Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

HALOTEL YAJIVUNIA MAFANIKIO YA MWAKA 2018, WAKATI IDADI YA WATEJA WAKE IKIFIKIA MILIONI 4 NCHINI KOTE

$
0
0

• Thamani ya HaloPesa hadi 356%
. Malengo kuwafikia wateja wa Halopesa 1.5 million 2019

2018 ulikuwa mwaka mzuri kwa Kampuni ya Halotel Tanzania ikiwa moja ya Kampuni ya Mawasiliano iliyosajiliwa nchini ikifanikiwa kuongeza idadi ya wateja na mawasiliano katika maeno mbalimbali nchini.

Takwimu zilizopo zinaonyesha watumiaji wa mtandao wa Halotel hadi Septemba imeweza kufikia wateja Milioni 4 ikikua kutoka wateja 3.7 Milioni Septemba Mwaka 2017 .Halkadhalika idadi ya watumiaji wa Halopesa ikionekana kuongezeka kwa kasi kutoka watumiaji 358,217 Septemba Mwaka 2017 hadi watumiaji 800,000 Septemba Mwaka 2018.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Nguyen Van Son, kuongezeka kwa mafanikio hayo ya Kampuni hiyo hususani katika huduma za watumiaji wa Halopesa kumetokana na mpango wa utoaji huduma kwa wateja uliozinduliwa na Kampuni mapema Mwaka 2018.

“Kwa kifupi kampuni imeweza kukua katika utoaji wa huduma zake mbalimbali kwa kipindi chote cha mwaka uliopita, katika kipindi hicho Halotel imezindua huduma mbalimbali ikiwemo huduma shirikishi inayomwezesha mteja kutuma au kupokea Fedha kutoka Halopesa kwenda katika akaunti yake au mtandao mwingine wowote wa simu; pia tulizindua huduma ya utoaji mkopo ijulikanayo kama ‘HaloYako’.

“Aidha katika kipindi hicho pia tulikuja na mpango wa ulipaji malipo mbalimbali Serikalini kumwezesha mteja kuondokana na usumbufu mbali na hiyo pia tumeweza kumrahisishia mteja kuweza kutuma fedha katika benki zaidi ya 20 zilizopo nchini” alisema Son.HaloPesa ilikuwa na mawakala hai wapatoa 10,367 Mwaka 2017 lakini hadi tunapozungumza hivi sasa idadi hiyo imeongezeka na kufikia Mawakala 155,000 nchini kote

Aidha alisema mapato yaliyotokana na thamani ya manunuzi ya HaloPesa pia yaliongezeka hadi kuifikia 183%, "Tuliona kiwango cha 356% katika thamani ya manunuzi ya HaloPesa na ongezeko kwa 167% alisema.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Nguyen Van Son, akizungumza mbele ya Waandishi wa habari leo jijini Dar kuhusu mafaniklio iliyopata katika kipindi cha mwaka 2018, ikiwemo kuimarika kwa huduma ya Halopesa na kwa mkongo wa mawasiliano wa kampuni hiyo ambao umefikisha katika vijiji zaidi ya Kumi na tatu elfu nchi nzima,kulia ni
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Mhina Semwenda.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Halotel, Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, leo kuhusu mafanikio iliyopata katika kipindi cha mwaka 2018, ikiwemo kuimarika kwa huduma ya Halopesa na kwa mkongo wa mawasiliano wa kampuni hiyo ambao umefikisha katika vijiji zaidi ya Kumi na tatu elfu nchi nzima. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji , Nguyen van Son.


WAZIRI MKUU AFUNGUA SOKO LA MAZAO SONGEA

$
0
0

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amefungua mradi wa maghala ya kuhifadhi nafaka na soko la mazao la OTC-Lilambo katika Halmashauri ya Songea uliogharimu sh. bilioni 1.5.

Amesema Rais Dkt. John Magufuli ameazimia kuwawezesha wakulima kuwa na mahala pa uhakika pa kuhifadhia mazao yao na sehemu ya kufanyia biashara ili kuwaongezea tija.Amefungua soko hilo leo (Alhamisi, Januari 3, 2019) akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku nne ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani Ruvuma.

Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na ujenzi wa soko hilo pamoja na maghala kwani umezingatia viwango. Maghala hayo mawili yana uwezo wa kuhifadhi tani 5,000 za nafaka.“Licha ya soko hili kuwapa wakulima wetu fursa ya kupata masoko ya kuuzia mazao yao, pia watapata mafunzo ya namna ya kuhifadhi bidhaa zao pamoja na taarifa za masoko.”Kadhalika, Waziri Mkuu ameiagiza bodi ya soko hilo kuhakikisha inatoa matangazo katika vyombo mbalimbali vya habari ili wakulima waweze kupeleka mazao yao sokoni hapo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akifungua  Soko la Mazao   la OTC Lilambo  wilayani Songea Januari 3, 2019. Wapili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, Watatu kushoto ni Waziri wa kilimo, Japhet Hasunga, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Jacqueline Ngonyani Msongozi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akifungua  Soko la Mazao   la OTC Lilambo  wilayani Songea Januari 3, 2019. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, Kulia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro,  wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vyakula mbalimbali vilitokana na unga wa mhogo vilivyoandaliwa na kikundi cha wanamawake wajasiriamali cha  Muungano - Mpandagindo,   wakati lipofungua  Soko la Mazao la OTC Lilambo wilayani Songea, Januari 3, 2019. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Ghala lenye uwezo wa kuhifadhi tani 5000 za nafaka  la OTC Lilambo wilayani Songea ambalo lilifunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Januari 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vyakula mbalimbali  vilivyoandaliwa na kufungashwa kitaalam  na Mtandao wa Wajsiriamali Wadogowadogo Ruvuma (MWARU) wakati alipofungua  Soko la Mazao la OTC Lilambo wilayani  Songea, Januari 3, 2019.  Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. Kushoto ni  Mkurugenzi wa Mtandao wa MWARU, Lucida Chowo (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .


KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

KATIBU MKUU WA CCM DKT. BASHIRU ALLY AWASILI MKOANI MARA,ATEMBELEA KABURI LA BABA WA TAIFA

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally amepokelewa Mkoa wa Mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera

Ndugu Bashiru anafanya ziara ya siku mbili kuimarisha Chama Mkoani Mara ikiwa na pamoja na kutembelea Wilaya ya Butiama alikozikwa mwasisi wetu Mwl. Julius kambarage Nyerere (Baba wa Taifa) Wilaya ya Bunda,Wilaya Musoma Mjini pamoja na Tarime.

Aidha, Ndg. Bashiru Ally amesema katika ziara yake hii ni kukijenga chama na kukiimarisha katika Misingi iliyowekwa na Mwasisi wetu Mwl.Nyerere. Ameyasema hayo Mbele ya wananchi aliapoanzia ziara yake Wilaya ya Bunda na baadaye kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa Utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi Mkuu wa CCM 2015/2020 wakiwa wanakagua kituo cha Afya jimbo la Bunda.

Ndugu Bashiru Ally, Baada ya Wilayani Bunda alielekea Wilayani Butiama kwa Mapokezi Makubwa ya asili ya Nyimbo za Kizanaki (LITUNGU na ZEZE) Huku wakiimba na kucheza na Baada ya Mapokezi hayo katibu Mkuu aliweka shada la Maua katika Kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwl J.Kambarage Nyerere akiwa ameongozana na Viongozi Mbali mbali wa Chama na Serikali.

Akitoa neno la Shukrani Balozi wa China Nchini Tanzania baada ya kuweka Shada la Maua ktk Kaburi la Mwalimu amesema Baba wa Taifa hayati Mwl Nyerere watu wa China tutaendelea kumkumbuka Daima ktk maisha yetu hasa alipowasili nchini China Mwaka 1964

Dkt.Bashiru Ally ametoa salamu za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Ndugu John Pombe Joseph Magufuli kwa wana Mara na kuwambia anawahakikishia kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Mkoa na Uwanja wa ndege wa kisasa Musoma itatekelezwa.

Katibu Mkuu aliongozana na Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Canal Lubinga,Mwenyekiti wa CCM Mkoani Mara ndugu Samweli Niboye(Namba tatu) Mjumbe wa baraza la wadhamini CHAMA Taifa ndugu Gachuma pamoja na Viongozi wa serikali ngazi ya Mkoa na Wilaya.

Katibu Mkuu wa CCM amehitimisha kikao hicho kwa kusisitiza Umoja kwa watumishi wa Chama na Serikali, kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaendeleza misingi iliyo asisiwa na Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Huu ni Mwendelezo Wa Uimarishaji wa Chama Cha Mapinduzi kanda ya ziwa

Imetolewa na:

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI 
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally akizungumza jambo mara baada ya kupokelewa na baadhi ya Viongozi wa Chama na Serikali alipowasili alikozikwa mwasisi wetu Mwl. Julius kambarage Nyerere,Butiama mkoani Mara .
Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally pamoja na Balozi wa China Nchini Tanzania wakiweka shada la Maua katika Kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwl J.Kambarage Nyerere,huku Viongozi Mbali mbali wa Chama na Serikali wakishuhudia tukio hilo.
Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally akiwa ameongozana na baadhi ya viongozi wa chama wakikagua kituo cha Afya jimbo la Bunda.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 4,2019

WANANCHI OLDONYOWASI WACHANGIA SEKTA YA ELIMU

$
0
0
Na Imma Msumba Arumeru

Wananchi wa Kata ya Oldonyowasi Wilayani Arumeru wameitikia wito wa serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuchangia miradi ya maendeleo kwa kuchanga zaidi ya sh. milioni 22.8 ili kuondoa adha ya watoto wao kutembea umbali mrefu kusaka elimu. 

