Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

KANISA LA UFUFUO LAFUNGA MILANGO YAKE HADI ITAKAPOTOLEWA TAARIFA NYINGINE,KUPINGA KODI ZA KIMABAVU ZA ISRAELI

$
0
0
 Mchungaji wa Mji Mtakatifu na kazi nyingine za Palestina na Jordan Theophilus III, kwa niaba ya wachungaji na viongozi wote wa Makanisa ya Jerusalemu (Makanisa ya Kigiriki, Kikatoliki na Kiarmenia),katika hatua ambayo haijawahi kutokea, Jumapili iliyopita ametangaza kulifunga Kanisa hilo la Ufufuo lililopo Jerusalemu ya kale hadi itakapotolewa taarifa nyingine,ikiwa ni kutokukubaliana na kupinga kwao na sera za utawala wa kivamizi wa Israeli dhidi ya Makanisa na kuyataka yalipe kodi.

Hayo yamesemwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika kiwanja cha Kanisa hilo la Ufufuo,ikiwa ni kupinga vitendo vya utawala wa kivamizi dhidi ya makanisa hayo. Kwani utawala huo hivi karibuni umeyataka Makanisa hayo ya Jerusalemu yalipe kodi ya mali ijulikanayo kama"Arnona",yenye thamani ya shekel milioni kila mwaka, huku ukiingilia mali za Kanisa la Orthodox la Kirumi kwa lengo hilohilo.

Nao Viongozi wa Makanisa ya Jerusalemu katika mkutano wa waandishi wa habari, wametoa tamko wakisisitiza ya kwamba,”Kuyatoza kodi Makanisa mjini Jerusalemu ni ukiukwaji wa mikataba yote iliyopo na wajibu wa kimataifa unaodhamini haki za Makanisa na mambo yake maalumu." Tamko hilo limesisitiza kuwa, hatua hiyo ni "jaribio la kudhoofisha uwepo wa Kikristo katika jiji hilo," Huku likionya kuupitisha mpango wa kamati ya wizara iliyo chini ya utawala wa kivamizi wa Israeli wa kutoza kodi kwa Makanisa mjini Jerusalemu,ambao unafanyika kupitia kuchukua kwa nguvu ardhi ya Makanisa hayo yaliyo mjini hapo.
Serikali ya Palestina imeizingatia hatua ya utawala wa kivamizi kutoza kodi nyumba za ibada yakiwemo makanisa, kuwa ni uadui mpya dhidi ya wananchi na maeneo yake matakatifu, jambo lililopelekea kufungwa kwa kanisa la Ufufuo lililopo katika mji mkuu unaokaliwa kimabavu. Huku ukiuchukulia uadui huo mpya kuwa unalenga mji wa Jerusalemu na taifa letu lote la kiarabu la kipalestina pia unagusa maeneo yake matakatifu, huku likionya juu ya madhara makubwa yanayoweza kunyakua ardhi za makanisa.

Serikali imeomba kuingilia kati kwa haraka kwa jumuiya ya kimataifa ili kusitisha vitendo hivyo vya Israeli, ambavyo vinahesabiwa kuwa ni mashambulizi mabaya ya mikataba,makubaliano na desturi zote za kimataifa, vinavyodhamini uwepo wa uhuru wa kuabudu na kuheshimu utakatifu wa sehemu za kidini,katika hali yoyote na popote. Serikali pia imetoa wito maalumu kwa ulimwengu wa kikristo na kiislamu, wa kuchukua hatua stahiki kwa ngazi zote ili kuzuia vitendo vya kivamizi, vinavyolenga kwa kiwango sawa sehemu takatifu za kikristo na kiislamu.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

MAKAMU WA RAIS AMSAIDIA MKAZI WA SALASALA KITI CHA MAGURUDUMU

$
0
0
Bi. Sidonia Ntibashigwa ambaye pia anafahamika kama Mama Sophia mkazi wa Machimbo ya Zamani, Sala Sala Mbuyuni amemshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumpatia kiti cha magurudumu (wheel chair).Mama Sophia ambaye alipata ya ajali ya kugongwa na roli tarehe 28 Mei, 2016 Mbuyuni, Salasala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kumkabidhi kiti hicho Msaidizi wa Makamu wa Rais Siasa Ndugu Nehemia Mandia alisema “Mheshimiwa Makamu wa Rais aliguswa na suala lako ambalo liliandikwa sana kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusiana na ajali uliyoipata na ulemavu ambao umekupata kutokana na ajali kutokana na kitendo hicho ameona akusaidie kiti cha magurudumu kwa ajili ya wewe kufanya shughuli ndogo ndogo unazoweza kufanya”.

Kwa upande wake Mama Sophia alishukuru sana kwa msaada huo wa Kiti na kumuomba Makamu wa Rais aendelee na moyo huo huo wa kusaidia wananchi wake .Alisema kwa sasa bado anaendelea na matibabu kwa sababu mguu wake mmoja bado haujawa na nguvu hivyo hawezi kusimama.

Mama huyo mwenye watoto sita na wajukuu wanne alisema pia bado anahitaji msaada ili aweze kupata matibabu zaidi.
Msaidizi wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Nehemia Mandia (kulia)akizungumza na Bi. Sidonia Ntibashigwa mkazi wa Machimbo ya Zamani Salasala kabla ya kumkabidhi Kiti cha Magurudumu kilichotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Bi. Sidonia Ntibashigwa mkazi wa Livingstone , Machimbo ya Zamani akikabidhiwa kiti cha magurudumu alichosaidiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

NAIBU WAZIRI NYONGO ASISITIZA UTULIVU NA AMANI KWA WACHIMBAJI WADOGO

$
0
0
Na Joel Maduka,Geita.

