Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Wananchi zaidi ya 1200 wajitokeza Songamebele zinduzi wa Ujenzi kituo cha afya Kirando

$
0
0
Zaidi ya wananchi 1200 wa kata ya Kirando inayojumuisha vijiji vinne vya Mtakuja, Mpata, Kichangani na Kamwanda, Wilayani nkasi Mkoani Rukwa, wajitokeza katika kuhakikisha uchimbaji na uwekaji wa msingi wa kituo cha afya cha kirando unakamilika ili kuweza kuanza upanuzi na ujenzi wa kituo hicho kitakachohudumia kata zaidi ya nne katika tarafa ya Kirando.  

Wananchi hao wamejitokeza kwa wingi kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha huduma hizo za kiafya zinasogezwa karibu na wananchi yao ili kuokoa maisha ya kina mama wajawazito, watoto na wahitaji wengine wa huduma hizo ambao wanaishi karibu na kituo hicho na kuongeza kuwa umbali wa kutoka Kirando hadi hospitali ya Wilaya iliyopo Namanyere ni Kilometa 61.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo aliyeongoza harambee hiyo amesema kuwa wameamua kuungana na wananchi pamoja na kuwashirikisha ili kuwajulisha wananchi juhudi zinazofanya na wananchi na kuonyesha mshikamano kuwa maendeleo hayaji bila ya mshikamano.

“Kila mtu anaguswa na afya, mtoto, mzee na kijana wote, serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli imeamua kuboresha na kupanua vituo vya afya ili huduma zisogee karibu kuliko kutegemea hospitali za wilaya, kwa hali hiyo ndio maana serikali inapanua vituo vya afya ili tuupunguze msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali zetu pamoja na kwenye vijiji na tarafa huduma ziwe bora zaidi.” Alifafanua.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiongea na kinamama walioshiriki kwenye Songambele ya Ujenzi wa upanuzi wa kituo cha Afya Kirando muda mfupi kabla ya kinamama hao kuruhusiwa na kuwaachia wanaume kuendelea na kazi.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa pili kutoka kushoto) akipokezana na wananchi mawe ya msingi yanayojengewa msingi wa kituo cha afya cha kirando siku ya uzinduzi wa songambele ya upanuzi wa ujenzi wa kituo hicho.
 Wanananchi wa Kirando waliojitokeza kushiriki katika Songambele ya ujenzi wa Kituo cha afya Kirando. 

 Wanananchi wa Kirando waliojitokeza kushiriki katika Songambele ya ujenzi wa Kituo cha afya Kirando.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

SIMBA YAANZA KUJIFUA UWANJA WA VETERANI

$
0
0

Na Agness Francis Globu ya jamii. 

 VINARA wa Ligi kuu Tanzania Bara Simba SC mara baada ya kurejea kutoka nchini Djibout katika mchezo wa marudiano na Gendarmarie sasa wanaanza mazoezi rasmi leo ili kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mbao FC. Mazoezi hayo yataanza leo jioni saa 10 jioni katika uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam. 

 Ikiwa ni mzunguko wa 2 round ya 19 katika michuano ya kuania Ubingwa wa Tanzania Bara ambapo mchezo uliopita Simba alitoka sare ya 2-2 dhidi ya Mwadui FC katika Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga. 

 Hata hivyo Kikosi hicho kilipewa muda wa mapumziko ya siku moja baada ya kurejea kutoka nchini Djibout katika mchezo wa marudiano dhidi ya Gendarmerie ambapo kikosi cha Simba kiliibuka na Ushindi wa goli 1-0 na kujiandikishia tiketi ya kwenda hatua ya mbele zaidi katika Michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.

UWEPO WA VIWANDA UTACHANGIA UZALISHAJI WA BIDHAA ZA KILIMO-MHANDISI STELLA MANYANYA

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

NAIBU Waziri wa Viwanda, Uwekezaji na Biashara Mhandisi Stella Manyanya amesema uwepo wa viwanda nchini utachangia kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa bidhaa za kilimo kwa kuwahakikishia wakulima wanakuwa na soko la uhakika.

Mhandisi Manyanya ameyasema hayo leo jijijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la wajibu wa taasisi za fedha katika kuendeleza viwanda nchini lililoandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA).

