Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

Dkt. Ndumbaro awaaga Watanzania wanaokwenda Japan kujifunza masuala ya Uongozi

$
0
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan, Mhe. Shinichi Goto aliyeambatana na washiriki kutoka Tanzania wanao kwenda Nchini Japan kwa ajili ya kupata mafunzo ya Uongozi katika sekta mbalimbali. Mafunzo hayo yatadumu kwa muda wa siku 50.

Aidha, Dkt. Ndumbaro amemshukuru Balozi Goto kwa kuendelea kuiwakilisha vyema nchi ya Japan hapa nchini ambapo aliahidi kuwa Japan itaendelea kuchangia maendeleo katika sekta mbalimbali.
 Dkt. Ndumbaro amewaasa Washiriki wanaokwenda katika mafunzo hayo kuitumia fursa hiyo vyema kwa kujifunza mambo mampya kutoka Taifa hilo.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Caesar Waitara (hayupo pichani) yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  jijini Dar Es Salaam.
Mazungumzo yakiendelea 
Dkt. Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Goto
Dkt. Ndumbaro pamoja na Balozi Goto wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki kutoka Tanzania wanao kwenda nchini Japani.  



CULTURE AND GLOBALISATION WORKSHOP AT LION HOTEL IN DAR ES SALAAM ON FEBRUARY 9

KAMISHNA WA FIU ATOA RAI KWA SEKTA YA BIMA NA MASOKO YA MITAJI JUU YA UTAKASISHAJI FEDHA

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii


Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) imeendesha  warsha kuhusu udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi kwa wadau wa sekta ya bima (insurance sector) na masoko ya mitaji na dhamana(capital markets and securities sector) kwa lengo la kuendelea kuwakumbusha wadau kuhusu umuhimu wa kuendelea kutekeleza wajibu  wao na kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na uhalifu wa kifedha.


    Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili juu ya udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi inayofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu Ndugu Onesmo H. Makombe anasema warsha hii muhimu ni muendelezo wa warsha kuhusu udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi katika sekta ya benki.

 Alieleza kuwa tatizo la utakasishaji wa fedha haramu ni tatizo kubwa ulimwenguni kote na katika jamii kwasababu ya kuwepo kwa vitendo mbalimbali vya uhalifu vinavyowapatia wahalifu pato haramu. Uhalifu huo ni pamoja na ukwepaji kodi, biashara haramu ya dawa za kulevya, biashara haramu ya watu, biashara haramu ya silaha, rushwa, kughushi, ujangili, uharamia, uvunaji haramu wa magogo, uuzaji wa bidhaa bandia, ujambazi na uporaji.
 “pamoja na utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi,  kuendelea kujenga na kuimarisha mifumo ya udhibiti katika taasisi ili kuzuia uwezekano wa sekta za bima na masoko ya mitaji na dhamana kutumika na wahalifu kama vyombo vya kutakasisha fedha haramu na kufadhili vitendo vya ugaidi. Kuendelea kuimarisha mifumo ya udhibiti katika sekta hizi kutasaidia kulinda mfumo wa fedha wa nchi yetu ili usitumiwe na wahalifu na watu wasio waaminifu”.
Aidha, aliainisha madhara ya utakasishaji wa fedha haramu kuwa ni ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiusalama. Madhara hayo pamoja na  uhalifu kuendelea kushamiri kwa uhalifu na wahalifu kujiimarisha; wahalifu kuwa na nguvu kiuchumi; kuhatarisha utawala wa sheria na usalama (threaten peace, stability and rule of law) kwani uhalifu unaposhamiri na makundi ya uhalifu yanapojiimarisha hupata nguvu na kujaribu kudhibiti  kushindana na vyombo vya dola; kuharibu ushindani (ruin competitiveness) wa kibiashara katika uchumi kutokana na wahalifu kuwa na mitaji inayotokana na fedha haramu, wafanyabiashara halali hushindwa kuhimili ushindani; kushusha hadhi ya nchi kimataifa (erosion of country’s integrity) na kusababisha nchi kutonufaika na mfumo wa fedha wa kimataifa.


 Aidha na kushusha imani ya wawekezaji na kusababisha uwekezaji kupungua na wawekezaji wapya kutotaka kuwekeza kutokana na kushamiri kwa uhalifu, wawekezaji huwa na hofu kuwa mitaji na mali zao havitakuwa salama; imani ya washirika wa maendeleo na jumuiya ya kimataifa hupungua na  nchi huathirika kiuchumi;  kushuka kwa hadhi ya taasisi za fedha na mfumo mzima wa fedha; na nchi kushindwa  kufikia malengo ya maendeleo kwani rasilimali huwa mikononi mwa wahalifu wachache badala ya kutumika kutekeleza ajenda pana ya maendeleo ya nchi.
Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu amewaasa na kuwakumbusha washiriki wa warsha hiyo kuendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali kutekeleza wajibu wao wa kisheria   kwa uadilifu na uaminifu ili kuendelea kusaidia katika kubaini wahalifu wanaoweza kutumia mfumo wa fedha wa nchi kutakasisha fedha haramu na kufadhili vitendo vya kigaidi na kuhatarisha usalama wa nchi.  


 Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu Ndugu Onesmo H. Makombe Akitoa neno wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili juu ya udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi inayofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam, 

Kamishna Msaidizi Huduma za Kompyuta kitengo cha kudhibiti fedha haramu(FIU),Gilbert Nyombi akitoa mada juu ya  udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi inayofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, 
Mmoja ya Washiriki wa Warsha hiyo Floransia Mrema akichangia jambo wakati wa Warsha hiyo.
Washiriki wa Warsha hiyo wakimsikiliza kamishna wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili juu ya udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi inayofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, 


Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu Ndugu Onesmo H. Makombe, akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya Bima na Masoko ya Mitaji ya Dhamana, katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT), Jijini Dar es Salaam

VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE ZA MIUNDOMBINU, MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA

$
0
0
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakiwa katika kikao  kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi wakati akiwasilisha mada katika kikao cha Kamati hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi wakati akiwasilisha mada katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Mindombinu katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma, kushoto kwake ni mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Moshi Kakoso.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakiwa katika kikao kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma wakimsikiliza Mwanasheria wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi wakati akiwasilisha mada katika kikao cha Kamati hiyo.
Mwanasheria wa Bunge, Ndugu Thomas Shawa akiwapitisha wajumbe wa Kamati ya Miundombinu katika Muswada Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wa mwaka 2018 unaotarajiwa kuwasilishwa na Serikali katika Kamati hiyo Januari 16, 2018. Wa kwanza ni mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Moshi Kakoso.Kikao hicho cha Kamati kimefanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Mussa Zungu akiongoza kikao cha kamati hiyo killichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo walipokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhusu utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa kipindi cha Julai mpaka Desemba mwaka 2018. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola akiwa katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama killichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo wizara yake iliwasilisha taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhusu utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa kipindi cha Julai mpaka Desemba mwaka 2018.pembeni yake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.

KAULI YA MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF KUHUSU UCHAGUZI WA YANGA

$
0
0
Ndugu Wana-habari, Ijumaa iliyopita niliwatangazia kusogezwa mbele kwa muda uchaguzi mdogo wa klabu ya Yanga kufuatia taarifa za wimbi la (tulioamini kuwa wana-Yanga) kufungua kesi sehemu mbalimbali nchini kuzuia uchaguzi huo usifanyike na kwamba baadhi ya Mahakama zilishatoa amri hiyo.  


