Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

NEWZ ALERT: WATU WATATU WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA KUFUATIA AJALI YA 'AMBULANCE' KUGONGANA NA LORI USIKU HUU.

$
0
0
 TAARIFA zilizoifikia Globu ya Jamii usiku huu kutoka eneo la ajali iliyotokea maeneo ya  Riverside-Ubungo,zinaeleza kuwa gari la kubebea Wagonjwa 'Ambulance' ya Chuo kikuu cha Dar es salaam iliyokuwa ikipeleka mgonjwa Mliman Campus tokea Mabibo hostel imegongana uso kwa uso na Lori la Mizigo,habari zaidi kutoka eneno la tukio zinabainisha kuwa Watu watatu wanahofiwa kupoteza maisha,akiwemo dereva wa 'Ambulance',Nesi na Dada mjamzito anaedaiwa kuwa ni Mwanafunzi. 

Globu ya Jamii inafuatilia taarifa kamili na sahihi kwa ukaribu kabisa kutoka kwa mamlaka husika.

Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi-Amen

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

BRAC YATOA VIFAA VYA SH MIL 69 KWA WASICHANA TANGA

$
0
0
SHIRIKA la Brac limetoa vifaa vya kazi vyenye thamani ya sh Mil 69 kwa wasichana 924 kwa ajili ya kuanza shughuli za ujasirimali ili kuweza kujikwamua kiuchumi .

Vifaa hivyo ambavyo vimetolewa maalum kupitia mradi wake wa kuwajengea uwezo na kujiajiri wasichana ambao wameshindwa kuendelea masomo ya sekondari mkoani Tanga.Akikabidhi msaada huo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa alisema kuwa vifaa hivyo vitaweza kuwasaidia wasichana hao kuweza kujiendeleza kiuchumi kwa kujihakikishi kipato chao.

“Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ili kuweza kufikia uchumi wa viwanda lakini kupitia Brac tunaona walivyofanikiwa kuwawezesha wasichana hao ili waweze kujikwamua kiuchumi”alisema DC Mwilapwa.

Kwa upande wake Mkurungenzi Mkuu wa Brac Assan Golowa alisema kuwa tayari mradi huo umefanikiwa kuwafikia wasichana 240 toka ulipoanzishwa mwaka 2016 mkoani humo.Alisema kuwa mradai huo unatoa fursa ya pili kwa wasichana walioshindwa kuendelea na masomo waweze kujifunza ujuzi wa mikono na kuweza kujiajiri ili kuweza kuwa wazalishaji mali.

“Mradi huu upo katika mikoa 23 hapa nchini lakini kwa mkoa wa Tanga umeonyesha mafanikio zaidi kutokana na muitikio mkubwa wa wasicahna kujivutika kujiunga na mradi huo”alisema Golowa.
 Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa vyenye thamani ya ya sh Mil 69 kwa wasichana 924 kwa ajili ya kuanza shughuli za ujasirimali ili kuweza kujikwamua kiuchum ambavyo ni vyerahani na madraya ya saloon na vifaa vyengine kushoto ni Mkurungenzi Mkuu wa Brac Assan Golowa.
Mkurungenzi Mkuu wa Brac Assan Golowa akizungumza katika halfa hiyo
PRO wa shirika la BRAC SEcilia Bosco akizungumza katika halfa hiyo
sehemu ya vyarahani vilivyotolewa
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akimkabidhi vifaa vya saloni moja wa wasichana waliopatiwa mafunzo na shirika la BRAC
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akiangalia baadhi ya vifaa v ya shuleni kabla ya kuvikabidhi kwa wahusika .

Waweka Hazina, Wahasibu Watakiwa Kuzingatiai Matumizi Sahihi ya Fedha

$
0
0
Mkurugenzi Msaidizi TEHAMA, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Bartazal Kibola akifungua mafunzo ya mfumo wa malipo (epicor 10.2) kwa Waweka Hazina na Wahasibu (hawapo pichani) kutoka Halmashauri za Mikoa ya Arusha na Manyara, leo Jijini Dodoma.

Na Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.

Waweka Hazina na Wahasibu kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya fedha zinazotumwa katika Halmashauri zao.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Mkurugenzi Msaidizi TEHAMA, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Bartazal Kibola alipokuwa akifungua mafunzo ya mfumo wa malipo (epicor 10.2) kwa Waweka Hazina na Wahasibu kutoka Halmashauri za Mikoa ya Arusha na Manyara. Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Wahasibu hao namna ya kutumia mfumo huo ambao umeboreshwa zaidi.

“Mfumo huu mpya utakapoanza kutumika lazima sheria na taratibu zifuatwe, matumizi ya fedha yaendane na bajeti ya Halmashauri husika, vilevile ni muhimu kuhakikisha kuwa vifungu vyenu vya fedha vinakaa vizuri,” alisema Kibola. Aliendelea kusema, mfumo huo umerahisha kazi na kupunguza gharama ambapo mabadiliko yote ya bajeti yatakuwa yakifanyika kupitia mfumo huo tofauti na ilivyokuwa awali ambapo Halmashauri zililazimika kutuma barua za mabadiliko ya bajeti ofisi za TAMISEMI.
Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bibi Beatrice Kimoleta akitoa maelekezo ya mafunzo ya mfumo wa epicor 10.2 kwa Waweka Hazina na Wahasibu (hawapo pichani) kutoka Halmashauri za Mikoa ya Arusha na Manyara, leo Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayoendelea jijini humo.

