Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

SERIKALI YAOMBWA KUENDELEA KUTENGA BAJETI KWA AJILI YA WANAWAKE NCHINI

0
0
Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imeombwa kuendelea kutenga bajeti kubwa katika bajeti zake kwa ajili ya kumuendeleza mwanamke wa Tanzania.

Ombi hilo limetolewa na Mbunge wa Jimbo la Hanang, Dk.Mary Nagu wakati akifungua Kongamano la Wanawake na Uongozi 2018 jijini Dar es Salaam jana.

"Tunaomba bajeti ya serikali ibadilike kwa kuangalia ajenda ya jinsia ukizingatia changamoto mbalimbali walizonazo wanawake" alisema Dk.Nagu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo.Dk. Nagu aliwataka wanawake wote kuungana na kuwa kitu kimoja ili kuzijua changamoto walizonazo na kuzitatua kwa msaada wa viongozi wanawake wastaafu.

Aliongeza kuwa wanawake ni jeshi kubwa na ndio wazalishaji wakubwa wa mali lakini kwa namna moja hama nyingine wamekuwa na changamoto nyingi ikiwemo ya mali zinazotokana na uzalishaji wao kutumiwa na wanaume wao.
 Mbunge wa Jimbo la Hanang, Dk.Mary Nagu, akihutubia wakati akifungua akifungua Kongamano la Wanawake na Uongozi 2018 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TGNP Mtandao, Vicensia Shule akizungumza kwenye kongamano hilo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akihutubia.
 Profesa Bernadeta Killian akitoa mada kuhusu hali halisi ya wanawake na uongozi hapa nchini.
 Spika wa Bunge Mstaafu Mama Anna Makinda na Naibu Waziri wa Walemavu (Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) – Stella Ikupa wakiwa kwenye kongamano hilo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

TANZANIA YADHAMIRIA KUONDOA TATIZO LA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA WANAWAKE NCHINI

0
0
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kupambana na Saratani ya mlango wa kizazi nchini kwa kuwapa kinga wasichana kuanzia umri wa miaka 9 mpaka 14 huku lengo likiwa ni kuondoa tatizo hilo nchini.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) mapema leo wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.

“Katika kukabiliana na ugonjwa wa Saratani na kuimarisha afya ya wanawake Tanzania na kupunguza vifo vitokanavyo na Saratani , Wizara ya Afya itaanza kutoa chanjo ya kuwakinga wasichana dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi”. Alisema Mhe. Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa kwa mujibu wa takwimu za taasisi ya Ocean Road Saratani ya Mlango wa kizazi zinazoongoza nchini kwa Asilimia 36 huku ikifuatia na saratani ya matiti, huku jumla ya wagonjwa wa Saratani nchini katika kila wagonjwa 100, wagonjwa 46 ni wa Saratani ya mlango wa kizazi na Saratani ya Matiti.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya Wadau wa Afya na waandishi wa habari wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi akimkaribisha mgeni rasmi Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
Wadau wa Afya na Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa kutoka kwa Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi.

WAFANYAKAZI JNIA,TAA WAMLILIA MAREHEMU SWAI

0
0
WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) wamesikitishwa na kifo cha Bw. Jerome Swai (58) aliyekuwa fundi bomba mahiri kilichotokea tarehe 26 , 2018 kwenye hospitali ya Amana baada ya kuugua kwa muda Mfupi.

Wafanyakazi hao kwa nyakati tofauti walisema marehemu Swai alikuwa hakubali kushindwa kwa kuhakikisha anatatua tatizo linalohusiana na mabomba ya maji kwa wakati wote anapokuwa kazini.

Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa, Bi. Hanna Kibopile alisema marehemu ameacha pengo kubwa kutokana na uchapakazi wake uliotukuka.
Naye meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mtwara, Bw. Daimon Mwakyosa alisema marehemu alikuwa akifanyakazi kwa bidii na hakukubali kushindwa.

