Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

WIZARA YA VIWANDA NA AFYA WAPOKEA WAWEKEZAJI WA SEKTA YA AFYA KUTOKA CHINA

$
0
0

Na Dotto Mwaibale.

WIZARA ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto wamepokea ujumbe wa wawekezaji wa sekta ya Afya kutoka kampuni ya Kimataifa ya Fosun kutoka China, ambao wamekuja kuwekeza kwenye viwanda vya uzalishaji dawa na vifaa tiba. 

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage (Mb.) ameeleza kuwa msimamo wa serikali ni kuhakikisha viwanda vinajengwa nchini ili kupunguza mzigo wa kununua dawa nje ya nchi kwa gharama kubwa,kupoteza ajira na pato la serikali.

Kwa upande wake,Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amesema asilimia 94 ya fedha za bajeti zinazotengwa kwa ajili ya kununua dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara hupelekwa nje ya nchi,na asilimia 6 tu ndio hununua kutoka viwanda vya ndani.Hii ni kwa sababu hakuna viwanda vinavyoweza kuzalisha dawa tunazozihitaji.

Wataalamu walioshiriki majadiliano na wawekezaji hao ni pamoja na Bohari ya Dawa(MSD),Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA),Kituo cha Uwekezaji nchini(TIC),Mamlaka ya Uwekezaji(EPZ) na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Rais wa Fosun Pharma,Willium Yifang WU amesema ili wawekeze wanahitaji ardhi ekari 10 kwa ajili ya kuanzisha kiwanda.Kwa mujibu wa Waziri Mwijage wawekezaji hao wakiwa tayari serikali itawapatia eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho cha dawa.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu Rugambwa (kulia), akiwa na viongozi wenzake kutoka Wizara ya ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dar es Salaam leo wakati wakiupokea ujumbe wa wawekezaji wa sekta ya Afya kutoka kampuni ya Kimataifa ya Fosun kutoka China, ambao wamekuja kuwekeza kwenye viwanda vya uzalishaji dawa na vifaa tiba. 
Mkutano na wawekezaji hao ukiendelea. 
Mkutano ukiendelea. Katikati kulia ni Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Charles Mwijage.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage (wa nne kutoka kushoto) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe huo kutoka China. Wa tatu kutoka kushoto ni Rais wa Fosun Pharma,Willium Yifang WU.

WAZIRI MKUU AONGOZA KUUAGA MWILI WA MBUNGE WA KOROGWE

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Korogwe Vijijini, Bw. Stephen Ngonyani maafufu Profesa Maji Marefu.

Bw. Ngonyani ambaye alifariki dunia Julai 2, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbi ameagwa leo (Jumatano, Julai 4, 2018) katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa pole kwa wanafamilia, wabunge, wananchi wa Korogwe pamoja na Watanzania kwa ujumla. Amewataka waendelee kumuombea marehemu.

“Natoa pole kwa wake wa marehemu, watoto na nawaomba tuendelee kuwa wavumilivu na watulivu katika kipindi hiki. Tulimpenda sana lakini Mwenyezi Mungu amempenda zaidi,”.Kwa upande wake, Katibu wa Bunge, Bw, Stephen Kagaigai akisoma wasifu wa marehemu amesema Bw. Ngonyani alizaliwa Mei 25, 1956 katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

Bw. Kagaigai amesema marehemu alianza kuugua Juni 17 mwaka huu na Juni 18 alilazwa katika Hopitali ya Mkoa wa Dodoma na Juni 20 alihamishiwa katika Hopitali ya Muhimbili.Shughuli hiyo ilihudhuriwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi. Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally, Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Wabunge na wanafamilia.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, JULAI 4, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini Kitabu cha Maombolezo ya kifo cha Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Hillary Ngonyani wakati alipowaongoza waombolezaji kuuga mwili wa mbunge huyo kwenye Viwanja vya Karimjee jijijini Dar es salam, Julai 4, 2018. 
Wapambe wa Bunge wakiwa wameubeba mwiili wa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stehen Hillary Ngonyani kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Hillary Ngonyani wakati alipowaongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa mbunge huyo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wanafamilia wakati alipowaongoza waombolezaji kuuaga mwili wa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Hillary Ngonyani kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Julai 4, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda (kushoto) wakati alipoongoza waombolezaji kuuga mwili wa mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Hillary Ngonyani kwenye viwanja vya Karaimjee jijini Dodoma Julai 4, 2018. Wapili kulia ni Spika wa Bunge Job, Ndugai na wapili kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.

