Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live

CBA BANK, DMF WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KWA AJILI YA WATOTO NJITI HOSPITALI YA WILAYA YA SAME

0
0
 Waziri wa Madini na Mlezi wa Taasisi ya Doris Mollel, Angellah Kairuki (wa tatu kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule (katikati) pamoja na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa wateja binafsi wa benki ya CBA Tanzania, Julius Konyani (wa pili kushoto) wakiungana na watu wengine kumsikiliza Afisa Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Wilaya ya Same, Entuja Mbwambo wakati akionyesha namna ya kutumia mashine maalum ya kumsaidia mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati (Njiti) kupumua vilivyotolewa na Benki ya CBA Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Doris Mollel kwa hospitali hiyo, ambavyo thamani yake ni zaidi ya shilingi 20 milioni.
Waziri wa Madini na Mlezi wa Taasisi ya Doris Mollel, Angellah Kairuki pamoja na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa wateja binafsi wa benki ya CBA Tanzania, Julius Konyani wakishirikiana kupanda mti katika eneo la Hospitali ya Wilaya ya Same, muda mfupi baada ya kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 20 milioni, vilivyotolewa na Benki ya CBA Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Doris Mollel kwa hospitali hiyo kwa ajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti).
Waziri wa Madini na Mlezi wa Taasisi ya Doris Mollel, Angellah Kairuki pamoja na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa wateja binafsi wa benki ya CBA Tanzania, Julius Konyani  wakimsikiliza Mganga Mkuu wa wilaya ya Same, Dkt Godfrey Andrew wakati akifafanua jambo kuhusu vifaa vita alivyovipokea Hispitalini hapo, vilivyotolewa na Benki ya CBA Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Doris Mollel kwa ajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti).
Waziri wa Madini na Mlezi wa Taasisi ya Doris Mollel, Angellah Kairuki pamoja na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa wateja binafsi wa benki ya CBA Tanzania, Julius Konyani, wakimjulia hali mtoto Amani John aliyelazwa katika wadi ya watoto ya Hospitali ya Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro aliyepata ajali ya kuungua na moto.


MAGAZETI YA LEO ALHAMISI SEPTEMBA 27,2018

TAWLA YAANDAA MKUTANO WA KUIMARISHA UWEZO WA MAJUKWAA YA WANAWAKE KWA VYAMA VYA SIASA

0
0
Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wanawake (TAWLA) Bi. Lulu Ng'wanakilala amesema TAWLA inatekeleza mradi wenye kuongeza ushiriki wa wawakilishi wanawake na vijana katika shughuli za kisiasa na Uongozi katika serikali na Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ikiwa ni pamoja na ngazi za serikali za mitaa na vijiji.

Ngw'anakilala ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa kuimarisha uwezo wa majukwaa ya wanawake na vijana katika kujadili Changamoto zinazowakabili wanawake katika kushiriki kwenye shughuli za kisiasa uliofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.

Amesema lengo la mkutano huo ilikuwa kujengeana na kuimarisha majukumu na kujadili Changamoto zinazowafanya wanawake washindwe kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kiuongozi na siasa.

"Nataka wanawake tuliomo katika mkutano huu tukishajadiliana tutoe mapendekezo namna ya kuainisha na kutatua changamoto ili kumwezesha mwanamke kushiriki kikamilifu katika shughuli za kisiasa na kupata fursa ya kuwa kiongozi katika serikali na Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Mkutano huo ulijumuisha majukwaa ya wanawake katika ngazi mbalimbali wakiwemo wabunge, Madiwani na wale waliowahi kugombea ubunge na udiwani kutoka vyama vya siasa vya CCM, CHADEMA, CUF na ACT Wazalendo.
Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wanawake (TAWLA) Bi. Lulu Ng'wanakilala akizungumza wakati akifungua mkutano wa kuimarisha uwezo wa majukwaa ya wanawake na vijana katika kujadili Changamoto zinazowakabili wanawake kushiriki kwenye shughuli za kisiasa uliofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo.
Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wanawake (TAWLA) Bi. Lulu Ng'wanakilala akisisitiza jambo wakati akizungumza alipofungua mkutano.
Sara Kinyaka Mwanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) akitoa mada katika mjadala wa mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam 
Isabela Nchimbi Mwanasheria wa Chama cha Wananasheria wanawake (TAWLA) akifafanua jambo wakati akichangia hoja katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.

SERIKALI YAWATAKA WATAFITI KUFANYA TAFITI ZENYE TIJA NA KUBORESHA SERA YA MAENDELEO

0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Serikali imewataka watafiti kote nchini kufanya tafiti katika maeneo ya vipaumbele vya serikali, badala ya kufuata matakwa ya wafadhili. Amesema kufanya hivyo kutasaidia kuboresha sera na mipango ya maendeleo itakayowezesha kufikia malengo katika sekta mbali mbali ikiwemo afya na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025 .

Akizungumza katika Kongamano la kuwasilisha tafiti za dawa za kulevya lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amewataka watafiti kufanya tafiti zitakazozingatia takwimu sahihi ambazo zinachangia katika kuboresha sera na programu za afya. 

"Natoa rai msifanye utafiti kwa sababu tu kuwa wafadhili wanatupatia fedha na msifanye tafiti na mkaridhika kwa vile tafiti zenu zimechapishwa kwenye majarida, bali mje na zile zitakazofanya mabadiliko ya sera mbali mbali hususani kuboresha upande wa afya," amesema. Nae Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha MUHAS Prof. Andrew Pembe amesema matokeo ya utafiti yanaonyesha tatizo la matumizi ya madawa ya kulevya bado ni kubwa na waathirika wa madawa ya kulevya hawawezi kushiriki katika shughuli za kuzalisha. 

