Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

WAZIRI KALEMANI AKEMEA KASI DUNI YA MKANDARASI UYUI

0
0
Na Veronica Simba – Tabora
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amekemea kasi duni ya Mkandarasi anayetekeleza mradi wa umeme vijijini wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora na kumtaka ndani ya siku 30 awe ameunganisha umeme vijiji vingine vipya 15. Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ibili wilayani humo, Desemba 14, 2018, alipokuwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme, Waziri Kalemani alimwagiza Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wa eneo hilo kumwandikia barua ya onyo la kukusudia kusitisha mkataba Mkandarasi husika endapo atashindwa kutekeleza agizo alilompa.

“Na siyo kusitisha tu; tukisitisha mkataba maana yake hatutakupatia kazi tena na tutakudai malipo ambayo tumekwishakulipa na hata kukupeleka mahakamani. Nataka kasi iongezeke maradufu,” alisisitiza Waziri. Aidha, Waziri aliwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kulipia gharama ya kuunganishiwa umeme ambayo ni shilingi 27,000 tu kwa kuwa ni huduma inayotolewa kupitia Mradi wa Umeme Vijijini (REA) huku akiwatahadharisha kuwa muda wa kutekeleza mradi huo ukipita watalazimika kulipia gharama kubwa zaidi.

Vilevile, aliwataka pindi wakishaunganishiwa umeme, wautumie kwa malengo ya kukuza vipato vyao na kuboresha maisha ikiwemo kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya kuchakata mazao wanayolima ambayo ni karanga, pamba na tumbaku. Pia, aliwataka viongozi wa taasisi zinazotoa huduma kwa umma kama shule, vituo vya afya, masoko, polisi, mitambo ya maji, makanisa, misikiti, kutenga pesa na kulipia kiwango hicho cha shilingi 27,000 tu ili kuhakikisha taasisi zao zinaunganishiwa umeme hivyo kutoa huduma bora kwa wananchi.

 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati) akikata utepe kabla ya kuwasha rasmi umeme katika nyumba ya mkazi wa kijiji cha Ibili wilayani Uyui, Mama Chausiku (mwenye fulana ya njano), Desemba 14, 2018. Kulia kwa Waziri ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Gift Msuya na wa kwanza kulia ni Mbunge wa Tabora Kaskazini, Almasi Maige.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia), akimpongeza Mama Chausiku (mwenye fulana ya njano), baada ya kuwasha rasmi umeme katika nyumba yake (inayoonekana pichani), akiwa katika ziara ya kazi kijijini Ibili, Wilaya ya Uyui, Desemba 14, 2018.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Gift Msuya (aliyesimama), akimkaribisha Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (anayesaini kitabu) mkoani Tabora alipofika kwa ajili ya ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme, Desemba 14, 2018.
 Mbunge wa Tabora Kaskazini, Almasi Maige, akimkaribisha Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (wa kwanza kulia-walioketi) mkoani Tabora alipofika kwa ajili ya ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme, Desemba 14, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WANAFUNZI 12,399 WACHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2019 AWAMU YA KWANZA SIMIYU

0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Jumla ya Wanafunzi 12,399 mkoani Simiyu wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 katika shule za Serikali za kutwa na bweni kwa awamu ya kwanza. Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini Desemba 14, 2019 wakati akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa Kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 Mjini Bariadi.

Sagini amesema jumla ya wanafunzi waliofaulu Mtihani wa Darasa la Saba ni 24,983 sawa na asilimia70.68 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani, ambapo amebainisha kuwa wanafunzi 12, 584 kati ya 24,983 waliofaulu hawajachaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa miundombinu ya elimu.

Sagini amesema lengo la Serikalini kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanaenda sekondari hivyo, amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani Simiyu kuhakikisha kuwa wanafanya jitihada katika ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu, ili wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba waweze kuanza kidato cha kwanza kwa wakati.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019, Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
  Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akitoa taarifa ya hali ya ufaulu katika Mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka 2018, katika kikao cha uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019 kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
 Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa,Mhe. Paul Maige  wakifuatilia kwa makini nyaraka zenye taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019, katika kikao kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kikao hicho na Katbu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifungua kikao hicho  Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Baadhi ya waandishi wa habari na wajumbe wa Kikao cha uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kikao hicho na Katbu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifungua kikao hicho  Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Mhagama:Taasisi za serikali na binafsi zatakiwa kujisajili OSHA

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI imeagiza amezitaka taasisi zote za na binafsi kuhakikisha  wanajisajili kupitia   Wakala Afya, Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) ili kutekeleza matakwa ya sheria. Hayo ameyasema Waziri  wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Kazi Vijana na Ajira Jenista Mhagama alipowatembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa OSHA na kuangalia utendaji wao wa kazi katika kusimamia masuala aya usalama mahala pa kazi

Amesema uwepo wa taasisi ya OSHA ni muhimu kwa kuwa inalenga  kuondoa dosari za aina mbalimbali hususani  madhara  katika maeneo ya kazi ambapo bila kufanya hivyo wafanyakazi wangekuwa waadhirika wakubwa katika sehemu za kazi zao.