KIFO CHA MTOTO PATRICK WA MUNALOVE CHAGUSA WENGI

WERRASON APATA MWALIKO KUTUA DAR KESHO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MWANAMUZIKI nguli kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Werrason Ngiama Makanda, anatarajia kuwasili nchini kesho kwa ajili ya kufanya maonyesho tofauti katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Dar es Salaam.

Mratibu wa ziara ya mwanamuziki huyo, Lengos VIP alisema kuwa mwanamuziki huyo nguli anawasili kesho saa 4 asabuhi kwa ajili ya maonesho hayo maalum yatakayofanyika sehemu tofauti nchini.

Alisema kuwa Mwanamuziki huyo ataanza onesho la kwanza mkoani Arusha siku ya Ijumaa ya Julai 6 na siku ya pili ya Julai 7, atakuwa mkoani Mwanza huku onyesho la mwisho litafanyika Mkoani Dar es Salaam.

Alisema mkoani Arusha Mwamuziki huyo atafanya onyesho kwenye ukumbi wa Mjengoni Club, wakati Mwanza atafanya mambo yake kwenye ukumbi wa Rock City na Mkoa wa Dar es Salaam Life Park uliopo Mwenge (zamani Word Cinema).

Werrason aliyeanzia katika bendi ya Wenge BCBG, miongoni mwa wanamuziki wa Congo wanaopata nafasi za kupata mwaliko wa kuja kutoa burudani hapa nchini, huku mratibu wa maonyesho hayo akiwataka mashabiki wajitokeze kupata burudani nzuri kutoka kwa nguli huyo.

Mwanamuziki huyo amekuwa akifanya ziara katika nchi mbali mbali ikiwemo Tanzania na kufanya vizuri kwa mashabiki kukubali ujio wake.

TFDA YAWAALIKA WENYE DHAMIRA YA KUANZISHA VIWANDA KUPATA USHAURI KATIKA MSIMU WA SABASABA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imewaalika watanzania wenye dhamira ya kuanzisha viwanda nchini kutembelea banda lao katika msimu huu wa sabasaba ili kupata msaada na miongozo kutoka katika mamlaka hiyo.

Akizungumza na Michuzi blog Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA Bi. Gaudensia Simwanza ameeleza kuwa katika msimu huu wa sabasaba wanasherekea mafanikio ya mamlaka hiyo kwa miaka 15, kuanzia 2003 hadi 2018 na katika kusherekea mafanikio hayo wanatoa elimu mbalimbali katika kuhakikisha uelewa kuhusiana na mamlaka hiyo unakua zaidi.

Bi. Simwanza ameeleza kuwa kama mamlaka wanatoa mwaliko kwa wanaotaka kuanzisha viwanda nchini katika kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli ya kuimarisha uchumi wa nchi kama mamlaka watatoa miongozo na elimu kwa wananchi wote watakaotaka kuanzisha viwanda nchini na kuwapatia miongozo ya kufikia malengo yao kwa viwanda watakavyoanzisha vikiwemo viwanda vya vyakula, dawa na vifaa tiba.

Akieleza kuhusiana na mafanikio ya mamlaka hiyo Simwanza ameeleza kuwa wananchi wamekuwa na uelewa kuhusiana na bidhaa ambazo zimepigwa marufuku na mamlaka hiyo na bado wanajitahidi kuhamasisha katika kutoa elimu zaidi.

Aidha ameeleza kuwa kama mamlaka wataendelea na shughuli ya kudhibiti bidhaa ambazo si faafu kwa matumizi ya binadamu na elimu kuhusiana na bidhaa wanazozisimamia itaendelea.

Simwanza ametoa wito kwa wananchi wote kutumia bidhaa zilizoainishwa na mamlaka hiyo na kutoa taarifa pindi waonapo biashara ambazo zimepigwa marufuku na mamlaka hiyo zikiuzwa na kutangazwa kwa kupiga bure 0800 110 084.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA Bi. Gaudensia Simwanza akifafanua jambo mbele ya mkemia mkuu wa Serikali Dr. Fidelice Mafumiko mara baada ya kutembelea banda lao la sabasaba.

Mkemia mkuu wa Serikali Dr. Fidelice Mafumiko (kushoto) akizungumza,Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA Bi. Gaudensia Simwanza alipotembelea katika maonesho ya kimata ya sabasaba jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka TFDA Bi. Gaudensia Simwanza akionyesha baadhi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku leo katika banda lao la sabasaba alipokuwa akifanya mahojiano na Michuzi blog

PROFESA KAMUZORA AWAASA WATUMISHI WA IDARA YA MPIGACHAPA MKUU WA SERIKALI KUZINGATIA UBORA NA UFANISI KATIKA UTENDAJI

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora amewataka watumishi wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali kuzingatia ubora na ufanisi katika uchapaji wa nyaraka za Serikali.