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Cornel Muro pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha DC, Dkt. Wilson Mahera katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana wilayani Arumeru.

Pongezi za Wananchi hao zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambaye yupo katika ziara Wilayani Arumeru baada ya kujionea changamoto za upungufu wa madarasa sambamba na kuzitatua ili Januari saba mwaka 2019 wanafunzi hao waweze kuingia madarasani kuanza masomo yao ya kidato cha kwanza. 

Rc Gambo alisema juhudi walizozifanya wananchi hao wa Kata ya Oldonyowasi zinapaswa kuigwa na wananchi wengine kwani wamejitolea nguvu kazi watu pamoja ni fedha za wadau wa maendeleo ikiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) waliotoa sh. milioni 237 pamoja na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) waliotoa sh. milioni 30, akiwemo mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha, Aminah Mollel kutoa mifuko kadhaa ya saruji huku Halmashauri ya Arusha Dc ikitoa sh. milioni 20.

Alisema tayari ameshaandika barua Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kwaajili ya kuomba usajili kwa shule kadhaa za Mkoa wa Arusha ikiwemo shule hiyo ya Oldonyowasi ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma badala ya kukaa nyumbani wakisubiri usajili wa shule huku wakikosa vipindi madarasani. "Nawapongeza kwa ushirikiano kati ya DC Muro na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Dc Dkt. Wilson Mahera pamoja na wananchi ambao mnajitajidi kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwa kujenga madarasa naomba ushirikiano huu udumu zaidi ili wananchi mfaidi matunda ya elimu bure "

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Ndugu Jerry Cornel Muro amempongeza Rc Gambo kwa kuhakikisha shule hiyo inapata usaili na kusisitiza kuwa shule hiyo itakuwa na kidato cha kwanza hadi cha sita ili watoto wa Kata hiyo na kata nyingine za Jirani waweze kupata elimu. Awali Mwakilishi wa Afisa Elimu Sekondari, Nelson Saro alisema halmashauri ya Arusha Dc wanafunzi 6,846 walifaulu wakiwemo wasichana 3,884 na wavulana 2,962.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro wakiwa wameambatana na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wakikagua madarasa Wilayani Arumeru.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Mashaka Gambo Akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Cornel Muro wakiwa katika moja ya shule walizozitembelea kukagua ujenzi wa madarasa katika Halmashauri ya Arusha Dc Wilayani Arumeru

KESI YA VIGOGO SIMBA KUENDELEA KUUNGURUMA JANUARI, 15

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wa Simba hadi January 15, 2019 kutokana na hakimu anayesikiliza kesi hiyo kutokuwepo.

Vigogo  wanaokabiliwa na kesi hiyo ya uhujumu uchumi ni pamoja na Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva (ambaye hakufika Mahakamani),  Makamu  wake,  Geofrey Nyange maarufu kama 'Kaburu' na Mwenyekiti wa  Kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba Zacharia Hans Poppe.

Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Leonard Swai amemueleza Hakimu Mkazi, Janeth Mtega kuwa shauri hilo liliititwa kwa ajili ya kusikilizwa na Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Thomas Simba hayupo.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi January 15,2019.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi,  kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji fedha haramu.

Katika shitaka la utakatishaji fedha linalomkabili Aveva, anadaiwa Machi 15, 2016 katika benki ya Baclays Mikocheni, jijini Dar es Salaam alijipatia Dola za Kimarekani 187,817, takriban Sh. Milioni 400 kutoka katika Timu ya Simba wakati akijua zimetokana na zao la kosa la kughushi.

Katika shitaka la kughushi linawakabili washtakiwa wote, ambapo wanadaiwa katika tarehe hizo hizo kwa pamoja walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28, 2016 wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zinathamani ya dola 40,577 sawa na zaidi ya Sh. Milioni 90 huku wakijua kwamba sio kweli.

Pia katika shtaka jingine inadaiwa Aveva, Nyange na Hans Poppe kati ya March10 na September 30, 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,577.

WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA MAJI WA LUYEHELA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua tangi la maji wakati alipoweka jiwe la msingi la  Mradi wa Maji wa Luyehe katika kijiji cha Muungano Zomba kwenye jimbo la Peramiho wilayani Songea, Januari 3, 2019. Kulia ni Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda juu tangi la Maji ili kujiridhisha kuhusu  ubora  wake wakati alipoweka jiwe la msingi la  Mradi wa Maji wa Luyehela katika kijiji cha Muungano Zomba kwenye jimbo la Peramiho wilayani Songea, Januari 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsaidia kubeba  ndoo ya maji, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, ikiwa ni ishara ya kuzindua   kituo cha kuchotea maji  katika kijiji cha  Lugagala wilayani Songea, Januari 3, 2019.  Wapili kushoto ni Waziri wa Maji, Juma Aweso na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kumsaidia  kubeba ndoo ya maji, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, ikiwa ni ishara ya kuzindua   kituo cha kuchotea maji  katika kijiji cha  Lugagala wilayani Songea, Januari 3, 2019.  Wapili kushoto ni Waziri wa Maji, Juma Aweso na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsaidia kubeba ndoo ya maji, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, ikiwa ni ishara ya kuzindua  kituo cha kuchotea maji  katika kijiji cha  Lugagala wilayani Songea, Januari 3, 2019.  Wapili kushoto ni Waziri wa Maji, Juma Aweso na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MWAKYEMBE ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MGONAHAZERU

HALOTEL KUKIWASHA MBAGALA KWA SHUKRANI CONCERT

Pata punguzo na unufaike kwa kuwa mteja wa akaunti ya muda maaulum

$
0
0

NOTES ON FIXED ACCOUNT.


·        Pata punguzo na unufaike kwa kuwa mteja wa akaunti ya muda maaulum

·        Riba hadi asilimia 12 kwa mwaka kwa mteja mwenye amana ya kuanzia Milioni 5 kwa kipindi cha miaka miwili na kuendelea

·        Ni fursa nzuri kwa Mstaafu  anayepokea pensheni yake badala ya kununua gari alipendalo awekeze TPB Bank

·        Mtu yeyote anaweza akafungua akaunti hii na kuwekeza

·        Riba inalipwa kila baada ya mwezi, miezi mitatu mpaka sita kulingana na matakwa ya mteja.


GROUP ACCOUNT

Katika kutambua uwepo wa makundi mbali mbali ya watu, kujali mahitaji yao ya huduma za kifedha na adha wanazozipata katika kupata huduma za kibenki, TPB Bank ina akaunti maalum kwa vikundi.  Vikundi rasmi na visivyo rasmi.


Vikundi kama vile, vikundi vya wafanyakazi, vikundi vya ndugu, vilabu vya michezo mbali mbali, wasuka nywele, wasuka mikeka, wavuvi, mafundi seremala, vikundi vya kidini, vikundi vya sehemu ya kazi n.k.


TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2018 NA MATOKEO YA DARASA LA NNE 2018

VIFAA VYA MILIONI 500 MRADI WA MAJI VYATEKETEZWA KWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA WILAYANI NAMTUMBO.

$
0
0
Na Yeremias Ngerangera,Namtumbo.

Mradi wa maji katika kijiji cha Likuyusekamaganga wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma umeingia dosari baada ya vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 500 vya kutekeleza mradi huo kuteketea kwa moto na watu wasiojulikana.

Mwakilishi wa kampuni ya Elegance Developers Company Ltd ya Dar es salaam inayojenga mradi huo,  fundi Ramadhan Abrahaman alisema vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 500 vimeteketezwa kwa moto na watu wasiojulikana .

Kaimu Mtendaji wa kata ya Likuyuseka bwana Petro Nyoni alidai jeshi la polisi linawashikilia watu wawili kuhusiana na tukio hilo akiwemo mlinzi wa kambi bwana Ramadhani Salumu Liyoka pamoja na Athumani Awami Kimbengite .

Aidha bwana nyoni alisema Serikali ya kijiji inatarajia kufanya kikao cha kulijadili swala hilo pamoja na baraza la wazee wa kijiji hicho nao wanatarajia kufanya kikao cha kujadili mienendo mibaya ya kijiji hicho ,kubaini chanzo cha kuibuka kwa matukio mabaya kijijini hapo na kutafuta njia sahihi za kutatua au kudhibiti matukio mabaya yasiendelee kutokea kijijin hapo.

Mhandisi mshauri bwana Nashoni Charles kutoka kampuni ya Norplan Tanzania Ltd ya Dar es salaam alisema kitendo cha kuchoma vifaa hivyo kimeiingizia hasara kampuni lakini pia kitafanya kampuni hiyo kutumia muda mwingine kwenda kununua vifaa , huku muda wa mkataba wa utekelezaji wa mradi huo upo palepale.

Kwa mujibu wa mhandisi mshauri wa kampuni hiyo bwana Nashon alidai mradi huo wa maji wa Likuyumandela umefikia asilimia 45 katika utekelezaji wake na unategemea kuhudumia watu 13,319 kwa kipindi cha miaka kumi baada ya kukamilika kwake.

