Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

WALIMU WATANO SHULE YA KIMATAIFA HAZINA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUWAPA WATAHINIWA MITIHANI YA TAIFA

$
0
0
Na Karama Kenyunko,  blogu ya jamii
MWALIMU Mkuu wa  shule  ya  msingi ya Kimataifa  ya Hazina iliyopo Magomeni jijini Dar Es salaam na walimu  wake wanne leo  Septemba  26.2018  wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya  Hakimu  Mkazi  Kisutu  kujibu  tuhuma za kupata  mitihani ya Taifa ya darasa la saba na kufanya mawasiliano ya maudhui yake na watahiniwa wa shule hiyo isivyo halali. 

Mwalimu Mkuu huyo Patrick Cheche (43) Wa shule hiyo ambayo mara kwa mara imekuwa ikitangazwa kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya darasa la nne na la saba na walimu wenzake wamesomewa mashtaka yao leo mbele  ya  Hakimu  Mkazi  Mfawidhi Huruma  Shahidi.

Mbali na Cheche (43), anayeishi Mpinga Bagamoyo, washtakiwa wengine ni Laurence Ochien (30), Justus James (32), Nasri Mohamed (32) na Mambo Idd (32), ambao wote wakazi wa Dar es Salaam.

Akisoma hati  ya  mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi  Mutalemwa Kishenyi  akisaidiana na Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono amedai washitakiwa hao Septemba 4, mwaka huu, katika Jiji na Mkoa wa  Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama  ya kutenda kosa la kuingilia mitihani ya Taifa ya darasa la saba isivyo halali.

Washtakiwa katika Shtaka hilo la  kula njama wanashtakiwa chini ya Sheria ya Kanuni za adhabu.

Katika shtaka la pili ambao washtakiwa hao wanashitakiwa chini ya Sheria ya Baraza la Mitihani la Taifa, wanadaiwa Septemba 5 mwaka huu katika shule hiyo ya Hazina, iliyoko Magomeni, kujibu, kinyume cha sheria walipata uwezo wa kupata mitihani wa taifa wa darasa la saba na kuonesha maudhui yake kwa watahiniwa waliosajiliwa Katina shule hiyo.

Pia imedaiwa Katika shtaka la tatu, Septemba 5 mwaka huu katika shule hiyo washtakiwa hao kwa makusudi walitoa mitihani kwa watahiniwa waliosajiliwa katika shule hiyo wakati hawakustahili kufanya hivyo.Hata hivyo washtakiwa wote wamekana kutenda kosa hilo  na wako  nje kwa dhamana.

 Kwa Mujibu wa  upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.Akisoma masharti ya dhamana,  Hakimu Shaidi amesema ili washtakiwa wawe nje kwa dhamana, kila mmoja anatakiwa awe na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho, vitambulisho na mmoja kati ya wadhamini hao awe anatambulika katika taasisi yoyote.

Pia kila mdhamini anatakiwa kusaini bondi ya Sh.milioni sita na mshtakiwa wa kwanza na wa pili watatakiwa kuwasilisha hati zao za kusafiria kwani wao ni raia wa Kenya.Hata hivyo washtakiwa hao walifanikiwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana kasoro mshtakiwa wa pili  ambaye alipelekwa rumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana.

Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 10, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama laa.

 Mwalimu Mkuu wa  Shule  ya  Msingi ya Kimataifa  ya Hazina iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam na walimu  wake wanne wakipandishwa katika kizimba cha Mahakama ya  Hakimu  Mkazi  Kisutu mapema leo.

RAIS MAGUFULI KUFUNGUA RASMI FLY OVER YA TAZARA KESHO

$
0
0
*Fly Over ya kwanza kujengwa nchini ,wananchi Dar watoa ya moyoni kwa Rais


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

FLY Over ya kwanza kujengwa nchini Tanzania inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho  na Rais  Dk.John Magufuli.

Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo ni wazi Tanzania imeingia kwenye historia ya aina yake katika kuhakikisha inaendelea kuboresha miundombinu ikiwemo ya Jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kupunguza adha ya msongamano wa magari.

Kwa sasa wananchi wa Dar es Salaam ambao wanapita katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere tayari wameanza kuonya raha ya uwepo wa Fly over hiyo iliyopo Tazara na kesho ndio siku ya uzinduzi rasmi.

 Taarifa ambayo imetolewa kwa vyombo vya habari jana na leo inaelezwa kuwa uzinduzi huo wa Fly Over ya Tazara utafanyika kesho asubuhi.Fly Over hiyo tayari imepewa jina la Mfugale.

Wakati uzinduzi huo ukisubiriwa kwa hamu na Watanzania na hasa wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam baadhi ya wananchi wametoa maoni yao kuhusu kukamilika kwa Fly over hiyo.

Wakizungumza zaidi na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam wananchi wamesema wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi madhubuti wa Rais Dk.John Magufuli kwa kuhakikisha ujenzi wa Fly Over hiyo unakamilika kwa wakati.

Wamesema wameanza kuona namna ambavyo kero ya msongamano wa magari iliyokuwepo eneo la Tazara ambayo kwa sasa haipo tena.

"Tunamshukuru Rais Magufuli kwa namna ambavyo Serikali yake ilivyodhamiria kuboresha maisha ya wananchi na hasa katika hili la ujenzi wa miundombinu.Imesaidia kutuondolea adha ya kutumia muda mwingi katika foleni ya Tazara ambayo kwetu ilikuwa kero kubwa.

