Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

ULINZI NI WA KILA MTANZANIA MRADI WA MTO RUFIJI-WAZIRI MKUU


BENKI YA STANBIC YATOA ZAWADI NA UJUMBE WA SHUKRANI KWA WATEJA

$
0
0
Ruth Bura mteja wa Benki ya Stanbic akifungua chupa ya ‘champagne’ na wafanyakazi wa benki hiyo, Edward Nyerere (kushoto), Jacquiline Michael (wa pili kushoto) na Elikaneny Uloto (kulia) wakati wa sherehe za wiki ya huduma kwa wateja katika Tawi la Centre.
Mteja wa Benki ya Stanbic, Aisha Sykes akimshukuru Bw. Fredrick Mushi, mhudumu wake wa benki, baada ya kumpatia ujumbe wa kumshukuru kwa kuwa mteja wa benki ya Stanbic. Benki ya Stanbic imesherehekea wiki hii ya huduma kwa wateja kwa kuwapa zawadi wateja wao na kuwashukuru kwa kuendelea kuwa wateja wa benki hiyo.
Mshauri wa wateja wa Benki ya Stanbic akimpa mteja wake ujumbe wa shukurani kwa kufanya miamala yake ya kibenki na Stanbic wakati wa sherehe za wiki ya huduma kwa wateja katika Tawi la Centre.
Meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Centre, Bw. Adelhem Msiagi akimpa mteja wao ujumbe wa shukurani kwa kuchagua kufanya miamala yake ya kibenki na benki ya Stanbic wakati wa sherehe za wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Centre.

TAARIFA YA KIFO CHA MWAJUMA GAMBO KILICHOTOKEA JIJINI DAR

$
0
0
Kwa masikitiko makubwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anatangaza kifo Cha Dada yake mpendwa Bi Mwajuma Gambo kilichotokea Jana tarehe 04/10/2018 kwenye Hospital ya Muhimbili  jijini Dar Es Salaam. 

Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi (kesho) tarehe 06/10/2018 Saa 6 Mchana kwenye makaburi ya MCHIKICHINI Ilala Dar Es Salaam. 

Msiba upo nyumbani kwao Kariakoo mtaa wa Mheza Karibu na Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa. 

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-AMEN
Bi Mwajuma Gambo enzi za uhai wake.

WAZIRI UMMY AUAGIZA UONGOZI WA HOSPITALI YA ST FRANCIS KUSHUSHA BEI ZA MATIBABU MARA MOJA

$
0
0

Na WAMJW – IFAKARA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameuagiza uongozi wa Hospitali ya Dini ya St.Francis kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi ndani ya mwezi mmoja kabla hajarudi kufanya ukaguzi wa mara ya pili.

Ameyasema hayo wakati akiwa katika ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Hospitali ya St Francis iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Ifakara Mkoa wa Morogoro kufuatia taarifa isiyoridhisha juu ya gharama za matibabu iyoripotiwa siku ya Octoba 3 na Televisheni ya Taifa (TBC).

Waziri Ummy alisema kwamba, Serikali inatoa Jumla ya Watumishi 243 sawa na Asilimia 68% katika Hospitali hiyo, lengo ni kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kupata huduma za bora za afya na zenye unafuu ikiwa ni moja kati ya ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati anaingia madarakani.

“Kati ya Watumishi 352, watumishi 219 wanalipwa mshahara na Serikali Kuu, ambapo kila mwezi tunalipa shilingi milioni 153.7, bila kuhesabu gharama za watumishi 12 walioshikizwa kutoka Wizara ya Afya, Watumishi 12 kutoka Halmashauri ya Kilombero, Katibu tawala Morogoro ameleta watumishi 2, jumla watumishi 243, ambao ni sawa na Asilimia 68% wanalipwa mshahara kutoka Serikali kwa Asilimia 100%”. Alisema Mhe. Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa mwaka wa bajeti 2015/2016 Serikali ilipeleka dawa zenye thamani ya shilingi Millioni 119.5, bajeti ya mwaka 2016/2017 shilingi milioni 177.9 huku kwa mwaka 2017/2018 dawa zenye thamani ya shilingi milioni 118.7 zilinunuliwa hospitalini hapo. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua cheti cha mgonjwa katika kituo cha Afya cha Kibaoni wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma kisha kuelekea Hospitali ya Rufaa ya St. Francis. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto aliefika na mama yake kupata huduma katika kituo cha Kibaoni. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo kwa Baba Askofu wa jimbo la Ifakara Salutaris Libenaambae baada ya kikao cha kuboresha hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo. 
Upande wa mbele wa Hospitali ya Rufaa ya St. Francis. 


BREAKING: DAKTARI FEKI ANASWA HOSPITALI YA BUGANDO, MWANZA, AWALIZA WENGI

$
0
0
Walinzi katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) ya Jijini Mwanza wamemnasa mtu mmoja ambaye inadaiwa amekuwa akijifanya daktari na kujichumia fedha kwa kuwarubuni wagonjwa na watu wenye shida mbalimbali.
Wauguzi na Madaktari walikuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu wakishirikiana na walinzi wa hospitalini hapo, baada ya kupokea malalamiko ya mara kwa mara toka kwa wananchi wanaokimbilia hospitalini hapo kupata huduma ndipo JUZI Jumatano ya tarehe 3/september 2018) majira  ya saa moja usiku, wakamnasa daktari huyo feki akiwa katika harakati zake za kufanya kinachodhaniwa kuwa ni utapeli.
Joseph Samwel (26) alikamatwa kwenye viunga vya hospitali hiyo akiwa kwenye harakati za kujifanya mtoa huduma akiwa na sare zenye kufanana na watumishi hospitalini hapo.  Lucy Mogele ni Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza naye anafunguka zaidi juu ya daktari huyu feki......



