Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAKUU WA MIKOA PAAMOJA NA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika kikao kilichowahusisha Wakuu wote wa Mikoa pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi, baadhi ya Mawaziri pamoja na Makatibu Wakuu wa baadhi ya Wizara, Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika, Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na Wakuu wa Mikoa yote mara baada ya kikao chao pamoja na Makatibu Tawala kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala bora George Mkuchika, Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa yote Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika, Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala mara baada ya Kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam.  PICHA NA IKULU

TTCL yasaini na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote kupeleka huduma vijijini

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga (kushoto) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) mara baada ya kuweka saini katika mkataba wa kusambaza mawasiliano maeneo ya vijijini leo jijini Dar es Salaam. Katikati wakishuhudia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Issack Kamwele pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dk. Maria Sasabo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) akisaini mkataba na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga (kushoto waliokaa) leo jijini Dar es Salaam. Katika makubaliano hayo TTCL itasambaza mawasiliano maeneo ya vijijini ili kuchochea maendeleo. Wanao shuhudia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Issack Kamwele pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dk. Maria Sasabo. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Issack Kamwele akizungumza katika hafla hiyo ya kutiliana saini na watendaji wakuu wa kampuni za simu zilizoshinda zabuni ya UCSAF na watendaji wa mfuko huo. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Issack Kamwele (kulia mbele) akizungumza na watendaji wakuu wa makampuni ya simu yalioshinda zabuni ya UCSAF kusambaza mawasiliano vijijini pamoja na watendaji wa mfuko huo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akibadilishana nakala ya mkataba na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Eng. Peter Ulanga (kushoto) mara baada ya kutiliana saini leo jijini Dar es Salaam. Katika makubaliano hayo TTCL itasambaza mawasiliano maeneo ya vijijini.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuelezea shirika hilo lilivyojipanga kutekeleza zabuni hiyo kwa ufanisi. 
Picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Issack Kamwele mara baada ya hafla hiyo. 

Halotel Wasaini Mkataba na UCSAF

$
0
0


(Halotel) Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Trieu Tanh Binh, (Kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga, wakitia saini mkataba wa makubaliano wa awamu ya tatu kwa ajili ya kusambaza mawasiliano vijijini, utakao wezesha kampuni hiyo kufikia Zaidi ya vijiji 300, anaeshuhudia ni Waziri wa Mawasiliano, Ujenzi na Uchukuzi Eng. Aisack. (Katikati)

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (ucsaf) Eng. Peter Ulanga (Kushoto) akipongezana na Naibu Mkurugenzi wa Halotel Trieu Tanh Binh (Kulia) mara baada ya kutia saini Mkataba wa wa Kusambaza mawasiliano vijijini utakao wezesha kampuni hiyo kufikia Zaidi ya vijiji 300, anaeshuhudia ni Waziri wa Mawasiliano, Ujenzi na Uchukuzi Eng. Aisack. (Katikati)

Nchi zilizoendelea zatakiwa kutimiza wajibu wa kutoa michango ya fedha ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima amezitaka nchi zilizoendelea kutimiza wajibu wao wa kutoa michango ya fedha na kuwezesha upatikanaji wa teknolojia za kisasa kwa nchi zinazoendelea kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya Tabianchi kwa mujibu wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi pamoja na Makubaliano ya Paris.

Akihutubia Mkutano wa 24 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi unaoendeleo Nchini Poland Mhe. Sima ameeleza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoathirika zaidi na athari za mabadiliko ya tabianchi duniani, ikiwa ni pamoja na kuathiriwa na ukame, mafuriko na kuongezeka kwa ujazo wa bahari, jambo ambalo huathiri zaidi wakazi wa mwambao wa bahari pamoja na shughuli zao za kiuchumi ambazo ni msingi wa maisha yao. 

Mhe. Sima amesema kuwa athari hizo zimethibitishwa pia katika taarifa maalumu ya kisayansi iliyotolewa na Jopo la Kimataifa la Wataalamu wa Mabadiliko ya Tabianchi kuhusu athari zitakazojitokeza iwapo joto la dunia litaongezeka zaidi ya nyuzijoto 1.5 (1.50C). “Kwa sasa joto la dunia limeongezeka kwa nyuzijoto 0.85 kulinganisha na kipindi kabla ya mapinduzi ya viwanda, natoa rai kwa jumuia ya kimataifa kuchukua hatua za haraka na za makusudi kukabiliana na changamoto hii” Sima alisisitiza.

