Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Londoni Sekondari yashinda Mashindano ya Vilabu vya kodi shule za Sekondari Ruvuma

$
0
0
 Mbunge wa Songea Mjini Dr. Damas Ndumbaro akizungumza wakati wa kufunga mashindano ya Vilabu vya Kodi kwa shule za Sekondari katika Tamasha la Majimaji Serebuka 2018 linaloendelea Mkoani Ruvuma. Wengine kutoka kushoto ni Meneja wa TRA mkoa wa Ruvuma Rosalina Mwenda, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA Richard Kayombo na Meneja wa NMB Ruvuma Ritha Majahasi.
 Mwanafunzi kutoka shule ya Sekondari Londoni akipongezwa na Mbunge wa Songea Mjini Dr. Damas Ndumbaro (wa pili kulia) baada ya shule yake kuibuka mshindi wa jumla wa mashindano ya Vilabu vya Kodi kwa shule za Sekondari katika Tamasha la Majimaji Serebuka 2018.
  Mwanaidi Hamisi mwanafunzi wa shule ya Sekondari Maposeni akipokea zawadi ya kibubu baada ya kuibuka mshindi wa pili katika shindano la uchoraji wa kibonzo kinachohusu masuala ya kodi.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA Richard Kayombo akimkabidhi kibubu ambacho ameweka fedha taslim shilingi 50,000 mmoja wa wanafunzi walioibuka washindi wa kuwasilisha vizuri mada kuhusu mashine za kodi za kielektroniki wakati wa mashindano ya Vilabu vya Kodi kwa shule za Sekondari  katika Tamasha la Majimaji Serebuka 2018.
 Washindi wa jumla wa mashindano ya Vilabu vya Kodi kwa Shule za Sekondari katika Tamasha la Majimaji Serebuka 2018 (waliosimama) wakiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Songea Mjini Dr. Damas Ndumbaro (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA Richard Kayombo (wa pili kushoto), Meneja wa TRA Ruvuma Rosalina Mwenda (wa kwanza kushoto) na Meneja wa NBM Ruvuma Ritha Majahasi (wa kwanza kulia).

 Majaji (waliosimama) walioshiriki kuchagua shule bora na wanafunzi bora katika mashindano ya Vilabu vya Kodi kwa shule za Sekondari katika Tamasha la Majimaji Serebuka 2018 wakiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Songea Mjini Dr. Damas Ndumbaro (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA Richard Kayombo (wa pili kushoto), Meneja wa TRA Ruvuma Rosalina Mwenda (wa kwanza kushoto) na Meneja wa NBM Ruvuma Ritha Majahasi (wa kwanza kulia).


BALOZI SEIF ATEMBELEA ZBC RADIO RAHALEO MJINI UNGUJA

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  amewashauri Wana Habari wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) kuendelea kuwa wabunifu zaidi wa vipindi  vitakavyoleta mvuto na hatimae kuwa na  wasikilizaji wengi zaidi wa Shirika hilo Nchini.

Alisema licha ya kuwepo kwa vipindi vingi vilivyokuwa maarufu  na kukubalika kwa wasikiizaji wengi akitolea mfano Kipindi cha Mawio na Maelezo baada ya Habari lakini bado juhudi za ubunifu zinahitajika katika kuona Mfumo wa Matangazo unawafikia Wananchi wengi zaidi Mjini na Vijijini.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa ushauri huo wakati alipofanya ziara fupi katika Kituo cha Matangazo cha Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC – REDIO) kiliopo Rahaleo Mjini Zanzibar kuangalia shughuli za utendaji kazi wa Taasisi hiyo ya Habari na kuridhika na jitihada zinazochukuliwa na Watendaji wawake.

Alisema upo umuhimu wa vipindi na matangazo ya ZBC Redio kuangaza zaidi kwa upande wa Majimboni na Vijijini ili Wananchi wa maeneo hayo wawe na fursa ya kuwasilisha changamoto zinazowakabili hasa katika harakazi zao za kujiletea maendeleo.

Balozi Seif alieleza kwamba wakati Serikali Kuu inafikiria jitihada za kusaidia changamoto zinazowakabili watendaji wa Kituo hicho cha Matangazo ya Radio ambapo pia kupitia nafasi yake ya Uwakilishi atajaribu kuwashawishi Wawakilishi wenzake majimboni kutoa ushirikiano utakaowezesha kuendelezwa kwa Vipindi vya kutoka Majimboni.

