Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

SERIKALI YAKANUSHA TAARIFA ILIYOSAMBAZWA KUPITIA CCTV-AFRIKA


Wanaowinda panya washauriwa kufuga kuku ili kupunguza uharibifu wa mazingira

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewashauri wananchi wote wanaoharibu misitu kwa kuchoma moto kwaajili ya kuwinda panya waanze kufuga kuku ili kuweza kuokoa mazingira huku

akiwataka wakurugenzi wa halmashauri za Mkoa huo kuhakikisha wanamuandalia mipango mikakati ya halmashauri zao katika upandaji wa miti ikiwa ni kufuata agizo la serikali la kuitaka kila halmashauri kupanda miti milioni 1.5 kila mwaka.

Alisema kuwa moja ya matokeo ya shughuli hizi za kibinadamu ni uharibifu mkubwa wa mistu na vyanzo vya maji  unaoweza kusababisha madhara makubwa kama kukosa mvua kwa wakati, uzalishaji mdogo wa chakula na hata maradhi mbalimbali yanayotokana na uharibifu wa mazingira na kuongeza kuwa ufanisi wa zoezi hili la upandaji miti unatia shaka kutokana na kutosimamiwa vizuri na Viongozi wa Halmashauri zetu zote.

“Kwa hiyo naagiza Wakurugenzi wote wa Halmashauri zetu kuwasilisha mpango mkakati wa upandaji miti kwa kipindi cha Mwaka huu, ikiwa ni pamoja na kubainisha idadi ya miti waliyonayo na mahali ilipo pamoja na ya Wadau wao wa utunzaji wa Mazingira, na maeneo ya kupanda.  Mpango huu unifikie ndani ya siku tano kuanzia leo,” Alisisitiza.

Vile vile alizitaka Taasisi za Serikali kama shule, magereza na vyuo vya elimu kuanza kutumia nishati mbadala ikiwemo ya “biogas” katika shughuli zao za mapishi ya chakula na kupunguza kasi ya matumizi ya kuni kwani mkoa una mitambo 2 ya “biogas” katika Manispaa ya Sumbawanga katika Vijiji vya Mtimbwa na Ntendo ambayo inatumika kama darasa la kujifunzia  ujuzi wa kutengeneza biogas kutokana na mabaki ya mifugo yetu.

Wakati akisoma taarifa ya halmashauri juu ya zoezi la upandaji miti, Afisa Ardhi na malisili wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Juma Chande alieleza kuwa katika msimu wa mwaka 2018/2019 katika kata 8 kati ya kata 27, halmashauri imeshapanda miti 292,899 ambayo ni asilimia 17.4 ya lengo na ufafanua kuwa halmashauri inaendelea kutoa elimu ya kutunza mazingira, kupanda miti na kilimo mseto huku akitaja changamoto zinazorudisha nyuma juhudi hizo.

“Miongoni mwa changamoto ni muitikio mdogo wa wananchi katika utunzaji wa mazingira pamoja na hamasa nyingi kutolewa kwao, mila na tamaduni za wananchi za uwindaji wa panya mathalani kusababisha uchomaji wa miti wakati wa kiangazi mfano maeneo ya vijiji vya Msandamuungano, Sandulula na Mpwapwa hivyo kuathiri misitu iliyopandwa.” Alimalizia.

CAG AFIKA MBELE YA KAMATI YA BUNGE YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE

$
0
0
 Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Mhe. Prof. Mussa Assad akishuka kwenye gari kuelekea kwenye kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuitikia wito wa tuhuma zinamkabili za kulidhalilisha Bunge, tukio lililotokea leo tarehe 21 Januari, 2019 katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
 Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Mhe. Prof. Mussa Assad (kulia) akisindikizwa na Msaidizi wa Mpambe wa Bunge, Ndg. Leonard Bushiri kuelekea kwenye kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuitikia wito wa tuhuma zinazomkabili za kulidhalilisha Bunge, tukio lililotokea leo tarehe 21 Januari, 2019 katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
 Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Mhe. Prof. Mussa Assad akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuelekea kwenye kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuitikia wito wa tuhuma zinazomkabili za kulidhalilisha Bunge, tukio lililofanyika leo tarehe 21 Januari, 2019 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
 Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Mhe. Prof. Mussa Assad akiingia kwenye kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuitikia wito wa tuhuma zinazomkabili za kulilidhalilisha Bunge, tukio lililotokea leo tarehe 21 Januari, 2019 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
 Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Mhe. Prof. Mussa Assad akitoa nyaraka zake mbele ya kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge wakati akiitikia wito wa tuhuma zinazomkabili za kulilidhalilisha Bunge, tukio lililotokea leo tarehe 21 Januari, 2019 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Mhe. Prof. Mussa Assad akiwa mbele ya kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge akiitikia wito wa hutuma zinazomkabili za kulilidhalilisha Bunge, tukio lililofanyika leo tarehe 21 Januari, 2019 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo  tarehe 21/01/2019 Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Angela Kairuki kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kutoka kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo  tarehe 21/01/2019 Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza na wanahabari mara baada ya kutoka kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo  tarehe 21/01/2019 Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kutoka kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo  tarehe 21/01/2019 Ikulu jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Waziri Ummy Mwalimu akaguaukarabati wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya Moyo

$
0
0
Na Genofeva Matemu – JKCI
20/01/2019 Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete (JKCI) imekuwa   taasisi ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kuwa na wodi pekee ya kuwahudumia watoto wenye magonjwa ya moyo bila kuwachanganya na watu wazima.

Eneo la wodi hiyo lilitolewa mwaka 2017 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk. John Pombe Magufuli alipokua akizindua Hospitali ya Mloganzila na kuiagiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoa sehemu ya jengo linalohudumia watoto kwa JKCI ili watoto wenye magonjwa ya moyo waweze kuwa na wodi yao katika kuleta ufanisi wa matibabu ya moyo kwa watoto hapa nchini.

Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi hiyo Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamaii, Jinsi, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alisema upatikanaji wa wodi hiyo ni juhudi za serikali katika kuhakikisha utolewaji wa matibabu ya moyo kwa watoto ya kibingwa yanaendelea kuboreshwa hapa nchini.
“Kwa wodi za watoto wenye magonjwa ya moyo peke yake kwa hapa Afrika Mashariki na kati hii ndio itakua wodi ya kwanza inayowahudumia watoto bila kuwachanganya na watu wazima na hii italeta ufanisi zaidi kwani nafasi ya kufanya makosa haitakuwepo kwasababu kutakuwa na wataalamu wanaohudumia watoto tu” alisema Waziri Ummy
Waziri Ummy, alisema  wodi hiyo ambayo ukarabati wake umekamilika inatarajiwa kuwa  na vitanda 32 na chumba cha uangalizi maalum (ICU) kitakachokuwa na vitanda 15 jambo ambalo litasaidia kuwafanyia upasuaji watoto wengi zaidi waliopo katika foleni ya upasuaji na kuokoa maisha yao. 
“Serikali ilitoa milioni 700 kwa ajili ya ukarabati wa wodi hii na sasa kwa mara nyingine tena serikali imetoa milioni 500 kukamilisha miundombinu ya ukarabati wa wodi hii. Nawashukuru sana taasisi ya Baps Charity ambao nao wamewekeza  milioni 800 katika kuhakikisha kuwa wodi hii inakarabatiwa, serikali tutazidi kuunga mkono juhudi hizi ”  alisema Waziri Ummy.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prf. Mohamed, Janabi alisema kwa shifti mbili za kliniki ya watoto zilizopo JKCI inaona wagonjwa wa moyo hadi sitini kwa siku thelathini wakiwa ni watoto, hivyo kulikuwa na umuhimu wa kuongeza wodi hiyo ya watoto. 
Akizungumzia upasuaji wa magonjwa ya moyo prof. Janabi amesema kuwa jumla ya wangonjwa 1356 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua kwa mwaka 2018, hii kwa mwaka jana ukiondoa Afrika kusini JKCI ndio hospitali iliyofanya upasuaji kwa wangonjwa wa moyo wengi zaidi kuliko nchi yoyote ya Afrika.
“Wodi hii mpya ni kwaajili ya watoto chini ya miaka 13 pekee na hii itatufanya kuwa taasisi ya kwanza Afrika Mashariki na kati kuwa na jengo lenye kuhudumia watoto bila kuwanchanganya na watu wazima “alisema prof. Janabi
 Meneja wa Jengo la Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) Kikwete Flora Kassembe akimwelezea Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu namna ambavyo wodi ya watoto itakavyotumika wakati wa ziara fupi ya waziri huyo kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuregenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na mtoto Shakira Athumani kutoka Tanga anayesubiria kufanyiwa upasuaji wa magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) baada ya ziara fupi ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo jana katika taasisi hiyo jijini Dar es Salaam. Wodi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza baada ya kufanya ziara fupi ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo jana katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuregenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi na kushoto ni Meneja wa Jengo la taasisi hiyo Flora Kassembe. Wodi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wadau wa taasisi ya Baps Charity  baada ya kufanya ziara katika taasisi hiyo na kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto  jana katika taasisi hiyo Jinini Dar es Salaam. Wodi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu akizungumza na baadhi ya wagonjwa wanaosubiri kupatiwa huduma za matibabu ya moyo baada ya kufanya ziara fupi kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo jana katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.  Wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo inayojengwa katika Taasisi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto Loveness Richard anayesubiri kuingizwa katika chumba cha upasuaji wa moyo kupitia tundu dogo kwa kutumia mtambo wa Cathlab baada ya kufanya ziara fupi kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo jana katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.  Wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo inayojengwa katika taasisi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
Na Genofeva Matemu – JKCI
20/01/2019 Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete (JKCI) imekuwa   taasisi ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kuwa na wodi pekee ya kuwahudumia watoto wenye magonjwa ya moyo bila kuwachanganya na watu wazima.

