Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live

MSEMAJI WA JESHI LA POLISI AFANYA ZIARA KATIKA STUDIO ZA WANENE ENTERTAINMENT, ZILIZOPO MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Msemaji  wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Barnabas Mwakalukwa akizungumza na Mkurugenzi  Mtendaji wa Studio ya Wanene Entertainment Darsh Pandit alipotembelea Studio hiyo iliyopo Mikocheni  jijini Dar es salaam.  Picha na Jeshi la Polisi.
Msemaji  wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Barnabas Mwakalukwa akizungumza na mtayarishaji wa muziki wa Studio ya Wanene Entertainment Goncher, alipotembelea Studio hiyo iliyopo Mikocheni   jijini Dar es salaam.  Picha na Jeshi la Polisi.

TAARIFA KWA UMMA

RC KAGERA -VIONGOZI WA WILAYA WATOE USHIRIKIANO KUTAMBUA VIKUNDI ILI WANUFAIKE NA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII(NSSF)

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya Jamii Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera amewataka viongozi wote wa Wilaya kuhakikisha wanatoa ushirikiano katika kutambua vikundi vyote katika maeneo yao ili Mfuko wa Hifadhi ya jamii Taifa (NSSF) waweze kuwafikia na kuweza kuingia katika mpango wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu katika ufunguzi wa semina juu ya mpango wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi.

"Maafisa biashara na maafisa ushirika natambua mnazo orodha za vikundi vyote vilivyopo kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Mkoa niwaombe muwapatie hizo orodha NSSF na muwaunganishe na vikundi husika ili waweze kuwafikia wote na kuwapa elimu ya manufaa yanayopatikana iwapo watakuwa wanachama wa NSSF"alisema

Kinawilo aliwataka viongozi wote wa vikundi waliohudhuria semina hiyo kuhakikisha ujumbe unawafikia wale wanaowaongoza na kuandaa mazingira ambayo yatawawezesha kufikiwa na NSSF kwaajili ya kunufaika nayo.Alisema wajasiriamali wengi wamekuwa na kilio cha mitaji,na mara nyingi wanapoomba mikopo wanapewa kwa riba za juu kiasi cha kuwafanya washindwe kupata faida inayositahili na kushindwa kuendelea.

"Nimeelezwa mpango huu wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi hasa kwa wanachama wa saccos na waliojiunga NSSF ambao wapo katika vikundi vyenye sifa husika wanaweza kukopeshwa kupitia usimamizi wa benki ya Azania na NMB tunaomba mtoe mikopo kwa riba nafuu na kwakuwa wahusika mpo mtaje kiwango cha riba wazi hapa"alisema

Mariam Muhaji Mwenyekiti wa kamati ya kuratibu sera ya hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi alisema kuwa serekali ya awamu ya tano ni serekali inayomjali kila mtu hasa watu wa hali ya kipato cha chini,kwa kutambua umuhimu huo bunge limeshapitisha sheria mpya namba 2 ya mwaka 2018 inayoboresha hifadhi ya jamii nchini ambapo sheria hiyo imeacha mifuko miwili ambayo ni PSSSF na NSSF.

Alisema mpango huo una manufaa mengi ikiwemo kugharamia matibabu,kinga za majanga,pensheni za uzee mafao ya uzazi na mafao mengine muhimu.

"Tunafahamu zamani swala la hifadhi ya jamii lilikuwa linalenga waajiriwa na kuacha nje waliojiajiri,takwimu zinaonyesha wastani watu 2000 kati ya zaidi ya watanzania milioni 50 wanaopata huduma ya hifadhi ya jamii na katika nchi yetu walioajiriwa ni wachache ukilinganisha na wale waliojiajiri"alisema.
Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawilo akisoma hotuba yake kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu katika ufunguzi wa semina ya mpango wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi kwa viongozi wa vikundi vya wajasiliamali na vyama vya ushirika Mkoani Kagera.
Baadhi ya viongozi 82 wa vikundi vya ujasiliamari na vyama vya ushirika Mkoani Kagera wakifuatilia mada mbalimbali zinazotolewa kuhusu mpango wa hifadhi ya jamii kwa sekta zisizo rasmi.

MAJERUHI WA AJALI MEATU WASAFIRISHWA KWENDA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Madiwani tisa kati ya 11 wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu waliojeruhiwa katika ajali iliyotokea Juni 10, 2018 kwenye msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri James katika Kijiji cha Kisesa wilayani humo wametolewa katika Hospitali ya Rufaa Bugando baada ya kupatiwa matibabu ya awali na kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu na uchunguzi zaidi.

Madiwani hawa walisafirishwa  jana jioni wakisindikizwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu, ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka, viongozi wa CCM Mkoa wa Simiyu na viongozi wengine wa wilaya ya Meatu na Bariadi katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Wakizungumza kabla ya kuondoka Uwanja wa ndege wa Mwanza wametoa shukrani kwa madaktari  na wauguzi waliowahudumia toka siku kwanza katika kituo cha Afya cha Mwandoya, Hospitali ya Wilaya ya Meatu, Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu na Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa namna walivyowahudumia hali iliyochangia kuimarisha afya zao.

