Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Tanesco Yapewa Siku Tatu Kuunganisha Umeme Wizara 10 zilizo katika Mji wa Serikali Jijini Dodoma


JAFO AWAPONGEZA KIBONDO KWA USIMAMIZI WA MIRADI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo amewapongeza Viongozi, watendaji, na wananchi wa wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo. Waziri Jafo amefurahishwa Sana na ujenzi wa vituo vya afya vya Kagezi Mabamba kwani ujenzi wake umekuwa mzuri Sana unaoendana na thamani ya fedha iliyo tolewa na serikali.

Katika ziara hiyo waziri Jafo alimpongeza Sana mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Eng. Nditiye kwani amekuwa akiwahangaikia Sana wananchi wake katika upatikanaji wa miradi hiyo ya maendeleo.

Aidha, Waziri Jafo alimalizia ziara yake kwa kukagua miradi ya barabara ya Kibondo mjini pamoja na kutembelea shule ya sekondari Malagarasi ambapo ukarabati na ujezi wa miundombinu umefanyika shuleni hapo kwa gharama ya shilingi milioni 400.

Waziri Jafo akikagua barabara za changarawe zilizojengwa na TARURA Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Malagarasi wakimskiliza Waziri Jafo(hayupo pichani) alipowatembelea shuleni hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(katikati) akisomewa taarifa wakati alipotembelea Kituo cha Afya Kibamba kilichopo Kibondo Mkoani Kigoma.

WADAU WA NYUKI WATAKIWA KUTUMIA MISTU ILIYOPO KUONGEZA UZALISHAJI WA ASALI NA MAZAO YAKE NCHINI

$
0
0
WADAU wa sekta ya ufugaji nyuki na uzalishaji wa asali na mazao yake wametakiwa kutumia uwepo wa utajiri wa mistu hapa nchini kuhakikisha wanazalisha asali kwa ubora na wingi kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi. 

Hatua hiyo itasaidia kuongeza nafasi za ajira kwa wananchi na kuingizia nchi fedha za kigeni zinazotokana na mauzo ya asali nje ya Nchi.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Profesa Adolf Mkenda wakati wa kufungua kongamano la siku mbili la wadau wa ufugaji nyuki na uzalishaji wa asali lililolenga uanzishaji wa viwanda vya kusindika na kuchakata asali na mazao yake. Alisema licha kuwa na mistu mikubwa hapa nchini bado uzalishaji wa asali uko chini ukilinganisha na baadhi ya Nchi ambazo zina mistu michache barani Afrika.

Profesa Mkenda alisema wakati umefika kwa wadau kuhakikisha wanakuja na mikakati itakayoongeza uzalishaji wa asali hapa nchini na kuwawezesha wakazi wa kando kando ya mistu nchini kunufaika na uwepo wake kwa kuongeza kipato chao kupitia ufugaji nyuki na uzalishaji asali. Alisema lengo ni kutaka asali iwe sawa na dhahabu nyingine inayoliingizia Taifa fedha za kigeni zinazotokana na mauzo nje ya nchi kwa kuwa soko la asali ya Tanzania ni kubwa ndani na nje ya bara la Afrika.

Aidha Katibu Mkuu huyo alisema ili kuhakikisha makazi ya nyuki hayaharibiwi Serikali kwa kushirikiana na wadau wa mistu wameanza kuedesha zoezi la kuwaondoa watu wote wanaondesha shughuli za kiuchumi katika maeneo ya mistu. Katika hatua nyingine Profesa Mkenda aliwaka wadau hao kuacha kulalamika kuwa uhaba wa asali unasababishwa na wanunuzi toka nje ya nchi wanaokwenda moja kwa moja kwa wafugaji wa nyuki na kununua bidhaa hizo kwa bei ya shilingi elfu 40,000/- kwa lita 20 wakati wao wananua kwa shilingi 120,000/- na kuwataka nao waende kwa wafugaji.
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa salamu za mkoa huo jana wakati wa kongamano la siku mbili linalojadili mikakati mbalimbali ya kuongeza uzalishaji wa asali na uanzishaji wa viwanda vya kuchakata na kusindika asali nchini. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasaili na Utalii Profesa Adolf Mkenda akifungua jana kongamano la siku mbili linalojadili mikakati mbalimbali ya kuongeza uzalishaji wa asali na uanzishaji wa viwanda vya kuchakata na kusindika asali nchini. 