Naibu waziri wa madini Stanslaus Nyongo amewata wachimbaji wadogo wa mgodi wa Nyakafulu na Bingwa kudumisha amani na utulivu katika shughuli zao ikiwemo kujenga desturi ya kufanya usafi wa mazingira ili kuepukana na magojwa ya mlipuko na iwapo hawatazingatia hayo migodi hiyo itafungwa.

Hayo aliyasema wakati wa ziara yake ya kuwatembelea wachimbaji wadogo kwenye wilaya za Mbongwe na Geita.Alisema ni vyema wachimbaji hao kuzingatia amani na afya zao kwani ndio utaratibu uliowekwa na serikali iwapo ikitokea magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu migodi hiyo itafungwa mara moja.

“Mpo hapa kwa sababu ya kauli ya Mheshimiwa Dkt, John Magufuli lakini vilevile akisikia kwamba hapa hakuna amani na sio wasafi mimi nitatoa amri ya kufunga mgodi huu kwani wizara yangu ndio inahusika kutoa leseni hivyo pamoja na hayo yote amani itawale”alisema Naibu waziri.

Kwa upande wake Rais wa shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini nchini Bw John Bina aliwasisitiza wachimbaji wadogo kujenga desturi ya kulipa kodi ili waweze kuchimba kwa kufata utaratibu, sheria, na kanuni za nchi bila bugudhi yoyote na wagawane kwa utaratibu bila kudhulumiana kwa sababu sehemu wanayochimba kuna leseni ya mtu kwa hiyo wachimbe kwa kuweka akiba ili na wao baadae wakate leseni zao za uchimbaji.

‘’ wachimbaji mmekuwa na tabia ya kula bata na kuhonga pesa zote mnapouza madini acheni tabia hiyo wekeni akiba mkate leseni zenu za uchimbaji zitawasaidia hapo baadae”Alisema Bina.Hata hivyo wachimbaji hao wamemuomba Naibu waziri wa madini Nyongo kuwasaidia kupata leseni ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira yao na vitendea kazi kwa sababu wamekuwa wakitumia njia za asili katika kufanya shughuli zao za uchimbaji.

Naibu waziri wa madini,Staslaus Nyongo amemaliza ziara yake ya siku tatu mkoani Geita,kwa kutembelea migodi mikubwa na midogo huku akisikiliza kero za wachimbaji wadogo na kutatua changamoto ambazo zilikuwa zikiyakabili maeneo hayo. 
Naibu Waziri wa nishati na madini,Stanslaus Nyongo akizungumza na wachimbaji wadogo wa Kijiji cha Nyakafulu wilayani Mbongwe wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi Mkoani Geita. 
Naibu Waziri wa nishati na madini,Stanslaus Nyongo akiwa kwenye shimo ambalo linatumika kuingilia ndani kwaajili ya kuchimba. 
Naibu Waziri wa nishati na madini,Stanslaus Nyongo akizunguka na kukagua baadhi ya maeneo ya mgodi wa Nyakafulu. 
Rais wa shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini nchini Bw John Bina akizungumza na wachimbaji wadogo wa Nyakafulu wilayani Mbongwe. 
Bw,Iddy Mrisho ambaye ni mchimbaji akielezea masikitiko yake na namna ambavyo wamekuwa wakinyanyasika kutoka kwa viongozi wa vikundi. 
Baadhi ya wachimbaji wadogo wakimsikiliza Naibu waziri wa madini,Staslaus Nyongo. 
Wachimbaji wadogo wakiwa wamebeba mabango ambayo yanamalalamiko

AZAM FC,SINGIDA UNITED KUPAMBANA JUMAMOSI HII

$
0
0
Na Agness Francis Globu ya jamii 

MABINGWA wa Afrika Mashariki na kati AzamFc wanatarajia  kukutana tena na Singida United kwenye michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara. 

Mtanange huo utapigwa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi  siku ya Jumamosi ya wiki hii ,saa 10 jioni huku Azam akiwa wenyeji wa Singinda united. 

Ambapo Singida  tangu kupanda daraja msimu huu hawajawahi kucheza na mabingwa hao katika  uwanja huo. Akizungumza leo katika ofisi zao Mzizima Jijini Dar es Salaam Ofisa Habari wa AzamFc  Jaffary Iddy Maganga  amesema katika raundi iliyopita timu hizo mbili zilitoka sare kwa kufungana 1-1 katika Uwanja wa  Jamuhuri Dodoma.

Wakati Singinda United walipokuwa wakiuchezea uwanja huo kama wa nyumbani kabla wa kwao kukamilika. Jaffary amesema kikosi cha Azam jana kimeingia kambini na kuanza mazoezi ya kujifua ili kukabiliana na Timu hiyo. 

"Tunakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Singinda Timu yao ni ya ushindani na imeonyesha ujasiri wa hali ya juu kutokana na jinsi Kikosi chao walivyokisajili,"amesema Maganga. Hata hivyo Maganga amesema licha ya kukabiliwa na mchezo huo mgumu wataakikisha pointi 3 zinabaki Nyumbani. 