Aidha, amesema mfumo huo utatatua baadhi ya changamoto zilizokuwepo katika mfumo uliopita epicor toleo Na. 9.05 ikiwa ni pamoja na changamoto ya kutoa taarifa za utekelezaji mara baada ya kufanya matumizi kwa kuzingatia mipango iliyojiwekea Halmashauri husika.

Hivyo basi epicor toleo namba 10.2 itaondoa kabisa tatizo la taarifa hizo kwani mfumo huo baada ya malipo kufanyika utakuwa na uwezo wa kupeleka taarifa hizo kwenye mfumo wa mipango na bajeti ambapo pia mfumo wa FFARS utakuwa umepokea taarifa hizo za matumizi ya vituo na hivyo taarifa zote za utekelezaji kupatikana moja kwa moja kutoka mfumo wa Plan Rep ambao pia umeunganishwa na mfumo wa epicor 10.2.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais, TAMISEMI Bibi Beatrice Kimoleta amewataka Wahasibu hao kuingiza takwimu sahihi katika mfumo huo ili mfumo uweze kuongea taarifa ambazo ni sahihi. Vile vile, ameshukuru Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (Ps3) kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) kwa kuwezesha uboreshaji wa mfumo huo ambao utaleta uwazi katika mapato na matumizi ya fedha za Umma katika Halmashauri zote hapa nchini.

Mfumo wa malipo (epicor 10.2) unatarajiwa kuanza kutumika katika Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini kuanzia Julai 1 mwaka huu. Mfumo huo utahusisha masuala yote ya fedha za Mamlaka hizo ikiwa ni pamoja na mapato, matumizi pamoja na bajeti nzima ya Mamlaka husika. 
Meneja wa Mradi wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Mkoani Dodoma, Bw. Gideon Muganda akitoa maelekezo kuhusu ushiriki wa PS3 katika mfumo wa malipo (epicor 10.2) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mfumo huo kwa Waweka Hazina na Wahasibu kutoka Halmashauri za Mikoa ya Arusha na Manyara, leo Jijini Dodoma.
Waweka Hazina na Wahasibu kutoka Halmashauri za Mikoa ya Arusha na Manyara wakimsikiliza mgeni rasmi Mkurugenzi Msaidizi TEHAMA, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Bartazal Kibola (aliyesimama) ambaye alifungua mafunzo ya mfumo wa malipo (epicor 10.2) kwa niaba ya Mkurugenzi wa TEHAMA, Ofisi Rais TAMISEMI, leo Jijini. Waweka Hazina na Wahasibu kutokana Mamlaka za zote za Serikali za Mitaa wanajengewa uwezo wa kutumia mfumo huo utakaohusisha masuala yote ya fedha ikiwemo mapato, matumizi pamoja na bajeti za Halmashauri husika. Mfumo huo utaanza kutumika rasmi Julai 1, mwaka huu.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BODI YA WADHAMINI KUTOKA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akizungumza na Bodi ya wadhamini kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma walioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo hicho(UDOM), Balozi. Ami Mpungwe (kushoto kwake) walipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), Balozi. Ami Mpungwe (katikati) na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Egid Mubofu walipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe kutoka Bodi ya wadhamini ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) walipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma. Wajumbe hao waliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Balozi Ami Mpungwe (wa tatu kushoto) (PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

TATHMINI YA MAZINGIRA MRADI WA UMEME RUFIJI YABAINISHA KUWA ATHARI ZAKE ZINAZUILIKA

$
0
0
Na Veronica Simba – Dodoma

Mtaalam Mwelekezi aliyeingia Mkataba na Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kufanya Tathmini ya Mazingira (EIA) katika Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya maji ya Mto Rufiji Profesa Raphael Mwalyosi, amesema kuwa athari za kimazingira zilizobainika kuweza kutokea, zinaweza kuzuilika.

Ameyasema hayo leo, Juni 11, 2018 wakati akiwasilisha Tathmini hiyo ya Mazingira kwa Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali zenye majukumu ya kutekeleza miundombinu wezeshi ya Mradi husika.

“Tathmini yetu imebainisha kuwa Mradi husika unaweza kutekelezwa pasipo shaka yoyote kwani athari zake kimazingira zinaweza kuzuilika. Muhimu ni kuweka mikakati ya kuzizuia,” alifafanua.

Uwasilishwaji wa Tathmini ya Mazingira kwa Kamati hiyo Tendaji, umefanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati jijini Dodoma, ambapo ni moja ya hatua muhimu zinazoendelea kufanyika kabla ya kuanza rasmi utekelezaji wa Mradi huo.

