Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

MGALU NA VULLU WAUNGA MKONO KAMPENI YA TOKOMEZA ZERO KISARAWE

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE

WABUNGE wa viti maalum mkoani Pwani ,Subira Mgalu na Zainab Vullu wamechangia magodoro 20 ili kupunguza changamoto ya upungufu wa magodoro uliopo shule ya sekondari Maneromango. 

Aidha Subira ametoa tanki la maji la lita 2,000 litakalosaidia kuhifadhi maji katika shule hiyo na tanki jingine shule ya sekondari Kolesa iliyopo kata ya Vikumburu.

Wakikabidhi msaada wa magodoro na matanki hayo ya kuhifadhi maji, walisema, msaada huo ni sehemu ya kuunga mkono kampeni ya Tokomeza Zero iliyoanzishwa hivi karibuni na mkuu wa wilaya Kisarawe Jokate Mwegelo.
“Tumejichanga kila mmoja magodoro kumi, kumi na kwa upande wa maji,mimi nipo karibu na shule ya Maneromango hivyo nimewataka wachote maji kwangu buree “alisema Zainab. 

Alieleza, wanafunzi wa kike wanahitaji zaidi maji hivyo kwa hakika kwa misaada hiyo itawasaidia kwa kiasi kikubwa. Zainab ,aliwaomba wadau wengine wajitokeze kuchangia katika tokomeza zero, ili kufikia malengo ya kiwilaya kuinua taaluma. Nae Subira alisema ,wazazi na walezi waelekeze nguvu zao kushirikiana na viongozi na serikali kusimamia watoto kuongeza ufaulu. 




“Fuatilieni watoto, kufuatilia maendeleo ya kimasomo kwa wanafunzi wetu, tusiachie walimu, tusijisahu wajibu wetu,”:Mkoa na wilaya imejikita kuinua sekta ya viwanda ,kama hatutoelimisha watoto jitihada hizo zitakuwa kazi bure “alifafanua Subira.

Subira alimpongeza Jokate kwa kufanya vizuri kwa kampeni hiyo kubwa.
Awali Jokate alibainisha, tangu kuanza kwa kampeni ya Tokomeza Zero, tayari wamejenga madarasa kumi na bweni moja kata ya Kurui kwa zaidi ya sh. mil. 100.


Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Pwani Mh. Zainab Vulu na Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgagalu wakimkabidhi vifaa mbalimbali mkuu wa wilaya ya Kisarawe ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya “Tokomeza Zero” wilayani humo.

Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Pwani Mh. Zainab Vulu na Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgagalu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbaoimbali baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali mkuu wa wilaya ya Kisarawe ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya “Tokomeza Zero” wilayani humo.
Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Pwani Mh. Zainab Vulu na Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgagalu wakimkabidhi vifaa mbalimbali mkuu wa wilaya ya Kisarawe ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya “Tokomeza Zero” wilayani humo. 


Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Pwani Mh. Zainab Vulu akizungumza katika kikao cha RCC kinachoendelea wilayani Kiswarawe wakati akitangaza utekelezaji wa msaada ambao wabunge hao waliuahidi katika ziara ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakati alipofanya ziara yake kulia ni Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgagalu na wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo katikati ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Kisarawe Musa Gama. 

AGIZO LATOLEWA KWA WANAOJENGA JENGO LA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KUENDELEA KULIPWA KWA WAKATI

$
0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, amemtaka mkandarasi SUMA JKT anayejenga jengo la wizara hiyo katika Mji wa Serikali Jijini Dodoma, kuhakikisha anaendelea kuwalipa wafanyakazi wanaojenga jengo hilo kwa wakati pamoja na kuhakikisha ubora wa jengo hilo unaendana na thamani hali pesa.

Mhe. Ulega amesema hayo leo (04.01.2019) mara baada ya kufika katika mji huo uliopo Kata ya Mtumba, kwa ajili ya kufanya tathmini ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la awali la Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kuonesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi inavyoendelea na kumtaka mkandarasi kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.

“Unamlipa mtu kabla jasho lake halijakauka palepale unakuwa tayari umeshampa ndiyo dini inavyosema, ni jambo jema sana maana hawa mafundi wanasema wanalipwa kwa wakati, sisi muda wowote tutakuwa tunakuja hapa tunataka hii kazi imalizike kwa wakati na kwa viwango” Amesema Mhe. Ulega.

