Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

'NCHI ZA AFRIKA KUENDELEA KUKABILIWA NA UHABA WA MBEGU BORA ZENYE KUTOA MAZAO MENGI'

$
0
0
Seif Mangwangi,Arusha
NCHI za Afrika zitaendelea kukabiliwa na uhaba wa mbegu bora za msingi zenye kutoa mazao mengi na bora kutokana na uzalishaji wa mbegu hizo kuwa mdogo kulinganisha na mahitaji halisi.

Hali hiyo itaendelea kusababisha uzalishaji wa vyakula kuwa wa chini na hivyo kushindwa kukabili tatizo la njaa linalozikumba nchi nyingi barani Afrika mara kwa mara.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Meneja Masoko wa Kampuni ya kuzalisha mbegu za msingi ya Quality Basic seed yenye makao yake mkuu nchini Kenya, Wycliffe Ingoi amesema mahitaji ya mbegu bora za msingi ni kilo 156250 kwa mwaka.

Amesema kiwango hicho ni kikubwa kutokana na ugumu wa kuzalisha mbegu hizo sanjari na uwepo wa kampuni chache zinazoweza kuzalisha mbegu hizo.

" Wakulima wamekuwa wakipata mazao machache kutokana na uhaba wa mbegu za msingi na hivyo kulazimika kutumia mbegu zisizo na ubora na ambazo hazijazalishwa kitaalam, sisi kama QBS tumekuja kujaribu kumaliza hili tatizo japo kwa kiasi fulani,"amesema.

Aliziomba Serikali za Afrika kushirikiana na kampuni zinazozalisha mbegu za msingi  ili kufanikisha zoezi la kupatikana kwa mbegu bora na zenye kutoa mazao mengi.

kwa upande wake Ofisa Habari wa taasisi ya kilimo ya African Agriculture Technology Foundation (AATF),inayosaidia kusambaz teknolojia ya kilimo Afrika, Everlyne Situma alisema kampuni za mbegu zimekuwa zikishindwa kuzalisha mbegu za kutosha kutokana na ugumu wa kutayarisha mbegu za msingi.

Amesema kampuni ya Quality Basic Seed imekuwa mfano wa kuanzisha utaalam huo na hivyo kuwa msaada kwa kampuni za uzalishaji wa mbegu Afrika.
Meneja masoko wa kampuni ya kuzalisha mbegu za awali ya Quality Basic Seed, Cliffe ingoi akiwaeleza waandishi wa habari namna kampuni yake inavyofanya uzalishaji wa mbegu hizo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano

DC KAWAWA APIGA MARUFUKU WANAOSHIRI KUKARIBISHA MIFUGO KIHOLELA

$
0
0


NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO 
MKUU wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa ametoa onyo kwa baadhi ya viongozi wa vijiji na watendaji wanaoshiriki kukaribisha wafugaji bila utaratibu na waache mara moja ,kwani ndio kichocheo cha uvunjifu wa amani na migogoro baina yao na wakulima.

Aidha, amepiga marufuku wafugaji kuingiza mifugo yao kiholela wilayani humo pamoja na maeneo ya wawekezaji ili kuondoa migogoro inayojitokeza mara kwa mara.

Rai hiyo aliitoa ,wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na madiwani na watendaji wa halmashauri ya Chalinze na Bagamoyo. 

Zainab alieleza ,wapo viongozi wanaokula na wafugaji suala linalosababisha ongezeko la mifugo kwenye maeneo yasiyo rasmi. 

Alisema kuwa, kumekuwa na migogoro kati ya wakulima na wafugaji kutokana na baadhi ya wafugaji kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima ama wawekezaji hali inayosababisha mapigano.

