Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live

KAMATI YA KIKAO CHA KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA CHAFANA MKOANI DODOMA

$
0
0

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mussa Zungu akiongoza kikao cha kamati hiyo killichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo walipokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhusu utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa kipindi cha Julai mpaka Desemba mwaka 2018.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiwa katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama killichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo wizara yake iliwasilisha taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhusu utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa kipindi cha Julai mpaka Desemba mwaka 2018.pembeni yake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.

J&M VIRGO YASHUSHA MALI MPYA KUELEKEA VALENTINES DAY

$
0
0
 KATIKA KUELEKEA MSIMU WA WAPENDANAO (VALENTINES), DUKA LAKO PENDWA LENYE "VIWALO" VIKALI TOKA MBELE LILILOPO PALE MIKOCHENI KARIBU KABISA NA KIOTA CHA ESCAPE ONE JIJINI DAR ES SALAAM  (J&M VIRGO), LIMESHUSHA MALI MPYA NA UKALI KWELI KWELI KWA KINA MAMA NA KINA BABA PIA.

HIVYO ILI KUTOKA KIPEKEE NA NA MAMSAP AU MZEE BABA FIKA DUKANI KWAO PALE KUJICHUKULIA PAMBA KALI, MOKA ZA KISASA NA MICHUCHUMIO MIKALI KWA KINA DADA PAMOJA NA MIKOBA.

KWA TAARIFA ZAIDI TEMBELEA LIBENEKE LAO






















Malinzi, Mwesigwa waitwa tena Takukuru

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) imeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumchukua aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi na Katibu wake, Selestine Mwesigwa ili kwenda kuwahoji.

Maombi hayo, yamewasilishwa mahakamani hapo leo Januari 16, 2019  na Wakili wa serikali kutoka Takukuru, Leornad Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipofika kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

Kesi hiyo ilipaswa kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa mashtaka lakini wakili Swai ameieleza mahakama kuwa mashahidi waliotarajiwa kufika leo wamepata udhuru, ambapo mmoja anaumwa na mwingine amepangiwa kazi Utumishi.

Aidha Swai ameiomba mahakama hiyo amchukue Malinzi na Mwesigwa kwa ajili ya kuwafanyia mahojiano Takukuru kwa sababu kuna vitu wanataka kuviongezea

Kufuatia hayo, upande wa utetezi wameiomba mahakama ichukulie suala hilo kwa uzito kwa sababu washtakiwa wapo ndani wanateseka.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 21, 2019 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Mbali ya Malinzi na Mwesigwa, washtakiwa wengine ni Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga, Meneja wa ofisi ya TFF, Miriam Zayumba na Karani Frola Lauya.
ambapo wote kwa pamoja wanashtakiwa na mashtaka 28 yakiwemo ya utakatishaji fedha na USD, 375,418.

MKOA WA DODOMA UKO KATIKA NAFASI TANO ZA JUU KATI YA MIKOA INAYOONGOZA KWA UKATILI

$
0
0
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bwa. Sebastian Kitiku amesema karibu nusu ya wanawake mkoani Dodoma wameolewa wakiwa chini ya umri wa miaka 18.

Akifafanua kuhusu hali ya mimba na ndoa za utotoni katika Mkoa wa Dodoma Bw. Kitiku alisema kati ya wanawake 100 waliolewa mkoani Dodoma 51 kati yao waliolewa na umri chini ya miaka 18 na kati ya wazazi 100 mkoani Dodoma wazazi 45 kati yao wamepata mimba za utotoni.

Mkurugenzi huyo alisema hayo mjini Dodoma wakati wa kikao kazi cha kuandaa ujumbe wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kama hatua ya umuhimu ya kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto mkakati unaotekelezwa kwa kipiandi cha miaka mitano.

Aliutaja mkoa huo pia kuwa unakiwango cha juu cha ukeketaji jambo linafanya mkoa huo kuwa katika nafasi za juu katika viwango vya ukatili Nchini kwani takwimu zinaonesha Mkoa uko katika nafasi ya 2 kitaifa kwa kuwa na asilimia 41 ya vitendo vya ukeketaji akitaja Manyara kuwa na kiwango cha juu zaidi kwa ukeketaji ikiongoza kwa asilimia 58.

‘’Sisi wataalamu tunachukulia ukeketaji kama ukatili dhidi ya watoto kwani unakiuka haki ya msingi ya ulinzi watoto kwa kuwa ukatili una madhara kiafya na kisaikolojia kwa binadamu akiwa mtoto na akiwa mtu mzima pia kwani anabaki na makovu moyoni kipindi chote cha maisha yake.”Alisistiza Bw. Kitiku.

Ameitaja Dodoma kuwa iko katika mikoa inayoongoza kitaifa katika suala la ndoa za utotoni ikiongozwa na Katavi  ambayo takwimu zake kwa ndoa za utotoni ni asilimia 45 lakini pia mkoa wa Dodoma una kiwango cha juu cha ukeketaji na mimba za utotoni.

Kazi ya kutengeneza ujumbe kwa ajili ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni pamoja na ukeketaji  inaendelea tayari imefanyika  katika mikoa yenye takwimu za juu katika ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambayo ni mikoa ya Shinyanga, Tabora, Singida na Rukwa na sasa Dodoma na jumbe hizi zikikamilika zitatumika katika kuhakikisha vitendo vya ukatili vinapungua kwa kiwango kikubwa au kwisha kabisa.  
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha watendaji wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Wizara ya Afya kujadili jumbe za kuelimisha jumii kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
 Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha watendaji wa Mkoa pamoja na Wizara ya Afya wanaokaa katika Jiji la Dodoma kujadili jumbe za kuelimisha jumii kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha watendaji wa Mkoa pamoja na Wizara ya Afya wanaokaa katika Jiji la Dodoma kujadili jumbe za kuelimisha jumii kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

TASUBA YATANGAZA NAFASI ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA SANAA

NAIBU WAZIRI NYONGO AAMURU KUKAMATWA WAMILIKI MGODI WA NYAKAVANGALA

$
0
0
Na Asteria Muhozya, Iringa
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ameamuru kukamatwa kwa Wamiliki wa mgodi wa Nyakavangala unaomilikiwa na  Thomas Masuka and Partners  kufuatia wamiliki hao kutofautiana juu ya taarifa  waliyoiwasilisha kwa Naibu Waziri kuhusu namna mgodi huo unavyoendeshwa ikiwemo ulipaji wa kodi na mrabaha wa serikali.
Aidha, Naibu waziri amewataka wamiliki hao kutoa maelezo ya kina kuhusu ni lini watalipa kodi zote wanazodaiwa na serikali baada ya kuonekana kuwa mgodi huo unadaiwa zaidi ya shilingi milioni 128 za mrabaha ambazo imedaiwa kuwa, wapo baadhi ya wamiliki ambao wamekuwa wakikusanya fedha hizo lakini zimekuwa hazilipwi.
Katika ziara yake mkoani humo, Naibu Waziri alisema kuwa pamoja na kujionea shughuli za uchimbaji katika migodi ya dhahabu ya Ulata na Nyakavangala, amebaini ukwepaji mkubwa wa kodi pamoja na mrabaha wa serikali.
Pia, amemtaka Afisa Madini kutoa maelekezo ya kina kuhusu suala zima la ulipwaji wa kodi na mrabaha wa serikali, huku akiagiza zoezi hilo pia limuhusishe Afisa Msimamizi wa madini aliyekuwepo katika kipindi ambacho fedha hizo hazikulipwa.
“Hatutaki ugomvi hapa kwenye migodi. Tunataka mgodi ufanye kazi. Dhahabu ziuzwe mahali panapoonekana. Hapa naona hesabu za viroba tu. Mnunuzi wa dhahabu hapa ni nani”, alihoji Naibu  Waziri.
Wakati akizungumza na wachimbaji katika mkutano wa hadhara, amewataka wachimbaji hao kuchimba kwa kuzingatia usalama  huku akisisitiza suala la kufuata sheria na taratibu  huku akiwataka kutoa taarifa za  uhakika kwa wale wote wanaokikuka sheria ikiwemo watoroshaji wa madini huku akisisitiza  utoaji  taarifa hizo usiwe wa majungu.
Akitolea ufafanuzi suala la fedha za mrabaha, amesema fedha hizo hazipaswi kuelekezwa katika masuala mengine na wamiliki wa migodi ikiwemo kutumiwa katika huduma za jamii badala yake  zinapaswa kulipwa serikalini. 
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwataka wamiliki hao kukaa chini na kukubaliana namna ya kulipa kiasi cha fedha ambacho wanadaiwa na serikali huku akimtaka Afisa kutoka Halmashauri anayehusika na masuala ya usimamizi wa fedha kuhakikisha kwamba fedha ambazo mgodi huo ulipaswa kuzilipa kama mrabaha zinapatikana.
Mgodi huo wa Nyakavangala unamilikiwa na Thomas Masuka kwa ushirikiano na wawekezaji wengine wazawa wapatao 20. Wakati akiagiza kukamatwa kwao, wamiliki 8 kati ya 20 ndiyo walikuwa wamehudhuria kikao kati yake na wamiliki hao.
Naibu Waziri Nyongo alitoa agizo hilo Januari 15 wakat akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani humo.
 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (katikati) akioneshwa jambo na wachimbaji katika mgodi wa Nyakavangala unaomilikiwa na Thomas Masuka and Partners.  Naibu Waziri alifika mgodini hapo kukagua hali ya uchimbaji madini inavyoendelea.
 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, akikagua moja ya mgodi  katika mgodi wa Nyakavangala wakati wa ziara yake mgodini hapo. Wa tatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.
 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akimweleza jambo mmoja wa wachimbaji wakati akikagua mazingira ya uchimbaji madini katika mgodi wa Nyakavangala. Wanaomfuata ni baadhi ya wachimbaji wadogo wanaochimba katika mgodi huo.
 Naibu Waziri wa Madini Stansaus Nyongo akisisitiza jambo wakati wa ziara yake ya kukagua mgodi wa Nyakavangala. Nyuma yake ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.
 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akijaribu kupandisha Kamba zinazotumika kungia na kutoka ndani ya migodi katika moja ya mgodi wa dhahabu, Kavangala.
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimwonesha jambo Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakati wa ziara yake ya kukagua migodi ya Nyakavangala.
 Sehemu ya wachimbaji wadogo wakifuatilia mkutano baina yao na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo. (Hayupo pichani)
 Afisa Madini anayesimamia Mikoa ya Iringa na Njombe Wilfred Machumu akieleza jambo wakati wa kikao baina ya Naibu Waziri  wa Madini Stanslaus Nyongo na wamiliki wa mgodi wa Thomas Masuka and Partners. Kulia ni Naibu Waziri Nyongo. Nayefuatia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akimsikiliza mmoja wa wawekezaji katika eneo la Nyakavangala Kazi Kuboma alipofika  katika eneo lake ili kuona namna anavyoendesha shughuli zake  uchenjuaji madini. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela na Maafisa Madini na Maafisa wa Wilaya.