"Wachezaji wetu,  Himidi Mau pamoja na Waziri Junior  tayari wamerejea kikosini kwa ajili ya mazoezi na itategemea mpaka kufikia Jumamosi,  Mwalimu ataamua Wachezaji  hao wacheze  mchezo au lah kutokana na unafuu wao utakavyokuwa," amesema Maganga

DK. MWANJELWA AMSIFU BINTI MKULIMA WA KITANZANIA ALIYEAJIRI WAFANYAKAZI 26 SHAMBANI

$
0
0
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiongea machache na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza alipofika kwa utambulisho na kuanza ziara katika Mkoa huo Februari 23 2018. Pamoja naye (kushoto) Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga viongozi wa wasaidizi wake mkoani humo.
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akisalimiana na mmoja wa wageni alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza (kulia) alipofika kwa utambulisho na kuanza ziara katika Mkoa huo Februari 23 2018. Kulia kwa Naibu Waziri ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga.
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiagana na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Amina Masenza baada ya kufanya naye mazungumzo ofisini wakati wa kuanza kwa ziara yake mkoani humo. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey.
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akikagua sehemu ya shamba lenye hekari 30 la GBRI Business Solutions Company Limited, Hadija Jabiri akiwa na mwenyeji wake mmiliki wake, Hadija Jabiri (wa pili kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Ukanda wa Kusini wa kukuza Kilimo (SAGCOT), Geoffrey Kirenga na Afisa kilimo wa mkoa wa Iringa Lucy Nyalu.
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akibadilishana mawazo na Mmiliki wa GBRI Business Solutions Company Limited, Hadija Jabiri alipotembelea shamba kitalu cha kampuni hiyo. 
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akibadilishana mawazo na wakina mama wanaojitegemea baada ya kukagua sehemu ya shamba lenye hekari 651 lililonunuliwa na Taasisi ya Ilula Programu 2013 mkoani Iringa kwa ajili ya kilimo cha biashara maalum kwa ajili yao, watoto yatima na wanafunzi wenye nia ya kukuza uelewa wa kilimo kutoka katika Wilaya ya Iringa hasa wa shule za primary na awali.

IGP SIRRO AZUNGUMZA NA WANANCHI WA KAHAMA MKOANI SHINYANGA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na wananchi wa Kahama mkoani Shinyanga mara alipowasili katika wilaya hiyo kwa ziara ya kikazi ya kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo, IGP Sirro amewataka wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo pamoja na kuwafichua wahalifu waliopo kwenye maeneo yao.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mkoa wa Shinyanga, wakiimarisha ulinzi wakati Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, aliposimamisha msafara wake ili kuzungumza na wananchi waliojitokeza barabarani katika mji wa Kahama mkoani Shinyanga leo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule (aliyesimama) akitoa hotuba mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, aliyewasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na Maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuwakumbusha kutimiza wajibu wao wa kutenda haki kwa wananchi wanaowahudumia.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiwa katika picha ya pamoja na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia wa mkoa wa Shinyanga leo akiagananao mpakani mwa mkoa huo na wilayani Mbogwe, Geita, IGP Sirro yupo mkoni humo kwa ziara ya kikazi. Picha na Jeshi la Polisi.

MADIWANI MUFINDI WAPITISHA BAJETI KWA MWAKA 2018/2019, ASILIMIA 60% IMEELEKEZWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mhe. Festo Mgina, akizungumza wakati wa kufunga kikao cha Baraza la Madiwani.
Sehemu ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi wakifuatilia Mjadala wa bajeti.

Na Afisa Habari Mufindi.
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi limejadili, kuridhia na kupitisha rasimu ya bajeti yenye zaidi ya shilingi bilioni 62.926, ikiwa ni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa Fedha 2018/2019, ambapo makusanyo ya ndani ya Halmashauri ni Bilioni 4.162 kati ya Fedha zote.

Akiwasilisha rasimu ya bajeti kwenye kikao maalum cha Baraza, kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Isaya Mbeje, amesema, Halmashauri inatarajia kukusanya, kupokea na kutumia zaidi ya Bilioni 62.926, ambapo kati ya Fedha hizo Bilioni 40.728 ni Fedha kutoka Serikali kuu maalum kwa ajili ya mishahara ya Watumishi, Bilioni 17.205 zimeelekezwa kwenye Miradi ya Maendeleo huku Bilioni 4.992 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.

Mbenje ambaye pia ndiye Afisa Mipango wa Halmashauri, amevitaja vipaumbele vya bajeti hiyo kwa mwaka wa Fedha wa 2018/2019 kuwa inaangazia ukamilishaji wa miradi ambayo haikukamilika kwa miaka ya nyuma hususani ukamilishaji wa Majengo ya sekta ya Afya na Elimu, Ukarabati wa Madarasa chakavu ya baadhi ya Shule za Msingi, ukusanyaji Mapato kwa njia ya kielekroniki, Kutoa huduma bora za kijamii, kuinua uchumi wa wananchi na kuimarisha Miundombinu.

”Mhe Mwenyekiti rasimu hii ya Mpango wa Bajeti ya Halmashauri ni Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/2019, rasimu hii itaendelea kujadiliwa na kupatiwa ushauri kwenye vikao vya ngazi ya Mkoa, Ofisi ya Rais TAMISEMI Pamoja na Wizara ya Fedha na Mipango kabla ya kujadiliwa na kupitishwa na Bunge” alibainisha Bw. Mbenje.