" Nchi yetu imeingia kwenye historia ambapo sasa nasi Watanzania tunayo nafasi ya kujivunia kukamilika kwa Fly Over hii ya Tazara,"amesema Shaban Chuma mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam.

Jamila Jonathan amesema hakuwa akifikiria kama ipo siku katika Jiji la Dar es Salaam kutakuwa na Fly over lakini anamshukuru Rais kwani ameweza kufanikisha hilo.

"Nimesikia kesho ndio inazinduliwa rasmi.Nashukuru binafsi nimeonja raha ya kupita katika Fly over ya Tazara.Hongera Rais wetu kwa kutuondolea  foleni iliyokuwa Tazara," amesema Jonathan ambaye ni Mkazi wa Pugu Stesheni.

 Ameongeza anatamani kuona katika makutano yote ambayo yanachangamoto kubwa ya msongamano basi yanakuwa na Fly over huku akieleza anafahamu kuwa kuna ujenzi unaendelea Ubungo ambao lengo ni kupu guza msongamano, hivyo anatoa pongezi kwa Serikali ya Rais Magufuli ambayo ikisema inatekeleza.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI MKAZI WA AfDB NA MABALOZI WAWILI

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Dkt. Alex Mubiru ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha.

Makamu wa Rais amesema kuwa AfDB imeahidi kuendelea kushirikiana na kuisaidia Tanzania kutokana na hatua kubwa ya kimaendeleo ambayo nchi yetu imeonyesha.Pamoja na mambo mengine Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika alisema kuwa wapo hapa kusaidia Serikali ya Tanzania pamoja na Watu wake.

Wakati huo huo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alikutana na kufanya Mazungumzo na Balozi wa Kenya nchi Mhe. Dan Kazungu ambaye alifika Ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha.Mwisho Makamu wa Rais alikutana na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida ambaye amemaliza muda wake hapa nchi.

Makamu wa Rais alimshukuru Balozi Yoshida kwa ushirikiano wote alioutoa kwa kipindi chote alichokuwa hapa nchini.Nae Balozi Yoshida aliishukuru Serikali ya Tanzania pamoja na watu wake kwa Ushirikiano mzuri waliompa  kwa kipindi chake alichohudumu kama Balozi wa Japan hapa nchini.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Japan nchini anayemaliza muda wake nchini Mhe. Masaharu Yoshida aliyefika Ofisini kwa Makamu wa Rais leo Ikulu jijini Dar es Salaam kuaga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Alex Mubiru (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha leo Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Alex Mubiru (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kujitambulisha leo Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Kenya nchini Mhe. Dan Kazungu (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam kujitambulisha. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Kenya nchini Mhe. Dan Kazungu (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam kujitambulisha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya picha ya Mwanamke shujaa katika Historia ya Kenya aliyefahamika kwa jina la Mekatilili Wa Menza kutoka kwa Balozi wa Kenya nchini Mhe. Dan Kazungu (kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam kujitambulisha. 

RAIS AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WAKALA WA UCHAPAJI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara Habari,Utalii na Mambo ya Kale,Uongozi wa Bodi ya Uwakala wa Uchapishaji wa Serikali na Wafanyakazi wa kiwanda cha Wakala wa Uchapaji ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo katika kuzungumzia mambo mballi mbali ya kiutendaji wa Kazi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara Habari,Utalii na Mambo ya Kale,Uongozi wa Bodi ya Uwakala wa Uchapishaji wa Serikali na Wafanyakazi wa kiwanda cha Wakala wa Uchapaji ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo katika kuzungumzia mambo mballi mbali ya kiutendaji wa Kazi
Viongozi wa Wizara ya Habari,Utalii na Mambo ya Kale,Uongozi wa Bodi ya Uwakala wa Uchapishaji wa Serikali na Wafanyakazi wa kiwanda cha Wakala wa Uchapaji wakiwa katika kikao cha siku moja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi katika Uongozi wa Wizara Habari,Utalii na Mambo ya Kale,Uongozi wa Bodi ya Uwakala wa Uchapishaji wa Serikali na Wafanyakazi wa kiwanda cha Wakala wa Uchapaji pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Mfanyakazi wa Kiwanda cha Wakala wa Uchapaji wa Serikali Jamal Khamis Juma alipokuwa akichangia katika kikao cha siku moja cha Uongozi wa Kiwanda hicho kilichofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),katika mkutano ulijumuisha Uongozi wa Wizara Habari,Utalii na Mambo ya Kale,Uongozi wa Bodi ya Uwakala wa Uchapishaji wa Serikali na Wafanyakazi wa kiwanda cha Wakala wa Uchapaji.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati pichani) akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Uchapaji wa Serikali Nd,Perera Ame Silima wakati wa kikao cha Uongozi wa Wizara Habari,Utalii na Mambo ya Kale,Uongozi wa Bodi ya Uwakala wa Uchapishaji wa Serikali na Wafanyakazi wa kiwanda cha Uchapaji ulipokutana na Rais, leo katika Ukumbi wa Ikulu MJini Zanzibar,
Picha na Ikulu.

ALIYEWAHI KUWA IGP SAMUEL H. PUNDUGU AFARIKI DUNIA

Chuo Kikuu mzumbe chaendesha Mafunzo ya Usafrishaji na Manunuzi

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
CHUO Kikuu Mzumbe kimesema kinaendelea kutoa elimu bora ikiwa ni katika kuendana na wakati ya kuhakikisha taaluma inayotolewa ni endelevu.

Hayo ameyasema Mkuu wa Tawi la Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Honest Ngowi wakati akifungua mafunzo ya masuala ya usafrishaji na manunuzi kwa taasisi mbalimbali za ulinzi, mamlaka na Halmashauri katika kuhakikisha masuala ya usafirishaji na manunuzi yanaleta maendeleo.

