Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

WATUMISHI WA TASAF WAELEKEZWA KUZIHUDUMIA VIZURI KAYA MASKINI ILI KUZIWEZESHA KAYA HIZO KUJIKIMU KIMAISHA NA KUONDOKANA NA UMASKINI

$
0
0





Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi alipowatembelea ofisini kwao jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga akieleza majukumu ya taasisi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa TASAF kilichofanyika Makao Makuu ya TASAF jijini Dar es Salaam chenye lengo la kuhumiza uwajibikaji.
Baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipowatembelea ofisini kwao jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) mara baada ya kuzungumza na watumishi wa mfuko huo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

…………………………

Watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wametakiwa kuhakikisha wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wanahudumiwa vizuri kwa kupata ruzuku zao kwa wakati ili kuziwezesha kaya hizo kujikimu kimaisha na kuondokana na umaskini.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akizungumza na watumishi wa TASAF makao makuu katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kufahamu kwa kina majukumu ya TASAF na kujiridhisha namna inavyotekeleza wajibu wake.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, kwa kuwahudumia vizuri wanufaika hao, TASAF pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itapata baraka za Mwenyezi Mungu ambaye kupitia vitabu vyake vitakatifu ameelekeza kuwasaidia maskini na pia watakuwa mfano bora wa kuigwa na nchini nyingine barani Afrika kwa kutekeleza vema Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi wa TASAF kuwa tayari muda wote katika kuhakikisha kaya zote maskini zinapata stahili zao kwa wakati na kufurahia matunda na jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kuziwezesha kaya maskini kuondokana na umaskini.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameitaka TASAF kuhakikisha inaweka taratibu madhubuti za kisheria zitakazowaadhibu na kuwadhibiti wote watakaobainika kufanya udanganyifu kujipatia fedha za mpango wakati hawana sifa za kuwa wanufaika, lengo likiwa ni kujenga nidhamu katika jamii ili fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ziwafikie walengwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anavyotaka.

Katika kutekeleza azma hiyo, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi wa TASAF kufanya kazi kwa ari na uzalendo mkubwa na kuipongeza TASAF kwa jitihada na mafanikio waliyoyapata katika kuzinusuru kaya maskini mpaka hivi sasa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga amemhakikishia Mhe. Dkt. Mwanjelwa kuwa, atahakikisha anasimamia vizuri utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini kama alivyoelekeza, ili uwe ni mpango bora zaidi katika bara la Afrika, na kuongeza kuwa, hadi sasa, tayari mpango umeonekana kuwa ni miongoni mwa mipango bora barani Afrika kwani umeweza kuboresha maisha ya kaya maskini ambapo utekelezaji wake umewezesha kuzitambua kaya maskini, umesimamiwa vizuri, malipo yanafanyika kwa wakati na hakuna ubadhilifu mkubwa wa fedha zilizotengwa kwa ajili ya wanufaika.

Akithibitisha ubora wa mpango, Bw. Mwamanga amesema, hivi sasa Rais wa Benki ya Dunia katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku, anapozungumzia programu za kupambana na umaskini, haachi kuutaja Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa nchini Tanzania kuwa ni bora na unasimamiwa vizuri.

Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. John P. Magufuli aliyejipambanua kwa vitendo kuwajali wanyonge, imedhamiria kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini kuwafikia walengwa katika kaya zote maskini nchini ili walengwa hao waweze kunufaika na kuboresha maisha yao.

RAIS MAGUFULI ATOA NDEGE MBILI ZA RAIS KWA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA,ZITOE HUDUMA

$
0
0

*Aagiza zipigwe rangi zisafirishe Watanzania...asema kwanza yeye hasafiri sana

*Azungumza mambo makubwa kuhusu Watanzania, Balozi wa Canada aacha somo

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli ameagiza ndege za Rais mbili zipigwe rangi ya Shirika la Ndege Tanzania(ATCL) ili zitoe huduma ya kusafirisha Watanzania kati ya eneo moja na jingine.

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza baada ya kupokea ndege mpya ya Airbus 220-300 iliyowasili leo Januari 11 ,2018 ambapo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia uamuzi wake wa ndege mbili za Rais zitumiwe na Shirika la Ndege.

Amefafanua kuwa ndege ambazo zimetengwa kwa ajili ya Rais zipo tatu na hivyo ndege mbili amezitoa ili zitumike kutoa huduma."Kwanza Rais mwenyewe sisafiri ,hivyo ndege hizo zipigwe rangi ya ATCL zitoe huduma ya kwenda mikoa mbalimbali nchini,"amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo Rais Dk.Magufuli amesema Shirika la Ndege la Air Tanzania kwa asilimia 100 linamilikiwa na Watanzania wenye na hilo ni jambo la kujivunia sana na hayo ndio matokeo ya kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo.

Amesema kuna mashirika makubwa ya ndege ambayo yameandikwa majina ya nchi zao lakini si za nchi hizo lakini kwa ndege za ATCL ni mali ya Watanzania huku akifafanua ndege hizo ni za Serikali kwa asilimia 100.

Amesema Tanzania tunaweza na moyo wa kizalendo wa Watanzania upo ukiondoa wachache ambao hawana uzalendo na hao hawakosekani."Niwaahidi kwa nguvu zangu zote na ajili zangu zote niwatumikie Watanzania.

"Namuomba Mungu nisiwe na kiburi na majivuno.Namuomba Mungu aniongeze mimi na Serikali tuwatumikie Watanzania na hasa wanyonge bila kujivuna," amesema Rais Magufuli.

Ametumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa Bunge ambalo limekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za Serikali na kwamba hata walipoamua kupitisha bajeti ya ununuzi wa ndege hizo ilitokana na uzalendo wao.

"Nawapongeza wabunge wote na haswaaa wabunge wa CCM ambao linapokuja suala la maendeleo wanaitikia ndiooo," amesema Rais Magufuli huku akisisitiza upendo na mshikamano kwa ajili ya kuleta maendeleo.

Akizungumzia ndege hizo amesema miaka ya nyuma ndege kubwa zilikuwa zipo kwa nchi nyingine lakini leo hii zipo Tanzania na ndege ambazo zimebunuliwa za Airbus zipo nchi kwetu tu na hazipo mahali popote Afrika.

Amesema kuwa Tanzania itakuwa kama Ulaya na amewataka Watanzania kuamini kwenye hilo na kwamba ukiwa na imani unafanikiwa na hivyo Watanzania watafanikiwa sana.Amesema Tanzania ambayo anaitaka yeye ni ile ambayo huduma mbalimbali za kijamii ziwe zimeboreshwa na kwamba anaamini ndege zitaendelea kuongezeka.

Amesema Tanzania mpya inakuja na wanaochonganisha washindwe kwa la Yesu na Mtume Muhhamad huku akifafanua dua ambazo zimeombwa na viongozi wa dini Mungu amesisikia.

Ametumia nafasi hiyo kuwaombea Watanzania wote wafanikiwe kwenye mambo yao mbalimbali.Wakati huo huo Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kumpongeza Balozi wa Canada nchini Tanzania kwa uamuzi wake wa kuzungumza Kiswahili na amewafundisha Watanzania umuhimu wa kuzungumza Kiswahili.

Amesema kuna Watanzania ambao wamekuwa wakizungumza Kingereza na kujiona ni ufahari ambapo wanashindwa kuwafundisha lugha ya makabila ya Tanzania."Balozi na kupongeza na wale Watanzania wanaona 
aibu kuzungumza Kiswahili uwe mwalimu wao."

