Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110176 articles
Browse latest View live

DC MJEMA AIHIMIZA WAANDISHI WA HABARI KUZINGATIA WELEDI

$
0
0

Na Chalila Kibuda,Blogu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Sophia Mjema amewapongeza kazi kubwa inayofanywa na waandishi wa habari katika kuuhabarisha umma wa Watanzania ila amehimiza pia waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi, kanuni na taratibu.


Mjema ametoa kauli hiyo jana Dar es Salaam wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari ambapo ametumia nafasi hiyo kuelezea umuhimu wa vyombo hivyo katika maendeleo ya nchi yetu.

Maadhimisho hayo yamefanywa na Jukwaa la Waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam kwa kukutana na kujadili masuala ya mbalimbali yanayoikumba tasnia ya habari.Kwa kukumbusha tu maadhmisho hayo duniani huadhimishwa kila ifikapo Mei 2 na 3 ya kila mwaka.

Mjema amehimiza pia waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi, kanuni na taratibu.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Waandishi wa habari Jane Mihanji amesema wanahabari wanaomba kulindwa ili watekeleze majukumu yao kwa uhuru zaidi.
Aidha changamoto ambazo zimeelezwa ikiwemo ya kukosa uhuru wa kufanya kazi ni vema nayo ikapatiwa ufumbuzi .

WAZAZI WAHIMIZWA KUWAINGIZA WATOTO WAO KWENYE MPANGO WA TOTO AFYA KADI KWA UHAKIKA WA MATIBABU

$
0
0

Na Editha Karlo wa blog ya jamii, Karagwe.

WAZAZI na walezi Mkoani Kagera katika kuelekea msimu wa sikukuu wametakiwa kuhakikisha wanawapatia watoto wao zawadi ya kuwaingiza kwenye mpango wa Toto afya kadi ili waweze kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua.

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheruka aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji wa Kadi za toto afya pamoja na upimaji wa afya bure kwa wananchi wa magonjwa yasiyoambukiza zoezi lililofanyika katika stand ya magari ya Omurushaka Wilayani Karagwe.

Mheruka alisema kuwa mzazi au mlezi kumpatia mtoto zawadi ya kadi ya toto afya ni muhimu badala ya kumpatia zawadi ya nguo ambazo atazivaa na zitaisha."Ndugu zangu wazazi wenzangu baada ya kumaliza kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani zawadi nzuri ya kuwapatia watoto wetu ni kuwaingiza katika mpango huu wa toto afya kadi kwani utamuwezesha mtoto kuwa na uhakika wa matibabu anapougua kwa kipindi cha mwaka mmoja"alisema Mkuu wa Wilaya

Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa wataendelea kuhimiza wananchi waweze kuingiza watoto wao katika mpango huo.Meneja wa Mfuko wa bima ya Taifa ya afya(NHIF)Elias Odhiambo alisema kuwa wiki hii NHIF wanafanya zoezi la upimaji wa afya wananchi bure na kutoa toto afya kadi katika maeneo ya Omurushaka na Kayanga Wilayani Karagwe.

Alisema kuwa magonjwa wanayopima wananchi ni uwiano wa uzito na refu(BMI)Kisukari,shinikizo la damu(BP)pamoja na kutoa ushauri.Odhiambo amewataka wananchi wa Wilaya ya Karagwe kutumia fursa hiyo kujua hali za afya zao sambamba na kupata elimu ya kujikinga na maradhi lakini pia kujiunga na mfuko huo."Nawaomba wananchi wote wafike maeneo ambayo tumeweka vituo kwaajili ya tutoa huduma ili waweze kupata huduma kwani huduma hizi tunatoa bure"alisema

Alisema huduma ya toto afya kadi inahusisha watoto wenye umri chini ya miaka 8,ambapoatatakiwa kujaza fomu zinazopatikana nchi nzima chini ya uangalizi wa mzazi au mlezi.Alisema mwanachama wa toto afya kadi atapata huduma zote ambazo mwanachama wa NHIF ambazo anapata na ambazo zimeorodheshwa katika huduma.Baadhi ya wananchi waliofika katika uzinduzi huo wameupongeza mfuko wa bima ya afya kwa jitihada zake za kuwafikia na kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.

