Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

TAASISI YA IMETOSHA YATOA MSAADA KWA MWENYE UALBINO ALIYEPATA UPOFU WA MACHO SHINYANGA

$
0
0
Taasisi ya Imetosha ya Jijini Dar es salaam imemtembelea na kumpatia msaada bwana Charles Kulwa Jagadi (41) mwenye Ualbino mkazi wa kijiji cha Mhunze kata ya Kishapu wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ambaye amepata upofu wa macho kutokana na ugonjwa wa saratani ya macho unaomsumbua uliopelekea jicho moja kung’olewa.

Mtendaji Mkuu wa Imetosha Foundation,Henry Mdimu aliyefika nyumbani kwa Jagadi leo Jumapili Novemba 11,2018 amesema taasisi yake imeguswa na hali ngumu ya maisha anayopitia Jagadi hivyo kuamua kumjengea kibanda cha kufanyia biashara ya mkaa ili kumsaidia katika maisha yake.
Alisema Imetosha Foundation kwa kushirikiana na Dar Marathon Club ya jijini Dar es salaam wameamua kuchangishana fedha kwa ajili ya kumsaidia Jagadi ili aweze kuendesha familia yake yenye watoto sita wote wakiwa na ualbino.

“Niliona picha ya Jagadi mtandaoni,baada ya mmoja wa watu wenye mapenzi mema kuipost kuonesha jinsi ndugu yetu anavyopitia wakati mgumu baada ya kupata upofu wa macho,nimeamua kuja kumuona na tayari tumemjengea kibanda kwa ajili ya kufanyia biashara ya mkaa ambayo amekuwa akifanya ili kupata kipato kuendesha familia yake”,alieleza Mdimu.
Mtendaji Mkuu wa Imetosha Foundation,Henry Mdimu (wa pili kulia) akijitambulisha kwa Charles Kulwa Jagadi (kulia).Wa kwanza kushoto ni mke wa Jagadi Esther Shija akifuatiwa na Mratibu wa Imetosha Foundation Kanda ya Ziwa,Janeth Chijanga.

“Nimetoka Dar es salaam kuja kumuona na kujionea hali halisi ya maisha yake,huyu ni baba mwenye mke na watoto sita,sasa haoni,tunaamini kibanda hiki kitamsaidia kuingiza kipato ili kuisaidia familia hii”,aliongeza Mdimu.

Alisema pia wamempatia magunia 18 ya mkaa kwa ajili ya biashara na kuahidi kuwasomesha watoto wawili kati ya 6 na kuahidi kutafuta kiwanja kwa ajili ya kuijengea nyumba familia hiyo ambayo inaishi kwenye nyumba ya kupanga.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI ZAIDI

RPC ARUSHA ATOA AHADI YA “KUMWAGA” VIFAA VYA TAEKWONDO

$
0
0
Nahodha wa timu ya Taekwondo ya Polisi Arusha Yohana Nicodem akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Nane Nane Taekwondo Club Championship Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Arusha (SACP) Ramadhani Ng'anzi mara baada ya timu hiyo kuwasili ofisini kwake.

Baada ya kuchukua ubingwa wa Nane Nane Championship ulioshirikisha timu kumi kati ya hizo tatu toka nchini Kenya, timu ya Taekwondo ya Polisi Arusha imeahidiwa vifaa vilivyokosekana katika Gym lao ili liweze kukamilika kila idara. Ahadi hiyo ilitolewa jana asubuhi na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi mara baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa huo toka kwa timu hiyo.

“Pamoja na changamoto kadhaa lakini mlitambua umuhimu wa mashindano hayo na mlionyesha uzalendo wa hali ya juu ambao umesaidia kuliwakilisha vyema Taifa letu na Jeshi la Polisi kwa kupata ubingwa ambao umekuwa fahari yetu sote, hivyo mimi kama mlezi wa timu hii naahidi kuendelea kutoa vifaa vya mazoezi ili liweze kukamika” Alisema Kamanda Ng’anzi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng'anzi akinyanyua kombe juu mara baada ya kukabidhiwa na nahodha wa timu ya Polisi Arusha Taekwondo askari Polisi Yohana Nicodem (kushoto kwake) huku wachezaji wengine wakishangilia.

Kwa upande wake Mwalimu wa timu hiyo Master shija Shija alisema ushindi wa timu hiyo ulitokana na nidhamu, kujituma kwa wachezaji lakini pia kufuatilia maelekezo yake.

“Hawa ni askari huwa wanatii na kuheshimu kila wanachoelekezwa lakini pia uungwaji mkono wa Kamanda wa Polisi umekuwa chachu ya ushindi kwani wachezaji wamekuwa na morali ya hali ya juu” Alisema Master Shija.

Kwa upande wake askari wa kike Edith Msafiri, alisema kwamba anajisikia furaha sana kushiriki mchezo huo kwa kuwa unamsaidia katika kazi yake kutokana na ujuzi alioupata na anaoendelea kuupata unaomuwezesha kupambana na wahalifu bila hata kulazimika kutumia silaha.

Timu hiyo ilichukua ubingwa huo katika mashinadano yaliyofanyika tarehe 3 na 4 mwezi huu katika ukumbi wa Triple A kwa kupata Medali 27 kati ya hizo Nane zilikuwa za Dhahabu, Saba za Fedha na 12 za Shaba wakati nafasi ya Pili na Tatu ilichukuliwa na Kilifi na Regional zote za nchini Kenya. 