Watanzania 70 wahitimu Chuo Kikuu cha Galgotias nchini India

$
0
0
Watanzania zaidi ya 70 wakiwemo wawili wa shahada ya uzamivu wamehitumu masomo yao katika Chuo Kikuu cha Galgotias nchini Indiakatika fani mbalimbalitarehe 14 Januari 2019.

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika mahafali ya nne ya chuo hicho aliwatunuku vyeti wanafunzi hao na wengine kutoka nchi mbalimbali duniani na kuwasihi  kutumia ujuzi walioupata kuchangia kikamilifu maendeleo ya nchi walizotoka.


‘Ulimwengu unasubiri uongozi mpya na mawazo mapya na kanuni na miiko madhubuti kutoka kwenu. Hivyo, kifanyeni chuo kijivune kupitia kwenu kwa kutoa michango yenye tija katika mataifa na jamii zenu, hususan kwa kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na uadilifu mkubwa katika kutimiza majukumu yenu', Balozi Luvanda alisema.


Balozi Luvanda alisema kuwa wanafunzi hao wanahitimu huku dunia ikishuhudia mapinduzi ya teknolojia mbalimbali zikiwemo za kidigitali, teknolojia ya matumizi ya sarafu za kidigitali (block chain), matumizi ya kiwango kikubwa cha data katika kufanya maamuzi (big data revolution), usalama wa mitandao (cybersecurity) na matumzi ya teknolojia katika kutekeleza kazi ambazo awali zilikuwa zinafanywa na mwanadamu (artificial intelligence). Alielezea matumaini yake kuwa chuo hicho kitakuwa kimewandaa vyema wahitimu hao  kukabiliana na changamoto za mapinduzi ya teknolojia katika kutekeleza majukumu yao.


Mhe. Balozi alihitimisha hotuba yake kwa kuwasihi wahitimu hao kuwa, kutunukiwa vyeti sio mwisho wa kujifunza. Wanatakiwa waendelee kusoma vitabu kwa kuwa kusoma vitabu ni sawa na kuufanyia matengenzo ubungo. ‘Akili ya mwanadamu ni kama bustani, bustani isipomwagiwa maji na kupaliliwa itaota magugu na kufa kabisa.   Mhe. Balozi alimaliza.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dodoma.

16 Januari 2019


Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu Galgotias kutunukuu vyeti kwa wahitimu wa chuo.
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akitoa heshima katika picha ya Mahatma Gandhi kwa kuweka shada la maua.
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akitoa hotuba katika mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Galgotias

Umati wa wahitimu wa chuo kikuu cha Galgotias
wakisikiliza kwa makini hotuba ya Balozi Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda.
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akipokea memento kutoka kwa mwanzilishi na mkuu wa chuo kikuu cha  Galgotias, Bw. Suneel Galgotia.






RPC WANKYO AWAKOMALIA TRAFIK WAOMBA RUSHWA PWANI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 
ASKARI wa usalama barabarani mkoa wa Pwani, wametakiwa kufanya kazi zao kwa weledi na kuacha kuomba na kupokea rushwa. Hayo yalisemwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Kamishina msaidizi Mwandamizi Wankyo Nyigesa ,wakati akizungumza na askari wa kikosi cha barabarani mkoa wa Pwani katika ukumbi wa Polisi Maisha plus Kibaha.

Alieleza yamekuwepo malalamiko kwa baadhi ya askari wa usalama barabarani kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa jambo ambalo limekuwa likichafua taswira ya Jeshi la Polisi.

"Katika kipindi cha uongozi wangu nitakuwa mkali na sitosita kuchukua hatua kwa askari yoyote atakayebainika kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa madereva"alisisitiza.


Aidha Wankyo,  aliwataka askari hao kuzingatia utoaji wa huduma bora kwa wateja wanaowahudumia kila siku na kuacha vitendo malumbano na majibu yasiyozingatia utu kwa wale wanaowahudumia katika barabara zetu.


Pia, aliwaasa ,madereva wanaoingia ndani ya mkoa wa Pwani kuzingatia sheria za usalama barabarani na wale watakaokaidi kutii sheria hizo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WATATU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mhe. Cho Tae-ick .Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 16, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mhe. Cho Tae-ick mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mhe. Cho Tae-ick mara baada ya kupokea Hati zake za Utambuliso Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mhe. Cho Tae-ick mara baada ya kupokea Hati zake za Utambuliso Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Malawi hapa nchini Mhe. Glad Chembe Munthali Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Malawi hapa nchini Mhe. Glad Chembe Munthali  mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Malawi hapa nchini Mhe. Glad Chembe Munthali  mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Balozi mteule wa Shirikisho la Jamhuri ya Brazil hapa nchini Mhe. Antonio Augusto Martin Cesar kabla  ya kupokea Hati zake za utambulisho Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Shirikisho la Jamhuri ya Brazil hapa nchini Mhe. Antonio Augusto Martin Cesar. Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Brazil hapa nchini Mhe. Antonio Augusto Martin Cesar mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho. Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Brazil hapa nchini Mhe. Antonio Augusto Martin Cesar mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho. Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019. 
 Balozi Mteule wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mhe. Cho Tae-ick akiandika katika kitabu cha wageni kabla ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 16, 2019.
  Balozi Mteule wa Malawi hapa nchini Mhe. Glad Chembe Munthali  akiandika katika kitabu cha wageni kabla ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.
 Balozi Mteule wa Shirikisho la Jamhuri ya Brazil hapa nchini Mhe. Antonio Augusto Martin Cesar akiandika katika kitabu cha wageni kabla ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 16, 2019.

PICHA NA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU WA NIGERIA OLUSEGUN OBASANJO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


MAWAKALA WA T-PESA KUHUDUMIWA NA TPB NCHI NZIMA

$
0
0
MAWAKALA wa T PESA sasa watakuwa wakihudumiwa na Benki ya TPB kwa huduma zote za kifedha ikiwemo kununua Floats za T Pesa kutoka katika Matawi yote 76 ya TPB yaliyopo mikoa na wilaya mbalimbali nchini.

Makubaliano hayo kati ya T PESA, kampuni tanzu ya TTCL Corporation na Benki ya TPB yamesainiwa leo jijini Dar es Salaam ambapo Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya TPB, Bw. Sabasaba Moshingi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba wamesaini mikataba ya ushirikiano huo.

Akizungumzia tukio hilo, Bw. Kindamba alisema kupitia makubaliano hayo taasisi zote zitanufaika kila mmoja kwa namna yake huku lengo letu kuu la kutoa huduma bora kwa Wananchi likitimia kwa kiasi kikubwa.

"...Kupitia makubaliano haya, Benki ya TPB itatoa huduma za kifedha kwa Mawakala wa T PESA ambao sasa wataweza kununua Floats za T Pesa kutoka katika Matawi yote 76 ya TPB yaliyopo katika Mikoa na Wilaya za Nchi yetu. Pamoja na fursa hii, Benki ya TPB inaendelea kuhudumiwa na Shirika la TTCL kwa huduma za Data, Simu za mezani, simu za Mkononi na Trust Account.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya TPB, Bw. Sabasaba Moshingi alisema Faida za ushirikiano huu ni nyingi lakini muhimu zaidi ni kuwawezesha Wananchi na hasa Wafanyabiashara wanaotoa huduma za Mawasiliano na Fedha Mtandao kuweza kufanya shughuli zao kwa urahisi na ufanisi mkubwa.

Benki ya TPB tutaendelea kushirikiana na TTCL ambao ni ndugu zetu kihistoria. Tunafanya mambo mengi kwa pamoja na tunafurahia ushirikiano uliopo kati yetu hasa kwa kuwa taasisi hizi mbili za Umma zina lengo kuu moja la kuwahudumia mwananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya TPB, Bw. Sabasaba Moshingi (kulia) wakisaini mkataba wa ushirikiano kibiashara, ambapo sasa Benki ya TPB itawahudumia mawakala wa T PESA tataweza kununua Floats za T Pesa kutoka katika Matawi yote 76 ya TPB yaliyopo katika Mikoa na Wilaya anuai nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya TPB, Bw. Sabasaba Moshingi (kulia) wakibadilishana nakala za mikataba ya ushirikiano kibiashara mara baada ya kusaini leo jijini Dar es Salaam.

