Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

WIZARA YA AFYA YATHIBITISHA HAKUNA UGONJWA WA EBOLA NCHINI

$
0
0
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.


NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto dkt. Faustine Ndugulile amethibitisha kuwa hakuna mtu aliyethibitika kuwa na ugonjwa wa EBOLA hapa nchini wala hakuna ugonjwa huo hapa Tanzania.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa wa EBOLA kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwepo kwa ugonjwa huo hapa nchini.

“Napenda kuwatoa hofu watanzania kwamba hakuna ugonjwa wa EBOLA na wala hakuna mtu aliyethibitika kuwa na ugonjwa huo, hivyo tuendelee na shughuli za kujenga Taifa ila tunatakiwa tuchukue tahadhari za kujikinga juu ya ugonjwa huu” alisema Dkt. Ndugulile. 

Aidha, Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa EBOLA usiingie nchini Serikali imeweka vifaa vya kupima joto la mwili (themo scaner) pia wapo wataalamu wa Afya ambao wanauliza hali ya wageni wanaoingia katika mipaka yote inayoizunguka nchi yetu ili kuzuia ugonjwa huo kuingia. 

Dkt. Ndugulile amesisitiza kuwa, Serikali haijafunga mipaka ya nchi kwa sababu ya kujikinga na EBOLA."Tanzania hatujafunga mipaka na hatuwezi kufunga biashara za mipakani ila tumeimarisha ufuatiliaji wa watu wanaoingia nchini hususani maeneo ya viwanja vya ndege na mipaka mingine yote." 

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile ameitaka mikoa yote iliyo mipakani kudhibiti watu wote wanaoingia nchini kwa njia za panya ili kuepusha uingizaji wa ugonjwa huo kwa wananchi huku akiwataka wafanyabiashara wa mipakani kutoa ushirikiano ili kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini. 

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani ambaye pia ni Afisa wa kushughulikia magonjwa ya kuambukiza Dkt. Grace Saguti amesema kuwa Wananchi wanatakiwa kupata elimu juu ya kujikinga na ugonjwa huo. 

“Elimu inahitajika ya kutosha kwa wananchi wote hasa katika kufichua wagonjwa wa Ebola kama watagundulika hasa wanaotoka nje ya nchi ili kupata msaada kutoka kwa watoa huduma za afya walio yao juu ya kujikinga na ugonjwa huo.


 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari, viongozi wa Wizara na wawakilishi wa WHO wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa wa Ebola mapema leo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.

Waandishi wa Habari kutoika vyombo mbali mbali wakifuatilia kwa makini tamko kuhusu gonjwa wa Ebola alilotoa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.

Airtel na VETA washirikiana kuandaa kongamano la elimu kupitia mtandao

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania VETA wameshiriki kongamano la elimu kupitia mtandao yenye lengo la kuhamasisha ubunifu kwa vijana na kuonesha jinsi kijana anavyoweza kusoma kwa kujitengemea kwa kutumia ubunifu wa  aplikesheni ya VSOMO inayotoa  elimu kwa mtandao.

Kwa miaka miwili sasa, VETA kupitia applikesheni ya VSOMO imekuwa ikitoa elimu kupitia mtandao kwa wanafunzi ambao wanataka kupata elimu ya ufundi stadi kwa udhamini wa Airtel Tanzania.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kongamani hilo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema kampuni ya Airtel iliamua kuwa mmoja wa wadau wa teknolojia hii ya kutoa elimu ya VSOMO ikiwa ni moja wa mkakati wake wa kurudisha sehemu ya faida yake katika kusaidia Jamii. Kwa kuweza kutambua umuhimu wa Jamii inayotuzunguka, tuna miradi ya kusaidia vijana kujikwamua yenye lengo ya kuwapa vijana ujuzi ili wajiajiri au wapate ajira kwenye sekta mbali mbali ili kuunga mkono juhudi za serikali za kujenga uchumi wa viwanda.

Airtel Tanzania inayo furaha kuona kuwa matumizi ya smartphone yakiwa ni darasa au ikiwa ni moja ya njia ya kutumika kupata elimu ya ufundi. Hii haiukuwa rahisi kufanya peke yetu ndio sababu tuliamua kushirikiana na VETA kama taasisi ya serikali yenye mamlaka ya kutumia elimu ya ufundi hapa nchini huku DTBi wakiwa ndio waliombuni applikesheni ya VSOMO, alisema Singano.

Airtel na washirika wake VETA na DTBi kwa sasa wana utaratibu mpya wa malipo kwa awamu ili kuwezesha wanafunzi wanaotaka kupata elimu ya ufundi stadi kufanya bila kupata changamoto za kulipa karo, aliongeza Singano.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano akitoa mada wakati kongamano la elimu kupitia mtandao yenye lengo la kuhamasisha kusoma kwa kujitengemea kwa miongoni mwa vijana hapa nchini kupitia teknologia ya VSOMO. Kongamano hilo liliandaliwa na Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania VETA na DTBi.
 Godfrey Magila kutoka taasisi ya DTBi akitoa mada wakati kongamano la elimu kupitia mtandao yenye lengo la kuhamasisha kusoma kwa kujitengemea kwa miongoni mwa vijana hapa nchini kupitia teknologia ya VSOMO. Kongamano hilo liliandaliwa na Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania VETA na DTBi
 Mratibu wa VSOMO kutoka Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania VETA Charles Mapuli  akitoa mada wakati kongamano la elimu kupitia mtandao yenye lengo la kuhamasisha kusoma kwa kujitengemea kwa miongoni mwa vijana hapa nchini kupitia teknologia ya VSOMO. Kongamano hilo liliandaliwa na Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania VETA na DTBi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Benki ya CRDB na Jeshi la Magereza kuendelea kuboresha uhusiano wa kibiashara