“Marehemu alikuwa akiijua vyema kazi yake na hakukubali kushindwa nakumbuka wakati nikiwa JNIA na tukiwa tumepangwa shift (zamu) moja hakuna kilichoshindikana kwake kuhusu fani yake aliijua vyema kazi yake,” alisema Bw. Mwakosya.
Marehemu Jerome Swai
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka (kulia), akimpa pole Bi. Honoratha Emmilian aliyefiwa na mume wake marehemu Jerome Swai aliyekuwa Fundi Bomba (JNIA), alifariki tarehe 26 Februari, 2018 kwenye hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam.
Meneja Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Vedastus Fabian, akitoa pole kwa Bi. Honoratha Emmilian ambaye ni mke wa marehemu Jerome Swai aliyekuwa fundi bomba.
Ndugu wa marehemu Jerome Swai wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka (mwenye tai) alipofika kuwafariji, ambapo marehemu alikuwa Fundi Bomba JNIA.

NAIBU WAZIRI WA ARDHI ATEMBELEA MPAKA WA TANZANIA NA KENYA NAMANGA ARUSHA

0
0
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akielekea kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga wilaya ya Longido mkoa wa Arusha.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa TRA aliyeko katika kituo cha Huduma za  Pamoja Mipakani (OSBC) Paul Kamkulu  kuhusu huduma zinazotolewa katika kituo hicho kilichopo eneo la Namanga mpaka wa Tanzania na Kenya.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi msaidizi Upimaji vijijini wa wizara Huruma Lugalla (wa pili kulia) wakati akikagua mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga wilaya ya Longido mkoa wa Arusha.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akitoa maelekezo kwa ujumbe alioambatana nao wakati wa  kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga wilaya ya Longido mkoa wa Arusha.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula  akiwa amemshika Ngamia aliyemkuta eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya wakati alipokuenda kukagua mpaka baina ya Tanzania na Kenya.


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI MTWARA

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimkabidhi mashine ya kubangulia korosho, Aziza Juma, katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Mary Majaliwa wakiwasalimia wananchi, wakati wakiwasili katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizungumza na wananchi wa Newala mjini, katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipokea zawadi ya bakora, kutoka kwa mzee Mohammed Abeid Liyanga, anaye wawakilisha wazee wa Newala, katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Newala Mjini, katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018.

SERIKALI YASHAURIWA KUISHIRIKISHA MAHAKAMA KWENYE UANZISHWAJI WA MIKOA NA WILAYA

0
0
Na Lydia Churi-Mahakama, Kigoma
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ameishauri Serikali kuishirikisha Mahakama ya Tanzania kwenye mipango yake ya uanzishaji wa maeneo mapya ya kiutawala ili kupunguza changamoto za upatikanaji wa haki kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa ziara yake mjini Kigoma, Jaji Mkuu amesema mipango ya Serikali ya uanzishwaji wa wilaya au mikoa izingatie pia uanzishwaji wa Mahakama. Aliongeza kuwa Mikoa na wilaya mpya ndizo zenye ukosefu wa Mahakama hali inayowafanya wananchi kufuata mbali huduma za kimahakama.
Alisema Mahakama kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (2015/16 hadi 2019/20) imejipanga kutatua tatizo la ukosefu wa huduma za Mahakama pamoja na kusogeza huduma hizo karibu Zaidi na wananchi. Kwa kushirikiana na Benki ya Dunia, tayari imeanza ujenzi wa Mahakama tano za Hakimu Mkazi katika mikoa ya Simiyu, Katavi, Geita, Njombe na Manyara pamoja na ujenzi wa Mahakama 16 za wilaya na Mahakama Kuu mbili katika Mikoa ya Kigoma na Mara.
Jaji Prof. Juma amesema kupitia ziara yake ya siku saba kwenye Mahakama Kuu kanda ya Tabora amebaini kuwa watanzania wengi hufuata mbali huduma za Mahakama na maeneo mengine ni kutokana na jiografia ya maeneo hayo. Akitolea mfano wa wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Jaji Mkuu amesema kutokana na wilaya hiyo kuzunguka mkoa, wananchi wake hulazimika kufuata huduma za Mahakama Kuu zilizopo umbali wa Zaidi ya kilometa 377.
  Jaji mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa pamoja na wakandarasi wa kampuni ya Masasi Contruction Ltd wanaojenga jengo la mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma. mahakama ya Tanzania inajenga jengo hili pamoja na mengine nchini ili kusogeza huduma za mahakama karibu zaidi na wananchi.
Jengo la mahakama kuu kanda ya Kigoma likiwa limefikia hatua hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WATANZANIA SASA WAFIKIA MILIONI 54.2, NUSU YA WATU WOTE NI WATOTO