Baadhi ya wadau wa ufugaji nyuki wakiwa katika kongamano la siku mbili linalojadili mikakati mbalimbali ya kuongeza uzalishaji wa asali na uanzishaji wa viwanda vya kuchakata na kusindika asali nchini. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasaili na Utalii Profesa Adolf  Mkenda(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa ufugaji nyuki jana mara baada ya kufungua kongamano la siku mbili linalojadili mikakati mbalimbali ya kuongeza uzalishaji wa asali na uanzishaji wa viwanda vya kuchakata na kusindika asali nchini. 

Wahitimu wa chuo cha NDF Waelezwa Fursa za Uwekezaji Zinazopatikana Rukwa

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amefafanua fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana katika Mkoa hasa sekta ya kilimo kwa wahitimu wa mafunzo kwa vitendo kutoka katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi waliotembelea mkoani hapa ili kujionea maendeleo ya mkoa.

Wahitimu hao kutoka katika nchi kadhaa barani Afrika wamelenga kutembelea katika viwanda vikubwa vinavypoaptikana katika mkoa, maeneo ya uwekezaji wa kilimo, kufika kwenye vivutio vya utalii, machimbo ya makaa ya mawe pamoja na hifadhi za misitu.

Mh.Wangabo alisema kuwa uwekezaji wa kwenye viwanda unahitajika kwasababu ya uwepo wa mazao ya kulisha viwanda hivyo ikiwemo viwanda vya kuchakata mahindi, maharage na mpunga na kuwaondoa shaka juu ya upatikanaji wa umeme kwani hadi kufikia mwaka 2020 vijiji vyote vya mkoa wa Rukwa vitakuwa na umeme.

“Maeneo mazuri ya uwekezaji upo kwenye viwanda hasa viwanda vya kuchakata mazao ndani ya mkoa wetu, pia mwaka huu tuna zao la alizeti kama zao la Kimkakati ambapo hadi sasa kuna tani za mbegu zaidi ya 11,000 ambazo zimeshanunuliwa na wakulima na kupandwa na hivyo tunategemea uzalishaji mkubwa wa alizeti kwa mwaka huu na hivyo tunawaalika wawekezaji kuweka viwanda vya uchakataji wa alizeti ikiwa ni zao la kimkakati kwenye mkoa wetu.” Alisema.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Benard Makali (kulia) akipokea moja ya zawadi alizopewa na Uongozi wa chuo cha Ulinzi nchini ikiwasilishwa na Kiongozi wa Msafara huo Commodore M. Mumanga
Picha ya apmoja kati ya Wahitimu wa Chuo cha Ulinzi nchini pamoja na Wataalamu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wakiongozwa na Mkuu wa mkoa Mh. Joachim Wangabo (wa tatu toka Kulia).
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia)akipokea moja ya zawadi alizopewa na uongozi wa chuo cha Ulinzi nchini kama shukrani ya kuwapokea vizuri katika Mkoa, zawadi iliyowasilishwa na Kiongozi wa Msafara huo Commodore M. Mumanga. 

KAMPUNI ZINAZOSAMBAZA NGUZO ZATAKIWA KULIPA USHURU KWA MUJIBU WA SHERIA-WAZIRI MKUU

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kampuni zote zinazosambaza nguzo za umeme zinatakiwa zilipe ushuru wa halmashauri wanakotoa nguzo hizo ambao ni asilimia tano ya gharama ya kila nguzo kama ilivyoelekezwa na Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Januari 7, 2019) baada ya kupata taarifa kuhusu kampuni ya New Forest ambayo inamkataba na TANESCO wa kusambaza nguzo za umeme, kwa muda mrefu kampuni hiyo imekuwa ikikaidi kulipa ushuru wa asilimia tano ya gharama ya kila nguzo. Ushuru huo umefikia sh. bilioni 2.9 hali iliyopelekea uongozi wa mkoa kuzuia nguzo hizo zisitoke.

Wiki iliyopita akiwa katika ziara ya mkoa Ruvuma, Waziri Mkuu alipokea malalamiko kuhusu mkoa wa Iringa kuzuia kusambazwa kwa nguzo za umeme ndipo alipoamua kuwaita Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi pamoja na wakuu wa wilaya, wakurugenzi pamoja na wenyeviti wa halmashauri wanaotoka katika wilaya zinazozalisha nguzo.

Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemevu, Jenista Mhagama, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Josephat Kandege, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya pamoja na maafisa wengine wa Serikali.