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (kushoto) akizungumza na baadhi ya maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini, juu ya kuangalia njia bora za kudumisha uhusiano baina ya Benki ya CRDB na Jeshi la Magereza nchini, katika Makao Makuu wa Magereza, jijini Dar es salaam, Mei 23, 2018. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dokta Charles Kimei leo amekutana na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Dokta Juma Malewa ili kuangalia njia bora zaidi za kudumisha na kuboresha uhusiano baina ya pande zote mbili. Akizungumza katika mkutano huo ambao pia ulijumuisha maafisa waandamizi kutoka Benki ya CRDB na Jeshi la Magereza, Dokta Kimei alilishukuru Jeshi hilo kwa kuwa mdau mkubwa wa Benki kupitia mikopo, akaunti za mishahara za askari na SACCOSS ya Magereza ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitoa huduma kwa askari Magereza.

“Nichukue fursa hii kulishukuru Jeshi la Magereza kwa biashara ambayo limekuwa likitupatia, niipongeze SACCOSS ya Magereza kwa uamuzi wa kuwa Wakala wa FahariHuduma, hii si tu itawaongezea kipato kupitia kamisheni za uwakala, pia itasogeza huduma za kibenki karibu na Maaskari Magereza”, alisema Dokta Kimei.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akizungumza katika kikao na uongozi wa Benki ya CRDB, uliomtembelea ofinisi kwake, Makao Makuu ya Magereza jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei. 


Akielezea juu ya fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB kwa wafanyakazi Dokta Kimei alisema hivi karibuni Benki imeshusha riba inayo toza katika mikopo binafsi toka 20% mpaka 17%, muda wa marejesho umeongezwa toka miezi 72 hadi miezi 84, wakati kiwango cha kukopa kimeongezwa kutoka shilingi milioni 50 mpaka kufikia Shilingi Milioni 100 hivyo kuwapa wateja wigo mpana zaidi wa kukopa ili kufikia malengo.
Dokta Kimei pia alitumia fursa hiyo kuwahamasisha askari wa Jeshi la Magereza kuchangamkia fursa hiyo ya mikopnnno huku akibainisha ya kuwa Benki ya CRDB imeanzisha utaratibu maalum wa kununua madeni na mikopo ya askari kutoka katika Taasisi zingine za Kifedha. Hivyo kutoa fursa kwa askari wenye mikopo Benki nyingine, kukopa toka Benki yao pendwa ya CRDB. Mpaka kufikia mwisho wa mwezi Aprili 2018 tayari Benki ya CRDB ilikuwa imeshakopesha zaidi ya maofisa 5,415 wa Jeshi la Magereza ambapo jumla ya shilingi 29.4 bilioni zilikuwa zimekopeshwa kwao.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (kushoto) akimkabidhi zawadi maalum, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa, wakati alipomtembelea ofisini kwake, Makao Makuu wa Magereza, jijini Dar es salaam, Mei 23, 2018. Mkutano huo ulikuwa na lengo kudumisha uhusiano wa kibiashara baina ya Benki ya CRDB na Jeshi la Magereza nchini. 


Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Dokta Juma Malewa alimshukuru Dokta Kimei kwa kutembelea Jeshi hilo na kuipongeza Benki ya CRDB kwa maboresho hayo katika huduma zake, huku akiisifu zaidi huduma ya Salary Advance ambayo alisema kwa kiasi kikubwa imesaidia kuboresha maisha ya askari. Dokta Malewa alisema katika maboresho hayo yanayoendelea Jeshi la Magereza lingependa kutumia mfumo wa kibenki katika kukusanya mapato yake katika miradi na huduma mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.

“Nikuombe Dokta Kimei na uongozi mzima wa Benki ya CRDB kuona uwezekano wa kuweka huduma za kibenki kama ATM na Matawi kwenye maeneo ya Magereza yenye uhitaji mkubwa wa huduma hiyo”, aliongezea Dokta Malewa. Dokta Malewa pia aliiomba Benki ya CRDB kushiriki katika miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa na Jeshi hilo ikiwamo ujenzi wa hospitali ya Jeshi la Magereza Ukonga, miradi ya Kilimo cha kisasa na chenye tija, mradi wa kokoto Msalato pamoja na uwekezaji katika miradi ya viwanda vidogo vidogo.
Baadhi ya Maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini, wakiongozwa na Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza,  Gaston Sanga wa kwanza kulia) wakati wa kikao maalum na uongozi wa Benki ya CRDB, uliotembelea Makao Makuu ya Magereza, jijini Dar es salaam leo.

“Ningependa kuona pia Benki ya CRDB kuwa mteja wa bidhaa na huduma zinazotolewa na Jeshi la Magereza mfano Benki kutumia samani za ofisi na Magereza kupewa Kandarasi za ujenzi wa miradi ya Benki inayodhaminiwa au kumilikiwa na Benki”, aliongezea Dokta Malewa akionyesha fursa ya kibiashara iliyopo baina ya Benki na Jeshi la Magereza.