GSENGOtv



WAFANYABIASHARA SOKO LA SAMAKI FERI WATOA YA MOYONI KUHUSU MILIONI 20/= WALIZOPEWA NA RAIS

$
0
0

Na Agness Francis,globu ya jamii 

WAFANYABIASHARA wa Soko la  Samaki Feri jijini Dar es Salaam wametoa ya moyoni kwa kumpongeza na kumshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kutimiza ahadi yake kwa kukabidhi Sh.Milioni 20 kwa ajili ya soko hilo.

Shukrani hizo za wafanyabiashara hao zimetolewa na Diwani wa Kata ya Kivukoni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya soko hilo Henry Massaba.

Akifafanua zaidi kwa waandishi wa habari kuhusu fedha ambazo zimetolewa na Rais kwa ajili ya wafanyabiashara wa soko hilo ,Massaba amesema  Rais Magufuli ametimiza ahadi aliyoiiahidi kwa wadau hao Desemba 9 mwaka 2015.

"Rais wetu mpendwa alipokuja kufanya usafi katika eneo hili la soko la zone 8 aliahidi  kutoa fedha,na tayari ametimiza ahadi,lazima tumshukuru," amesema.Ameongeza kuwa "fedha hizo Sh. milioni 20 zilizokabidhiwa  kwa wadau wa soko hili zitatumika katika ujenzi wa ofisi ya kikundi cha Umoja wa Wavuvi Tanzania.

Aidha Massaba  amesama  Mama Janeth Magufuli pia aliongezea kutoa mchango mkubwa kwa wakinamama wajasiriliamali wa sokoni hapo ambapo yeye amewakabidhi milioni 5."Fedha hizo zilizotolewa kwa  kinamama hao wa soko hilo la feri zitawasaidia kukuza mitaji na vikundi vyao katika biashara zao,"amesema Massaba .

Kwa upande wa Naibu Katibu wa soko hilo Abeid Bura amewashukuru viongozi wa Serikali ya Awamu ya tano  kwa  kutembelea sokoni na kutambua changamoto na mambo yanayoendelea.
Baadhi ya WAFANYABIASHARA wa Soko la  Samaki Feri jijini Dar es Salaam wakiendelea na shughuli zao.

WANACHUO WA KIUT KUENDELEA NA MASOMO OKTOBA 29 MWAKA HUU

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Kimataifa Tanzania Kampala(KIU) umewataka wazazi kuondokana na wasiwasi kwani chuo hicho hakijafungiwa wanafunzi waliopo wataendelea na masomo.

Chuo cha Kampala kitaendelea na masomo yake kwa wanafunzi wanaoendelea katika kitivo cha Sayansi na chuo kitafunguliwa Oktoba 08 na kwenye kitivo kingine watafungua Oktoba 29 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa mahojiano yake na waandishi wa habari, Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Jamidu Katima amesema kuwa wamekuwa wanapokea simu nyingi sana kutoka kwa wazazi wa wanafunzi wanaosoma kwenye chuo hicho.Profesa Katima amesema kuwa, chuo chao hakijafungiwa kama walivyosikia katika vyombo mbalimbaki vya habari bali wamesimamishwa kudahili wanafunzi wapya mpaka pale watakapokamilisha baadhi ya changamoto zilizoanishwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

"Ni kweli chuo chetu kimesimamishwa kudahili toka mwaja 2017 na hilo lilikuja baada ya kushindwa kukidhi baadhi ya vigezi vilivyokuwa vimewekwa na tume ya vyuo vikuu na tutakapokuwa tumekamilisha tutaanza kudahili tena," amesema Profesa Katima.Amesema, taarifa ya tume ya vyo vikuu iliyotolewa hivi karibuni ilivigawa vyuo katika makundi matatu ambayo kundi la kwanza ni vyuo vilivyofungiwa, la pili ni vyuo vilivyoambiwa wahamishe wanafunzi wao na kukatazwa kudahili ili chuo cha Kampala kipo kundi la tatu la kusimamishwa kudahili kwa mwaka huu.

Profesa Katima ameeleza kuwa, kulikua na changamoto mbalimbali katika Chuo chao na kipindi Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako alivyotembelea akiwa na viongozi wa TCU na maafisa uhamiaji aliviona na kuwapatia miezi sita ya kuhakikisha wanayafanyia kazi.Ameeleza kuwa, moja ya vigezo walivyotakiwa kuvitimiza ni kuwa na walimu wa Shahada ya kwanza  wenye GPA ya 3.5 kwa shahada ya pili  GPA 4.0 na hilo wameshalifanyia kazi kwa kuwaondoa walimu wote ambao hawajakidhi vigezo hivyo pamoja na wale walimu wa kigeni waliokosa vibaki vya kazi na kuishi.

Aidha, katika kukidhi vigezo kama walivyoagizwa na tume ya vyo vikuu Profesa Katima amesema kuwa wamepunguza vitivo kutoka 7 hadi 3 ili kuweza kupata walimu watakaojitosheleza kulingana na maagizo waliyopewa ya kuwa na walimu wanne kwenye kila somo, kupunguza idara kutoka 21 hadi 10 vyote ni katika kuhakikisha wanakamalisha maagizo yote.

Aliongezea kwa kuwataka wazazi watambue kwamba chuo chao bado kinaendelea na masomo ila wapo kwenye jitihada za kukamikilisha yale waliyoambiwa na tume kabla ya muda waliopewa kuisha na mpaka sasa takribani walimu wenye vigezo zaidi ya 60 wameshawaajiri.

Chuo hicho kimesimamishwa kudahili toka mwaka 2017 wakipewa muda wa kufanyia marekebisho changamoti zilizopo chuoni kwao na kupewa masharti ya kunyang'anywa leseni ya kudumu iwapo hawatakidhi vigezo.
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa Tanzania Kampala(KIU) Profesa Jamidu Katima akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taswira mbalimbali zilizowekwa na wazazi pamoja na wanachuo kuhusu kusimamishwa kudahili wanafunzi wapya mpaka pale watakapokamilisha baadhi ya changamoto zilizoanishwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) leo katika ukumbi wa Chuo hicho.