Alisema vipo vipindi vinavyoweza kusaidia Wananchi kuelimika zaidi ambavyo vinapaswa kupewa umuhimu wa pekee ili kupunguza kero zinazowakabili sambamba na kumrahisishia Mwakilishi kutekeleza majukumu yake badala ya kusubiri Vikao vya Baraza la Wawakilishi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilakiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale anayesimamia Habari Dr. Yussuf  Mnemo alipofanya ziara fupi  katika Kituo cha Matangazo cha Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC – REDIO). Kulia ya Dr. Mnemo ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar Bibi Iman Duwe na Naibu Wake Bibi Nasra Mohamed.
Msaidizi Mhariri Mkuu wa Chumba cha Habari ZBC –Redio Amour Nassor akimuelezea Balozi Seif  aliyepo (katikati) Majukumu ya Wana Habari katika uwajibikaji wao wa kila siku. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa ZBC Bibi Iman Duwe  nas kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma N’hunga.
Fundi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar Ali Boud Talib aliyevaa kofia ya Kiua akimpatia maelezo balozi Seif   ndani ya moja ya Studio ya Watangazaji wakati wa ziara yake katika Kituo cha Matangazo ya Redio Rahaleo. Wa kwanza kutoka Kushoto ni Mtangazaji mahiri wa Redio na Televisheni Khamis Mohamed na Mkuu wa Kitengo cha Watangazaji Bibi Suzan Peter Kunambi.
Mtangazaji wa Spice FM ambae pia mpiga picha wa ZBC – TV Said Golo na watangazaji wenzake wakifurahia ujio wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ndani ya Studio yao iliyopo Rahaleo.
Balozi Seif akisisitiza umuhimu wa Uongozi wa ZBC kutumia Bajeti zao za Mwaka katika kutanzua baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwemo Vikalio. Picha na – OPMR – ZNZ.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Wafanyakazi wa JKCI wamuaga Afisa Muuguzi Mwandamizi Mama Hadija Mradi aliyestaafu utumishi wa Umma

$
0
0
 Afisa Muuguzi Mwandamizi Mstaafu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mama  Hadija Mradi (kulia) akikata keki wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Taasisi hiyo ilizopo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi  Robert Mallya
 Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akimlisha keki Afisa Muuguzi Mwandamizi Mstaafu Mama  Hadija Mradi wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo katika  ukumbi wa mikutano wa  Taasisi hiyo uliopo jijini Dar es Salaam . Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi (kushoto) akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wake katika utumishi wa umma kwa kufanya kazi kwa miaka 41 Afisa Muuguzi Mwandamizi Mstaafu Mama  Hadija Mradi katika  hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi Robert Mallya.
 Afisa Muuguzi Mwandamizi Mstaafu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mama  Hadija Mradi (kulia) akifuatilia yaliyokua yakiendelea wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Delila Kimambo.
Baadhi ya wafanyakazi  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa hafla fupi ya kumuaga Afisa Muuguzi Mwandamizi Mstaafu Hadija Mradi (hayupo pichani) iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo uliopo jijini Dar es Salaam. Picha na JKCI

JALADA LA KESI DHIDI YA MKE WA BILIONEA MSUYA LIKO MKONONI MWA DPP

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

Upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mke wa bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita (41), umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi lipo mikononi kwa  kwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP).

Wakili mwandamizi wa Serikali, Patrick Mwita ameeleza hayo leo Jumatatu Julai 23, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Mbali na Mrita, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ya mauaji namba 5 ya mwaka 2017 ni mfanyabiashara Revocatus Muyela (40)  ambapo wote wanakabiliwa na shtaka mmoja la mauaji ya dada yake Erasto Msuya, Aneth Msuya.

"Shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na jalada la kesi kwa sasa lipo mikononi mwa DPP bado tunalifuatilia "amedai Mwita.

Kufuatia taarifa hiyo, Hakimu Simba amewataka upande wa mashtaka kulifuatilia jalada hilo ambalo mwanzoni walidai liko ofisini kwa DPP na sasa liko mikononi mwake.

Wakili wa utetezi Peter Kibatala alikubaliana na upande wa mashtaka na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine fupi.

 Hakimu Simba ameahirisha  kesi hiyo hadi Julai 30, 2018 itakapotajwa tena.

Februari 23, 2017, washitakiwa hao waliachiwa huru na mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa na kisha wakakamatwa tena na baadaye kusomewa upya shtaka moja la mauaji.

Washtakiwa wanadaiwa kumuua kwa makusudi Aneth tukio linalodaiwa kutokea Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU WA KOREA AONDOKA NCHINI BAADA YA ZIARA YA SIKU TATU

$
0
0
WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-yon amemaliza ziara yake ya kiserikali ya siku tatu hapa nchini na kusindikizwa na mwenyeji wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

 Waziri Mkuu huyo wa Korea ambaye ameondoka leo Jumatatu, Julai 23, 2018 saa 9.14 alasiri, ameelekea Oman ambako atakuwa na ziara ya kikazi ya siku mbili. Aliwasili nchini juzi akitokea Kenya ambako pia alikuwa na ziara ya siku mbili.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius  Nyerere, Waziri Mkuu wa Korea Kusini alisindikizwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Eng. Stella Manyanya na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam

Kabla ya kuondoka alishuhudia burudani kutoka vikundi vya ngoma na matarumbeta uwanjani hapo.

Mara baada ya mgeni wake kuondoka, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alizungumza na wasanii waliokuwepo uwanjani na kuwapongeza kwa kujitokeza kutoa burudani kila wakati wageni wanapoitembelea Tanzania.

“Tunawashukuru sana wasanii kwa sababu mlikuja wakati wa mapokezi ya mgeni wetu na sasa mmekuja tena kumsindikiza. Mgeni wetu amefurahia sana ngoma zetu na amesema atarudi tena Tanzania.”

“Kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Serikali kwa ujumla, tunatambua kuwa mnajitoa muda wenu kila mnapokuja kupokea na kusindikiza wageni ili kuweka sura nzuri ya Taifa letu wakati wa kupokea wageni wetu, tunawashukuru sana,” amesema.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak - yun wakifurahia burdani ya kikundi cha matarumbeta kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere wakati mgeni huyo alipoondoka nchini Julai 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na mgeni wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-yon wakati akiondoka kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya ziara ya siku tatu nchini, Julai 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Ndege iliyombeba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak - yun ikiruka kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere baada ya kiongozi huyo kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Julai 23, 2018.