Amesema lengo la kikao hicho lilikuwa kupata ufafanuzuzi kuhusu malalamiko yaliyotolewa dhidi ya uongozi wa mkoa wa Iringa kuhusu kuzuia usafirishaji wa nguzo za umeme zinazotomika kwenye miradi ya Kusambaza Nishati ya Umeme Vijiji (REA).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza kikao alichokiitisha cha Mawaziri, Naibu Mawaziri na Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Nishati, Maliasili na Utalii, Fedha, Katiba na Sheria na Viwanda Biashara na Uwekezaji. Wengine walioshiriki katika kikao hicho ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, TANESCO, REA na TFC. Kikao hicho kilifanyika ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma, Januari 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Zao la Korosho lapata soko Nchini Algeria

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria, Mhe. Saad Belabed. Katika mazungumzo hayo Mhe. Balozi alieleza kuwa Algeria ipo tayari kununua korosho ya Tanzania. Dkt. Ndumbaro amesema mazungumzo hayo ni moja ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kuwakomboa kiuchumi Watanzania kwa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima nje ya nchi. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam. 
Mazungumzo yakiendelea.
Dkt. Damas Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Saad Belabed mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. 

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 07.01.2019

Biteko Awaeleza Watanzania Kuwa Serikali Ina Macho

$
0
0

Aeleza itafika kokote madini yanakochimbwa pasipo vibali halali

Na Nuru Mwasampeta

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amewaeleza watanzania wasiofuata Sheria katika utafutaji, uchimbaji na biashara ya madini nchini kuwa Serikali inaona na itafika popote madini yanapochibwa pasipo vibali halali vya kufanya shughuli hiyo.

Biteko ameyasema hayo mwishoni mwa wiki, Tarehe 5 mwezi Januari, 2019 alipofanya ziara ya kukagua eneo ambako shughuli za uchimbaji wa madini ya shaba ulifanywa pasipo kibali na kubaini viashiria vya uchimbaji katika hifadhi ya Wanyama pori ya Makao iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.

Akizungumzia lengo la ziara hiyo, Biteko alisema kumekuwa na viashiria vya kuwepo kwa watu wasiokuwa waaminifu na kujiingiza katika shughuli ya uchimbaji pasipokuwa na vibali jambo ambalo halikubaliki na halitavumilika. “Sisi madini yanatuuma, tukisikia kuna watu wanachimba tutafika mahali popote kujua madini hayo yanachimbwa na kupelekwa wapi” Biteko alikazia.

Aliendelea kwa kusema, huu mchezo ulifanyika sana na sasa nimekuja kuwaambia hautajirudia tena. Endapo mtu yeyote anataka kuchimba madini ya yoyote ikiwa ni pamoja na madini ya ujenzi kama vile mchanga wa kutengenezea barabara sharti afike katika ofisi zetu za madini aeleze nia na eneo analotakiwa kutengeneza barabara na wahusika watamuonesha eneo la kuchimba mchanga kwa utaratibu wa kisheria kwa matumizi hayo si kujiamlia tu. 
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wakwanza kulia) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila na wajumbe aliambatana nao wakiwa katika eneo linaloonesha dalili za uchimbaji wa madini katikati ya hifadhi ya wanyama ya Makao wilayani Meatu 
Pori kwa pori mbugani, Prof. Simon Msanjila akiongoza wajumbe walioambatana kujiridhisha, kukagua pamoja na kutoa kauli ya serikali kwa wafanya biashara wa madini wanaojihusisha na biashara hiyo kinyume na taratibu na sheria ya nchi, Nyuma yake mwenye suti ni Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani 
Wajumbe walioambatana na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Simon Msanjila, Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani katika hifadhi ya wanyama ya Makao wilayani Meatu mkoani Simiyu. 
Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani akiongea jambo mara baada ya kupokea ugeni kutoka Wizara ya Madini katika wilaya yake ya Meatu 
Afisa Madini wa Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Fredy Mahobe akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya ujumbe kutoka Wizara ya Madini, Mkuu wa Wilaya ya Meatu Joseph Eliaza Chilongani na kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Meatu. 


Kasulu Mmejipanga- Jafo Alonga

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ametoa la Moyoni kwa kuwaeleza Mkuu wa Wilaya ya Kasulu pamoja na viongozi wenzake kwamba wamejipanga vyema katika kuwatumikia wananchi wa Kasulu. 

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo ya kufurahishwa baada ya kutembelea miradi minne ya sekta ya afya pamoja na barabara wilayani humo na kuridhishwa Sana na usimamizi mzuri wa miradi Hiyo. Miradi aliyo ikagua ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Lami katika Halmashauri ya mji wa Kasulu, ukarabati wa Hospitali ya Mji Kasulu na Kituo cha Afya Kiganamo. 

Pia katika halmashauri ya wilaya Kasulu Waziri Jafo alifanikiwa kukagua kituo kimoja cha Afya cha Rusesa ambacho ni moja ya kituo cha afya kati ya vituo vya afya vitatu vilivyojengwa na Serikali katika halmashauri hiyo. 

