanachama wengine wanne kutoka chama hicho wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM. 

Akimpokea Ndembo wakati wa sherehe za maadhimisho hayo wilaya ya Bagamoyo, yaliyofanyika Pingo kata ya Pera, mwenyekiti wa CCM Bagamoyo, Abdulsharif Zahoro alisema ilani ya chama inatekelezwa na kuleta heshima kwa wananchi. 

Alisema, serikali ya awamu ya tano inaitendea haki ilani hiyo hivyo kazi kubwa kwa wanaCCM ni kuisemea serikali kwa yale inayotekeleza na kutatua changamoto mbalimbali kwa watanzania. "Nampongeza mwenyekiti wetu wa CCM Taifa, Dk.John Magufuli kwa kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM kwa vitendo "alisema Sharif. 

Sharif ,alisema uongozi ni dhamana mwenyekiti wa kitongoji na vijiji wafanye ziara za kuelezea utekelezaji wa ilani na kutimiza wajibu wao ili kukiweka chama sehemu nzuri uchaguzi serikali za mitaa 2019.

Hakusita kukemea makundi ambayo kwa upande mwingine yanasababisha migongano baina ya wanachama na kusababisha kukiyumbisha chama. 
Aliwaasa viongozi na wanaCCM kujenga umoja,upendo,mshikamano ili kukiimarisha chama hicho. 

Awali akirudisha kadi ya CHADEMA, Ndembo alimpongeza na kumwagia sifa Rais dk. John Magufuli kwa kuitendea haki ilani ya chama kivitendo. 
"Vyama vya upinzani vilikuwa vikihitaji utatuzi wa kero na changamoto, sasa Tanzania inaneemeka, uchumi unapanda siku hadi siku, kutokana na hayo ni vema nije CCM ,kwakuwa kule nilipotoka hakuna jipya "alifafanua Ndembo. 

Nae mwenezi wa CCM Bagamoyo ,John Francis Bolizozo alisema tukielekea katika chaguzi mbalimbali zijazo, wamejipanga kushinda kwa kishindo uchaguzi wa serikali ya mitaa na hatimae madiwani na urais 2020.

Katika maadhimisho hayo kiwilaya waliweza kujitolea nguvu kazi kwenye ujenzi unaoendelea shule ya sekondari Pera na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa ofisi ya tawi la CCM Pingo .
Mwenyekiti wa CCM Bagamoyo, Abdulsharif Zahoro (kulia) akimpatia kadi ya CCM, katibu wa CHADEMA kata ya Pera, Shawali Ndembo ambae amekihama chama hicho na kujiunga na CCM, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 42 ya CCM wilaya ya Bagamoyo, yaliyofanyika Pingo kata ya Pera.(picha na Mwamvua Mwinyi) 
Mwenyekiti wa CCM Bagamoyo, Abdulsharif Zahoro akimvisha fulana ambayo ni sare ya chama cha mapinduzi, katibu wa CHADEMA kata ya Pera, Shawali Ndembo ambae amekihama chama hicho na kujiunga na CCM, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 42 ya CCM wilaya ya Bagamoyo, yaliyofanyika Pingo kata ya Pera.(picha na Mwamvua Mwinyi) 

Ofisi za RC na Dc zisiwe mahakama

$
0
0
Wiki ya kutoa  elimu na ushauri wa kisheria imezinduliwa katika Mkoa wa Shinyanga mapema leo tarehe 02/02/2019 huku watendaji wa Idara mbalimbali wakitakiwa kutenda haki kwa wananchi ili kupunguza malalamiko kwenye ofisi za Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa. 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amesema wananchi wengi wanakwenda kwenye Ofisi yake na Mkuu wa Wilaya kulalamika kuhusu kutokamilika kwa mashauri yao Mahakamani.

" Nimechoka kusikia Shinyanga ikizungumziwa kwa rushwa rushwa, watu wanakimbia mahakamani kwa sababubhawatendewi haki, wanakuja Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wilaya ndiyo kwenye haki"

Mhe. Telack amesisitiza kuwa, hawezi kukaa akaangalia wananchi wakilalamika watumishi kuwataka rushwa ili kutekeleza majukumu yao.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe,. Zainab Telack akisaini kitabu cha wageni huku akipata maelekezo ya Afisa Huduma kwa jamii kutoka Idara ya huduma za uangalizi,Wizara ya mambo ya ndani, Bi Monica Dawa.
Mkuu w Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, akielekea kwenye mabanda ya wadau wa sheria katika kuzindua wiki ya sheria Duniani, Mkoani Shinyanga mapema leo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Venant Mboneko.

JUSTINE KASUSURA: MBONGO ALIYEFUNGWA 'KWA KUPIGA PESA NDEFU.

$
0
0

JUSTINE KASUSURA:  MBONGO ALIYEFUNGWA "KWA KUPIGA PESA NDEFU" KTK HISTORIA YA TZ NA KISHA KUKIPANGUA KIFUNGO HICHO BILA WAKILI MAHAKAMA YA RUFAA TZ!!!


1. Usuli:

Watanzania nchini kote, kuanzia Ntwara hadi Kagera, Ijumaa ya tarehe 3.8.2001 saa 2 usiku, walipigwa bumbuwazi na kushindwa kuamini, pale walipomshuhudia luningani, SACP ALFRED TIBAIGANA, aliyekuwa RPC Kanda Maalum Dsm kuanzia 2001-2008, akitoa "Breaking Newz" kwa waandishi wa habari kuhusu unyan'ganyi wa $ 2M (TZS 4.400.000.000/=) uliokuwa umetokea jana yake majira ya saa 5 asubuhi nje kidogo ya "Airport" ya JKIA, ukiwa ni unyang'anyi wa kihistoria wa fedha nyingi kuwahi kutokea nchini ulioweka rekodi kipindi hicho.

RPC TIBAIGANA aliujuza umma kwamba mtuhumiwa wa unyang'anyi huo ni  pandikizi la mtu lenye wajihi wa miraba minne liitwalo JUSTINE KAKURU KASUSURA, dereva wa kampuni ya ulinzi ys Knight Support yenye makao makuu yake eneo la Victoria, Dsm. Mzee baba" huyo alikuwa "amesepa na burungutu la fweza kama zote" na kutokomea kusikojulikana na kwamba "msako wa kufa mtu" ulikuwa umeanza kurindima nchi nzima hususan maeneo ya mipakani. Mwisho, RPC TIBAIGANA alitoa rai kwa wananchi na wasamaria wema kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kufanikisha kumkamata mtuhumiwa huyo.

2. Miezi 5 Ikapita KASUSURA Hajulikani aliko

Licha ya kumtafuta maeneo mbalimbali, lakini KASUSURA hakuweza kutiwa mbaroni kwa miezi 5.

2. KASUSURA Abambwa Hotelini, Mbeya Usiku wa Manani!

Baada ya kupita miezi 5, huku wananchi wengi wakiamini kuwa kwa "mbumba" zote zile lazma "Mzee Mzima" KASUSURA atakuwa "amesepa" kwenda nje ya nchi na kwamba sasa atakuwa "akila bata refu" kwenye "viwanja vya mbele" kama Hawaii au Bahamas, walipigwa mshangao mkubwa ilipotangazwa kwamba KASUSURA amekamatwa  usiku wa manani, jumatatu ya tarehe 24.12.2001(Christmas Eve), kwenye hoteli ijulikanayo kama "Three In One" iliyoko maeneo ya Soweto, Mbeya.

KASUSURA alikuwa amefikia hotelini hapo siku ya Jumapili, tarehe 23.12.2001 saa 12 jioni akitokea Sumbawanga na kujifanya ni mfanyabishara. Wakati akiwasili hotelini hapo, KASUSURA alikuwa amevaa kofia kubwa kuficha uso wake na akapewa chumba na. 101K ambapo katika rejista hakuandika jina la KASUSURA bali aliandika jina JOHN LAIZER na akalipia malazi ya siku moja kwa "buku tatu jero" (TZS 3,500/=).

Jioni ya Jumatatu hiyo, "mandata" walitinga kwenye hoteli hiyo na kuweka mtego kabambe nje na ndani ya hoteli hiyo huku wengine "wakizama" uvunguni na kabatini kama makomandoo wa Kiisraeli!.

Usiku wa manani, siku hiyo ya mkesha wa krisimasi, KASUSURA, huku akiwa yuko "bwaksi" baada ya kuwa "amepiga vyombo" kisawasawa baa, alirejea hotelini hapo akiwa na nungayembe alilojihomolea kwenye baa alikokuwa "akipombeka".

