Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

KAMANDA WA POLISI NJOMBE ALIA NA WANAOTUPA VICHANGA

$
0
0
 Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Kupitia Mtandao wa Wanawake  umechukizwa na kulaani Vikali  vitendo vya akina mama kutupa watoto mara baada ya jeshi hilo nyakati za usiku  kumuokota  mtoto mwenye umri wa  takribani wiki mbili katika Dampo la Kipagamo mjini  Makambako akiwa mtupu.
 Tukio hilo limetokea Novemba 02,  mwaka auu Ambapo Jeshi la Polisi wilaya ya kipolisi Makambako wakati likiwa kwenye doria ndipo lilipomuona mtoto huyo akiwa hai na kulazimika kumuokota kwa kushirikiana na Ustawi wa Jamii na kisha kumpeleka katika kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Tumaini Ilunda Wilayani Njombe.
 "Askari wakiwa kwenye doria walipomsikia mototo analia wakaenda kwenye jalala na kumkuta mototo huyu akiwa katika uchi wa mnyama, tunawaomba sana hasa wakina mama ni vema kama hata umeshindwa kabisa kutunza mtoto ukamleta katika vituo hivi ukamuweka pale nje masista kama hawa wangemuona na kumchukua kuliko vitendo kama hivi vya kinyama" alisema kamanda Mzinga
Katika hatua nyingine Mtandao wa Wanawake wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe ikiwa ni muendelezo wa siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia kwa kushirikiana na Kamanda wa Polisi Mkoa Renatha Mzinga wametumia nafasi yao kama jeshi la polisi akina mama kutembelea katika kituo cha kulea watoto yatima cha Tumaini kilichopo Ikelu na kuonana na watoto pamoja na kutoa Misaada mbalimbali kama vile sabuni, sukari, pipi, unga na vitu vingine mbalimbali  vyenye thamani ya shilingi Laki Nne.

WANAFUNZI 600 S/M VIKAWE KATA YA PANGANI, KIBAHA MJINI WASOMEA KATIKA MADARASA MANNE

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA

SHULE ya msingi Vikawe ,kata ya Pangani ,Mjini Kibaha ,Mkoani Pwani ina upungufu wa vyumba vya madarasa hali inayosababisha ,wanafunzi 600 kusomea kwenye vyumba vinne vinavyotumika shuleni hapo .

Aidha wakazi wa Vikawe ,wanakabiliwa na adha ya ukosefu wa maji safi na salama hali inayosababisha kutumia maji ya visima ambayo sio salama kwao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano wa hadhara wa wakazi wa Vikawe Bondeni, Vikawe Shule na Mtaa wa Miwale, ulioitishwa na mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka , mkazi Amina Seif alisikitishwa kuona baadhi ya vyumba vya madarasa vina majani ya miba badala ya wanafunzi.Akizungumzia suala la ukosefu wa maji , Majawa Mtwana alisema ,hawapaswi kuwa na tatizo la maji kwakuwa bomba limepita kwenye eneo lao .Alisema wangefaidika na mradi huo ulioanzia Ruvu Chini -Vikawe Shuleni hadi Miwale ."Tunaomba utusaidie mbunge ,hatupaswi kuishi mjini wakati tunashida ya maji ,ndoa za watu zipo matatani kwa kukosa maji ,tunaoga maji ya visimani,tunataka ushughulikie suala hili ili tuondokane na kero hii" alielezea.

Kaimu afisa elimu msingi ,Ramadhani Lawoga alisema,shule ya msingi Vikawe ina jumla ya vyumba vya madarasa saba,kati ya vyumba hivyo viwili na ofisi ya mwalimu ni jengo la zamani ambalo limechakaa.Hata hivyo alisema ,nalo jengo jipya lililojengwa shuleni hapo nalo ni bovu .Lawoga alieleza, kutokana na hali hiyo ,vyumba vitatu kati ya saba vilivyopo ni vibovu na hivyo vinatakiwa kujengwa upya ,ambapo wanatarajia kuanza kujenga vyumba viwili kwa bajeti ya mwaka 2018/2019. Akijibu juu ya upungufu wa madarasa ,aliahidi kwenda kushauriana na mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha Jennifer Omolo ili kuangalia namna ya kukarabati baadhi ya madarasa .

Kuhusu changamoto ya maji ,halmashauri ya mji huo imekiri kuwepo deni la bili walilokuwa wakidaiwa na DAWASA ya sh.milioni 4.8 ambapo imeshalipa kiasi cha sh.milioni 3.4 na imebakia deni la milioni 1.4 .Kutokana na ubovu pamoja na wataalamu kutofanya kazi ya usambazaji ipasavyo ya mradi huo ,Koka alisema kinachofuata ni hatua ya uchunguzi na mradi kurudishwa chini ya DAWASA ili kuondoa tatizo hilo .