0
0
*Serikali yapiga marufuku mashirika kutoa takwimu ambazo hazina uthibitisho wa ofisi ya Takwimu

Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii

WAZIRI wa Fedha na Mipango,Dk. Philip Mpango amesema Tanzania inakadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao milioni 54.2 huku asilimia 50 wakiwa ni wa umri chini ya miaka 18.

Pia Dk.Mpango amewakumbusha wadau wote wa ndani na nje ya nchi kuwa takwimu za idadi ya watu kwa nchi ya Tanzania ni hizo ambazo amezitangaza leo na si vinginevyo.
.
Hivyo amepiga marufuku kwa shirika lolote kufanya makadirio ya idadi ya watu wa Tanzania na kuchapisha matokeo hayo bila kushirikisha Ofisi ya Taiga ya Takwimu na atakayebainika kufanya hivyo watamchukulia hatua kali za kisheria.

Dk.Mpango amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazondua taarifa ya makisio ya idadi ya watu Tanzania amvapo amesema kwa makadirio yaliyotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.

Na kuzingatia viwango vya uzazi na vifo kwa takwimu za mwaka 2016, idadi ya watu Tanzania sasa ni milioni 52.6 ambapo Tanzania Bara ni watu milioni 52.6 na Tanzania Bara watu milioni 1.6 kwa mwaka 2018.Dk.Mpango amesema idadi hiyo inakadiriwa kufikia watu milioni 59.4 mwaka 2021 na ifikapo mwaka 2030 idadi ya watu itafikia milioni 77.5.

Amefafanua kwa kuzingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 inakadiriwa kuwa kila mwaka kuna ongezeko la wastani watu wapatao milioni 1.6 hapa nchini.Dk.Mpango amesema ongezeko hill linatokana na idadi kubwa vya vizazi vipatavyo milioni 2.0 ikilinganishwa na idadi ndogo ya vifo ambavyo ni takribani 400,000 kwa mwaka.

Hotuba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo katika kumbukizi ya vita vya Maji Maji mjini Songea Mkoani Ruvuma


FARM AFRICA YAHAMASISHA WAKULIMA WADOGO WA NAFAKA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MASOKO YA MAZAO

0
0
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Shirika la Kimataifa la Farm Africa limewataka wakulima wadogo wa mazao ya nafaka hapa nchini kutumia mifumo ya mitandao kupitia simu za mkononi kutangaza bei ya mazao ya nafaka na kupata taarifa za kilimo bora ili kuwasaidia kupata kipato chenye tija na kuondokana na hali duni katika familia zao.

Meneja Program ya FoodTrade wa Shirika hilo la Kimataifa la Farm Africa,Bi. Beatrice Muliahela alisema hayo jijini Arusha katika warsha ya siku moja kuwa wakulima wadogo wanahitajika kutumia mifumo ya mitandao kupitia simu katika kutangaza bei ya mazao yao na kupata taarifa za kilimo bora ili kuwasaidia kupata kipato chenye tija na kuondokana na hali duni katika familia zao.

Mradi huu ni wa miaka miwili na unafadhiliwa na Department for International Development (DFID) kupitia DAI kwa kuhusisha wadau wengine kama Taasisi ya Maendeleo Vijijini na Mijini (RUDI) na VECO kwa sasa Rikolto ambao umesaidia wakulima wadogo 70,000 nchini Tanzania na Uganda.