Mhe. Ulega amefafanua kuwa siyo jambo jema endapo kutatokea taarifa mara baada ya kumalizika kwa mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kuwa wafanyakazi waliokuwa wakijenga jengo hilo wanamdai mkandarasi ilhali wizara imemlipa pesa zote mkandarasi huyo SUMA JKT ili aweze kufanya kazi kwa wakati.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akipewa maelezo ya ujenzi wa jengo la wizara na Mkandarasi Msimamizi wa SUMA JKT Injinia David Pallangyo, katika Mji wa Serikali Jijini Dodoma
Baadhi ya wafanyakazi wanaojenga jengo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Mji wa Serikali Jijini Dodoma wakiendelea na hatua mbalimbali za ujenzi wa jengo hilo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BEI ZA MATUNDA MBAGALA KWA SIKU YA LEO

$
0
0
Na Emmanuel Massaka, MMG  
WAFANYABIASHARA wa matunda katika kituo cha mabasi Mbagala Rangi jijini Dar es Salaam wameeleza kuwa kwa sasa matunda yameongezeka, huku wakibainisha wazi bei ambazo wanauza kwa wateja wao. 

Wakizungumza leo na Michuzi Blog jijini Dar es Salaam wafanyabiashara  hao kuhusu bei ya  hapo katika kituo cha mabasi Mbagala Rangi.
 Bei hizo ni kama ilivyo hapo chini 
Picha zote na Emmanuel Massaka, MMG.

KATIBU MKUU WIZARA YA KATIBA NA SHERIA PROF. SIFUNI ATEMBELEWA NA BALOZI MELLO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Balozi wa Tanzania wa kudumu wa Umoja wa Mataifa Balozi Modest Mello (wa tatu kulia) baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Katibu Mkuu. Wengine pichani ni Maafisa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushierikiano wa Afrika Mashariki.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akiagana na mgeni wake Balozi wa Tanzania wa kudumu wa Umoja wa Mataifa Balozi Modest Mello baada ya mazungumzo ofisini kwa Katibu Mkuu.

ULEGA AFUNGA MWAKA KWA KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA YA AFYA BARABARA

$
0
0
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa jimbo la mkuranga Abdalah Hamis Ulega ametoa mafuta ya diesel Lita 1000 kwa ajili ya greda ambalo husaidia kutatua changamoto za barabara jimboni humo pamoja na shuka 100 kwa kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga.

Akizungumza katika mkutano wa kufunga mwaka wa kutathimini  changamoto na maendeleo uliofanyika wilayani humo, Ulega amesema kuwa ameamua kutoa mafuta  changamoto iliyotokana na  Halmashauri kununua greda muda mrefu lakini limekaa bila kufanya kazi.

"Nilitoa msukumo kwa kukaa pamoja na madiwani na kushauriana kwa pamoja tuwe na greda letu wenyewe    ili itusaidie kutatua changamoto za barabara hasa za vijijini ambako barabara nyingi hazipitiki na tumenunua greda hilo kwa zaidi ya milioni 700 ikiwa ni fedha zetu wenyewe na likachonge barabara zetu." Amesema Ulega.

Ulega amesema kuwa greda hilo alikodishwi kwa wananchi ila kinachotakiwa vijiji vijichangishe wanunue mafuta kwa shughuli za kutatua kero za barabara. "Sio kwamba   nimeshindwa kutoa hela Mkurugenzi hela  nakukabidhi mapipa haya matano ya mafuta kila moja lina Lita 200 yakatumike ipasavyo."Amesema Ulega.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akikabidhi shuka 100 Mkurungenzi wa Halmashauri Mkuranga, Mhandisi Mshamu Munde zenye thamani zaidi ya milioni moja.kushoto ni Mganga Mkuu wa wa wilaya ya
Mkuranga, Dkt.Stephen Mwandembo
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akimsikiliza Mzee Athuman Mtalu katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mkuranga mko wa Pwani.

 Mkurugenzi wa Halmashauri Mkuranga, Mshamu Munde akizungumza na   wananchi  katika mkutano wa kufunga mwaka wa kutathimini  changamoto na maendeleo uliofanyikawa wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
 Baadhi ya wananchi wakimsiki Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Mh.Abdallah Ulega

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UYUI KUJENGA DAHARIA(HOSTEL) 15 ZENYE THAMANI YA BILIONI 1.5 KUWALINDA WANAFUNZI WA KIKE

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT, TABORA
SERIKALI Wilayani Uyui imesema inakusudia kuendesha Kampeni maalumu ya Nishike Mkono Mwezi Machi mwaka huu kwa lengo la kukusanya shilingi bilioni 1.5 (1,500,000,000/-) ambazo zitasaidia ujenzi wa dahari(hosteli) 15 kwenye Sekondari 15 za Kata ili kuwalinda watoto wa kike na mimba na ndoa za utotoni.