MNYALUKOLO SAID MWAMWINDI ALIMUUA RC DR. KLERUU SIKU YA KRISMASI HUKO IRINGA!!!

$
0
0
Leo tarehe 25/12/2018, siku ya Krismasi, ni miaka 47 imepita toka Mnyalukolo, SAID ABDALLAH SIULANGA MWAMWINDI, ammimimie risasi na kumuua aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa, marehemu Dr. WILBERT KLERUU. Mauaji hayo yaliyokea tarehe 25/12/1971 kijijini Mkungugu, Isimani, Iringa.

Dr. WILBERT KLERUU alikuwa ni mzaliwa wa Mwika, Kilimanjaro ambaye alikuwa ni mmoja wa Watanzania wachache wakati huo waliokuwa na shahada ya uzamivu(PHD) ya uchumi wa kijamaa. 

Dr. KLERUU alikuwa ni kipenzi cha Baba wa Taifa, Mwalimu JK NYERERE, kutokana na weledi na utendaji wake usio na mfano. Mwanazuoni mwa mwaka 1971, DR.
.KLERUU alikuwaamehamishiwa mkoani Iringa kutokea Mtwara. 

Dr. KLERUU alikuwa ni kiongozi machachari sana na ilikuwa kawaida kwake na alikuwa hana hiana kuwafokea hadharani watumishi wa umma wazembe. Kwa hakika,  Dr. KLERUU alikuwa mbabe sana. Akiwa Iringa, kuna wakati gari yake ilipigwa "overtake" na gari hilo lililompiga"-overtake" likamziba kwa mbele. Kufumba na kufumbua, Dr. KLERUU alishuka kama komandoo na kwenda kumuwasha vibao dreva wa gari hilo! Dr. KLERUU, mara kwa mara, alipenda kuwafokea watu kwa kuwaambia "Hamnijui Mimi? Kawaulizeni watu wa Mtwara"  na yeye hakuwa mtu wa kukaa ofisini kama viongozi wengi wa wakati huo, bali alijumuika na wananchi na kufanya nao shughuli za maendeleo bega kwa bega ambapo ilikuwa ni kawaida kwake kushika jembe kwa masaa kadhaa bila kula!.

Kipindi hicho kulikuwa na kampeni kubwa ya kuwafanya wananchi walime mashamba ya pamoja na hivyo wakulima waliokuwa na mashamba makubwa walinyang'anywa, kitendo ambacho hakikuwapendeza Wanyalukolo waliokuwa matajiri wenye  mashamba makubwa ya mahindi. 

Dr. KLERUU alihamishiwa Iringa ili akatekeleze mpango huo wa serikali na alipofika tu akatangaza kwamba mashamba yote binafsi yanapaswa kuwa ya ujamaa kufikia Novemba  1971.   



Bw. MWAMWINDI alihamia eneo la  Mkungugu, Isimani mwaka 1954 akitokea Iringa mjini alikokuwa dreva. Alianza kilimo kidogo kidogo hatimaye akawa na mashamba makubwa ya mahindi ya hekari  takriban 160. Akawa analima mashamba yake kwa trekta katika eneo hilo ambalo awali lilikuwa ni pori. Kipindi hicho, hakukuwa na sehemu Tanzania iliyokuwa ikizalisha mahindi mengi kama Isimani.

Jumamosi ya tarehe 24/12/1971, Dr. KLERUU alitembelea mashamba mbalimbali maeneo ya Tarafani, Igulu na Ndolela kuhamasisha kilimo cha pamoja. Kesho yake, Jumapili ya tarehe 25/12/1971, Dr. KLERUU( ambaye hakuwa na  Jumapili wala skukuu) aliendelea na shughuli hizo za kutembelea mashamba ya wakulima.

Muda wa saa 11 jioni, Dr. KLERUU  alifika kwenye shamba la MWAMWINDI  na kumkuta akilima kwa trekta lake. Pamoja nae kulikuwa na mtoto wake(Mohamed) na watu wawili aliowaajiri( Yadi Chaula na Charles Mwamalata), Bw. Joseph Kusava ambaye ni mkwe wake pamoja na wake zake waliokuwa wakishirikiana nae kulima siku hiyo. Dr. KLERUU alifika shambani hapo akiendesha gari lake binafsi aina ya Peugeot 404 rangi ya bluu na ubavuni ikiwa imeandikwa RC-Iringa. Baada ya kushuka alimfuata moja kwa moja MWAMWINDI na kuanza kumuhoji maswali mengi kwanini hataki mashamba yake yawe ya ujamaa. Akamwambia "Unafanya nini hapo?"Shuka shenzi we". MWAMWINDI akamuuliza "kwanini unanitukana?" Dr. KLERUU akamjibu "Funga mdomo wako, n'ge n'ge n'ge nini? Kwanini nawaambia hamsikii? Blood fool". Katika eneo hilo walikuwa wao wawili tu kwani watu wengine walikuwa mbali kidogo. Dr. KLERUU aliyekuwa na kawaida ya kutembea na kifimbo kidogo akakitumia kumchomachoma nacho MWAMWINDI. 

MWAMWINDI akafura sana hivyo akaanza kwenda ndani kupitia eneo la makaburi ya baba yake na ndugu wengine huku Dr. KLERUU akimfuata na alipoyaona makaburi akasema "Tazama unaendelea kujenga nyumba za kudumu". MWAMWINDI akamjibu "Hizi sio nyumba, ni mahali ninapozika ndugu zangu".  Dr. KLERUU akajibu "Ni mahali unapozikia mirija wenzio, mbwa we!".

Mnyalukolo MWAMWINDI akawaamehamaki sana. Akasema "Swela", akaingia ndani akachukua gobore akatoka nalo nje na kumfyatulia risasi Dr. KLERUU ambaye alianguka na kufariki hapohapo!!! MWAMWINDI aliuchukua mwili wake akauweka kwenye buti ya gari ya Mkuu huyo wa Mkoa, akachukua na kofia ya Pama ya Mkuu wa Mkoa akaivaa yeye na kuanza safari ya kilometa 40 kwenda Iringa mjini.

Mjini Iringa, watu walishangaa kuona gari ya Mkuu wa mkoa inapita upande wa kulia kwa vile mtaa wa Jamatini ulikuwa ni "One way" lakini wakahisi huenda Mkuu wa mkoa ana dharura. Saa 1 jioni, MWAMWINDI akafika kituo kikuu cha polisi akaenda moja kwa moja kaunta akamkuta PC MBETA KASONDA na kukwambia  "Ebu nenda kwenye buti ukaitoe mbwa yenu nimeishaiua" na kumkabidhi bunduki pamoja na funguo za gari. PC KASONDA hakuamini macho yake alipouona mwili wa Dr. KLERUU ukiwa umetapakaa damu. Dr. KLERUU alikuwa amevaa ovaroli nyeusi na miwani. Hivyo,  mara moja PC KASONDA akamuweka MWAMWINDI chini ya ulinzi. Mtu mwingine aliyekuwepo kituoni hapo ni mzee DAVID BUTITINI(ambaye alikuwa askari polisi na baadaye kada wa CCM Iringa). Tarumbeta likapulizwa na askari wakakusanyika na kupewa rasmi taarifa ya kifo hicho cha Mkuu wao wa mkoa na gari lake likahifadhiwa nyuma ya kituo cha polisi. Askari wanne wakaenda kuleta kitanda cha magurudumu toka hospitali na hatimaye mwili wa Dr. KLERUU ukapelekwa "mortuary". Kesho yake, siku ya jumatatu, mji mzima wa Iringa uligubikwa na simanzi kubwa.

Kuna kundi la watu ambao walikuwa wakimchukia sana Dr. KLERUU kutokana na aina ya uongozi wake hivyo lilipopata tu taarifa za kifo chake wakanunua makreti ya bia usiku huohuo na kuanza kunywa kwa kushangilia hadharani!  Msako ulipoanza  usiku huohuo, jamaa hao walikuwa wa kwanza kukamatwa!.    

Mzee BUTININI ambaye pia alikuwa Mtwara wakati DR. KLERUU alipokuwa Mkuu wa Mkoa, anakiri kuwa ni kweli DR. KLERUU alikuwa mtu wa shoka- "Ni kweli hata kule Mtwara alionekana mtemi sana mwenye kuhimiza mambo kwa nguvu. Lakini lazma muelewe maeneo ya Mtwara yalikuwa ya vita na tulikuwa tukiwasaidia ndugu zetu wa Frelimo hivyo kule kulihitaji mtu kama DR. KLERUU. Mtwara DR. KLERUU hakukumbana na upinzani ila Iringa hali ilikuwa tofauti. Kwa mawazo yangu, Dr. KLERUU alipaswa kwanza kujifunza juu ya mila na desturi za watu wa Iringa. Maana watu wa Iringa ni watu wa Iringa tu."   
Mauaji hayo ya Dr. KLERUU yalimsikitisha sana Mwalimu NYERERE, wakuu wa mikoa na wananchi mbalimbambali. Lilikuwa ni tukio lililoongelewa nchi nzima. Majirani na wazee wengi waliokuwa wakilima pamoja na MWAMWINDI walisombwa na vyombo cha usalama na kumwekea ndani kuisaidia polisi ambapo walikuwa wakikamatwa na kusafirishwa usiku kwa ndege za jeshi. Takribani watu 30 walikamatwa wakiwemo wazee maarufu kama IBRAHIM KHALILI, PESAMBIL, MURSALI na wengineo na kupelekwa sehemu mbalimbali za nchi mf Shinyanga, Mwanza na Zanzibar. Cha kusikitisha ni kwamba ndugu zao hawakujua wamepelekwa wapi! Aidha,  nyumbani kwa MWAMWINDI huko Mkungugu kukawa kunalindwa na askari wa FFU muda wote.

