Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

PTF YAPONGEZWA KWA KUTEKELEZA SERA YA UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0
Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) umepongezwa kwa utekelezaji mzuri wa Sera ya Uchumi wa Viwanda inayohimizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa mikopo kwa makundi maalumu ya watu wenye ulemavu, akina mama na vijana wanaojihusisha na shughuli za ujasiriamali jijini Dar es Salaam.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa ziara ya kikazi ya kuwatembelea watumishi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea  kwa lengo la kufahamu majukumu ya mfuko huo na kuhimiza uwajibikaji, ambapo alipata fursa ya kujionea wanufaika wa mikopo inayotolewa na mfuko huo.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, makundi yaliyopatiwa mikopo ambayo ni kundi maalumu la walemavu la Furaha ya Wanawake Wajasiriamali Viziwi Tanzania (FUWAVITA), kikundi cha UWAZI  SHALOOM cha akina mama wasindikaji, Kikundi cha MAKINI FOOD SUPPLIES cha akina mama wasindikaji na kikundi cha MAB cha vijana ni mfano mzuri wa kuigwa kwa kutekeleza sera ya Uchumi wa viwanda kwa vitendo kwani wanazalisha bidhaa zenye ubora ambazo ni mvinyo, viungo vya mchuzi, viungo vya chai, siagi ya karanga, mango pickle na mabeji ya wanafunzi wa shule za awali, za msingi na vyuo.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) wakati wa ziara ya kikazi alipowatembelea ofisini kwao jijini Dar es Salaam  kwa lengo la kufahamu majukumu ya mfuko na kuhimiza uwajibikaji, ambapo pia alipata fursa ya kujionea wanufaika wa mikopo inayotolewa na mfuko huo.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akikabidhiwa nyaraka mbalimbali na Mkurugenzi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) Bi. Haigath Kitala mara baada ya mkurugenzi huyo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji  wakati wa ziara ya kikazi ya Dkt. Mwanjelwa katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam,  ziara ilikuwa na lengo la kufahamu majukumu ya mfuko na kuhimiza uwajibikaji.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza maelezo ya Bi. Rose Kalulika kuhusu bidhaa zinazozalishwa  na kikundi cha akina mama cha UWAZI SHALOOM  wakati wa ziara ya  kikazi katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam,  ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika hao wa mikopo inayotolewa na PTF.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishuhudia bidhaa zinazotengenezwa na  kikundi cha Furaha ya Wanawake Wajasiriamali Viziwi  Tanzania (FUWAVITA), kikundi cha UWAZI  SHALOOM cha akina mama wasindikaji, Kikundi cha MAKINI FOOD SUPPLIES cha akina mama wasindikaji na kikundi cha MAB cha vijana  wakati wa ziara yake ya  kikazi katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam,  ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika hao wa mikopo inayotolewa na PTF.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


TAARIFA KUHUSU WAGONJWA 45 KUFANYIWA UPASUAJI WA MOYO WA KUFUNGUA NA BILA KUFUNGUA KIFUA

$
0
0
WAGONJWA 45 KUFANYIWA UPASUAJI WA MOYO WA KUFUNGUA NA BILA KUFUNGUA KIFUA KATIKA KAMBI MAALUM YA MATIBABU YA MOYO INAYOFANYIKA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KUANZIA TAREHE 7/01/2019  HADI 18/01/2019


Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kupitia madaktari wake bingwa wa magonjwa ya moyo kwa kushirikiana na Madaktari Afrika na Shirika la Cardio Start wote kutoka nchini Marekani  wameanza  kambi maalum ya matibabu ya moyo  ya siku 12  kwa watu wazima .

Matibabu yanayofanyika  katika kambi hiyo ni upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua. Upasuaji wa bila kufungua kifua unafanyika kupitia tundu dogo linalotobolewa kwenye paja kwa wagonjwa kuzibuliwa mishipa ya moyo iliyoziba (Percutaneous Coronary Intervention - PCI) na kuwekewa vifaa  vinavyosaidia kurekebisha mapigo ya moyo ambavyo ni (Permanent Pacemaker na High powered devices CRT-P, CRT –D) .

Wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo ya moyo ambayo ni  valve, mishipa ya moyo iliyoziba, moyo kushindwa kufanya kazi vizuri, matibabu kwa watu wazima waliozaliwa na matatizo ya moyo na wale wenye matatizo ya moyo yaliyotokana  na ugonjwa wa Kisukari

Kambi hii inaenda  sambamba na utoaji wa elimu kwa madaktari na wauguzi pamoja na kubadilishana ujuzi wa kazi kwa wageni na wataalamu wetu. Katika kambi hii tunatarajia kufanya upasuaji wa kufungua kifua kwa wagonjwa  20 na bila kufungua kifua kwa wagonjwa 25. Hadi leo tarehe 8/1/2019 jumla ya wagonjwa nane wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua na wagonjwa wanne wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua.

Hii ni kambi ya kwanza ya matibabu ya moyo tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2019 na ni mara ya kwanza kwa shirika Cardio Start  kuja  hapa nchini kufanya kazi na sisi.
Imetolewa na:

Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
08/01/2019

WALIOVAMIA SWAGASWAGA WAPEWA SIKU 14 KUONDOKA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Kondoa Sezaria Makota ametoa siku 14 kwa wananchi wote waliovamia hifadhi  ya pori la akiba la Swagaswaga kuondoka ndani ya hifadhi kabla ya kuondolewa kwa nguvu. Ameyasema hayo alipokuwa akiongea katika mikutano ya hadhara  na wananchi wa mitaa ya Mongoroma na Serya ili iliyofanyika katika maeneo hayo.

Aliongeza kuwa serikali inayafanya hayo ili kuendelea kuhifadhi rasilimali muhimu zilizomo ndani ya hifadhi hiyo ili ziongezeke na kuongeza idadi ya watalii ambao watakuja kwa wingi kupumzika ndani ya hifadhi baada viongozi mbalimbali kuhamia Dodoma. “Ni wakati maalum sasa watu waheshimu mipaka ya hifadhi na wasikae ndani ya hifadhi sababu serikali ina mkakati  wake madhubuti wa kuendeleza hifadhi zote kama sehemu ya kuongeza pato la nchi”.Alisema Makota

Aliongeza kuwa kaya zote zilizomo ndani ya hifadhi na zinafahamika hivyo ni wakati muafaka kwa wao kuondoka  na kuacha kulima kwa mwaka huu kwani wapo waliokata misitu na kuandaa mashamba. “Pia kwasasa serikali imefanya utaratibu wa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika maeneo ya wananchi wanaopakana na hifadhi ambapo kwa sasa wapo katika vijiji vinavyopakana na Tarangire ambapo pia ipo katika wilaya ya Kondoa lengo likiwa ni kuweka matumizi ya kila ardhi husika.”Alifafanua Sezaria

Aidha akiuliza kwa niaba ya wananchi wengine Bwana Hassan Juma alitaka kujua wananchi walio ndani ya hifadhi na walishafanyiwa tathmini watalipwa lini sababu wameshaambiwa wahame?Akijibu meneja wa pori la Swagaswaga Bwana Choya Alex alisema kuwa kuna zoezi lililofanyika ni la kutambua kuna kaya ngapi  ndani ya hifadhi kutokana na maelekezo ya wizara na ilifanyika kama   kama sensa na si uthaminishaji ambao huusisha watu wa kada mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya Kondoa Sezaria Makota akitoa maelekezo ya kuondoka katika pori la hifadhi ya Swagaswaga wananchi wa mtaa wa Mongoroma.
Wananchi wa mtaa wa Serya wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Sezaria Makota (Hayupo pichani) katika mikutano ya hadhara  na wananchi wa mitaa ya Mongoroma na Serya 
Mkuu wa Wilaya Sezaria Makota akisistiza jambo kwa wananchi katika mikutano ya hadhara  na wananchi wa mitaa ya Mongoroma na Serya.