Kaimu Mhandisi wa maji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Salumu Nachundu alidai mradi unatekelezwa chini ya progamu ya maendeleo ya sekta ya maji (WSDP)kupitia program ndogo ya maji na usafi wa mazingira vijijini (RWSSP)

Gharama za ujenzi wa mradi huo ni shilingi 4,915,864,910 ikiwa mkataba wa mradi huo unategemea kukamilika tarehe 16 marchi 2019 na kiasi cha shilingi 983,172,982 zimelipwa kwa mkandarasi kama malipo ya awali.
 Baadhi ya vifaa vilivyoteketezwa kwa moto na watu ambao mpaka sasa hawajajulikana 
Baadhi ya Mabomba ya kupitishia maji yakiwa yamechomwa moto na watu wasiojulikana.

BARABARA YA MBINGA-MBAMBA BEY KUKAMILIKA 2021

$
0
0
*Waziri Mkuu akagua ujenzi, aridhishwa na kasi ya mkandarasi
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekagua mradi wa ujenzi wa barabara ya lami kutoka Mbinga kwenda Mbamba bey yenye urefu wa kilomita 69 itakayogharimu sh. bilioni 129.3. Amekagua barabara hiyo leo (Ijumaa, Januari 4, 2019) wakati akielekea wilayani Mbinga akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma.

Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo wa barabara inayojengwa na kampuni ya Chico ya nchini China, ambapo ameuagiza uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kusimamia vizuri mradi huo. “Kazi hii inafanywa kwa uhogari mkubwa, naipongeza kampuni ya Chico kwa hatua waliyoifikia na ninaamini kwamba barabara hii inayotarajiwa kukamilika Januari 2021 itakamilika mapema zaidi.”

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutachochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi na mkoa kwa ujumla kwani itarahisisha usafiri kwa watu pamoja na usafirishaji wa mizigo. Amesema pia barabara hiyo itakuza sekta ya utalii na uvuvi katika mkoa wa Ruvuma kwa sababu itawezesha watalii na wafanyabiashara kufika kwa urahisi katika wilaya ya Nyasa ambako ni kuingo cha biashara kati ya nchi jirani na mikoa inayopitiwa na ziwa Nyasa.

Mkuu huyo wa mkoa ametumia fursa hiyo kuushukuru uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwapelekea fedha za ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya hospitali, vituo vya afya, shule, nishati na maji.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimina na Mbunge wa Nyasa na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya Mbinga- Mbamba bay kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilomita 66, Januari 4, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi ya CHICCO kutoka China inayojenga barabara ya Mbinga – Mbamba bay  kwa kiwango cha lami, yenye urefu wa Kilomita 66 wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo, Januari  4, 2019. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma,  Christina Mndeme. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Ruvuma na wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi ya CHICCO kutoka China inayojenga barabara ya Mbinga – Mbamba bay yenye urefu wa Kilomita 66 wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo, Januari 4, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi  wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya Mbinga – Mbamba bay kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilomita 66 unaofanywa na Kampuni  kutoka China ya CHICCO, Januari 5, 2019.  
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu wa Jimbo la Mbinga, John Ndimbo wakati alipowasili kwenye kijiji cha Nyoni wilayani Mbinga kuhutubia mkutano wa hadhara Januari 4, 2019. Kulia ni Sheikh wa wilaya ya Mbinga, Said Majid

NAIBU WAZIRI MABULA AWATUMBUA WAKUU WA IDARA YA ARDHI KIGOMA

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM Kigoma
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amewavua nyadhifa zao Wakuu wa Idara za Ardhi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya wilaya ya Kigoma pamoja na Afisa Ardhi Mteule kutokana na watendaji hao kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Waliovuliwa nyadhifa zao ni Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Brown Nziku, Emanuel Magembe Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na Afisa Ardhi Mteule wa Manispaa ya Kigoma ambaye pia Afisa Mipango Miji Paul Misuzi.

Mabula alifanya maamuzi hayo jana tarehe 3 Januari 2019 alipofanya ziara ya kushtukiza katika manispaa na halmashauri ya Kigoma wakati akiwa mkoani humo kuhudhuria kikao cha utatuzi wa mgogoro wa matumizi ya ardhi katika hifadhi ya Moyowosi mkoani Kigoma.