“Nasema inatosha, wilaya kwasasa ina mifugo hiyo 300,000 yaani halmashauri ya Chalinze ina ng'ombe 240,000 na Bagamoyo ng'ombe 60, 000,"

Zainab alielezea, baaadhi ya viongozi wamekuwa wakijihusisha na uingizaji mifugo kwa kutumia njia ambazo ni kinyume cha sheria hali ambayo inasababisha madhara makubwa ndani ya jamii .
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa akizungumza na watendaji na madiwani. 
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Baadhi ya watendaji na madiwani wa Bagamoyo wakifuatilia yaliyojiri kwenye kikao cha baraza.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Azzan Mussa Zungu akiongoza kikao cha saba cha mkutano wa kumi na mbili cha Bunge hilo leo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt Ashatu Kijaji akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa  kikao cha saba cha mkutano wa kumi na mbili cha Bunge hilo leo Jijini Dodoma.

Naibu Waziri  wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso akijibu hoja mbalimbali za wabunge leo wakati wa  kikao cha saba cha mkutano wa kumi na mbili cha Bunge hilo leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba akizungumza jambo na Mbunge wa Babati Mjini Mhe.Pauline Gekul  wakati wa  kikao cha saba cha mkutano wa kumi na mbili cha Bunge hilo leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola akimskiliza Mbunge wa Bunda Mjini Mhe.Ester Bulaya leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof Joyce Ndalichako akijibu maswali mbalimbali ya wabunge leo Bungeni Jijini Dodoma.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jitegemee wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu leo  Bungeni Jijini Dodoma.
Picha zote na Idara ya Habari-MAELEZO.

HISTORIA YA UTALII ILIYOSAHAULIKA KATI YA TANZANIA NA MSUMBIJI

$
0
0
Unapozungumzia nchi ya Msumbiji kuhusu kupata uhuru lazima utaigusa nchi ya Tanzania, Tanzania ni miongoni mwa nchi iliyotoa mchango mkubwa katika kuhakikisha nchi ya Msumbiji inapata Uhuru. Makazi ya wapigania uhuru wa Msumbili yalikuwa kijiji cha Masonya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, leo hii kambi ya Masonya imekuwa ni Shule ya Sekondari ya wasichana, je unafahamu kama sehemu hiyo inahistoria ndefu iliyosahaulika basi fatilia katika Video Hii.

SERIKALI KUKUZA UCHUMI KWA KUDHIBITI FEDHA ZA ZIADA KATIKA MZUNGUKO

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).
FEDHA za ziada kuwepo katika mzunguko wa uchumi sio kigezo cha kukua kwa uchumi wa Taifa bali ni ishara ya Taifa hilo kushindwa kudhibiti ukuaji wa uchumi wake.
Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Konde Mhe. Khatib Said Haji, aliyehoji kuhusu dhana ya kukua kwa uchumi nchini ilihali kuna upungufu wa uuzaji bidhaa nje na wananchi kukosa fedha.
Dkt. Kijaji alieleza kuwa matatizo ya kuwepo kwa fedha za ziada katika uchumi ni makubwa, hivyo inapongezwa hatua ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kudhibiti hali hiyo kwa manufaa ya ukuaji wa uchumi wa Taifa.
“Uchumi wa Tanzania unakua kutokana na hali halisi na takwimu zilizopo, ambapo katika Mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC) uliofanyika hivi karibuni ulieleza kuwa nchi nyingi mwanachama wa Jumuiya hiyo hazijafanikiwa katika ukuaji wa viashiria vya uchumi mkubwa isipokuwa nchi ya Botswana, Lesotho na Tanzania”. Alieleza Dkt. Kijaji.
Akijibu swali la Msingi la Mbunge huyo kuhusu vigezo vinavyoainisha ukuaji wa uchumi wa Tanzania, Dkt. Kijaji alisema kuwa vigezo kwa mujibu wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa ni ongezeko la pato la Taifa, ongezeko la pato la wastani la mwananchi kwa mwaka na ongezeko la uuzaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi.
Vigezo vingine ni kupungua kwa uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi, utulivu wa bei za bidhaa na huduma, utulivu wa viwango vya ubadilishaji wa fedha za kigeni,  kuongezeka kwa akiba ya fedha za kigeni na kuongezeka kwa makusanyo ya Serikali kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo na huduma za kijamii.
Vilevile alieleza kuwa, uwekezaji unaofanyika katika nchi ni kigezo cha msingi cha ukuaji wa uchumi kwa kuwa huongeza kasi ya uzalishaji wa bidhaa na huduma, ajira, kipato cha mwananchi mmoja mmoja na pato la Taifa hivyo kupunguza umaskini katika jamii.
Naibu Waziri Dkt. Kijaji alibainisha kuwa, mchango wa Serikali katika ukuaji wa uchumi ni pamoja na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, kuwekeza zaidi kwenye shughuli zinazochochea ukuaji wa uchumi, kupunguza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi na kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya uwekezaji wa bidhaa na huduma nchini.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango.

