Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live

DC JOKATE MWEGELO AWEKA WAZI MADINI YALIYOPO KISARAWE YATAKAVYOWANUFAISHA WANANCHI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo ameweka wazi kuwa atapambana kwa juhudi na maarifa kuhakikisha uwepo wa madini katika ardhi ya Kisarawe unaleta tija na neema kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Akizungumza kuhusu hilo leo DC Jokate amesema chini ya uongozi wake kuanzia mwishoni mwa mwaka 2018 alianza mchakato wa kufanya Geological Survey/Mapping kwakushirikiana na Geological Survey of Tanzania na Ofisi ya Kamishna wa Madini Ukanda wa Mashariki.

Lengo likiwa kutambua aina ya madini na ubora wake na kiasi ambacho kitapatikana ili kuanza kuweka mikakati endelevu na yenye tija ya muda mrefu kwa wilaya na Taifa kwa ujumla.

Amefafanua madini ambayo wilaya ya Kisarawe imejaaliwa kuwanayo kuwa ni; Madini ya udongo jasi, madini aina ya chokaa, malighafi za ujenzi kama vifusi/mchanga, mawe, na kokoto.

Mwegelo amesema Kisarawe haiwezi kuendelea kuwa masikini na kuwa na upungufu wa huduma muhimu za afya na elimu wakati kuna madini katika aridhi ya kisarawe ambayo watu wa Kisarwe wamepewa zawadi na Mungu.

Ameeleza kuwa nia yake ya kushirikiana na vyombo vyote vinavyohusika kuhakikisha kunawekwa utaratibu mzuri utakao hakikisha mapato yote yanayotokana na madini wilayani Kisarawe yanawekewa utaratibu mzuri wa matumizi ikiwa ni pamoja na kuongeza na kuboresha miundombinu ya afya, elimu kama vile kujenga madarasa na kufikia lengo la kuwa na matundu ya vyoo ya kutosha ili kukidhi haja na viwango vinavyohitajika.

Pia DC Mwegelo amesema niwakati wa yeye kusimama imara na viongozi wote waliochini yake na Serikali kwa ujumla kuunganisha nguvu pamoja na kushirikisha wananchi ambao ndiyo wadau muhimu katika kuleta maendeleo.

"Naamini kuwa jambo hili litasaidia sana kutimiza muono mpana na ndoto kubwa ya Rais wa awamu ya tano na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.John Magufuli ya kulifanya Taifa la Tanzania kuwa Taifa lenye uchumi wa kati na kuwa taifa lenye kutegemewa na mataifa mengine.

" Uanzishwaji wa vituo maalumu vya biashara ya madini kama ilivyoelekezwa na kuagizwa na Rais Dk. Magufuli ni njia bora ya kuhakikisha madini yanainufaisha jamii kwa kuondoa umasikini na kuwa na jamii yenye kupata huduma bora katika nyanja zote za maisha,"amesema.

Amesisitiza ni kuwa, niwakati muafaka wa wananchi wa Kisarawe kutambua thamani ya madini yaliyopo katika kuongeza fursa za uchumi na maendeleo kwa kushirikiana na viongozi waadilifu, waanaojali uzalendo na wenye kutanguliza maslahi ya Taifa kwanza.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema niwakati sasa wa jamii yote ya Kisarawe kutambua kuwa fursa ya kuwepo madini ya aina tofauti wilayani humo ni mkombozi muhimu katika nyakati hizi ambazo Taifa la Tanzania linakua kiuchumi kwa kasi na kutumia rasilimali zake za ndani katika kukuza uchumi.

Mugabe: Mkoba wa rais wa zamani wa Zimbabwe uliojaa Dola za Marekani waibiwa

$
0
0
Watu watatu wamefikishwa mahakamani nchini Zimbabwe, wakishtakiwa kuiba mkoba uliokuwa na $150,000 (£117,600) pesa taslimu mali ya rais wa zamani wa taifa hilo Robert Mugabe.

Washukiwa hao wa wizi wanadaiwa kutumia pesa hizo kununua magari, nyumba na mifugo.

Jamaa wa rais huyo wa zamani, Constantia Mugabe, ni miongoni mwa walioshtakiwa, kwa mujibu wa taarifa katika vyombo vya habari vya serikali.

Mwanamke huyo anadaiwa kuwa na funguo za nyumba ya kijijini ya Bw Mugabe iliyo eneo la Zvimba karibu na mji mkuu wa Harare, na ndiye aliyewasaidia hao wengine kuingia humo na kufika ulikokuwa mkoba huo.

Washukiwa hao wengine walikuwa wameajiriwa kama wafanyakazi wa kufagia na kusafisha nyumbani humo wakati wa kutekelezwa kwa wizi huo siku moja kati ya tarehe 1 Desemba na mapema Januari.

"Johanne Mapurisa alinunua gari aina ya Toyota Camry... na nyumba ya $20,000 baada ya kisa hicho," mwendesha mashtaka wa serikali Teveraishe Zinyemba aliambia mahakama ya hakimu eneo la Chinhoyi."Saymore Nhetekwa alinunua gari aina ya Honda... na mifugo wengine wakiwemo nguruwe na ng'ombe wa thamani ambayo haijulikani."

Bw Mugabe, ambaye kwa sasa ana amiaka 94, aliondolewa madarakani na jeshi la Zimbabwe kwama 2017.Kufikia wakati wa kufurushwa madarakani, alikuwa amekaa madarakani kwa miaka 37, mwanzoni kama waziri mkuu na baadaye kama rais wa taifa hilo.

Wakati mmoja anakumbukwa kwa kusema kwamba taifa lolote lile haliwezi kufilisika.

Air Tanzania Ends Dominance, Debuts 2nd Airbus 220

$
0
0
By Special Aviation Correspondent, Montreal, 10-01-2019: 
TANZANIA is about to make history again, when its national airline, Air Tanzania, debuts the second Airbus 220 in a grand plan to consolidate its fleet, intensifying competition in the regional aviation business. 
Air Tanzania, continues to keep East Africans’ heads up. It is a growing airline that operates all new aircraft, solidifying its positioning deep in the pristine African skies.
Air Tanzania is the only African airline on the continent that flies Airbus’ newest product, A220 series. Aviation business experts sees an end to the dominance of giant airlines in the region.


This January 2019, hardly a month since the Air Tanzania became the first African airliner to introduce the airbus 220 in African skies, Tanzania brings its sister aircraft, right from the manufacturer’s workshop in Mirabel in Montreal. 
Tanzania's newest Airbus, thanks to President Magufuli's devoted axctions

Success Story
In December last year, Tanzania became the first nation in Africa and the fifth in the world to fly Airbus 220 in an ambitious and comprehensive programme to consolidate its airline business.
Three years on, Tanzania continue to witness rapid economic transformations in all key sectors of the economy. Business gurus would say, “it is the man on top.” 

This is correct, thanks to President John Pombe Magufuli who continues to introduce management efficiency in Tanzania, a new culture that transforms the continent right from Tanzania. Efficiency is the only credible way to deliver great results in both corporate world and in the running of governments. 