Alipojongea mapokezi, huku akiongea "Kikristu" kiiiingi, kama ilivyo kawaida kwa walevi wengi kupenda kuongea lugha ya "kwa mama" wanapokuwa "bwii", aliomba ufunguo na kuelekea chumbani kwake.

Baada tu ya kufungua mlango na kuwasha taa, KASUSURA akakutana uso kwa uso na "mandata" walioibuka kama "Bruce Lee" kutoka uvunguni na kabatini na kumtia KASUSURA nguvuni kiulaiini kama kumsukuma mlevi! Baada ya KASUSURA kunyakwa "hakuna rangi aliacha kuiona" na pombe zote ghafla zikamuisha kichwani akawa ameduwaa kama "zombi"!. Aliposachiwa alikutwa na TZS 200.000/= tu.!.

3. IGP MAHITA Aeleza Polisi Wamtorosha KASUSURA

Huku wananchi wengi wakilipongeza Jeshi la Polisi kwa kufanikiwa kumkamata KASUSURA, zikaenea taarifa zisizo rasmi kwamba kuna polisi wengi wasio waaminifu walikuwa "wamevuta mkwanja mrefu" na kumsaidia KASUSURA kutokamatwa.  Ilidaiwa kwamba kila polisi walipokuwa wakimkamata KASUSURA  walikuwa "wanavuta mkwanja" kisha wanawapigia simu wenzao mkoa mwingine na "kuwapigia pasi" ili wamkamate na "akizama mfukoni" wanamwachia.Kutokana na sintofahamu hiyo, IGP wa wakati huo, aliyekuwa mtu wa shoka asie na mchezo, Alhaj OMAR IDD MAHITA, ikabidi aongee na waandishi wa habari tarehe 9.1.2002 na kukanusha vikali huku akibainisha kuwa si kweli kwamba polisi wengi wamehusika bali ni wachache tu. IGP MAHITA alifafanua kwamba kuna polisi 8 tu wakiwemo 3 waandamizi wanaodaiwa kumsaidia KASUSURA kutoroka walikuwa wamekamatwa na kusimamishwa kazi.

IGP MAHITA aliwataja polisi hao kuwa ni SSP BONAVENTURE MSHONGI(RCO- Tanga), ASP BEATRICE MAONA na ASP DEUSDEDIT KAJUNA(Ofisi ya RCO, Dsm), C.236 Sgt EMMANUEL na Konstebo ROGATHE(Tanga), E.7014 Konstebo ISAACK, E. 7603 Konstebo DAVID na E. 8042 Konstebo JEREMIAH.

4. DCI ADADI Aeleza "Kufyekelewa mbali" kwa Polisi 5"

Tarehe 15.1.2002, aliyekuwa DCI, ADAD MOHAME RAJAB, aliufahamisha umma kwamba Jeshi la Polisi lilikuwa limewafikisha Mahakama ya Kijeshi polisi 5 ambapo walipatikana na hatia ya utovu wa nidhamu na kutozingatia maadili ya polisi.

DCI ADADI, akiwa amekunja ndita na kuonesha kukerwa, alitiririka:
"Jeshi la Polisi limewafukuza kazi polisi wafuatao C. 236 Sgt EPHRAIM, E. 635 Konstebo ROGATHE, E.7014 Konstebo ISAACK, E. 7603 Konstebo DAVID na E. 8042 Konstebo JEREMIAH. Hawa walikuwa wamefunguliwa mashtaka Mahakama ya Kijeshi na wamefukuzwa kazi kwa kukiuka maadili ya polisi na watashtakiwa mahakama za kiraia. Polisi hao walimkamata na kumuachia KASUSURA zaidi ya mara 3 Dsm, Tanga na Arusha, kitendo ambacho kimelitia aibu jeshi la polisi".

5. KASUSURA na "Wenzake" 6 Wafikishwa kwa "Pilato" Kisutu

KASUSURA, baada ya kuandika maelezo yake, alifikishwa mahakama ya Kisutu tarehe 7.1.2002 na Land Rover Defender No. PT 0881 akiwa pamoja na washtakiwa wengine 6 ambao ni WICKLIFF URASSA, LEONARD URASSA, LUCY URASSA(32-Mwanafunzi wa IFM) PROFILY KWEKA, WÌLLIAM MBETWA na LIBENT LIKUNDWA. Mahakama ya Kisutu ilijaa hadi pomoni kwani wakazi wa jijini la Dsm wanaosifika kwa kupenda "ubuyu" walitinga mahakamani hapo mapema kabisa kujione wenyewe huyo KASUSURA anafananaje.

Mwendesha mashtaka, ACP RAINHARD LISAPITA,  aliwasomea mashtaka 5 ya Kula njama, Unyang"anyi wa kutumia silaha, Wizi na Makosa 2 ya Kupokea Mali ya Wizi. KASUSURA alikuwa akitetewa na Wakili nguli na bingwa a kupangua kesi za jinai, MAJURA MAGAFU. Washtakiwa wote walikana mashtaka yao hivyo upande wa mashtaka ukaita mashahidi kuthibitisha mashtaka.

6. Mahakama ya Kisutu yaelezwa "Mchezo -Mzima" Ulivyokuwa:

Mashahidi wa upande wa mashtaka walieleza kwamba asubuhi ya siku ya tukio, 2.8.2002, KASUSURA alikabidhiwa na viongozi wake gari aina ya Toyota Hilux Double Cabin TZL 3742 isiyopenya risasi ili kwenda JNIA kuchukua mzigo.

KASUSURA akaelekea JKIA akiwa na mwenzake, SAID MUSSA, aliyekuwa na jukumu la kupokea mzigo uliokuwa umewasili kwa Swiss Air ukiwa ni mali ya Citibank ambaowalikuwa wameingia kandarasi na kampuni ya Knight Support kuwapelekea mzigo huo ofisini kwao.

DAHACO walimkabidhi SAID MUSSA mzigo huo majira ya saa 4.30 asubuhi na akauweka vizuri nyums ya gari kisha akafunga kwa ufunguo. 

KASUSURA akawasha gari na kuanza kuondoka JNIA na alipokunja kulia ili kuanza kuelekea mjini, "Mzee baba" KASUSURA "alijifanya kama anajikuna" kisha akaliegesha gari hilo mbele ya magari 2 aina ya Toyota Landcruiser na Toyota Corrola. Ghafla bin vuu, KASUSURA, kama VAN DAME, akatoa pisto na kumnyooshea SAID MUSSA na kumwambia _"Huu ndio mwisho wa mchezo"_na kumwamu "aishie". KASUSURA akamnyang"anya MUSSA funguo akaushusha mzigo huo akisaidiwa na watu wengine waliokuwa kwenye gari zile 2. MUSSA, baada ya kimuhemuhe hicho, alienda kuripoti kituo cha polisi ambapo alishikiliwa na kuanza kuisaidia polisi.

Upande wa mashtaka ulipofunga kesi yao, mahakama ilimuona KASUSURA peke yake ndiye mwenye kesi ya kujibu hivyo iliwaachia huru washtakiwa wengine wote.

Huku kesi hii ikiwa inaunguruma,  tarehe 16.1.2002, maafisa 8 wa polisi(3 wa ngazi za juu aliwemo mwanamke mmoja) na 5 wa ngazi za chini walifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali na kusomewa mashtaka 2 ya Kula njama ya kumtorosha KASUSURA na Kupokea rushwa toka kwa KASUSURA.

KASUSURA, bada ya kuonekana ana kesi ya kujibu,  alitoa utetezi na kuelezea kuwa mashahidi wote wa upande wa serikali walikuwa "wameipiga fiksi" mahakama kwa hekaya zao za Abunuwasi. KASUSURA alidai kwamba ukweli ni kuwa yeye wakati aliendesha ile "ndinga" aliyokabidhiwa na ofisi yao ya Knight Support na baada ya kuchukua mzigo huo uliokuwa na "mbumba za kufa mtu" ghafla alipoanza kuendesha na akiwa nje kidogo ya JNIA "Watu wenye Kazi zao" yaani "Mabandido" walimteka na kusepa na "Mkwanja" wote!.

Huku kesi ikiwa inanguruma, KASUSURA alifiwa na mkewe,  Bi. FAUZIA LAIZER  tarehe 22.2.2005. KASUSURA alimuomba hakimu ruhusa ya kwenda kumzika mkewe ambaye alikuwa akifika mahakamani hapo kila mara na mtoto wao wa miaka 9. 

Mh. Hakimu "alimchinjia baharini" KASUSURA kwa kusema: "Mahakama imetupilia mbali ombi la KASUSURA. Hatusemi kama itatokea, lakini ikitokea mshtakiwa akatoroka, wote tutawajibika".

Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote, Mh. Hakimu SILVANGILWA MWANGESI alitoa hukumu siku ya Ijumaa tarehe 30.3.2007 ambapo "alimpiga" KASUSURA "mvua" 30 kwa kosa la unyang'anyi na "mvua" 5 kwa kosa la wizi na kwamba atatumikia miaka 35 lupango (consecutively).

7. Polisi 8 Waachiwa huru

Polisi 8 waliokuwa wameshtakiwa kwa kudaiwa "kuvuta mbumba" na kumtorosha KASUSURA waliachiwa huru na mahakama hiyo.

SSP BONAVENTURE MSHONGI, aliyekuwa RCO wa Tanga wakati wa msala huo, alikuja kupandishwa cheo na kuwa ACP. Aidha, aliteuliwa kuwa RPC Pwani kabla ya kuhamishiwa Simiyu ambako analitumikia taifa lake vizuri tu na kwa weledi na uadilifu wa hali ya juu.

8. Wakili MAJURA MAGAFU Akata Rufaa Mahakama Kuu

MAJURA MAGAFU, wakili wa KASUSURA, alikata rufaa Mahakama Kuu huku akiainisha sababu 6 za kukata rufaa.

Rufaa hiyo ikapangwa kwa Mh. Jaji THOMAS MIHAYO ambapo pande zote 2 zilisikilizwa.

Tarehe 23.6.2010  Mh. Jaji MIHAYO, akitoa hukumu,  "aliimchinjia baharini" KASUSURA kwa maelezo kwamba rufaa hiyo haikuwa na "mashiko" ingawa alipunguza kifungo kutoka miaka 35 hadi 30 kwa maana ya kuzitumikia zile adhabu mbili za miaka 30 na pia 5 kwa pamoja concurrently badala ya kwa kufuatana consecutively.

9. KASUSURA Akata Rufaa Mahakama ya Rufaa

Baada ya kutoridhishwa na hukumu ya Mh. Jaji THOMAS MIHAYO, KASUSURA aliamua "kuingia fronti" mwenyewe bioa wakili kwa kukata rufaa Mahakama ya Rufaa nchini ambayo ndiyo ngazi ya juu kabisa katika mfumo wa mahakama zetu ambapo Majaji 3 hukaa na kusikiliza na kuamua rufaa.

_"Mnyamblis" KASUSURA aliainisha sababu 9 za Rufaa.

Baada ya rufaa hiyo kupokelewa, Majaji 3 walipangiwa kuisikiliza. Majaji hao ni Mh. SEMISTOCLES KAIJAGE , MBAROUK MBAROUK na SAIDA MJASIRI.

Mahakama hiyo ikiketi jijini A-Town" ilisikiliza rufaa hiyo tarehe 11.4.2016. Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na TUMAINI KWEKA(PSA) akisaidiwa na CECILIA MKONONGO wakati "Mzee Baba" KASUSURA alionesha "unyamblis" kwa kujisimamia mwenyewe kwenye rufaa hiyo bila wakili.

KASUSURU, katika jitihada kubwa za kuhakikisha "anaipotezea lupango", aliainisha "matundu" kedekede kwenye ushahidi wa upande wa mashtaka.

Miongoni mwa "nondo na misumari ya moto" iliyodadavuliwa na "Bush Lawyer" KASUSURA ni Kwanza, Polisi walimhoji kwa masaa mengi kupita kiasi bila kuomba ruhusa ya korti kitu ambacho ni kinyume na sheria, Pili, Jamhuri haikumleta mtu hata mmoja wa Citibanki kuthibitisha kuwa mzigo ni wao na Tatu, Kulikuwa na tofauti ya kiasi cha fedha kilichotajwa kwenye Hati ya mashtaka na ushahidi uliotelewa na mashahidi wa upande wa mashtaka kitu kinachoonesha hawajui kilichowaketa mahakamani au walikurupuka!.

Majaji hao waliwaweka "Kitimoto" Mawakili wa serikali ambao kijasho chembamba kiliwatiririka licha ya kuwa jiji la Arusha ni baridi na AC ilikuwa ikinguruma kortini! Hatimaye, majaji hao wakapanga kutoa hukumu siku ya Jumatatu, tarehe 9.5.2016.

"Siku ya Siku" ilipowadia, Mahakama hiyo, kama ilivyotarajiwa na walioskiliza jinsi rufaa hiyo ilivyosikilizwa, huku "ikiwachana" vilivyo Polisi na Waendesha Madhtaka, ilimwachia huru KASUSURA ambaye alionesha meno yote 32 kwani alikuwa amekaa Lupango kwa miaka 15.

Katika hukumu hiyo, Majaji hao walitiririka ifuatavyo:

"...With due respect, We wish to state from the outset that We have noted with great concern that this case has been badly investigated and consequently poorly prosecuted. We agree with the appellant, KASUSURA, that his cautioned statement was taken outside the prescribed four hours as required by Section 50 and 51 of the Criminal Procedure Act, 1985. The record does not show that an extension of time was granted by the magistrate in terms of Section 51 (1)(a) of the CPA. In the event, We expunge the cautioned statement which was admitted in contravention of the requirements of the law".

"The Charge sheet shows that the money belongs to Citibank but for no apparent reason the prosecution did not bring any witness from Citibank to testify that the money is, indeed, theirs hence We agree with KASUSURA that the prosecution failed to prove its case without any reasonable doubt".

Hivyo KASUSURA aliachiwa huru ambapo Jumanne, tarehe 10.5.2016 alitolewa gerezani huku akiwa "amepigilia" suti na kuonekana kama Diwani na si mfungwa!. KASUSURA alipokelewa kwa bashasha na nduguze ambao walimvisha shada la maua.

Hadi anaachiwa, polisi walikuwa wameambulia kupata TZS 2,500,000/= kati ya TZS 4.400.000/=.

10. Maisha ya KASUSURA Akiwa Lupango:

KASUSURA, akiwa gerezani Ukonga akitumikia kifungo chake, alikuwa "mtu poa sana" kwani alikuwa mpole, mtiifu, mwenye nidhamu na mnyenyekevu sana. Kutokana na umri wake na tabia yake nzuri alichaguliwa kuwa Mnyapala. KASUSURA akiwa Mnyapala aliwasaidia vijana wengi kwa ushauri mujarab uliopelekea baadhi ya wafungwa kubadilika tabia na wengine kushinda kesi zao. Aidha, hata yeye alijifunza mengi kwani alipoingia lupango hakujua baadhi ya kazi mfano ushonaji lakini akatokea kuwa mmoja wa mafundi wazuri hadi kushiriki kushona nguo za wafungwa wenzake.

Tafakuri Tunduizu:

1. Je , zile TZS 4,397,500,000/= ziliyeyukia wapi?

2. Je, kampuni ya Knight Support iliilipa Citibank au Citibank ililipwa "insurance"?

3. Je, kuna kifungu cha sheria kinachomkataza Jaji/Hakimu kumkataza mshtakiwa kwenda kumzika mtu wake wa karibu au anatumia "common sense"?

4. Je, ni kwanini polisi walishindwa kufuata taratibu za kumhoji mtuhumiwa?  Je, ni kwanini haikutumia weledi hadi kutukanwa na majaji wa Mahakama ya Rufaa? Je, kwanini haikumleta mtu wa Citibank?

5. Je, ni haki mtu kukaa miaka 15 kisha kuambiwa hana hatia?

NB: Kujua KASUSURA sasa yuko wapi na anafanya mishemishe gani baada ya kutoka Lupango, na kujua nani aliwatonya polisi kuwa KASUSURA yuko  hoteli ya _ Three In One_ na mengine mengi subirini KITABU....Siku si nyingi!!





Wananchi wa Igando waanza kupata huduma ya umeme

$
0
0
Wananchi katika Kijiji cha Igando, wilayani Chato, mkoa wa Geita, wameanza kupata huduma ya umeme kupitia mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ndiye aliyewasha rasmi umeme jana katika Kijiji hicho, ambapo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Mtemi Semeon na viongozi wengine kutoka Wilaya hiyo, Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Aidha, kabla ya kuwasha umeme katika Kijiji cha Igando, Dkt Kalemani alifika katika Kijiji cha Imwelu kilichopo Kata ya Buseresere wilayani humo ili kukagua kazi ya upelekaji wa miundombinu ya umeme katika Kijiji hicho.