Eneo la wodi hiyo lilitolewa mwaka 2017 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk. John Pombe Magufuli alipokua akizindua Hospitali ya Mloganzila na kuiagiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoa sehemu ya jengo linalohudumia watoto kwa JKCI ili watoto wenye magonjwa ya moyo waweze kuwa na wodi yao katika kuleta ufanisi wa matibabu ya moyo kwa watoto hapa nchini.

Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi hiyo Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamaii, Jinsi, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alisema upatikanaji wa wodi hiyo ni juhudi za serikali katika kuhakikisha utolewaji wa matibabu ya moyo kwa watoto ya kibingwa yanaendelea kuboreshwa hapa nchini.
“Kwa wodi za watoto wenye magonjwa ya moyo peke yake kwa hapa Afrika Mashariki na kati hii ndio itakua wodi ya kwanza inayowahudumia watoto bila kuwachanganya na watu wazima na hii italeta ufanisi zaidi kwani nafasi ya kufanya makosa haitakuwepo kwasababu kutakuwa na wataalamu wanaohudumia watoto tu” alisema Waziri Ummy
Waziri Ummy, alisema  wodi hiyo ambayo ukarabati wake umekamilika inatarajiwa kuwa  na vitanda 32 na chumba cha uangalizi maalum (ICU) kitakachokuwa na vitanda 15 jambo ambalo litasaidia kuwafanyia upasuaji watoto wengi zaidi waliopo katika foleni ya upasuaji na kuokoa maisha yao. 
“Serikali ilitoa milioni 700 kwa ajili ya ukarabati wa wodi hii na sasa kwa mara nyingine tena serikali imetoa milioni 500 kukamilisha miundombinu ya ukarabati wa wodi hii. Nawashukuru sana taasisi ya Baps Charity ambao nao wamewekeza  milioni 800 katika kuhakikisha kuwa wodi hii inakarabatiwa, serikali tutazidi kuunga mkono juhudi hizi ”  alisema Waziri Ummy.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prf. Mohamed, Janabi alisema kwa shifti mbili za kliniki ya watoto zilizopo JKCI inaona wagonjwa wa moyo hadi sitini kwa siku thelathini wakiwa ni watoto, hivyo kulikuwa na umuhimu wa kuongeza wodi hiyo ya watoto. 
Akizungumzia upasuaji wa magonjwa ya moyo prof. Janabi amesema kuwa jumla ya wangonjwa 1356 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua kwa mwaka 2018, hii kwa mwaka jana ukiondoa Afrika kusini JKCI ndio hospitali iliyofanya upasuaji kwa wangonjwa wa moyo wengi zaidi kuliko nchi yoyote ya Afrika.
“Wodi hii mpya ni kwaajili ya watoto chini ya miaka 13 pekee na hii itatufanya kuwa taasisi ya kwanza Afrika Mashariki na kati kuwa na jengo lenye kuhudumia watoto bila kuwanchanganya na watu wazima “alisema prof. Janabi
 Meneja wa Jengo la Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) Kikwete Flora Kassembe akimwelezea Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu namna ambavyo wodi ya watoto itakavyotumika wakati wa ziara fupi ya waziri huyo kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuregenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na mtoto Shakira Athumani kutoka Tanga anayesubiria kufanyiwa upasuaji wa magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) baada ya ziara fupi ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo katika taasisi hiyo jijini Dar es Salaam. Wodi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza baada ya kufanya ziara fupi ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuregenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi na kushoto ni Meneja wa Jengo la taasisi hiyo Flora Kassembe. Wodi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wadau wa taasisi ya Baps Charity  baada ya kufanya ziara katika taasisi hiyo na kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto katika taasisi hiyo Jinini Dar es Salaam. Wodi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu akizungumza na baadhi ya wagonjwa wanaosubiri kupatiwa huduma za matibabu ya moyo baada ya kufanya ziara fupi kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo  katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.  Wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo inayojengwa katika Taasisi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto Loveness Richard anayesubiri kuingizwa katika chumba cha upasuaji wa moyo kupitia tundu dogo kwa kutumia mtambo wa Cathlab baada ya kufanya ziara fupi kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.  Wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo inayojengwa katika taasisi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimsikiliza aliyemfikisha mjukuu wake katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupata matibabu ya moyo Donata John (kushoto) baada ya kufanya ziara fupi kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.  Wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo inayojengwa katika taasisi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimsikiliza mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo kupitia tundu dogo kwenye paja alipotembelea wodi za wagonjwa wa moyo baada ya kufanya ziara fupi kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam. 

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimsikiliza aliyemfikisha mjukuu wake katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupata matibabu ya moyo Donata John (kushoto) baada ya kufanya ziara fupi kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo jana katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.  Wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo inayojengwa katika taasisi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimsikiliza mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo kupitia tundu dogo kwenye paja alipotembelea wodi za wagonjwa wa moyo baada ya kufanya ziara fupi kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo jana katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam. 

WAGONJWA MOI KUFANYIWA UPASUAJI BILA NUSU KAPUTI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuwapokea wakufunzi wa kutoa dawa usingizi kutoka nchini Latvia katika ukumbi mpya wa mikutano wa MOI 
Dkt Iveta Gobovska kutoka Chuo Kikuu cha Ltvia akizungumza jambo katika hafla maalumu ya kupokelewa na kuanza kwa mafunzo ya kuwapatia wagonjwa dawa za usingizi kwa njia ya kisasa (Regional block anaesthesia) hifla hiyo imefanyika leo katika Taaisisi ya MOI
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akipokea vifaa tiba ambavyo vitatumika kutolea mafunzo ya kutoa dawa za usingizi kwa mbinu ya kisasa (Regional Block anesthesia) kutoka kwa Dkt Iveta Gobovska kutoka Chuo Kikuu cha Ltvia cha nchini Latvia
1. Madaktari bingwa wa usingizi wa MOI pamoja na madaktari wanafunzi wakifuatilia jambo katika hafla ya kuwapokea wakufunzi wawili wa dawa za usingizi kutoka nchini Latvia



Taasisi ya tiba ya Mifupa MOI imeanzisha huduma ya kutoa dawa za usingizi (Reginal block Anaesthesia) ambapo eneo husika linalofanyiwa upasuaji ndilo litakolo husika kwa kuzuia mishipa ya fahamu na hivyo mgonjwa kuwa macho na kuzungumza au hata kusoma gazeti

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface katika hafla ya kuwapokea wakufunzi wawili kutoka Chuo kikuu cha Latvia cha nchini Latvia ambao watatoa mafunzo hayo ya kibingwa ya kuzuia mishipa ya fahamu katika eneo linalofanyiwa upasuaji badala ya kumlaza mgonjwa usingizi (Nusu kaputi) kwa zaidi ya siku kumi kwa madaktari bingwa wa MOI na madaktari walio mafunzoni

“Huu ni muendelezo wa mafunzo ambayo tulishayaanzisha kwa mdakatari wetu , lengo kubwa la mafunzo haya na ujio wa wakufunzi hawa ni kuhakikisha huduma hii inaendlea kutolewa hapa MOI. Ni mbinu bora na salama ya kumlaza mgonjwa kwaajili ya upasuaji ambapo mgonjwa anaweza kufanyiwa upasuaji huku anasoma kitabu (Novel) ambapo baada ya upasuaji mgonjwa hapati maumivu makali na anaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani siku hiyohiyo” Alisema Dkt Boniface