Kwa kuheshimu mamlaka ya ki-Katiba ya Mahakama nchini na kwamba nchi yetu inaheshimu na kufuata utawala wa sheria, Kamati yangu ya Uchaguzi haikuwa na njia nyingine ya kufanya bali kuusogeza mbele kwa muda uchaguzi wa Klabu ya Yanga uliopangwa ufanyike siku mbili baadaye, yaani Jumapili ya tarehe 13/01/2018.  

Kwa upande wa pili, Kamati ilijikuta na deni kubwa kwa wana-Yanga, deni la kuelezea kilichojiri, kuelezea msingi wa kesi hizo mahakamani zilizosababisha kusogezwa mbele kwa muda uchaguzi katika klabu yao. 

Hivyo kuanzia Ijumaa jioni, yaani mara tu baada ya kutangaza kusogezwa mbele kwa muda kwa uchaguzi huo, Kamati ilitumia njia mbalimbali kuwafikia wale wote waliofungua kesi ili kujua msingi wa malalamiko yao na uhalali wao kusimama mahakamani dhidi ya Klabu hiyo ya Yanga kwa mujibu wa Katiba ya Yanga.  

Tumejiridhisha kuwa malalamiko yote yamejikita kwenye maeneo makuu matatu: (i) mosi, uhalali wa wanachama wenye kadi za zamani, kadi za CRDB na kadi za Benki ya Posta kupiga kura; (ii) pili, kukataliwa majina ya wanachama katika baadhi ya matawi ya Yanga kuingizwa kwenye rejista ya wanachama wa Yanga; na (iii) tatu, sintofahamu ya nafasi ya Mwenyekiti wa Yanga hivyo kusababisha baadhi ya wanachama wenye sifa za uongozi, kuwa na mashaka kujitokeza.  

Kamati ya Uchaguzi, mbali na kuchambua sifa ya uanachama ya walalamikaji hao (ambapo Kamati imebaini kuwa walalamikaji wote kasoro mmoja, si wanachama hai wa Yanga), imepitia malalamiko yote hayo kwa kina na kuwapelekea ujumbe ufuatao walalamikaji wote kwamba: 
(i)  uanachama wao Yanga una hitilafu ki-Katiba, hivyo hawakuwa na sifa (locus) kupeleka malamamiko yao popote pale kwa kivuli cha uanachama wa klabu hiyo; 
(ii) Katiba za Yanga, TFF, CAF na FIFA haziruhusu wanachama wao kupeleka malalamiko mahakamani, hivyo utaratibu huo hauna tija mbali na kuiondolea klabu sifa ya kuheshimu taratibu (compliance); 
(iii) malalamiko yao yote waliyoainisha yanatatulika kwa taratibu zilizopo ndani ya shirikisho, hivyo hawana budi kuondoa kesi hizo mahakamani mara moja. 
Napenda kuwataarifu kuwa walalamikaji wote wametuelewa na wamekubali kuondoa kesi zao zote mahakamami na hivyo, kuruhusu Kamati yangu kuwasilisha TFF malalamiko yote tuliyoainisha ili yafanyiwe kazi ndani ya siku 7 kuanzia jana na baada ya hapo Kamati itatangaza ratiba ya kukamilisha uchaguzi mdogo wa Yanga.  

Naomba vilevile nisisitize kwamba uchaguzi huu ni uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi zilizoachwa wazi. 

Hivyo viongozi wa Yanga tunaowachagua sasa ni wa kipindi kifupi kilichobaki cha takriban mwaka mmoja, kabla ya mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Yanga kuanza. 
 Nihitimishe taarifa yangu kwa kuwashukuru Watanzania na wana-Yanga wote kwa utulivu na uvumilivu mkubwa mliouonesha baada ya uchaguzi wenu mdogo kusogezwa mbele kwa muda. 

Aidha nawaomba wana-Yanga wote wakiongozwa na Wajumbe wa Baraza la Wadhamini, Sekreterieti na Wajumbe waliobaki wa Kamati ya Utendaji, wasichoke maana tumekaribia mwisho wa zoezi hili lenye afya kwa ustawi na maendeleo ya klabu hii kongwe Afrika ya Mashariki na Kati. Timu bora inategemea uongozi bora unaowajibika kwa wanachama.   

AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA

Malangwe Ally Mchungahela 
Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi ya TFF

Introducing "Tinasha" by Top Band artist Innovator

TUNTEMEKE SANGA: MTANGANYIKA ALIYEKUWA NA IQ YA KIPEKEE NA SHAHADA NYINGI KULIKO WOTE!!!

$
0
0
 Asubuhi ya Jumatatu, tarehe 8 Desemba 1930 huko Lupaso, kijiji cha Bulongwa, Njombe, alizaliwa mtoto wa kiume mwenye afya tele. Mtoto huyo, ambaye alikuja kuweka historia ya kipekee nchini, si mwingine bali ni TUNTEMEKE MESAKA NNUN'GWA SANGA. Wazazi wake, Bw. na Bi SANGA, walikuwa ni watoto wa Chifu. Watoto wengine wa wazazi hao walikuwa ni RWIJISO, ANNA, GEOFREY na ALFRED (Mwenyekiti wa Simba SC 1979-1982).

TUNTE alianza shule ya msingi mwaka 1942 huko Njombe akiwa na miaka 12 kama ilivyokuwa kwa Mwalimu JK NYERERE.

TUNTE alifanya mtihani wa darasa la 4 na kufaulu na hivyo akaendelea "middle school" hadi 1946 alipofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi  huko na kufaulu.  

TUNTE alijiunga na shule ya sekondari ya Ilboru mwaka 1947 na kumaliza mwaka 1950 ambapo alifaulu vizuri sana. Kidato  cha tano na sita alisoma shule ya "Tabora Boys" kuanzia mwaka 1951 hadi 1952.

Baada ya hapo akasomea ualimu(kazi  iliyokuwa na heshima sana enzi hizo kwani hata Mwalimu NYERERE alikuwa mwalimu pia). TUNTE, baada ya kupata cheti cha ualimu, akaenda kufundisha shule ya sekondari ya Ilboru.

TUNTE, akiwa kijana mdogo wa miaka 26, alikuwa mmoja wa Watanganyika wa kwanza kwenda kusoma Marekani kwani alipata fursa hiyo mwaka 1956.

TUNTE alikuwa kijana  mwenye IQ ya kipekee na malengo yasiyo ya kawaida ambapo alidhamiria kusoma fani mbalimbali kwa kadri itakavyowezekana.

Dhamira hiyo ilimfikisha katika vyuo mbalimbali nchini humo vya Gustav Adolphus, Chicago, Columbia na Princeton.

Dhamira hiyohiyo ya aina yake ndiyo iliyomuwezesha kuwa Mtanganyika wa kwanza na pekee kupata shahada 7 za fani za  Biashara, Uhusiano wa Kimataifa, Utawala, Sheria, Kilimo, Sayansi ya Jamii na Dini. Kuhusu dini alikujakusema mwenyewe bungeni tarehe 24.8.1993 - "Nikiwa Marekani nilijifunza na nayajua sana masuala ya dini kwa upande wa Wakristo, Waislamu na Bhuda".
TUNTE pia alikuwa akifundisha na kutoa mihadhara kwenye vyuo mbalimbali nchini humo na alikuwa na uwezo mkubwa wa lugha akiongea kwa ufasaha Kiingereza, Kiswahili, Kijerumani na Kifaransa. Mwaka 1962, alianza masomo ya PHD huko "Yale University". PHD hiyo ilihusu maendeleo ya utendaji vijijini. Kozi hiyo ilimpasa kwenda pia chuo cha Nuffield, UK na Chuo  Kikuu cha Dsm. 

