Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

UFUMBUZI WA KUONDOA KITAMBI, MANYAMA UZEMBE, KUPUNGUZA UNENE NA UZITO

$
0
0
 Habari njema kwa watu wenye tatizo la kiriba tumbo ( Kitambi ), Manyama Uzembe, Unene na Uzito ulio zidi. Neema Herbalist ni duka la kuuza dawa mbalimbali za asili. Tunapenda kuwataarifu wateja wetu wapendwa kuwa tunayo mafuta ya asili ambayo yanasaidia kuondosha kabisa kitambi na manyama uzembe pamoja na kupunguza unene na uzito kwa kiwango kizuri sana . 

 Mafuta haya ni ya asili kabisa ( Pure herbal ) yasiyo na kemikali yoyote ya viwandani na yanaondoa kitambi na manyama uzembe ndani ya siku thelathini. Mafuta haya ya asili yanatumika pamoja na dawa nyingine ya asili ambayo ipo katika mfumo wa unga. Tiba hii ya asili imegawanywa katika dozi mbili. Dozi ya kwanza utatumia dawa hii ya asili iliyo katika mfumo wa unga pamoja na vichupa kumi na tano na utatumia kwa muda wa siku kumi na tano. 

 Yaani kwa siku moja utatumia kula kichupa kimoja cha mafuta haya asubuhi na usiku pamoja na dawa iliyo katika mfumo wa unga. Na dozi ya pili utaitumia kwa muda wa siku nyingine kumi na tano ambapo kama ilivyo kwa dozi ya kwanza utatumia kula kichupa kimoja kwa siku kwa muda wa siku kumi na tano mfululizo pamoja na dawa iliyo katika mfumo wa unga. 

 Tiba hii inaondoa kitambi na kupunguza uzito na unene pila mtumiaji kuharisha kwa hiyo hakuna suala la kuharisha katika tiba hii. Tiba hii pia ni nzuri sana kwa watu wenye kusumbuliwa na sukari kwani inasaidia pia kusawazisha kiwango cha sukari katika damu. Kupata dawa hizi fika katika duka la kuuza dawa za asili la NEEMA HERBALIST. Tunapatikana UBUNGO jirani na SHULE YA MSINGI UBUNGO NATIONAL HOUSING nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA. 

 Kwa wateja wetu waliopo jijini DAR ES SALAAM ambao hawana nafasi ya kufika ofisini kwetu tunayo huduma ya kuwapelekea dawa mahali popote pale walipo ndani ya jiji la DAR ES SALAAM ( HOME AND OFFICE DELIVERY ) Na kwa wateja wetu waliopo nje ya mkoa wa Dar Es Salaam, tunawatumia dawa kwa njia ya mabus mbalimbali na wale waliopo Zanzibar tunawatumia dawa kwa njia ya boti. 
 WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0693 005 189. 
 Na kwa taarifa zaidi kuhusu huduma zetu, tutembelee kila siku kupitia blogu yetu : www.neemaherbalist.blogspot.com

Introducing Brand new track "Zimepita kwa hapa" by Chaba 009

Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti wa 2019/2020 wafana

$
0
0
Majid Abdulkarim
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia maswala ya Afya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa Sehemu ya Mipango na Uratibu na Maafisa Mipango wote wa Halmashauri nchini kutumia taaluma zao katika kukuza uchimi wanchi ili kuleta matokeo bora kwa watanzania wanao watumikia.

Hayo yamebainishwa leo wakati  wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 yatakayo fanyika leo na kesho hapa jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Royal Vilage Hoteli. Dk. Chaula amesema mafunzo hayo ni fursa kwa maafisa hao  kuhakikisha wanapata ujuzi wa kuweza kupata matokeo bora katika kukuza uchumi wanchi hii.
“Ili kufikia matokeo bora ya kukuza uchumi wa nchi hii mnatakiwa kuwa wabunifu kwa kuchukua changamoto na kuzigeuza kuwa fursa ili kuinua uchumi nchi hii” Alisema Dk. Chaula.