Uamuzi wa kuwavua nyadhifa watendaji hao wa sekta ya ardhi unafuatia kushindwa kusimamia maagizo na maelekezo yaliyotolewa tangu mwaka 2017 kuhusu ukusanyaji kodi ya ardhi, uingizaji wamiliki wa viwanja na mashamba kwenye mfumo wa malipo kwa njia ya kielektronik, utoaji hati kwa wamiliki wa ardhi pamoja na utoaji hati za madai kwa wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi jambo lillosababisha manispaa na halmashauri husika kukosa mapato yanayotokana na kodi ya ardhi.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akipata maelezo mara baada ya kuwasili ofisi za halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji alipofanya ziara ya kushtukiza katika manispaa hiyo jana ambapo aliwavua nyadhifa wakuu wa Idara ya Ardhi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya wilaya ya Kigoma pamoja na Afisa Ardhi Mteule kutokana na kushindwa kusimamia majukumu yao ipasavyo, wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Mwailwa Pangani.
 Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Brown Nziku (kulia) na Afisa Ardhi Mteule Paul Misuzi (wa pili kulia) ambao wamevuliwa nyadhifa zao, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kustukiza katika Manispaa ya Kigoma wakati akihudhuria kikao cha utatuzi wa mgogoro wa matumizi ya ardhi katika hifadhi ya Moyowosi Kigoma.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angeline Mabula akimsikiliza mkazi wa Kigoma Iddy Salum alipowasilisha malalamiko yake kuhusiana na fidia kwenye Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZ) alipofanya ziara ya kushtukiza katika Manispaa ya Kigoma jana wakati akihudhuria kikao cha utatuzi wa mgogoro wa matumizi ya ardhi katika hifadhi ya Moyowosi Kigoma, Katikati ni Kamishna Msaidizi Kanda ya Magharibi Idrisa Kayera (Picha zote na Hassan Mabuye Wizara ya Ardhi).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MAKAMBA AONGOZA KAMPENI UPANDAJI MITI MJI WA SERIKALI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo ameongoza watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais kupanda miti zaidi ya elfu moja (1000) katika eneo la Mji wa Serikali, inapojengwa Ofisi ya Makamu wa Rais.

Waziri Makamba amesisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu na takribani miti 1000 ya aina ya mdodoma inayostahimili ukame imepandwa hii leo. “Sisi ni watu wa Mazingira, ni lazima tuonyeshe mfano, hapa kila mtumishi atakuwa na wajibu wa kutunza miti atakayokabidhiwa na kuhakikisha inakua” Makamba alisisitiza.

Waziri Makamba amesema kuwa Jiji la Dodoma linakabiliwa na changamoto ya mandhari kutokana na ardhi yake kuwa kame na kupelekea uoto wa asili kupungua kwa kiasi kikubwa. Hivyo, ametoa wito kwa kila taasisi na Idara kuunga mkono kwa vitendo kampeni iliyozinduliwa na Mhe. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Novemba 2017 ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani, kwa kupanda miti kwa wingi katika Mji wa Serikali na Dodoma kwa ujumla ili uwe mji wa mfano kwa kuwa na mandhari yakuvutia.

“Kwa kuwa sisi ndio wasimamizi wa Mazingira, upandaji na usimamizi wa miti ni sehemu ya Hifadhi ya Mazingira, hivyo lengo la Ofisi yetu ni kuonyesha mfano, watumishi wote kuanzia Waziri mpaka Mhudumu kila mmoja atakuwa na miti yake ya kutunza na kuhakikisha inakua” Makamba alisisitiza.

Awali Waziri Makamba alipata fursa ya kutembelea eneo inapojengwa Ofisi ya Makamu wa Rais na kuridhishwa na kasi ya ujenzi katika eneo hilo na kumtaka Mkandarasi wa Mradi kutoka (Vikosi vya Ujenzi) Mhandisi Simeo Machibya kukamilisha kazi yote kwa wakati. “Ujenzi huu ufanyike usiku na mchana” Makamba alisisitiza.

Katika zoezi la leo Waziri Makamba ameambatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo, Naibu Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali kutoka kwa Mhandisi Simeo Machibya ambae ni Meneja Msimamizi wa Mradi kutoka Vikosi vya Ujenzi. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizindua zoezi la upandaji miti katika mji wa Serikali Dodoma. Miti 800 aina ya “midodoma” imepandwa katika eneo hilo na miti 200 ya aina nyingine pia imepandwa ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuifanya Dodoma kuwa ya kijani. Kulia ni Bw. Timothy Mande Afisa Misitu kutoka Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais.

Mkazi wa Simiyu ashinda Milioni 56.1 za M-bet

$
0
0
Mkazi Bariadi Mkoa wa Simiyu, Golesu Maduhu (23) ameshinda Sh 56,137,550 baada ya kubahatisha kwa usahihi mchezo wa Perfect 12 unaoendeshwa na Kampuni ya M-Bet Tanzania.

Maduhu ameweza kubahatisha matokeo ya droo ya Desemba mwaka jana na kuwa mshindi wa kwanza kuzawadiwa fedha kutoka kampuni ya M-Bet kwa mwaka huu. Maduhu alipatia kiusahihi michezo yote 17.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Maduhu alisema kuwa amefurahi sana kupata kiasi hicho cha fedha ambacho kitamsaidia katika maisha yake. Maduhu amesema kuwa ametumia sh 1,000 kupata mamilioni hayo ya fedha na kuwaomba Watanzania kujiunga na michezo ya kampuni ya M-BET ambayo inachangia kubadili maisha. Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa katika fedha hizo, Serikali imepata Sh milioni 11.2 ikiwa ni kodi ya ushindi. “Nawaomba Watanzania washiriki katika michezo ya kubahatisha ya M-bet ambayo mwaka 2018 iliwazawadia jumla ya washindi 20 ambao walipata mamilioni ya fedha na kubadili maisha yao,” alisema Mushi.

Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Kubahatisha Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoa wa Ilala, Shabani Rashid Mwanga naye aliwaomba Watanzania kushiriki katika michezo hiyo ili kuchangia maendeleo ya nchi. Mwanga alisema kuwa unaoposhinda kiasi chochote, serikali inapata kodi yake moja kwa moja na kuongezea fedha za kufanyia maendeleo nchini. “Naishukuru M-Bet ambayo kila mara imekuwa ikitoa washindi wamekuwa wakipata mamilioni ya fedha na kuchangia pato la Taifa, ni chanzo kizuri sana cha mapato kwa ajili ya maendeleo ya nchini,” alisema Mwanga.

Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Catherine Lamwai aliipongeza kampuni ya M-bet kwa kuweka kuendelea kupata washindi wengi na kujizolea mamilioni ya fedha. “Bodi ya Michezo ya Kubahatisha imekuwa ikifuatilia na kusimamia michezo ya kubahatisha kutokana na kupata washindi wengi. Wametufurahisha sana kutokana kuchangia pato la Taifa kupitia mchezo wa Perfect 12,” alisema Lamwai.

Mshindi wa Droo ya 20 ya mchezo wa Perfect 12 wa kampuni ya M-bet, Golesu Maduhu (wa pili kushoto) akipokea mfano wa hundi baada ya kushinda Sh milioni 56.1 kutoka kwa meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi (wa tatu kushoto) baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 17. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Kubahatisha Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoa wa Ilala, Shabani Rashid Mwanga na wa kwanza kulia ni Meneja wa Leseni na Huduma za Sheria wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Catherine Lamwai. 

DC JOKATE MWEGELO AANZA KUKABIDHI VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI WADOGO WILAYANI KISARAWE

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani Jokate Mwegelo ameanza ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wilayani humo kwa lengo la kuhakikisha wanatambuliwa na kufanya shughuli zao za kiuchumi bila kusumbuliwa.

Jokate ametoa vitambulisho hivyo leo kwa baadhi ya wajasiriamali wa Wilaya ya Kisarawe ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu Rais Dk.John Magufuli alipozindua utoaji wa vitambulisho hivyo kwa kuwapa wakuu wa mikoa yote nchini ili vigawiwe kwa wajasiriamali.

Akizungumza leo wilayani hapo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Wilaya ambao wameshiriki kushuhudia tukio la ugawaji wa vitambulisho hivyo, Jokate amesema katika wilaya hiyo kuna wajasiriamali 502 na hivyo ugawaji huo utaendelea kwa kuhakikisha wote wanaostahili kuvipata wanapewa.

Amesema wilaya ya Kisarawe inatambua mchango wa wajasiriamali hao na kwamba wamedhamiri wote wapewe vitambulisho hivyo ambavyo pamoja na mambo mengine kwa wale ambao watakuwa na vitambulisho hivyo watafanyakazi zao za ujasiriamali bila kusumbuliwa.

"Mkuu wa Mkoa wetu wa Pwani ametukabidhi hivi vitambulisho kwa ajili ya kuwapatia wajasiriamali, hivyo leo tumeanza kuvigawa.Ni mchakato endelevu ambao tutaufanya kwa wakati na hapa kwetu tunao wajasiriamali 502, na wote tutawapa," amesisitiza Jokate.

Wakati huo huo amezungumzia mikakati ya Wilaya ya Kisarawe katika kuhakikisha wanapiga hatua ya kimaendeleo ikiwa pamoja na kuitangaza Wilaya hiyo ambayo ina fursa za kila aina za kiuwekezaji .

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo akimkabidhi kitambulisho cha ujasiriamali mjasiriamali Indiana Mohamed Mnyukwa katika kikao cha RCC kinachofanyika mjini Kisarawe leo wilaya ya Kisarawe imeanza kutekeleza agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli aliyetoa vitambulisho kwa ajili ya wajasiriamali nchini kote.

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajasiriamali waliokabidhiwa vitambulisho vyao leo.

Jafo Asisitiza Viongozi Kutembelea Miradi

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemank Jafo amesisitiza Viongozi na watendaji kutembelea miradi ya maendeleo inayo tekelezwa katika maeneo hayo ili miradi hiyo iweze kutekelezwa vizuri Kama inavyotakiwa.

