Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

MTENDAJI MKUU TEMESA AFANYA ZIARA MIKOA YA PWANI, MANYARA,TABORA, NA KIGOMA.

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa pili kushoto aliyevaa suti) akipewa maelezo na wafanyakazi wa kivuko cha MV. MKONGO mara baada ya kukagua kivuko hicho. Kivuko cha MV. MKONGO kinatoa huduma katika mto Rufiji kati ya Mkongo na Utete wilayani Rufiji mkoani Pwani na kina uwezo wa kubeba abiria 40 kwa wakati mmoja.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akikagua mashine ya kupimia uwiano wa tairi za magari katika karakana ya TEMESA mkoa wa Manyara wakati wa ziara yake mkoani humo. Kushoto ni Meneja wa Temesa mkoani Manyara Mhandisi Margreth Julian.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa pili kushoto) akishuka kutoka kwenye kivuko cha MV. MALAGARASI mara baada ya kumaliza kukagua utendaji kazi na hali ya usalama wa kivuko hicho kinachotoa huduma katika mto Malagarasi kati ya Ilagala na Kajeje mkoani Kigoma, kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50. Wa kwanza Kushoto ni Nahodha wa kivuko Kassimu Mkitege. 
Abiria wakiingia katika kivuko cha MV. MALAGARASI tayari kuanza safari kutokea upande wa Ilagala kuelekea upande wa Kajeje, kivuko cha MV MALAGARASI kinatoa huduma katika mto Malagarasi kati ya Ilagala na Kajeje mkoani Kigoma na kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50. 
Kivuko cha MV. MALAGARASI kikielea katika mto Malagarasi, kivuko hicho cha tani 50 kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 kwa wakati mmoja na kinatoa huduma kati ya Ilagala na Kajeje mkoani Kigoma.
Nahodha wa Kivuko cha MV. MALAGARASI Kassimu Mkitege kushoto akiwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle kulia wakati alipokua akikagua hali ya usalama na utendaji kazi wa kivuko hicho. Kivuko cha MV MALAGARASI kinatoa huduma katika mto Malagarasi kati ya Ilagala na Kajeje mkoani Kigoma. 

PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO - (TEMESA)


Halmashauri 4 zatuhumiwa kwa ubadhilifu

$
0
0

Angela Msimbira OR-TAMISEMI.

Halmashauri nne (4) zimetuhumiwa kwa ubadhilifu wa zaidi ya shilingi milioni 785 fedha zilizotolewa kupitia mradi wa Equip-T kwa ajili ya kutekeleza kazi mbalimbali za Elimu katika halmashauri hizo. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya tuhuma za ubadhilifu katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya TAMISEMI, Jijini Dodoma 

Amezitaja Halmashauri ambazo zimetumia fedha hizo kinyume na utaratibu kuwa Manispaa ya Kigoma, Butiama, Liwale na Bahi ambapo hadi kufikia sasa halmashauri hizo hazijaweza kurejesha fedha hizo TAMISEMI tangu agizo lilipotolewa. 

Mhe. Jafo amesema OR-TAMISEMI iliziagiza Halmashauri 8 ambazo zilituhumiwa kwa ubadhilifu wa fedha hizo kuzirejesha lakini mpaka sasa ni Halmashauri nane tu ndizo zilizorejesha fedha hizo kwa wakati na hizo zilizobakia kuonyesha utovu wa nidhamu kwa kutotii maagizo ya Serikali. 

“Inasikitisha kuona baadhi ya Halmashauri kushindwa kutii maagizo yanayolewa na Serikali ya kutaka Halmashauri zilizotuhumiwa kwa ubadhilifu wa fedha za Equipt T kurejesha fedha hizo ili ziweze kutekeleza miradi ya elimu nchini” anasema. 

Ameendelea kufafanua kuwa amesikitishwa zaidi na Manispaa ya Kigoma Ujiji na Butiama kutokana na kuwa na tuhuma nyingi za ubadhilifu wa fedha za miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo. 

Mhe. Jafo ameziagiza Halmashauri ambazo bado hazijakamilisha kurejesha fedha hizo kuhakikisha zinawasilishwa kabla ya tarahe 28/3/2019. 

Amezielekeza mamlaka husika kuwachukulia hatua za kinidhamu na kuwashusha vyeo Afisa Mipango, Mweka Hazina na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama kwa kushindwa kutimiza wajibu wao. 

Mhe. Jafo ameitaka mamlaka inayohusika kufanya uchunguzi wa aliyekuwa Mkurugenzi, amemuagiza Katibu MMkuu OR-TAMISEMI kuwachukulia hatua Mweka Hazina wa Halmashauri ya Bahi Said Ishabairu ambaye alihamishiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa. 

“Kumekuwa na tabia kwa baadhi ya watumishi kuhamishwa maeneo ya kazi pale wanapokosea, hili si jambo jema Serikali haitavumilia bali itawachukulia hatua za kinidhamu watumishi wote wanaoihujumu Serikali popote pale watakapokuwa” alisema. 

Aidha ameziagiza Mamlaka husika kumtafuta aliyekuwa Mweka Hazina wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambaye kwa sasa amestaafu ili aweze kuhojiwa kwa tuhuma hizo. 

Jafo aliongeza kuwa Serikali haitavumilia mambo yeyote ambayo yanaleta hujuma katika suala zima la kuwahudumia watanzania hivyo amewataadharisha Wakurugenzi wote katika Halmashauri za Mamlaka za Serikali za Mitaa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa katika matumizi ya fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo. 

Jafo alimalizia kwa kumuagiza Naibu Waziri Mhe. Mwita Waitara kusimamia kwa makini miradi ya elimu na kuangalia namna fedha zilizvyotumika katika miradi hiyo agizo ambalo Mhe. Mwita amesema alalitekeleza kwa umakini mkubwa. 

MILIONI 1500 ZILIZOTOLEWA NA OFISI YA RAIS –TAMISEMI KUJENGA HOSPITALI YA KISASA HALMASHAURI YA MUFINDI

$
0
0
Na Ofisa Habari Mufindi 

Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imetiliana saini na Mafundi Uashi saba (07), watakaotekeleza kandarasi za awamu ya kwanza ya ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya Wilaya katika kata ya Igowole, eneo ambalo liliteuliwa rasmi kuwa makao makuu mapya ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.