FAO Yaahidi Ushirikiano Zaidi na Serikali

$
0
0
Ndugu Fred Kafeero akimkabidhi Naibu Waziri wa Kilimo baadhi ya machapisho yanayoonyesha mikakati ya FAO 
Mheshimiwa Innocent Bashungwa akimueleza muwakilishi wa FAO nchini mipango ya Serikali ya awamu ya tano katika kuinua kilimo
Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akizunguza na mwakilishi wa Shirika laUmoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) Ndugu Fred Kafeero na msaidizi wa mwakilishi huyo Ndugu Charles Tulahi katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam


Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) limeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika kuiinua sekta ya kilimo nchini. Hayo yamesemwa na Ndugu muwakilishi wa Shirika hilo nchini Ndugu Fred Kafeero alipokutana na Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa katika ofisi za FAO jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho Ndugu Kafeero alieleza namna ambavyo shirika hilo limekuwa mstari wa mbele kushirikiana na serikali katika kutunga sera na kuandaa mikakati yenye lengo la kuhakikisha Tanzania inasonga mbele katika kilimo. Amesema FAO kwa miaka ya karibuni imefanya kazi kwa ukaribu na Shirika la Takwimu Tanzania (NBS) kwa kulijengea uwezo wa ndani unaoisaidia pia serikali katika ufuatiliaji wa bei ya mazao nchini.

Nae Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa alimueleza muwakilishi huyo mpango wa Serikali ya awamu ya tano wa kuorodhesha wakulima wote nchini ili kuweza kupanga vizuri kuhakikisha kila mkulima anapata huduma muhimu zitakazomsaidia toka hatua za uandaaji shamba mpaka masoko, na kuiomba FAO kama mdau muhimu wa kilimo kuipa Serikali ushirikiano ambapo Ndugu Kafeero aliahidi kulifanyia kazi ombi hilo.

Aidha, Naibu Waziri Bashungwa ameomba IFAD (shirika tanzu la FAO) isaidie Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Kilimo nchini kuwapatia wakulima nchini kupata mikopo ya riba nafuu, kusaidia taasisi za utafiti wa kilimo nchini, kujenga uwezo wa kuzalisha mbegu za mazao ya kimkakati na mchanganyiko, kujenga maghala ya kuhifadhi mazao ili kupunguza hasara wakati wa mavuno shambani (post harvest losses) na kuwajengea uwezo maafisa ugani nchini kufundisha kilimo cha tija kwa wakulima nchini. 

Mwakilishi wa FAO nchini amekubaliana na Naibu Waziri Bashungwa kufanyika kikao mwezi Februari 2019 cha Wizara ya Kilimo, FAO na mashirika mengine ya kimataifa yanayohusika na kilimo nchini kujadili vipaumbele tajwa ili kuijengea uwezo Wizara wa kuweza kuihudumia sekta ya kilimo nchini ili iendelee kukua na kutimiza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kufikia uchumi wa kati.

TUNA KAZI KUBWA YA KUPANDA MITI NCHI ISIGEUKE KUWA JANGWA-PROFESA MKENDA

$
0
0


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania Profesa Adolf Mkenda akizungumza na akizungumza katika Mkutano wa Saba wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Wakala wa mbegu za miti waliokutana Jijini Arusha leo. Picha na Vero Ignatus

Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Wakala wa Misitu Nchini Profesa D.Santos Silayo akizungumza katika Mkutano wa Saba wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Wakala wa mbegu za miti waliokutana Jijini Arusha.

Mwenyekiti wa TFS Francis Kiondo Mwenyekiti Tughe,Meneja Misitu Wakala wa Huduma za Misitu wilaya ya Temeke

Hamisi Jori Afisa misitu wa wakala wa huduma za misitu kanda ya kati Dodoma na mjumbe Baraza

Wakwanza kushoto Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania Profesa Adolf Mkenda akifuatiwa na Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Wakala wa Misitu Nchini Profesa D.Santos Silayo. Picha na Vero Ignatus

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) walipokutana Jijini Arusha leo.

Mgeni rasmi pamoja na walio Meza kuu wakiwa wameshikana mikono wakiimba wimbo wa wafanyakazi wa Solidarity Forever.

Mgeni rasmi Profesa Adolf Mkenda akiwa katika picha ya pamoja na Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Wakala wa mbegu za miti waliokutana Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus.
Na. Vero Ignatus, Arusha


KATIBU Mkuu wa Wizra ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania Tafori na Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo kufanya tafiti maeneo ilioisha miti ili ipandwe mingine kwa ajili ya uvunaji wa haraka utakaoingizia serikali kipato.

Ametoa agizo hilo leo wakati akifungua mkutano wa saba wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Wakala wa mbegu za miti waliokutana Jijini Arusha kukumbushana utawala,haki na wajibu wa Mfanyakazi.

Amesema wajibu mkubwa wa wafanyakazi hao ni kulinda rasilimali za Umma kwa kupambana na uvunaji haramu usiokuwa na utaratibu,uchomaji moto misitu na uvamizi wa mapori kwa ajili ya malisho ya mifugo."Kutokana na hali hii lazima mtafute njia mbadala ya ufugaji wenye tija ili kulinda misitu na mapori yetu na pia kuhakikisha haturuhusu kilimo cha uharibifu wa mazingira,"Alisema Profesa Mkenda

Prof.Mkenda alisema serikali inatambua kazi inayofanywa na wafanyakazi hao na mazingira magumu yanayohatarisha maisha yao,ikiwemo kuzushiwa vitu vya uongo,kupigwa hata kuuwawa, hivyo hawatafungia macho suala hilo.

Ameagiza wafanyakazi hao kuhakikisha wanaacha tabia ya kutoa mizinga bure kwa wafugaji wa nyuki,badala yake wawakodishie ili kuipatia kipato serikali.
"Mizinga hii mnatoa bure lakini wengi hawaitumii,kodisheni ili watu waone uchungu wawese kuitumia ipasavyo kuzalisha asali,"alisema Prof. Mkenda

Alisema Tanzania ina uwezo wa kuongoza dunia kwa uzalishaji asali endapo misiti na mapori iliyopo itatumika vizuri kufunga nyuki ili kujipatia asali ambayo masoko yake yapo.Akitoa mfano alisema mapori ya Kakonko na Kibondo yana misitu na mapori makubwa ambayo tayari serikali imeshapeleka timu ya wataalamu wa kufundisha uzalishaji wa asali kwa wingi ili kukidhi soko la Uholanzi lililopatikana.

Naye Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) D.Santos Silayo, alisema changamoto kubwa walizonazo kwa sasa ni ongezeko la uhalifu maeneo ya misitu,uvamizi,kupambana na ugumu katika kudhibiti wahalifu kwani wengi wao wana silaha za moto.Pia alitaja changamoto nyingine kuwa ni misiti mingi ipo nje ta maeno yaliohifadhiwa rasmi,watumishi kutishiwa na kuzuiwa kutekeleza majukumu yao na baadhi ya watumishi wasiozingatia kanuni na sheria za uwajibikaji kazini.

"Kutokana na hali hiyo TFS inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kinidhamu za kudhibiti hali hiyo kwa watakaobainika,"alisema Pofesa Silayo.Pia amesema TFS wanatarajia kuanzisha mfuko wa kuweka akiba na kukopa SACCOS, kwa wafanyakazi wao na kujali afya za wafanyakazi wao wawapo kazini.

MFANYABIASHARA MAARUFU NA MFANYAKAZI WAKE WASOMEWA MASHTAKA 601,LIKIWEMO LA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA ZAIDI YA BILIONI 14

$
0
0
Mfanyabiashara maarufu Mohamed yusufali na mfanyakazi wake Arital Maliwala wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 601 likiwemo la kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bilioni 14.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na jopo la mawakili wa kutoka Takukuru wakiongozwa na Hashimu Ngole, Pendo Makondo, Leornad Swai ambao walikuwa wakisaidiana na wakili wa serikali Patrick Mwita mbele ya hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.

Katika mashtaka hayo, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kughushi, kuwasilisha taarifa za mwezi za mahesabu ya uongo kwa TRA, kukwepa kodi na kuisababishia serikali hasara ya sh. 14,987,707,044.58

Katika shtaka la kuisababishia serikali hasara, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa la kusabisha hasara ambayo imetokana na kukwepa kodi ya serikali kwa kipindi cha mwaka 2008 hadi 2015 kupitia kampuni ya Pamplant ltd iliyokuwa inamilikiwa na mshtakiwa Yusufali ambapo mshtakiwa Paliwala alikuwa mfanyakazi wake.

Imeendelea kudaiwa kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo wakiwa wanatumia stakabadhi za kughushi pamoja na kutumia makampuni ya kughushi wakidai kuwa wamenunua vitu kutoka katika makampuni mbali mbali wakati wakijua baadhi ya kampuni hizo ni za kughushi huku zikiwa hazijasajiliwa brella.