Katika Zara hiyo waziri Jafo alimshukuru sana Mhe. Daniel Nsanzugwako Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini na Mhe. Vuma Mbunge wa Jimbo la Kasulu vijijini kwa kufikisha kilio cha wananchi wao serikalini hadi serikali imefanikisha kutekeleza miradi hiyo muhimu yenye maslahi mapana kwa wananchi. 

Wakati huo huo waziri Jafo amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuwezesha upatikanaji wa malighafi za ujenzi wa barabara ya Lami Kasulu Mjini kwani mkandarasi anayejenga barabara hiyo iliyo chini ya TARURA amekwama kupata malighafi za CRS ambayo inapatikana kwa eneo la wakandarasi wa Ki-China anayejenga barabara za TANROADS.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (katikati) akipata maelezo toka kwa Meneja wa TARURA Wilaya ya Kasulu kuhusu ujenzi wa barabara ya lamo ya katikati ya mji wa Kasulu
Barabara ya Kasulu inayojengwa kwa kiwango cha Lami
Kituo cha Afya Rusesa kinachoendelea kujengwa katika Wilaya ya Kasulu

HALMASHAURI YA BUKOBA, YAGAWA VITAMBULISHO KWA WAJASILIAMALI WADOGO.

$
0
0
Na Abdullatif Yunus - Bukoba.

Katika kutekeleza Agizo la Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Wamezindua zoezi tekeleza agizo la Mh. Rais Magufuli la kugawa Vitambulisho kwa wajasiliamali wadogo wadogo katika Halmasahauri yao, Zoezi ambalo limefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Bukoba (chemba) mnamo Januari 7, 2019. 

Akizungumza mara baada ya kugawa Vitambulisho hivyo Mh. Deogratius Muganyizi Kashasha (Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba) Amewataka wajasiliamali hao kuwa mabalozi wa wengine ambao hawajapata Vitambulisho hivyo ili wafanye Hima kujipatia Vitambulisho, sambamba na kuwakumbukusha jukumu la kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg, Solomon Kimilike Amenukuliwa akisema kuwa Zoezi hilo la Ugawaji wa Vitambulisho linaendelea kwa wajasiliamali wengine ambao wameshindwa kufika katika Uzinduzi, kutokana na sababu mbalimbali na kuongeza kuwa Kuanzia Januari 09, 2019 Watakuwa na ziara ya kuzungukia Vijiji na Kata ndani ya Halmashauri ili kugawa Vitambulisho hivyo kwa Wajasiliamali wenye sifa na vigezo.

Aidha kwa upande mwingine Mkurugenzi huyo amewataka wananchi hasa wafanyabiashara wakubwa kutofanya Udanganyifu kwa kuwatumia wajasiliamali wadogo kujipatia vitambulisho, na kuwa kwa yeyote atakayebainika kufanya hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Tayari Vitambulisho 37 kati ya 1,317 vimegawiwa kwa Wajasiliamali baadhi ambao wamejitokeza kuchukua Vitambulisho hivyo huku wakionekana kuwa na Imani na Serikali ya awamu ya Tano, chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kuwasaidia watanzania wenye hali ya chini.

Pichani ni Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Mh. Kashasha akimkabidhi Kitambulisho chake Mjasiliamali Kutoka Kata ya Rubale Bwn.Edisoni Nicholaus, Katikati ni Mkurugenzi Ndg. Solomon.


Pichani: Wanaonekana wajasiliamali Bi. Praxeda Rauliani, Bi. Liliani Richard na Bi Alistidia Petro wakiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa Vitambulisho vyao katika ukumbi wa Halmashauri ya Bukoba.
Makamu Mwenyekiti Mh. Kashasha akisitiza jambo mara Baada ya Kukabidhi Vitambulisho 37 kwa wajasiliamali wadogo kati ya Vitambulisho 1,317, pembeni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bukoba Ndg. Solomon Kilimike.
Bwn Edisoni Nicholausi mkazi wa Rubale, akiwa ameshikilia Kitambulisho cha ke mara baada ya kukabidhiwa

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 8,2019

OFISI YA WAZIRI MKUU YATOA MAFUNZO KWA MAMA WADOGO MKOANI TABORA

$
0
0
Na OWM (KVAU) – Tabora

Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu inaratibu mafunzo maalum kwa mama wadogo yanayolenga kuwawezesha kujitambua na kujithamini.

Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Uyui iliyopo Mkoani Tabora ambapo mama wadogo takribani 45 wamefundishwa mada mbalimbali ikiwemo Ujasiriamali, kilimo biashara, taratibu za kuunda vikundi vya uzalishaji mali, fursa za uwezeshaji wa vijana kiuchumi, malezi bora na familia, afya na lishe.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift Msuya amesema kuwa Serikali inatambua tatizo la mimba za utotoni na imeonesha dhairi ufuatiliaji wa suala hilo kwa kuwachukulia hatua za kisheria wanaohusika na vitendo hivyo.

“Takribani asilimia 45 ya mabinti wanaoandikishwa kujiunga na kidato cha kwanza wanashindwa kumaliza kidato cha nne kutokana na changamoto za mimba za utotoni, ndoa za utotoni na umbali wa kupata huduma ya elimu.” alisema Msuya .Aidha, Msuya alieleza kuwa Halmashauri yake imeanzisha kampeni ya “Nishike Mkono, Boresha Elimu Uyui” inayolenga kuwainua watoto wa kike kwa kuwaboreshea mazingira ya elimu yatakayo wawezesha kupata elimu bora.


Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift Msuya akizungumza na Mama Wadogo (Young Mothers) wakati wa ufunguzi wa mafunzo yaliyofanyika Wilaya ya Uyui, Mkoa wa Tabora. 
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. Julius Tweneshe akifafanua jambo kwa Mama wadogo walioshiriki mafunzo hayo kuhusu malengo ya mafunzo hayo yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). 
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Atupokile Mhalila akitoa mada kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa Mama wadogo walioshiriki kwenye maunzo hayo yalifanyika Wilaya ya Uyui. 


Baadhi ya Mama wadogo wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift Msuya (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Uyui. 

IFAHAMU TAASISI YA WAJIBU NA NAMNA INAVYOHAMASISHA UWAJIBIKAJI NA UTAWALA BORA

$
0
0

 Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii.

KATIKA kujenga taifa lenye mlengo wa uwajibikaji pamoja na usimamizi mzuri wa rasilimali za umma kwa manufaa kwa wote taasisi ya WAJIBU imekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu pamoja na kukuza uwajibikaji na utawala bora nchini.

Mtazamo na dhima ya taasisi ya WAJIBU vinaenda sambamba na na kasi na mlengo wa serikali wa awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli ambaye amekuwa akisisitiza kuhusu uwajibikaji na utawala bora pamoja na kupiga vita masuala ya rushwa na ufisadi.

WAJIBU ni taasisi ya ya fikra ya uwajibikaji wa umma iliyoanzishwa mwaka 2015 ikiwa na malengo mbalimbali hasa kukuza uwajibikaji na utawala bora hapa nchini na kushikilia dira ya usimamizi faafu na bora zaidi wa rasilimali za umma kwa manufaa ya wote.
Taasisi ya WAJIBU imebeba dhima ya kuendelea kukua kama taasisi ya fikra ya uwajibikaji ambayo inaongeza thamani katika huduma inazotoa ili kuweza kufanikisha ustawi wa uwajibikaji na utawala bora nchini katika sekta mbalimbali za umma.

Katika kutekeleza majukumu yao taasisi ya WAJIBU inasimamia misingi ya kiutendaji na hiyo ikiwa ni pamoja na kujali watu na kuwahudumia watanzania ambao ndio walengwa wa mambo yote yanayohusu uwajibikaji na utawala bora nchini na wanaamini haki katika kuwahudumia wananchi ni moja ya msingi katika kutekeleza uwajibikaji na utawala bora.

Aidha WAJIBU ni taasisi ambayo haifungamani na upande wowote kisiasa, kijamii na kidini bali wao hutekeleza yale yanayohusu uwajibikaji pamoja na kuangalia masuala ya usawa, uvumilivu na uwazi sambamba na kuwajibika.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

World Bank Group President Kim to Step Down February 1

$
0
0
World Bank Group President Jim Yong Kim today announced that he will be stepping down from his position after more than six years in which the institution’s shareholders provided strong support to multiple initiatives to ensure that the Bank Group retains strong leadership in the world of global development.

“It has been a great honor to serve as President of this remarkable institution, full of passionate individuals dedicated to the mission of ending extreme poverty in our lifetime,” said Kim. “The work of the World Bank Group is more important now than ever as the aspirations of the poor rise all over the world, and problems like climate change, pandemics, famine and refugees continue to grow in both their scale and complexity. Serving as President and helping position the institution squarely in the middle of all these challenges has been a great privilege.”