Wito huo ameutoa hii leo Julai 4, 2018 alipotembelea katika Idara hiyo ili kuangalia namna wanavyoendesha shughuli zao za kila siku.

Prof.Kamuzora alieleza umuhimu wa kuendelea kuwa na ubunifu katika utendaji kwa kuzingatia unyeti wa nyaraka za Serikali wanazochapisha na kuongeza wigo wa uzalishaji kwa kuwa na machapisho yenye ubora na viwango vya kuendana na soko ili kuongeza mapato ya nchi.

“Niwaombe watumishi wote mzingatie uzalishaji wenye tija kwa kuchapisha nyaraka zenye ubora na ufanisi utakao saidia kuongeza mapato ya nchi hivyo ni vyema kuwa na ubunifu wa hali ya juu,”alisema Prof.Kamuzora

Pamoja na maagizo hayo aliwasisitiza kuzingatia uzalendo wa nchi yao kwa kuwa waadilifu katika kuitumikia kwa uaminifu bila kutoa siri za Serikali.

 Kaimu Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.John Kaswalala akimuonesha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora moja ya mtambo unaotumika kuchapisha nyaraka za Serikali unaoitwa Original Heidelberg alipotembelea katika Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Julai4, 2018 Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora akipata ufafanuzi kutoka kwa Kaimu Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.John Kaswalala juu ya moja ya kitabu kilichochapishwa na Idara hiyo, alipotembelea Kuona namna idara inavyotekeleza majukumu yake.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora akiuliza jambo kwa Kaimu Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.John Kaswalala kuhusu mitambo ya Kidijitali inayotumika kuchapa nyaraka za Serikali, wa kwanza kushoto ni Mpigachapa Msaidizi Bw.Cornel Chikokoto.
 Kaimu Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.John Kaswalala akikabidhi vitabu vya maandiko yanayoeleza juu ya Idara hiyo kuwa Wakala kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora alipotembelea Idara ya Mpigachapa tarehe 4 Julai, 2018 Jijini Dodoma.
 Mhudumu Mkuu wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw Jackson Ainea akieleza jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora (hayupo pichani) wakati alipotembelea katika Ofisi hizo Jijini Dodoam Julai 4, 2018.
 Afisa Tawala Mwandamizi wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Severin Kapinga akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora (hayupo Pichani) wakati wa kikao chake na Watumishi wa Idara hiyo alipowatembelea Julai 4, 2018.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora akizungumza jambo na Watumishi wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali (hawapo pichani) alipofanya ziara ofisini hapo kuona namna wanavyotekeleza majukumu yao.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali alipowatembelea Julai4, 2018.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAFANYABISAHARA KUTOKA NCHI SABA WATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM

$
0
0
WAFANYABIASHARA kutoka nchi saba zinazotumia Bandari ya Dar es Salaam wameipongeza Serikali kwa kuondoa changamoto walizokuwa wakilalamikia hivyo kuahidi kuendelea kupitia mizigo yao bandarini hapo.

Hayo yamezungumzwa leo jijini Dar es Salaam wakati wafanyabiashara hao walipotembelea Bandari hiyo kujionea namna shuguli mbalimbali zinavyoendeshwa ambapo walisema hatua ya serikali kuondoa vikwazo imewapa moyo wa kurudi kupitiasha vizigo bandarini hapo.

Rais wa Wafanyabiashara wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sumaili Edouard, alisema wamejipanga kurudi kwa kishindo kwa sababu dosari ambazo zilikuwa zimewakimbiza tayari zimeondolewa.

“Tunaipongeza serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Bandari (TPA) kwa kufanya juhudi kubwa ya kutuunganisha wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali ili kwa pamoja kuendeleze biashara hapa nchini.