Dkt Boniface amesema pamoja na wakufunzi hawa kutoa mafunzo , Taasisi ya MOI itasiani mkataba wa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Latvia lengo kuu ikiwa ni kubadilishana uzoefu katika utoaji wa huduma za kibingwa za Usingizi (Anaesthesia)

“Kwa kuanza tutasaini mkataba wa ushirikiano wa miaka mitatu ambapo watalaamu kutoka hapa watapata fursa ya kujifunza kwenye Chuo chao lakini pia watakuja hapa kutoa mafunzo ya muda mfupi kama ambavyo hawa wamekuja” Alisema Dkt Boniface

Dkt Boniface ameongeza kwamba kwa sasa Taasisi ya MOI imeanzisha huduma ya kulazwa na kufanyiwa upasuaji siku hiyohiyo yaani (Same day Surgery) hivyo huduma hii itatumika katika wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji na kuruhusiwa kwani wagonjwa hawapati maumivu makali baada ya upasuaji na hakuna masharti magumu baada kufanyiwa upasuaji

Kwa upande wake Profesa Alex Miscuks kutoka Chuo Kikuu cha Latvia amesema ni heshma kubwa kupata fursa ya kuja kubadilishana uzoefu hapa Tanzania kwani pamoja na kutoa mafunzo atapata fursa ya kujifunza mambo mengi.

“Nashukuru sana kwa kunialika, nimefurahi kukutana na madaktari wazuri na wazoefu hapa MOI, naamimi mimi pia nitajifunza mambo mengi kwenu, ahsnteni sana” alisema Prof Miscuks

Kwa upande wake Dkt Iveta Gobovska ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha wagonja mahututi katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Latvia amesema amefarijika kupata fursa ya kuja kubadilishana uzoefu na madaktari wa Tanzania na anamini pande zote mbili zitanufaika na mafunzo haya.

MIAKA 20 YA FEMINA YAWAFIKIA VIJANA NCHINI KOTE

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
WAKATI  shirika lisilo la Kiserikali la FEMINA likitimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake wameeleza kujivunia kwao kwa kufanikiwa kuwafikia vijana wengi zaidi katika kila Wilaya iliyopo Tanzania bara na baadhi ya shule za Visiwani Zanzibar na kutoa elimu ambayo imewasaidia na wengi wao kutoa mirejesho chanya kwa shirika hilo.

Akizungumza na  waandishi wa habari Mkurugenzi wa habari wa FEMINA Amabilisi Batamula amesema kuwa hadi sasa kuna klabu zaidi ya 2300 ambazo zimesajiliwa na zinapata majarida, pia kuna muunganiko wa klabu zaidi ya 2900 ambazo ni muunganiko wa klabu za Wilaya, Mikoa na Kanda pamoja na klabu za FEMA za walimu walezi wa klabu hizo zipatazo 38.

Batamula amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa shirika hilo wamekuwa wakijikita katika utoaji wa elimu kwa vijana kuhusiana na afya ya uzazi na ujinsia kwa kuwapa stadi za maisha na huwafundisha  mbinu ya kusubiri hadi watakapotimiza malengo yao bila kujihusisha na masuala la ngono.

Amesema kuwa FEMINA huwasaidia vijana katika kujikwamua kiuchumi na hiyo ni kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kupata taarifa na wao huzichakata na kuwapa vijana kupitia majarida na kusema kuwa hutoa taarifa kwa vijana juu ya  fursa zinazowazunguka  na sio kuwapatia fedha wala mitaji.

Pia amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa shirika hilo wamekuwa wanawahimiza vijana kushiriki katika mikutano mbalimbali ya vijiji, kata na Wilaya pamoja na kujua haki na wajibu wao katika jamii na kujitolea katika masuala ya kijamii kama vile kufanya usafi katika hospitali, masoko na kujitolea damu pamoja na kupinga tamaduni potofu zikiwemo mimba za utotoni na ukeketaji.

"Wana klabu wa FEMA jijini Dodoma wamekuwa na utaratibu wa kujitolea damu katika hospitali mbalimbali na hata tatizo la damu likitokea wana klabu hutafutwa na kushiriki zoezi hilo ambalo huokoa maisha ya wengi." ameeleza Batamula.

Kuhusiana na njia wanazotumia kuwafikia vijana kote nchini ameeleza kuwa, FEMINA huwafikia vijana hao kupitia jarida la FEMA linalotoka mara nne kwa mwaka na kusambazwa katika shule zote za sekondari zilizosajiliwa kama wana klabu, pia amesema kuwa wanawafikia vijana hao kupitia vipindi vya redio na televisheni na vipindi vingi hufanyika vijijini ili kuwafikia vijana wengi zaidi.

Amabilisi amesema kuwa lazima wazazi pamoja na walezi wawe wawazi kwa vijana ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha kuhusiana na afya ya uzazi pamoja na kukabiliana na changamoto katika ukuaji wao.

Kuhusiana na mchango wa FEMINA katika klabu za FEMA kote nchini Afisa ufuatiliaji na tathimini kutoka FEMINA Martha Samwel amesema kuwa ufaulu kwa shule zenye klabu za FEMA uameongezeka na hiyo ni kutokana na mirejesho wanayoipata kutoka kwa walimu na walezi wa klabu hizo kwani kupitia klabu hizo wanafunzi wamekuwa wakielimishana na kuhimizana kuhusu masomo na katika baadhi ya maeneo wanafunzi watoro darasani wamerudi shule kutokana na nguvu ya klabu za FEMA.

"Kuna baadhi ya shule zimekuwa na misimamo yao ambapo wanakauli mbiu zao za kutoruhusu mwanaklabu ya FEMA afeli darasani, hii inawapa nguvu na ari ya wao kusoma zaidi na hatimaye kufanya vizuri katika masomo yao" ameeleza Martha.

Aidha amesema kuwa mafanikio waliyoyapata kwa miaka 20 ni makubwa sana hasa kwa kuwafikia vijana wengi Tanzania kote na kutoe elimu ambayo imewasaidia kwa kiasi kikubwa hivyo wanajivunia kuwa sehemu ya maisha kwa  vijana hao.

Pia amewashauri vijana wengine kujiunga na klabu za FEMA ili waweze kupata elimu ya afya na ujinsia pamoja na elimu ya ujasiriamali ambayo itawasaidia katika kujenga taifa na kujenga nchi ya viwanda kwa kuwa wao ndio nguvu kazi ya taifa.
Mkurugenzi wa habari wa FEMINA, Amabilis Batamula akizungumza na wanahabari katika warsha iliyowakutanisha  na kujadili  changamoto na mafanikio ya shirika hilo wakielekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwake.
Mmoja wa waandishi wa habari akiwasilisha mada katika warsha hiyo iliyofanyika katika ofisi za FEMINA jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari wakijadiliana katika makundi kuhusiana na namna vyombo vya habari vinavyochangia kuleta maendeleo nchini.

MTANGAZAJI MAARUFU WA BBC AMTAABISHA NA KUMSHUSHUA TUNDU LISSU KWENYE MAHOJIANO LONDON

$
0
0

Leo (21-01-2019), mahojiano ya Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki, alipelekwa kuhojiwa katika kipindi maarufu cha BBC cha HARDtalk, jijini London.

Katika mahojiano hayo, Mtangazaji alionekana kujiandaa vizuri baada ya kuchimbua taarifa zinazomhusu Tundu Lissu na utendaji wa Raisi John Pombe Joseph Magufuli, ambao ulionekana kumkuna mtangazaji.

Watoto wa mjini wangesema, ama kweli Mbunge huyo mropokaji, ameingia choo cha kike. Mtangazaji alichimbua na kujiridhisha, ili asije akavunja heshina ya BBC kwa uchochezi na madai ya kufikirika yasiyokuwa na chembe ya ushahidi.

Katika siku ambazo Tundu Lissu hatazisahau, basi ni leo. Angekuwa katika masuala ya dini, leo alistahili kuokoka.

MTANGAZAJI STEPHEN SACKUR: Wewe ni mwanasheria mwandamizi. Unaifahamu Sheria vizuri kuliko mimi. Ni hatari sana kukurupuka na kudandia mambo serious pasipokuwa na uthibitisho au ushahidi thabiti wa unayoyasema. Baadhi ya watu unaowatuhumu ni wapinzani wenzio na misimamo yao inakinzana na kukanusha madai yako kabisa.