Katika Hotuba yake Naibu Waziri ameeleza juhudi za Tanzania katika kukabiliana na changamoto hizi ambazo zinaendana na mpango wa maendeleo wa Taifa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), Mfumo wa usafiri wa mwendo kasi katika jiji la Dar es Salaam, ujenzi wa barabara za juu (flyovers and interchange) na ujenzi wa bwawa la umeme wa maji katika mto Rufiji ambao unatarajiwa kuzalisha umeme kiasi cha MW 2,115.

Mhe. Sima amesema kuwa nishati ya umeme ambayo ni salama kimazingira itasaidia katika ukuaji wa uchumi wa viwanda, undeshaji wa treni za umeme na kurahisisha upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa matumizi ya majumbani na kusisitiza kuwa kuwa hizi ni hatua muhimu katika kusaidia kupunguza uzalishaji wa gesijoto zinazochangia ongezeko la joto duniani.

Mhe. Mussa Sima yuko nchini Poland akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu ulioanza tangu tarehe 2 Desemba 2018 na utamalizika tarehe 14 Desemba, 2018.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akihutubia katika Mkutano wa 24 wa Nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Katowice Poland. Pamoja na mambo mengi Mhe. Sima amezitaka Nchi zilizoendelea kutimiza wajibu wao wa kutoa michango ya fedha ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi kwa nchi zinazoendelea.

MASHAHIDI 15 KUTOA USHAHIDI KESI YA ZITTO

$
0
0
Na Karama Kenyunko,  Blogu  ya Jamii.
UPANDE wa mashtaka katika kesi ya uchochezi inayomkabili, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa inatarajia kuleta mashahidi 15 na vielelezo vitatu katika kesi hiyo.

Wakili wa Serikali, Wankyo Saimon akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga wameeleza hayo leo Desemba 13.2018 mbele ya Hakimu Mkazi  Mkuu,  Huruma Shaidi Mara baada ya kumaliza kumsomea Zitto maelezo ya awali ( PH). Katuga amedai watakuwa na mashahidi 15 na vielelezo viwili vya kimaandishi na kielelezo kimoja cha kieletroniki.

Ameongeza kudai kuwa jinsi kesi itakavyoendelea kusikilizwa wanaweza kuongeza mashahidi na vielelezo au kupunguza mashidi, kwa sababu hata baada ya Zitto kusomewa maelezo hayo Leo na kuyajibu wanaweza kuwapunguza. Kufuatia maelezo hayo, Hakimu Shaidi alimpa nafasi Wakili wa Zitto, Peter Kibatala kuzungumza, ambapo alidai kuwa wataongea baada ya upande wa mashtaka kufungua ushahidi wao.

Pia Katuga aliiomba Mahakama  iwape muda wa wao kuweza kutoa nakala ya mtoa  taarifa ili waweze na kuwapatia upande wa utetezi kama sheria inavyoelekeza. Awali, wakili Wankyo akimsomea Zitto PH amedai Oktoba 28, 2018 mshtakiwa akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, uliyofanyika katika Makao Mkuu ya ofisi ya  Chama cha ACT_Wazalendo alitoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.

Iliendelea kusomwa kuwa,  maneno hayo yaliyotamkwa sio tu yalichochea chuki lakini pia yalitengeneza uhusama kwenye mamlaka halali nakupelekea mijadala miongoni mwa makundi mbali mbali katika jamaii na kweny mitandao na vyombo vya habari kwa ujumla. Pia, alidai kuwa maneno hayo yaliwafanya watu wafikirie kuwa Serikali haiwajali raia wake.

Kutokana na maneno hayo, Zitto alikamatwa Oktoba 30 mwaka huu akiwa nyumbani kwake Masaki na kuwekwa mahabausu ya polisi na pia nakala ya taarifa ya vyombo vya habari polisi wali ikuchukua baada ya kuwa Zitto amekamatwa. Baada ya  kumsomewa maelezo hayo, Zitto alikubali majina yake, alikubali kuwa yeye ni Mbunge na pia alikubali kuwa alikamatwa nyumbani kwake Masaki.