"Mfuko huu umetusaidia kutuletea hii huduma ya upimaji wa afya kwani inatusaidia kujua afya zetu lakini pia tunapata fursa ya kuujua vizuri mfuko na huduma zake ambazo ndo mkombozi wa maisha ya kila mwananchi,tunaomba huduma kama hizi ziwe endelevu"alisema Edson Kamugisha.
Meneja wa mfuko wa bima ya afya Taifa(NHIF)Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akiongea jambona wananchi(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa afya bure kwa magonjwa yasiyoambukiza na utoaji wa toto afya kadi katika stand ya magari ya Omurushaka Wilayani Karagwe.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheruka akimkabithi kadi ya toto afya kadi mmoja wa watoto waliopatiwa kadi katika zoezi la uzinduzi wa kupima afya bure na utoaji wa toto afya kadi kwenye stand ya magari ya omurushaka Wilayani Karagwe
Ofisa matekelezo kutoka mfuko wa bima ya Taifa Mkoa wa Kagera Adam Kanza akiongea na wananchi katika stand ya magari ya Omurushaka juu ya umuhimu wa kuwakatia watoto wao toto afya kadi
Baadhi ya Wananchi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo.

Minister Mhagama to Officiate National Dialogue on Local Participation for Effective Industrialisation

$
0
0

Minister of State in the Prime Minister’s Office, Policy, Parliamentary Affairs, Labour, Employment, Youth and the Disabled, Hon. Jenista Joakim Mhagama (pictured ) will officiate a National Roundtable Dialogue on Enhancing Local Content and Local Participation for Effective Industrialisation in Tanzania today.
The event, which will run for two days from the 24th-25th May, 2018, is organised by UONGOZI Institute in collaboration with the National Economic Empowerment Council (NEEC) in the Prime Minister’s Office.

According to a statement released by UONGOZI Institute, the objective is to create a common understanding among key stakeholders on the concept of local content and local participation, and how it can be used to promote the country’s industrialization agenda.

The organisers intend to use the contributions and recommendations from the Dialogue to inform a draft local content strategy by NEEC, “National Multi-Sector Local Content Strategy”, which has a vision of ensuring that the majority of Tanzanians participate, own and benefit from investments.  
The two-day event will include high level government officials, private sector and civil society representatives from across Tanzania.

USAJILI KWA VIJANA WA JKT/JKU WALIOOMBA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI KUANZA LEO

SERIKALI YA MTAA UPANGA YAJIVUNIA UHALIFU KUPUNGUA KWA ASILIMIA 85

$
0
0
SERIKALI ya Mtaa ya Upanga Mashariki Dar es Salaam imesema vitendo vya uhalifu katika mtaa huo kwa sasa vimepungua baada kuanzishwa ulinzi shirikishi wa bodadoda wa mtaa huo. 

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Rukiya Ritani amesema hayo leo kuwa wameanzisha Polisi jamii kwa kuwashirikisha madereva wa bodaboda ambao wanafanya kazi zao kwa umakini na hatimaye wamefanikiwa kupunguza uhalifu.

 "Iwapo atapatikana mhalifu huwa wanamchukua na kumpeleka kituo cha Polisi ili sheria ichukue mkondo wake,"amesema Rukiya .

Amesema kwa sasa mafanikio makubwa ambayo yamepatikana wananchi wanaishi bila hofu yoyote na hata wanapopita barabarani usalama na mali zao ni mkubwa.Pia amesema mtaa huo una wakazi  4, 800  na changamoto iliyopo wanaolipa fedha kwa ajili ya ulinzi ni wachache , hivyo amewaomba wananchi kulipa fedha wa wakati.

Kwa upande wa Kiongozi  wa Ulinzi shirikishi Upanga Mashariki, Seleman Abdallah amesema uhalifu umepungua kwa asilimia 85.
Mwenyekiti wa Upanga Mashariki Rukiya Ritani, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuelezea mafanikio katika ulinzi Shirikishi  (Kushoto) kiongozi wa ulinzi wa mtaa huo Abdalah Seleman .

WANANCHI WA VIJIJI VYA LITISHA, MDUNDUALO NA LUGAGARA SONGEA MKOANI RUVUMA WATOLEA UFAFANUZI WA KUFUNGWA VITUO VYA AFYA

$
0
0
Wananchi wa vijiji vya Litisha, Mdundualo na Lugagara katika halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, wamekanusha taarifa zilizosambaa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba kuna zahanati zao zimefungwa kwa kukosa wahudumu wa Afya na nyingine kufunguliwa duka.

TAARIFA KUTOKA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Mufti ahimiza uadilifu futari ya Standard Chartered

$
0
0
Na mwandishi wetu
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally amesema Waislamu na walimwengu kwa ujumla wananafasi kubwa ya kujifunza mawaidha yanayotolewa katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwamo kumcha Mungu na uadilifu.