MASENETA KUTOKA BUNGE LA UFARANSA WAKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WENYEVITI WATATU WA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Mussa Azzan Zungu (katikati) akiongoza kikao kilichokuwakutanisha Wenyeviti wa Kamati tatu za Bunge (kushoto) na Maseneta kutoka Bunge la Ufaransa (kulia) katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Balozi wa Ufaransa nchini.
Mkuu wa Msafara wa Maseneta toka Bunge la Ufaransa Seneta Ronan Dantec (wakwanza kushoto) akizungumza wakati wa kikao kilichokuwakutanisha Wenyeviti wa Kamati tatu za Bunge (kulia) na Maseneta kutoka Bunge la Ufaransa (kushoto) katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Wenyeviti wa Kamati tatu za Bunge na Maseneta toka Bunge la Ufaransa katika picha pamoja mara baada ya kuzungumza katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Toka kulia ni Mweyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Mhe. Emmanuel Mwakasaka, Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Nape Nnauye, Seneta Cyril Pelleah, Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mkuu wa Msafara wa Maseneta toka Bunge la Ufaransa Seneta Ronan Dantec na Seneta Bernard Jomier.

NIDA YAANZA KUTOA VITAMBULISHO VYA UTAIFA KWA WALEMAVU KINONDONI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo amezindua rasmi zoezi la utambuzi na usajili kwa watu wenye ulemavu ili waweze kupata vitambulisho vya utaifa na hii ni kwa kushirikiana na mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) na ofisi ya ustawi wa jamii Wilayani humo.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ameipongeza mamlaka hiyo na ofisi ustawi wa jamii Kinondoni kwa kuwajali watu wenye mahitaji maalumu na kuandaa jukwaa maalumu la kuwatambua na kuwasajili na kutoa vitambulisho vya utaifa.

Amesema kuwa vitambulisho hivyo vitawasaidia katika kupata huduma mbalimbali ya kijamii na amewataka wanajamii kuwahimiza na kuhakikisha kila mtu mwenye ulemavu wa aina yoyote anapata huduma hiyo ya utambuzi na usajili na kupatiwa kitambulisho chake cha utaifa.

Aidha Chongolo amewahaidi walemavu hao kuwapatia fungu la fedha lililopo katika bajeti ya serikali ili waweze kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.