Hata hivyo Zito alikataa maelezo mengine yote ikiwemo kuwa yeye si Mwenyekiti wa ACT Wazalendo na nakala ya taarifa hiyo haikukutwa nyumbani kwake wakati anakamatwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 14, 2019 kwa ajili ya kutajwa na itaendelea kusikilizwa Januari 29,2019.

Shilawadu ndani ya DStv

$
0
0
Hatimaye kipindi maarufu cha Shilawadu kuanza kuonekana live ndani ya DStv kupitia chaneli ya Maisha Magic Bongo (DSTV160) kuanzia Ijumaa Desemba 14, 2018. Shilawadu Xtra itaruka hewani kila siku ya Ijumaa saa moja jioni na kurudiwa siku za Jumapili muda huo huo.

Akitambulisha rasmi wa kipindi hicho, Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria amesema kuwa kipindi cha Shilawadu Xtra kimeongezwa ladha kadha wa kadha tofauti na awali  na kitagawanyika katika sehemu tofauti tofauti ikiwamo Chemba la Msengenyo, Ubuyu wenye Vitamin Xtra, Kiti cha Moto na Mikikimikiki ya mastaa  ili kuwapatia wateja wa DStv na watazamaji kwa ujumla burudani isiyo kifani .

Amesema kuwa watazamaji wa Maisha Magic Bongo na wapenzi wa Shilawadu hasa wale wapenzi wa umbea wakae mkao wa kula kwani kwa sasa wataweza kushuhudia visa na matukio yote yanayojiri hapa mjini kupitia Shilawadu Xtra chini ya makamanda mahiri wa kipindi hicho akiwemo mkali wa kunyapianyapia Soudy Brown sambamba na kamanda Kwisa ‘Mzee mti mkavu’.

“DStv kupitia Chaneli yake pendwa ya Maisha Magic Bongo(MMB), siku zote tunafanya jitihada kuhakikisha kuwa tunatoa kipaumbele na kuunga mkono maudhui ya ndani na kipindi hiki ni muendelezo wa jitihada hizo”, alisema Alpha.

Kipindi hiki kitakuwa kikiruka hewani kila siku ya Ijumaa saa moja hadi saa mbili usiku na kurudiwa kila Jumapili kwa muda huo huo. Hii itawapa fursa mashabiki na watazamaji wa Maisha Magic Bongo kupata burudani zaidi na haswa kwa wale ambao hawataweza kukitazama kwa siku ya Ijumaa.


BENKI KUU TAWI LA DODOMA WAANIKA MAJUKUMU YAO ILI KUFANIKISHA SHUGHULI ZA UCHUMI KWA WANANCHI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Dodoma limefafanua kwa kina majukumu yake mbalimbali na miongoni mwa majukumu hayo ni kutunza na kusambaza fedha (noti na sarafu) safi za thamani mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha wananchi kutekeleza shughuli mbalimbali za uchumi katika Kanda ya kati. 

Tawi la BoT, Kanda ya Kati, Dodoma, ni tawi la tano kufunguliwa tangu nchi ipate uhuru; na ni moja ya matawi mawili ambayo yamefunguliwa miaka ya hivi karibuni.Wakati tawi la Dodoma limefunguliwa 15/10/2015, Tawi la Mtwara limefunguliwa Machi 2017. 

Awali Tawi la Dodoma lilitarajiwa kutoa huduma za benki kuu katika mikoa ya Dodoma, Singida Iringa and Tabora. Hata hivyo kutokana na kukamilika ujenzi wa tawi la Mtwara, na kama ilivyokuwa kwa matawi mengine ya awali, mgawanyo wa mikoa katika kanda za Benki Kuu ulibadilika. 

Meneja wa masuala ya Fedha na Takwimu kutoka Benki Kuu ya Tanzania(BoT) tawi la Dodoma Dk.Camilius Kombe ametaja baadhi ya majukumu ya tawi hilo wakati anazungumzia majukumu ya benki hiyo kwa waandishi wa habari waliokuwa kwenye mafunzo ya habari za fedha na uchumi.

