Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI(WCF) UMEKUWA MSHINDI WA PILI KATIKA MASUALA YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI

$
0
0
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeibuka mshindi wa pili katika masuala ya usalama na afya mahala pa kazi katika maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi nchini ambayo huadhimishwa duniani kote tarehe 28 Aprili kila mwaka.

Maadhimisho haya huratibiwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) nchini na kwa mwaka huu yamefanyika Mkoani Iringa yakitanguliwa na maonyesho kutoka kwa wadau kuanzia tarehe 26 Aprili na kufikia kileleni leo tarehe 29.

Mgeni Rasmi katika kilele cha Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu ameipongeza WCF kwa ushindi walioupata na kuwasihi kuendelea kutoa elimu kwa wadau wake. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF Masha Mshomba, amefafanua kuwa moja ya malengo ya uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni kukuza na kuendeleza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo mahala pa kazi. Mshomba ametoa ufafanuzi huo leo katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa baada ya kupokea tuzo na cheti cha Mshindi wa pili katika masuala ya afya ya usalama mahala pa kazi. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba (kulia), akipokea tunzo na cheti kutoka kwa Bw. Eric Shitindi katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu baada ya MFuko kushinda nafasi ya pili katika masuala ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi katika maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani tarehe 28 Aprili katika Uwanja wa Kichangani Iringa.
Katikati Bw. Eric Shitindi Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko baada ya kupokea tunzo na cheti katika maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi katika Uwanja wa Kichangani Iringa. (Akishikilia kombe pamoja na Bw. Shitindi ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba
Bw. Ibrahim Mussa Afisa Madai Mwandamizi – WCF akimhudumia mteja aliyetembelea banda ya WCF katika maonyesho yaliyofanyika katika viwanja vya Kichangani Iringa.
Bw. Masha Mshomba akionyesha tuzo na cheti ambavyo Mfuko umetunukiwa.
Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Uendeshaji Bw. Anselim Peter wakiwa ameshika tuzo hiyo huku, Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko huo, Bi. Naanjela Msangi, (kulia) na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Bi. Amina Likungwala, wakionyesha vyeti vya ushindi wa pili na cha ushiriki.


WAZIRI MKUU AFUNGUA KIKAO CHA KAZI MKOANI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifungua Kikao cha Kazi cha Mawaziri, Naibu Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi na Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Aprili 29, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SIMBA YAIBAMIZA YANGA BAO 1-0

$
0
0
Simba wameibuka washindi kwenye mechi dhidi ya mahasimu wao Yanga sasa unawafanya Wekundu Wa Msimbazi kuhitaji pointi 5 kutawazwa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Kikosi cha Timu ya Yanga
Kikosi cha Timu ya Simba




Shabiki wa Yanga akiwa ahamini kilichotokea




Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia kwa furaha mara baada ya timu yao kufunga goli

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA IRINGA-DODOMA KATIKA SEHEMU YA IRINGA-MIGORI-FUFU KM 189 ILIYOKAMILIKA KUJENGWA KATIKA KIWANGO CHA LAMI

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Jeremy Aguma wa pili kutoka kulia  wakivuta utepe kwenye jiwe la msingi kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami. Sherehe hizo za ufunguzi zilifanyika katika kijiji cha Ndolela kilichopo Isimani nje kidogo ya mji wa Iringa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Jeremy Aguma, Balozi wa Japan Masaharu Yoshida wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa , Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na viongozi wengine wa Serikali na wageni kutoka nje ya nchi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika sherehe hizo za ufunguzi wa barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Isimani Mkoani Iringa
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa jukwaa kuu pamoja na Balozi wa Japan Masaharu Yoshida, Waziri wa Ardhi Wiliam Lukuvi, pamoja na Waziri wa Mambo ya nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga wakifatilia sherehe za ufunguzi wa barabara ya ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Iringa mjini waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili akitokea Isimani mkoani Iringa.
Mwananchi wa Iringa mjini akipuliza pembe ya ng’ombe  wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili Iringa mjini katika ziara ya kikazi. PICHA NA IKULU

WAZIRI WA NISHATI DKT KALEMANI AZINDUA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MITA ZA LUKU JIJINI DAR

$
0
0
Na Leandra Gabriel,  ya jamii

KATIKA kuelekea uchumi wa kati wa viwanda kampuni ya Baobao Energy Systems Tanzania (BEST) imefungua kiwanda cha kutengeneza mita za umeme za luku na hii ni kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika ujenzi wa Tanzania ya viwanda na kufikia uchumi wa kati kufikia 2025.