Ameongeza kuwa watumiaji wengi wa madawa ya kulevya wanajishughulisha katika vitendo vya uharifu, na wanauwezo mkubwa wa kupata magonjwa mbali mbali likiwemo UKIMWI. Upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS anayeshughulikia Taaluma, Tafiti na Ushauri Prof. Appolinary Kamuhabwa amesema kuwa chuo kimejipanga kutoa taarifa inayotokana na matokeo ya tafiti ambayo itakuwa imeandikwa kwa lugha nyepesi na kuwapelekea wizara ya afya ambao badae wanaweza kuangalia ni mambo gani yanaweza kuwasaidia katika kuborsha sekta ya afya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (ambaye alikuwa mgeni rasmi) akizungumza katika Kongamano la kuwasilisha tafiti za dawa za kulevya lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) na kufanyika jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna- Kajunason/MMG. 
Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha MUHAS Prof. Andrew Pembe akitoa maneno ya kutambulisha Kongamano la kuwasilisha tafiti za dawa za kulevya lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) na kufanyika jijini Dar es Salaam. 
Wageni waalikwa na Wanafunzi wa MUHAS waliohudhulia kongamano hilo
 
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS anayeshughulikia Taaluma, Tafiti na Ushauri Prof. Appolinary Kamuhabwa akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Dkt. Ndugulile. 

HOW TO MAKE MANDAZI FROM LONDON BY BAYSAN

PROFESA MBARAWA AAGIZA MKANDARASI ACHUNGUZWE NA TAKUKURU

0
0

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa ameagiza mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji wa Manga uliopo Wilaya ya Mpanda Mjini, mkoani Katavi achunguzwe na TAKUKURU kutokana na kutumia mabomba yasiyokidhi viwango. 

Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo wakati wa kikao cha majumuisho na uongozi wa mkoa mara baada ya kumaliza ziara yake ya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Katavi.

Mradi huo wa Manga wenye thamani ya Shilingi milioni 575 unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingia mjini Mpanda (MUWASA) na kutekelezwa na mkandarasi anayejulikana kama Nyalinga Investment Co. Ltd, uligundulika kuwa una kasoro ya mabomba mara baada ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji mji wa Mpanda (MUWASA), Mhandisi Zacharia Nyanda kubaini ubovu wa mabomba hayo na kuyapeleka Shirika la Ubora wa Viwango Tanzania (TBS) kwa ajili ya vipimo na kuonekana hayakidhi viwango.

Amesema kuwa ripoti hiyo ya TBS imeonyesha kuwa kuna tofauti kubwa ya vipimo vya mabomba yaliyotumika na vipimo vinavyoonekana kwenye mkataba, hivyo kuthibitisha udanganyifu wa mkandarasi huyo na kumpongeza Mhandisi Nyanda kwa kugundua mapungufu hayo.

‘‘Nampa pongezi Mkurugenzi wa MUWASA kwa kugundua jambo hili; mabomba haya hayaonyeshi hata yametengenezwa wapi, achilia mbali kutofautiana kwa vipimo na vile vilivyo kwenye mkataba. Huu ni udanganyifu wa hali ya juu, ambao nimekuwa nikiusema kuhusu wakandarasi wababaishaji na sitafumbia macho wakandarasi wa aina hii’’, amesema Profesa Mbarawa.

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwaonyesha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mpanda Mjini ushahidi wa ripoti ya TBS juu ya mabomba mabovu yaliyotumika kwenye mradi wa Manga, mkoani Katavi. 
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mratibu wa Mradi, Mhandisi Edward Mulumba (kushoto) na mbele yao ni Mkurugenzi wa Mamalaka ya Maji mjini Tabora (TUWASA), Mhandisi Mkama Bwire. 
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwa na wakandarasi eneo la mradi Nzega. 

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO SEPTEMBA 26, 2018

Jumia na Amadeus zashirikiana kuzindua soko la ndege Afrika

0
0
Hii ni kufuatia huduma za ndege kupitia Jumia kukua kwa 400% ndani ya Julai 2017 na Julai 2018.

Katika kuadhimisha siku ya Utalii Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Septemba 27 ya kila mwaka, Jumia imejitanua tena katika huduma za ndege, safari hii ni kupitia ushirikiano baina yake na Amadeus, kampuni inayoongoza kwa teknolojia za usafiri duniani. Ushirikiano huu ni msingi wa soko jipya la huduma za ndege kwenye mtandao wa Jumia, ikiwa ni hatua nyingine mbele katika kufanya huduma za usafiri barani Afrika kuwa rahisi na nafuu.

Jukwaa hili linalenga kuwawezesha mawakala wa usafiri, ndege, na tovuti za usafiri kuleta masuala yote yahusuyo huduma za ndege mtandaoni, kwa kuwapatia wateja bei nzuri za huduma za ndege zinazopatikana. Takwimu za sasa zinaonyesha kwamba 90% ya soko la huduma za ndege bado liko nje ya mtandaoni wakati ni 10% tu ndiyo lipo mtandaoni. Hii inakuja kufuatia kuongezeka kwa wateja wa huduma za ndege kupitia Jumia, ikiwa imeongezeka kwa kasi mpaka kufikia 400% ndani ya kipindi cha Julai 2017 na Julai 2018.

“Jumia inaendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika bidhaa zenye ubunifu kwa wasafiri na watoa huduma za ndege ambazo zitawasaidia kufanya mapinduzi kwenye uendeshaji wa shughuli zao na kuongeza mapato,” anasema Kijanga Geofrey, Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia. “Tunalielewa soko na tunayashughulikia mahitaji yake. Jukwaa lenye ushindani litawaunganisha kwa pamoja watoa maudhui wote kutoa viwango vya chini na tozo ndogo ili kukidhi kuongezeka kwa mahitaji ya wasafiri kupata huduma bora zaidi kwa gharama nafuu,” anaongezea.