Mufti alisema hayo kwenye futari iliyoandaliwa na benki ya Standard Chartered katika hoteli ya Serena.

Alisema katika hafla hiyo ambayo pia walikuwemo wageni wastahiki Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mheshimiwa Prof. Dk. Ratlan Pardede na Balozi wa Heshima wa Siera Leone nchini Tanzania, Hussein Hamadi, kuwa mwezi wa Ramadhani ni chuo ambacho kinafunza mambo mbalimbali.

Alisema mafunzo hayo yanatarajiwa kutumika muda wote katika miezi 11 iliyobaki katika mwaka.

Alisema mambo ambayo yanazungumzwa katika Chuo hicho ni mengi lakini makubwa ni mahusiano katika masuala ya kiroho, kijamii, kiuchumi na kimaadili.

Alisema mafunzo yanayopatikana katika mwezi huo mmoja wa kumcha Mungu wenye siku takribani 29 hadi 30 yanatengeneza uaminifu si kwa Mungu pekee bali na kwa viumbe wake.
 Mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally akitoa mawaidha kwa wateja wa benki ya Standard Chartered wakati wa futari iliyoandaliwakwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akizungumza na wateja pamoja na wageni waalikwa wakati wa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Indonesia nchini, Prof Dk Ratlan Pardede akizungumza na wateja wa benki ya Standard Chartered wakati wa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Heshima wa Siera Leone nchini, Mh. Hussein Hamadi akitoa salamu za mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa wateja wa benki ya Standard Chartered wakati wa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akibadilishana mawazo na mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally (kulia) wakati wa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki ya Standard Chartered katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Kutoka kulia kwenda kushoto ni Mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani, Balozi wa Indonesia nchini, Prof Dk Ratlan Pardede pamoja na Balozi wa Heshima wa Siera Leone nchini Hussein Hamadi wakiwa meza kuu wakati wa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Pichani juu na chini ni baadhi ya wateja na wadau wa benki ya Standard Chartered waliohudhuria futari iliyoandaliwa na benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

 Mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally katika picha ya pamoja na meza kuu na baadhi ya viongozi wa Bakwata mara baada ya kumalizika kwa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki ya Standard Chartered katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS AJUMUIKA NA WATU MBALIMBALI MKOANI DODOMA WAKATI WA FUTARI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma Bi. Jamila Yusuph wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais jana jioni tarehe 23 Mei, 2018 kwenye makazi yake Ikulu Ndogo, Kilimani Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mtoto Samiri Abdallah wa kituo cha kulelea na kuwasomesha watoto yatima cha Zam Zam kilichoo Miyuji Dodoma wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais jana jioni tarehe 23 Mei, 2018 kwenye makazi yake Ikulu Ndogo, Kilimani Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) ​

Watendaji wanaochangia kuenea kipindupindu Rukwa kushughulikiwa

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesema hatamvumilia mtendaji wa serikali atakaechangia kuenea kwa ugonjwa kipindupindu katika mkoa kwani elimu ya ugonjwa huo imeshatolewa kwa muda mrefu hivyo ni jukumu la kila mtendaji kuhakikisha ugonjwa huo unatokomezwa.
Amesema kuwa kumekuwa na tabia iliyojengeka ya watendaji kuanza kufanya majukumu yao baada ya mlipuko wa ugonjwa huo kutokea na kuonya kuwa kaya ambayo haitakuwa na choo katika ngazi ya Kijiji basi mtendaji wa Kijiji atawajibishwa.

“Wakati hatua mbalimbali zikiendelea kuchukuliwa, tukikidhibiti kipindupindu halafu kikatokea tena hapo mahali ambapo kimetokea hatutapaelewa, watendaji wetu wakitilia maanani  wakahakikisha kaya zetu zina vyoo na kuchemsha maji hatuwezi kuwa na kipindupindu, sasa kinatokea kipindupindu halafu kaya haina choo, mtendaji wa Kijiji hicho hana sababu ya kuwa mtendaji,” Alisisitiza.

Ameyasema hayo alipokuwa akifunga kikao cha dharura kilichoitishwa na kamati ya afya ya mkoa ili kujadiliana juu ya mbinu za kutokomeza ugonjwa huo ambao umeathiri zaidi ya watu 600 tangu kulipukwa kwake mwezi November mwaka 2017 na kutoweka mwezi Machi mwaka 2018 na hatimae kuibuka tena tarehe 6, Mei mwaka 2018.