Kwa upande wake Afisa msajili (NIDA) Wilaya ya Kinondoni Dickson Mbanga amesema kuwa mchakato wa utoaji wa vitambulisho kwa walemavu umekuwa na changamoto kubwa hivyo kama mamlaka kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya wameweka mazingira rafiki ya kuwasajili watu wenye ulemavu hivyo wajitokeze kwa wingi ili waweze kujipatia vitambulisho vya uraia.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akizungumza na walemavu katika viwanja vya shule ya msingi Ndugumbi wakati wa uzinduzi wa zoezi la utambuzi na usajili wa watu wenye ulemavu ili waweze kupata vitambulisho vya utaifa.
 Afisa Msajili (NIDA) Wilaya ya Kinondoni Dickson Mbanga akisoma hotuba kwa Mkuu wa Wilaya wakati wa uzinduzi wa mchakato wa utoaji wa vitambulisho vya utaifa kwa walemavu Wilayani humo.
 Baadhi ya walemavu waliojitokeza katika zoezi hilo la kujipatia vitambulisho vya utaifa, leo katika viwanja vya shule ya Ndugumbi.
Mmoja wa walemavu akiwa katika hatua ya mwisho ya upigaji picha ili aweze kupata kitambulisho cha utaifa katika mchakato wa utoaji wa vitambulisho vya utaifa kwa watu wenye ulemavu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS MAGUFULI AMUAGIZA DK. JINGU KUSIMAMIA UTENDAJI KAZI WA NGOs

$
0
0
Na Mwandishi Wetu Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Njingu kusimamia kwa karibu Usajili na Uratibu wa NGOs nchini kwani kumekuwa na vitendo vya ovyo vinavyofanywa na NGOs.

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ikulu ya Chamwino Dodoma wakati akiwaapisha viongozi watatu aliowateua hivi karibuni akiwemo Mkurugenzi wa TAKUKURU Kamishna wa Polisi Diwani Athumani na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Balozi Dkt Azizi Malima .
Dkt Magufuli amesisitiza kuwa NGOs zinatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria ambazo pamoja na mambo mengine zinayataka kuendesha shughuli  zao kwa uwazi hususani katika masuala ya mapato na matumizi ya fedha za ufadhili wa shughuli zake.
 “Nataka ukasimamie Usajili na Uratibu wa NGOs najua zipo chini ya Maendeleo ya Jamii kasimamie kuwe na uwazi wa utendaji kazi wa NGOs” alisisitiza Rais Magufuli.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu amemuhakikishia Rais Magufuli kutekeleza majukuu yake kwa akili, moyo na nguvu zake zote ili kufikia mafanikio anayoyatarajiwa na yanayotarajiwa na watanzania.
“Nikuahidi Mhe. Rais nitafanya kazi kwa nguvu na akili zangu zote kwa kushirikiana na wenzangu katika Wizara ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana”alisema Dkt. Jingu.
 Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akipokea ua kutoka kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mtoto Bi. Magreth Mussai wakati alipowasili katika Oifisi za Wizara mara baada ya kuapishwa kuwa Katibu Mkuu katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ( Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) mara baada ya kuapishwa kuwa Katibu Mkuu katika Ikulu ya Chamwino Dodoma. 
 Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu (kulia) akizungumza na wajumbe wa Menejimenti ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara baada ya kuapishwa kuwa Katibu Mkuu katika Ikulu ya Chamwino Dodoma. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba akitoa shukurani kwa niaba ya Menejimenti ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara baada ya kuapishwa kuwa Katibu Mkuu katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

WAMILIKI WA VIWANDA WANAOKIUKA SHERIA YA MAZINGIRA NCHINI KUCHUKULIWA HATUA KALI - SIMA

$
0
0
Serikali imetoa wito kwa wamiliki wa viwanda kuzingatia utekelezaji wa Sheria ya Mazingira na Mikakati mbalimbali iliyopo kwa ajili ya kuwezesha usimamizi endelevu wa hifadhi ya mazingira kwa faida yetu na ya vizazi vijavyo. 

Hayo yamesemwa leo bungeni Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima wakati wa kipindi cha maswali na majibu na kusisitiza kuwa Tanzania inachangia kiasi kidogo sana katika tatizo la uzalishaji wa gesijoto ambazo ndio chanzo cha mabadiliko ya   tabia nchi. Hata hivyo, pamoja na kuchangia kidogo kiasi hicho, Tanzania imeendelea kuathirika kutokana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi kama vile kupungua kwa barafu ya mlima Kilimanjaro, kuongezeka kwa usawa wa bahari; ukame, mafuriko ya mara kwa mara na mlipuko wa magonjwa.