Shahidi katika kesi ya kumiliki Mali zaidi ya kipato chake adai mtuhumiwa hakutamka magari 10 katika mali zake

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa Ofisa Msaidizi wa Forodha wa TRA  Jennifer Mushi anayekabiliwa na kesi ya kumiliki magari 19 yenye thamani ya Sh. Mil 197 wakati wa uhakiki wa mali zake, walibaini kuwa na magari 10 ambayo hayakutamkwa.

Afisa Mchunguzi wa TRA, Tumaini Fadhir ameieleza hayo leo wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Akiongozwa na wakili wa serikali, Vital Peter amedai baada ya kupitia fumo za matamko mbali mbali ya Mali na madeni, walibaini magari zaidi ya kumi yaliyoonekana kwenye miliki za mshtakiwa yakiwa hayajatamkwa kwa mujibu wa taratibu.
"Nilifanya uchunguzi wa mali zote zinazohusika na zisizohusika na kibaini kuwa magali hayo hayakutamkwa ukichilia, magari hakuna mali zingine tulizobaini", amedai Tumaini.
Amedai kuwa, baada ya kubaini hayo, alitoa taarifa kwa menejimenti.

Katika ushahidi wake, Tumaini amedai  yeye ni mchunguzi wa ndani wa TRA, huku majukumu yake ni kuchunguza malalamiko ya watumishi,  kuhakiki mali za watumishi  zinazohusu matamko ya mali na madeni  kwa lengo la kuthibiti vitendo vya rushwa.

Aidha akihojiwa na wakili wa uetezi Furgence Masawe kama anamfahamu Jennifer, alijibu kuwa anamfahamu kwa sababu aliwahi kumchunguza. 

Pia aliulizwa kama anafamu idadi ya mali za Jennifer na thamani yake , Tumaini alijibu anafahamu. 

Pia aliulizwa Jennifer alianza kazi lini TRA, alijibu kuwa tangu mwaka 2011 lakini awali aliajiriwa katika sekta binafsi. 

Baada ya kutolewa ushahihidi huo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo  hadi August 16,2018.

Jenifer anakabiliwa na kosa la kumiliki magari 19 mali ambayo hailingani na kipato chake, anadaiwa aliyaingiza magari hayo nchini kutokea Japan yakiwa na thamani ya shilingi  Milioni 197,601, 207.

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI KITUO CHA AFYA CHA TUNDUMA NA KUHUTUBIA WANANCHI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Utawala Bora ni moja ya ahadi waliyoitoa kwa wananchi wakati wa kampeni.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Tunduma ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake katika mkoa wa Songwe.
 “Lazima tunapofanya kazi zetu sheria zifuatwe, unapoacha kufuata sheria kwa sababu ya Matakwa binafsi, kwa sababu ya kunufaika wewe binafsi hili ni Tatizo hapa hapana utawala bora” 
alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais alisema Utawala bora usisukumwe tu upande wa Serikali unapaswa kupimwa kwenye ngazi zote mpaka za chini zikiwemo ngazi za Udiwani.
Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Utawala bora ni pamoja na maendeleo ya Serikali yanapatikana.
Makamu wa Rais amesema Serikali itajenga pamoja na kuboresha vituo vya Afya 9 katika mkoa wa Songwe ambapo wilaya ya Momba kutakuwa na vituo vitatu.
Mapema leo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefungua kituo cha Afya cha Tunduma kilichofanyiwa maboresho na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 500 na ambacho kitahudumia wakazi zaidi ya elfu 80.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la  Kituo cha Afya cha Tunduma ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe.  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi waTunduma  kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Tunduma ikiwa siku ya tatu ya ziara yake mkoani Songwe. 

 Sehemu ya Umati wa wakazi wa Tunduma waliojitokeza kumsikiliza Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wauguzi wa Kituo cha Afya cha Tunduma mara baada ya kukifungua  ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Esther Luila mwenye umri wa miaka 7 mara baada ya kukifungua  kituo cha Afya Tunduma  ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na Wajasiriamali wa Wilaya ya Momba muda mfupi kabla hajahurubia kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Tunduma ikiwa siku ya tatu ya ziara yake mkoani Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS MAGUFULI APOKEA MAGAWIO TOKA KATIKA TAAISI, MASHIRIKA NA MAKAMPUNI YA UMMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya TIPER Profesa Abdulkarim Mruma  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Bw. Edwin Rutageruka.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mfuko wa Misitu Tanzania akiwa na Katibu Dkt. Tuli Salum Msuya  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na (EWURA) Maji Profesa Jamidu Kamika akiwa na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa  EWURA Bw. Nzinyangwa Mchani  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekliti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Profesa Rutasitara akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Balozi Ben Moses akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa TFDA Bi. Agnes Kijo   katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Shirika la Viwango (TBS)  Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko akiwa na  Mkuruigenzi wa TBS Profesa Egird Mubofu  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari  Profesa Ignas Rubaratuka aliye pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi Deusdedit Kakoko  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu wakipata picha ta pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumua ya Bunge ya Uwekezaji wa Mtaji wa Umma baada ya kupokea magawio kutoka katika taasisi, mashirika na Makampuni ya Umma katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 23, 2018. Picha na IKULU

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

PUMA ENERGY TANZANIA LIMITED YATANGAZA GAWIO LA BILIONI 18 KWA MWAKA 2017 KWA WANAHISA WAKE

$
0
0
*Wakabidhi gawio lao kwa Rais Dk.Magufuli leo Dar 

KAMPUNI ya mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited imetangaza gawio la Sh.bilioni 18 kwa mwaka wa fedha wa 2017 kwa wanahisa wake.