Ambapo katika majukumu hayo yapo pia ya kukusanya fedha zilizotumika kutoka vituo maalum vya kusambazia fedha vilivyo katika baadhi ya mabenki ya biashara na kuondoa katika mzunguko fedha ambazo zimechakaa na hazifai kutumika tena.
Meneja Msaidizi wa Idara ya Uhusiano na Itifaki katika Benki Kuu ya Tanzania(BoT) akifafanua jambo kuhusu namna ya kutambua fedha bandia kwa waandishi wa habari za Fedha na Uchumi baada ya kutembelea BoT tawi la Dodoma kuangalia namna wanavyotunza fedha
Meneja Msaidizi kutoka Kurugenzi ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania(BoT) tawi la Dodoma Nolasco Maluli akizungumzia majukumu ya tawi hilo wakati wa semina ya waandishi wa habari mjini Dodoma leo
Meneja Msaidizi wa Huduma za kibenki BoT tawi la Dodoma Lilian Silaa akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa semina ya mafunzo ya uandishi wa habari za fedha na uchumi
Mtangazaji na Mwaandishi wa redio Clouds FM akizungumza kwenye semina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi.

MAAGIZO YA NAIBU WAZIRI MIFUGO NA UVUVI KWA WATENDAJI HALMASHAURI YA KILOMBERO

$
0
0
Na Emmnuel Masaka,Globu ya jamii
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewaagiza watendaji wa Halmashauri ya Kilombero kuhakikisha wavuvi wote wanasajiliwa na kuwa na vikundi ndani ya mwezi mmoja ili waweze kufanya shughuli zao na kuchangia pato la taifa.

Pia amewataka kuwaangalia wavuvi hao kama wanauhitaji wa kupata vitambulisho vya wajasiriamali alivyovitoa Rais John Magufuli wapewe ili wafanye kazi zao bila bugudha.

Akizungumza katika ziara aliyoifanya katika kijini cha Miwangani kata ya Idete wilayani humo na kutatua migogoro mbalimbali Ulega amesema kuwa wavuvi lazima wathaminiwe na kupatiwa haki zao hasa za kuwa na vikundi mbalimbali hivyo haina budi kufanya tathimini na kuwasajili ili waweze kutambulika kwani nao husaidia katika kuchangia pato la taifa.

Amesema kuwa kabla ya Januari mwakani atatembelea na kuzungumza na wavuvi hao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kama maagizo hayo yametekelezwa vyema.

Kwa upande wao wavuvi na wafugaji wamempongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake za kujenga Tanzania mpya na hasa kwa kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini na wamemshukuru Waziri na Naibu waziri wa mifugo na uvuvi kwa ushirikiano wanaoutoa katika kukuza na kuimarisha sekta hiyo.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wafungaji na wavuvi wa kijiji cha Miwangani wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro,wakati wa zaiara yake ya kuzisikiliza kero mbalimbali za wananchi hao na kuzitafutia ufumbuzi .
Sehemu ya Wananchi wa kijiji cha Miwangani wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro wakimsikiliza Naibu wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alipokuwa akizungumza nao.
Mmoja wa Wanakijiji cha Miwangani akimshukuru Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega kwa kufika katika kijiji hicho na kuwatalulia kero zao na muda mrefu.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG) 
Katibu Tawala wa wilaya ya Kilombero,Robert Sidasela akizungumza na wafungaji na wavuvi wa kijiji cha Miwangani wilaya ya Kilombero kuhusu kuheshimu mipaka ya wakulima na wafungaji iliyowekwa na Serikali.

TIGO YAANDAA HAFLA KWA WAKALA WAKE ,YATANGAZA NEEMA KWA MAWAKALA WATAKAOFANYA VIZURI

$
0
0


Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha kutoka Tigo Hussein Sayed, akimuuliza swali mmoja wa mawakala walihudhuria hafla ya chakula cha jioni ambapo Tigo ilitangaza promosheni ya mwisho wa mwaka inayojulikana kama Wakala Chief itakayotoa zawadi ya mamilioni kwa mawakala watakaofanya vizuri katika biashara zao.
Meneja wa Tigo Pesa, James Sumari akizungumza na baadhi ya mawakala wa Tigo Pesa katika hafla iliyofanyika jijjini Dar es Salaam ambapo Tigo ilitangaza promosheni ya mwisho wa mwaka inayojulikana kama Wakala Chief itakayotoa zawadi ya mamilioni kwa mawakala watakaofanya vizuri katika biashara zao.
Baadhi ya Wakurugenzi wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo wakiwa katika picha ya pamoja na mawakala wa Tigo Pesa katika hafla ambapo Tigo ilitangaza promosheni ya mwisho wa mwaka kwa inayojulikana kama Wakala Chief itakayotoa zawadi ya mamilioni kwa mawakala watakaofanya vizuri katika biashara zao.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha kutoka Tigo Hussein Sayed, akitoa zawadi ya kofia lwa mmoja wa mawakala wa Tigo Pesa aliyefanikiwa kujibu kwa usashi swali alilouliza kuhusu Tigo Pesa wakati wa hafla ya chakula cha jioni ambapo Tigo ilitangaza promosheni ya mwisho wa mwaka kwa inayojulikana kama Wakala Chief itakayotoa zawadi ya mamilioni kwa mawakala watakaofanya vizuri katika biashara zao.