Mbunge huyo alilazimika kuunda kamati ya watu sita akiwemo injinia wa DAWASA Kibaha, Injinia wa maji Halmashauri ya Mji Kibaha, Diwani wa Pangani ,katibu wa nbunge na wananchi wawili kwa ajili ya kwenda Bagamoyo ili kufuatilia jambo hilo na kutoa mrejesho ndani ya wiki moja .

DKT. KIKWETE ASIMULIA KILICHOPELEKEA KUANDIKA KITABU CHAKE, KUANZISHA TAASISI YAKE

$
0
0
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mwanzilishi wa Taasisi ya Jakaya Kikwete Dkt. Jakaya  Kikwete amesema kuwa  taasisi yake pamoja na kitabu chake cha The Journey Of My Life alifikiria kuanzisha vitu ambavyo vitakuwa kumbukizi 
kabla ya kumaliza uongozi wake akiwa kama Rais.

Dkt. Kikwete ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika hafla maalum ya Chakula cha jioni iliyoandaliwa na Chemba ya Biashara ya Marekani hapa nchini (AMCHAM) kwa lengo yakuishukuru Serikali ya Tanzania.

Amesema katika uongozi wake marafiki  walifikiri jambo ambalo atalifanya mara baada ya kumaliza utumishi wa umma aliohudumu kwa miaka 40, ambapo alitaka kuweka uzoefu na mawazo yake katika maandishi ili yasiweze kufutika.

Kikwete amesema katika kitabu cha The Journey of My Life  ameeleza kuhusiana na taasisi ya Jakaya na maisha yake tangu akiwa mdogo huko kijijini Msoga pamoja na uzoefu wa uongozi kwa miaka 40.

Dkt. Kikwete amesema katika kitabu chake amegusia maeneo mbalimbali yakiwemo kilimo, afya, vijana na utawala.

Kwa upande wake, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania  Dkt. Inmi Patterson amempongeza Dkt. Kikwete kwa uthubutu na amewashukuru watanzania kwa ukarimu, upendo na ushirikiano pamoja na kutunza amani hapa nchini.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo kuhusu historia ya maisha yake pamoja na uanzishwaji wa Taasisi ya Dkt Kikwete katika hafla ya iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania  Dkt. Inmi Patterson akitoa shukrani kwa mchango pamoja na mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Marekani katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka MMG)

Sehemu ya wandau mbalimbali wa maendeleo wakiwa katika hafla hiyo.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mwanzilishi wa Taasisi ya Jakaya Kikwete Dkt. Jakaya  Kikwete(kulia) akionyeshwa moja ya Picha na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Marekani hapa nchini (AMCHAM) Garry Friend(kushoto) iliyotoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ikiashiria kutambua mchango wa Serikali ya Tanzania.

MAHAKAMA YAELEZWA UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MFANYABIASHARA AKRAM AZIZI HAUJAKAMILIKA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi dhidi ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara Akram Azizi ambaye ni mdogo wa mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Azizi bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali Elia Athanas ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile kesi hiyo ilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa."Mheshimiwa keai hii leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika, tunaimba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa" amedai wakili Athanas.

Kufuatia malezo hayo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 26 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.Katika kesi hiyo, Mshtakiwa Azizi anakabiliwa na mashtaka 75 yakiwemo mashtaka 71 ya kukutwa na Silaha za aina mbali mbali mbali, utakatishaji wa fedha kiasi cha USD 9018.

Pia anakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na nyara za serikali zenye thamani ya sh milioni 108, risasi 6496 na pia anakabiliwa na kosa la kukutwa na nyama ya Nyati, Kilogramu 65 yenye thamani ya Shilingi Mil 4.35 bila kuwa na kibali, ambalo anadaiwa kulitenda Oktoba 30,2018 huko Oysterbay Kinondoni Dar es Salaam.

Katika shtaka la utakatishaji mshtakiwa anadaiwa, kati ya Juni 2018 na Oktoba 30. 2018 katika eneo la Osterbay, alijipatia jumla ya USD 9018 huku akijua kuwa kiasi hicho cha fedha ni zao la kosa tangulizi la kujihusisha na biashara haramu ya nyara za serikali pamoja na kukutwa na silaha bila kibali.

Katika mashtaka ya kukutwa na risasi mshtakiwa anadaiwa, Oktoba 30. 2018 (Jana) huko Osterbay, alikutwa na risasi 4092 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mrajisi wa kibali cha silaha.

Pia Imedaiwa Oktoba 31.2018 (leo) huko huko Osterbay mshtakiwa alikutwa na risasi 2404 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mrajisi wa silaha.
Mfanyabiashara Akram Azizi ambaye ni mdogo wa mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Azizi akiwasili leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi yake ya uhujumu uchumi inayomkabili .