“Taasisi zote na kampuni kujisajili na OSHA ili ziweze kufanya kazi kwa utaratibu wa kisheria, hii aina maana ina faida kwa Serikali, bali ni  faida kwa   taasisi , wafanyakazi wote kwa kuwa zaidi imelenga kuhakikisha inaondoa mazingira yote hatarishi ambayo pengine yangeweza kuleta madhara mahala Pa kazi ” amesema Mhagama.
Waziri  wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Kazi Vijana na Ajira Jenista Mhagama akizungumza na wafanyakazi wa Dawasa walioko katika mafunzo ya Ukimwi yanayoendeshwa  na Wakala Afya, Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) wakati alipotembela ofisi za OSHA jijini Dar es Salaam.
Kaimu  Mtendaji Mkuu wa OSHA Hajida Mwenda akizungumza na waandishi habari kuhusiana na usimamizi wafanyakazi mahala pa kazi katika utoaji wa elimu wakati Waziri  wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Kazi Vijana na Ajira Jenista Mhagama alipotembelea ofisi za OSHA jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Dawasa wakiwa katika mafunzo ya UKIMWI yanayoendeshwa na OSHA jijini Dar es Salaam.
afanyakazi wakiwa katika mkutano na Waziri  wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Kazi Vijana na Ajira Jenista Mhagama alipotembelea ofisi za OSHA jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

VIJANA WANAOHITIMU VYUO WATAKIWA KUZITUMIA FEDHA ZINAZOTENGWA NA HALMASHARI KUJIONGEZEA KIPATO

0
0
Na Josephine Majura na Peter Haule WFM- Mwanza
Serikali imewataka wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini kuhakikisha wanatumia fursa ya uwepo wa fedha zinazotengwa na Halmashauri katika Wilaya zote nchini kila mwaka kwa ajili ya kuwawezesha vijana na wanawake kiuchumi.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu, kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Philip Isdor Mpango, wakati wa Mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza.

Dkt. Kazungu alisema kuwa, Halmashauri zote nchini hutenga asilimia tano ya mapato yake ya ndani kila mwaka ili kuwawezesha vijana na wanawake kutumia fedha hizo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo na kuwataka wahitimu wa vyuo ambao hawana ajira katika Sekta rasmi, waanzishe vikundi vya umoja wa uzalishaji mali ikiwa ni moja ya kigezo cha kuweza kupata fedha hizo.

“Serikali ya Awamu ya Tano imejidhatiti kuwaletea wananchi maendeleo endelevu kwa kuhakikisha kila mtu kwa nafasi yake anafanya kazi uzalendo, uadilifu,  bidii na maarifa lakini pia kudumisha amani na mshikamano ili kuwa na maendeleo endelevu kwa manufaa ya kizazi hiki na  kijacho.”alisema Dkt. Kazungu.
 Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), Prof. Hozen Mayaya, akiishukuru Serikali kwa kuboresha Sekta ya huduma za jamii wakati wa mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza ikiwa ni mahafali ya sita kufanyika katika Chuo hicho.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza, akiwataka wahitimu hao (hawapo pichani) kuchangamkia fursa zilizopo katika  mtengamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kupata ajira kwa kuwa wanavigezo vya ushindani wa ndani na nje ya nchi.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu, akimtunuku mmoja wa wahitimu wa ngazi ya Stashahada za Uzamili wakati wa mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza.
 Wahitimu wa ngazi ya Stashahada za Uzamili wakiwa tayari kutunukiwa vyeti wakati wa mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza.
 Baadhi ya wahitimu wa stashahada wakipunga kofia kwa furaha baada ya kutunukiwa vyeti vya kuhitimu wakati wa mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wahitimu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza. (Picha na Josephine Majura, Wizara ya Fedha na Mipango)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KATIBU MKUU DOTO:SERIKLI INATAMBUA MCHANGO WA TIA

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI imesema kuwa inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)katika kuandaa watalaam wa Tasnia ya Uhasibu, Ununuzi na Ugavi Biashara pamoja na uongozi wa Rasilimali Watu.

Hayo ameyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James wakati alipomwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango  katika mahafali ya 16 ya Taasisi Uhasibu Tanzania  kwa Kampasi za Dar es Salaam pamoja na  Mtwara yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hio jijini Dar es Salaam.

James amesema kuwa serikali itaendelea kuunga mkono pamoja na taasisi kutekeleza majukumu kwa weledi katika kubuni mbinu mpya za  kuimarisha mapambano ya kupata mafanikio makubwa.
Amesema Taasisi hiyo iendelee kubuni mbinu kujitangaza zaidi na kujiuza kwa bidhaa wanazozitoa kwa ndani na nje nchi katika ili  kuongeza  wanachuo zaidi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza katika mahafali ya 16 ya Taasisi Uhasibu Tanzania (TIA)  kwa Kampasi za Dar es Salaam pamoja na  Mtwara yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hio jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa TIA, Wakili Said Chiguma akizungumza kuhusiana na hali ya uendeshaji wa Taasisi hiyo katika mahafali ya 16 ya Taasisi Uhasibu Tanzania (TIA)  kwa Kampasi za Dar es Salaam pamoja na  Mtwara yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hio jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)Dkt. Joseph Kihanda akizungumza historia ya taasisi hiyo mahafali ya 16 ya Taasisi Uhasibu Tanzania (TIA)  kwa Kampasi za Dar es Salaam pamoja na  Mtwara yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hio jijini Dar es Salaam
Wahitimu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania  (TIA) katika  mahafali ya 16 ya Taasisi hiyo   kwa Kampasi za Dar es Salaam pamoja na  Mtwara yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hio jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wakicheza muziki baada ya kutunukiwa shahada mbalimbali zinazotolewa na Taasisi ya Uhasibu Tanzania  (TIA)katika katika  mahafali ya 16 ya Taasisi hiyo   kwa Kampasi za Dar es Salaam pamoja na  Mtwara yaliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hio jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU AZINDUA TANZANIA SAFARI CHANNEL