Amesema ili kufikia malengo hayo kunahitajika ushirikiano mkubwa kati ya sekta binafsi na Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara."Tasisi za fedha mnatakiwa kuhakikisha mnatatua changamoto za wajasiriamali za ukosaji wa mitaji jambo ambalo limekuwa likiwasumbua wengi wao, ili kuhakikisha tunafikia Tanzania ya viwanda" amesema.

Mhandisi Manyama, amesisitiza ikiwa taasisi za fedha zitasaidia kukuza uchumi kupitia viwanda maana yake itakuwa chachu ya kukuza kipato cha wawekezaji na kuongeza mnyororo wa thamani.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara , Mhandisi Stela Manyanya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA) kuhusu wajibu wa taasisi za fedha katika kuendeleza Viwanda Tanzania.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Nchini na Mwenyekiti wa jumuiya ya Mabenki , Charles Kimei akichokoza mada wakati wa Kongamano kuhusu wajibu wa Tasisi za fedha katika kuendeleza Viwanda Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tasisi ya Sekta Binafsi Nchini(TPSF),Geoffrey Simbeye, akichokoza mada wakati wa kongamano la kujadili umuhimu wa mabenki na sekta binafsi katika maenedeleo ya Viwanda.

KAIMU KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MBUNGE KUTOKA UTURUKI

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan M. Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Mhe. Zehra Taskesenlioglu, Mbunge na Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge wa Bunge la Uturuki wanaounda Kundi la Wabunge Marafiki na Wabunge wa Bunge la Tanzania alipofika Wizarani tarehe 23 Februari, 2018. Katika mazungumzo yao walizungumzia umuhimu wa kukuza na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Uturuki katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu. 
Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Ali Davutoglu (kulia) akiwa pamoja na Bw. Aytak Dincer, Mwekezaji na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Tanzania na Uturuki wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mwinyi na Mhe. Zehra (hawapo pichani) 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salvator Mbilinyi (kulia) akiwa na Bw. Hassan Mwamweta, Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo 
Kikao kikiendelea 

ALICHOSEMA WAZIRI MKUU KWA RAIS WA FIFA, GIANNI INFANTINO.

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MKUTANO WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA AFRIKA MASHARIKI ULIOMALIZIKA LEO JIJINI KAMPALA NCHINI UGANDA

$
0
0
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Rais wa Uganda Yoweri Museveni pamoja na viongozi wengine wa Jumuiya hiyo katika siku ya mwisho ya Kikao chao kilichofanyika Kampala nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anatoka katika ukumbi wa mkutano pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kumalizika kwa vikao vya Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC vilivyofanyika Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir pamoja na viongozi wengine wa Jumuiya hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi mbalimbali waliohudhuria mkutano wa EAC katika siku ya mwisho jijini Kampala nchini Uganda. PICHA NA IKULU