“Farm Africa inahitaji kuona wakulima wadogo nchini Tanzania wanatumia mifumo ya mitandao kupitia simu katika kutangaza bei ya mazao yao na kuuza kwa bei nzuri zaidi,” na hii tunahamasisha katika nchi zote kumi za Afrika Mashariki kutumia mifumo hii, aliongeza kusema,Bi. Muliahela.
 Mkurugenzi wa Msaidizi Kitengo cha Kuzuia Upotevu wa Mazao baada ya Mavuno Wizara ya Kilimo, Bi. Josephine Omolo kushoto akifuatilia mada katika warsha iliyokuwa ikizungumzia jinsi wakulima wanavyoweza kutumia mifumo ya mitandao kupitia simu za mkononi kutangaza bei ya mazao yao na kupata taarifa za kilimo bora na kipato chenye tija kuwawezesha kuondokana na hali duni katika familia zao, katikati ni Meneja Program ya FoodTrade wa Shirika la Kimataifa la Farm Africa,Bi. Beatrice Muliahela na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo Vijijini na Mijini (RUDI), Lameck Kikoka.
 Wadau wa Shirika la Kimataifa la Farm Africa wanaojihusisha na shughuli za kilimo wakifuatilia  mada katika warsha iliyokuwa ikizungumzia jinsi wakulima wanavyoweza kutumia mifumo ya mitandao kupitia simu za mkononi kutangaza bei ya mazao yao na kupata taarifa za kilimo bora na kupata kipato chenye tija kuwezesha kuondokana na hali duni katika familia zao. 
Meneja Program ya FoodTrade wa Shirika la Kimataifa la Farm Africa,Bi. Beatrice Muliahela akifafanua jambo katika warsha iliyokuwa ikizungumzia jinsi wakulima wanavyoweza kutumia mifumo ya mitandao kupitia simu za mkononi kutangaza bei ya mazao yao na kupata taarifa za kilimo bora kupata kipato chenye tija na kuondokana na hali duni katika familia zao, katikati ni Mkurugenzi wa Msaidizi Kitengo cha Kuzuia Upotevu wa Mazao baada ya Mavuno Wizara ya Kilimo, Bi. Josephine Omolo na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo Vijijini na Mijini (RUDI), Lameck Kikoka.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KESI YA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA INAYOMKABILI TIDO MHANDO KUANZA KUSIKILIZWA MACHI 28

0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

KESI  ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando kuanza kusikilizwa Machi 28, mwaka huu

Hatua hiyo inakuja baada ya mtuhumiwa huyo leo Februari 28, 2018 kusomewa maelezo ya awali (PH), Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa

Kabla ya kusomewa PH, Mhando alikumbushwa mashtaka yake yanayomkabili na Wakili wa Serikali Dismas Mganyizi. Katika maelezo hayo ya awali, Tido amekubali maelezo yake binafsi ya kwamba alikuwa Mkurugenzi  Mkuu wa TBC  mwaka 2006 hadi 2010 na kuwa alikuwa msimamizi katika shughuli za TBC lakini  siyo kwa shughuli zote.

Pia alikubali kutoa maelezo katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) lakini hakukiri na kuwa alifikishwa mahakamani Januari 26,mwaka 2018. Aidha Mhando alikana mashtaka yote yanayomkabili na kesi hiyo itaanza kusikilizwa kwa upande wa mashtaka kuleta mashahidi wao Machi 28,mwaka 2018. Mhando anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh.milioni 887.1.

Inadaiwa kuwa Juni 16,mwaka  2008 akiwa  Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhando ambaye alikuwa Mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.

Katika shtaka la pili, Mhando anadaiwa kutumia vibaya madaraka yake Juni 20,mwaka 2008 aliposaini makubaliano kwa utangazaji wa digitali duniani kati ya TBC na BVl.
Katika shtaka la tatu, anadaiwa Agosti 11,mwaka 2008 na Septemba 2008 akiwa Dubai, Mhando alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano kwa ununuzi, usambazaji kufunga vifaa vya usambazaji na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuifaidisha BVI.

Katika shtaka la nne, anadaiwa kuwa  Novemba 16, mwaka 2008 akiwa Dubai, Mhando alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano kwa kuendesha miundombinu ya utangazaji (DTT Broadcast Infrastructure) kati ya TBC na BVI na kuinufaisha BVI.