Akizungumza katika uzinduzi huo mgeni rasmi ambaye pia Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ameeleza kufurahishwa  na kufarijika kwa kupata mwaliko wa kuzindua kiwanda hicho kwani mita za luku zinategemewa na wadau wengi nchini na amewapongeza na kuwataka TANESCO kujipanga katika kukabiliana changamoto za kukidhi mahitaji ya kutoa huduma za umeme kwa wananchi.

Aidha Dkt Kalemani ameeleza kuwa Julai mosi mwaka huu hakuna mita za luku zitakazoagizwa kutoka nje na hii ni baada ya kufanya tathimini kwa miezi mitatu na kujiridhisha na uzalishwaji wa mita hizo hapa nchini na kuanzia Mei mwaka huu mita za luku zitanunuliwa kutoka Baobab.

Pia Dkt Kalemani amewataka wamiliki wa kiwanda hiki kuzingatia uharaka wa utengenezaji, wingi wa mita hizo, ubora na upatikanaji wake kirahisi, Na ameeleza umuhimu wa mita hizi ikiwa pamoja na matengenezo pindi zinapoharibika, gharama nafuu na uharaka tofauti na zile zinazoagizwa nje na amewataka TANESCO kuunganisha umeme kwa siku zisizozidi 7.

Mwakilishi wa Wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji Aristides Mbwasi amewapongeza wamiliki na kiwanda hicho na kuahidi ushirikiano pale watakapohitaji kwani kwa sasa taifa lipo katika malengo ya kuijenga Tanzania mpya kama Serikali ya awamu ya tano ilivyoazimia.

Naye Meneja mkuu wa kampuni ya Baobab Energy Systems Tanzania, Mhandisi Hashim Ibrahim amemshukuru waziri wa nishati kwa kuja kufungua kiwanda hicho na kueleza kuwa kampuni hiyo ni ya ubia baina ya kampuni ya Comfix Engineering Ltd ya Tanzania inayomiliki hisa kwa asilimia 51 na hii ni kwa kutoa mchango wa fedha, majengo, rasilimali watu na fedha na kampuni ya EDMI ya nchini Singapore inayomiliki hisa kwa asilimia 49 
na kuchangia mtaji kupitia mitambo na teknolojia kwa ujumla.

Hashim ameeleza kuwa hawaogopi ushindani na kampuni za nje ila tatizo lao ni pale kampuni hizo zinapopewa unafuu wa gharama na uzalishaji na ameiomba serikali kutoa ushirikiano ili kuweza kujenga Tanzania ya viwanda na ameeleza kuwa wana mpango wa kutengeneza mita za gesi na maji hapo baadaye.

Kuhusu uzalishaji wa mita katika kiwanda hicho Hashim ameeleza kuwa mita zitakazotengenezwa na kuuzwa nje na ndani ya nchi zitaliongezea taifa mapato yanayotarajiwa kufikia shilingi Bilioni 97 kwa mwaka.

Pia Mkurugenzi mkuu mauzo wa Kampuni ya EDMI ya nchini Singapore Lam Wee Chee ameeleza kuwa kwa miaka 10 kampuni ya EDMI imefanya kazi na Shirika la Umeme (TANESCO) hasa kwa kusambaza mita hizo na zaidi ya mita 100000 zimenunuliwa na TANESCO kutoka EDMI na kwa sasa watawapa mfumo utakaowasaidia kusoma taarifa zote na kudhibiti wizi wa umeme.