Soko pia litatoa uchambuzi wa taarifa ambazo watoaji huduma wa tiketi za ndege wanaweza kuzitumia kutambua fursa mpya, njia na kuwasaidia kutengeneza vifurushi vya wateja wa ndege wanaowalenga.

MAKONDA ASEMA FLYOVER YA MFUGALE ITANUSURU NDOA, ATUMA UJUMBE KWA RAIS

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kukamilika kwa Flyover ya Mfugale iliyopo Tazara kutasaidia kunusuru ndoa za watu wa mkoa huo.

Makonda amesema hayo leo mbele ya Rais Dk.John Magufuli wakati wa uzinduzi wa Flyover  ya Mfugale iliyopo makutano ya Tazara jijini Dar es Salaam ambapo amesema kwamba kukamilika kwa Flyover hiyo ni wazi sasa wananchi wanaondokana na changamoto ya foleni kubwa.

"Kuna ndoa za watu zimeingia kwenye kutoaminiana kwa sababu tu ya msongamano wa magari makutano ya Tazara.Wapo waliokuwa wanachelewa kurudi nyumbani na wakiulizwa na wenza wao wanasingizia foleni.

" Kuna baadhi yao walikuwa wanatumia foleni ya Tazara kama kificho kwani wanakwenda gesti na wakiulizwa wanasema walikuwa kwenye foleni,"amesema Makonda na kuongeza kwamba

"Sasa kuanza kutumika kwa flyover hii kutaimarisha ndoa kwani hakutakuwa na visingizio tena,"amesema Makonda huku akitumia nafasi hiyo kufikisha salamu za wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa Rais.

Pia amesema flyover hiyo itarahisisha shughuli za kiuchumi kwa mkoa wa Dar es Salaam ambapo ameeleza kufurahishwa kwake na namna ambavyo Rais Magufuli amedhamiria kuboresha maisha ya wananchi na hiyo imesababisha Watanzania kutembea kifua mbele.

Makonda ametumia nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo Rais Magufuli ameendelea kuboresha miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam kwani kuna barabara nyingi ujenzi unaendelea.Amesema kuna miradi mingi ya maendeleo ambayo inaendelea kujengwa ambapo amesema kuna kilometa chache ambazo zimesalia.

Makonda amesema kutokana na kazi kubwa ambayo inaendelea kufanyika wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam ombi lao ni moja tu ambalo ni Rais kufanya ziara katika mkoa huo.

"Nafikisha ujumbe wa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam ni kwamba wanatamani kukuona ukipita kwenye mitaa yao na hivyo kiu na hamu yao ni kukuomba ufanye ziara ili uwatembelee nao wakuone",amesema Makonda.

Kwa upande wake Mkurugenzi  Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Japan(JICA)nchini Tanzania Toshio Nagase amesema kukamilika kwa Flyover ya Mfugale kutasaidia kuboresha maisha ya watu wa Dar es Salaam na nchi jirani.

Pia amesema awali ukitaka kwenda Uwanja wa Ndege walikuwa wanaondoka mapema katikati ya Jiji kwa sababu ya makutano ya Tazara lakini sasa wanaweza kuchelewa kuondoka kwa sababu ya daraja la juu la Mfugale

MADAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA MOYO KWA WATOTO TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA MENDING KIDS LA NCHINI MAREKANI WAFANYA UPASUAJI WA KUFUNGUA KIFUA NA BILA KUFUNGUA KIFUA KWA WATOTO 23

0
0
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao wa Shirika la Kimataifa la Mending Kids la nchini Marekani kufanya upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua kwa watoto 23.
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao wa Shirika la Kimataifa la Mending Kids la nchini Marekani kufanya upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua kwa watoto 23.
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao wa Shirika la Kimataifa la Mending Kids la nchini Marekani kufanya upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua kwa watoto 23.
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao wa Shirika la Kimataifa la Mending Kids la nchini Marekani kufanya upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua kwa watoto 23

WAZIRI LUGOLA AWAPA WIKI MBILI POLISI KIGOMA KUSAMBARATISHA UJAMBAZI WILAYANI KIBONDO

0
0
Na Felix Mwagara, MOHA-Kibondo

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametoa wiki mbili kwa Jeshi Polisi Mkoa wa Kigoma, kuhakikisha linakomesha matukio ya ujambazi yaliyokithiri katika Wilaya ya Kibondo pamoja na sehemu zingine mkoani humo.

Lugola aliongeza kua, katika kupambana na majambazi hao ambao wanasumbua wananchi wilaya hiyo ya Kibondo na kukosa amani katika maeneo yao, polisi ifanye operesheni maalumu kuwatia mbaroni watuhumiwa hao. Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Community Centre mjini Kibondo, leo, Lugola alisema katika operesheni hiyo pia itambatana na utoaji onyo kwa watu wasio waaminifu wanaowahifadhi raia wa kigeni ambao wengi wao ni wahalifu. 

‘’Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, natoa wiki mbili tu, kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya fanyeni operesheni ya kuwasaka majambazi hawa usiku na mchana mpaka jambazi wa mwisho awe amekamatwa,’’ alisema Lugola.