TUNTE alirejea nchini mwanzoni mwa mwaka 1964 akawa Afisa Uhusiano wa kampuni ya Riddoch Motors (1964-1965). Aidha, kwa mikono yake, akajenga nyumba kijijini Bulongwa.

TUNTE, tarehe 20.9.1964, alifunga ndoa na Bi. BETTY ANN FITZGERALD, mmarekani mweusi aliyezaliwa Marekani mwaka 1939. Ndoa hiyo ya kukata na shoka ilifungwa huko Bulongwa baada ya TUNTE kulipa mahari iliyojumuisha ng'ombe, kondoo, mbuzi na kuku. Kwa hakika ilikuwa harusi ya aina yake ambapo watoto 122 waliovalia nadhifu waliwarushia maua maharusi hao, waliokuwa wamevaa nguo maridadi za kiafrika zilizotengenezwa nchini Ghana, na kuwaimbia nyimbo kedekede za Kikinga na Kizungu. Wazee kwa vijana, kwa wiki nzima, walisheherekea ndoa hiyo huku wakila beche lililopikwa kwenye mapipa 15 na pombe ya ulezi iliyokuwa "ya kumwaga". Ilikuwa ni harusi ya kihistoria ambayo, hadi leo, haina mfano wake Bulongwa! Aidha, harusi hiyo iliweka rekodi ya kuwa harusi ya kwanza Tanzania kuandikwa, kwa mapana na marefu, kwenye gazeti maarufu la Marekani (The New York Times la tarehe 1.11.1964 chini ya kichwa cha habari: "Pittsburgh Girl's Wedding in African village")!.

TUNTE alimuona kwa mara ya kwanza Bi. Betty alipoenda kutoa mhadhara huko Pittsburgh, Marekani mwaka 1960 ambako ndio kwao Bi. Betty, msomi mwenye shahada ya uzamili. Baada ya uchumba wa miaka 4, wawili hao ndipo walipooana.

TUNTE akaanza kufanya shughuli mbalimbali za biashara, kilimo, sheria na pia akajiingiza kwenye siasa ambayo ilikuja kumletea matatizo makubwa na Mwalimu NYERERE.

TUNTE, kwa kusoma Marekani kwa muda mrefu, aliamini kwamba siasa ya Ujamaa ni feki na haiwezi kuleta maendeleo na hakuwa akificha msimamo huo licha ya kuwa mwana-TANU iliyokuwa ikiamini katika Ujamaa.

TUNTE alieleza kwamba yeye ndio anafaa kuwa Rais hivyo Mwalimu NYERERE ampishe ili ailetee nchi maendeleo kwa falsafa za ubepari na abadili "mentality" ya wananchi wa Tanzania ambao wengi ni wavivu wapendao kujirusha na kuoneana wivu. TUNTE alidai shahada zake 7 zilimfanya awe na fikra sahihi za kuleta maendeleo kuliko Mwalimu aliyekuwa na shahada mbili tu na muumini wa ujamaa aliouona "unailostisha" nchi!.

Hiyo ilimkera mno  Mwalimu ambaye, kwa kutumia "The Preventive Detention Act, 1962", alimsweka mara moja TUNTE kizuizini kijijiji kwake Bulongwa na kumuamuru kutotoka kijijini hapo hadi apate kibali maalumu. 

TUNTE alikuwa kizuizini Bulongwa kwa miaka mingi na hii ilipelekea ashindwe kumaliza kozi yake ya PHD ambapo miaka ya baadae alipenda kutania:  
"Mimi ni PHD Candidate. Nilirudi nchini ili nifanye utafiti kuhusu PHD yangu lakini nikawekwa  kizuizini kwa miaka mingi hivyo nikashindwa kuikamilisha ndio maana najiita "DR. MTAHINIWA"!.

Mwalimu NYERERE, baada ya miaka mingi, alimsamehe TUNTE  ambaye aligombea ubunge jimbo la Makete mwaka 1980 na kushinda kwa kishindo.

TUNTE, akiwa bungeni, alikuwa mtata sana huku akiwapeleka puta mawaziri na hata maspika.!  

Siku moja bunge lilipokuwa pale Karimjee Hall, Dar Es Salaam, Mh. TUNTE alitinga na suruali ya "jeans" na shati la kitenge. Maofisa wa bunge hawakumruhusu kuingia ndani kwani hilo halikuwa vazi rasmi la bunge. Mh TUNTE akaondoka lakini akarudi na shati zuri lilishonwa kiwanda cha Nguo Urafiki lakini akiwa amevaa kaptura! Walinzi, kwa mara nyingine, wakamzuia lakini hakukubali hivyo ukazuka mtafaruku wa "kufa mtu"!. Mh Spika, ADAM SAPI MKWAWA alipoingilia kati, Mh TUNTE alimjia juu na kutaka amuoneshe Kifungu cha kanuni alichovunja. Hatimaye ilibidi arudi nyumbani!.   

Mh. TUNTE kuna wakati alipewa dakika 15 tu na Mh Spika PIUS MSEKWA aongee lakini akazisisha na kutumia dakika  30. Mh. MSEKWA alipomtaka akae, Mh TUNTE, aliyemzidi Mh. MSEKWA miaka 5 kiumri, alihamaki na kusema- ""Hivi kwenu hakuna Wakubwa? Huoni mambo niyaongeleyao ni muhimu kwa wananchi wetu?"  . Ukumbi mzima wa bunge  ulizizima kwa vicheko na hata Mh MSEKWA mwenyewe aliangua kicheko na hatimaye Mh TUNTE akakaa!. Kwa hakika,  Mh TUNTE hakuwa mtu wa Mchezo-mchezo!.

Mh TUNTE alikuwa mtu wa msimamo mkali asiyeyumbishwa wala kuogopa kusema alichokiamini na aliheshimiwa sana na Wabunge wenzake na aliposimama bungeni hata waliokuwa nje walikuwa wakirudi ndani kumsikiliza kwani alipenda sana kujenga hoja baada ya kufanya tafakuri tunduizu !.

Wananchi wa Makete walimpenda sana na alishinda ubunge mara zote alizogombea. Aliweza kuongea Lugha za Kikinga, Kibena,  Kihehe na Kinyakyusa kwa ufasaha.

Mwaka 1995 alikuwa mmoja wa wana-CCM waliochukua fomu kugombea Urais. Hii ni kwavile alitaka kutimiza azma yake ya kuliongoza Taifa hili kama alivyomwambia Mwalimu NYERERE ambae aliamua kumuweka kizuizini. Wengine waliochukua fomu walikuwa J. Warioba,  N. Kasaka, M. Bomani, J. Malecela, C. Msuya, H. Kolimba, R. Lugendo, J. Kikwete, E. Lowasa, R. Fred, K. Malima na B. Mkapa aliyechaguliwa kuipeperusha bendera ya chama na hatimaye kuwa Rais wa awamu ya tatu. 

Mh TUNTE alianza kupata matatizo ya macho muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha bunge mwaka 1996 Dodoma na akapelekwa hospitali ya Muhimbili ambako alilazwa. Mwezi Julai 1996, alipelekwa London, UK kwani aliishapoteza uwezo wa kuona kwa 95% ambako alifanyiwa operesheni  ya macho.

Wizara ya Afya ikamrudisha nchini kwa kudai ilikuwa imemaliza fungu ililotenga kwaajili ya matibabu yake hivyo akalazwa wodi ya Mwaisela mwezi Septemba 1996 baada ya kurejea nchini mwezi Agosti 1996. Alikuwa hawezi kumtambua mtu kwa kumuona bali kwa sauti tu. Viongozi wa serikali, Mh Dr. OMARI na Mh F. SUMAYE walimtembelea wodini hapo kumjulia hali. 