‘Vikwazo vyote ambavyo tulikuwa tunavilalamikia kama mizani, kodi nakadhalika, sasa hivi vimeondolewa hivyo tumerudi kwa kishindo ili kuleta changamoto kwa sababu tumeona Tanzania imeamka kwa kiasi kikubwa,’ alisema Edouard.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akizungumza na wafanyabiashara kutoka nchi za Rwanda, Uganda, Burundi, Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zambia, Malawi na Comoro kuhusu ufanisi wa bandari hiyo pamoja na mikakati waliyoiweka ili kuhudumia nchi nyingi waliotembelea bandari ya Dar es Salaam leo.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Freddy Liundi akizungumza na wafanyabiashara kutoka nchi za Rwanda, Uganda, Burundi, Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zambia, Malawi na Comoro kwenye kituo cha kuhifadhi mizigo ya nchini Uganda leo kwenye bandari ya jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Masomo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Lydia Mallya akizungumza kuhusu TPA wanavyoshirikiana na nchi hizo ili mizogo yao inayoshushwa kupitia bandari hiyo inakuwa salama.
Afisa Mkuu wa Uendeshaji  kutoka TICTS Charlie Darazi akitoa ufafanuzi jinsi kampuni ya TICTS wanavyojishughulisha na kazi ya kushusha na kupakia mizigo katika bandari ya jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya wafanyabiashara kutoka nchi za Rwanda, Uganda, Burundi, Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zambia, Malawi na Comoro.
 Wafanyabiashara kutoka nchi za Rwanda, Uganda, Burundi, Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zambia, Malawi na Comoro wakitembelea bandari kujionea ufanisi wa wandari ya Dar es Salaam leo.
 Kaimu Mkurugenzi Masomo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Lydia Mallya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa ziara ya  Wafanyabiashara kutoka nchi za Rwanda, Uganda, Burundi, Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zambia, Malawi na Comoro waliotembelea bandari hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Wafanyabiashara wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sumaili Edouard akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wafanaya biashara na nchi hiyo walivyoona ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam.


WAZIRI MBALAWA KUTOWAFUMBIA MACHO WAFANAYAKAZI WAZEMBE

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Waziri wa maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amesema hatamfumbia macho mfanyakazi atakayezembea kazini kwa namna yoyote badala yake atamsafisha mara moja na kumtoa kabisa kwenye idara na kumuhamishia hata chuoni.

  
Profesa Mbarawa ameyasema hayo leo wakati alipotembelea ofisi za Dawasa zilizopo Mwanayamala jijini Dar es Salaam.


“Tunataka kufanya maendeleo, sitamtoa mtu kwa kumuonea nikikuona wewe umekaa pale na miradi yetu uliyochelewesha nitakuacha,  kwa nini nikuache, najua utafanya vile vile, na sitakuacha kwenye idara, nitakupeleka chuo cha maji, si kwa ajili ya kuwakomesha wanafunzi hapana, ila sitamuacha mtu aliyefanya ujinga aendelee”.


Amesema, uteuzi huu ni heshma kubwa kwani sasa anakwenda moja kwa moja kutatua matatizo ya watanzania ambao hasa ukienda vijijini ndio utajua kuwa kuna watanzania wana shida ya maji.


Amewaasa wafanyakazi hao kuwa na lengo la pamoja la kuhakikisha wanamsaidia Mtanzania yule masikini, kuweza kupata maji 
“Tunasema tumtue mama ndoo kichwani kwa kumpelekea maji karibu”.


“Ninaamini tukiungana wote kwa pamoja tutaweza, hakuna jambo lisilowezekana, muhimu ni kujipanga na kuwa na nia thabiti ya kuwasaidia watanzania kupata maji.


Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), wakati akiwasili kuzungumza nao makao makuu ya mamlaka hiyo, Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) leo alipotembelea makao makuu ya mamlaka hiyo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wakimsikiliza Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa alipotembelea ofisini hapo leo.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa(kushoto) akizungumza na  Mkurugenzi wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja alipotembelea katika ofisi za  DAWASA leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akiagana na wafanyakazi wa DAWASA  mara baada ya kumaliza ziara yake katika ofisi za mamlaka hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



COSOTA YAWATAKA WASANII KUSAJILI KAZI KWA MANUFAA YAO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
CHAMA cha Hakimiliki Tanzania COSOTA kimewataka wasanii wa filamu na muziki kutambua umuhimu wa kusajili kazi zao kabla ya kuzipeleka sokoni au kuuza kwa makampuni makubwa.

Hayo yamesemwa na COSOTA leo katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea ndani ya Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Globu ya Jamii, Afisa Hakimiliki na Leseni Ngutunyi David amesema wasanii wengi sana walishindwa kunufaika kwa kazi walizozifanya kutokana na kuuza kazi zao kwa makampuni makubwa ambayo yanakuja kufaidika kwa muda mrefu.

Ngutunyi amesema, msanii anashindwa kuelewa kuwa unapouza kazi yako kwa kampuni kubwa na kupewa kiasi kikubwa cha hela kwa wakati mmoja hakiwezi kuja kukusaidia baadae na kuacha watu wengine wakifaidika kwa muda wote.