Amesema mafunzo hayo yanafadhiliwa Taasisi ya Kuehne na kuendeshwa na  Chuo Kikuu Mzumbe amesema kuwa aliyeanzishwa taasisi hiyo amekuwa bilionea katika masuala ya usafirishaji na manunuzi ambapo ni kuhakikisha watu wanapata mbinu mpya za usafirishaji na manunuzi.

Mratibu wa mradi huo katika Chuo Kikuu Mzumbe Dk. Omary Swalehe amesema kuwa mradi huo ni wa miaka mitatu ambapo nia kutoa mafunzo kwa taasisi mbalimbali katika masuala ya usafirishaji na manunuzi.

Amesema kuwa hadi sasa wameshafanya katika awamu mbili ambapo katika maeneo tofauti ikiwa ni kuwajengea mbinu mpya za usafrishaji na manunuzi na kuweza kuona tija katika maendeleo ya nchi.
 Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam Profesa Honest Ngowi akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya watu wa masuala ya usafirishaji na manunuzi wa taasisi za Serikali na Ulinzi katika Tawi hilo
 Mratibu wa mradi huo katika Chuo Kikuu Mzumbe Dk. Omary Swalehe akizungumza na waandishi habari kuhusiana na mradi wa masuala ya usafirishaji na manunuzi.

Baadhi ya wadau wakiwa katika mafunzo ya usafirishaji na manunuzi.

OOHOOO YALE YALEEEEE....

$
0
0
 Kamera ya Globu ya Jamii, ililinasa tukio hili la ajali ya Lori lililobeba nguzo za umeme za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Basi la Kampuni ya Tilisho kwa nguzo zilizokuwepo kwenye lori hilo kugonga sehemu ya juu ya basi hilo, lililokuwa limepunguza mwendo katika sehemu ya kivuko cha watembea kwa miguu, eneo la Same, Mkoani Kilimanjaro. 
 Askari wa Usalama Barabarani wa Kituo cha Same (kulia) akipima ajali hiyo huku mashuhuda wa tukio hilo wakiwa wamemzunguka.
hivi ndivyo hali ilivyokuwa.

SUMATRA YAENDELEA KUFANYIA KAZI AGIZO LA NAIBU WAZIRI NDITIYE

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Udhibiti ya Usafiri wa Maji na Nchi Kavu (Sumatra) imesema kuwa inafanyia kazi agizo la Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye kuhusiana na safari za masafa ya kuanzia masaa nane kuanza kuondoka katika kituo cha mabasi Ubungo saa 11 pamoja na kuanza kwa safari za Dodoma-Dar es Salaam kwa masaa 24.

Akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara wa Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), Johansen Kahatano amesema kuwa katika wiki mbili alizotoa Naibu Waziri huyo wanaendelea kufanyia kazi kwa kushirikiana na jeshi la polisi na baada ya hapo watawatangazia wananchi.

Amesema kuwa katika kuanza huko wanaangalia mazingira ya usalama wa abiria kutoka muda uliozoeleka na kuingia muda mwingine wa kufanya safari hizo.

“Bado tunaendelea kufanyia kazi agizo la Naibu Waziri Nditiye na tukimaliza kazi kuangalia mazingira ya usafiri huo kuanza safari saa 11 na ile ya Dodoma ya masaa 24 ni kuwatangazia wananchi ambayo itafabywa na (Sumatra)”amesema Kahatano.

Aidha amesema wananchi waendelee kuendelea na muda uliokuwepo katika kituo cha mabasi ubungo kuondoka saa 12 kukiwa na mabadiliko watapata taarifa juu ya mabadiliko hayo.
Basi zikikaguliwa kabla ya kuanza kuondoka katika kituo cha mabasi Ubungo kwa ajili ya safari za kwenda mikoa mbalimbali ya hapa nchini na nje ya nchi.

WATANZANIA WAASWA KULINDA UOTO WA ASILI KATIKA MAJIJI

$
0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
MRADI wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira Asili wa (Interact-Bio) chini ya Baraza la Kimataifa la Mazingira utashiriki katika maonyesho ya sekta ya ujenzi yatakayofanyika kwa siku tatu jijini Dar es Salaam kuanzia kesho kwa lengo la kuonyesha njia za kiubunifu za kuwawezesha wakazi wa mijini kunufaika na viumbe na mazingira asilia.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Mazingira ya Nipe Fagio, Bi. Ana Rocha amesema leo kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba mradi huo umejenga bustani ya wima, gudulia la kuhifadhia mbolea na kifaa cha makazi ya wadudu (insect hotel) ili kuwawezesha wakazi wa jiji la Dar es Salaam watakotembelea maonyesho hayo kujionea namna ya kujumuisha na kunufaika na viumbe asili katika maisha ya mijini.

“Tunashirikiana na Halmashauri za Miji katika jitihada za kuongeza uelewa kuhusu manufaa yatokanayo na viumbe asili katika majiji ya Dar es salaam na Arusha pamoja na manispaa ya Moshi. Tunataka wananchi waone thamani ya kuwa na viumbe asili katika jiji na jinsi ambavyo jambo hili linaweza kutatua changamoto ya ongezeko la joto na changamoto nyingine zinazowakabili wakazi wa mijini kutokana na mabadiliko ya mazingira pamoja na hali ya hewa”. 