Under Kim’s leadership, and with the backing of the Bank Group’s 189 member countries, the institution in 2012 established two goals: to end extreme poverty by 2030; and to boost shared prosperity, focusing on the bottom 40 percent of the population in developing countries. These goals now guide and inform the institution in its daily work around the globe.

In addition, shareholders strongly supported measures to ensure that the Bank Group be even better positioned to respond to the development needs of clients: 

· The Bank Group’s Fund for the Poorest, IDA, achieved two successive, record replenishments, which enabled the institution to increase its work in areas suffering from fragility, conflict, and violence.

· In April 2018, the Bank Group’s Governors overwhelmingly approved a historic USD$13 billion capital increase for IBRD and IFC that will allow the Bank Group to support countries in reaching their development goals while responding to crises such as climate change, pandemics, fragility, and underinvestment in human capital around the world.

FOR MORE NEWS CLICK HERE

Balozi Seif azindua Mradi wa huduma za Umeme kisiwa cha Uvinje Mkoa wa Kaskazini Pemba

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati Serikali Kuu ikijitahidi kuondoa tofauti ya Kimaendeleo baina ya Visiwa Vikubwa na Vidogo Wananchi wanapaswa kukataa ushawishi unaofanywa na baadhi ya Watu wa kuwataka waache kutumia huduma za maendeleo zinazoimarishwa na Serikali kila kukicha.

Alisema upuuzi wa Watu hao kamwe hautaleta maana yoyote kwa vile Ilani ya Chama cha Mapinduzi inayosimamiwa na Serikali zote mbili Nchini Tanzania imeahidi kuleta mabadiliko  makubwa ya Maisha kwa kila Mwananchi bila ya kujadi utofauti wao wa Majimbo, Dini na hata itikadi za Kisiasa.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kuzindua Mradi wa huduma za Umeme katika  Historia ya Kisiwa kidogo cha Uvinje kilioko Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya kusherehekea kutimia Miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964.

Alisema kila Mwananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba  ana haki ya kupatiwa huduma muhimu za Kijamii, bila ya kujali anakotoka hata kama ataamua kuishi kwenye Visiwa vidogo vidogo atakuwa na haki ya kupata huduma hizo kwa faid ya ustawi wake na familia yake.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wananchi wa Kisiwa cha Uvinje wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Umeme Kisiwani humo. Picha na –OMPR – ZNZ.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi huduma za Umeme katika Kisiwa cha Uvinje baada ya kukamilika kwa mradi huo muhimu katika Historia ya Kisiwa hicho. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Nd. Hassan Ali Mbarouk, Kulia ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati Mh. Juma Makungu na Mkuu wa Wilaya ya Wete Nd. Abeid Ali Juma.
 Balozi Seif akibonyeza kitufe kuashirika kuwaka wa Umeme katika eneo la Skuli ya Uvinje iliyomo ndani ya Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU WAZIRI MABULA AWAONYA WATENDAJI WA SEKTA YA ARDHI BIHARAMULO

$
0
0
Na Munir Shemweta, Biharamulo 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amewataka watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera kujipanga na kufanya kazi kwa bidii ili kupunguza migogoro ya ardhi na wasipotekeleza majukumu yao vizuri atawawajibisha. 

Akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Biharamulo katika ofisi za halmashauri hiyo mkoani Kagera,  Dk. Mabula alisema pamoja na changamoto zinazoikabili sekta ya ardhi katika halmashauri hiyo lakini watumishi wa sekta hiyo wanapaswa kujipanga na kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kupunguza migogoro ya ardhi na wakati huo kuwawezesha serikali kukusanya mapato kupitia sekta ya ardhi. 

"Kama kazi haziendi migogoro ya ardhi haiwezi kuisha na ninyi hapa mna viwanja vichache lakini mmeshindwa kuviingiza katika mfumo hivyo mkimaliza kuviingiza viwanja hivyo hapo mnaweza kurekebisha takwimu" alisema Dk Mabula. 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewataka wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanaziangalia idara za ardhi katika halmashauri zao kwa kuwa hakuna miradi inayokamilika bila kuhusisha ardhi hivyo sekta hiyo ni muhimu na inapaswa kuangaliwa kwa umakini mkubwa.
 Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akikagua jalada la ardhi katika ofisi ya masijala ya ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera alipofanya ziara ya kushtukiza katika halmashauri hiyo kufuatilia maelekezo aliyoyatoa kwenye halmashauri hizo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri Sospiter Mwishamba na kushoto ni Mpimaji Ardhi Vedastus Masige
 Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera Novatus Babu alipofanya ziara ya kushtukiza katika halmashauri hiyo kufuatilia maelekezo aliyoyatoa kwenye halmashauri hizo.
Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akiwasili Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera alipofanya ziara ya kushtukiza katika halamashauri hiyo kufuatilia maelekezo aliyoyatoa kwenye halmashauri hizo.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AANZA ZIARA YA KIKAZI ZANZIBAR