NEWZ ALERT: Waziri wa Nishati avunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini

$
0
0

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani leo tarehe 12 Novemba, 2018 amevunja rasmi Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) iliyokuwa ikiongozwa na Dkt. Gideona Kaunda.

Uamuzi huo ameutoa katika Mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dodoma. Alisema kuwa, Bodi hiyo iliundwa mwaka 2017, kwa mujibu wa Sheria ya Wakala Vijijini Na.8 ya Mwaka 2005 (The Rural Energy Act. No.8 of 2005). 

“ Bodi hii imetekeleza majukumu yake kwa takriban mwaka mmoja (1) sasa na katika kipindi hicho ambapo Bodi hii imekuwepo, ninapenda kuwajulisha kwamba kwa ujumla sijaridhishwa na utendaji wake,” alisema Dkt Kalemani.Hivyo alieleza kuwa, kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu 9(3)(b) cha Sheria Na. 8 ya Nishati Vijijini ya 2005, ameamua kuivunja Bodi hiyo kwa kutengua uteuzi wa Mwenyekiti pamoja na Wajumbe wa Bodi.

Aliongeza kuwa, Bodi nyingine mpya itaundwa baadaye kwa mujibu wa Sheria ya Nishati Vijijini ya mwaka 2005. Bodi hiyo ilizinduliwa mwezi Aprili mwaka 2017 na ina wajumbe Saba.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuivunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua.

WAKUU WA MAGEREZA NCHINI WATAKIWA KUWA WABUNIFU UTATUZI WA NYUMBA ZA ASKARI

$
0
0
Na Lucas Mboje, Njombe

WAKUU wa Magereza yote nchini wametakiwa kuwa wabunifu ili kutatua changamoto ya uhaba wa makazi ya askari kwa kutumia nguvukazi ya wafungwa na rasilimali nyinginezo zilizopo katika maeneo yao.

Wito huo umetolewa leo Novemba 12, 2018 na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua magereza yote ya Mkoa wa Njombe ambayo yanaendeshwa na Jeshi hilo. Kamishna Jenerali Kasike amesema kuwa lazima wakuu wa magereza wawe wabunifu katika kutatua tatizo hilo la uhaba wa nyumba kwani Jeshi hilo linazo fursa nyingi ikiwemo nguvu kazi ya wafungwa.

“Mkoa wa Njombe na mingineyo nchini haipo sababu ya kuwa na tatizo la uhaba wa nyumba za askari kwani kuna fursa ya kutosha ya kufyatua tofali za kuchoma kwa kuwatumia wafungwa ili kumaliza tatizo hili nchini”. Amesisitiza Jenerali Kasike. Aidha, Kamishna Jenerali Kasike amewataka mafisa na askari wote kuendelea kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia maadili, sheria na kanuni mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo.

Awali, akisoma taarifa ya Gereza la Wilaya Njombe, Mkuu wa Gereza hilo, SP. Charls Mihinga amesema kuwa tayari wameanzisha mradi wa ufyatuaji wa tofali za kuchoma katika kambi ya mdandu ili kumaliza tatizo la uhaba wa nyumba za watumishi wa gereza hilo. “Katika msimu huu tumeweza kufyatua tofali kubwa zipatazo 30,000 ambazo tayari zimeshachomwa, tofali hizi zitatumika katika ujenzi wa nyumba za askari pamoja na ujenzi wa Ofisi mpya ya Mkuu wa Magereza Mkoani Njombe”. Alisema SP. Mihinga.

Pia, ameongeza kuwa malengo ya baadaye ni kuifanya kambi hiyo ya Gereza Njombe kuwa na taswira ya uzalishaji wa matofali kwa wingi kwa ajili ya kufanya biashara na hivyo kuongeza maduhuri serikalini.

Jeshi la Magereza linakabiliwa na uhaba wa nyumba za kuishi za Maafisa na askari hapa nchini, mkakati uliopo hivi sasa chini ya uongozi wa Kamishna Jenerali wa Magereza ni kuhakikisha kuwa tatizo hilo linatatulika kwa kutumia njia ya ubunifu pamoja na fursa mbalimbali zilizopo ndani ya Jeshi hilo. 
 Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike(wa kwanza kulia) akizungumza jambo alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Njombe. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo.
 Mkuu wa Gereza Njombe, SP. Charles Mihinga(kushoto) akimtembeza Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike(kulia) alipotembelea gereza hilo leo Novemba 12, 2018.
 Baadhi ya Askari wa Gereza la Wilaya Njombe  wakifuatilia maelekezo katika Baraza lililoongozwa na  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike ambapo askari hao wameelezea changamoto zao kiutendaji leo Novemba 12, 2018.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa na askari wa Gereza Njombe( Picha na Jeshi la Magereza).