“Ninashukuru kwa matibabu ya awali niliyopewa Meatu na Bariadi  yamenisadia sana, baada yaajali nilikuwa na maumivu makali sana lakini kutokana na huduma niliyoipata nina nafuu, yamebaki maumivu  ya kifua kwa ndani” alisema Mhe. Pius Machungwa Diwani wa Kata ya Ngh’oboko ambaye pia  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.
 Diwani wa Kata ya Itinje wilayani Meatu Mhe.Seni Sitta  Mizumali ambaye ni miongoni mwa waliojeruhiwa katika ajali , kwenye Msafara wa Mweyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James wilayani Meatu akisaidiwa kuingia kwenye ndege kabla ya kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na viongozi wengine wakimsaidia Diwani wa Kata ya Mwamanongu wilayani Meatu Mhe.Emmanuel Sayi Mboje ambaye ni miongoni mwa waliojeruhiwa kwenye ajali ya Msafara wa Mweyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James wilayani Meatu kuingia kwenye ndege kabla ya kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumzana baadhi ya madiwani waliojeruhiwa kwenye ajali ya Msafara wa Mweyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James wilayani Meatu kabla ya kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na madiwani sita waliojeruhiwa kwenye ajali ya Msafara wa Mweyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James wilayani Meatu kabla ya kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi, madiwani watatu hawapo pichani kutokana hali za kutoruhusu kusimama walikuwa wameshaingizwa kwenye ndege.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akizungumza na Diwani wa Viti Maalum Consolatha Lushu  katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza kabla ya diwani huyo na wenzake kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SPRITE BBALL KINGS MSIMU WA PILI WAZINDULIWA, USAILI JUNI 16 MLIMANI CITY

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mashindano ya Mpira wa Kikapu ya Sprite BBall Kings yamezinduliwa jana usaili ukitarajiwa kufanyika Mei 16 mwezi huu katika Viwanja vya Mlimani City Mall Jijini Dar es salaam kuanzia majira ya saa 3 asubuhi hadi sa 10 jioni.

Kituo cha East African Television (EATV), East Africa Radio kwa kushirikiana na Kinywaji cha Sprite wameanzisha mashindano hayo kwa lengo la kuinua na kurejesha heshima ya mpira wa kikapu.

Mashindano ya Sprite BBall Kings yanafanyika kwa mara ya pili ambapo mwaka 2017 ambapo timu ya Mchenga BBall Stars wakiondoka na ubingwa na kujinyakulia kitita cha Shiiling Milion 10 na kombe na mshindi wa pili akijinyakulia Milion 3 huku mchezaji bora wa mashindano (MVP) akipata Milion 2 na kikombe.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Masoko wa East Africa Television Basilisa Biseko amesema kuwa dhumuni kuu la mashindano haya ni kuutangaza na kuibua vipaji katika mchezo wa mpira wa kikapu nchini.

Basilisa amesema," mashindano haya yamelenga kuinua mchezo wa mpira wa kikapu hususani kwa vijana pia kurejesha heshima ya mchezo huu unaopendwa sana na watu".

"Nawashukuru sana TBF tulikua nao mwaka jana na mwaka tunaendelea tena kuwa nao katika kuhakikisha tunarejesha heshima ya mpira wa kikapu,"amesema Basilisa.

Meneja Mauzo wa Kinywaji cha Sprite Sialouise Shayo amesema kuwa hii ni fursa nzuri ya kuinua mpira wa kikapu nchini kupitia kwa vijana walioko mtaani.

Amesema kuwa kwa muda sasa Sprite wamekuwa wanatafuta vipaji vya mpira wa kikapu katika mashule ila kwa sasa vijana wote watashiriki kuupeleka mchezo wa kikapu mbele  na lengo kuu likiwa ni kusapoti mchezo huo.

Sialouise ameongezea na kusema kupitia mashindano haya watapata wachezaji wazuri zaidi hata ikiwemo kwenda kucheza nje ya nchi

Kwa upande wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini, Katibu Mkuu Mike Mwita amesema kuwa aanawashukuru sana EATV kwa kuanzisha mashindano haya yanayofanyika kwa mara ya pili na anaamini awamu hii yatakuwa mazuri zaidi.

Mwita ameongezea kuwa mwamko kwa mwaka huu umekuwa mkubwa sana ingawa kulikuwa na changamoto ila liliweza kutatuliwa na mashindano kuendelea huku akitoa ushauri kwa EATV na Sprite kupeleka mashindano hayo mikoani.

Katika usaili wa timu siku hiyo, atahitajika kufika nahodha wa timu husika akiwa na majina ya wachezaji wasiopungua 10, wakiwa ni raia wa Tanzania na wenye umri usiopungua miaka 16 pamoja na kwenye kikosi chao wasizidi wachezaji watatu wa ligi daraja la kwanza nchini.