LISSU: Wapigie simu.

MTANGAZAJI STEPHEN SACKUR: Mfano Lawrence Masha aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Serikali ya Kikwete, badae akahamia upinzani na kuwa mpinzani mkubwa wa Rais Magufuli, baada ya kuridhishwa na utendaji wa Rais Magufuli, sasa anamkubali Sana. Anasema, japokuwa huwezi kukubaliana na kila jambo analofanya Magufuli, lakini dhamira yake na utendaji wake unagusa maisha ya watanzania wengi, hasa wale wa kawaida.

Madai yako ni ya kuunga unga, (allegations, connections, claims using inflammatory language) pasipokuwa na ushahidi wa kuhusika kwa serikali katika shambulio lako.

Lissu: Kwasababu nilikuwa nafuatiliwa na watu.

MTANGAZAJI akapigwa butwaa.

Mbona inaweza kuwa mtu yeyote mbaya katika jamii aliyemuudhi? Wewe ulikuwa mnadhimu wa upinzani Bungeni, ulikuwa Rais wa TLS na mpinzani maarufu. Ingeweza kuwa mtu yeyote. Una uthibitisho gani wa madai yako?

LISSU: Siku hiyo hapakuwa na walinzi getini. 

(Mtangazaji anazidi kumshangaa na madai yasiyokuwa na chembe ya ushahidi). 

MTANGAZAJI STEPHEN SACKUR:

Mbona Rais Magufuli alilaani tukio la kushambuliwa kwako na akaagiza uchunguzi ufanyike Mara moja.

LISSU: Rais Magufuli kamwe hajasema lolote kuhusu hilo shambulio. Lakini, alituma ujumbe wa twita haraka haraka halafu ukapotea.

MTANGAZAJI STEPHEN SACKUR:

Lakini ulienda mbali sana kumuita Rais wako dikteta uchwara, hivi kweli angekuwa mbaya hivyo, Magufuli angekubalika na watu wengi Tanzania, asilimia 70 na wengi ndani na nje ya Tanzania wanathibitisha kuwa anafanya kazi nzuri sana.

Magufuli ameondoa wafanyakazi hewa, ambayo ilikuwa wizi na rushwa na hili sio jambo dogo kwa nchi za kiafrika, anatekeleza ahadi zake vizuri, ameongeza makusanyo ya kodi na kufanya maendeleo makubwa hadi Tanzania inakuwa mfano, ameongeza ufanisi na uwajibikaji katika Serikali na jamii. Mwingereza mmoja was Oxford ameandika kuwa Magufuli ameweza kuutafuna mfupa uliowashinda wengi kwamba Taifa la kiafrika haliwezi kushindana na mashirika makubwa ya kimataifa na likashinda, lakini Magufuli ameweza kwenye sekta ya madini. 

Wewe katika upinzani huyapendi hayo mafanikio? (Akagongwa)

MTANGAZAJI STEPHEN SACKUR: Lakini lugha yako ni ya kuudhi, unatoa madai bila kuwa na ushahidi, je lugha yako ya kuudhi itachochea moto au itapoza joto la mifarakano?

· Umesema 2020 umedhamiria kupambana na Magufuli katika uchaguzi mkuu, utatumia mkakati wa kigomvi au njia ya amani?

· Sasa unamtuhumu Magufuli kwa mambo mengi mabaya (hata kwa mazuri yanayoonekana). Uko tayari kurudi nyumbani Tanzania kupambana na Magufuli?

LISSU: Hadi nitakapopona. Madaktari wakisema niko fiti tu, kesho yako nitapanda ndege kurudi (Mtangazaji anamtazama kama anachosema ni kweli)

MTANGAZAJI STEPHEN SACKUR: Utakuwa na ulinzi wowote?

LISSU: Serikali itanilinda saa 24. (Mtangazaji akamstukia kama ni mzima. Kweli mlinzi wako ndiye utajaribu kumkandia hivyo).

MTANGAZAJI STEPHEN SACKUR: Utalinda haki za mashoga na wanafunzi wa shule za msingi wasome wakiwa na mimba?

LISSU: Mashoga wana haki ya kutoingiliwa vyumbani mwao. Wana haki ya usiri. Wasichana wenye mimba wataendelea na shule.


FIKIRIA BINTI YAKO YUKO DARASANI KATIKA SHULE YA MSINGI, PEMBENI WASICHANA WENZAKE 10 NI WAJAWAZITO, WAVULANA 15 NI MASHOGA. MWANAO ATAKUWA SALAMA? BASI UJUE HUYU JAMAA MGONJWA.

MTANGAZAJI AMEMUUMBUA. KUMBE AMEKARIRI SHERIA TU. LEO BBC IMEMUUMBUA. KUMBE NI KIMEO. “HIVI KWELI MAFANIKIO HAYA YA MAGUFULI WEWE HUYATAKI,” MTANGAZAJI ALIPOMUULIZA, LISSU KAMBADILISHIA MADA.

KALAGHABAHO

Wahamiaji haramu 35 wakamatwa jijini Dar

$
0
0
WAHAMIAJI haramu 35 kati ya 81 wamekamatwa wakiuza pipi, karanga na kahawa na kujifanya machinga. Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake, Kaimu Afisa Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam, Mrakibu Novaita Mrosso alisema kati ya watu hao 35 ni raia wa Burundi ambao walikuwa wanafanya biashara hiyo kama machinga kwa kutembeza sehemu mbalimbali.

Wahamiaji hao, wamekamatwa mwishoni mwa wiki na Idara ya Uhamiaji wakifanya biashara hiyo jijini Dar es Salaam. Operesheni kali imekuwa inafanyika jijini zima ili kuhakikisha wahamiaji wote wanatiwa mbaroni ambapo wahamiaji hao baadhi wamejifanya machinga kukwepa kukamatwa. Hatua hiyo, imekuja baada ya mwishoni mwa mwaka jana, Rais Dkt. Magufuli kutoa vitambulisho maalum kwa ajili ya kuwatambua wafanyabiashara wadogo wadogo nchini ambapo kila Mkuu wa Mkoa alikabidhiwa.

Vitambulisho hivyo jumla 25,000 na kila kitambulisho kitagharimu shilingi 20,000 kwa machinga. Uhamiaji imeingia kazini baada ya kugundua kuwa wapo baadhi ya wahamiaji haramu wamekuwa wanafanya biashara kama wamachinga na kazi hiyo ilifanyika Januari 17, mwaka huu hadi Januari 20 ambapo jumla ya watu 81 walikamatwa.

Mrakbu Mrosso alisema wahamiaji hao wamekuwa wanauza kahawa, karanga, pipi na vitu vidogo sehemu mbalimbali za jiji huku wakijifanya kama sehemu ya machinga kujificha.

"Tumewanasa na wanafikishwa mahakamani haraka kisha watarudishwa kwao,"alisema. Aliongeza kuwa bado wanaendelea kuwahoji wahamiaji wengine 46 kujua wanatoka nchi gani na kujua uhalali wao wa kuwepo hapa nchini. "Hapa tumebaini wapo wasomali,wanigeria, Mcameroon na wengine,"alisema. Mrakibu Mrosso alisema kazi ya kuwasaka wahamiaji haramu ni endelevu na wamekuwa wanashirikiana na viongozi wa serikali za mitaa ili kuwabaini wote.

"Nawaomba watu wenye taarifa watupe habari, sisi tutaendelea kuwaficha wale wote wanaopa ushirikiano ili kuwakamata wahamiaji,kamwe hawaponi tutawakamata wote na wale wanaowaleta,"alisema. Pia, amewaomba viongozi walioajiri wageni kutoa taarifa kwa vile hivi sasa wanaendelea na kazi ya kupitia kila sehemu ikiwemo viwanda,ofisi, baadhi ya makazi ili kuwanasa wageni wote wanaoishi kinyemela.

Alisema wamefanya kazi hiyo toka Novemba na Disemba,mwaka jana na kuhakiki jumla ya wageni 16,102 ambapo 7,000 walihakikiwa katika ofisi ya mkoa.Wengine 3,613 walihakikiwa katika ofisi ya Ilala, 3,668 Kinondoni,1,267 Temeke,356 Ubungo na 198 Kigamboni. Mrakibu Mrosso alisema kwenye zoezi hilo,wamefanya utambuzi na uandikishaji wa raia wa Malawi na wahamiaji walowezi ambapo jumla waliandikishwa ni 1,770.