WANAWAKE WENYE UALBINO WADAIWA KUONGOZA KUFARIKI KWA KANSA DAR

$
0
0

Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

Elimu kuhusiana na namna ya kujikinga na kansa kwa wenye ulemavu wa ngozi imetakiwa kufika katika maeneo yote nchini ili kuweza kuwakinga na kupata matatizo ya kansa ya ngozi.

Akizungumza na blogu ya jamii Mwenyekiti wa watu wenye ualbino Wilaya ya Ilala Seif Ulate ameeleza kuwa tatizo kubwa linalowaondoa duniani ni kansa na hii ni kutokana na athari za jua akitolea mfano wa kanda ya ziwa ambako shughuli zao ni kilimo na uchungaji ambazo ni za kukaa muda mrefu juani hali inayopelekea kupata kansa kwa urahisi zaidi.

Akieleza hali ya kansa kwa jiji la Dar es salaam Ulate amesema kuwa wanawake jijini hapo huongoza kwa kufa kwa kansa na kwa mwaka huu takribani wanawake 8 wamefariki kwa ugonjwa huo na hiyo ni kutokana na kuiga kwa mitindo ya maisha kutoka kwa wanawake ambao hawana ualbino hasa katika mavazi na nywele bila kujali hali yao ya ngozi.

Aidha amesema kuwa licha ya kuwepo kwa chama hicho ila bado elimu haijafika hasa katika maeneo ya vijijini na ameiomba serikali kuhakikisha elimu kuhusu wao inaenea nchi nzima hasa katika kuwakinga watoto wenye ualbino kwa wazazi, walimu kuwa na uelewa juu ya uoni hafifu walionao na kutoa kipaumbele wawapo darasani na wazazi kutowatenga na kuwabagua watoto kutokana na hali ya ngozi zao.

Pia ameiomba serikali kuongeza idadi ya chupa za mafuta wanayotumia ili kulinda ngozi zao na amesema kuwa  kwa kuwa hiyo ndio dawa inayowasaidia hivyo hayana budi kupatikana muda wote na kila  sehemu nchini hasa vijijini.

Ulate ametoa wito kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kuishi katika mitindo bora ya maisha inayoendana na hali za ngozi zao hasa kujikinga na jua.
Badhi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) wakiwa kwenye moja ya mikutano yao.

IGP AKUTANA NA BALOZI WA UTURUKI NCHINI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Balozi wa Uturiki nchini Mhe. Ali Davutoglu wakati balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake Makao Mkauu ya Polisi Dar es Salaam ambapo walijadiliana mambo mbalimbali ya kuimarisha uhusiano. ( Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiongea na Balozi wa Uturiki nchini Mhe. Ali Davutoglu wakati balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake Makao Mkauu ya Polisi Dar es Salaam ambapo walijadiliana mambo mbalimbali ya kuimarisha uhusiano. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiongea na Balozi wa Uturiki nchini Mhe. Ali Davutoglu wakati balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake Makao Mkauu ya Polisi Dar es Salaam ambapo walijadiliana mambo mbalimbali ya kuimarisha uhusiano. ( Picha na Jeshi la Polisi)

NAJUA TUUMEJIFUNZA AJALI YA MV NYERERE, SASA TUJADILI MWENDO KASI NA TRENI DAR…

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

KABLA yakuendelea naomba msomaji wangu alau kwa dakika moja fumba macho. Kisha wewe na mimi tumuombe Mwenyezi Mungu azipumzishe roho za ndugu zetu 226 mahala pema peponi Amina.

Ni ndugu zetu  ambao wamepoteza uhai wao baada ya Kivuko cha MV. Nyerere kupinduka Septamba 20 mwaka huu katika Kisiwa cha Ukara mkoani Ukewere mkoani Mwanza. Ni moja ya ajali mbaya kuwahi kutokea ndani ya nchi yetu. Ni ajali ambayo sitaki hata kuisikia ikizungumzwa au kujadiliwa.

Ni ajali ambayo inasikitisha, inahuzunisha na inaumiza moyo. Huo ndio ukweli. Watanzania 226 kupoteza maisha kwa siku moja si jambo ambalo linaweza kusahaulika kwenye maisha yetu.

Waliopona katika ajali hiyo ni watu 41 tu. Inaumiza kwa kweli. Wakati naendelea kukusanya nguvu ili kueleza kile ambacho nimekikusudia naomba nitumie nafasi hiyo kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa namna ambavyo wameshughulikia tukio hilo.
Rais Magufuli pamoja na walio chini yake walihakikisha wanafuatilia hatua kwa hatua kuhusu ajali hiyo. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amezungumza mara kadhaa namna ambavyo alikuwa anapigiwa simu na Rais.

Kwa ujinga wangu na akili zangu fupi ambazo zinashindwa kuwaza mbali, baada ya kutokea ajali hiyo nikawa najiuliza maswali mengi lakini sikuwa na majibu yake. Sitaki kujiuliza tena maana najua sitaweza kujijibu mwenyewe. Acha nikae kimya huenda ninayojiuliza kuna watu wenye akili nyingi na maarifa nao wanajiuliza kama mimi. Lakini Najua watakuwa na majibu.
Kwa mfano swali la kwanza kujiuliza ndani ya Kivuko kulikuwa na watu wangapi? Nilijiuliza swali hili zaidi ya mara 100 sikuwa na majibu. Hata hivyo jibu nikajakulipata baadae kwamba idadi ya watu waliokuwa kwenye Kivuko hicho siku ya tukio walikuwa zaidi ya 265.

Baada ya kufahamu idadi ya watu...nikajiuliza tena wakati wanaingia walipita wapi? Walipita njia sahihi au? Wahusika wa Kivuko hicho wanajua idadi halisi ya waliokuwa wanatakiwa kubebwa na Kivuko? Kama walikuwa wanajua kwanini waliacha watu wote wakaingia?