Mashindano hayo yatakuwa na hatua kuu sita ambazo usaili, kufuzu, kumi na sita bora, robo fainali, nusu fainali  na fainali.
Afisa Masoko wa East Africa Television ( EATV)  Basilisa Biseko (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa mpira wa kikapu nchini wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Sprite BBall Kings 2018 ikiwa ni kwa mwaka wa pili yanayotarajiwa kuanza mwishoni kwa mwezi June, kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF) Mike Mwita na Kushoto ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Vinywaji ya Sprite Sialouise Shayo.

DKT TIZEBA AFUNGUA MASOKO YA TUMBAKU KITAIFA WILAYANI KAHAMA

$
0
0
Na Mathias Canal, WK, Kahama-Shinyanga

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amefungua masoko ya tumbaku Kitaifa huku akitoa onyo kali kwa wakulima waliolima zao hilo nje ya mfumo wa ushirika kwa mujibu wa sheria ya zao hilo kwa kuwataka kuacha mara moja kwani serikali itashughulika na wote wanaokiuka taratibu za kilimo hicho.

Dkt Tizeba ameyasema hayo leo 12 Juni 2018 katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga wakati akihutubia mamia ya wakulima wa tumbaku kwenye sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa.

Dkt Tizeba amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Zainabu Telack kufanya kikao na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Wilaya zote za Mkoa huo kuhakikisha wanazuia wananchi kulima nje ya mfumo wa ushirika kwa mujibu ya sheria ya zao la tumbaku.Alisema kuwa wigo wa soko la tumbaku unazidi kuwa finyu kutokana na viongozi mbalimbali kuwakumbatia baadhi ya wakulima wa tumbaku wanaolima nje ya mfumo wa zao hilo.

Katika sherehe hiyo Mhe Dkt. Tizeba amekabidhi vyeti vya pongezi kwa wakulima waliofanya vizuri katika msimu wa kilimo wa mwaka 2017/2018 ambao ni mkulima Emmanuel Cherehani kutoka Wilaya ya Ushetu aliyeshika nafasi ya kwanza, nafasi ya pili ni Jimson Mwanjwenga kutoka Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya na Jonas Blakali kutoka Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akimkabidhi cheti cha pongezi Mkulima Jonas Blakali kutoka Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita ambaye ameshika nafasi ya tatu katika msimu wa kilimo cha tumbaku wa mwaka 2017/2018 wakati wa sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.
Mgeni rasmi-Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akikata utepew kuashiria ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa katika sherehe iliyofanyika kwenye viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akishuhudia ununuzi wa tumbaku wakati wa sherehe za ufunguzi wa masoko ya tumbaku Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Mwendakulima Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, leo 12 Juni 2018.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MGENI RASMI KAMPENI YA UPIMAJI VIRUSI VYA UKIWMI

HESHIMA YA MJUMBE CCM YASABABISHA RAIS KUTOA MAAGIZO UJENZI WA BARABARA KINONDONI SHAMBA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli ametoa maagizo kwa Wakala wa Barabara ya Vijijini (TARURA)wilayani Kinondoni Dar es Salaam kujenga barabara inayounganisha Kinondoni Shamba na Biafra jijini.

Amesisitiza baada ya kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo Rais ametaka ipewe jina la Rashid Mashaushi ambaye ni mjumbe wa CCM mtaa wa Kinondoni Shamba ambaye ndio aliyetoa ombi la ujenzi wa barabara hiyo kwa Rais.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam baada ya kutoka kukagua ujenzi wa Msikiti unaojengwa katika Makao Makuu ya Baraza la Waislam Tanzania(Bakwata) ambapo pia alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Kinondoni.

Hivyo akiwa anazungumza na wananchi hao ndipo Mjumbe wa CCM mtaa wa Kinondoni Shamba aliejitambulisha kwa jina la Rashadi Mashaushi alipomuomba Rais kuangalia namna ya kuwasaidia  ujenzi wa barabara hiyo.

Baada ya Rais Magufuli kumsikiliza Mashaushi alitoa maagizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuchukua namba ya mjumbe huyo ili aweze kuwasiliana naye na kumuonesha eneo ambalo atanataka litengenezwe.

Hivyo Rais akatoa agizo hapo hapo kwa Mfuko wa Barabara Kinondoni kuhakikisha wanaanza ujenzi wa barabara hiyo na ikikamilika kwa heshima ya mjumbe huyo wa CCM ipewe jina la Rashidi.

Awali Rashid wakati anazungumza mbele ya Rais amemueleza wananchi wa Kinondoni Shamba wanasumbuliwa na mafuriko huku akiomba pia kujengwa kwa barabara hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akimsikiliza mjumbe wa Nyumba Kumi wa Konondoni Shamba Bw. Rashidi Mohamed Mashaushi anayeeelezea kuhusu changamoto ya barabara na mfereji wa maji eneo lao baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Juni 12, 2018.PICHA NA IKULU.