Dk. Chaula ameongeza kuwa kila mtumishi wa Umma anadhamana kubwa kwa taifa hili , na dhamana yenyewe ni kuhakikisha tunawatumikia vyema watanzania wenzetu ili kuleta matokeo bora kwa nchi yetu kama Muhasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyo fanya mpaka leo kupitia matokeo yake tunamkumbuka. Aidha Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango OR-TAMISEMI, amesema kuwa kupitia mafunzo hayo maafisa hao watanufaika kwa kupata  uelewa wa kuandaa bajeti iliyobora na kuwa walimu wazuri kwa maafisa wengine katika maeneo yao ya kazi.
 Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia maswala ya Afya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Royal Vilage Hoteli. 
Baadhi ya  Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa Sehemu ya Mipango na Uratibu na Maafisa Mipango  wa Halmashauri nchini wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia maswala ya Afya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula (hayupo pichani) leo katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2019/2020, leo jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Royal Vilage Hoteli.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UTT AMIS YATOA ELIMU YA MIFUKO YAO KWA WANANCHI MBALIMBALI NA WASHIRIKI WA SEMINA JIJINI MOROGORO

$
0
0
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS Ndugu Daudi Mbaga akitoa mada juu ya uwekezaji wa pamoja kwa wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali katika semina iliyoandaliwa na National Institute of Productivity jijini iliyofanyika Morogoro.
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS Ndugu Daudi Mbaga akitoa mada juu ya uwekezaji wa pamoja kwa wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali katika semina iliyoandaliwa na National Institute of Productivity jijini iliyofanyika Morogoro.
Afisa Masoko Mwandamizi wa UTT AMIS Bi. Martha Mashiku akifundisha jinsi mifuko ya uwekezaji wa pamoja yaweza kuwa suluhisho kwa maisha baada ya kustaafu katika Semina iliyoandaliwa na TAGLA Morogoro.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.

DNA, UJUE UTARATIBU WA KISHERIA WA KUJUA MTOTO NI WAKO AMA SI WAKO

$
0
0
Na Bashir Yakub.
Huna haja ya kuvutana na mtu kuhusu iwapo wewe ni baba wa mtoto au hapana. Nimesema baba kwasababu wasiwasi wa aina hii mara zote upo kwa wanaume. Kuwa fulani ni mama wa fulani karibia mara zote hapana utata.

Basi wapo wanaopenda au ambao wangependa kufanya vipimo vya vinasaba(DNA) kuthibitisha kama ni wazazi kweli ama hapana. Nitaeleza utaratibu mzima hapa kutokana na Sheria ya Usimamizi wa Vinasaba vya Binadamu ya 2009,Sura ya 73.

1. NANI ANAWEZA KUPIMWA DNA.
Yeyote ambaye anahitaji kujua kuhusu uhalali wa uzazi wake anaweza kupima DNA. Upimaji huu hauna umri. Hata hivyo DNA si kwa jili ya masuala ya kuthbitisha uzazi tu, bali hutumika hata katika masuala ya ushahidi na upelelezi.

2. NANI ANA MAMLAKA YA KUOMBA DNA KUPIMWA.
Si kila mtu anaweza kuomba kupima DNA. Hata kama mwenye uhitaji ni wewe lakini bado huna mamlaka ya kuomba kupima DNA. Kifungu cha 25(2) cha Sheria niliyotaja hapo juu kinawataja wafuatao kuwa na mamlaka ya kuomba DNA kupimwa. Kinamtaja hakimu ambapo kuna kesi/shauri fulani linaendelea, Wakili, afisa ustawi wa jamii, afisa polisi mwenye cheo zaidi ya inspector,daktari, na mkuu wa wilaya.Hawa ndio wenye mamlaka(Requesting Authority).Kwahiyo wewe ukiwa na shida ya DNA unaweza kumuona mmoja kati ya hawa ili aandae maombi ya kupima DNA na kuyapeleka kunakostahili.

3. MAOMBI YA DNA YANAPELEKWA WAPI
Kifungu cha 24 cha Sheria ya Usimamizi wa Vinasaba kinaitaja maabara ya Vinasaba vya binadamu ya Mkemia Mkuu wa serikali kuwa na Mamlaka ya kupima DNA. Pia kinazitaja na maabara nyingine ambazo zitakuwa na leseni maalum ya kupima DNA kuwa na mamlaka hayo.

Kwahiyo maombi ya DNA yatapelekwa moja kati ya sehemu hizo mbili.