Mwanzoni mwa mwezi Octoba 1996, Mh TUNTE akatolewa hospitalini. Katikati ya Juni 1997, alikimbizwa hospitali ya Aga Khani ambako alilazwa ICU kwa wiki 2. Mh TUNTE akafariki saa 7 usiku wa Jumatano, tarehe 2.7.1997 akiwa na umri wa miaka 66.

Aliyekuwa Naibu Spika, Mh PHILLIP MARMO alilitangazia bunge kesho yake asubuhi kuhusu msiba huo  mkubwa na kwamba marehemu alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo na moyo. Simanzi kubwa ikashamiri bungeni.

Jijini Dar es Salaam, shughuli za mazishi ziliendeshwa na Brigedia Jenerali PETER LIGATE na msiba ulikuwa mtaa wa Mansfield kwa mdogo wake TUNTE, ALFRED SANGA.

Mwili  wake uliagwa Muhimbili jumamosi ya tarehe 5.7.1997 ambapo Rais MKAPA aliongoza mamia ya wananchi kutoa heshima zao za mwisho ambapo alisema:

"Kifo cha Mh. SANGA kimetuondolea kiongozi mashuhuri ambaye ametoa mchango mkubwa wa maendeleo si tu Makete bali nchi nzima kwani alikuwa Mzalendo mwenye uchungu mkubwa na nchi  yake. Hakuwa mwoga bali alikuwa mkweli daima. Nafasi aliyoiacha itakuwa ngumu sana kujazwa na kwamba mchango wake katika taifa hili utaandikwa katika historia ya nchi yetu".

Mwili wake ulisafirishwa kwa ndege na akazikwa kijijini Bulongwa Jumapili tarehe 6.7.1997. Wakati huo alikuwa ameachana na mkewe Bi Betty. Msiba huo ulihudhuriwa na watu wengi huku Wabunge 4 waliwakilisha wenzao.  Wabunge hao walikuwa T. NYIMBO, J. MAKWETA, M. KIBASSA na J. NHUNGA aliyekuwa Katibu wa Wabunge wa CCM.

Huyo ndiye  TUNTEMEKE MESAKA NNUN'GWA SANGA aliyeacha historia ya kipekee nchini!.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 16,2019


JUMUIYA YA WATANZANIA UGHABUNI YAPATA UONGOZI MPYA DALLAS , TEXAS, MAREKANI.

$
0
0
Kwa mujibu wa taarifa toka Jumuiya ijulikanayo kama Tanzanians Dallas, ambayo ni jamii ya watanzania wanaoishi katika jiji la Dallas, Texas na vitongoji vyake, limefanya mabadiliko siku ya Jumamosi tarehe 12, 2019 kwa kuwachagua viongozi mpito watatu. Uchaguzi huo ulihudhuliwa na wakazi wengi wa sehemu hizo zilizolizunguuka jiji la Dallas na kufanya maamuzi ya uongozi wa dharura kutokana na kujiudhuru kwa uongozi uliyopita.

Watanzania katika jiji hilo la Dallas na vitongoji vyake wanaamini kwamba, mshikamano wao ambao ndio kilikuwa ni chanzo kikubwa cha wao kuwa kitu kimoja wakati wa misiba na dharura za aina yote kimaishi wanavyoishi huko ughabuni. Kufuatana na katiba ya jumuiya hiyo hakuwa nabudi kuitisha kikao na kuwa na maamuzi ya kuteuwa wagombea mpito mpaka hapo mwezi Julai katika uchaguzi mkuu chini ya utaratibu mpya.

Uongozi uliotumikia jumuiya hiyo kwa muda sasa na hatimae kujiudhuru kwa hiyari, ni mwenyekiti Bw. Benedict Kazora, Bi Maria Musomi, Makamo mwenyetkiti na Bi Viola mbise, Katibu. Maamuzi hayo ya ghafla yaliwakilishwa kwenye kamati ya ushauri na kutangazwa rasmi katika tofuti za mitandao ya kijamii mara moja. Harakati zipo mbioni kuwasiliana na uongozi uliopita kukabidhiana nyaraka na uongozi mpya mpito haraka iwezekanovyo.

Jumuiya hiyo, imewachagua viongozi wake mpito wapya kupitia utaratibu wa kuwapigia kura wale wote walioteuliwa na wanajumuiya baada ya mkutano huo mahususi kuziba hizo nafasi hizo. Yafuatayo ni majina ya wachaguliwa wapya, Mwenyekiti ni Bw. Everest M. Michael, Katibu Bw. Godfrey Mwamsoyo na mweka hazina ni Bi Jocyline Vadesto. Wateuliwa wote hao ni wakazi wa Dallas na vitongoji vyake. Jumuiya mzima ya Watanzania Dallas inatoa pongezi na shukrani nyingi kwa wale wote walio pata wasaa na kujitokeza kufanya zoezi hili muhimu.

Pia vilevile, sambamba na mkutano huo lilichaguliwa baraza la ushuri la watu wa jumuiya hiyo chini ya mapendekezo ya wanajumuiya wake, na sio tena kama jinsi baraza lile la zamani kuteuliwa na mwenyekiti. Hii ni kuhamasisha dhamira na malengo ya jamii kupewa kipaumbele katika maswala ya jamii hiyo. Misiba na matatizo yasiyo tabirika, ndivyo vigezo vikuu vilivyo waleta wanajumuiya hao pamoja na kusaidiana kutatua yanayojiri wakati kama huo mgumu kwao.

Hivyo basi, baraza la ushauri lina takribani watu kumi na moja ambao watakuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na uongozi wa juu na kujaribu kuwa na ufumbuzi wa matitizo au misiba inapotokea katika uzio wa mipaka ya vitongoji vyao. Hivyo, walioteuliwa na jamii hiyo katika baraza au kamati hiyo hadi hapo mwezi Julai uchaguzi mkuu ni:
Bw. AloyceChissanga; 2. Bw. Peter Kapanga; 3. Bi Anna Ngoti; 4.Bw. Felix Maganjila; 5. Bw. Kibwana Rumadha; 6. Bi Arafa Manganji; 7. Bw. Ibrahim Kulindwa; 8. Bi Rosemary Kessy; 9. Bw. Erick Joshua; 10. Bi Sofia Lesso; na 11. Bw. Godlisten Lyimo.

Hao ndio wanaoiwakilisha baraza au kamati ya ushuri mpito iliyopo madarakani tokea uchaguzi wake wa tarehe 12 January mwaka 2019.

Juhudi zinaendelea kuhakikisha kwamba kwa mujibu wa katiba, yote yanayojiri katika makabidhiano ya kifedha na vitega uchumi ya Jumuiya vinatendwa chini ya utaratibu sahihi na wenye nidhamu. Hii utawapo urahisi fasaha wale viongozi wapya kufuatialia harakati zote zinazo husiana na jumuiya na kuitangaza nchi yetu ya Tanzania kupitia vivutio vyake asilia vya kitalii na maliasili.

Kwa mujibu wa taarifa toka kwa mwenyekiti mpya wa mpito, ndugu Everest, inaeleza kwamba, kazi kubwa iliyopo ni kuwa hamasisha wanajumuiya wote wa asili ya Tanzania kushiriki katika ufumbuzi wa maswala yanayotukabiri na kuwa bora, imara zaidi ya jumuiya zinginezo toka Afrika. Tanzania, hususani sekta ya utalii, madini na nyanja nyinginezo tofauti, tutazidi kuwa mstari wa mbele kuhakikisha nchi yetu inazidi kutambulika hapa na kuwavutia jamaa na marafiki wetu wa Marekani waje tembelea mbuga zetu za wanyama, mlima wa Kilimanjaro na mengineyo zaidi toka Tanzania.