RC MONGELLA ASISITIZA UMUHIMU WA MAADILI KATIKA JAMII

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella (kushoto) amefanya uzinduzi wa albamu ya Injili ya “Jerusalem Band” kutoka kanisa la EAGT Kiloleli chini ya Mchungaji Dkt. Jacob Mutashi, uliofanyika Novemba 11, 2018 katika ukumbi wa Belmont Fairmont Hotel Jijini Mwanza.

Mhe. Mongella ametumia fursa hiyo kusisitiza suala la maadili katika jamii na kukemea viashiria/ vitendo vya mapenzi ya jinsia moja (ushoga).
Tazama Video hapa chini

BASATA YAUTAKA UONGOZI WA WCB KUFUTA WIMBO WA 'MWANZA' KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KABLA YA SAA KUMI KAMILI JIONI LEO

$
0
0
Na Agness Francis, blogu ya Jamii

BARAZA la sana Taifa (BASATA) limeufungia rasmi leo Novemba 12 mwaka huu wimbo Ujulikanao kwa jina la Mwanza ulioimbwa na msanii wa lebo ya Wasafi Raymond Mwakyusa, maarufu Kama Rayvanny. 

Ambapo wimbo huo wa Mwanza alimshirikisha msanii mwenzake Naseeb Abdul (Diamond Platinumz). 

Amesema hayo Katibu wa baraza la sana Taifa Geofrey Mngereza kuwa baraza limeamua kuufungia wimbo huo kutokana na ukiukwaji wa maadili ya kitanzania kwa msanii Rayvanny kutumia maneno yanayohasisha ngono katika wimbo huo. 

Mgereza amesema pamoja na kuufungia wimbo huo baraza linawaonya wasanii hao, vyombo vya habari ama mtu yoyote kutoutumia kucheza au kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. 

"Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa sheria la Baraza namba 23 ya mwaka 1984 na kanuni zake limepewa mamlaka ya kusimamia Sanaa, wasanii na mtu yoyote anayejishughulisha na kazi za sana hapa Nchini"amesema Mngereza. 

Katibu huyo amesema kuwa Baraza hilo linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny,Diamond pamoja na Uongozi wa Wasafi Limited na kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuunda kazi za sanaa. 

"Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi, sambamba na onyo hili pia Baraza linawakumbusha wasanii chini ya Wasafi kutoutumia wimbo huo na nyimbo zingine zilizofungiwa kwa namna yoyote ile "amesema katibu Mngereza. Vile vile Baraza hilo limewataka WCB kuondoa wimbo huo mara moja kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kufika saa kumi kamili jioni ya Leo.
Wasaniii Ray Vany na Diamond Platinumz

WATALAAM KUTOKA MUHIMBILI WAWASILI LINDI KUTOA HUDUMA ZA AFYA

$
0
0
Madaktari Bingwa 11 pamoja na wataalam wengine wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) wamewasili katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi Sokoine kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali za afya kwa wananchi wa mkoa huo sanjari na kuwajengea uwezo wataalam wa hospitali hiyo.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi kutoka MNH Geofrey Marandu amesema lengo la ujio wao katika hospitali hiyo ni kuwaongezea ujuzi watalaam wa hospitali za rufaa za mikoa nchini kupitia madaktari bingwa wa Muhimbili lakini pia kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa Muhimbili.

‘’Hospitali imeweka mkakati wa kuzitembelea hospitali mbalimbali za rufaa za mikoa nchini ili kushirikiana nao katika kutoa huduma za afya na kuwajengea uwezo , lakini pia kama Muhimbili tunatekeleza agizo la serikali linaloelekeza kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibwa nje ya nchi hatua ambayo tayari MNH inaitekeleza hivyo utoaji wa huduma za fya kwa njia ya mkoba utasaidia kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda Muhimbili endapo wangepewa rufaa ya kwenda kutibiwa huko’’.amesema Dkt. Marandu.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine Dkt. Jumanne Shija amesema ujio wa watalaam wa afya wakiwemo Madaktari Bingwa utainufaisha hospitali hiyo kwakua watalaam wake watajengewa uwezo kiutendaji na kupata ujuzi wa kutosha.Ametaja maeneo ambayo wataalam wa hospitali ya Sokoine watanufaika na kujengewa uwezo ni upasuaji, magonjwa ya kike na uzazi, meno, macho, watoto, magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya koo ,pua na masikio pamoja na masuala ya maabara.

Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi Sokoine kwa ajili ya kutoa huduma za afya na kuwajengea uwezo watalaam wa hospitali hiyo.
Madaktari Bingwa wa MNH pamoja na Madaktari wa Hospitali ya Sokoine wakiwa katika kikao cha asubuhi cha kiutendaji kabla ya kuanza kutoa huduma.
Wauguzi wa hospitali hiyo wakiwa katika kikao cha asubuhi kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya utoaji huduma za afya.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi Geofrey Marandu akizungumza na mgonjwa ambaye amefika leo katika Hospitali ya Sokoine kwa ajili ya kupata huduma.

Dokta Willybroad Massawe ambaye ni Dkt. wa upasuaji , pua , koo na masiko (kushoto) pamoja na muuguzi Monica Mngoya (kulia) wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimpatia maelezo mgonjwa ambaye amefika kwa ajili ya kupata huduma za afya.

Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Lindi ambao wamejitokeza katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi Sokoine wakisubiri kupatiwa huduma hii leo.
 

FLY YOUR IDEAS STUDENTS COMPETITION

$
0
0
The United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization (UNESCO) in collaboration with the Airbus have prepared 6thFly Your Ideas (FYI) Competition.

The competition needs the students across the world to develop new ideas using the latest digital technologies to create smart solutions for a safer, cleaner and better connected world aimed at contributing to an eco-efficient aviation industry of the future.


The competition is open to students who studying bachelor, masters or PHD degree in any academic discipline.


The competition will involve several rounds concluding with live final where up to 6 finalist teams will present their ideas to a jury of experts for a chance to win a share of €45,000.


The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation call upon students around the country to participate in the competition which its registration deadline is on 16th November 2018 and the final will be in May-June 2019.


For more information about the Competition, Please visit: https://www.airbus-fyi.com


For inquiries, you can contact Rovani Sigamoney, Engineering Specialist of the capacity-building in Science and Engineering Section (email: r.sigamoney@unesco.org; tel +33145682237).   


Issued by;

Government Communication Unit,

Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,

Dar es Salaam.

12 November  2018.


MWENYEKITI UVCCM AFUNGUA SEMINA YA KIMKAKATI KWA VIONGOZI NA WATENDAJI WAKE

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chma Cha Mapinduzi Ndg Kheri Denis James akizungumza wakati akifungua Semina ya Kimkakati ya Siku Saba kwa Viongozi na Watendaji wa UVCCM Ngazi ya Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM akizungumza wakati wa Kumkaribisha Mwenyekiti kufungua Semina hiyo
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala akitoa Ufafanuzi kuhusu lengo la Mafunzo haya.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Comred Kheri Denis James (kulia|) pamoja na Makamu Mwenyekiti Comred Thabia Mwita  wakifurahia jambo pamoja na Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Comred Hassan Bomboko leo mara baada ya Ufunguzi waSemina ya Kimkakati ya Siku Saba kwa Viongozi na Watendaji wa UVCCM Ngazi ya Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dodoma.(Picha zote na Fahadi Siraji wa Uvccm)
Picha ya Pamoja ya Viongozi washiriki wa Semina ya Kimkakati ya Siku Saba kwa Viongozi na Watendaji wa UVCCM Ngazi ya Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dodoma. (Picha zote na Fahadi Siraji wa Uvccm).

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI SABA (7) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kuwaapisha Viongozi saba wakiwemo Mawaziri wawili, Naibu Mawaziri wanne, pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mwita Waitara kuwa Naibu Waziri  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Joseph Kakunda kuwa Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Mary Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Constantine Kanyasu kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Japhet Ngailonga Hasunga kuwa Waziri wa Kilimo Ikulu jijini Dar es Salaam huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma wakishuhudia tukio hilo. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Innocent Bashugwa Naibu Waziri wa Kilimo Ikulu jijini Dar es Salaam huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma wakishuhudia tukio hilo. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Mstaafu January Msofe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria.
 Viongozi mbalimbali waliopishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakila Kiapo cha Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kulia ni Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga, Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Mary Mwanjelwa, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu, Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashugwa, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mwita Waitara pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mstaafu January Msofe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ngugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Kamishna wa Maadili Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela pamoja na Viongozi mbalimbali waliopishwa pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU

MAHAKAMA YAMPA NAFASI YA MWISHO MBUNGE MSIGWA KUTAFUTA WAKILI WA KUMTETEA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa nafasi ya Mwisho kwa Mshtakiwa Peter Msigwa ambaye in Mbunge wa Iringa Mjini kutafuta wakili wa kumtetea katika kesi ya uchochezi inayomkabili pamoja na viongozi wenzake nane wa Chadema ma sivyo, Mahakama itaendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo bila uwepo wa wakili wake.

Msigwa pia ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anatukanwa Kisheria na mawakili wa upande wa mashtaka kwa sababu mawakili wake wanajitoa kumtetea.Hatua hiyo imefikwa leo Novemba 12. 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuanza kwa usikilizwaji wa upande wa mashtaka ambao walidai mahakamani hapo kuwa wako tayari kwa kuendela na hatua hiyo na kwa leo walikuwa na shahidi mmoja.