Kauli hiyo imetolewana Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa mama wadogo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tabora-Uyui yaliandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuwajengea uwezo watoto wa kike ambao walikubwa na tatizo la mimba za utotoni.

Alisema lengo la kujenga daharia hizo ni kuwaepusha wanafunzi wa kike wa shule za Sekondari na mimba, vishawishi vinavyowafanya washindwe kuendelea na shule na kuozeshwa na wazazi wao , kuwapa utulivu wa kujisomea kwa kuwa karibu na mazingira ya shule na kuwaepusha kuacha shule kwa sababu ya kutembea umbali mrefu wa kwenda shule ambapo wakati mwingine wanakutana na matatizo ya kutaka kubakwa.

Mkuu huyo wa Wilaya hiyo alisema kuwa kukamilika kwa Daharia hizo sio tu kutasaidia watoto wa Kata husika bali wale wanaotoka Kata jirani ambazo hazina Sekondari ambapo wanafunzi wao wanatembelea umbali mrefu kwenda jirani.
  Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Tabora Baraka Makona akitoa maelezo mafupi mafunzo mafupi kwa mama wadogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora yaliyojenga kuwajengea uwezo wa kujitambua na kufanya maamuzi sahihi ya kujiwekea 
malengo katika maisha yao.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Julius Toneshi akitoa maelezo mafupi mafunzo mafupi  kwa mama wadogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora yaliyojenga kuwajengea uwezo wa kujitambua na kufanya maamuzi sahihi ya kujiwekea malengo katika maisha yao.
 Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akifungua  mafunzo mafupi  kwa mama wadogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora yaliyolenga kuwajengea uwezo wa kujitambua na kufanya maamuzi sahihi ya kujiwekea malengo katika maisha yao.
 Baadhi ya mama wadogo wakiwa katika mafunzo ya siku mbili mafunzo yalilenga kuwajenga kuwajengea uwezo wa kujitambua na kufanya maamuzi sahihi ya kujiwekea malengo katika maisha yao.
 Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na mama wadogo  mara baada kufungua  mafunzo mafupi  kwa mama wadogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora yaliyolenga kuwajengea uwezo wa kujitambua na kufanya maamuzi sahihi ya kujiwekea malengo katika maisha yao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

ZFA YATANGAZA MAPUMZIKO YA LIGI KWA MWEZI MZIMA

$
0
0
Na Ripota Wetu, Zanzibar

Chama cha mpira wa miguu Zanzibar (ZFA) kimetangaza mapumziko ya ligi kupisha mashindano ya Mapinduzi Cup ili yachezwe kwa ufanisi zaidi. 

Mapumziko hayo ni ya mwezi mzima kuazia 01/01/2019 hadi 05/02/2019 wakati huo wa mapumziko pia ZFA utautumia muda huo kwa mujibu wa kalenda kufanya uhamisho na usajili wa dirisha dogo kuazia 01/01/2019 hadi 25/01/2019 baada ya hapo zfa itaendelea na utaratibu wa kuhakiki na kupitisha uhamisho, usajili na kutoa block ya usajili wa dirisha dogo. 

Ligi Kuu Zanzibar inakwenda mapumziko huku timu zote zikiwa zimecheza nusu ya mechi zao yaani kila timu imecheza mechi kumi na nane (18) ligi hiyo inaongwa na KVZ kwa kujikusanyia point arubaini na tatu (43) .

Ligi daraja la kwanza Kanda inakwenda mapumziko huku timu zote zikiwa zimecheza mechi kumi na tatu (13) na kwa upande wa ligi ya daraja la pili Taifa ambayo inachezwa kwa mfumo wa makundi makundi yote matatu timu zote zimecheza nusu ya michezo yao na baada ya kumaliza mapumziko watarudi viwanjani kwa michezo ya marudiano 

Mapumziko hayo ni yale ambayo yameandikwa kwenye kalenda ya ZFA ya 2018/2019 haijabadilishwa na ZFA haina mpango wa kupunguza wala kuongeza siku katika usajili huo wa dirisha dogo kila timu inatakiwa kufuata kalenda ili kuondoa usumbufu. 