Tanzania and Africa are grappling with this challenge. Throughout his office tenure as Minister in three different ministries, Dr Magufuli is a proven performer and efficient administrator. 
Clearly, as in any corporate world, performance determines the future of the organization. Successful growth of the Tanzania’s flag carrier is, therefore, another pragmatic testament of Dr. Magufuli’s unbeatable record. 
Tanzania is the fifth fastest growing economy in Africa. It is also projected as the fourth fastest growing economy in the world for the next decade. Indeed this is a success story.
Airbus 220
The A220 is unrivalled passenger comfort aircraft with remarkable performance. It makes a lot of economic sense to operate the aircraft profitably. It has a seating capacity of above 130. It is 38.7m long and 11.5m wide. The wings extend to 35.1m and flies 5,920km without refueling. The aircraft’s fuel tanks host 21,918 liters. 

The airbus, already tried in Tanzania, provides unmatched fuel efficiency and environmental performance with fewer emissions. The passengers would enjoy more freedom with wide and comfortable seats. 

“This aircraft makes an excellent asset to further develop Air Tanzania’s business network,” says Tito Kasambala, CEO for the Government’s Flight Agency.

The plan works. Comparing to 2016 where the airliner had on only one aircraft with a market share of just 2.5 per cent, three years today, its market share has grown to hold 32 per cent.

Investments and Performance
The Government of Tanzania which owns the aircrafts and leases them out to Air Tanzania Corporation (ATC), has made significant investments in the past three years.

The sister Airbus 220 to be delivered, brings Air Tanzania’s active fleet to six. The fleet comprises three propeller-driven Bombardier Dash-8s, a Boeing 787 Dreamliner, and the two Airbus 220. 
The Government of Tanzania has pressed another order for two more aircrafts. They are expected to bring the fleet to 8.The aircrafts are Bombardier Q400 and Boeing 787 Dreamliner. The two jets are expected to be delivered by 2020. 
  
The Airline business could not always be an end in itself. It could be the means to an end. All large economies in the world were complemented by their airlines. It is hard to do without. 
Apart from improving the tourism industry, one of key stable sources of revenues, the airline would boost trade and investments. 

Air Tanzania’s contribution to trade, business, investments, diplomacy and branding cannot be played down. 
The model is proven right. Air Tanzania’s revenues doubled in less than three years of operation. The service demand is huge and continues to grow. The number of passengers has increased tremendously. The airline flies 432,000 passengers per year up from 48,000 in 2015. 
“When we talk of Magufuli’s incredible performance, we do not blow things out of proportions. Plenty of evidence is all around for the world to verify. The new era most of us waited for too long is finally here,” says Rosemary John, a nursing practitioner. 

Air Tanzania resumes International Flights in 10 years
Air Tanzania resumed international flights in September last year (2018), the first time in nearly 10 years. 

Air Tanzania now flies to Bujumbura, Entebbe and Moroni. President Magufuli, the brain behind these achievements, says more international routes (out of Africa) were in pipeline. They include Bombay (India), Bangkok (Thailand), Guangzhou (China), United Kingdom and others to be announced later. 

Tanzania is ready for Change to serious business 
“This is a clear testimony of our resolve as a people; that Tanzanians are capable of making things happen,” President Magufuli says. 

When sworn in office on 5 November 2012, Tanzania’s flag carrier, Air Tanzania, had only one aircraft with barely 50 seating capacity. Today, a number of active fleet is six and growing.

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA WAZIRI MHAGAMA OFISI ZA PSSSF NA NSSF MOSHI

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Mghwira wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli kwa mifuko ya hifadhi ya jamii NSSF na PSSSF aliyoyatoa Desemba 28, 2018 alipokutana na viongozi wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (kulia) akimsikiliza Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF Bi. Neema Kuwite wakati wa ziara yake katika ofisi hizo Januari 10, 2019.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akimsalimia Bi.Mary Kiramvu  mmoja wa wastaafu waliojitokeza kuhakiki taarifa zake katika Ofisi za PSSSF Moshi ikiwa ni utekelezaji wa majukumu ya Mhe.Rais alipokutana na viongozi wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akifurahi na baadhi ya wastaafu walioripoti katika ofisi za PSSSF Moshi wakati wa zoezi uhakiki wa taarifa za uanachama ili kubaini wastaafu hewa.
 Baadhi ya wastaafu wakijaza fomu za taarifa zao wakati wa zoezi la uhakiki katika ofisi za PSSSF Moshi  mkoani Kilimanjaro Januari 10, 2019.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo na baadhi ya wastaafu wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa maagizo ya Mhe.Rais  Dkt. John Magufuli kwa mifuko ya NSSF  na PSSSF.
 Meneja wa Mfuko wa Hifadhi wa NSSF Tawi la Moshi Bi.Mary Onesmo akimuonesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama namna huduma zinavyotolewa katika madirisha ya kusikiliza wastaafu katika Ofisi hizo alipotembelea Januari 10, 2019.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya jamii NSSF Bw.William Erio (katikati) akieleza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama wakati wa ziara yake katika Ofisi za NSSF Moshi.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiangalia namna watumishi wa NSSF wanavyotoa huduma kwa wateja wao wakati wa ziara yake katika Ofisi hizo Moshi Mjini.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya jamii NSSF Bw.William Erio maelezo ya ufafanuzi kuhusu mifuko ya Hifadhi nchini kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama alipotembelea Mfuko wa NSSF Moshi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (wan ne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Serikali pamoja na wale wa mifuko ya Hifadhi wakati wa ziara yake katika ofisi za Moshi mkoani Kilimanjaro.Kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya jamii NSSF Bw.William Erio
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

MBUNGE NA MWAKILISHI WA JIMBO LA KIEMBESAMAKI WAWEKA TAA KIWANJA CHA MPIRA CHA KWALA KILIOPO MOMBASA KWA MCHINA UNGUJA.

$
0
0
Khadija Khamis – Maelezo  Zanzibar
Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Ibrahim Raza amesema ushirikiano wa wananchi na viongozi wa jimbo ndio hatua bora inayoleta ufanisi wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya kuhakikisha ahadi zilizotolewa zinatekelezwa kwa vitendo. Aliyasema hayo huko katika kiwanja cha mpira cha Kwala, Mombasa, wakati akizungumaza na waandishi wa habari walipofika kuangalia Taa zilizowekwa katika kiwanja hicho na kukiwezesha kutumika wakati wa usiku

Taa hizo zimewekwa kwa ajili ya kuwapa fursa vijana kucheza wakati wote na kukuza vipaji walivyanavyo na hatimae kupata nafasi ya usajili kwa vilabu vikubwa.  Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe samaki Mahamoud Thabit Kombo alisema baada ya kiwanja hicho kuwekwa taa, wanampango wa kukiimarisha zaidi kwa kukiweka nyasi badia.

Alisema lengo ni kuimarisha michezo katika jimbo la Kiembesamaki ikiwa ni moja ya njia ya kutengeneza ajira kwa vijana na kuwaepusha na vitendo viovu. Aliwataka vijana wanaoishi karibu na kiwanja hicho kuwa walinzi wa raslimali iliyowekwa ili kidumu kwa muda mrefu na kiweza kutumiwa na vizazi vya sasa na vinavyokuja

Mwenyekiti wa C.C.M Jimbo la Kiembe Samaki Ramadhani Mrisho Rupia alisema kuimarisha michezo ni moja ya ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kuwasaidia vijana kujiajiri kutokana na vipaji walivyonavyo. Taa za kiwanja cha mpira cha Kwala zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi Februari 22, mwaka huu kwa mechi maalum itakayofanyika wakati wa usiku.