MICHUZI TV: IJUE BUSTANI YA FORODHANI KIVUTIO KWA WATU WENGI ZANZIBAR

RELI TV: SGR Yaleta Neema Kisarawe, TRC na YAPI Merkez Watimiza Ahadi ya Ujenzi wa Madarasa kwa DC JOKATE KISARAWE

Rais Magufuli afuta maelekezo kuhusu Bendera, Nembo na Wimbo wa Taifa


NEWS ALERT: Air Tanzania's FIRST Airbus A220-300 (BCS3) in action in Montreal

Introducing Alikiba's new drop "Kadogo" (Official Music Video)

Introducing Darassa's new club banger "Achia Njia" (Official Music Video)

BREAKING: MBUZI AMPONZA DEREVA WA BENKI YA MAENDELEO (TIB) KWA KUKIUKA HAKI ZA WANYAMA

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 14/12/2018

Habari za UN Disemba 14, 2018

WAZIRI UMMY ASHIRIKI MKUTANO MAALUM WA MAWAZIRI WA AFYA KUHUSU AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI INDIA

$
0
0
Tanzania imeshiriki katika Mkutano Maalum unaojadili Afya ya Mama na Mtoto unaojulikana kama "4th Partnership for Maternal,Newborn and Child Health 2018" uliofanyika katika jiji la New Delhi, India kuanzia tarehe 12 hadi 14 Desemba,2018.

Katika Mkutano huu,Tanzania imewakilishwa na Mhe.Ummy Mwalimu,Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.Mkutano huu ulifunguliwa na Mhe.Shri Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India tarehe 12 Desemba, 2018. 

Mkutano huu unawakutanisha pamoja Mawaziri wa Afya kutoka nchi mbalimbali duniani kwa lengo la kujadili changamoto zilizopo katika eneo la Afya ya Mama na Mtoto na kuweka mikakati ya pamoja ya kuzitatua changamoto hizo ili kuboresha upatikanaji wa huduma za Afya ya Mama na Mtoto.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Waziri Mkuu wa India alieleza mafanikio yaliyopatikana katika kupunguza vifo vya mama mjamzito na watoto wachanga kufuatia mikakati mizuri iliyowekwa na Serikali ya India na kuzitaka nchi washiriki kuweka mipango thabiti itakayotekelezeka katika kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza kwenye Mkutano Maalum wa 4 wa Mawaziri wa Afya kuhusu Afya ya Mama na Mtoto (Partnership for Maternal, Newborn and Child Health Forum 2018) uliofanyika New Delhi, India kuanzia tarehe 12 hadi 14 Desemba, 2018. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akisalimiana na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi wakati wa ufunguzi wa Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Afya uliofanyika katika jiji la New Delhi, India kuanzia tarehe 12 hadi 14 Desemba, 2018.
Picha ya pamoja ya Mawaziri wa Afya pamoja na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo
Picha ya pamoja ya Mhe.Waziri Ummy Mwalimu na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano Maalum wa Afya ya Mama na Mtoto jijini New Delhi, India. Wa pili kukia ni Mhe. Baraka Luvanda, Balozi wa Tanzania nchini India

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto, Mhe. Ummy Mwalimu akijadiliana jambo na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda (kushoto} wakati wa Mkutano Maalum wa 4 wa Mawaziri wa Afya kuhusu Afya ya Mama na Mtoto

Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA, Marekani, Bibi Natalia Kanem wakati wa Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Afya kuhusu Afya ya Mama na Mtoto uliofanyika New Delhi, India


AGPAHI ARIEL CAMP 2018 YAFUNGWA DAR

$
0
0
Kambi ya watoto na vijana inayosimamiwa na Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) maarufu kama Ariel Camp 2018’ iliyoshirikisha washiriki 50 kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu imefungwa leo Ijumaa Disemba 14,2018 jijini Dar es salaam.

Akifunga kambi hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS), Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa Tume hiyo Bw. Jumanne Issango aliipongeza AGPAHI kwa kuanzisha kambi hizo zinazolenga kuwapa watoto na vijana msaada wa kisaikolojia utakaowawezesha kukabialiana na changamoto zinazowakabili.

“Naishukuru AGPAHI kwa kutoa msaada huu wa kisaikolojia kwa watoto na vijana kwani huduma hiyo ni muhimu sana kwa afya na ustawi wao hasa ikizingatiwa kuwa changamoto hizo zinawaathiri  kimwili, kiafya, kijamii na kisaikolojia,” alisema Bw. Issango.