Hafla fupi ya kusaini kandarasi hizo imefanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, ambapo, jumla ya Majengo saba muhimu yatajengwa ambayo ni Jengo la Utawala, Jengo la Wagonjwa wa nje, Jengo la kuhifadhia dawa, Jengo la kufulia, Jengo la Mionzi, Jengo la Wazazi sanjari na Jengo la Maabara ambayo yanatajikiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi nane (08)

Aidha, kiasi cha Fedha kitakachotumika kutekeleza awamu ya kwanza ya mradi huu mkubwa na muhimu kwa ustawi wa Afya za wakazi wa Mufindi ni shilingi Milioni elfumoja na miatano (1,500) sawa na shilingi Bilioni 01 na Milioni 500 zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

Akizungumza katika hafla ya kutiliana saini, Mwenyekiti wa Halmashari Mhe. Festo Mgina, amewataka Mafundi hao kutekeleza maradi kwa wakati sanjari na kuzingatia viwango vilivyokubalika na atahakikisha wanapata vifaa na malipo yao kwa wakati ili Hospitali hiyo ikamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wakazi wa Halmashauri ya Mufindi.

Naye kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bw. Isaya Mbenje, ametoa rai kwa wataalamu hao wa ujenzi kufanya kazi kwa weledi mkubwa, kuacha visingizio vya mara kwa mara vitakavyochelewesha kukamilika kwa mradi.

“Pigeni kazi Fedha tunayo, yote ipo kwenye akaunti inawasubiri ninyi, hivyo yeyote atakayekwamisha tutavunja mkataba, atafukuzwa pamoja na kufunguliwa mashitaka” akihitimisha Ofisa Mtendaji Mkuu huyo.

Imetolewa na
Ofisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano
HALMSHAURI YA WILAYA MUFINDI
  ikionesha ramani ya majengo mara baada ya kukamilika
Mafundi wateule wakisaini kandarasi za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mhe. Festo Mgina kushoto, akikabidhi mkataba kwa mmoja kati ya Mafundi Saba walioshinda zabuni ya kujenga Hospitali.

SEKRETARIETI YA AJIRA YATAKIWA KUTENDA HAKI KUIWEZESHA SERIKALI KUPATA WATUMISHI WENYE SIFA STAHIKI

$
0
0


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi ya Sekretarieti hiyo Magogoni jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier M. Daudi akieleza majukumu ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika katika ofisi ya Sekretarieti hiyo Magogoni jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao cha kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika Magogoni katika ofisi ya Sekretarieti hiyo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier M. Daudi akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuhusu namna mfumo wa upokeaji wa maombi ya kazi (Recruitment Portal) na mfumo wa kupanga wasailiwa waliofaulu inavyofanya kazi wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na Menejimenti ya Sekretarieti ya Ajira alipoitembelea ofisi hiyo kuhimiza uwajibikaji.


Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetakiwa kuendelea kutenda haki katika kuratibu mchakato wa ajira ili kuiwezesha Serikali kupata watumishi wenye sifa stahiki na maadili mema ambao watatoa huduma kwa umma kwa kuzingatia weledi na kuwajali wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa huduma zinazotolewa na Taasisi za umma. 

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi hiyo iliyopo Magogoni jijini Dar es Salaam, yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kufahamu kwa kina majukumu ya Sekretarieti hiyo na kujiridhisha namna Sekretarieti hiyo inavyotekeleza majukumu yake ya kila siku. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kinatakiwa kutenda haki ili Serikali ya Awamu ya Tano ipate watumishi wenye sifa na vigezo watakaoendana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuliletea taifa maendeleo katika sekta za miundombinu, afya, viwanda, biashara, kilimo, usafiri wa anga, elimu na uchumi kwa ujumla wake. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, awali Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilikuwa ikilalamikiwa sana kuwa, mchakato wa kuomba kazi Serikalini ulikuwa ukichukua muda mrefu kiasi cha waombaji kusahau kama waliwasilisha maombi, hivyo ameipongeza Sekretarieti kwa kubuni mfumo wa upokeaji wa maombi ya kazi (Recruitment Portal) na mfumo wa kupanga wasailiwa waliofaulu ambayo kwa kiasi kikubwa imepunguza malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na waombaji wa ajira Serikalini na kuongeza kuwa, hivi sasa mchakato wa ajira mpya unachukua siku 52 tu licha ya kuwepo taratibu nyingi zinazozingatiwa kukamilisha mchakato mzima. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amefafanua kuwa, mfumo huo una kanzi data ya waombaji wote waliofanyiwa usaili na kupata ufaulu mzuri lakini kutokana na uwepo wa fursa chache za ajira hawakupangiwa vituo vya kazi, hivyo unaiwezesha serikali kupata watumishi kwa wakati pindi wanapohitajika haraka katika Taasisi za Umma. 

Sanjari na hayo, Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameitaka Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kutobweteka kwa mafanikio waliyoyapata kupitia mfumo wa Ajira Portal na badala yake waongeze kasi ya ubunifu ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imedhamiria kwa dhati kuboresha huduma zinazotolewa na Taasisi za Umma nchini. 

Kwa upande wake, Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier M. Daudi, amesema ofisi yake ilianzishwa kwa lengo mahususi la kukabiliana na changamoto za ajira zilizokuwa zikijitokeza hapo awali, hivyo iliundwa ili kuongeza uwazi, kutenda haki na kuhakikisha kuwa ajira zinapatikana kwa kuzingatia sifa. 

Bw. Daudi amesisitiza kuwa, ofisi yake kwa kushirikiana na waajiri inazingatia Sera ya Ajira, Sheria, Kanuni na Taratibu katika kusimamia mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma kwa lengo la kuiwezesha Serikali kupata watumishi wenye sifa na maadili mema watakaoisaidia Serikali kufikia malengo yake makubwa iliyojiwekea, ikizingatiwa kuwa watumishi ndio injini ya utekelezaji wa majukumu ya Serikali. 

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Mbarak Abdulwakil amemshukuru Mhe. Dkt. Mwanjelwa kwa nasaha zake za kuitaka Sekretarieti kuzingatia weledi katika jukumu zito la kuwezesha ajira za watumishi wa umma na kumhakikishia kuwa, maelekezo yote aliyoyatoa yatatekelezwa kikamilifu na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inatekeleza majukumu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutafuta wataalam wenye ujuzi maalum na kuandaa mfumo wa kuifadhi taarifa za wataalam, kutangaza nafasi wazi za kazi zinazojitokeza katika Utumishi wa Umma, kuhusisha wataalam ili kushirikiana nao kwa ajili ya kufanya usaili kulingana na mahitaji, kuwashauri waajiri kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na mchakato wa ajira, kuandaa orodha ya wahitimu wa vyuo na wataalam kwa weledi kwa madhumuni ya kurahisisha rejea za ujazaji nafasi na kuendesha mchakato wa ajira wa Watendaji Wakuu wa Wakala na Idara zinazojitegemea za Serikali.

WADAU WA MAENDELEO WAMUUNGA MKONO DC MURO UJENZI WA MADARASA

$
0
0
Wadau mbalimbali wa maendeleo Wilayani Arumeru wameendelea Kujitokeza na kumuunga mkono Mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu Jerry Cornel Muro katika ujenzi wa madarasa.

