Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KITUO CHA AFYA CHA NANYALA WILAYANI MBOZI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amefungua kituo cha Afya cha Nanyala kilichopo kata ya Nanyala wilayani Mbozi kitakachotoa huduma kwa wakazi zaidi ya elfu kumi ikiwa siku ya pili ya ziara yake ya siku 5 katika mkoa wa Songwe. Pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mh.Chiku Galawa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Muonekano wa jengo la  kituo cha Afya cha Nanyala kilichopo kata ya Nanyala wilayani Mbozi kitakachotoa huduma kwa wakazi zaidi ya elfu kumi
 Jiwe la Msingi lililowekwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (hayupo pichani) alipokuwa akiwahutubia mapema leo mara baada ya kufungua kituo cha Afya cha Nanyala kilichopo kata ya Nanyala wilayani Mbozi kitakachotoa huduma kwa wakazi zaidi ya elfu kumi ikiwa siku ya pili ya ziara yake ya siku 5 katika mkoa wa Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wananchi  mapema leo mara baada ya kufungua kituo cha Afya cha Nanyala kilichopo kata ya Nanyala wilayani Mbozi kitakachotoa huduma kwa wakazi zaidi ya elfu kumi ikiwa siku ya pili ya ziara yake ya siku 5 katika mkoa wa Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


MAZUNGUMZO RASMI YA KISERIKALI KATI MAWAZIRI WAKUU WA TANZANIA NA JAMHURI YA KOREA

$
0
0

*Wote wawili washuhudia uwekaji saini 
mkataba wa kuondoa hitaji la viza

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya mazungumzo rasmi ya kiserikali na mgeni wake, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-yon ambaye yuko hapa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Viongozi hao wawili, kwa pamoja, leo mchana (Jumapili, Julai 22, 2018) wameshuhudia uwekaji saini mkataba wa kuondoa hitaji la viza kwa watu wenye hati za kusafiria za kidiplomasia na za kikazi (diplomatic and service passports).

Uwekaji saini huo ulifanywa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga na Makamu wa Kwanza Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea, Bw. Lim Sung-nam kwenye ukumbi wa Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya uwekaji saini, Waziri Mkuu amesema kwenye mazungumzo yao wamejadiliana mambo mengi ambayo yamelenga kukuza uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili.

“Tumejadili namna ya kuimarisha mahusiano yetu kidiplomasia; kuimarisha ushirikiano katika sekta ya uchumi na maendeleo; ushirikiano katika elimu, sayansi na TEHAMA ushirikiano katika sekta ya utamaduni na utalii,” amesema.

“Pia tumeongelea fursa ya mradi mkubwa wa reli, ujenzi wa daraja la Salender, mradi wa hospitali ya Mloganzila; mradi wa NIDA ambao tumepata mkopo wa masharti nafuu kwa ajili ya kuendelea kutoa vitambulisho vya uraia; ujenzi wa daraja la Kigongo - Busisi lenye urefu wa mita 3,200; ujenzi wa barabara ya Kazirambwa – Chaya yenye urefu wa km. 42 na uimarishaji wa sekta ya afya kwa kujenga hospitali tano za rufaa kwenye kanda zetu,” amesema.

Waziri Mkuu amesema amewaalika makampuni ya kutoka Jamhuri ya Korea yaje kuwekeza nchini ili kuiwezesha Tanzania kufikia azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025. “Pia wafanyabiashara aliokuja nao, kesho watashiriki kongamano la kibiashara baina ya Korea na Tanzania ili waweze kubadilishana uzoefu na wenzao wa Tanzania.”

“Tumewaomba pia watangaze vivutio vya utalii vya hapa nchini huko kwao na Balozi wetu wa Tanzania huko Korea atasimamia utangazaji wa vivutio vya hapa nchini kwetu. Sisi pia tumewapongeza kwa uamuzi wa Korea Kusini kukaa pamoja na Korea Kaskazini na kuimarisha amani kwa nchi zao,” amesema.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Isack Kamwele; Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani; Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zanzibar, Balozi Amina Salum Ally; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Zanzibar, Bw. Issa Gavu na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Eng. Stella Manyanya. Wengine ni Makatibu Wakuu wa wizara mbalimbali na wakuu wa taasisi.  

Waziri Mkuu Lee Nak-yon anatembelea Tanzania ikiwa ni hatua ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili. Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa ngazi ya juu wa nchi hiyo kufanya ziara ya kiserikali tangu nchi hizo zianzishe mahusiano ya kidiplomasia mwaka 1992.

Jamhuri ya Korea ni mshirika mkubwa wa maendeleo wa Tanzania ambapo kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo (KOICA) na Mfuko wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo (EDCF) yamekuwa yakitoa misaada na mikopo ya masharti nafuu ikiwemo misaada ya fedha katika bajeti, ujenzi wa miundombinu ya jamii, mafunzo ya muda mfupi na mrefu, wataalamu wa kujitolea, vifaa na mashine kwa ajili ya sekta mbalimbali ikiwemo ya afya.

Baadhi ya miradi ambayo imegharamiwa na Serikali ya Korea ni pamoja na Mradi wa kuboresha Huduma ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Chanika, Mradi wa Mfumo wa Usajili wa Meli na Mabaharia kwa Njia ya Mtandao Zanzibar, Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Taifa ya Taaluma na Tiba (MUHAS) kampasi ya Mloganzila na ujenzi wa daraja katika mto Malagarasi.