Puma Energy Tanzania ni kampuni ambayo inayomilikiwa kwa pamoja na Serikali(kupitia Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha) pamoja na Puma Investments Limited, kila moja ikiwa na umiliki wa hisa kwa asilimia 50 imetanza gawio hilo leo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti, ni kwamba ni kampuni ya mkondo wa kati kimataifa katika masula ya mafuta na pia kampuni ya mafuta inayojihusisha na uhifadhi mkubwa na usambazaji. 

Amesema majukumu ya makuu ya kampuni ni masoko na usambazaji wa bidhaa za petroli ndani ya Tanzania. "Kampuni inauwezo wa kuhifadhi jumla ya lita za mafuta 94 milion, vituo 52 vya mafuta maeneo mbalimbali nchini na inahudumia viwanja vinane vya ndege. "Kufikia mwisho wa mwaka ulioishia 31 Desemba 31 2017 kampuni ilitengeneza faida kabla ya kodi ya jumla ya Sh. bilioni 31,"amesema.

Amefafanua kampuni iliwekeza takribani Sh.bilioni 9 bilioni kwa mwaka 2017 kununua na kuendeleza miundombinu ikiwemo kununua vituo viwili vya mafuta kwenye Jiji la Dodoma ikiwa ni juhudi za kuiunga Serekali mkono katika kuhamia Dodoma.Ameongeza wakurugenzi wa kampuni hiyo wamependekeza gawio la Sh.bilioni 18 kwa mwaka ulioishia Disemba 2017.

Ameongeza kila mwanahisa atapata Sh.bilioni 9 na kwamba mwaka 2016 Gawio lilikua Sh.bilioni 14 na 2015 gawio lilikua Sh.bilioni 9 .) "Kutokana na utendaji mzuri wa kampuni ya Puma Energy, gawio limekua kwa asilimia 100 ikilinganishwa na gawio la mwaka 2015 na kwa asilimia 29 ikilinganishwa na gawio na mwaka 2016. 

"Ukuaji huu unaendana sambamba na mikakati ya kampuni ya kuhakiksha kampuni inaendelea kukua, kutengeneza faida, kukuza ajira nchini, kuchangia pato la taifa kupitia kodi, na kuendelea kuiunga serekali mkono katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo,"amesema Corsaletti.

Amesisitiza kuwa “Ufanisi wa kibiashara wa Puma Energy Tanzania kwa mwaka 2017 ulikua mzuri kwa pande zote za mauzo pamoja na mapato.
"Ufanisi wetu mkubwa unatokana zaidi na biashara ya mafuta ya ndege ambako kwa sasa sisi ndio tunaongoza katika soko,"amesema.
 Rais John Pombe Magufuli  (katikati) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh bilioni tisa ikiwa ni sehemu ya gawio la sh bilioni 18 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  pamoja na Puma Investments Limited wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr Phillip Mpango  (kushoto kwake), Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo Bw Prof Joseph Buchweshaija (kushoto) na Meneja Uendeshaji wa  Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bw Lameck  Hiliyai (kulia)
 Meneja Uendeshaji wa  Kampuni ya Puma Energy Tanzania Bw Lameck  Hiliyai (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh bilioni tisa kwa Rais John Pombe Magufuli  (katikati) ikiwa ni sehemu ya gawio la sh bilioni 18 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  pamoja na Puma Investments Limited. Hafla hiyo fupi imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr Phillip Mpango  (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo Bw Prof Joseph Buchweshaija.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>>

SERIKALI YA MAGUFULI SIO YA 'WALIMILA DOLE'

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo leo ametembelea halmashauri ya wilaya ya Kibaha kufanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo. 

Katika Ziara hiyo, Waziri Jafo amefanikiwa kutembelea kituo cha afya Mlandizi, ukarabati wa sekondari ya wasichana ya Ruvu, pamoja na uboreshaji wa Kituo cha afya cha Magindu ambapo zaidi ya sh. bilioni 1.9 zimeshatolewa na serikali kufanikisha miradi hiyo. 

Akizungumza na wananchi wa Magindu waziri Jafo amewaambia wananchi hao kwamba serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli ni serikali ya vitendo sio ya kuahidi bila kutekeleza na kwamba kwa kizaramo "Sio ya walimila Dole". 

Jafo alitumia neno hilo la Lugha ya kizaramo kwa wakazi hao wa magindu ambao wengi wao ni wazaramo ili kuleta msisitizo.Waziri Jafo amempongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Hamood Abuu Jumaa kwa kazi kubwa anayoifanya ya kiwaletea wananchi wa kibaha vijijini maendeleo ya kweli. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Kibaha vijijini Hamood Jumaa katika kituo cha afya Mlandizi mkoani Pwani.
Viongozi wakiwa Katika zoezi la ukaguzi wa miradi ya maendeleo ndani ya halmashauri ya kibaha vijijini.
Mbunge wa Kibaha Vijijini Hamood Abuu Jumaa akimkaribisha Waziri wa Nchi, Tamisemi Selemani Jafo kijijini Magindu ili aongee na wananchi.