Wajumbe walioshiriki katika zoezi la uwasilishwaji wa Tathmini husika ni Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Maliasili na Utalii; Mambo ya Ndani ya Nchi, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; Kilimo; Mifugo na Uvuvi pamoja na Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Nyingine ni Wizara ya Fedha na Mipango; Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira; Ofisi ya Waziri Mkuu; Wizara ya Madini pamoja na Wizara ya Nishati, ambayo ndiyo yenye dhamana.

Aidha, wadau wengine walioshiriki ni Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Wakuu wa Taasisi za Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA), Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na TANESCO.
Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali zenye majukumu ya kutekeleza miundombinu wezeshi ya Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya maji ya Mto Rufiji, wakimsikiliza Mtaalam Mwelekezi, Prof Raphael Mwalyosi (aliyesimama), alipokuwa akiwasilisha Tathmini ya Mazingira ya Mradi husika, Juni 11, 2018 Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof Simon Msanjila, wakifuatilia uwasilishwaji wa Tathmini ya Mazingira ya Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya maji ya Mto Rufiji, Juni 11, 2018 Dodoma.

WASHINDI WA TUZO ZA MO SIMBA 2018

$
0
0
1.GOLIKIPA BORA WA MWAKA
A.Aishi Manula - WINNER
B.Said Mohamed 'Nduda'
C. Emmanuel Elias Mseja

2.BEKI BORA WA MWAKA
A.Yusuph Mlipili
B.Erasto Nyoni - WINNER
C.Shomari Kapombe

3.KIUNGO BORA WA MWAKA
A.Jonas Mkude
B.James Kotei
C.Shiza Kichuya – WINNER

4.MSHAMBULIAJI BORA WA MWAKA
A.Emmanuel Okwi - WINNER
B.John Bocco
C.Shiza Kichuya

5.MCHEZAJI BORA MWANAMKE WA MWAKA
A.Rukhia Salum
B.Zainabu Rashidi Pazzi - WINNER
C.Dotto Makunja

6.MCHEZAJI BORA MDOGO WA MWAKA
A.Ally Salim (GK)
B.Rashid Juma – WINNER
C.Salumu Shabani

7.GOLI BORA LA MWAKA
-John Bocco (Simba VS Mwadui)

8.TUZO YA BENCHI LA UFUNDI
A.Pierre Lechantre – Kocha Mkuu
B.Masoud Djuma – Kocha Msaidizi
C.Mohamed Aymen – Kocha wa Viungo
D.Muharam Mohamed – Kipa wa Makipa
E.Richard Robert – Meneja wa Timu
F.Yassin Gembe – Daktari wa Timu
G.Abbas Selemani – Mratibu

9. SHABIKI BORA WA MWAKA
- Fihi Salehe Kambi

10. MHAMASISHAJI BORA WA MWAKA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
A.Hamis Mwinjuma (Mwana FA) - WINNER
B.Salama Jabir – WINNER
C.Zitto Kabwe
D.Vyonne Cherrie (Monalisa)
E.Omary Nyembo (Ommy Dimpoz)

11. MHAMASISHAJI BORA
- Haji Manara

12. TAWI BORA LA MWAKA
A.Wazo Hill
B.Ubungo Terminal - WINNER
C.Vuvuzela

13. KIONGOZI BORA WA MWAKA
- Kaimu Rais wa klabu ya Simba, Salim Abdallah Muhene

14. TUZO YA WASIMAMIZI WA MCHAKATO WA MABADILIKO
A.Jaji Mstaafu Thomasi Mihayo
B.Wakili Damasi Ndumbaro
C.Abdulrazak Badru 
D.Mussa Hassan Zungu
E.Yusuph Nassoro
F.Brenda Mrema
G.Mzee Hamis Boma
H.Revocatus Cosmas Sangu
I.Hashim Nyendage
J.Gervas Alpha Honest
K.Emmanuel Metusela Urembo
L.Mulamu Nghambi
M.Selemani Omari
N.Aziz Kifile
O.Salim Abdallah Muhene
P.Arnold Kashembe
Q.Omari Bakari Mtika
R.Evodius Mtawala

15. TUZO YA HESHIMA (LIFETIME ACHIEVEMENT)
- Selemani Matola – WINNER

16. MCHEZAJI BORA WA MWAKA
A.Emmanuel Okwi
B.John Bocco - WINNER
C.Shiza Kichuya

KAMPUNI ZITAKAZOLETA UBABAISHAJI KATIKA MALIPO YA PAMBA YA WAKULIMA KUFUTIWA LESENI

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT, RS TABORA

SERIKALI imesema haitasita kuzifuta na kuzinyang’anya leseni Kampuni ambazo zinanua pamba hapa nchini ikiwa zitachelewesha fedha za wakulima  wa zao hilo na kuanza kuwazungusha bila kuwalipa fedha zao.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Kilimo Dkt Charles Tizeba wakati akizindua ununuzi wa Pamba katika Kijiji cha Muhilidede wilayani Uyui Mkoani Tabora

Alisema ni jukumu la Kampuni zinapomaliza kununua pamba ya mkulima kumlipa palepale siku hiyo hiyo kwa kuwekea fedha katika Akaunti yake au kupitia simu ya mkononi na kisha pesa ikishaingia anaone ujumbe wa kumhakikisha kulipwa

Waziri huyo aliwataka Viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika, Halmashauri za Wilaya na Wakulima walisikubali Kampuni ziondoe pamba katika Vituo vya kununulia pamaba kama malipo kwa wakulima hajafanyika na chama cha mshingi na Halmashauri hazijalipwa.