Amesema bustani wima ni bustani ambayo inatengenezwa kutokana na fremu za mbao, chuma, mbolea na chupa za plastiki kuotesha maua na mboga mboga kwenye kuta za nyumba au nguzo ikiwa ni njia mbadala wa kupanda mimea hiyo ardhini. Mbinu hii ya ubunifu inaweza kutumika kuweka mpaka wa mimea kati ya maeneo tofauti na kutoa nafasi kwa mimea hiyo kustawi huku ikiwasaidia wakazi wa mijini kutumia vizuri nafasi ndogo waliyonayo kwa ajili ya bustani.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mazingira wa Nipe Fagio, Bi Ana Rocha (kulia) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya mradi wa kimataifa wa uhifadhi wa Mazingira ya Asili wa “Interact Bio”. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mazingira wa Nipe Fagio, Bi Ana Rocha (kulia) akiwaonyesha waandishi wa habari Bustani wima ambayo imetengenezwa kutokana na fremu za mbao,chuma, mbolea na chupa za plastiki, na Kifaa cha Makazi ya wadudu ikiwa ni Mradi wa kimataifa wa uhifadhi wa Mazingira ya Asili wa “ Interact Bio”. 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mazingira wa Nipe Fagio, Bi Ana Rocha (Kulia) wakionyesha bango linaloonyesha umuhimu wa uoto asili katika majiji ya Dar es Salaam, Arusha na Moshi, (Kushoto) ni Afisa Tehama wa Taasisi ya Nipe Fagio Olarip Tomito.
Moja ya bustani za wima iliyotengenezwa na inazotarajiwa kufundishwa kwa wananchi ili zichangie katika utunzaji wa mazingira. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

JONESIA RUKYAA AKABIDHIWA RUNGU DERBY YA SIMBA NA YANGA

$
0
0
Na Agness Francis, Globu ya jamii.
ZIKIWA zimesalia Siku nne kuelekea mpambano wa  watani wa jadi Simba na Yanga kufanyika   katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar as Salaam, Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limemtangaza mwamuzi wa kati atakayecheza mechi hiyo.

Mchezo huo  wa Ligi kuu wa Tanzania Bara (TPL) utachezwa  Septemba 30 siku ukiwakutanisha miamba ya soka Nchini Simba na Yanga kuanzia majira ya saa 11 jioni.

Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam, Afisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo amesema kuwa mcezo huo utakaoanza saa 11 jioni utachezeshwa na Mwamuzi kutoka Mkoani Kagera Jonesia Rukyaa mwenye eji ya FIFA akisaidiwa na waamuzi wa pembeni Ferdinand Chacha wa Mwanza na Mohamed Mkono kutoka Tanga. huku msaidizi wa mezani akiwa Heri Sasii.

Amesema kuwa, mbali na michezo hiyo kutakuwa na mechi zingine za ligi kuu zitakazoendelea kwenye viwanja tofauti kuanzia kesho Alhamisi mpaka Jumamosi kukamilisha mzunguko wa nane na wa tisa.

Katika kuelekea mchezo huo wa vuta nikuvute kikosi cha Simba  kilichoweka  kambi yake   Jijini Dar es Salaam kitamkosa mshambuliaji wake mahiri John Boko aliyepewa kadi nyekundu  katika mchezo uliopita na mwadui fc,Apambo Yanga wakiwa mji kasoro bahari Morogoro kwa matayarisho ya mtanange huo.

Michezo iliyopita simba walitoka na ushindi wa mabao 3-1dhidi ya wachimba Madini  Mwadui ya Shinyanga, Yanga wakiibuka  kidedea kwa kuwafunga walima alizeti  Singida United mabao 2-0.

Kurwa na Doto hao wametofautiana pointi mbili ambapo Yanga ana alama 12 wakiwa wamecheza michezo 4,huku wekundu wa msimbazi Simba wana pointi 10 michezo 5 ligi kuu Tanzania bara TPL.

Timu hizo zimekutana kwa mara ya mwisho ligi kuu ya msimu wa 2017/18 Simba wakitoka na ushindi wa goli 1-0 goli likifungwa na Erasto Nyoni.

Jonesia aliwachezesha Simba na Yanga katika msimu wa 2016/17 Yanga akiibuka kidedea kwa kuondoka na ushindi wa goli 2-0.

Mashabiki wa pande zote mbili wakiwa na shauku kubwa  ya siku hiyo kushuhudia mchezo huo utakopigwa  jumapili hii septemba 30 majira ya saa 11 jioni kujua nani mbabe kati ya majirani hao wa Kariakoo kwa kiingilio cha VIP A  30000,VIP B na C 20000,kwa viti vya bluu,kijani na rangi ya chungwa ni 7000.

Muhimbili yaandika historia nyingine, yatenganisha watoto walioungana

$
0
0

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imefanya upasuaji mkubwa wa watoto pacha walioungana sehemu ya tumboni na kufanikiwa kuwatenganisha watoto hao wenye jinsia ya kiume.

Upasuaji huo ambao ulitumia saa tano ulifanywa na wataalamu wa upasuaji wa Muhimbili kwa kushirikiana na watalaamu kutoka Ireland. Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema hospitali imefanikiwa kufanya upasuaji kwa mafanikio na kwamba upasuaji huo umewezekana baada ya kuboreshwa kwa miundombinu ya utoaji huduma katika vyumba vya upasuaji ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wataalamu.

Prof. Museru amesema kuongezwa kwa vyumba hivyo kumesaidia kupunguza msongamano wa huduma ya upasuaji na hivyo kurahisisha utoaji huduma kwa watoto kutoka mara 4 hadi mara 10 kwa wiki.Amesema awali baada ya watoto hao kufikishwa Muhimbili walilazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha.