TANROAD YADAIWA KUKWAMISHA MRADI KUFUNGULIWA

$
0
0
Wakala wa barabara Mkoani Ruvuma TANROAD walikwamisha mradi wa ujenzi wa Daraja mto Litete lililopo katika kijiji cha Mkongo Gulioni wilayani Namtumbo liweze kufunguliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Charles Fransis Kabeho.

Akitoa maelezo ya kutofungua mradi huo kwa mkuu wa wilaya ya Namtumbo kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge kitaifa alisema kuwa hawezi kufungua mradi huo kutokana na kumkosa mtu sahihi wa kumwuliza maswali ili aweze kujiridhisha na ujenzi wa daraja hilo .

Bwana Kabeho aliongeza kwa kumwambia mkuu wa wilaya kuwa haiwezekani kufungua mradi wakati wahusika waliojenga Mradi hawapo katika mradi wao na kina nipa wasiwasi kwa nini hawajafika katika mradi wao na mimi kukosa kujiridhisha kwa maswali ambayo ningeweza kuwauliza alisema Kabeho.

Pamoja na kukagua mradi wa ujenzi wa Daraja hilo alitaka kuwauliza maswali wahusika wa mradi TANROAD ambao hawakujitokeza kuhudhuria ufunguzi wa daraja hilo na kuwashangaza wananchi wa kijiji cha Mkongo ambao walitegemea daraja hilo liweze kufunguliwa.

RAIA 19 WA CHINA, WATANZANIA SITA KORTINI KWA TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii

RAIA 19 wa China na watanzania sita, wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka ya uhujumu uchumi.

Washtakiwa hao wanashtakiwa chini ya vifungu vya sheria ya uhamiaji, chini ya sheria ya watu ambao siyo raia wa Tanzania na uhujumu uchumi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shaidi washtakiwa hao walitajwa kuwa ni, Bo Song, Liu Yunley, Chen Chao Hui, Fu Zeng, Wu Hai Quing, Ke Qiu Fang na Frederick Kumalija.

Wengine Jing Jing Lin, Ku Liao, Yan Yan Geng, Chen Ying Gong, Salim Mahsein Al-Amry, George Elikana, Fatuma Songoro, Bhoke Mwita, Kelvin Ponela, Chen Gwandi, Lin Ben, Rui Guo, Lin Xiangqui, Chen Fa, Wan Li, Robert Mkini na Revocatus Mugisha.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa  Serikali Patrick Mwita akisaidiana na Shedrack Kimaro alidai, kati ya Juni 1 mwaka 2017 na Mei 18 mwaka 2018 walitenda kosa la kwanza, ambapo wanadaiwa siku hiyo, chini ya sheria ya watu ambao siyo raia wa Tanzania, walitoa taarifa za uongo kwa lengo la kupata kibali cha kufanya kazi nchini.

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Kilimo Mary Mwanjelwa, Bungeni jijini Dodoma  Juni 12, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika, Stephen Masele ambaye ni Mbunge wa Shinyanga Mjini, Bungeni jijini Dodoma  Juni 12, 2018. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba, akizungumza Bungeni jijini Dodoma  Juni 12, 2018. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiteta jambo na Mbunge wa Katavi, Inj. Gerson Lwenge Bungeni jijini Dodoma  Juni 12, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mbunge wa Kilindi, Omari Kigua kwenye viwanja vya  Bunge jijini Dodoma  Juni 12, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwanafunzi Isack Chidodolo wa shule Chinangali Sekondari Dodoma, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma  Juni 12, 2018. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mbunge wa Moshi vijijini,Anthony Komu, kwenye viwanja vya  Bunge jijini Dodoma  Juni 12, 2018, katikati ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mbunge wa Kasulu mjini, Daniel Nsanzugwanko, nje ya jengo la utawala Bungeni jijini Dodoma  Juni 12, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mawakala Halo pesa sasa kuweka na kutoa fedha kupitia NMB

$
0
0
Katika kutekeleza azma ya  kuboresha utoaji huduma za kifedha kwa wananchi wenye vipato tofauti,  Kampuni ya mawasiliano ya Halotel na benki ya NMB zimeingia katika ushirikiano  utakao wawezesha mawakala wa Halo Pesa kutumia huduma za kibenki za NMB kupitia "huduma kabambe kwa Wakala" (Super-Agency service.) kwa ajili ya kuweka na kutoa fedha kupitia benki hiyo.

Hatua hii itawawezesha mawakala wote wa huduma za kifedha kupitia Halo Pesa  nchi nzima kuweza kuweka na kutoa pesa taslim kupitia tawi lolote la benki ya NMB na kuweza kuwanufaisha mamilioni ya watanzania na huduma za kifedha  kwa njia ya mtandao kwa ukaribu na urahisi zaidi.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Halo Pesa, Vu Tuan Long, amesema Ushirikiano huo ni hatua nyingine kubwa katika utoaji wa huduma za kifedha kupitia mawakala  ambapo sasa  huduma ya  kutoa na kuweka pesa kwa mawakala zitafanyika kupitia benki ya NMB.