Kikao hicho kilichojumuisha, Wakuu wa ilaya, Wakurugenzi wa halmashauri, Wenyeviti wa halmashauri, madiwani, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na wilaya, Maafisa Afya wa mkoa na halmashauri, wataalamu wa afya pamoja na waganga wakuu wa wilaya na mganga mkuu wa mkoa kiliazimia kutokomeza ugonjwa huo na kuweka mikakati ya kutorejea tena wa ugonjwa huo.

Akisoma baadhi ya maazimio Katibu Tawala wa Mkoa Benard makali amesema kuwa kamati ya afya za vijiji na vitongoji zisimamiwe kutenda majukumu yake kwani wao ndio wanaojuana zaidi katika utekelezaji wa maagizo na sheria za serikali kuanzia ngazi hizo na kuitaka kamati za afya za Wilaya kuwa na mbinu za kudumu za kuthibiti ugonjwa huo na kutaka elimu zaidi iendelee kutolewa.

Tangu kulipuka tena kwa ugonjwa huo tarehe 6, Mei mwaka 2018 wagonjwa 9 wamefariki na wengine 214 wakiendelea kupatiwa matibabu katika vituo mbalimbali vya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ambayo imeathirika zaidi huku wananchi wake wakiwa na asilimia 36 ya umiliki wa vyoo bora.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo akitoa nasaha kuhusu ugonjwa wa Kipindupindu kwa wananchi wa kambi ya Nankanga iliyopo kwenye bonde la ziwa Rukwa.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akisoma dua ya kuliombea Bunge wakati wa kikao cha thelathini na sita cha mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri-TAMISEMI Mhe. Joseph Kakunda akitolea ufafanuzi swala la mapato ya halmashauri kwa ajili ya kinamama na vijana wakati wa kikao cha thelathini na sita cha mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango wakati wa kikao cha thelathini na sita cha mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiteta jambo na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani wakati wa kikao cha thelathini na sita cha mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.
 Wageni mbalimbali  wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu wakati wa kikao cha thelathini na sita cha mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma. Picha zote na Daudi Manongi, Dodoma.

Jaji Mkuu Awataka Viongozi na Watendaji wa Mahakama Kutenda Haki

$
0
0
Na Beatrice Lyimo- Maelezo, Dodoma
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amewataka viongozi mbalimbali wa mahakama ikiwemo Naibu Wasajili, Mahakimu, Watendaji, Wakuu wa Idara na Vitengo kutenda haki kwa watumishi walio chini yao.
Jaji Mkuu ameyasema hayo leo Mkoani Dodoma wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa baraza la wafanyakazi wa mahakama Tanzania.
“Sisi kama wasimamizi wakuu wa haki nchini tunawajibu mkuu wa kutenda haki kwa watumishi kwa vitendo, ni ukweli usiopingika kwamba kimbilio la mtumishi yeyote aliyefikwa na matatizo ni kwa kongozi wake katika sehemu yake ya kazi, hivyo basi kila kiongozi anapaswa kufungua milango kwa watumishi waliopo chini yake” amesema Jaji Mkuu.
Jaji Mkuu ameongeza kuwa, ubora wa viongozi unapimwa kwa namna wanavyosaidia wafanyakazi walio chini yao, hivyo kuwataka viongozi hao kutokufunga milango yao kwa watumishi wanaowaongoza.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akihutubia Baraza la Wafanyakazi wa  Mahakama  ya Tanzania leo Jijini Dodoma.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof.  Ibrahim Juma (katikati) akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano kabla ya kufungua  Baraza la Wafanyakazi wa  Mahakama ya Tanzania leo Jijini Dodoma.
 Wajumbe wa menejimenti ya Mahakama ya Tanzania wakishiriki kuimba wimbo wa mshikamano wakati wa kikao cha Baraza la wafanyakazi leo Jijini Dodoma.
 Sehemu ya washiriki  wa Kikao cha Baraza la wafanyakazi kutoka Kanda ya  Dar es Salaam wakifuatilia kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania leo Jijini Dodoma.
 Wajumbe wa Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi ambaye ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.  Prof. Ibrahim Juma.
 Wajumbe wa Menejimenti  ya Mahakama ya Tanzania wakifuatilia hotuba ya Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma  wakati wa Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania .
 Katibu wa Baraza la Wafanyakazi  Mahakama ya  Tanzania Bibi Rose  Tengu akitoa maelezo ya awali kuhusu  Baraza la Wafanyakazi wa  Mahakama Tanzania leo Jijini Dodoma.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

PRECISION AIR NA MAXMALIPO WAINGIA MKATABA WA MIAKA MITATU WA HUDUMA KWA WATEJA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Shirika la ndege la Precision Air limeingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya MaxMalipo ikiwa ni katika kuboresha huduma za ulipaji wa tiketi kwa njia ya kieletroniki.