Naye Daktari Bingwa Upasuaji wa Watoto, Dkt. Petronila Ngiloi amesema walishirikiana vyema na wataalamu wa upasuaji kutoka Ireland katika kuhakikisha watoto hao wanatenganishwa na kwamba lengo kubwa lilikuwa ni kupunguza hatari yoyote inayoweza kutokea kwa watoto hao wakati wa upasuaji.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto, Dkt. Zaituni Bokhary amesema upasuaji huo ulihusisha timu ya wataalamu 10 wa upasuaji wa watoto, wauguzi na wataalamu wa tiba ya usingizi.

“Nashauri watoto pacha walioungana au wenye matatizo ya kiafya waletwe Muhimbili ili wafanyiwe uchunguzi wa kina na baada ya kujiridhisha tutawapatia huduma stahiki,” amesema Dkt. Bokhary.
 Watoto pacha wakiwa wamelazwa wodini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kabla ya kufanyiwa upasuaji na wataalamu wa hospitali hiyo kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Ireland.
 Mama wa watoto pacha waliokuwa wameungana, Ester Simon akiwa amembeba mmoja wa watoto pacha baada ya kufanyiwa upasuaji na kutenganishwa na mwenzake ambaye amebebwa na Meneja wa Jengo la Wazazi namba mbili, Bi. Stella Medadi Rushagara
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu upasuaji wa kuwatenganisha watoto pacha waliokuwa wameungana sehemu ya tumboni. Watoto hao hivi sasa wanaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji.
Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutoka kulia, Dkt. Zaitun Bokhary,  Dkt. Petronila Ngiloi na Dkt. Victor Ngotta wakiwafanyia upasuaji wa kuwatenganisha watoto pacha waliokuwa wameungana kwa kushirikiana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto kutoka Ireland, Prof. Martin Carbally. 

Article 1

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 
WIZARA ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 
imeziasa halmashauri kuhakikisha zinapima maeneo ya wananchi na kuyaingiza kwenye mfumo ili kutambua idadi ya viwanja na mashamba wanayopaswa kulipa na kupatiwa hati miliki. 

Imetoa rai kwa halmashauri hizo kutotumia kigezo cha kutopewa fedha na wizara hiyo kwa ajili ya bando la kuweka katika mfumo kama kikwazo cha kushindwa kukusanya mapato yatokanayo na ardhi.

Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Angeline Mabula.

Alisema , suala hilo ni aibu kwa halmashauri kudai wanakosa kiasi cha sh. 20,000 ama 30,000 ya vocha .

Angeline alieleza, halmashauri wasigeuze jambo hilo kama ni changamoto ya kushindwa kukusanya mapato yatokanayo na ardhi na kusubiri kupewa na wizara wakati hilo liko ndani ya uwezo wao.

“Mnakusanya mabilioni ya fedha kupitia viwanja mnashindwaje kukusanya mkiwa mnasubiri vocha ya shilingi 20,000 au 30,000 hili halikubaliki "

Angeline alifafanua,, halmashauri zihakikishe zinawezesha idara ya ardhi iweze kukusanya mapato badala ya kuiacha kama mtoto yatima .

“Tumerejesha maeneo mengi lakini nia njema ya kufanya hivyo baadhi halmashuri zimekiuka mnaweza kuwa na kasi ya kutaka maendeleo lakini unapaswa kufuata taratibu hatuwezi kutoa maeneo bila kufuata taratibu,” alisema Angeline. 

Ofisa ardhi mteule wilaya ya Kibaha ,Majaliwa Jafari alieleza viwanja 1,700 vimepimwa lakini havijauzwa ambapo Kisabi 800 Disunyala 700 .

Awali akisoma taarifa ya wilaya katibu tawala wa wilaya hiyo Sozi Ngate alisema , halmashauri ya wilaya ilikusanya milioni 504 na kutoa hatimiliki za kimila na imepima vijiji 22.

Anasema, mpango shirikishi wa matumizi bora ya ardhi umegusa maeneo tisa kati 25 vilivyopo ikiwemo Lukenge, Gumba, Magindu, Mpiji Station, Kwala, Dutumi, Minazimikinda, Mperamumbi.
 Mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama akizungumza wakati Naibu Waziri wa wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Angeline Mabula alipofanya ziara ya siku moja wilayani Kibaha.
 Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa akieleza jambo, wakati Naibu Waziri wa wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Angeline Mabula alipofanya ziara ya siku moja wilayani Kibaha.
Naibu Waziri wa wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Angeline Mabula ( wa katikati) akimsikiliza mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama (wa kwanza kulia )wakati alipofanya ziara ya siku moja wilayani Kibaha, (wa kwanza kushoto) ni mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa.
(Picha na Mwamvua Mwinyi) 

NSSF YASHIRIKI MAONESHO YA KWANZA YA MADINI MKOANI GEITA

$
0
0
          Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF limeshiriki maonyesho ya kwanza ya madini yanayoendelea mkoani Geita kwa lengo la kuwafikia kwa ukaribu zaidi watanzania wote watakaoshiriki maonyesho hayo kwaajili ya kutoa elimu na kuandikisha.

Maonyesho hayo ambayo yameshirikisha wadau wote wa sekta ya madini yameanza Septemba 24 hadi Agosti 30 2018 katika viwanja vya kalangalala mkoani Geita.

Kufuatia mabadiliko ya sheria, NSSF sasa inalenga kuandikisha wale wote waliopo sekta binafsi ya ajira na sekta isiyo rasmi, ili wanufaike na mafao yatolewayo na shirika hilo ikiwemo fao la matibabu bure kwa mwanachama na familia yake.