Wadau hao wa maendeleo Waliahidi kuchangia mifuko 100 ya Saruji na kwa Awamu ya kwanza leo Hii wamemkabidhi Dc Muro mifuko 50 ya saruji na kuahaidi ndani ya wiki mbili zijazo watakamilisha ahadi yao. 

Wakizungumza mara baada ya kukabidhi mifuko hiyo ya saruji wameeleza kuwa Lengo la kumuunga mkono Dc Muro katika ujenzi wa madarasa ni kwamba wanaamini Katika kujenga jamii imara lazima kuhakikisha Elimu inapewa kipaumbele cha pekee pia wameeleza hawana budi kuunga mkono juhudi za serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amewashuku wadau hao wa maendeleo kuendelea kujitolea katika kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanapata madarasa ya kutosha

Pia Dc Muro amewaomba Wadau wengine kuja kumuunga mkono katika kuchangia ujenzi wa madarasa katika Halmashauri ya Arusha Dc na Halmashauri ya Meru. 

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
20/01/2019

ANAANDIKA MHE. HUSSEIN BASHE MBUNGE WA NZEGA MJINI.

$
0
0
Salaam,

Kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Nzega Mjini na Halmashauri ya Mji wa Nzega ninapenda kutumia fursa hii kuishukuru serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kutuunga mkono katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora za kijamii ndani ya jimbo la Nzega Mjini.

Lakini pia ninaishukuru serikali kupitia wizara ya elimu kwa kutupatia fedha jumla ya shilingi za kitanzania Milioni Mia Tatu kumi na sita (Tzs 316,000,000) kwa ajili ya uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu ndani ya Jimbo la Nzega Mjini ambazo kwa nyakati tofauti tuliziomba serikalini kupitia Waziri wa Elimu Mhe. Joyce Ndalichako.

Aidha, mchanganuo wa fedha hizi ni kama ifuatavyo;
1. Shule ya Sekondari Mwanzoli. 
Mwanzoli imetengewa jumla ya shilingi Milioni Hamsini (Tzs 50,000,000).
Matumizi: Fedha hii itatumika kwa ajili ya Ujenzi wa Maabara.

2. Shule ya Sekondari Kitangili
Kitangili imepewa jumla ya Shilingi Milioni Mia moja na hamsini (Tzs 150,000,000)

-Matumizi:
Fedha hizi zimetolewa kwa ajili ya kukamilisha shughuli zifuatazo;
a) Ujenzi wa Utawala - 50,000,000
b) Ujenzi Madarasa 2 - 40,000,000
c) Ujenzi wa matundu 6 ya vyoo- 6,000,000
d) Bwalo na Nyumba kaya mbili - 54,000,000

3. Shule ya Sekondari Nzega
Jumla ya shilingi Milioni arobaini na sita (Tzs 46,000,000) imetengwa kwa shughuli zifuatazo;
a) Ujenzi wa madarasa mawili - 40,000,000
b) Ujenzi wa matundu sita ya vyoo - 6,000,000

4. Shule ya Sekondari Chief Ntinginya
Jumla ya shilingi Milioni Sabini (Tzs 70,000,000) ambayo matumizi yake ni kukamilisha Ujenzi wa Hosteli ya wanafunzi katika shule hii iliyopo kwenye Kata ya Nzega Magharibi.

Hata hivyo tunaendelea kuwakaribisha wadau wengine kwa ushirikiano zaidi ili kuweza kusaidia ujenzi wa mabweni kwenye kila kata ili kuongea hamasa ya ushiriki wa watoto wa kike kwenye elimu na kupambana na changamoto za umbali.

Kwa upande mwingine ninapenda kuwashukuru wananchi kwa kujitolea kwao kwenye miradi ya elimu na afya ndani ya jimbo letu bila kuwasahau Wataalamu mbalimbali wa Halmashauri ya Mji chini ya Mkurugenzi ambao nimekuwa nikiwasumbua mara kwa mara katika kuhakikisha jambo hili linafanikiwa lakini pia katika usimamizi wa miradi inayoendelea kutekelezwa jimboni na ndani ya Halmashauri yetu.

Madiwani wa maeneo ambayo miradi hii inatekelezwa pia ninawashukuru sana kwa kuendelea kuwa na umoja na ushirikiano bila kusahau Baraza la Madiwani kwa ushauri wa mara kwa mara.

Aidha ninawashukuru watendaji wote katika Ofisi ya Mbunge kwa namna ambavyo mmeendelea kufanya kazi muda wote bila kuchoka kwa ajili ya kuhakikisha tunatekeleza ahadi na ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Mwisho ninawashukuru sana Sungusungu pamoja na jumuiya zao ambao wamekuwa wakishirikiana nasi sana kwenye utekelezaji wa miradi hii na kusimamia ushiriki wa wananchi wa ngazi za chini; juhudi zenu zimesaidia sana kuamsha morali ya wananchi kuja pamoja kushiriki kwenye maendeleo.

Akhsante sana,
Hussein Bashe (Mb)
Nzega Mjini.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 21 2019

LIPENI KODI YA SERIKALI WACHENI KONA KONA-ASKOFU KIVUYO

$
0
0
Na. Vero Ignatus, Arusha


Waumini wa dini ya Kikristo Jijini Arusha wametakiwa kulipa kodi ya serikali kama inavyotakiwa siyo kuiba, kwani wao wanatakiwa kuwa mfano bora wa kuigwa katika jamii inayowazunguka

Hayo yamesemwa na Makamu wa Askofu Dayosisi ya kaskazini Kati Gidion Kivuyo alipokuwa akihubiri katika katika la KKKT Usharika wa Engarenarok uliopo Jiji Arusha.

Amesisitiza kuwa kumjua Mungu Pamoja na kukataa rushwa, kutokuiba mali ya serikali kwani hata neno la Mungu linasisitiza kulipa kodi.'' Lipeni kodi ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mpeni Mungu nanukuu maandiko siyo mimi''Alisema Mchungaji Kivuyo.Amewataka waumini hao kuishi maisha safi ya kuigwa maana ni chachu katikati ya kwa watu wengine wanaowatazama ambapo uadilifu, nidhamu na uchaji ambao kizazi kijacho kitajifunza kutoka kwao.

Amewasisitiza kuwa na utayari na kujifunza,akisema uanafunzi ni pamoja na kujikana wenyewe, kuepuke mambo ambayo siyo sahihi katika imani yao, na waenende sambamba na neno la Mungu linavyowataka.