Imebaini kuwa tatizo la mabadiliko ya tabia nchi kwa kiwango kikubwa linasababishwa na uzalishaji wa gesijoto unaotokana na matumizi ya nishati (47%), uzalishaji viwandani (30%) na usafirishaji (11%) kwa shughuli za maendeleo katika nchi zilizoendelea kiviwanda hususan za Ulaya, Amerika, Asia na Australia. Bara la Afrika kwa ujumla limechangia gesijoto kiasi kisichozidi asilimia    tatu (3). Tanzania huzalisha    kiasi cha tani 0.09 za hewa ukaa (Per Capital emission) kwa mwaka.

Mheshimiwa Sima amesema kuwa, tatizo kubwa linatokana na uchafuzi wa mazingira unaofanywa na baadhi ya viwanda nchini ni kutiririsha maji taka yenye sumu  na kemikali ambazo huathiri sana viumbe hai pamoja na mazingira kwa ujumla.

 “Tanzania inayo Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004, Sheria hii imeweka misingi ya Usimamizi, Tathmini na Kuchukua tahadhari kuhusu madhara kwa mazingira yakiwemo ya viwandani. Kwa kuzingatia Sheria hii, Serikali imekuwa ikielimisha na kuwatoza faini wamiliki wa Viwanda wanaokiuka Sheria hii na wanaoendelea kukaidi maelekezo na masharti waliyopewa hufungiwa kufanya shughuli na kupewa masharti kabla ya kuruhusiwa kuendelea na shughuli zao tena.” Alisisitiza Mhe. Sima. 

Wakati huo huo Mhe. Sima amewataka wamiliki wa viwanda kote nchini kuhakikisha Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Environmental Impact Assessment) na Ukaguzi wa Mazingira (Environmental Audit) vinafanyika na kuzingatiwa. Aidha, wamiliki wa viwanda wanapaswa kutumia nishati rafiki kwa mazingira na kutumia teknolojia banifu katika uzalishaji wa bidhaa zao ili kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akitoa majibu ya Serikali wakati wa kipindi cha maswali na majibu hii leo Bungeni mjini Dodoma.

NAIBU WAZIRI MHANDISI NDITIYE AZINDUA WIKI YA SHIRIKA LA RELI NCHINI

$
0
0
Na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii
Naibu Waziri wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiy amefungua wiki ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) pamoja na kuzindua nembo na kuzindua nembo mpya ya shirika hilo.

Akizungumza na waaandishi  wa habari leo jijini Dar es Salaam Mhandisi Nditiye amesema juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano  kupitia ilani ya CCM katika sekta ya usafirishaji zitapelekea kuondoa kero mbalimbali na kukuza vipato vya wananchi

Mhandisi Nditiye amesema ili huhakikisha kauli mbiu ya uchumi wa viwanda inatekelezwa kwa ufanisi kwa kutumia miundombinu ya reli ya kisasa na uboreshaji wa reli ya kati kuelekea Dar -Isaka.
Mhandisi amesema juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano kwa wananchi wa Tanzania tushirikiane kwa pamoja kuunga mkono juhudi za serikali inayoongozwa na Mh.Rais Dkt.John Joseph Pombe Magufuli.

"Nawahakikishi kuwa serikali ya awamu tano itaendelea kuboreha huduma kwa wananchi na kuimarisha miundombinu ya reli na yenye lengo la kuleta manufaa na maendeleo ya Taifa la leo na kesho,"alisema Mhandisi Nditiye
 Mwenyekiti wa bodi ta Wakurugenzi Shirika la Reli Tanzania (TRC),Profesa John Wajanga akizungumza waandishi wa habari katika ufunguzi wa wiki ya Shulilika la reli Tanzania leo hadi September 15 mwaka huu.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza leo na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa wiki ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na  kuwapongeza kwa nzuri na kusimamia vema shunguli za miradi mbalimbali inayoendelea ikiwemo wa ujenzi wa reli.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa bodi ta Wakurugenzi Shirika la Reli Tanzania (TRC),Profesa John Wajanga (picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
 Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kushoto) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa wiki ya Shirika la reli Tanzania.
Meneja Uhusiano shirika la Reli Tanzania-TRC,Jamila Mbarouk akifafanua jambo katika ufunguzi wa shirika la Reli Tanzania.
 Wanafanyakazi wa shirika la Reli Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja.