Aidha Kamanda Ng,anzi alisema mbali na kuwepo kwa timu hiyo pia Jeshi la Polisi mkoani hapa limeanzisha Programu ya kushirikisha askari wote kila Ijumaa ili kila mmoja ashiriki katika mchezo anaoutaka kama vile riadha, Mpira wa miguu, Mpira wa Pete, kunyanyua vyuma “Gym” na kadhalika  kwa nia ya kuimarisha afya zao.
Askari wa kike wa timu ya Taekwondo ya Polisi Arusha Eva Laswai akipiga " Kick Pad Target" iliyokuwa juu zaidi ya kichwa chake kwa teke huku Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (SACP) Ramadhani Ng'anzi akimshuhudia.
Askari wa kike Edith Msafiri (Kushoto) akionyesha umahiri wa kukwepa na kupangua teke la askari mwenzake Eva Laswai katika mpambano usio rasmi uliofanyika Makao Makuu ya Polisi Arusha kabla ya kumkabidhi kombe la ubingwa mlezi wa timu ya Arusha Polisi Taekwondo Kamanda wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng'anzi. Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha

BARAZA LA WADHAMINI YANGA LATOA TAMKO NAFASI YA MANJI HAIJAZWI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Baraza la Wadhamini wa Yanga limetoa msimamo wake wa kumtambua Yusuf Manji kama Mwenyekiti wa Klabu hiyo.

Uamuzi huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Mkuchika akionesha barua aliyojibiwa na Manji baada ya kurejea kwake Yanga.Akizungumza na waandishi wa habari Jioni hii katika Makao Makuu ya Klabu ya Yanga, George Mkuchika amesema kuwa baada ya mkutano mkuu wa Yanga uliohudhuriwa na wanachama takribani 4500 uliamua kwa pamoja kukataa kujivua uongozi kww Yusuf Manji.

Mkuchika amesema kuwa, baada ya uamuzi huo wa wanachama waliamua kumuandikia barua Manji na aliwajibu hawezi kukataa maamuzi ya wanachama ila atarejea kuanza kazi rasmi Januari 15 2019.Amesema kuwa, katika barua yake aliyojibiwa Manji aliandika kuwa kutokana na ushauri wa daktari uliomtaka akae nje mpaka Desemba 15 kwa ajili ya matibabu ameomba kuanza majukumu rasmi ya kuitumikia klabu hiyo Mwakani.

"Ni kweli mimi nilimuandikia barua Yusuf Manji baada ya maamuzi ya wanachama katika Mkutano Mkuu ya kutokubali kujiuzulu kwake na akanijibu mimi Mkuchika kuwa hawezi kupingana na maamuzi ya wanachama ww Yanga ila ameomba kwanza amalizie tiba kama alivyoelekezwa na daktari kuwa kufikia Desemba 15 atakuwa ameshamaliza matibabu na kazi rasmi ataanza Januari 15, 2019,"amesema Mkuchika.

Akiongelea suala la uchaguzi wa Yanga na nafasi zinazotakiwa kujazwa, Mkuchika amesema kwakuwa Mwenyekiti bado yupo hivyo nafasi yake haitajazwa na amewaomba kamati ya utendaji ya Yanga kuwasilisha barua hiyo kwa TFF ili kuwapa uthibitisho.

"Sisi kama Baraza la wadhamini tunafurahi sana kuona Yanga inafanya uchaguzi tena ni jambo la faraja kwani taasisi kama Yanga haiwezi kuendeshwa bila ya kuwa na uongozi, ila tumesikia kuwa TFF wameamua kutaka kusimamia uchaguzi huu kupitia kamati yao jambo ambalo linavunja katiba ya Yanga, " amesema Mkuchika.

Amesema kuwa, katiba ya Yanga inaruhusu kamati tendaji iliyopo kuchagua kamati ya uchaguzi na inaelekeza hivyo kwahiyo TFF kuchagua kamati yake na kwenda kinyume na maagizo ya Baraza la Michezo Taifa (BMT) sio sahihi, wanachofahamu BMT waliagiza TFF wakae meza moja na Yanga wajadiliane.Kutokana na hilo Baraza limetoa ushauri kwa kamati ya utendaji wa Yanga kukaa meza moja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kujadili uchaguzi wa klabu hiyo.
Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini Yanga George Mkuchika akionesha barua aliyojibiwa na Yusuf Manji.

KANISA HILI TOKA MWAKA 1904 MPAKA LEO LINATUMIKA...

BALOZI WA JAPAN ATEMBELEA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

$
0
0
Na.Alex Sonna,Dodoma

Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto ametembelea eneo la mji wa Serikali kwa dhumuni la kuona maendeleo ya ujenzi wa miondombinu pamoja na kiwanja kilichotengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za ubalozi huo, jiji Dodoma.

Akizungumzia ziara ya balozi huyo, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwini Kunambi, amesema kuwa zaidi ya mabalozi 20 wameshafika Dodoma kujionea maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi zao.

“Balozi wa Japan amekuja kuona eneo ambalo ubalozi wa nchi yake utajengwa, pamoja hilo amekuja miondombinu ambayo inaendelea kujengwa," ameeleza Kunambi.Aidha Kunambi amesema kuwa Jiji la Dodoma lipo kwenye ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhia maji kwenye eneo hilo ambalo litakuwa na ujazo wa lita milioni moja.

Hata hivyo amesema kuwa ujenzi huo utakamilika Januari mwakani kwa lengo la kusambaza maji kwenye eneo la mji wa serikali kabla ya kufikiwa na miundombinu ya Mamlaka ya Majisafi ya Jiji la Dodoma (DUWASA).Mkurugenzi huyo aliwahakikishia watumishi wanaohamia Dodoma kuwa huduma muhimu zinapatikana ikiwemo maji kwani wanazalisha lita 61,000 kwa siku huku mahitaji yakiwa lita 48,000.
Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwini Kunambi alipotembelea ofisini kwake kabla hajaenda kukagua eneo ambapo zitajengwa ofisi za ubalozi wa Japan
Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto akiangalia mchoro wa ramani wa eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Ubalozi wa Japan Mkoani Dodoma baada ya kufanya ziara ya kukagua.
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwini Kunambi akisisitiza jambo kwa Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto baada ya kufanya ziara ya kukagua eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani Jijini Dodoma
Baada ya kumaliza kukagua eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani Jijini Dodoma Balozi wa Japan akiwa na Mkurugenzi wanaelekea katika kupanda gari 
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhia maji kwenye eneo hilo ambalo litakuwa na ujazo wa lita milioni moja.

