Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109979 articles
Browse latest View live

RC MAKONDA AKUTANA NA WATENDAJI NA TPSF KUZUNGUMZA MIKAKATI YA KUONGEZA TIJA


TRA YAKAMATA WATU WAWILI KWA KOSA LA KUGUSHI RISITI ZA EFD

$
0
0


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewakamata watu wawili mwanamke na mwanaume kwa kosa la kugushi Risiti za Kielektroniki za EFD katika maeneo ya Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo Richard Kayombo, amesema kuwa, watuhumiwa hao ni Doreen Urassa (40) mkazi wa Kunduchi na Raymond Alexander (31) mkazi wa Kinondoni Mkwajuni jijini hapa.

"Tarehe 4 Oktoba, 2018 majira ya saa 1 jioni, tulifanikiwa kuwakamata watu wawili maeneo ya Sinza Mori wakiwa wanagushi risiti za EFD. Watuhumiwa hawa tutawafikisha mahakamani kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria", alisema Kayombo. 

Kayombo ametoa wito kwa watu wote wanaojishughulisha na makosa hayo kuacha mara moja kwa kuwa TRA itaendelea kufanya msako mkali na mtu yeyote akibainika anagushi risiti, atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.Aidha, Mkurugenzi Kayombo amewaomba wasamalia wema waendelee kutoa taarifa za kuwafichua wanaogushi risiti na kuwahakikishia kuwa, majina yao hayatatajwa popote.

“Mamlaka haitamvumilia mtu yeyote anayejaribu kukwamisha ukusanyaji mapato ya serikali iwe kwa kugushi risiti au biashara ya magendo au njia nyingine yoyote ya udanganyifu. Hivyo, tunawaomba wasamalia wema waendelee kutupa ushirikiano kwa kuwafichia watu wadanganyifu na tunawahakikishia kutunza siri kwa kutoyataja majina yao popote pale”, alifafanua Kayombo.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendelea na zoezi la kuwasaka watu wote wanaojishughulisha na vitendo vya kugushi risiti ikiwa ni pamoja na kukamata biashara za magendo ambapo wanaobainika hufikishwa mahakamakani kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Rais Magufuli amteua Bw. Habbi Gunze kuwa Mwenyekiti wa BASATA

AZAM TV: NYUNDO YA BARUAN MUHUZA: Manara amvaa kocha wa Yanga, asema Aussems ni 'Profesa wa football'

MICHUZI TV: KAMPENI UCHAGUZI WA UBUNGE ZAPAMBA MOTO JIMBO LA LIWALE

MSANII DIAMOND PLATNUMZ ALIVYORUDI KWAO TANDALE KUTOA SHUKRANI

ULINZI NI WA KILA MTANZANIA MRADI WA MTO RUFIJI - WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

DIAMOND PLATINUMZ AKIZUNGUMZIA SIRI YA MAFANIKIO LEO MBELE YA WAKAZI WA TANDALE


MICHUZI TV: BALAA LA MANARA TANDALE

MICHUZI TV: CHID BENZ Alichokifanya Tandale imebaki historia

MICHUZI TV: DIAMOND PLATINUMZ, Siri ya mafanikio

MICHUZI TV: DIAMOND PLATINUMZ AMLIZA MAMA HUYU..

NHIF KAGERA WAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUTOA MSAADA WA MASHUKA YA WAGONJWA HOSPITAL YA RUFAA YA MKOA WA KAGERA

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera

KATIKA kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja mwaka 2018 uongozi wa bima ya afya Mkoa wa Kagera(NHIF) wameahadhimisha wiki hii kwa kwa kutoa msaada wa mashuka 60 yenye thamani ya shilingi 720,000 kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Bukoba.

Meneja wa mfuko wa bima ya afya (NHIF)Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo amesema wiki hii wameitumia kuwa karibu na wanachama wao kwa kutembelea vituo vya tiba na kupata maoni kutoka kwa wanachama wao.

"Tumetumia wiki hii kutembelea vituo mbalimbali vya kutolea huduma na kushuhudia upatikanaji wa huduma kwa wanachama wetu na kupata maoni yao, katika kuwa karibu na wanachama wetu kwa wiki hii mrejesho tumeupata toka kwa wanachama wetu unaonyesha wanachama wetu wamekuwa wakipata huduma nzuri na bora"alisema Odhiambo

Odhiambo aliishukuru serekali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwa kusimamia nidhamu kwa watumishi pamoja na kuondoa tatizo la uhaba wa dawa na vitendanishi kwani hivi sasa vituo vingi vina dawa za kutosha.

Meneja huyo pia amehaidi kuyafanyia kazi maoninyote yaliyotolewa na wanachama wa mfuko huo kwa kushirikiana na watoa huduma.Maofisa wa hao wa mfuko wametembelea vituo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa pamoja na Bukoba town Health.mwingine,Odhiambo amehadi kuyafanyia kazi kwa haraka maoni yaliyotolewa na wanachama kwa kushirikiana na watoa huduma.

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera Dkt John Mwombeki ameshukuru mfuko wa bima ya afya (NHIF) kwa msaada kwakuwa utasaidia kuboresha huduma kwa wagonjwa wanaolazwa hapo.Alisema hospitali inafanya jitihada mbali mbali za kutatua changamoto ya muda wa upatikani wa huduma ikiwa ni pamoja na kuajiri madaktari wa muda.
Meneja wa mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Kagera akiongea na wagonjwa waliolazwa katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera katika wiki ya maadhimisho ya huduma kwa wateja 
Meneja wa NHIF Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akiongea na wanachama wa mfuko huo waliofika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwaajili ya kupata matibabu.
Uongozi wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Kagera wakikabidhi mashuka 60 kwa uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya huduma kwa wateja.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KOZI MBALIMBALI KATIKA CHUO CHA USTAWI WA JAMII


MICHUZI TV:MWIZI NA MDOKOZI HAWA HAPAAA...

DIAMOND ALIVYOMWAGA MISAADA KWA WANATANDALE,WAIBUA HISIA TOFAUTI

Babu Tale, Mkubwa Fella wafunguka haya kuhusu Diamond Platnumz

BENKI YA AZANIA YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA

$
0
0
Benki ya Azania yenye matawi yake sehemu mbali mbali nchini imeadhimisha wiki ya huduma kwa mteja, lengo kuu likiwa ni kuwashukuru wateja wake kwa kuwa nao bega kwa bega katika ukuaji wa benki hiyo.
Katika maadhimisho hayo benki ya Azania imewatembelea wateja kwenye sehemu zao za kazi lengo likiwa ni kuona namna gani wanaweza kuboresha huduma zao, mbali na hilo waliweza kutoa zawadi na vyeti kwa wateja wao lengo likiwa ni kuwashukuru kwa kuichagua benki hiyo. 
Baadhi ya wateja waliopatiwa Vyeti na Zawadi kwenye maadhimisho ya Wiki ya huduma kwa mteja.

Benki ya Azania imeelekeza nguvu zake katika kuhakikisha kila mteja anapata huduma bora kulingana na mahitaji yake.  
Baadhi ya wateja wakipata maelezo kutoka kwa watoa huduma.
Azania Bank bega kwa bega!
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

J&M VIRGO BIG SALE ....

Viewing all 109979 articles
Browse latest View live




Latest Images