Nae kijana Nasir Ali Hemed  Mkaazi wa kwa Mchina ambae ni mmoja ya vijana wanaotumia kiwanja cha Kwala , alisema amepata faraja  kuona viongozi wao wametekeleza ahadi zao kwa vitendo. Aliwaomba viongozi wa Jimbo hilo kuwapatia mashine ya kukoshea gari (Presha Pampu) ili vijana waweze kujiajiri wenyewe. Jumla ya shiling milion 20 zimetumika kwa ajili ya kuweka miundombinu ya umeme katika kiwanja hicho.
Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki ambae pia ni Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo na Mbunge wa Jimbo hilo Ibrahim Raza pamoja na Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Kiembesamaki Ramadhan Mrisho Rupia wakizungumza na wandishi wa habari walipokua wakikagua kiwanja cha Mpira cha Kwala Mombasa Kwamchina kilichowekwa Taa. Picha na Makame Mshenga.
 Mbunge wa Jimbo la Kiembesamaki Ibrahim Raza akizungumza na vijana wa Jimbo hilo alipofika kukagua Taa zilizowekwe kwenye uwanja wa Mpira wa Kwala Mombasa kwa Mchina Mjini Unguja. 
 Kijana Nasir Ali Hemed akiwashukuru Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki kwa kutekeleza ahadi zao walizoweka wakati wa kampeni. 
  Muonekano wa kiwanja cha mpira cha Kwala na moja ya Taa zilizowekwa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki ikiwa ni miongoni mwa ahadi walizozitoa wakati wa Kampeni. 

Mambo ya kutarajia katika sekta ya biashara za mtandaoni 2019

$
0
0
Kwa mujibu wa mtandao wa Statista, mpaka kufikia mwaka 2021 mauzo yatakayotokana na biashara za mtandaoni yatafikia Dola za Kimarekani trilioni 4.88. Kiasi hiko kitakuwa ni maradufu ya sasa ambapo mauzo yaliyopatikana kwa mwaka 2018 ni Dola za Kimarekani trilioni 2.84. 

Hii inaasharia kukua kwa sekta hii pamoja na kutengeneza faida kubwa kwa wauzaji wa bidhaa mbalimbali kwa njia ya mtandao duniani. 

Kasi ya ukuaji wa biashara za mtandaoni inaenda sanjari na maendeleo ya sayansi na teknolojia yanayopelekea tabia za wateja kubadilika kwa kasi. Wateja wa sasa wamekuwa na tabia tofauti ukilinganisha na awali ambapo hakukuwepo na matumizi ya mifumo ya kidigitali.

Mifumo ya kidigitali imebadili kwa kiasi kikubwa tabia za wateja ambapo watoa huduma hawana budi kubadilika ili kuendana nao. Kwa mfano, sasa hivi mtu anaweza kufanya shughuli tofauti akiwa eneo moja. Malipo ya huduma mbalimbali kwa kutumia simu ya mkononi kama vile ada, umeme, visimbuzi, maji, faini, benki, leseni na mengineyo yanawezekana bila ya kwenda moja kwa moja kwenye ofisi za watoa huduma. Pia, mtu anaweza kuwa ofisini akiendelea na shughuli zake lakini akafanya huduma za manunuzi, malazi na hata kuagiza chakula pale pale alipo.

Siku za hivi karibuni biashara nyingi zimekuwa zikikumbwa na changamoto ya kupokea idadi ndogo ya wateja wanaotembelea madukani mwao. Sababu kubwa iliyopelekea hili kutokea ni kutokana na kuibuka kwa sekta ya mtandaoni ambayo huwapatia wateja uwezo wa kupata huduma na bidhaa tofauti kwa urahisi na haraka ndani ya muda mfupi. Hivyo basi, imekuwa ni vigumu kwa wafanyabiashara wasiotaka kubadilika kushindana na mahitaji ya sasa ya wateja.

Tunapouanza mwaka mpya wa 2019, Jumia inawashauri wafanyabiashara kuwa hawana budi kutumia fursa zote za kiteknolojia zinazopatikana kwa sasa ili kukuza biashara zao na kupata faida zaidi. Tanzania kwa sasa ina watumiaji wa simu za mkononi zaidi ya milioni 40, kati yao zaidi ya milioni 23 wanatumia huduma ya intaneti. 

Pongezi kubwa kuendelea kuongezeka kwa uwekezaji kwenye sekta za mitandao ya mawasiliano ya simu, makampuni ya uuzaji wa simu pamoja na watoa huduma wa intaneti kwa kuchochea kwa kiasi kikubwa watanzania wengi kuweza kutumia huduma za simu na intaneti.

Kutokana na upatikanaji wa huduma za intaneti hususani kupitia simu za mkononi miongoni mwa watanzania wengi, kumepelekea shughuli nyingi kufanyika mtandaoni. Asilimia kubwa ya wateja hivi sasa wakihitaji bidhaa au huduma yoyote ni rahisi kwa wao kuingia mtandaoni kupitia simu zao za kiganjani kupata taarifa zaidi kabla ya kufanya maamuzi ya kufanya manunuzi.

Hivyo basi, wafanyabiashara hawana budi kuwa na uwepo wa kutosha mtandaoni. Hapa inamaanisha kuwa na tovuti, kufungua akaunti katika kurasa tofauti za mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Instagram, Youtube na hata blogu kama ikiwezekana. 

Uwepo tu mtandaoni hautoshi endapo hakutokuwa na taarifa za kutosha zinazoendana na wakati. Imekuwa ni kasumba kwa wafanyabiashara wengi kuwa na kurasa za mitandao ya kijamii au tovuti lakini taarifa nyingi si sahihi au zimepitwa na wakati. Hivyo, hakikisha kunakuwa na taarifa za kutosha, sahihi na zinazokwenda na wakati ili kujibu maswali yote ya mteja atakayokuwa nayo. 

Kingine ambacho wafanyabiashara wanatakiwa kukizingatia kwa umakini ni kutambua wateja wao wanataka nini. Wateja wengi wa sasa hivi ni werevu na wanakwenda na wakati. Takribani kila mteja anapendelea bidhaa au huduma atakayoiona mtandaoni apalekewe mpaka pale alipo, tena kwa ubora na sifa zilezile kama alivyoziona mtandaoni. Hii itapelekea kujenga imani baina ya mfanyabiashara na mteja kuendelea kununua bidhaa siku zijazo.