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia mpunga uliovunwa tayari wa Bw. Emmanuel Paschal(kushoto) wakati alipotembelea Skimu ya Umwagiliaji ya Lower Moshi katika eneo la Mabogini ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua na kuhimiza shughuli za kimaendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wakulima wa mpunga alipotembelea Skimu ya Umwagiliaji ya Lower Moshi katika eneo la Mabogini ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua na kuhimiza shughuli za kimaendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia aina mbali mbali za kahawa wakati wa maandalizi ya kujaribiwa kwenye maabara ya shamba ya Kahawa la Kilimanjaro Plantation Ltd. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia aina mbali mbali za kahawa wakati wa maandalizi ya kujaribiwa kwenye maabara ya shamba ya Kahawa la Kilimanjaro Plantation Ltd. 
21
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa Uru Kusini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Polisi Uru. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo. 
6
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa Polisi Uru Kusini.Makamu wa Rais yupo mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za Maendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI KUJADILI MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA JIJINI DODOMA

$
0
0

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akiteta jambo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Frolens Luoga, nje ya viwanja vya Bunge, Jijini, Dodoma, baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, kujadili  Muundo na Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018, unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni siku chache zijazo.
2
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. David Silinde (Mb), akimwonesha Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kijitabu cha Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha, wakati kamati hiyo ilipokutana na Waziri huyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi (Mb)  na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga, kujadili Muundo na Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018, utakaowasilishwa kwa hati ya Dharura katika Bunge linaloendelea Jijini Dodoma
3
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Geroge Simbachawene (Mb), akizungmza jambo wakati kamati yake ilipokutana na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi (Mb) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, na wataalamu wa Sera na Uchumi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma, kujadili Muundo na Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018.
4
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Andrew Chenge (Mb) na Prof. Anna Tibaijuka (Mb) wakifuatilia kwa makini mjadala wa Muundo na Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018, unaotarajiwa kuwasilishwa na Wizara ya Fedha na Mipango, Bungeni, Jijini Dodoma, siku chache zijazo.
9
Mjumbe wa Kamati ta Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hussen Bashe, akichangia hoja wakati kamati hiyo ilipokutana na Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kujadili Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha ya Mwaka 2018,  unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni wakti wa vikao vya Bunge vinavyoendelea Jijini Dodoma
8
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi (Mb) (katikati) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, wakiandika hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, kuhusu Muswada wa Sheria Ndogo za Fedha unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma, siku chache zijazo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

PUMA ENERGY TANZANIA YATUMIA KLABU YA WANAFUNZI USALAMA BARABARANI KUTOA ELIMU, ZAWADI ZA MADAFTARI,MABEGI NA KALENDA KWA MADEREVA

$
0
0
*Lengo ni kukumbusha na kusisitiza umuhimu wa wadau kuzingatia sheria za usalama barabarani, wanafunzi watoa neno

KLABU ya Usalama barabarani ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge wametoa elimu ya usalama wa barabarani kwa madereva wa magari na bodaboda kuzingatia sheria za usalama barabarani haswa vivuko vya watembea kwa miguu ili kuepusha ajali na vifo.

Pia wametoa elimu hiyo wanafunzi hao wametoa zawadi ya madaftari,kalenda na mabegi ya shule yenye jumbe mbalimbali zinahusu masuala ya usalama barabarani kwa madereva mbalimbali kama sehemu ya kuhakikisha elimu ya usalama barabarani inafika kila mahali.

Wanafunzi hao 18 ambao ni mabalozi wa usalama barabarani kutoka kwenye Klabu hiyo wametoa elimu hiyo na zawadi hizo Novemba 10, 2018 wakiwa kwenye Kituo cha Mafuta cha Puma kilichopo Upanga jijini Dar es Salaam ambapo madereva waliofika kuweka mafuta walikuwa wakipewa elimu hiyo inayohusu usalama barabarani.

Akizungumza wakati wa utoaji elimu kwa madereva, Rosenice Senyandumi ambaye ni Mwanafunzi wa shule hiyo amesema ajali za barabarani zimekuwa zikikatisha uhai wa binadamu wasio na hatia wakiwemo wanafunzi na mara nyingi huchangiwa na madereva wazembe.

"Ajali za barabarani zinapunguza nguvu kazi ya Taifa na kuathiri watoto kwa kuwa wengi hupoteza wategemezi wao na wakati mwingine watoto wenyewe kupoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali," amesema.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah akishuhudia wakati wanafunzi kutoka Klabu ya Usalama barabarani ya Shule ya Msingi Bunge Raymond Chuwa kulia na Abbas Abdalla wa darasa la tano wakitoa elimu ya usalama barabarani na kugawa zawadi za madaftari na mabegi kwa dereva Mary Carneiro aliyefika kwenye kituo cha mafuta cha Puma Upanga jijini Dar es salaam ili kujipatia huduma ya mafuta aliyesimama nyuma katikati ni Boniface Mench Meneja Usalama Kazini Puma.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, Dominic Dhanah akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya kushuhudia wanafunzi hao wakati wakitoa elimu ya Usalama barabarani kwa madereva.

Mwanafunzi Samira Jaffari akitoa elimu ya usalama barabarani na kugawa zawadi ya madaftari kwa mmoja wa Madereva waliofika kwenye kituo cha mafuta cha Puma Upanga ili kujipatia huduma ya mafuta.
Loveness Hoyange Meneja Rasilimali Watu Kampuni ya Puma Energy Afrika Mashariki na Boniface Mench Meneja Usalama Kazini Puma wakikabidhi zawadi mbalimbali za Mabegi, Madaftari na Kalenda kwa wanafunzi wa Kalabu ya Usalama Barabarani kutoka shule ya msingi Bunge ili kugawa kwa madereva wakati walipokuwa wakitoa elimu ya usalama barabarani katika kituo cha mafuta cha Puma Energy Upanga jijini Dar es salaam.


