Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

Dk.Tulia azindua Tulia Marathon jijini Dar es Salaam

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Taasisi ya Tulia Trust imezindua Tulia Marathon itakayofanyika Mei 6 katika uwanja Sokoine jijini Mbeya.

Akizungumza na waandishi habari wakati wa uzinduzi wa Tulia Marathon, Mratibu wa mashindano hayo na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson amesema kuwa mashindano ya mbio hizo kwa fedha zitakazopatikana ni kwa ajili ya afya hususan afya ya mtoto kwa jamii ya Mbeya.

Dk. Tulia amesema kuwa amekuwa anaungwa mkono na wadhamini katika kufanikisha taasisi hiyo kuendelea kusaidia jamii katika maeneo mbalimbali katika kuandaa michezo.Amesema kuwa mashindano ya mbio hizo yatakuwa na muonekano tofauti na mengine yaliyowahi kufanyika nchini kutokana na kujumuisha kila kundi katika jamii.

Aidha amesema kuwa mashindano hayo yatakuwa ya kilomita 42 Full , Half Marathon 21 , wanafunzi kwa mbio za kilomita Tano , mbio za baiskeli kilomita 150 kwa wanaume na kilomita 75 kwa wanawake, Kilomita tano watakimbia watu kwa ajili ya kujifurahisga pamoja na watoto watakimbia kilomota mbili.

Fomu kwa ajili ya maombi ya kushirikia mashindano ya Tulia Marathon zinapatikana katika tovuti yawww.tuliatrust.org

Wadhamini wa mashindano ya Tulia Marathon hayo ni Mo Dewj Foundation, Mantra Tanzania, Tatu Muzuka pamoja na Derm Electrics T LTD.
01.Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akizungumza na waandishi habari kuhusiana na uzinduzi wa Tulia Marathon itakayofanyika Mbeya, leo jijini Dar es Salaam.
02. Afisa Mkuu wa Masoko wa wa Tatu Mzuka , Sebastian Maganga akizungumza kuhusiana na kudhamini mashindano ya Tulia Marathon
Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akimkabidhi tshirt, Afisa Mkuu wa Masoko wa wa Tatu Mzuka , Sebastian Maganga kwa kutambua mchango wa Tatu Muzuka katika kudhamini mashindano hayo katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

MUHIMBILI KUPANDIKIZA FIGO WAGONJWA 200 KWA MWAKA

$
0
0
Dar es salaam, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeweka mipango ya muda mrefu na muda mfupi ili kuhakikisha huduma ya upandikizaji figo inakuwa endelevu, na imedhamiria kupandikiza figo kwa wagonjwa zaidi 200 kwa mwaka.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dare es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja wa MNH, Aminiel Aligaesha wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuruhusiwa wagonjwa wawili ambao wamepandikizwa figo Aprili mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Amesema katika mpango wa muda mfupi, kila mwezi hospitali hiyo itapandikiza figo wagonjwa watano, hivyo kwa mwaka itakuwa imefanikiwa kupandikiza figo wagonjwa 60.

“Mipango ya muda mrefu ni kuwa na sehemu maalum ya upandikizaji figo na hivi karibuni MNH itaanza ujenzi wa jengo jipya la ghorofa saba na katika jengo hilo tutatenga sehemu maalum ya upandikizaji figo , kila siku mgonjwa mmoja atapandikizwa figo, kwa wiki tutakuwa tumepandikiza figo wagonjwa watano, kwa mwezi wagonjwa 20 na kwa mwaka tutafanikiwa kupandikiza figo wagonjwa 240,’’ amesema Aminiel.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Magonjwa ya Figo Muhimbili , Dkt. Jacqueline Shoo amesema tukio hilo ni la kihisoria kwani mwaka jana hospitali ilifanikiwa kupandikiza figo mgonjwa mmoja na Aprili mwaka huu hospitali hiyo imepandikiza figo wagonjwa wanne kwa mfululizo.Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo MNH, Dkt. Onesmo Kisanga amesema takribani wagonjwa 800 nchini wanasubiri huduma ya upandikizaji figo na kati ya hao 50 tayari wameandaliwa.