Azungumza wakati wa kufunga kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi ambaye pia ndiye Diwani wa kata ya Mninga Mhe. Festo Mgina, amewataka Madiwani kutoa ushirikiano kwenye zoezi la ukusanyaji wa mapato pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapoto ili yasaidie kuharakisha maendeleo kwa kuzingatia kuwa asilimia 60% Mapato ya ndani yanatakiwa kuelekezwa kwenye miradi ya Maendeleo.

“Mkurugenzi wewe pamoja na timu yako tuendelee kuchapa kazi, tunasifa ya Ushirikiano kati ya timu ya Madiwani na Timu yako, tuendeleee kufanya kazi kwa umoja, uadilifu na ushirikiano Kwani sisi kama Viongozi tunatakiwa kuwa chachu ya Maendeleo”

Rasimu ya bajeti ya 2018 – 2019, aimeandaliwa kwa kuzingatia, Ilani ya Chama cha tawala CCM, Mwongozo wa bajeti wa mwaka 2018/2019, Mpango wa pili wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/2017, Malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs), Dira ya Taifa pamoja na mpango mkakati wa miaka 05 wa Halmashauri.

MAMBO YA VIFUNGUA KINYWA NA VITAFUNWA MBAGALA

$
0
0
Wajasiriamali wanaojihusisha na uandaaji na uuzaji wa vitafunwa mbalimbali wakiendelea na shughuli yao hiyo kando ya kituo cha mabasi, Mbagala  jijini Dar es Salaam. Wateja wao wakubwa ni Madereva na Makondakta wa Daladala pamoja wapita njia.
 Mihogo au Chips dume ikiandaliwa tayari kwa kuuzwa kipande kimoja kwa Sh.200.


TTCL WAZINDUA HUDUMA MPYA YA FIBER CONNECT BUNDLE

$
0
0
MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL CORPORATION) Waziri Kindamba ametangaza uzinduzi wa huduma mpya iliyopewa jina la Fiber Connect Bundle  huku akitumia kauli mbiu yao inayosema Rudi nyumbani, kumenoga.

Amefafanua huduma hiyo mpya ambayo wameizindua leo jijini Dar es Salaam ni mwendelezo wa ubunifu wa kampuni hiyo ya kizalendo katika kuwapatia watanzania huduma za kipekee na zenye ubora wa hali ya juu. Kindamba amesema  TTCL Corporation imechukua hatua kwa kuwafuata wateja nyumbani na kufanya mapinduzi makubwa ya kimawasiliano hasa ya mtandao wa intanenti yenye kasi balaa.

 Amesema kupitia huduma hiyo mpya ya Fiber Connect Bundle, wateja wao watapata huduma nne kwa pamoja zikiwa na unafuu mkubwa wa gharama na ubora wa hali ya juu ukilinganisha na kwa majirani zao. Kindamba amefafanua huduma kwa kuanzia wanatarajia kuzifikia nyumba 500 katika maeneo ya Mikocheni na nyumba nyingine 500 katika eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam pamoja na nyumba 200 eneo la Medeli mkoani Dodoma.

Amesema baada ya hapo wataendelea na maeneo mengine kwani lengo lao ni kuhakikisha kila mahali katika nchi yetu kunakuwa na huduma za mawasiliano ya Shirika hilo hasa kwa kuzingatia wao ndio wanaousimamia mkongo wa Taifa wa mawasilano. Kindamba amesema kupitia kifurushi cha Fiber Connect, mteja wao atanufaika na huduma mbalimbali ikiwamo ya  kupata intanenti yenye kasi isiyo na kikomo (Unlimited)

Pia mteja atapata huduma ya simu za sauti kwa simu za mezani na simu card ambayo ataitumia kwenye simu yake ya mkononi na kupata huduma ya Intanenti sawa na simu ile anayopata katika simu ya mezani. Ameongeza kuwa mteja wao pia atapata huduma za Wireless Service (WIFI) katika nyumba yake ambapo vifaa vyote vinavyotumia teknolojia ya intaneti vitaunganishwa  ili kutumia kutumia huduma hiyo.

Ametoa mfano kuwa huduma ambayo wameizundua mteja anaweza kuunganisha kwenye Smart Tv, Tablets na kompyuta mpakato.Pia mteja atapatiwa vifaa vyote bure na uhakika wa huduma za baada (After Sell Services) endapo itahitajika. Kindamba amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa ajili ya Watanzania ambao kimsingi shirika hilo ni mali yao na wanatakiwa kuunga mkono jitihada hizo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL Corporation),Waziri Kindamba akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu huduma mpya ambayo wameizindua inayojulikana Fiber Connect yenye kasi balaa ya intanent kwa ajili ya wateja wao.

TIGO NA MILVIK TANZANIA ZACHAGULIWA KUWANIA TUZO ZA GSMA ZA UVUMBUZI WA SIMU ZA MKONONI KATIKA SOKO LINALOCHIPUKIA

$
0
0
Milvik Tanzania na Tigo wamechaguliwa katika tuzo za Uvumbuzi Bora wa simu za mkononi katika soko linalochipukia katika kundi la Ubora kwa jamii (Social good) katika Tuzo za Simu za Mkononi za GSMA. Tuzo hizi za heshima zinalenga kutambua na kusherehekea mchango uliotolewa katika sekta ya simu za mkononi inayoendelea kubadilika duniani kote.