PICHA MBALIMBALI ZA ZIARA YA WAZIRI KANGI LUGOLA JIJINI ARUSHA

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto), akiongozana na Naibu Waziri  Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (kulia) na  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (wapili kulia), kutembelea eneo la Kaloleni zilipo nyumba za polisi, jijini Arusha.Kushoto ni mmoja wa wadau waliojitolea kujenga nyumba hizo,Hans Pol.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Waziri  wa Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi,  Kangi Lugola (wapili kushoto),  akimsikiliza Kamanda wa  Polisi  Mkoa  wa  Arusha, Ramadhani  Ng’anzi (kulia) baada ya kutoka kutembelea Kituo cha Polisi Utalii.Wapili  kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

 Waziri  wa Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi,  Kangi Lugola (wapili kushoto),  akimsikiliza Kamanda wa  Polisi  Mkoa  wa  Arusha, Ramadhani  Ng’anzi (kulia) baada ya kutoka kutembelea Kituo cha Polisi Utalii.Wapili  kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na mdau wa maendeleo mjini Arusha,Hans Pol.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo.Waziri Lugola yupo mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, Naibu Waziri  Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (kushoto)  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia),wakisikiliza taarifa ya Kituo cha Polisi Utalii baada ya viongozi hao kutembelea kituo hicho.

MAHAKAMA YAWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WAKE KUHUSU MASUALA YA HABARI

$
0
0
Na Lydia Churi-Dodoma 

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Mohamed Awadh leo amefungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari wa Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama Kuu na Mahakama za Mikoa na kuwataka washiriki hao kujifunza namna ya kutoa taarifa za Mahakama zilizo sahihi ili kuboresha suala zima la utoaji wa haki kwa wananchi.

Akifungua mafunzo hayo mjini Dodoma, Jaji Awadh amesema Mahakama ya Tanzania kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (2015/16-2019/20) inalenga kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama na kuimarisha ushirikishwaji wa wadau katika shughuli zake ambapo kwa kuwapatia mafunzo wawakilishi wa habari ni moja ya mikakati ya kufanikisha jambo hilo. 

Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari wa Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama Kuu na Mahakama za Mikoa yanawahusisha Watumishi wa Mahakama wakiwemo Maafisa Habari, Maafisa Utumishi, Maafisa Tawala, Maafisa Tehama pamoja na Wasaidizi wa Kumbukumbu.

Aidha mafunzo hayo pia yanawahusisha Maafisa Habari wa Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakama ya Tanzania zikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume ya Kurekebisha Sheria, Wizara ya katiba na Sheria na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. 

Alisema mafunzo hayo yatasaidia kuimarisha utoaji wa habari za mahakama kwa wananchi kwa kuwa Maafisa hao watajengewa uwezo utakaowawezesha kuandika taarifa za mahakama zitakazoongeza uelewa kwa wananchi juu ya maboresho yanayoendelea kufanyika na hatimaye kurejesha imani ya wananchi kwa Mhimili huo.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Mhe. Mohamed Awadh akifungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari za Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama kuu ya Tanzania na kwenye Mahakama za Mikoa yaliyoanza leo mjini Dodoma. Kushoto ni Mshauri Mwelekezi wa Mawasiliano kutoka kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama (Judiciary Delivery Unit- JDU) Dkt. Cosmas Mwaisobwa na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mahakama ya Tanzania Bw. Nurdin Ndimbe.
Maafisa Habari, Maafisa Tawala, Maafisa Utumishi, Maafisa

Tehama na Wasaidizi wa Kumbukumbu wanahudhuria mafunzo hayo. Mafunzo hayo pia yanahudhuriwa na Maafisa habari kutoka baadhi ya Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakama zikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume na Tume ya Kurekebisha Sheria. 
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Mhe. Mohamed Awadh akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washirikiwa Mafunzo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari za Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama kuu ya Tanzania na kwenye Mahakama za Mikoa yaliyoanza leo mjini Dodoma. Mafunzo hayo pia yanahudhuriwa na Maafisa habari kutoka baadhi ya Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakama zikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume na Tume ya Kurekebisha Sheria. 
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Mhe. Mohamed Awadh akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washirikiwa Mafunzo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari za Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama kuu ya Tanzania na kwenye Mahakama za Mikoa yaliyoanza leo mjini Dodoma. Mafunzo hayo pia yanahudhuriwa na Maafisa habari kutoka baadhi ya Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakama zikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume na Tume ya Kurekebisha Sheria.

VODACOM YAPATA LESENI YA MASAFA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Vodacom imepata leseni ya masafa ya mawasiliano katika bendi ya 700MHZ baada ya kuibuka mshindi katika mnada wa masafa hayo.

Vodacom ilishinda masafa hayo kwa jumla ya bei dola za Kimarekani 1,0005,000 ambapo masafa hayo yatalipiwa kodi kila mwaka dola za Kimarekani 40,000.

Akizungumza baada ya Vodacom kupata leseni Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzu Mhandisi Isaac Kamwelwe amesema kuwa TCRA imekuwa ikifanya kazi nzuri ambapo imetoa gawio la sh.bilioni 81.Amesema kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) kuhakikisha Vodacom inatekeleza masharti ya leseni yanatekelezwa kama ilivyokusudiwa katika utoaji wa huduma ya mawasiliano.