Vile vile, Korea ni mshirika mkubwa katika kusaidia maendeleo ya Bara la Afrika ambapo hivi karibuni katika mkutano wa Sita wa Jukwaa la Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na Afrika (KOAFEC VI) uliofanyika Mei 2018, Busan, Korea ambapo Serikali ya Korea ilitangaza msaada wa dola za Marekani bilioni 5 kwa ajili ya Bara la Afrika kwa kipindi cha 2018-2020. Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazonufaika na msaada huo.
  
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JULAI 22, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimina na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea ,  Lee Nak -Yon wakati mgeni huyo alipowasili kwenye ukumbi wa Kikwete, Ikulu jijini Dar es salaam kwa mazungumzo rasmi ya kiserikali, Julai 22, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mgeni wake, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea,  Lee Nak - Yon  (kushoto ) wakiwa katika mazungumzo rasmi ya kiserikali kwenye ukumbi wa Kikwete, Ikulu jijini Dar es salaam Julai 22, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak - Yon (kushoto) wakishuhudia wakati Waziri wa Mambo ya Nje, Dkt. Augustine Mahiga  na  Makamu wa Kwanza wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Korea, Lim Sung - Nam  (kushoto) walipotia saini Mkataba  wa kuondoa Hitaji la Viza za Kusafiria kwa Watu Wenye Hati za Kusafiria za Kidiplomasia na Kikazi, kwenye ukumbi wa Kikwete, Ikulu jijini Dar es salaam Julai 22, 2018
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumnza na waandishi wa habari wakati alipotoa taarifa kuhusu mazungumzo rasmi ya kiserikali kati yake na Waziri Mkuu na Korea, Lee Nak- Yon (kushoto) kwenye ukumbi wa Kikwete, Ikulu jijini Dar es salaam Julai 22, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri  Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak - Yon baada ya mazungumzo rasmi ya kiserikali kati yao yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Kikwete, Ikulu jijini Dar es slaam, Julai 22, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DKT MWIGULU NCHEMBA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA JIMBONI KWAKE,ACHANGIA BATI 200

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi mkoa wa Singida Dkt Mwigulu Nchemba akikagua ujenzi wa kituo cha Afya cha kata ya kinampanda kinachojengwa kwa nguvu za wananchi wakishirikiana na Mbunge pamoja na serikali kuu, kituo hicho ni cha kwanza tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika. 
Mbunge wa jimbo la Iramba magharibi mkoa wa Singida Dkt Mwigulu Nchemba akikabidhi Bati 200 kwa wananchi kwa ajili ya kuezekea majengo ya kituo cha afya cha kinampanda .
Mbunge wa jimbo la Iramba magharibi mkoa wa Singida Dkt Mwigulu Nchemba akiwahutubia Wananchi wa kata ya Kinampanda kutoa taarifa ya ulipofikia ujenzi wa kituo cha afya ambacho kilikua ni moja ya ahadi zake akiomba ridhaa ya kuongoza jimbo hilo.

MSHINDI MBIO ZA BAISKELI TAMASHA LA MAJIMAJI SELEBUKA HUYU HAPA

$
0
0

 Mbunge wa Songea Mjini, Dk. Damas Ndumbaro akimkabidhi zawadi ya nishani ya baiskeli mshindi wa kwanza katika mbio za baiskeli 100KM za Tamasha la Majimaji Selebuka, Masunda Duba wa Simiyu. Pia alitwaa zawadi ikiwamo ya washindi watatu wa kwanza kupata fursa ya kutafutiwa mashindano nje ya nchi na kugharimiwa kila kitu na Taasisi ya SOMI. 
 Bingwa wa mbio za baiskeli 100KM za tamasha la kila mwaka la Majimaji Selebuka, Masunda Duba akishangalia baada ya kuhitimisha mbio hizo ambazo zilikuwa ni kutoka Wilaya ya Mbinga hadi Manispaa ya Songea.
 . Bingwa wa mbio za baiskeli 100KM, Masunda Duba, akichuana vikali na Boniphace Masuda aliyeshika nafasi ya pili katika shindano lililoratibiwa na Taasisi ya SOMI kupitia Tamasha la Majimaji Selebuka.

MZEE MKAPA, DKT. BILAL, JAJI RAMADHAN WATOA POLE KWA RAIS MSTAAFU DKT KIKWETE KWA KUFIWA NA BABA MKWE WAKE, MAREHEMU MZEE RASHID MKWACHU

$
0
0
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamini Mkapa alipowasili nyumbani kwake Msasani, jijini Dar es salaam leo kuhani msiba wa Baba Mzazi wa Mama Salma Kikwete, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu.
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamini Mkapa akisalimiana na Mke wa Mh. Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete wakati alipofika kuhani Msiba wa Baba yake, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu uliotokea hivi karibuni. Mh. Mkapa aliambatana na Mkewe Mama Anna Mkapa. Kulia ni Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwaeleza jambo Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamini Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa, wakati walipofika nyumbani kwake, Msasani jijini Dar es salaam leo kuhani msiba wa Baba Mzazi wa Mama Salma Kikwete, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamu Wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohamed Gharib Bilal alipowasili nyumbani kwake Msasani, jijini Dar es salaam leo kuhani msiba wa Baba Mzazi wa Mama Salma Kikwete, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu.
 Makamu Wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akimpa pole Mama Salma Kikwete, kwa kufiwa na Baba yake Marehemu Mzee Rashid Mkwachu. Dkt. Bilal aliambatana na Wake zake, Mama Zakhia na Mama Asha Bilal.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimueleza jambo Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal na Wake zake, Mama Zakhia na Mama Asha Bilal, walipofika nyumbani kwake, Msasani jijini Dar es salaam leo kuhani msiba wa Baba Mzazi wa Mama Salma Kikwete, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Kangi Lugola akitoa pole ya msiba kwa Mama Salma Kikwete, aliyefiwa na Baba yake Marehemu Mzee Rashid Mkwachu. 

Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha nyumbani kwake, Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhan wakati alipofika kuhani msiba wa  Baba Mzazi wa Mama Salma Kikwete, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kushoto) akimkabidhi Mke wa Rais Mstaafu, Mama Salma Kikwete Rambirambi iliyotolewa na Wabunge kufuatia kufiwa na Baba yake, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu. kushoto ni Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia. Naibu Waziri Mgalu aliambatana na Mh. Hawa Ghasia.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

MAGAZETI YA LEO JULAI 23, 2018

SAKATA LA MESUT OZIL KUJIONDOA TIMU YA TAIFA YA UJERUMANI

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Nyota wa Kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Arsenal ya Uingereza, Mesut Ozil  (pichani) ametangaza kustaafu kucheza timu ya taifa ya nchi hiyo kwa kile alichodai ni Ubaguzi na kutoheshimiwa na Shirikisho la Soka nchini humo (DFB).
Ozil na mwenzake anayekipiga na Manchester City, Ilkay Gundogan wote wana asili ya Uturuki na walionekana katika picha ya pamoja wakiwa na Rais wa hiyo, Recep Tayyip Erdogan. Picha hiyo imeleta mzozo kwa kuhusishwa na masuala ya Kisiasa. Hata hivyo, Ozil kupitia Ukurasa wake wa Twitter ametoa taarifa iliyokuwa ikikanusha shutuma hizo.
Katika taarifa hiyo, Ozil amevishutumu Vyombo vya Habari nchini Ujerumani haswa Magazeti kwa kuandika vibaya dhidi yake kuhusu picha ya pamoja na Rais Erdogan pamoja na kuwashutumu Wadhamini wa Shirikisho la Soka nchini humo. Moja ya sehemu ya taarifa hiyo Ozil ameelezea kuwa Mama yake amefundisha asisahau alipotoka, na kudai angewakosea heshima Waturuki endapo angekataa kupiga picha ya pamoja na Rais wao'.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa baadhi ya Magazeti nchini Ujerumani yamekuwa yakiandika kuhusu picha hiyo na Rais wa Uturuki na kuhusisha  na masuala yake (Erdogan) ya Kisiasa nchini humo.
Ozil katika miaka tisa akiwa na timu ya taifa ya Ujerumani amecheza michezo 92 katika kikosi cha timu ya taifa nakufunga mabao 23. Pia alikuwa moja wapo ya Wachezaji walioipeleka Ujerumani Kombe la Dunia 2014 pia kuivusha hadi Nusu Fainali ya Kombe la Ulaya 2012 na 2016, alikuwa na Kikosi hicho kwenye Michuano ya Kombe la Dunia 2010 na 2018.

PROGRAMU YA 'UNI LIFE CAMPUS' YAFANIKISHA NDOTO ZA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU TANZANIA

$
0
0

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania waaswa kuzilinda na kuzitunza fursa wanazozipata ili ziweze kuwaletea maendeleo endelevu katika maisha yao. Hayo yamesemwa na Mwanzilishi wa programu ya 'Uni Life Campus' Mbunge wa Viti Maalum Mheshimiwa Esther Mmasi ambaye anawakilisha Vyuo Vikuu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita katika semina elekezi ya kuwaasa wanafunzi waliopata nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo (field) katika tasisi mbali mbali za serikali na mashirika binafsi.

"Nawaomba sana wanavyuo wenzangu huko mnapokwenda mkawe mabalozi wema, mzingatie kuwa watiifu na muwe na moyo wa kujifunza huku mkifanya kazi kwa bidii hapo mnaweza kupata maarifa mapya," amesema Mhe. Esther Mmasi. Amesema kuwa tatizo la vijana wengi kwa sasa wamekuwa ni wakaidi na wanaoendeleza uvivu huku simu ikiwa ni kikwazo kikubwa pindi wanapofanya kazi. 

"Mkienda kwenye mafunzo kwa vitendo (field) mzingatie kufanya kazi na si kushinda unachezea simu maana wengi wenu kutwa kucha ni kuchat tu unasahau hata kilichowapeleka katika ofisi za watu, nangoja ripoti njema zitakazowajenga mbeleni" Amesema. 

Aidha amesema kuwa mpka sasa Programu ya 'Uni Life Campus' imewatafutia nafasi za mafunzo kwa vitendo (field) wanafunzi wapatao 100 waliokuwa wameomba kutoka vyuo mbali mbali Tanzania na watakwenda Shirika la Taifa la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Benki ya NMB na Benki ya Posta Tanzania (TPB). 