Kwa upande wao wagonjwa waliopandikizwa figo na kuruhusiwa leo, Bi. Suzana John na Bi. Asha Athuman Kisebengo wameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbii pamoja na waaalam wake kwa kuwapatia matibabu ya ubingwa wa juu ambayo awali hayakuwepo nchini.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Dkt. Jacqueline Shoo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya wagonjwa wawili; Suzana Athanas John (22) na Asha Atuman Kisabengo (28) kupandikizwa figo kila mmoja na kuruhusiwa kurejea nyumbani leo. Kutoka kushoto ni mtaalamu katika vyumba maalumu vya wagonjwa wa waliopandikizwa figo, Elizabeth Sephen, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Dkt. Onesmo Kisanga na Dkt. Muhidini.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Wateja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha akitoa maelezo ya awali kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu upandikizaji figo kwa wagonjwa wanne. Upandikizaji huo ulianza tarehe 16-18 Aprili, 2018.
Asha Kisabengo (28) akiwashukuru madaktari na wataalamu wengine kwa mwezesha kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya kupandikizwa figo katika hospitali hiyo.
Mtaalamu kwenye vyumba maalumu vya wagonjwa wa waliopandikizwa figo, Elizabeth Stephen akieleza jinsi walivyokuwa wakitoa huduma maalumu kwa ndugu waliotoa figo na kwa wagonjwa waliopandikizwa figo hadi kufanikiwa kuruhusiwa kurejea nyumbani leo.
Asha Kisabengo akilia kwa furaha baada ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kupandikiza figo na kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya figo zake kushindwa kufanya kazi.

Woolworths yafungua duka Mlimani City, yajipanga kufunga lingine Dodoma

$
0
0
Kampuni ya nguo la Woolworths imefungua duka mpya la nguo lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam, likiwa ni duka la tano la kampuni hiyo kwa hapa nchini.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi huo, Mwenyekiti wa Woolworths Tanzania, Ali Mafuruki alisema huo ni mwendelezo kampuni hiyo kufungua maduka ambayo yanauza nguo zenye viwango bora na hivyo kuwataka wananchi kutembelea maduka hayo ili kununua nguo.

Alisema baada ya ufunguzi wa duka hilo wamejipanga kufunga duka lingin makao makuu ya nchi Dodoma ili kuwasogezea bidhaa zao wateja wao na hasa katika kipindi hiki ambacho viongozi wengi wa serikali wamehamia mkoani humo.

"Ni hatua nzuri kwenda mbele, uchumi kwa sasa ni mgumu, wakati wengine wafunga maduka sisi tunafungua kubwa nchini kuliko yote, tumeweza kudhibiti mdororo wa uchumi pamoja na kuwa tumeshindwa kufikia malengo yetu lakini tumekuwa imara,

"Kuanzia mwaka kesho tutaanza kuangalia ujenzi wa duka Dodoma, Dodoma ni makao makuu ya nchi, wapo viongozi wa Serikali na hakuna huduma kama hizi. Tumeanza kuongea na wajenzi ili katika miaka miwili ijayo tufungue duka Dodoma," alisema Mafuruku.

Aidha alizungumza kuhusu wafanyabiasha ambao wanakwepa kodi ambapo kuhusu kampuni yao alisema wamekuwa wakilipa kodi zote ambazo wanatakiwa kulipa na kutumia nafasi hiyo kuwataka wanaokwepa kulipa kodi waache tabia hiyo.

"Mtu anayefanya biashara kwa kutokuwa mwaminfu ipo siku atapambana na serikali, ila sisi sitaki kusikia mfanyakazi anakuja kusema bosi hii pesa nimemhonga mtu wa TRA, sisi kila siku tunawafundisha wafanyakazi wetu walipe kodi zote, hata kama ni kubwa," alisema.
Mwenyekiti wa Woolworths Tanzania, Ali Mafuruki akikata utepe kuashirikia ufunguzi wa duka duka la nguo la Woolworths lililopo jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Woolworths Tanzania, Ali Mafuruki akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa duka la nguo la Woolworths lililopo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Rabi Hume)
Mwenyekiti wa Woolworths Tanzania, Ali Mafuruki akiingia katika duka la nguo la Woolworths lililopo jijini Dar es Salaam. 

TANAPA YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU MKOANI SIMIYU

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .

Shirika la Hifadhi za Taifa leo limekabidhi mchango wa Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule tatu za vipaji maalumu katika mkoa wa Simiyu za Simiyu Ufundi , Simiyu Wavulana na Simiyu Wasichana .

Mchango huo umekabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka.

Fedha hizi zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa shule maalum ya sekondari ya ufundi mkoani Simiyu ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya mkoa katika kuimarisha sekta ya elimu ambapo pia mkoa umepanga kuje nga shule nyingine maalum mbili za sekondari za wasichana na wavulana.