Pia imedaiwa kampuni hizo zina majina ya makampuni ambayo hayapo brella na yana namba  za usajili ambazo brella haijazifikia huku pia wakiwa wanaghushi stakabadhi za malipo.Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali kutoka kwa DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umeishakamilika na kesi hiyo itakuja tena mahakamani hapo January 24  mwaka huu kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo yao (commital).

POLISI SABA WASIMAMISHWA KAZI, WAFIKISHWA MAHAKAMANI

$
0
0
Jeshi la Polisi Tanzania leo tarehe 11/01/2019, limewasimamisha kazi askari saba (7) wa vyeo mbalimbali kwa kutenda kosa kinyume na mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi na tayari wamefikishwa mahakamani kusomewa mashitaka yanayo wakabili. 
Hatua hii imechukuliwa, baada ya askari hao kuomba rushwa ya bilioni moja na baadae kupokea rushwa ya milioni mia saba toka kwa mfanyabiashara wa dhahabu aitwaye Sajid Abdalah Hassan ambaye walimkamata akiwa na dhahabu kiasi cha kilogramu 319.59, yenye thamani ya mabilioni ya shilingi za kitanzania.
Askari hao waliosimamishwa kazi ni;
E.4948 CPL Dani Isack Kasala
F.1331 CPL Matete Maiga Misana
G.1876 PC Japhet Emmanuel Lukiko
G.5080 PC Maingu Baithaman Sorrah
G.6885 PC Alex Elias Nkali
G.7244 PC Timoth Nzumbi Paul
H.4060 PC David Kadama Ngelela.
Aidha, kuhusu Afisa SSP: Moris Okinda ambaye alikuwa kiongozi wa askari hao walioomba na kupokea rushwa ya 

kiasi hicho cha fedha, mamlaka yake ya kinidhamu tayari imemsimamisha kazi na tayari amefikishwa mahakamani pamoja na askari hao. 
Pamoja na askari hao, pia wamefikishwa mahakamani watuhumiwa wengine wa nne waliokamatwa huko Kigongo feri Wilayani Misungwi wakitorosha madini hayo ya dhahabu kutoka Tanzania kwenda Nchi jirani ya Rwanda.
Watuhumiwa waliokamatwa wakitorosha madini hayo ya dhahabu ni;
Sajid Abadalah Hassan, miaka 28, mfanyabiashara wa dhahabu, mkazi wa Ilala Dar es Salaam na Mwanza mtaa wa pamba ‘A’.
Kisabo Kija @ Mkinda , miaka 55, mfanyabiashara wa dhahabu, mkazi wa mwatulole –Geita
Emmanuel Ntemi, miaka 63, dereva, mkazi wa kijiji cha mwatulole –Geita
Hassan Sadiq Hassan, miaka 28, Mhindi, Raia wa Pakistani, mkazi wa Mwanza mtaa wa Pamba ‘A’, Mfanyakazi wa duka la kuuza vito.
Kufuatia sakata hili, Jeshi la Polisi Tanzania kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tunaendelea na uchunguzi wa kina ili tuweze kuwakamata watuhumiwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine katika sakata hili. 

Imetolewa na;
CP: Robert Boaz
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Tanzania
11 January, 2019.

NATAMANI NIKIKUWA NIWE KAMA RAIS DK.MAGUFULI-MAKONDA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar Salaam,Paul Makonda amesema anatamani akikuwa awe Kama Rais Dk.John Magufuli.

Makonda amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la upokeaji wa ndege mpya ya Airbus 220-300 ambayo imewasili nchini leo ambapo wakati anazungumza amesema anaomba viongozi wa dini wamuombee awe kama Rais Magufuli.

Amesema siku zote amekuwa akimuomba Mungu siku atakapokuwa na kuwa na umri wa utu uzima basi awe kama Rais na hivyo kuwaomba viongozi wa dini wamuombee ili ndoto yake itimie.

Ametoa sababu mbalimbali za kutaka kuwa kama Dk.Magufuli ambapo kubwa ni ile ambayo amesema Rais anachokipanga ndicho anachokitekeleza,Rais ambaye hayumbushwi anapoamua kufanya maendeleo.

Makonda amesema anataka kuwa kama Rais Magufuli kwasababu ameweza kutenganisha nafasi yake ya urais na familia yake ,pia ametofautisha urais wake na urafiki."Rais Magufuli amebaki kuwa kwenye nafasi yake mwenyewe.Ingekuwa wengine leo familia ya Rais tungekuwa tunapishana nayo huko mtaani." 

Wakati huo huo Makonda amzungumzia miradi mikubwa inayoendelea nchini chini ya uongozi wa Rais Magufuli na kwamba kwenye sekta ya anga kila mwananchi ni shahidi kwa mambo yanayofanyika.Amesema idadi kubwa ya wanachi ambao wamejitokeza uwanjani hapo ni ushahidi wa kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli ambaye anatekeleza kila ambacho amekiahidi.

"Wananchi hawa ambao wapo hapa wamekuja kwa ajili ya luunga mkono jitihada zako ambazo unazifanya kwa ajili ya Watanzania wote, tunakupongeza Rais wetu mpendwa," amesema Makonda.

RAIS MAGUFULI: NITAENDELEA KUWATUMIKIA WATANZANIA WOTE

$
0
0
RAIS Dkt. John pombe Magufuli amewaongoza wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuipokea ndege mpya ya pili aina ya Airbus A220-300 na kuwataka Watanzania kuamini kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuwatumia katika kuwaletea Maendeleo.

Akizungumza katika hafla ya upokeaji wa ndege hiyo leo Ijumaa (Januari 11, 2019) Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema ili kufikia kwa haraka kasi ya kasi maendeleo ya kiuchumi, Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kutekeleza kwa vitendo dhana ya msingi wa kujitegemea na kupunguza kutegemea misaada kutoka mataifa ya nje.

Rais Magufuli alisema kuwasili kuwasili kwa ndege hiyo ya Airbus A220-300 ni ushuhuda wa nguvu za Watanzania katika kuungana na Serikali katika juhudi mbalimbali za Maendeleo ikiwemo kulipa kodi, jambo ambalo limekuwa likipewa msukumo na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta Maendeleo ya Watanzania walio wengi zaidi.

“Wakati mwingine misaada inalemaza, hivyo ili nchi iendelee ni lazima tujitegemee na sisi tumeamua kuimarisha Shirika letu la ndege la ATCL, kwa sasa zipo ndege sita na tumepanga kuongeza nyingine mbili ambapo moja aina ya Dreamliner ya pili inategemea kuwasili nchini mwishoni mwa mwaka huu” alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alilitaka Shirika la Ndege Nchini (ATCL) kuhakikisha linajipanga kikamilifu katika kuhakikisha kuwa linatoa huduma bora na kuhakikisha kuwa Shirika hilo linajiendesha kibiashara na hivyo kuleta tija na makusudio yanayotarajiwa na Serikali kulingana na Mpango Mkakati uliowekwa na Shirika hilo.

Akifafanua zaidi Rais Magufuli alisema Serikali haitasita kulinyang’anya ATCL ndege hizo iwapo shirika hilo litashindwa kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali na hivyo kulitaka Shirika hilo kujipanga kikamilifu ikiwemo kuongeza mtandao wa huduma zake katika vituo vya ndani na nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, alisema katika kuliongezea nguvu Shirika hilo, Serikali imepanga kutoa ndege mbili zinazotumiwa na Viongozi Wakuu wa Serikali aina ya Focal 28 na Focal 50 kuanza kutoa huduma ya kubeba abiria katika muda ambao ndege hizo zitakuwa hazitumiki na Viongozi hao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Nchini (ATCL), Mhandisi Ladislaus Matindi alisema katika kufikia malengo yaliwekwa na Serikali, ATCL imeendelea kutekeleza kwa kasi kubwa kuimarisha mtandao wa huduma katika Shirika hilo kupitia Mpango Mkakati wa Miaka mitano wa Shirika hilo (2017/22) uliolenga katika kuliendesha shirika hilo katika kuongeza faida.