"Tunamshukuru Mungu tumeweza kuwatolea changamoto wanafunzi hasa waliokuwa wakiomba mafunzo kwa vitendo, tulipotangaza mwaka jana mwishoni zaidi ya vijana 1,900 waliweza kuomba ila tumeweza wapatia nafasi 100 ambao tulizipata licha ya kuendelea kuongea na taasisi mbali mbali za serikali ambazo zimetuahidi kutupatia nafasi zaidi ya 600," amesema. 
  Mwanzilishi wa programu ya 'Uni Life Campus' Mbunge wa Viti Maalum Mheshimiwa Esther Mmasi ambaye anawakilisha Vyuo Vikuu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na wanafunzi wa vyuo mbali mbali vya Tanzania wakati wa semina elekezi juu ya kuzitunza fursa wanazozipata katika maisha yao ikiwa ni pamoja na kupatiwa nafasi za kufanya mafunzo kwa vitendo (field) katika taasisi mbali mbali za serikali na mashirika binafsi mwishoni mwa wiki iliyopita katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam. Picha zote na Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.   Mkurugenzi DM Saikolojia Limited Bw. Dosi Said Dosi akitoa neno kwa wanafunzi wanaotarajia kuanza mafunzo yao kwa vitendo (field) wakati wa semina elekezi juu ya kuzitunza fursa wanazozipata katika maisha yao katika taasisi mbali mbali za serikali na mashirika binafsi mwishoni mwa wiki iliyopita katika Chuo cha CBE jijini Dar es Salaam.. 
Mmoja ya maofisa katika Programu ya 'Uni Life Campus' Gladness akitoa maelezo machache kwa wanafunzi.



SPRITE BBALL KINGS YAFIKIA PATAMU, TIMU NNE ZATINGA NUSU FAINALI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
ROBO fainali ya Michuano ya Sprite BBall Kings imefanyika mwishoni mwa wiki hii na timu nne kufanikiwa kuvuka kwenda hatua inayofuata ya nusu fainali.

Mechi hizo zilizochezwa ndani wa Uwanja wa Ndani wa Taifa zilikuwa za ushindani mkubwa sana huku Bingwa mtetezi Mchenga BBall Stars akifanikiwa kushinda na kusonga hatua inayofuata.

Katoka mchezo wa kwanza uliokwakutanisha Water Institute dhidi ya Flying Dribblers uliweza kumalizika kwa Flyinh Dribllers kuibuka na  ushindi wa vikapu 100 dhidi ya 64

Mchezo wa pili uliwakutanisha Team Kiza akichuana na DMI, na katika mchezo huo DMI walikubali kichapo cha vikapu 82 kwa 47 vya DIM.

Mchenga Bball Stars alichuana na St Joseph katika mchezo wa tatu, mechi iliyokuwa na ushindani mkubwa na mpaka filimbi ya mwisho inapulizwa Mchenga akafanikiwa kuvuka kwa vikapu 84 dhidi ya vikapu 67 vya St Joseph.

Mechi ya mwisho ilikua ni Temeke Heroes dhidi ya Portland iliyohitimisha idadi ya timu nne za kuingia nusu fainali, na Portland wakihitimisha mechi hiyo kwa kuibuka mshindi kwa vikapu 83 dhidi ya vikapu 70 vya Temeke Heroes.
 Nahodha wa Timu ya Mchenga BBall Stars Mohamed Yusuph akijaribu kuwatoka wachezaji wa St Joseph wakati wa mechi ya robo fainali ya Michuano ya Sprite BBall Kings uliomalizika kwa Mchenga kuibuka na ushindi wa Vikapu 84 kwa 47 vya St Joseph.

 Vuta nikuvute wakati wa mechi ya robo fainali ya Michuano ya Sprite BBall Kings uliomalizika kwa Mchenga kuibuka na ushindi wa Vikapu 84 kwa 47 vya St Joseph.
Mashabiki waliojitokeza kuangalia michuano ya Sprite BBall Kings katika Uwanja wa Ndani wa Taifa.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) Phares Magessa (kulia) akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa TBF Mike Mwita wakishuhudia robo fainali ya Michuano ya Sprite BBall Kings.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BREAKING NEWS: MAKAMU MWENYEKITI WA YANGA CLEMENT SANGA AJIUZULU NAFASI YAKE

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement  Sanga amejiuzulu nafasi yake katika klabu hiyo kuanzia leo hii.

Amesisitiza kuendelea kuwa mwanachama na kuisaidia klabu ya Yanga katika kila hali.

Kwa upande wa hela zinazozungumziwa za Milioni 240 za kutoka CAF, Sanga amesema Yanga imekuwa na changamoto nyingi sana katika upande wa fedha na wamekuwa wana madeni makubwa ambayo wanakatwa katika mapato ya mlangoni ikiwemo Deni la Ardhi na madeni mengine pia.

Habari kamili inakuijia hivi punde

PRECISION AIR YAANZISHA MPANGO WA MAFUNZO KAZINI KUTATUA UHABA WA WAHANDISI SEKTA YA ANGA TANZANIA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Shirika la Ndege la Precision Air limezindua mpango maalumu  wa mafunzo kazini kwa ajili ya vijana wa Kitanzania wenye ndoto za kua wahandisi wa Ndege ili kukabiliana na uhaba wa wahandisi katika sekta ya anga nchini katika siku za usoni.