Lugola alisema haiwezekani tukasalimu amri kwa majambazi, haiwezekani kunyoosha mikono kwa jambazi waliopo katika maeneo mbalimbali wa wilaya hiyo pamoja na mkoa kwa ujumla.Waziri Lugola pia aliwataka wananchi wilayani humo kutoa taarifa polisi za wahalifu hao ili kuwezesha operesheni hiyo ifanikiwe zaidi na wananchi waweze kuishi kwa amani na kufanya shughuli zao za kuijenga nchi. 

Waziri huyo pia licha ya kusema anajua changamoto mbalimbali zinazowakibili polisi ikwemo ukosefu wa magari lakini aliwataka aliwataka wawahi katika matukio ya uhalifu yanapotokea, wanaweza kutumia pikipiki ili kuwahi kwa wakati katika matukio hayo. 

Waziri Lugola yupo katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kigoma ambapo anatembelea Wilaya zote mkoani humo kwa kufanya kikao na watumishi walio chini ya wizara yake pamoja na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwa ajili ya kusikiliza kero zao pamoja na kuzitatua.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kibondo, Mkoani Kigoma (hawapo pichani) wakati alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo jana kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi pamoja na Taasisi zilizopo ndani Wizara yake. Lugola ametoa wiki mbili kwa Jeshi Polisi mkoani humo, kuhakikisha linakomesha matukio ya ujambazi yaliyokithiri katika Wilaya hiyo pamoja na sehemu zingine mkoani humo. Kulia ni Mwanasheria wa Sekretaireti ya Mkoa wa Kigoma, Said Kamugisha ambaye pia ni Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa huo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Louis Bura. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Louis Bura, wakiingia katika ukumbi wa mikutano wa Community Centre mjini Kibondo, kwa ajili ya kuzungumza na watumishi waliopo chini ya Wizara yake. Lugola katika mkutano huo alitoa wiki mbili kwa Jeshi Polisi mkoani humo, kuhakikisha linakomesha matukio ya ujambazi yaliyokithiri katika Wilaya hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Meja Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akizungumza katika Kikao cha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto) kuhusu masuala mbalimbali ya mkoa wake, baada ya Waziri Lugola kufanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Kibondo mkoani humo, jana. Lugola katika mkutano wa hadhara na wanannchi mjini humo, alitoa wiki mbili kwa Jeshi Polisi mkoani humo, kuhakikisha linakomesha matukio ya ujambazi yaliyokithiri mkoani humo. Kulia ni Mwanasheria wa Sekretaireti ya Mkoa huo, Said Kamugisha. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Louis Bura. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kibondo, katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa wilaya hiyo. Waziri Lugola akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kibondo, alitoa wiki mbili kwa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma, kuhakikisha linakomesha matukio ya ujambazi mkoani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

CCM YAPONGEZA MAENDELEO YA UJENZI WA RELI YA KISASA (STANDARD GAUGE)

0
0


Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepongeza maendeleo ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Standard Gauge inayoendelea kujengwa kwa awamu ya kwanza kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro.

Mwaka 2015, CCM iliweka ahadi kwa Wananchi wake kuimarisha, kuboresha na kuiunda upya Miundombinu ya Usafirishaji nchini ikijumuisha Usafiri wa Ardhini na Ndege.

Akizungumza wakati wakutembelea maendeleo ya ujenzi wa Reli hiyo eneo la Soga mkoani Pwani, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amesema kukamilika kwa kipande hicho (Dar hadi Morogoro) itasukuma malengo ya dira ya maendeleo ya Taifa mwaka 2020/2025 kufikia Uchumi wa Kati.

Polepole amesema Reli ni kiungo muhimu kuchochea Taifa la Tanzania kufika katika Uchumi wa Kati wenye sifa ya wingi wa Viwanda vitakavyoongeza ajira kwa vijana.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Ramadhan Maneno amesema Chama hicho kimefika katika eneo hilo la Pwani kuthibitisha ujenzi wa Reli hiyo iliyoahidiwa mwaka 2015, amesema Mkoa wa Pwani umetoa ushirikiano kwa Kampuni ya Yapi Merkezi kutoka Uturuki ambayo imechukua tenda ya ujenzi wa Reli hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema wamepata faraja kwa ujumbe wa CCM kufika katika eneo la Pwani kutembelea ujenzi wa Reli hiyo ya Kisasa. "Tuna Wataalamu 57 Wanajeshi maeneo mbalimbali ya Ujenzi wa Reli hii, tunafarijika sana", amsema Kadogosa.

Pia Kadogosa ametoa wito, Wataalamu wanaoendelea na ujenzi wa Reli hiyo kutoka hapa nchini watapata mafunzo ya vitendo kusomea nje ya nchi, amesema mapaka sasa Reli hiyo imetandikwa zaidi ya Urefu wa Kilometa 5 akisisitiza kuwa Reli zilizofika ni Kilometa 60.

Akizungumza kwa niaba ya Bodi ya Shirika la Reli nchini, Prof. John Kondoro amesema kuna watu wanafaidika na uwepo wa Kampuni zinazotengeneza Reli ya Kisasa, pamoja na maendeleo ya ujenzi wake.