DEKULA BAND colours Kenya Jamhuri Day in Stockholm, Sweden

$
0
0


Vocalist: Gaby Nkomba Kababa Lead guitar: Dekula Kahanga Rythm guitar: Göran Larsson Bass: SugarRay Jah'neral Poetafari Napunyi Drums: Lalo Cissokho Congas: Kabara Kabamba Cameraman: Moses Menza Calypso Gichia
Venue: Kenya Embassy, Stockholm, Sweden

DIGITAL PIPELINE UK (COMPUTERS 4 AFRICA) KUZINDUA MRADI WA ELIMU KWA NJIA YA MTANDAO SEHEMU YA KWANZA YA KOMPYUTA, PRINTERS, KOMPYUTA MPAKATO, PROJECTORS NA VIFAA MBALIMBALI VYA ICT VYENYE THAMANI ZA SHILINGI ZA KITANZANIA MILLIONI MIA SITA VIMEONDOKA UINGEREZA LEO KUJA TANZANIA.

$
0
0
Katika kuungana na juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mh. Rais Dkt John Pombe Magufuli, Shirika la Digital Pipeline UK, kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia wameanzisha mradi mkubwa utakaobadilisha na kuboresha utoaji wa elimu nchini kuanzia shule za msingi za serikali hadi kidato cha sita kwa njia ya mtandao salama (Secured School Network) utakaobeba mtaala (curriculum) na vitabu vya maarifa mbalimbali vinavyokwenda na wakati ili kuwafanya walimu na wanafunzi kujinoa ipasavyo na kuwa wabunifu wanaoweza kushindana katika ulimwengu wa maarifa kwa wakati. (Communication Tool).
Hayo yameelezwa jijini Kent nchini Uingereza leo, tarehe 12/12/18 na Ndugu Abraham Sangiwa, Mkurugenzi na Mwenyekiti wa DIGITAL PIPELINE UK ambayo inafadhiliwa na Bill and Melinda Gate Foundation, Metropolitan Police UK, National Health Services UK and Vauxhall Motors UK, Katika hafla iliyofanyika katika ofisi kuu Priory Park jijini Kent nchini Uingereza
Uzinduzi huo pia ulishuhudiwa na wadau mabalimbali akiwemo Deputy Lieutenant of Kent Trevor Sturgess, Bevil Williams C.E.O at Digital Pipeline, board members, wafanyakazi wa Digital Pipeline UK na wadau mbalimbali
Ndugu Abraham Sangiwa aliendelea kusema napenda kuishukuru wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia kwa kuniteua kuwa Balozi wa Wizara katika Mradi huu wa Digital Campus in Tanzania, haikuwa kazi rahisi kufanikisha mradi huu kwa Tanzania kwani Digital Pipeline UK inafanya shughuli zake katika nchi zaidi ya ishirini na saba barani Afrika, nchi nane bara la Asia, baadhi ya nchi bara la  Ulaya, Amerika ya Kati na Kusini, na kila moja ilipenda mradi huu mkubwa wa kujenga Digital Campus Plant kubwa na ya pekee barani afrika unfanyike katika nchi zao, lakini kutokana na uzalendo na uelewa kwa timu nzima ya Wizara ya Elimu na viongozi wake na  kwa kuzingatia vigezo vilivyo wazi kwa serikali ya Tanzania vimesaidia kuleta mradi huu wenye manufaa makubwa nchini.

 Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Bodi, Digital Pipeline UK (Computers 4 Africa) Ndugu Abraham Sangiwa (Kushoto), Bevil Williams C.EO.  Katikati ni Deputy Lieutenant of Kent Uingereza - Trevor Sturgess wakibadilishana mawazo katika ofisi kuu ya DP jijini Kent nchini Uingereza, wakati wa kushuhudia upakiaji wa vifaa vya kielektroniki kwa ajili ya mradi wa “Digital Campus on Education in Tanzania” utakaofanywa kwa pamoja na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia. 
Vifaa mbalimbali vya kielektroniki vikipakiwa kwenye container tayari kwa safari ya kuelekea Tanzania. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

WEMA SEPETU AWASILISHA SEHEMU YA UTEKELEZAJI KWA ADHABU ALIYOPEWA NA BODI YA FILAMU TANZANIA

$
0
0
Msanii wa  Tasnia ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini Wema Isaac Sepetu mapema leo amewasilisha katika ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) baadhi ya maelekezo aliyopewa kuyafuata kufuatia adhabu aliyopewa tarehe 26 Oktoba mwaka huu kutokana na ukiukwaji wa Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Na. 4 ya mwaka 1976. 
Bodi ya Filamu ilimfungia kwa muda usiojulikana na kumtaka kuyafanyia kazi maeneo muhimu matatu ambayo ni kuandika kwa maneno yasiyozidi 1500 mambo yote mazuri aliyowahi kuyafanya kwenye maisha yake, aandike changamoto alizowahi kukutana nazo kwenye maisha yake na aandike ni kwa namna gani anaweza kusafisha taswira yake kutokana na matendo yake hasi aliyoyafanya. 
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo Alieleza kuridhishwa na mwenendo wa nguli huyo wa Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini kufuatia utiifu wake wa adhabu aliyopewa na kusema Tasnia ya Filamu bado inamuhitaji na kama akiendelea na mwenendo mzuri basi atafunguliwa kutoka kwenye adhabu aliyopewa. 
“Tunamuhitaji sana Wema Sepetu katika Tasnia ya Filamu kutokana na umahiri wake katika kazi lakini tunachukia maadili mabovu aliyoyaonesha katika jamii na sisi kama Bodi ya Filamu hatutasita kumfungia moja kwa moja kama akiendelea na matendo yauvunjifu wa maadili yetu kama Watanzania.”Alisema Fisoo. 
Kwa upande wake Wema Sepetu amesema anajutia sana kufungiwa kwake kutokushiriki kwenye kazi za Filamu kwakuwa anakosa fursa nyingi za kufanya kazi za kimataifa na ameahidi kuendelea na mwenendo mzuri ili aweze kuwa mfano wa kuigwa na jamii inayo mtazama, hivyo akaiomba Bodi ya Filamu ijaribu kumfikiria na kumfungulia mapema kwa kuwa anategemea kuendesha maisha yake kupitia kazi ya Filamu. 

“Filamu ndio kitu ninacho kitegemea kwenye maisha yangu na tangu nimefungiwa nimekosa fursa nyingi za kazi ambazo zingetutangaza kimataifa, hivyo naahidi kuendelea kuwa na mwenendo chanya katika jamii pasipo kuharibu maelekezo niliyopewa na Bodi ya Filamu katika kuisafisha taswira yangu ambayo imechafuka” 

Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa Wema Sepetu kuhakikisha anarudisha Taswira yake chanya iliyopotea na kuwa mfano wa kuigwa katika jamii na ikiwa mwenendo wake utazidi kuwa mzuri basi atafunguliwa kutoka kwenye adhabu aliyopewa.


 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) bi. Joyce Fissoo (kulia) akipokea sehemu ya adhabu kutoka kwa  msanii wa Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini bi. Wema Sepetu mara baada ya kuwasilisha sehemu ya utekelezaji kwa adhabu aliyopewa na bodi hiyo leo kwenye ofisi za Bodi ya Filamu Mtaa wa Samora Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) bi. Joyce Fissoo (kulia) akiwaonesha Waandishi wa Habari (hawapo pichani) sehemu ya utekelezaji kwa adhabu waliyokuwa wamempa Wema Sepetu.
Wema Sepetu akiwajibu Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kufuatia kuwasilisha sehemu ya utekelezaji kwa adhabu aliyokuwa amepewa na Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) kwenye ofisi za Bodi hiyo Mtaa wa Smora Jijini Dar es Salaam.