Kitendo cha kukamatwa majirani na marafiki wa MWAMWINDI kilileta uhasama mkubwa baina ya ndugu wa majirani hao na familia ya MWAMWINDI.

Ikabidi mwanae (AMANI MWAMWINDI)(21) alazimike kutafuta kibali cha  DC Iringa kwenda gereza la Dodoma alikokuwa anashikiliwa MWAMWINDI. Alipoganikiwa kukipata alikwenda na akamueleza hali hiyo ambayo ilimsukitisha sana Mzee MWAMWINDI. AMANI akamshauri baba yake aandike barua kwa Rais NYERERE, nae akafanya hivyo siku hiyohiyo. Katika barua hiyo, MWAMWINDI alimueleza Mwalimu kwamba yeye  ndiye aliyemuua Dr. KLERUU hivyo wengine hawahusiki hivyo waachiwe. Baada ya kupita siku kadhaa,  wazee hao majirani wakaachiwa na kurejea kijijini hapo, Isimani. Hata hivyo, tafrani hiyo iliyokuwaimewakumba ikafanya wengi wahame eneo hilo kwani waliishaona "togwa limeingia nzi"!.
Upelelezi wa mauaji hayo ulienda haraka na MWAMWINDI akafunguliwa kesi ya mauaji ya kukusudia Mahakama kuu. Kesi ilipoanza kusikilizwa, ilivuta hisia za watu wengi na umati wa watu uliokuwa ukitamalaki kila siku mahakamani ulikuwa "si wa nchi hii!. 

Tarehe 2/10/1972, baada ya mashahidi wa pande zote kutoa ushahidi wao akiwemo RPC wa Iringa (Abubakar Hassan) aliyetoa ushahidi upande wa   MWAMWINDI kwamba hakuwa na taarifa kwamba Mkuu huyo wa Mkoa angetembelea eneo hilo ndio maana hakumpa "Police escort",  Jaji GABRIEL CHIKE ONYIUKE toka Nigeria(aliyehudumu Tanzania toka 1970-1973) alimtia MWAMWINDI hatiani na kumuhukumu kunyongwa hadi afe. Hii ilikuwa ni baada ya kuukataa utetezi wake kwamba alitenda kosa hilo baada ya kurukwa na akili na pia alikasirishwa "provoked" na marehemu, Mh. Jaji aliona kwamba ingawa ni kweli MNYALUKOLO wa kawaida huwa si mtu wa mchezo-mchezo anapodhihakiwa hasa mbele za wake zake lakini  kitendo cha MWAMWINDI cha kwenda ndani kufuata bunduki kilionesha, pasina shaka, kwamba aliua kwa kudhamiria.    

Adhabu hiyo ya kifo ilitekelezwa mara moja kwani Mwalimu NYERERE alisaini hati ya kifo cha MWAMWINDI
. Hayo hiyo, ilikuwa ni moja ya hati tatu za vifo zilizosainiwa na Mwalimu NYERERE kuidhinisha kunyongwa kwa binadamu katika uongozi wake wa miaka 24 katika taifa hili.  

Kesi hii ilikuwa ya aina yake na haikuchukua hata mwaka mmoja toka tukio kutokea na adhabu kutolewa   tofauti na kesi nyingine za mauaji ambazo, kwa kawaida, huchukua miaka mingi kabla ya hukumu kutolewa. Kesi hii ilichukua miezi kumi tu.

Baada ya msiba, familia ya DR. KLERUU ilirudi Kilimanjaro. Hata hivyo, Mwalimu NYERERE na KARUME na baadae ABDU JUMBE walikuwa karibu sana na mjane wa DR. KLERUU na wakawasomesha wanawe nchini Urusi na Bulgaria.  Aidha, viongozi wengine waliwatia moyo na kuwafariji sana mf.  Marehemu Mzee RASHID KAWAWA na mama GETRUDE MONGELA. Dr. KLERUU aliacha watoto wanne ambao ni Eva, Andrew, Carmen na Edwin.

Mwezi Machi 2014, familia ya DR. KLERUU na ya MWAMWINDI zilikutana kwa furaha ili kusameheana kwa tukio hilo. Bi. EVA KLERUU(60) ambaye ni mtoto mkubwa wa Dr. KLERUU na Bw. AMAN MWAMWINDI(67) (aliyekuwa Meya wa mji wa Iringa) walifanya jambo hilo la kihistoria na hivyo kuyaishi kivitendo maandiko ya vitabu vitakatifu yatutakayo wanadamu kusameheana. Picha hii chini inawaonesha wawili hao wakiwa na bashasha baada ya tendo hilo la kihistoria na lisilo la kawaida. 

Mnara wa DR. KLERUU umejengwa kwenye "mji" wa MWAMWINDI mahali ambapo alipigwa risasi . Nyumba ya Mkuu wa Mkoa  DR. KLERUU bado ipo. Picha hizi hapa chini zinamuonesha Mnyalukolo MWAMWINDI baada ya kujisalimisha polisi pamoja na nyumba ya DR. KLERUU.

REST IN PEACE:

1. Dr. W. KLERUU
2. S. A. MWAMWINDI

WANACCM DAR WAUCHAMBUA MUSWADA WA SHERIA MPYA YA VYAMA VYA SIASA NCHINI

$
0
0
*Polepole afafanua kwa kina ubora na umuhimu wa sheria mpya,agusia wanaosema Msajili kapewa madaraka makubwa

*Mwenyekiti UVCCM ataka vijana kutoa maoni kuhusu muswada huo, wengine wazungumzia vikosi vya ulinzi

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WANACHAMA,makada na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) akiwamo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Humphrey Polepole ameuchambua na kutoa maoni yake kuhusu mchakato wa muswada wa sheria mpya ya vyama vya siasa.

Kwa upande wake Polepole amesema sheria mpya iwapo itapitishwa baada ya watanzania wakiwamo wadau wa vyama viasa kuujadili ni wazi itakuwa na tija kwani kwa sasa kuna mambo mengi ambayo hayaendi sawa na Msajili wa Vyama vya Siasa anakosa nguvu ya kisheria kuchukua hatua.

Akizungumza leo Januari 16 jijini Dar es Salaam Polepole amesema kuna faida nyingi ambazo zitapatikana kwenye sheria mpya ya vyama vya siasa na kwamba sheria mpya itavifanya vyama vya siasa kutekeleza majukumu yake kwa ajili ya watu na sio kukifanya chama cha siasa kuwa mali ya mtu binafsi.

"Tunataka vyama vya siasa ambavyo vitakuwa taasisi kwa ajili ya watu na si kuwa na vyama kwa ajili ya watu.Umma wa watanzania jicho lao katika kuvitazama vyama vya siasa ni Msajili wa Vyama vya Siasa kwani ndio mlezi wao na hivyo sheria mpya itampa uhalali wa kisheria kusimamia vyama hivyo.

" Kwetu CCM tunaunga mkono kipengele hicho kwani lazima Msajili wa Vyama vya Siasa ambayo ni taasisi lakini vyama vingine havitaki na wanatoa upotoshaji mkubwa eti oooo msajili sasa atakuwa kama Mungu mtu iwapo muswada huo utapita na kuwa sheria,"amesema Polepole.

Amefafanua katika sheria ya sasa kuna mambo ambayo yapo lakini hayampi nafasi Msajili wa vyama vya siasa kuchukua hatua.Kwa mfano Msajili kwa sasa anayo nafasi tu ya kukifuta chama cha siasa lakini hana nafasi nyingine,wakati kuna uwezekano angeweza kuwa na uwezo wa kuangalia kosa na kutoa adhabu inayofaa.

"Hivyo wameona ni vema kukatengenezwa sheria ambayo itafanya vyama kuwa bora zaidi na hiyo italeta manufaa kwa umma.Tunataka kuona Msajili anakuwa na nguvu ya kisheria pale chama.kinapokosea hata kwenye matumizi ya fedha za ruzuku awe na uwezo wa kuchukua hatua.

" Kwa CCM inajitajidi kusimamia mambo yake, na ndani ya Chama chetu ukienda kinyume na utaratibu utachukuliwa hatua.Hata kwenye za ruzuku na fedha za Chama tuko sahihi na ukila fedha za CCM utapata tabu sana,"amesema Polepole.

Amefafanua katika baadhi ya vyama vingine hakuna utaratibu mzuri wa kutunza fedha zake,hivyo inahitajika sheria ambayo itakuwa na jicho la upole lakini wakati huo huo kuwe na kali kwa mambo ya hovyo.

Amesema sheria hiyo ni nzuri na sio mbaya kama wanavyosema baadhi ya watu na kwba ametaka ifahamike kuwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ni taasisi na si mtu."Sheria ya sasa inatamka Msajili wa vyama vya siasa atasimamia vyama vya siasa bila kusema anasimamia mambo gani na ndio maana kwetu tunaona umuhimu wa kisheria ambao yale ambayo anayasimamia yawepo kisheria kwa kuandikwa,"

Kuhusu baadhi ya majukumu ambayo Msajili atatakiwa kuzisimamia ni Msajili atahusika kusajili vyama, atasimamia shughuli za uchaguzi ndani ya vyama na hilo ni jambo nzuri kwani kuna vyama ambayo havizingatii uchaguzi.