Akiwa kijijini hapo, Dkt Kalemani aliwaagiza REA, TANESCO pamoja na mkandarasi aliyepewa kazi ya kusambaza umeme kijijini hapo, kuhakikisha kuwa, ifikapo tarehe 28 mwezi huu, kijiji hicho kiwe kimeshawashiwa umeme.

Kwa nyakati tofauti akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo, alisisitiza kuwa, bei ya uunganishaji umeme katika vijiji vyote nchini ni shilingi 27,000, tu, hivyo wananchi wa vijijini wasitozwe zaidi ya kiasi hicho.

Aidha, amewataka wananchi hao kutumia umeme huo pia kwa shughuli za maendeleo ambazo zitawaongezea kipato na kukuza uchumi katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Tatu kulia) akikata utepe kuashiria kuanza kupatikana kwa huduma ya umeme katika Kijiji cha Igando, Kata ya Bwera wilayani Chato. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Mtemi Semeon.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Imwelu, Kata ya Buseresere wilayani Chato ambapo alimwagiza mkandarasi kuwasha umeme katika Kijiji hicho ifikapo tarehe 28 mwezi huu.
Wananchi katika Kijiji cha Igando, Kata ya Bwera wilayani Chato wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati alipofika kijijini hapo kuzindua huduma ya umeme.

KANALI MATAMWE-TUMEJIPANGA KUKABILI MAAFA NCHINI

$
0
0

Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kanali Jimmy Matamwe akizungumza na wajumbe walioshiriki warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini (hawapo pichani) wakati wa kufunga warsha hiyo Februari 1, 2019 iliyofanyika Ukumbi wa Mazengo Dodoma Hotel.
Meneja wa Programu elimu ya majanga kutoka UNISDR Bi.Katarina Mouakkid akieleza jambo wakati wa kufunga warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini iliyofanyika Jijini Dodoma Februari 1, 2019
Baadhi ya washiriki wakifuatilia uwasilishwaji wa hotuba kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kanali Jimmy Matamwe (hayupo pichani) wakati wa Warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini.
Mratibu wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. John Kiriwai akiwasilisha mada wakati wa warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini iliyofanyika Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kanali Jimmy Matamwe (wa kwanza kulia) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo anayeshughulikia Mipango na Utafiti Bw.Bashiru Taratibu (wa kwanza kushoto) na Katarina Mouakkid Meneja wa Programu ya elimu ya majanga kutoka UNISDR (katikati) wakifuatilia uwasilishwaji wa mada wakati wa warsha hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kanali Jimmy Matamwe akimkabidhi cheti cha ushiriki Bw. Bashiru Taratibu ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo anayeshughulikia Mipango na Tafiti wakati wa kufunga Warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini iliyofanyika Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kanali Jimmy Matamwe akimkabidhi cheti cha ushiriki kwa Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma Dkt.Wilhelim Kiwango mara baada ya kufungwa kwa wa Warsha ya hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kanali Jimmy Matamwe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi kutoka Mashirika ya Kimataifa ikiwemo, UNISDR, CIMA na mwakilishi kutoka VU.NL na kulia kwake ni Bw.Charles Msangi mratibu wa maafa wa ofisi hiyo. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)



Serikali imedhamiria kuendelea kuchukua hatua za upunguzaji wa athari za maafa kwa kuwa ni moja ya eneo lililopewa kipaumbele katika Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka wa Mitano, 2016/17- 2020/21.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kanali Jimmy Matamwe alipokuwa akifunga warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini na kuimarisha uthabiti kwa nchi na jamii dhidi ya majanga ya asili katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara Februari 1, 2019 Jijini Dodoma.

Ameeleza kuwa, hatua hiyo ni muhimu katika mkakati wa upunguzaji wa madhara yatokanayo na maafa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya msingi ya Mfumo wa Sendai wa Kupunguza Madhara ya Maafa wa mwaka 2015 – 2030 sambamba na malengo endelevu ya mwaka 2030 na makubaliano ya Paris juu ya mabadiliko ya tabianchi.

“imeelezwa kuwa mmepata fursa ya kuandaa mkakati wa kupunguza madhara mafuriko na ukame kwa kutumia taarifa ya muhtasari wa vihatarishi mlioujadili na hii imetoa fursa ya kujiamini katika kusimamia na kutatua majanga haya ambayo yamekuwa yakiikumba nchi mara kwa mara na kusababisha hasara kubwa za kiuchumi na kuongeza wigo wa umasikini nchini”,alisema Kanali Matamwe

Katika kuhakikisha mipango hiyo inakuwa endelevu Kanali Matamwe alitoa rai kwa washiriki wa warsha hiyo kuainisha maeneo yanayohusu sekta zao na kuyafanyia kazi katika mipango ya bajeti na kuendelea kuongeza nguvu kwa kutenga bajeti ya kutosha katika masula ya kukabiliana na majanga. “Tukumbuke uwekezaji katika kupunguza madhara ya maafa ni hatua muhimu katika kupunguza matumizi ya fedha nyingi kwa ajili ya kukabiliana na madhara ya yanayoweza kutokea”,alisisitiza Kanali Matamwe

Serikali kwa kuzingatia Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na.7 ya mwaka 2015 na kanuni za usimamizi wa maafa za mwaka 2017 zimeanzisha Kamati za Usimamizi wa maafa ngazi ya Mkoa hadi Kijiji kwa lengo la kupunguza madhara ya maafa ili kuwa na jamii stahimilivu.

Kwa upande wake mshiriki wa warsha hiyo Bw. John Kiriwai alieleza kuwa, kuna umuhimu wa kuwekeza nguvu na fedha katika masuala ya maafa kulingana na takwimu na taarifa zinazoeleza umuhimu wa kuwa na mikakati madhubuti ili kuwa mipango endelevu katika kukabili maafa. “Ni wakati sasa kuendelea kutumia fursa zilizopo kwa kuwekeza kwa kiwango kikubwa na kutumia taarifa za watafiti mbalimbali na kuziweka katika mipango yetu ya maendeleo ili kupunguza athari za maafa,”alisema Kiriwai.

Naye Mwakilishi kutoka Wakala wa Barabara Bi.Zaharani Madai alieleza kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hawana budi kuendelea kuwa na jitihada za makusudi za kuimarisha miundombinu kwa kuzingatia mazingira yaliyopo kwa kutumia wataalam katika kujenga na kuimarisha maeneo yanayodhaniwa kuwa hatarishi pindi maafa yanapotokea.

“Ni wakati sasa wa kujijenga upya ili kuwa na mikakati inayotekelezeka katika kutatua na kukabili maafa kwa kuimarisha miundombinu tuliyonayo ili kuendana na mazingira ya kukabili maafa nchini,”alisisitiza Madai.

NDUGULILE AITAKA IDARA YA USTAWI WA JAMII KUAHARAKISHA SHERIA NA SERA MPYA YA WAZEE

$
0
0
Na Anthony Ishengoma

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameiagiza Idara ya Ustawi wa Jamii kuhakisha inandaa haraka sana Sera ya Wazee kwa kuwa sera iliyopo ni ya siku nyingi na ilianza tangu mwaka 2003 hivyo inatakiwa sera mpya itakayoendana mabadiliko ya sasa.

Aidha Dkt Ndugulile amesema hayo wakati wa hotuba yake ya kufunga kikao kazi kilichokaa Jijini Dodoma kwa siku mbili kujadili mbinu mpya za kukabiliana na mauaji ya vikongwe lakini pia kujijengea uelewa wa Mkakati mpya wa Kutokomeza mauaji ya wazee nchini.

Aidha Dkt. Ndugulile ameitaka Idara ya Ustawi wa Jamii pia kuarakisha mchakato wa kukamilisha mapema mswada wa sheria ya wazee wa nchini ili haki na stahili za wazee zisiwe suala la hiari bali ziweze kutekelezwa kwa mujibu wa Sheria.

Dkt. Ndugulile pia ameitaka Idara ya Ustawi wa Jamii kuzingatia maelekezo aliyoyatoa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa tarehe 29 Januari Mwaka huu wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maofisa Ustawi wa Jamii kukamilisha mapema sheria ya masuala ya ustawi wa jamii Nchini ili ofisi yake iweze kutoa mrejesho kwa ofisi ya Waziri Mkuu juu ya utekelezaji wa suala hilo.

Aidha Dkt. Ndugulile pia ameagiza sambamba na utekelezaji huo pia ameitaka Idara ya Ustawi wa Jamii pia kuharakisha maandalizi ya muundo wa kada ya ustawi wa jamii ambao utaainisha madaraja, kazi na nini watapaswa kufanya suala ambalo pia ni agizo la Waziri Mkuu.