Mapumziko hayo ya ligi yataishia 05/02/2019 kutoka hapo timu zitarudi viwanjani kwa kuaza rasmi na michezo ya FA CUP ambayo itachezwa kwa kushirikisha timu zote za daraja la pili taifa na timu ishirini na nne (24) za daraja la kwanza kanda ya Pemba na Unguja.

Timu kumi na tisa (19) za ligi kuu na timu nane (8) daraja la kwanza Kanda zitabaki kusubiri hatua ya pili ya mashindano hayo ya FA CUP .Ikumbukwe kwa mujibu wa kanuni bingwa wa Mashindano ya FA CUP atakuwa muakilishi wa nchi kwa mashindano ya kombe la shirikisho barani Africa Mashindano hayo ya FA CUP yatachezwa kwa mfumo wa mtoano na yataaza kwa timu za Pemba kucheza kwao na timu za Unguja kucheza kwao timu zitaungana hatua ya robo fainal Pemba timu nne (4) na timu Unguja nne (4) 

ZFA inawatakia mapumziko mema ya dirisha dogo familia yote ya mpira wa miguu huku ikiwasisitiza viongozi wa vilabu kufanya uhamisho usajili kwa wakati na mambo yote yanayo husu fedha iwe kununuwa fomu za usajili uhamisho au kulipia wachezaji malipo yafanywe kwa njia ya bank kupitia account ya ZFA TAIFA PBZ 0406097000 vifaa vyote vinavyo hitajika kwa ajili ya usajili uhamisho wa dirisha dogo vipo ofisini vya kutosha. 

Bosi Lake FM aibuka na kipindi cha televisheni cha Tena na Tena

$
0
0
Mbunifu wa mavazi vyota nchini, Doreen Peter Noni anayetamba na lebo ya Eskado Bird ameibuka na kipindi maalum cha televisheni kijulikanyo kwa jina la ‘Tena Na Tena’ ambacho kinazungumzia shughuli mbalimbali za kutafuta riziki katika maisha mpaka kufanikiwa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Doreen ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi na mmiliki wa kituo cha redio, Lake FM cha Mwanza alisema kuwa, sababu kubwa ya kuanzisha kipindi hicho ambacho kitarushwa katika moja ya vituo vya televisheni hapa nchini mwakani, ni kutoa hamasa kwa vijana kuendelea ‘kupambana’ katika kutafuta riziki bila kukata tamaa.

Doreen alisema kuwa kipindi cha Tena na Tena ambacho pia kitaonyeshwa ‘Online’, kimerekodiwa kwenye gari inayotembea ambapo muhusika atatoa ushuhuda wake wa maisha katika mfumo wa majadiliano. Alisema kuwa mbali ya kuburudisha, lengo lingine la kipindi cha Tena na Tena ambacho kitaanza kurushwa hewani hivi karibuni ni kutoa elimu kwa vijana katika kukabiliana na changamoto za maisha.

Alifafanua kuwa kuna vijana wengi wanakata tamaa katika maisha bila kujua walikosea wapi, jambo ambalo limemfanya kuandaa kipindi hicho ili kutumika kama nyenzo ya mafanikio. “Wahusika katika kipindi hiki watapata fursa ya kuzungumzia jinsi alivyohangaika mpaka kupata mafanikio. Ni kumbukumbu ambazo haziwezi kusaulika na kutumiwa na waangaliaji wa kipindi hicho kama nyenzo kwa mafanikio ya vijana wa sasa, ” alisema Doreen.

Alifafanua kuwa ndani ya kipindi hicho, kutakuwa na nafasi ya kutoa burudani kama kuimba kwa mtindo wa karaoke, hali ambayo kinamfanya mtazamaji kutochoka kuangalia. Kwa mujibu wa Doreen, mbali ya wajasiriamali, kipindi cha Tena na Tena pia kitafanya mahojiano na watu mbalimbali maarufu, wanasiasa, wanamichezo kwa lengo la kuhamasisha vijana kutokukata tamaa katika shughuli za kujitafutia vipato. Unaweza kupata taarifa zaidi katika mitandao ya kijamii ya Tena na Tena kupitia @tenanatenashow facebook, instagram, twitter na youtube.
Mbunifu wa Mavazi na Mkurugenzi wa Kituo Cha Redio cha Lake FM, Doreen Peter Noni akirekodi kipindi cha Tena na Tena na wasanii Nevi Kenzo
 Mbunifu wa Mavazi na Mkurugenzi wa Kituo Cha Redio cha Lake FM, Doreen Peter Noni akirekodi kipindi cha Tena na Tena na msanii Vanessa Mdee
  Mbunifu wa Mavazi na Mkurugenzi wa Kituo Cha Redio cha Lake FM, Doreen Peter Noni katika pozi  

MAKAMBO, ZAHERA WABEBA TUZO ZA MWEZI DISEMBA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 

MSHAMBULIAJI wa kimataifa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wa timu ya Yanga Heritier Makambo amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019 ikiwa ni mara ya pili mfululizo.