Waziri Jafo aliyasema hayo Leo hii alipokuwa katika ukaguzi wa miradi ya DMDP wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo ya kikazi ya waziri wa TAMISEMI ni muendelezo wa kazi tokea kuanza kwa mwaka 2019 iliyoanzia Wilayani Chemba, Kilosa, Kibiti, Rufiji, na Temeke.

Katika ziara hiyo Jafo alifanikiwa kufanya ukaguzi wa barabara za DMDP katika Kata ya Buza, ujenzi wa kituo cha afya Buza, pamoja na soko la kisasa linalojengwa eneo la Makangarawe.

Katika ukaguzi huo Jafo alifurahishwa Sana na kazi nzuri inayo tekelezwa katika eneo hilo. Ameagiza kituo hicho pamoja na soko hilo la kisasa likamilike kabla mwezi June mwaka 2019.

Waziri Jafo anaendelea na ziara ya kikazi mkoani Kigoma kwa lengo la kufuatilia thamani ya fedha zilizotewa chini ya ofisi ya Rais TAMISEMI kutekeleza miradi ya maendeleo katika Halmashauri zote Nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(katikati) akikagua barabara zinazokengwa na mradi wa Dmdp katika kata ya Buza eneo la Makangarawe
Soko la kisasa linaloendelea kujengwa katika Kata ya Buza eneo la Makangarawe kupitia mradi wa Dmdp
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(katikati) akikagua ujenzi aa Kituo cha Afya kinachojengwa katika Kata ya Buza

Biteko Asisitiza Sekta za kiserikali Kupunguza Urasimu, Kuondoa Rushwa

$
0
0
Ni baada ya kubaini ucheleweshaji wa utoaji vibali vya uwekezaji sekta ya madini.

Na Nuru Mwasampeta, Geita.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kutoa kibali kwa wamiliki wa Kiwanda cha Kuchenjua Dhahabu kinacho milikiwa na kampuni ya Pedalu ili waweze kupewa leseni na kuendelea na shughuli ya kuchenjua madini hayo.

Biteko aliyasema hayo wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la kiwanda cha kuchenjua dhahabu kinachomilikiwa na kampuni ya wazawa ya Pedalu, katika kijiji cha Lumasa mjini Chato, iliyofanyika Desemba 2, 2019.

Alisema kuwa, kibali kingine kinapaswa kutolewa na Mkemia Mkuu wa Serikali na kubainisha kuwa, baada ya hafla hiyo atawasiliana naye ili awezeshe upatikanaji wa kibali hicho kwa lengo la kuiwezesha wizara ya madini kuendelea na mchakato wa kuandaa leseni itakayowaruhusu wawekezaji hao wazawa kuendelea na kazi ya uchenjuaji wa adini.“Jamani, Rais anataka viwanda, isitokee mtu hapa katikati anaweka urasimu na kuchelewesha azma ya Rais wetu, nchi hii tunaondoa urasimu tunataka kuondoa na rushwa,” alisisitiza Biteko.

Aidha, alibainisha kuwa, miongoni mwa masuala yanayowakimbiza wawekezaji nchini ni mawili tu, rushwa na urasimu na wala si sheria, na kusema kuwa, vitu hivyo ni kikwazo kikubwa katika kutimiza azma ya Serikali ya Tanzania ya Viwanda.

Aliwapongeza wawekezaji katika kiwanda cha Pedalu kwa kufanya uwekezaji huo mkubwa kwani anaamini madini yatakayopatikana kutoka katika kiwanda hicho yataiwezesha serikali kupata  kodi stahiki. Pia, Biteko aliwaomba wawekezaji hao wazawa kujenga viwanda vingine kama hivyo katika maeneo tofauti na kuahidi kupeleka wadau wenye nia ya kujifunza ili waweze kupata ujuzi wa namna ya kuwekeza ili kukuza sekta ya madini kwa pamoja.


Naibu Waziri wa Madini (kulia) na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (Kushoto) wakifungua kitambaa katika jiwe la msingi ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa kiwanda hicho cha kuchenjua dhahabu kilichopo mkoani Geita wilaya ya Chato mnamo tarehe 02 Januari, 2019.

????????????????????????????????????


Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (Kushoto) akisalimiana na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato  Dkt. Medard Kalemani (kulia) mara baada ya kuwasili katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwenye kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Pedalu kilichopo wilayani Chato mkoani Geita.
TWO
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (Wa tatu kutoka Kushoto), Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato Dkt. Medard Kalemani (wa pili kutoka kulia) wakielekea eneo maalum kwa ajili ya kupata maelezo pamoja na kuweka rasmi jiwe la msingi la kiwanda cha Pedalu uliofanyika tarehe 02 Januari, 2019 mjini Chato.
THREE
Msimamizi wa kiwanda cha kuchakata dhahabu cha Pedalu mjini Chato akitoa maelezo ya namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi ya uchenjuaji wa dhahabu kwa Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko na wajumbe alioambatana nao wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>


Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images