Shirika hilo limeanzisha mpango huo katika jitihada za kuendeleza rasilimali watu inayohitajika katika katika kitengo chake cha ufundi kupitia mafunzo maalumu kwa wanafunzi wa ufundi  pamoja na mpango wa mafunzo kazini na tayari limeajiri mafundi 22 kupitia mpango wa mafunzo kazini katika kitengo chake cha Uhandisi na ufundi na watakua wakifanya kazi huku wakiendelea na mafunzo ya vitendo. 

Akizungumzia mpango huo, Mkurugenzi Mkuu wa Precision Air, Sauda Rajab amesema, upatikanaji wa rasilimali watu katika sekta ya anga umekua changamoto kubwa nchini. Ameongeza kuwa Precision Air kama shirika lenye uzoefu haliwezi kubaki kulalamika na ndo sababu shirika limechukua hatua ya kuanzisha mpango huo ili kusaidia katika kutatua tatizo. 

“Tunajivunia mchango wetu katika kuendeleza rasilimali watu wenye ujuzi unaohitajika katika sekta ya anga Tanzania.Kupitia mpango wetu huu wa mafunzo kazini nimatumaini yetu tutaweza kutengeneza wahandisi wengi wa ndege ili kuweza kukidhi mahitaji ya soko na mahitaji yetu kama shirika,"amesema 

Kwa upande mwingine Sauda, ameeleza kuwa inachukua takribani miaka nane (8) kumuandaa Muhandisi kamili  mwenye leseni, huku pia ikigharimu fedha nyingi katika kusomesha wahandisi, hivyo anatarajia wadau wengine kwenye sekta ya anga watafanya jitihada kama za Precision Air, badala ya kutegemea wataalamu kutoka nje pekee, ili kuimarisha sekta na kutengeneza ajira nyingi zaidi kwa vijana wa Kitanzania.

Katika kutekeleza hilo Shirika la ndege la Precision Air pia lilisaini mkataba na Chuo cha Usafirashaji (NIT) mnamo mwaka 2017, mkataba unaowawezesha wanafunzi kutoka chuo hiko kupata nafasi za mafunzo ya vitendo kupitia shirika hilo na mpaka sasa wameshatoa mafunzo kwa wanafunzi 33.

WANANCHI WA VIJIJI VITATU WILAYANI ITILIMA WACHANGIA MILLIONI 24 KATIKA UJENZI WA ZAHANATI NA KITUO CHA AFYA

$
0
0
Na WAMJW Simiyu
Wananchi wa Kijiji cha Itindilo Wilaya ya Itimilo, Nangale na Migato vilivyopo Wilaya ya Itimila mkoani Simiyu wameungana  kuunga mkono  jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuleta maendeleo  kwa kuchangia nguvu kazi zenye thamani ya Shilling Millioni 24 kujenga Zahanati na kituo cha Afya vijiji hapo.

Hayo yamebainika wakati Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile wakati akikagua huduma za Afya na Maendeleo ya Jamii katika mkoa wa Simiyu.

Taarifa ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Ikindilo  imesema kuwa mradi huo unaogharimu jumla ya shilling 541,000,000 Shillingi 250,000,000 kutoka Serikalini, Shillingi Millioni 275,000,000 kutoka wadau wa Maendeleo UNFPA na Shillingi Millioni 16 kutokana na nguvu za wananchi.

Pia mradi ujenzi wa wodi ya Mama na Mtoto katika Zahanati ya Kijiji cha Nangale unaogharimu jumla ya shilling 36,321,000 Shillingi 30,000,000 kutoka Serikalini kwa kushirikiana na UNFPA, na Shillingi Millioni 6,321,000 kutokana na nguvu za wananchi.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiweka  jiwe la msingi la jengo la wodi ya mama na mtoto ya Zahanati ya Kijiji hicho kilichopo wilaya ya Itimila mkoa wa Simiyu.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wanakijiji wa Migato na kuwahimiza kujitola katika kufanya shughli za kujiletea maendeleo wakati mara baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la wodi ya mama na mtoto ya Zahanati ya Kijiji hicho kilichopo wilaya ya Itimila mkoa wa Simiyu.
  Wananchi wa kijiji cha magito wakisikiliza hotuba ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile( hayupo pichani) mara baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la wodi ya mama na mtoto ya Zahanati ya Kijiji hicho kilichopo wilaya ya Itimila mkoa wa Simiyu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na mtoto mkaziwa Kijiji cha Migato mara baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la wodi ya mama na mtoto ya Zahanati ya Kijiji hicho kilichopo wilaya ya Itimila mkoa wa Simiyu. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Tanzania inayo fursa kubwa kunufaika na utalii wa ndani na Afrika

$
0
0

Na Jumia Travel Tanzania

Msimu wa majira ya joto au ‘Summer Season’ kama unavyojulikana kwa nchi za Ulaya na Marekani huwa ni kipindi cha mapumziko miongoni mwa watu wengi. Mapumziko haya si hufanywa tu na watu wa kawaida kutokea nchi hizo bali pia watu mashuhuri kama vile wacheza soka, wanamuziki, wafanyabiashara na wanasiasa.