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika maandalizi mapya ya Sera ya Afya nchini suala la wazee limepewa kipaumbele kwa kuzingatia masuala ya tiba kwa wazee na kwa mala ya kwanza Wizara imetambua sayansi ya tiba ya wazee na imetamkwa wazi katika sera ya Afya kwa mantiki hiyo katika Wizara ya Afya kutakuwa na kitengo maalumu kwa ajili ya tiba na afya za wazee.

Wakati huohuo Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Nchini Bw. Rabikira Mushi alimwambia Naibu Waziri Ndugulile kuwa moja ya maazimio ya Kikao kazi hicho kuarakisha mchakato wa kuanzisha mabaraza ya wazee kuanzia ngazi ya kata ili kuwezesha kuundwa kwa Baraza la Wazee la Taifa.

Aidha Bw. Mushi pia aliongeza kuwa azimio jingine la msingi ni kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii juu ya suala la msingi la kuhakikisha jamii inajenga uelewa kuwa suala la kutunza wazee ni jukumu la familia na jamii yake.

Aidha wazee hao pia wameazimia kuwa lazima serikali ihakikishe madirisha ya wazee yanakuwa na dawa muda wote kwani pamoja na uwepo dirisha hilo wakati mwingine madirisha hayo yanakuwa hayana dawa za kutosha kukidhi mahitaji ya matibabu ya wazee.

Aidha wazee kupitia maazimio yao wazee wameiomba serikali kuwapa kipaumbele cha kupatiwa mikopo kama ilivyo kwa makundi mengine tete katika jamii ambayo yanapewa mikopo na serikali kama vile wanawake vijana na walemavu ili nao waweze kujikwamua kiuchumi.

Aidha Kamishna Mushi alisema kuwa wazee pia walipendekeza kuwepo kwa kampeni ya nyumba kwa nyumba, mkono kwa mkono ili kukabiliana na mauaji ya wazee akiongeza kuwa kama kampeni hii ikifanikiwa Maafisa Ustawi wa Jamii wataweza kubaini wazee wote walioko katika hatari kuuawa.

Kikao kazi hiki kimefanyika kufuatia kukamilika na kuzinduliwa kwa Mkakati wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee na uliwakutanisha wawakilishi wazee, Maafisa Ustawi wa Jamii pamoja na Makanda wa Jeshi la Polisi kutoka kanda ya ziwa.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa hotuba kwa wazee wakati wa kufunga kikao kazi kilichokaa Jijini Dodoma kwa siku mbili kujadili mbinu mpya za kukabiliana na mauaji ya vikongwe lakini pia kujijengea uelewa wa Mkakati mpya wa Kutokomeza mauaji ya Wazee Nchini.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa hotuba kwa wazee wakati wa kufunga kikao kazi kilichokaa Jijini Dodoma kwa siku mbili kujadili mbinu mpya za kukabiliana na mauaji ya vikongwe lakini pia kujijengea uelewa wa Mkakati mpya wa Kutokomeza mauaji ya Wazee Nchini.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikao mara baada ya kufunga kikao kazi kilichokaa Jijini Dodoma kwa siku mbili kujadili mbinu mpya za kukabiliana na mauaji ya vikongwe lakini pia kujijengea uelewa wa Mkakati mpya wa Kutokomeza mauaji ya Wazee Nchini.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akibadilisha na mawazo na Bibi Corotrida Kokupima muda mchache baada kufunga kikao kazi kilichokaa Jijini Dodoma kwa siku mbili kujadili mbinu mpya za kukabiliana na mauaji ya vikongwe lakini pia kujijengea uelewa wa Mkakati mpya wa Kutokomeza mauaji ya Wazee Nchini.

Vodacom Tanzania yajipanga kuzindua huduma ya kutunza pesa kwa vikundi na vikoba

$
0
0
Kampuni ya inayoongoza kwa mafanikio ya kidijitali Vodacom Tanzania Plc kwa kushirikiana na benki ya Posta Tanzania wanajipanga kuanzisha huduma maalum itakayokuwa maalum kwa ajili kuweka akiba na kutunza pesa itakayojulikana kama ‘Pamoja Group Saving’. Huduma hii mpya itawezesha wajumbe wa kikundi husika kuhifadhi fedha, kupata mikopo na kuwekeza kupitia M-Pesa. 

Inakadiriwa kwamba asilimia 16 ya Watanzania (Watu wazima) ambayo ni sawa na watu milioni 4.4 wengi wao wakiwa ni wanawake, wameungana na kuanzisha Zaidi ya vikundi 50,000 vya kuweka na kukopa pesa vijulikanavyo kama Vicoba na vikiwa vimekusanya fedha taslimu zaidi ya Shilingi bilioni 100 za Kitanzania 

Kama kiongozi katika soko la mfumo wa pesa za simu, Vodacom M-Pesa, ilizindua na kubuni njia mbali mbali ambazo zinakidhi mahitaji ya soko na kuwavuta wateja wake katika mfumo wa kidigitalli, hivyo huduma ya Vodacom Pamoja Group Savings imelenga katika kufanikisha hili. 

“Naamini kwamba kila mmoja wetu anatambua au amejiunga katika SACOSS, Kikoba au upatu. Vodacom inatambua umuhimu wa vikundi hivi katika kuinua vipato vya watu mbali mbali katika jamii, ndio maana tumetengeneza huduma hii ili kuvifanya vikundi hivyo kuwa fanisi zaidi, lakini pia kuwavuta katika huduma za kifedha za kidijitali” alisema Mkurugenzi wa M-Commerce, Vodacom Tanzania, Epimack Mbeteni. 

Huduma hii imelenga kutatua matatizo ambayo vikundi hivi vimekuwa vikikumbana nayo kwa muda mrefu, ikiwa ni pamoja na usalama, utunzaji wa taarifa, ukusanyaji wa fedha pamoja na ugawaji wa faida ipatikanayo kwa hisa ambazo wamekuwa wakijiuzia ndani ya vikundi hivi. hivyo basi itawawezesha familia, marafiki na vikundi vya upatu kupata huduma za kifedha kwa usalama zaidi na muda muafaka. 

Kwa kutumia Pamoja Group Saving washiriki wote wa makundi wataweza kufuatilia mwenendo mzima wa kifedha wa kundi, ikiwemo kiasi cha fedha kilichopo ndani ya kundi. Huduma hii ni ya kipeekee na unaongeza uwazi na kupunguza ugumu na utofauti katika uongozaji wa vikundi, Huduma hii itakuwa kwa wateja wote wa Vodacom pale itakapozinduliwa na itatumika na vikundi vyote vya fedha.

UVCCM MKOA WA SHINYANGA WASHEREHEKEA MIAKA 42 YA CCM KWA BONANZA KUBWA

$
0
0
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM mkoa wa Shinyanga umefanya Bonanza la michezo lililohusisha michezo mbalimbali kwa lengo la kusherehekea miaka 42 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Bonanza hilo limefanyika Februari 2,2019 katika uwanja wa mpira wa CCM Kambarage uliopo mjini Shinyanga. 

Akifungua bonanza hilo mgeni rasmi,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amepongeza jitihada zilizofanywa na serikali ya CCM kwa awamu nne zilizopita mpaka sasa awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza kwa kiwango kikubwa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kupiga hatua za kimaendeleo. 

“Vitu vingi vikubwa vimefanyika kupitia CCM na serikali yake na jumuiya zake kwa ujumla, nchi yetu imeendelea kuwa salama miundombinu imeboreshwa barabara ndiyo usiseme Shinyanga haikuwa hivi, sekta ya afya , elimu vimeboreshwa na tulikuwa na ndege moja leo tunazo saba vyote hivi vipo ndani ya Ilani ya Chama”,alisema Mlolwa. 

“Na mimi niombe tuendelee kuyaenzi maendeleo haya yaliyoletwa na CCM kwa vitendo”,aliongeza Mlolwa. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge aliwakumbusha vijana kuendelea kudumisha ushirikiano katika mambo yote yanayofanywa na chama pamoja na serikali katika kuleta maendeleo ya wananchi wanaowatumikia. 

“Nawashukuru sana ndugu zangu wote na viongozi wote wa serikali na chama mlioshiriki katika Bonanza hili tudumishe umoja na mshikamano kati yetu hivi ndivyo serikali yetu inataka” ,alisema Shemahonge. 