Ulikuwa mpango maalum? Kwanini hawakuchukua tahadhari? Yaani najiuliza maswali mengi mengi mnooo… Ndio maana nasema acha nikae kimya tu. Najua ipo Tume ambayo imeundwa kuchunguza ajali ya MV.Nyerere.Hata hivyo kwa nafasi yangu ninayo nafasi ya kujadili kama ambavyo wengine wanajadili. Kwani kuna ubaya gani? Naomba niseme tu siingilii  Tume inayochunguza ajali hiyo maana sijui wao wanauliza maswali ya aina gani. Wakiuliza kama yangu nayo si tatizo.

Sitaki kuzungumza. Naomba niwe mkweli tayari tumeelezwa kuwa uwezo wa Kivuko cha MV. Nyerere ilikuwa ni kubeba watu 101. Hivyo siku ambayo Kivuko hicho kimepinduka kulikuwa na idadi ya watu zaidi ya 265. Najuliza kwanini iwe hivyo? Huenda nikawa na jibu langu acha nawe msomaji uwe na jibu lako.


Ukweli utabaki kuwa kivuko hicho kilibeba idadi ya watu tofauti na uwezo wake. Hiki ni chanzo namba moja cha Kivuko hicho kupinduka. Najua watalaam wanayo nafasi ya kufanya uchunguzi wao na kuja na majibu halisi ya kilichosababisha ajali.
Rais wangu Dkt. Magufuli wakati anazindua Flyover ya Mfugale iliyopo makutano ya Tazara jijini Dar es Salaam amewaambia Watanzania kila mmoja kwa nafasi yake ajitafakari.

Nami kama Mtanzania nikaanza kuitafakari kauli ya Rais ya kututaka sote tujitafakari kuhusu ajali ya MV.Nyerere.Kuna somo la kujifunza kutokana na ajali ya MV. Nyerere. Hata hivyo swali la msingi la kujiuliza tumejifunza nini? Jibu la swali hili nadhani kila mmoja atakuwa na lake.

Kwangu mimi nilichojifunza kuna uzembe wa kusimamia Sheria, Kanuni na Taratibu kuhusu vivuko. Si vyote. Ni kwa hicho cha MV Nyerere. Sitaki ugomvi wala shari na mtu. Pia nimejifunza iko haja ya kuhakikisha Sheria, Kanuni na Taratibu zinaheshimiwa. Tukifuata sheria naamini tutakuwa salama na tutaepuka ajali.  Kwa kuwa kuna tume inachunguza acha hili nisiendelee kulizungumza. Tutafahamu ukweli wakati ukifika.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAHAKAMA YA RUFANI JIJINI DAR YATUPILIA MBALI RUFAA YA VIONGOZI TISA WA CHADEMA

$
0
0

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam leo Oktoba 5.2018 imetupilia mbali Rufaa iliyofunguliwa na viongozi tisa wa Chadema akiwamo mwenyekiti wake Freeman Mbowe kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu dhidi ya mwenendo wa kesi ya uchochezi unayowakabili katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu sababu taarifa ya kusudio la kukata rufaa hiyo inamapungufu kisheria.

Mapema mwaka huu, Mahakama kuu ilitupilia mbali maombi ya viongozi hao ya kutaka kufanya marejeo mwenendo wa kesi hiyo kwa sababu ya kuwepo mapungufu kisheria.

Rufaa hiyo ni mwendelezo kutokana na kesi ya msingi ya jinai inayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo wanapinga uamuzi na amri mbalimbali ambazo mahakama hiyo imekuwa ikizitoa.

Uamuzi dhidi ya rufaa hiyo iliyoandaliwa na jopo la Majaji watatu, wakiongozwa na Mbarouk Mbarouk, Shaban Lilla na Jacobs Mwambegele,imesomewa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Eddy Fusi

Katika uamuzi huo, jopo hilo la Majaji limesema taarifa ya kusudio la kukata rufaa ya waombaji hao haielezi ni sababh au amri ipi wanayoitakatia rufaa kisheria.

Jopo hilo la Majaji limeeleza kukubaliana na Wakili wa serikali Mkuu, Paul Kadushi kuwa kwa mujibu wa kanuni ya 68(2) ya kanuni ya Mahakama ya rufaa, kuwa rufaa hiyo inamapungufu kisheria kwa kuwa waleta maombi hawaelezi ni amri ipi wanayoikatia rufaa kwani waombaji kwenye taarifa yao ya kukata rufaa wameeleza kuwa wanakatia rufaa uamuzi wote wa mahakama Kuu.

" mapungufu haya yanaenda kinyume na kanuni hiyo sababu kwenye mashauri ya jinai, taarifa ya kukata rufaa ndio inayoanzisha rufaa na kwa vile rufaa hii inamapungufu basi rufaa iliyopo mahakamani haiwezi kusimama na kwa sababu hiyo rufaa hiyo pia imefutwa.

Kutokana na hatua hiyo, imetupilia mbali rufaa ya vigogo hao 9, pamoja na kuyaondoa maombi ya kutaka kusitisha mwenendo wa kesi yao inayoendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu, Dk Vicent Mashinji, manaibu katibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar) na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

Pia wamo Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha), Esther Matiko, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 12 ambayo ni kufanya mikusanyiko na maandamano yasiyo halali yanayowakabili wote, huku Mbowe, Msigwa Mdee na Heche kila mmoja peke yake akikabiliwa na mashataka zaidi.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo Februari 16 katika barabara ya Kawawa, Mkwajuni, Kinondoni, siku wakihitimisha kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kinondoni na kusababisha vurugu zilizosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline.

MADAKTARI BINGWA WA MOYO, USINGI KUTOKA SAUDIA ARABIA WAAGWA JKCI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Prof. Mohamed Janabi akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hiyo walioshiriki tukio la kuagwa kwa madaktari Bingwa wa magonjwa ya moyo, usingizi, wauguzi na watalaam wa mashine za moyo kutoka Saudi Arabia wapatao 11 waliokuwa wakisaidia kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii.