Amewataka kujifunza na kutafakari siyo kufuata mkumbo bila Kuwa na mipangilio katika maisha bila kusahau uzalendo na kuchunguza mambo kwa kina.
'' Kuna watu wanaojifunza bila kufuzu mafunzo ya kweli, msiwe watu wasiopenda mema na kupenda anasa bali dumuni katika kweli ya Mungu ambayo itawaweka huru,epukeni kutangishwatangishwa kwenye mafundisho ya uongo nakupenda fedha" Alisema.

Amewataka kuwa na uelewa kwamba Imani haijengwi juu juu bali kwa mafundisho, huku akiwataka kuepuka utumwa ambao utawafanya mateka.
Amewaonya waumini hao na kuwataka makini na mafundisho ya uongo ambayo yanayogusa hisia lakini hayafundishi ukweli bali ni misisimko na wala hayana ukweli sawasawa na Mungu anavyoamuru.

Kadhalika amewasisitiza kufanya kazi kwa bidii iliwaweze kupata mafanikio sambamba na kulipa kodi ya serikali, na siyo kuzurura hovyo. '' Wacheni kuzunguka kwenye maombi kila mahali unachelewa wenzio wamefungua biashara zao na wamefanikiwa, wewe kutokana na kutokutulia kwako unabakia ukilaumu'' alisema

Amewaataka viongozi wa kanisa hilo kuwakumbusha waumini wao neno la Mungu mara kwa mara na kuwafundisha, Kutambua, kujuta, kutubia, kupokea, kuishi maisha na dhamiri safi mbele za Mungu. Amewataka kuweka malengo ya mwaka 2019 na siyo kuishi bila utaratibu ili waweze kurejea katika msingi mzuri wa kanisa hilo.

BENKI YA NMB YATOA MFUNGAJI BORA BBL 2018/19

$
0
0


Mshambuliaji wa NMB, Kaikai Leka, akipaa hewani kuifungia timu ya kikapu ya NMB wakati wa fainali ya Michuano ya Mabeki (BBL 2018/19), dhidi ya DTB, iliyopigwa Januari 19 kwenye Uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es Salaam. DTB ilishinda kwa pointi 90-73.
Mfungaji Bora wa mashindano ya kikapu kwa taasisi za fedha (BBL 2018/19), Kaikai Leka wa NMB, akipokea kombe dogo kama zawadi ya ufungaji bora kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, Juma Kimori, baada ya pambano la fainali ya michuano hiyo Januari 19 kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa NMB, Kaikai Leka, akipaa hewani kuifungia timu ya kikapu ya NMB wakati wa fainali ya Michuano ya Mabeki (BBL 2018/19), dhidi ya DTB, iliyopigwa leo Januari 19 kwenye Uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es Salaam. DTB ilishinda kwa pointi 90-73.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, Juma Kimori, akimkabidhi nahodha wa timu ya kikapu ya NMB, Danford Kisinda, kombe la ushindi wa pili wa Michuano ya Mabeki (BBL 2018/19), dhidi ya DTB, iliyopigwa leo Januari 19 kwenye Uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es Salaam. DTB ilishinda kwa pointi 90-73.



Na Ripota Wetu.


NYOTA wa mpira wa kikapu wa kikosi cha Benki ya NMB, Kaikai Leka, ameibuka Mfungaji Bora (Best Scorer) wa Ligi ya Kikapu kwa Taasisi za Fedha (Bankers Basketball League - BBL 2018/19), baada ya kufunga pointi 160 katika mechi za michuano hiyo iliyofikia tamati juzi, jijini Dar es Salaam.

Katika fainali ya kukata na shoka jana kwenye Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam, Benki ya DTB iliibuka mshindi baada ya kuifunga NMB kwa pointi 90-73, huku mchezaji wa NMB Leka akifunga zaidi ya nusu ya pointi zao hivyo kutangazwa Mfungaji Bora akifuatiwa na Acram Majid wa DTB, aliyefunga pointi 129.

Leka alizawadiwa Tuzo ya Mfungaji Bora, kama ilivyokuwa kwa Mchezaji Bora (MVP) Leonard Benedict wa DTB, Beki Bora Frank Mwemezi wa DTB na kinara wa kufunga pointi tatu kwa mtupo mmoja (Leading Three Pointer), Acram Majid aliyefanya hivyo mara 13 katika michuano yote.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi na kufunga mashindano, Mratibu wa BBL 2018/19, Gozbert Boniface, alizipongeza timu sita zilizoshiriki michuano hiyo kwa upande wa mpira wa kikapu na kuzitaka kujiandaa kwa ajili ya msimu ujao, utakaoanza baadaye mwaka huu.

“Tunaipongeza DTB kwa kutwaa taji, lakini pia kwa NMB kwa kutwaa medali za fedha za ushindi wa pili na pia kwa kutoa Mfungaji Bora wa michuano hii, iliyoshirikisha mabenki sita ya NMB, DTB, Azania, CRDB, TADB na NBC,” alisema Boniface wakati akitoa neno la shukrani.

Kwa upende wake, Mgeni Rasmi wa fainali hiyo, Juma Kimori, ambaye ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, aliwapongeza waratibu kwa wazo zuri la kuanzisha michuano hiyo, iliyoimarisha mahusiano baina ya taasisi za kifedha nchini, huku akiwapongeza mabingwa na washindi wa pili wa michuano hiyo.


Mshambuliaji wa NMB, Kaikai Leka, akiwatoka walinzi wa timu ya kikapu ya DTB wakati wa fainali ya Michuano ya Mabeki (BBL 2018/19), dhidi ya timu hizo mbili uliyopigwa Januari 19 kwenye Uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es Salaam. DTB ilishinda pointi 90-73.

HATIMAYE TAMASHA LA PASAKA KUREJEA KWA KISHINDO,KUANZIA JIJINI DAR

$
0
0
Hatimaye tamasha la Pasaka ambalo limekuwa likisindikizwa na kishindo cha muziki wa injili chini ya uratibu wa  kampuni ya Msama Promotions Ltd ya jijini Dar es Salaam, limerejea tena kwa maandalizi makubwa.

Tamasha hilo kongwe ambalo limekuwa likifanyika tangu mwaka 2000, kwa miaka miwili halikuweza kufanyika katika jiji la Dar es Salaam kutokana na sababu maalumu zilizowahi kuelezwa na waratibu wa tukio hilo la kimataifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mbele ya Waandishi wa habari jana Januari 21, 2019, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alisema baada ya tafakuri ya kina pia kwa kuzingatia maoni ya wadau wa muziki wa injili, wameamua kurejesha tukio hilo jijini humo.