Akielezea umuhimu wa kusajili na kupata hakimiliki kwa kazi wasanii, Ngutunyi amesema msanii anaposajili kazi yako inakupa nguvu ya kudai maslahi yako pindi pale mtu anapokuja kutengeneza au kubuni kitu kama cha kwako.

"Msanii anapokuja COSOTA na kusajili kazi zake zinampa nguvu ya kudai maslahi pindi pale mtu anapokua amenakili kazi yako kwa kupeleka malalamiko na sisi kama watoaji hakimiliki tunamuita na kukaa chini kwa ajili ya majadiliano,"amesema Ngatunyi.

"Malalamiko yamekuwa mengi sana kwa wasanii hususani wa filamu wameshindwa kunufaika na kazi zao baada ya kuziuza kwa makampuni makubwa na sasa wamepata matatizo wanakosa msaada,"amesema Ngutunyi.

Mbali na wasanii wa filamu na muziki, Ngatunyi amewataka waandaaji wa vipindi mbalimbali vya redio na televisheni kusajili kazi zao ili kuepukana na suala la kazi kuingiliana.

COSOTA inafanya kazi ya kutoa leseni na hakimiliki kwa wasanii wa aina mbalimbali na waandaaji wa vipindi na wamewashauri wasanii kufuata taratibu za usajili kwa kazi zao ili ziwanufaishe kwa kipindi kirefu.
Mtoa huduma COSOTA upande wa Kumbukumbu Aneth Maimu akizungumza na Globu ya Jamii  akiwa pamoja na Afisa Hakimiliki na Leseni Chama cha Hakimiliki COSOTA Ngutunyi David (kushoto)  akielezea umuhimu wa wasanii kusajili kazi na kuacha kuuza kwa makampuni makubwa.Picha na Emmanuel Massaka.

NiDA NA RITA WAENDELEA KUTOA HUDUMA KWENYE MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0

Afisa Habari wa RITA Jaffar Malema akiendelea na zoezi la kuita majina kwa ajili kuwapatia vyeti vya kuzaliwa kwenye maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa RITA wakiwa wanatoa huduma kwa wananchi waliojitokeza katika banda hilo kupata huduma ya vyeti vya kuzaliwa kwenye maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Wananchi waliojitokeza katika Banda la Mamlaka ya Vitambulisho ya Taifa (NIDA) kwa ajili ya kujipatia huduma za vyeti vya kuzaliwa kwenye maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)



Wananchi waliojitokeza katika Banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA kwa ajili ya kujipatia huduma ya vitambulisho vya Taifa kwenye maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

MAWAZIRI WAWILI WAWASILI MBEYA KUCHUNGUZA CHANZO CHA AJALI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza katika kikao kilichowakutanisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya, baada ya kuwasili jijini hapo kwa ziara ya kikazi.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akisalimiana na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya, Mratibu wa Polisi, Leopard Fungu, baada ya kuwasili jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akiongozana na Kamanda wa Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi, Fortunatus Musilimu (wakwanza kulia), baada ya kuwasili jijini Mbeya leo  kwa ziara ya kikazi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwele, akimuongoza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, kusalimiana na wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege Songwe, baada ya kuwasili jijini Mbeya, leo kwa ziara ya kikazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMKABIDHI DKT TIZEBA MATREKTA 500 YA URSUS

$
0
0
Na Mathias Canal, Dar es salaam

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) leo 4 Julai 2018 amemkabidhi Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba jumla ya matrekta 500 yatakayopelekwa kwa vyama vya ushirika vya msingi ili wakulima kunufaika na tija katika kilimo hususani zao la Pamba.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 42 ya sabasaba katika viwanja vya Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam, Mhe. Dkt Tizeba alisema kuwa sekta ya kilimo nchini bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo tija ndogo inayosababishwa na matumizi madogo ya pembejeo, huduma duni za ugani na matumizi ya zana duni za kilimo ambapo wakulima wengi wanatumia majembe ya mkono au kutumia maksai wakati wa kulima.