Aidha aliitaka jamii kubadilika na kuacha vitendo vya kunyanyapaa wanaoishi na maambukizi ya VVU huku akiwahamasisha watoto na vijana hao kutumia kwa usahihi dawa za kufubaza makali ya VVU ili kuimarisha afya zao.

“Ili kuishi maisha bora na kukamilisha ndoto zenu za baadaye nawakumbusha kuwa ARV ndiyo mpango mzima, Watu wasiotumia vizuri dawa hizi afya zao zimekuwa zikitetereka na kushambuliwa na magonjwa nyemelezi na hata kufa. Kamwe msiache kutumia dawa kwa sababu yoyote ile,” alisisitiza.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa TACAIDS Bw. Jumanne Issango akizungumza katika ukumbi wa Serene Beach Resort wakati akifunga Ariel Camp 2018 kwa niaba ya Mkurugenzi wa TACAIDS. Kushoto ni Mkurugenzi wa Taarifa za Kimkakati wa AGPAHI, Dk. Boniface Idindili,kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za mama na mtoto AGPAHI, Dk. Akwila Temu.
Washiriki wa Ariel Camp wakimsikiliza mgeni rasmi.
Mkurugenzi wa Taarifa za Kimkakati wa AGPAHI, Dk. Boniface Idindili akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI wakati wa kufunga Ariel Camp 2018.
Waliokaa ni washindi wa shindano la Mr & Miss AGPAHI Ariel Camp wakiwa katika picha ya pamoja na jaji Lugano Maclean (wa kwanza kulia) na kiongozi wa washiriki wa shindano la Urembo 'Mr & Miss Ariel Camp' Agnes William ( wa kwanza kushoto) na washiriki wa shindano hilo. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Biteko afungua Ofisi ya Madini Mahenge mkoani Morogoro

$
0
0


Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Afisa Migodi Mkazi Mahenge-Ulanga mkoani Morogoro, jana Disemba 14, 2018. Wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali wa Serikali, Tume ya Madini pamoja na wachimbaji madini.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akisaini kitabu cha wageni baada ya kufungua ofisi ya Afisa Migodi Mkazi Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro. Aliyesimama ni mbunge wa Jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga.
Mkuu wa Wilaya Ulanga, Ngolo Malenya akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Afisa Migodi Mkazi wilayani humo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa tatu), Mkuu wa Wilaya Ulanga, Ngolo Malenya (wa pili kulia),  Kamishna wa Madini kutoka Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeke (wa kwanza kushoto), Mbunge Jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga (wa pili kushoto) pamoja na Afisa Migodi Mkazi Wilaya ya Ulanga, Tandu Jilabi (wa kwanza kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa ofisi hiyo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Serikali, Tume ya Madini pamoja na wachimbaji madini wilayani Ulanga.

VIJIJI VILIVYOPAKANA NA MKUZA WA BOMBA LA GESI ASILIA VYAPEWA ELIMU YA ULINZI NA USALAMA WA BOMBA

$
0
0
Kutokea kusini mwa Tanzania katika mikoa ya Lindi na Mtwara, limelala bomba lenye kipenyo cha inchi 36 na urefu wa kilometa 551 kuelekea jijini Dar es Salaam. Bomba hili lina uwezo wa kupitisha gesi asilia futi za ujazo milioni 784 kwa siku na lina matoleo yapatayo 16 ambayo yamewekwa kimkakati kuruhusu uunganishwaji wa gesi kwa wateja maeneo bomba linapopita. Bomba hili linapita katika vijiji takribani 136 ambapo suala la ulinzi limefanywa kuwa ni la kushirikiana kwa kuwawezesha wananchi wa vijiji husika kutoa huduma ya ulinzi katika mkuza wa bomba. 

Kwa kuzingatia kwamba suala la elimu na uhamasishaji ni suala endelevu, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ambalo ndio msimamizi wa miundombinu hiyo limekuwa na utaratibu wa kutembelea vijiji husika na kutoa elimu juu ya umuhimu wa miundombinu hiyo kwa Taifa na namna ya kung’amua hatari na kutoa taarifa kwa mamlaka husika. 

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara na wanakijiji wa Somanga Simu, Afisa Uhusiano wa TPDC, Ndg. Malik Munisi alisema “TPDC inatambua mchango wa kizalendo unaotolewa na wakazi wa maeneo bomba la gesi linapopita, inatambua kwamba mlinzi wa kwanza wa miundombinu hii ni mwananchi na hivyo tutaendelea kushirikiana nanyi kila wakati kuhakikisha miundombinu hii inaendelea kuwa salama na kudumu kwa kipindi kirefu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho”. 