Msigwa amepewa nafasi hiyo ya mwisho baada ya wawakili wake wawili waliokuwa wawili waliokuwa wakimtetea kujitoa kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa kesi.Mchungaji Msigwa ameeleza hayo baada ya wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi kudai kuwa inaonekana Msigwa amepanga njama ili mawakili wake wajitoe.

Kutokana na hatua hiyo, Msigwa alisimama na kueleza kuwa anaona Wakili wa Serikali kama anamtukana kisheria na kumnyanyapaa."Hakimu wewe ni shahidi mawakili wangu wamejitoa kwa sababu ya kutoridhishwa na mwenendo wa kesi, wakili wa serikali hana haki wala haimuhusu kuhusu mawakili wangu,"ameeleza.Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri amesema ni haki ya Kikatiba kwa mshtakiwa kuwakilishwa na Wakili, lakini anatoa nafasi ya mwisho kwa Msigwa na akishindwa ataonekana amefanya makusudi na kesi itaendelea bila ya yeye kuwa na wakili

BENKI YA MAENDELEO TIB YATOA FEDHA KUSAIDIA UJENZI WA VITUO VYA MABASI MKURANGA NA KAHAMA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

BENKI ya Maendeleo (TIB) imesaini mikataba ya msaada wa kiufundi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga  na Halmashauri ya Mji wa Kahama  na kwa mujibu wa mkataba huo benki ya TIB itatoa jumla ya shilingi 873,000,000 ili kusaidia Halmashauri hizo mbili kulipia gharama za wataalamu washauri watakaofanya upembuzi yakinifu na pia kuandaa michoro na makisio ya gharama na nyaraka za zabuni kwa ajili ya vituo vipya vya mabasi vitakavyojengwa kwenye Halmashauri hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makubaliano hayo Kaimu Mkurugenzi uendeshaji wa Benki ya TIB Patrick Mongela amesema kuwa lengo la mkataba huo ni kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo ina manufaa kwa jamii na taifa kwa ujumla, amesema kuwa wao kama Benki hawatoi mikopo pekee pia wanasimamia kikamilifu miradi ya kimaendeleo katika maendeleo ya jamii.

Amesema kuwa katika miradi hiyo Wilaya ya Mkuranga imepata jumla ya shilingi milioni 409.5 na kituo cha mabasi kitajengwa katika kijiji cha Kipala Mpakani na kituo hicho kitahudumia mabasi yaendayo Mikoa ya Kusini ikiwemo Lindi, Mtwara na Ruvuma na kwa upande wa Mji wa Kahama kituo cha mabasi kitakachojengwa kitarahisisha usafiri kwa wakazi wa Shinyanga, Singida, wakazi wa ukanda wa ziwa Victoria pamoja na nchi za Burundi, Rwanda na Uganda.

Mongela amesema kuwa miradi itakayonufaika na mikataba hiyo  ni miongoni mwa miradi ya kimkakati inayopewa kipaumbele na Serikali ya awamu ya tano, na mradi utakaojengwa Wilayani Mkuranga ni moja ya miradi inayopangwa kutekelezwa na Serikali ili kuweza kusaidia kupunguza msongamano katika barabara za Dar es salaam.
 Kaimu Mkurungenzi wa Benki ya Maendeleo (TIB) Patrick Mongela akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utiaji wa saini za makubaliano baina ya Benki hiyo na Halmashauri za Mkuranga na Kahama katika utekelezaji ya mradi wa ujenzi wa vituo vya mabasi katika Halmashauri hizo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbeto Sanga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuingia maakubaliano hayo na Benki ya maendeleo TIB ambapo Halmashauri hiyo imepata takribani shilingi milioni 490.2 ambazo zitatumika katika ujenzi wa kituo cha mabasi katika kijiji cha Mpala Mpakani Wilayani humo.
Mkurugenzi wa Manispaa  ya Kahama Anderson Msumba akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya makubaliano hayo ambapo jumla ya shilingi milioni 382.5 zilizotolewa na Benki ya maendeleo (TIB) zitatumika kujenga kituo cha basi katika mji wa Kahama. (Picha na Erick Picson, Blogu ya jamii).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

OBREY CHIRWA AANZA KUJIFUA AZAM FC

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MSHAMBULIAJI mpya wa Klabu ya Azam FC, Obrey Chirwa, leo asubuhi ameanza kufanya mazoezi kwa mara ya kwanza kwenye timu yake hiyo mpya.

Staa huyo wa zamani wa Yanga na FC Platinum, amejiunga na Azam FC akitokea Nagoon ya Misri kwa usajili huru baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na timu hiyo.