RAIS DKT. SHEIN AFUNGUA JENGO JIPYA LA WAKALA WA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI NA UZINDUZI WA MAABARA YA VINASABA MARUHUBI LEO

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Jengo Jipya la Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, pamoja na Uzinduzi wa Maabara ya Vinasaba.(DNA),hafla hiyo imefanyika maruhubi Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kulifungua Jengo Jipya la Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Maruhubi Zanzibar, kushoto Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar, Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Mhe. Rashid Ali Juma.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Slim Rashid Juma, akitowa maelezo ya picha ya jengo hilo jipya la Mkemia Mkuu baada ya kulifungua leo rasmin, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar,
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mchunguzi wa Maabara ya Vinasaba (DNA) (Genitic Analyzer) Bi. Saide Abdalla Mbarak,akitowa maelezo ya matumizi ya mashine hiyo wakati wa ufunguzi wa Maabara ya Vinasaba (DNA) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jengo la Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Maruhubi Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na Kaimu Waziri wa Afya na Waziri wa Kilimo,Maliasili Mifugo na Uvuvi Mhe. Rashid Ali Juma,wakiongea wakati wakielekea katika eneo maalum kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi na Wafanyakazi wa Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya Uzinduzi wa Jengo Jipya na Maabara ya Vinasaba (DNA) ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
WAFANYAKAZI wa Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali  wakishangilia wakati wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Jengo Jipya la Mkemia Mkuu wa Serikali Maruhubi.(Picha na Ikulu) 
  

DKT.NDUGULILE: TUNATAKA TAIFA LA MABINTI WASOMI

$
0
0
Na Mwandishi Wetu Mbinga
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile ameitaka jamii kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu ili kuwa na Jamii yenye mabinti wasomi na kuondokana na ukandamizaji wa watoto wa kike na wanawake.

Dkt. Ndugulile ametoa rai hiyo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakati akishirikiana na wananchi katika ujenzi wa Bweni la shule ya Sekondari Mikalanga ambalo kwa kiasi kikubwa wananchi wametoa nguvu zao katika kufanikisha ujenzi huo.

Dkt. Ndugulile amesisitiza kuwa suala la elimu kwa mtoto wa kike na muhimu kutokana na changamoto za mtoto wa kike hasa suala la mimba za utotoni ambazo zinapelekea kupotea kwa ndoto za wanafunzi wa kike wengi.

Naibu Waziri Ndugulile amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu zilizopo Mtoto mmoja kati ya watoto watatu wa kike hupata mimba za utotoni na kukatisha ndoto za Mtoto wa kike kupata elimu kati ya miaka 15 mpaka 19 ikiwa sawa na asilima 27.


  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiwasili katika shule  ya Sekondari Mikalanga akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Cosmas Nshenye na Mbunge wa Viti Maalum kwa mkoa wa Ruvuma Mhe. Jacquiline Ngonyani kwenda kushirikiana na wananchi katika ujenzi wa bweni la wasichana shuleni hapo.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia kikundi cha ngoma za asili  katika shule  ya Sekondari Mikalanga akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe.Cosmas Nshenye na Mbunge wa Viti Maalum kwa mkoa wa Ruvuma Mhe. Jacquiline Ngonyani kwenda kushirikiana na wanachi katika ujenzi wa bweni la wasichana shuleni hapo.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akishirikiana na  Mbunge wa Viti Maalum kwa mkoa wa Ruvuma Mhe. Jacquiline Ngonyani katika ujenzi wa bweni la wasichana katika Shule  ya Sekondari Mikalanga.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi waliojitokeza kushirki katika ujenzi wa bweni la wasichana katika shule  ya Sekondari Mikalanga ikiwa ni juhudi za  wananchi kupunguza adha ya watoto wa kike kupata mimba shuleni.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikabidhi mmoja ya mifuko 50 aliyochangia katika ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Mikalanga ikiwa ni juhudi za  wananchi kupunguza adha ya watoto wa kike kupata mimba shuleni.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAMADUNI ZENYE MADHARA ZALETA ATHARI KWA WANAWAKE MKOANI MARA

$
0
0
Na Anthony Ishengoma-Mara.
Jamii mkoani Mara bado inaendeleza mila potofu ya kuamini kuwa mwanamke asiyekeketwa ni mkosi kwa familia jambo ambalo linaendeleza vitendo vya kwa ukatili wa hali ya juu dhidi ya wanawake Mkoani humo.

Akiongea wakati wa ufanguzi wa Kikao kazi cha uzinduzi wa Kampeini ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto   leo Mkoani Mara Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Karolina Mtaphula amesema inapotokea binti anayekeketwa akapoteza maisha kutokana na ukeketaji binti huyo amekuwa akitupwa polini bila kuzikwa kwa taratibu za kawaida kwasababu jamii pia inaamini ni mkosi kwa jamii na kwa familia yake.