Katika shtaka la mwisho,  anadaiwa kuwa kati ya Juni 16 na Novemba 16,mwaka 2008 akiwa UAE, Mhando aliisababishia TBCli hasara ya Sh.887,122,219.19.

UAE kuwajengea nyumba waliopata maafa

0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed  Aboud Mohammed kulia akizungumza na Ujumbe wa  Mwezi Mwekundu wa  Emarates kuhusiana na utiliaji saini Ujenzi wa Nyumba za msaada kwa waathirika wa mafuriko Zanzibar.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed  Aboud Mohammed aliesimama kulia akiwa pamoja na Msaidizi Balozi wa Emarates, Muhammed Ibrahim Al-Bahri wakishuhudia utiaji saini  Ujenzi wa Nyumba za msaada kwa waathirika wa mafuriko Zanzibar.
 Mkurugenzi wa Kamisheni ya Maafa zanzibar Shaaban Seif Mohammed akibadilishana hati ya saini na Mkurugenzi wa Maafa wa Emarates, Said Mohammed Al-humaini kuhusiana na  Ujenzi wa Nyumba za msaada kwa waathirika wa mafuriko Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed  Aboud Mohammed akiwa katika picha ya pamoja na  Ujumbe wa  Mwezi Mwekundu wa Emarates baada ya  kutiliana  saini Ujenzi wa Nyumba za msaada kwa waathirika wa mafuriko Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

ANGELINA MABULA ATEMBELEA MRADI WA NYUMBA WA SAFARI CITY ARUSHA

0
0
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akipokewa na Meneja Mradi wa Safari City. James Kisarika alipotembelea mradi huo kujionea nyumba zilizojengwa na Shirika la Nyumba (NHC).
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akipata naelezo kutoka kwa Meneja Mradi wa Safari City, James Kisarika(kulia)  alipotembelea mradi huo kujionea nyumba zilizojengwa na Shirika la Nyumba (NHC). 
 Baadhi ya Nyumba za Safari city 

NEWS ALERT: TAARIFA KUTOKA NEC KUHUSU SHUTUMA ZA MBOWE

0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
nembo%20ya%20NEC

                           TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesikia malalamiko yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambayo aliyawasilisha jana kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Malalamiko yaliyotolewa na Mhe. Mbowe yametusikitisha kwa sababu mbali na kumjibu kwa barua, Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani aliongea na Mhe. Mbowe kwa njia ya simu. Madai kwamba tume haikuwajibu malalamiko yao sio kweli. Ni upotoshaji wa hali ya juu ambao haupaswi kufanywa na kiongozi kama yeye.
Tume ya taifa ya uchaguzi haijibu malalamiko kwa matakwa ya mtu anavyotaka kujibiwa, bali inajibu hoja kwa mujibu matakwa ya katiba, sheria, kanuni na maadili ya uchaguzi na maelekezo yote ambayo yapo kwa mujibu wa sheria. Kama majibu ya tume hayakuwafurahisha CHADEMA, tume inasisitiza kuwa walijibiwa  kwa matakwa ya sheria na katiba na sio matakwa ya mkurugenzi wa uchaguzi, Tume, Chadema au chama chochote cha siasa.
Kanuni, sheria, maelekezo na maadili ya uchaguzi yameweka utararatibu wa kushughulikia malalamiko na changamoto zinazojitokeza wakati wa uchaguzi.  Utaratibu uko wazi kwa changamoto zinazotokea wakati wa uteuzi, wakati wa kampeni ambako kuna kamati za maadili na jinsi ya kukata rufaa.
Kwa masikitiko CHADEMA walitekeleza hatua moja tu katika vipengele hivyo wakati wa uchaguzi, kipengele walichotekeleza ni pale baadhi ya wagombea wao walipoenguliwa kugombea, walifuata utaratibu kwa kuwasilisha rufaa tume ya uchaguzi na Tume ilipitia na ikawarudisha wagombea wao kwenda kugombea.
CHADEMA walitaka wakati wa kampeni, Tume ifanye maamuzi kinyume cha maadili waliyoyasaini. Wakati wa kampeni kuna kamati za maadili ngazi ya jimbo ambayo mwenyekiti ni msimamizi wa uchaguzi na wajumbe ni kutoka vyama vyote vilivyosimamaisha wagombea na ndio wanaofanya uamuzi. Chadema waliwasilisha malalamiko kwa Tume badala ya kuwasilsiha malalamiko kwenye kamati hizo za maadili zinazosimamia malalamiko yote.
Sio sahihi kusema Tume hatukujibu malalamiko yao. Mfano tarehe 15 Chadema waliwasilsiha barua mbili Tume ya Uchaguzi, waliwasilisha barua moja asubuhi na saa 1.30 jioni waliwasilisha barua nyingine, jumla barua hizo zikiwa na hoja tano na Tume ikawaandikia barua zenye ufafanuzi wa hoja hizo.
Hoja ya kwanza, CHADEMA walitaka kuapishwa mawakala wao mbadala asilimia 15. Tuliwajibu kwamba hakuna kifungu cha sheria kinachokipa fursa chama chochote cha siasa kuapishiwa mawakala mbadala asilimia 15. Kifungu 57 (3) kinafafanua vizuri namna ya mawakala wanavyotakiwa kuwepo na kuapishwa
Lakini pia hata kama kifungu hicho kingekuwa kinatoa fursa hiyo, Chadema walileta malalamiko yao  tarehe 15 Februari 2018 wakati uteuzi wa mawakala ulikuwa tarehe 10 Februari 2018, hivyo hakukuwa na muda wa kuwaapisha mawakala wengine kwa mujibu wa sheria kwa kuwa hawakuwemo kwenye orodha.