"Huduma za   kifedha  kwa njia ya mtandao ni  sekta  inayokua  kwa  kasi hapa  nchini. Ushirikiano huu utawawezesha Mawakala wa Halo Pesa kuweza kupata huduma ya kuweka na kutoa pesa kiurahisi kupitia matawi yote ya NMB nchi nzima “Alisema Long.

Mpaka hivi sasa Halotel ina mawakala zaidi ya 55,000 walioenea nchi nzima. Mawakala wa HaloPesa watatumia namba za USSD za Halo Pesa ambazo ni (*150*88#) kwa kutoa fedha katika benki ya NMB pamoja na kutoa fedha, kwa fomu maalumu za kuweka fedha wakiwa katika matawi ya benki ya hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa wateja wa kati na wadogo wa benki ya NMB Boma Raballa, amesema benki ya hiyo imekuwa ya kwanza katika kutoa huduma zenye ubunifu ambazo zinalenga kutatua changamoto mbalimbali ndani ya jamii, Tulitambua kuna uhitaji katika upatikanaji wa fedha kwa mawakala” Alisema Raballa.

“Mtandao mkubwa wa matawi yetu unaoenda sambamba na kauli mbiu yetu ya “Karibu Nawe” imekuwa sehemu kubwa ya mafanikio katika utoaji wa huduma za kifedha. Hadi sasa tuna matawi Zaidi ya 220 ambayo yako kwa Zaidi ya asilimia 98 ya wilaya za nchi hii zitarahisisha sana upatikanaji wa huduma kwa mawakala”. Alisema Raballa.

Nchi ya Tanzania ni miuongoni mwa nchi zinazoripotiwa kuwa na watumiaji wengi wa huduma za kifedha wakifikia Takribani milioni 19, hivyo uhitaji na upatikanaji wa fedha kwa watumiaji hao imekuwa ni changamoto kubwa kwa baadhi ya watumiaji, Kupitia benki ya NMB sasa mawakala na watoa huduma za kifedha sasa watakuwa na nafasi ya kupata huduma karibu yao.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel Mhina Semwenda akitoa ufafanuzi  mbele ya mkutano wa waandishI wa Habari katika  uzinduzi wa kusaini  mapatano ya ushirikiano baina ya Halotel (Halopesa) na benki ya NMB, utakao wawezesha mawakala wa Halopesa nchi nzima kutumia huduma za kibenki (kutoa na kuweka pesa) kupitia tawi lolote la benki ya NMB . Kushoto  ni Kaimu mkuu wa wateja wa kati na wadogo  kutoka benk ya NMB.
aibu Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma za kifedha Vu Tuan Long(kulia) na Kaimu Mkuu wa wateja wa kati na wadogo wa benki ya NMB wakibadilishana mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika  uzinduzi wa kusaini  mapatano ya ushirikiano baina ya  Halotel (HALOPESA) na benki ya NMB. Ambapo mawakala wa Halopesa wataweza kupata huduma za kifedha kupitia tawi lolote la NMB nchini. (Kulia) Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda, (kushoto) moja ya mwakilishi kutoka Benki ya NMB

SPRITE BBALL KINGS MSIMU WA PILI WAZINDULIWA, USAILI KUFANYIKA JUNI 16 MLIMANI CITY

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 

MASHINDANO ya Mpira wa Kikapu ya Sprite BBall Kings yamezinduliwa jana huku usaili ukitarajiwa kufanyika Mei 16 mwezi huu katika Viwanja vya Mlimani City Mall Jijini Dar es salaam kuanzia saa 3 asubuhi hadi sa 10 jioni.

Kituo cha East African Television (EATV), East Africa Radio kwa kushirikiana na Kinywaji cha Sprite wameanzisha mashindano hayo kwa lengo la kuinua na kurejesha heshima ya mpira wa kikapu.Mashindano ya Sprite BBall Kings yanafanyika kwa mara ya pili ambapo mwaka 2017 timu ya Mchenga BBall Stars wakiondoka na ubingwa na kujinyakulia kitita cha Sh.Milion 10 na kombe na mshindi wa pili akijinyakulia Milion 3 huku mchezaji bora wa mashindano (MVP) akipata Milion 2 na kikombe.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Masoko wa East Africa Television Basilisa Biseko amesema kuwa dhumuni kuu la mashindano haya ni kuutangaza na kuibua vipaji katika mchezo wa mpira wa kikapu nchini.Basilisa amesema," mashindano haya yamelenga kuinua mchezo wa mpira wa kikapu hususani kwa vijana pia kurejesha heshima ya mchezo huu unaopendwa sana na watu.