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” Silima Haji Haji, wakati akiwasili Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya siku moja Januari 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI LUGOLA AMPA SIKU 30 MKUU WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KUFANYA UKAGUZI TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI NCHINI KAMA ZINA VIFAA VYA ZIMAMOTO

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA-Biharamulo.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amempa siku 30 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kufanya ukaguzi taasisi mbalimbali za umma na binafsi nchini kuwa na vifaa vya zimamoto.
Lugola alisema ukaguzi huo pia ulenge zaidi katika shule za msingi, sekondari na vyuo, vituo vya kutolea huduma za afya ili kuepukana na ajali zitokanavyo na vyanzo vya moto.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi, ambao ulifanyika katika uwanja wa mpira Mjini Biharamulo, Mkoani Kagera, leo, Lugola alisema atafuatilia utekelezaji wa agizo lake kama litakua limefanyiwa kazi jinsi anavyotaka yeye. Pia Waziri Lugola amewaomba Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatenga fedha za mapato ya ndani kununua vifaa za zimamoto katika taasisi za Serikali wanazoziongoza.
“Haiwezekani wanafunzi, wagonjwa katika zahanati mbalimbali au vituo vya afya wapate tatizo la ajali la moto halafu wakurugenzi na mameneja au wakuu wa taasisi hizo wakishindwa kuweka vifaa vya zimamoto licha ya kupokea fedha za kutolea huduma,” alisema Lugola. Aidha, Waziri Lugola amezitaka taasisi za dini kuendesha ibada kwa kuhakikisha majengo yanasajiliwa na pia Miiskiti na Makanisa yasitumike kuhifadhi wahalifu wanaotumia migongo ya kuwa wachungaji na mashekhe kama mwavuli wa maadili mema bila uzalendo.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Biharamulo, Mkoani Kagera, leo. Lugola amempa siku 30 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kufanya ukaguzi taasisi mbalimbali za umma na binafsi nchini kuwa na vifaa vya zimamoto.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Kagera, Raymond Mwampashe, lipokua anamfafanulia jambo wakati Waziri huyo alipofika katika Gereza la Biharamulo mkoani humo kujua utendaji wa kazi wa Gereza hilo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Saada Malunde.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akitaka ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, (RPC) Revocatus Malimi (kushoto), wakati Waziri huyo alipopata malalamiko kuhusu ng’ombe za Mkazi wa Mji wa Biharamulo (kulia) kukamatwa na Polisi Wilayani Biharamulo. Hata hivyo, RPC alimfafanulia Waziri huyo kuhusiana na malalamiko hayo dhidi ya mifugo iliyokamatwa na Polisi na kuhifadhiliwa katika Gereza la Biharamulo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BENKI YA MAENDELEO (TIB) YATEULIWA KUWA MWENYEKITI KAMATI NDOGO YA TAASISI ZA FEDHA SADC, YAORODHESHWA KAMA TAASISI BORA ZA MAENDELEO BARANI AFRIKA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
BENKI ya maendeleo ya TIB imechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ndogo ya taasisi za fedha za maendeleo ya jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa muda wa miaka miwili na kuhaidi ushirikiano pia amewataka watanzania kutumia fursa hiyo katika biashara na ushirikiano.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya taasisi ya fedha za maendeleo za ukanda wa SADC Charles Singili amesema kuwa aliteuliwa nafasi hiyo mwezi Disemba mwaka jana na atahudumu nafasi hiyo kwa miaka miwili, kuanzia Disemba 2018 hadi Disemba 2020.

Singili amesema kuwa uteuzi huo ni muhimu kwa taifa na kwa benki ya maendeleo TIB pamoja na Serikali kwa ujumla na amewahimiza  wananchi kutumia fursa hiyo kwa kuwa kuna viongozi wanaoshikilia nafasi muhimu katika jumuiya ya SADC akiwemo Rais Dkt.John Magufuli ambaye ni Makamu Mwenyekiti  wa marais wa jumuiya hiyo na Agosti 2019 Rais Magufuli atashika usukani kama Mwenyekiti wa SADC pia Katibu mkuu wa sasa wa jumuiya hiyo Dkt. Stergomena Tax ambaye  ni mtanzania pia.