Tuzo za Uvumbuzi Bora wa simu za mkononi katika soko linalochipukia zinatambua uvumbuzi halisi katika jitihada za simu za mkononi ambazo zinalenga kutambua mchango unaotolewa na makampuni katika ushirikishaji, upatikanaji na uhai wa masoko yanayochipukia. Uteuzi huo unalenga kutambua juhudi za Milvik na Tigo kwa jamii kwa kuwapatia wateja ambao mwanzo walikuwa wamesahaulika katika huduma za bima ya afya kwa gharama nafuu.

Milvik imeleta gharama ndogo za upatikanaji wa huduma ya bima Afrika kwa masoko yanayochipukia (3% tu) kwa kuunganisha pamoja nguvu ya teknolojia ya simu za mkononi na makampuni ya simu kufungua upatikanaji mpya wa huduma nafuu za mawasiliano, na kuunganisha jamii za pembezoni zilizokuwa zimesahaulika katika huduma muhimu za bima kwa lengo la kuleta ushirikishwaji jumuishi wa kifedha.

Milvik na Tigo wameanzisha mfumo wa kwanza wa kidigitali wa bima katika simu za mkononi kwa kuunganisha mfumo wake wa bima katika simu za mkononi na miundombinu ya teknolojia ya makampuni ya simu, jambo ambalo linawawezesha wateja kujiunga na kulipia bima kupitia simu zao za mkononi.

Nchini Tanzania, Milvik inashirikiana na Tigo kuleta huduma za bei nafuu za bima kwa wateja wa Tigo ambapo wataweza kulipia bima zao kwa kutumia fedha zilizoko katika simu. Ushirika huu wa Tigo/Milvik kwa sasa unatoa moja kati ya huduma kubwa zaidi ya bima ya kulipia kupitia simu za mkononi duniani.

Hussein Sayed, Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, amesema: “ninafuraha kwamba kazi ambayo Tigo na Milvik wamefanya katika kuleta ushirikishwaji wa kifedha kupitia uvumbuzi huu unaanza kutambulika. Kwa kuwezesha upatikanaji wa bima kupitia simu za mkononi, wateja ambao kwa kawaida wamekuwa wakikabiliwa na changamoto za kupata huduma za kifedha kupitia taasisi zingine, kwa sasa wataweza kupata ulinzi wa kifedha, wao na familia zao. Tunajisikia furaha kushirikiana na Milvik kutoa bidhaa zenye thamani kubwa za bima kwa wateja wetu pamoja na kuchangia maendeleo ya jamii kwa ujumla.”

Tom Chaplin, Meneja wa Milvik Tanzania, kwa upande wake alisema: “Kupitia mfumo wetu wa bima kwa simu za mkononi na ushirika wetu na Tigo, tumeweza kusambaza huduma rahisi ya bima na yenye bei nafuu kwa watu wengi na kuwezesha upatikanaji wa bidhaa za msingi za kifedha. Kadri ambavyo huduma za simu zinavyozidi kujipenyeza katika masoko yanayochipukia, tunaona fursa nyingi katika kushirikiana na makampuni ya simu na kuwapatia watu zana za kifedha wanazohitaji kuhakikisha mafanikio yajayo ya kiuchumi na familia zao.”

Mshindi wa Tuzo hizo atatangazwa katika Kongamano la Simu za Mkononi Duniani (Mobile World Congress) Barcelona, litakalofanyika kuanzia tarehe 26 Februari mpaka tarehe 1 Machi mwaka huu.

MWANGA: AMCHINJA MWANAYE SHINGO NA KUFICHA MWILI UVUNGUNI.

$
0
0
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Hadija Msangi (30 ) mkazi wa Mwanzini  kwa tuhuma za kumchinja mtoto wake  mwenye umri wa miezi tisa na kitu chenye ncha kali shingoni hadi kufa .

Mtoto aliyeuawa ametambulika kwa jina la Hashim Msuya na kwamba mtuhumiwa baada ya kufanya unyama huo aliuweka mwili wa mtoto huyo kwenye mfuko wa Safleti na kuuhifadhi kwenye uvungu wa kitanda chake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo mnamo Februari 26 mwaka huu majia ya saa 10:00 katika kata ya Msangeni wilaya ya Mwanga na kwamba tayari uchunguzi wa kidaktari umefanyika.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Media Group -Kilimanjaro.

WIZARA ZAWEKA MKAKATI WA KUIMARISHA MUUNGANO

$
0
0
Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania Bara na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ya Zanzibar zimeweka mkakati wa pamoja wa kuimarisha ushirikiano wa usimamizi wa maliasili, malikale na kuendeleza utalii kwa maslahi ya pande zote za Muungano. 

Hayo yameelezwa  na Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi baada ya mkutano wa pamoja wa wizara hizo uliofanyika hivi karibuni katika Chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo wa siku moja uliongozwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Joseph Meza.

Akifungua Mkutano huo wa siku moja,  Maj. Gen. Milanzi alisema pamoja na Wizara hizo kutokuwa za muungano imekuepo haja kubwa ya kukutana kwa ajili kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha sekta ya maliasili na utalii na kukabiliana na changamoto zinazogusa sekta hiyo katika Muungano.

"Tumejadiliana kuona ni namna gani tunaweza kushirikiana kwenye masuala mbalimbali ya biashara ya mazao ya misitu, biashara ya Wanyamapori inayohusiana na mikataba ya CITES na mikataba mingine ya ndani na ya Kimataifa.