Kwenye mabao Kinondoni(756),Ilala (548)Temeke(162),Ubungo (144) na Kigamboni ni 150. Ametoa onyo kali kwa wananchi wanaohifadhi wahamiaji haramu kuacha mara moja kwa vile mali zao na kifungo huenda kikawakumba. "Unajua sheria imebadilika hivi sasa kifungu cha 46 cha sheria uhamiaji sura ya 54 rejeo la 2016,mtu akikamatwa amehifadhianaweza kufungwa miaka 20,gari au nyumba inataifishwa pia na adhabu zote zinaweza kuwa za pamoja,"alionya.
 Wahamiaji haramu waliokamatwa mkoa wa Dar es Salaam wakiwa wamechuchumaa  baada ya kufikishwa makao makuu ya uhamiaji.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Kaimu Afisa Uhamiaji  jijini Dar es Salaam, Novaita Edmund Mrosso akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wahamiaji haramu  waliokamatwa  maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam .
Kaimu kamishina wa Uhamiaji jijini Dar es Salaam,Novaita Edmund Mrosso akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.


SIMBA SC, YANGA SC ACHENI MZAHA KWENYE MASHINDANO YA SPORTPESA CUP MWAKA HUU - TARIMBA

$
0
0
Na Bakari Madjeshi,  Globu y'all Jamii
Wakati Michuano ya Sportpesa Cup 2019 yakitarajiwa kuanza hapo kesho, Januari 22, Mkurugenzi wa Udhibiti na Utawala wa Sportpesa Tanzania,  Abbas Tarimba amezitaka timu za Tanzania zinazoshiriki Michuano hiyo kuacha mzaha kwa kuingiza uwanjani time za vikosi vya pili

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Tarimba amesema kuwa anapenda kuona Taji la Michuano hiyo kwa mwaka huu linabaki hapa nchini kutokana na tayari Kenya kulibeba mara mbili mfululizo. 

"Nimekutana na Viongozi wa timu zote mbili za Simba na Yanga zimeongea nao kuelekea kwenye Michuano hii, niwewaambia waache mzaha safari hii, kuna zawadi nono tusingependa ziondoke tena Kenya", amesema Tarimba. 

Katika Michuano hiyo itakayoshirikisha timu Nane kutoka Kenya na Tanzania itaanza kesho kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar huku timu za Singida United na Young Africans zitarajiwa kutupa karata zao. Yanga SC itamenyana na Kariobangi Sharks majira ya saa 10 za jioni wakati Singida United ikichuana na Bandari majira ya Saa 8 mchana kwenye dimba hilo hilo la Uwanja wa Taifa.

Kuelekea kipute hiko cha ufunguzi majira ya saa 10, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa wamejiaanda vizuri kushiriki Michuano hiyo, ambapo amesema kuwa watajitahidi kuwaangalia wapinzani wao (Kariobangi Sharks) ili kuwajua zaidi ili kufanya vizuri kwenye mchezo huo.

Naye Nahodha wa Kikosi hicho, Ibrahim Migomba amesema kuwa watajitahidi kufanya vizuri kwenye Michuano hiyo kutokana name maandalizi walionayo kuelekea mchezo wao dhidi ya Kariobangi Sharks, Ajib amesema kuwa kuna siri wamepewa na Kocha wao Mwinyi Zahera hivyo kuna uwezekano wakupata ushindi mzuri dhidi ya timu hiyo ya Kenya.
Mkurugenzi wa Udhibiti na Utawala wa Sportpesa Tanzania, Abbbas Tarimba akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam kuelekea Michuano ya Sportpesa Cup 2019 yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Kesho, Januari 22.

ZIARA TUMEJIFUNZA NA MAMBO MENGI SANA -MWAMUNYANGE

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wamehitimisha ziara ya siku tatu ya kutembelea miradi mbalimbali inayosimamiwa na Mamlaka hiyo. Ziara hiyo iliyokuwa ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani imemalizika kwa Mwenyekiti wa bodi Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange kutoa tathmini ya jumla ya mambo waliyojifunza.

Akizungumza baada ya kuhitimisha ziara hiyo, Jenerali Mstaafu Mwamunyange amesema wananchi wana matarajio makubwa na DAWASA ya kupata huduma ya majisafi inayoaminika. Mwamunyange amesema kwenye ziara ya siku tatu wamejifunza mengi sana na wameona ni namna gani DAWASA wanafanya jitihada kubwa kuhakikisha wanafikisha maji kwa wananchi wote ili kufikia malengo ya serikali.

Amesema kuwa,  pamoja na yote kuna changamoto zinazoikabili DAWASA ikiwa ni pamoja na kupasuka kwa mabomba kutokana na miundo mbinu chakavu na kupelekea kupotea kwa maji mengi na watu wanaojiunganishia maji kiholela kitu kinachopelekea Mamlaka kupoteza fedha nyingi sana. 

Ameeleza kuwa Changamoto nyingine ni majitaka na hilo linasababishwa na kuwa na maeneo machache yaliyokaribu na wananchi yanayopokea maji hayo na DAWASA wanaendelea kufanya jitihada za kujenga miundo mbinu itakayokuwa rafiki ikiwemo na kuleta magari yao yatakayokuwa yanachukua majitaka kwa bei nafuu.

“Mradi wa kuchakata majitaka ni jambo la msingi sana na utakuwa na faida kwa wananchi wanaoishi kwenye maeneo jirani ila bado una changamoto kwani maji yanayozalishwa na kupelekwa kwa wananchi ni mengi tofauti na yale yanayoenda kuchukuliwa,”amesema Jenerali Mstaafu Mwamunyange.

Akizungumzia  miradi mbalimbali iliyojengwa na inayoendelea kujengwa na DAWASA, Mwamunyange amesema kuwa wananchi wanatakiwa kulipia bili za maji kwa wakati ili mamlaka iweze kupata kipato kitakachotosheleza na kuwekeza nguvu zaidi kujenga miradi kwa fedha za ndani.

Kwa upande wa Mjumbe wa Bodi wa DAWASA Mhandisi Gaudence Aksante amesema kuwa, lazima kuweka mkakati wa kupunguza upotevu wa maji ili Mamlaka kuongeza kipato na maji hayo yamekuwa yanapotea kutokana na mtandao wa zamani kuwa mdogo na kwa sasa maji ni mengi sana.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja amepokea ushauri huo kutoka kwa bodi ya wakurugenzi ikiongozwa na Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange na watajitahidi kuhakikisha wanapanua mtandao wa maji ili kupunguza upotevu wa maji.

Ziara ya Bodi ya Wakurugenzi ilitembelea miradi ya ndani ya Dar es Salaam na ile ya Mkoa wa Pwani ikiwemo mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Juu na Ruvu Chini, Ujenzi wa matanki Bagamoyo, Changanyikeni, Kibamba, Kisarawe, maunganisho mapya ya wateja Salasala, mradi wa uchakataji majitaka Toangoma na mradi wa maji Kijichi, Kiwalani, Bonyokwa na maeneo mengine ya Jijini Dar es Saalam.
 Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Mhandisi Charles Makoye akimuelezea Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange mradi mzima wa Kuchakata majitaka uliopo Toangoma Leo Jijini Dar es Salaam.
 Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Mhandisi Charles Makoye akimuonesha Mkurugenzi wa Bodi ya DAWASA Jenerali Davis Mwamunyange na wajumbe wa bodi wa Mamlaka hiyo moja ya Chemba inayohifadhi majitaka katik mradi wa Kuchakata majitaka Toangoma Leo Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA Jenerali Davis Mwamunyange akisikiliza maelekezo kutoka kwa Msimamizi wa miradi DAWASA Mhandisi Charles Makoye mradi wa Kijichi unaohudumia wananchi wa eneo hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akionyeshwa eneo linaloanzia mradi wa Bonyokwa utakaohudumia wananchi kuanzia Kimara mwisho hadi Bonyokwa.

Serikali ya Rwanda imepiga marufuku aina yoyote ya matangazo ya biashara ya dawa za asili

$
0
0
Serikali ya Rwanda imetangaza kupiga marufuku aina yoyote ya matangazo ya biashara ya madawa ya kijadi au asili na kuamuru vyombo vya habari vya nchi hiyo kusitisha vipindi vya waganga wa kijadi kunadi umaarufu wao.

Biashara ya madawa ya kijadi imeshamiri Rwanda na wizara ya afya inasema waganga wengi wa jadi wamekuwa wakitumia vyombo vya habari kupotosha wananchi.