Hoja nyingine ya CHADEMA ni msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni alikataa kuwapa mawakala barua na fomu za viapo. Tulifanya hesabu tukaona kwamba msimamizi alitakiwa kusaini barua 22,000 na fomu za viapo 14,000. Tukasema kwamba kutakuwa na utaratibu wa mawakala kupewa fomu na viapo vyao kupitia kwa wawakilishi wao na walipewa kwa njia hiyo. Hili tuliwajibu hivyo katika barua yetu.
Hoja nyingine mawakala wa CHADEMA waliambiwa kwenda na vitambulisho kwenye vituo vya kupigia kura. Katika hoja hii tuliwajibu kwamba wakala chama cha siasa ni mpiga kura kama walivyo wapiga kura wengine. Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia sheria ya uchaguzi kifungu namba 61 na namba  62 cha sheria za Serikali za mitaa, Tume ilitoa ridhaa kwa wapiga kura kutumia vitambulisho mbadala ili nao waweze kupiga kura ndio maana wakaelekezwa kwenda navyo.

Hoja nyingine ni kwamba msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni, hajatoa maelekzo ni wapi pa kuhesabia kura. Tukawajibu kwamba Tume ina barua kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi akiwajulisha vyama vya siasa kwamba sehemu ya kujumlishia kura itakuwa ni sehemu ya Biafra. Kanuni inasema wangejulishwa eneo hilo la kujumlishia baada ya kura kupokelewa, lakini msimamizi wa uchaguzi alijiongeza akawajulisha mapema eneo la kujumlishia kura.
Hoja nyingine ni wasimamizi wa vituo hawakuteuliwa kwa utaratibu. Majibu ya hoja hii ni kwamba sheria ya uchaguzi imeweka utaratiibu wa namna wasimamizi hao wanavyopatikana. Lakini kanuni za uchaguzi wa Rais namba 15 na kanuni 11 za Serikali za Mitaa zinaeleza namna msimamizi wa kituo anavyopatikana.

Kanuni hiyo inasisitiza kuwa msimamizi wa uchaguzi atatoa tangazo, Kwa jimbo la Kinondoni msimizi alitoa tangazo, watu waliomba, walifanya usahili na kabla ya uteuzi mkurugenzi wa uchaguzi alitoa matangazo ya majina katika mbao zote za kata 10 za jimbo la Kinondoni.
Msimamizi wa uchaguzi aliwaandikia barua vyama vyote kama vina pingamizi vijitokeze. Kama kulikuwa na tatizo vyama vilikuwa na fursa ya kuweka pingamizi, lakini hawakufanya hivyo na Tume tuliwajibu hivyo. Unaposema tume haikuwajibu sio kweli, labda CHADEMA waseme tuliwajibu nje ya matakwa yao waliyotaka na sio kwa mujibu wa sheria.