Kamwelwe ameiataka TCRA kuendelea na utaratibu wa kugawa masafa kwa njia ya mnada kutokana na faida ya kiuchumi kwa fedha inayopatikana kuendeleza miundombinu ya huduma za simu za mikononi na data zenye kasi kubwa , ubora , kupunguza gharama za uwekezaji.Nae Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhadisi James Kilaba amesema kuwa kuna njia mbalimbali za ugawaji wa masafa ikiwemo kutoa masafa kwa anayewahi kuomba pamoja na njia ya mnada.

Amesema masafa ya simu za mkononi ya faida katika kuendeleza huduma za simu za mkononi na data zenye ubora ,kupunguza gharama za matumizi ya huduma za mawasiliano kwa mtoa huduma ya masafa hayo.Kilaba amesema faida nyingine ni kukuza na kuchochea ubunifu wa huduma mpya na matumizi ya teknolojia za habari na mawasiliano pamoja na serikali kupata mapato kutokana na mauzo ya masafa hayo.
 01.Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzu Mhandisi Isaac Kamwelwe akizungumza na waandishi habari mara baada ya kampuni ya Vodacom kupata leseni ya masafa kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa TCRA jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini TCRA, Mhadisi James Kilaba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na utoaji wa leseni ya masafa kwa kampuni Vodacom katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa TCRA jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini TCRA, Mhadisi James Kilaba akimkabidhi leseni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom(T) Plc katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa TCRA jijini Dar es Salaam

SINGIDA UNITED YAENDELEA KUIPIGA TAFU YANGA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Uongozi wa klabu ya Singida United kupitia kwa Rais wake Dkt Mwigulu Nchemba imeendelea kuipiga tafu timu ya Yanga baada ya kuwapatia mchezaji mwingine wa kigeni raia wa Zimbabwe.

Huyu anakuwa ni mchezaji wa pili baada ya Jana kuweka wazi kuwa Kiungo kutoka JKU Feisal Abdala 'Fei toto' kuwa wamemruhusu kwenda kukipiga katika klabu ya wanajangwani hao ikiwa ni moja ya mchango wake wa kuisaidia Yanga.

Ikiwa imepita siku moja toka kuweka wazi hilo, leo Uongozi wa Singida umetuma baru Katibu Mkuu wa Yanga na nakala nyingine kwa TFF na Bodi ya ligi kuwapa taarifa kuwa mchezaji Elisha Moroiwa kuanzia sasa ni mali ya Yanga.

Barua hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Singida United   AbdulRahman Sima imeweka wazi kuwa mchezaji huyo tayari ameshapatiwa fedha zake zote na hadai mkataba wowotena lengo kuu ni kuisaidia Yanga.

Yanga ambayo ipo katika kipindi kigumu wakiwa wanaandamwa na ukata wa fedha pamoja na viongozi kujiuzulu mpaka sasa walikuwa wameshafanya usajili wa wachezaji wanne wakimrejesha Mrisho Ngasa na Deus Kaseke ambao awali walikuwa wanacheza kwenye timu hiyo.

Takribani wachezaji saba ndiyo waliokuwa na mikataba huku wengine wakiwa wanataka kuongezewa mikataba na dirisha la usajili linatarajiwa kufungwa Julai 26 saa 6 usiku huku TFF wakisistiza hakutakuwa na muda wa nyongeza katika suala hilo.

Balozi Mabumba awasisitiza Watanzania waishio nchini Comoro (TADICO) kuwekeza nyumbani

$
0
0
Balozi wa Tanzania Visiwani Komoro Mhe. Sylvester Mabumba alikutana na kufanya mazungumzo na uongozi mpya wa Diaspora ya Watanzania waishio Komoro (TADICO) tarehe 23 Julai 2018. Viongozi hao wapya walifika ofisi za Ubalozi kwa ajili ya kujitambulisha ambapo miongoni mwa mambo waliyojadili ni pamoja na kutoa ahadi ya kuinua Diaspora ya Watanzania waishio Comoro ambapo kwa muda mrefu Diaspora hiyo imeonekana kuwa nyuma kimaendeleo ikilinganishwa na Diaspora za nchi nyingine.

Kwa upande wake Mhe. Balozi Mabumba alichukua fursa hiyo kuwapongeza viongozi hao wapya waliochaguliwa pamoja na kuwatakia kila la kheri katika nafasi zao hizo mpya walizoaminiwa na Watanzania wenzao. Aidha, Mhe. Mabumba alisisitiza juu ya umuhimu wa wanachama kulipa michango ya uanachama na vilevile kuwaomba viongozi kuwa wasimamizi wazuri wa matumizi ya fedha za wanachama hao.

Katika hatua za kuhuisha chama hicho wajumbe walishauriwa pia kuwa wabunifu katika mikakati yao na vilevile waangalie njia gani bora za kuibua vyanzo vipya vya mapato badala ya kutegemea michango ya wanachama pekee. Pia Balozi Mabumba aliwahimiza viongozi hao kutosahau kuwekeza nyumbani na vilevile kuchangamkia fursa za biashara ambazo zinapatikana Tanzania na kuzitangaza Visiwani humo.
Balozi wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Balozi Sylivester Mabumba (kati) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa Ubalozi na viongozi wa Diaspora visiwani Comoro. Kutoka Kushoto ni Bw.. Hussein Banoga, Makamu Mwenyekiti; Bw.. Khamis Salum, Mweka Hazina; Bw.. Thabit Khamis, Afisa Ubalozi; Bw.. Fikiri Salum, Katibu Mkuu; Bw. Salum Ali, Mwenyekiti; Bw. Fuastine, Bw. Isakwisa na Bw. Mudrick Soragha. 
Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja. 