Sababu kubwa zinazopelekea watu wa mataifa hayo kuchukua muda wa likizo ni kutokana na kipindi hiki kuwa na hali ya hewa nzuri. Kipindi kirefu cha mwaka kwenye maeneo yao hutawaliwa na baridi kali pamoja na barafu katika maeneo mengi.

Matokeo ya hali hii ni nchi tofauti zenye vivutio vya kitalii kunufaika kwa kiasi kikubwa kwani hupokea maelfu ya watalii. Miongoni mwa sehemu zinazotembelewa kwa kiasi kikubwa ni pamoja na Afrika, Tanzania ikiwemo.
Kwa mfano hivi karibuni tumeshuhudia watu mashuhuri kama vile Rais aliyepita wa Marekani, Barack Obama na familia yake wakitembelea Hifadhi ya Mbuga ya Serengeti kwa muda wa takribani wiki nzima. Naye, Rais wa sasa wa nchi ya Uswizi, Mh. Alain Berset aliyeingia Tanzania na kutarajiwa kutumia siku 15 kutalii vivutio kadhaa kama vile Serengeti, Tarangire, Manyara, Ngorongoro na Zanzibar. 

Pia tumeshuhudia mchezaji wa timu ya Taifa ya Hispania na klabu ya Atletico Madrid, Koke akiwa amekuja kupumzika na familia yake katika mbuga ya Serengeti mara baada ya timu yake kuondolewa katika michuano ya Kombe la Dunia.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zinazohusu masuala ya utalii, visiwa vya Zanzibar, Mlima Kilimanjaro, mbuga ya Serengeti na hifadhi ya bonde la Ngorongoro ni miongoni mwa vivutio vilivyopo kwenye orodha ya watalii wengi duniani.
Akizungumzia juu ya sababu zinazopelekea kukua kwa utalii wa ndani ya nchi pamoja na bara la Afrika, Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Travel Tanzania, Bw. Kijanga Geofrey amebainisha kuwa kujitangaza ndani na kimataifa, gharama nafuu za malazi na usafiri pamoja na uboreshwaji wa miundo mbinu ya usafiri ni vichocheo vikubwa.

“Tumeshuhudia taasisi zilizopewa mamlaka na serikali zikishiriki maonyesho ya kimataifa ya utalii ndani na nje ya nchi. Hii hutoa fursa kwa watalii na wadau wa sekta kujua vivutio vilivyopo na taratibu za kuvitembelea. Lakini maboresho katika sekta za usafiri hususani wa anga ambao ndio hutumiwa na asilimia kubwa ya watalii duniani umeleta chachu nchini,” alisema Bw. Geofrey.

Tanzania imekuwa ni kitovu cha utalii wa ndani ya Afrika ambapo hupokea watalii wengi kutokea nchi za Afrika ya Kusini, Nigeria na Kenya. Nchi hizi ambazo zina idadi kubwa ya watu barani Afrika na uchumi mzuri ni fursa kubwa ya kimasoko endapo zitatumiwa vizuri kutangaza vivutio vilivyopo.

NEWZ ALERT: WATANO WAHUKUMIWA KUNYONGWA BAADA YA MAHAKAMA KUWATIA HATIANI KWA MAUAJI YA BILIONEA MSUYA.

$
0
0
Na Dixon Busagaga,Moshi .

MAHAKAMA kuu ya Tanzania ,Kanda ya Moshi imewahuku Washtakiwa watano kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mfanyabiashara wa Madini ya Tanzanite ,Erasto Msuya huku ikimwachia huru mshtakiwa mmoja baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kumtia hatiani.

WAZIRI MKUU AFUNGUA KONGAMANO LA PILI LA BIASHARA LA KOREA NA TANZANIA

$
0
0
*Aalika wawekezaji kwenye viwanda vya kuongeza thamani ya mazao

*Ataka waangalie fursa za uwekezaji zilizopo kwenye sekta ya utalii
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaalika wafanyabiashara kutoka Korea Kusini waanzishe miradi ya uwekezaji kwenye sekta ya viwanda kwa kushirikiana na wawekezaji wa ndani.

Ametoa mwaliko huo leo (Jumatatu, Julai 23, 2018) akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-yon wakati akifungua Kongamano la Pili la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Korea lililofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kongamano la kwanza lilifanyika jijini Seoul, Februari 2018.

Amesema Serikali inahamasisha uwekezaji katika ujenzi wa viwanda vinavyotumia rasilimali za ndani ambavyo vitasaidia kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo, misitu, madini na bahari.

“Tunakaribisha uwekezaji wa viwanda katika maeneo ya uanzishaji wa viwanda vya kuzalisha bidhaa za walaji (consumer goods), pamoja na viwanda vya kuunganisha bidhaa mbalimbali, yaani (assembling plants) kama vile magari, simu na majokofu,” amesema.

Waziri Mkuu pia aliwaalika wafanyabiashara kutoka Korea waliohudhuria kongamano hilo waje kuwekeza kwenye sekta ya utalii ambako alisema kuna vivutio vya mbuga za wanyama kama Serengeti, Mlima Kilimanjaro, Olduvai Gorge na fukwe za bahari za Tanzania bara na Zanzibar.

“Tanzania ina kilometa 1,200 za fukwe kuanzia Tanga hadi Mtwara, ziko pia fukwe za Zanzibar, ziko fukwe kwenye maziwa yetu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa ambazo ni kivutio kingine cha utalii,” amesema.