Chirwa amejumuika mazoezini kwa mara ya kwanza na wenzake, wakati timu hiyo ikianza rasmi kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) dhidi ya Ruvu Shooting utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Novemba 22 mwaka huu.

Kwa mara nyingine tena Cirwa anaungana na rafiki yake wa siku nyingi, Donald Ngoma, ambaye walicheza naye Platinum ya Zimbabwe kwa takribani miaka sita kabla ya kufanya tena kazi pamoja wakiwa Yanga na sasa Azam FC, mara zote mbili hapa Tanzania wakiunganishwa na Kocha Mkuu, Hans Van Der Pluijm, ambaye kwa sasa anaifundisha Azam FC.

Mazoezi hayo yaliyosimamiwa na Kocha Pluijm, yalikuwa ni makali lengo kuu ni kurudisha ufiti kwa wachezaji baada ya mapumziko ya takribani siku sita.

Aidha mazoezi hayo yalihudhuriwa na wachezaji wote ukiondoa sita waliojiunga na timu za Taifa, nahodha Agrey Moris, Abdallah Kheri, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mudathir Yahya, Yahya Zayd (wote Taifa Stars) huku Nickolas Wadada akiwa na Uganda ‘The Cranes’.

Nyota mwingine Tafadzwa Kutinyu, ambaye alikuwemo mazoezini leo anatarajia kujiunga na timu ya Taifa ya Zimbabwe muda keshokutwa Jumatano.

Wakati mechi za ligi zikielekea raundi ya 14, kikosi cha Azam FC hadi sasa kinashika usukani kikiwa na pointi 30 baada ya kushinda mechi tisa na sare tatu huku wakiwa hawajapoteza mchezo wowote na nyavu zikitikiswa mara mbili tu.
Mshambuliaji mpya wa Azam Fc Obrey Chirwa akiwa katika mazoezi ya pamoja na klabu yake mpya hiyo kujiandaa na ligi kuu Tanzania Bara (TPL)

HATMA YA DHAMANA MWENYEKITI WA CHADEMA NA MBUNGE WA TARIME KUJULIKANA NOVEMBA 23,2018

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema Novemba 23.2018 itatoa uamuzi wa kumfutia dhamana ama la Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko baada ya wiki iliyopita kutoa amri ya kukamatwa kwa washtakiwa hao kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Hatua hiyo imekuja baada ya watuhumiwa hao kufika mahakamani wenyewe na kujieleza.

Akitoa maelezo yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, Mbowe amedai kuwa anaiheshimu mahakama sana na anatambua kama kiongozi na kama raia nafasi ya Mahakama katika kusimamia haki kwenye taifa.

Amesema, ni ukweli usiopingika kuwa yeye na washtakiwa wenzake ni viongozi na wana majukumu mengi ya kiungozi ya kutendaji ndani na nje ya nchi.

Mbowe ameeleza kuwa Oktoba 28, alisafiri kwenda Washington DC kwenye mkutano wa Oktoba 30, mwaka huu na kwamba kwa ratiba yake alistahili kuondoka huko Oktoba 30, usiku na kurejea Dar es Salaam Oktoba 31 kwa ajili ya kuendelea na Kesi Novemba Mosi, mwaka huu lakini bahati mbaya kabla hajaanza safari hiyo alipata matatizo ya ugonjwa ambapo kwa mazingira aliyokuwepo haikumruhusu kusafiri safari ndefu ya ndege kwa ushauri wa kitabibu na miiko ya kinachomsumbua.

Ameongeza, katika jitihada za kujaribu kupata Matibabu nchini Marekani zilikwamishwa na bima yake ya Matibabu ya kimataifa kwa sababu nilikuwa ikimruhusu kutibiwa katika nchi ambazo siyo Marekani wala ulaya bali inaruhusu atibiwe kati nchi za Afrika mashariki, Afrika Kusini na Dubai.

Amedai kufuatia hivyo, ilimlazimu kutafuta miadi kwenda kwenye Matibabu katika nchi za Emirate na kwamba hiyo ni kutokana na ushauri aliopewa mbali na bima, kutokana na utofauti wa Masaa kati ya matano iwapo atatoka alipo kwenda Dubai kwamatibabu na ni zaidi ya 24 iwapo angekuwa nchini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

RAIS ATANGAZA SERIKALI KUNUNUA KOROSHO ZOTE ZA WAKULIMA

$
0
0




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati akitangaza uamuzi wa Serikali kununua korosho zote za wakulima msimu huu kwa bei ya shilingi 3,300 kwa kilo baada ya wanunuzi binafsi kushindwa kutimiza maagizo ya Serikali kwa kuanza kununua kwa kusuasua na kwa bei isiyoridhisha.