Daraja la Wami Kukamilika ndani ya Miezi 24

$
0
0
Frank Mvungi- MAELEZO 

Serikali kutumia zaidi ya Bilioni 67 katika ujenzi wa Daraja la mto Wami na linatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24 na hivyo kuchochea ukuaji wa sekta ya uchukuzi hapa nchini. 

Akijibu swali la kuhusu ujenzi wa Daraja hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kuandikwa amesema kuwa kwa sasa Mkandarasi yupo kwenye maandalizi ya kuanza ujenzi ambapo baada ya maandalizi hayo kazi ya ujenzi wa daraja utaanza ukigharimiwa na Serikali kwa asilimia 100. 

“ Wakati wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Mkandarasi Power Construction Corporation kutoka China walisaini mkataba wa ujenzi wa daraja hili tarehe 28/05/2018 hivyo tayari kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza wakati wowote”; Alisisitiza Mhe. Kuandikwa 

Akifafanua Mhe. Kuandikwa amesema kuwa Daraja jipya la Wami litakuwa na urefu wa mita 513.5 na upana wa mita 11.85 na litajengwa umbali wa mita 670 pembeni ya daraja la zamani upande wa kulia ukiwa unaelekea Segera. 

Aliongeza kuwa upana wa daraja hilo umezingatia sehemu ya barabara, waenda kwa miguu pamoja na vizuizi kwa ajili ya usalama. Daraja hilo litakuwa kichocheo cha maendeleo katika mikoa ya Kaskazini kwa kuchochea shughuli za usafirishaji na uchukuzi kwa njia ya barabara. 

Daraja la sasa la mto Wami lenya urefu wa mita 88.75 liko mkoa wa Pwani na lilijengwa mwaka 1959 na ni kiungo muhimu kutoka Chalinze kwenda mikoa ya ukanda wa Kaskazini mwa nchi yetu na nchi za jirani. 
Daraja la Wami 

Maandalizi yakamilika, watoto 10 kupandikizwa vifaa vya usikivu Muhimbili

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),kuanzia Novemba 12 hadi 16, 2018 inatarajia kufanya upasuaji wa kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto 10 ambao wana matatizo ya kusikia baada ya kukamilika kwa maandalizi ya mwisho. 

Watoto hao watapandikizwa vifaa vya usikivu baada ya wataalam kuwafanyia uchunguzi wa kina pamoja na wazazi kupatiwa ushauri wa kitaalamu. Baada ya watoto hao 10 kupandikizwa vifaa vya usikivu, jumla ya watoto watakaokuwa wamepandikizwa vifaa hivyo itafikia 21 tangu kuanza kwa upasuaji huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). 

Daktari Bingwa wa upasuaji wa Masikio, Pua na Koo wa hospitali hiyo Dkt. Edwin Liyombo amesema maandalizi kwa ajili ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto hao yamekamilika. Dkt. Liyombo amesema kwamba leo wamefanya kikao cha pamoja na wazazi wa watoto hao kwa ajili ya kuwaandaa na kuwapatia maelekezo jinsi ya kuwa karibu zaidi na watoto hao ili waweze kusikia vizuri na kuzungumza baada ya kupandikizwa vifaa vya usikivu. 

“Wazazi wanatakiwa kuwafutilia kwa karibu watoto baada ya kupandikizwa vifaa vya usikivu. Zinahitajika nguvu za ziada ili watoto waweze kuzungumza vizuri na kusikia,” amesema Dkt. Liyombo. Katika mkutano huo wazazi wa watoto hao wameonyesha imani kunbwa kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa za kuhakikisha Watanzania wanapatiwa huduma bora za kibingwa. 

Upandikizaji wa vifaa hivyo utafanywa na timu ya wataalam 10 wa Muhimbili na wataalam wawili kutoka Misri akiwamo Prof. Lobna El Fiky, Mohamed El Disouky.
Mmoja wa wazazi akiwa kwenye kikao leo cha mwisho katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) cha maandalizi ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto 10 wenye matatizo ya kusikia. 
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo kutoka nchini Misri, Prof. Lobna El Fiky akijadili jambo kwenye kikao cha maandalizi ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto wenye matatizo ya kusikia. 
Kulia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Shaban Mawalla akitoa taarifa ya mmoja wa watoto wenye tatizo la usikivu kwenye kikao hicho. Katikati ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Mkoo wa Muhimbili, Dkt. Edwin Liyombo, mtaalam wa usikivu, Fayaz Jaffer na kushoto ni wazazi wakiwa kwenye kikao hicho leo. 
Wataalam wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi wa watoto ambao watafanyiwa upasuaji wa kupandikizwa vifaa vya usikivu kuanzia Novemba 12 hadi 16, 2018 

KATIBU MKUU CCM,DK.BASHIRU ATEMBELEA ENEO LA UWEKEZAJI LA UHURU MEDIA GROUP

$
0
0

Alex Sonna,Dodoma

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali, ametembele shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru, ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama.

Dk. Bashiru aliambatana na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, Msimamizi Mkuu wa Vyombo vya Habari vya Chama, Ernest Sungura pamoja na baadhi ya wataalam wa mipango miji.

Katibu mkuu alisisitiza umuhimu wa vyombo hivyo kuhamia Dodoma kuunga mkono uamuzi wa waasisi wa taifa pamoja na ule wa Rais Dk. John Magufuli, wa kuhamishia makao makuu ya nchi kwenye mkoa huo. "Nimekuja kuangalia eneo linalomilikiwa vyombo vya habari vya CCM kwa sababu sasa maeneo yanabadilika kuwa ya mipango miji. Tumekuja kuangalia usalama wa mipaka ili tuweze kupanga matumizi yake na vyombo vyetu viweze kuhamia Dodoma.