WAZAZI, WATOTO OMBAOMBA KUSHTAKIWA

$
0
0


Na Fatma Salum – MAELEZO
SERIKALI imewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuwakamata na kuwashitaki mahakamani watoto pamoja na wazazi wao ambao huzagaa mitaani kuombaomba.

Agizo hilo limetolewa leo bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Joseph Kakunda, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kiembesamaki, Ibrahim Raza, lililohoji ni lini Serikali itachukua hatua ya kuwaondoa ombaomba Jijini Dar es Salaam.

Kakunda alibainisha kuwa ni kweli ombaomba wengi zaidi wapo Jijini Dar es Salaam kutokana na kuwepo kwa vivutio vingi ikiwemo watu wenye imani mbalimbali ambao wengine huwapatia fedha ombaomba hao kama sehemu ya ibada.

“Kuzagaa kwa ombaomba kimekuwa chanzo kimojawapo cha uchafuzi wa mazingira na mara kadhaa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imechukua hatua mbalimbali za kuwaondoa ikiwemo kuwakamata na kuwarudisha kwao lakini wamekuwa wakirudi,” alisema Kakunda.

Alieleza kuwa mwaka 2013 ombaomba wapatao 253 na watoto 135 walikamatwa na kurejeshwa kwao ambapo watoto 33 walirejeshwa shuleni, hivyo inathibitisha kwamba wapo watu wazima wanaowatumia watoto kuombaomba na kuwakosesha fursa ya kupata elimu au kuwa watoro.

“Nawaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri chini ya usimamizi wa Wakuu wa Mikoa kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama, kuwakamata watoto wote ambao badala ya kwenda shuleni huzagaa mitaani kuombaomba,” alisisitiza Kakunda.

Alisema kuwa watoto hao wakamatwe pamoja na wazazi wao na washitakiwe mahakamani chini ya Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 inayokataza utoro na Sheria ya Kanuni ya Adhabu kifungu cha 166, 167 na 169 (a) vinavyohusu Wajibu wa Wazazi na Walezi kwa Watoto.

Pia Kakunda alishauri Mabaraza ya Madiwani kutunga sheria ndogondogo za kuzuia utoro pamoja na kudhibiti mienendo ya baadhi ya watu wanaoombaomba.

Aidha, alitoa rai kwa watanzania kutumia fursa za kupambana na umaskini zilizoandaliwa na Serikali ikiwemo elimu ya msingi bila malipo, huduma za afya vijijini, fursa za mikopo na matumizi bora ya ardhi yenye rutuba ili waweze kujikwamua kiuchumi.

GARI LAACHA NJIA BA KUINGIA MTARONI WAZO JIJINI DAR

$
0
0
 Deleva wa bajaji,pikipiki wakiangalia namna gari hilo lilivyoongia mtaroni jijini Dar es Salaam.
Gari  limeacha njia na kuingia mtaroni katika eneo la  Wazo barabara ya Madale Jijini Dar es Salaam  chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika kwa haraka.(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)