Aidha ameeleza juhudi zao katika kuunga mkono azma ya serikali ya awamu ya tano na kuahidi kutoa huduma bora kwa wateja wao kupitia TANESCO ambao ndio wasambazaji wa mita hizo.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani sambamba na wabia wa kampuni ya Baobao Energy System akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa kiwanda hicho.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na baadhi wawakilishi kutoka Taasisi mbalimbali za kiserikali na wafanyakazi wa kiwanda cha Baobao Energy System Tanzania wakati wa kuzindua kiwanda hicho kinachojihusisha na utengenezaji wa mita la LUKU, tukio lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mkuu wa  kampuni ya Baobao Energy System Mhandisi Hashim Ibrahim akizungumzia kiwanda hicho kitakachokuwa kinatengeneza mita za LUKU hapahapa nchini wakati wa uzinduzi kilichozindukiwa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani.
 Mkurugenzi wa Mkuu wa Mauzo wa EDMI Lam Wee Chee akizungumza wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Baobao Energy System jana Jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Nishati akizindua kiwanda cha Baobao Energy System jana Jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mkuu wa Baobao Energy System Hashim Ibrahim akimuelezea jambo Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani alipokua akikagua chumba kinachotumika kutengeneza mita za LUKU wakati wa uzinduzi wa Kiwanda hicho.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akikagua mitambo inayotumika kwa ajili ya utengenezeaji wa mita za LUKU wakati wa uzinduzi wa Kiwanda hicho jana Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho namna wanavyoweza kutengeneza mita za LUKU zenye ubora.Picha zote na Zainab Nyamka.

PROFESA KABUDI AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI TUME YA KUREKEBISHA SHERIA

$
0
0

Na Munir Shemweta, Morogoro

Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi amesisitiza umuhimu wa kuwashirikisha watumishi katika mipango ya uendeshaji Taasisi kwa kuwa suala hilo lipo kisheria.

Aidha, alisema kwa miaka yote Serikali imekuwa ikisisitiza Taasisi kujenga na kutekeleza utaratibu wa kushirikisha watumishi na hali hiyo inatokana na ukweli kuwa palipo na watumishi wengi pana mawazo mengi.Profesa Kabudi alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati akifungua mkutano wa kumi na tatu wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro.

‘’Ushirikishwaji watumishi kwenye mipango ya uendeshaji ofisi unasaidia kupata mawazo mengi na mapya yanayoweza kurahisisha uendeshaji wa ofisi na kutoa fursa ya kusikiliza kero na changamoto kwenye uendeshaji wa Taasisi na kushirikiana katika kutafuta ufumbuzi’’ alisema profesa Kabudi.

Aliongeza kuwa, kwa kushirikiana na watumishi ni dhahiri wanapata morari wa kushiriki kikamilifu kwenye utekelezaji wa mipango ya taasisi ambayo wao wenyewe walishiriki kuiandaa.Waziri huyo wa Katiba na Sheria alisema, ushirikishwaji unafanywa kupitia baraza la wafanyakazi kwa kuwa baraza ni chombo kinachowashirikisha wafanyakazi katika kupanga , kusimamia na kutekeleza mipango mbalimbali inayohusu shughuli za kazi za Taasisi kama zilivyoainishwa katika sheria za nchi.
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume Casmir Kyuki na kulia ni Katibu wa Baraza Ambokile Mwakasungula (Picha na Munir Shemweta-TUMESHERIA)
Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Casmir Kyuki (Kushoto) akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi kufungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro, kulia ni Katibu wa Baraza Ambokile Mwakasungula (Picha na Munir Shemweta-TUMESHERIA)
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akimsikiliza Katibu Msaidizi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Khalist Luanda mara baada ya kufunguka mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Tume ya Kurekebisha Sheria uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro, katikati ni Katibu Msaidizi wa Tume (Idara ya Mapitio) Angelah Bahati (Picha na Munir Shemweta-TUMESHERIA)
Sehemu ya Wajumbe Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano huo uliofanyika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mkoani Morogoro.

WAZIRI MHAGAMA : SERIKALI HAITAPUUZA USALAMA NA AFYA ZA WAFANYAKAZI

$
0
0
Serikali imesema kamwe haitapuuza suala la Usalama na Afya mahali pa kazi hususani katika kipindi hiki ambacho msisitizo mkubwa ni katika kujenga uchumi wa viwanda.