"Tumekubaliana pia kuhuisha sheria zinazokinzana katika usimamizi wa sekta tunazozisimamia ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza katika utekekezaji na hivyo kuathiri Muungano wetu," alisema Maj. Gen. Milanzi. 

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

NDITIYE AITAKA TMA IJITANGAZE UMUHIMU WAKE KIUCHUMI NA KIJAMII

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akizungumza na Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wakati alipotembelea makao makuu ya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Buruhani Nyenzi na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Dkt. Hamza KabelwaJPEG. NA. 2
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Nditiy (hayupo pichani) akiangalia picha za usafiri wa anga na majini ambazo usafiri wake unategemea utabiri wa hali ya hewa wakati alipotembelea makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania jijini Dar es SalaamJPEG. NA. 3
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akipatiwa taarifa ya hali ya hewa kwa usafiri wa anga na Meneja wa Utabiri wa Hali ya Hewa Bwana Samwel Mbuya wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wakati alipotembelea makao makuu ya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam
JPEG. NA. 4
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Nditiye (hayupo pichani) akiangalia picha ya ujenzi wa barabara ya mabasi ya mwendokasi ambapo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli unategemea utabiri wa hali ya hewa wakati alipotembelea makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania jijini Dar es Salaam
JPEG. NA. 5
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Nditiye (hayupo pichani) akiangalia picha ya rada ya hali ya hewa iliyopo kwenye vituo vya  utabiri wa hali ya hewa wakati alipotembelea makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania jijini Dar es Salaam
JPEG. NA. 6
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Nditiye (hayupo pichani) akipatiwa maelezo na msomaji wa taarifa ya hali ya hewa kwenye vituo mbalimbali vya televisheni Bi. Hellen Msemo kuhusu namna wanavyotoa taarifa za utabiri wa hali ya hewa wakati alipotembelea makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania jijini Dar es Salaam
……………………
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameilekeza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kujitangaza umuhimu wake katika nyanja ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Mhandisi Nditiye ameyasema hayo alipotembelea makao makuu ya TMA na kuzungumza na bodi ya Mamlaka hiyo, menejimenti na wafanyakazi kwa lengo la kutambua majukumu yao na kufuatilia utekelezaji wake ili kufikia malengo ya Serikali ya kuwatumikia wananchi.
Akizungumza na Bodi, menejimenti na wafanyakazi, Mhandisi Nditiye amewaeleza kuwa TMA ni chombo muhimu sana kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya taifa letu na wananchi kwa ujumla kwa kuwa sekta ya usafiri wa anga, majini, ujenzi wa majengo mbalimbali, miundombinu ya barabara na reli, afya, kilimo na mazingira vyote vinategemea taarifa za hali ya hewa kutoka kwenye Mamlaka hii. “Mtambue kuwa hakuna ndege inayoweza kutua wala kuruka bila kupata taarifa kutoka kwenu, vile vile mkandarasi anayejenga reli ya kisasa ya SGR nae anategemea taarifa zenu kwa kiasi kikubwa, hivyo mtambue ninyi ni muhimu na mjitangaze,” amesema Mhandisi Nditiye.
Amesisitiza kuwa ni vema mjitangaze ili wananchi na wadau mbalimbali wafahamu majukumu na umuhimu wa taasisi yenu kwa kuwa uchumi wa taifa hili unategemea taarifa zenu ambapo wananchi wengi wamezoea kusikia na kuwaona mkitoa taarifa za tahadhari za hali ya hewa zinazohusiana na majanga na matukio mengine yanayohusiana na utabiri wenu angali ninyi mna taarifa muhimu zaidi na tofauti na mtazamo wa wananchi walio wengi.
Amefafanua kuwa wananchi wanaziamini taarifa zenu za hali ya hewa kwa kuwa kwa kiasi kikubwa yale mnayotabiri na kuwaeleza ndiyo yanayotokea iwe ni mvua kubwa, upepo mkali au joto kali kama ilivyo sasa. “Nimetembea na kukagua mitambo, vifaa vya kisasa na namna wanavyofanya kazi na nimebaini kuwa taarifa zinazotolewa hapa zimekusanywa kutoka vituo mbali mbali vya hali ya hewa nchini ambapo hapa makao makuu wataalamu wanazichakata, kusambaza kwa wahusika na kuhifadhiwa, na zinaonesha kuwa ni taarifa za uhakika kwa kiwango cha asilimia 87.5 ambapo imeongezeka kutoka asilimia 82.1 kwa miaka mitatu iliyopita,” amesema Mhandisi Nditiye.
Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Dkt. Buruhani Nyenzi wakati akiwasilisha taarifa yake kwa Mhandisi Nditiye amesema kuwa Mamlaka hii ni muhimu kwa ustawi na maendeleo ya taifa letu na wananchi kwa ujumla kwa kuwa utoaji wa taarifa na huduma za hali ya hewa nchini zimewezesha uokoaji wa maisha ya watu na mali zao; kuepuka au kupunguza athari na hasara zinazosababishwa na matukio ya hali ya hewa; kuongeza tija na mafanikio katika shughuli za kiuchumi kama vile kilimo, ufugaji, uvuvi; kuwa na miundombinu imara kama vile barabara, madaraja; kuongeza ufanisi katika sekta za usafiri na mawasiliano; kuchangia katika sekta za ujenzi na uendeshaji wa viwanda nchini na kukuza pato la taifa.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Hamza Kabelwa amemueleza Mhandisi Nditiye kuwa wahitaji wa taarifa za hali ya hewa kutoka kwa taasisi na wadau mbalimbali ambao wanahitaji kwa ajili ya kutekeleza shughuli za kiuchumi na kijamii wamekuwa wengi na teknolojia ya utabiri wa hali ya hewa na utoaji wa taarifa zake umebadilika ambapo inatulazimu kuhuisha Sheria Na. 6 ya Hali ya Hewa ya Mwaka 1978 na kukamilisha Sera ya Taifa ya Hali ya Hewa ili ziweze kwenda na wakati pamoja na kuboresha chuo cha Hali ya Hewa Kigoma kwa kuwa ndio chuo pekee nchini kinachotoa elimu ya awali na ya kati ya hali ya hewa.
Ameongeza kuwa TMA imepatiwa cheti cha ubora wa utoaji huduma na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO) kwa kutoa huduma kwa sekta ya anga nchini. Pia, inashirikiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa jangwa la Afrika (SADC), Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kwa kubadilishana taarifa za hali ya hewa, mabadiliko ya hali ya hewa yanayohitaji ushirikiano wa kimataifa, na kuendeleza na kutunza mtandao wa vituo vya uangazi wa hali ya hewa ili kukidhi makubaliano ya kimataifa ya kubadilishana taarifa hizo.
Dkt. Nyenzi amemshukuru Mhandisi Nditiye na kumueleza kuwa TMA inafarijika kusikia kuwa anafahamu kwa undani umuhimu wa utabiri wa hali ya hewa nchini, hivyo ni imani yake kuwa ataisamimia vema ili ifikie malengo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