Aidha Mtapula aliongeza kuwa Jamii ya Mkoa wa Mara inatakiwa ijilinganishe na mikoa mingine ambayo haina mila ya ukeketaji ili kujenga ufahamu kuwa wanawake kutoka jamii hizo kama wamekuwa wakileta mikosi katika familia zao kama amabavyo mila zao inawafanya waamini.

‘’Wanawake katika Mikoa ambayo haina ukeketaji wanazidi kupiga hatua za kimaendeleo na kufaidika kielimu lakini katika Mkoa wa Mara mila potofu imeendelea kurudisha nyuma maendeleo ya wanawake hivyo nawaomba mlinganishe na jamii hizi kuona kama kweli wanawake wasipokeketwa wanaleta mikosi’’. Alendelea kusema Mtapula.
 Katibu Tawala Mkoa wa Mara Karolina Mtaphula akitoa hutuba yake wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kinachoendelea Mkoani Mara kuandaa ujumbe utakaotumika katika mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Afisa Maendeleo ya Jamii  Mkoa wa  Mara  Neema Ibamba akitoa maelezo wakati wa  kuandaa ujumbe utakaotumika katika mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Wajumbe wakikao kazi cha kuandaa ujumbe kwa ajili kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Mara Karolina Mtaphula akitoa mara baada ufunguzi wa kikao kazi leo Mkoani humo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAKONDA AELEZEA MIPANGO YA KUFANIKISHA WANAFUNZI WOTE WALIOFAULU WANAENDELEA NA MASOMO KIDATO CHA KWANZA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKOA wa Dar es Salaam umeweka wazi mipango yake ya kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa madarasa 622 unakamilika kwa wakati lengo la kufanikisha wanafunzi 31,092 ambao ni sawa na asilimia 47 ya watoto 64,861 waliofaulu katika mkoa huo wanaendelea na masomo yao ya kidato cha kwanza.

Lengo kuu ni kuhakikisha hakuna mwanafunzi yoyote ambaye ataachwa kwasababu ya kigezo cha uhaba wa madarasa huku Mkoa huo ukisisitiza umejipanga vema katika hilo kwa kuweka mikapango sahihi yatakayofanikisha lengo hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaambiwa waandishi wa habari leo kwamba wanafunzi hao wote watakwenda shuleni na kwamba ongezeko la wanafunzi na ufaulu ni matokeo ya mafanikio ya Rais Dk.John Magufuli kutokana na kutengwa kwa fedha zaidi ya Sh.bilioni 29 kila mwezi kwa ajili ya kufanikisha elimu bure na kati ya fedha hizo Sh.bilioni 17.46 zinaenda kwenye elimu ya sekondari.

"Tayari Serikali imejipanga na tayari tangu Januari 7 mwaka huu shule zote za sekondari 147 zimefunguliwa, hivyo kila mzazi ahakikishe anamuandikisha mtoto ili kuendelea na kidato cha Kwanza,"amesema na kusisitiza wanafunzi, wazazi na walezi wasiwe na wasiwasi kwenye hilo kwani wanaotakiwa kwenda shule wote watakwenda.

Wakati huo huo Makonda amesisitiza katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa Mkoa wa Dar es Salaam umekuwa kinara kutokana na kufaulisha wanafunzi 64,861 sawa na asilimia 92 ambapo kati ya hao wanafunzi 31,092 walikosa vyumba vya madarasa jambo lililoilazimu Serikali kupambana kuhakikisha kila aliefaulu anaendelea na masomo.