Mwisho kabisa, Jumuiya hiyo ya watanzania wanaoishi Dallas na vitongoji vyake vya karibu pia wakazi wake ambao kwa namna moja au nyingine waliowahi kuishi huko wanawatakia uongozi huu mafanikio mema yenye mshikamano wa dhati na uzalando halisia kama Tanzania Diaspora.
Everest Michael, Mwenyekiti mpya.
Godfrey Mwamsoyo Katibu mkuu .
Bi Jocylne devosta mweka Hazina.
Wanajumuiya wa Tanzania Dallas,TX Wakisikiliza hoja kwa makini.


TAEC KUANZISHA MRADI KWA KUHIFADHI CHAKULA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akisoma moja ya kitabu alichokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu Tume ya nguvu za Nyuklia Nchini (TAEC) Profesa Lazaro Busagala alipotembelea ofisi hiyo leo kujitambulisha. Picha na Vero Ignatus.
Mkurugenzi Mkuu Tume ya nguvu za Nyuklia Nchini (TAEC) Profesa Lazaro Busagala akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Arusha moja ya nyaraka mbalimbalimbali zinazohusiana na TAEC. Picha na Vero Ignatus. 



Na Vero Ignatus, Arusha.

Tume ya nguvu za Atomiki nchini ipo mbioni kuanzisha mradi wa uhifadhi wa chakula kwa kutumia nyuklia (food Irradiator) ambayo itachangia kupunguza upotevu wa vyakula na biashara

Mkurugenzi mkuu wa TAEC Prof. Lazaro Busagala amesema kuwa hiyo ni mipango iliyopo kwa sasa ikiwa ni pamoja na kuanzisha kinu cha tafiti za nyuklia, kuzalisha dawa za kutibu saratani (Research Reactor) ambapo ikifanikiwa Tanzania itakuwa ya pili kwani kwa sasa kipo Afrika ya kusini 

Profesa Lazaro Busagala amemueleza mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo leo alipotembelea ofisini kwake kujitambulisha kuwa wanatazamia kuanzisha kituo cha mafunzo ya fani ya sayansi za teknolojia ya nyuklia na kuboresha miundombinu ya udhibiti wa matumizi salama ya nyuklia. 

Amesema maeneo ambayo nchi imenufaika kwa mwaka wa fedha uliopita kwa upande wa ni sekta ya Afya, maji, kilimo na mifugo waliweza kupata jumla ya shilingi Bilioni 6.1,na upande wa mafunzo shilingi bilioni 3.2

Amesema maeneo mengine waliyofaidika kwa kutumia teknolojia ya nyuklia ni sekta ya Afya waliweza kupata mashine ya kutibu ugonjwa wa saratani iliyosimikwa mwaka jana hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam na Bugando jijini Mwanza. 

Kwa upande wa kilimo teknolojia hii ya nyuklia imeweza kuwasaidia kuongeza ubora wa mbegu kwa kutumia mionzi katika upandikizaji wa kitaalamu, na kupata mifugo bora zaidi.'' Zanzibar teknolojia hii imewasaidia kwa kuteketeza mbung'o wote kwa kuwaasi madume ya mbung'o hivyo magonjwa yite yanayoenezwa na mbung'o Zanzibar hayapo'' 

Amezitaja changamoto zinazo wakabili ni kutofahamika zaidi kwa kazi za TAEC, uhaba wa fedha za kuleta maendeleo na manunuzi ya haraka, uhaba wa vifaa kwenye kanda, mipakani na Zanzibar pamoja na upungufu wa wafanyakazi kwa sasa jumla 108 wakati mahitaji halisi ni 215

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema Elimu hiyo ya nyuklia ni vyema ikatolewa kwa wajumbe wote wa kamati ulinzi na usalama ya mkoa kwani inahisika moja kwa moja na usalama na itawasaidia katika kutekeleza majukumu yao. 

Amesema hiyo ni fursa adimu kwao kama mkoa na nchi kwa ujumla kwani itawasaidia kuangalia vitu vinavyoingizwa mipakani, mifugo, chakula na hata katika uwanja wa kimataifa wa KIA ambao Arusha nao washea kuangalia vitu vinavyoingia na kutoka. 

Gambo amesema kuwa serikali ngazi ya mkoa ipo tayari kushirikiana na TAEC katika changamoto ambazo wataweza kuzitatua huku akuwataka wasikae kimya hadi changamoto iwe kubwa ndipo waiwasilishe.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

RC Wangabo asisitiza ushirikiano Kutatua changamoto za elimu

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi, kuhakikisha kila mtumishi kwa nafasi yake na majukumu yake anashirikishwa katika kutatua changamoto za wananchi ikiwemo elimu, afya, maji na kilimo pamojana kushirikiana na wananchi kutatua chnagmoto hizo.

Amesema kuwa ili kutatua hayo halmashauri inapaswa kuongeza vyanzo vya mapato ikiwemo kuzidisha malengo ya makusanyo kwa mwaka ili kuweza kukabiliana na changamoto anazokuwa anasomewa kila anapofanya ziara katika shule mbalimbali za halmashauri na kumuomba achangie kutatua changamoto zao.

“Mpige hesabu zote muwarudishie huko jamii ili jamii iguswe kwamba alaa! Kumbe kuna changamoto kubwa sana zisingoje sisi viongozi ambao pengine hatuna nafasi ya kuzunguka sekondari zote, lakini kama tutafanya hivi tutaondoa changamoto zote hizi na matatizo na haya yote mliyoyasema yako chini ya uwezo wenu, sio mambo ya mkuu wa mkoa haya, ni mambo ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi, kata na vijiji vyenu, kama ni “support” tunatoa ya kuhamasisha,naweza kusema nanunua bati mbili tatu, je, ninatatua matatizo yote hayo?”Alibainisha.

Ameongeza kuwa kazi ya shule ni kuandaa taarifa nzuri na kuikabidhi kwa watendaji wa halmashauri kuanzia Mtendaji wa kata na vijiji pamoja na viongozi wa kisiasa akiwemo diwani wa kata husika ili taarifa hizo ziwafikie wananchi watambue kupitia vikao vya kamati ya maendeleo ya kata ambao ni mfumo mzuri uliowekwa na serikali katika kutambua changamoto na kuzitatua.

Ameyasema hayo baada ya kupokea taarifa ya shule ya sekondari Chala, iliyopo kata ya Chala Wilayani Nkasi na mkuu wa shule hiyo Fatma Mchomvu aliyemuomba kufanya harambee ya haraka kutoka kwa msafara alioambatana naoi li kuweza kukarabati nyumba ya “Matron” ambapo hadi wanafikisha ombi hilo waalimu walikwishajichangisha shilingi 50,000/-.

“Walimu wamejitolea kuchangia 50,000/- kusaidia kukarabati nyumba moja ya mwalimu ya “matron” kwasababu kule wanafunzi wako peke yao hakuna ulinzi kwahiyo nao wakaomba kupitia msafara wako, na wewe ndio kiongozi wetu tupate harambee ya haraka ili angalau tuanze kufanya ukarabati wa jengo hilo ili angalau wanafunzi wawe salama kwasababu wanakaa mbali na hakuna mlezi wa kukaa nae kule,” Alifafanua.

TUTAENDELEA KUSAIDIA SEKTA ZA ELIMU NA AFYA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI-NMB

$
0
0
BENKI ya NMB imesema inatambua umuhimu wa elimu na afya kwa Watanzania hivyo itaendelea kusaidia katika sekta hiyo ikiwa ni sehemu ya kuunga juhudi za Serikali za kuwahudumia wananchi wake.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Meneja wa Benki hiyo, Kanda ya Nyanda za Juu, Straton Chilongola wakati akikabidhi msaada wa madawati 102 kwa shule za Msingi Mwasanga na Hekima za Jijini Mbeya.