"Ni sehemu ya kuenzi mawazo na firka za viongozi, waasisi wa chama chetu na Baba wa taifa aliyeona mbali kwa kuichagua Dodoma kuwa Makao Makuu ya Chama na Serikali," Dk. Bashiru alisisitiza.Hata hivyo amesema kuwa tayari maombi ya kubadilisha matumizi ya eneo hilo kutoka shamba hadi kutumika kwa shughuli za kibiashara au viwanda, yameshafikishwa kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji ambaye ndie mwenye jukumu la kusimamia sheria kwani chama hakipaswi kuwa sehemu ya kuvunja sheria.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma,Godwin Kunambi (kulia) alipotembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama.
Mlinzi wa shamba hilo Zebeayo Lemgoha (kushoto) akimueleza jambo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali alipotembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali ,akizungumza na Mlinzi wa shamba hilo Zebeayo Lemgoha (kushoto) ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma,Godwin Kunambi alipotembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama.

NMB YAFANYA KONGAMANO LA MAWAKALA WA BENKI YAKE

$
0
0




BENKI ya NMB leo imefanya kongamano la mafunzo kwa mawakala mbalimbali wanaotoa huduma za kibenki kwa wateja wa benki hiyo, lengo likiwa ni kuboresha huduma zake na kuwajengea uwezo wa kibiashara mawakala hao.

Akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika Sinza jijini Dar es Salaam, Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd alisema benki hiyo itaendelea kuwajengea uwezo mawakala hao kwani wao ni sehemu ya benki hivyo huduma zao zinatakiwa kufafana na zinazotolewa kwenye matawi yao.

Aliwataka kuendeleaa kutoa huduma kwa uaminifu kwa wateja na kuzingatia taraatibu walizopewa na Benki ili wateja wanaowahudumia waendelee kuiamini benki yao. Aliongeza NMB itaendelea kuboresha huduma zake na kuendelea kuwa kinara katika sekta ya fedha nchini.

Katika kongamano hilo la kuwajengea uwezo mawakala wa NMB ikiwa ni muendelezo wa semina hizo nchi nzima, NMB imetoa zawadi na vyeti kwa mawakala wanaofanya vizuri katika kutoa huduma kwa wateja ili kuwapa motisha ya kuendelea kufanya vizuri.


Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (kulia) akimkabidhi mmoja wa mawakala wa Benki ya NMB cheti kwenye semina ya mawakala wake wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (kulia) akimkabidhi mmoja wa mawakala wa Benki ya NMB cheti kwenye semina ya mawakala wake wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.


Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd akizungumza na mawakala wa Benki ya NMB walioshiriki kwenye kongamano la mawakala wake wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.


Sehemu ya mawakala wa NMB waliohudhuria kongamano hilo wakionesha vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa.



KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 12,2018

TAARIFA YA MAHAFALI YA 12, 2018 CHUO KIKUU ARDHI

Benki ya Stanbic yazindua huduma ya soko la fedha za kigeni kidijitali iitwayo eMarket Trader

$
0
0
Benki ya Stanbic Tanzania imezindua mfumo utakaoruhusu mauzo na manunuzi ya fedha za kigeni kimtandao uitwao ‘eMarket Trader’. Hii ni jitihada ya benki hiyo kuwapatia wateja wao huduma mahususi katika kubadilisha fedha za kigeni, huduma hii inajumuisha wateja binafsi pamoja na makampuni makubwa na madogo. Kupitia mtandao huu, wateja wanaweza kujua taarifa za thamani ya fedha za kigeni kwa wakati husika pia kupata taarifa juu ya mwenendo wa soko.

Huduma hii ni ya kwanza na ya kipekee nchini Tanzania na inapatikana mtandaoni. eMarket Trader inawawezesha wateja kubadilisha fedha zao kwa urahisi zaidi na kuwapatia zaidii ya aina 64 za fedha zilizopo sokoni kwa wakati huo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Meneja wa Masoko ya fedha kutoka Benki Kuu (BoT), Bw Lameck Kakulu alisema “Tunafuraha kuona benki ya Stanbic, moja ya wadau muhimu katika sekta ya fedha nchini wakijikita katika teknolojia. Kupitia uboreshaji huu wenye vipengele muhimu vya kidijitali kama kupata taarifa za soko katika muda halisi na upatikanaji wa tafiti za Benki ya Standard Bank.”

“Hapo zamani wateja wetu walihitaji kupiga simu kitengo cha ubadilishaji fedha kwa ajili ya kununua au kuuza fedha zao, na huduma hii iliwezekana tu wakati wa saa za kazi za benki. Hivyo basi, kupitia e-Market Trader, wateja wetu wanaweza kubadilisha fedha zao na kupata taarifa juu ya soko kwa wakati” alisema Mkuu wa Kitengo cha Masoko ya Fedha za kigeni wa Benki ya Stanbic, Bw Erick Mushi.

Bidhaa hii imelenga kuhakikisha wateja wote wa Benki ya Stanbic ambao biashara zao zinahusiana na masoko mbali mbali ya kimataifa wanapata maendeleo ya kifedha. Mpaka sasa miamala inayofanyika katika mtandao huu kwenye benki za Stanbic Africa ni dola za Kimarekani bilioni 18 na watumiaji zaidi ya 5,000 huwepo mtandaoni kila siku. Uzinduzi huu unaashiria utekelezaji wa ahadi iliyowekwa na Benki ya Stanbic ambayo ni kuchochea maendeleo ya wateja wake na Tanzania kwa ujumla.