“Kama mnavyojua, kwa miaka kama mitatu hivi, tamasha la Pasaka lilikuwa likifanyika mikoani tu, lakini kwa mwaka huu litatafanyika pia katika jiji hilo kwa sababu vilio vya wadau wa muziki wa injili ni vikubwa mno,” alisema Msama."Kutokana na maombi ya Wadau kuw mengi kuhusu tamasha hilo, Wadau kilio chao kimesikika,hivyo tamasha hili litaanzia hapa hapa jijini Dar na kuendelea mikoa mingine ambayo itatajwa hapo baadae"aliongeza Msama

Alisema mbali ya malengo ya msingi ya kueneza ujumbe wa Neno la Mangu na sehemu ya mapato kusaidia makundi maalumu, safari hii tamasha hilo litatumika pia kuhimiza hali ya amani chini ya kaulimbiu isemayo ‘Upendo, haki na Amani ndio msingi wa amani.’

Msama alisema, kwa kuzingatia uhalisia huo tamasha hilo litabeba agenda ya kuombea amani taifa na kumwombea Rais John Magufuli aweze kuongoza kwa ufanisi na mafanikio zaidi kwa maslahi ya watanzania wote.

Kwa upande wa maandalizi, Msama alisema tofauti na miaka mingi, safari hii wamejiandaa kuhakikisha linakuwa la kimataifa zaidi ikiwemo kuwaleta waimbaji mahiri wa kutoka nje watakaoshirikiana na wengine wa Tanzania.

Mbali ya Dar es Salaam, Msama alisema tamasha hilo litafanyika pia katika mikoa mingine 10 ambayo itajulikana baadaye kwa kuzingatia vigezo stahiki vilivyowekwa na kamati ya maandalizi.

Chini ya maudhui ya msingi ya Tamasha hilo, ni kueneza ujumbe wa Neno la Mungu kupitia waimbaji, kukuza muziki wa injili ili kutoa ajira kwa vijana wenye vipaji vya kuimba na kumiliki jukwaa na wauzaji wa kazi za kimuziki.

Tangu kuanza kwa tamasha hilo, waratibu wamekuwa walitumia sehemu ya mapato ya viingilio kuyafariji makundi maalumu katika jamii; walemavu, yatima pamoja na wajane.

Tukio hilo ndilo limechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa injili nchini kutokana na waratuibu kuwaleta waimbaji mbalimbali wa kimataifa kama Solly Mahlangu, Sipho Makabane na Rabeca Malope wa Afrika Kusini. 

Wasanii wengi wamekuwa wakishiriki katika tamasha hilo wakiwepo wa Tanzania kama Upendo Nkone, Christopher Mahangila, Rose Mhando, Sifael Mwakabuka , Matha Mwaipaja, Beatrice Mwaipaja, Joshua Mlelwa pamoja na kwaya mbalimbali, huku katika mataifa kama ya Kenya wasanii wa Injili kama Solomon Mukubwa,Kutoka Afrika kusini kama vile  Solly Mahlangu, Sipho Makabane na Rabeca Malope na wengine wengi.
 Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama akizungumza jijini Dar es Salaam mbele ya Waandishi wa habari jana Januari 21, 2019,kuhusu ujio upya na maandalizi ya tamasha la Pasaka 2019,linatarajiwa kuanza kufanyika jijini Dar.Msama amesema kuwa kwa miaka kama mitatu hivi, tamasha la Pasaka lilikuwa likifanyika mikoani tu, lakini kwa mwaka huu litaanzia jijini Dar  kwa sababu vilio vya wadau wa muziki wa injili ni vikubwa mno



 Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alipokuwa akifafanua zaidi kuhusu ujio mpya na maandalizi makubwa ya tamasha la Pasaka 2019,ambalo linatarajiwa kuanza kufanyika jijini Dar.

Gerezani Bridge gets Japanese Contractor

$
0
0

                                                    January 21st, 2019: Contract agreement for the construction of a new road bridge along Bandari Road of Gerezani is scheduled to be signed between Tanzania National Roads Agency (TANROADS) and Sumitomo Mitsui Construction Company (SMCC) on 22nd January, 2019 (Tue). 

The project is funded by the Government of Japan through Japan International Cooperation Agency (JICA) as a Japanese Grant.

The project will replace the existing 2-lane bridge by a new 4-lane bridge in response to increasing traffic volume together with a rapid economic growth of the United Republic of Tanzania. In addition, its well-considered design can accommodate a new service route of Bus Rapid Transit (BRT), and Standard Gauge Railway passing under the bridge.


SMCC is a Japanese contractor which successfully completed the first flyover project in Tanzania (Mfugale Flyover) in September last year. Mfugale Flyover demonstrates Japanese quality infrastructure by its well finished concrete structure. 

Moreover, SMCC achieved a safety record that is more than 2.5 million man/hour safety record (no minor/fatal injuries for both pedestrian, motorist and workers of the project was recorded during its 35-month construction period) and completion ahead of the original schedule.


Moreover in response to increasing demand, the city of Dar es Salaam is remarkably developing.  Since the port of Dar es Salaam is under rehabilitation and improvement of its facilities, it is essential to widen the bridge located on the route connecting the port of Dar es Salaam to up-country areas and neighboring countries through the Central Corridor. 

JICA continues to support comprehensive development of infrastructure of Dar es Salaam.


Date:

22nd January, 2019

Time:

10:00am -

Venue:

Tanzania Harbor Building (TPA) conference room, Dar es Salaam

Attendance:

·       Minister of Works, Transport and Communication

·       Reginal Commissioner (RC) of Dar es Salaam

·       CEO of TANROARDS

·       Chief Representative of JICA Tanzania office


BABA AMWOKOA MWANAE KULIWA NA MAMBA WILAYANI NAMTUMBO, RUVUMA

$
0
0

NA Yeremias  Ngerangera…Namtumbo.
Mohamedi Mbawala (kasorobo)mkazi wa kijiji  cha Mgombasi wilayani Namtumbo  mkoani Ruvuma amemwokoa mtoto wake  Mashaka mbawala (17)aliyeshikwa na mamba katika mto luegu.
Mashaka Mbawala alishikwa na mamba katika mto luegu wakati wa mchana akiwa na kaka yake Juma Mbawala (21)pamoja na kijana Awadi  simba (18) wakioga  katika mto huo.
Kwa  mujibu wa Juma Mbawala ambaye  ni kaka  ya mashaka alisema walikuwa  shambani pamoja na baba yao wakilima shamba na ilipofika majira ya saa nane mchana  walimwomba baba yao ruhusa kwenda kuoga kupunguza joto na jasho mwilini kutokana  na jua kali lililokuwa linaendelea wakiwa shambani hapo.
Baba yao Mohamedi aliwaruhusu wote watatu waende wakapunguze jasho na joto mwilini na kisha warudi  shambani kuendelea na kulima  kwa kuwa shamba lao hulima mpaka kwenye ukingo wa mto huo.
Watoto hao kwa  pamoja walienda kwenye mto huo na kuanza  kutoa jasho na mara mmoja kati yao akaanza kupiga kelele za kuhitaji msaada na wenzake baada ya kumwona mamba wakaanza nao kupiga kelele na ndipo baba yao alikuja haraka  na panga na alipofika pale alimwona mwanae amechukuliwa  na mamba na ndipo alipojitupa kwenye maji na kumfuata mtoto wake na kuibua ugomvi mkali kati yake na mamba.
Mohamedi Mbawala alidai aliridhika nayeye kupoteza maisha kuliko kumwacha mtoto wake aende huku yeye akimwona alimkata panga mamba mkiani lakini mamba huyo hakumwachia mwanae  badala yake aliacha kumshika kwenye paja la mguu wa kulia akamshika kwenye  goti na alipompiga panga la pili mamba huyo aliachia kwenye goti na kushika mguu maeneo ya vidole na alipompiga panga la tatu mgongoni alikubali kumwachia mwanae huku akiendelea kupambana nae  eneo la mto huo likitapakaa damu tupu.
Baada ya mamba huyo kumwachia mwanae  alimtoa nje ya mto na kumlaza kwenye mchanga  akiwa amezimia kutokana na kunywa maji mengi alipigwa mchanga tomboni ili kuyaondoa maji  na baadae mtoto huyo aliweza kupata ufahamu na ndipo walipomkimbiza Zahanati ya Mgombasi kwa Matibabu ya awali.
Mtendaji wa kata ya Mgombasi bwana Abeid kilosa alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa mtoto huyo amekimbizwa hospitali ya peramiho kutibiwa majeraha aliyopewa na mamba sehemu ya paja la mguu wa kulia ,kwenye goti na sehemu ya vidole katika mguu huo.
Afisa ardhi na maliasili bwana Saimon Sambalu alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuwahatarisha wananchi na vijiji vilivyopo kandokando na mto luegu kujihadhari  kutumia maji ya mto huo kutokana na kutapakaa mamba katika mto huo.
Aidha aliwataka wazazi katika maeneo yanayopita mto huo kutowataka watoto wao kuoga ,kuchota maji katika mto huo wakiwa peke yao kwani kwa sasa mamba katika mto huo wameongezeka hasa nyakati hizi za masika ambapo maji yanakuwa mengi katika mto huo na mamba kusambaa katika maeneo mengi wakisaka chakula alisema Sambalu.
Kijiji cha mgombasi ni miongoni  mwa vijiji vya Luegu,Mtonya na Libango wilayani Namtumbo  vilivyogubikwa na matukio ya mara kwa mara ya watu kuliwa na mamba hasa nyakati za masika .

Introducing "Unanibamba" Official video by Don Masika & Razz Collo

MADIWANI SIMANJIRO WAMFAGILIA RAIS MAGUFULI KWA KUTATUA MIGOGORO MAENEO YA HIFADHI ZA TAIFA

$
0
0
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, limesoma maazimio ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa kutatua migogoro ya maeneo ya hifadhi na vijiji 366 na kurejesha kikokotoo cha awali cha wastaafu. 
 Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi akisoma maazimio hayo, alisema baraza hilo linampongeza kwa dhati Rais Magufuli kutokana na matukio hayo mawili. Myenzi alisema baraza limeona maamuzi hayo ya Rais Magufuli ni kielelezo tosha cha uongozi mahiri, uliotukuka na sikivu kwa wananchi wanyonge ambao ni nguzo muhimu ya ujenzi wa Taifa. Alisema uamuzi wa kurejesha kikokotoo katika utaratibu wa awali, ni kielelezo tosha cha uongozi mahiri na kutatua migogoro ya watumiaji wa ardhi na mipaka ya maeneo ya hifadhi ni ya kupongezwa. 
 "Kwa upendo huu aliouonyesha Mheshimiwa Rais Magufuli, baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro linampongeza kwa dhati na kuomba aendelee na moyo huu wa upendo kwa Taifa lake," alisema Myenzi. 
 Diwani wa kata ya Terrat, Jackson Ole Materi alisema mgogoro wa hifadhi na vijiji 366 ulikuwa unaathiri ustawi wa wananchi hasa jamii za wafugaji, wakulima, wavuvi na watumiaji wa ardhi katika mipaka ya vijiji na maeneo ya hifadhi. 
 Ole Materi alisema kwa uamuzi huo imedhihirika azma ya Rais Magufuli ya kuwajali wanyonge na kuhakikisha jamii yenye utulivu inayotumia muda mwingi kwa uzalishaji badala ya kutatua migogoro. 
 Diwani wa kata ya Loiborsiret, Ezekiel Lesenga (Mardad) alisema wananchi wa eneo hilo nao wanampomgeza Rais Magufuli kwa uamuzi wake kwani nao ni waathirika wa ardhi. Mardad alisema kwenye kijiji cha Kimotorok kuna taasisi mbalimbali ikiwemo shule, zahanati, kanisa na makazi ya watu waliotakiwa kufukuzwa sababu ya kupakana na hifadhi ya jamii ya Mkungunero. 
 Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Albert Msole alisema baraza hilo linaundwa na jamii ya wafugaji na wakulima linampongeza Rais Magufuli na kumtakia maisha marefu na ufanisi kwenye majukumu yake. 
 Msole alisema wilaya ya Simanjiro nayo ni miongoni mwa wanufaika wa matamko hayo mawili kwani watumishi wa serikali wamenufaika na wafugaji pia wamefaidika. Diwani wa kata ya Emboreet, Christopher Kuya alisema Rais Magufuli amejali maslali na matakwa ya wafanyakazi ambao walikuwa waathirika wakubwa pindi wakistaafu. 
 "Uamuzi huu wa Rais Magufuli ni kielelezo tosha cha uongozi wake thabiti na sisi madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro tunampongeza mno," alisema Kuya.
 Diwani wa kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Ezekiel Lesenga Mardad akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kwa kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuwatetea wafugaji hasa kijiji cha Kimotorok kjnachopakana na hifadhi ya jamii ya Mkungunero. 
 Diwani wa kata ya Terrat wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Ole Materi akisoma taarifa ya hoja ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuwatetea wafugaji na watumishi wa serikali.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Yefred Myenzi akisoma maazimio ya Baraza la Madiwani la kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuwatetea wafugaji na watumishi, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Albert Msole. 
 Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara na watumishi wa Halmashauri hiyo wakifuatilia kikao cha Baraza la Madiwani. 
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhe Albert Msole akifunga kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo ambao walimpongeza Rais John Magufuli kwa kuwatetea wafugaji na watumishi wa serikali, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Yefred Myenzi. 

Kitabu Changu Kutafsiriwa kwa kiSomali

$
0
0
Na Profesa Joseph Mbele
Mara moja moja, katika miaka kadhaa iliyopita, nimekuwa nikiwazia kufanya mpango wa kutafsiriwa kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, kwa kiSomali. Niliwazia lugha hiyo kwa kuwafikiria waSomali waishio Marekani. Hapa kuna waSomali wengi kuliko sehemu yoyote duniani ukiachilia mbali Somalia yenyewe. Jimbo hili la Minnesota ninapoishi linaongoza kwa kuwa na waSomali wengi.