MADAKTARI Bingwa wa magonjwa ya moyo, usingizi, wauguzi na watalaam wa mashine za moyo kutoka Saudi Arabia ambao waliokuwa wakisaidia kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam wameagwa rasmi.

Tukio la kuagwa kwa madaktari hao wapatao 11 limefanyika katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ambapo madaktari wa taasisi hiyo wamewapongeza kwa ushirikiano waliounesha kipindi chote wakiwa hapo.

Akizungumzia madaktari hao, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janab amesema wamekuwa nao tangu Septemba 29 mwaka huu na sasa wamemaliza muda wao, hivyo wanarejea nchini kwao kuendelea na shughuli za utoaji huduma za matibabu ya moyo.

Profesa Janab amesema katika kundi hilo lenye madaktari 11 kulikuwa na madaktari bingwa wa moyo, madaktari bingwa wa usingizi, wauguzi na wataalam wa mashine za moyo.

Pia baadhi ya madaktari wa JKCI wametoa shukrani kwa madaktari hao na kubwa zaidi ni utaalam ambao wameupata kutoka kwao.

Madaktari wa JKCI wamesema pamoja na kwamba madaktari hao wanaondoka bado kile ambacho wamekipata kutoka kwao kitaendelea kuwa msaada katika kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa moyo na kuwaaga madaktari hao huenda lisiwe nano sahihi zaidi, hivyo wanawaambia milango ili iko wazi hivyo wanaweza kuja tena wakati wowote.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo na Mshauri Mkuu wa magonjwa ya moyo kutoka Albalsam, Dk. Emad Bukhari amesema wamefurahia ushirikiano walioupata kutoka kwa madaktari wa kada mbalimbali wa JKCI.

Amesifu huduma za matibabu zinazotolewa kwenye taasisi hiyo ambayo ni moja kati taasisi yenye watalaamu wabobezi katika tiba ya magonjwa ya moyo huku akitumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali kwa uamuzi wa kuanzisha taasisi hiyo.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo na Mshauri Mkuu wa magonjwa ya moyo kutoka kutoka Albalsam, Dk. Emad Bukhari akizungumza wakati akitoa shukrani kwa baadhi ya madaktari waliokuwepo ukumbini hapo.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo na Mshauri Mkuu wa magonjwa ya moyo kutoka kutoka Albalsam, Dk.Emad Bukhari akimkabidhi cheti mmoja wa Madaktari wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dkt. Viviene Mlawi kwa niaba ya madaktari wengine. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Prof. Mohamed Janabi. 

HOSPITAL YA BAGAMOYO YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WATUMISHI NA BAADHI YA MAJENGO KUWA CHAKAVU - DKT. MULOKOZI

$
0
0
Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoani Pwani walipotembelea hospital ya wilaya ya Bagamoyo kuadhimisha wiki ya wanawake UWT kimkoa ,(wa pili kulia ) Mganga Mfawidhi hospitalini hapo dokta Erick Mulokozi.

NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO

HOSPITAL ya wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa madawa, watumishi na uchakavu wa baadhi ya majengo. Akieleza changamoto hizo wakati umoja wa wanawake (UWT ) Mkoani Pwani ,ulipotembelea wodi ya wanawake hospitalini hapo, Mganga Mfawidhi wa hospital ya Bagamoyo, Dokta Erick Mulokozi alisema, tatizo la madawa limekuwa kubwa kutokana na miaka mitatu iliyopita kuwa na deni la milioni 200 walilokuwa wakidaiwa na bohari kuu ya madawa (MSD).

Alisema, walikubaliana na bohari ya dawa kwamba ikija fedha za ruzuku inakata fedha ,kulipa deni ambapo sasa wamelipunguza na kubakia na deni la sh. milioni 78. Dokta Mulokozi alieleza, fedha wanazozipata wanajiendesha kwa tozo ambayo wananunulia dawa ,kulipa posho wafanyakazi ,lakini hakuna tatizo la dawa muhimu kwa asilimia 95.

"Dawa muhimu zote zipo ,licha ya changamoto chache zilizopo na tunaendelea kupambana na hali hiyo ili kuwahudumia wananchi " alielezea dokta Mulokozi .
Kuhusiana na uchakavu wa baadhi ya majengo alisema ,hospital hiyo imejengwa mwaka 1892, hivyo yapo majengo  ambayo ni lazima yawe chakavu. Akizungumzia changamoto ya upungufu wa watumishi, dokta Mulokozi alisema, imetokana na tatizo la vyeti feki, ambapo zoezi hilo lilisababisha upungufu kuzidi lakini wameshapangiwa watumishi 19, suala ambalo wanaamini itasaidia kupunguza tatizo hilo.

Nae mbunge wa viti maalum mkoani Pwani, Subira Mgalu alisema, kutokana na uhaba wa watumishi mkoa wa Pwani serikali imeshapeleka watumishi 273 wa sekta ya afya. Aliishukuru serikali chini ya Rais dk.John Magufuli kwa kutatua changamoto hiyo awamu kwa awamu. Subira alieleza, kati ya watumishi hao wilaya ya Bagamoyo wamepata watumishi 19 na Chalinze 44.

Alisema ,jitihada zinaendelea na kwamba ikitangazwa watapeleka maombi ili kuomba watumishi wanaohitajika.

Kwa upande wake ,kaimu mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani ,Arafa Kisela alisema mkoa huo, una wilaya nane za kichama na matawi 1,097 ya UWT na kata 113 .

Alifafanua ,wanaadhimisha wiki ya wanawake ya UWT ,kimkoa kwa kufanya shughuli za kijamii na kutembelea wodi ya wanawake na kujua changamoto zilizopo katika hospital ya wilaya ya Bagamoyo ,gereza la Kigongoni ,kituo cha watoto yatima na ujenzi wa kituo cha afya Yombo .