Msimamo huo wa serikali umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mh. Jenista Mhagama, alipokuwa akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji wa Iringa na wageni mbali mbali waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa kazi Duniani.

Mh. Mhagama ambaye alikuwa Mgeni Rasmi wa maadhimisho ya siku hiyo ambayo huadhimishwa kila ifikapo Aprili 28, alisema katika kipindi hiki ambapo mwelekeo wa nchi ni kujenga uchumi wa viwanda, suala la usalama na afya za wafanyakazi ni lazima lizingatiwe.

“Ningependa kusisitiza kuwa, serikali ya awamu ya tano kamwe haitapuuza suala la usalama na afya mahala pa kazi hasa wakati huu tunapojenga uchumi wa viwanda ambao utaambatana na vihatarishi vingi vipya,” alisema Mh. Waziri na kuongeza: “Kwa hivyo, itaendelea kushirikiana na wadau wote ili kupunguza au hata ikiwezekana kuondoa kabisa vifo, ajali, magonjwa na madhara yatokanayo na kazi”.

Kwahapa nchini, masuala ya Usalama na Afya katika sehemu za kazi, yapo chini ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ambao husimamia utekelezaji wa Sheria Na. 5 ya Bunge ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003.
OSHA husajili sehemu zote za kazi nchini na kuzitembelea kwaajili ya kufanya kaguzi za kiusalama na afya ili kuhakikisha kwamba kunakuwa na mifumo madhubuti ya kuwalinda wafanyakazi dhidi ya vihatarishi mbali mbali vitokanavyo na kazi wanazozifanya.
Na Eleuter Mbilinyi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mh. Jenista Mhagama, akisalimiana na watumishi wa OSHA mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Kichangani mjini Iringa ambako maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa kazi Duniani yalifanyika. Aliombatana nao ni Katibu Mkuu katika Wizara yake, Eric Shitindi na Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mh. Jenista Mhagama, akiwa katika banda la OSHA katika maonesho ya Usalama na Afya mahali pa kazi yanayofanyika katika viwanja vya Kichangani mjini Iringa. Alioongozana nao ni Katibu Mkuu katika Wizara yake, Eric Shitindi na Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda. 

WAZIRI MKUU AFUNGUA KIKAO CHA MAWAZIRI, WAKUU WA TAASISI

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifungua Kikao cha Kazi cha Mawaziri, Naibu Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi na Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Aprili 29, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mku

IGP SIRRO AKUTANA NA KAMATI YA UKARABATI NYUMBA ZA MAKAZI YA ASKARI MKOANI MOROGORO

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na askari wa Kituo cha Polisi Mikumi mkoani Morogoro leo, wakati akiwa safarini kuelekea mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi, ambapo aliwakumbusha askari wajibu wao wa kufanyakazi kwa kufuata sheria na taratibu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akitoa maelekezo kwa kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei, wakati akizungumza na askari wa Kituo cha Polisi Mikumi mkoani Morogoro leo, ambapo aliwakumbusha askari wajibu wao wa kufanyakazi kwa kufuata sheria na taratibu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na wadau welevu wa Jeshi hilo wanaojenga ofisi za kituo cha Polisi Usalama barabarani Mikumi mkoani Morogoro leo, wakati akiwa safarini kuelekea mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi.Picha na Jeshi la Polisi.

JE WAJUA ATHARI ZA MAUMIVU MAKALI YA MGONGO?.

$
0
0
Watu wengi huchukuliaTatizo la Maumivu ya Mgongo kama jambo la kawaida na hawafahamu kuwa linaweza kupelekea matatizo makubwa katika mwili.

Tatizo la mgongo likiachwa kwa muda mrefu linaweza kupelekea:

1.Ulemavu: Mtu anakuwa hana tena uwezo wa kusimama sawasawa na hivyo akitembea huelemea mbele. Hali hii humpa changamoto katika kuziendea shughuli za kila siku.