"Nawashukuru sana TBF tulikua nao mwaka jana na mwaka tunaendelea tena kuwa nao katika kuhakikisha tunarejesha heshima ya mpira wa kikapu,"amesema Basilisa.Meneja Mauzo wa Kinywaji cha Sprite Sialouise Shayo amesema kuwa hiyo ni fursa nzuri ya kuinua mpira wa kikapu nchini kupitia kwa vijana walioko mtaani.

Amesema kwa muda sasa Sprite wamekuwa wanatafuta vipaji vya mpira wa kikapu katika mashule ila kwa sasa vijana wote watashiriki kuupeleka mchezo wa kikapu mbele  na lengo kuu likiwa ni kusapoti mchezo huo.Sialouise ameongezea na kusema kupitia mashindano haya watapata wachezaji wazuri zaidi hata ikiwemo kwenda kucheza nje ya nchi.

Kwa upande wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini, Katibu Mkuu Mike Mwita amesema kuwa aanawashukuru EATV kwa kuanzisha mashindano haya yanayofanyika kwa mara ya pili na anaamini awamu hii yatakuwa mazuri zaidi.Mwita ameongezea kuwa mwamko kwa mwaka huu umekuwa mkubwa sana ingawa kulikuwa na changamoto ila liliweza kutatuliwa na mashindano kuendelea huku akitoa ushauri kwa EATV na Sprite kupeleka mashindano hayo mikoani.

Katika usaili wa timu siku hiyo, atahitajika kufika nahodha wa timu husika akiwa na majina ya wachezaji wasiopungua 10, wakiwa ni raia wa Tanzania na wenye umri usiopungua miaka 16 pamoja na kwenye kikosi chao wasizidi wachezaji watatu wa ligi daraja la kwanza nchini.Mashindano hayo yatakuwa na hatua kuu sita ambazo usaili, kufuzu, kumi na sita bora, robo fainali, nusu fainali  na fainali.
Afisa Masoko wa East Africa Television ( EATV)  Basilisa Biseko (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa mpira wa kikapu nchini wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Sprite BBall Kings 2018 ikiwa ni kwa mwaka wa pili yanayotarajiwa kuanza mwishoni kwa mwezi June, kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF) Mike Mwita na Kushoto ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Vinywaji ya Sprite Sialouise Shayo.

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI OMBI LA UPANDE WA UTETEZI KESI YA AKINA MBOWE, WENZAKE

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jami

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali ombi la upande wa utetezi katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema na wenzake saba lililokuwa linatoa taarifa ya kusudio la kukata rufaa dhidi ya uamuzi mdogo uliotolewa mahakamani hapo jana.

Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa mashtaka Juni 11mwaka 2018 kuamuriwa na Mahakama wafanye marekebisho katika hati ya mashtaka baada dhidi ya washtakiwa hao badaa ya hati hiyo, kuonekana kuwa na mashtaka batili na yenye mapungufu ya kisheria.

Kutokana na kutupwa kwa kusudio hilo la kukata rufaa, washtakiwa hao wamesomewa mashtaka mapya 13 na na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.


WAZIRI JAFO: MABARAZA YA BIASHARA NI CHACHU YA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0
Uwepo wa Mabaraza ya Biashara nchini unachochea azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania inakuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati.

Haya yamebainishwa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo wakati wa akifungua warsha ya viongozi wa ngazi ya Mikoa na Wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara iliyoandaliwa na Mradi wa uboreshaji mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini (LIC) kwa kushirikiana na TAMISEMI.

"Mabaraza ya biashara ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi yetu hivyo ni vyema kuendelea kuimarisha vyombo hivi vya majadiliano na kupanga mipango ya pamoja kati ya Serikali na Sekta Binafsi,"alisisitiza Jafo.Warsha hiyo ya siku mbili imelenga kuwajengea uwezo viongozi hao ili kutambua fursa na umuhimu wa mabaraza hayo katika kujenga uchumi imara.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge amepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi kwa kuandaa warsha kama hizo ambazo zinasaidia kuwaongezea na kuwajengea uwezo pamoja na kuvutia wawekezaji nchini.

"Mkoa wa Dodoma tumeweza kutumia fursa kupitia warsha hizi na zimesaidia uwekezaji kuongezeka katika sekta ya kilimo cha Alizeti na Zabibu, ambapo viwanda vidogo vidogo vya kuchakata mafuta ya alizeti na vinywaji vya mvinyo vimeweza kufunguliwa," alisisitiza Dkt. Mahenge

Naye Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TNBC), Bi. Oliver Ligula amesema kuwa semina hiyo itasaidia kuwajengea uwezo viongozi hao wa Mikoa na Wilaya pamoja na wadau mbalimbali juu ya fursa zitokanazo na mabaraza hayo ya biashara.

“Baraza la Taifa la Biashara kwa kushirikiana na TAMISEMI na wadau mbalimbali wameweza kushiriki katika semina hii ambayo itawajengea uelewa wadau na sekta binafsi ili kuweza kuleta maendeleo ya pamoja na yenye ufanisi.” alisema Bi. Ligula.