Tamko la UWT mkoa , wanakemea vitendo vinavyofanywa na baadhi ya madereva wa vyombo vya moto na majini kwa kusababisha vifo kwa uzembe kwani waathirika wakuu ni wanawake ,watoto na wazee.
Mbunge wa viti maalum mkoani Pwani ,Subira Mgalu alipoungana na baadhi ya viongozi wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoani Pwani na wilaya ya Bagamoyo kutembelea kituo cha watoto yatima ikiwa ni moja ya shughuli walizozifanya kuadhimisha wiki ya wanawake UWT kimkoa .(Picha na Mwamvua Mwinyi)

ALICHOKIFANYA DIAMOND TANDALE NI MFANO WA KUIGWA-MEYA SITTA

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya jamii
MEYA wa Manispaa ya Kinondoni katika Jiji la Dar es Salaam Benjamin Sitta amesema msanii wa muziki wa kizazi kipya maarufu kwa jina la Bongo Fleva Nassib Abdull a.k.a Diamond ni mfano wa kuigwa katika jamii.

Sitta amesema Diamond ameona haja na umuhimu wa kurudisha shukrani kwa jamii na watu wa aina yake ni wachache sana.

Meya Sitta amesema hayo leo wakati sherehe iliyopewa jina la Ahsante Tandale ambapo Diamond ameamua kurejesha shukrani kwa wananchi wa maeneo hayo ambako yeye amezaliwa na kukulia.

Sitta amesema pamoja na mambo mengine uamuzi wa Diamond kutoa kadi za bima ya afya ambazo zitaweza kumpa nafasi kila aliyejiunga na huduma hiyo kupata matibabu bure kwa muda wa mwaka mmoja.

Wakati huo huo msaani Rashid Chid Benz amesema Diamond amefanya jambo kubwa na ni mfano ambao unastahili kuigwa na wasanii wote nchini.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta akizungumza wakati wa sherehe iliyopewa jina la Ahsante Tandale ambapo Diamond ameamua kurejesha shukrani kwa wananchi wa maeneo hayo ambako yeye amezaliwa na kukulia.

DIAMOND ASIPOOA MWAKA HUU NAMFUNGA - MAKONDA

$
0
0
MAKONDA kweli noma! Ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Mkuu ya Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amtengaza hadharani kwamba iwapo msanii Nasseb Abdull a.k.a Diamond asipooa mwaka huu basi atamfunga.

RC Makonda amesema hayo leo wakati anazungumza kwenye sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwa Diamond ambapo tukio linakwenda sambambamba na msanii huyo kurejesha shukrani kwa wananchi wa Kata ya Tandale.

"Mama Diamond naomba nieleze hapa wazi kuwa mwaka huu kabla ya kuisha lazima Diamond awe ameoa.Asipooa namfunga,"amesema.

Amesisitiza ni lazima msanii huyo akaoa na kutoa mifano kwenye orodha ya watu ambao anataka waoe mwaka huu wapo watatu na mmoja wao ni Diamond.
MAKONDA kweli noma! Ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Mkuu ya Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amtengaza hadharani kwamba iwapo msanii Nasseb Abdull a.k.a Diamond asipooa mwaka huu basi atamfunga.

RC Makonda amesema hayo leo wakati anazungumza kwenye sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwa Diamond ambapo tukio linakwenda sambambamba na msanii huyo kurejesha shukrani kwa wananchi wa Kata ya Tandale.

"Mama Diamond naomba nieleze hapa wazi kuwa mwaka huu kabla ya kuisha lazima Diamond awe ameoa.Asipooa namfunga,"amesema.

Amesisitiza ni lazima msanii huyo akaoa na kutoa mifano kwenye orodha ya watu ambao anataka waoe mwaka huu wapo watatu na mmoja wao ni Diamond.
Msanii wa Kizazi kipya Diamond Platinum akiwapungia mikono mashabiki wake wakati wa sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwake ambapo tukio linakwenda sambambamba na msanii huyo kurejesha shukrani kwa wananchi wa Kata ya Tandale.

HATIMAYE DIAMOND ATAJA SIRI YA KUFANIKIWA KWAKE

$
0
0
Na Khadija Seif , Globu ya Jamii
HATIMAYE msanii maarufu nchini katika muziki wa Bongo Fleva Nasseb Abdull a.k.a Diamond  amevunja ukimya kwa kutaja siri iliyomfanya afanikiwe kwenye muziki huo.

Wakati Diamond anataka kutaja siri iliyomfikisha katika kilele cha mafaniko mamia ya wananchi wa Tandale, viongozi wa ngazi wa Mkoa wa Dar es Salaa pamoja na wageni waalikwa walikuwa kimya.

Diamond alianza kueleza hatua hatua sababu ambazo zimemfanya awe na mafanikio katika maisha yake ni siri kubwa ya kufanikiwa kwake anasema hachagui kazi ya kufanya.

"Katika maisha yangu sijawahi kuchagua kazi ya kufanya.Ndio maana kwenye maisha yangu nimefanya kazi nyingi sana.Nimefanya kazi ya kuuza mafuta sheli.nimefanya kazi ya kupiga picha kwenye kumbi za harusi pamoja na nimefanya kazi ya kuuza nguo Tandale.

"Siri nyingine ni kujenga uaminifu kwa watu ambao unafanya nao kazi.Uaminifu umenisaidia sana na ndio maana leo niko hapa,"amesema Diamond.

Amesema siri nyingine ni ubunifu na kufafanua baada ya kufanya kazi kwa bidii aliamua kuwa mbunifu kwa kila alichokuwa akikifanya.

Pia amesema kuomba Mungu ni jambo la msingi sana na katika maisha yake moja ya jambo ambalo lazima alifanye ni kumuomba Mungu na amemsadia kumfikisha hapo alipofika.