Nae Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka TPDC, Ndg. Oscar Mwakasege alieleza namna ambavyo TPDC hujihusisha na dhana ya uwajibikaji kwa jamii (Corporate Social Responsibility-CSR) na kusisitiza kwamba maeneo ya kipaumbele katika kuwajibika kwa jamii ni masuala yahusuyo afya, elimu, maji na michezo. 
Wananchi wa Kijiji cha Somanga Simu wakiwa katika mkutano wa hadhara kusikiliza masuala yahusuyo usalama na ulinzi wa bomba la gesi yaliyokuwa yakizungumzwa na wataalamu kutoka TPDC .
Wananchi wa Kijiji cha Kiwanga wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka TPDC baada ya kupata elimu kuhusu masuala ya usalama na ulinzi wa miundombinu ya gesi asilia. 

BENKI KUU KUHAKIKI WAFANYAKAZI WA BENKI ZOTE NCHINI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inatarajia kufanya uchambuzi na kuwakagua wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika benki zote nchini.

Hayo yamesemwa na Gavana wa Benki Kuu Profesa Florens Luoga wakati akifunga semina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi iliyoandaliwa na BoT Mjini Dodoma Profesa Luoga amesema uamuzi huo unalenga kulinda fedha za wananchi ambazo wameweka benki pamoja na kuondoa wafanyakazi wasio waaminifu.

"Benki Kuu tunao mkakati wa kuhakikisha tunafanya ukaguzi ambao lengo lake litakuwa kuhakikisha wanapatikana wafanyakazi waliowaamini na wenye uwezo wa kulinda fedha za wateja.Tunahitaji kuona wafanyakazi wa benki ambao wanatambua na kuheshimu misingi ya kaziza benki,"amesema Profesa Luoga na kuongeza ni muhimu kwa BoT kulinda za wateja.

Amefafanua siku za nyuma kulikuwa na baadhi ya fedha za wateja wadogo zilizohifadhiwa kwenye baadhi ya benki, ziliibwa kwa ujanja na wafanyakazi wa benki hizo jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Ameongeza kiongozi mzuri wa benki lazima awe mwaminifu na ndio maana BoT wanataka kuhakiki wafanyakazi wa benki zote nchini.

Amefafanua huu ni wakati wa kuwa na wafanyakazi wa benki amabo ni sahihi kwa kazi hiyo, hivyo kupitia uchambuz wa kina ambao utafanyika watabaini wafanyakazi waliopo na uwezo wao na waamini kazini.

Profesa Luoga ameeleza namna ambavyo kuna baadhi ya wateja wa benki ambao si waaminifu walivyokuwa wanatengeneza mazingira ya kujipatia fedha ambapo walikuwa tayari kutafuta watu na kuwajazia fomu na kisha kuwapatia mkopo.

"Anakuja mfanyakazi wa benki fulani anakwambia fungua akaunti ili upate mkopo, baadae anakupa mkopo wa Sh.milioni 50 halafu yeye anachukua Sh.milioni 20 na kukuachia Sh.milioni 30.Lazima ifike wakati tuwe na wafanyakazi waamini katika sekta ya kibenki,"amesema. Amesema BoT imejipanga kwa kila hali kuhakikisha inalinda haki za wateja ikiwamo kulinda fedha zao kwenye benki huku akieleza kuwa wanataka huduma za kifedha zimfikie mwananchi kila mahali na bila kikwazo.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Profesa Florens Luoga akizungumza na waandishi wa habari za fedha na uchumi wakati akifunga mafunzo yaliyoandaliwa na BoT kwa waandishi hao
 Mtunza Muda katika mafunzo ya semina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi Bakari Kimwanga(aliyesimama) akitoa shukrani kwa Gavana wa BoT pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo kwa kuandaa mafunzo ya habari za fedha na uchumi
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga akiwa ameshikana mkono na Mwakilishi wa Michuzi Blog Said Mwishehe baada ya kufunga mafunzo ya uandishi wa habari za fedha na uchumi iliyofanyika BoT tawi la Dodoma.Wanaoshuhudia ni sehemu ya maofisa wa benki hiyo na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini

VOA SWAHILI: Duniani Leo December 14th, 2018

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images