Dokta Kimei alimhakikishia Mkuu wa Jeshi la Magereza kuwa Benki ya CRDB ipo tayari kushirikiana na Jeshi hilo katika miradi mbalimbali ambayo wamepanga kuitekeleza, huku akihaahidi kutuma timu ya wataalam kutoka Benki ya CRDB kufanya upembuzi yakinifu juu ya kuweka ATM na kufungua vito vya kutolea huduma katika maeneo ya Jeshi la Magereza ilikufikisha huduma kwa akari kwa urahisi.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akieleza jambo kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Juma Malewa (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Magereza, jijini Dar es salaam leo.

“Matarajio yangu ni kuona uhusiano baina yetu ukikua zaidi, naihidi kuwa kupitia Wakurugenzi na Mameneja wetu wa matawi tutaweka utaratibu wa kutembelea ofisi za Magereza nchi nzima ili kuhakikisha haya tuliyokubaliana hapa yanatekelezwa”, alisema Dokta Kimei.

BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI 

WAZIRI LUKUVI AFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekutana na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dkt. Reginald Mengi ili kuzungumza na kutambua fursa zinazopatikana za uwekezaji katika sekta ya Ardhi nchini.

Dkt. Mengi amekutana na Mhe. Lukuvi ofisi kwake kanda ya Dar es salaam ambapo wamejadili mambo mbalimbali ambayo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeyafanya katika sekta ya ardhi ambayo na kutoa fursa  kwa wawekezaji wa ndani kuwekeza kwa urahisi.

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kushoto) akizungumza  na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dkt. Reginald Mengi(kulia) alipomtembelea ofisini kwake kanda ya Dar es salaam .
    Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akipokea nyaraka ya makusudio ya kuwekeza katika ardhi kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dkt. Reginald Mengi.

WANAWAKE WAJAWAZITO WATAKIWA KUHUDHURIA KLINIKI MARA KWA MARA KUZUIA FISTULA.

$
0
0

NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

WANAWAKE wajawazito wanatakiwa kuhudhuria Kliniki mara kwa mara ili kuangalia maendeleo ya ujauzito wao na kupata vipimo na matibabu kama itagundulika kuna uwezekano wa kupata ugonjwa wa Fistula.Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kutoa tamko la ugonjwa wa Fistula katika kuadhimisha siku ya ugonjwa huo duniani.

“Asilimia 60 ya wanawake nchini ndiyo wanahudhuria Kliniki mara kwa mara hii ni dalili mbaya kwani kama mwanamke mjamzito anaweza kuwa na viashiria vya fistula hatoweza kugundulika mapema na kupata matibabu na badala yake asilimia 40 tu ndo wanaohudhuria Kliniki” alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kutokomeza ugonjwa huo Serikali kupitia Wizara ya Afya imeandaa mkakati wa kupeleka wataalam kwenye kila mkoa kujua idadi ya wagonjwa wa fistula ili kuweza kutokomeza ugonjwa huo.

Vilevile Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeimarisha na kukarabati vituo vya Afya vipatavyo 288 katika vitengo vya kuhudumia wenye uzazi pingamizi kwani hiyo nayo ni sababu inayopelekea kwa wanamke kupata fistula.Hata hivyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa huduma za Fistula zinapatikana Bure nchini hasa kwenye hospitali za CCBRT,Bugando na Celian hivyo mwanamke akijiona ana dalili za ugonjwa huo anatakiwa kuwahi katika kituo cha kutolea huduma za afya na kupata ushauri.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linayoshughulikia mambo ya afya Dkt. Frolence Temu amesema kuwa katika kupambana na ugonjwa wa Fistula nchini wanajenga uwezo kwa watumishi wa Hospitali za Wilaya na Mkoa.
Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia idadi ya Watu UNFPA Bi. Jacqueline Mahon amesema kuwa Shirika hilo limetoa mafunzo kwa watoa huduma za afya wapatao elfu nne ili kupamabana na ugonjwa huo.

“Mbali na kujengea uwezo watumishi hao pamoja na ukarabati wa vituo vya afya ,watanzania wanatakiwa kuacha vitendo vya udhalilishaji kwa wagonjwa wa fistula na wenye ugonjwa huu wajitokeze mara moja kwa ajili ya kupata matibabu” alisema Bi. Mahon.

Mbali na hayo Mkurugenzi Mkuu wa uendeshaji hospitali ya CCBRT inashirikkiana na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Fistula Hospitali yake inafanya matibabu kwa wagonjwa 1500 kila mwaka .Ugonjwa wa Fistula huadhimishwa Mei 23 kila mwaka na maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo “BILA YA KUMUACHA MWANAMKE YEYOTE MWENYE TATIZO LA FISTULA NYUMA SHARTI TUDHAMIRIE KUTOKOMEZA FISTULA SASA”

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wakati akitoa tamko la ugonjwa wa Fistula katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Shirika la Amref Afrika Dkt. Floriance Temu akiongea na waandishi wa habari wakati maazimisho ya siku ya ugonjwa wa fistula Duniani mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile
akizunguza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,kulia kwake ni Mgeni rasmi Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kimataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA) Bi Jacqueline Mahon.