UPASUAJI WA KIHISTORIA WAFANYIKA MOI KWA MAFANIKIO

$
0
0
Madaktari Bingwa wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na Madaktari wa Hosipitali ya BLK India leo wamefanya upasuaji maalum wa mgongo kwa kutumia matundu (Minimal Invasive Spine Surgery) kwa mgonjwa aliyedhoofika uti wa mgongo.

Kwa Mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam, Upasuaji huo umefanywa kwa mafanikio makubwa ukiwashirikisha Madakatari Bingwa wanne wakiongozwa na Profesa Joseph Kahamba wa MOI na Dkt. Puneet Girdhan kutoka hosipitali ya BLK.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa upasuaji huo umefanyika kwa mafanikio makubwa kwa muda wa masaa manne ambapo pamoja na upasuaji huo, MOI imeanzisha huduma za upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu ( Athroscopy ).

“ Tayari wagonjwa 300 wameshafanyiwa upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu kwa ufanisi mkubwa na wagonjwa wengine wameendelea kunufaika na huduma hii” Inasisitiza sehemu ya Taarifa hiyo

Kutokana na mabadiliko ya teknolojia ya matibabu, upasuaji wa kupanua njia za mishipa ya fahamu na kuimarisha uti wa mgongo kwa nyenzo za kisasa umeshika hatamu na Taasisi hiyo imeendelea kufanya mabadiliko ili kuendana na hali hiyo.

Taasisi ya MOI na Hospitali ya BLK ya India zilianzisha ushirikiano mwaka 2016 na hii ni mara ya pili kwa wataalamu kutoka hosipitali hizi kufanya upasuaji kwa kushirikiana.

MRAJISI WA USHIRIKA ANGALIA UTENDAJI WA MAMCU-MAJALIWA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mrajisi wa Ushirika Dkt. Titto Haule aangalie kwa umakini utendaji na ufanisi wa chama cha Ushirika cha MAMCU na viongozi wote ili kubaini kama wanakidhi makusudio yake

Amesema ikiwezekana chama hicho kivunjwe ili waanzishe vyama kilele viwili vitakavyoweza kuhudumia wakulima katika maeneo yao ili waweze kuongeza tija.Waziri Mkuu alitoa agizo hilo leo (Jumanne, Februari 27, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Chiungutwa wilayani Masasi.

Pia Waziri Mkuu amerudia kutoa agizo hilo alipozungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Newala na Halmashauri ya wilaya ya Newala.Amesema anapata mashaka kuhusu uwezo wao wa kuwahudumia wakulima, hivyo ameagiza kuharakishwa kwa utekelezaji wa agizo hilo ili kurahisisha utoaji wa huduma.

MAMCU inahudumia wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Manispaa ya Mtwara, Halmashauri ya Nanyamba, Nanyumbu na Halmashauri ya wilaya ya Masasi.Amesema kwa takwimu hizo haamini kama chama hicho kina uwezo wa kuhudumia maeneo hayo, hivyo kusababisha wakulima kutofikiwa kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaagiza wakulima wa korosho wajiwekee akiba ya fedha ili ziweze kuwasaidia katika ununuzi wa pembejeo.
Amesema kwa mwaka huu Serikali haitogawa pembejeo ya salfa kwa sababu mwaka jana iligawa bure ili kuwahamasisha wakulima kufufua zao hilo.

Kadhalika amewataka wakulima wa korosho wapande miche mipya ya mikorosho na kuiondoa mikorosho ya zamani iliyozeeka ili waweze kuzalisha mazao bora.

WASHIRIKA WA MAENDELEO WAAHIDI KUSHIRIKIANA KWA KARIBU ZAIDI NA TANZANIA KULETA MAENDELEO

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) imekubaliana na Washirika wa Maendeleo kurejesha uhusiano wa karibu na wenye tija ili kusaidia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka Mitano pamoja na Mkakati wa Kukuza Uchumi Zanziba (MKUZA III).