MZEE WA MIAKA 71 AKUTWA NA NYARAKA BANDIA ZA SERIKALI .

$
0
0
. ALIKUWA NI MTUMISHI WA SERIKALI OFISI YA MKUU WA WILAYA -MOSHI
. AKUTWA NA VYETI 240 NA MIHURI 159.
. RPC KILIMANJARO ATAKA WALIOCHONGEWA VYETI NA MZEE HUYO KUJISALIMISHA.

Na Dixon Busagaga ,Moshi

JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mzee wa miaka 71 na watu wengine watatu baada ya kukutwa na Nyaraka  bandia za serikali  240 ambazo wamekua wakiziandaa kwa njia ya udanganyifu pamoja na Mihuri 159 na kuuzwa kwa bei ya Sh 20,000.

Nyaraka zilizo kamatwa ni pamoja na Vyeti vya kuzaliwa ,vyeti vya ndoa ,vyeti vya ubatizo,vyeti vya Kliniki na matamko ya vizazi na vifo pamoja na mihuri mbalimbali miongoni mwao ikionyesha ni ile inayotumika wakati wa usajili vizazi na vifo katika manispaa ya Moshi na Kitete mkoani Tabora.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Msaidizi wa Polisi,Hamisi Issa alisema vifaa vingine vilivyo kamatwa ni pamoja na Mashine moja ya kuandikia (Type Writer) na kifaa cha kuwekea namba huku akiwataja watuhumiwa kuwa ni pamoja na Athuman Selemani (71) anayetajwa kuwa aliwahi kuwa mtumishi wa serikali katika ofisi ya mkuu wa wilaya .

Wengine ni Justine Mziray (55) anayetajwa kuwa ni mtaalamu wa kuchonga mihuri,Sporah Daud anayetajwa kushiriki katika uandaaji wa nyaraka hizo kwa kuchapa maandishi kwa kutumia mashine maalumu (Type writer) na Costa Lyatuu  anayetajw kuwa mtaalamu wa kughushi sahihi.
 Sehemu ya nyaraka  mbalimbali za bandia zilizokutwa kwa mtuhumiwa huyo.
 JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mzee wa miaka 71 na watu wengine watatu baada ya kukutwa na Nyaraka  bandia za serikali  240 ambazo wamekua wakiziandaa kwa njia ya udanganyifu pamoja na Mihuri 159 na kuuzwa kwa bei ya Sh 20,000.
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Msaidizi wa Polisi,Hamisi Issa akionesha baadhi ya mihuri iliyokutwa kwa mtuhumiwa huyo
 Mihuri iliyokuwa ikitumika
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Msaidizi wa Polisi,Hamisi Issa akionesha baadhi ya mashine aliyokuwa akitumia mtuhumiwa huyo kutengenezea nyaraka bandia za serikali

MKURUGENZI WA ZAMANI NSSF AKABIDHI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA

$
0
0
Aliyekuwa Mkurugenzi mkuu wa Shirika  la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF ,Professa Godius Kahyarara (pichani kulia) akimkabidhi  baadhi ya nyaraka kwa MKurugenzi mkuu mpya wa NSFF Ndugu William  Erio kwenye makabidhiano ya ofisi leo makao makuu ya Shirika hilo.
 Mkurugenzi mkuu wa Shirika  la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF ,Professa Godius Kahyarara akizungumza jambo na MKurugenzi mkuu mpya wa NSSF Ndugu William  Erio mara baada ya makabidhiano ya ofisi leo makao makuu ya Shirika hilo.

NEWS ALERT: WAZIRI MHAGAMA ATENGUA BODI YA NSSF

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari alipokutana nao hii leo Jijini Dodoma.
==============
Waziri Mhagama ametengua Bodi ya Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Utenguzi huo umeanza hii leo tarehe 24 Julai, 2018, baada ya hatua mbalimbali za Serikali ya Awamu ya Tano kuendelea kuimarisha utendaji kazi wa Taasisi na Mashirika yake.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (MB) alipokutana na waandishi wa habari hii leo Mjini Dodoma Julai 24, 2018.
Waziri Mhagama alieleza kuwa, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo kama Waziri wenye dhamana kwenye masuala ya hifadhi ya jamii ninatangaza rasmi kuivunja Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii pamoja na uteuzi wa Wajumbe wote wa bodi hiyo.
“Lengo kuu la madiliko haya ni kuhakikisha kuwa shirika hilo linaimarishwa zaidi sambamba na kusimamia mwenendo wa kila siku wa shirika ikiwemo zile kazi za msingi kuongeza wanachama, kukusanya michango, kulipa mafao kwa wakati na kusimamia vitega uchumi kwa uzalendo na weledi” alisisitiza Mhe. Mhagama 
Aidha, Waziri Mhagama alitoa taarifa rasmi kuhusu mfumo utakao tumika kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya Mashujaa ambayo hufanyika tarehe 25 Julai kila mwaka. Katika kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, fedha zilizopangwa kufanyia maandalizi ya sherehe hizo Kitaifa ambazo ilikuwa zifanyike kwenye Jiji la Dodoma zitatumika kuboresha miundombinu ya barabara katika Jiji la Dodoma. 
“Mwaka huu 2018 hakutakuwa na maadhimisho ya pamoja ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa, baadala yake kila Mkoa, Wilaya, Kata na Vijiji watafanya maadhimisho ya siku hiyo kwa kufanya usafi katika maeneo waliyozikwa Mashujaa wetu na maeneo yoyote ambayo yanakumbukumbu za Mashujaa wetu nchini” alisema Mhe. Mhagama.