Nimekuwa na mahusiano ya miaka mingi na waSomali wa Minnesota, hasa katika miji ya Faribault na Minneapolis. Nimehusika katika kuwashauri kuhusu maisha ya hapa Marekani, mifano ikiwa ni mihadhara yangu Mankato na Faribault.

WaSomali ambao wamesoma kitabu changu wanakipenda sana na wananikumbusha tunapokutana. Mmoja wao ni rafiki yangu Mohamed Dini. Huyu ndiye tumekubaliana akitafsiri kitabu hicho. Yeye ni mmoja wa waSomali wachache sana wanaotambulika katika fani hiyo hapa Minnesota. Kazi hiyo itaanza mwezi huu.

Ni faraja kubwa kwangu kwamba tafsiri hii itakapochapishwa itapunguza kwa kiasi kikubwa matatizo yanayowakabili waSomali Marekani, ambayo ni mara dufu kuliko yanayowakabili waAfrika wengine wengi. Tofauti na waAfrika wengi, waSomali wengi hawajui kiIngereza ambayo ndio lugha ya Marekani. Vile vile, waSomali ni waIslam, dini ambayo ni ya wachache hapa Marekani, na sehemu nyingi hakuna yale ambayo waIslam wanahitaji kwa mujibu wa dini yao. Kuna juhudi zinafanyika, lakini bado hazijatosheleza.

Ninangojea kwa hamu maendeleo ya shughuli hii hadi ifikie lengo.


Tanzania kushiriki Maonesho ya Biashara ya Dunia ya EXPO 2020

$
0
0

Tanzania itashiriki Maonesho ya Dunia ya Biashara (Expo 2020 yatakayofanyika Dubai kuanzia mwezi Oktoba 2020 na kumalizika mwezi April 2021.
Uwekaji saini wa Mkataba wa ushiriki wa Tanzania katika Maonesho hayo ulifanywa tarehe 16 Januari 2019 na Balozi wa Tanzania nchini UAE ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa Tanzania wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk.
Kwa upande wa UAE, mkataba huo uliwekwa saini na Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Najeeb Mohammed Al Ali.
Baada ya uwekaji saini wa Mkataba huo, Mhe. Balozi Mbarouk alieleza kuwa Serikali inayapa umuhimu mkubwa maonesho hayo kwa kuwa ni fursa adhimu ya kuitangaza Tanzania kwenye sekta za uwekezaji, biashara, viwanda, utalii na mila na utamaduni.
Aidha, Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020 alieleza kuwa amefurahishwa na hatua ya Tanzania kusaini Mkataba huo ambapo itatoa fursa kwa nchi kujiandaa mapemana taratibu nyingine za ushiriki.
Baada ya uwekaji saini wa Mkataba huo,` kitakachofuata ni utayarishaji wa simulizi ya maudhui ya maonesho (pitch story) ambayo inatakiwa kuthibitishwa na Kamati ya Kitaifa ya Tanzania ya DUBAI Expo 2020. Simulizi ya maudhui hayo yatahusu vipaumbele vya Tanzania kama vile maendeleo ya viwanda, miundombinu, masuala ya biashara na uwekezaji, utalii, kilimo, elimu, afya, sanaa na utamaduni.  Simulizi ya maudhui pia itatumika katika kusanifu muonekana wa banda la maonesho la Tanzania.

Tanzania inakuwa miongozi mwa nchi washiriki zipatazo 100 ambazo tayari zimesaini Mkataba wa Ushiriki tangu Dubai ilipochaguliwa kuwa mwenyeji wa maonensho hayo.
Wengine walioshuhudia uwekaji saini wa Mkataba huo ni Bw. Ali Jabir Mwadini, Kansela Mkuu, Ubalozi Mdogo wa Tanzania, Dubai; Bi Samira Ahmed Diria, Afisa Ubalozi; na kwa upande wa DUBAI EXPO 2020 ni  Bi Manuela Garcia Pascual, Mkurugenzi wa Washiriki wa Kimataifa na Bi. Esther Omondi, Meneja wa Nchi/Afisa dawati la Tanzania.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
Balozi wa Tanzania nchini UAE ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa Tanzania wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) na Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Najeeb Mohammed Al Ali wakiweka saini Mkataba wa ushiriki wa Tanzania katika Maonesho ya Biashara ya Dunia (Dubai Expo 2020. Uwekaji saini huo ulifanyika Dubai tarehe 16 Januari 2019.  
Balozi wa Tanzania nchini UAE ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa Tanzania wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) na Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Najeeb Mohammed Al Ali wakionesha Mkataba mara baada ya zoezi la kuweka saini kukamilika.
Balozi wa Tanzania nchini UAE ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa Tanzania wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) na Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Najeeb Mohammed Al Ali wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wao.

Balozi wa Tanzania nchini UAE ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa Tanzania wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) na Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Najeeb Mohammed Al Ali wakibadilishana mawazo mara baada ya zoezi la kuweka saini kukamilika.