Ameongeza lengo la ujenzi wa madarasa hayo ni kuhakikisha kila mwanafunzi anatumia fursa ya elimu bure inayotolewa na Rais Magufuli ya kuhakikisha mtoto wa maskini anasoma ili kujikwamua kiuchumi na mwisho wa siku Taifa liwe na wataalamu wa kutosha.Makonda ametumia nafasi hiyo kutoa onyo kwa wanafunzi ambao watabainika kukwepa masomo kwani watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa kisheria na hivyo wote ambao wamefaulu na wanatakiwa kuingia kidato cha kwanza waendelee na masomo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh.Paul Makonda akisikiliza kwa makini baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa na baadhi ya Waandishi wa Habari aliyokuwa akizungumza nao leo Ofisini kwake kuhusu mipango yake ya kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa madarasa 622 unakamilika kwa wakati, lengo la kufanikisha wanafunzi 31,092 ambao ni sawa na asilimia 47 ya watoto 64,861 waliofaulu katika mkoa huo wanaendelea na masomo yao ya kidato cha kwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh.Paul Makonda akisizungumza mbele ya Waandishi wa Habari leo Ofisini kwake  kuhusu mipango yake ya kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa madarasa 622 unakamilika kwa wakati, lengo la kufanikisha wanafunzi 31,092 ambao ni sawa na asilimia 47 ya watoto 64,861 waliofaulu katika mkoa huo wanaendelea na masomo yao ya kidato cha kwanza.

WAFUGAJI WATAKIWA KUACHANA NA KUHAMAHAMA

$
0
0
Jamii ya wafugaji imetakiwa kuhakikisha watoto wao wanajiunga na shule za msingi na sekondari, mara baada ya shule hizo kufunguliwa wiki hii na kuachana na mtindo wa kuhamahama na mifugo. Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Sipitieck ameyasema hayo wakati akimsimika Diwani wa Kata ya Naisinyai Kilempu Ole Kinoka kuwa kiongozi wa kimila (Laigwanani) wa Jumuiya ya Kishapuy. 

Sipitieck alisema jamii ya wafugaji inatakiwa kubaki eneo moja kusomesha watoto wao na kuachana na maisha ya kuhamahama na watoto wao ili kutafuta malisho ya mifugo. "Hivi sasa serikali imewekeza miundombinu bora kwenye elimu hivyo jamii ya wafugaji inapaswa kutumia fursa hiyo kwa kusomesha watoto," alisema. 

Hata hivyo, alisema wilaya hiyo imejipanga kuhakikisha wanafunzi wapya wa shule za msingi na sekondari wanapata nafasi kwa kuongeza vyumba vya madarasa. Ole Kinoka akizungumza baada ya kusimikwa ameomba ushirikiano kwa viongozi na jamii kwa ujumla ili aweze kutumikia vyema nafasi hiyo.
 Diwani wa Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Kilempu Ole Kinoka akizungumza baada ya kusimikwa kuwa kiongozi mkuu wa kimila (Laigwanani) wa jamii ya Kishapuy. 
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Sipitieck (kulia) wakishuhudia ngoma ya jamii ya wamasai wakati wa kusimikwa kwa Diwani wa Kata ya Naisinyai Kilempu Ole Kinoka (wapili kulia) kuwa kiongozi wa kimila (Laigwanani) wa jamii ya Kishapuy. 
 Diwani wa Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Kilempu Ole Kinoka akikabidhiwa katiba ya jamii ya Kishapuy na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Jackson Sipitieck baada ya kusimikwa kuwa kiongozi wa kimila (Laigwanani) wa jamii hiyo. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Leskary Sipitieck akizungumza baada ya kumsimika Diwani wa Kata ya Naisinyai, Kilempu Ole Kinoka kuwa kiongozi wa kimila (Laigwanani) wa jamii ya Kishapuy. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MISRI YAPEWA WENYEJI WA MICHUANO YA KOMBE LA AFRIKA (AFCON 2019)

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Globu ya Jamii

Shirikisho la Kandanda Barani Afrika (CAF) limeipa wenyeji wa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika taifa la Misri kwa mwaka huu wa 2019 baada yakuishinda Afrika Kusini kwa kura zakuwania uandaaji wa Michuano hiyo.

Mashindano hayo yalikuwa yaandaliwe na taifa la Cameroon kwa mwaka huu, mwezi Novemba CAF iliipokonya maandalizi hayo kutokana na kuwa na maandalizi hafifu. Misri itakuwa na muda wa miezi 6 tu kufanya maandalizi kwa ajili ya ugeni wa Mataifa 24 yatakayoshiriki Michuano hiyo mwezi June.

Hata hivyo itakuwa ni mara ya Tano kwa Misri kuandaa Mashindano hayo tangu mara ya mwisho mwaka 2006 ilipoandaa Mashindano hayo."Napenda kuishukuru Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Kandanda barani Afrika (CAF) kwa kutuamini kuandaa Mashindano haya makubwa barani Afrika na naishukuru Serikali yetu kwa kuunga mkono suala hili,’ amesema Rais wa Shirikisho la Kandanda nchini Misri (EFA), Hany Abu Rida.