Pia Benki ya NMB imekabidhi jumla ya mabati 324 kwa shule za Msingi Mlima Reli ya Wilaya Mbeya na Mapinduzi ya Jijini Mbeya na vitanda, magodoro na mashuka kwa Hospitali Teule ya Mbalizi vyote vikiwa na thamani ya milioni Sh25. Alisema NMB ni wadau muhimu kwa Serikali na Watanzania hivyo wanao wajibu wa kuunga mkono juhudi za maendeleo kwa sababu jamii wanayoisaidia ndiyo inayowawezesha kupata faida katika biashara yao.

“Tunambatua changamoto ya elimu na afya, sisi NMB tunazipa kipaumbele sana kwa sababu hizi sekta mbili ni muhimu mno katika ustawi wa jamii yetu,” alisema Chilongola.Chilongola alisema katika kipindi cha mwaka huu wa 2019, NMB imetenga Sh1 bilioni kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii ikiwamo afya, elimu na yanapotokea majanga kwa nchi nzima.

Awali Mwalimu Mkuu wa Shule Msingi Mwasanga, Keneth Amon alisema shule yake inakabiliwa na msongamano wa mkubwa wa wanafunzi madarasani kutokana uhabawa wa vyumba vya madarasa, upungufu wa madawati.Alisema ‘Msongamano ni mkubwa sana darasani, shule nzima tuna madawati 237 lakini kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi, tunakabiliwa na upungufu wa madawati 140, lakini vile vile tuna upungufu wa ofisi za walimu. Shule ina walimu 22 na wote tunatumia ofisi moja ambayo nayo ni finyu mno jambo ambalo kwa kweli inatuwia vigumu kumudu majukumu ya kila siku’.

Akizungumza na baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika alisema Benki ya NMB inatambua umuhimu wa kusaidia jamii kama walivyo fanya ikitambua kwamba Serikali pekee haiwezi kufanya kila jambo kwa wananchi wake licha ya kuwa ndio wajibu wake.

Alisema ‘Niwatake wazazi kwamba shule zimeshafunguliwa sasa hivyo asiwepo mwanafunzi ambaye hafiki shuleni, na nyinyi wanafunzi hakikisheni mnatunza madawati haya na msome kwa bidii. Leo NMB imetambua umuhimu wa elimu bora kwa kuwatengenezea mazingira bora ya kusomea na ndiyo maana imeleta madawatin haya’.

Ntinika amefafanua kuwa mahitaji ya huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu yanahitaji kuungwa mkono na taasisi na mashirika mbalimbali ya kijamii kama ilivyofanywa na Benki ya NMB ambayo imechangia vitanda na mashuka kwa Hospitali Teule ya Mbalizi.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya - William Pauk Ntinika akipokea Msaada wa madawati 51 kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za juu - Straton Chilongola kwa ajili ya shule ya Msingi Mwasanga Jijini Mbeya. Benki jana ilikabidhi jumla ya madawati 102 kwa shule ya Msingi Mwasanga na Hekima, Mabati 324 kwa shule za Msingi Mlima Reli, vitanda magodoro na mashuka kwaajili ya Hospitali teule ya Mbalizi jijini Mbeya vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 25.
Mkuu wa wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika akipokea mashuka kwa ajili ya Hospitali Teule ya Ifisi ya jijini Mbeya kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu - Straton Chilongola. Kwa ujumla, Benki jana ilikabidhi jumla ya madawati 102 kwa shule ya Msingi Mwasanga na Hekima, Mabati 324 kwa shule za Msingi Mlima Reli, vitanda magodoro na mashuka kwaajili ya Hospitali teule ya Mbalizi jijini Mbeya vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 25.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu Straton Chilongola akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Mbeya William Paul Ntinika mabati 144 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Msingi Mapinduzi Jijini Mbeya. Kwa ujumla, Benki jana ilikabidhi jumla ya madawati 102 kwa shule ya Msingi Mwasanga na Hekima, Mabati 324 kwa shule za Msingi Mlima Reli, vitanda magodoro na mashuka kwaajili ya Hospitali teule ya Mbalizi jijini Mbeya vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 25. 


Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwasanga wakiwa wameketi kwenye madawati yaliyotolewa na Benki ya NMB baada ya makabidhiano yaliyofanyika shuleni hapo. Benki jana ilikabidhi jumla ya madawati 102 kwa shule ya Msingi Mwasanga na Hekima, Mabati 324 kwa shule za Msingi Mlima Reli, vitanda magodoro na mashuka kwaajili ya Hospitali teule ya Mbalizi jijini Mbeya vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 25.

MRADI UJENZI UPANUZI WA BARABARA YA KIMARA-KIBAHA UKIENDELEA

$
0
0
Muonekano wa barabara ya Morogoro eneo la Kimara stop over jijini Dar es salaam hivi leo ambapo tayari Ujenzi wa Upanuzi wa barabara hiyo  Kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye Urefu wa Kilometa 19.2 unaendelea.Upanuzi huo utahusisha kuongeza njia za magari kutoka mawili mpaka nane,Mradi huo muhimu ukikamilika utasaidia kupunguza msongamano mkubwa wa Magari takribani 50,000 yanayopita katika barabara hiyo kila siku .Mradi huo utafanyika kwa miezi 30 kuanzia Julai 21,2018 ambapo utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 141.56 Fedha zote kutoka serikali ya Tanzania

MKUU WA WILAYA TUNDURU JUMA HOMERA APOKEA NG'OMBE ZA MRADI,AKABIDHI KWA WANANCHI

$
0
0
Na Ripota Wetu,Tunduru

MKUU wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera amepokea ng'ombe zaidi ya 200 kutoka kwa wafadhili na kuzigawa katika kaya za wilaya hiyo katika kata 16 na vijiji 64 vinavyotekelezewa mradi wa Boresha afya ya mama na mtoto (AMCC) maarufu CHIP chini ya ifadhili wa Kanisa Anglican dayosisi ya Masasi.

Homera amekabidhi ng'ombe hizo jana ambapo ametumia nafasi hiyo kufafanua ni vema wananchi wakatunza mifugo hiyo ili kupata tija katika kuinua maisha yao.

Amefafanua hadi sasa zaidi ya Sh. million 405 zimetumika katika programu ya kopa ng'ombe lipa ng'ombe na kaya nyingi zimenufaika na mpango huo huku akisisitiza kwa kuwaeleza wananchi wahakikishe ng'ombe hizo zinatunzwa kama ambavyo inafanyika kwa wananchi ambao tayari walishapatiwa ng'ombe hao ambao wanatolewa bila gharama yoyote zaidi ya mhusika kutengeneza banda la kufugia tu.

Aidha Mkuu wa Wilaya Homera alieleza pia huo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2020 ibara ya 25 kifungu (f). Pia pamoja na mifugo hiyo pia kupitia mpango huo wananchi wamenufaika na mbuzi wa Maziwa,Kuku,Bata,Kondoo,Kanga,na Sungura .

Hivyo amesema wananchi wanaimarisha afya zao kutokana na kupata kitoweo na maziwa na kuendelea kupunguza wimbi la changamoto ya utapiamlo na udumavu kwa kuzingatia kanuni za lishe bora.

Ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha wananchi wote wa Wilaya ya Tunduru kuendelea kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za maendeleo huku akitoa shukrani zake kwa Kanisa hilo ambalo limeamua kujikita katika kuona jamii inanufaika na uwepo wao kupitia mradi huo.