Yapo mengi ya kutarajia katika mwaka huu kwa upande wa biashara kwa njia ya mtandaoni, pengine kwa kufanya tathmini ya ndani utakuwa umegundua ni vitu gani zaidi vya kufanya marekebisho. Je, ni kwa upande wa bidhaa? Huduma kwa wateja? Huduma baada ya mauzo? Au pengine namna za malipo wanazopendelea wateja? Ni lazima kuyazingatia yote haya ili kuwa na mwaka wenye mafanikio zaidi.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AZINDUA JENGO LA TAASISI YA UTAFITI WA AFYA ZANZIBAR

$
0
0
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Hussein Ali Hassan amesema tafiti za kisayansi za Afya zinasaidia kujua chanzo cha maradhi na tiba yake ikiwemo matumizi ya dawa asilia. Dk.Husein alieleza hayo Binguni Wilaya ya Kati Unguja wakati wa Ufunguzi wa Jengo la Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI) ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema tafiti za kisayansi ya afya katika nchi zinamchango mkubwa katika kupunguza maradhi kwani baadhi ya maradhi yanaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kutumia vyakula vya kawaida bila kutumia dawa za Hospitali. Aliwataka wananchi kupokea matokeo ya tafiti zitakazofanywa na Taasisi hiyo na Taasisi nyengine ili kuleta mabadiliko katika maisha yao.

Dkt. Hussein aliwashauri wataalamu wa Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar kufanyakazi kwa juhudi na maarifa na  kuhakikisha mimea na dawa za asili zinazotumika kwa ziko katika hali ya usalama kwa matumizi ya binaadamu. Alieleza kuwa shabaha ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kumkomboa mwananchi na madhila mbali mbali yakiwemo maradhi na kuwafanya wawe na afya bora.  

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Asha Ali Abdalla lisema lengo la kuanzishwa Taasisi hiyo ni kufanya tafiti kujua ukubwa na chanzo cha maradhi maradhi na kushirikiana na Taasisi nyengine kutoka nje ili kupata tiba sahihi. Alisema zaidi ya shiling million mia mbili zimetumika katika ujenzi wa jengo la Taasisi ya Utafiti ya afya Zanzibar lenye wafanyakazi 21 na mipango ya kuajiri wataalamu wa fani ya utafiti zinaendelea kuchukuliwa ili kiweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Mashavu Sukwa aliitaka Wizara ya Afya kuangalia uwezekano wa kuwachukua wananchi wa karibu kufanyakazi ndogo ndogo zisizohitaji utaalamu katika Taasisi hiyo na kushirikishwa katika ujenzi wa hospitali ya rufaa itakayojengwa kijijini hapo.

“Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja wapo tayari kufanyakazi mbalimbali wakati wa ujenzi wa Hospitali ya Binguni kwani wako imara katika kazi zinazohitaji nguvu," alisema Mkuu wa Wilaya ya Kati. Mfamasia Mkuu wa Serikali Habibu Ali Sharifu alisema suala la utafiti linawahusu wananchi wote wa Zanzibar hasa katika  kupunguza matumizi ya dawa bila mpangilio na hatimae kusababisha athari.

Aliwashauri wananchi wa Binguni kutoa ushirikiano kwa Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar kwani wanamchango mkubwa kufanikisha kazi za Taasisi hiyo. Alisema wananchi wakipewa  elimu ya matumizi ya njia mbadala za tafiti za kisayansi zitasaidia kuondoa mawazo potofu na kupata matokeo chanya ya tafiti zilizofanya na wataalamu.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Hassan akikagua jengo la Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar liliopo kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati baada ya kuluizindua rasmi ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Muonekana wa Jengo la Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI) liliopo Binguni ambalo lilifunguliwa rasmi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Hassan ikiwa miongoni mwa maadhimisho ya mika 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Asha Abdalla Juma akitoa maelezo ya ujenzi wa Jengo la Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI) na kumkaribisha Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Hassan kuzungumza na wananchi baada ya kulizindua jengo hilo katika kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Hassan akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa Jengo la Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI), katika kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Binguni walioshiriki uzinduzi wa Jengo la Taasisi ya Utafiti wa Afya (ZAHRI) wakimsikiliza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Hassan (hayupo pichani)  
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Hassan (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI) baada ya kulizindua jengo hilo katika kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati. 

AKINAMAMA WALIOJIFUNGUA 67 PAMOJA NA WATOTO WACHANGA 475 WAMEFARIKI MKOANI PWANI KUTOKANA NA UZAZI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2018

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 
JUMLA ya watoto wachanga 475 wamefariki dunia baada ya akinamama 41,064 kujifungua mkoani Pwani, mwaka 2018 ,hali ambayo inaonyesha idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi kimkoa bado ipo juu. Aidha kati ya akinamama hao 41,064 waliojifungua akinamama 67 walifariki dunia kutokana na uzazi. 

Hayo yalisemwa na mganga mkuu wa mkoa wa Pwani, dokta Gunini Kamba wakati mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo aliposaini hati ya makubaliano na wakuu wa wilaya ya kampeni ya kuzuia vifo vya uzazi, kampeni ambayo itafanyika kwa miezi 12 nchini. Alisema, vifo vya watoto wachanga na akinamama wanaojifungua hali hairidhishi hivyo kampeni hiyo itasaidia kupunguza idadi hiyo. 

Kamba alisema, lengo hilo linaweza kufikiwa endapo akinamama watafuata maelekezo ya kiafya wanayopatiwa wakati wa uzazi ili waweze kuvuka salama katika kipindi cha uzazi. "Vifo 67 kwa waliojifungua na watoto wachanga 475 ukilinganisha na malengo ya Kitaifa bado hali sio nzuri sana "alisisitiza Kamba. Pamoja na hayo Kamba aliwataka ,akinamama wajawazito kuhakikisha wanaanza klinik ndani ya miezi 12 ya kwanza ili kujua afya zao. 

Pia waendelee na kufuatilia afya zao kulingana na utaratibu watakaopatiwa hadi wakati wa kujifungua bila kupuuzia. "Na wakijifungua inapaswa kuhakikishwa ndani ya lisaa limoja baada ya kujifungua mtoto anyonye "alifafanua Kamba. Awali mkuu wa mkoa wa Pwani, Ndikilo aliwaasa wakuu wa wilaya kwenda kusimamia malengo hayo ili kufanikisha kampeni hiyo kiwilaya, mkoa na Taifa kijumla. 


RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA SUNIL MITTAL MWENYEKITI WA BHARTI AIRTEL IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel  ( kampuni ya Simu ya Airtel ) mara baada ya kuwasili kwaajili ya mazungumzo , Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel  ( kampuni ya Simu ya Airtel ) Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba John Mwaluko pamoja na mwakilishi kutoka kampuni ya Bharti Airtel. Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel aliyeambatana na ujumbe wake kutoka kampuni ya Simu ya Airtel pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba John Kabudi, Gavana wa BOT Profesa Luoga, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James, Mtendaji mkuu wa kituo cha Uwekezaji (TIC ) Geoffrey Mwambe  pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL  Mhandisi Omary Nundu. Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma taarifa ya majadiliano kutoka kwa mgeni wake Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel ( kampuni ya Simu ya Airtel ) mara baada ya Mazungumzo yao . Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel aliyeambatana na ujumbe wake kutoka kampuni ya Simu ya Airtel pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba John Kabudi, Gavana wa BOT Profesa Luoga, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James, Mtendaji mkuu wa kituo cha Uwekezaji (TIC) Geoffrey Mwambe  pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL  Mhandisi Omary Nundu, Mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Mwenyekiti wa Bharti Airtel (kampuni ya Simu ya Airtel) Bw. Sunil Mittal akizungumza na Wana habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo  yao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wana habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo  yao na Mwenyekiti wa Bharti Airtel (kampuni ya Simu ya Airtel) Bw. Sunil Mittal, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11, 2019.
PICHA NA IKULU

KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI YAFANYA KIKAO JIJINI DODOMA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda  na Kimataifa, Dkt. Damas Ndumbaro akiwasilisha Taarifa ya Wizara yake kuhusu Utekelezaji wa afua za UKIMWI mahali pa kazi kwa wizara na namna inavyoshirikiana na Mataifa mengine katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI, Mhe. Oscer Mukasa akiongoza kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masula ya UKIMWI, wakiwa katika kikao kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kamati hiyo ilipokea na kujadili Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa kuhusu Utekelezaji wa afua za UKIMWI mahali pa kazi kwa wizara na namna inavyoshirikiana na Mataifa mengine katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masula ya UKIMWI, wakiwa katika kikao kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kamati hiyo ilipokea na kujadili Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa kuhusu Utekelezaji wa afua za UKIMWI mahali pa kazi kwa wizara na namna inavyoshirikiana na Mataifa mengine katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya

NEWZ ALERT: BOSI WA ZAMANI TRA NA WENZAKE ,MTUHUMIWA WA KUiIBIA SERIKALI MIL 7 KWA DAKIKA WAACHIWA HURU,WAKAMATWA TENA

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia kesi ya utakatishaji fedha  aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya, na wenzake wawili kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea na kesi  hiyo.

Pia Mahakama hiyo imemfutia kesi mfanyabiashara aliyewahi kutajwa na Rais John Magufuli kuiibia serikali Mil.7 kwa dakika, Mohamed Yusufal na wenzake kwa sababu DPP hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Kesi hizo zote zimefutwa mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mbando baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Hashim Ngole kueleza kuwa kesi hizo leo zilikuja kwa  kutajwa.

Wakili Ngole ameeleza kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashauri hayo kwa kutumia kifungu cha 91(1) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 marejeo ya mwaka 2002.

Kifuatia taarifa hiyo, Hakimu Mmbando ameziondoa kesi hizo mbili.
Hata hivyo, baada ya kutoa uamuzi huo washtakiwa wote walikamatwa na sasa wako ndani ya ukumbi wa wazi wa mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando wakisomewa mashtaka mapya.

 Kitilya anashtakiwa pamoja na aliyekuwa miss Tanzania (1996), Shose Sinare na Ofisa wa benk ya Stanbic Sioi Solomon.

Katika kesi ya awali, washtakiwa walikabiliwa na makosa ya utakatishaji fedha, kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka kiasi cha Dola za Marekani Milion 6 katika akaunti tofauti tofauti  za benki ambapo inadaiwa walitenda makosa hayo kati ya March 2013 na September 2015.

UJIO WA NDEGE AIRBUS 220-300 MAPOKEZI YAMEDAMSHI...SHANGWE TUPU UWANJANI,NDEGE KUTUA SAA 8:30

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SHANGWE,nderemo na vifijo vimetawala katika Uwanja wa Ndege jijini Dar es Salaam wakati wa Watanzania zaidi ya milioni 50 wakiangalia angani wakisubiri kuipokea ndege mpya ya Airbus 220-300 inayowasili leo mchana huu.

Mamia ya wananchi wamejitokeza kwa ajili ya kushuhudia ujio wa ndege hiyo ambapo pia viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwamo mawaziri wamewasili uwanjani hapo.

Kwa mujibu wa ratiba ambayo imetolewa kuhusu ujio wa ndege hiyo inaeleza kuwa  Rais Dk.John Magufuli atawasili uwanjani hapo saa nane kamili mchana.Na kabla ya hapo atawasili Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Baada ya viongozi hao kuwasili utaimbwa wimbo wa Taifa na kisha itafuata dua kutoka kwa viongozi wa dini  .Kwa mujibu wa ratiba itafuata hatua ya kutambulisha viongozi wa ngazi mbalimbali.

Itakapofika saa 8:30 hadi 8:40 ndege itawasili na kisha kupokea water Salute na baadae itafuata taarifa ya ndege.Saa 8:50 hadi 9:00 ndege itazinduliwa na baada ya hapo yatafanyika makabidhiano.

Kutakuwa na maelezo ya Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano ambaye atamkaribisha mgeni rasmi .Saa 9:20 Rais Magufuli atazungumza na watanzania kupitia hotuba yake atakayoitoa uwanjani.

Mtanzania angalia angani...Endelea kufuatilia Michuzi Blog na Michuzi Tv kwa taarifa mbalimbali zinazoendelea kuhusu ujio wa ndege hiyo.

Tamthilia ya “Wildflower” Inarejea kwa Msimu wa pili kwenye ST Novela E Plus

$
0
0
Tamthilia kali ya Wildflower inarudi tena kwenye king’amuzi cha StarTimes. Msimu wa pili wa tamthilia hiyo ya kifilipino utaanza kuonekana Usiku wa Januari 20 mwaka huu kupitia ST Novela E Plus pekee. 

Wildflower ni miongoni mwa tamthilia zilizofanya vizuri zaidi nchini Ufilipino katika mauzo pamoja na kupokelewa vizuri na watazamaji na pia Msimu wake wa kwanza ulifanya vizuri sana kwa nchi za Afrika mwaka jana.

“Tulifahamu kwamba Wildflower ni tamthilia nzuri ila hatukujua kwamba ingefanya vizuri kuliko tamthilia zote. Mashabiki na wafatiliaji wa tamthilia hii wamekuwa wakiulizia msimu wa pili tangu msimu wa kwanza ulipoisha”. Zamaradi Nzowa,  Meneja Maudhui StarTimes. “Tunafurahi sana kuanza mwaka 2019 kwa kuwaletea tamthiliya hii, niamini napokwambia, kama uliupenda Msimu wa kwanza basi huu wa pili ni kiboko zaidi”. Aliongeza.

Muhusika mkuu kwenye tamthiliya, Maja Salvador anashukuru tamthilia hiyo kupokelewa vizuri na watazamaji. “Tungependa kuwashukuru watazamaji wetu kwa upendo na kuipokea vizuri tamthiliya yetu kwa msimu wa kwanza. Msimu huu wa pili tunawaahidi mambo makubwa na visa mbalimbali. Tuna imani mtaendelea kutuunga mkono,” Maja alisema kwenye mahojiano.

Tamthiliya ya Wilflower inatengenezwa na ABS-CBN, ni kisa kinachomuhusu mwanamke mwenye Ujasiri, malengo na ustahimilivu wa kutafuta haki kwa ajili ya familia yake na watu wa mji wake. Akisukumwa na upendo na matumaini, mhusika mkuu Lily/Ivy anapigania kile anachokiamini bila kujichukulia sheria mkononi.