YANGA KUCHEZA MECHI 11 UWANJA WA TAIFA

$
0
0
Raundi ya nne ya Ligi ya Tanzania Bara (TPL) inaendelea tena wikiendi hii kwa timu mbalimbali kukutana kwenye viwanja tofauti nchini.
Ratiba hiyo ya Ligi inaonesha Yanga na Simba wote wakiwa Jijini Dar es Salaam. Yanga akicheza michezo 11 katika dimba la Uwanja wa Taifa, minne akiwa ugenini na saba nyumbani. Kwa upande wa Simba atacheza mechi nane, katika mechi hizo sita akiwa nyumbani na mbili ugenini,


Mechi za Yanga  Uwanja wa Taifa
1.Yanga SC vs Stand Utd (Nyumbani)
2.Yanga SC vs Coastal Union (Nyumbani)
3.Yanga SC vs Singida Utd (Nyumbani)
4.JKT Tanzania vs Yanga SC (ugenini)
5.Simba SC vs Yanga SC (ugenini)
6.Yanga SC vs Mbao FC (Nyumbani)
7.Yanga SC vs Alliance FC (Nyumbani)
8.KMC vs Yanga SC (ugenini)
9.Yanga SC vs Lipuli FC (Nyumbani)
10.Yanga SC vs Ndanda FC (Nyumbani)
11.African Lyon vs Yanga SC (ugenini)


Mechi za Simba Uwanja wa Taifa
1.Simba SC vs Biashara Utd (Nyumbani)
2.Simba SC vs Yanga SC (Nyumbani)
3.Simba SC vs African Lyon (Nyumbani)
4.Simba SC vs Stand Utd (Nyumbani)
5.Simba SC vs Alliance FC (Nyumbani)
6.Ruvu Shooting vs Simba SC (ugenini)
7.JKT Tanzania vs Simba SC (ugenini)
8.Simba SC vs KMC (Nyumbani)


RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU, KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA PAMOJA NA BALOZI MMOJA IKULU YA CHAMWINO JIJINI DODOMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. John Kiang’u Jingu kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Azizi  Mlima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Kiang’u Jingu wa kwanza kulia, akifatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt. Azizi Ponary Mlima pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Diwani Athuman Msuya wakila Kiapo cha Uadilifu mara baada ya kuapishwa katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Kiang’u Jingu wa kwanza kulia, akifatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt. Azizi Ponary Mlima pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Diwani Athuman Msuya waki tia saini kwenye hati ya Uadilifu katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Diwani Athuman Msuya akizungumza mara baada ya kuapishwa katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya tukio la Uapisho lililofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Diwani Athuman Msuya pamoja na Balozi mteule Valentino Mlowola mara baada ya tukio la Uapisho katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU

CHUO KIKUU ARDHI CHAANZA KUTUMIA NDEGE TIARA KATIKA UKUSANYAJI TAARIFA NA USOMAJI RAMANI NCHINI

$
0
0
Mtaalam wa ndege tiara kutoka kampuni ya China TOPRS Tech Limited, Yu Jing Run akiiandaa ndege tiara tayari kwa kuirusha katika viwanja vya Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Septemba 12 2018, wakati wa uzinduzi wa ndege hiyo itakayokusanya taarifa na upimaji ramani. Wanaoshuhudia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa (wa tatu kushoto), Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (Taaluma), Profesa Gabriel Kassenga na wana taaluma mbalimbali. 

Mhandisi upimaji ramani wa kampuni ya China TOPRS Tech Limited, Ren Ya Feng akitoa muhtasari wa jinsi ndege tiara inavyofanya kazi muda mfupi kabla ya kuirusha kwa upigaji picha jijini cha Dar es Salaam Septemba 12 2018. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa, Naibu Mkuu wa chuo Kikuu Ardhi (Taaluma), Profesa Gabriel Kassenga (Kushoto Makamu Mkuu) na wana taaluma mbalimbali. 