Kwa pamoja Mhe Mtaka aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga waliahidi kuzitumia fedha hizo kama zilivyokusudiwa na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha umuhimu wa wananchi kuheshimu sekta ya uhifadhi kwa kuwa ina manufaa makubwa kwao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi aliahidi kuendelea kuwaunga mkono wana Simiyu kwa kuwa mkoa huo umekuwa mstari sa mbele katika kusimamia sheria za hifadhi hususan Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kuzuia uingizaji wa mifugo pamoja na majangili.

Shule ya Ufundi ya Simiyu inatarajiwa kugharimu kiasi cha Shilingi Milioni 350 hadi itakapokamilika na wadau mbalimbali wameombwa kuunga mkono jitihada hizo za Simiyu.
 Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akitoa neno la utangulizi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Hundi kwa ajili ya kuendeleza sekta ya elimu katika mkoa wa Simiyu. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Hundi kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu katika mkoa wa Simiyu.kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw Festo Kiswaga . 
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa( TANAPA) Allan Kjazi akikabidhi Hundi ya Kiasi cha Sh Mil 50 kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu katika mkoa huo ,wengine kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi ,Bw Festo Kiswaga . 
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ,Anthony Mtaka akiteta jambo na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za TAifa (TANAPA) Pascal Shelutete mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya makabidhiano ya hundi kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu katika mkoa wa Simiyu.

KONGAMANO LA TANZANIA YA VIWANDA LAFANA MKOANI IRINGA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano wakati wa Kongamano la Tanzania ya Viwanda lililohusu maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi Mkoani Iringa.
Baadhi ya wajumbe wa Kongamano la Tanzania ya Viwanda wakati wa maandalizi ya kuifikia Siku ya Mei Mosi wakiimba wimbo wa umoja na mshikamano, Mkoani Iringa.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage akiongea umuhimu wa kuwa na Tanzania ya Viwanda wakati wa Kongamano la maandalizi ya Mei Mosi lililofanyika mkoani Iringa Aprili 27, 2018.
Baadhi ya wajume wakifuatilia Kongamano la maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi walipokutana kujadili masuala ya Tanzania ya Viwanda Aprili 27, 2018.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

UMISSETA YAZINDULIWA MTWARA

$
0
0

JOSEPH MPANGALA -Mtwara.

Mashindano ya Copa CocaCola Umisseta 2018 yamezinduliwa rasmi katka mkoa wa Mtwara.

Akizindua mashindano hayo kaimu mkuu wa mkoa wa Mtwara, ambaye ni mkuu wa wilaya, Evod Mmanda ametaka washiriki ambao ni wanafunzi kuyatumia kuboresha afya na akili ili kuepuka kushiriki katika matendo ya kihalifu kama matumiz ya madawa ya kulevya na kutojihusisha na mapenzi kabla ya wakati.

Mmanda amesema michezo inajenga afya na kuboresha mwili na kusema mwanafunzi atakayejihusisha katika mapenzi na kumpa mwenzake ujauzito sheria zitachukuliwa kama ilivyo kwa watuhumiwa wengine hivyo watumie muda huo kushiriki michezo.

“Hakuna muda wa ziada usiotumika vizuri wa kwenda kufanya mahusiano yaliyo nje ya utaratibu yanayopelekea mapenzi kwa watoto wa shule wote wa pande mbili,sheria iko pale pale atachukuliwa hatua kama mtu mwingine kwa watoto wa kike wakiwa kama waathirika wa kwanza na watoto wa kiume,ukamataji unakamata vile vile,”amesema Mmanda

Brand meneja wa Coca Cola Tanzania, Sialovise Shayo amesema kikubwa kinachofanyika ni kugawavifaa vya michezo kwa mpira wa miguu na mpira wa kikapu na kutoa viburudisho vinavyozalishwa na kampuni hiyo kwa wanafunzi. “Kama kampuni tunaamini vijana ili wawe imara kakili ni lazima wafanye michezo hivyo tunawapatia vifaa vya michezo,maji na Cocacola kwasababu vipaji haviboreshi tu elimu lakini pia wakiwa wachezaji bora wanaweza kucheza lgi za kimataifa kama anavyofanya Mbwana Samata,”amesema Shayo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda akipokea zawadi ya Mpira kutoka kwa Brand Meneja wa Cocacola Tanzania Sialovise Shayo katika uzinduzi wa Mashindano ya Copa cocacola Umisseta Mtwara.
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda akimkabidhi Vifaa vya michezo Mwalim wa shule ya seminary ya Mtwara Sisters Philipo Milanzi
 Mkuu wa Wilaya Avod Mmanda akikagua moja ya Timu zinzoshiriki katika Mashindani ya copa cocacola Umisseta mkoani Mtwara.
 Mkuu wa Wilaya Avod Mmanda akikagua moja ya Timu zinzoshiriki katika Mashindani ya copa cocacola Umisseta mkoani Mtwara.