“Katika kilimo cha Pamba msimu wa mwaka 2017/2018 ushahidi unaonyesha kwamba wakulima walichelewa kuanza kuandaa mashamba yao kwa sababu Maksai wakati wa kiangazi wanadhoofu sana, na mara mvua inaponyesha hawawezi kulima mpaka majani yawe mengi ndio wapate nguvu za kuanza kulima, hali hii inaondoa uwezekano wa wakulima kutumia teknolojia mpya katika kilimo kama vile kilimo hifadhi ambacho kimedhihirika kuongeza tija zaidi ya mara mbili” Alikaririwa Mhe Dkt. Tizeba

Aliitaja mikoa itakayoanza kunufaika na mpango huo katika awamu hii ya kwanza kuwa ni pamoja na Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Tabora na Geita, awamu ya pili ikijumuisha mikoa ya Singida, Kagera, na Kigoma huku awamu ya tatu ikitarajiwa kuhusisha mikoa ya Kanda ya Mashariki kwa kuzingatia ongezeko la uzalishaji wa pamba katika maeneo hayo.

Mhe Tizeba alisema mtazamo wa mpango huo ni kuunganisha nguvu za mkulima mmoja mmoja ili kuharakisha kuleta maendeleo yao ambapo utatekelezwa kwa kutumia sehemu ya fedha zinazolipwa AMCOS kama kamisheni ya kusimamia ununuzi wa pamba ambapo matarajio ni kukusanya Bilioni 6 kama uzalishaji wa pamba utafika kilo milioni 400 kwa mwaka.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim M. Majaliwa (Mb) akimkabidhi hati ya makabidhiano Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba ya matrekta 500 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi matrekta 560 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara ya Uwekezaji, Charles Mwijage, Wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na kulia ni Naibu Waziri wake, Dkt, Mary Mwanjelwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba Kitabu cha Mwongozo wa Taratibu za Kujenga Kiwanda Nchini Tanzania baada ya kufungua Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba (Mwenye maiki) akizungumza kabla ya kukabidhiwa matrekta 500 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe ikiwa ni ishra ya kukabidhi matrekta 560 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara ya Uwekezaji, Charles Mwijage na kushoto ni Naibu Waziri wake, Mhandishi Stella Manyanya. Wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na kulia ni Naibu Waziri wake, Dkt, Mary Mwanjelwa



JIJI HALINA MAMLAKA KUTOA KIBALI CHOCHOTE BILA MAMLAKA HUSIKA KUJUA-DC HAPI

WAZIRI KIGWANGALLA AHITIMISHA ZIARA YAKE MKOANI MBEYA, ATEMBELEA MAPOROMOKO YA KIMANI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga picha ya pamoja (Selfie) kwa kutumia simu yake ya mkononi na baadhi ya wafanyakazi wa Pori la Akiba Mpanga Kipengere alipotembelea pori hilo jana kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi. Nyuma yao ni Maporomoko ya Mto Kimani ambayo yana urefu wa mita 70, na ni chanzo kikuu cha maji yanayounda mto Ruaha hadi mto Rufiji. 

Mbali na maporomoko hayo pori hilo pia lina wanyamapori mbalimbali ikiwemo Tumbili, Nyani, Tandala, jamii ya ndege mbalimbali ikiwemo wahamao kutoka ulaya wakati wa baridi kali na aina mbalimbali za maua ya asili ya kuvutia. 

Dk. Kigwangalla amesema maporomoko hayo hayakuwahi kutumika ipasavyo kiutalii kutokana na kukosekana kwa miundombinu muhimu ikiwemo barabara ya kufika eneo hilo. Amesema katika mwaka huu wa fedha Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuboresha barabara hizo pamoja na kujenga ngazi kushuka kwenye kina cha maporomoko hayo hadi upande wa pili. Pori hilo pia lina kivutio cha pango alilojificha chief Mkwawa wakati wa vita ya pili ya dunia. 

Kuna aina mbalimbali za utalii katika pori hilo ikiwemo utalii wa kupanda mlima, utalii wa kuogelea, utalii wa kutembea kwa miguu na utalii wa picha.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa ramani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Dk. Chris Timbuka (wa pili kulia) alipotembelea bonde la Ihefu kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Mbeya jana. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfaume.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa Maporomoko ya Mto Kimani na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi alipotembelea Pori la Akiba Mpanga Kipengere ambalo lipo katika wilaya za Mbarali (Mbeya), Makete na Wanging'ombe (Njombe). Maporomoko hayo yenye urefu wa mita 70 ni chanzo kikuu cha mto Ruaha Mkuu na Mdogo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Wawindi iliyopo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo iliyofadhiliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) shuleni hapo.

TANCDA YATOA HUDUMA YA USHAURI NA UPIMAJI WA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA BURE KATIKA MSIMU WA SABASABA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya Jamii.

SHIRIKISHO la vyama vya magonjwa yasiyoambukiza (TANCDA) linalojihusisha na utoaji wa elimu ya afya, ushauri na upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza, imepiga kambi katika viwanja vya sabasaba wakihudumia wananchi bure kabisa.