2.Kuwa tegemezi: Kwa watu wazima tatizo la mgongo la muda mrefu linawea kupelekea kushindwa kutembea mwenyewe hadi atumie fimbo. Hivyo mtu huwa tegemezi kwa fimbo katika kutembea kwake.

3.Kukosa usingizi. Kutokana na maumivu makali ya mgongo.

4.Ganzi ya mgongo na kusababisha matatizo ya mfumo wa fahamu.Maumivu ya mgongo pia hupelekea ganzi na kupoteza uwezo wa kuhisi vichocheo (joto,baridi, mguso) kwani katika pingili za mgongo katikati hupita neva za fahamu ambazo zinatoa mawasiliano kati ubongo na viungo vya mwili.

5. Inapunguza ufanisi katika tendo la ndoa: Utafiti uliofanywa na SpineUniversemwaka 2008 ulibaini kwamba Maumivu makali ya mgongo hupelekea Ufanisi mdogo wa kushiriki tendo la ndoa, kutoridhika katika tendo la ndoa, na ugumu katika mahusiano.

6. Maumivu makali ya mgongo yanaweza kupelekea msongo wa mawazo ambao pia hupelekea matatizo katika mahusiano na kushindwa kushiriki katika shughi za kiuchumi.

Happiness Massage ndio suluhisho pekee la maumivu makali ya mgongo

Tembelea ofisi zetu zilizopo Lamada Hotel, Ilala, Apartment no. 27.

Fanya Booking sasa kwa
SMS +255 787 343 161

Tupigie simu
+255 715 343 161
+255 756 343 161

KWA MAELEZO ZAIDI NA KUJIFUNZA BOFYA HAPA

IRINGA NA MAJIRANI TUCHANGAMKIE FURSA KWENYE UTALII - MBUNGE WA MAFINGA MHE COSATO CHUMI

$
0
0
Baada ya uzinduzi wa barabara ya Migori-Iringa ambayo ni sehemu ya Barabara ya Dodoma hadi Iringa, Mhe Rais alizungumzia nia yake ya kuhakikisha Utalii unanyanyuka Southern Circuit ambapo Mkoa wa Iringa ndio kitovu.

Kati ya mambo ambayo Serikali imedhamiria kuyafanya ni pamoja na kuufanya uwanja wa ndege wa Nduli kuwa mkubwa na wa kisasa, na kujenga barabara ya Iringa hadi geti la Ruaha National Park.

Hatua hizi ni wazi kuwa zitaifungua Iringa kifursa mbalimbali. Ni muhimu kuanza kujiweka sawa kuanzia mafunzo katika masuala ya Utalii.Ni wajibu wetu kuwa-encourage vijana wetu kujihusisha na masuala ya Utalii ikiwa ni pamoja na kujifunza lugha za nje kama Kispaniola, kifaransa, kijerumani nk

Ukienda Zanzibar kwa mfano, kuna vijana wengi sana wamejikita katika shughuli za utalii kama kuongoza watalii nk. Vijana hao wamefanikiwa kwa sababu waliona hiyo fursa na kuichangamkia japo kwa kupata basic courses za masuala ya Utalii.

Kwa mujibu wa taarifa za Serikali, mpaka kufikia 2017, sekta ya utalii ndio ilikuwa inaongoza kwa kuliingizia Taifa fedha za kigeni, kiasi cha zaidi ya 17%. Kwa hiyo kuna fursa katika Utalii. Iringa na maeneo/mikoa ya jirani tujiandae katika kuchangamkia fursa hii inayokuja mbele yetu.