Prof Kondoro amesema hadi kufika mwisho wa mwaka lengo ni kuondoa miinuko na mabonde ili kufanikisha utandikaji wa Reli hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania - TRC Ndugu Masanja Kadogosa (kushoto) akimuelezea Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole (kulia) maendeleo ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa wakati wa ziara kuona maendeleo ya ujenzi wa SGR nje kidogo ya kambi ya Soga Kibaha mkoani Pwani Septemba 26, 2018.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Mhandisi Maizo Mgedzi akiwaelezea, Katibu wa Itikadi na Uendezi wa CCM Humphrey Polepole, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC Prof. John Kondoro, Mkurugenzi Mkuu wa TRC ndugu Masanja Kadogosa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Bi. Kate Kamba kuhusu maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la treni ya Umeme linalojengwa kuanzia Stesheni ya ¬Dar es Salaam hadi Ilala Septemba 26, 2018.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole (kulia) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa ziara kuona maendeleo ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR nje kidogo ya kambi ya Soga Kibaha Septemba 26, 2018.
Mhandisi kutoka kampuni ya Yapi Merkezi akiwaelezea Katibu wa Itikadi na Uendezi wa CCM Humphrey Polepole, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC Prof. John Kondoro, Mkurugenzi Mkuu wa TRC ndugu Masanja Kadogosa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Bi. Kate Kamba kuhusu hatua za ujenzi wa daraja la treni ya umeme linalojengwa kuanzia Dar es Salaam Stesheni hadi Ilala Septemba 26, 2018.

NAIBU WAZIRI WA ARDHI ABAINI UJANJA UNAOFANYWA NA WAMILIKI WA MASHAMBA KILOSA MOROGORO

0
0


Na Munir Shemweta, Morogoro

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amebaini ujanja wa baadhi wa wawekezaji katika mashamba makubwa wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro kumilikishwa mashamba huku wengi wao wakiwa hawajaendeleza jambo alilolieleza kuwa ni kinyume na taratibu za uwekezaji.

Aidha, Mabula alijionea jinsi baadhi ya mashamba yakionekana kwa nje kama yameendelezwa lakini kwa ndani hakuna kitu kilichofanyika na badala yake umiliki unaendeshwa kinyume kabisa na taratibu za umiliki mashamba hayo.

Akiwa katika ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro jana, Mabula alisema lengo la kutembelea mashamba ya uwekezaji katika wilaya hiyo ni kubaini wawekezaji wasiofuata taratibu za uwekezaji mashamba na kutoa rai kuwa wale wote wasiozingatia sheria za uwekezaji basi mashamba yao yatafutwa.

Alisema yeye na timu yake wamebaini ujanja unaofanywa na baadhi ya wawekezaji wa mashamba kwa kuhodhi maeneo makubwa huku wakiwa hawayaendelezi na kubainisha kuwa kazi ya kutoa mapendekezo ya kunyang’anywa mashamba kwa wale wasiyoyaendeleza ishaanza kufanywa na halmashauri husika huku baadhi ya mashamba yakiwa tayari yamefutwa na kusisistiza kinachoangaliwa ni kama wamiliki wamefuata sheria.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akiangalia uwekezaji uliopo katika shamba la Farm Africa Agro Focus (T) Ltd kwa kutumia ndege ya anga (Drones) wakati akikagua mashamba yaliyopo katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro. Anayechukua picha ni Afisa Habari wa Wizara ya Ardhi Hassan Mabuye.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akikagua eneo la shamba la Magore wakati akikagua mashamba yaliyopo katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro.


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akioneshwa eneo la shamba la Farm Africa Agro Focus (T) Ltd na Meneja wa Shamba hilo Venkat Chelikani wakati akikagua uwekezaji wa mashamba katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MH. ABDALLAH ULEGA APOKEA BOTI MBILI ZA DORIA WILAYANI KILWA

0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah HamisUlega amekabidhi boti mbili za doria kwa BMU za Kilwa Kivinje na Mafia. Zoezi hili limefanyika katika Wilaya ya Kilwa eneo is Kivinje. Boti hizo zina thamani ya fedha za Kitanzania milioni 144 ambazo zimefadhiliwa na Umoja wa Ulaya kupitia miradi ya WWF. 

Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya Bibi Jenny amesema wanafadhili miradi ya WWF hapa Tanzania yenye jumla ya bilioni 7 za Kitanzania. Aidha, amefurahi kusikia kwa uvuvi wa mabomu umepungua sana na hii ni sababu ya juhudi za serikali na wananchi wa maeneo haya. Pia alisema wao wamenunua boti ila jukumu za kuzilinda ni la Serikali ya Wilaya husika. Naye Mkurugenzi wa WWF nchini amesema wamepata taarifa kutoka kwa wavuvi kwamba sasa samaki wanaongezeka na kupatikana kwa samaki ambao walishapotea na haya yote ni kwa sababu ya kupungua kwa asilimia kubwa uvuvi wa mabomu. 

Mhe Ulega Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi amesema Umoja wa Ulaya umenunua hizi boti kuunga mkono kati kubwa inayofanywa na Mhe Rais John Pombe Magufuli ya Serikali yake ya awamu ya tano. Alisema amezunguka wilaya za Mkinga, Tanga Mjini, Muheza, Pangani na Lindi kote huko wavuvi wanakiri samaki wameongezeka kwa sasa. 