Akizungumza na Michuzi blogu Meneja mradi wa shirikisho hilo bi. Happy Nchimbi ameeleza kuwa katika maadhimisho hayo ya sabasaba wanatoa huduma kwa wananchi bure kabisa ikiwemo kutoa elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa.

Aidha ameeleza kuwa wanapima magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza ikiwemo kisukari, shinikizo la damu na uwiano wa uzito na urefu bure kabisa.Pia ameeleza kuwa wanatoa ushauri kuhusiana na mtindo bora wa maisha hasa katika kuepukana na magonjwa hayo yasiyo na maambukizi.

Huduma hiyo imeanza kutolewa kuanzia Julai 2 mwaka huu na yatamalizika Julai 7 na kuendelea kutolewa bure katika hospitali ya taifa ya Muhimbili katika jengo la kliniki ya kisukari kwa ushauri na upimaji.
Watoa huduma wa afya katika banda la Shirikisho la Vyama vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza TANCDA wakitoa huduma kwa wananchi waliojitokeza kwa ajili ya kupata huduma za upimaji wa afya kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwenye maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea ndani ya Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es salaam.
Meneja mradi wa Shirikisho la Vyama vya magonjwa yasiyo yakuambukiza TANCDA Happy Nchimbi akizungumza na Globu ya Jamii akielezea huduma wanazozitoa kwenye banda lao kwenye maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara ndani ya Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mauzo wa Kampuni ya Belva Consult Elizabeth Charles akimkabidhi Under Pad mwana Globu ya jamii alipotembelea banda lao ndani ya maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam. Picha na Emanuel Massaka.

KIWANDA CHA ASAS DAIRIERS LTD CHAIBUKA MSHINDI KIPENGELE CHA "FOOD AND BEVERAGES" MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akimkabidhi kikombe cha ushindi wa jumla kipengele cha (Foods and Beverages) Bw. Jimmy Kiwelu Meneja wa Masoko na Matukio kiwanda cha ASAS DAIRIERS LTD katika maonyesho ya biashara ya Sabasaba kwenye viwanja vya TANTRADE barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-TANTRADE)
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa Masoko na Matukio kiwanda cha ASAS DAIRIERS LTD Bw. Jimmy Kiwelu wakati alipotembelea katika banda hilo katika maonyesho ya biashara ya Sabasaba kwenye viwanja vya TANTRADE barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Masoko na Matukio kiwanda cha ASAS DAIRIERS LTD Bw. Jimmy Kiwelu wakati alipotembelea katika banda hilo leo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiakionyeshwa na Meneja wa Masoko na Matukio kiwanda cha ASAS DAIRIERS LTD Bw. Jimmy Kiwelu vikombe mbalimbali ambavyo Kiwanda hicho kimewahi kujishindia wakati alipotembelea katika banda hilo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akitembelea kitengo cha wateja wakubwa cha kiwanda cha ASAS DAIRIERS LTD wakati alipotembelea katika banda hilo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiendelea kutembelea mabanda mengine katika viwanja vya Sabasaba mara baada ya kuzindua rasmi maonesho hayo.

Watoto wa Kitanzania waweka lengo la kuipeleka Tanzania Kombe la Dunia

$
0
0

  RAIA wa Tanzania Laigwanani Mollel na Ziporah Godfrey Mollel walioshiriki michuano ya soka kimataifa ya Football for Friendship(F4F) wameondoka Urusi kurejea Tanzania wakiwa na ndoto yakuiwakilisha Tanzania katika Kombe la Dunia siku moja.

Michuano hiyo ya F4F ilishirikisha watoto wenye miaka 12 kutoka nchi 211 na imefanyika kwa mwaka wa sita tangu kuanzishwa kwake. Laigwanani na Ziporah wakitokea akademi ya Lengo Football ya Arusha Tanzania wameondoka Urusi kurejea Tanzania wakisema ndoto yao kubwa ni kuiwakilisha Tanzania katika Kombe la Dunia siku za usoni.

“Niiwakilisha vizuri Tanzania kwa kupeperusha bendera ya taifa kwenye sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia mwaka huu, ilikuwa kabla ya mechi ya ufunguzi ya Urusi na Saudi Arabia. “Nilikuwa na uchovu sana baada ya kazi ya siku ile lakini naamini nimepata hamasa ya kuiwakilisha nchi yangu katika Kombe la Dunia siku zijazo kwa mimi mwenyewe kucheza uwanjani,” alisema Laigwanani.