Cosato Chumi
Mafinga Mjini
30 April, 2018
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Mafinga Mhe.Cosato Chumi mapema jana mara baada ya kuwasili mkoani Iringa 

Waziri Ummy amjulia hali Mzee Majuto Muhimbili

$
0
0
 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akizungumza jambo na Mchekeshaji mkongwe almaarufu kwa jina la Mzee Majuto mapema jana,alipokwenda kumjulia hali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili,anakopatiwa matibabu

MADIWANI WATATU WA CHADEMA MONDULI WAACHIA NGAZI,WAJIUNGA CCM

$
0
0
  
Madiwani watatu wa CHADEMA wilayani Monduli wamejiuzuru nafasi zao na kujiunga na chama cha Mapinduzi (CCM) mapema jana tarehe 29.04.2018 Madiwani hao kuanzia pichani kulia ni Bariki Sumuni Libilibi wa kata ya Monduli Juu,Einoti N. Leringa wa viti maalum kata ya Monduli Juu pamoja na Dominic Mawalla Kadogoo diwani wa kata ya Migungani.Wote kwa pamoja walikabidhi barua za kujiuzulu kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Monduli
  Einoti N. Leringa wa viti maalum kata ya Monduli Juu akikabidhi barua yake ya kujiuzuru kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Monduli
Benedict Mawalla kata ya Migungani akikabidhi barua yake ya kujiuzuru kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Monduli

KIPINDI MAALUM CHA RAIS DKT.JOHN MAGUFULI KWENYE UZINDUZI WA BARABARA DODOMA-BABATII

NEW PROPERTY AVAILABLE FOR IMMEDIATE LEASE

$
0
0
New Property available for immediate lease at UDOE HOUSE is a spacious new building located on plot no 30 block 61 at UDOE Street, Kariakoo, Ilala - Dar es Salaam.

UDOE House is a brand new property with 8 floors whereby each floor comes with 2 units of 3 bedroom apartments, each unit has a master bedroom, balconies, store, kitchen and large living room. The living room of Master bedroom comes with Air condition anemity.
Each apartment has 79 square metres, There is 16 apartment units in the building, Ground floor has area space of 82 square metres.

Looking for potential leaser for different business purposes such as banks, hospital, schools, religious communities, even if it will include alterations on the property.

For serious inquiries please contact +255713 465 336 or +255713 272 203.

INVITATION TO ICT SHORT COURSES

UN yataka vyombo vya habari kukazania uwajibikaji

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Umoja wa Mataifa (UN) umetaka Vyombo vya Habari nchini kuweka mkazo katika kuandika na kutangaza masuala ya maendeleo na ya kiutu, hasa yale yanayoweza kujenga uelewa zaidi na kuchochea vitendo na uwajibikaji kwa manufaa ya Watanzania walio wengi.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez, katika mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)  uliofanyika mwishoni mwa juma mjini Morogoro.
Katika hotuba yake hiyo iliyosomwa na Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Hoyce Temu alisema, kwa kuwa Vyombo vya habari ndiyo kiunganishi kikuu kati ya watu, serikali na mashirika ya kimataifa hivyo ni wajibu wao kuandika habari zinazochochea maendeleo.
Aidha alisema kwa namna ya pekee, angependa kusisitiza umuhimu wa kuandika habari za hatua zinazopigwa katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano na vilevile MKUZA II na III.
“Haya ni maeneo muhimu kwa sababu aina ya mabadiliko tunayotaka kuyaona nchini Tanzania katika miaka michache ijayo yatawezekana tu ikiwa mipango hii mitatu itatekelezwa kwa ufanisi na kikamilifu kwa kuzingatia muda uliopangwa. Ni wajibu wenu, kama waandishi wa habari wanaojua kazi yao kushiriki kikamilifu katika wajibu huu wa kusimamia na kutolea taarifa masuala haya ili kuimarisha uwajibikaji” alisema Rodriguez.
Aidha alisema kwa kuwa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania unatekeleza mpango wa UNDAP II, ambao ni mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo unaolenga kuainisha vema programu ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Timu ya UN ya Nchi, ambao hatimaye utaimarisha fursa za maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa, vyombo vya habari vitaweza kusaidia kuhakikisha kwamba hakuna yeyote anayeachwa nyuma.
Serikali ya Tanzania na Timu ya Nchi ya UN zinashirikiana Dira ya Taifa na SDGs kwa kushughulikia maeneo matano ya kimaudhui  ambayo ni Utawala wa Kidemokrasi, Haki za Binadamu & Usawa wa Jinsia—kuleta taasisi zenye uwazi na zenye kuwajibika na kuleta usawa wa jinsia.
 Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile akifungua kikao kati ya Jukwaa hilo na Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
 Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu akisoma hotuba kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
 Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika linaloshughulikia Watoto la Umoja wa Mataifa, Usia Nkhoma-Ledama  akizungumzia uhusiano na ushirikiano kati ya TEF na mashirika ya Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
 Washiriki wa kikao cha Jukwaa  la Wahariri (TEF) wakifuatilia kwa umakini mada ya Malengo ya Dunia na ushirikiano wa kuwezesha malengo hayo kutekelezeka wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.

 Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu akisaini kanuni za ushirikiano kati ya TEF na UN kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu na Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile wakibadilishana nakala za ushirikiano kati ya TEF na UN wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERENGETI BOYS KUTUA JUMATANO ALFAJIRI,RAIS TFF WALLACE KARIA AWATUMIA SALAMU ZA PONGEZI

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Ndugu Wallace Karia ametuma salamu za pongezi kwa timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17(Serengeti Boys) kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Vijana kwa nchi za Africa Mashariki na kati Cecafa mashindano yaliyofanyika nchini Burundi.

Serengeti Boys wametwaa ubingwa huo wa Cecafa baada ya kuifunga Somalia katika mchezo wa fainali iliyochezwa Uwanja wa Ngozi kwa mabao ya EdsonJeremiah na Jaffar Juma Mtoo.

Rais wa TFF Ndugu Karia aliyekuwa nchini Burundi amesema Vijana hao waliocheza kwa kujituma mwanzo wa mashindano mpaka fainali wameiletea sifa kubwa Tanzania na ni jambo la kujivunia kwa kila MTanzania.Amesema ushindi huo unatoa picha nzuri ya muelekeo wa mpira wa Tanzania kupitia soka la vijana.

“Vijana wetu wameonesha soka zuri na wamefanya kazi nzuri sana katika mashindano ya Cecafa ,kwa niaba ya TFF nawapongeza vijana wetu na benchi la ufundi ambalo pia limefanya kazi nzuri kuhakikisha vijana wanafanya vyema,tutaendelea na jitihada zetu za kuendelea kuwekeza kwenye soka la vijana ambalo ndilo msingi” amesema Rais wa TFF Ndugu Karia.

Amesema timu hiyo ya Serengeti Boys iliyokwenda Burundi ndio inayoandaliwa kwa fainali za vijana za Africa chini ya miaka 17 ambazo Tanzania itakua mwenyeji wa fainali hizo zitakazofanyika mwakani.

Ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na TFF katika kuendeleza mpira na kushirikiana kwa karibu na uongozi wa TFF uliopo madarakani.Pia amewashukuru WaTanzania kwa kuendelea kuziunga mkono timu za Taifa ikiwemo Serengeti Boys na kuwaomba kujitokeza kwa wingi kuwapokea vijana hao watakaporudi kutoka nchini Burundi.

Serengeti Boys wanatarajia kutua nchini Jumatano Saa 8 usiku kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA).

Katika mashindano hayo Serengeti Boys ilitoka sare 1-1 na Uganda kabla ya kuifunga Sudan 6-0 na baadaye kuichapa Kenya kwa mabao 2-1 kwenye nusu fainali na kushinda mabao 2-0 dhidi ya Somalia kwenye mchezo wa fainali.

Meya Ilala afanya ziara ya mafunzo nchini sweden, amtembelea Balozi Dkt. Slaa

$
0
0
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamin Sitta akiwa nchini Swedeni katika  manispaa ya Strangnas ambayo ni marafiki wa jiji la Dar es salaam kujifunza mambo mbalimbali ya uendeshaji wa Manispaa na Jiji,Mhe.Benjamin Sitta analiwakilisha jiji la Dar es salaam na pia alipata wasaa wa kumtembelea Ofisini kwake Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe.Balozi Dkt.Slaa.
 Picha ya pamoja

KESI YA AKINA AVEVA,MAHAKAMA YAAMURU HANS POPE , LAUWO WAKAMATWE

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba Sports Club  Zacharias Hans Pope na Mkandarasi wa uwanja wa club hiyo, Frank Peter Lauwo wakmatwe na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.