Aliongeza kuwa katika Mpango Mkakati huo, Shirika hilo limepanga kuongeza idadi ya mtandao wa huduma katika vituo vilivyopo ndani nan je ya nchi ikiwemo nchi za Zambia, Afrika Kusini na Zimbabwe pamoja na kuimarisha utoaji huduma katika mikoa yenye idadi kubwa ya wateja ikiwemo Mwanza, Kilimanjaro na Mbeya.

“Kuanzia Januari 16, tutaanza kuboresha huduma za ndege kwa safari za kila siku katika Mji Mkuu wa Serikali kutokana na wingi wa wateja waliopo ambapo hapo awali tulikuwa tukienda mara moja kwa wiki ili kuhakikisha kuwa mji sasa unakuwa kiunganishi na maeneo mengine ya nchi” alisema Mhandisi Matindi.

Alisema mbali na uboreshaji wa huduma za abiria, Shirika hilo limejipanga pia kuhakikisha kuwa linaboresha uwezo wa kusafirisha shehena za mizigo ambapo ndege za Bombadier Q-400 zina uwezo wa kubeba mzigo wa tani 8.6, ndege ya Dreamliner ina uwezo wa kubeba mzigo wa tani 44, na ndege mbili aina ya Airbus ina uwezo wa kubeba tani 19.

Kkwa kwa mujibu wa Mhandisi Matindi alisema kuwa ATCL kwa kushirikiana na Ofisi ya Ubalozi wa Uingereza nchini, imepanga kukutana na wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri wa anga ikiwemo watoa huduma na wafanyabiashara ili kuwawezesha kupata fursa mbalimbali ikiwemo masoko ya bidhaa mara baada ya Shirika hilo litakapoanza kupeleka ndege nchini Uingereza.

Naye Balozi wa Canada Nchini, Pamela O'Donnel alisema Serikali ya nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha sekta muhimu za kiuchumi ikiwemo usafiri wa anga zinapiga hatua kubwa za maendeleo ikiwemo utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo.

MAMLAKA YA NGORONGORO YAKABIDHI SH.BILIONI MOJA KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI,VITUO VYA AFYA KARATU

$
0
0
  Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Professa Abiud Kaswamila akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mfano wa hundi ya Sh milioni 500,000 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya Samunge na Arash wilayani humo zilizotolewa na NCAA kama sehemu ya mchango wa shughuli za maendeleo.
 Viongozi wa wilaya ya Ngorongoro na Karatu mkoani Arusha wakiwa wameshika hundi za mfano wa fedha zilizotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Sh Bilioni 1 walizokabidhiwa kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Karatu na vituo viwili vya afya wilayani Ngorongoro.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka mfano wa hundi ya Sh milioni 500 zilizotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya ujenzi wa vituo viwili vya afya katika Kijiji cha Samunge na Arash wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo mfano wa hundi ya Sh milioni 500 zilizotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya ujenzi wa vituo viwili vya afya katika Kijiji cha Samunge na Arash wilayani humo. 


NA MWANDISHI WETU, ARUSHA


MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), Profesa Abiud Kaswamila amekabidhi Sh bilioni 1 za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Karatu na vituo viwili vya afya wilayani Ngorongoro.

  Mchango huo wa maendeleo kutoka NCAA ulipokelewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, ambapo wilaya ya Karatu imepokea Sh milioni 500 na Ngorongoro Sh milioni 500.Akizungumza wakati wa kukabidhi mchango huo Prof. Kaswamila alisema, msaada huo utakuwa chachu ya uhifadhi endelevu ikizingantiwa wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo ni wadau wakubwa.

 “Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inayo majukumu makubwa matatu, kuhifadhi maliasili na malikale, kuendeleaza wenyeji na kuendeleza utalii,” alisema Prof Kaswamila na kuongeza:“Katika kuendeleza majukumu hayo chanzo kikuu cha mapato ni utalii, aidha maendeleo ya utalii yatafikiwa iwapo maliasili zilizopo ndani ya hifadhi wakiwamo wanyamapori wanahifadhiwa kwa kushirikiana na wenyeji wa Ngorongoro na jamii inayozunguka hifadhi,” alisema.

Alisema NCAA imekuwa ikichangia miradi ya maendeleo kupitia ujirani mwema ambapo mwaka 2016-2017 ilitumia Sh 359,117,500 na mwaka 2017-2018 Sh 295,000,000 na mwaka 2018-2019 imetenga Sh 1,415,000,000 kufadhili miradi ya ujirani mwema.Kwa upande wake Gambo akipokea hundi hizo kisha kuzikabidhi kwa wakuu wa wilaya husika alisema, tangu nchi ilipopata Uhuru ni wilaya ya Monduli na Arumeru ndio zilizokuwa na hospitali za wilaya.

 Kutokana na juhudi hizo Gambo aliishukuru Bodi ya NCAA kwa kutoa fedha hizo akisema zimekua chachu kwa wananchi wa Kata ya Samunge wilayani Ngorongoro ambao baada ya kusikia habari hizo walianza kuchimba misingi nane ya ujenzi wa kituo chao cha afya kwa kujitolea.“Kwa wilaya ya Ngorongoro Sh milioni 400 zitakwenda kujenga kituo cha Afya Samunge na Sh milioni 100 zitakwenda Kata ya Arash kujenga Kituo cha Afya, wilaya ya Karatu wao watazielekeza zote kwenye ujenzi wa Hospitali ya wilaya,” alisema Gambo.

Aidha Mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo alishukuru kupokea fedha hizo na kuahidi kuwahamasisha wananchi kuanza kufanya kazi za kujitolea kuanzia wiki ijayo.Naye Mkuu wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka alisema, mchango huo umekuwa ni neema kwao kwani umewafungulia ukurasa mpya wa maendeleo ya sekta ya afya.

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA WANANCHI KUPOKEA NDEGE YA PILI YA AIRBUS A220-300

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria kupokea ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 iliyowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Isaack Kamwelwe wakipewa maelezo na  Rubani Patrick kuhusu ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 walipoipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia wananchi baada ya kupokea ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019

 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na mkewe Mama Mary Majaliwa wakiwa na viongozi wengine mbalimbali wakishuka kutoka katika ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 ilipowasili na kupokelewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019.
 Maafisa waliokwenda Canada kuipokea ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 wakilakiwa kwa shangwe Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019
Picha na IKULU
 Ndege mpya ya kisasa aina ya Airbus 220-300 iliyopewa jina la moja ya hifadhi ya  mbuga za wanyama  (Ngorongoro), ikikaribishwa kwa water salute mara baada ya kutua leo 11 Januari 2019 katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere  ikitokea Canada ilikotengenezwa.  
 Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ikiwasili kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mapema leo, ndege hiyo imepewa jina la moja ya hifadhi  ya mbuga za wanyama  Ngorongoro kama inavyoonekana kwenye picha. 
 Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) wakiwa wamesimama mbeleya  ndege mpya aina ya Airbus 220-300 mara baada ya kuipokea leo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ndege hiyo ni ya kwanza kununuliwa na serikali ya Afrika (Tanzania). 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ndege mpya aina ya Airbus 220-300 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius  Nyerere, kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Ally Bashiru, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa na Balozi wa Canada nchini Tanzania Pamela O’Donnel ,na Kulia ni Mkrugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)  Mhandisi Ladislaus Matindi, Mwenyekiti wa  Kamati ya Bunge ya Miundombinu Suleiman Kakoso na Waziri  wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa mara baadya ya kuzindua ndege mpya aina ya Airbus 220-300 iliyowasiri leo 11 Januari, 2019 kulia ni , Mwenyekiti wa  Kamati ya Bunge ya Miundombinu Suleiman Kakoso na Waziri  wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson na Balozi wa Canada nchini Tanzania Pamela O’Donnel

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na , Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi mara baada ya mapokezi ya Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 iliyopokelewa uwanja wa Kimataifa Julius Nyerere leo 11 Januari 2019.
(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)


KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Simba na Yanga kuchuana vikali katika ligi kuu ya soka la wanawake ya SERENGETI LITE

$
0
0

DAR ES SALAAM, Januari 11, 2019: Kwa mara ya kwanza katika historia ya soka la Wanawake hapa nchini Klabu za Simba na Yanga zinatarajia kukutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite utakaochezwa Jumapili, Januari 13,2019. Mchezo huo utachezwa saa 10 Jioni katika Uwanja wa Karume, Ilala makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). 