Hoja nyingine ni kwamba kuna wizi wa kura. Katika kituo cha kupigia kura kuna msimamizi wa kituo, msimamizi msaidizi na wakala wa chama cha siasa na kuna waandishi wa habari. Utaratibu ulikuwa wazi. Pia kuna utaratibu wa kisheria wa kuwasilisha malalamiko kama mtu haridhiki kabla wakati na baada ya kupiga kura, wakati wa kuhesabu na baada ya kuhesabu kura.
Mtu au chama kisipofuata uratibu huo, lazima utalalamika tu na utaona tume ni korofi. Hii ni kwa sababu mtu akija Tume kulalamika, ataelekezwa kufuata utaratibu huo. Mgombea akikataa kufuata utaratibu huo hata akija Tume kulalamika,ataelekezwa na Tume atumie wakala wake kujaza fomu zote namba 14 na 16 zinazohusika kisheria kuwasilisha malalamiko.

Tunamsihi Mbowe na chama chake, wasome sheria za uchaguzi na kuzielewa. Tume iko tayari kumpa elimu ya mpiga kura kuzifahamu sheria hizi kwa mapana yake.
Pia tunamwomba Mhe. Mbowe kama hakuridhika na taratibu za uchaguzi, ana fursa ndani ya siku 30 za kuwasilisha malalamiko yake mahakamani ndicho chombo pekee cha kutoa haki. Aende mahakamani kwa kutumia ushahidi ambao mawakala wake walijaza kwenye fomu namba 14 na 16 kwa sababu Tume ya Uchaguzi haina tena fursa ya kupokea malalamiko kisheria baada ya uchaguzi kupita.
Kailima, R.K
MKURUGENZI WA UCHAGUZI

MICHUZI TV: TTCL CORPORATION YAJA NA KASI BALAA KWA KUTUMIA MKONGA

MICHUZI TV: WAKILI WA TIDO MHANDO AZUNGUMZIA MWENENDO WA KESI YA MTEJA WAKE


TCRA YASITISHA NYIMBO ZISIZOKUWA NA MAADILI

LUNDENGA ATANGAZA KUBWAGA MANYANGA KUANDAA MASHINDANO MISS TANZANIA

0
0

Na Leandra Gabriel , Globu ya Jamii

MKURUGENZI wa Kampuni inayoandaa mashindano ya Miss Tanzania ya Lino International Agency LTD Hashim Lundenga ametangaza rasmi kuacha shughuli za kuendesha mashindano hayo kuanzia Februari 13 mwaka huu.

Hivyo kuanzia sasa mashindano ya Miss Tanzania nchini yataendeshwa na The Look Company Limited, chini ya Mkurugenzi Basila Mwanukuzi aliyewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1998.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Hashim Lundenga amesema uamuzi huo umetokana na malengo yao ya kutaka mashindino hayo kusimamiwa na damu changa kwa lengo la kuleta chachu katika tasnia ya urembo nchini.

“Tumefikia uamuzi huu baada ya kuona kampuni yetu tayari imejijengea sifa na heshima nchini.Hata hivyo tunaamini The Look Company Limited chini ya Mkurugenzi Mwanukuzi watasimamia taratibu, kanuni, sheria na miiko ya uongozi na hatimaye kumpeleka mrembo katika mashindano ya dunia kama ilivyo kawaida,”amesema. Amewataka waandaaji wapya wa mashindano ya urembo wasisite kuomba ushauri au mawazo ya kujenga kutoka kwao pale watakapohitaji.