MAKAMU WA RAIS AHANI MSIBA WA KANDORO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu ya maombelezo ya Marehemu Abbas Kandoro aliyefariki jana kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole mke wa Marehemu Abbas Kandoro, Mariam Kandoro nyumbani kwa marehemu Mbweni jijini Dar es salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  

RMO,DMO TENGENI SIKU ZA UCHUNGUZI WA SARATANI-WAZIRI UMMY

$
0
0
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka waganga wakuu wote wa mikoa na wilaya nchi nzima kutenga siku moja kwa mwezi kwa ajili ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti kwa wanawake na tezi dume. 

Waziri huyo ametoa agizo hilo mkoani Tanga leo wakati akizindua kampeni ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi na uchunguzi wa saratani kwa wakina mama katika kituo cha Afya cha Ngamiani jijini hapa.

Amesema kuwa hali ya saratani kwa nchi zinazoendelea haswa zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania wagonjwa wa saratani wamekuwa wakiongezeka kila mwaka. Amesema kuwa Tanzania kunakuwa na wagonjwa 50,000 waliogunduliwa na tatizo la saratani.

Amesema kuwa katika wagonjwa hao asilimia 33 wanakutwa na saratani ya shingo ya kizazi na asilimia 12 wanagundulika na saratani ya matiti. Amebainisha kuwa kila katika wagonjwa 100,wagonjwa 80 wanakuwa katika hatua za mwisho za ugonjwa na kufanya matibabu kuwa magumu. 



WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza leo Jijini Tanga wakati alipozindua kampeni ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi na uchunguzi wa saratani kwa wakina mama katika kituo cha Afya cha Ngamiani jijini hapa.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni Mkuu wa wilaya ya
Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni
hiyo
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimuakifurahia jambo mara baada ya kuzindua kampeni hiyo ya chanjo


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

RUVUSHOOTING APAPASWA NA MAJI MAJI 3 – 1, MARCEL AONDOKA NA MPIRA

$
0
0
Mchezo kati ya Maji Maji na Ruvu shooting katika uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma umemalizika na Maji Maji kuibuka mbabe wa bao 3 – 1 Mabao yote matatu ya Maji Maji yamefungwa na Marcel Boniventure na baada ya mpira kumalizika amekabidhiwa Mpira baada ya kufunga magoli yote matatu.

Chuo cha Kodi Chapongezwa Kuwajengea Uwezo Wanafunzi Wake

$
0
0


Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani kutka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Michael Muhoja akizungumza alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inayowakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea. Kutoka kulia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Kodi (ITASO), Bi. Happines Gherabaster, Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Dkt. Lewis Ishemoi na Naibu Mkuuwa Chuo cha Kodi A
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Dkt. Lewis Ishemoi akizungumza wakati wa maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inayowakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Kodi (ITASO), Bi. Happines Gherabaster akifafanua jambo wakati wa maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inayowakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea. 

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouely akielezea namna anavyofurahishwa na jinsi Serikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya kodi wakati wa maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inatwakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea.

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Kodi wakifuatilia hutuba ya mgeni rasmi Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani kutka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Michael Muhoja (hayupo pichani) ambaye alimwakilisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere katika maadhimisho ya tatu ya Siku ya Ujuzi na Taaluma ya Chuo cha Kodi (ITA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ya Ujuzi na Taaluma (Career Day) inatwakutanisha wanafunzi na wadau mbalimbali ambapo wanafunzi uonyesha umahiri wao katika fani wanazosomea 

AfDB YAAHIDI KULING'ARISHA JIJI LA DODOMA NA KUONGEZA MABILIONI YA DOLA KUCHOCHEA MAENDELEO YA TANZANIA

$
0
0

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma 

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina, amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini na kuahidi kuwa atahakikisha Tanzania inaendelea kunufaika na misaada na mikopo yenye masharti nafuu kutoka Benki hiyo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kisasa katika Jiji la Dodoma na mradi wa kuzalisha umeme wa Stieglers Gorge. 

Akiwa katika uwanja wa ndege Jijini Dodoma, Dkt. Adesina amemmwagia sifa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna anavyosimamia ukuaji wa uchumi uliofikia wastani wa asilimia 7 kwa mwaka pamoja na kupambana na vitendo vya ufisadi, rushwa, kuimarisha uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi, kupiga vita matumizi mabaya ya rasilimali za umma ili kuwaondoa wananchi wake katika umasikini. 