Hayo yamebainishwa mjini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, wakati akifungua mkutano wa Mazungumzo ya kimkakati kama ilivyobainishwa kwenye Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo.

Bw. James amesema kuwa Mwongozo huo wa miaka 7, kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 hadi 2014/2025, umelenga kuipa Serikali nafasi ya kuongoza mchakato wa maendeleo na kuijengea Serikali uwezo wa kukusanya mapato yake ya ndani, kuchambua fursa muhimu za uwekezaji na kutumia masoko ya kikanda na kimataifa kupata faida.
Meza Kuu ikiongozwa na Mwenyekiti wa Mkutano kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa tatu kulia), kushoto kwake ni Mwenyekiti Mwenza na Mratibu wa Umoja wa Mataifa na kiongozi wa washirika hao wa Maendeleo Bw. Alvaro Rodriguez, mjini Dodoma.
Mratibu wa Umoja wa Mataifa na kiongozi wa washirika wa Maendeleo nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez, akihutubia mkutano wa kimkakati wa maendeleo kati ya Serikali ya Tanzania na Washirika wa Maendeleo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper Mjini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James akihutubia washiriki wa mkutano wa kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo uliofanyika mjini Dodoma ukilenga kuimarisha mahusiano kati ya pande hizo mbili ili kuiwezesha nchi kufikia malengo yake ya maendeleo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi na Somalia, Bi. Bella Bird, nje ya ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper Mjini Dodoma, walipokutana kujadili namna pande hizo mbili zinavyoweza kuimarisha ushirikiano wa kimkakati zaidi ili kuharakisha maendeleo ya nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani- USAID Bw. Andy Karas, nje ya ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper Mjini Dodoma, walipokutana kujadili namna Serikali na Washirika wa Maendeleo wanavyoweza kuimarisha ushirikiano wa kimkakati zaidi ili kuiwezesha nchi kuharakisha maendeleo yake kwa manufaa ya wananchi wake.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Jezi za Ajib na Shishimbi Zauzika-Mtwara.

$
0
0
Kuelekea mchezo kati ya Ndanda FC ya Mkoani Mtwara na Yanga Sc ya Jijini Dar es Salaam tayari wafanyabiashara wa Kuuza Jezi wameanza Kutundika Bidhaa hizo Huku Jezi ya Ibrahim Ajibu na Papikabamba Shishimbi Zikiongoza kwa Kuuzwa.

Jezi hizo ambazo zimesambazwa Pembeni ya Uwanja wa Umoja Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara,ambapo hata Hivyo ni Jezi za Simba FC na Yanga FC ndio Zinaonekana Kuuzwa Zaidi Huku Jezi za Ndanda SC Zikikosekana.

Mmoja wa Wafanyabiashara Saleh Hassan anasema Jezi zinazouzika ni wa Simba SC lkn kwa Timu ya Yanga SC wateja Waliowengi wamekuwa wakiulizia Jezi ya Ajibu pamoja na Shishimbi ambazo ndio zinaonek

Kwa Muonekana Hakuna Jezi ya Timu wenyeji Ndanda FC inayouzwa zaidi ya Jezi za Yanga SC na Simba SC.Mchezo wa Ndanda FC ya Mkoani Mtwara dhidi ya Simba SC unatarajia kufanyika Jtano ya Wiki hii.

MAGAZETI YA JUMATANO LEO FEBRUARY 28,2018

Wizara ya Mambo ya Nje yaahidi kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa vitendo

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akitoa taarifa ya ufunguzi katika kikao cha Wizara na wadau kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Februari 2016.

Lengo la kikao hicho ni kujadili maandalizi ya maonesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yanayotarajia kufanyika Nairobi, Kenya kuanzia tarehe 25 hadi 28 Aprili 2018 ambayo yanatarajiwa kwenda sambamba na sherehe za Siku ya Tanzania (Tanzania day) ambayo husherehekewa tarehe 26 Aprili 2018 siku ya Muungano. Maonesho hayo ni njia mojawapo za kutekeleza Diplomasia ya Uchumi inayosisitiza katika kukuza biashara, utalii na uwekezaji. 
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Chana akizungumza. Balozi Chana alieleza kuwa Ofisi za Ubalozi zimejidhatiti kuhakikisha zinasimamia fursa zote za Watanzania hususan masuala ya biashara ili kuweza kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa Taifa na Watanzania kwa ujumla. 
Wajumbe wa meza kuu wakifuatilia taarifa ya ufunguzi kuhusiana na maonyesho iliyokuwa ikiwasilishwa na Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani). Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Juma Ali Juma, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Chana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE), Bw. Edwin Rutageruka. 
Sehemu nyingine ya Wajumbe wa meza kuu wakifuatilia taarifa ya ufunguzi. Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Anisa Mbega, Mkurugenzi Mtendaji-Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye na Mwakilishi kutoka Chama cha Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda Tanzania (TCCIA), Bw. Godfrid Muganda. 
Wajumbe kutoka Serikalini na sekta binafsi wakifuatilia kikao. Waliokaa mstari wa kwanza ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Salehe. 
Wajumbe wakifuatilia kikao. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga na nyuma yake ni Afisa Mambo ya Nje, Bi. Bertha Makilagi. 
Wajumbe wakifuatilia kikao. 
Sehemu nyingine ya wajumbe wakifuatilia kikao. 
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images