Ukanda huu wa Pwani hauna viwanda vya samaki na kumuomba Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya kutafuta wawekezaji kuja kuwekeza viwanda vya samaki katika mwambao wa bahari ya Hindi, pia alimuomba kufadhili ujenzi wa soko la samaki Kilwa Kivinje. Mhe. Ulega aliwaasa umoja wa vikundi vya BMU kutunza boti hizo na kuwaagiza Wilaya kusimamia ulinzi wa boti hizo. Mwisho aliwaomba WWF kuwaangalia BMU na wavuvi wa maeneo mengine kama Mkinga, Pangani, Lindi Vijijini na Mkuranga kwani nao wana mahitaji ya boti kama hizi katika ulinzi wa rasilimali zetu za bahari.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu, Mh. Abdallah Hamis Ulega, akizungumza akipokea mkataba kutoka Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Jenny Correia Nunes, baada ya kusaini makubaliano ya kupokea msaada wa boti mbili za doria zenye thamani ya Shilingi Millioni 144 zilizotolewa na EU kupitia miradi ya WWF nchini kwa Wilaya mbili ya Kilwa Kivinje na Mafia katika Viwanja wa Maalim Kilwa Kivinje mkoani Lindi Tarehe 26.7.2018 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu, Mh. Abdallah Hamis Ulega, akizungumza na Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Jenny Correia Nunes, na Mkurugenzi Mkazi wa WWF Tanzania, Dkt. Amani Ngusani baada ya kuwasili katika Uwanja wa Maalim Kilwa Kivinje mkoani Lindi Tarehe 26.7.2018 kupokea msaada wa boti mbili za doria zenye thamani ya Shilingi Millioni 144 zilizotolewa na EU kupitia miradi ya WWF nchini kwa Wilaya mbili ya Kilwa Kivinje na Mafia 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu, Mh. Abdallah Hamis Ulega, akiwa ameongozana na Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Jenny Correia Nunes, na Mkurugenzi Mkazi wa WWF Tanzania, Dkt. Amani Ngusani kuelekea baharini kupokea msaada wa boti mbili za doria zenye thamani ya Shilingi Millioni 144 zilizotolewa na EU kupitia miradi ya WWF nchini. 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu, Mh. Abdallah Hamis Ulega, Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Jenny Correia Nunes, na Mkurugenzi Mkazi wa WWF Tanzania, Dkt. Amani Ngusani wakisaini makubaliano baada ya kupokea msaada wa boti mbili za doria zenye thamani ya Shilingi Millioni 144 zilizotolewa na EU kupitia miradi ya WWF nchini kwa Wilaya mbili ya Kilwa Kivinje na Mafia katika Viwanja wa Maalim Kilwa Kivinje mkoani Lindi Tarehe 26.7.2018 

Naibu Waziri Nyongo Afungua Maonesho ya Dhahabu,Atoa Maagizo kwa Wachimbaji Wadogo na GGM


RC GEITA AMPA AHADI MSEMAJI MKUU WA SERIKALI, VIONGOZI WA TAGCO

0
0
Na Mwandishi wetu-MAELEZO GEITA

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Robert Gabriel ameahidi kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya habari katika Mkoa wake ili kuhakikisha taarifa za mkoa huo zinawafikia watanzania.

Akiongea wakati wa kikao kilichowakutanisha Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashari katika Mkoa wa Geita Mhandisi Gabriel amesema kuwa Mkoa unatekeleza miradi mingi ya maendeleo hivyo ili kuweza kuwafikia wananchi ataviwezesha vitengo vya mawasiliano ili viweze kutekeleza jukumu hilo

“Nawaahidi Viongozi wa TAGCO na Msemaji Mkuu wa Serikali nitawanunulia vifaa vyote muhimu Maafisa Habari katika Mkoa wa Geita, wanipe mahitaji yao najua nitakapopata fedha tutavinunua hivyo vifaa vyote ili kuweka mazingira mazuri ya kuwahabarisha watanzania, Serikali inatekeleza hivyo lazima watanzania wajue”-Alisema Mhandisi Robert

Akiongea wakati wa Semina elekezi kwa Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashari katika Mkoa wa Geita Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amewaeleza viongozi hao umuhimu wa kufikisha taarifa kwa wananchi juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuwataka kuwashirikisha Maafisa Habari kwenye vikao vya kawaida vya maamuzi ili wawe Maafisa Habari wenye Habari

Aidha Dkt. Abbasi alisisitiza Kuwa ni muhimu kwa viongozi wa Serikali kuwekeza katika Mitandao ya kijamii kwani huko ndio dunia ilipo kwa sasa. Naye Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano (TAGCO) Bw. Pascal Shelutete watahakikisha Maafisa Mawasiliano Serikalini Wanatumia Taaluma yao kuwafikia wananchi na kuwaeleza yale yanayotekelezwa na Serikali.

“Makandarasi wako kazini wanatengeneza madaraja, wengine wanatengeneza reli ya kisasa hivyo kama ilivyo wao na sisi tutaingia kazini na kuhakikisha tunatumia taaluma yetu vizuri lengo ni kuieleza jamii mambo makubwa mazuri yanayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano .Katibu Tawala Mkoa wa Geita aliwataka Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashari kufanya vikao vya kila mara ili kupeana mrejesho wa kile kinachofanyika katika mkoa ikiwemo utekelezaji wa Miradi.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Pascal Shelutete akiongea na Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashari na kuwahakikishia viongozi hao kuwa Maafisa Mawasiliano Serikalini watatumia Taaluma yao kuwafikia wananchi na kuwaeleza yale yanayotekelezwa na Serikali. 


Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashari katika Mkoa wa Geita na kuwasisiitiza umuhimu wa kuitumia kada ya habari katika kufikisha taarifa kwa wananchi juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashari katika Mkoa wa Geita na kuwasisiitiza umuhimu wa kuitumia kada ya habari katika kufikisha taarifa kwa wananchi juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.  
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Gabriel Robert akiongea katika kikao Kilichowahusisha Wakuu wa Wilaya, wakurugenzi wa Halmashari, Viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Maafisa Habari katika Mkoa wa Geita na Kumhakikishia Msemaji Mkuu wa Serikali na Viongozi wa TAGCO kuwa Mkoa utafanya mageuzi katika sekta ya habari ikiwamo kuwanunulia vifaa muhimu maafisa Habari katika mkoa wa Geita..