Dkt. Adesina amesema kwa kutambua mchango huo pamoja na umahili wa Waziri wa Fedfha na mipango Dkt. Philip Mpango, wa kusimamia uchumi na sera ya bajeti na fedha, benki yake itaendelea kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha ili nchi iweze kupiga hatua kubwa kupitia miundombinu mbalimbali inayotekelezwa kupitia benki yake na washirika wengine wa maendeleo. 

Miongoni mwa miradi ambayo Benki hiyo imepanga kusaidia ni ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa utakaojengwa katika eneo la Msalato, nje kidogo ya Jiji la Dodoma ambapo kwa kuanzia benki hiyo itatoa zaidi ya shilingi bilioni 200. 

“Tumekuwa na majadiliano ya kina na Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kuhusu mradi wa kuzalisha umeme wa Stieglers Gorge ambao utazalisha Kw 2100, Benki yetu itaangalia namna ya kutoa fedha kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa mradi huo mkubwa” alisema Dkt. Adesina. 

MAKAMU WA RAIS AZINDUA SIKU YA MWANAMKE WA MFANO TANZANIA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Wanawake walikuwa na mchango mkubwa katika harakati za Uhuru wan chi hii. 

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Siku ya Mwanamke wa Mfano Tanzania iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) .

Makamu wa Rais alisema Ni dhahiri kuwa wanawake walikuwa na mchango mkubwa sana. Walifanya kazi kubwa katika uhamasishaji, malezi ya watoto na vijana na kusimama bega kwa bega na kuunga mkono wanaume waliokuwa mstari wa mbele katika mapambano. 

Walifanya mengi nyuma ya pazia ambayo yalikuwa na mchango mkubwa katika Taifa letu. Mapenzi yao, subira yao na mchango wao wa hali na mali ndio uliowapa nafasi wanaume kufanikisha harakati za uhuru kwa kuwa wanawake waliwapa wepesi kwa kuwapunguzia mzigo mzito uliokuwa mabegani mwao. Haiyumkini, katika ngao yetu ya Taifa, ikatambua nafasi ya mwanamke kwa kuwekwa sambamba na mwanaume. 

Makamu wa Rais aliendelea kusema kutokana na kazi kubwa ya wanawake jasiri na mashujaa waliotutangulia, wanawake wa nchi yetu wameendelea kutoa mchango mkubwa katika Uongozi katika nchi yetu na nje ya mipaka yake. 

Makamu wa Rais alitoa wito kwa Wanawake na kusema Tuzo za “Mwanamke wa Mfano Tanzania” ziwe chachu yetu Wanawake katika kuchapa kazi, kuungana, kushikamana katika kuleta maendeleo miongoni mwetu na jamii nzima ya Watanzania. Sisi wanawake ni nusu ya watu wote nchini. Sisi tukijiongeza tukaendelea, kaya zetu zinaendelea na hatimaye nchi inaendelea. 

Makamu wa Rais aliwataka Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) kuchukua jukumu lenu la kuwasemea, kuwatetea na kuwaunganisha wanawake wote wa Tanzania wana CCM, wasio wana CCM na wasio na vyama. Ndio wajibu wa UWT mliopewa na Katiba ya CCM. Katika nchi yetu, hamna chombo chochote kikubwa cha kuwaunganisha wanawake isipokuwa ninyi. Nawakumbusha kuwa nanyi mnatazamwa na wanawake wa nchi yetu. 

Jumla ya Tuzo 26 za Mwanamke wa Mfano zilitolewa .
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akizindua Siku ya Wanawake wa Mfano Tanzania iliyoandaliwa na Umoja wa wanawake wa Tanzania (UWT) katika ukumbi wa PTA, jijini Dar es Salaam 
Mama Fatma Karume akionyesha juu tuzo ya Mwanamke wa Mfano Tanzania ikiwa sehemu ya kutambua mchango wake katika harakati za Mapinduzi ambapo yeye alikuwa mke wa Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Abeid Aman Karume 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi tuzo ya Mwanamke wa Mfano mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete. 
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Anna Makinda akionyesha juu Tuzo yake ya Mwanamke wa Mfano mara baada ya kukabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 
Mama Fatma Karume mke wa Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akitoa nasaha zake mara baada ya kupokea tuzo ya Mwanamke wa Mfano iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT). 
Picha na Ofisi ya Makamu 

KIGOMA WAOMBWA KUICHANGIA TIMU YA WANAWAKE YA MKOA HUO ILI IFANYE VEMA

$
0
0
Na Ripota Wetu, Kigoma
WADAU mbalimbali wa maendeleo na soka wameombwa kuiunga mkono timu ya Wanawake wa Mkoa ya Kigoma Sisters ili waweze kuendelea kufanya vema kwenye michuano mbalimbali wanayoshiriki.