Makambo , alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Miraji Athumani wa Lipuli ya Iringa na Idd Selemani wa Mbeya City alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam wiki hii na Kamati ya Tuzo ya TPL. 

Kwa mwezi huo wa Desemba, Yanga ilicheza michezo mitano, ambapo Makambo alitoa mchango mkubwa kwa Yanga kupata pointi 15 ikishinda michezo yote mitano iliyocheza, huku mshambuliaji huyo akitoa mchango mkubwa kwa timu yake ikiwa ni pamoja na kufunga mabao manne.

Kwa upande wa Miraji Athumani alikuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya timu ya Lipuli kwa mwezi huo, ambapo timu yake ilicheza michezo minne ikishinda mitatu na kutoka sare mmoja ikijikusanyia pointi 10 na kupanda kutoka nafasi ya 14 hadi ya nane, huku Idd Selemani naye alionesha uwezo wa hali ya juu kwa timu yake ya Mbeya City kwa mwezi huo. 

Pia Kamati ya Tuzo, imemchagua Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kuwa Kocha Bora wa mwezi Desemba akiwashinda Kocha Mkuu wa Lipuli, Samuel Moja na Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Mecky Maxime aliongia nao fainali. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DC JOKATE KUMPA SHAVU BONDIA DULLA MBABE

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE 

SERIKALI ya wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani inatarajia kutoa eneo kwa ajili ya kujenga ukumbi utakaotumika kuwapatia mazoezi ya ngumi vijana wa wilaya hiyo.

Aidha imempongeza bondia Dulla Mbabe mzawa wa wilaya ya Kisarawe kwa ushindi alioupata dhidi ya mpinzani wake Fransis Cheka lillilofanyika hivi karibuni. 

Hatua hiyo ya kupatiwa eneo hilo imetokana na bondia huyo kutoa kauli ya kutaka kutoa mafunzo kwa vijana wa kisarawe ili waweze kujifunza mchezo huo. Akizungumza  kuhusu mpango huo Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amesema,Mbabe amewatendea haki kwa kushinda pambano lililofanyika Desemba 26 mwaka uliopita dhidi ya Cheka. 

Jokate alieleza, Kisarawe imejaa vipaji sio tu mpira wa miguu bali katika michezo mbalimbali. Aliahidi serikali ya wilaya kumpa uahirikiano kuhakikisha kipaji chake kinakua na kuibua vijana wengine. 

Nae bondia huyo Mbabe alijigamba kwa kasema amecheza mipambano zaidi ya 20 ikiwemo ya kimataifa. Hata hivyo aliwaahidi watanzania kufanya vizuri katika Mchezo wa kimataifa unaokuja ambao unatarajiwa kufanyika mwezi march mwaka huu. 

Katika hatua nyingine mbunge wa viti maalum mkoani Pwani Zainab Vullu, alimhakikishia bondia huyo, wabunge wa mkoa huo watamkaribisha Dodoma katika bunge ili kumtambulisha na kuitambulisha Kisarawe kuwa inawanamichezo lukuki sio tu wa mpira wa miguu bali na masumbwi.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akimpongeza Bondia Dulla Mbabe,ambaye ni mzawa wa wilaya ya Kisarawe kwa ushindi alioupata dhidi ya mpinzani wake Fransis Cheka lillilofanyika hivi karibuni. SERIKALI ya wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani inatarajia kutoa eneo kwa ajili ya kujenga ukumbi utakaotumika kuwapatia mazoezi ya ngumi vijana wa wilaya hiyo.