RAIS MAGUFULI AAGIZA FLYOVER YA MFUGALE KUFUNGWA KAMERA HARAKA ILI KUDHIBITI AJALI

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli ameagiza flyover ya Mfugale iliyopo makutano ya Tazara ifungwe kamera haraka ili watakaosababisha ajali wawe wanajulikana huku akisisitiza umuhimu wa daraja hilo kutunzwa na isiwe chanzo cha ajali.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazindua rasmi flyover ya Mfugale ambapo pamoja na mambo mengine amesema ni lazima kamera zifungwe tena haraka.

Rais Magufuli amefafanua "Nataka hapa katika flyover ya Mfugale pafungwe kamera.Tangazenu zabuni haraka kama mtaamua kumpa aliyejenga daraja sawa kama kumpa zawadi." Daraja hili ni la Mfugale na bahati nzuri Mhandisi Mfugale yupo ,hivyo naamini mtalifanyia kazi haraka,"amesema Rais Magufuli.

Amefafanua kwamba kukiwa na kamera itakuwa rahisi hata ambaye amelewa na akasababisha ajali na kukimbia iwe rahisi kumfahamu na ajulikane.Pia amesema madaraja mengine makubwa na flyover ambazo zitajengwa lazima kufungwe kamera na hiyo itasaidia kulinda miundombinu mbalimbali ya madaraja na flyover.

Rais Magufuli amesisitiza umuhimu wa watanzania kulinda miuondombinu hiyo na kubwa zaidi kuhakikisha haiwi sehemu ya kusababisha ajali na kupoteza maisha ya Watanzania.Wakati huo huo Rais Magufuli amewahakikishia wananchi wa Dar es Salaam kwamba kuna mikakati mingi inaendelea ya kuhakikisha adha ya msongamano wa magar inapungua.

Amezungumzia ujenzi wa flyover mataa ya Chang'ombe pamoja na eneo la Magereza ambapo amesema mazungumzo yalikwishaanza.Pia amesema kuna ujenzi unaendelea eneo la mataa ya Ubungo jumla ya sh.Bilioni 247 zitatumika kwa ajili ya eneo hilo ambapo  katika eneo hilo kutakuwa na daraja la ghorofa tatu,hivyo magari yatakuwa yanapishana juu kwa juu.

Pia amesema tayari ujenzi wa barabara ya mwendo kasi kutoka Mbagala hadi Grezani mchakato wake unakwenda vizuri na itaanza kujengwa.Amesema anataka kuipendeza Jiji la Dar es Salaam na kwamba mipango na mikakati inakwenda vizuri huku akiwahakikishia wananchi wa Jiji hilo kwamba atafanya ziara.

MAHAFALI YA 18 YA TIOB YAFANYIKA DAR

0
0
TAASISI ya Taaluma za kibenki Tanzania(TIOB) imefanya mahafali ya 18 ambapo wahitimu 157 wametunukiwa vyeti

Sherehe za mahafali hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam ambapo pia wahitimu 22 wametunukiwa ngazi ya cheti, 133 wametunukiwa ngazi ya taaluma ya juu na 2 wametunukiwa vyeti vya kubobea katika masomo maalumu ya kibenki.


Pia katika sherehe za mahafali hayo wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani yao walitunukiwa zawadi. 

Akizungumza wakati wa mahafali hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker amesema Sherehe ya mahafali zilitanguliwa na mkutano mkuu wa 20 wa mwaka kwaajili ya kutekeleza mpango wa 2018 wa TIOB pamoja na uteuzi wa Mkaguzi wa hesabu kwa mwaka 2018.

Aidha Amesema kuwa taasisi ya TIOB imetoa wahitimu ambao wamebobea kwenye masuala ya benki. 

Pia amewashauri wahitimu wote kufanya kazi kwa weledi kutokana na mafunzo waliyoyapata pia amewapongeza wahitimu wote kwa ushirikiano wao kwani wengine ni wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za benki. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Benki TIOB Patrick Msusa amewapongeza Wahitimu wote.

Amewaomba watekeleze vyema majukumu yao katika kazi kwa misingi ya kibenki.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, ambaye alikuwa mgeni rasmi akitoa hotuba yake.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIOB, Patrick Msusa, akitoa hotuba yake katika mahafali iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker
Wahitimu wakiwa wamenyanya kofia tayari kwa kuvaa baada ya mgeni rasmi kutamka maneno ya kuwatunukia uhitimu wa masomo yao.
Wahitimu wakisikiliza neno kutoka kwa 


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker jijini Dar es Salaam wakati wa mahafari 18 ya mafunzo ya kibenki.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

CRDB Bank yazindua kampeni ya “Shinda na SimAccount”

0
0
Benki ya CRDB leo imezindua kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma zake ya kibenki kupitia simu ya mkononi ijulikanayo kama SimAccount ambayo inawapa wateja wa benki pamoja na Watanzania kwa ujumla nafasi kujishindia fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 200.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama “Shinda na SimAccount”, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei alisema Benki ya CRDB imeamua kuanzisha kampeni hiyo ili kuwahamasisha watanzania kujiunga na kutumia mfumo wa SimAccount ambao ni rahisi, nafuu na haraka.
Katika kampeni hii ya “Shinda na SimAccount”, wateja waliojiunga na kutumia huduma mbalimbali zinazopatikana ndani ya mfumo wa SimAccount watajishindia zawadi za fedha ambapo kila siku washindi 24 watakuwa wanapatikana, pamoja na washindi 12 wa wiki, washindi wa 3 wa mwezi na mshindi wa kampeni nzima "Jackpot Winner" atakaye patikana mwishoni mwa kampeni na kujishindia zawadi ya shilingi milioni ishirini.