Polepole amesema kuna vyama Mwenyekiti wa Chama ndio mwenye kuamua nani awe Viti Maalum na asipoongea vizuri na Mwenyekiti basi viti maalum atasikia kwenye bomba."Kwa CCM tunajitahidi kusimamia chaguzi za ndani kwa kufuata utaratibu.Hivyo kipengele cha Msajili kuwa na nguvu kisheria kufuatilia chaguzi za ndani ni jambo nzuri na tunaunga mkono.
Pia kupitia sheria mpya Msajili anatakiwa kuhakiki fedha za vyama ambazo zinatolewa na Serikali, lakini wengine wanasema huko ni kuingilia haki za chama," amesema.

Ameongeza kuwa kna vyama ambavyo Mwenyekiti anadai amekopesha chama na huu ni mwaka wa 17 anadai tu, watu wanaogopa kuhoji kwani wakihoji wanachukuliwa hatua lakini sasa Msajili ataweza kuhoji matumizi ya fedha za ruzuku ambavyo zinatumika kwa vyama vyote na hilo ni jambo nzuri kwani fedha hizo ni za umma.

Pia amezungumzia kipengele ambacho kinazungumzia utolewaji wa elimu ya uraia kwa vyama vya siasa,na msajili atakuwa msimamizi wa elimu hiyo inayotolewa."Msajili atakuwa na nafasi ya kujua hiyo elimu ambayo inatolewa ni kweli ni ya uraia maana kuna vyama vinahubiri mambo ambayo ukiyaangalia kwa kina hayana nia njema,"

Kuhusu Msajili wa vyama vya siasa kupewa madaraka makubwa katika sheria mpya na anakuwa kama Mungu mtu ,ambapo amejibu sio kweli kwani sheria mpya yote ambayo yatasimamiwa na Msajili yatakuwa kwa mujibu wa sheria.Amefafanua sheria ya sasa ilikuwa inampa nafasi Msajili kufuta vyama vya siasa lakini mchakato wa kumuwezesha kufuta ndio ilikuwa haijafikiwa.

"Kwa sasa Msajili wa Vyama vya Siasa kwenye sheria mpya atakuwa na uwezo wa kutoa onyo,kuelekeza na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria inavyotaka kama ambavyo imeandikwa." Vyama vinakosea lakini Msajili sio kosa basi ni kufuta chama atakuwa na nafasi ya kuonya kwanza na kuchukua hatua mbalimbali kabla ya kuchukua hatua,"amefafanua.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Hery James amesema muswada huo wa sheria ya vyama vya siasa umekuja wakati sahihi na kuomba vijana kutoa maoni yao kwani sheria inayotumika sasa ilipitishwa miaka 10 iliyopita.

Amewataka vijana kutumia akili zao kutoa maoni yao kuhusu muswada na kwamba kwa namna ambavyo yeye ameuchambua kuna faida nyingi lakini kwa kuwa muswada huo umeandikwa na binadamu na ndio maana unajadiliwa ili kuuboresha na baada ya kuwa sheria iwe na tija.

Ametumia nafasi hiyo kuonesha mashaka na kipengele ambacho kinazungumzia kuwa mtu anapotaka kuanzisha Chama cha siasa bas wazazi wake wafuatiliwe uraia wao kama ni wa Tanzania au laa ambapo anaona eneo hilo libaki tu anayetaka kuanzisha chama ndio anayetakiwa kuangaliwa uraia wake.

Wakati huo huo wana-CCM wengine wameupongeza muswada huo kwani umekidhi mahitaji hasa kuhakikisha vyama vya siasa nchini kufanya kazi zake za siasa kwa misingi iliyopo.Hata hivyo kuna baadhi ya maeneo ambayo wametoa maoni yao ambapo baadhi yao wamesema katika eneo la kuondoa kikosi cha usalama cha aina yoyote ni vema kikaangaliwa upya.

Tunasheherekea utajiri wa muziki wa Kiafrika huku tukipambana na rushwa-sauti za busara.

$
0
0
Homa ya Maandalizi ya tamasha la 16 la Sauti za Busara imezidi kupanda, kwani wahudhuriaji kutoka ndani na wale wageni wa kimataifa wanajiandaa kwa ajili ya msimu mwingine wa muziki unaopigwa (live) mubashara kutoka katika kila kona ya bara la Afrika. 

Busara Promotions limethibitisha kuwa mpangilio wa tamasha hilo lililojizolea heshima kubwa miongoni mwa watu upo vizuri kwani lilianza rasmi siku ya Jumanne, Februari 7 na linaendelea. 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Yusuf Mahmoud kauli mbiu ya tamasha la mwaka huu inalenga kupambana na rushwa kwa kuwa wanaamini wasanii wanaweza kutumia sauti zao kukabiliana na tatizo hilo wakati wanasheherekea utajiri na mkusanyiko wa tamaduni mbalimbali za muziki wa Afrika. 

“Katika kuunga mkono wasanii wanaotumia muziki kusimamia amani, umoja, haki za binadamu na uhuru wa kujieleza, ujumbe wenye nguvu ambao unaonekana katika tamasha la mwaka huu ni (“Potezea Rushwa, Sio Dili!),” alisema Mahmoud. 

Aliongeza kuwa, “Rushwa ni janga linalotafuna/ linalomomonyoa maadili ya jamii zetu barani Afrika na nje ya Afrika. Kibaya zaidi imefikia hatua kuwa hata baadhi ya watu wamekuwa wakichukulia ni jambo la kawaida. Hata hivyo, tamasha moja pekee haliwezi kubadili jamii yote kikamilifu, hivyo, tunashirikiana pamoja na washirika wa ndani na wa kimataifa kuendeleza majadiliano/mazungumzo, kubadili mitazamo na kuchochea hatua mbalimbali kwa ajili ya uongozi bora,” anasema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara. 

Baadhi ya wasanii watakaounga mkono jitihada za kusambaza ujumbe wa kukabiliana na rushwa ni pamoja na Faith Mussa (Malawi), Fadhilee Itulya (Kenya), Fid Q (Tanzania), BCUC (Afrika Kusini) na wengineo watakaokuwa wakitumbuiza katika tamasha. “Hatua hizi ndogo ndogo zitasaidia kuweka muongozo mwishoni katika kuleta mabadiliko yale tunayoyakusudia kwa pamoja,” anasema Mahmoud. 

Meneja wa Tamasha la Sauti za Busara, Journey Ramadhan anasisitiza kuwa tamasha hili la Sauti za Busara linaendelea kuzitangaza Tanzania na Zanzibar ulimwenguni kote, kwa kuwa tamasha huvuta waandaaji wengi wa matamasha wa kimataifa, hivyo linatoa fursa kwa wasanii wa muziki wa Afrika Mashariki kusambaza muziki wao na kuifikia hadhira ya kimataifa. 

“Orodha yetu ambayo inaonekana kuwa ni ya kawaida sana lakini yenye utajiri mkubwa wa vipaji, inahusisha upekee wa sauti kutoka Zanzibar na Tanzania, pamoja na makundi yale yanayojiandaa kwa ajili ya kuudhihirishia ulimwengu mkusanyiko wa aina mbalimbali ya miziki ya wazawa hasa,” alisema Ramadhan. 

Tiketi za mwanzo bado zinaendelea kufanya vizuri katika mauzo na waandaaji wanaamini kuwa fedha hizo zitasaidia kugharamia kwa takriban asilimia 30 ya matumizi ya tamasha. Hata hivyo, licha ya kufanikiwa kwake katika miaka iliyopita, tamasha hilo kwa miaka ya hivi karibuni halikuweza kwenda vizuri kutokana na changamoto za ufadhili ambazo zinalifanya tamasha hilo liendelee kufanyika kwa bajeti hafifu/ndogo jambo linalosababisha hatua za uombaji msaada kwa wahisani. 

“Mvuto wa tamasha unaendelea kukua, licha ya vikwazo vya kifedha kuendelea kuliandama. Kumekuwa na msaada mdogo sana kutoka kwa Serikali kuhusiana na Sanaa hii. Sekta binafsi nazo bado hazifanyi masuala ya kuzisaidia jamii zinazowazunguka na ufanyaji harambee umekuwa mgumu kila mwaka. Wakati huo huo, ukilinganisha na matamasha mengine, tumekuwa tukiendelea kujiendesha kwa bajeti finyu huku tukiendelea kuweka kiingilio wanachomudu wazawa, mauzo ya tiketi yanagharamia asilimia 30 ya gharama zote,” anasisitiza 

Mkurugenzi wa Tamasha, Yusuf Mahmoud. Kipaumbele cha Tamasha la Sauti za Busara ni kuendelea kuwa tamasha ambalo Watanzania wanaweza kumudu kuhudhuria kwa gharama nafuu, hivyo kiingilio kwa mzawa ni Sh 10, 000

RPC HANS POPPE: A HERO FROM IRINGA MURDERED BY IDDI AMIN AND HIS HENCHMEN!!!

$
0
0
This is a HEROES week. Early this week, we read articles about two Tanzanian heroes namely; Captain NAZIZ PETER MAPUNDA, a daredevil Tanzanian pilot who, in 1977, clandestinely took off with an East African Airways plane from Nairobi to Dar Es Salaam; and Dr. WILBERT KLERUU, a no nonsense, uncompromising and results-oriented RC who was shot dead by one SAID MWAMWINDI on 25/12/1971 in Iringa. 

Today, it is the turn of another hero ie the former West Lake region (Kagera) Regional Police Commander, Senior Assistant Commissioner of Police, HANS POPE who was murdered by the then President IDDI AMIN of Uganda and his henchmen in September 1972, aged 54.