Dkt. Tizeba alisema Serikali inaachukua hatua hiyo ili kurejesha imani kwa wakulima juu ya ushirika ambao umekuwa ukipigwa vita na baadhi ya watu.

Aidha Waziri huyo aliwaagiza Viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika kuhakikisha vinawakamata na kuwapeleka Polisi watu wote ambao watapeleka pamba iliyochanganywa na uchafu na ile wekewa maji kwa sababu watu hao ni sawa na wezi.

Alisema mkulima anaweka maji kwenye pamba na yule anayeweka uchafu anataka kuhujumu zao hilo  kwa kusababisha mbegu zitakazolishwa zisiote na wanunuzi watoe bei mbaya kwa pamba chafu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliwataka viongozi wa Vyama vya Ushirika kutumia sehemu ya asilimia 33 ya kila kilo watakayopata kununua Matrekta ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo msimu ujao.

Alisema kuwa kupitia kilimo cha matumizi ya jembe la mkono hakiwezi kuleta mapinduzi ya kilimo na manufaa kwa mkulima mkoani humo.

Makala: Mazingira na hali ya hewa

$
0
0
Wafanyakazi wa TMA wakishiriki katika zoezi la kupanda miti wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Agnes Kijazi.

Na Monica Mutoni

WAKATI huu ambapo tunaadhimisha wiki ya mazingira ni vyema tukakumbuka tulikotoka, wakati wazee wetu wakitumia busara zao kutushauri kutunza mazingira ili yatutunze.

Moja ya msisitizo wao ulikuwa ni pamoja na kutuaminisha kwamba utunzaji wa mazingira ni kupanda miti, lakini umefika wakati na sisi tujiulize kupanda miti ndio utunzaji wenyewe wa mazingira? 

Kwa mujibu wa wataalamu wa mazingira, ushauri wa wazee juu ya kupanda miti ni sahihi kabisa, nadharia ambayo pia inaungwa mkono na wataalamu wa hali ya hewa kote duniani ambao wanaamini maeneo yenye misitu mizito, ndiko kunapokuwa na mvua nyingi zaidi. 

Wataalam hao wanatolea mfano wa misitu mikubwa duniani ikiwemo misitu ya Congo ambapo wanasema pamoja na kupata mvua nyingi maeneo hayo  yanakuwa na hewa safi kulinganisha na maeneo ambayo hayana misitu kwani miti ina tabia ya kuondoa hewa chafu kwenye anga na kuongeza hewa safi.
Eneo la jangwani likiwa limezungukwa na maji yaliyotokana na vipindi vifupi za mvua kubwa katika msimu wa mvua za VULI 2017.

Kwa maana hiyo, kama waaminivyo wataalamu hatuna budi kufahamu kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya mazingira kwa maana ya uwepo wa misitu na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ni taasisi inayoshughulikia masuala ya hali ya hewa nchini na kuiwakilisha nchi kikanda na Kimataifa. Taasisi hii imepewa jukumu la kutoa huduma za hali ya hewa kupitia sheria ya hali ya hewa Na. 6 ya mwaka 1977. Mamlaka hii pia hutoa tahadhari ya hali mbaya ya hewa kila inapotarajiwa kuwepo na huwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kutumia taarifa za hali ya hewa. 

Kwa kuzingatia  matumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa tutaweza kupunguza athari za uharibifu wa mazingira. 

TMA inasema takwimu za hali ya hewa zilizokusanywa kwa kipindi cha miongo kadhaa iliyopita zinaonesha dhahiri kuwa uharibifu wa mazingira umechangia kwa kiasi kikubwa kusababisha mabadiliko ya hali ya hewa nchini na duniani kwa ujumla.  

Mfano mkubwa wa viashirikia hivyo ni kuongezeka kwa joto na kupungua kwa mvua  katika maeneo mbalimbali nchini  kama ilivyooneshwa kwenye mwenendo wa mvua wa kitaalamu katika vielelezo vya maeneo mbalimbali nchini. 
Ongezeko la joto kwa mkoa wa Dar es salaam kuanzia mwaka 1953-2015.

Kwa vielelezo hivi, ni wazi kuwa joto limeendelea  kuongezeka miaka ya karibuni katika  mkoa wa Dar es Salaam na Kilimanjaro ukilinganisha na miaka iliyopita.
Aidha, kiwango cha mvua kinapungua kwa kiasi fulani ukilinganisha na miaka ya nyuma kama inavyoonekana kwa mkoa wa Kilimanjaro. 

MKUU WA MAJESHI ATOA WITO KWA WAZAZI KUWEKEZA KWENYE ELIMU

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Jenerali Venance Mabeyo ametoa wito  kwa wazazi kuwekeza katika elimu kwa watoto  wao ili waweze kutimiza ndoto za maisha yao, badala ya kuwaoza wakiwa na umri mdogo.