Bonanza hilo limeshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete , mchezo wa kuvuta kamba,kukimbia kwenye magunia ambapo viongozi wa serikali na chama cha CCM walishiriki. Kauli mbiu kwa mwaka huu inasema “Kazi ni kipimo cha utu ,chapa kazi tulinde uhuru na utaifa wetu”.
Mgeni rasmi katika Bonanza la UVCCM Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akifungua bonanza la michezo lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM mkoa wa Shinyanga katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga. Picha zote na Steve Kanyefu- Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack katika bonanza hilo ambapo aliwataka vijana kushirikiana katika kuijenga Shinyanga wakishirikiana pamoja na serikali yao.
Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge (kushoto) akimpatia zawadi ya jezi mgeni rasmi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa katika ufunguzi wa bonanza hilo.
Awali Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Husein Egabano akiongoza msafara wa vijana kuingia katika uwanja wa CCM Kambarage lilipofanyika bonanza hilo.
Mgeni rasmi katika bonanza hilo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akifungua michezo katika bonanza hilo kwa kupiga penati.
Baadhi ya wadau waliohudhuria katika bonanza hilo wakifuatilia kwa umakini matukio yanayoendelea uwanjani.
Timu ya wanawake ambao ni wanachama wa CCM (wenye jezi za kijani) wakichuana vikali na timu ya watumishi wa serikali (wenye jezi za rangi nyekundu) katika mchezo wa pete, ambapo timu ya watumishi ilishinda kwa goli 14 dhidi ya wanachama 9.
Mgeni rasmi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa( katikati) akiwa pamoja mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba(kulia) pamoja na mwenyekiti UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge (kushoto) wakifuatilia michezo katika uwanja wa CCM Kambarage.
Mpira wa miguu ukiendelea katika uwanja wa Kambarage hapa ni mchezo kati ya timu ya walimu kutoka chuo cha Shy com (wenye jezi ya kijani) na Timu ya Stand United chini ya miaka 20(jezi rangi ya chungwa)
Mchezo wa kukimbiza kuku ukiendelea. Kijana mshindi wa mbio za kukimbiza kuku akipongezwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba.
Mchezo wa kukimbia kwenye magunia ukiendelea. 
Vijana wa kikundi cha dance kijulikanacho kama The Fighter cha mjini Shinyanga wakionesha moja ya mchezo ambapo waliigiza mtu akicheza kama amechomwa kisu shingoni. Mgeni rasmi akikabidhi zawadi ya kikombe kwa timu ya watumishi wa serikali walioshinda michezo mingi katika bonanza la michezo lililoandaliwa na UVCCM mkoa wa Shinyanga.

JUSTINE KASUSURA: MBONGO ALIYEFUNGWA "KWA KUPIGA PESA NDEFU" KATIKA HISTORIA YA TZ NA KISHA KUKIPANGUA KIFUNGO HICHO BILA WAKILI MAHAKAMA YA RUFAA TZ!!!

$
0
0

1. Usuli:


Watanzania nchini kote, kuanzia Ntwara hadi Kagera, Ijumaa ya tarehe 3.8.2001 saa 2 usiku, walipigwa bumbuwazi na kushindwa kuamini, pale walipomshuhudia luningani, SACP ALFRED TIBAIGANA, aliyekuwa RPC Kanda Maalum Dsm kuanzia 2001-2008, akitoa "Breaking Newz" kwa waandishi wa habari kuhusu unyan'ganyi wa $ 2M (TZS 4.400.000.000/=) uliokuwa umetokea jana yake majira ya saa 5 asubuhi nje kidogo ya "Airport" ya JNIA, ukiwa ni unyang'anyi wa kihistoria wa fedha nyingi kuwahi kutokea nchini ulioweka rekodi kipindi hicho.

RPC TIBAIGANA aliujuza umma kwamba mtuhumiwa wa unyang'anyi huo ni  pandikizi la mtu lenye wajihi wa miraba minne liitwalo JUSTINE KAKURU KASUSURA, dereva wa kampuni ya ulinzi ya Knight Support yenye makao makuu yake eneo la Victoria, Dsm. Mzee baba" huyo alikuwa "amesepa na burungutu la fweza kama zote" na kutokomea kusikojulikana na kwamba "msako wa kufa mtu" ulikuwa umeanza kurindima nchi nzima hususan maeneo ya mipakani. Mwisho, RPC TIBAIGANA alitoa rai kwa wananchi na wasamaria wema kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kufanikisha kumkamata mtuhumiwa huyo.

2. Miezi 5 Ikapita KASUSURA Hajulikani aliko

Licha ya kumtafuta maeneo mbalimbali, lakini KASUSURA hakuweza kutiwa mbaroni kwa miezi 5.

2. KASUSURA Abambwa Hotelini, Mbeya Usiku wa Manani!

Baada ya kupita miezi 5, huku wananchi wengi wakiamini kuwa kwa "mbumba" zote zile lazma "Mzee Mzima" KASUSURA atakuwa "amesepa" kwenda nje ya nchi na kwamba sasa atakuwa "akila bata refu" kwenye "viwanja vya mbele" kama Hawaii au Bahamas, walipigwa mshangao mkubwa ilipotangazwa kwamba KASUSURA amekamatwa  usiku wa manani, jumatatu ya tarehe 24.12.2001(Christmas Eve), kwenye hoteli ijulikanayo kama "Three In One" iliyoko maeneo ya Soweto, Mbeya.

KASUSURA alikuwa amefikia hotelini hapo siku ya Jumapili, tarehe 23.12.2001 saa 12 jioni akitokea Sumbawanga na kujifanya ni mfanyabishara. Wakati akiwasili hotelini hapo, KASUSURA alikuwa amevaa kofia kubwa kuficha uso wake na akapewa chumba na. 101K ambapo katika rejista hakuandika jina la KASUSURA bali aliandika jina JOHN LAIZER na akalipia malazi ya siku moja kwa "buku tatu jero" (TZS 3,500/=).

Jioni ya Jumatatu hiyo, "mandata" walitinga kwenye hoteli hiyo na kuweka mtego kabambe nje na ndani ya hoteli hiyo huku wengine "wakizama" uvunguni na kabatini kama makomandoo wa Kiisraeli!.

Usiku wa manani, siku hiyo ya mkesha wa krisimasi, KASUSURA, huku akiwa yuko "bwaksi" baada ya kuwa "amepiga vyombo" kisawasawa baa, alirejea hotelini hapo akiwa na nungayembe alilojihomolea kwenye baa alikokuwa "akipombeka".

Alipojongea mapokezi, huku akiongea "Kikristu" kiiiingi, kama ilivyo kawaida kwa walevi wengi kupenda kuongea lugha ya "kwa mama" wanapokuwa "bwii", aliomba ufunguo na kuelekea chumbani kwake.

Baada tu ya kufungua mlango na kuwasha taa, KASUSURA akakutana uso kwa uso na "mandata" walioibuka kama "Bruce Lee" kutoka uvunguni na kabatini na kumtia KASUSURA nguvuni kiulaiini kama kumsukuma mlevi! Baada ya KASUSURA kunyakwa "hakuna rangi aliacha kuiona" na pombe zote ghafla zikamuisha kichwani akawa ameduwaa kama "zombi"!. Aliposachiwa alikutwa na TZS 200.000/= tu.!.

3. IGP MAHITA Aeleza Polisi Wamtorosha KASUSURA

Huku wananchi wengi wakilipongeza Jeshi la Polisi kwa kufanikiwa kumkamata KASUSURA, zikaenea taarifa zisizo rasmi kwamba kuna polisi wengi wasio waaminifu walikuwa "wamevuta mkwanja mrefu" na kumsaidia KASUSURA kutokamatwa.  Ilidaiwa kwamba kila polisi walipokuwa wakimkamata KASUSURA  walikuwa "wanavuta mkwanja" kisha wanawapigia simu wenzao mkoa mwingine na "kuwapigia pasi" ili wamkamate na "akizama mfukoni" wanamwachia.Kutokana na sintofahamu hiyo, IGP wa wakati huo, aliyekuwa mtu wa shoka asie na mchezo, Alhaj OMAR IDD MAHITA, ikabidi aongee na waandishi wa habari tarehe 9.1.2002 na kukanusha vikali huku akibainisha kuwa si kweli kwamba polisi wengi wamehusika bali ni wachache tu. IGP MAHITA alifafanua kwamba kuna polisi 8 tu wakiwemo 3 waandamizi wanaodaiwa kumsaidia KASUSURA kutoroka walikuwa wamekamatwa na kusimamishwa kazi.

IGP MAHITA aliwataja polisi hao kuwa ni SSP BONAVENTURE MSHONGI(RCO- Tanga), ASP BEATRICE MAONA na ASP DEUSDEDIT KAJUNA(Ofisi ya RCO, Dsm), C.236 Sgt EMMANUEL na Konstebo ROGATHE(Tanga), E.7014 Konstebo ISAACK, E. 7603 Konstebo DAVID na E. 8042 Konstebo JEREMIAH.