0
0
*Awataka waliopewa dhamana wazingatie viwango vya kimataifa
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezinduaChaneli ya Taifa ya Utalii iitwayo Tanzania Safari Channel na amewataka watu wote waliopewa dhamana ya kuiendesha wahakikishe wanazingatia viwango vya kimataifa katika vipindi watakavyokuwa wanaviandaa. “Vipindi vyenu ni lazima vivutie kama vile tunavyoviangalia katika chaneli za wanyama za kimataifa kama vile National Geographic, Discovery, Travel na zingine ili lengo lililokusudiwa wakati wa kuanzishwa kwake litime.”


Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Desemba 15) wakati akizindua chaneli hiyo kwenye Ofisi za TBC, Mikocheni, jijini Dar es Salaam, ambapo ametoa wito kwa Wizara zote zinazohusika na uanzishwaji wa Chaneli hiyo kuhakikisha zinailea wakati ikijijenga kujiendesha kibiashara.

Amesema Tanzania ni moja ya nchi duniani zilizotenga moja ya tatu ya eneo lote la nchi kwa ajili ya uhifadhi, ambapo kuna tamaduni za makabila mbalimbali, ngoma za kuvutia, vyakula vya asili, sinema za maisha yetu na lugha adhimu ya Kiswahili.

“Hivyo, kwa kuanzishwa kwa chaneli hii inayotengeneza vipindi na kuonesha vivutio hivi ndani na nje ya Tanzania itasaidia watalii huko waliko kujua huu utajiri wetu na kuchagua kuja kutalii nchini. Ni matumaini yangu kuwa hii Tanzania Safari Channel ninayoizindua leo itaongeza thamani katika kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea Tanzania.”

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Chaneli ya Tanzania Safari Channel kwenye  Viwanja vya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jijini Dar es salaam Desemba 15, 2018.  Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Ryoba. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Chaneli ya Tanzania Safari Channel kwenye  Viwanja vya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jijini Dar es salaam Desemba 15, 2018.  Kushoto ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, wapili kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Ryoba. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Upendo Mbele wakati alipotembelea Studio mpya za TBC kabla ya kuzindua chaneli ya Tanzania Safari Channel, Desemba 15, 2018. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC,  Dkt. Ayoub Ryoba.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Chaneli ya  Tanzania Safari Channel kwenye viwanja vya Ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Mikocheni jijini Der es slaaam, Desemba 15, 2018. 
 Baadhi ya viongozi na wageni waalikwa wakimsikiliza Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa wakati alipozindua Chaneli ya Tanzania Safari Channel kwenye viwanja vya Ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jijini Dar es salaam, Desemba 15, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) baada ya kuzindua Chaneli ya Tanzania Safari Chanmnel Kwenye viwanja vya TBC,  Mikocheni jijini Dar es salam, Desemba 15, 2018. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN, AWAAPISHA WAJUMBE WAPYA WA KAMISHENI YA UTUMISHI WA UMMA ZANZIBAR

0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimwapisha Mjumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma  Zanzibar, Dkt. Mohammed Sheikh Khatib, hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Zanzibar,15-12-2018
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisaini Hati ya Kiapo ya Mjumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar,Dkt. Mohammed Seif  Khatib baada ya kiapo, hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Zanzibar.15-12-2018.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mjumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar,Ndg. Mbaraka Mohammed Abdulwakil, hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar leo,15-12-2018.
 RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi hati ya Kiapo Mjumbe Mpya wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar Ndg. Mbaraka Mohammed Abdulwakil, hafla hiyo imefanyika Zanzibar leo,15-12-2018. 
 BAADHI YA Wakuu wa Wilaya na Viongozi wa SMZ wakihudhuria Hafla ya kuapishwa kwa Wajumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar, iliofanyika Ikulu Zanzibar leo,15-12-2018.
 MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, akiwa na Viongozi wengine wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Wajumbe Wapya wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.leo 15-12-2018.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar, baada ya kuwaapiosha leo Ikulu Zanzibar,kulia Dkt. Mohammed Sheif Khatib na kushoto Ndg. Mbaraka Mohammed Abdulwakil.(Picha na Ikulu) 

Picha mbalimbali katika ukaguzi wa mabasi katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo

0
0
 Mkurugenzi wa Barabara wa Mamlaka ya Usafiri wa nchi Kavu na Majini (Sumatra) Johansen Kahatano akizungumza na Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Ibrahimu Samwix wakati  ukaguzi wa mabasi ya mikoani na nchi jirani katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Barabara wa Mamlaka ya Usafiri wa nchi Kavu na Majini (Sumatra) Johansen Kahatano akipata maelezo kwa Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Ibrahimu Samwix wakati  ukaguzi wa mabasi ya mikoani na nchi jirani katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Ibrahim Samwix wakiwa katika ukaguzi wa mabasi ya mikoani na nchi jirani katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Ibrahim Samwix akiwa katika uvungu basi wakati akifanya ukaguzi wa mabasi ya mikoani na nchi jirani katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Dereva akipata maelekezo na askari aliyechini ya uvungu ya basi wakati akifanyiwa ukaguzi wa mabasi ya mikoani na nchi jirani katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Grant Pawa akimpa maelekezo fundi wa basi wakati akifanyiwa ukaguzi katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nuru Seif akimpa maelekezo fundi wa basi wakati akifanyiwa ukaguzi wa basi atika kituo kikuu cha katika mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.( Picha zote na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii)

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA NNE LA KIMATAIFA LA KISWAHILI-ZANZIBAR LEO

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameitaka Jamii kubadili fikra kwa kuchunguza na kufikiria jinsi ya kutumia vipengele mbalimbali vya lugha ya Kiswahili na Utamaduni wake kama bidhaa ya biashara.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama Cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) na kuratibiwa na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA). “Sote ni mashahidi wa namna lugha ya Kiswahili imeendelea kukua kwa kasi na kuwa si lugha tena bali ni bidhaa yenye tija katika soko la utandawazi” alisema Makamu wa Rais.

Kaulimbiu ya Kongamano hilo la siku mbili inayosema KISWAHILI CHETU UMOJA WETU KWA MAENDELEO YETU limehudhuriwa na wadau na wataalamu kutoka Mataifa ya Uingereza, Poland, Marekani, Misri, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Pakistan Ujerumani na Austria. Makamu wa Rais ameipongeza CHAKIDU kwa kuhakikisha Kiswahili hakimezwi na lugha za kigeni na kukifanya kiendelee kukita mizizi kwa kusambaa maeneo mbalimbali.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kampasi ya Vuga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 
 Sehemu ya Wadau na Wataalamu wa Kiswahili waliohudhuria  ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kampasi ya Vuga. 
Watoto wa Skuli ya Kisiwandui wakipendezesha Kongamano kwa kuimba nyimbo ya Mwanandege wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kampasi ya Vuga.
 Baadhi ya Vitabu mbalimbali vilivyoonyeshwa leo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kampasi ya Vuga.  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

HATUNA MPANGO WA KUTOA SARAFU MPYA-PROFESA LUOGA

0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga amesema hawaoni sababu ya kubalisha sarafu na kwamba zilizopo zinatosha na wanataka ziwe nyingi zaidi kwa lengo la kuhakikisha noti zilizopo zinatumika kwa muda mrefu.

Profesa Florens ametoa kauli hiyo leo Mjini Dodoma wakati anajibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari za fedha na uchumi kabla ya kufunga semina ya mafunzo ya uandishi wa habari zinazohusu fedha na uchumi iliyoandaliwa na BoT.

Ambapo waandishi walitaka kufahamu kama Tanzania nayo itabadili sarafu yake kama ambavyo nchi ya Kenye imefanya kwa kutoa sarafu mpya ambapo amesema hakuna mpango huo kwa sasa."Tanzania tuna sarafu za kutosha na tunataka ziwe nyingi zaidi ili zitumike kwa wingi na lengo ni kuona noti zetu zinaishi muda mrefu zaidi.Kuhusu Kenya na uamuzi wa kubadili sarafu yao ni uamuzi wao na hauna tatizo kwenye uchumi wetu," amesema.

Hata hivyo amesema wakati Kenya imeamua kufanya uamuzi wa kutoa sarafu mpya tayari Jumuiya ya Afrika Mashariki imeshapitisha sheria ya Benki ya Afrika Mashariki na ifikapo mwaka 2024 nchi wanachama zinatakiwa kuwa na sarafu moja.Pia ametumia nafasi hiyo kuzungumzia ubora wa noti ya Tanzania ambayo asilimia 100 inatengenezwa kwa pamba , hivyo kuifanya kuwa imara zaidi kuliko Dola."Noti yetu ni imara sana na ukiwambia watu uimara wake ni zaidi ya Dola wanaweza wasiamini."
 Gavana wa  Benki Kuu Profesa Florens Luoga akifafanua jambo wakati anazungumza na waandishi wa habari za fedha na uchumi ambapo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia sarafu ya Tanzania
 Mkurugenzi wa BoT tawi la Dodoma Richard Wambali akitoa neno la shukrani kwa Gavana wa BoT Profesa Florens  Luoga kabla ya kufunga mafunzo ya habari za fedha na uchumi kwa waandishi wa habari
Meneja wa Idara ya Uhusiano kwa umma na Itifaki kutoka BoT Zaria Mbeo akitoa majumuisho ya mafunzo ya habari za fedha na uchumi kwa Gavana BoT Profesa Florens Luoga

ULEGA AENDELEA KUTATUA MIGOGORO MALALAMIKO YA WAFUGAJI KATIKA MKOA WA MOROGORO

0
0

Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amefanya ziara mkoani Morogoro katika Wilaya za Kilombero na Malinyi ili kutatua migogoro na malalamiko ya wafugaji.