Meneja wa Masoko ya fedha kutoka Benki Kuu (BoT), Bw Lameck Kakulu akizindua huduma ya soko la fedha za kigeni kidijitali ya Benki ya Stanbic iitwayo eMarket Trader jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko ya Fedha za kigeni wa Benki ya Stanbic, Bw Erick Mushi (kulia) na Mkuu wa Huduma za kibenki za mashirika na uwekezaji wa Benki ya Stanbic Bw Manzi Rwegasira. 
Meneja wa Masoko ya fedha kutoka Benki Kuu (BoT), Bw Lameck Kakulu akipeana mkono na Mkuu wa Kitengo cha Masoko ya Fedha za kigeni wa Benki ya Stanbic, Bw Erick Mushi (kulia) baada ya uzinduzi wa huduma ya soko la fedha za kigeni kidijitali ya Benki ya Stanbic iitwayo eMArket Trader jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Katikati ni Mkuu wa Huduma za kibenki za masharika na uwekezaji wa Benki ya Stanbic Bw Manzi Rwegasira.


WATUNGA SERA, WAWEKEZAJI NA WABUNIFU KATIKA SEKTA YA AFYA KUJADILI FURSA ZILIZOPO KUELEKEA TANZANIA YA UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0
Zaidi ya wataalamu 600 katika sekta ya afya nchini Tanzania and kwingineko duniani wanakutana jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la 5 la afya (Tanzania Health Summit) linaloanza Novemba 13(kesho). Litahitimishwa Jumatano Novemba 14. Kwa mara ya kwanza, kongamano hili lilifanyika nchini mwaka 2014.

Kongamano la mwaka huu linakuja na fursa mbalimbali kwa wadau wote walioko katika mfumo mzima wa afya nchini. Viongozi wa serikali, wawekezaji, watafiti na wabunifu watakutana kujadili mada kuu kuhusu dira ya Tanzania katika kuelekea uchumi wa viwanda. Kaulu mbiu ya mwaka huu ni, Ukuaji wa viwanda nchini Tanzania: Tathmini ya ukuaji na jinsi ya kutatua changamoto zilizokithiri.


Waandaaji na waratibu wa kongamano hili ni TAMISEMI)Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Afya ya Zanzibar, BAKWATA na Tume ya Kuratibu Huduma zitolewazo na makanisa (CSSC), Tindwa Medical and Health Services na Wasimamizi wa Hospitali za Binafsi(APHFTA).


 Wataalamu wa afya kunufaika

 Kwa mara ya pili, wataalamu wa afya nchini watakao hudhuria kongamano na watakaowasilisha machapisho yao watapewa alama za kufuzu viwango vya kitaaluma. Hii itawasaidia kukuza taaluma zao na kuongeza alama za ujuzi katika kile kinacho itwa Continuing Professional Development (CPD).


Kongamano la afya la Tanzania (THS) limepewa ithibati ya kutoa alama hizo na Chuo kikuu ya tiba na sayansi shirikishi(Muhas). Hii ni baada ya serikali, kupitia wizara ya afya, kutoa mwongozo kwamba wataalu wa afya ni lazima watafute njia za kujiendeleza kitaaluma wawapo makazini ili kukuza ujuzi na weledi katika taaluma zao.


Rais wa Kongamano la Afya Tanzania, Dkt Omary Chillo, amesema, “Wataalamu wa afya wasibweteke baada ya kupata na kuanza kufanya kazi. Utaalamu huwa unapotea taratibu na baada ya muda. Bila kuongeza ujuzi kitaaluma wataalamu wengi wanaweza kujikuta wakibaki nyuma. Haijalishi kama wana uzoefu kiasi gani. Kuna mabadiliko makubwa katika teknolojia za tiba na utandawazi. Kongamano hili ni fursa pekee kwa hivi sasa kujieongezea alama kitaaluma.”


Zaidi ya taasisi 100 kushiriki, watoa mada 40

Zaidi ya taasisi 100 zinashiriki katika kongamano hili. Katika majukwaa yaliyoandaliwa katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), taasisi ya JHPIEGO itaonyesha mbinu maalumu ya kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi usio salama hapa nchini.


NAMNA YA KUZUIA UKAZAJI/UTEKELEZAJI WA HUKUMU.

$
0
0


Na  Bashir  Yakub.


1.UKAZAJI WA HUKUMU NI NINI.


Ukazaji wa hukumu ni hatua inayochukuliwa na mtu aliyeshinda kesi/shauri kwa kuiomba mahakama kumlazimisha mtu aliyeshindwa katika kesi/shauri kufanya au kutekeleza kile ilichoamua dhidi yake/mshindwa. Kawaida mtu akishindwa kesi/shauri mahakama huwa inatoa maagizo mbalimbali. Mathalan, agizo la kulipa hela, agizo la kurudisha nyumba au mali fulani, agizo la kubomoa, agizo la kuondoka katika pango au katika nyumba,kiwanja fulani, agizo la kujenga, agizo la kulipa fidia, faini, gharama n.k. Maagizo  yako ya aina nyingi inategemea na shauri na shauri.

Hivyo basi, ukazaji hukumu/utekelezaji huwa ni kulazimisha agizo aumaagizo  ya aina tuliyoona hapo juu yaweze kutekelezwa kama ilivyoamriwa.


2.  NI WAKATI GANI HUKUMU HUTAKIWA KUKAZWA.

Kwa ujumla mahakama inapotoa hukumu basi yule aliyeshindwa mara moja au ndani ya muda aliopewa kama amepewa,hutakiwa kutekeleza kile kilichoamuliwa kwa hiari yake. Aliyeshindwa akikataa kutekeleza kile kilichoamuliwa kwa hiari yake basi ni wakati huu ambapo  suala la kukaza/kutekeleza hukumu kwa njia mahakama huja.  Kwa maana nyingine mtu aliyeshndwa akiamua kwa hiari yake kufanya yale aliyoagizwa na mahakama basi suala ukazaji wa hukumu haliwezi kuwepo.