Kulingana na tangazo la wizara ya afya ya Rwanda ni marufuku kutangaza biashara ya madawa kwa kutumia picha, mabango au pia kutumia vipaaza sauti barabarani kote nchini Rwanda.

Vyombo vya habari pia kama magazeti, mitandao ya kijamii , redio na televisheni vimekatazwa kupitisha vipindi na matangazo yoyote ya biashara kuhusu uganga wa kijadi.

Matangazo au vipindi kuhusu waganga na madawa ya kijadi siku hizi imekuwa biashara kubwa sana kwa karibu vituo vyote vya redio na televisheni za kibinafsi nchini Rwanda.

Waganga wa kijadi wenyewe wakipishana moja kwa moja kila mmoja akitangaza umaarufu wake kutibu magonjwa sugu wanayosema kwamba yamekosa tiba ya kizungu.Wengine wanakwenda mbali na kutangaza kuwa wanatoa madawa ya Baraka na kutibu umaskini huku wengine wakisema wazi kuwa wachawi.Tangazo hilo limezua hisia mbali mbali miongoni mwa waganga wa jadi.

Baadhi wamesikitishwa na uamuzi wa wizara ya afya wa kuwakataza kutangaza biashara yao kupitia vipindi vya redio:

''Sijafurahishwa na uamuzi huu kwa sababu ingekuwa vizuri wizara ya afya kwanza ikatuuliza ukweli wa yale tunayozungumzia, halikadhalika ubora na uhalali wa madawa tunayotumia.

Mimi nilikuwa nafanya matangazo mengi ya biashara yangu kupitia vyombo vya habari ili watu wafahamu umaarufu wangu wa kutibu magonjwa, ila ninachosema kama kuna mmoja wetu aliyefanya kosa la kusema kwamba anafanya miujiza, sote hatuwezi kuathirika kutokana na yeye.'' amesema mmoja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA BBC Swahili.

Makabidhiano ya ofisi Wizara ya Ujenzi yafana

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Eng. Joseph Nyamhanga akimpongeza Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga mara baada ya kumkabidhi ofisi kufuatia kuhamishiwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI wengine ni wajumbe wa Menejimenti ya sekta ya ujenzi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Eng. Joseph Nyamhanga akisisitiza jambo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga katika hafla ya kumkabidhi ofisi wengine ni wajumbe wa Menejimenti ya sekta ya ujenzi.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga katikati akiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Eng. Joseph Nyamhanga katika picha ya pamoja na wajumbe wa Menejimenti ya sekta ya ujenzi katika hafla ya makabidhiano ya ofisi mjini Dodoma.

Waziri Mkuu Majaliwa kufungua Mkutano wa Maafisa Ustawi wa Jamii

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI 

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kufungua mkutano wa siku tatu wa maafisa ustawi wa jamii mikoa 26 na halmashauri zote nchini wenye lengo la kujadili utendaji kazi, utoaji huduma za ustawi wa jamii na mifumo ya utendaji kazi. 

Akizungumza na habarileo jijini hapa, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais Tamisemi, Rashid Maftaha, alisema mkutano huo unatarajia kuanza Januri 29 hadi 31 mwaka huu jijini Dodoma. 

Alisema mkutano huo unatarajia kushirikisha washiri takribani 370 ikiwamo maafisa ustawi wa jamii wa mikao 26, halmashauri 184, wadau wa maendeleo, na wizara za kisekta ambazo zinahusiana na utoaji wa huduma za ustawiwa jamii, kama wizara ya elimu, afya, Katiba na Sheria, Viwanda na Biashara, madini na kilimo. 

“ Unaweza jiuliza, Wizara ya Madini inahusikajie na huduma za ustawi wa jamii, hawa ni wadau muhimu, kwani kwenye migodi kuna utumikishwaji wa watoto, na hata watumishi wake wanakuwa wako mbali hivyo ni lazima wafikiwe na huduma za jamii, halii hii pia iko kwenye viwanda. 

“Pia unaweza kujiuliza kwa nini wizara ya kilimo, lakini ukweli ni kuwa asimia 80 ya watanzania wanafanya shughuli za kilimo na asilimia 70 yao wako vijijini, na takwimu zetu zinaonesha kuwa watoto wengi walio katika mazingia hatarishi wanatoka vijijini ambaochanzo kikubwa na umasikini na jangwa la Ukwimi. 

Maftaha aliongeza:” Tunashuku wenzetu wa kilimo katika Mpango wa Maendeleo ya Kilimo kwa kwanza na huu wa pili ni jumuishi kwani kuna dirisha maalumu kwa ajili ya watu walio katika mazingira hatarishi wakiwemo, wenye ulemavu, wajane, wazee ambao wanapata pembejeo na wana uwakilishi katika kamati za ugawaji pembejeo 

Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Weledi, uadilifu, uwajibikaji ni nguzo ya msingi katika kuleta usatawi wa makundi maalumu kuelekea katika uchumi wa kati wa viwanda.” 

Maftah alisema: “ Tunaamini watendaji wetu kwenye halmashauri na mikoa wakifanya kazi zao kwa kuzingatia uadilifu, weledi, wakifuata sheria, kanuni na taratibu tunaamini makundi yenye uhitaji maalumu wanaweza kufikiwa inavyotakiwa hivyo mchango wao ukaongezeka katika uchumi wa viwanda, 

Mkutano huu ni wa kwanza ikiwa ni takribani miaka 15 baada ya kutokea mabadiliko ya kimuundo kwa kuiondoa Idara ya Ustawi wa Jamii kutoka Serikali kuu kwenda Serikali za Mitaa. 

Akifafanua zaidi, Maftaha alisema serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ikifanya kwa vitendo katika kuwahudumia wananchi hususani wale wanyonge ikiwamo wazee, wenye ulemavu, watoto wa mitaani na wale wanaoishi katika mazingira magumu, wanawake wenye mahitaji maalumu kama wajane, wenye magonjwa sugu na walio katika kaya masikini. 

Alisema lengo la mkutano ni kuwakutanisha watendaji hao na kutoa mrejesho wa utekelezaji wa huduma za jamii katika maeneo ya serikali za mitaa, utendaji kazi na namna mfumo inavyofanya kazi. 

“ Pia tutaangalia mafanikio na changamoto na kwa upamoja na kuja na mapendekezo ya kutatua changamoto stahiki za za kiutendaji na mfumo ili kusogeza na kuimarisha zaidi hudumua za ustawi wa jamii kwenye mamlaka ya serikali za mitaa. Kama kuna yale ambayo yatataka kuwepo mabadilko ya kisera basi tutafikisha katika mamlaka husika. 

Aidha, Maftah ametumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kuendelea kuwalinda watoto kwa kutoa taarifa haraka kwa mamlaka pale panapokuwa na viiashiria ay dalili au kitendo cha ukatili kwa mtoto. 

Alisema pamoja na pamekuwa na changamoto ya ushahidi pale kesi zinapofika mahakamani au wahanga na mashahidi kubadili taarifa walizotoa awali, lakini ni vyama jamii ikaungana kutakabiliana na ukatili kwa watoto. 

“Hatuwezi kukubali vitendo vya ukatili anavyofanyiwa mtoto alafu tuambiwe kuwa wamekubaliana pembeni hilo hatulikubali mpaka sheria ichukue mkondo wake.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais TAMISEMI, Rashid Maftaha.

KAMATI YA BUNGE YAISHAURI SERIKALI KUWEKA MKAZO KATIKA KAMPENI YA UPANDAJI MITI

$
0
0
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira imeishauri Serikali kuona namna bora ya kuendeleza kampeni ya upandaji miti kwa mafanikio zaidi katika ngazi zote. Ushauri huo umetolewa katika kikao  baina ya Kamati hiyo na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakati wa kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa kipindi cha miezi sita yaani (Julai 2018 – Desemba 2018).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Waheshimiwa Wabunge wameishauri Serikali kuhuisha kampeni ya upandaji miti katika Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo Vikuu ili kasi ya upandaji miti iendane na kasi ya ukuaji wake, ikiwa ni pamoja na kutekeleza kwa vitendo mpango wa kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.

“Wekeni utaratibu wa kutoa motisha kwa wanafunzi wanaofanya vizuri zaidi katika kupanda na kutunza miti” alisisitiza Mhe. Dotto Gimbi Mjumbe wa Kamati hiyo. Akitoa ufafanuzi mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima amesema katika kipindi cha miezi sita, Ofisi ya Makamu wa Rais imepata mafanikio mengi ikiwa ni pamoja na kutimiza malengo waliojiwekea na kuahidi kuendelea kuzipatia ufafanuzi changamoto nyingine zilizoibuliwa na wajumbe wa Kamati likiwemo suala la utekelezaji wa miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi kwa upande wa pili wa Muungano.

Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge vinaendelea katika kumbi za Bunge Jijini Dodoma na siku ya kesho Kamati hii itapokea taarifa ya Usimamizi na Matumizi salama ya Bioteknolojia ya Kisasa na Maandalizi ya Mpango wa Taifa wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki kwa Wachimbaji wadogo wa dhahabu chini ya Mkataba wa Minamata.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima aliesimama akitoa ufafanuzi wa hoja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira mara baada ya Kamati kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kipindi cha Julai – Desemba, 2018.

Mwenyekiti wa Bodi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Prof. Esnati Osinde Chaggu akijitambulisha kwa mara ya kwanza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira. Prof. Chaggu ameteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Joseph Magufuli. Kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Kanali Mstaafu Masoud Khamis.



Wananchi wahimizwa kuanza ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya kabla ya Serikali kusaidia

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga kufuatilia na  kusimamia wananchi wa vijiji 12 vya bonde la ziwa Rukwa kuhakikisha kuwa wanaanza kujenga zahanati ili zahanati hizo ziweze kupunguza mzigo kwa vituo vya afya na hospitali ya wilaya.

Amesema kuwa ili hospitali ya Wilaya isiweze kuzidiwa na wagonjwa ni vyema vijiji vikawa na zahanati zao na kwa ngazi ya kata kuanza ujenzi wa vituo vya afya ili mgonjwa apitie katika ngazi hizo na hatimaye kufika katika ngazi ya hospitali ya wilaya tofauti na hapo hospitali hiyo inaweza kutumiwa na hata wagonjwa ambao wanaweza kutibiwa katika ngazi ya zahanati.

“Kwa upande wa vituo vya afya, jamani nisikitike hapa, katika kata 13 ambapo kila kata inapaswa iwe na kituo chake cha afya tunavyo vituo vya afya viwili peke yake, tuna kituo cha afya pale milepa na kituo cha afya hapa mtowisa, kwahiyo kata 11 hazina vituo vyake vya afya, kwahiyo hapa pia DC jipange tuanze,” Alisema.

Mh. Wangabo aliyasema hayo wikiendi hii katika songambele ya kuchimba msingi wa majengo saba kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya katika kata ya Mtowisa na kuhusisha wananchi kutoka katika vijiji 10 na madiwani 13 wa kata zote za bonde la ziwa Rukwa ambapo hospitali hiyo inajengwa.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo, mganga mkuu wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Fani Musa alisema kuwa hospitali hiyo itatumika kama kituo cha rufaa kutoka vituo vya afya na zahanati zote za halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga na kuongeza kuwa mradi utagharimu shilingi Bilioni 7.5 hadi kumamilika kwake ambapo itakuwa na majengo 22 na mpaka sasa halmashauri imepokea shilingi bilioni 1.5 kwaajili ya kuanza ujenzi huo.

“Fedha hizi za awamu ya kwanza zitatumika kujenga majengo saba, jengo la Utawala ambalo litatumia shilingi milioni 332, jengo la wagonjwa wa nje litatumia shilingi milioni 271, jengo la “Pharmacy” litatumia shilingi milioni 120, jengo la maabara litatumia shilingi milioni 171, jengo la vipimo vya mionzi (radiology, X-ray na Ultra Sound) litatumia shilingi milioni 121, jengo la kufulia litatumia shilingi milioni 110 na jengo la mwisho ni la wazazi litakalotumia shilingi milioni 379,” Alisema.

Katika hatua nyingine Mh. Wangabo amewataka wakala wa umeme vijijini kuhakikisha wanaongeza kasi ya kufikisha umeme kwenye bonde hilo ambalo lina wakulima wengi wa mahindi na mpunga pamoja na wavuvi ambapo mazao yao mengi huvushwa na kupelekwa mikoa ya jirani hivyo kuukosesha mkoa mapato na pia kwaajili ya kusaidia huduma za kiafya katika bonde hilo na kuongeza kuwa bila ya halmashauri kuongeza kasi ya kukusanya mapato malengo hayo ya kumalizia maboma hayatafikiwa.

Bonde la ziwa Rukwa lina vijiji 63, kati ya vijiji hivyo vijiji 24 vina zahanati, vijiji 17 vina maboma ya zahanati ambayo hayajaezekwa na vijiji 12 havina zahanati wala maboma, na kati ya kata 13 zilizopo katika bonde hilo ni kata 2 tu ndio zenye vituo vya afya na kufanya kata 11 kukosa vituo vya afya huku kata 3 zikiwa na maboma ya vituo hivyo.
Baadhi ya wananchi waliokuwa wamejitokeza kwenye songambele ya kuchimba misingi kwaajili ya majengo saba ya Hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga itakayojengwa katika Bonde la Ziwa Rukwa, kata ya Mtowisa, Kijiji cha Mtowisa. 
 Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa pili toka kushoto ndani ya msingi) akisaidia kuchimba msingi wa itakayokuwa hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga baada ya kushirikiki na wananchi wa bonde la ziwa Rukwa kwenye songambele ya uchimbaji wa misingi ambao ungegharimu shilingi milioni 8 kama wangetumika mafundi. 
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akihamasisha wananchi waliojitokeza kwenye songambele ya uchimbaji wa misingi kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (ndani ya msingi) akisaidia kuchimba msingi wa itakayokuwa hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga baada ya kushirikiki na wananchi wa bonde la ziwa Rukwa kwenye songambele ya uchimbaji wa misingi ambao ungegharimu shilingi milioni 8 kama wangetumika mafundi. 
 Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule (kulia) akiendelea kuhamasisha wananchi walioshiriki kwenye songamebele ya kuchimba misingi kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga. 

MIKUTANO YA KIMATAIFA KUCHOCHEA UTALII NA BIASHARA

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud,Arusha.

Wadau nchini wametakiwa kutumia fursa ya mikutano ya kimataifa kuchochea utalii na biashara ili kukuza pato la taifa na kuleta maendeleo yanayotokana na fursa za mikutano,biashara na utalii.

Hayo yameelezwa jijini Arusha katika mkutano wa Wadau wa Utalii,Wafanyabiashara pamoja na wamiliki wa kumbi za mikutano uliongazia fursa zinazotokana na mikutano ya kimataifa katika kukuza biashara na utalii .

Mwakilishi wa taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) Antony Chamanga alisema kuwa kwa sasa wanashirikiana na serikali katika kuhakikisha kuwa mikutano ya kimataifa inaleta tija nchini kwa Wafanyabiashara,wamiliki wa hoteli pamoja na kusababisha ongezeko la utalii.

Aidha alisema kuwa kwa sasa sekta binafsi inashiriki vyema katika maendeleo na kukuza vipato vya watu waliojiajiri katika biashara na utalii hivyo mpango wa kushirikiana na serikali utasaidia kukuza mapato ya taifa.

Mratibu wa mikutano ya kimataifa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dorothea Massawe licha ya soko la watalii kwenda mbugani kujionea wanayamapori bado tunahitaji kuwa na zao lingine la mikutano ya kimataifa .

“Tukipata mkutano wa watu 1000,2000 kati yao wako watakaokwenda kutembelea vivutio vya utalii kama lilivyoagizo la serikali la kuongeza watalii bodi ya utalii inashirikiana na sekta binafsi katika kufanikisha biashara ya mikutano ya kimataifa” Alisema Dorothea

Mdau wa Hoteli Farida Hatibu anasema kuwa mkoa wa Arusha umekua kivutio kikubwa cha mikutano na watalii ambao hupendelea huduma zilizoko hivyo ubora wa huduma za mikutano ya kimataifa na miundombinu utasaidia kuvutia mikutano ya kimataifa.

MADIWANI SIMANJIRO WAMFAGILIA RAIS MAGUFULI

$
0
0
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, limesoma maazimio ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa kutatua migogoro ya maeneo ya hifadhi na vijiji 366 na kurejesha kikokotoo cha awali cha wastaafu. Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi akisoma maazimio hayo, alisema baraza hilo linampongeza kwa dhati Rais Magufuli kutokana na matukio hayo mawili. 