Ligi kuu ya wanawake inadhaminiwa na kinywaji cha Serengeti Premium Lite kwa msimu wa pili mfululizo. Katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa na msisimko mkubwa, kiingilio kitakuwa shilingi 2,000. Mashabiki wanahakikishiwa usalama huku vyombo husika vikihakikisha mchezo salama bila bughudha ya aina yoyote. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, Amina Karuma, akizungumza kuelekea mchezo huo amesema msimu huu umeanza kwa msisimko mkubwa na ushindani wa aina yake hivyo ni matarajio yake kuwa mchezo huo wa watani wa jadi utaakisi ubora wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite. 

“Mchezo huo unaingia kwenye rekodi za Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite kwa kuwa ndio mchezo wa kwanza kuzikutanisha timu hizo tokea kuanza kwa soka la Wanawake hapa nchini,” alisema Amina. Aidha amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo na kujiona vipaji pamoja na ushindani wa hali ya juu kutoka pande zote za mchezo. 

Naye Afisa masoko wa Serengeti Breweries Bw. George Mango amewahakikishia wadau wa soka la wanawake, mashabiki wa mpira wa miguu kuwa kinywaji cha Serengeti Lite kimejidhatiti kuhakikisha wanapata burudani ya hali ya juu kupitia mchezo huo kama ilivyokuwa kwa michezo mingine iliyotangulia. 

“Mashabiki wakae tayari kuona namna kinyaji cha Serengeti Lite kilivyo tayari kuwaletea burudani ya hali ya juu kwenye mechi hii ya kusisimua,” amesema Mango. 
Serengeti Premium Lite ni bidhaa ya kwanza Tanzania kujitokeza kudhamini ligi ya wanawake, na imejidhatiti kusaidia kupandisha viwango vya ligi hii kupitia kupitia udhamani, matangazo kwenye magazeti pamoja na viwanjani. Bia ya Serengeti Premium Lite inadhamini Ligi Kuu ya Wanawake kwa kitita cha Shilingi 450 milioni kwa kipindi cha miaka mitatu. MWISHO.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, Amina Karuma akiongea na waandishi wa habari  (hawapo pichani ) wakati wa kutangaza mchuano wa  ligi kuu ya soka la wanawake ya SERENGETI LITE kati ya  Klabu za Simba  Queens na Yanga Princess ambazo   zinatarajia kukutana kwenye mchezo utakaochezwa Jumapili, Januari 13,2019.Kushoto  kwake ni Afisa masoko wa kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Bw. George Mango na kulia kwake ni  Kocha wa Yanga Princess Hamis Kinonda .
 

Afisa masoko wa kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL)  akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza mchuano wa  ligi kuu ya soka la wanawake ya SERENGETI LITE kati ya  Klabu za Simba  Queens na Yanga Princess ambazo   zinatarajia kukutana kwenye mchezo utakaochezwa Jumapili, Januari 13,2019.Kulia kwake Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, Amina Karuma na kushoto kwake ni  Kocha wa Simba Queens  Omari Mbweze.

Nahodha wa Simba Queens Mwanahamis Omar akiongea na waandishi wa habari jinsi walivyojiandaa na Mchezo huo wa watani wa jadi hapa nchini Klabu za Simba na Yanga zinatarajia kukutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite utakaochezwa Jumapili, Januari 13,2019

MIAKA 55 YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wajivunia upatikanaji wa huduma bora nchini.

$
0
0

NA. WAMJW, Dar es Salaam.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umejivunia kuongeza wigo wa wanufaika kwa kuwafikia Wananchi mbalimbali ikiwemo Wakulima kupitia vyama vyao vya ushirika kwenye huduma ya Ushirika Afya na watoto kupitia huduma ya Toto Afya Kadi. Mfuko pia umewezesha upatikanaji wa huduma za Madaktari Bingwa katika mikoa ya pembezoni pamoja na kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa katika Hospitali hapa nchini.

Hayo yameelezwa na Meneja Uhusiano wa Mfuko huo Bi. Anjela Mziray wakati wa ziara maalum ya Maafisa Habari wa Wizara ya Afya na taasisi zake katika kampeni maalum ya ‘Tumeboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

Wakiwa Makao Makuu ya NHIF, Maafisa hao waliweza kutembelea maeneo mbalimbali ya Mfuko huo kujionea namna huduma zinazotolewa na Mfuko huo sambamba na mafaniko waliyofikia katika sekta ya Afya.

Awali akizungumza mambo mbalimbali Bi. Anjela Mziray aliwaeleza Maafisa hao kuwa Serikali inakusudia kuwafikia wananchi wote na huduma bora za afya. Katika kutekeleza hili Mfuko umewezesha Madaktari Bingwa wa magonjwa ya mbalimbali kama ya Wanawake, watoto, moyo, macho, kinywa na pua na mabingwa wa upasuaji kutoa huduma katika mikoa ya pembezoni kwa kipindi maalum.

"Kwa ujumla watu zaidi ya 20,289 wamefikiwa na huduma hii na kati ya hao watu 938 wamefanyiwa upasuaji wa kitalaam na hii ni katika mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa, Lindi, Mara, Manyara, Geita, Njombe na Ruvuma huku baadhi ya mikoa tukienda mara mbili” alieleza Bi. Anjela Mziray.

Aidha, katika mafaniko mengine ya kuboresha upatikanaji wa huduma, Mfuko unashiriki juhudi za Serikali za uwekezaji katika viwanda. Mfuko kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi zingine unawekeza katika kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa za hospitali zitokanazo na malighafi ya pamba na kiwanda hiko kitajengwa Bariadi Mkoani Simiyu huku kikitarajiwa kuzalisha aina 24 za bidhaa hizo. Wadau wengine wanaoshiriki katika uwekezaji huu ni pamoja na Serikali ya mkoa wa Simiyu, WCF, TFDA, TBS, MSD, TIB, TIRDO na taasisi zingine.

Katika jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata huduma, alieleza kuwa Mfuko kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani umenawezesha wamama wajawazito kupata bima ya afya ili waweze kupata huduma katika hospitali. Mpaka sasa wajawazito wapatao 1,044,000 wameshafikiwa na mpango huu katika mikoa ya Tanga, Mbeya, Njombe, Lindi na Mtwara.

Mfuko huo pia umeweza kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa kutumia mifumo ya Tehama inayowezesha kutambua wanachama katika vituo, kurahisisha ulipaji wa madai ya watoa huduma kwa wakati, kurahisisha usajili wa wanachama na kuharakisha utoaji wa vitambulisho.

Akizungumzia hili Meneja wa Mifumo ya Tehama Bw. Bakari Yahaya alisema kwa sasa mifumo inamwezesha mwanachama kupata ujumbe mfupi kwenye simu yake mara tu kadi yake au ya mtegemezi wake inapotumika kwa matibabu. 

Mfuko huu sasa umefanikiwa kuwa na ofisi zake katika mikoa yote ikiwemo Tanzania Bara na Zanzibar huku wakiboresha mfumo wa mawasiliano kwa kuwa na kituo cha huduma kwa wateja kwa ajili ya kupokea simu za wadau siku zote za juma bila malipo kwa wapigaji. Simu hiyo ni 0800 110063.

Akimalizia maelezo yake alisema, Mfuko umefanikiwa kupata cheti cha ubora wa huduma kwa viwango vya kimataifa ( ISO 9001:2015). "Katika hili tunajivunia kuimarika kwa huduma na ufanisi katika utekelezaji majukumu ya Mfuko kwa manufaa ya wadau wote wa Mfuko" alisema Bi. Mziray.

 Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bi. Angela Mziray akizungumza wakati wa ziara maalum ya Maafisa habari wa Wizara ya Afya na taasisi zake katika kampeni maalum ya ‘Tunaboresha Sekta ya Afya’ inayolenga kueleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.  leo 11.1.2019, Makao makuu ya Mfuko huo Jijini Dar es Salaam
 Afisa wa kitengo cha Tehama Charles Charles akionesha namna ya mfuko wa kisasa unavyofanya kazi katika kitengo cha tehama
 Msimamizi wa nyaraka wa NHIF, Erasto Msigwa akieleza namna mfumo huo unavyofanya kazi  wa kutunza kumbukumbu kwa njia ya kisasa
Sabrina Mponda wa kitengo cha CALL CENTER akitoa maelezo namna huduma wanayotoa ikiwemo kupokea simu zaidi ya 200 kwa siku katika kituo hicho ambapo wamefanikiwa kuwafikia watanzania mbalimbali 


KAMPENI YA KUMTUA MAMA NDOO INAENDELEA KUTEKELEZWA KAGERA

$
0
0

Naibu Waziri wa Maji  Jumaa Aweso anaendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera akiwa tayari amemaliza Ziara ya kutembelea, Kukagua na Kuzindua Miradi ya Maji ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mnamo  Januari 11,Magufuli Mh. Aweso ametembelea na kukagua mradi wa Maji katika Kata ya Ibwera eneo la Rugaze ambapo mradi huo tayari unafanya kazi na unauwezo wa kuhudumia Wananchi 500 wa Vijiji jirani.

Kisha Mh. Aweso ameendelea na Ziara hiyo katika kata ya Kibirizi ambapo ameweza kuzindua Mradi mpya wa Maji wenye zaidi ya Shilingi Milioni 500. Mradi huo uliopo katika Kijiji cha Kibirizi umeanza kuhudumia takribani vitongoji 10 kati ya 14 vinavyopatikana ndani ya Kijiji hicho na huku juhudi zikiendelea kufanyika kuwafikia wananchi wengine.

Kwa upande mwingine mradi wa Maji Kijiji cha Kyamulalile na Mashule kwa sasa haufanyi kazi kutokana na athali ya tetemeko licha ya kuwa tayari Halmashauri imekwishatenga zaidi ya shilingi milioni 80, kwa ajili ya Ukarabati na tayari mkandarasi ameanza upembuzi yakinifu.

Naibu Waziri Aweso ameendelea kuwaomba wananchi kutunza na kulinda miradi hiyo, huku pongezi nyingi zikimmiminikia Mh. Rais John Pombe Magufuli na Serikali yake jinsi anavyoendelea kupambana na adha hii ya Maji, na sasa akina asilimia kubwa ya akinamama hawatembei tena mwendo mrefu kufuata Maji na kampeni ya kuwatua Ndoo vichwani inaendelea.
 Pichani kati ni Naibu Waziri wa Maji  Mh.Jumaa Aweso akiwa na baadhi akibeba ndoo kichwani kuashiria uzinduzi wa Maji katika Kijiji cha Kibirizi, Halmashauri ya Bukoba,ambapo pia ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kampeni ya kumtua Mama Ndoo ikiendelea kutekelezwa mkoani Kagera.Mh.Aweso anaendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera akiwa tayari amemaliza Ziara ya kutembelea, Kukagua na Kuzindua Miradi ya Maji ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba  
 Pichani jiwe la msingi Kijiji Kibiri
Naibu Waziri wa Maji  Jumaa Aweso akitoka kuzindua mradi wa maji kijiji cha Kibirizi,Bukoba mkoani Kagera,Mh Aweso anaendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera akiwa tayari amemaliza Ziara ya kutembelea, Kukagua na Kuzindua Miradi ya Maji ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ,ambapo pia ametembelea na kukagua mradi wa Maji katika Kata ya Ibwera eneo la Rugaze,ambao tayari unafanya kazi na unauwezo wa kuhudumia Wananchi 500 wa Vijiji jirani.

BWENI LA SHULE YA SEKONDARI MLANGARINI LATEKETEA KWA MOTO LEO ASUBUHI

$
0
0
 Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

BWENI la wavulana katika  Shule ya Sekondari Mlangarini ambayo ni shule ya Serikali  iliyo katika kata Mlangarini Halmashauri ya Arusha Wilaya ya Arumeru limeungua moto.

Taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Jerry Muro amesema leo Januari 12,2019 amepata taarifa za kuungua kwa bweni saa moja asubuhi.

Amesema taarifa za awali zinaeleza moto huo ulianza Alfajiri na kuteketeza chumba kimoja kati ya vyumba 14  vya bweni hilo lililokuwa na wanafunzi 84 na kwamba hakuna majeruhi wala vifo.

"Japo kuna uharibifu wa mali ikiwemo kuungua kwa  vitanda (double) vitatu (3),magodoro (6),Masanduku ya kuhifadhia nguo na madaftari.      Kutokana na changamoto hiyo nililazimika kufika eneo la tukio mapema na kuungana na wanafunzi pamoja na wananchi waliojitokeza katika hatua za awali ambapo pia kikosi cha Zimamoto kiliwahi kufika kwenye eneo la tukio na kukuta moto umezimwa kwa ( fire extinguisher 11)," amesema Muro.       

  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Jerry Muro akizungumza jambo mbele ya baadhi ya waalimu wa shule hiyo pamoja na majirani wanaoinzunguka shule hiyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Jerry Muro akimsikiliza mmoja wa Waalimu wa shule hiyo mara baada ya tukio 
 Moja ya chumba kilichoteketea moto
      

Uchaguzi DRC: Martin Fayulu atangaza kwenda mahakamani kupinga ushindi wa Tshisekedi

$
0
0
Martin Fayulu amedai kuwa mshindi ameteuliwa na utawala wa Kabila ili akidhi matakwa yao


Mgombea wa upinzani aliyeshindwa katika uchaguzi wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) uliofanyika Disemba 30 ameapa kuyapinga matokeo mahakamani.

Martin Fayulu ameiambia BBC kuwa raia wa Congo wanastahili kujua ukweli wa uchaguzi, mabao ameutaja kuwa ni "mapinduzi".

Mgombea mwengine wa upinzani Felix Tshisekedi, alitangazwa kuibuka na ushindi katika kinyang'anyiro hicho, lakini kumekuwa na tuhuma kuwa mshindi huyo ameingia makubaliano ya kisiasa na rais aondokaye Joseph Kabila.

Tayari watu kadha wanaripotiwa kuuawa na wengine kujeruhiwa toka matokeo hayo yalipotangazwa.Uchaguzi huo unakamilisha safari ya miaka 18 madarakani ya Joseph Kabila.

Matokeo hayo, endapo yatathibitishwa, yataweka historia ya makabidhiano ya amani ya hatamu za uongozi toka nchi hiyo ilipopata uhuru wake toka kwa wakoloni wa Ubelgiji mwaka 1960.

Kanisa lenye ushawishi mkubwa la Katoliki ambalo lilikuwa na waangalizi wa uchaguzi 40,000 limesema matokeo yaliyotangazwa hayaendani na matokeo waliyonayo.

Fayulu amesema nini?

Akiongea na mhariri wa BBC wa Afrika Fergal Keane, Bw Fayulu amesema atayapinga matokeo hayo kwenye mahakama ya katiba.


Waziri Biteko Aanza kazi

$
0
0


Waziri wa Madini Doto Biteko (katikati) akieleza jambo wakati wa kikao cha Menejimenti ya Wizara na Taasisi zake. Kulia ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. Simon Msanjila.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza jambo wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya Watendaji wa Wizara na Taasisi wakifuatilia kikao hicho
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula akizungumza jambo katika kikao hicho.

…………………… 

Waziri Biteko aanza kazi  Awataka watumishi kufanyia kazi maagizo ya Rais Magufuli Amshukuru Waziri Kairuki kuwa, amemfundisha Mengi
Aitaka STAMICO kuanza kutoa gawio kwa Serikali

Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Menejimenti ya Wizara ya Madini, Taasisi zake pamoja na Wenyeviti wa Tume ya Madini na Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), jijini Dodoma, katika kikao ambacho pia kimejadili namna ya kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliyoyatoa wakati akimwapisha Waziri Biteko kushika wadhifa huo Januari 9, 2019.