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 23.02.2018

MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO FEBRUARY 24,2018


MAHOJIANO YA ZARI HASSAN NA BBC SWAHILI JIJINI LONDON IJUMAA FEBRUARI 23, 2018

UNNewsKiswahili:Watu zaidi ya 40 kuwajibishwa kwa uhalifu wa kivita Sudan kusini

Article 8

$
0
0
 NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akilakiwa na Osmund Ueland Mshauri wa Shamba sehemu ya shamba lenye hekari 651 lililonunuliwa na Taasisi ya Ilula Programu 2013 wakati wa ziara yake mkoani Iringa Februari 23 2018. Shamba hilo ni la kilimo cha biashara ni maalum kwa ajili ya kina mama wanaojitegemea, watoto yatima na wanafunzi wenye nia ya kukuza uelewa wa kilimo kutoka katika Wilaya ya Iringa hasa wa shule za primary na awali. Pamoja naye (kushoto) Mwasisi wa Ilula Orphan Program (IOP), Berit Skaare.
 NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akipata maelezo ya ujenzi wa makazi maalumu ya kujifunzia kutoka kwa Osmund Ueland Mshauri wa Shamba (kulia) kwenye eneo la shamba lenye hekari 651 lililonunuliwa na Taasisi ya Ilula Programu 2013 wakati wa ziara yake mkoani Iringa Februari 23 2018. Shamba hilo ni la kilimo cha biashara ni maalum kwa ajili ya kina mama wanaojitegemea, watoto yatima na wanafunzi wenye nia ya kukuza uelewa wa kilimo kutoka katika Wilaya ya Iringa hasa wa shule za primary na awali. Pamoja naye (kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga na Mwasisi wa Ilula Orphan Program (IOP) Berit Skaare. 
 NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akikagua sehemu ya shamba lenye hekari 651 lililonunuliwa na Taasisi ya Ilula Programu 2013 wakati wa ziara yake mkoani Iringa Februari 23 2018. Shamba hilo ni la kilimo cha biashara ni maalum kwa ajili ya kina mama wanaojitegemea, watoto yatima na wanafunzi wenye nia ya kukuza uelewa wa kilimo kutoka katika Wilaya ya Iringa hasa wa shule za primary na awali. Pamoja naye (kulia) ni Mshauri wa Shamba hilo, Osmund Ueland, Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga (nyuma kulia), Mwasisi wa Ilula Orphan Program (IOP), Berit Skaare na viongozi wengine wa serikali wa mkoa huo
NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiwabadilishana mawazo na wakina mama wanajitegemea 'Single mothers' baada ya kukagua sehemu ya shamba lenye hekari 651 lililonunuliwa na Taasisi ya Ilula Programu 2013 mkoani Iringa kwa ajili ya kilimo cha biashara maalum kwa ajili yao, watoto yatima na wanafunzi wenye nia ya kukuza uelewa wa kilimo kutoka katika Wilaya ya Iringa hasa wa shule za primary na awali. 
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

MAFUNZO YA MADAKTARI WA KANDA YA KASKAZINI YALIYORATIBIWA NA WCF YAMALIZIKA

$
0
0
.
Baadhi ya Madaktari na watoa huduma za afya wakionyesha stika, watakazobandika kwenye milango ya ofisi zao ili kumrahisishia mfanyakazi anayehitaji kufanyiwa huduma ya tathmini. Stika hizo zimetolewa na WCF kwa washiriki wa mafunzo ya siku tano ya kufanya tathmini ya mfanyaakzi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi yaliyomalizika Februari 23, 2018 mjini Moshi.
Katibu Tawala  Msaidizi wa Manispaa hiyo, Bw. Sebastian Masanja, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, akitoa hotuba ya kufunga mafunzo hayo
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ambao ndio waandaaji wa mafunzo hayo, Dkt. Abdulsalaam Omar, akizungumza.
Bi. Naanjela S.Msangi, Meneja tathmini ya hatari mahala pa kazi wa WCF, (mbele), akiwa na washiriki
 
Dkt. Peter Mabula kutoka Arusha Lutheran Medical Centre, akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge, akionyesha stika hizo za utambuzi wa ofisi ya mtoa huduma ya tathmini.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

KAIMU KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA MASUALA YA AFRIKA KUTOKA CANADA

$
0
0

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan M. Mwinyi akizungumza na Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kusini na Mashariki mwa Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Canada, Bw. Marc-André Fredelte. Katika mazungumzo yao walijadili masuala ya ushirikiano katika masuala ya diplomasia, biashara na maendeleo. Bw. Fredelte yupo nchini kwa ziara ya kikazi. Habari zaidi BOFYA HAPA

RC TELACK AHAMASISHA WANANCHI KUTOA TAARIFA SAHIHI UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack akielezea umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu katika Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi unaoendelea mkoani Shinyanga. Kushoto niMeneja wa Takwimu (NBS) wa  mkoa wa Shinyanga, Evarist Tairo. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Dk. Rashid Mfaume ambaye ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
.
Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, waandishi wa habari ,maafisa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, waandishi wa habari ,maafisa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu. 