"Tuliandaa Mashindano haya 2006 ambapo ilitupa sana changamoto kufanya vizuri, lakini kwa sasa tuko vizuri,’ amesema Abu Rida."Serkali imetuhakikishia kutusaidia ili kuhakikisha tunashuinda dhidi ya Afrika Kusini ambapo pia itatusaidia kufanya vizuri katika mashindano haya, Mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi viwanjani naamini tutakuwa vizuri katika mashindano haya, amesema Makamu wa Rais wa EFA, Ahmed Shobair.

Misri itatumia viwanja Nane katika Mashindano hayo, vitakavyokuwa katika Miji Mitano ya Alexandria, Ismailia, Port Said, Suez na Mji Mkuu wa Cairo.CAF inatarajia kuitangaza rasmi Misri Jumatano ya Januari 9 kuwa ni mwenyeji wa Mashindano hayo.

CHANZO: BBC SPORTS

SERIKALI KUSAINI MIKATABA YA UBANGUAJI WA KOROSHO JANUARI 10

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara

Serikali imesema kuwa tarehe 10 Januari 2019 itasaini mikataba na wamiliki wa viwanda vya ubanguaji wa korosho waliojitokeza kwa ajili ya kubangua korosho za serikali za msimu wa mwaka 2018/2019 zilizonunuliwa na serikali kwa bei ya Shilingi 3300 kwa kilo.

Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 8 Januari 2019 wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) Mkoani Mtwara.Alisema kuwa hivi karibuni serikali ilitangaza kuwa korosho ghafi zote zitabanguliwa nchini hivyo utekelezaji wa jambo hilo umeanza, ambapo Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko itaingia mikataba ya ubanguaji.

Pamoja na wamiliki wa viwanda kupewa kazi ya kubangua korosho lakini pia serikali imewakaribisha wananchi kujitokeza kubangua korosho za serikali kupitia vikundi au mtu mmoja mmoja. “Wananchi wenye uwezo wa kubangua tunawaomba waende Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo-SIDO) kwa ajili ya kujiandikisha ambapo mpaka sasa watu 126 kwa ajili ya ubanguaji na Tani 29 zimechukuliwa kwa ajili ya kuanza kubanguliwa” Alisisitiza Mhe Hasunga

Katika mkutano huo Waziri huyo wa kilimo Mhe Japhet Hasunga amempongeza Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kushuhudia utiaji wa saini mkataba wa mauziano ya mahindi kati ya Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) wa Bilioni 21 zitakazoiwezesha NFRA kunua mahindi kwa wakulima hivyo kuimarisha soko la nafaka nchini. 
Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza mpango wa serikali kusaini mikataba ya ubanguaji wa korosho wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) Mkoani Mtwara, leo tarehe 8 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) Mkoani Mtwara, leo tarehe 8 Januari 2019.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Prof Siza Tumbo akifatilia mkutano wa Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) Mkoani Mtwara, leo tarehe 8 Januari 2019.



MICHUZI TV; VMAKAMU WA RAIS AALIVYOZINDUA JENGO LA HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO KMKM KIBWENI-ZANZIBAR

RAIS DKT. SHEIN AMTEMBELEA MZEE ALI HASSAN MWINYI NYUMBANI KWAKE MAISARA

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais Mstaaf wa Tanzania Mzeee Ali Hassan Mwinyi alipofika nyumbani kwake Maisara Zanzibar , kumtembelea na kumjulia hali leo 8-1-2019. (Picha na Ikulu)
 RAIS Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, akiongozana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, wakifurahia jambo wakati alipofika nyumbani kwake maisara Zanzibar kumjulia hali leo 8-1-2019, wakitoka baada ya mazungumzo yao.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Rais Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, alipofika nyumbani kwake maisara Zanzibar kumtembelea na kumjulia hali leo 8-1-2019.wakifurahia jambo wakati wa mazungumzo hayo.(Picha na Ikulu)   

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA MABADILIKO MADOGO YA BARAZA LA MAWAZIRI NA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI

BENKI KUU YAFAFANUA KUHUSU USIMAMIZI KWA WATOA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imetoa tangazo kwa umma kupitia tovuti yake (www.bot.go.tz) likiwataka watu na taasisi zote zinazofanya biashara ya huduma ndogo za fedha zilizoko Tanzania Bara (isipokuwa vyama vya ushirika vya
akiba na mikopo – SACCOS) kutoa taarifa zitakazotumika katika utayarishaji wa Kanuni za Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha.