Ombi hilo limetolewa leo na moja ya viongozi wa UWT Mkoa wa Kigoma Miriam Ntakisivya pamoja na Kaimu Katibu wa Vijana mkoa huo Adam Kagoma baada ya wao kukabidhi chakula kwa Nahodha wa timu hiyo Sophia Mwasikili.

Lengo la chakula hicho ni kuwapa nguvu kwa lengo kuwapa hamasa ya kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi za ndani na zile watakazocheza nje ya Mkoa Kigoma.

Akizungumza baada ya kukabidhi chakula hicho Ntakisivya amesema ni vema wananchi wa Mkoa wa Kigoma wakaendelea kuichangia timu hiyo kwani inafanya vizuri na ana uhakika ikisaidiwa itafika mbalimbali kisoka.

"Nitoe ombi watu waendelee kuipambania timu yetu ya Mkoa ambayo kwa sasa inafanya vizuri.Pia nimpongeze Miss Ubungo mwaka 2014 Diana Kato kwa kuguswa na kuchangia kile alichokuwa nacho,"amesema.

Amesema watu watakapoisaidia timu hiyo mbali ya kuwafanya wachezaji na viongozi kuandaa mazingira mazuri ya kimchezo pia itatoa nafasi ya timu hiyo kutatua changamoto ambazo wanakabiliana nazo ambazo nyingine zinatokana na kutokuwa na vyanzo vya kutosha kumaliza yale ambayo wanakabiliana nayo.
 Mwakilishi UWT vijana Mkoa wa Kigoma, Miriam Ntakisivya akikabidhi msaada kwa Capten wa timu ya Kigoma Sisters, Sophia Mwasikili kwa ajili ya kuendeleza mpira wa miguu kwa wanawake wa Mkoa wa Kigoma.
 Mwakilishi UWT vijana Mkoa wa Kigoma, Miriam Ntakisivya pamoja na Kaimu Katibu wa Vijana moa wa Kigoma, Adam .M. Kagoma wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wanawake wa Mkoa ya Kigoma Sisters

RAMADHAN KAREEM 2018 (1439 A.H.)

MEYA JIJI LA DAR KUSHUHUDIA MTANANGE WA SIMBA, YANGA LEO

$
0
0
MEYA wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita atakuwa miongoni mwa watazamaji wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaowakutanisha Simba na Yanga.

Mchezo huo wa aina yake utachezwa leo saa 10 jioni katika dimba la Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Ofisa Habari Ofisi ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam Christina Mwagala Meya huyo atakuwa miongoni mwa watazamaji wa mtanange huo mkali.

Kwa kawaida mechi ya Simba na Yanga huwa na watazamaji wengi wakiwemo viongozi mbalimbali wa Serikali na Wabunge,Ifahamike kuwa Mwita ni miongoni mwa maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu .

Katika mchezo huo Simba wanaingia uwanjani wakiwa wanaongoza ligi baada ya kujikusanyia pointi 59 ikicheza michezo 25 wakati Yanga wana pointi 48 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 23.

IDADI YA WAATHIRIKA MAFURIKO YA MVUA KATA YA MWARU YAFIKIA ZAIDI YA WAKAZI 700

$
0
0
Na Jumbe Ismailly, IKUNGI 

IDADI ya wakazi wa vijiji vya Kaugeri na Mduguyu,kata ya Mwaru,wilaya ya Ikungi waliokosa makazi kutokana na nyumba zao kuanguka kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani hapa zimeongezeka kutoka kaya 22 zanye zaidi ya wakazi 154 hadi kufikia kaya 177 zenye zaidi ya wakazi 700 baada ya nyumba189 kuanguka.

Ongezeko la idadi hiyo ya wakazi linatokana na mvua kubwa iliyonyesha apr,16 hadi 18,mwaka huu na kusababisha mto kuacha njia yake na kulenga katika Kitongoji cha Mwasusu,na ndipo kaya 22 zenye zaidi ya wakazi 154 katika vijiji vya Kaugeri na Mduguyu,Kata ya Mwaru kukosa makazi baada ya nyumba 34 kuanguka.u

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mwaru,Hamisi Malongo alisema hayo alipokuwa akitoa taarifa za athari zilizotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa Mkoani Singida na kuongeza kwamba pamoja na nyumba hizo vile vile makanisa matatu ya FPCT na AIC yalianguka kufuatia mvua hizo.