Washtakiwa hao wameongezwa katika kesi ya utakatishaji fedha na kugushi inayomkabili Rais wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange maarufu Kaburu.
Amri hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wa mahakama hiyo baada ya Swai kudai amewatafuta washtakiwa hao toka Machi mwaka huu bila mafanikio na kuomba hati ya kuwakamata washtakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani

Kutokana na mabadiliko hayo washtakiwa wamesomewa upya hati ya mashtaka na wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 10 tofauti na hati ya mashtaka ya zamani iliyokuwa na mashtaka matano.

Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania(Takukuru) Leornad Swai ameda kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa hao maelezo ya awali lakini ameomba kufanyia madaliko hati ya mashtaka.Katika mashtaka hayo washtakiwa wanakabiliwa na shtaka la kula njama, kutoa nyaraka za uongo, matumizi mabaya ya madaraka, kughushi, utakatishaji, kuwasilisha nyaraka za kughushi na kuendesha biashara bila kufuata sheria.

Akisoma mashataka hayo, Swai amedai, kwenye shtaka la kwanza, Aveva na Nyange, walikula njama ya kutenda kosa la kutumia madaraka vibaya, pia wanadaiwa kati ya Machi 10 na 16 jijini Dar es Salaam, walitumia madaraka yao vibaya kwa kuandaa fomu ya maombi ya Machi 15/2016 na kuhamisha dola za Marekani 300,000 kutoka kwenye akaunti ya Simba iliyopo CRDB tawi la Azikiwe kwenda kwenye akaunti binafsi ya Barclays kwa madhumuni ya kujipatia faida.

Katika tarehe hizo hizo wakiwa Dar es Salaam kwa pamoja walighushi nyaraka iliyokuwa ikionyesha simba inalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000 kwa Aveva kitu ambacho si kweli.

Aidha wote kwa pamoja waliwasilisha nyaraka ya kughushi, inadaiwa kuwa Aveva Machi 15 mwaka 2016 katika benki ya CRDB aliwasilisha nyaraka ya uongo ikionesha Simba wanalipa mkopo wa dola 300,000.Katika shtaka la utakatishaji fedha linalomkabili Aveva, imedaiwa Machi 15 mwaka 2016 katika benki ya Baclays Mikocheni alijipatia Dola 187,817 wakati akijua zimetokana na zao la kosa la kughushi.

Pia katika shitaka la sita la imedaiwa Nyange alimsaidia Aveva kujipapatia dola 187,817 kotoka kwenye akaunti ya Simba wakiwa wanajua fedha hizo zimetokana na zao la kughushiKatika na shtaka la saba la kughushi, linaloqakabili mstakiwa wa Aveva, Nyange na Poppe.

Imedaiwa katika tarehe hizo hizo kwa pomoja walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28/ 2016 wakionesha nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zinathamani ya USD 40,577 huku wakijua kwamba sio kweli.Katika shtaka la nane imedaiwa, , Aveva aliwasilisha hati ya madai (commercial invoice), ya uongo kwa Levison Kasulwa ya Mei 28/ 2016 kwa madhumuni ya kuonyesha kwamba Simba wamenunua nyasi bandia zenye thamani ya dola 40,577

Katika Shtaka la tisa Aveva, Nyange na Zacharia Machi 10 mwaka 2016 na Septemba 30 mwaka 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya USD 40,577.


Katika shtaka la mwisho imedaiwa, kati ya Machi na Septemba 2016 Lauwo aliendesha biashara kama mkandarasi kwa kujenga uwanja wa Simba uliopo Bunju jijini Dar es Salaam wakati akiwa hajasajiliwa

Hata hivyo washtakiwa wamekana mashtaka hayo yote na wamepelekwa rumande kwa sababu shtaka la utakatishaji fedha linalowakabili halina dhamana.Kesi hiyo imahirishwa hadi Mei 14, mwaka 2018 kwa ajili ya kutajwa na kufuatilia kama washtakiwa hao wawili watakuwa wamekamatwa.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images