BALOZI WA INDIA ATEMBELEA BUNGE NA KUZUNGUMZA NA SPIKA NDUGAI

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza na na Balozi wa India nchini Mhe. Sandeep Arya Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Balozi wa India nchini Mhe. Sandeep Arya akimueleza jambo Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiagana na na Balozi wa India nchini Mhe. Sandeep Arya mara baada ya kuzungumza naye Ofisini kwake Jijini Dodoma. PICHA NA BUNGE

VIONGOZI WA KLABU YA MALINDI WANAOTAMBULIWA NA BODI YA WADHAMINI WASEMA UCHAGUZI WA KLABU HIYO ULIOFANYIKA HIVI KARIBUNI NI BATILI

$
0
0
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Malindi Sports Club anaetambuliwa na Bodi ya Wadhamini Mtumwa Said Haji (Kijiba) akitowa maelezo kwa Waandishi wa habari kuhusu mgogoro wa Uongozi unaoikabili klabu hiyo. (kushoto) Kaimu Katibu Mkuu wa Malindi Spoti Club Ali Salum Nassor (Mkweche.)
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Malindi Sports Club Mtumwa Said Haji (hayupo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika Ukumbi wa sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
Mwandishi wa Habari wa Chuchu fm Redio Yahaya Saleh akiwauliza swali viongozi wa klabu ya Malindi wanaotambuliwa na Bodi ya wadhamini wakati wa mkutano uliofanyika Ukumbi wa sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar. Picha Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.

WAZAZI, WATOTO OMBAOMBA KUSHTAKIWA

$
0
0
Na Fatma Salum – MAELEZO

Serikali imewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuwakamata na kuwashitaki mahakamani watoto pamoja na wazazi wao ambao huzagaa mitaani kuombaomba. Agizo hilo limetolewa leo bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Joseph Kakunda, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kiembesamaki, Ibrahim Raza, lililohoji ni lini Serikali itachukua hatua ya kuwaondoa ombaomba Jijini Dar es Salaam.

Kakunda alibainisha kuwa ni kweli ombaomba wengi zaidi wapo Jijini Dar es Salaam kutokana na kuwepo kwa vivutio vingi ikiwemo watu wenye imani mbalimbali ambao wengine huwapatia fedha ombaomba hao kama sehemu ya ibada.

“Kuzagaa kwa ombaomba kimekuwa chanzo kimojawapo cha uchafuzi wa mazingira na mara kadhaa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imechukua hatua mbalimbali za kuwaondoa ikiwemo kuwakamata na kuwarudisha kwao lakini wamekuwa wakirudi,” alisema Kakunda.

Alieleza kuwa mwaka 2013 ombaomba wapatao 253 na watoto 135 walikamatwa na kurejeshwa kwao ambapo watoto 33 walirejeshwa shuleni, hivyo inathibitisha kwamba wapo watu wazima wanaowatumia watoto kuombaomba na kuwakosesha fursa ya kupata elimu au kuwa watoro.

“Nawaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri chini ya usimamizi wa Wakuu wa Mikoa kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama, kuwakamata watoto wote ambao badala ya kwenda shuleni huzagaa mitaani kuombaomba,” alisisitiza Kakunda.

Alisema kuwa watoto hao wakamatwe pamoja na wazazi wao na washitakiwe mahakamani chini ya Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 inayokataza utoro na Sheria ya Kanuni ya Adhabu kifungu cha 166, 167 na 169 (a) vinavyohusu Wajibu wa Wazazi na Walezi kwa Watoto.

Pia Kakunda alishauri Mabaraza ya Madiwani kutunga sheria ndogondogo za kuzuia utoro pamoja na kudhibiti mienendo ya baadhi ya watu wanaoombaomba.

Aidha, alitoa rai kwa watanzania kutumia fursa za kupambana na umaskini zilizoandaliwa na Serikali ikiwemo elimu ya msingi bila malipo, huduma za afya vijijini, fursa za mikopo na matumizi bora ya ardhi yenye rutuba ili waweze kujikwamua kiuchumi.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO SEPTEMBA 12, 2018

Mkuu wa wilaya ya Kibaha Asumpter Mshama mzigoni

Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images