MADINI YOTE NCHINI NI SHARTI YA WANUFAISHE WATANZANIA - BITEKO

$
0
0
Na Mathias Canal, Rukwa
Serikali imesema kuwa sheria mpya ya Madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 inaelekeza wazi kuwa Madini yote nchini ni Mali ya watanzania hivyo wanapaswa kutambua umuhimu wa rasilimali.
Wawekezaji na wachimbaji wote wa madini nchini wanapaswa kutambua kuwa wanalo jukumu muhimu la kurejesha kwa jamii asilimia chache ya kile wanachozalisha kwa kuunga mkono juhudi za serikali Back to the Community) katika kuboresha miundombinu, sekta ya elimu, afya N.K
Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko amesisitiza hayo Leo 23 Februari 2018 wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe Mkoani Rukwa Magharibi mwa Tanzania.
Mradi huo unaosimamiwa na kampuni ya Edenville Tanzania Ltd kwa ubia na kampuni ya Edenville Energy of Uk na Upendo Group (Kampuni ya kizawa) ilianza shughuli za majaribio ya uchimbaji na uoshaji mwezi wa kumi mwaka Jana 2017 na mkaa wa kwanza kuuzwa kwa majaribio ni mwezi Novemba mwaka 2017.
"Nataka niwajulishe tu watanzania wenzangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli aliniteua kusimamia Wizara ya Madini nikimsaidia Waziri wetu Mhe Anjelina Kairuki ili kuboresha sekta hii ya Madini hatimaye kuwanufaisha watanzania kuliko ilivyokuwa awali ambapo Madini yalikuwa yanachimbwa nchini lakini faida inaenda nchi zingine" Alisema Mhe Biteko na Kuongeza kuwa.
Wawekezaji hao wanapaswa kutoa ajira zisizo za utaalamu kwa wananchi wanaozunguka migodi yao sambamba na watanzania wote huku akiwaagiza kuwaajiri wataalamu wa Madini wa ndani ya nchi kwa kazi ambazo wanaweza kuzifanya sio kuajiri wageni.
Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018. 
Mhandisi Joseph Mwakabage Meneja Mradi wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe (Aliyenyoosha mkono) akimuonyeshaNaibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko mitambo ya uchimbaji madini  alipotembelea mgodi huo uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua eneo la uchimbaji madini ya makaa ya mawe alipotembelea mgodi wa Edenville Tanzania Ltd uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018.
Mhandisi Joseph Mwakabage Meneja Mradi wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe (Kulia) akimueleza Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko juu ya uchimbaji wa makaa ya mawe alipotembelea mgodi huo uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018. 
Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog

SERIKALI YAANZISHA MFUKO WA MAJI ILI KUWA SULUHISHO LA UPATIKANAJI WA MAJI KWENYE MAENEO MBALI MBALI YA VIJIJINI

$
0
0
MBUNGE wa jimbo la Hanang,Mkoani Manyara,Mary Michael Nagu amesema kuanzishwa kwa mfuko wa maji unaotokana na fedha zinazopatikana kwenye mauzo ya mafuta ya vyombo vya moto utakuwa sukuhisho la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwenye maeneo mengi ya vijijini.
Akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Diyagwa baada ya kupokelewa na wananchi wa Kijiji hicho waliokuwa wakipeperusha bendera ya CCM huku wakiwasilisha kilio chao cha maji,Mbunge huyo alisema moja ya changamoto inayowasumbua wananchi wa Hanang ni tatizo la huduama ya upatikanaji wa maji safi na salama.
“Tena niwaambie ni miaka na Tanzania kama kuna shida ni maji na bila maji hakuna maendeleo,sisi hapa tumshukuru mungu nilikaa huko serikalini tukasemaa bila kuunda mfuko wa maji,maji Tanzania hayatakuwa”alisisitiza Mbunge huyo.
Aidha Mbunge huyo hata hivyo aliweka bayana pia kwamba baada ya serikali kulitambua tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji  imeshaunda mfuko huo ambao fedha zake zinapatikana kwa njia ya kununua mafuta ya petroli,dizeli na mafuta ya taa kila shilingi 50 huingia kwenye mfuko huo.
Kwa mujibu wa Nagu idadi kubwa ya miradi ya maji inakwamishwa na wakandarasi wasiokuwa na uwezzo wa kifedha za kukamilisha kwa wakati kazi walizokabibidhiwa,ambapo hata hivyo alionekana kukerwa na mamlaka zenye dhamana ya kuchagua wakandarasi wa miradi hiyo kutoa kazi kwa watu wasiokuwa na sifa na uwezo kifedha za kukamilisha shughuli wanazopewa.
“Sasa jamani tukiweka watu wabovu hapo ndiyo inakuwa shida kubwa ya kukamilika kwa miradi yetu ya maji lakini sasa na kuhusu maji tumesema tuweke wakala wa maji kama wa barabara ili asimamie kama Yule wa barabara”alifafanua mwakilishi huyo wa wananchi.
Mbunge Nagu hata hivyo alibainisha kuwa mpaka sasa bado serikali haijaweka wakala wa maji,kazi ambayo itafanywa katika kikao cha Bunge lijalo ili uwepo uhakika wa upatikanaji wa huduma hiyo ya maji safi na salama.
 Wanachama wa CCM wa Kijiji cha Diyagwa wakimpokea Mbunge wa Jimbo la Hanang,Mkoani Manyara,Dk.Mary Nagu pamoja na msafara wake huku wakipeperusha bendera ya CCM kuashiria kutoridhishwa na kukosekana kwa huduma ya maji safi na salama katika Kijiji hicho.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Hanang,Methew Darema( wa pili kutoka kulia) akiwa na Katibu wa CCM wilaya ya Hanang,Teddy Athumani(wa kwanza kutoka kushoto) na katibu wa UVCCM Wilaya ya Hanang,Ole Ngotick walipowasili katika Kijiji cha Dang'aida.
 Mbunge wa jimbo la Hanang,Dk.Mary Nagu(wa kwanza kutoka kushoto) akionekana kufurahishwa na wimbo alioimbiwa na wananchi wa Kijiji cha Dang'aida kuhusu kukosekana kwa huduma ya maji safi na salama huku wakimwonyesha maji machafu wanayokunywa.
Kikundi cha akina mama wakitumbuiza kwa wimbo uliokuwa ukipeleka ujumbe kwa Mbunge wa jimbo la Hanang pamoja na serikali ya wilaya hiyo kwa ujumla kuhusu  wananchi wanavyopata shida ya kufuata maji umbali mrefu huku yakiwa machafu. Habari na picha na Jumbe Ismailly.

NAIBU WAZIRI MANYANYA MGENI RASMI KONGAMANO LA MAENDELEO YA VIWANDA

UBALOZI WA KUWAIT NCHINI TANZANIA WAADHIMISHA SIKUKUU YA KITAIFA NA UKOMBOZI

$
0
0


Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania uliandaa hafla ya kuadhimisha miaka 57 ya Uhuru wa Kuwait, miaka 27 ya Ukombozi na miaka 12 tangu Mfalme wa Kuwait Mheshimiwa Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah apokee uongozi wa nchi hiyo. 
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali wakiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Suzan Kolimba, Waziri mkuu mstaafu Dr.Salim Ahmed Salim, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid, Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally, Naibu Waziri wa Ndani Mhandisi, Hamad Masauni pamoja na viongozi wa juu wa serikali, mabalozi wa nchi za kigeni na mashirika ya kimataifa na wataalamu wa fani mbalimbali na vyombo vya habari

SIMON GROUP YACHANGIA MILIONI 25 UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU SIMIYU

$
0
0

Na Stella Kalinga, Simiyu

Kampuni ya Simon Group imechangia kiasi cha Shilingi Milioni 25 kwa ajili ya Ujenzi wa Miundombinu ya Elimu katika mkoa wa Simiyu

Akikabidhi hundi hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Simon Group, Ndg. Leonard Kitwala amesema Kampuni hiyo imetoa fedha hizo ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika maendeleo ya Sekta ya Elimu na kwa kuwa Simiyu ni mahali alipozaliwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ndg. Simon Kisena ameona ni vema asaidie maendeleo ya elimu nyumbani kwao.

Aidha, Kitwala amesema kama kampuni wameamua kuunga mkono ujenzi wa miundombinu ya Elimu Simiyu kwa kuwa wamependezwa na juhudi za Viongozi wa Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka katika kuwaletea maendeleo wananchi katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu.