Ameongeza kuwa Kanisa hilo mbali ya kutoa mifugo kwa wananchi pia limesaidia jamii ya Wana Tunduru kwa kuchimba visima vya maji 25 ikiwa ni mkakati wao wa kuhakikisha wanashiriki kufanikisha maji yanapatikana.

"Niwapongeze zana meneja wa mradi huo pamoja na timu yako yote kwa uamuzi wenu wa kushirikiana nasi wananchi wa Tunduru katika kuleta maendeleo," amesema Homera.
MKUU wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera amepokea ng'ombe zaidi ya 200 kutoka kwa wafadhili na kuzigawa katika kaya za wilaya hiyo  katika kata 16 na vijiji 64 vinavyotekelezewa mradi wa Boresha afya ya mama na mtoto (AMCC) maarufu CHIP chini ya ifadhili wa Kanisa Anglican dayosisi ya Masasi.

NEWZ ALERT: KANGI LUGOLA ATUMBUA MAKAMANDA WATATU WA POLISI,AMTAKA KAMANDA USALAMA BARABARANI KUJITATHMINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ametengua uteuzi wa Makamandaa wa polisi watatu wa mikoa ya Temeke,Ilala, na Arusha kwa makosa mbalimbali ikiwemo kujihusisha na vitendo vya Rushwa kulinda Askari wanaohusishwa katika kusindikiza utoroshwaji wa Bidhaa, na madawa ya kulevya.

Lugola ametaja Makamanda hao kuwa ni Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula na Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng'azi

Waziri Lugola ametangaza uamuzi wake huo leo Jumatano Januari 16, 2019, katika mkutano na waandishi wa habari akibainisha kuwa amefanya hivyo baada ya kushauriana na vyombo anavyoviongoza.

Lugola pia amemtaka Kamanda Wa kikosi cha Usalama barabarani nchini kujitathmini kama anatosha katika nafasi hiyo. "Mimi ndio waziri wa mambo ya ndani ya nchi nasimamia vyombo vyote hivyo, nikitengua uteuzi inabaki kazi ya IGP kuteua mtu mwingine kujaza nafasi" amesema waziri Kangi Lugola.

Vodacom yatoa msaada wa kompyuta 30 shule ya Msingi Mbwanga mjini Dodoma

$
0
0
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu akimkabidhi Afisa Elimu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mwisungi Kigosi (wapili kulia) na Mkuu wa shule ya Msingi Mwanga, Rajabi Bakari (Kulia), moja kati ya kompyuta 30 zilizotolewa na kampuni ya Vodacom kwa shule ya Msingi Mbwanga Dodoma hivi karibuni kama mpango wa kuisaidia serikali kuboresha miundombinu ya elimu pamoja na kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu ya kidijitali kuanzia elimu ya msingi.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano Vodacom, Jacquiline Materu akitoa mkono wa shukrani na Afisa Elimu wa Wilaya  ya Dodoma Mjini Mwisungi Kigosi (katikati) na Mkuu wa shule ya Msingi Mbwanga, Rajab Bakari, kwa msaada wao, katika hafla ya kukabidhi kompyuta 30 zilizotolewa na Vodacom kwa shule ya Msingi Mbwanga Dodoma hivi karibuni kama mpango wa kuisaidia serikali kuboresha miundombinu ya elimu pamoja na kuhakisha wanafunzi wanapata elimu ya kidijitali kuanzia elimu ya msingi .

Watanzania 70 wahitimu Chuo Kikuu cha Galgotias nchini India

$
0
0

Balozi wa Tanzania nchini India, Baraka Luvanda akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu Galgotias kutunukuu vyeti kwa wahitimu wa chuo.

Balozi wa Tanzania nchini India, Baraka Luvanda akitoa heshima katika picha ya Mahatma Gandhi kwa kuweka shada la maua.

Balozi wa Tanzania nchini India, Baraka Luvanda akitoa hotuba katika mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Galgotias

Umati wa wahitimu wa chuo kikuu cha Galgotias wakisikiliza kwa makini hotuba ya Balozi Tanzania nchini India, Baraka Luvanda.

Balozi wa Tanzania nchini India, Baraka Luvanda akipokea memento kutoka kwa mwanzilishi na mkuu wa chuo kikuu cha Galgotias, Bw. Suneel Galgotia.




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Watanznaia 70 wahitimu Chuo Kikuu cha Galgotias nchini India


Watanzania zaidi ya 70 wakiwemo wawili wa shahada ya uzamivu wamehitumu masomo yao katika Chuo Kikuu cha Galgotias nchini India katika fani mbalimbali tarehe 14 Januari 2019.


Balozi wa Tanzania nchini India, Baraka Luvanda ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika mahafali ya nne ya chuo hicho aliwatunuku vyeti wanafunzi hao na wengine kutoka nchi mbalimbali duniani na kuwasihi  kutumia ujuzi walioupata kuchangia kikamilifu maendeleo ya nchi walizotoka.


‘Ulimwengu unasubiri uongozi mpya na mawazo mapya na kanuni na miiko madhubuti kutoka kwenu. Hivyo, kifanyeni chuo kijivune kupitia kwenu kwa kutoa michango yenye tija katika mataifa na jamii zenu, hususan kwa kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na uadilifu mkubwa katika kutimiza majukumu yenu', Balozi Luvanda alisema.


Balozi Luvanda alisema kuwa wanafunzi hao wanahitimu huku dunia ikishuhudia mapinduzi ya teknolojia mbalimbali zikiwemo za kidigitali, teknolojia ya matumizi ya sarafu za kidigitali (block chain), matumizi ya kiwango kikubwa cha data katika kufanya maamuzi (big data revolution), usalama wa mitandao (cybersecurity) na matumzi ya teknolojia katika kutekeleza kazi ambazo awali zilikuwa zinafanywa na mwanadamu (artificial intelligence). Alielezea matumaini yake kuwa chuo hicho kitakuwa kimewandaa vyema wahitimu hao  kukabiliana na changamoto za mapinduzi ya teknolojia katika kutekeleza majukumu yao.


Balozi alihitimisha hotuba yake kwa kuwasihi wahitimu hao kuwa, kutunukiwa vyeti sio mwisho wa kujifunza. Wanatakiwa waendelee kusoma vitabu kwa kuwa kusoma vitabu ni sawa na kuufanyia matengenzo ubungo. ‘Akili ya mwanadamu ni kama bustani, bustani isipomwagiwa maji na kupaliliwa itaota magugu na kufa kabisa.  Balozi alimaliza.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dodoma.

16 Januari 2019

RC TABORA AIAGIZA KAMPUNI YA L AND T KUREKEBISHA KASORO UJENZI WA TANKI LA MAJI LA KIJIJI CHA IBELAMILUNDI

$
0
0
Na Tiganya Vincent, Tabora
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imemwagiza Makandarasi wa L and T kufanyia marekebisho ya kasoro na udhaifu uliojitokeza katika utekelezaji wa ujenzi wa tenki la maji la ujazo lita milioni moja uliokuwa ukijengwa katika Kijiji cha Ibelamilundi wilayani Uyui baada ya Kamati iliyoundwa kubaini baadhi ya mapungufu kwenye maendeleo ya mradi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ametoa maagizo hayo hiyo jana baada ya kupokea taarifa ya Kamati aliyokuwa ameiunda kuchunguza ubora wa kazi katika ujenzi wa hilo kubaini uwepo wa kasoro katika usukaji wa nondo na Mkandarasi kutumia michoro ambayo hajaidhinishwa na Mshauri wa Mkandarasi.