WAZIRI WA MAJI KAMWELWE ATAHADHARISHA KUWAFUKUZA WAHANDISI

$
0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwelwe ametahadharisha kuwafukuza kazi na kuwashitaki wahandisi wa serikali wanaokosa uzalendo na kuhujumu miradi ya maji katika hatua ya usanifu na usimamizi kwa kupitisha vifaa vilivyo chini ya viwango.

Mhandisi Kamwelwe ametoa tahadhari hiyo wakati wa ziara yake Mkoani Songwe ya kukagua utekelezaji wa miradi mitatu ya maji ya Iyula na Itaka katika halmashauri ya Mbozi, mradi wa Umwagiliaji Naming’ongo katika halmashauri ya Momba na mradi wa Maji Tunduma katika halmasahuri ya Tunduma.

“Miradi mingi inakamilika na kuzinduliwa na viongozi wakubwa wa kitaifa lakini mabomba yanaanza kupasuka muda mfupi tu baada ya wananchi kuanza kupata maji kwakuwa hayana viwango, wahandisi badilikeni na hili likitokea hauna ajira na kushitakiwa juu”, amesisitiza Kamwelwe.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa miradi ya maji hakutakuwa na tija endapo shughuli za utafiti wa vyanzo vingine imara vya maji hazitafanyika pamoja na kutunza vyanzo vya maji vilivyopo kwa ajili ya uendelevu wa miradi hiyo kwa muda mrefu.

“Hatutaki kusikia mradi unatoa maji kwa muda mfupi kisha maji yanaisha kwenye vyanzo, hivyo naagiza taasisi ya bonde la ziwa Rukwa washirikiane na taasisi nyingine pamoja na ofisi za wakuu wa wilaya kutafuta vyanzo vingine vya maji pamoja na ulinzi wa vyanzo vilivyopo”, amebainisha Mhandisi Kamwelwe.

Kwa Upande wao wananchi wameiomba serikali kuwepo kwa uwazi na ushirikishwaji katika hatua zote za ujenzi wa miradi tangu hatua ya usanifu ili kujenga uelewa juu ya miradi hiyo na kuondoa migogoro.

Ujenzi wa miradi ya maji ya Iyula, Itaka na Tunduma inatarajiwa kutoa huduma ya maji kwa wananchi takribani laki moja ambao watakuwa wanapata maji kwa umbali usiozidi mita 400 sawa na mwongozo wa sera ya maji ya mwaka 2002.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwelwe akisisitiza jambo kwa wataalamu alipotembelea mradi wa maji Iyula halmashauri ya Mbozi, kushoto kwake ni Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya maji Mkoa wa Songwe Mhandisi Tanu Deule.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwelwe akikagua chanzo cha maji Itaka katika halmashauri ya Mbozi pamoja na wataalamu wengine kutoka ngazi ya mkoa na wilaya.

RAIS JOHN POMBE MAGUFULI ARIDHIA KUPANDISHWA HADHI KWA MAPORI YA AKIBA KUWA HIFADHI ZA TAIFA

TFF YATANGAZA MAJINA YA WACHEZAJI 30 WATAKAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA MSIMU HUU

$
0
0
Na Agnes Francis Blogu ya Jamii.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)limetangaza majina ya wachezaji 30 katika kuelekea mwisho wa Ligi  kuu  ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ambao watawania Tuzo za Mchezaji Bora mwaka huu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Msemaji wa TFF Clifford Ndimbo amesema utaratibu huo hufanyika kila mwaka baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Vodacom.

Ndimbo amefafanua wachezaji hao 30 watachujwa na kubaki 10 na baadae watabaki wachezaji wa tatu wataoinga hatua ya fainali ili kumpata Mchezaji bora kwa msimu huu.

Amewataja wachezaji wanaowania tuzo hiyo ni Habibu Kyombo (Mbao),Khamis Mcha,(RuvuShooting),Yahya Zayd(Azam),Razack Abalora(Azam), Bruce  Kangwa(Azam) Aggrey Morris(Azam),Himid Mao (Azam),Awesu Awesu(Mwadui) na Adam Salamba(Lipuli).

Wengine ni Mohammed Rashid(Prisons), Shafiq Batambuze(Singida),Mudathir Yahya (Singida), Marcel Kaheza(Majimaji),Ditram Nchimbi(Njombe Mji) na Eliud Ambokile(Mbeya City).

Pia Shaaban Nditi(Mtibwa), Tafadzwa Kutinyu(Singida) Ibrahim Ajibu(Yanga), Gadiel Michael(Yanga),Papy Tshishimbi(Yanga),Kelvin Yondani(Yanga),Obrey Chirwa(Yanga),Aishi Manula(Simba), Emmanuel Okwi(Simba),John Bocco(Simba), Jonas Mkude(Simba),
Erasto Nyoni(Simba),Shiza Kichuya(Simba),Asante Kwasi(Simba),Hassan Dilunga(Mtibwa).