Kupitia makubaliano hayo Precision Air itatumia mfumo wa malipo wa MaxMalipo kuwezesha wateja wake kulipia tiketi tiketi zao kwa njia ya malipo ya mitandao ya simu, Benko na Mawakala wa MaxMalipo.

Akizungumza baada ya kuwekeana saini mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Sauda Rajab utakuwa na faida kwa wateja wa Precision Air kulipia tiketi zao kwa urahisi zaidi ambapo watalipa kwa njia ya simu kupitia mitandao yote ya simu za mkononi, malipo kupitia akauntibza benki zinazokubali malipo kupitia mfumo wa MaxMalipo na mawakala wote nchini takribani elfu thelathini (30,000).

Sauda amesema kuwa, makubaliano haya ni kwa muda wa miaka mitatu kuanzia Juni 2017 hadi Juni 2020 na kukiwa na mkakati wa ongezeko la abiria kwa asilimia 20 hadi 30 kwa mwaka wa kwanza mkataba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Precision Air Sauda Rajab (kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa MaxMalipo Tanzania Charles Natal wakitia saini makubaliano ya kimkataba ya huduma za ulipaji tiketi kwa njia ya kieletroniki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Precision Air Sauda Rajab akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuingia nakubaliano na kampuni ya MaxMalipo, kulia ni Makurugenzi Mkazi MaxMalipo Tanzania Charles Natal.

"Mkataba wetu na MaxMalipo ambapo ni wa miaka mitatu umewekewa makubaliano ya ongezeko la abiria ambapo kwa mwaka tunachukua takribani wateja laki nne (400,000) ila mkakati uliowekwa zaidi ni kufikia malengo ya kuongeza wateja kwa asilimia 20 hadi 30 kwa mwaka wa kwanza,"amesema Sauda.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkazi wa MaxMalipo nchini Tanzania Charles Natal amesema kuwa ubia huu baina ya MaxMalipo na Precision Air unawezesha wateja wote kufanya malipo ya tiketi za usafiri wa ndege kwa urahisi zaidi na kwa haraka.

Amesema kwa sasa MaxMalipo ipo katika nchi tano za Afrika na ikiwemo Tanzania, Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia na tayari nchini Kenya wataanza huduma zao hivi karibuni.
Mkurugenzi Mkazi wa MaxMalipo Tanzania Charles Natal akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uwekaji saini makubaliano na Shirika la Ndege la Precisio Air kwa ajilo ya huduma za ulipaji wa tiketi kwa njia ya Kieletroniki, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Air Sauda Rajab na Menena Masoko na Mawasiliano Precision Air Hillary Mremi

"Tumejizatiti zaidi kutoa huduma za malipo ya tiketi kwa njia ya kieletroniki badala ya kufanya booking online au kupitia kwenye ofisi za Precision Air na kupatiwa nambari ya malipo (booking reference number),"amesema Natal.
Mkataba huo umesainiwa mbele ya waandishi na wahabari na ubadilishana hati za makubaliano hayo kuonyesha kuanza kazi mara moja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Precision Air Sauda Rajab na Mkurugenzi Mkazi wa MaxMalipo Tanzania Charles Natal wakipeaa mikono baada ya kubalishana hati za makubaliano baina yao. 
Picha ya pamoja baina ya uongozi wa Precision Air na MaxMalipo Tanzania.Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Air Sauda Rajab, Mkurugenzi Mkazi wa MaxMalipo Tanzania Charles Natal. Meneja Masoko Na Mawasiliano Precision Air Hillary Mremi na Mkuu wa Kitengo cha Biashara Deogratius Lazaro.Picha na Emmanuel Masaka.