The late HANS POPPE was captured by AMINI's troops on August 24th, 1971 at Mutukula. He was shot in the right thigh at 11 in the morning on that fateful day during an attempt to reach a receiver to warn of AMINI's invasion of Tanzania after he had seen two AMINI's tanks rambling into the country. "Do not kill me. Do not kill me pleeeeese", HANS POPPE appealed to his captors. The plea was heard by people close to the scene including Col. GB KUSIGA and ABDALLAH KABONGO. However, the plea fell on deaf ears. He was whisked away to an unknown destination.

After thirteen months, HANS POPPE's body was sent by AMIN soldiers to the Mulago's hospital's anatomy department and handed over to Prof. SEG TUMWINI on September 21st, September 1972. Upon observation, the body was found with deep stab wounds all over and bullet holes on the upper part of the left arm and another on the pelvic girdle. It appears that HANS POPPE underwear hell during the thirteen months he was kept captive. Apart from the deep wounds and bullet holes, the body had hundreds of bruises, the later suggesting torture. The two brave Ugandan doctors aforementioned preserved his body secretly for eight years until President AMIN was  overthrown in 1979.


In Uganda, HANS POPPE capture became a political publicity stunt for AMIN who labelled him as a Chinese mercenary due to his complexion. President AMIN humiliated him even after his death, by displaying his body at Kalolo airstrip in Kampala, despite the fact that HANS POPPE was neither Chinese nor Mercenary.


On 23rd May 1979, the body of the late HANS POPPE was handed over to Hon. BEN MKAPA, the then Minister for Foreign Affairs, by his counterpart, Hon. OTEMA ALLIMADI at the old Entebe airport. Hon. ALLIMADI paid tribute to the late HANS POPPE who died defendiñg the co-existence and cooperation between the peoples of the two countries.

Hon. MKAPA , on his part, said briefly that "HANS POPPE died in a battle. He died in defence of his country's freedom, its people and its territorial integrity. He fought against an enemy of the people of Tanzania. So, he is a martyr, for freedom, for unity, for law and for African brotherhood and for African unity...........".

The body of the late HANS POPPE was laid to final rest with full military honours at Makanyagio cemetery in Iringa, in his home town on 26th May 1979.

The funeral, believed to be the biggest ever to be held in the Iringa region, was attended by hundreds of mourners. Almost the entire population of Iringa-joined by mourners from Mbeya, Morogoro, Dar Es Salaam and West Lake Zone turned up to accord a heroic burial. 
The Government was represented by HON. ALLY MCHUMO, the then Deputy Minister, Home Affairs who, in his speech, thanked and congratulated Prof. SET TUMWINI of Makerere and Dr. JAMES MAKUMBI, a Medical Superitendant at Mulago, Kampala who took the risk of preserving and hiding the body of the late HANS POPPE from 1972 to 1979.

The late HANS POPPE was the only son of Mr. HOPPMANN POPPE, a whiteman from Germany while his wife, ANNA MERCAT was a black woman from Iringa.

The late HANS POPPE was survived  by the said widow, sons HARRY, ZACHARIA, MOSES, EDDIE, CEASER, OTTO, ADAM and a daughter, SOPHIE.

Two of his sons namely ZACHARIA and HARRY were arrested by police in connection with an unsuccessful attempt to stage a coup d'etat with a view to overthrowing NYERERE's government in the early 1980s. As there was no credible evidence against HARRY, he was allowed to leave scot-free but ZACHARIA and some other co-accused were convicted and a life sentence was consequently mete out to them.

However, in 1995 just before he left office, President ALLY HASSAN MWINYI, by virtue of article 45 of the Constitution of the United Republic of Tanzania 1977, pardoned them. 

Unfortunately, HARRY passed away in 2012 in Canada where he was living with his family. ZACHARIA is a successful business man based in Iringa and also one of the leaders of Simba Sports Club.

It is now 46 years since HANS POPPE was murdered by AMINI. In my view, he is one of our heroes who deserve to be recognized and posthumously awarded.

RIP EX-RPC HANS POPPE: A HERO FROM IRINGA!!!

WAZIRI MKUU APOKEA LESENI YA USAJILI WA TANZANIA SAFARI CHANNEL

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea leseni ya usajili wa chaneli ya utalii ya Tanzania Safari ambayo itaiwezesha kuoneshwa kwa umma bila ya malipo yoyote (a must-carry channel) na wamiliki wa visimbusi.

Waziri Mkuu amekabidhiwa leseni hiyo leo mchana (Jumatano, 16 Januari, 2019) kwenye kikao alichokiitisha ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma ambako alitaka apewe mrejesho kutoka kwa wajumbe wa Kamati Maalum ya kusimamia uboreshaji wa Chaneli ya Utalii (Tanzania Safari Channel).

Akikabidhi leseni hiyo kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Rioba amesema kukamilika kwa usajili huo kumeiwezesha chaneli hiyo ianze kuonekana kwenye kisimbusi cha AZAM namba 109.

Akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Dkt. Rioba amesema Kamati hiyo iliundwa Desemba 21, mwaka jana na inajumuisha wajumbe kutoka taasisi ambata za maliasili na utalii kutoka Tanzania bara na Zanzibar.

“Baada ya kupata leseni, sasa hivi tunaonekana kwenye kisimbusi cha AZAM chaneli namba 109 na pia kwenye intelsat ambako tutaweza kuonekana kwenye nchi zote barani Afrika, sehemu kubwa ya bara la Ulaya na Uarabuni,” amesema.

Mapema, akichangia hoja kwenye kikao hicho, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali (Mst.) Hamisi Semfuko alisema chaneli hiyo inaweza kunufaika kwa kupata matangazo kutoka kwa wamiliki wa mahoteli, makampuni ya kutoa huduma za utalii na wenye magari ya utalii.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Dkt. Allan Kijazi alisema chaneli ya Tanzania Safari imekuja katika wakati muafaka kwa kuwa itaongeza juhudi za taasisi zao kutangaza vivutio vilivyopo nchini na hivyo kuongeza idadi ya watalii wa ndani na wa nje.

“Uwepo wa chaneli hii utasaidia kuondoa upotoshaji wa makusudi uliokuwa ukifanywa na baadhi ya nchi kuwa vivutio fulani viko kwenye maeneo yao wakati siyo kweli,” alisema.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza  na wajumbe wa Kamati Maalum iliyoundwa na serikali ya kusimamia uboreshaji wa Channel ya Utalii ya  TBC ya Tanzania Safari Channel, Ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma Januari 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Katibu, Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji), Bibi Doroth Mwaluko  (kushoto) wakati alipokabidhiwa Hati ya Usajili wa Channel ya Utalii ya TBC ya  Tanzania Safari Channel  katika kakao cha kuboresha Channel hiyo alichokiitisha, Ofisini kwake jijini Dodoma, Januri 16, 2019. Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC),  William Kallaghe na Watatu kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Ayoub Ryoba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha  Cheti cha Usajili wa Channel ya Utalii ya Shirika la Utangazaji Tanzania  (TBC) ya Tanzania Safari  Channel baada ya kuzungumza na Kamati  Maalum iliyoundwa na Serikali ya Uboreshaji wa  Channel hiyo, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa  jijini Dodoma, Januari 16, 2019.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Ayoub Ryoba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha  Cheti cha Usajili wa Channel ya Utalii ya Shirika la Utangazaji Tanzania  (TBC) ya Tanzania Safari Channel  baada ya kuzungumza na Kamati  Maalum iliyoundwa na Serikali ya Uboreshaji wa  Channel hiyo, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa  jijini Dodoma, Januari 16, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji), Bibi Doroth Mwaluko,  Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazji Tanzania (TBC)  William Kallaghe na  Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Ayoub Ryoba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya  Mamlaka ya Usimazi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali Mstaafu, Hamisi Semfuko baada ya kuzungumza na  Kamati ya Maalum ya Uboreshaji wa   Channel ya  Utalii ya TBC ya Tanzania Safari Channel, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma,  Januari 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DOCUMENTARY KUHUSU MAONESHO YA UTALII WA NDANI - 'UWANDAE EXPRO 2019' YAZINDULIWA DAR

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha wanawake katika fani ya Utalii Tanzania (AWOTTA) Mary Kalikawe (kushoto) akiongea na wandishi wa habari ( hawapo pichani ) jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wa kutangaza Maonyesho ya biashara ya Utalii wa Ndani ya Kwanza nchini yatakayofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa Posta Dar es Salaam, Februari 15 hadi 17 ,2019. ” Kauli mbiu ya maonyesho hayo ni Tambua Ushindi wa Kibishara katika Utalii wa Ndani Tanzania” Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa TTB ,Geofrey Tengeneza na Mwenyekiti wa chama cha wanawake Tanzania katika biashara (Tanzania Women Chamber of Commerce) Jacqueline Maleko. 
Mwenyekiti wa Chama cha wanawake katika fani ya Utalii Tanzania (AWOTTA) Mary Kalikawe (kushoto) Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania ( TTB) ,Geofrey Tengeneza (katikati) na Mwenyekiti wa chama cha wanawake Tanzania katika biashara (Tanzania Women Chamber of Commerce) Jacqueline Maleko, wakiwa wameshikana mikono kuonyesha ushirikiano wao kwa wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wa kutangaza Maonyesho ya biashara ya Utalii wa Ndani ya Kwanza nchini yatakayofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa Posta Dar es Salaam, Februari 15 hadi 17 ,2019.” Kauli mbiu ya maonyesho hayo ni Tambua Ushindi wa Kibishara katika Utalii wa Ndani Tanzania. 

Chama cha Wanawake katika fani ya Utalii Tanzania (AWOTTA) kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na shirika la maendeleo la Ujerumani GIZ, wameandaa documentary ambayo imeziduliwa leo jijini Dar es Salaam. 