uamuzi wa akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kuwaapisha Viongozi saba wakiwemo Mawaziri wawili, Naibu Mawaziri wanne, pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Ikulu jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA MISA YA SHUKURANI YA UHAI YA RAIS MSTAAFU BENJMANIN MKAPA KUTIMIZA UMRI WA MIAKA 80

$
0
0




Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimpa zawadi ya kadi na kisha kumpongeza Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa akiwa na mkewe Mama Anna Mkapa kwa kutimiza umri wa miaka 80 katika Misa ya Shukurani ya uhai iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2018
Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa pamoja na Maaskofu wakati wa Misa ya Shukrani kwa Mhe. Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2018
Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongea kwa furaha na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa baada ya Misa ya Shukurani kwa Mhe. Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2018
Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Misa ya Shukurani ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2018. Kulia kwa Mhe. Mkapa ni mkewe Mama Anna Mkapa

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA WILAYA YA SAME NA MWANGA LEO

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hakuna Maendeleo pasipo Utawala bora.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mwanga mkoani Kilimanjaro.

“Viongozi wa Halmashauri, Viongozi wa Wilaya wasipokuwa na Utawala bora, wasiposhirikiana, Chama, Serikali, Wilaya, Halmashauri tusitegemee kuwa na maendeleo tutalalamika siku zote” alisema Makamu wa Rais. Leo katika ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo Makamu wa Rais alitembelea miradi mbali mbali katika Wilaya ya Same na Mwanga.

Akiwa Wilayani Same, Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya New Dawn, Shule ambayo itakuwa ya mchepuo wa masomo ya sayansi na ni maalum kwa Watoto wenye mahitaji maalum na Yatima pamoja na kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ofisi za Wakala wa Misitu Wilaya ya Same.

Makamu wa Rais amewahimiza Wakala wa Misitu nchi kuwapa wananchi miche ya kutosha na kuimarisha ulinzi katika hifadhi ya misitu. Akiwa Wilayani Mwanga, Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji Same-Mwanga-Korogwe ambao awamu ya kwanza imekamilika kwa asilimia 76%.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji Same-Mwanga-Korogwe,pichani kulia ni 
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Clelia Felician wa kampuni ya M.A Kharafi & Sons wakati alipotembelea mradi mkubwa wa maji wa Same –  Mwanga – Korogwe ambao awamu ya kwanza imekamilika kwa asilimia 76%. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Sehemu ya Miundombinu ya Mradi wa Maji Same-Mwanga-Korogwe ambao asilimia 76% imekamilika. wanga-Korogwe ambao asilimia 76% imekamilika. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya (katikati) muda mfupi kabla ya mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Mwanga kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira . Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Kilimanjaro. 

Msaada wa Tshs. 86 Mil kunufaisha Wagonjwa wa Saratani ya Koo Muhimbili

$
0
0

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa vifaa tiba aina ya Stents vyenye thamani ya Tshs. 86.2 milioni kutoka kampuni ya Boston Scientific ya Marekani kwa ajili ya wagonjwa wenye tatizo la saratani ya koo la chakula. 

Stents ni vifaa maalum mithili ya springi ambavyo vinaweza kuwa vya plastiki au chuma vyenye uwazi katikati wanavyowekewa wagonjwa wenye uvimbe kwenye koo lililoziba ili kupanua sehemu hiyo na kuruhusu kupitisha chakula. Kuna stents za aina mbalimbali kutegemeana na mgonjwa ana shida ya aina gani. 

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini, Dkt. Masolwa Ng’wanasayi amesema kampuni hiyo imetoa stents 25 ambazo zitatumika kwa wagonjwa 25 wenye satarani ya koo la chakula ili kuwasaidia kumeza chakula na kuendelea na matibabu ya mionzi. 

“Mgonjwa mwenye tatizo la saratani ya koo la chakula, anakuwa hawezi kumeza chakula na hali hii inasababisha mgonjwa kupungua uzito na kushindwa kuendelea na matibabu mengine, hivyo vifaa hivi vitawasaidia kumeza chakula na kuendelea na matibabu mengine,” amesema Dkt. Ng’wanasayi. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Hopitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akipokea kifaa tiba cha aina ya STENTS kwa ajili ya wagonjwa wenye tatizo la saratani ya koo la chakula kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Boston Scientific ya Marekani, Troy Lengel. Wengine kushoto ni wawakilishi kutoka hospitali ya Muhimbili, Mayo Clinic ya Marekani na Chuo Kikuu cha San Francisco nchini Marekani na kulia ni wawakilishi kutoka MUHAS na Hospitali ya Muhimbili.
Pichani ni vifaa tiba aina ya STENTS ambavyo wagonjwa wenye tatizo la saratani ya koo la chakula wameanza kuwekewa ili kuwasaidia kumeza chakula kutokana na mfumo wa koo kuharibiwa na ugonjwa huo. 

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images