"Unachotakiwa kufanya katika kampeni hii ni kujiunga na SimAccount kwa kupiga *150*62#, pamoja na kuitumia kufanya miamala mbalimbali ikiwemo kuweka na kutoa pesa kwenye matawi ya Benki ya CRDB, Mawakala wetu wa SimAccount na FahariHuduma Wakala” alifafanua Mkurugenzi huyo Mtendaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei (kushoto) akibonyeza kitufe kwenye luninga kuashiria uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma ya kibenki kupitia simu ya mkononi ijulikanayo kama SimAccount iliyo chini ya Kampuni tanzu ya Benki (CRDB Micro Finance) katika promosheni ya “Shinda na SimAccount”, iliyofanyika jijini Dar es salaam leo. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa, Mkurugenzi wa CRDB MicroFinance, Sebastian Masaki pamoja na Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha nchini, Humud Mohamed. 

SimAccount ni mfumo maalum wa utoaji huduma unaowezesha watanzania kujisajili na kufungua akaunti kupitia simu za mkononi. Mfumo huu ulizinduliwa rasmi tarehe 26 Agosti Mwaka jana na Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano mama Samia Suluhu Hassan, ukiwa na lengo la kusaidia upatikanaji wa huduma za kifedha kwa urahisi na usalama kwa watanzania wengi hata wale wasio na akaunti za benki kupitia simu zao za mikononi “Simu Yako, Akaunti Yako”.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei (katikati) akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma ya kibenki kupitia simu ya mkononi ijulikanayo kama SimAccount katika promosheni ya “Shinda na SimAccount”, iliyofanyika jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa CRDB Micro Finance, Sebastian Masaki pamoja na Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha nchini, Humud Mohamed. 

Akielezea baadhi ya faida za kujiunga na mfumo wa SimAccount kwa wateja, Dkt Charles Kimei alisema mfumo huu unawapa fursa wateja;
  •  kufungua na kusimamia akaunti za vikundi mbalimbali ikiwemo vya kusaidiana, VICOBA, Harambee, harusi n.k.
  • uwezo kufungua akaunti mbalimbali kwa ajili ya kuweka akiba ili kutimiza malengo mbalimbali mteja aliyojiwekea.
  •  mfumo huu mteja ataweza kulipia manunuzi ya bidhaa kwenye maduka ya kawaida yanayopokea malipo kwa SimAccount kwa Mangi, Saluni, Mama Ntilie n.k
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei (kulia) akishuhudia zoezi la upigaji simu kwa washindo wa  promosheni ya “Shinda na SimAccount”.

Dkt. Kimei alisema uzinduzi wa kampeni hiyo ya “Shinda na SimAccount” unaleta chachu kwa watumiaji wa SimAccount kuendelea kufurahia huduma hizo huku wakijiweka katika nafasi nzuri ya kijishindia zawadi kubwa ya magari.

Akimalizia hotuba yake Dkt. Kimei alitoa rai kwa wateja na watanzania wote kwa ujumla kujiunga na SimAccount kwani ni mfumo madhubuti wa kibenki utakaowawezesha kufanya miamala yao kwa urahisi zaidi, pamoja na kijishindia zawadi mbalimbali katika kipindi cha miezi minne ya kampeni.

MAWAKALA WA FORODHA WAELIMISHWA MABADILIKO YA SHERIA ZA KODI

0
0
Na Avila Kakingo, Globu ya jamii.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewaelimisha Mawakala wa Forodha  mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2018.

Akizungumza wakati wa semina ya mawakala hao, Katibu Mkuu wa Chama cha Mawakala Tanzania (TAFFA), Tony Swai  amesema kuwa ujio wa sheria hii utapunguza na kuongeza Ushuru wa Forodha kwa baadhi ya bidhaa zinazoingizwa hapa nchini. 

"Maboresho ya sheria hiyo itasaidia nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kukusanya kodi kwa urahisi na hatimaye kuongeza ukusanyaji mapato kwa kila nchi husika," alisema Swai.

Aidha, Swai amewaomba mawakala hao kutoa taarifa sahihi kuhusu bidhaa zinazoingia nchini na kulipa ushuru wa forodha na kodi stahiki kwa maendeleo ya Taifa. 

Kwa upande wake Kaimu Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Juma Hassan amesema kuwa, uboreshaji wa Sheria ya Forodha ya Afrika Mashariki utasaidia uingizwaji wa malighafi ambazo zitasaidia utengenezaji wa bidhaa za ndani kwa gharama nafuu ili kukuza Uchumi wa Viwanda hapa  nchini na kupelekea bidhaa za ndani kuwa na gharama nafuu. 

Amesema wakala wa forodha watasaidia zaidi utekelezaji wa Sheria ya Forodha ya Afrika Mashariki kwa kushiriki na kusimamia bidhaa zinazoingizwa hapa nchini.

Kwa wakati tofauti, baadhi ya washiriki wa semina hiyo wamesema kuwa, mawazo waliyoyatoa yakifanyiwa kazi na TRA yatasaidia kuleta ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya serikali. 
 Kaimu Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Juma Hassan akizungumza na wananchama wa chama cha mawakala wa Forodha jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuwajengea uwezo wanachama hao kuhusu sheria ya forodha na mapato ya Afrika Mashariki.
 Meneja msaidizikituo cha huduma cha Forodha Oswald Masawe akizungumza na waandishi wa haabari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuwajengea uelewa wanachama cha mawakala wa forodha kuijua sheria ya mapato ya Afrika Mashariki.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mawakala Tanzania (TAFFA), Tony Swai  akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wanachama wa chama cha Forodha jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi  ya wanachama wa Chama cha Mawakala Tanzania wakisikiliza maada.
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live




Latest Images