MAJALIWA AFUNGUA VITUO VYA POLISI MBURAHATI, KILUVYA NA MBWENI - DAR Inbox x

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kufungua Kituo cha Polisi cha Kiluvya wilayani Ubungo Mei 24, 2018. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhadisi, Hamad masauni na wanne kukhoto ni Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Siro, Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa a Dar es salaam na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva. (Picha na Ofiosi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Siro baada ya kufungua Kituo cha Polisi cha Mbweni Wilayani Kawe, Mei 24, 2018. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MHE. STEPHEN MASELE (MB) NA MHE. MBONI MHITA (MB)

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati)akizungumza na Mbunge wa Shinyanga mjini Mhe. Stephen Masele ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika pamoja na Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini Mhe. Mboni Mhita ambaye pia amechaguliwa kuwa  Rais wa Caucus ya Vijana ya Bunge la Afrika , ofisini kwa Makamu wa Rais , Kilimani Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mbunge wa Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika, Mheshimiwa Masele  alimshukuru Makamu wa Rais kwa jitihda zake zilizofanikisha ushindi wake.  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja  na Mbunge wa Shinyanga mjini Mhe. Stephen Masele ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika pamoja na Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini Mhe. Mboni Mhita ambaye pia amechaguliwa kuwa  Rais wa Caucus ya Vijana ya Bunge la Afrika  wengine pichani ni Mbunge wa Mbozi Magharibi Mhe. David Silinde (kulia) na Mbunge wa Viti Maalum Wanawake Zanzibar Bi. Asha Juma (kushoto) , ofisini kwa Makamu wa Rais , Kilimani Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pongezi Mbunge wa Shinyanga mjini Mhe. Stephen Masele ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika, leo Kilimani jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati)akimpa mkono wa pongezi Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini Mhe. Mboni Mhita ambaye pia amechaguliwa kuwa  Rais wa Caucus ya Vijana ya Bunge la Afrika , ofisini kwa Makamu wa Rais , Kilimani Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

‘VITA’ SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI YAZINDULIWA DODOMA

$
0
0
Na Ramadhani Juma, Ofisi ya Mkurugenzi
ZOEZI la utoaji wa chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake limezinduliwa rasmi katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma huku wasichana waliopatiwa chanjo hiyo wakitoa wito kwa wenzao kujitokeza na kuhakikisha wanakingwa dhidi ya ugonjwa huo.
Uzinduzi huo umefanyika jana katika ukumbi wa Dodoma Sekondari ambapo mgeni rasmi katika hafla fupi ya uzinduzi huo alikuwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Deo Ndejembi huku Mganga Mkuu wa Halmashauri Hamadi Nyembea akimwakilisha Mkurugenzi Godwin Kunambi.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Kaimu Mkuu huyo wa Wilaya alisema uzinduzi huo ni kiashiria cha kuwafikia Wasichana wote wenye chini ya umri wa miaka 14 ndani ya Wilaya ya Dodoma.
Alisema zoezi hilo litaendeshwa na Halmashauri kupitia Ofisi ya Mganga Mkuu, na litashirikisha viongozi wa ngazi zote ikiwemo Kata na Mitaa ili kuhakikisha kila msichana anayehusika anafikiwa na kupatiwa chanjo hiyo.
Awali, Mganga Mkuu wa Halmashauri Hamadi Nyembea alisema katika kipindi cha Mwaka mmoja ujao, jumla ya Wasichana 7,828 walio na umri wa chini ya miaka 14 wanatarajiwa kufikiwa na kupatiwa chanjo hiyo katika Wilaya ya Dodoma.
Alisema  baada ya miezi sita Wasichana wote waliopatiwa chanjo hiyo watapatiwa tena kwa awamu ya pili ili kukamilisha kinga yao dhidi ya virusi vinavyoeneza ugonjwa huo.
Alimweleza Mgeni rasmi na wajumbe kuwa, chanjo hiyo imethibitishwa na Shirika la AfyaDuniani (WHO) hivyo Wasichana na Wazazi wasiwe na mashaka badala yake watoe ushirikiano wa kutosha ili kufikia lengo la Serikali la kutokomeza ugonjwa huo kama ilivyofanya kwa magonjwa kama Polio.
 Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Hamadi Nyembea akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya kizazi kwa Wasichana walio chini ya umri wa miaka 14 katika Wilaya ya Dodoma jana. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Deo Ndejembi na wa kwanza ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Dodoma palikofanyika uzinduzi huo Mwalimu Amani Mfaume.  
 Muhudumu wa Afya Ruth Azaliwa akimchoma Sindano ya chanjo dhidi ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake Mwanafunzi wa kidato cha pili wa Shule ya Sekondari ya Dodoma Huda Khalid Rabash kuashiria uzinduzi wa zoezi la utoaji wa chanjo hiyo katika Wilaya ya Dodoma jana. Wanaoshuhudia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Deo Ndejembi (kushoto) na Mwalimu wa Afya wa Shule hiyo Caritas Burchard (kulia).
 Zoezi la utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya kizazi kwa Wasichana walio chini ya umri wa miaka 14 likiendelea katika Sekondari ya Dodoma mara baada ya kuzinduliwa rasmi na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Deo Ndejembi.
 Mwanafunzi wa Kidato cha pili katika shule ya Sekondari ya Dodoma Huda Khalid Rabash akionesha kadi yake aliyokabidhiwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Deo Ndejembi (kushoto) kama ishara ya uzinduzi rasmi wa utoaji wa chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya kizazi kwa Wanawake. Kadi hiyo itamuwezesha kupata chanjo hiyo kwa awamu ya pili baada ya miezi sita ili kukamilisha kinga yake dhidi ya ugonjwa huo. Wengine wanaoshuhudia ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Hamadi Nyembea (mwenye miwani katikati nyuma)  na Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Amani Mfaume (mwenye miwani katikati mbele). Kushoto ni Mwalimu wa Afya wa Shule hiyo Caritas Burchard.
 Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Deo Ndejembi akimkabidhi kadi maalum kwa ajili kupata huduma ya chanjo awamu ya pili dhidi ya ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya kizazi kwa Wanawake Mwanafunzi wa kidato cha pili wa Shule ya Sekondari ya Dodoma Huda Khalid Rabash kama ishara ya uzinduzi wa zoezi la utoaji wa chanjo hiyo katika Wilaya ya Dodoma jana katika ukumbi wa Shule hiyo.  
Sehemu ya Wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari ya Dodoma wakifuatilia shughuli ya uzinduzi wa utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi  uliofanyika katika Shule hiyo jana. Picha na Ramadhani Juma.