“Na tuliloligundua sisi kama viongozi kama serikali upande wa kata kwamba vijiji vya Kaugeri na Mduguyu ni vijiji vya mpakani na Mkoa wa Tabora ambavyo ndiyo bonde la Mto Wembere unapita kwa hiyo mvua inaponyesha pande zote za dunia kwa hiyo wao ni rahisi sana kuathirika na mvua hizo.”alisisitiza Malongo.
Mmoja wa wananchi walioathirika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha akiwa kwenye makazi yake mapya yaliyopo kitongoji cha Mwasusu,Kijiji cha Kaugeri akihofia wingu lililotanda kama alivyokutwa na kamera ya kituo hiki(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Baadhi ya wakazi wa vijiji vya Kaugeri na Mduguyu,kata ya Mwaru,wilayani Ikungi wakihamisha baadhdi ya vitu vilivyosalia kwenye makazi yao ya zamani na kuhamia kwenye eneo lililotengwa na serikali kwa ajili ya wahanga hao wa mafuriko yaliyotokana na mvua zilizonyesha kwa sisku tatu mfululizo na hivyo kusababisha zaidi ya wakazi 700 kukosa mahali pa kuishi
Ni Miundombinu ya barabara ya kutoka Mlandala kwenda kwenye Kitongoji cha Mwasusu,Kijiji cha Kaugeri sehemu iliyotengwa kwa ajili ya wahanga wa mafurriko ya mvua zilivyoharibika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani Singida.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KUMEKUCHA MISS TABORA 2018

$
0
0

Kumekucha: Fomu za kushiriki mashindano ya Miss Tabora zitaanza kutolewa tarehe 02/05/2018 hadi tarehe 20/05/2018 katika ofisi zote za utamaduni za Wilaya na Halmashauri za Mkoa wa Tabora. 

Auditions kwa Wilaya zote zitaanza kufanyika tarehe 21.05.2018 hadi tarehe 04.06.2018.

Warembo wote 16 watakaokidhi vigezo wataingia kambini na kupata mafunzo mbalimbali na kushiriki kampeni na shughuli za kijamii wakisubiria fainali tarehe 07/07/2018.

Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa habari zaidi za Miss Tabora 2018.

@genevieve.tz 
@genevieve_updates
@newmisstanzania
@genampangala

👑👑👑👑👑

#MissTabora2018 
#UremboNiMalengo
#UremboNaKaziKwaMaendeleoYaJamii

SERIKALI KUENDELEA KUKOMESHA AJIRA HATARISHI ZA WATOTO

$
0
0

Serikali imedhamiria kuendelea kukomesha ajira hatarishi za watoto ili kuhakikisha kuwa watoto wanalindwa na kuwapa nafasi stahiki kulingana na sheria na kanuni zilizopo nchini. 

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipohudhuria katika kilele cha Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 28 Aprili ambapo Kitaifa ilifanyika Mkoani Iringa. 

Waziri alieleza kuwa, katika mapambano haya ya ajira hatarishi kwa watoto ni moja ya utekelezaji wa kampeni zinazolenga kuharakisha utekeleezaji wa vipaumbele vilivyomo kwenye lengo namba (8) la Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ambalo ni kuboresha mazingira ya wafanyakazi na kukomesha ajira mbaya kwa watoto. 

“Tuendelee kupiga vita ajira mbaya kwa watoto kwa kuzingatia kampeni zilizopo hasa ile ya kuboresha mazingira ya wafanyakazi ifikapo mwaka 2030 pamoja na kukomesha ajira mbaya za watoto ifikapo mwaka 2025,” alisema Waziri 
Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya washiriki wa maonesho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018 iliyoadhimishwa Kitaifa Mkoani Iringa.
Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia mfano wa namna bora ya kumuokoa mfanyakazi pindi apatapo ajari sehemu ya kazi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018 Iringa. 
Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Mzee Juma Nyinge aliyetembelea katika mabanda ya maonesho wakati wa Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani Aprili 28, 2018. 

WAJASIRIA MALI Z'BAR WAPEWA MBINU MPYA.

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

WANAWAKE visiwani Zanzibar wameshauriwa kutumia vizuri fursa ya ujasiriamali kwa lengo la kujiongezea kipato na kujiajiri wenyewe.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya New Vision Consortium (NVCT) Pily Khamis Lapda, amesema wanawake wengi hapa nchini wamekuwa wakifanya shughuli za ujasiriamali kwa mazoea jambo linalopelekea kushindwa kufikia malengo yao ya kumiliki mitaji mikubwa ya kibiashara.