Myenzi alisema baraza limeona maamuzi hayo ya Rais Magufuli ni kielelezo tosha cha uongozi mahiri, uliotukuka na sikivu kwa wananchi wanyonge ambao ni nguzo muhimu ya ujenzi wa Taifa. Alisema uamuzi wa kurejesha kikokotoo katika utaratibu wa awali, ni kielelezo tosha cha uongozi mahiri na kutatua migogoro ya watumiaji wa ardhi na mipaka ya maeneo ya hifadhi ni ya kupongezwa. 

"Kwa upendo huu aliouonyesha mheshimiwa Rais Magufuli, baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro linampongeza kwa dhati na kuomba aendelee na moyo huu wa upendo kwa Taifa lake," alisema Myenzi. Diwani wa kata ya Terrat, Jackson Ole Materi alisema mgogoro wa hifadhi na vijiji 366 ulikuwa unaathiri ustawi wa wananchi hasa jamii za wafugaji, wakulima, wavuvi na watumiaji wa ardhi katika mipaka ya vijiji na maeneo ya hifadhi. 

Ole Materi alisema kwa uamuzi huo imedhihirika azma ya Rais Magufuli ya kuwajali wanyonge na kuhakikisha jamii yenye utulivu inayotumia muda mwingi kwa uzalishaji badala ya kutatua migogoro. Diwani wa kata ya Loiborsiret, Ezekiel Lesenga (Mardad) alisema wananchi wa eneo hilo nao wanampomgeza Rais Magufuli kwa uamuzi wake kwani nao ni waathirika wa ardhi. 

Mardad alisema kwenye kijiji cha Kimotorok kuna taasisi mbalimbali ikiwemo shule, zahanati, kanisa na makazi ya watu waliotakiwa kufukuzwa sababu ya kupakana na hifadhi ya jamii ya Mkungunero. Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Albert Msole alisema baraza hilo linaundwa na jamii ya wafugaji na wakulima linampongeza Rais Magufuli na kumtakia maisha marefu na ufanisi kwenye majukumu yake. 

Msole alisema wilaya ya Simanjiro nayo ni miongoni mwa wanufaika wa matamko hayo mawili kwani watumishi wa serikali wamenufaika na wafugaji pia wamefaidika. 

Diwani wa kata ya Emboreet, Christopher Kuya alisema Rais Magufuli amejali maslali na matakwa ya wafanyakazi ambao walikuwa waathirika wakubwa pindi wakistaafu. 

"Uamuzi huu wa Rais Magufuli ni kielelezo tosha cha uongozi wake thabiti na sisi madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro tunampongeza mno," alisema Kuya. 
 Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhe Albert Msole akifunga kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo ambao walimpongeza Rais John Magufuli kwa kuwatetea wafugaji na watumishi wa serikali, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Yefred Myenzi. 
 Diwani wa kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Ezekiel Lesenga Mardad akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kwa kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuwatetea wafugaji hasa kijiji cha Kimotorok kjnachopakana na hifadhi ya jamii ya Mkungunero. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Yefred Myenzi akisoma maazimio ya Baraza la Madiwani la kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuwatetea wafugaji na watumishi, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Albert Msole. 
 Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara na watumishi wa Halmashauri hiyo wakifuatilia kikao cha Baraza la Madiwani. 
Diwani wa kata ya Terrat wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Ole Materi akisoma taarifa ya hoja ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuwatetea wafugaji na watumishi wa serikali.  

JIJI LA ARUSHA LINA ZIADA YA UMEME MEGAWATI 50, TANESCO YAALIKA WAWEKEZAJI ZAIDI KWENYE VIWANDA

$
0
0
NA MWANDISHI WETU, MIRERANI 
 UWEKEZAJI kwenye miundombinu ya umeme uliofanywa na Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania TANESCO umeanza kuzaa matunda eneo la machimbo ya madini Mirerani mkoani Manyara. 
 Serikali kupitia TANESCO iliwekeza kwa kujenga kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha KIA na hivyo kuwezesha hali ya upatikanaji umeme ulio bora na wa uhakika kwenye eneo la Mirerani kuongezeka. 
 Kwa sasa matumizi ya umeme kwenye eneo lote la Mirarani ni kiasi cha Megawati 3.5 lakini kubwa zaidi miongoni mwa watumiaji wakubwa walioanza kufaidika na uwekezaji huo ni pamoja na kiwanda cha Godmwanga Gems Limited kinachojihusisha na kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe (Graphite) na kile cha Mirerani Tanzanite vyote viko Mirerani. 
 Meneja wa Shirika la Umeme wilaya ya Ki-TANESCO Mirerani Mhandisi Zacharia Masatu amewaambia waandishi wa habari wanaotembelea eneo hilo kuwa kiwanda hicho pekee kinatumia kiasi cha Megawati 1.1 ya umeme. 
 Aidha Meneja wa TANESCO jijini Arusha Mhandisi Herini Mhina amesema jiji lina ziada ya umeme Megawati 50, na hivyo amewahimiza wawekezaji katika sekta ya viwanda vikubwa, vya kati na vidogo kuwekeza ili kufaidi uwekezaji wa serikali katika miundombinu ya umeme nchini. 
 “Wito wetu kwa wafanyabiashara na wawekezaji, waje wawekeze kwenye mkoa wetu wa Arusha sababu kama tulivyoeleza awali tuna umeme wa kutosha, kwa mkoa mahitaji ni Megawati 75 na uwezo wa kituo chetu ni Megawati 120 kwahiyo unaweza kuona tuna ziada inayofikia Megawati 50.” alisema Mhandisi Mhina. 
 Mhandisi Mhina alibainisha kuwa, viwanda vinaweza kuleta matokeo makubwa ya uwekezaji katika miundombinu ya umeme uliofanywa na serikali kwani matumizi ya kiwanda kimoja inaweza kuwa ni mahitaji ya wilaya nzima. 
 “Viwanda ni njia mojawapo inayoweza kutupeleka kwenye uchumi wa kati tunaotaka kwa haraka zaidi.” Alisisitiza. TANESCO ilifunga mitambo ya kuingiza umeme wa kutosha kwenye kiwanda cha Godmwanga Gems Limited na kwamba kinajitegemea ambapo kuna jumla ya transfoma pozo kubwa tatu na gharama za ufungaji wa mitambo hiyo zinakadiriwa kufikia shilingi Milioni 60.
Aidha afisa wa kiwanda hicho cha kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe (graphite), Nai Mainga alisema kiwanda kilianza uzalishaji wa madini hayo ya graphite (kinywe) Juni 2018 na kwamba tangu uzalishaji uanze hadi hivi sasa, tayari wamezalisha kiasi cha tani 5,600 na wateja wakubwa wa madini hayo ni China. 
 “Matumizi makubwa ya madini hayo ya kinywe hutumika kutengeneza vitu maka betri na tunapozungumzia betri ni pamoja na betri zile kubwa za magario na mitambo, lakini pia kuna taarifa kuwa madini hayo hutumika kutengeneza bati maalum la kuzuia injini ya ndege ili isipate moto sana kwani madini haya huchomwa sana ili kupata zao la mwisho.” Alifafanua. 
 Alisema kuna baadhi ya nchi ambazo tayari zimeanza mchakato wa kusitisha matumizi ya petrol kuendeshea magari na hivyo kuna uwezekano wa kutumia madini haya ili kutengeneza betri za kuendesha magari.

  Meneja wa TANESCO jijini Arusha Mhandisi Herini Mhina(kushoto), akimsikiliza Meneja wa Shirika hilo wilaya ya Ki-TANESCO Mirerani, Mhandisi Zacharia Masatu, akifafanua kuhusu namna TANESCO ilivyoweza kufikisha umeme wa kutosha kwenye eneo la Mirarani leo Januari 21, 2019. 
Meneja wa TANESCO jijini Arusha Mhandisi Herini Mhina
 Kituo cha kupokea umeme kilichoko ndani ya kiwanda cha kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe, (graphite) huko Mirerani mkoani Manyara ambapo TANESCO imefu nga mitambo na transfoma kubwa tatu ili kutoa umeme toshelezi kwa kiwanda hicho.
transfoma pozo kubwa tatu zilizofungwa na TANESCO kwenye kiwanda hicho.


 Kiwanda cha Godmwanga Gems Limited kinachojihusisha na kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe (Graphite)
 Kiwanda cha Godmwanga Gems Limited kinachojihusisha na kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe (Graphite)
 Mhandisi Zacharia Masatu, akifafanua jambpo ndani ya kituo cha kupokelea umeme kwenye kiwanda cha Godmwanga Gems Limited kinachojihusisha na kuchimba na kuchakata madini ya Kinywe (Graphite)





VOA Swahili: Duniani Leo January 21, 2019

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live


Latest Images