INTRODUCING "NASTAY" BY B GWAY @ MIX TOUCHEZ SOUND STUDIO

WANAOHUSIKA NA KUUZA VIWANJA ENEO LA KAMBI YA WAZEE NUNGE WAKAMATWE-SERIKALI.

$
0
0

NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeutaka uongozi wa Kambi ya Wazee na watu wasiojiweza Nunge kuwakamata wahusika wanaouza viwanja katika eneo la kambi hiyo .

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akijibu kero za Wazee wa Nunge alipotembelea kambi hiyo iliyopo Kigamboni jijini Dar es salaam.

Sambamba na hilo Dkt. Ndugulile alisimamisha ujenzi wa nyumba ya mwananchi wan je na kambi hiyo uliokuwa unaendelea katika eneo hilo ambalo inadaiwa sio muhusika wa eneo la kambi ya wazee ya Nunge na kusema aliyeuziwa katika eneo hilo Serikali haitamtambua. “Marufuku kwa mtu yeyote kuuza,kununua wala kujenga pamoja na kuchimba mchanga katika eneo la kambi hii na mtu atakayebainika anajihusisha na vitendo hivyo basi hatua za sharia zitafuata zidi yake “ alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa misaada inayokuja katika kambi hiyo iwe inawekwa kwenye utaratibu maalumu ili kila mmoja aweze kupata mahitaji anayostahili kwa wakati husika na viorodheshwe kwenye daftari la kambi hiyo kama kumbukumbu ili kuondoa changamoto ya kurumbana kuhusu mahitaji kwa wazee hao.

Mbali na hayo Dkt. ametoa muda wa wiki mbili tatizo la usafiri kwa wazee wa kambi hiyo liwe limeshughukulikiwa kwa kutengeneza bajaji iliyotolewa na Serikali kwa manufaa ya Wazee wa kambi hiyo na si vinginevyo.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha kambi ya wazee Nunge Dkt. Dismas Chihwalo wakati akisoma taarifa fupi ya kituo hiko amesema kuwa ili uwepo utaratibu mzuri wa kuhudumia walengwa katika kambi hiyo ni lazima kuwepo na makualiano maalumu kwa kutia saini baina ya wanaoletwa kwa mahitaji maalum na viongozi wa kambi hiyo.