MICHUZI TV: GIGY MONEY AWAPA GENGE MASHABIKI ZAKE KATIKA WASAFI FESTIVAL ZANZIBAR

MICHUZI TV: Zanzibar yaonesha mapenzi ya dhati kwa COUNTRY BOY katika WASAFI FESTIVAL 2018

MICHUZI TV: CASSIM MGANGA athibitisha utajiri wake wa mahaba Zanzibar


Wanawake Watajwa Kama Sehemu ya Hamasa, Toharakinga kwa Wanaume Geita

$
0
0
Ikiwa zimesalia siku chache kabla ya kumalizika kwa robo ya kwanza, ya Kampeni ya Toharakinga kwa Wanaume wenye umri kuanzia miaka kumi na kuendelea inayoendeshwa mkoani Geita, kundi la wanawake limebainika kuwa chachu ya kufanikisha mpango huo kutokana na wengi wao kuwahimiza wanaume wao na watoto kwenda kufanyiwa Tohara.

Hadi kufikia Sepetemba 2018, wanaume 115, 000 kati ya 119, 000 waliolengwa kufanyiwa tohara Mkoani Geita walikuwa wamefikiwa na kuhudumiwa katika kampeni inayoendeshwa na Serikali kwa ushirikiano na Shirika lisilo la kiserikali la IntraHealth International kwa ufadhili wa Mfuko wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) PEPFAR kupitia CDC,

Kituo cha Afya Katoro ni kati ya vituo 23 vya muda na 13 vya kudumu vinavyotoa huduma hiyo ambayo kabla ya kutolewa wanaume wanaofika kufanyiwa tohara hupitia hatua kadhaa ikiwemo kuandikishwa, kuelimishwa na kupimwa virusi vya UKIMWI kabla ya huduma.

Msimamizi wa Kituo hicho, Bw. Faustine Edward alisema muitikio wa wananchi umekuwa mkubwa kiasi cha kuwafanyia tohara wanaume kati ya 10 hadi 30 kwa siku.

“Mwitikio ni mkubwa sana, wateja ni wengi, hadi tunafikiria kuongezewa muda kwakuwa tulianza zoezi hili mwezi Novemba 15, 2018 na mwisho ni mwezi Desemba 15, 2018; Lakini pia niwapongeze akinamama, wamekuwa mabalozi wazuri kwa kuwaleta watoto wao lakini pia kuwashawishi waume zao kuja kufanya Toharakinga salama hadi kutuwezesha kupata watu 10 hadi 30 kwa siku,” alisema Bw. Edward
Wakazi wa Katoro wakisubiri kupata huduma ya Tohara ya bila malipo, inayotolewa na Taasisi ya Kimataifa inayojihusisha na masuala ya Afya ya IntraHealth katika kituo cha afya Katoro.

Madaktari wakimtahiri mmoja wa wakazi wa Katoro,wakati wa huduma hiyo ya bila malipo inayotolewa na Taasisi ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya Afya ya IntraHealth katika kituo cha afya Katoro.

Msimamizi wa kituo cha Tohara cha Katoro Bw. Faustine Edward, akizungumza na wakazi wa Katoro waliojitokeza kupata huduma hiyo ya bila malipo, inayotolewa na Taasisi ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya Afya ya IntraHealth katika kituo cha afya Katoro, ambapo wanatahiri watu 20 hadi 30 kwa siku. Hapa hupewa elimu kabla ya kufanyiwa tohara.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 14, 2018

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

SAFARI NDANI YA MTO MNYERA- MALINYI MOROGORO

$
0
0
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Ngombo wilaya ya Malinyi mkoa wa Morogoro  wakiwa katika Fibre  wakivuka mto  Mnyera, ambapo nauli ya kuvuka ni  ni shilingi 500 na pikipiki,shilingi 3000.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG) 
 Wananchi wa jiji cha Ngombo wilaya ya Malinyi mkoa wa Morogoro wakipakiza pikipiki katika Fibra ilikuvuka mto Mnyera.ambapo pikipii moja wanalipa shilingi 3000.
Safari ya kuvuka mto Mnyera ukiendelea.

HOTUBA YA RAIS DKT. MAGUFULI HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA WA UJENZI MRADI WA UMEME WA RUFIJI

Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images