 Katika Wilaya za Kilombero na Malinyi  Ulega aliwataka wafugaji waliopo katika bonde la mto Kilombero kuondoka na kwenda kwenye maeneo waliyotengewa ili kuepusha madhara kwa mto huo ambao ndiyo chanzo muhimu cha maji ya mto Rufiji. 

Ulega alisema wafugaji hao wanapeleka mifugo hiyo bonde la mto Kilombero kufuata maji na kuagiza Halmashauri za Kilombero na Malinyi kutengeneza mabirika ya kunyweshea maji mifugo ili wafugaji wasiende kufuata maji katika bonde hilo. Aidha, aliwataka TAWA kushirikiana na Halmashauri za Kilombero na Malinyi kutengeza mabirika hayo ambapo moja ni takribani Sh. milioni 20 (birika milioni 5 na kisima Sh.milioni 15).

Pia wafugaji wa maeneo hayo walikiri kutokwenda bonde la mto Kilombero wakitengenezewa miundombinu ya mifugo hasa maji katika maeneo yao.
Ulega amesisitiza umuhimu wa kutunzwa maeneo hayo oevu ili kutunza mto Kilombero kwa lengo la kuendelee kupata maji mengi katika mto Rufiji itakayosaidia kufanikisha agenda ya Rais Dkt. John Magufuli ya mradi wa Stieglers Gorge.

Aidha,  Ulega aliwaagiza Wakala wa Mafunzo na Elimu ya Mifugo (LITA) kuandaa mafunzo ya mda mfupi kwa ajili ya wafugaji hao ili waweze kufuga kisasa wawe na mifugo wenye tija. Pia, aliwataka Serikali ya kijiji kuheshimu mipango ya matumizi bora ya ardhi iliyopo ili kuepusha migogoro.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega(wambele)akiwa ameambatana na viongozi wa wilaya Malinyi mkoa wa Morogoro wakati wakiwasili kwenye kijiji cha Ngombo,wakati wa ziara yake ya kuzisikiliza kero migogoro mbalimbali ya wafungaji,wavuvi na kuzitafutia ufumbuzi.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ngombo wilaya ya Malinyi mkoa wa Morogoro,katika mkutano wa hadhara wa  kusikiliza kero mbalimbali za wafugaji,wavuvi  na kuzitatua.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega wapili (kushoto) akiwa ameambatana na viongozi wa wilaya Malinyi mkoa wa Morogoro wakiwasili katika kijiji cha Ngombo kwenye ziara yake ya kuzisikiliza kero na migogoro mbalimbali ya wafungaji,wafungaji na kuzitatua.

HASUNGA AAGIZA WALIOKOPA SACCOS KULIPA MADENI HAYO NDANI YA MIAKA MITATU

0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameagiza kurejeshwa ndani ya miezi mitatu madeni yote yaliyokopwa kwenye vyama vya akiba na mikopo (SACCOS).

Alisema kuwa mwananchi watakaoshindwa kutii maelekezo hayo katika kukamilisha deni lake ndani ya miezi mitatu hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.“ Nataka kila aliyekopa kwenye Saccos arejeshe deni lake kwa kufuata utaratibu wa makubaliano na kama wasipotekeleza ndani ya miezi mitatu niliyotoa serikali itaagiza wahusika wote kukamatwa maana dawa ya deni ni kulipa” Alisisitiza

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ametoa agizo hilo tarehe 14 Disemba 2018 wakati wa kikao cha kazi katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara alipokuwa akizungumza na viongozi wakuu wa vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) sambamba na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Kaimu Mrajisi wa vyama vya Ushirika nchini, Mkaguzi wa vyama vya ushirika na Saccos, Kaimu Mrajisi msaidizi wa mkoa wa Mtwara, Wenyeviti na watendaji wa SACCOS pamoja na vyama vya msingi vya ushirika vilivyopo mkoani Mtwara. 

Mhe Hasunga amelitaka Shirika la Ukaguzi wa Hesabu za Vyama vya Ushirika (COASCO) kutimiza majukumu yake kwa weledi kwa kukagua na kuhakikisha vyama vyote vinafunga mahesabu huku akitaka vyama ambavyo sio hai kuchukuliwa hatua.Pia ameagiza kila chama Tanzania kiwe na daftari la wanachama walio hai na wafu sambamba na kuhakikisha kuwa viongozi wote wawe na maadili na uwezo wa kuvisimamia vyama vyao ipasavyo.