Mambo yatakuwa magumu kadri mvutano unavyozidi kuongezeka. Kufuatia kifo cha Nay Carlota, Ivy anazidi kushawishika kuwaangusha familia ya Ardiente. Ivy atafanya nini kupata haki ya Carlota? Hakuna cha kumzuia Diego kugombea ugavana wa Poblacion Ardiente dhidi ya kaka yake, Arnaldo. Je atashinda au atazungukwa na familia yake? Kwenye mapenzi, Arnaldo ataangukia mtego wa Ivy? Je Diego ataweza kutenganisha hisia zake kwa Ivy na wito wake?
Majibu ya maswali yote haya yapo ST Novela E Plus Ijumaa hadi Jumapili saa 2:50 Usiku, sehemu mbili kila siku kuanzia tarehe 20 Januari.

Tazama Coppa Italia kwenye StarTimes pekee

$
0
0
Ronaldo kuanza kazi dhidi ya Bologna Katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Coppa Italia ni timu mbili tu zinatoka Serie C huku zikikutana na vilabu kutoka jijini Roma, Novara watakaocheza dhidi ya Lazio huku Virtus Entella wakicheza dhidi ya AS Roma siku ya Jumatatu.

Timu nyingine ambayo haitokei Serie A ni Benevento ambao watasafiri kuelekea Milan ambako watacheza dhidi ya Inter. Huku ikitarajiwa kwamba vilabu vingi vikubwa vitashinda, mechi kati ya Bologna na Juventus itakuwa kivutio zaidi. Juventus tayari wako kileleni mwa Serie A wakiwa alama 9 mbele ya Napoli ambao wako nafasi ya pili.

Klabu hiyo ya jijini Turin itataka kujihakikishia ushindi dhidi ya Bologna ambao ni wa tatu kutoka mwoisho katika msimamo wa Serie A, ili wawe katika nafasi nzuri ya kushinda kombe hilo kwa mara ya 14.

Kikosi cha Massimilano Allegri bado hakijapoteza mchezo wowote katika ligi za ndani kwa msimu huu, huku kikosi chao kikiwa na utajiri hasa eneo la ushambuliaji wachezaji kama Cristiano Ronaldo, Paulo Dybala na Mario Mandzukic, itakuwa jambo la kushangaza endapo watapoteza mchezo huo licha ya kuwa ugenini.

Ronaldo amefunga jumla ya magoli 14 katika ligi, goli moja pungufu ya magoli ambayo kikosi kizima cha Bologna kimefunga (15), mreno huyo amekuwa katika kiwango kizuri tangu alipowakacha mabingwa wa Ulaya Real Madrid. Mchezo mwingine wenye burudani utapigwa jijini Genoa ambapo Sampdoria watacheza dhidi ya AC Milan siku ya Ijumaa.

Wapenzi wa Soka nchini wataweza kutazama mechi hizi kupitia StarTimes pekee. Mechi kati ya Bologna na Juventus itachezwa Jumapili saa 2 Usiku na kurushwa moja kwa moja kupitia ST World Football pekee, ambapo wateja watatakiwa kulipia kifurushi cha MAMBO Tsh 14,000 kwa watumiaji wa Antenna na SMART Tsh 21,000 kwa watumiaji wa Dish.

Wagonjwa 11 wafanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua

$
0
0
 Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kubadilisha valvu katika kambi maalum ya matibabu ya siku 12 inayoendelea katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.
 Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kubadilisha valvu kwenye  kambi maalum ya matibabu ya siku 12 inayoendelea  katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.
  Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani wakijadili maendeleo ya  wagonjwa waliolazwa katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) ambao wamefanyiwa upasuaji wa moyo. Jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu inayoendelea katika Taasisi hiyo na hali zao zinaendelea vizuri ambapo wengine wamesharuhusiwa kutoka  ICU  na kurudi wodini kwa ajili ya kuendelea na matibabu ikiwa ni pamoja na mazoezi.
Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kubadilisha valvu kwenye  kambi maalum ya matibabu ya siku 12 inayoendelea  katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.
Picha na JKCI

FAO Yaahidi Ushirikiano Zaidi na Serikali

$
0
0
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) limeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika kuiinua sekta ya kilimo nchini. Hayo yamesemwa na Ndugu muwakilishi wa Shirika hilo nchini Ndugu Fred Kafeero alipokutana na Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa katika ofisi za FAO jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho Ndugu Kafeero alieleza namna ambavyo shirika hilo limekuwa mstari wa mbele kushirikiana na serikali katika kutunga sera na kuandaa mikakati yenye lengo la kuhakikisha Tanzania inasonga mbele katika kilimo. Amesema FAO kwa miaka ya karibuni imefanya kazi kwa ukaribu na Shirika la Takwimu Tanzania (NBS) kwa kulijengea uwezo wa ndani unaoisaidia pia serikali katika ufuatiliaji wa bei ya mazao nchini.

Nae Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa alimueleza muwakilishi huyo mpango wa Serikali ya awamu ya tano wa kuorodhesha wakulima wote nchini ili kuweza kupanga vizuri kuhakikisha kila mkulima anapata huduma muhimu zitakazomsaidia toka hatua za uandaaji shamba mpaka masoko, na kuiomba FAO kama mdau muhimu wa kilimo kuipa Serikali ushirikiano ambapo Ndugu Kafeero aliahidi kulifanyia kazi ombi hilo.

Aidha, Naibu Waziri Bashungwa ameomba IFAD (shirika tanzu la FAO) isaidie Serikali kwa kushirikiana na  Benki ya Kilimo nchini kuwapatia wakulima nchini kupata mikopo ya riba nafuu, kusaidia taasisi za utafiti wa kilimo nchini, kujenga uwezo wa kuzalisha mbegu za mazao ya kimkakati na mchanganyiko, kujenga maghala ya kuhifadhi mazao ili kupunguza hasara wakati wa mavuno shambani (post harvest losses) na kuwajengea uwezo maafisa ugani nchini kufundisha kilimo cha tija kwa wakulima nchini. 

Mwakilishi wa FAO nchini amekubaliana na Naibu Waziri Bashungwa kufanyika kikao mwezi Februari 2019 cha Wizara ya Kilimo, FAO na mashirika mengine ya kimataifa yanayohusika na kilimo nchini kujadili vipaumbele tajwa ili kuijengea uwezo Wizara wa kuweza kuihudumia sekta ya kilimo nchini ili iendelee kukua na kutimiza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kufikia uchumi wa kati
 Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akizunguza na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) Ndugu Fred Kafeero na msaidizi wa mwakilishi huyo Ndugu Charles Tulahi katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam
 Mheshimiwa Innocent Bashungwa akimueleza muwakilishi wa FAO nchini mipango ya Serikali ya awamu ya tano katika kuinua kilimo
 Fred Kafeero akimkabidhi Naibu Waziri wa Kilimo baadhi ya machapisho yanayoonyesha mikakati ya FAO 
 Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akiagana na msaidizi wa muwakilishi FAO nchini Ndugu Charles Tulahi mara baada ya kumalizika kwa kikao
 Innocent Bashungwa akimsikiliza kwa makini muwakilishi wa Shirika la FAO wakati akimuelezea shughuli za shirika hilo
Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akiagana na msaidizi wa muwakilishi FAO nchini Ndugu Charles Tulahi mara baada ya kumalizika kwa kikao

ASKOFU KAKOBE ASHINDWA KUVUMILIA,AKIRI KUTAMBUA KAZI KUBWA INAYOFANYWA NA RAIS

$
0
0
*Asema pamoja na ubishi wake lakini amethibitisha Rais Magufuli anastahili sifa,heshima

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

ASKOFU Zacharia Kakobe amesema Rais Dk.John Magufuli anafanya mambo makubwa kiasi cha kwamba amemkosha na kwamba pamoja na ubishi wake kwa sasa anakubali kazi ambayo inafanywa na Rais.