Alisema pia Kamati imebaini udhaifu katika usimamizi wa Mhandisi Mshauri(Consultant ) mradi huo ikiwemo na ule upande wa Serikali kutotembelea mradi na kutoa ushauri wa kuboresha kasoro na kutokuwa na mawasiliano ya karibu wakati wa ujenzi wa mradi huo.

Mwanri alisema baada ya kupokea taarifa ya Kamati amemtaka Mkandarasi kuendelea na shughuli wakati akiendelea kurekebisha mapungufu yote yaliyojitokeza na kuwataka wasimamizi kwa upande wa Serikali kutembelea mara kwa mara maeneo ya mradi ili kuhakikisha unakuwa na ubora kulinga na mkataba wa ujenzi wake.

Alisema lengo ni kupata mradi ambayo utadumu kwa muda mrefu badala ya kujengwa kisha inaharibika katika kipindi kifupi. Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliitaka Kamati hiyo kufanya ukaguzi wa miradi yote ya ujenzi wa bomba la maji hilo ili kuona kama kweli Mkandarasi anazingatia michoro iliyopo kwenye mkataba.

Naye Mwenyekiti wa Kamati maalumu  iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Injinia Damian Ndabalinze alisema kuwa Kamati ilibaini mapungufu kadhaa ikiwemo matumizi ya micho ya ramani ambayo hakuidhinishwa na Mhandisi Mshauri na kuwepo na udhaifu katika usimamizi katika mradi huo.

Alisema Kamati inashauri kuwepo na usimamizi wa karibu na mawasiliano ya maandishi yawe yanafanyika kuonyesha kama kwenye pande zinahusika zimekutana kwa kuandika katika kitabu maalumu(log book). Kwa upande wa Meneja Mradi kutoka Kampuni ya Mhandishi Mshauri ya Wapcos LT Bw. Manohar Mattendda alisema atahikisha anamsimamia vema Mkandarasi ili kuhakikisha anfanyia kazi mapendekezo ya Kamati na kuweza kuwepo na ubora kwa kazi iliyokusudiwa na inakamilika kwa wakati.

Naye Meneja wa Kampuni inayotekeleza ujenzi mradi huo ya L and T Giresh Krishnamoorthy aliahidi kufanyia marekebisho kasoro na mapungufu yaliyojitokeza ili aweze kutekeleza kazi nzuri kulingana mkataba alioingia na Serikali ya Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa  Mamlaka ya Maji Safi katika Manispaa ya Tabora(TUWASA) Mkama Bwire alisema watajitahidi kushirikiana na pande ili kuhakikisha wanaboresha mapungufu yaliyojitokeza.
 Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya kuchunguza ubora wa tenki katika Kijiji cha Ibelamilundi Injinia Damiani Ndabalinze akitoa ripoti ya uchunguzi wa ubora walioifanya hivi karibuni. 
 Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya kuchunguza ubora wa tenki katika Kijiji cha Ibelamilundi Injinia Damiani Ndabalinze (kulia) akikabidhi  ripoti ya uchunguzi wa ubora walioifanya hivi karibuni kwa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (katikati) ili naye akabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto).
 Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora ili apokee ripoti ya uchunguzi wa ubora wa tenki lililokuwa likijengwa katika Kijiji cha Ibelamilundi wilayani Uyui.
 Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu(kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) ripoti ya uchunguzi wa ubora wa tenki lililokuwa likijengwa katika Kijiji cha Ibelamilundi wilayani Uyui.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akitoa ufafanunuzi jana mara baada ya kupokea ripoti ya uchunguzi wa ubora wa tenki lililokuwa likijengwa katika Kijiji cha Ibelamilundi wilayani Uyui. Picha na Tiganya Vincent

“Asiyetaka kuchukua kitambulisho cha ujasiliamali asubiri kubughudhiwa” RC Wangabo

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Joachim Wangabo amewataka wajasiliamali wote mkoani humo kujitokeza kupatiwa vitambulisho vya ijasiliamali vilivyotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa mikoa na wilaya zote nchini ili kuwaepusha wajasiliamali hao na bughudha wanazozipata katika kuendesha biashara zao za kila siku.

Amesema kuwa kila halmashauri kati ya halmashauri nne za mkoa wa Rukwa ilipatiwa vitambulisho 6,250 katikati ya mwezi Disemba mwaka 2018 lakini hadi kufikia leo katikati ya mwezi wa kwanza vitambulisho vilivyogawiwa havizidi 150 kwa mkoa mzima hali iliyopelekea Wangabo kuahirisha ziara ya siku nne aliyopanga kuifanya katika halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ili kujionea miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Nawataka waende katika halmashauri zote haraka iwezekanavyo vinginevyo watakosa hii nafasi ya kuapata vitambulisho na kitakachofuata kinaweza kisiwe kizuri kwa wajasiliamali, kwasababu hiki ni kitambulisho ndicho kinachomfanya mjasiliamali huyu mdogo atambulike na asibughudhiwe kama mheshimiwa rais alivyosema, sasa usipopata kitambulisho maana yake ni kinyume chake ndicho kitakachokuja, unapata kitambulisho ili usibughudhiwe, lakini wewe hujapata kitambulisho inamaana utabughudhiwa, mimi nisingependa wajasiliamali wapate bughudha,” Alibainisha.

Ameyasema hayo baada ya kupata taarifa ya Wilaya ya Kalambo juu ya miradi mbalimbali ya kimaendeleo, mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza, ukusanyaji wa mapato na matumizi ya halmashauri, ugawaji wa vitambulisho hivyo pamoja na hali ya kilimo ya Wilaya kabla ya kutaka kuanza ziara yake katika wilaya hiyo.

Aidha amesisitiza kuwa tathmini ya ugawaji wa vitambulisho hivyo itafanyika baada ya siku kumi tangu leo tarehe 15.1.2019 hadi tarehe 25.1.2019 ili kuona muitikio wa wajasiliamali hao kwa halmashauri zote na kuwaagiza wakurugenzi wa halmashauri hizo kuhakikisha wanaongeza kasi ya kuwasajili na kuwakabidhi wajasiliamali hao vitambulisho vyao bila ya bughudha yoyote.

Wakati akiwasilisha taarifa ya wilaya, katibu tawala wa wilaya ya Kalambo Frank Sichalwe alisema kuwa tangu kufanyika kwa uzinduzi wa ugawaji wa vitambulisho hivyo mwanzoni mwa mwaka huu ni wajasiliamali kumi tu ndio waliopatiwa vitambulisho hivyo pamoja na kuendelea na hamasa ya kuwatambua wajasiliamali wengine.

“Zoezi la hamasa na ugawaji wa vitambulisho linaendelea ili vitambulisho vingi zaidi viweze kutolewa na kuwanufaisha wajasiliamali katika sekta isiyorasmi kama mheshimiwa Rais alivyokusudia, mpaka sasa Ulumi tumepata wajasiliamali 80, Mwimbi 30, Kasanga 30, Mwazye 20 na Matai wamejitokeza wajasiliamali zaidi ya 100 mpaka sasa,” Alisema.

Vitambulisho vya ujasiliamali viligagiwa kwa wakuu wote wa mikoa 26 mwanzoni mwa mwezi Disema mwaka 2018 na kila mkoa kupata vitambulisho 25,000 ili kuweza kuvigawa kwa wakuu wa wilaya na hatimae kufika mikononi mwa wakurugenzi ili kuwapatia wahusika wa vitambulisho hivyo kwa lengo la kupunguza bughudha kwa wajasiliamali wataopata vitambulisho hivyo vyenye gharama ya shilingi 20,000 kwa kila kitambulisho.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live


Latest Images