Hafla ya uzinduzi wa documentary hiyo ambayo inahusu tukio la maonyesho maonesho ya Utalii wa ndani UWANDAE EXPO 2019 yatakayofanyika mwezi ujao mwezi wa Februari tarehe 15 hadi 17 katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa (National Museum –Posta). ilifanyika katika katika ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii na waandishi wa habari. 

Akizungumza kuhusu maonyesho haya ambayo yanafanyika nchini kwa mara ya kwanza, Mwenyekiti wa AWOTTA, ambayo inaratibu maonyesho hayo, Mary Kalikawe, alisema AWOTTA na washirika wake waamua kutekeleza mpango mkakati wa Bodi ya Utalii wa kuutangaza utalii wa ndani kwa vitendo kupitia UWANDAE EXPO 2019 na kauli mbiu ya maonyesho haya ni “Tambua ushindani wa Kibiashara katika Utalii wa Ndani Tanzania”. 

“Kuzindua kwa documentary hii ikisisitiza mchango wa akina mama “Nani kama mama” kunaenda sambamba na kuzindua matangazo kwa umma wa Tanzania juu ya uwepo wa sekta kubwa ya utalii humu nchini ambayo ni muhimu ikatambuliwa kusudi ihudumiwe na kupewa umuhimu wake. Sekta hii inachochea uwekezaji kwa wingi kama tunavyoona mahoteli, usafirishaji tangu wa ndege hadi wa bodaboda, biashara ya chakula kila pembe ya nchi, burudani na utalii wa aina nyingine nyingi. 

Sambamba na uwekezaji huu, sekta ina uwezo mkubwa wa kutengeneza ajira kwa wakubwa na wadogo pia inabeba uwezo mkubwa wa kutengeneza kipato kwa mtu mmoja mmoja, makundi na kuchangia kipato cha taifa kwa kiasi kikubwa. Kwa sasa utalii wa mbuga za wanyama unachangia asilimia 17 ya pato zima la taifa ambayo ni takribani dola Bilioni 2.1 au shillingi zaidi ya trillion 4.7 kila mwaka”. alisema Kalikawe. 

Maonesho haya yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Mhe. Dr. Hamisi Kigwangala, Waziri wa Maliasili na Utalii siku ya Ijumaa tarehe, 15 Februari 2019. Lengo la Maonyesho haya ni kuanzisha utambuaji wa mapana ya sekta ya Utalii wa ndani na fursa kubwa za uwekezaji na ajira zinazoambatana na kukua kwa sekta hii muhimu. 

Maonyesho yatawaunganisha wafanyabiashara wa bidhaa na huduma katika maeneo mbali mbali yanayosababisaha safari za watanzania. Wafanya biashara hawa na vyombo vinavyowezesha uwekezaji, watatumia jukwaa hili kukuza uhusiano baina ya washiriki na Watembeleaji wa maonesho. Watu elfu tatu wanategemewa kuhudhuria maonyesho. Taarifa ya tovuti https://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/Br/2014_15_SBR.pdf inaonesha takwimu zifuatazo: Kuwa mwaka 2014 jumla ya vitengo rasmi vya chakula vinywaji na malazi wakati huo Tanzania bara vilikuwa 11,136. Kati ya hivi asilimia 51.7 vilikuwa vya chakula na vinywaji wakati asilimia 48.3 vilikuwa ni sehemu za watu kulala. Kwa upande wa sanaa na burudani, jumla ya vitengo rasmi katika utafiti wa mwaka 2014/15 vilikuwa 239 ambayo ni chini ya asilimia 1 ya vitengo vyote vya biashara vilivyotambuliwa mwaka huo. 

Kati ya hivi ubunifu na burudani vilikuwa asilimia 35.6, michezo na starehe vilikuwa asilimia 24.3, michezo ya kubahatisha na kubeti ilikuwa asilimia 23.8 na vitengo vya library, kujisomea, makumbusho na burudani za utamaduni ilikuwa asilimia 16.3 Waandaaji wa maonesho wanapenda kutangaza kuwa kupitia uelewa wa upana wa sekta zilizomo katika utalii wa ndani, takwimu hizo hapo juu zimekwishaanza kubadilika na kupanda na mwamko wa watanzania na watoa huduma katika kuboresha utalii wa ndani utapandisha sana ukuaji wa vitengo hivi vya biashara.

 Ni muhimu mikoa yote itambue umuhimu wa kuvuta wageni wa ndani kwenda kutembea kwa sababu mbali mbali katika mikoa yao. Kuwasili kwa wageni ndio ukuaji wa sekta ya utalii wa ndani. Takwimu hizo hapo juu zitajidhihirisha katika mikoa mbali mbali ikifanya bidii kuvuta wageni wa ndani na kuwapa huduma nzuri kama vile wanataka wageni wasahau kurudi kwao! 

Faida ya kushiriki: -Kuonyesha bidhaa au huduma wanazozalisha au wanazotoa; -Kupata fursa ya kujifunza teknonolija mpya na ujuzi kutoka kwa washirikiwengine; -Kupata fursa ya kushiriki katika kongamano na semina ya bure itakayofanyika sambamba na maonyesho hayo; -Kukutana na Wafanyabiashara, Wawekezaji, washauri wa kibiashara na Wasambazaji wa huduma mbalimbali; -Kupata kutangazwa kwenye utandawazi wa kitaifa na kimataifa kwa njia mbalimbali; -Kupata fursa mbali mbali ambazo ni pamoja na tiketi ya raffle, vocha ya malazi, zawadi za kusafiri n.k. Aidha, ni fursa ya kimkakati ya kuwahamasisha wananchi wa Tanzania kupenda kutumia huduma zinazotolewa na wadau wa sekta ya utalii hapa nchini. Maonyesho haya yanatarajiwa kushirikisha, Wizara, Taasisi, Makampuni pamoja na Wafanyabiashara wa sekta mbalimbali. Kongamano litakuwa juu ya "Biashara, Uwekezaji na Ajira katika Utalii wa Ndani ambalo litatolewa bure (idadi ni watu 250 tu kwa siku moja wataruhusiwa, hivyo jiandikishe mapema kabla nafasi hazijaisha). Kiingilio kwenye maonesho ni bure asubuhi hadi saa 10 jioni. Kisha yanafuata masaa ya burudani ambayo inalipiwa kiasi kidogo.

Benki ya Kilimo, TPB, NMB wakubaliana kuwasaidia wakulima wadogo nchini

$
0
0
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeingia makubaliano na Benki za Biashara za NMB na Benki ya Posta (TPB) lengo likiwakuwasaidia wakulima wadogo wadogo kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo chini ya TADB. Makubaliano hayo yamefikiwa ili kumwezesha na kumwinua mkulima mdogo aweze kumudu kilimo chenye tija, kupunguza umaskini na kufikia malengo ya serkali ya kufikia uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo hayo, Meneja anayesimamia Mfuko, Bw. James Mwakilima alisema Serikali imeshatoa kiasi cha shilingi bilioni 45 kwa mfuko kwaajili ya  kuwakopesha wakulima wadogo  sehemu mbalimbali hapa nchini.

“Katika kutimiza azma yake ya kujenga uchumi wa kati na viwanda, Serikali imeshatoa shilingi bilioni 45 kwa TADB kupitia  mfuko  wake wa dhamana kwa wakulima wadogo ili wakulima waweze kujikita  kwenye kilimo chenye tija.” alisema Bw. Mwakilima

 Bw. Mwakilima alitoa wito kwa wakulima nchini kuitumia vyema fursa hiyo kwa kuwa itakuwa fahari kubwa kwa Benki ya Kilimo kuona wakulima wanainuka kiuchumi na kufikia malengo ya serikali ya uchumi wa kati na viwanda kwa kuwa hakuna viwanda visivyo na malighafi.

“Ni nafasi pekee kwa  wakulima wadogo hapa nchini kuitumia vyema fursa hii kwani Benki ya kilimo ni moja ya madaraja ya kumvusha mkulima kutimiza malengo yake. alisisitiza Bw. Mwakilima.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya Posta (TPB), Bw. Ramadhan Mganga alisema kuwa kupitia Mfuko huo Benki yake imefanikiwa kuwakopesha wakulima wadogo hapa nchini. Bwana Mganga alitumia nafasi hiyo  kutaja mikoa ambayo imenufaika na mikopo kuwa ni pamoja na Simiyu, Iringa na Singida.

Aliongeza kuwa katika kuhakikisha wakulima wananufaika na mikopo hiyo, Benki ya Posta imekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa wakulima wadogo juu ya mazao gani walime na kwa wakati gani ili waweze kuwa na kilimo chenye tija

TADB imejipanga kuhakikisha kuwa inashirikiana na mabenki  ya biashara ili kunifanikisha azma ya serikali ya Awamu ya Tano ya kuleta mageuzimakubwa katika sekta ya kilimo ikiwemo kuwainua wakulima wadogo na kuchagiza maendeleo ya sekta ya viwanda. .