NCHI ZA AFRIKA ZATAKIWA KUFANYA MAPINDUZI YA UCHUMI KWA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA NA MIUNDOMBINU

$
0
0
Magavana wa nchi za Afrika wametakiwa kuwa na utayari wa kuzisaidia nchi zao kutatua changamoto za kiuchumi na kuhamasisha maendeleo endelevu ili kuendana na mapinduzi makubwa yanayotokea kote Duniani kwa kuhamasisha ukuaji wa viwanda. 
Rai hiyo imetolewa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina, wakati wa Mkutano wa 6 wa jukwaa la ushirikiano kati ya Jamhuri ya Korea Kusini na Nchi za Afrika uliolenga kujadili namna bora ya kuchochea ukuaji wa sekta ya viwanda katika Nchi za Afrika. 
Wadau wa Mkutano huo uliofunguliwa na Makamu wa Waziri Mkuu wa Korea Kusini  Bw. Kim Dog – Yeon, wamezitaka nchi za Afrika  kuhakikisha zinafanya mapinduzi  ya kiuchumi kwa  kuwekeza kwenye viwanda na miundombinu kwa kuwa  itasaidia uchumi wa nchi kukua kwa kasi na  kuleta maendeleo yenye tija. 
Vilevile nchi za Afrika zinahitaji kuwa na na ushirikiano wenye manufaa na wahisani ikiwemo nchi ya  Jamuhuri ya Korea Kusini  ili kuharakisha maendeleo hayo ya kiuchumi kwa kubadilishana uzoefu na kubaini fursa za ukuaji wa uchumi utakaochochea ushirikiano huo.
Afrika inafursa nyingi za kukuza uchumi kwa kuwa inarasilimali za kutosha kwa takribani sekta zote muhimu za maendeleo ikiwemo ya madini, kilimo, mifugo na Uvuvi. 
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Dkt. Akinwumi Adesina, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis. Shaaban wakati wa Mkutano wa 6 wa jukwaa la ushirikiano kati ya Jamhuri ya Korea Kusini na  Magavana wa nchi za Afrika  Jijini Busan-Korea Kusini.
Makamu wa Waziri Mkuu wa Korea ya Kusini Mhe. Kim Dog – Yeon (wa tatu kulia ) akiwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Dkt. Akinwumi Adesina (kushoto) wakati wa majadiliano ya fursa na changamato mbalimbali zilizopo nchi za Afrika, Jijini Busan- Korea Kusini
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis. Shaaban (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Magavana kutoka nchi za Afrika kwenye Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea Kusini na nchi za Afrika, Jijini Busan- Korea Kusini. 

WALIOAHIDI KUCHANGIA UJENZI CHOO CHA MTOTO WA KIKE ILALA WAENDELEA KUTIMIZA AHADI ILI KUFANIKISHA UJENZI

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii


KAMPENI ya ujenzi wa Choo cha Mtoto wa kike katika Halmashauri ya Manispaa jijini Dar es Salaam inakwenda vizuri kutokana na wadau walioahidi kuchangia kwa lengo la kufanikisha ujenzi wa choo hicho kuendelea kutimiza ahadi zao zikiwamo za fedha ambapo Mratibu wa kampeni hiyo Tabu Shaibu amekabidhiwa Sh.milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa manispaa Benadetha Mwaikambo.

Akizungumza leo baada ya kukabidhiwa fedha hizo, Shaibu ambaye pia ni Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala jijini amesema ahadi zilizotolewa na wadau wa maendeleo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ujenzi wa choo cha mtoto wa kike iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema zimeendelea kutekelezwa kwani wameendelea kupokea michango ya fedha na vifaa vya ujenzi kwa nyakati tofauti.

Amesema kampeni hiyo imetokana na uamuzi wa Watumishi Wanawake wa Manispaa hiyo uanzisha ujenzi wa choo hicho katika hivyo vitakavyojengwa kwenye shule za msingi na Shaibu amefafanua choo cha mfano kinajengwa Shule ya Msingi Chanika.Ujenzi umefikia hatua ya linta na kilichobaki ni kupaua.

"Tunashukuru kwa namna wadau mbalimbali wanavyoendelea kutimiza ahadi zao kwa lengo la kufanikisha ujenzi wa choo cha mtoto wa kike.Tuendelee kusisitiza wale ambao bado hawajatimiza 
ahadi aidha ya fedha au vifaa vya ujenzi basi kuitekeleza."Lengo letu ni kutimiza lengo la kampeni hii ambayo tunakwenda kumkoamboa mtoto wa kike wa Manispaa ya Ilala ambaye leo yupo shuleni na siku zijazo atakuwa mtumishi wa manispaa yetu,"amesema Shaibu.

Kuhusu mchango wa Sh.milioni moja uliotolewa na Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala wa manispaa hiyo, Shaibu amesema anamshukuru kwa kutekeleza ahadi yake na hakika ameonesha dhamira njema ya kufanikisha ujenzi huo na kusisitiza amekuwa akipokea michango kwa nyakati tofauti kutoka kwa wadau mbalimbali.

Kwa upande wa Mwaikambo amesema kikubwa ni kufanikisha ujenzi wa choo cha mtoto wa kike katika manispaa ya Ilala huku akisisitiza walioahidi watekeleze na kwamba ataendelea kushirikiana na watumishi wanawake na wadau wa maendeleo ili kampeni ifanikiwe."Niliahidi kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa choo hicho ambacho ni maalumu kwa mtoto wa kike.Hivyo nitaendelea kushirikiana na wadau wote kwa lengo la kufanikisha malengo yetu na wale ambao wameahidi niwaombe waendelee kutimiza ahadi zao,"amefafanua.

Wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika mwanzoni mwa mwezi huu Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mjema alisema ipo haja ya kufanikisha ujenzi wa choo cha mtoto wa kike na akifafanua vyoo kufafanua vyoo hivyo vitakuwa vya kisasa na ndani kutakuwa na mahitaji yote muhimu. 

 Mratibu wa Kampeni ya Ujenzi wa choo cha mtoto wa kike Tabu Shaibu ambaye pia Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam(katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo wakati anapokea fedha Sh.milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa manispaa Benadetha Mwaikambo(kulia) kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa choo hicho.Kushoto ni Mhasibu wa Idara ya Elimu Msingi Manispaa hiyo Yasinta Endrew ya Ilala.

 Mratibu wa Kampeni ya ujenzi wa choo cha mtoto wa kike Tabu Shaibu ambaye pia Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam(kushoto) akipokea fedha Sh.milioni moja leo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa manispaa Benadetha Mwaikambo(kulia).Anayeshuhudia ni Mhasibu wa Idara ya Elimu Msingi Manispaa hiyo Yasinta Endrew ya Ilala .

MENEJA WA DIAMOND APELEKWA MAHABUSU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imeamuru Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam, Hamis Taletale a.k.a Babu Tale,  kurudishwa Mahabusu ya polisi mpaka Msajili wa Mahakama hiyo atakaporudi kutoka Dodoma.

Amri hiyo imetolewa leo na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Lucy Massam baada ya Babu Tale na Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kushindwa kufikia makubaliano licha ya msajili kuwapa muda wa dakika 10 pande zote wajadiliane namna ya kulimaliza suala hilo.

Babu Tale ambaye pia ni Meneja wa mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva Nassib Abdul 'Diamond Platnumz', amefikishwa mahakamani hapo leo akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi kusikiliza kesi inayomkabili.

Babu Tale, amekamatwa kutokana na amri iliyotolewa Februari 16 mwaka huu na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Wilbard Mashauri iliyoamuru mtuhumiwa huyo na ndugu yake, Idd Taletale wakamatwe.

Amri hiyo pia, ilielekeza watuhimiwa hao wakikamatwa wapelekwe Gereza la Ukonga wakiwa wafungwa wa kesi ya madai, hadi hapo Mahakama hiyo itakapotoa maelekezo mengine.Hata hivyo, mtuhumiwa Babu Tale baada ya kufikishwa mahakamani hapo jana kesi yake ilishindikana kusikilizwa kwa kuwa Msajili Mashauri yuko Dodoma kikazi.

Kutokana na kushindwa kufikia muafaka baada ya dakika hizo kumi kuisha, Msajili Massam ameamuru babu Tale arudishwe mahabusu ya polisi mpaka Msajili Mashauri atakaporudi kwa ajili ya maelekezo mengine.

Hata hivyo kipindi chote cha majadiliano Babu Tale alikuwa katika mahabusu ya mahakama hiyo wakati ndugu zake wanajadiliana na mdai wake kabla ya kuieleza mahakama muafaka watakaofikia na kisha mahakama kutoa maelekezo.

Awali Mahakama hiyo iliwaamuru watuhumiwa hao kumlipa Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kiasi cha Sh.milioni 250 baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa haki za hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Katika kesi ya msingi, Sheikh Mbonde alikuwa akidai kuwa aliingia mkataba na kampuni ya kina Babu Tale (Tiptop Connection) ili wamrekodi mahubiri yake kisha wayauze na kugawana mapato.Hata hivyo baada ya kurekodi masomo saba, walimkatia mawasiliano na alipowatafuta na kukutana nao wakamweleza kuwa wameamua kuachana na mpango huo.

Sheikh Mbonde alidai kuwa akiwa kwenye mahubiri Dodoma ndipo akakutana na mikanda ya video katika mfumo wa DVD yenye mahubiri yake huku kukiwa na namba za simu za viongozi hao wa Tiptop.

Sheikh Mbonde alidai baada ya kufanya uchunguzi alibaini kuwa DVD hizo zilikuwa zikiuzwa katika mikoa mbalimbali, ndipo akawafungulia kesi ya madai ya fidia kutokana ukiukwaji wa Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA CHAI NA MKURUGENZI TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO

NAIBU SPIKA, DKT. TULIA AZUNGUMZA NA BAADHI YA WANACHAMA WA CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA LEO OFISINI KWAKE JIJINI DODOMA

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akisalimiana na Mlezi Chama cha Viziwi Tanzania, Ndg. Hashim Ismail (kulia) walipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akizungumza na Mlezi Chama cha Viziwi Tanzania, Ndg. Hashim Ismail (kulia) walipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akimsikiliza Mlezi Chama cha Viziwi Tanzania, Ndg. Hashim Ismail (kulia) walipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Chama cha Viziwi Tanzania wakiongozwa na Mlezi Chama cha Viziwi Tanzania, Ndg. Hashim Ismail (wa pili kulia) walipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.

(PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

BALOZI WA INDIA NCHINI TANZANIA AFAFANUA UBORA WA ELIMU INAYOTOLEWA NCHINI INDIA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
BALOZI wa India nchini Tanzania Sandeep Arya amewahimiza Watanzania kuchangia fursa za elimu ya juu inayotolewa katika nchi yao huku akifafanua mkakati walio nao ni kutoa elimu kwa wanafunzi 200,000 kutoka nje ya nchi na kuwasaidia kupata elimu bora na ufanisi kutoka vyuo mbalimbali nchini humo.