3. UMUHIMU WA  KUZUIA HUKUMU KUKAZWA.

Sababu za msingi zinazoweza kupelekea kuzuia hukumu kukazwa ni pamoja na sababu kuwa umekata rufaa na hivyo ukazaji wa hukumu usimame ili rufaa yako isikilizwe kwanza, sababu nyingine ni iwapo kesi imeendeshwa bila wewe kujua au kuwepo isipokuwa umeshtukia tu watu wanakuja kukaza hukumu, sababu nyingine ni iwapo una maslahi  katika mali inayokaziwa hukumu kwa mfano ni mali ya ndoa na hukuwa na taarifa na kilichoendelea,  ni mali yako lakini inataka kuuzwa au kutumika kutekeleza hukumu kwa kesi ambayo sio yako na pengine hukuwahi kujua uwepo wake, nk.

                  
KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com



Tamasha la Tigo Fiesta laacha gumzo jijini Arusha

$
0
0

-Whozu apanda stejini na Briefcase lililojaaa mishkaki
-Roma, Stamina waangusha bonge moja la show


JIJI la Arusha, jana lilishuhudia show za kufunga mwaka zilizojaa ubunifu na vituko vya aina yake kutoka kwa wasanii mbali mbali waliopanda jukwaani kutumbuiza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyilka katika  uwanja wa Sheikh Amri Abeid.


Msanii Whozu alikuwa ni kivutio kikubwa kutokana na staili aliyotumia kupanda jukwaani na madensa wake wakiwa  wamevalia  nguo za wapishi  huku akiwa na briefcase lililojaa mishkaki.Mashabiki wengi walipigwa na butwaa baada ya kuona Whozu akifungua briefcase ambalo lilionekana ni la thamani na kutoa mishkati kisha kutuimbuiza na simbo wa Ita Boda boda Twende Kwa Mromboo ambao ulikuwa ni kivutioa Whozu na madensa wake, walifanikiwa kuliteka vyema jukwaa ambapo wakitumbuiza huku wakiwa wanatafuna mishkaki.

Wasanii wengine ambao walifanikiwa kuteka nyoyo za mamia ya mashabiki waliofurika kwenye tamasha la  hilo  ni pamoja na Roma, Stamina ambao walipanda jukwaani  pamoja na mwanadada Maua Sama anayetamba na kibao chake cha Iokote.Wasanii wengine walipanda sjejini ni pamoja na Dogo janja, Lulu Diva, Rich Mavoko, Fid Q, Weusi na wengine.

Ikiwa ni sehemu ya Vibe la Tigo Fiesta 2018, kampuni ya simu za Simu za mkononi ya Tigo imewaletea promosheni bab-kubwa inayojulikana ya Data Kama Lote inayowapa wateja bonasi ya hadi mara mbili kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#.


Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika cha bei ya tiketi kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.


Wateja wa Tigo pia wanaweza kujaribu umahiri wao wa kujibu maswali yanayohusiana na msimu wote wa vibes kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia.  Washindi wanajinyakulia zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla.
Msanii Maua Sama anayetamba na kibao chake cha Iokote akitoa burudani ya aina yake kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya walioshiriki katika tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki.

Msanii Whozu na madensa wake wakitumbuiza katika Tamasha la Tigo Fiesta 2018 lilofanyika katika kiwanja cha Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
Wasanii wanaounda kundi la Weusi wakiongozwa na Joh Makini wakiwapagawisha mamia ya mashabiki walioshiriki katika tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki.


Rich Mavoko Msanii Rich Mavoko akitoa burudani kwa maimia ya mashabiki waliofurika katika Tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki.

BENKI YA AMANA YAKABIDHI HATI ZA VIWANJA KWA WATEJA WAO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Benki ya Amana imetimiza miaka mitatu ya kufanya biashara na kutimiza ndoto ya watanzania kwa kuwawezesha kumiliki viwanja katika maeneo mbalimbali wakishirikiana na Kampuni ya Property International (PIL).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya Amana, Munir Rajab amesema katika kipindi cha miaka mitatu wamefanikiwa kuwawezesha wateja zaidi ya 300 kumiliki viwanja vyao na kupatiwa hati halali.

Rajab amesema kuwa, Katika mkopo huo watu wengi wameweza kunufaika kutumia viwanja hivyo kupata mkopo kupitia benki hiyo ili  kuwezesha kuinua uchumi na kukuza biashara zao.

"Mteja anatakiwa atangulize asilimia 20 ya thamani ya kiwanja kama malipo ya awali na kulipa kiasi kilichobaki kwa muda uziodi mwaka mmoja na nusu ila kwa sasa tumeongeza hadi miaka mitatu,"amesema Rajab.

Amesema, kutokana na kuwajali wateja wao wameongeza muda wa malipo kutoka mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu na kuwapunguzia faida toka asilimia 14 hadi asilimia 12 kwa mwaka mmoja.

Rajab ameeleza kuwa kuelekea Wiki ya huduma kwa wateja itakayoanza Novemba 19 mwaka huu, wateja watapata fursa ya kununua viwanja kwa punguzo maalum la bei na kutakuwa na mwakilishi kutoka PIL ndani ya wiki nzima ya huduma kwa wateja katika matawi yote Jijini Dar es Salaam.

Afisa Mkuu Mwendeshaji wa Kampuni ya Property International (PIL), George Obad0 amesema kuwa wameweza kushirikiana na Benki ya Amana na kufanikisha watanzania wengi kupata viwanja vilivyopimwa pia wamekuwa wanafanya marekebisho ya barabara kwa kiwango cha Changarawe ili  kufika kwenye maeneo yaliyo na viwanja.

Obad0 amesema, mbali na hilo kwa sasa viwanja vipo katika miradi ya Kimbiji Sea View Kigamboni, Magodani Mkuranga, Mapinduzi Residence, Chekeni Farm Mwasonga -Tundwi, Fukayose Residence Barabara ya Bagamoyo -Msata, The Dar es Salaam Automobile Zone (DAZ), Riverside Residence, Coco Palm, Royal Palm Mwasonga, African Palm Estate na Dege Residence.