Akizungumza leo kutoka viwanja vya kalangalala Meneja wa NSSF Mkoa wa Geita Bwana Shaban Mpendu ametoa wito kwa watanzania wote kutembelea maonyesho hayo ya migodi na kufika katika banda la NSSF ili kuweza kupata elimu ya mafao yanayotolewa na NSSF pamoja na elimu ya hifadhi ya jamii kwa ujumla. 

Vilevile meneja amewataka wananchi hasa wa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi kujiandikisha na NSSF. Uandikishaji unaofanyika katika banda la NSSF ni pamoja na uandikishaji wa waajiri, wanachama na usaijili wa matibabu bure.
 Meneja wa NSSF  mkoa wa Geita akimkaribisha mgeni rasmi Mh Stanslaus Nyongo Naibu Waziri wa Nishati na Madini katika banda la NSSF kwenye maonyesho ya kwanza ya madini mkoani Geita
 Meneja wa NSSF mkoa wa Geita Shaban Mpendu akitoa elimu kwa wadau wa sekta ya madini juu ya huduma zitolewazo na nssf katika maeonyesho ya kwanza ya madini yanayoendelea mkoani geita
Afisa mafao wa NSSF mkoa wa Geita bi Annastazia Ngallaba akimjazisha fomu ya uandikishaji mdau aliyetembelea banda la nssf kupata elimu na kuelewa somo hatimaye akaamua kujisajili.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stanslaus Nyongo akipewa maelezo kwa ufupi katoka kwa Meneja wa NSSF Geita Ndugu Shaban Mpendu juu ya huduma zitolewazo na NSSF alipotembelea banda la NSSF muda mchache kabla ya ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo. 

AGIZO LA WAZIRI LUGOLA LAANZA KUTEKELEZWA

$
0
0
Ikiwa imepita miezi miwili tangu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kuagiza pikipiki zote zinazotumika kusafirisha abiria zifungwe tela katika kile kinachoaminika kudhibiti wimbi la ajali za bodaboda,Taasisi mbalimbali za Serikali zimekutana jijini Dodoma ikiwa ni mazungumzo ya awali kuelekea mkakati huo wa kupunguza ajali.

Akizungumza jijini Dodoma baada ya mkutano na ukaguzi wa pikipiki ya mfano iliyofungwa tela iliyotengenezwa na Shirika la Mzinga,lililoko chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, amesema Serikali imedhamiria kuondoa na kukomesha ajali za bodaboda pamoja na kulinda usalama wa watumiaji wa usafiri huo.

Akielzezea juu ya mazungumzo hayo yaliyokutanisha taasisi hizo, Katibu Mkuu Meja Jenerali Jacob Kingu, amesema Wizara yake kwa kushirikiana na wadau wengine kutoka taasisi za serikali; Shirika la Mzinga, Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Kiwanda cha Kutengeneza Magari (NYUMBU) na Jeshi la Polisi watahakikisha wanakuwa na mpango wa pamoja wa kuratibu na kuhakikisha mkakati huo utakaosaidia kupunguza ajali unakamilika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akiwa amepanda Pikipiki ya mfano iliyotengenezwa na Shirika la Mzinga, lililoko chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ikiwa ni hatua za awali katika utekelezaji wa agizo la Serikali ili kukabiliana na ajali za bodaboda pamoja na usalama wa watumiaji wa chombo hicho cha usafiri. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akiwa amepanda Pikipiki ya mfano iliyotengenezwa na Shirika la Mzinga, lililoko chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ikiwa ni hatua za awali katika utekelezaji wa agizo la Serikali ili kukabiliana na ajali za bodaboda pamoja na usalama wa watumiaji wa chombo hicho cha usafiri. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu(aliyepanda pikipiki), akisikiliza maelezo ya kiufundi kutoka kwa mmoja wa wataalamu kutoka Shirika la Mzinga, Whemy Lyimo(kulia) waliotengeneza pikipiki hiyo yenye tela ikiwa ni hatua za awali katika utekelezaji wa agizo la Serikali ili kukabiliana na ajali za bodaboda pamoja na usalama wa watumiaji wa chombo hicho cha usafiri, Kushoto ni dereva wa pikipiki hiyo,Stanley MsuyaTukio hilo limefanyika leo, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akizungumza na timu ya wataalamu kutoka Taasisi za Serikali baada ya kukagua Pikipiki ya mfano iliyotengenezwa na Shirika la Mzinga, lililoko chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ikiwa ni hatua za awali katika utekelezaji wa agizo la Serikali ili kukabiliana na ajali za bodaboda pamoja na usalama wa watumiaji wa chombo hicho cha usafiri. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA TAASISI YA WALEMAVU

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Taasisi ya watu wenye ulemavu ya Dk Reginald Mengi (DRMP), Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Dk Reginald Mengi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi, Shimimana Ntuyabaliwe.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipiga makofi baada ya kuzindua Taasisi ya watu wenye ulemavu ya Dk Reginald Mengi (DRMP), Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Dk Reginald Mengi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi, Shimimana Ntuyabaliwe.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifunua kitambaa kuzindua Taasisi ya watu wenye ulemavu ya Dk Reginald Mengi (DRMP), Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Dk Reginald Mengi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi, Shimimana Ntuyabaliwe na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, vijana na Ajira, Anthony Mavunde.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na mlemavu wa viungo aliyepooza viungo baada ya kupata ajali akiwa shuleni, kabla ya kuahidi kumsomesha mpaka hapo atakapomaliza elimu yake, baada ya kuzindua Taasisi ya walemavu ya Dk Reginald Mengi, Dar es Salaam.