Lundenga ambaye ni maarufu kama Uncle Hashim amewashukuru Baraza za sanaa la Taifa (BASATA), na Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo kwa ushirikiano mkubwa kwa muda wote tangu kuanza kwa mashindano hayo mwaka 1994.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Look Limited, Mwanukuzi amesema wamejiwekea mikakati kuendeleza fani ya ulimbwende pale ambapo kampuni ya Lino imeishia. Amesema kuwa pale penye changamoto katika kuandaa masuala ya warembo watakuwa karibu na Kampuni ya Lino pamoja na BASATA ili kufanikisha na kuleta tija katika Taifa.
 MKURUGENZI wa Kampuni inayoandaa mashindano ya Miss Tanzania ya Lino International Agency LTD Hashim Lundenga akitangaza uamuzi wake rasmi kuacha shughuli za kuendesha mashindano hayo kuanzia Februari 13 mwaka huu,pichani kati ni Mkurugenzi wa The Look Company Limited Basila Mwanukuzi pamoja na Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Godrey Mngereza akishuhudia tukio hilo.
 Mkurugenzi wa The Look Company Limited Basila Mwanukuzi akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar,wakati akikabidhiwa jukumu la kuendesha shughuli za shindalo la Miss Tanzania

IGP SIRRO AKUTANA NA KIKOSI MAALUM CHA KUPAMBANA NA UHALIFU WA KUTUMIA SILAHA ZA MOTO

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiwa katika picha ya pamoja na askari wa kikosi maalum cha kupambana na uhalifu hususani katika barabara kuu ya mkoa wa Shinyanga, inayounganisha mikoa ya jirani ya Mwanza na Geita ambapo kikosi hicho kimepata mafanikio makubwa kutokana na kupambana na wahalifu waliokuwa wakitumia silaha za moto. Picha na Jeshi la Polisi.

RAIS SHEIN AKUTANA NA VIONGOZI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage akiwa na ujumbe aliofuatana nao walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo (katikati) Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe.Hamid M.Mahmoud.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage (wa pili kulia) alipokuwa akiwatambulisha Viongozi aliofuatana nao  walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa mazungumzo na Rais (katikati) Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe.Hamid M.Mahmoud.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo pamoja na ujumbe aliofuatana nao.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na mgeni wake   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo pamoja na ujumbe aliofuatana nao
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifurahia jambo alipokuwa akibadilishana mawazo na  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage (kushoto)wakiwepo na Viongozi wengine baada ya mazungumzo yao walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo, (Picha na Ikulu).

JAFO AZITAKA HALMASHAURI KUANZISHA MADUKA YA DAWA

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo amezitaka Halmashauri kuanzisha maduka ya dawa katika wilaya zao ili kuondokana na tatizo la ukosefu wa dawa kwenye maeneo hayo.

Waziri Jafo ameitoa kauli hiyo leo alipokuwa akifungua duka la dawa la kisasa lililofunguliwa katika Hospitali ya wilaya ya Kisarawe ambapo duka linatarajiwa kuondoa tatizo la ukosefu wa dawa katika hospitali ya wilaya, vituo vya afya, na zahanati wilayani Kisarawe. 


Akifungua duka hilo, Jafo amesema endapo dawa zitakosekana katika duka la hospitali au katika vituo vingine vya kutolea huduma ya afya wilayani basi watanunua dawa katika duka hilo.


Aidha amezitaka Halmashauri zingine kuiga mfano wa Halmashauri za Kisarawe, Muheza, Jiji la Tanga na zingine ambazo tayari zimejipanga vyema kuwahudumia vyema wananchi wao katika suala la Afya. 


Waziri Jafo ameipongeza Bohari ya Dawa(MSD) kwa msaada mkubwa wanaoutoa katika kufanikisha uanzishaji wa maduka hayo ya dawa.


Duka hilo limeanzishwa kwa gharama ya sh. milioni 89 ambapo kiasi cha Sh.Milioni 10 alizitoa Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe na Sh.Milioni 79 zilitolewa na Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe. 

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akizungumza na wananchi katika ufunguzi wa duka maalum la dawa Kisarawe.

 Mganga Mkuu wa wilaya ya Kisarawe akitoa maelezo kuhusu uanzishaji wa duka la dawa wilayani humo.

 1.  Wananchi wa Kisarawe wakiwa katika ufunguzi wa duka la dawa.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akikagua madawa yaliyohifadhiwa katika stoo ya duka la kisasa la dawa.

 Stoo kubwa ya duka la dawa Kisarawe.


Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images