Amesema zipo njia mbali mbali za kuwakomboa wanawake kiuchumi zikiwemo kupenda na kuamini shughuli za ujasiriamali kama nyenzo ya kujikomboa kiuchumi.Amewashauri wanawake nchini kujiamini pindi wanapoanzisha biashara zao sambamba na kujiwekea malengo ya kudumu ya kibiashara yatakayowasaidia kumiliki mitaji mikubwa ya kibiashara. 

Mkurugenzi huyo Pily, akizungumzia malengo ya taasisi yake inayoendesha na kusimamia mafunzo ya kuyajengea uwezo wa kitaaluma makundi mbali mbali ya kijamii ili kupata uwezo wa kutumia ipasavyo fursa za ujasiriamali wenye maendeleo.“Wanawake tuwe mstari wa mbele kujifunza mbinu mbali mbali za kujikwamua kiuchumi, pia tujitume na kuwa wabunifu katika biashara zetu ili nasi tuwe miongoni mwa wajasiriamali wa kimataifa.”, amesema Mkurugenzi huyo.

Akitoa mada ya Uvumbuzi binafsi, mtaalamu wa Saikolojia na maendeleo ya vijana, Joseph Mrindo amesema wanawake waliopo katika sekta ya ujasiriamali wanatakiwa kuondokana na dhana ya ujasiriamali mdogo mdogo kwani hali hiyo inasababisha kudumaa kiakili na kushindwa kufikia malengo yao ya kumiliki biashara kunwa na makapuni.

Ameeleza kuwa Zanzibar ni sehemu muhimu yenye fursa za kibiashara hivyo wanawake wanatakiwa kutumia nafasi hiyo kujiongeza kibiashara.Mtaalamu huyo, amewasihi wajasiriamali kufuata maelekezo na mbinu mbali mbali za maendeleo ya kibiashara ili wawe na mitaji mikubwa itakayowawezesha kupewa mikopo kwa wakati na benki mbali mbali nchini.

Naye mshiriki wa mafunzo hayo, Munawar Sleiman Mbarouk amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili wajasiria mali ni ukosefu wa mitaji na ujuzi wa kufanya biashara zenye tija kwa mjasiria mali mmoja mmoja na vikundi.Mafunzo hayo ya siku mbili yanatolewa na taasisi ya New vision consortium (NVCT)iliyopo Zanzibar na jumla ya washiriki 200 kutoka taasisi binafsi na za umma wanapewa ujuzi huo wa ujasiriamali.

Wadhamini wa mafunzo hayo ni pamoja na NMB, ZSSF, ZURA na IQUITY BANK
MKURUGENZI wa New vision consortium Pily Khamis Lapda(aliyekaa katikati) akifungua mafunzo ya siku mbili ya ujasiriamali kwa wanawake wa Zanzibar yaliyofanyika katika Skuli ya Haile-Sela-ssie.
BAADHI ya washiriki katika mafunzo hayo kutoka taasisi binafsi na za umma wakifuatilia kwa makini mada mbali mbali zilizowasilishwa katika mafunzo hayo, huko Skuli ya Haile-Sela-ssie.
MSHIRIKI wa mafunzo ambaye pia ni mjasiria mali kutoka U.WT. jimbo la Mwera Salama Mohamed Tahir akichangia mada ya uvumbuzi binafsi.

WANAFUNZI WAELEMISHWA KUHUSU CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

$
0
0

Muuguzi wa kituo cha Afya Madaba wilayani Songea Ponsiana Haule akimpatia chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Madaba Day wilayani Songea Happines Kinyunyu siku ya kwanza ya uzinduzi wa chanjo hiyo.
Mganga mkuu wa halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma Janeth Makoye akiongea na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha 1 hadi 3 wa shule ya sekondari Madaba Day ikiwa ni juhudi za kuwashawishgi wanafunzi hao kukubali kupewa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi, kufuatia mgomo wa wanafunzi hao baada ya kuelezwa na wazazi wao wasikubali kupatiwa chanjo hiyo baada ya kiongozi mmoja wa dini akiwa katika ibada ya Jumapili mwishoni mwa wiki kuwataka wazazi wasikubali watoto wao kupatiwa chanjo hiyo. 
Muuguzi wa kituo cha Afya Madaba wilayani Songea Ponsiana Haule akimpatia chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Madaba Day wilayani Songea Happines Kinyunyu siku ya kwanza ya uzinduzi wa chjanjo hiyo.PICHA NA MUHIDIN AMRI
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images