 Jenerali Mabeyo ametoa  wito huo wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Ilumya  iliyofanyika Kijiji cha Masanza Kona  kata ya Kiloleli Wilayani Busega, na kuhudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka, mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt Vicent Naano  marafiki wa mkuu wa majeshi kutoka Dar es Salaam , Wajenzi Enterprises ,wafanyabiashara wa Simiyu na waumini wa kanisa hilo .

Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo pamoja na kuongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa amesema pamoja na jamii kushiriki katika ujenzi wa nyumba za ibada ,wazazi wanapaswa kutoa kipaumbele cha elimu kwa watoto badala ya kuwakatisha masomo hususani  wa kike ili waolewe .

“Sasa hivi mmewekewa shule ya sekondari hapa na mimi nimeshiriki kujenga shule hii DC analijua hili, sasa wazee wangu mlioko hapa changamkieni elimu, watoto muwapeleke shule, waacheni wasome elimu ndiyo ufunguo wa maisha, wasiposoma hata mkiomba nafasi za kuingia jeshini hakuna nafasi” alisema Jenerali Mabeyo
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Ilumya wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa, iliyofanyika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka akionesha sehemu ya fedha alizochangia katika harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la Kanisa Parokia ya Ilumya iliyoongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo katika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani humo.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akikabidhi  sehemu ya fedha zilizochangwa na Kamti ya Ulinzi na Usalama na Wafanyabiashara wa Mkoa huo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la Kanisa Parokia ya Ilumya iliyoongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo katika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani humo.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akiongoza Kwaya ya Kanisa Katoliki Parokia ya Ilumya wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa ejngo la  Kanisa, iliyofanyika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, (wa pili kushoto) Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka akicheza pamoja na wanakwaya.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye kipaza sauti) akikabidhi  sehemu ya fedha zilizochangwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wafanyabiashara wa Mkoa huo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la Kanisa Parokia ya Ilumya iliyoongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo katika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani humo.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mbele ya jiwe la msingi la Ujenzi wa Kanisa Parokia ya Ilumya, baada ya harambee ya kuchangia ujenzi wa ejngo la  Kanisa, iliyofanyika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, (katikati) Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MUHIMBILI KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI KWA UMMA KWA KUTOA ELIMU YA AFYA KWA WANANCHI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili imeandaa maonesho rasmi ya wiki ya utumishi kwa umma kwa mwaka 2018 yenye kauli mbiu ya "Mapambano dhidi ya rushwa kwa kushirikisha wadau na kujenga uongozi bora ili kufikia malengo ya ajenda 2063 ya umoja wa Afrika na malengo ya maendeleo endelevu."

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Aminiel Aligaesha amesema kuwa maonesho hayo yatafanyika ndani ya hospitali ya taifa ya Muhimbili kuanzia  Juni 18 hadi 20 mwaka huu na yatafunguliwa rasmi Juni 18 na Waziri mwenye dhamana ya Afya na ustawi wa jamii Ummy Mwalimu.

Aligaesha amesema kuwa maonesho hayo yataonesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na hospitali hiyo na wananchi watapata fursa ya kukutana na madaktari bingwa na kupata elimu ya afya na matibabu sambamba na kutoa maoni na malalamiko kuhusiana juu ya huduma wanazopata hospitalini hapo.

Aidha imeeleza kuwa wananchi watapata fursa ya kujua hali ya upambanaji wa vitendo au viashiria vya rushwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi hospitalini hapo na kuwaeleza wananchi mipango iliyopo katika kutoa huduma za afya endelevu.

Maonesho hayo huratibiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na hufanyika kila mwaka na ni moja ya matukio katika kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo wanachama huadhimisha kwa kuonesha kazizifanywazo na Serikali na taasisi zake.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,  Aligaesha Aminiel akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maonesho ya huduma ya afya katika hospitali ya taifa Muhimbili.

TAKUKURU MKOA WA PWANI WAKIRI KUONGEZEKA KWA VITENDO VYA KUPOKEA NA KUTOA RUSHWA

$
0
0
Na Linda Shebby, Pwani 

TAASISI YA Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema kasi ya kujihusisha na  vitendo  vya kupokea na kutoa rushwa  imeongezeka katika Mkoa wa Pwani.

Imeelezwa kuwa katika kipindi cha  cha Julai 2017 hadi Juni 8 mwaka huu huku Mkoa huo  umekuwa na kesi zipatazo 34 zinazoendelea  katika Mahakama mbalimbali zilizopo mkoani hapa.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Susan Raymond ambapo ameyataja maneneo yenye kesi hizo  kuwa ni Mkuranga ,Kisarawe , Bagamoyo , Rufiji ,  Mafia , Chalinze na Ikwiriri.
Aidha Kamanda Susan amekiri kuwepo kwa changamoto katika uendeshwaji wa kesi kutoka kwa mashahidi ambao mara nyingi wamekuwa wakiharibu ushahidi pindi kesi  hizo zinapofikishwa Mahakamani.

"Hivyo kutokana na ukosefu wa uaminifu kesi nyingi zimekuwa zikipoteza ushahidi  na kushindikana kuendelea,"amesema.