4. DCI ADADI Aeleza "Kufyekelewa mbali" kwa Polisi 5"

Tarehe 15.1.2002, aliyekuwa DCI, ADAD MOHAMED RAJAB, aliufahamisha umma kwamba Jeshi la Polisi lilikuwa limewafikisha Mahakama ya Kijeshi polisi 5 ambapo walipatikana na hatia ya utovu wa nidhamu na kutozingatia maadili ya polisi.

DCI ADADI, akiwa amekunja ndita na kuonesha kukerwa, alitiririka:
"Jeshi la Polisi limewafukuza kazi polisi wafuatao C. 236 Sgt EPHRAIM, E. 635 Konstebo ROGATHE, E.7014 Konstebo ISAACK, E. 7603 Konstebo DAVID na E. 8042 Konstebo JEREMIAH. Hawa walikuwa wamefunguliwa mashtaka Mahakama ya Kijeshi na wamefukuzwa kazi kwa kukiuka maadili ya polisi na watashtakiwa mahakama za kiraia. Polisi hao walimkamata na kumuachia KASUSURA zaidi ya mara 3 Dsm, Tanga na Arusha, kitendo ambacho kimelitia aibu jeshi la polisi".

5. KASUSURA na "Wenzake" 6 Wafikishwa kwa "Pilato" Kisutu

KASUSURA, baada ya kuandika maelezo yake, alifikishwa mahakama ya Kisutu tarehe 7.1.2002 na Land Rover Defender No. PT 0881 akiwa pamoja na washtakiwa wengine 6 ambao ni WICKLIFF URASSA, LEONARD URASSA, LUCY URASSA(32-Mwanafunzi wa IFM) PROFILY KWEKA, WÌLLIAM MBETWA na LIBENT LIKUNDWA. Mahakama ya Kisutu ilijaa hadi pomoni kwani wakazi wa jijini la Dsm wanaosifika kwa kupenda "ubuyu" walitinga mahakamani hapo mapema kabisa kujione wenyewe huyo KASUSURA anafananaje.


Mwendesha mashtaka, ACP RAINHARD LISAPITA,  aliwasomea mashtaka 5 ya Kula njama, Unyang"anyi wa kutumia silaha, Wizi na Makosa 2 ya Kupokea Mali ya Wizi. KASUSURA alikuwa akitetewa na Wakili nguli na bingwa a kupangua kesi za jinai, MAJURA MAGAFU. Washtakiwa wote walikana mashtaka yao hivyo upande wa mashtaka ukaita mashahidi kuthibitisha mashtaka.


6. Mahakama ya Kisutu yaelezwa "Mchezo -Mzima" Ulivyokuwa:

Mashahidi wa upande wa mashtaka walieleza kwamba asubuhi ya siku ya tukio, 2.8.2001, KASUSURA alikabidhiwa na viongozi wake gari aina ya Toyota Hilux Double Cabin TZL 3742 isiyopenya risasi ili kwenda JNIA kuchukua mzigo.

KASUSURA akaelekea JNIA akiwa na mwenzake, SAID MUSSA, aliyekuwa na jukumu la kupokea mzigo uliokuwa umewasili kwa Swiss Air ukiwa ni mali ya Citibank ambao walikuwa wameingia kandarasi na kampuni ya Knight Support kuwapelekea mzigo huo ofisini kwao.

DAHACO walimkabidhi SAID MUSSA mzigo huo majira ya saa 4.30 asubuhi na akauweka vizuri nyuma ya gari kisha akafunga kwa ufunguo. 

KASUSURA akawasha gari na kuanza kuondoka JNIA na alipokunja kulia ili kuanza kuelekea mjini, "Mzee baba" KASUSURA "alijifanya kama anajikuna" kisha akaliegesha gari hilo mbele ya magari 2 aina ya Toyota Landcruiser na Toyota Corrola. Ghafla bin vuu, KASUSURA, kama VAN DAME, akatoa pisto na kumnyooshea SAID MUSSA na kumwambia "Huu ndio mwisho wa mchezo"na kumwamu "aishie". KASUSURA akamnyang'anya MUSSA funguo akaushusha mzigo huo akisaidiwa na watu wengine waliokuwa kwenye gari zile 2. MUSSA, baada ya kimuhemuhe hicho, alienda kuripoti kituo cha polisi ambapo alishikiliwa na kuanza kuisaidia polisi.

Upande wa mashtaka ulipofunga kesi yao, mahakama ilimuona KASUSURA peke yake ndiye mwenye kesi ya kujibu hivyo iliwaachia huru washtakiwa wengine wote.

Huku kesi hii ikiwa inaunguruma,  tarehe 16.1.2002, maafisa 8 wa polisi (3 wa ngazi za juu aliwemo mwanamke mmoja) na 5 wa ngazi za chini walifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali na kusomewa mashtaka 2 ya Kula njama ya kumtorosha KASUSURA na Kupokea rushwa toka kwa KASUSURA.

KASUSURA, bada ya kuonekana ana kesi ya kujibu,  alitoa utetezi na kuelezea kuwa mashahidi wote wa upande wa serikali walikuwa "wameipiga fiksi" mahakama kwa hekaya zao za Abunuwasi. KASUSURA alidai kwamba ukweli ni kuwa yeye wakati akiendesha ile "ndinga" aliyokabidhiwa na ofisi yao ya Knight Support na baada ya kuchukua mzigo huo uliokuwa na "mbumba za kufa mtu" ghafla alipoanza kuendesha na akiwa nje kidogo ya JNIA "Watu wenye Kazi zao" yaani "Mabandido" walimteka na kusepa na "Mkwanja" wote!.

Huku kesi ikiwa inanguruma, KASUSURA alifiwa na mkewe,  Bi. FAUZIA LAIZER  tarehe 22.2.2005. KASUSURA alimuomba hakimu ruhusa ya kwenda kumzika mkewe ambaye alikuwa akifika mahakamani hapo kila mara na mtoto wao wa miaka 9. 

Mh. Hakimu "alimchinjia baharini" KASUSURA kwa kusema: "Mahakama imetupilia mbali ombi la KASUSURA. Hatusemi kama itatokea, lakini ikitokea mshtakiwa akatoroka, wote tutawajibika".

Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote, Mh. Hakimu SILVANGILWA MWANGESI alitoa hukumu siku ya Ijumaa tarehe 30.3.2007 ambapo "alimpiga" KASUSURA "mvua" 30 kwa kosa la unyang'anyi na "mvua" 5 kwa kosa la wizi na kwamba atatumikia miaka 35 lupango (consecutively).

7. Polisi 8 Waachiwa huru



Polisi 8 waliokuwa wameshtakiwa kwa kudaiwa "kuvuta mbumba" na kumtorosha KASUSURA waliachiwa huru na mahakama hiyo.

SSP BONAVENTURE MSHONGI, aliyekuwa RCO wa Tanga wakati wa msala huo, alikuja kupandishwa cheo na kuwa ACP. Aidha, aliteuliwa kuwa RPC Pwani kabla ya kuhamishiwa Simiyu ambako analitumikia taifa lake vizuri tu na kwa weledi na uadilifu wa hali ya juu.

8. Wakili MAJURA MAGAFU Akata Rufaa Mahakama Kuu

MAJURA MAGAFU, wakili wa KASUSURA, alikata rufaa Mahakama Kuu huku akiainisha sababu 6 za kukata rufaa.

Rufaa hiyo ikapangwa kwa Mh. Jaji THOMAS MIHAYO ambapo pande zote 2 zilisikilizwa.

Tarehe 23.6.2010  Mh. Jaji MIHAYO, akitoa hukumu,  "aliimchinjia baharini" KASUSURA kwa maelezo kwamba rufaa hiyo haikuwa na "mashiko" ingawa alipunguza kifungo kutoka miaka 35 hadi 30 kwa maana ya kuzitumikia zile adhabu mbili za miaka 30 na pia 5 kwa pamoja concurrently badala ya kwa kufuatana consecutively.

9. KASUSURA Akata Rufaa Mahakama ya Rufaa

Baada ya kutoridhishwa na hukumu ya Mh. Jaji THOMAS MIHAYO, KASUSURA aliamua "kuingia fronti" mwenyewe bila wakili kwa kukata rufaa Mahakama ya Rufaa nchini ambayo ndiyo ngazi ya juu kabisa katika mfumo wa mahakama zetu ambapo Majaji 3 hukaa na kusikiliza na kuamua rufaa.