Aidha Singili amesema kuwa hiyo ni nafasi pekee kwa Tanzania hivyo lazima majukumu yapokelewe na kuchapa kazi ili kuwa chachu ya maendeleo katika ukanda wa maendeleo kusini mwa Afrika. Aidha amesema kuwa Benki ya maendeleo TIB itatumia fursa hiyo kuhamasisha taasisi za fedha nchini na zile za nchi wanachama wa SADC katika kuhakikisha miradi ya maendeleo yenye maslahi ya kikanda inatekelezwa na hiyo ni pamoja na usafiri, nishati, maji na kuhakikisha fedha za kutosha zinapatikana.

Kuhusiana  fursa watakazozipa kipaumbele  Singili amesema kuwa watashirikiana na taasisi nyingine kwenye mtandao ili kuwezesha maandalizi ya miradi inayokopesheka kwa kutumia mfuko wa SADC wa kuandaa miradi mbalimbali.
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Fedha za maendeleo za ukanda wa SADC Charles Singili akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uteuzi wa benki hiyo uliofanya Disemba mwaka jana pamoja na heshima iliyopata Benki hiyo kwa kuwekwa kwenye jedwali la heshima baada ya kupata daraja A katika masuala ya utawala bora na makundi ya uendeshaji tuzo iliyotolewa na taasisi ha AADFI, leo jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WASHINDI WATANO WAPATIKANA KWENYE DROO YA MWISHO YA JIDABO NA I&M BENKI.

$
0
0
Na Khadija Seif,Globu ya jamii
BENKI ya I&M  imetangaza washindi watano droo ya tatu na ya mwisho  promosheni ya JIDABO

Meneja Masoko na Mawasiliano Emmanuel Kiondo amesema Kampeni ya "JIDABO na I&M Benki ilizinduliwa mwanzoni mwa mwezi Oktoba na imedumu kwa miezi mitatu ambapo kila mwezi washindi watano wamekua wakipatikana na kutangazwa.

 Washindi watano waliopatikana leo wanafanya jumla ya idadi ya washindi wote waliopatikana katika kipindi cha miezi mitatu ya promosheni ya "JIDABO na I&M Benki" kufikia 15 ambapo kila mshindi hupata mara mbili ya akiba iliyopo kwenye akaunti yake hadi kufikia kiasi cha juu cha sh.milioni tano za " amesema Kiondo.

Hata hivyo Kiondo amefafanua jinsi vigezo vilivyopaswa mshiriki azingatie ikiwemo kufungua Akaunti ya Akiba,Akaunti ya Biashara ,Akaunti ya Mshahara,Akaunti ya mtoto katika tawi lolote la benki ya I&M katika kipindi cha promosheni.

Kwa upande wa muwakilishi kutoka  Bodi ya Taifa ya Michezo ya kubahatisha Humud Abdul Hussein amesema ni muamko mkubwa kuona watanzania wengi wameshabadilisha maisha ya kupitia Michezo ya kubahatisha kama ya JIDABO na I &M Benki ambapo washindi wengi wameweza kusomesha watoto,kuendesha familia zao pamoja na biashara.

Hata hivyo ametoa pongezi kwa benki hiyo kwa kufanya promosheni hiyo na leo kufika tamati na kutangaza washindi watano waliopatikana katika droo hiyo ya mwisho wakiwemo Poulomi Joshi ,Jenipher Fredrick ,Thomas Obadia Malisa,Kefren Charles Buhongo  pamoja na Kampuni ya Unisoft Technologies.

 Aidha  mshindi wa droo ya promosheni hiyo iliyopita ya mwezi Novemba  Kennedy George amesema pesa alizoshinda ataweza kufanyia biashara zake pamoja na kumalizia ujenzi wa nyumba yake.Pia ametoa rai kwa watanzania kuwa Michezo ya kubahatisha ni michezo ambayo hakuna mtu ambae anapangwa na hakuna njia ya panya yoyote inayotumika katika kutafuta mshindi.
 Meneja Masoko na Mawasiliano Emmanuel Kiondo, Benki ya I & M akiwa na muwakilishi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha Humudi Abdul pamoja na mshindi wa droo ya mwezi novemba Kennedy George wakichezesha droo ya pili iliyofanyika leo na kuwatangaza washindi  watano wa Promoshei ya JIDABO na I & M Bank chini ya usimamizi kutoka bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha.
 Muwakilishi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha Humudi Abdul akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati wa kutangaza washindi watano walioshinda kwenye promosheni ya JIDABO na I&M benki jijini Dar es salaam
 Meneja Masoko na Mawasiliano Emmanuel Kiondo  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati wa kutangaza washindi wa  droo ya mwisho ya promosheni ya JIDABO na I&M benki
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images