Akizungumzia kuhusu kadhia hiyo amesema kuwa TAKUKURU hawatokata tamaa katika kupambana na rushwa  na kuahidi kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutoa ushirikiano kwenye kesi hizo za kuzuia na kupambana na rushwa.

Amesema   kati ya kesi  34 zinazoendelea Mahakamani katika kipindi  cha Julai  mwaka 2017  hadi Juni 8 mwaka huu kesi 10 ambazo sawa na  asilimia 29.4 zinahusu  kifungu cha 15 cha sheria  ya kuzuia na kupambana na rushwa  kinachohusiana  na kosa la kushawishi, kutoa na kypokea rushwa.

Huku kesi 22 ambazo  ni sawa na asilimia 70.7 zinahusu vifungu vingine vya sheria  ya kuzuia na  kupambana na rushwa pamoja na sheria nyinginezo.

Aidha  Kamanda amesema katika kipindi hicho kesi nane zimekamilika na kutolewa hukumu  na kati ya hizo kesi sita  watuhumiwa wamekutwa na hatia  ambayo ni sawa na asilimia 75 ya kesi zote Ilizosikilizwa nankutolewa hukumu kwa kipindi tajwa.

Kamanda Susan amesema kuwa zipo hatua za kuwachukulia kisheria watu wanaoharibu ushahidi hivyo ametoa onyo na kusema  hatua kali zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayehusika ikiwa ni kufikishwa mahakamani mara moja.

Wakili wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Bwana Joseph Sang'wa  hapa anafafanua zaidi juu ya kifungu cha sheria ambacho kinaelezea hukumu  kwa shahidi anayepotosha ama kuharibu ushahidi wa kesi yeyote hapa aneleza zaidi.

TANZIA

$
0
0
Mzee Solomon Seth Gwassa na mama Phaines Gwassa wa Forest Jijini Mbeya,  wanasikitika kutangaza kifo cha binti yao mpendwa Anna Solomon Gwassa kilichotokea ghafla kwa ajali ya barabarani tarehe 11/06/2018 huko Kyela, Mbeya. Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Mzee Solomon Gwassa huko Mbeya. 
Habari ziwafikie kaka wa marehemu Salathiel Gwassa aliyepo Mafinga Iringa, mdogo wa marehemu Neema Gwassa aliyepo Goba, Dar es salaam, mdogo wa marehemu Lusekelo Gwassa na familia yake waliopo Beijing China, mdogo wa marehemu Atuganile Gwassa aliyepo Kijitonyama, Dar es salaam, mdogo wa marehemu Lusajo Gwassa aliyepo Shanghai China, na mtoto wa marehemu Johnson Robert aliyepo Beijing China, pamoja na ndugu jamaa na marafiki popote walipo. Bwana alitoa na tena ametwaa jina lake lihimidiwe.

HATIMAYE RAIS TRUMP, KIM JUNG UN WAKUTANA WAFANYA MAZUNGUMZO

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

RAIS wa Marekani Donald Trump na Kim Jung Un wa Korea  Kaskazini wamekutana katika mkutano uliokua ukisubiriwa kwa hamu ambao umefanyika katika Hotel ya Capella katika Kisiwa cha Utalii cha Sentosa, Singapore. 

Trump na Kim Jung Un wamefanya mazungumzo yanayoaminika ni ya kuleta amani na umoja baina ya mataifa hayo mawili.

Wawili hao walikutana kwanza faragha kwa dakika 38 kwa mujibu wa Ikulu ya White House, na walikuwa faragha na wakalimani wao lakini baadaye maofisa wa pande zote mbili walijumuika katika mazungumzo hayo.

Awali, Mkutano huo ulianza kwa viongozi wawili kusalimiana kwa kufurahi na kisha kuelekea ukumbi wa maktaba ya Cappela Hotel kwa ajili ya sehemu ya kwanza ya mkutano wa ana kwa ana baina yao.

Rais Trump amesema wawili hao walipiga hatua kubwa na kwamba karibuni kutakuwa na sherehe ya kutia saini nyaraka ya makubaliano.

Imeelezwa wamekuwa wakijadiliana kuhusu njia za kupunguza uhasama rasi ya Korea na kati ya Korea Kaskazini na Marekani na pia jinsi ya kupunguza silaha za nyuklia.

Baadaye walitia saini waraka wa makubaliano ambayo yatawezesha  kurudishwa kwa wafungwa na mateka katika nchi zao.

Katika kuupa umuhimu mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema kuwa umoja huo utatoa msaada wowote wa kuhamasisha makubaliano katika mkutano huo.
''Viongozi wawili, wanajaribu kujadiliana jinsi ya kufikia makubaliano ambayo yalileta sana utata mwaka jana, amani na suala la kusitisha nyuklia ndio vinabaki kuwa lengo kuu.

"Kama nilivyowaandikia mwezi uliopita kutahitajika ushirikiano wa hali ya juu na kutakua na changamoto za hapa na pale katika makubaliano, Marekani wanatakiwa kusimamia kwa vyovyote," amesema Guterres.