Hayo yamesemwa leo na Meneja Usimamizi wa Maduka ya Fedha na Huduma Ndogondogo za Fedha Victor Tarimu kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania(BoT).Tarimu amesema taarifa hizo zinatakiwa kutumwa Benki Kuu ya Tanzania hadi 31 Januari 2019 na kwamba inatoa ufafanuzi ufuatao kuhusu tangazo hilo kuwa lengo la siyo kuvifunga au kuvibana vikundi vya kijamii kama VICOBA, watu binafsi na taasisi zinazotoa huduma ndogo za fedha kama ambavyo inapotoshwa na baadhi ya watu na mitandao mbalimbali ya kijamii.

"Bali ni kukusanya taarifa za awali kuhusu huduma hizo, kama amnavyo ilivyoainishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kupitisha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, lengo la
sheria hiyo ni kuwalinda wadau wote wanaohusika na huduma hizi (watoaji na watumiaji) kwa kuziwekea utaratibu mzuri zaidi wa uwekaji kumbukumbu, uendeshaji na uongozi kwa ujumla," amesema

Pia kuwalinda wamiliki na watumiaji wa huduma hizo dhidi ya vitendo vinavyoweza kusababisha kupoteza fedha na mali zao, pamoja na
kuzuia watu binafsi, taasisi na vikundi vya kijamii kutumika kufanya uhalifu ikiwemo utakasishaji fedha haramu.

Balozi Seif aweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la shule ya Sekondari ya Uweleni kisiwani Pemba

$
0
0
Wazanzibar wana kila sababu ya kujivunia Maendeleo makubwa yaliyopatikana katika Sekta ya Elimu yaliyosimamiwa na Chama cha Afro Shirazy Party  na Baadae CCM katika kipindi chote cha  Miaka 55 tokea kufanyika kwa Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 yaliyoondoa Utawala wa Kibaguzi katika Elimu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Skuli ya Sekondari ya Uweleni iliyopo Mkoani Kisiwani Pemba katika Smra shamra za kusherehekea Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  ya Mwaka 1964 kutimia Miaka 55.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hatua iliyofikia Taifa hivi sasa katika Sekta ya Kielimu ni kubwa kiasi kwamba wale wanaokebehi wanashindwa kujifahamu kwamba wanajidharau wao wenyewe  na dawa yao ni kupuuzwa kwa sababu hawajui thamani ya kuwa na chao na wala sio watu wanaothamini cha wenzao. Alisema tokea Wananchi wa Zanzibar walipojitawala  kutoka katika makucha ya kibeberu, Vijana wa Visiwa hivi wanaendelea kupata Elimu bila ya malipo, kuanzia maandalizi hadi Sekondari ya Juu ambapo pia wakifikia Vyuo Vikuu kuna utaratibu wa kuwapatia udhamini kwa wale wanaofanya vizuri.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo Jipya la Skuli ya Sekondari ya Uweleni Mkoa wa Kusini Pemba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akizungumza na Wananchi wa Pemba  baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Jengo Jipya la Skuli ya Sekondari ya Uweleni Pemba. Picha na – OMPR – ZNZ.
 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mheshimiwa Mmanga Mjengo Mjawiri akitoa ufafanuzi wa takwimu za ongezeko la Skuli Nchini kabla na baada ya Mapinduzi.
 Baadhi ya Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Uweleni wakifuatilia hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Skuli yao inayojengwa ya Ghorofa.
 Haiba ya Jengo Jipya linalojengwa katika Skuli ya Sekondari ya Uweleni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU WAZIRI DK MABULA AKERWA MAKUSANYO MADOGO YA KODI YA ARDHI KATIKA HALMASHAURI

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM Geita.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amekerwa na makusanyo madogo ya mapato katika halmashauri mbalimbali nchini kupitia kodi ya ardhi.

Akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi wa Halmashauri za Mji na Wilaya ya Geita jana mkoani Geita alipofanya ziara ya kushtukiza kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa katika halmashauri hizo, Dk Mabula alisema, mapato ya sekta ya ardhi katika halmashauri nyingi hayaridhishi na kueleza kuwa halmashauri nyingi mapato yake yako chini ya asilimia 30.

Alisema pamoja na halmashauri hizo kuwa na mapato kidogo kupitia sekta ya ardhi lakini watendaji wake hawaoneshi jitihada zozote kuhakikisha wanakusanya mapato ya kutosha kupitia sekta hiyo na hivyo aliwataka watendaji hao kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato kwa kuwa msisitizo wa serikali ya awamu ya tano ni kukusanya kodi.

‘’Kwa staili hii tutafika kweli? Mna bahati mbaya sasa watendaji wa sekta ya ardhi katika halmshauri mtakuwa chini ya wizara moja kwa moja na rais amepiga kelele kuhuisiana na kodi ninyi mnarelax’’ alisema Dk mabula.
Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akizungumza alipowasili ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita alipofanya ziara katika mkoa huo jana kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake kuhusiana na sekta ya ardhi katika halmashauri za Mji na Wilaya ya Geita.

WAZIRI MKUU AZINDUA JENGO TAASISI YA KARUME

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kufungua jengo jipya la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, iliyopo Mbweni Wilayani Magharibi “B” - Unguja Januari 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi wa jengo jipya la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, iliyopo Mbweni Wilayani Magharibi “B” - Unguja Januari 8, 2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia kitabu kwenye maktaba ya jengo jipya la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, iliyopo Mbweni Wilayani Magharibi “B” – Unguja baada ya kufungua jengo hilo Januari 8, 2019. 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia mfumo wa umeme uliyebuniwa na mwanafunzi Abdulhamid Marijani, baada ya kufungua jengo jipya la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, iliyopo Mbweni Wilayani Magharibi “B” - Unguja Januari 8, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa kitengo cha kompyuta Safaa Haroub, baada ya kuweka jiwe la msingi wa jengo jipya la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, iliyopo Mbweni Wilayani Magharibi “B” - Unguja Januari 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SIMBA KUTUMIA 'YES WE CAN' KUUJAZA UWANJA KATIKA MECHI YAO DHIDI YA JS SAOURA YA ALGERIA ,KUCHUKUA POINT 3

$
0
0
*Manara asema wametumwa na Rais, lazima wachukue ubingwa, wachezaji kutua kesho wakitokea Z'bar

*Asifu uwezo wa Kocha wao,agusia umuhimu wa kununua jezi kuichangia Klabu yao

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KLABU ya Soka ya Simba imesema maandalizi ya mchezo wao dhidi ya JS Saoura ya Algeria Jumamosi ya Januari 12 katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam yanakwenda vizuri ,hivyo imewataka mashabiki ,wanachama wao na wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi na uwanja utakuwa wazi kuanzia saa nne asubuhi.

Pia imesema kutokana na jukumu ambalo lipo mbele yao la kutumwa nchini kwenye mchezo huo la ligi hiyo ya mabingwa Afrika ,wameamua wachezaji wao waliopo kwenye Kombe la Mapinduzi Zanzibar watarudi kesho kwa ajili ya mechi iliyopo mbele yao.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Msemaji wa Klabu ya Simba Hajji Manara amesema wakati wakijiandaa na mchezo huo wa Jumamosi ,mchezaji wao Eras to Nyoni amepata majeraha wakati wa mchezo dhidi ya KMKM ya Zanzibar.

Amefafanua jopo la madaktari wa Simba pamoja na madaktari wataasisi nyingine wametoa ripoti kuwa Nyoni anahitaji tiba maalum na mapumziko ya kutosha,kimsingi ni kwamba atarudi uwanjani katikati ya Februari.Kuhusu mchezo wao dhidi ya JS Saoura amesema wanakwenda kucheza na timu kubwa na kwamba lengo lao la kwanza lilikuwa ni kuingia hatua ya makundi na baada ya hapo wanafikiria malengo makubwa zaidi.

My Neighbor, Charles | 이웃집 찰스 Ep170 / Mika, the smiling guy from Tanzania!

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 08.01.2019

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images