MATAYARISHO JENGO LA KIHISTORIA MJI MKONGWE YAANZA RASMI

$
0
0

Na Mwashungi Tahir Maelezo 

Matayarisho ya matengenezo ya Jengo la Kihistoria la Mji mkongwe la Beit el Ajaib yameanza rasmi kwa ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Oman

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Issa Makarani Sariboko alieleza hayo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya maandalizi yanavyoendelea katika jengo hilo Forodhani.

Alisema ujenzi wa jengo hilo mashuhuri katika Ukanda wa Afrika Mashariki lililoporomoka mwaka 2012 litagharimu zaidi ya Dola za Marekani milioni nne na nusu na matengenezo yake yatachukua miezi 18.

Aliwaeleza waandishi wa habari kwamba wataalamu wazalendo wamemaliza kufanya uchambuzi wa matengenezo hayo na kazi ya ujenzi wa jukwaa kuelekea sehemu ya juu unaendelea.

“Tayari wataalamu wetu wamemaliza kufanya ufafanuzi wa jumba lote kuanzia sehemu ya juu iliyoporomoka, sehemu za ndani na eneo la chini ya ardhi ya jengo hilo’’, alisema Mkurugenzi Makarani.

Alisema kutakuwa na mchanganyiko wa timu ya wataalamu kutoka nchi za nje na wataalamu wazalendo wa Zanzibar ili kupata ufanisi mzuri wa ujenzi huo.

Nae Mkurugenzi wa Makumbusho Salim Kitwana Sururu alisema Serikali ya Oman ilifikia makubaliano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya kulifanyia matengenezo jengo hilo la kihistoria lililohifadhi kumbukumbu muhimu za tawala zilizopita.

Muhandisi wa Mji Mkongwe Suhad Sultani Alawi alitoa wito kwa wananchi wanaotumia eneo hilo kuwa tahadhari kubwa wakati wa matengenezo ya jengo hilo kwa kulinda usalama wao.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

UZINDUZI WA SHOWTIME ENTERTAINMENT KUFANYIKA NGOME KONGWE MJINI ZANZIBAR

$
0
0
MKURUGENZI wa Kampuni ya Showtime Intertiment Ibrahim Mitawi amesema kuwa wanatarajia kuzindua  Kampuni yao ifikapo tarehe 27 mwezi wa saba mwaka huu katika Ukumbi wa Ngome Kogwe Zanzibar.

Hayo aliyasema huko katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar wakati akizungumza na Waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa Kampuni ya Showtime Intertiment inayotarajiwa kuanza saa moja Usiku.

Alisema kuwa lengo kuu la uzinduzi wa Kampuni hiyo ni kutaka kuijuilisha  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Wananchi kwamba Vijana wa Kampuni ya showtime wanauwezo mkubwa wa kuitangza Zanzibar kiusanii .

Aidha alisema kuwa Zanzibar ni Kisiwa cha Utalii hivyo watahakikisha kupitia Kampuni yao kwa kutumia vipaji walivyonavyo kuhakikisha wanaitangaza Zanzibar kupitia Matamasha mbali mbali ili  kuimarisha Utalii utaoengeza uchumi wa Nchi.

Hata hivyo alisema kuwa hawatoweza kuacha Utamaduni wao hivyo katika ufunguzi wa Kampuni hiyo kutakuwepo burudani mbali mbali za Utamaduni wa asili. 

Hata hivyo Ibrahim Mitawi alisema ili Sanaa ifike mbali zaidi kuutangaza Utalii  ni muhimu kuwepo na  mashirikiano baina ya Makampuni mbali mbali pamoja na Serikali.
 Msemaji wa  Showtime Intertinment Musilim Nassor akizungumza na Waandishi wa Habari hawapo pichani juu ya Uzinduzi wa Showtime itakayozinduliwa tarehe 27/07 2018 katika Ukumbi wa Ngome Kongwe Mjini Zanzibar.
 Mkurugenzi wa Showtime Intertinment Ibrahim Mitawi akitoa ufafanizi  wa masuali aliyokua akiulizwa na Waandishi juu ya Uzinduzi wa Showtime  hiyo itakayozinduliwa tarehe 27/07 2018 katika Ukumbi wa Ngome Kongwe Mjini Zanzibar (kushoto) ni Saleh Nassor Abdallah ( Dj CARTEL) na Msaidizi Itifaki Issam Ramadhan Mussa.
  Mwandishi wa Habari wa Gaziti la Majira Mwajuma Juma akiuliza maswali katika mkutano kuhusiana na Show hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 27/07/2018  katika Ukumbi wa Ngome Kongwe Mjini Zanzibar.
Msaidizi Itifaki Issam Ramadhan Mussa akijibu baadhi ya maswali yaliokua yakiulizwa na Waandishi kuhusiana na Show hiyo (kulia) ni Dj CARTEL, Mkurugenzi wa Showtime Intertinment Ibrahim Mitawi na Msemaji wa Taasisi hiyo Musilim Nassor. Picha na Abdalla Omar  Maelezo – Zanzibar.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images