Biteko amewataka watumishi wa Wizara na Taasisi zake ambao hawayajayasikiliza maagizo yaliyotolewa na Rais Magufuli kuhakikisha kuwa wanayasikiliza ili kuweka uelewa wa pamoja na kushirikiana katika kutekeleza majukumu ya wizara kwa lengo la kuhakikisha kwamba sekta ya madini inaimarika.

“ Tuliulizwa dhahabu inauzwa wapi? Basi tusisubiri tena Rais atuulize inauzwa wapi,” amesisitiza Biteko. Aidha, amesisitiza kuwepo kwa ushirikiano wa pamoja miongoni mwa watumishi wa wizara katika utekelezaji wa majukumu hayo na kusisitiza kuhusu mabadiliko yanayoonekana kupitia sekta ya madini ikiwemo kufanya kazi na kuongeza kuwa, “ Kinachotuunganisha mahali hapa ni kazi na wala si dini ama jambo lingine,”.

Ameongeza kuwa, kiu kubwa ya Rais Magufuli ni kuona kuwa watanzania wote wananufaika na rasilimali madini huku akisisitiza kuwa, kiu yake binafsi ni kuona taswira nzuri inajengeka kuhusu sekta hiyo ikiwemo kufanya kazi kwa weledi na kuongeza kuwa, matokeo bado hayaonekani.

“Vipaji mlivyonavyo mvitumie vizuri vitoe matokeo yanayoonekana. Fanyeni kazi ambazo zitaacha matokeo yatakayo dumu. Natamani ningezungumza na watumishi wote ili kila mmoja aelewe kile ninachosema,” amesisistiza Biteko.

Vilevile, amewataka watendaji kuchukua hatua badala ya kutumia muda mrefu kutafuta miongozo wakati wanapotekeleza majukumu jambo ambalo linachelewesha utekelezaji wa majukumu. “ Unasubiri mwongozo gani ilhali unayo Sheria ya Madini?amehoji Waziri Biteko. Pia, amechukua fursa hiyo kumshukuru aliyekuwa Waziri wa Madini Angellah Kairuki na kueleza kuwa, ni kiongozi ambaye amemfundisha mambo mengi.

“ Namshukuru sana dada yangu, rafiki yangu Angellah. Alinipokea vizuri sana. Hakuna ushirikiano nilioukosa kwake. Amenifundisha mengi ikiwemo kukaa kwenye kikao na kujadili mambo kwa kina,” amesema Biteko. Pamoja na hayo, Biteko ametumia fursa hiyo kumshukuru Naibu Waziri Nyongo kwa kuwa naye pamoja katika kipindi chote ambacho alikuwa Naibu Waziri katika wizara ya madini.

Katika hatua nyingine, Waziri Biteko ameitaka STAMICO kuhakikisha kuwa, inaanza kutoa gawio kwa Serikali na ikiwezana, jambo hilo lifanyike kabla ya mwaka ujao wa fedha. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, awali akizungumza katika kikao hicho, amewataka watumishi ambao hawakupata fursa ya kusikia maagizo ya Rais Magufuli kufanya hivyo ili kila mmoja asimame kwa lengo moja.

“ Hatukusemwa vizuri. Nchi nzima imesikia na dunia imesikia. Tukiendelea hivi, hatutavumiliwa,” amesisitiza Nyongo. Pia, ameitaka Tume ya Madini kuhakikisha inazingatia na kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Rais Magufuli ikiwemo kutekeleza wajibu wao.

Awali, akizungumza katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila amesema kwamba, kikao hicho ni cha kwanza na Waziri Mpya ikiwemo Mjumbe wa Bodi ya STAMICO na kuongeza kuwa, kinalenga kutoa utambulisho rasmi wa Waziri Mpya wa Madini na kusikia maelekezo ya Waziri Biteko kufuatia maagizo yaliyotolewa na Waziri.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO, Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo amemweleza Waziri Biteko kuwa, anayapokea majukumu yote yaliyo mbele yake ya kuhakikisha kwamba shirika hilo linatekeleza majukumu yaliyo mbele yake.

Kikao hicho kimefanyika tarehe 11 Januari, 2019

WANAFUNZI WA KIKE 235 MKOANI PWANI WAPATA MIMBA KIPINDI CHA MWAKA 2018

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

WANAFUNZI wa kike 235 wa shule za msingi na sekondari mkoani Pwani wamepata mimba katika kipindi cha mwaka 2018 ,hali ambayo ni mbaya. 

Kutokana na takwimu hiyo, kamati ya ushauri ya mkoa wa Pwani (RCC) imekemea vikali masuala ya mimba za utotoni ,na kuagiza sheria ichukue mkondo wake kwa wale ambao wamehusika kuwapa mimba wanafunzi hao.

Akizungumza kwenye kikao cha ushauri cha mkoa huo, ofisa elimu mkoa wa Pwani, Abdul Maulid alisema kati ya wanafunzi hao, 155 ni wanafunzi wa shule za sekondari.

Alieleza, wanafunzi wengine 80 waliopata mimba katika kipindi hicho ni wa shule za msingi. "Mikoa ya wenzetu kama Kilimanjaro tujiulize kwanini wanafunzi hawapati mimba ,tushirikiane kupiga Vita tatizo hili ,"

"Madereva bodaboda, jamii ishirikiane na serikali kupambana na namba hii, bodaboda msiwe chanzo cha kupakia wanafunzi hawa na kuwarubuni kuwapa mimba "alisisitiza Maulid. Hata hivyo, alielezea, changamoto ya shule kuwa umbali mrefu, wanafunzi kukosa chakula mashuleni ni chanzo moja wapo cha wanafunzi kupata mimba. 

Nae mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo alisema vyombo vya dola visiwafumbie macho wahusika wa mimba hizo. Alisema, namba hiyo ni kubwa hivyo sheria ichukue mkondo wake na wafungwe miaka 30 jela ili iwe fundisho. 

Ndikilo anawataka ,wazazi na walezi kuacha kumalizana kesi za mimba za utotoni majumbani na kurubuniwa fedha ili kuwaachia huru wanaobainika kuwapa mimba watoto wao wakike. 

KWA UNAYOFANYA...RAIS WANGU MAGUFULI YAANI AGIZIA CHOCHOTE TU MIMI NITALIPA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JANUARI 11,2019 yaani jana tu nami niliungana na mamilioni ya Watanzania kutazama angani wakati wa ujio wa ndege yetu mpya ya Airbus 220-300 inawasili.

Ndege hiyo iliwasili katika ardhi ya Tanzania saa 8:30 mchana ,ilikuwa kwenye Uwanja wa Ndege wa zamani katika Jiji la Dar es Salaam.Hakika ilikuwa raha wakati ndege hiyo mpya na kisasa inawasili .

Kwa kuwa nami ni mkazi wa Dar es Salaam nikaona haitoshi kutazama tu angani wakati naweza kwenda kuiona kwa karibu.Nikaona isiwe taaabu bwana, saa nne asubuhi nikawa nipo uwanjani nasubiri mali mpya ya Tanzania.

Unashangaa ninaposema mali mpya? Huo ndio ukweli wenyewe maana Serikali yetu imenunua ndege hiyo kwa fedha tasilimu.Ni ndege ambayo ndio toleo jipya kwa sasa ni Tanzania tu ndio tunayo kwa Bara zima hili la Afrika.

Unayesoma makala haya ningekuwa nakuona au nakuelezea mbele yangu ningekwambia piga makofi.Ila kwa kuwa unaisoma utachagua mwenyewe unataka kushangilia kwa staili gani.Ujue si jambo dogo kununua ndege tena bila kukopa fedha kwa mtu.

Kabla ya kwenda mbali naomba niwapongeze Watanzania wote kwa kukubali kutenga muda wenu wa kuangalia angani wakati ndege inawasili.Mlikubali kubadili ratiba ya kazi ya macho ya kuona kwa siku ya jana.Uzuri wa Mungu kila mtu alimmilikisha viuongo na kisha kumuacha apange mwenyewe anavitumiaje.

Huenda bila ujio wa ndege hiyo kuna Watanzania macho yao yangekuwa yanaangalia mashamba ya mpunga,yangekuwa yanaangalia shughuli za kilimo au hata yangekuwa yanaangalia marudio ya mechi za mpira ambazo zinaendelea katika ligi mbalimbali duniani.