"Mnyamblis" KASUSURA aliainisha sababu 9 za Rufaa.

Baada ya rufaa hiyo kupokelewa, Majaji 3 walipangiwa kuisikiliza. Majaji hao ni Mh. SEMISTOCLES KAIJAGE , MBAROUK MBAROUK na SAIDA MJASIRI.

Mahakama hiyo iliketi jijini A-Town" ilisikiliza rufaa hiyo tarehe 11.4.2016. Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na TUMAINI KWEKA(PSA) akisaidiwa na CECILIA MKONONGO wakati "Mzee Baba" KASUSURA alionesha "unyamblis" kwa kujisimamia mwenyewe kwenye rufaa hiyo bila wakili.

KASUSURA, katika jitihada kubwa za kuhakikisha "anaipotezea lupango", aliainisha "matundu" kedekede kwenye ushahidi wa upande wa mashtaka.

Miongoni mwa "nondo na misumari ya moto" iliyodadavuliwa na "Bush Lawyer" KASUSURA ni Kwanza, Polisi walimhoji kwa masaa mengi kupita kiasi bila kuomba ruhusa ya korti kitu ambacho ni kinyume na sheria, Pili, Jamhuri haikumleta mtu hata mmoja wa Citibanki kuthibitisha kuwa mzigo ni wao na Tatu, Kulikuwa na tofauti ya kiasi cha fedha kilichotajwa kwenye Hati ya mashtaka na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka kitu kinachoonesha hawajui kilichowaleta mahakamani au walikurupuka!.

Majaji hao waliwaweka "Kitimoto" Mawakili wa serikali ambao kijasho chembamba kiliwatiririka licha ya kuwa jiji la Arusha ni baridi na AC ilikuwa ikinguruma kortini! Hatimaye, majaji hao wakapanga kutoa hukumu siku ya Jumatatu, tarehe 9.5.2016.

"Siku ya Siku" ilipowadia, Mahakama hiyo, kama ilivyotarajiwa na walioskiliza jinsi rufaa hiyo ilivyosikilizwa, huku "ikiwachana" vilivyo Polisi na Waendesha Mashtaka, ilimwachia huru KASUSURA ambaye alionesha meno yote 32 kwani alikuwa amekaa Lupango kwa miaka 15.

Katika hukumu hiyo, Majaji hao walitiririka ifuatavyo:

"...With due respect, We wish to state from the outset that We have noted with great concern that this case has been badly investigated and consequently poorly prosecuted. We agree with the appellant, KASUSURA, that his cautioned statement was taken outside the prescribed four hours as required by Section 50 and 51 of the Criminal Procedure Act, 1985. The record does not show that an extension of time was granted by the magistrate in terms of Section 51 (1)(a) of the CPA. In the event, We expunge the cautioned statement which was admitted in contravention of the requirements of the law".

"The Charge sheet shows that the money belongs to Citibank but for no apparent reason the prosecution did not bring any witness from Citibank to testify that the money is, indeed, theirs hence We agree with KASUSURA that the prosecution failed to prove its case without any reasonable doubt".

Hivyo KASUSURA aliachiwa huru ambapo Jumanne, tarehe 10.5.2016 alitolewa gerezani huku akiwa "amepigilia" suti na kuonekana kama Diwani na si mfungwa!. KASUSURA alipokelewa kwa bashasha na nduguze ambao walimvisha shada la maua.

Hadi anaachiwa, polisi walikuwa wameambulia kupata TZS 2,500,000/= kati ya TZS 4,400,000,000/=.

10. Maisha ya KASUSURA Akiwa Lupango:

KASUSURA, akiwa gerezani Ukonga akitumikia kifungo chake, alikuwa "mtu poa sana" kwani alikuwa mpole, mtiifu, mwenye nidhamu na mnyenyekevu sana. Kutokana na umri wake na tabia yake nzuri alichaguliwa kuwa Mnyapala. KASUSURA akiwa Mnyapala aliwasaidia vijana wengi kwa ushauri mujarab uliopelekea baadhi ya wafungwa kubadilika tabia na wengine kushinda kesi zao. Aidha, hata yeye alijifunza mengi kwani alipoingia lupango hakujua baadhi ya kazi mfano ushonaji lakini akatokea kuwa mmoja wa mafundi wazuri hadi kushiriki kushona nguo za wafungwa wenzake.

Tafakuri Tunduizu:

1. Je , zile TZS 4,397,500,000/= ziliyeyukia wapi?

2. Je, kampuni ya Knight Support iliilipa Citibank au Citibank ililipwa "insurance"?

3. Je, kuna kifungu cha sheria kinachomkataza Jaji/Hakimu kumkataza mshtakiwa kwenda kumzika mtu wake wa karibu au anatumia "common sense"?

4. Je, ni kwanini polisi walishindwa kufuata taratibu za kumhoji mtuhumiwa?  Je, ni kwanini haikutumia weledi hadi kutukanwa na majaji wa Mahakama ya Rufaa? Je, kwanini haikumleta mtu wa Citibank?

5. Je, ni haki mtu kukaa miaka 15 kisha kuambiwa hana hatia?

NB: Kujua KASUSURA sasa yuko wapi na anafanya mishemishe gani baada ya kutoka Lupango, na kujua nani aliwatonya polisi kuwa KASUSURA yuko  hoteli ya  Three In One na mengine mengi subirini KITABU....Siku si nyingi!!

WACHIMBAJI WADOGO KUFIKISHIWA UMEME KWENYE MASHIMO YAO

$
0
0
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Imwelu kilichopo wilaya ya Chato mkoani Geita.
 Wataalamu wa Tanesco ,REA na Mkandarasi wakipokea maagizo kutoka kwa Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani
Sehemu ya wananchi wakifuatilia mkutano huo leo

WACHIMBAJI wadogo mkoani Geita wanatarajiwa kufikishiwa Umeme katika mashimo yao ili kuwawezesha kufanya shughuli zao za uchimbaji kwa ufanisi mkubwa.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Imwelu kilichopo wilaya ya Chato mkoani Geita.

Alisema kuwa Serikali inatambua mchango wa wachimbaji wadogo katika maendeleo ya nchi na kwa sasa umeme utafikishwa katika mashimo ya wachimbaji ili kurahisisha shughuli zao za uchimbaji.

“Ndugu zangu wachimbaji tumeshaanza kuwapa transfoma kwa hiyo kama wewe ni mchimbaji na unataka uchimbaji wao uwe wa kisasa,utajaza fomu itakayowezesha kuendesha mashine zenu za kuchakata madini”Alisema.

Waziri huyo aliwasihi wachimbaji wadogo kutumia fursa ya umeme ili kuleta tija katika uchumbaji wao na hivyo kuweza kuongeza pia ufanisi mkubwa.

Hata hivyo Waziri Kalemani alimtaka Mkandarasi na Tanesco kufikisha umeme katika kijiji hicho ndani ya siku ishirini (20)


Wanariadha mbio za Nyika Taifa waiahidi NCAA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Arusha
WANARIADHA watakaoshiriki mashindano ya mbio za Nyika za Taifa Februari 16, mwaka huu katika viwanja vya Magereza Moshi, mkoani Kilimanjaro wameahidi kufanya makubwa zaidi.
Kufanya vizuri kwenye mashindano hayo kutawapa fursa ya kushiriki mashindano ya mbio za Nyika za Dunia zinazotarajiwa kufanyika nchini Denmark Machi 30, mwaka huu.  Wakizungumza kwenye mazoezi yaliyofanyika viwanja vya Magereza Arusha wanariadha hao walisema chini ya mdhamini wao Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA),wamejaa tumaini la kufanya vizuri zaidi.
Mwanariadha kutoka timu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Anjelina Daniel aliwashukuru NCAA kwa kuwadhamini ambapo amekuwa na wakati mzuri zaidi wa kufanya mazoezi.   “Ninawaahidi mashindano ya Nyika Moshi nitashika namba ya kwanza hapa nimekuwa wa pili,” alisema Anjelina.
Kaimu Meneja wa Uhusiano NCAA Joyce Mgaya alisema Mamlaka ya Ngorongoro ilitambua fursa ya uzalendo kwenye mchezo huo na mingine.“Hili ni jukwaa linaloweza kutangaza vivutio vya utalii. Tuliona vizuri kuungana na RT kuwatia moyo wachezaji, tunaamini watakuwa mabalozi wazuri wa utalii,” alisema Mgaya.
Naye Katibu Mkuu wa RT Wilhelm Gidabuday aliwashukuru NCAA kwa kuwashika na mkono.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live


Latest Images