MKUU WA KIKOSI DHIDI YA UJANGILI KANDA YA ARUSHA KUSIMAMISHWA KAZI KUPISHA UCHUNGUZI WA TUHUMA ZINAZOMKABIRI

RAIS DKT. MAGUFULI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA WA MAUZIANO YA MAHINDI KATI YA NFRA NA WFP IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia utiaji saini Mkataba wa Mauziano ya Mahindi kati ya Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi. Vumilia Zikankuba na  Mwakilishi Mkazi wa  Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Duncan kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 4, 2019. Walioketi kushoto ni Manaibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bashungwa na Dkt Omary Mgumba na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias Kuandikwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia kubadilishana nyaraka baada ya utiaji saini Mkataba wa Mauziano ya Mahindi kati ya Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi. Vumilia Zikankuba na  Mwakilishi Mkazi wa  Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Duncan kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 4, 2019.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa utiaji saini Mkataba wa Mauziano ya Mahindi kati ya Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi. Vumilia Zikankuba na  Mwakilishi Mkazi wa  Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Duncan kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 4, 2019.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa WFP nchini Bw. Michael Dunford  pamoja na  Manaibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bashungwa na Dkt Omary Mgumba na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias Kuandikwa, Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na maafisa wengine waandamizi wa taasisi hizo baad ya  hafla fupi ya utiaji saini Mkataba wa Mauziano ya Mahindi kati ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 4, 2019. Kati ni Manaibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bashungwa na Dkt Omary Mgumba..

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa WFP nchini Bw. Michael Dunford  pamoja na  Manaibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bashungwa na Dkt Omary Mgumba na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias Kuandikwana maafisa wengine waandamizi wa UNFPA baada ya  hafla fupi ya utiaji saini Mkataba wa Mauziano ya Mahindi kati ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 4, 2019. Kati ni Manaibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bashungwa na Dkt Omary Mgumba. PICHA NA IKULU

RC MAKONDA ATAKA WATENDAJI KUONGEZA KASI YA MAKUSANYO YA KODI PASIPO KUWASUMBUA WANANCHI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewataka watendaji kuhakikisha wanasimamia ipasavyo makusanyo ya kodi ikiwa ni pamoja na kubuni mbinu mpya na rafiki za ukusanyaji pasipo kuwatisha wala kuwabugudhi wananchi. 

RC Makonda ametoa kauli hiyo wakati wa kikao mkakati baina yake ya mamlaka za ukusanyaji wa kodi ambapo amesema mwaka huu jiji hilo limedhamiria kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ili kuendelea kuwa kinara.Aidha RC Makonda amewataka watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato, kuongeza idadi ya walipa kodi, kufanya mabadiliko ya sheria kandamizi zilizopitwa na wakati pamoja na kuanzisha mfumo wa malipo kwa kadi Kama ilivyo kwa mataifa mengine.

Pamoja na hayo RC Makonda ameshauri kuanzisha kwa kitengo cha ushauri kwa wafanyabiashara jambo litakalowajengea wananchi hamasa ya kulipa kodi na kuondoa dhana ya kuonekana ni watu wa kukusanya mapato pekee.

RC Makonda anaamini kuwa wananchi wapo tayari kulipa kodi serikalini endepo watawekewa mazingira rafiki ya kuwawezesha kulipia ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara kuwekwa katika data base moja.

Kikao hicho kimehusisha wakuu wa wilaya, makatibu tawala, TRA, BOT, TIC, NBS, Wizara ya fedha na kamati za ulinzi na usalama.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na na Watendaji kuhusu kuhakikisha wanasimamia ipasavyo makusanyo ya kodi ikiwa ni pamoja na kubuni mbinu mpya na rafiki za ukusanyaji pasipo kuwatisha wala kuwabugudhi wananchi.

LIGI KUU TANZANIA BARA (TPL) MZUNGUKO WA PILI KUANZA WIKIENDI HII

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BODI ya Ligi imetangaza kuendelea kwa lii Kuu Tanzania Bara (TPL) wikiendi hii kwa mzunguko wa pili kuanza kwa raundi ya Ishirini (20) kuchezwa kwenye viwanja tofauti

Akitolea ufafanuzi huo, Afisa MtendajI Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema kuwa ligi itaendelea kwa zile timu zilizosalia baada ya zingine kwenda kwenye michuano ya Mapinduzi Visiwani Zanzibar.

Wambura amesema kuwa, kuna timu tayari zimeshamaliza raundi ya kumi na tisa (19) kwa mzunguko wa kwanza na wao wataendelea na mzunguko wa pili wa ligi kwa ingawa kuna timu zingine zina mechi hadi tano hawajacheza.