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza fursa za kielimu zinazopatikana nchini India ambapo hafla hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi wa Serikali, shule, vyuo na taasisi ya elimu ya juu.

Hivyo, amesema anawaalika watanzania kwenda kusoma nchini India ili kupata uzoefu na kukutana na wanafunzi kutoka nchi nyingine katika elimu ya juu katika vyuo vya nchini humo na kuongeza Tanzania na India wana urafiki wa muda mrefu na hiyo imesaidia Watanzania wengi kusoma nchini India .

"Kuna watanzania wengi ambao wamesoma kwenye vyuo vilivyopo nchini India na mchango wao katika maendeleo ya nchi ni mkubwa.Hivyo tunaendelea kuwakarabisha kwa wanaotoaka kusoma masomo ya elimu ya juu kusoma India , tunajivunia elimu bora ambayo inatolewa na yenye tija ya kuleta maendeleo,"amesema Balozi Arya.

Aidha amesema wanaotaka kwenda kusoma India wanaweza kupata taarifa kupitia tovuti ya www.studyinindia.gov.in portal.

Amefafanua kuwa elimu wanayoitoa ipo katika uhalisia katika masuala ya elimu, uchumi na jamii kwa ujumla na hivyo watanzania kusoma nchini India ni fursa ya kubadilisha sekta mbalimbali kutokana na elimu watakayoipata.

Kwa upande wake Mhitimu wa Symbiosis International (Deemed University)India Angelelda William amewahimiza vijana wa kitanzania kwenda kusoma kwenye chuo ambacho yeye amesoma kutokana na ubora wa elimu inayotolewa chuoni hapo. Amesema kwa atakayekwenda kusoma chuoni hapo hatajua ada ambayo anaitoa huku akisisitiza baada ya kuhitimu katika chuo hicho uwezo wake katika kufanya mambo ni mkubwa.

Kuhusu elimu inayotolewa nchini India amesema vyuo vingi vya nchini hiyo vimejikita kutoa elimu ya vitendo zaidi badala ya kuandika na sababu kubwa ni wanamuandaa mwanafunzi kufanya kazi kwa vitendo zaidi badala ya kuandika kwenye makaratasi.

”Nimesoma katika Chuo cha Symbiosis ambacho kimejikita kutoa elimu yenye ubora wa hali ya juu.Nitumie nafasi hii kuwaomba vijana wenzangu wanapofikia kwenda kusoma India basi chaguo lao la kwanza liwe kwenye chuo hiki maana nimekaa na nakijua vizuri,"amesema William.
 Balozi wa India nchini Tanzania Sandeep Arya akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu ubora wa elimu ya juu unaotolewa na vyuo vya nchini India.
 Baadhi ya wadau mbalimbali wa elimu wakimsikiliza Balozi wa India nchini Tanzania Sandeep Arya wakati anazungumzia elimu ya juu inayotolewa nchini India
 Mhitimu wa Symbiosis International (Deemed)Univesity Angelelda Willim(kushoto) akiwa na Ofisa wa Ofa za Kimataifa na Mahusiano ya Wanafunzi wa Symbiosis(kulia)wakitoa maelezo kuhusu ubora wa chuo chao leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa Kituo cha Chanel Ten jijini Dar es Salaam Fred Mwanjala na Beatrice Erick wakipata maelezo kuhusu namna ya kujiunga na moja ya chuo cha nchini India.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA


WAZIRI KIGWANGALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ITALIA NCHINI, ROBERTO MENGONI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Balozi wa Italia nchini, Roberto Mengoni ofisini kwake Jijini Dodoma leo ambapo wamekubaliana kuimarisha ushirikiano kwenye tafiti za binadamu wa kale katika eneo la Olduvai, kuboresha utoaji wa elimu hususan ya mapishi ya vyakula vya Kiitaliano katika Chuo cha Taifa cha Utalii na Utangazaji wa vivutio vya utalii nchini. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Italia nchini, Roberto Mengoni baada ya mazungumzo ofisini kwake Jijini Dodoma leo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiagana na Balozi wa Italia nchini, Roberto Mengoni baada ya mazungumzo ofisini kwake Jijini Dodoma leo. (Picha na Hamza Temba-WMU)

DKT ABBASI: HII NDIO SIRI YA MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO YA MHE. RAIS DKT JOHN POBE MAGUFULI

Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yapitishwa na Bunge

$
0
0

   
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisoma hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 bungeni jijini Dodoma. 

Mapema leo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepisha kiasi cha Shilingi Bilioni Mia Moja Sabini na Saba, Milioni Sita na Mia Mbili Thelathini na Mbili Elfu.

Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni Mia Moja Sitini na Sita, Milioni Mia Sita na Sita, na Mia Mbili Thelathini na Mbili Elfu ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, na Shilingi Bilioni Kumi na Milioni Mia Nne ni kwa ajili ya bajeti ya maendeleo. 
Pro. Adolf F. Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,(wa kwanza kushoto) akifuatilia uwasilishwaji wa hotuba ya bajeti ya Wizara. Wa pili kutoka kushoto, ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi akifuatilia hotuba. 
Sehemu ya Watendaji wa Wizara wakifuatilia hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 iliyowasilishwa na kupishwa bungeni jijini Dodoma .
Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akijibu maswali bungeni mara baada ya kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 
Mhe. Dkt. Susan Kolimba Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto), akifuatilia hotuba ya bajeti bungeni jijini Dodoma 
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifafanua jambo mara baada ya kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara. 
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisalimiana na Dkt. Stergomena Tax Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) walipokutana katika viunga vya Bunge jijini Dodoma mara baada kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara. 
Mhe. Waziri Mahiga akijadili jambo na Mhe. Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Mjini katika viunga vya Bunge jijini Dodoma mara baada ya kupitishwa kwa hotuba ya bajeti ya Wizara 
Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Naibu Waziri Kolimba wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi na Watendaji wa Wizara waliohudhuria tukio la uwasilishwaji wa bajeti ya Wizara bungeni jijini Dodoma.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KIWANDA CHA NYAMA CHAPIGWA FAINI YA MILION 5 KWA KUSHINDWA KUKIDHI VIGEZO VYA USAFI WA MAZINGIRA

$
0
0
Na Mahmoud Ahmad Dodoma

Kiwanda cha nyama cha Tanzania (TMC) kimepigwa faini ya Milion 5 baada ya kukiuka kanuni za uhifadhi wa mazingira na kuchelewa kutekeleza agizo walilopewa kuhakikisha wanafanyiakazi maagizo waliyopewa juu ya kufanyiakazi kanuni za utunzaji wa mazingira ikiwemo kufanya tathmini mazingira kabla ya kuanza kazi.

Akizungumza wakati akikagua machinjio hayo na kiwanda hicho cha nyama, Naibu waziri wa nchi Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kangi Lugola ambapo Ameelezea kutoridhishwa na hali ya mazingira kiwandani hapo.

Akitoa tamko hilo ,Naibu waziri Lugola alisema kuwa kulingana na sheria za usimamizi na usafi wa mazingira ni sharti kiwanda hicho kitozwe faini ili iwe fundisho kwa viwanda vingine kufuata taratibu ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya mazingira kabla ya kuanza shughuli za uzalishaji.

Pamoja na mambo mengine Lugola alikiagiza kiwanda hicho kuelekeza taka ngumu kwenye dampo la jiji lililopo Chidaya -Ntyuka ili kuepuka madampo yasiyo rasmi yanayozagaa katikati ya jiji na kukuta mizoga ya nyama ikiwa imezagaa maeneo mbali mbali.

Awali akisoma taarifa kwa naibu waziri Lugola,Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho Aron Luziga alizungumzia changamoto zilizopo kiwandani hapo kuwa ni pamoja na mfumo wa maji taka usio rasmi kutokana na gharama kubwa ya ujenzi pamoja na upatikanaji wa umeme wa uhakika hali inayokwamisha shughuli za uzalishaji .Alisema,hali ya kukatika katika kwa umeme kiwandani hapo inakwamisha shughuli za uzalishaji hivyo kuiomba serikali kuangalia namna ya kuboresha miundombinu ya umeme ili kukidhi mahitaji 

"Lengo la kiwanda hiki ni kuwa kinara katika uzalishaji wa nyama na kusafirisha nchi nyingi zaidi duniani hii ikiwa ni pamoja na uchakataji wenye kiwango kuendana na soko La kimataifa," alisema Luziga.Wakati huo huo Naibu waziri Kangi Lugola ameliagiza Baraza la usimamizi wa mazingira la Taifa (NEMC) kushirikiana na uongozi wa jiji la Dodoma kukagua kwa undani mifumo ya maji taka ya kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti cha Sunshine kilichopo katika kijiji cha Zuzu.

Hatua hiyo imekuja kutokana na kushindwa kuibaini mifumo ya majitaka kiwandani hapo kutokana na kuwa kiwanda kimesitisha uzalishaji kutokana uhaba wa malighafi kiwandani hapo.Kutokana na hayo Naibu waziri Lugola emeutaka uongozi wa kiwanda hicho kuingia mkataba na wakulima ili waweze kupata malighafi ambazo zitawezesha kiwanda hicho kuwa na uzalishaji wakati wote.

"Ni kweli tunahitaji Tanzania ya viwanda,lakini viwanda hivyo vije kwa kuzingatia sheria za mazingira ili kuyahifadhi na kwa manufaa ya vizazi vijavyo," alisema.Hata hivyo alisema viwanda vinapaswa kuchochea wananchi kuondokana na umaskini hivyo ni wajibu kushirikiana na wananchi bega kwa bega kupata solo la uhakika.
Naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano na mazingira Kangi Lugora akitoa maelekezo kwa Mtendaji mkuu wa kiwanda cha nyama Aroan Luziga kushoto pichani wakati alipotembelea kiwanda hicho eneo la zuzu njee kidogo ya jiji la Dodoma 
Pichani ni sehemu ya bidhaa za nyama ikiwa teyari kusafirishwa nje ya nchi kama ilivyokutwa wakati wa ziara ya naibu waziri wa muungano na mazingira Kangi Lugora jana jijini hapa 
Daktari wa mifugo katika kiwanda hicho akitoa maelekezo ya sehemu mbali mbali za kiwanda hicho mbele ya Naibu waziri wa muungano na mazingira Kangi lugora jana jijini hapa

DKT ABBASI: SERIKALI YA AWAMU YA TANO IMEFIKIA HATUA HII KATIKA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images