"Nimekuwa nikimuomba Mungu anisaidie katika shughuli zangu za muziki .Napoomba nataja kaabisa kile ambacho nahitaji ili kumrahisisha Mungu kile ambacho nahitaji kwake.Sitaki kumchanga kwa kuomba mambo mengi.

"Leo hii nimefanikiwa kwasababu namshikirisha Mungu,"amesema Diamond na kuongeza kuwa kwa anayetaka kufanikiwa lazima ajiepushe na matumizi ya dawa za kulevya.
Bongo Fleva Naseeb Abdull a.k.a Diamond Plutnumz akizungumza na
mashabiki wake wakati wa sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwake ambapo tukio linakwenda sambambamba na msanii huyo kurejesha shukrani kwa wananchi wa Kata ya Tandale.

HAJI MANARA ATOA ZAWADI YA JEZI NA MIPIRA KWA SHULE ZOTE ZA TANDALE

$
0
0
Na Khadija Seif ,Globu ya jamii

Msemaji wa timu ya Simba Haji Sunday Manara ametoa  zawadi ya jezi pamoja na mipira kwa shule zote za Kata ya Tandale na kutoa wito kwa wazazi kutowanyima fursa watoto wao ambao wanavipaji ili kuwa mfano mzuri kama alivofanya msanii huyo Daimond Platinum .

Aidha amewapa taarifa rasmi atashirikiana bega kwa bega kwa wana michezo wa kata hiyo kuanzisha michuano ya Tandale Cup na kutoa fedha ya taslim kwa mshindi wa kwanza shilingi million 1, na kwa mshindi wa pili na watatu .

Manara ametoa fursa kwa Wanafunzi wa ulemavu wa ngozi pamoja na viungo kuwalipia ada mwakani kwa Wanafunzi watakaoingia kidato cha kwanza na darasa la kwanza.

VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA WATAKIWA KUZINGATIA UBORA WA KUROSHO

$
0
0
Viongozi wa vyama vya ushirika Manispaa ya Mtwara Mikindani wametakiwa kuzingatia ubora wa korosho ghafi pindi wanapozipokea kwa wakulima wa zao hilo ikiwa tayari kwa kuingia katika mnada wa ununuzi wa zao hilo.

Akizungumza katika kikao na viongozi hao Mkuu wa wilaya ya Mtwara Evod Mmanda amesema kumekuwa na changamoto zilizojitokeza Katika baadhi ya maeneo msimu wa wa korosho mwaka 2017/2018 ikiwemo viongozi hao kupokea zao hilo kutoka kwa wakulima bila ya kuzingatia vigezo na sifa zilizowekwa.

Kwaupande wake Afisa ushirika kutoka tume ya maendeleo ya ushirika(TCDC),Coster Robert  amewataka viongozi hao wa ushirika kufanya kazi kwa kufuata taratibu zilizowekwa ili kuondoa mkanganyiko kati ya mkulima na mnunuzi wa zao hilo.

Baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika waliohudhuria kikao hicho wamesema kuwa watafanyia kazi maagizo hao ili kuondoa changamoto hizo zilizojikeza katika msimu wa korosho uliopita.

Mkuu wa mkoa huyo, Evod Mmanda ameendelea kufanya vikao na viongozi wa ushirika katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo lengo ikiwa ni kuondoa changamoto zote zilizo jitokeza katika msimu wa korosho 2017/2018.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda akizungumza na viongozi wa vyama vya ushirika Manispaa ya Mtwara Mikindani  kuhusu kuzingatia ubora wa korosho ghafi pindi wanapozipokea kwa wakulima wa zao hilo ikiwa tayari kwa kuingia katika mnada wa ununuzi wa zao hilo.
.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara 
Evod Mmanda
 na kulia kwake ni Afisa Ushirika Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) Bw.Castor Robert wakiwa katika kikao kazi na viongozi wa vyama vya ushirika manispaa ya mtwara mikindani.

Afisa Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika Manispaa ya Mtwara Mikindani Aisha Fanuel na kulia kwake ni Afisa Tarafa Mtwara Mikindani Octavian  Lyaoembile wakiwa katika kikao kazi na viongozi wa vyama vya ushirika.








Viongozi wa vyama vya ushirika Manispaa ya Mtwara Mikindani wakiwa katika kikao kazi na Mkuu wa wilaya ya Mtwara Evod Mmanda..

DIAMOND AFANYA BALAA TANDALE... AREJESHA SHUKRANI KWA WANANCHI

$
0
0
*RC Makonda aongeza muda wa kupiga muziki
*Asema mwisho iwe saa nane usiku,atoa maagizo

Na Khadija Seif ,Globu ya jamii
NI upendo wa aina yake ambao msanii Nassem Abdull 'Diamond'ameamua kuufanya kwa wananchi wa Kata ya Tandale jijini Dar es Salaam.
Unajua kwanini?Iko hivi msanii huyo leo ameamua kusheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kujumuika na wananchi hao na kubwa zaidi ametumia nafasi hiyo kurejesha ahsante kwa wananchi hao.
Katika sherehe hizo Diamond ameamua kufanya mambo yenye kugusa jamii kutokana na aina ya misaada ambayoa ameitoa kwa wananchi hao ambapo ameamua kugawa bodaboda kwa vijana wa Tandale na kugawa kadi za bima 1000 kwa wananchi wa Tandale.

Pia msanii huyo ameamua kutoa msaada wa bajaji kwa mama mwenye ulemavu baada ya kuona anahitaji msaada kwa kumpatia chombo hicho ambacho kitamsaidia mama huyo.

Wakati wa sherehe hiyo ikiendelea Diamond hakusita kueleza changamoto ambazo amezipitia katika maisha yake hadi kufika hapo alikofikia.

Pamoja na yote Diamond ametoa ombi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuondoa zuio la kufanya muziki mwisho saa sita usiku."Tunaomba Mkuu wa Mkoa hili zuio la mwisho saa sita usiku uliondoe kwani limetubana sana.