 Kaimu Mkurugenzi  wa Mikopo toka Benki ya Posta  Bw,  Ramadhan Mganga (wapili kulia) akizungumza wakati wa mkutano na wanahabari kuhusu Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo nchni (SCGS). Mkutao ulifanyika Makao Makuu ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Meneja Miradi wa TADB, Bw. James Mwakilima (wapili kushoto), Meneja Masoko na Uhusiano wa TADB, Bw. Said Mkabakuli (kushoto) na kulia ni Meneja Mikopo  wa Benki ya Posta Bw. Mtewele Lucius.
 Meneja Miradi wa TADB, Bw. James Mwakilima (wapili kushoto) akifafanua jambo kuhusu Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo nchini (SCGS) wakati wa mkutano na wanahabari kuhsu Mfuko huo. Kushoto kwake ni  Kaimu Mkurugenzi  wa Mikopo toka Benki ya Posta  Bw,  Ramadhan Mganga. Wengine pichani ni Meneja Masoko na Uhusiano wa TADB, Bw. Said Mkabakuli (kushoto) na  Meneja Mikopo  wa Benki ya Posta Bw. Mtewele Lucius (kulia).
Maafisa kutoka TADB na TPB wakionesha nyaraka kuhusu Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo nchini (SCGS) . SCGS inalenga kuwawezesha wakulima kukopa katika taasisi za fedha za ikiwemo benki za biashara pamoja na kuziwezesha taasisi hizo kuwa na uwezo wa kuwakopesha wakulima nchini.

ACACIA YATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI WA SHULE KAHAMA

$
0
0
Kampuni ya Uchimbaji madini ya dhahabu ya Acacia kupitia migodi yake ya Buzwagi na Bulyanhulu imetoa msaada wa mabati 2347 yenye thamani ya shilingi milioni 70 kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu katika shule za msingi na sekondari kwenye halmashauri za wilaya ya Msalala na Kahama Mji mkoani Shinyanga. 

Mabati hayo yenye geji 28 yamekabidhiwa leo Januari 16,2019 kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha na Meneja Mwendeshaji mgodi wa Buzwagi, Arthur Mgongo akimwakilisha Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu. 

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mgongo alisema Acacia inaunga juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha kila mtoto anapata elimu kama ilivyoainishwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025. 

"Katika muitikio wa ombi la msaada wa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya madarasa na nyumba za walimu,migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu imechangia vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 150,mpaka sasa tumechangia mifuko ya saruji 3200 ambapo halmashauri ya Kahama Mji imepokea mifuko 1600 ya saruji na Msalala mifuko 1600 jumla ina thamani ya shilingi milioni 80",alieleza Mgongo. 

"Kiasi cha ziada ya fedha iliyobaki ambacho ni sh. Milioni 70 kimetumika kununua mabati haya 2347 yaani mabati 1173 kwa Halmashauri ya Kahama Mji na mabati 1174 Msalala",aliongeza Mgongo. Alisema msaada huo utasaidia kuongeza miundo mbinu katika shule ili kukidhi ongezeko la wanafunzi kwani tangu serikali ianze utekelezaji wa mpango wa kutoa elimu bure,uandikishaji wa wanafunzi shuleni umeongezeka na uhitaji wa miundombinu umeongezeka. 

Mgongo alielezea kuwa, kupitia mpango wake wa maendeleo ya jamii, Acacia imeendelea kuboresha upatikanaji wa elimu katika jamii zinazozunguka migodi yake na kuleta mapinduzi ya kijamii na kiuchumi nchini sambamba na ajenda kuu ya viwanda. Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha aliishukuru Acacia kwa kuwa sehemu ya jamii kuchangia sekta ya elimu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Macha alisema wilaya yake ina uhitaji wa madarasa 250 na kubainisha kuwa mabati yaliyotolewa na Acacia yatatumika kwenye ujenzi wa madarasa 50 huku akitaja kipaumbele ni kwenye shule ambazo tayari wazazi wamejenga maboma. Aidha aliwataka wadau kushirikiana na serikali kuchangia kwenye elimu kwani kila mmoja ni sehemu ya jamii hivyo anatakiwa kuchangia badala ya kuiachia serikali pekee. 
Mwendeshaji mgodi wa Buzwagi, Arthur Mgongo akizungumza kwa niaba ya Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu wakati akikabidhi mabati 2347 yaliyotolewa na Acacia kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya Kahama Mji na Msalala leo katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kahama.Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Mgongo akishikana mkono na Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha (kulia) wakati akikabidhi mabati 2347 (pichani nyuma) yaliyotolewa na Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya Kahama Mji na Msalala. Kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji, Abel Shija.
Mgongo akielezea shughuli zinazofanywa na Acacia katika jamii ikiwa ni pamoja na ujenzi wa maktaba mjini Kahama,Nyang'hwale na Tarime lakini pia maboresho na utanuzi wa shule za msingi na sekondari ikiwemo ujenzi wa maabara na mabweni. Acacia pia inadhamini wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu kupitia programu ya CanEducate.
Awali Mkurugenzi wa halmashauri ya Kahama Mji, Anderson Msumba akiangalia mabati matatu kati ya 2347 ambapo 1173 ni kwa ajili ya Kahama Mji yaliyotolewa na migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha akizungumza wakati akipokea mabati yaliyotolewa na Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia kupitia migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha akiishukuru Acacia kwa kuendelea kuwa mdau muhimu wilayani Kahama kwa kuchangia shughuli za maendeleo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kahama Mji, Abel Shija akielezea jinsi Acacia wanavyoshirikiana na halmashauri hiyo kuwaletea maendeleo wananchi.
Katibu wa CCM wilaya ya Kahama Alexandrina Katabi (kwanza kushoto) akizungumza wakati wa makabidhiano ya mabati ambapo alisema mchango wa Acacia ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM. 
Viongozi mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji na Msalala na waandishi wa habari wakiwa katika hafla fupi ya makabidhiano ya mabati. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Hospitali ya Kibong'oto yajizidhatiti katika utoaji tiba ya kifua Kikuu

$
0
0

Na.WAMJW,Siha

Hospitali ya Magonjwa ambukizi Kibong'oto inayotoa huduma ya Kifua Kikuu 'TB' na magonjwa mengine ya kuambukiza hasa UKIMWI imeendelea kutoa huduma bora kutokana na serikali ya awamu ya tano kuwekeza katika ununuzi wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi na tiba.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo Dkt.Riziki Kisonga wakati akizungumza na maofisa habari na uhusiano wa wizara na taasisi walofika hospitalini hapo katika kampeni ya "Tumeboresha Sekta ya Afya" ambayo inaelezea mafanikiao ya miaka mitatu inayofanyika katika sekta hiyo.

Dkt.Kisonga alisema kuwa ununuzi wa vifaa hivyo umeweza kurahisisha utoaji wa huduma katika hospitali hiyo.

Aidha, alisema katika kufanya kazi na jamii ya wachimbaji wadogo wadogo kutoka machimbo ya Tanzanite Mererani,kumekuwepo na idadi kubwa ya wanaougua ugonjwa wa kifua kikuu.

"Ufuatiliaji uliofanywa unaonyesha maambukizi ya TB katika jamii hiyo ni mara kumi na tano(15) zaidi ikilinganishwa na jamii isiyofanya kazi katika machimbo".Alisema Dkt.Kisonga.Alisemaa hospitali yake imeendelea kutoa elimu ya kujikinga na vumbi ambayo ni chanzo kikubwa cha uharibifu wa mapafu hivyo kufanya iwe rahisi kwa jamii ya wachimbaji wadogo wadogo na familia zao kupata maambukizi ya mimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu.

Hata hivyo Serikali imenunua mashine ya zinazorahisisha ugunduzi wa haraka wa vimelea hivyo katika muda wa masaa mawili na mara wanapogundua wanaanza tiba mara moja.Dkt.Kisonga amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo pia wameanzisha kituo cha afya Mirereni ambacho kinatoa huduma za matibabu ya TB.

“Tumenunua mashine za kisasa zenye thamani ya Sh.milioni 201 ambazo zina uwezo wa kubaini kifua kikuu ambacho hakijaanza kuwa na dalili zilizozoelekea na kubaini usugu wa dawa kwa mgonjwa ambaye haponi licha ya kutumia dawa," alisema Dk. Kisonga.Amesema hospitali hiyo kwa sasa ina wagonjwa waliolazwa wagonjwa 123 na kati yao wagonjwa 86 ni wagonjwa wa kifua kikuu sugu

Aidha, kutokana na kuboresha huduma ya matibabu ya TB, serikali imeanzisha huduma za kifua kikuu sugu katika hospitali za serikali kwenye mikoa nchini na hivyo hospitali hiyo kupokea wagonjwa sugu na wanaohitaji uchunguzi zaidi.

Pia alisema wana mpango wa kuanzisha maabara inayotembea ili kufika kwenye jamii kwa ajili ya kutoa elimu na kufanya vipimo.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Dunuani (WHO) watu 246 kati ya watu 100,000 wanaugua TB duniani.
 
Mtaalam wa Mionzi Bw. Faustine Kavishe akiwa kwenye mashine hiyo katika kituo cha kuhudumia wagonjwa yanayotokana na kazi (occupational health service centre). Na wa pili upande wa kulia ni Bw. Emmanuel Darabe akiwa kwenye chumba cha kupima uwezo wa kusikia kwa wagonjwa kutoka katika migodi ya madini . 
 Pichani ni  Mashine za kisasa za Gene expert module 4 na 16 za uchunguzi wa vimelea vya kifua kikuu na usugu wa vimelea kwa dawa za kifua kikuu ambapo pia zinapima viral load kwa wateja wa VVU
 Meneja wa Maabara ya hospitali ya Kibong'oto Bi.Mary Mtui  akielezea jinsi wanavyotoa huduma kutumia mashine moya ambazo zinatumia masaa mawili kutoa majibu
 Kaimu Mkurugenzi wa hospitali ya magonjwa ambukizi Kibong'oto Dkt.Riziki Kisonga akizungumza na maofisa habari wa wizara na taasisi waliofika kwenye hospitali hiyo iliyopo Wilayani siha
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>