"Kuna timu zina mechi hadi tano hawajacheza ila hatuwezi kusimamisha ligi hadi hao wengine wacheze, tutakachokifanya ni kuwapangia ratiba zao pindi watakaporejea kutoka kwenye michuano ya Mapinduzi,"amesema Wambura.Amesema, kuwa kuna ratiba za mechi zimeondolewa kwa muda huu wakati baadhi ya timu zikiwa zinashiriki michuano ya Mapinduzi ila kama zitarejea mapema basi ratiba yao ya Ligi itaendelea kama kawaida.

Wambura ameeleza kuwa kwa msimu huu kwa zile timu zinazoshiriki michuano ya Kimataifa, kumekuwa na na mabadiliko ya ratiba kwa upande wa CAF ilakama bodi ya Ligi watajitahidi kuweza kuzipanga ratiba ili ziende sawa na ya ligi.

Katika ratiba ya Ligi Kuu Timu ya Simba imecheza michezo 14 akiwa na mechi tano mkononi ambazo ni Azam, Kagera,Coastal Union, Mtibwa na Biashara United , huku Yanga akiwa na mechi 18 akibakisha mchezo mmoja dhidi ya Azam huku wenyewe Azam akiwa na mechi mbili dhidi ya Yanga na Simba.
Afisa MtendajI Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura

MAKAMBO AENDELEZA WEMBE WAKE, ACHAGULIWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI DISEMBA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 

MSHAMBULIAJI wa kimataifa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wa timu ya Yanga Heritier Makambo amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019 ikiwa ni mara ya pili mfululizo. 

Makambo , alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Miraji Athumani wa Lipuli ya Iringa na Idd Selemani wa Mbeya City alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam wiki hii na Kamati ya Tuzo ya TPL. 

Kwa mwezi huo wa Desemba, Yanga ilicheza michezo mitano, ambapo Makambo alitoa mchango mkubwa kwa Yanga kupata pointi 15 ikishinda michezo yote mitano iliyocheza, huku mshambuliaji huyo akitoa mchango mkubwa kwa timu yake ikiwa ni pamoja na kufunga mabao manne. 

Kwa upande wa Miraji Athumani alikuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya timu ya Lipuli kwa mwezi huo, ambapo timu yake ilicheza michezo minne ikishinda mitatu na kutoka sare mmoja ikijikusanyia pointi 10 na kupanda kutoka nafasi ya 14 hadi ya nane, huku Idd Selemani naye alionesha uwezo wa hali ya juu kwa timu yake ya Mbeya City kwa mwezi huo. 

Pia Kamati ya Tuzo, imemchagua Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kuwa Kocha Bora wa mwezi Desemba akiwashinda Kocha Mkuu wa Lipuli, Samuel Moja na Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Mecky Maxime aliongia nao fainali. Zahera aliiongoza timu yake katika michezo minne kati ya mitano iliyocheza, ambayo Yanga ilishinda michezo yote mitano na kuvuna pointi 15 hivyo kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikipanda kutoka nafasi ya pili. 
MSHAMBULIAJI wa kimataifa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wa timu ya Yanga Heritier Makambo ambaye amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019 ikiwa ni mara ya pili mfululizo.


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUANZA KWA VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE, JANUARI 2019