(Picha  na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William awasili Tanzania leo

$
0
0
Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla alipowasili Nchini leo Septemba 26, 2018 kwa ziara maalu. Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na kushoto Balozi wa Uingereza nchini, Bi. Sarah Cooke.
NA ANDREW CHALE, DAR

MJUKUU wa Malkia wa Uingereza, Prnce William ametua Nchini Tanzania jioni ya leo Septemba 26, 2018 kwa ziara maalum ya siku tatu ambapo kesho Septemba 27, anatarajiwa kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano Ikulu ya Magogoni Jijini Dar es Salaam.

Prince William katika kukutana na Rais Magufuli atafanya mashauriano kuhusu juhudi zinazochukuliwa na Tanzania katika kukabiliana na ujangili na ulanguzi wa wanyama pori.

Prince William ametua mchana wa leo na ujumbe wake ambapo amepokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Katiba Sheria Profes Kabudi  pamoja na viongozi wengine akiwemo Balozi wa Uingereza hapa Nchini na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha Nchi zao Nchini.

Akiwa uwanjani hapo wa Mwalimu Julius Nyerere eneo la wageni mashuhuri, Prince William amepata wasaha wa kuteta na viongozi hao kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa ratiba ya Mwanamfalme huyo, kesho hiyohiyo ya Septemba 27, anatarajiwa kutembelea bandari ya Dar es salaam katika kitengo cha Polisi Marine (Marine Polisi Unit) na ambapo pia atatembelea maeneo mbalimbali ikiwemo yale ya kupokelea mizigo, upekuzi na ukaguzi wa vinavyoingia na kutoka katika eneo hilo la bandari.

Pia Prince William anatarajiwa kukutana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo Mpingo Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Prince William na ugeni wake huo unatarajiwa kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi na baadae Chuo cha Wanyamapori cha Mwika (College of African Wildlife Management, Mwika (CAWM), kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro na kisha kuendelea na ziara yake Nchini Kenya.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa lengo kuu ya ziara hiyo ya Prince William ni pamoja na kufuatilia juhudi za kukabiliana na ujangili na uhifadhi wa wanyama.

Prince William atafanya ziara hiyo katika wadhifa wake kama rais wa mashirika yanayotetea uhifadhi wa wanyama ya United for Wildlife na Tusk Trust. Amekuwa pia mlezi wa shirika la Royal African Society linalolenga kukuza uhusiano kati ya Afrika na Uingereza na hushiriki sana juhudi za kukabiliana na ujangili.
Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William akisalimiana na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Afrika Mashariki waliomwakilisha Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Augustino Maige. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla.

RAIS DKT. MAGUFULI KUFUNGUA "FLYOVER" YA MFUGALE, TAZARA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kuutaarifu Umma kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atakuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za ufunguzi wa Flyover ya Mfugale katika makutano ya barabara za Mandela na Nyerere eneo la TAZARA tarehe 27 Septemba, 2018 jijini Dar es Salaam.

Ujenzi wa Flyover ya Mfugale ulianza tarehe 15 Oktoba, 2015 ambapo jiwe la msingi liliwekwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli tarehe 16 Aprili, 2016.

Flyover ya Mfugale inajumuisha barabara mbili za juu; moja kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kuelekea katikati ya jiji na nyingine kutoka katikati ya jiji kuelekea Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Kukamilika kwa Flyover ya Mfugale kutapunguza msongamano wa magari katika eneo la TAZARA na kupunguza muda wa safari toka katikati ya jiji kwenda Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa wa  Julius Nyerere na kurudi, na pia kurahisisha usafiri na usafirishaji kwa watumiaji wa barabara za Mandela na Nyerere.

Wananchi wote mnakaribishwa katika ufunguzi huo.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
26 Septemba, 2018.

TRA YATOA ELIMU YA MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU

$
0
0
JOSEPH MPANGALA, MTWARA      
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imetoa mafunzio kwa Wafanyabiashara wa Mkaoni Mtwara kuhusiana na Msamaha wa Riba na adhabu ya malimbikizo ya Madeni ya kodi kwa lengo la kuwawezesha wafanyabishara hao kuweza kutambua masuala yanayohusu Kodi pamoja na kuwahi Kuomba Msamaha wa Riba na Adhabu zake.
Akifungua mafunzo hayo kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda,Katibu Tawala Msaidizi  wa Mkoa wa Mtwara  Renatus Mongogwela amesema katika kipindi kirefu walipakodi wengi walikuwa wanashindwa kulipa Kodi zao kikamilifu kutokana na kuelemewa na malimbikizo makubwa ya Madeni yaliyotokana na Riba na Adhabu.
“Nipende Kuwafahamisha Kuwa Serikali imesikia kilio cha Walipa kodi na kuweka taratibu maalim wa kuyaondoa hayo malimbikizo ya madeni ya riba,hivyo niwasihi ndugu zangu tutumie fursa hii adhim kuweka sawa masuala yenu ya kikodi na kupitia Msamaha huu Serikali inaaamini walipa kodi wataanza upya kuzifuata na kuzitii Sheria hizi”amesema Mongogwela.
Mafunzo hayo ya Siku moja yamejumuisha mabadiliko ya Sheria ya kodi ya  mwaka 2018 pamoja na mfumo wa maadili wa watumishi wa mamlaka ya Mapato Tanzania {TRA} kwa lengo la kuwawezesha wafanyabiashara  kuweza kutoa maoni na kapata huduma Bora.
 Katibu Tawala Msaidi wa Mkoa wa Mtwara Renatus Mongogwela akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na mamlaka ya mapato Tanzania {TRA} juu ya elimu ya Msamaha wa riba na adhabu kwa wanyabishara wa Mkoa wa Mtwara.
 Afisa maadili mwandamizi Mika Kiremera  kutoka mamlaka ya mapato Tanzania {TRA}makao makuu akiwasilisha mada kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi pamoja na maadili kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Mtwaa.
 Msimamizi wa Shule ya Sekondari Aquinas Sister Paula Ngagani akiongea na Afisa Mkuu wa elimkwa Mlipa Kodu Makao Mkauu  Julius Ceasar  pamoja na Meneja wa Mamlaka ya mapato mkoa wa Mtwara  Naomi Mwaipola mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya TRA kwa Wafanyabiashara Mkoa wa Mtwara.
 Baadhi ya wafanyabishara waliohudhuria Mafunzo yaliyoandaliwa na Mamlaka ya mapato Tanzania {TRA}Mkoani Mtwara kwa lengo la kutoa elim ya msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya Kodi,mabadiliko ya sheria ya kodi ya mwaka2018 pamoja na Maadili.
 Wafanyabishara Mkoa wa Mtwara wakiwa pamoja na maafisa wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA mara baada ya Kumalizika kwa mafunzo ya siku moja kuhusina na elimu ya Msamaha wa Riba na adhabu pamoja na maadili kwa watumishi wa TRA>