Mabaraza ya Biashara Tanzania yalianzishwa kwa mujibu wa Wakala wa Rais Na.1 wa mwaka 2001 na kuchapishwa katika Gazeti la Serikali Na.691 la tarehe 28Septemba, 2001.Madhumuni ya kuanzishwa kwa Mabaraza haya ni kuunda jukwaa la majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta ya Biashara katika kila jukwaa la utawala ili kujadiliana namna bora ya kuboresha mazingira ya boashara na uwekezaji Nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR -TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha ya viongozi wa ngazi za Mikoa na Wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara ya mikoa ya Dodoma na Kigoma Juni12, 2018 Jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya viongozi wa ngazi za Mikoa na Wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara ya mikoa ya Dodoma na Kigoma Juni12, 2018 Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR -TAMISEMI), Selemani Jafo akipitia nyaraka wakati wa ufunguzi wa warsha ya viongozi wa ngazi za Mikoa na Wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara ya mikoa ya Dodoma na Kigoma Juni12, 2018 Jijini Dodoma.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa toka TAMISEMI,Charles mhina.


Baadhi ya washiriki wa warsha ya viongozi wa ngazi za mikoa na wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara ya mikoa ya Dodoma na Kigoma wakifuatilia hafla ya uziduzi wa warsha hiyo leo Juni12, 2018 Jijini Dodoma.

Mwezeshaji wa warsha ya viongozi wa ngazi za mikoa na Wilaya kuhusu uendeshaji wa Mabaraza ya Biashara ya Mikoa ya Dodoma na Kigoma, Profesa Lucian Msambichaka akiwasilisha mada kuhusu nafasi ya Sekta ya Umma katika kuboresha mazingira ya biashara leo Juni12, 2018 Jijini Dodoma.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

CHINA YAIOMBA TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA KIDUNIA WA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeombwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa kidunia wa viongozi wa vyama vya kisiasa, maombi haya yamewasilishwa na Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke alipotembelea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba kuonana na Ndg. Bashiru Ally Kakurwa, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Balozi Wang Ke amefika Ofisi Ndogo za CCM kumletea Ndg. Bashiru Kakurwa ujumbe wa salamu za pongezi kwa kuteuliwa na Ndg. John Pombe Joseph Magufuli, Mwenyekiti wa CCM na kwa kauli moja kuchaguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Katika salamu zake Balozi Wang Ke ameeleza China na Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) kinampongeza Ndg. Bashiru na kwamba wako tayari kushirikiana naye katika masuala mbalimbali kama sehemu ya mahusiano ya muda mrefu kati ya Tanzania na China na vyama vya CCM na CPC. Aidha, Balozi Wang ametumia mkutano huo kuwasilisha ombi la China kwa Chama Cha Mapinduzi kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kidunia wa Viongozi wa Vyama vya Siasa ambao kwa mara ya kwanza unafanyika barani Afrika na unaotarajiwa kufanyika mwezi wa Julai 2018.
Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) kimeichagua Tanzania na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mwenyeji wa mkutano huu mkubwa na wa kihistoria "CPC Dialogue with World Political Leaders in Africa". Mkutano huu wa kidunia unabeba kauli mbiu isemayo nadharia na vitendo katika kutambua njia sahihi za maendeleo ambazo ni endelevu na halisia kwa nchi zetu. Tunayo furaha na heshima kubwa kuwa na mkutano huu mkubwa Afrika na Tanzania kama sehemu ya Mpango wa kuiunganisha dunia kwa barabara na usafiri wa maji ulioasisiwa na Ndg. Xi Jinping Katibu Mkuu wa CPC na Rais wa China amesema Bi. Wang Ke.

Akipokea salamu hizo za pongezi Ndg. Bashiru Ally amemhakikishia Balozi Wang kwamba Chama Cha Mapinduzi kitaendeleza mahusiano ya kidugu na ya kihistoria kati ya CCM na CPC na nchi zetu mbili.
Tunataka kujifunza zaidi kutoka China na hasa namna ya kujipanga kimkakati katika kushughulika na kuendeleza mapambano dhidi ya dhuluma na unyonyaji ili nchi yetu iinuke na kuleta manufaa makubwa kwa watu wetu wa Tanzania. Ndg. John Pombe Joseph Magufuli, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayo kazi ya kujenga uchumi utakaowezesha kujitegemea, uchumi wa kitaifa, uchumi utakaowaondoa watanzania kutoka katika maisha ya umasikini kama China na kwa msingi huu kama Chama na Ilani tumejitambulisha kuhudumia wanyonge na kushughulika na shida za watu amesema Ndg. Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa CCM

Huu ni mwendelezo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuimarisha mahusiano ya ndani na ya nje katika eneo la siasa, diplomasia na uchumi.

Imetolewa na,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
OND LUMUMBA

Breaking news:: Kocha wa timu ya taifa ya Hispaniai kuinoa Real Madrid

$
0
0

Real Madrid CF imetangaza kwamba Julen Lopetegui atakinoa kikosi hicho cha kwanza kwa misimu mitatu ijayo.
Julen Lopetegui ataungana na timu hiyo baada ya michuano ya kombe la dunia, baada yakukinoa kikosi cha Hispania kwa miaka miwili.