Amesema ili kusimamia matumizi ya fukwe hizo, Serikali inakamilisha uundaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Fukwe kama ilivyo ile ya Ngorongoro ambayo alisema taratibu zikikamilika, itaanza kazi hivi karibuni.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Kongamano la Pili la  Biashara na Uwekezaji  Kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam Julai 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea,  Lee Nak- yon akihutubia  katika  Kongamano la Pili la Biashara  na Uwekezaji Kati ya Tanzania na  Korea kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Julai 23, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mgeni wake, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak - yon (kulia kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katika Kongamano la Pili la Biashara na Uwekezaji  Kati ya Tanzania na Korea kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam Julai 23, 2018. Kushoto kwa Waziri Mkuu Majaliwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

PASS NA TALIRI WAJIPANGA KUONGEZA BIDHAA YA NYAMA KATIKA JIJI LA DODOMA

$
0
0
Na Dixon Busagaga ,Dodoma.

TAASISI ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) imetumia fursa ya mkoa wa Dodoma kuwa makao makuu ya nchi kuingia mashirikiano na Taasisi Binafsi ya kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ( PASS) ya kuwekeza katika sekta ya Mifugo kwa kuwaandaa Wajasiliamali vijana.

Hatua hiyo inatajwa kuondoa moja ya changamoto ya upatikanaji wa bidhaa ya Nyama katika jiji la Dodoma ambalo kwa sasa idadi ya watu imeanza kuongezeka baada ya ofisi na taasisi mbaimbali za serikali na umma kuhamia Dodoma.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini makubalinao hayo iliyofanyika katika kituo cha Kongwa Dodoma ,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Binafsi ya kusaidia Sekta ya Kilimo Nchini(PASS) ,Nicomed Bohay alisema PASS kupitia kituo cha ubnifu wa Biasharaza Kilimo wameamua kuanzisha Vituo atamizi vya Mifugo katika kituo cha TALIRI Kongwa .

“Tumelenga kuanza na mifugo aina ya Mbuzi katika kituo hiki ,zipo sababu zilizotupelekea tuweze kuchagua eneo hili la Kongwa moja wapo ni uwep wa soko la karibu ,… PASS tutawekeza kwenye Miundo mbinu ya ufugaji wa Mbuzi ,pamoja na gharama za kuendesha mradi na malisho hadi mbuzi watakapo weza kuuzwa sokoni .”alisema Bohay .

Alisema kazi hiyo itafanyika kwa kutumia wajasiliamali Vijana wa Kitanzania na kwamba utaratibu wa kuwapata vijana wenye sifa utatangazwa baadae na watakao pata nafasi hiyo watapata nafasi ya kuunganishwa na taasisi za kifedha kwa ajili ya kupata mitaji.
Meneja wa Kituo cha Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Kongwa Dodoma,Wilfredy Munisi akizungumza wakati wa utamburisho wa wagei waliofika katika kituo hicho kwa ajili ya hafla fupi ya utiaji saini katika makubaliano kati ya TALIRI na Taasisi Binafsi ya kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ( PASS) ya kusaidia Wajasiliamali Vijana katika sekta ya Mifugo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed Bohay (katikati) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini kati ya Taasisi hiyo na TALIRI ya kusaidia Wajasiliamali vijana.Kulia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Ubunifu katika Kilimo Biashara ,Tamim Amijee na kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt Jonas Kizima.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed Bohay pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt Jonas Kizima wasaini Makubaliano kati ya Taasisi hizo mbili kusaidia Wajasiliamali vijana katika sekta ya Mifugo .Kulia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Ubunifu katika Kilimo Biashara ,Tamim Amijee na kushoto ni Meneja wa Kituo cha Utafiti wa Mifugo Kongwa,Wilfredy Munisi.

WANANCHI WA BUZA WAISHUKURU SERIKALI

$
0
0
Wananchi wa eneo la Buza katika Manispaa ya Temeke Jijini Dar es salaam wameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa ujenzi wa kituo cha afya Buza. 

Shukrani hizo wamezitoa leo wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo alipofanya ziara ya kushtukiza kituoni akiwa safarini kuelekea wilayani Kibaha kukagua miradi ya maendeleo. 

Alipofika kituoni hapo, Waziri huyo alikutana na umati wa kinamama na watoto wakisubiri kupata huduma katika Majengo yenye changamoto kubwa. Akizungumza na wananchi na wagonjwa waliokuwepo Kituoni hapo, Waziri Jafo amesema ameamua kufanya ziara hiyo ili kujionea hali halisi ya wananchi hao wanavyopata huduma ya afya. 

“Serikali inatambua changamoto zinazowakabili lakini nimeleta habari njema kwenu kuwa serikali itakiboresha kituo hicho ili kuondoa kero zinazowakabili,”amesema.Ameeleza kuwa kituo hicho kitajengewa jengo la upasuaji, wodi, maabara, jengo la wagonjwa wa nje ikijumuisha vyumba vya madaktari pamoja na jengo la X-Ray na mradi unaotarajiwa kugharimu zaidi ya sh.Bilioni moja.