Amesema hayo leo wakati amepata nafasi ya kuomba dua ambapo kabla ya kuomba alianza kwa kuzungumza kutoa la moyoni ambapo amekiri yeye ni mgumu wa kukubali lakini hakika Rais Magufuli anafanya mambo makubwa katika nchi na anastahili kupongezwa.

"Mimi pamoja na ubishi wangu lakini niseme hadharani nimekukuwa lakini sasa nimekubali.Niseme amenikosha.Maandiko ya Biblia yanasema huwezi kupendwa na kila mtu.

"Ukiona unapendwa na watu wote ujue kuna shida.Pamoja na hayo niseme kazi ambayo unaifanya kwa ajili ya nchi yetu unastahili sifa na heshima.Wapo wanaosema ndege zinatokana na kodi zetu wafahamu tunaye Rais ambaye anatuongoza na kufanya mambo makubwa ndani ya nchi yetu,lazima tukusifu na kukuheshimu," amesema Askofu Kakobe mbele ya Rais Magufuli.


Balozi Seif aongoza matembezii ya miaka 55mya Mapinduzi ya Zanzibar

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema Vijana walioshiriki matembezi ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar wanapaswa kujenga ufahamu wa kujuwa Mapinduzi ndio yaliyoleta Ukombozi na kupatiana Mamlaka kamili ya Mwafrika yanayoharakisha Maendeleo ya Jamii hivi sasa.

Alisema jukumu la Vijana hao kwa wakati huu waelewe kwamba Uhuru wa Taifa hili wakati wowote utalindwa na wao wenyewe kwa vile hakuna Mtu au Kikundi kitakachokuja Zanzibar na Tanzania Nzima  kuwalindia Uhuru walioachiliwa kama urithi wao.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akiyapokea na kuyafunga Matembezi ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi {UVCCM} ya kuunga mkono Mapindui ya Zanzibar ya Mwaka 1964 yaliyohitimishwa hapo katika Uwanja wa Gombani ya Kale Chake Chake Kisiwani Pemba.

Alisema Vijana hao ndio warithi halali wa Mapinduzi hayo kwa sababu Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 yalifanywa na Vijana chini ya Viongozi wa ASP Youth Leagae kwa wakati huo wakitekeleza Muongozo wa Afro Shirazy Party uliolenga kuondoa matendo mabaya, madhila na manyanyaso kwa Waafrika wa Zanzibar.

Balozi Seif aliwataka Vijana hao kuziepuka fitina za kudharauliana wenyewe kwa wenyewe na badala yake waimarishe Umoja na Mshikamano waliokuwa nao miongoni mwao na kamwe wasikubali kutenganishwa kwa vile makundi ni sumu ya Umoja wao.

Alieleza kwamba Waafrika wa Zanzibar baada ya kuchoshwa na Utawala wa Kikoloni waliendelea kushikamana , kuungana kuwa wamoja  kulikowasaidia kuikomboa Nchi yao toka mikononi mwa wageni kwa nia ya kujitawala na kujiamulia mambo yao wenyewe katika Ardhi yao.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM Taifa alifahamisha kwamba wakati wananchi na Viongozi wanaposema Mapinduzi Daima inamaanishwa kwamba Serikalki itaendelea kuondoa matendo mabaya, udhalilishaji wa Wanawake na Watoto pamoja na mambo yote yanayorejesha nyuma  au kukwamisha juhudi za kujiletea Maendeleo.

Balozi Seif alielezea faraja yake kutokana na ushiriki wa Vijana kwenye Matembezi  hayo ukiwa  mkubwa jambo ambalo linadhihirisha wazi jinsi gani walivyokomaa Kisiasa pamoja na utayari wao wa kutetea, kulinda na kuyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar  kwa vitendo.

Alisema Nchi imetoka mbali kutokana na majaribu mengi iliyopata zilizotokana na changamoto nyingi zinazoonekana kusababishwa na wale wasioitakia mema ambao ni vibaraka wa hao waliopinduliwa Mwaka 1964.

Aliwapongeza Vijana wa kuendelea kulinda Amani ya Taifa huku wakitambua kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zimepiga hatua kubwa ya Maendeleo kutokana na  Amani hiyo.

Balozi Seif Ali Iddi akiwa pia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliendelea kuwakumbusha Wananchi kushiriki sherehe za Mapinduzi katika misingi ya Amani na utulivu kama ilivyozoeleka.

Alisema ni vyema kwa Mtu au Kikundi chochote kilichotia niya ya kushiriki sherehe hizo katika mazingira ya kutaka kufanya ushawishi wa vurugu Vyombo vya Dola havitakuwa na mzaha wa kuwadhibiti watu hao hao.

Akitoa Taarifa ya Matembezi  hayo ya Umoja wa Vijana wa CCM Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Nd. Mussa Haji Mussa alisema matembezi hayo yaliyozinduliwa Tarehe 5 Januri na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdullah Juma Saadala katika Kijiji cha Chokocho Mkoa Kusini Pemba.

Nd. Mussa alisema zaidi ya Vijana 400 walishiriki matembezi hayo kwa kuamua kubadilika katika kushiriki zaidi kwenye kazi za Jamii ikiwemo ujenzi wa Taifa wa  Majengo ya Skuli na Matawi ya Chama cha Mapinduzi kwa kuweka alama mote walimopita.

Alisema Umoja wa Vijana utaendelea kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa gharama yoyote ile na kamwe hakutakuwa na Mapinduzi mengine tena kwa vile kila Mwana jamii ameshuhudia kuwa huru kufanya analotaka kwa mujibu wa sheria.

Nd. Mussa alieleza kwamba Mapinduzi hayo ya Zanzibar yameleta utu na usawa wa Wananchi wote wa Zanzibar licha ya baadhi ya Wanasasa uchwara wakijaribu kudhihaki Mapinduzi hayo.

Akimkaribisha Mgeni rasmi kuyafunga matembezi hayo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Nd. Kheri Denis James alisema Vijana wa CCM wana jukumu la kutangaza kazi kubwa inayoendelea kutekelezwa na Marais wote wawili wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Nd. Kheri alisema tafsiri sahihi ya Mapinduzi Daima inayoendelea kutekelezwa hivi sasa imelenga katika kuimareisha Uchumi na Maendeleo ya Taifa ambayo Vijana wanalazimika kupigana kiume katika kuyalinda Maendeleo pamoja na Uchumi huo.

Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa aliwaeleza Washiriki wa Matembezi hayo kwamba Wazee Waasisi wa Bara na Zanzibar waliacha Vyama vyenye nguvu kubwa  Vya TANU na ASP na baadae CCM zinazopaswa kudumishwa kwa ustawi wa Kizazi kijacho.