RC MAKONDA AKABIDHI KADI 220 ZA BIMA YA AFYA KWA WATOTO YATIMA NA WAISHIO KWENYE MAZINGIRA MAGUMU

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda amekabidhi kadi 220 za Bima ya Afya (Toto Afya Card) zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 11 kwa watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu ili wapate uhakika wa matibabu mwaka mzima ikiwa ni sehemu ya Mwezi mtukufu wa Ramadhan. 

Makonda amekabidhi kadi hizo leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema kwa kawaida Mwezi wa Ramadhan watu wamekuwa wakifuturisha watoto yatima lakini inakuwa ni chakula cha siku moja kwa hiyo katika mwendelezo wa mwezi mtukufu ameona ni vyema aguse maisha ya watoto yatima kwa kuwapatia Bima ya Afya.
Aidha  Makonda amesema kadi hizo zitawawezesha watoto kupatiwa matibabu Bure kwa kipindi cha mwaka mmoja katika Hospital yoyote hapa nchini.
Makonda amesema watoto waliopatiwa kadi hizo hawahusiani na wale waliojitokeza kwenye mchakato wa kutafuta haki ya mtoto ambapo ameshukuru Hospital ya Regency na TMJ kwa kujitolea kutoa kadi hizo.

Pia Makonda amesema atakabidhi pia mabegi 400 yaliyosheheni vifaa vyote vya Shule kwa vituo vya watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu ili wawe na uhakika wa kupata masomo mwaka mzima na kuweza kutumia vyema fursa ya elimu bure.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospital ya Regency Dk. Kanabar Rajni na Mkurugenzi wa Hospital ya TMJ  Parul Chhaya wamesema wameguswa kutoa msaada huo Kama sehemu ya kuunga mkono hamasa anayoitoa RC Makonda kwa wazazi kuwa na kadi za bima za afya (Toto Afya Card).
Meneja Masoko na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Bima ya Afya Nchini Angela Mziray amesema kuwa ugonjwa hauna muda kwahiyo kupatikana kwa kadi hizi kutasaidia sana waotot hawa kuwa na uhakika wa tiba pindi pale wanapopata maradhi na watatibiwa katika hospitali yoyote nchini.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utoaji wa kadi za bima ya Afya ( Toto Afya Kadi) kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu katika vituo vya kulelea watoto yatima Jijini Dar es Salaam.

Meneja Masoko na Elimu kwa umma NHIF Angela Mziray akizungumza na waandishi wa habari na kuwashukuru hospitali ya Regency na TMJ kuweza kulipia kadi za bima ya Afya kwa watoto 220 wanaoishi kwenye mazingira magumu Jijini Dar es Salaam.
 Moja ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu akifurahi baada ya kupatiwa kadi yake ya Bima ya Afya leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwapatia kadi za bima ya Afya (Toto Afya Kadi) watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu  zilizotolewa na hospitali ya Regency na TMJ leo Jijini Dar es Salaam.

HARAMBEE KWA AJILI YA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA KIKAPU KANDA YA TANO KWA VIJANA

$
0
0

Let's walk the talk members...
Naomba kuwashirikisha wadau wote katika matukio yetu yajayo ya kikapu, naomba mjumuike nasi kufanikisha mashindano ya kimataifa ya kikapu ya kanda ya tano kwa timu za Taifa za vijana chini ya miaka 18 (FIBA ZoneV U18) 17-22 June 2018, yatakayofanyika hapa Dar es Salaam.

Kanda ya tano ina nchi 12 ; Egypt, Sudan, South Sudan, Eritrea , Ethiopia, Somalia, Djibouti, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania. 
Bingwa wa mashindano haya atapata tiketi ya kushiriki mashindano ya kutafuta bingwa wa Kikapu Mataifa ya Afrika (Afrobasket 2018). 

Tunahitaji fedha za kusaidia mashindano na kusaidia timu zetu za wanawake na wanaume kukaa kambini, jumla tunahitaji 100M. 

Corporate Sponsors karibuni na wachangiaji binafsi pia karibuni. Makundi mbali mbali ya kijamii eg. WhatsApp groups, Telegram groups, Facebook groups, Google groups etc mnakaribishwa kuratibu na kuchanga kimakundi na mnakabidhi pamoja, Admins watakabidhi kwa niaba ya kila kikundi. 

Pamoja tunaweza, ahsanteni na Mungu awabariki wote kwa moyo wa upendo kwa vijana wetu na Taifa letu. 

Kwa mawasiliano na michango :
0713 /0784 /0767 618320. 
Phares Magesa, 
Rais, 
Tanzania Basketball Federation, magesa@hotmail.com
#WeAreBasketball

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA JUNI 12, 2018

Viewing all 110021 articles
Browse latest View live




Latest Images