Singapore ni nchi ya tatu ambayo Kim Jong-Un ameitembelea tangu alipokuwa Kiongozi mwaka 2011.
Safari yake ya kwanza ilikuwa nchini China Machi na Aprili akawa kiongozi wa kwanza wa Korea Kaskazini kutembelea Korea Kusini ambapo alikutana na Moon Jae-in. 

Na mkutano huo na Trump unatarajia kufungua njia itakayowezesha kuondolewa kwa vikwazo mbalimbali ilivyowekewa nchi yake ya Korea Kaskazini.

MICHUZI TV: NAIBU WAZIRI WA KILIMO AKILI KUPOKEA MAAGIZO YA KAMATI YA KILIMO MIFUGO ...


KILIMO CHA UMWAGILIAJI TATUZI MUAFAKA LA CHANGAMOTO ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI.

$
0
0
Mwandishi Maalum - Dar es Salaam

Imeelezwa kuwa Kilimo kinachotumia teknolojia ya kisasa ya umwagiliaji ndiyo tatuzi muafaka la changamoto zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi katika sekta ya kilimo.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Uendelezaji wa Teknolojia ya Uwagiliaji Bwana. Anthon Nyarubamba, kutoka tume ya Taifa ya Umwagiliaji, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake.

Bw. Nyarubamba Amesema kuwa, Kilimo hiki cha Umwagiliaji kinatumia teknolojia ya kisasa ya njia ya matone ya maji pamoja na kuvuna maji ya mvua katika mwabwawa maalum, yaliyojengwa katika maeneo ya mashamba ya umwagiliaji, maji ambayo yanatumika kwa kilimo katika kipindi chote cha mwaka bila kujali upatikanaji wa mvua za msimu.

Aidha Bw. Nyarubamba aliendelea kusema kuwa , uvunaji huu wa maji ya mvua unapelekea kuzuia mafuriko mengi yanayosabishwa na kubadilika kwa hali ya hewa kunakoharibu kwa kiasi kikubwa miundombinu mingine kama vile madaraja na barabara.

“Serikali iongeze Rasilimali za kutosha katika kilimo cha umwagiliji, ili kuweza kujenga mabwawa ya kutosha kupokea maji katika maeneo yenye skimu za umwagiliaji na kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi, Alisisitiza.”


Sehemu Picha shamba la vitunguu lililopo katika eneo la skimu ya umwagiliaji la Mbalali Mkoani Mbeya.
sehemu ya Shamba la umwagiliaji lililopo katika skimu ya umwagiliaji ya Lemkuna Manyara.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Uendelezaji wa Teknolojia ya Uwagiliaji kutoka katika Tume ya taifa ya Umwagiliaji,Anthon Nyarubamba akifafanua jambo kuhusu kilimo cha umwagiliaji alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Dar es Salaam leo.

RAIS DKT MAGUFULI AKAGUA UJENZI WA MSIKITI WA BAKWATA KINONDONI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa  Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane alipokagua  maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
  Sehemu ya  msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa  na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally akimshukuru Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane   baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa  na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane  na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akimsikiliza  mjumbe wa Nyumba Kumi wa Konondoni Shamba Bw. Rashidi Mohamed Mashaushi anayeeelezea kuhusu changamoto ya barabara na mfereji wa maji eneo lao baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga wananchi  baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally aliye na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane  aliye  na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

SPIKA NDUGAI AONGOZA WABUNGE KUUAGA MWILI WA BABA MZAZI WA MBUNGE WA MANYONI MASHARIKI LEO KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai aongoza Waheshimiwa Wabunge katika kuuaga mwili wa Ndg. Mtuka Daniel Nguluba ambaye ni Baba Mzazi wa Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka katika tukio lililofanyika leo tarehe 12 Juni, 2018 katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wakibeba mwili wa Baba mzazi wa Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka aliefariki juzi  tarehe 10 Juni, 2018 katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma. Mwili huo uliagwa leo katika hospital hiyo Jijini Dodoma
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akimfariji  Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka baada ya kuondokewa na Baba yake mzazi aliefariki  juzi tarehe 10 Juni, 2018 katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge, ndugu, jamaa na marafiki waliofika katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma kabla ya kuuaga mwili wa Baba mzazi wa Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka katika tukio lililofanyika  leo tarehe 12 Juni, 2018  katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Spika wa Bunge, Job Ndugai (wa tatu kulia mbele), katibu wa Bunge, Ndg. Stephen kagaigai (kulia mbele) wakiwa pamoja na Waheshimiwa Wabunge, ndugu, jamaa na marafiki kabla ya kuuaga mwili wa Baba mzazi wa Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka aliefariki  juzi tarehe 10 Juni, 2018 katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma. ​
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

WAZIRI MKUU KUZINDUA KAMPENI YA FURAHA YANGU YA KUHAMASISHA KUPIMA VVU JUNI 19 MJINI DODOMA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kampeni ya Furaha Yangu yenye lengo la kuhamasisha huduma za kupima UVVU na kuanza ARV mapema.

Kampeni hiyo itakayozinduliwa rasmi Juni 19 mwaka huu mkoani Dodoma inaratibiwa na  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania(TACAIDS).