Ujumbe wa Mwaka huu wa Matembezi hayo ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi {UVCCM} ya kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar YA Mwaka 1964 unaeleza kwamba “ CCM na Vijana Mapinduzi yanaendelea kufana”.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif  akiwa pamoja na Viongozi wa UVCCM Wakijiandaa kuyapokea Maandamano ya Umoja wa Vijana wa CCM kuadhimisha kumbukumbu za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 hapo Uwanja wa Gombani ya Kale Chake Chake Pemba.
Kanyaga kanyaga ni nyimbo wanaoimba Vijana hao wa UVCCM wakati wakiingia kwenye Uwanja wa Gombani ya Kale baada ya kumaliza Matembezi yao katika sehemu mbali mbali za Kisiwa cha Pemba.
Vijana wa UVCCM  wakionekana kuhamasika na umalizaji salama wa Matembezi yao ulioambatana na kazi za kujitolea  katika Miradi ya Kijamii na Kisiasa.
 Balozi Seif  akimpongeza Kiongozi wa Matembezi ya UVCCM Abdullah Ali Chum { Koti } baada ya kukabidhiwa  salama Picha ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Dr. John Pombe Magufuli iliyotumika kwenye Matembezi hayo.
Vijana wa matembezi ya kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 wa UVCCM wakifurahia na kushukuru huduma nzuri za Afya na lishe walizozipata wakati wa Matembezi yao ya Siku Tano Pemba.
Baadhi ya Vijana wa UVCCM wakifuatilia matukio mbali mbali yaliyokuwa yakifanyika katika Uwanja wa Michezo wa Gombani ya Kale wakati wa kuhitimisha Matembezi yao yaliyoanzia katika Kijiji cha Chokocho Mkoa wa Kusini Pemba.
Balozi eif akikabidhi Vyeti Maalum kwa Vijana wa UVCCM walioshiriki matembezi ya kumbukuimbu ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 yaliyomng’oa Mkoloni katika Ardhi ya Visiwa vya Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa (UVCCM ) Mkoa wa Kibaha  Azilongwa Bohari akipokea Cheti Maalum kwa niaba ya Washiriki wenzake  cha Kuchiriki Matembezi hayo. Picha na – OMPR – ZNZ.

WAWILI WONGEZWA KESI YA KITILYA, WAACHIWA HURU NA KUKAMATWA TENA. WASOMEWA MASHTAKA MAPYA 58

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imemsomea mashtaka mapya 58 yakiwemo ya utakatishaji  fedha na kuisababishia serikali hasara ya dola milioni sita aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake wawili ambao ni, aliyekuwa Miss Tanzania 1999 Shose Sinare na Sioi Solomon baada ya mapema leo asubuhi kuwafutiwa mashtaka nane yaliyokuwa yanawakabili.

Hata hivyo katika mashtaka mapya TAKUKURU imewaongeza watuhumiwa wawili kwenye kesi hiyo ambao ni  Bedason Shallanda  ambaye ni Kamishina wa  uchambuzi wa  madeni kutoka Wizara ya Fedha  na msaidizi wake Alfredy  Misana.

Katika kesi hiyo mpya washtakiwa wanakabiliwa na  na mashtaka matatu ya kughushi, mashtaka mawili ya kutoa nyaraka za uongo, shatka moja la kujipatia pesa takribani dola milioni mia sita kwa njia za udanganyifu shtaka moja la kutoa nyaraka za uongo kwa lengo la kumdanganya Katibu Mkuu Wizara ya fedha, shtaka moja la kuongoza uhalifu, mashtaka 49 ya  utakatishaji fedha na shtaka moja la kuisababishia Serikali hasara ya dola milioni  sita.

Akisoma mashtaka hayo wakili wa wa Serikali Mkuu Hasan Ngole amedai mbele ya hakimu mkazi mwandamizi Agustina Mmbando ,kuwa kati ya Machi 15,2013 na Januari 10 2014 ndani ya jiji la Dar es salaam kwa nia ya kudanganya washtakiwa wote walijipatia USD milioni sita kutoka Serikali ya Tanzania wakionyesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji wa upatikanaji wa mkopo na zililipwa  kupitia kampuni ya  EGMA Ltd na benki ya Stanbic

Aidha, miongoni mwa kosa la utakatishaji fedha inadaiwa washtakiwa wote walilitenda March 18, 2013 na January 10, 2014 wakiwa jijini Dar es Salaam ambapo walitakatisha USD 6,000,000 kwa kuzitoa fedha hizo kupitia njia ya benki kwa jina la Enterprises Growth Market Advisors (EGMA) katika benki ya Stanbic Tanzania.

Pia katika kosa la kusababisha hasara kwa serikali, wanadaiwa kwa pamoja walilitenda kosa hilo Mei 1, 2012 na Juni 1, 2015 wakiwa jijini Dar es Salaam walijipatia USD Milioni 600, 000,000 kama ada ya mkopo uliochukuliwa na Serikali ya Tanzania kutoka katika asilimia 1.4 hadi 2.4 na kusababisha serikali ipate hasara ya USD Milioni 6,000,000.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote,wamerudishwa rumande, kwa sababu mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, wakili Ngole amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 24, 2019.

 

MAKAMU WA RAIS AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA NYUMBA ZA POLISI MFIKIWA ZANZIBAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makaazi ya Askari Polisi Mfikiwa Chake Chake Pemba. Makamu wa Rais ambaye yupo Pemba kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ambapo jana tarehe 10 Januari 2019 aliweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Makaazi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar eneo la Pagali Chake Chake Pemba.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo Makamu wa Rais aliwataka Viongozi wa Vikosi kuongeza nguvu na kuhakikisha usimamizi wa shughuli za ujenzi wa makaazi ya askari unakamilika kama ulivyopangwa. “Mwaka jana tarehe 20 Machi 2018 niliweka jiwe la msingi wa ujenzi wa nyumba za makaazi wa askari wetu hivyo basi lazima lengo litimie kama tulivyozungumza siku ya uwekaji jiwe la msingi” alisema Makamu wa Rais.

Kwa upande mwingine Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Mohamed Hassani Haji amesema kuwa mipango ya kumalizia ujenzi wa makaazi bora ya askari polisi bado inaendelea na kuahidi kuikamilisha kwani ni dhamira ya jeshi la polisi kuhakikisha askari wake wanaishi sehemu salama.

Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais aliwasalimia Askari wa Kike waliokuwa kwenye maandalizi ya gwaride maalum la siku ya maadhimisho ya kilele cha miaka 55 ya Mapinduzi Takatifu ya Zanzibar yatakayofanyika kesho kwenye uwanja wa Gombani, Chake Chake Pemba.

“Mtapanda vyeo kwa jitihada ya kazi si vinginevyo hivyo Askari unatakiwa ufanye kazi kwa bidii sana” aliwahusia Makamu wa Rais.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makaazi ya askari Polisi  Mfikiwa Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na askari polisi wa kike waliokuwa wakijiandaa kwa ajili ya gwaride la maadhimisho ya sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi Takatifu ya Zanzibar mara baada ya kuwaliza kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makaazi ya askari Polisi  Mfikiwa Pemba. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Kamishina wa Polisi Zanzibar (CP) Mohamed Hassan Haji wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makaazi ya askari Polisi  Mfikiwa Pemba.



Viewing all 110182 articles
Browse latest View live


Latest Images