Akipokea hundi ya shilingi milioni 25 kwa niaba ya Viongozi na wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka amesema anaishukuru Kampuni ya Saimon Group ambayo inaendesha mradi wa Usafrishaji wa Mabasi Dar es Salaam(UDA) kwa kuamua kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu mkoani humo.

“Nawashukuru sana SAIMON GROUP kwa kuamua kusaidia ujenzi wa miundombinu ya elimu Simiyu, shilingi milioni 25 ni fedha nyingi sana kwenye kufanikisha ujenzi wa mundombinu ya elimu hasa kwa mkoa kama wa kwetu ambao shughuli nyingi za ujenzi tunatumia “Force Account” , tunatumia nguvu za wananchi na Serikali ina nafasi yake katika ujenzi wa miradi hiyo” alisema

“ Zaidi sana namshukuru Mkurugenzi wa SIMON GROUP ndugu Robert Kisena ambaye ni mzaliwa wa Mkoa huu kwa kuona arudishe sehemu ya faida ya biashara zake nyumbani, kwa niaba ya viongozi wenzangu ninamkikishia kwamba mchango huu utaenda kwenye matokeo yanayoonekana, hata wakati wa uzinduzi wa madarasa yatakayojengwa tutaipa nafasi Kampuni ya SIMON GROUP kuja kuona alama waliyoweka katika mkoa wetu” alisisitiza Mtaka.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe.Robert Lweyo amesema mchango huo wa SIMON GROUP umekuja katika muda muafaka ambao mkoa huo una uhitaji mkubwa wa vyumba vya madarasa hivyo alimshukuru Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ndg. Robert Kisena na kuahidi pia kuwa fedha hizo zitafanya kazi iliyokusudiwa. 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akipokea hundi ya shilingi milioni 25 iliyotolewa na Kampuni ya SIMON GROUP kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu kutoka kwa Ndg.Leonald Kitwala ambaye aliyekabidhi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampun hiyo Ndg.Robert Kisena. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe.Robert Lweyo akitoa shukrani kwa Kampuni ya SIMON GROUP kupitia kwa Ndg.Leonald Kitwala aliyekabidhi hundi ya Shilingi Milioni 25 kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo picha) kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ndg.Robert Kisena, kwa ajili ya Ujenzi wa Miundombinu ya Elimu. 

UBUNIFU WA KIJANA OMARY WAMVUTIA DK.KAMALA, AAHIDI KUSAIDIA VIJANA KILIMO CHA MBOGAMBOGA NKENGE

$
0
0
Na Ripota Wetu, Misenyi

MBUNGE wa Jimbo la Nkenge mkoani Kagera Balozi ,Dk. Kamala amempongeza kijana Rosh Omary ambaye ameamua kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda kando ya mto Nkenge.

Kijana Omary wakati Rais Dk.John Magufuli akiwa kwenye ziara katika mkoa huo Novemba mwaka jana alitoa kilio chake kwa Rais kuwa kuna moja ya maofisa mifugo alifika kwenye shamba lake na kufyeka mazao yake.

Hata hivyo kijana huyo bado anaendelea na kilimo hicho baada ya Rais kutaka asisumbuliwe bali aachwe.

Hivyo Dk.Kamala ameamua kwenda kwenye shamba la kijana Omary kuona shughuli anazofanya, ambapo ametumia nafasi hiyo kumpongeza kwa jitihada zake kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda.

Dk.Kamala ameona haja ya kutembelea shamba hilo na alipofika akavutiwa na ubunifu wa kijana huyo na hivyo ameshauri ni vema vijana wakaanzisha kikundi ambacho kitajikita kwenye aina hiyo ya kilimo.Amesema yeye ameahidi kutoa vitendea kazi ikiwamo mashine za umwagiliaji.
 Sehemu ya shamba la Rosh Omary ambaye ameamua kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda kando ya mto Nkenge.
 Mbunge wa Jimbo la Nkenge mkoani Kagera Balozi ,Dkt. Kamala akikagua shamba la kijana Rosh Omary ambaye ameamua kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda kando ya mto Nkenge.
Mbunge wa Jimbo la Nkenge mkoani Kagera Balozi ,Dkt. Kamala akiungumza jambo na kijana Rosh Omary ambaye ameamua kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda kando ya mto Nkenge.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images