Akizungumzia uzinduzi wa kampeni hiyo leo Dar es Salaam Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Angella Ramadhan amesema kampeni ya kitaifa ya Furaha Yangu ni kampeni inayohamasisha mkakati mpya wa Serikali wa upimaji VVU na kuanza kutumia ARV mapema kwa wale watakaokutwa na VVU.

"Kupitia furaha yangu ujumbe wa Serikali ni kuwa kutambua hali yako ya VVU huleta amani, na kuanzishiwa ARV mapema kwa wale wenye VVU inawasaidia kuimarisha afya na kupunguza hatari ya kuambukiza VVU kwa wenza wao.

"Katika dira ya kuwa na Taifa bila Ukimwi, Tanzania imeridhia malengo ya UNAIDS ya 90-90-90:ambapo 90% ya watu wote wanaoishi na VVU kutambua hali zao za VVU.

"Asilimia 90 ya watu wote wenye VVU kuanza ARV, na asilimia 90 ya wote walioanza ARV kupunguza kiwango cha VVU mwilini, "amesema.

Ameongeza uzinduzi wa kampeni ya Furaha Yangu ambayo imekuwa ikiandaliwa kwa miezi kadhaa na Wizara kupitia NACP kwa kushirikiana na TACAIDS, mradi wa USAID Tulonge afya na wadau wengine ni mchango muhimu katika kutimiza malengo hayo.

"Waziri Mkuu ndio atazindua kampeni hii rasmi Juni 19 mwaka huu mkoani Dodoma ambayo pia itakuwa na siku tano za kutoa huduma za afya bila malipo ikiwemo huduma ya upimaji wa VVU kuanzia Juni 18 mwaka huu.

"Wizara kupitia NACP pamoja na TACAIDS inatoa mwito kwa wakazi wote wa Jiji la Dodoma na mikoa jirani kushiriki katika uzinduzi huu na kupima afya zao na kuonesha dhamira yao ya kumaliza VVU na Ukimwi nchini,"amefafanua.

Wakati huo huo Dk.Ramadhan ametoa shukrani kwa wanasayansia ambao wamekuwa wakiendelea kufanya tafiti kila siku zenye lengo la kuboresha utoaji huduma kwa wanaoishi na VVU.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TACAIDS Dk.Leonard Maboko ametoa ombi kwa wananchi wa makundi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika kampeni hiyo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kuhusu kasi ya watu kupima Ukimwi, Dk. Maboko amesema wanawake ndio wanaojitokeza zaidi kupima kuliko wanawaume na hivyo ametoa rai kwa wanaume kuhakikisha wanajenga tabia ya kupima ili wakibaini kuwa na Ukimwi waanze kutumia dawa kwa wakati.

Akizungumzia kampeni za kuhamasisha watu kupima Ukimwi amesema lugha zinazotumika kuhamasisha si za kutisha.

Ameeleza hivyo baada ya waandishi kutaka kufahamu matangazo yenye ujumbe wa kutisha yanachangia vipi kuogopesha watu kupima Ukimwi.

Ambapo amejibu kwa siku hivi mabango yenye kuzungumzia kampeni za Ukimwi hazina maneno ya kutisha akitolea mfano kampeni ya Furaha Yangu ambayo imeambatana na maneno mengine kama Pima, Jitambue, Ishi.

"Yale mabango yaliyokuwa yanasema kuwa Ukimwi unaua siku hizi hayapo tena. Hivyo mabango ya siku hizi yanamhamasisha mtu kutambua afya yake bila vitisho,"amesema Dk.Maboko.

Hata hivyo imeelezwa mbali ya kuzinduliwa mkoani Dodoma kampeni hiyo itafanyika maeno yote nchini.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonald Maboko, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa kampeni ya furaha ya yangu kuhamasisha huduma za kupima VVU na kuanza ARV mapema ambayo itazinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 19 jijini Dodoma.
 Kaimu Mkurugenzi wa Kinga toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Angela Ramadhani akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa kampeni ya furaha yangu ya kuhamasisha huduma za kupima VVU na kuanza ARV mapema ambayo itazinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 19 jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonald Maboko, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa kampeni ya furaha yangu kuhamasisha ya huduma za kupima VVU na kuanza ARV mapema ambayo itazinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 19 jijini Dodoma.
 Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonald Maboko (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya furaha yangu ya kuhamasisha huduma za kupima VVU na kuanza ARV mapema ambayo itazinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 19 jijini Dodoma.
Naibu Mkurugenzi wa Afya toka Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Bi. Ananthy Thambinayagan Ramadhani akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa kampeni ya furaha yangu ya kuhamasisha huduma za kupima VVU na kuanza ARV mapema ambayo itazinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 19 jijini Dodoma.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA BALOZI WA VATICAN NCHINI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Vatican Nchini Mhashama Askofu Mkuu Mrek Solezyriski Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Balozi wa Vatican Nchini Mhashama Askofu Mkuu Mrek Solezyriski baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Vatican Nchini Mhashama Askofu Mkuu Mrek Solezyriski baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018.

PICHA NA IKULU
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>