Katika hatua nyingine alimtaka Mrajis wa ushirika Tanzania Bw Tito Haule kuwasilisha mpango kazi wa namna ya kukutana na wanachama wa ushirika nchi nzima katika kutatua changamoto zao. “ Na ni lazima taarifa itengenezwe ikionyesha idadi ya vyama mlivyokutana navyo na kueleza ni mambo gani mmezungumza kila mwezi” Alisema

Aliongeza kuwa Viongozi ni lazima kutoa mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya Ushirika itakayosaidia kuondoa usumbufu kwenye ushirika ili uendelee kuwa mkombozi wa wananchi. “Mje na mfumo wa namna ya kuwasaidia wananchi kupata pembejeo bila kuingia madeni yasiyokuwa na tija” Alisisitiza
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi alipokuwa akizungumza na viongozi wakuu wa vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) sambamba na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, tarehe 14 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Viongozi wakuu wa vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) sambamba na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, tarehe 14 Disemba 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi alipokuwa akizungumza na viongozi wakuu wa vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) sambamba na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopo katika Mkoa wa Mtwara katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, tarehe 14 Disemba 2018.



WANAOIHUJUMU ATCL SASA KUFUATILIWA KWA KARIBU.

0
0
Na John Nditi, Morogoro
NAIBU waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Atashasta Nditiye ameiagiza Baraza la Wafanyakazi  la Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) pamoja na   Menejimenti ya  Kampuni  kuimarisha kitengo cha masoko na kufanya ufuatiliaji  kwa watumishi  na mawakala wanaoihujumu Kampuni  hiyo.
Naibu Waziri alisema hayo  katika hotuba yake ya   ufunguzi wa kikao cha tatu cha  baraza la wafanyakazi wa ATCL lililofanyika  mjini Morogoro.
 Alisema , kwa muda mrefu kumekuwa na  manenoo mengi yanayosemwa juu ya kuwepo hujuma dhidi ya  Ndege za ATCL   hasa kwenye  njia  ya Kilimanjaro na Mbeya .Mbali na njia hizo pia huduma hizo zinafanywa kwa maeneo mengine ambapo wateja wanapohitaji huduma za  ATCL huambiwa kuwa ndege zimejaa wakati  jambo hilo si kweli na matokeo yake ndege zinaondoka bila kujaa abiria.
“ Baadhi ya makawala wanaouza tiketi za ATCL wanaonwa na makampuni mengine ya Ndege  ili wajaze kwanza ndege  zao kwa kutoa maelezo kwa wateja wanaohitaji kusafiri na ndege zetu za umma kuwa zimejaa , lakini baadaye zinaondoka bila kujaa abiria” alisema Naibu Waziri Nditiye.
Naibu Waziri huyo alisema “ Huduma za ndege zetu ni nzuri  na nauli yake ni ndogo  na pia ndege zetu zote ni mpya lakini hazijai  tofauti na za makampuni binafsi ambayo bei zake ni za juu na huduma zao hazifanani na za ATCL “ alisema Naibu Waziri Nditiye .
 Naibu waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Atashasta Nditiye ( kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi mkuu wa ATCL,  Ladislaus Matindi  ( wa pili kushoto ) baada ya Naibu Waziri kufungua   kikao cha tatu cha  baraza la wafanyakazi wa ATCL lililofanyika  mjini Morogoro.
 Naibu waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandisi Atashasta Nditiye ( kulia ) akijadiliana jambo  na  Mkurugenzi mkuu wa ATCL,  Ladislaus Matindi  (  kushoto ) kwa ajili ya kufungua  kikao cha tatu cha  baraza la wafanyakazi wa ATCL kilichofanyika  mjini Morogoro.
 Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa ATCL wakimsilikiza  Naibu waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Atashasta Nditiye (  hayupo pichani ) alipofungua  kikao cha tatu cha  baraza  hilo  mjini Morogoro.

MGALU AIAGIZA TANESCO KUFIKISHA UMEME VITUO 300 VYA AFYA NCHINI

0
0
VICTOR MASANGU, KIBAHA 

NAIBU waziri wa nishati Subira Mgalu katika kuumga mkono Juhudi za Rais Dk . John Pombe Magufuli ya kuboresha sekta ya afya hapa nchini ameliagiza Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha wanapeleka miundombinu ya nishati ya umeme haraka iwezekanavyo katika maeneo ya vituo vipya vya afya 300 pamoja na hospitali 69 ambazo zinajengwa na serikali kwa lengo la kuboresha huduma ya matibabu kwa wananchi wake.

Mgalu ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu kupitia Mkoa wa Pwani alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopo katika halmashauri ya mji Kibaha pamoja na kukagua mwenendo wa ujenzi wa upanuzi katika kituo cha afya mkoani kilichopo Wilayani Kibaha.

“Kwa kweli nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inafikisha kwa haraka miundombinu ya umeme katika vituo vipya vya afya ambavyo vinajengwa pamoja na hospitali hivyo nachukua nafasi hii kuwaagiza Tanesco pamoja na REA kufikisha umeme haraka iwezekanavyo katika maeneo hayo ili wananchi waweze kupata huduma ya afya katika mazingira ambayo ni rafiki kwao na katika hili tunamshukuru sana Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli,”alisema Mgalu.