Kufuatia hali hiyo, Wananchi hao wameishukuru serikali kwa kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili na kwamba uboreshaji huo utawawezesha waweze kupata huduma bora za afya.
Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo(hayupo pichani) alipofanya ziara ya kukagua utoaji wa huduma katika zahanati ya Buza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akizungumza na wananchi alipokuwa akikagua utoaji wa huduma katika zahanati ya Buza.
Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo(hayupo pichani).
Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo(hayupo pichani) alipofanya ziara ya kukagua utoaji wa huduma katika zahanati ya Buza.
Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo(hayupo pichani) alipofanya ziara ya kukagua utoaji wa huduma katika zahanati ya Buza.

MWENGE WA UHURU WAINGIA GAIRO NA KUZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA MILIONI MIASABA NA ZAIDII

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe akipokea Mwenge kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Morogoro Regina Chonjo mara ulipofika katika eneo la Makabidhiano mpakani kati ya Morogoro na Gairo ambapo Mwenge huo umekimbizwa kwa Kilometa 72 katika Wilaya ya Gairo.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018 Charles Kabeho akiweka udongo wenye Saruji pembeni ya tofali wakati aliposhiriki ujenzi wa shule mpya ya sekondari iliyopo Wilayani Gairo kama Sehemu ya Miradi iliyotembelewa na Mwenge.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018 Charles na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Sirile Mchembe wakipiga makofi mara bada ya kuweka jiwe la kwenye Majengo Matano Mapya yanayojengwa katika Hospitali ya Gairo.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018 Charles Kabeho akizungumza na Wakazi w Gairo mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Majengo Matano ya Hospitali ya Gairo.

WAZIRI MKUU KUANZA ZIARA YA SIKU NNE MKOANI KIGOMA

$
0
0
Na Editha Karlo,Kigoma

WAZIRI Mkuu Kasimu  Majaliwa anatarajia kuanza ziara yake ya kikazi siku nne Mkoani Kigoma ambapo atatembelea Wilaya nne.

Akizungumza na Waandishi wa habari jana (leo) ofisini kwake  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia mstaafu Emanuel  Maganga juu ya ziara hiyo, alisema  ugeni wa Waziri Mkuu ambae ataambatana na Waziri wa Kilimo, Naibu waziri wa madini na Naibu Waziri wa Tamisemi watawasili Mkoani humo Julai 28,2018 saa nne asubuhi. 

Alisema ziara hiyo  imelenga Kuamsha ari na Muendelezo wa zao la mchikichi Kwa wakulima na wawekezaji wa zao hilo Mkoani Kigoma kwakuwa  mafuta yanachukua nafasi ya pili katika Kuingiza fedha za kigeni  na hivyo wakulima wakiongeza tija ya uzalishaji zao hilo litawainua.

"Waziri Mkuu  atawasili Mkoani Kwetu siku ya Jumamosi,na atatembelea Wilaya nne za Kigoma , Kasulu , Uvinza na Buhigwe katika ziara hiyo  itahusisha Kikao cha ndani na Viongozi wa Mkoa kufanya mkutano wa wadau wa zao la michikichi na  atatembelea wakulima wa Michikichi na kahawa ambapo atasikiliza kero za wakulima na kubadilishana nao mawazo", alisema Brigedia Jenerali Maganga .

Alieleza kuwa serikali imejipanga kuinua zao la mchikichi na kuwataka wamiliki wote wa mashamba ya michikichi ambayo hayatumiki  wayarudishe iliwaweze kupatiwa watu ambao wanaweza kuwekeza na kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Aidha Maganga aliwaomba Wananchi kujitokeza kwa Wingi katika mikutano  atakayo ifanya na kutoa kero zao kwa kufuata utaratibu na kuwasilisha mambo yote ambayo yameshindwa kutatuliwa na Viongozi wa  wilaya na Mkoa  waziwasilishe kwa Waziri Mkuu ziweze kutatuliwa kwa wakati.

RAIS MAGUFULI NA WAZIRI MKUU WA KOREA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA WA UJENZI WA DARAJA JIPYA LA SELANDER IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Lee Nak-yeon mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Lee Nak-yeon wakati wakielekea katika ukumbi wa Jakaya Kikwete uliopo Ikulu kwa ajili ya kushuhudia tukio la Utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Daraja jipya la Selander litakalopita baharini kuanzia katika Hospitali ya Agha Khan mpaka Coco beach jijini Dar es Salaam.
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Lee Nak-yeon wakishuhudia tukio la utiaji saini Mkataba wa mradi wa ujenzi wa Ujenzi wa Daraja jipya la Selander litakalopita baharini kuanzia katika Hospitali ya Agha Khan hadi maeneo ya  Coco beach jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali  mara baada ya tukio la utiaji saini wa mradi wa ujenzi wa Ujenzi wa Daraja jipya la Selander litakalopita baharini kuanzia katika Hospitali ya Agha Khan mpaka Coco beach jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Lee Nak-yeon mara baada ya tukio la utiaji saini wa mradi wa ujenzi wa Ujenzi wa Daraja jipya la Selander litakalopita baharini kuanzia katika Hospitali ya Agha Khan mpaka Coco beach jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Lee Nak-yeon watatu kutoka (kushoto)pamoja na viongozi wengine wa Jamhuri ya Korea, Serikali ya Tanzania, Wabunge, Wakuu wa Wilaya pamoja na viongozi wa Mkoa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya Picha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Lee Nak-Yeon mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>