“Serikali inatakiwa kuhakikisha wanaoletwa kwa ajili ya huduma maalum na kwa muda maalum wanatia saini mkataba wa makubaliano ili kuweza kuepusha migogoro ya kutoa huduma katika kambi hiyo kwa wanaostahili” alisema Dkt. Chihwalo.Kambi ya Wazee na wasiojiweza Nunge ilianzishwa mwaka 1936 kwa makusudi ya kuwahudumia Wazee na wasiojiweza pamoja na wenye ukoma ili wasipate shida za mahittaji muhimu na huduma za afya kwa wakati sahihi. 
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua chakula wanachopikiwa wazee wa kambi ya Nunge iliyopo Kigamboni wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma kituoni hapo mapema leo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na moja ya binti wa Mhitaji anaeishi katika kambi hiyo ya Nunge iliyopo Wilaya ya Kigamboni, huku lengo la ziara hiyo likiwa kukagua hali ya utoaji huduma kituoni hapo.
 Baadhi ya Wazee waliojitokeza katika ukumbi wa Kituo cha kulelea Wazee wa Nunge ili kupata fursa ya kuzungumza na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile pindi alipofanya ziara kituoni hapo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi wake wa jimbo la Kigamboni Wilayani Kigamboni pindi alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma kituoni hapo mapema leo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya viongozi wa kituo cha kulelea wazee cha Nunge na wazee waliojitokeza kumsikiliza pindi alipofanya ziara kituoni hapo.

TIB Corporate Bank washiriki jukwaa la biashara jijini Arusha

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu TIB Corporate Bank Frank Nyabundege akitoa ufafanuzi juu ya riba zinazotolewa na Bank wakati wa jukwaa linawakutanisha wadau mbalimbali katika masuala ya kuwezesha na kuendeleza biashara pamoja na kujadili fursa mbalimbali na namna gani wadau wanaweza kusaidia kuinua fursa hizo.
Mkurugenzi wa matawi na masoko TIB Corporate Bank  Theresia Soka akitoa mada juu ya Bank hiyo wakati wa Jukwaa hilo linawakutanisha wadau mbalimbali katika masuala ya kuwezesha na kuendeleza biashara lililofanyika leo jijini Arusha.
Meneja wa Tawi la TIB CBL Arusha Juliana Mwansuva akiwakaribisha wananchi wa Arusha kufika katika Tawi ili kujipatia huduma za kibenki za Hali ya juu wakati wa jukwaa hilo.
 Washiriki mbalimbali kwenye mkutano iliowakutanisha wa watu zaidi ya 500 ili kujadili fursa mbalimbali na namna gani wadau wanaweza kusaidia kuinua fursa hizo.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa kwenye picha ya pamoja na wadhamini wa jukwaa hilo lililofanyika jijini Arusha.

AfDB YASISITIZA NIA YA KUFADHILI MRADI WA KUONGEZA MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO

$
0
0
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeahidi kufadhili mradi wa Kuongeza Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Chakula ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kujenga uchumi wa viwanda na kuinua kipato cha wakulima.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na  Meneja  wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeshughulikia Maendeleo ya Miundombinu Vijijiji, Bw. Olagoke Oladapa, kwenye Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB unaoendelea Jijini Busan- Jamhuri ya Korea Kusini.

Bi. Amina Shaaban anayemwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango,  Dkt. Philip Isdor Mpango, katika Mkutano huo, alisema kuwa mwanzoni mwa mwezi Mei, 2018, AfDB ilituma timu ya wataalam nchini  Tanzania kufanya mazungumzo ya awali na Serikali kuhusu utekelezaji wa mradi huo ambao ni ahadi ya  Rais wa AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina kwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wakati wa  ziara yake ya  kikazi nchini Tanzania mwishoni wa mwezi Aprili, 2018.

Miongoni mwa viongozi wa Serikali waliokutana nao ni pamoja Mawaziri kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

“Serikali imefurahishwa na utayari wa AfDB kufadhili mradi huo kwani utachangia ukuaji wa uchumi na kuleta maendeleo katika sekta ya viwanda na kilimo nchini Tanzania” alisema Bi. Shaaban

Naibu Katibu Mkuu Bi. Shaaban alisema utekelezwaji wa mradi wa kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao ya chakula utanufaisha watu wengi hasa wa kipato cha chini kwa kuwa sekta ya kilimo Tanzania inachukua nafasi kubwa katika kuinua uchumi wa nchi.

Aidha, Naibu Katibu Mkuu, aliahidi kuwa Serikali itaharakisha ukamilishaji wa taratibu za maandalizi ya awali ya mradi huo utakao chochea maendeleo ya Sekta ya Kilimo na Viwanda kwa kiasi kikubwa kwa kuwa tayari Benki ya AfDB imeonesha utayari wa kuupatia fedha.  
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis. Shaaban (kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Meneja wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB anayeshughulikia Maendeleo ya Miundombinu Vijijiji Bw. Olagoke Oladapa (katikati), kuhusu utekelezaji wa mradi wa Kuongeza Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Chakula  Jijini Busan- Korea Kusini.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)
Viewing all 110176 articles
Browse latest View live




Latest Images