Aidha alibainisha kwamba kwa sasa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inaboresha miundombinu ya umeme katika maeneo mbali mbali ili zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali ziweze kupata nishati ya umeme wa uhakika ambao utasaidia kuboresha zaidi katika utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi wa Tanzania ambao hapo awali walikuwa wanateseka.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa halmashauri ya mji Kibaha Tulitweni Mwinuka alisema kwamba wamepokea kiasi cha shilingi milioni 500 kutoka serikali kuu kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho cha afya mkoani katika maeneo ya wodi ya wazazi,jengo la mionzi jengo maalumu kwa ajili ya kufulia pamoja na jengo la upasuaji ambapo kukamilika kwake kutaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya mlundikano kwa wagonjwa.

Nao baadhi ya wanawake Wilayani Kibaha Elina Mngonja na Selina Wilsoni wamemshukuru Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kuboresha sekta ya afya hapa nchni ambapo wamesema kukamilika kwa upanuzi wa kituo hicho hasa katika wodi za kinamama wajawazito utakuwa ni mkombozi mkubwa katika suala zima la utoaji wa huduma hasa wakati wanapokwenda kujifungua.
  Mganga mkuu wa halmashauri ya mji Kibaha Tulitweni Mwinuka kushoto akimwonyesha ujenzi unavyoendelea  wa mradi wa upanuzi wa kituo cha afya cha Mkoani kilichopo Wilayani Kibaha, Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu kulia kwake ambaye alifanya ziara kwa ajili ya kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo.(PICHA NA VICTOR MASANGU). 
  Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu kulia akipokea taarifa ya ujenzi wa upanuzi wa kituo cha afya mkoano kutoka kwa Mganga mkuu wa halmashauri ya mjini Kibaha Tulitweni Mwinuka.
 Naibu Waziri wa nishati Subira Mgalu kulia akiangalia mwenendo wa upanuzi wa ujenzi wa kituo cha afya mkoani kushoto kwake ni Mganga mkuu wa halmasshauri ya mji Kibaha

RAIS WA ZANZIBAR AZUNGUMZA NA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA LEO IKULU ZANZIBAR.

0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Wilaya Zanzibar Ikulu Zanzibar, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na kulia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Wilaya ya Zanzibar , mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, leo.15/12/2018.kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu)

TAARIFA YA HABARI YA ITV SAA MBILI USIKU DESEMBA 15,2018

ULEGA AMPA MWEZI MMOJA MKURUGENZI HALMASHAURI WILAYA YA BABATI KUANDAA MIUNDOMBINU YA WAFUGAJI

0
0

Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamiii

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega amempa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara mwezi mmoja wa kuandaa miundombinu ya wafugaji wa vijiji,Vilima Vitatu,Minjingu waliohamishwa katika hifadhi ya wanyamapori ya Burunge.

Ulega amesema Mkurugenzi huyo Hamis Malinga anapaswa kuandaa miundombinu hiyo ya wafugaji ili wakiondolewa kwenye hifadhi ya jamii ya Burunge waweze kuhamia Mfulang'ombe kwenye eneo lililojengwa.

Amesema wafugaji hao wanapaswa kuwekewa miundombinu rafiki ikiwemo malambo na majosho ili waweze kuanza maisha mapya ya ufugaji. Amesema wafugaji hao walikuwa wanalalamikia kuondolewa kwenye eneo hilo na kupelekwa sehemu nyingine ambayo haina miundombinu rafiki.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Babati, Hamis Malinga amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa wapo kwenye mchakato wa kuandaa miundombinu rafiki ya wafugaji hao. "Kila mfugaji atapatiwa ekari tatu kwa ajili ya kuhakikisha anazimiliki na tutaandaa malambo na majosho kwa ajili ya mifugo ya hizo kaya 17 zilizoondolewa kwenye hifadhi," amesema.

Kwa muda mrefu kaya 17 za wafugaji wa jamii ya kifugaji ya wabarbaig waliamriwa kuondoka kwenye eneo hilo lakini waligoma.

Eneo la jamii la hifadhi ya wanyamapori Burunge lenye ukubwa wa kilomita za mraba 283 linaundwa na vijiji 10 vya Sangaiwe, Mwada, Ngoley, Vilima Vitatu, Minjingu, Kakoi, Olasiti, Manyara, Magara na Maweni. 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Minjingu na Vilima Vitatu wilaya ya Babati mkoani Manyara ,katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero mbalimbali za wafugaji,wavuvi na kuzitafutia ufumbuzi .
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Babati mkoa Manyara wakiangalia hifadhi ya jamii ya Burunge.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwasikiliza wafugaji wa wilaya ya Babati mkoa Manyara walipokuwa wakiwasilisha changamoto zao.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na watumishi wa mkoa wa Manyara katika ziara yake ya kusikiliza kero mbalimbali za wafugaji na wavuvi na kuzitafutia ufumbusi.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