Mmoja wa wateja walionufaika na ukopeshaji wa viwanja hivyo na kukabidhiwa hati yake leo,  Aisha Sufana amesema kuwa ameweza kumilili kiwanja ambacho hakutegemea kukipata tena kikiwa cha thamani kubwa kulingana na kipato chake ambapo yeye ni mjasiriamali wa kawaida.

Aisha amesema kuwa amekabidhiwa hati yake na kwa sasa anaweza kuitumia kama dhamana ya kuchukulia mkopo na kuendeleza biashara zake.

Amana Bank wamekabidhi hati kwa wateja watatu waliofanikiwa kumaliza mkopo wao wa viwanja .
 Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya Amana, Munir Rajab akizungumza na wateja pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu ya ushirikiano wa Benki hiyo na kampuni ya Propert International Ltd(PIL) yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Afisa mkuu Mwendeshaji wa Propert International Ltd(PIL) George Obado akizunguza na wateja pamoja na wafanyakazi wa benki ya Amana kuhusu utoaji wa mikopo ya viwanja kwa wateja wa benki hiyo leo wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu ya ushirikiano wao.
Mmoja wa wateja wa benki ya Amana Stephano Matesi akipokea hati ya kiwanja kutoka kwa  Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya Amana, Munir Rajab leo kwenye maadhimisho ya miaka mitatu ya ushirikiano kati ya benki hiyo na kampuni ya Propert International Ltd(PIL) 
 Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya Amana, Munir Rajab(kushoto) akikata keki ya maadhimisho ya miaka mitatu kati ya benki hiyo na kampuni ya Property International Ltd(PIL) pamoja na Afisa mkuu Mwendeshaji wa Propert International Ltd(PIL) George Obado  na Baadhi ya wateja wa Viwanja 
Picha ya pamoja

RPC ARUSHA ATOA AHADI YA “KUMWAGA” VIFAA VYA TAEKWONDO

$
0
0
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Baada ya kuchukua ubingwa wa Nane Nane Championship ulioshirikisha timu kumi kati ya hizo tatu toka nchini Kenya, timu ya Taekwondo ya Polisi Arusha imeahidiwa vifaa vilivyokosekana katika Gym lao ili liweze kukamilika kila idara.

Ahadi hiyo ilitolewa jana asubuhi na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi mara baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa huo toka kwa timu hiyo.
“Pamoja na changamoto kadhaa lakini mlitambua umuhimu wa mashindano hayo na mlionyesha uzalendo wa hali ya juu ambao umesaidia kuliwakilisha vyema Taifa letu na Jeshi la Polisi kwa kupata ubingwa ambao umekuwa fahari yetu sote, hivyo mimi kama mlezi wa timu hii naahidi kuendelea kutoa vifaa vya mazoezi ili liweze kukamika” Alisema Kamanda Ng’anzi.

Kwa upande wake Mwalimu wa timu hiyo Master shija Shija alisema ushindi wa timu hiyo ulitokana na nidhamu, kujituma kwa wachezaji lakini pia kufuatilia maelekezo yake.

“Hawa ni askari huwa wanatii na kuheshimu kila wanachoelekezwa lakini pia uungwaji mkono wa Kamanda wa Polisi umekuwa chachu ya ushindi kwani wachezaji wamekuwa na morali ya hali ya juu” Alisema Master Shija.

Kwa upande wake askari wa kike Edith Msafiri, alisema kwamba anajisikia furaha sana kushiriki mchezo huo kwa kuwa unamsaidia katika kazi yake kutokana na ujuzi alioupata na anaoendelea kuupata unaomuwezesha kupambana na wahalifu bila hata kulazimika kutumia silaha.

Timu hiyo ilichukua ubingwa huo katika mashinadano yaliyofanyika tarehe 3 na 4 mwezi huu katika ukumbi wa Triple A kwa kupata Medali 27 kati ya hizo Nane zilikuwa za Dhahabu, Saba za Fedha na 12 za Shaba wakati nafasi ya Pili na Tatu ilichukuliwa na Kilifi na Regional zote za nchini Kenya. 

Aidha Kamanda Ng,anzi alisema mbali na kuwepo kwa timu hiyo pia Jeshi la Polisi mkoani hapa limeanzisha Programu ya kushirikisha askari wote kila Ijumaa ili kila mmoja ashiriki katika mchezo anaoutaka kama vile riadha, Mpira wa miguu, Mpira wa Pete, kunyanyua vyuma “Gym” na kadhalika  kwa nia ya kuimarisha afya zao.
 Nahodha wa timu ya Taekwondo ya Polisi Arusha Yohana Nicodem akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Nane Nane Taekwondo Club Championship Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Arusha (SACP) Ramadhani Ng'anzi mara baada ya timu hiyo kuwasili ofisini kwake.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng'anzi akinyanyua kombe juu mara baada ya kukabidhiwa na nahodha wa timu ya Polisi Arusha Taekwondo askari Polisi Yohana Nicodem (kushoto kwake) huku wachezaji wengine wakishangilia. (Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha)
 Askari wa kike Edith Msafiri (Kushoto) akionyesha umahiri wa kukwepa na kupangua teke la askari mwenzake Eva Laswai katika mpambano usio rasmi uliofanyika Makao Makuu ya Polisi Arusha kabla ya kumkabidhi kombe la ubingwa mlezi wa timu ya Arusha Polisi Taekwondo Kamanda wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng'anzi
 Askari wa kike wa timu ya Taekwondo ya Polisi Arusha Eva Laswai akipiga  " Kick Pad Target" iliyokuwa juu zaidi ya kichwa chake kwa teke huku Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (SACP) Ramadhani Ng'anzi akimshuhudia. (Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha)
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images