"Watu wa Dar ikifika saa sita ndio wanataka kuoka kwenda kwenye kumbi za sterehe lakini kwa katazo lililopo inakuwa ngumu.Hivyo tunaoma ulitazame hili ili tuendelee kudamshi,"amesema Diamond.

Pia ameomba kwa Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kuwapatia eneo WCB ili wajenge studio kwa ajili ya wasanii wa muziki wa Tandale.

Kwa upande wa watu waliokuwa eneo hilo wengi wao wameonesha kufurahishwa na kitendo cha Diamond na kumpongeza kwa uamuzi wake wa kusaidia jamii.

Hata hivyo Makonda akizungumza kenye tukio hilo ametoa maagizo ya kuhakikisha linapatikana eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja cha mpira pamoja na kiwanja ambacho kitajengwa shule ya msingi kwa ajili ya wananchi wa Tandale.

Kuhusu kuongezwa muda kwa ajili ya burudani Makonda amesema suala hilo lipo kisheria na la muda mrefu kidogo na kufafanua kuna sheria ya mazingira ambapo kilele nayo ni sehemu ya uchafuzi wa mazingira.

Hata hivyo baada ya maelezo mengi ametangaza kuanzia leo ameongeza muda wa kupiga muziki ambapo sasa watapiga hadi saa nane usiku badala ya saa sita usiku.

Hivyo ametoa maagizo kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kutowakamata watu wanaopiga muziki hadi saa nane usiku na kwamba Jiji la Dar ndio jiji la starehe na ushauri wake ni vema watu wakajenga kumbi za ndani.

Wasanii mbalimbali nao wamepata nafasi ya kuzungumza na kutoa maoni yao na kubwa zaidi ni namna ambavyo Diamond amethibitisha wananchi wa Tandale ni sehemu ya maisha yake.
 Msanii wa Bongo Fleva Naseeb Abdull a.k.a Diamond Plutnumz akizungumza na mashabiki wake wakati wa sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwake ambapo tukio linakwenda sambambamba na msanii huyo kurejesha shukrani kwa wananchi wa Kata ya Tandale.
 Mkuu ya Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza wakati wa sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwa Msanii Naseeb Abdul ' Diamond'  ambapo tukio linakwenda sambambamba na msanii huyo kurejesha shukrani kwa wananchi wa Kata ya Tandale.
Aliyewahi kuwa Miss Tanzania Jacqueline Mengi akiwasalimia wananchi wa Tandale  wakati wa sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwa Msanii Naseeb Abdul ' Diamond'  ambapo tukio linakwenda sambambamba na msanii huyo kurejesha shukrani kwa wananchi wa Kata ya Tandale.
Msemaji wa Simba Haji Manara akizungumza jambo kwenye hafla hiyo iliyofanyika Tandale 
Msanii wa Hip Hop nchini Rashid Makwiro 'Chid Benz' akitoa burudani kwenye hafla hiyo 
Baadhi ya wananchi wa Tandale wakiwa katika sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwa Msanii Naseeb Abdul ' Diamond'  ambapo tukio linakwenda sambambamba na msanii huyo kurejesha shukrani kwa wananchi wa Kata ya Tandale.

RIDHIWANI ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MRADI WA MAJI CHALINZE

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


BAADA ya ziara ya siku mbili ya Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka (DAWASA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange kutembelea mradi wa Chalinze Mbunge wa jimbo hilo aweka wazi msimamo wake na kusema kero ya maji inamalizika.

Akiwa katika ziara ya Mkoa wa Pwani, Halmashauri ya Manispaa ya Chalinze Jenerali Mwamunyange aliweza kutembelea mradi wa Chalinze akiambatana na mbunge wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo wa ujenzi wa Matenki 19, ulazaji wa mabomba ya ukubwa mbalimbali kwa kilometa 1, 203, ujenzi wa vizimba vya kuchota maji pamoja na upanuzi wa mtambo wa kusafisha maji wa Chalinze ukiwa na Lengo la kuongeza uzalishaji kufikia mita za ujazo 900 kwa siku kutoka mita za ujazo 500, Mbunge Rudhiwani kikwete ameishukuru serikali kwa kuja kuona hali halisi ya upatikanaji wa maji jimboni kwake.


Ridhiwani amesema kuwa hatua ya Mwenyekiti wa Bodi kutembelea chanzo cha maji cha Chaliwasa kwani kilio kimefika na kuanzia sasa yale matatizo ya maji yatakwisha.Amesema kuwa, anaipongeza serikali kwa kuweka utaratibu mpya wa kutenga akaunti maalumu ya kupokea pesa za miradi na hilo litasaidia kukamilika mradi kwa mapema zaidi.

Ridhiwani amesema, yale malengo mazuri ya kupata maji kabla ya 2019 yatafikiwa kama matarajio ya wananchi kupata maji muda wote. Katika ziara hiyo, Jenerali Mwamunyange amewataka kampuni ya Jain Irrigation System kukamilisha mradi huo kufikia Desemba 30 kwani wameshawapa muda mwingi na bado hawajakamilisha.

Kazi hii itakapokamilika, wakazi waliopo maeneo ya Manga hadi Tengwe katika Mkoa wa Tanga; mji na vitongoji  vya wa Chalinze na baadhi ya maeneo ya Bagamoyo na Kibaha katika mkoa wa Pwani watafaidika.

 Mradi pia utanufaisha baadhi ya maeneo ha Mkoa wa Morogoro ikiwa ni pamoja na  maeneo ya Kizuka A na B, Ngerengere, Kinoko A and B, Tukamisasa, Lulenge, Visakazi hadi Bwawani  pamoja na Sangasanga A na B. Hadi utakapokamilika, mradi utagharimu dola za Marakani 41,362,023.43 ambazo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya EXIM ya India.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi wa maji wa Chalinze utakaowapatia maji ya kutosha wananchi ya jimboni kwake
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Meneja wa Mradi huo P. G. Rajon wakati wa ziara yake katika mradi wa Chalinze.

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>