KAULIMBIU YA HAPA KAZI TU KATIKA UTUMISHI WA UMMA ITEKELEZWE KWA VITENDO KUPITIA USIMAMIZI NA UTEKELEZAJI MZURI WA OPRAS

0
0



Watendaji Wakuu katika Taasisi za Umma nchini wametakiwa kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya HAPA KAZI TU ya Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kuhakikisha wanasimamia vizuri utekelezaji wa Mfumo wa  Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) wa mtumishi mmoja mmoja ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi kwa maslahi ya maendeleo ya taifa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa alipoitembelea Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini ya Ofisi yake kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, usimamizi na utekelezaji mzuri wa Mfumo wa  Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) utaondoa tatizo la ufanyaji kazi wa mazoea kwa baadhi ya watumishi wa umma nchini na kuongeza kuwa, utawezesha kufikia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga utamaduni wa kila mtumishi wa umma katika nafasi aliyonayo kufanya kazi kwa bidii, ufanisi na weledi ili utumishi wake uwe na tija katika maendeleo ya taifa.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano inataka kuwa na OPRAS ambayo ni chachu ya kuimarisha utendaji kazi na uwajibikaji kwa kila mtumishi wa umma, hivyo ameitaka Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini ambayo ina majukumu la kutoa miongozo na kusimamia OPRAS, kuweka msingi imara wa usimamizi na utekelezaji wa OPRAS katika Taasisi za Umma.
 
 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza  na watumishi wa Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini wa Ofisi yake kuhusu utekelezaji wa Mfumo wa  Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) kwa watumishi wa umma, alipoitembelea Idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.
002
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akielezwa majukumu ya Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini na mkurugenzi wa Idara hiyo,  Bw. Hassan Kitenge, alipoitembelea Idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.
003
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akihimiza usimamizi mzuri wa Mfumo wa  Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS)  kwa Mkurugenzi wa Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini, Bw. Hassan Kitenge, alipoitembelea Idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.

WANAFUNZI 12,399 WACHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2019 AWAMU YA KWANZA SIMIYU

0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu .

Jumla ya Wanafunzi 12,399 mkoani Simiyu wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 katika shule za Serikali za kutwa na bweni kwa awamu ya kwanza. Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini Desemba 14, 2019 wakati akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa Kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 Mjini Bariadi. 

Sagini amesema jumla ya wanafunzi waliofaulu Mtihani wa Darasa la Saba ni 24,983 sawa na asilimia70.68 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani, ambapo amebainisha kuwa wanafunzi 12, 584 kati ya 24,983 waliofaulu hawajachaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa miundombinu ya elimu. 

Sagini amesema lengo la Serikalini kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanaenda sekondari hivyo, amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani Simiyu kuhakikisha kuwa wanafanya jitihada katika ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu, ili wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba waweze kuanza kidato cha kwanza kwa wakati. 

“Lengo la Serikali ni kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba wanapata nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza ; nimetoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kukamilisha miundombinu inayohitajika ili wanafunzi watakaochaguliwa awamu ya pili waweze kuripoti shuleni kabla ya Februari 15, 2019” 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019, Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi. 
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akitoa taarifa ya hali ya ufaulu katika Mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka 2018, katika kikao cha uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019 kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi. 
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa,Mhe. Paul Maige wakifuatilia kwa makini nyaraka zenye taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019, katika kikao kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi. 

UKARABATI KIWANDA CHA BUCO WASHIKA KASI

0
0


Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akisaidiana na wahandisi na mafundi wa kikosi kazi cha kufufua kiwanda cha kubangua korosho cha Lindi (BUCO) kushusha kaangio la korosho ghafi kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati. Kiwanda cha BUCO kinafanyiwa ukarabati tayari kwa kuanza kubangua korosho zilizonunuliwa na serikali. 
Fundi wa kurekebisha mashine za kubangua korosho Dastan Milanzi akifanya marekebisho ya mwisho kwenye moja ya mashine za kubangua korosho za kiwanda cha kubangua korosho cha Lindi (BUCO) kama alivyokutwa na mpiga picha wetu. 
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya, akipata maelezo ya ukarabati wa mashine ya kubangua korosho kutoka kwa mratibu wa kikosi kazi cha kufufua kiwanda cha kubangua korosho cha Lindi (BUCO) Dkt. Isack Legonda (kushoto) wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa kiwanda hicho kilichokabidhiwa kwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Profesa Sylvster Mpanduji. 
Baadhi ya wahandisi na mafundi wa kikosi kazi cha kufufua kiwanda cha kubangua korosho cha Lindi (BUCO) wakibeba kaangio la korosho ghafi. Kikosi kazi hicho kinatekeleza agizo alilolitoa wiki iliyopita Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Viwanda Vidogo (SIDO), Profesa Sylvester Mpanduji, akikagua shughuli za ubanguaji wa korosho unaofanywa na wabanguaji wadogo kwenye eneo la SIDO Mtwara. SIDO kwa kushirikiana na wajasriamali wadogo inatekeleza azma ya serikali kuhakikisha korosho zinabanguliwa nchini. 
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akishuhudia zoezi la kubangua korosho linalofanywa na wabanguaji wadogo kwenye eneo la SIDO mjini Mtwara. Mhandisi Manyanya yuko kwenye ziara ya kukagua uwezo wa viwanda vya kubangua korosho mikoa ya Mtwara na Lindi kujiridhisha kabla ya kuingia makubaliano ya kubangua korosho ya serikali. (Picha zote na Idara ya Habari-MAELEZO)
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images