SERIKALI IMEWEKA MIKAKATI KUBORESHA SEKTA YA MIFUGO - MHE. ULEGA

$
0
0
11
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega,akizungumza na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Singida kabla ya kuanza ziara ya uhamasishaji wa kuogesha ng'ombe katika kijiji cha Mgori.
13
Bw.Rashid Mandoa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Singida akitoa taarifa kwa Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega.
14
Bw.Elia Digha,Mwenyekiti wa halmashauri ya Singida akitoa ujumbe kwa Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega (hayupo pichani)kuhusu kuweka mikakati katika sekta ya mifugo nchini.
10
4
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega akikagua ng'ombe katika kijiji cha Mgori kilichopo Singida vijijini alipokuwa ameenda kuzindua zoezi la uhamasishaji wa kuogesha mifugo.
2
Baadhi ya ng'ombe wakisubiri kuogeshwa dawa katika josho la Mgori katika hamshauri ya wilaya ya Singida vijini ambapo Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega alizindua zoezi la uhamasishaji wa kuogesha mifugo.
12
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega,akichanganya dawa za kudhibiti magonjwa ya mifugo katika kijiji cha Mgori kwa ajili ya kuhamasisha kuogesha ng'ombe katika majosho yalipo nchini ambapo Serikali imeamua kutoa dawa bure kwa wafugaji.
36354
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega akisaidiana na baadhi ya wafugaji kuingiza mifugo katika josho lenye dawa ambazo zimetolewa bure na Serikali zoezi hilo la uzinduzi katika mkoa wa Singida lilifanyika katika kijiji cha Mgori kilichopo halmshauri ya wilaya ya Singida vijijini.Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
........................
Na.Alex Sonna,Singida
Serikali imeandaa mkakati wa kuboresha sekta ya mifugo pamoja na kudhibiti magonjwa ya mifugo huku ikiwahimiza wafugaji kuzingatia matumizi ya majosho yenye dawa.
Akizungumza na wafugaji Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega wakati wa zoezi la uhamasishaji wa uogeshaji wa ngo’mbe kanda ya kati mkoani Singida, katika kijiji cha Mgori kilichopo halmshauri ya wilaya ya Singida vijijini.
Katika uhamasishaji huo waziri Ulega aliwataka wafugaji kufanya zoezi la uogeshaji wa mifugo uliyoanzishwa uwe wenye tija na endelevu, kwa vile hivi sasa hakuna sababu za kushindwa kuogesha mifugo yao katika majosho yenye dawa ya kudhibiditi kupe.
Aidha amesema kuwa kwa sasa serikali katika zoezi hili, imetoa dawa bure kwa halmashauri zote nchini, na kukarabati majosho yote yaliyokuwa hayafanyi kazi, ili wafungaji waweze kuogesha mifugo yao , kukinga ugonjwa hatari unaoenezwa na kupe, ambao unaoongozwa katika vifo vya ng’ombe hapa nchini.
"Mwanzo shughuli hizo zilikuwa zikifanywa kwa ,kutofuata taratibu nzuri za makusanyo yalikuwa yakitoka kwa wafugaji walipokuwa wakipata huduma za kuongesha mifugo yao, hazikuwa na taarifa ya mapato na matumizi na hivyo kushindwa kuwa na utaratibu endelevu wa shughuli hiyo, majosho mengi yalisimama kufanya kazi"amesema Ulega
Katika kampeni hii ya uhamamishaji wa uongeshaji wa mifugo tozo imepunguwa ambapo hivi sasa kila ng’ombe ana ogeshwa katika majosho ni shilingi 50 tu, huko nyuma uogeshaji ulikuwa unatozwa wastani wa shilingi mia 2 kwa kila ngo’mbe na kwa mbuzi ilikuwa shilingi 10.
“Nyie wafugaji msikalie rasialimali hii ya mifugo mliokuwa mnayo, kwani ni uchumi mkubwa sana mliyokuwa nayo kwenu na pia kwa Taifa ili kuongeza mapato, yanayotokana na mifugo yenu”amesisitiza Ulega.
Aidha alifafanua kuwa ufungaji kwa kufuata taratibu za ufugaji wa kisasa na kibiashara kwa kuvuna mifugo inapozidi katika eneo uliyokuwa nayo, itakusaidia kupata kipato katika kuboresha maisha yako na ya familia.
Uhamasishaji huu unafuatia uzinduzi wa kampeni ya uogeshaji wa mifugo,iliyofanywa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina katikati ya mwezi jana katika kijiji cha Buzirayombo halmashauri ya chato.

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: Pierrette Adams - Journal Intime

MTUMISHI WIZARA YA MIFUGO APOTEA, ANATAFUTWA

Wakazi wa Dar es Salaam wanufaika na Promosheni ya Tusua Ada na Omo

$
0
0
Meneja wa Game Supermakert ya Mlimani City, Josephat Okumu (kushoto), akimkabidhi mshindi wa droo ya pili, Grace Mboka mkazi wa Goba jijini Dar es Salaam pesa taslimu Shilingi laki tano(500,000/=) aliyoshinda katika Promosheni ya “Tusua Ada na Omo” inayoendelea.Dro hiyo iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika Supermarket hiyo.Katikati ni Meneja wa Omo, Upendo Mkusa.
Meneja msaidizi wa Coppies Supermaket ya Mlimani City Edger Matilya(kulia), akimkabidhi mshindi wa droo ya pili, Shidu Abubakari mkazi wa Tegeta Dawasco jijini Dar es Salaam pesa taslimu Shilingi laki tano(500,000/=) aliyoshinda katika Promosheni ya “Tusua Ada na Omo” inayoendelea.Dro hiyo iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika Supermarket hiyo.Katikati ni Meneja wa Omo, Upendo Mkusa.


WAKAZI sita wa jiji la Dar es Salaam wafanyao manunuzi katika Supermarket za Game,Choppies Mlimani City na Shoppers Mikocheni,Masaki na Mbezi wamejishindia jumla ya shilingi milioni tatu(3,000 000) ikiwa ni shilingi laki tano(500,000/=) kila mmoja baada ya droo ya pili kufanyika mwishoni mwa wiki. Washindi hao walipatikana mara baada ya kununua Omo na kuingia rasmi kwenye droo kubwa inayochezeshwa katika Supermakert kila jumamosi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Meneja wa Omo, Upendo Mkusa kwanza aliwapongeza washindi wote haswa watatu waliopatikana katika droo ya pili kukamilisha idadi ya washindi sita ambao ni Grace Mboka mkazi wa Goba aliyeshinda katika Supermaket ya Game Mlimani City, Shidu Abubakari alishinda katika Supermaket ya Choppies Mlimani City na Lilian Patrick aliyeshinda katika Supermakert ya Shoppers ambapo aliwaomba pesa walizoshinda wakazielekeze kwenye elimu kwa watoto wao kama kauli mbio ya kampeni inavyo sema “Tusua Ada na Omo”.

Kampuni ya Unilever kupitia bidhaa yake ya Sabuni ya Omo wanatambua kama jamii ya Watanzania imetoka katika kipindi cha Siku kuu ya Chrismass na Mwaka mpya hivyo wakaona ni jambo jema kuungana na wanafamilia katika kipindi hiki cha watoto kwenda shule kuchangia kwa namna moja ama nyingine kupitia promosheni hii.

Alisema Upendo, katika Promosheni hii ya Tusua Ada na Omo jumla ya Shilingi milioni sita (6,000 000/=) zitatolewa kwa washindi 12 ikiwa kila mmoja atajishindia pesa taslimu Shilingi laki tano(500,000/=).

Alisema Upendu ushiriki uko wazi kwa kila mtu lakini lazima uwe na umri zaidi ya miaka 18, ni lazima ununue Omo 1kg moja ziwe pakti mbili au 500gm pakti ziwe nne au 3.5kg pakti moja,ambapo mshiriki utapewa kuponi ya itakayoingizwa kwenye droo itakayochezesha kila jumamosi ya juma hilo.

Mwisho Upendo aliwaomba wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuchangamkia fursa ya pesa hiyo kwani ushiriki na ushindi wake uko wazi. Nikufanya manunuzi ya Omo katika Supermakert ya Game,Choppies au Shoppers Mikocheni, Msaki au Mbezi tayari unaweza kujishindia pesa taslimu Shilingi 500,000/=.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images