BancABC YAWAKUTANISHA WATEJA PAMOJA NA WADAU WAKE KATIKA MKUTANO ULIOFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0



Muwakilishi wa wadau wa BancABC Mr. Michael Wilkerson, akizungumza na wateja pamoja na wadau wa BancABC wakati wa mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena Dar es Salaam. Mkutano huo ulikuwa mahususi kwa ajili ya kusisitiza juu ya ahadi ya BancABC kuendelea kutoa na kutengeneza bidhaa bora kwa ajili ya wateja wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Mara Group Mr. John Staley akiongea na wateja, wadau na wafanyakazi wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam hivi karibuni, kwa lengo la kusisitiza ahadi ya kuendelea kutoa bidhaa za kipekee haswa kwa “retail banking” ambayo anajivunia uzoefu wake. Stejini ni muwakilishi wa wanahisa Mr. Michael Wilkerson, Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa BancABC Mr. Imani John.
Wateja wa BancABC walipowasili kwa ajili ya hafla. Hafla hii iliwaleta pamoja wadau, wateja, uongozi pamoja na wafanyakazi wa benki.
Katika picha ya pamoja, toka kulia Mkurugenzi mtendaji wa Atlas Mara Group Mr John Staley, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Mr. Imani John pamoja na muwakilishi wa wanahisa wa BancABC Mr. Michael Wilkerson
Wafanyakazi wa BancABC katika picha ya pamoja baada ya hafla yenye mafanikio iliyoandaliwa na BancABC

NMB KUCHOCHEA UCHUMI WA VIWANDA TANZANIA

$
0
0

BENKI ya NMB Plc imesema itaendelea kusaidia jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kukuza uchumi wa viwanda nchini Tanzania.

Akizungumza na vyombo vya habari jana katika mkutano mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaoendelea jijini Dodoma, Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi, amesema benki yake imetengeneza program mbalimbali za kusaidia kuchochea kasi ya uchumi wa viwanda nchini Tanzania.

Hata hivyo, amesema, benki ya NMB ambayo inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 31, ni miongoni mwa taasisi chache za fedha hapa nchini zinazofanya kazi kwa ukaribu sana na Serikali.“Kwa mfano, NMB imekuwa mdhamini mkuu wa mikutano mikuu ya ALAT miaka sita sasa, na kwa mwaka huu, benki imetoa udhamini wa shilingi milioni 100. Hii inaonyesha utayari wetu katika kufanya kazi pamoja na Serikali,” alisema.

Aidha, amesema NMB inafanya kazi pamoja na wilaya na halmashauri zote nchini, ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo rafiki kwa wafanyakazi wa Serikali.“Lengo ni kuhakikisha huduma za kifedha za NMB zinawafikia Watanzania wote nchini hususani wale wanaoishi katika jamii za vijijini ambapo kunachangamoto nyingi za kimaisha na kiuchumi,” alieleza.

Amesema kwa sasa benki imetenga kiasi cha shilingi bilioni 500 kwa ajili ya kutoa mikopo rafiki kwa wajasiliamali wa kati na wadogo nchini, lengo kuu likiwa ni kuchochea uchumi wa viwanda kupitia sekta ya kilimo na mifugo.“Uchumi wa viwanda unategemea sana sekta ya kilimo na mifugo na hivyo, NMB itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia wajasiliamali wadogo wadogo kupata mikopo nafuu na rafiki ili waweze kujikita katika miradi husika,” aliongeza.
Wajumbe wa Mkutano Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT) wakishiriki mkutano huo ndani ya ukumbi wa mikutano wa Dr. Jakaya Kikwete Jijini Dodoma- mkutano huo umedhaminiwa na Benki ya NMB. 
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT) wakipata maelezo walipotembelea banda la Maonesho la Benki ya NMB Ukumbi wa Dr. Jakaya Kikwete Jijini Dodoma jana- mkutano huo umedhaminiwa na benki ya NMB.

Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma jana kwenye Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT) unaoendelea Jijini hapo. Mkutano huo unaoshirikisha zaidi ya washiriki 500 kutoka Halmashauri, Wizara na Idara mbalimbali za Serikali umedhaminiwa na benki hiyo. 

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>