Kwa jana Watanzania wakasema isiwe tabu macho yote angani.Hongereni kwa uzalendo wenu kwa Taifa letu la Tanzania.Taifa ambalo linakila kitu cha kujivunia.Ni Taifa ambalo lilikosa ndege tu lakini nalo limebaki historia.Tunazo.

Hadi kufika jana sasa tunamiliki ndege zetu wenyewe mpya kabisa sita na ndege ya saba aina ya Dream liner itaingia nchini mwaka huu huu.Usishingae ndio hivyo tena.Kwa lugha za mtaani tunasema kwenye sekta ya ndege Tanzania kumenoga,kumedamshi na hata ukitaka kusema mambo ni moto utakuwa sawa.

Jana kama ambavyo nimetangulia kueleza hapo juu sikutaka kujipunja kwani mapema nilishaingia uwanja wa ndege na ikabaki kusubiri ndege yetu itue.Uwanjani kila ambaye nilikuwa namuangalia usoni alikuwa ametawaliwa na furaha.Ugumu wa Januari hakufanya tushindwe kuonesha furaha iliyopo moyoni.

Tanzania imekubali kuanza katika kuboresha sekta ya anga.Basi wakati tunasubiri ndege ije wananchi waliokuwepo hapo walikuwa wakipata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiongozwa na bendi ya TOT.

Sauti ya mwanamama Hadija Kopa ilipenya kwenye sikio la kila akiyekuwa uwanjani.Kama unavyomjua Hadija kwa mashauzi yake akiwa ameshika kipaza sauti.Mbona ilikuwa raha.Mama anazeekana uhodari wake.

Ujue bwana pamoja na yote hayo moyo,akili na mwili vyote vinaniambia nachelewa kutoa pongezi kwa Rais wetu mpendwa Dk.John Magufuli.Kwa kuwa moyo wangu unaona nachelewa na mimi sitaki kugombana nao,naomba niseme hivi "Hongera Rais Magufuli kwa uzalendo wako kwa Taifa letu.Hongera Rais kwa mipango na mikakati inayotekelezeka.

" Hongera Rais Magufuli kwa dhamira yako njema kwa Taifa letu,tangu Watanzania tukuchague ili uwe Rais wetu ndani ya miaka mitatu umenunua ndege sita na ya saba itakuja karibuni.Hongera kwa kazi nzuri unayofanya ya kuboresha sekta ya anga.

Hongera Rais Magufuli kwani dhamira yako kuhusu Tanzania mpya tunaiona kwa vitendo.Hongera....Hongera...Hongera Rais,jukumu langu na Watanzania wengine ni kuendelea kukuombea kwa Mungu akupe afya njema na maisha marefu."

Eti unajiuliza hongera zote hizi kwa Rais za nini? Sitaki kumjibu anayeulizwa swali la aina hii maana huenda haishi ndani ya nchi.Watanzania wanaona yanayofanywa na Rais Magufuli. Watanzania ni mashuhuda wa mambo makubwa yanayofanywa na Rais.Kuna ndege sita tayari zipo nchini halafu tusimsifu na kumpongeza.Itakuwa dhambi tena dhambi kubwa.Binafsi sitaki kuwa kwenye dhambi hiyo acha nirudie tena kusema "Hongera Rais wangu."

Najua wako wanaoumizwa na kasi ya maendeleo ambayo Tanzania inayafanya kwa sasa.Hata hivyo watu wa aina hiyo wamechelewa na wataendelea kuumia sana.Walitamani tubaki hatuna ndege waendelee kusema.

Najua wengine ndio mtaji wao wa kuombea kura.Wakati wa kampeni tulikuwa tunawasikia wanasema hooo Rwanda ni nchi ndogo wanandege kibao lakini Tanzania pamoja na ukubwa wake haina ndege.Walikuwa wanapata kura kwa kusema maneno kama hayo.

Unadhani kesho watazungumza lugha gani ya kuombea kura kwa wananchi.Walioona hiyo ndio stahili ya kuombea kura kwa kuorodhesha matatizo yetu.Kwa sasa wameumia.Tena wameumia haswa.Hata hivyo hiyo si ajenda yangu maana naona unakunja sura.

Kwanza Rais wetu ameshasema maendeleo hayana chama.Watanzania wote ni jukumu letu kuijenga Tanzania mpya.Na kweli Watanzania wameamka haswaa.Wamekuwa wamoja na wanachotaka kusikia ni kauli za kuhamasisha maendeleo. Zile kauli za kukejeli mambo ya maendeleo hakuna mwenye muda nazo tena.Kweli Rais amefanikiwa kutuondoa kwenye aibu.Leo kila kinachofanyika kinatokana na fedha zetu.

Kila unachokiona kinafanyika msingi mkubwa ni kodi ya Mtanzania.Hivyo kama tunazungumzia ujio wa ndege mpya maana yake wewe unayelipa kodi fedha yako imetumika kununua ndege.Kwa lugha rahisi unamiliki ndege ambayo umeinunua kwa fedha yako kupitia kodi.

Halafu nikwambie kitu,nilitaka kusahau .Jana wakati ndege inakuja viongozi wa dini walipata nafasi ya kuombea dua kwa akili ya Taifa.Ni jambo la kawaida kuomba dua lakini nikiri Askofu Zacharia Kakobe kabla ya kuomba dua aliomba azungumze japo kidogo.

Kwanza nilianza kujiuliza Askofu Kakobe anataka kuzungumza nini? Ujue Askofu Kakobe kwa miaka mingi amekuwa akionekana zaidi kwenye mikutano ya na vikao vya wapinzani.Amekuwa akitoa matamko ya kuonesha hakuna ambacho kimefanyika.Mzee yule amekiri kazi ambayo Rais Magufuli anaifanya yeye pamoja na ubishi wake lakini amekubali.Ametamka mwenyeweee.Kweli tena.

"Mimi ni mbishi sana katika kukubali,leo mpaka nimekuja hapa Rais amenikuna kwa mambo anayoyafanya kwa akili ya nchi yetu.Anastahili sifa na heshima.Najua hawawezi kukusifu watu wote Rais Na ukiona unasifiwa na kila mtu basi kuna tatizo.Niseme tu unafanya kazi nzuri Rais Na lazima tuseme hadharani kwa kukusifu na kukuheshimu," amesema Askofu Kakobe.

Amezungumza mengi lakini hicho ambacho nimekinukuu ni moja ya kauli zake muhimu ambazo zitadumu kwenye masikio ya Watanzania kwa miaka mingi ijayo.Hongera Askofu Kakobe kwa kueleza ukweli wa kutoka moyoni mwako.Najua wapo watakaokubeza lakini umesema ukweli na kweli itakuweka huru.

Pamoja na yote hayo ukweli ni kwamba Watanzania huu ni wakati wa kuungana na Rais Magufuli kuhakikisha mipango yake ya kuiletea nchi maendeleo inafanikiwa.Nakumbuka wakati anazungumza uwanjani hapo Rais amesema Watanzania tunaweza kufanya mambo makubwa zaidi na kama ndege kuja basi zitaendelea kuja zaidi na zaidi.

Amehimiza Watanzania kuijenga Tanzania mpya.Tanzania ambayo itakuwa na huduma bora katika sekta mbalimbali na kwake anaamini anaiona Tanzania mpya ambayo itakuwa haina tofauti na Ulaya.Rais Watanzania wamekusikia na kiuu ya kila nmoja wetu ni kuiona Tanzania mpya chini ya uongozi wako .

Nikwambie tu Rais wangu huko mtaani Watanzania wanakukubali sana.Wanasema umekuja wakati sahihi na wanaamini huenda ujio wako ni mpango wa Mungu.Naomba kama itakupendeza Mheshimiwa Rais kwa hii kazi nzuri ambayo unaifanya naomba agizia chochote nitakuja kulipa.Najua kwa nafasi yako unaweza kupata chochote na kwa wakati wowote,lakini kwa furaha niliyonayo naomba agiza chochote mimi nitalipa tu.

Tuwasiliane kwa 0713833822.


Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images