MICHUZI TV :DC JOKATE AANZA MCHAKATO WA UGAWAJI VITAMBULISHO KWA WAJASIRIAMALI WADOGO KISARAWE

WAZIRI LUGOLA ATAKA ASKARI WAPANDISHWE VYEO, WAREKEBISHIWE MISHAHARA, WALIPWE FEDHA ZA UHAMISHO NA LIKIZO

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, MOHA-Karagwe.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka viongozi Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini wahakikishe wanawapandisha vyeo pamoja na kuwarekebishia mishahara askari wote wanaostahili.
Lugola amesema kuna idadi kubwa ya askari wanaostahili kupandishwa vyeo na kurekibishiwa mishahara hivyo askari hao wana haki kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Askari na Watumishi wa Wizara yake, mjini Missenyi na Karagwe Mkoani Kagera, leo. Lugola alisema alitoa agizo kuwa ifikapo  mwezi Agosti mwaka jana agizo hilo liwe limefanyiwa kazi, lakini mpaka umefika mwaka mpya bado halijafanyiwa kazi.
“Kwanini bado hamjapanda vyeo na kubadilishiwa mishahara yenu mpaka sasa wakati nilishatoa maelekezo mpandishwe, nitahakikisha nalifuatilia hili mapema zaidi ili nijue tatizo ni nini.” Alisema Lugola. Pia Lugola alizungumzia kuhusu ukosefu wa nyumba za makazi ya askari, kuwa licha ya Rais Dkt. Magufuli anatoa mchango mkubwa kwa kulisaidia Jeshi, lakini bado kuna upungufu mkubwa wa nyumba hizo.
“Pamoja na fedha kidogo tunazopata lakini bado tuna tatizo la ukosefu wa makazi wa nyumba za askari, lakini bado Serikali inatafuta fedha ili kuhakikisha changamoto hiyo inaisha,” alisema Lugola. Pia lugola alisema changamoto nyingine inayowakabili askari wa vyombo vyake ni kutopata fedha za kuhamishwa na atahakikisha madai yote ya askari hao yanafanyiwa kazi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera, Wallace Mashanda, wakati alipokuwa anawasili Makao Makuu ya Wilaya hiyo, leo. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Luteni Kanali Denice Mwila. Lugola katika kikao chake na Baraza la Askari wilayani humo, aliwataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wahakikishe wanawapandisha vyeo pamoja na kuwarekebishia mishahara askari wote wanaostahili. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera, Luteni Kanali Denice Mwila akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, kilichofanyika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya huyo, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akizungumza katika kikao cha Baraza la Askari na Watumishi wa Wizara yake, katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera, jana. Katika hotuba yake Waziri Lugola aliwataka Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake wahakikishe wanawapandisha vyeo pamoja na kuwarekebishia mishahara askari wote wanaostahili. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera. Lugola aliwataka wananchi wa mji huo wahakikishe wanafuata sheria za nchi kwa kuwa nchi ipo salama. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Wilayani humo, Balozi Dkt. Deodarus Kamala, ambaye alipandishwa jukwaani na Waziri huyo ili aweze kuzungumza na wananchi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA

WAZIRI UMMY ATOA MABATI 100 KATA YA KIRARE JIJINI TANGA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WANANCHI.

$
0
0
MBUNGE wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo amekabidhi mabati 100 katika Kata ya Kirare Jijini Tanga kwa ajili ya zahanati za Mapojoni na Ujenzi wa Bweni la Wasichana Shule ya Sekondari Kirare

Ujenzi huo wa Bweni la Wasichana kwenye shule hiyo litasaidia kuondosha changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu umbali wa kilomita 15 jambo ambalo linaweza kupelekea kukumbana na vishawishi ambavyo vinaweza kukwamisha ndoto zao.

Halfa ya makabidhiano hayo yamefanyika leo kwenye Kata hiyo ikiwa ni juhudi kubwa zinazoonyeshwa na Mbunge huyo kwa ajili ya kuhakikisha changamoto mbalimbali zinazowakabili wananachi anashirikiana nao kuweza kuzipatia ufumbuzi. kizungumza mara baada ya kukabidhi mabati hayo Waziri Ummy alisema serikali ya awamu ya tano itaendelea kuchapa kazi kwa ufanisi mkubwa ili kuweza kutatua changamoto wa wananchi ili ziwez kupata ufumbuzi .

Sambamba na Waziri huyo kuchangia mabati hayo wakati huo huo Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imeguswa na changamoto hiyo na kuchangia mabati 50 na saruji 70 katika ujenzi wa bweni la wasichana la shule ya Sekondari Kirare na kushiriki kwenye shughuli za ujenzi.

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kushoto akimkabidhi mabati 100 Diwani wa Kata ya Kirare Jijini Tanga Mwagilo ambazo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa zahanati za Mapojoni na Ujenzi wa Bweni la Wasichana Shule ya Sekondari Kirare wanaoshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudu Mayeji kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mganga wa Mfawidhi wa Zahanati ya Mapojoni mara baada ya kukabidhi mabati hayo wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji 
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu akizungumza mara baada ya kukabidhi mabati hayo kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji 
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kulia akimsikilkiza kwa  umakini Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mapojoni wakati alipokwenda kukabidhi mabati 100
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kushoto akikagua dawa  kwenye zanhanati ya Mapojoni wakati alipokwenda kuwakabidhi mabati 100.

TAARIFA YA MSIBA

$
0
0


Ndugu Lister Joseph Muro wa Dar es Salaam anatangaza kifo cha Mama yake AMIN-RUTH LAZARO JOSEPH MURO, kilichotokea Machame Nkuu Kilimanjaro,Januari 1,12019, Mazishi
 yatafanyika Machame Nkuu Jumamosi hii Januari 5,2019 saa Saba mchana.


MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN

Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images