Kwa upande wake, Ziporah alisema; “Nitakua na faraja sana kwa sababu Tanzania haijawahi kufuzu katika fainali za Kombe la Dunia, hivyo nitakuwa ni mimi ninaye iwakilisha nchi yangu. “Nitajisikia ujasiri na nitaiwakilisha nchi yangu vizuri na najua katika mawazo yangu kuwa siku moja Tanzania itakuwa hapa katika fainali za Kombe la Dunia.”

Program hii ya Kijamii ya F4F ni programu ya kijamii inayojumuisha siku tatu za mafunzo ya soka na kila timu kati ya timu 32 kutoka duniani kote zilizipewa majina ya wanyama walio hatarini kupotea. Timu zilizoundwa zilijumuisha wachezaji kutoka kila pembe ya dunia, kutoka mataifa makubwa na wadogo bila kujali, dini, tamaduni na ushawishi wa kisiasa na wa kiitikadi.





PROPERTY INTERNATIONAL WAFURAHIA USHINDI MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
pr01
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akimkabidhi kikombe cha ushindi wa jumla kipengele cha (Trade in Services Exhibitor) Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International Tanzania Bw. Masoud Alawi leo. Mara baada ya kutangazwa washindi katika uzinduzi wa maonesho ya biashara ya kimataifa Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya TANTREADE Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
pr1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International Tanzania Bw. Masoud Alawi kushoto akiwa na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Leila Maingu na baadhi ya waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
pr3
Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International Tanzania Bw. Masoud Alawi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi mara baada ya ushindi huo.
pr01
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akimkabidhi kikombe cha ushindi wa jumla kipengele cha (Trade in Services Exhibitor) Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International Tanzania Bw. Masoud Alawi leo. Mara baada ya kutangazwa washindi katika uzinduzi wa maonesho ya biashara ya kimataifa Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya TANTREADE Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
pr1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International Tanzania Bw. Masoud Alawi kushoto akiwa na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Leila Maingu na baadhi ya waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
pr3
Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International Tanzania Bw. Masoud Alawi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi mara baada ya ushindi huo.

KATIBU MKUU MPYA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AWASILI OFISINI KWAKE DODOMA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto) akimsalimia Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Kuwahudumia Wakimbizi, Deudedit Masusu wakati kiongozi huyo ambaye ameteuliwa hivi karibuni na Rais Dkt. John Magufuli, alipowasili ofisi za Wizara hiyo, jijini Dodoma leo, na kupokelewa na maafisa wa Wizara hiyo. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Winston Mruma (katikati), watatu kulia ni Mhasibu Mkuu wa Wizara hiyo, Perfect Kilenza, na  Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu, Ernest Maalugu.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (mstaafu), Meja Jenerali (mstaafu), Projest Rwegasira (kushoto) akimkaribisha Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, ofisini kwake jijini Dodoma leo. Rwegasira ambaye amestaafu nafasi hiyo alizungumza na Kingu masuala mbalimbali ya uongozi wa wizara hiyo kabla ya kukabidhiwa rasmi ofisi hiyo.
 Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara hiyo, Winston Mruma wakati alipokua anatoa taarifa mbalimbali ya watumishi waliopo ofisi ya Wizara hiyo, jijini Dodoma. Meja Jenerali Kingu aliwasili katika ofisi hizo mara baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli kuiongoza wizara hiyo.
 Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akizungumza na watumishi wa wizaya yake waliopo jijini Dodoma, mara baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli kuiongoza wizara hiyo. Watatu kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Winston Mruma, na watatu kulia ni Mhasibu Mkuu wa Wizara hiyo, Perfect Kilenza. Kingu aliwasili jijini humo leo, na pia alikutana na Katibu Mkuu anayemaliza muda wake, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira.
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Winston Mruma alipokua akimuonyesha sehemu ya majengo ya ofisi za wizara hiyo wakati Katibu Mkuu huyo mpya alipowasili jijini Dodoma leo, mara baada ya kiongozi kuteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli kuiongoza wizara hiyo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

NSSF YANYAKUWA USHINDI WA JUMLA KATIKA MAONYESHO YA 42 YA BIASHARA YA KIMATAIFA DAR

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara Tuzo ya Ushindi wa Jumla ya Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. 
PMIO 1252 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkurugenzi Mkuu, Mamalaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Edwin Rutaberuka (kushoto) wakifurahia baada ya Waziri Mkuu kumkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara, Tuzo ya Ushindi wa Jumla ya Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam, Julai 4, 2018 Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images