Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

STUDY IN RUSSIA

0
0
Grab your chance to study in one of the most Prestigious Universities in Russia with options from over 20 Universities and over 300 Specialities.
ADMISSIONS ARE NOW OPEN!

For more details contact the Country Representative for RACUS in Tanzania, Mr. Philip Benedict Nkuwi located at The Russian Centre of Science and Culture, Seaview Rd. (off Barrack Obama Drive) near Al-Muntazir Boys Primary School on Monday to Friday from 9AM to 5PM.

Mobile: +255 715 90 22 70
Email: philipbenedict88@yahoo.com
Facebook page: RACUS Tanzania
Instagram: @racus_tz

KNOWLEDGE, EXPOSURE, NEW EXPERIENCE AND NETWORKS.

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA KAMPALA NCHINI UGANDA

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza mazungumzo yao jijini Kampala nchini Uganda. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza mazungumzo yao jijini Kampala nchini Uganda. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya mazungumzo yao Kampala nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kupiga picha ya pamoja na Mawaziri pande zote mbili za Kenya na Tan
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir kabla ya mazungumzo yao jijini Kampala.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Kampala Uganda-PICHA NA IKULU

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

JESHI LA POLISI KITENGO CHA POLISI JAMII KWA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA CRDB WAFANYA ZIARA YA MIKOA YA LINDI NA MTWARA

0
0
 Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi ambaye ndiye Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii, DCP Ahmada. A. Khamis (wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja  Maafisa wa benki ya CRDB na viongozi wa serikali ya Kata ya Kitangari, Tarafa ya Kitangari wilaya ya Newala mkoani Mtwara  leo baada ya kufanya mkutano katika Kata hiyo kwa kushirikiana na Bank ya CRDB kutoka Makao Makuu ya Bank hiyo Dar es salaam, juu ya Mtumizi salama ya huduma za kibenki na namna ya kuepukana na wizi wa mtandao. Picha na jeshi la Polisi 
 Afisa kutoka benki ya CRDB makao Makuu Dar es salaam, Abel Laswai akitoa elimu kwa wananchi wa Newala Mjini leo juu ya matumizi salama ya huduma za kibenki katika uhifadhi wa pesa na namna ya kuondokana na wizi wa fedha kwa njia ya mtandao, elimu hiyo ilitolewa katika viwanja vya mahakama ya Mwanzo iliyopo mjini hapo. Picha na Jeshi la Polisi.
Inspekta Issa Asali kutoka katika kitengo cha Polisi Jamii akizungumza na wananchi wa Newala Mjini leo katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Mahakama ya Mwanzo iliyopo mjini hapo, juu ya matumizi salama ya huduma za kibank na namna kuondokana na uhalifu kwa njia ya mtandao. Picha na Jeshi la Polisi 

JAMII YAASWA KULIANGALIA KWA UZITO SUALA LA NAFASI YA MWANAMKE KATIKA UONGOZI

0
0
Na Anil Ricco, Globu ya Jamii
Jamii ya Kitanzania imeaswa kuliangalia kinaga ubaga suala la nafasi ya uongozi katika jamii kwa kulijadili suala hilo mara kwa mara.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Wanachama wa Mtandao wa Wanawake na Katiba wameomba  Sheria ya Vyama vya Siasa itungwe katika uwiano wa kijinsia ili kuwapa nafasi katika Uongozi.

Mjumbe wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), Bi. Leticia Mkulasi amesema kuwa sio vizuri kujadili suala hilo mpaka zinaposimama Chaguzi, bali kuna umuhimu wakuhamasisha jamii mara kwa mara.

Pia amesema anaamini Waandishi wa Habari wanaweza kutoa taarifa zitakazo elimisha jamii juu ya nafasi ya Mwanamke katika Uongozi na masuala ya kisiasa kwa ujumla.

Naye Mwanachama wa Mtandao wa ULINGO, Bi. Maria Kigalu amesema Msajili wa Vyama vya Siasa yuko katika mchakato wakuchakata Sheria mpya ya Vyama vya Siasa, hivyo anaamini itasaidia Wanawake kupata nafasi ya uongozi wa siasa.

Amesema Mchakato wa mwaka huu wa Sheria ya Vyama vya Siasa utakaojadiliwa Bungeni utakuwa tofauti na mchakato wa mwaka 2013 ambao haukufanyiwa kazi kipengele cha nafasi ya Mwanamke katika Uongozi.
Mmoja wa Watoa Maada katika Mkutano huo, Dkt. Dina Mbaga akielekeza jambo kwa baadhi ya Waandishi wa Habari na Wanachama wa Mitandao mbalimbali waliohudhulia Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mwanachama wa Woman Fund Tanzania (WFT), Bi. Leticia Mkulasi akitoa mada kwa Waandishi wa Habari na baadhi ya Wanachama wa Mitandao mbalimbali ya Wanawake nchini kuhusiana na Suala la nafasi ya Mwanamke katika Uongozi.

OPARESHENI ZA KUZUIA UHALIFU ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA

0
0
Na Lydia Churi-Mahakama ya Tanzania
Viongozi wanaohusika na Oparesheni za kuzuia uhalifu wameshauriwa kufuata na kuzingatia sheria inayoongoza namna ya ukusanyaji wa ushahidi ili kuepuka kuharibu ushahidi kabla haujawasilishwa Mahakamani na kupelekea kesi nyingi kuharibika kwa kukosa ushahidi au Mahakama kushindwa kutoa hukumu zinazoendana na kosa husika.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Uyui alipomtembelea Mkuu wa wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake inayoendelea Mahakama Kuu kanda ya Tabora. 
 Akitolea mfano wa Oparesheni za uteketezaji wa dawa za kulevya yakiwemo mashamba ya bangi, Jaji Mkuu amesema ushahidi kuteketezwa bila ya kufuata utaratibu huathiri mienendo ya kesi Mahakamani.
Akizungumzia suala la Maadili ndani ya Mahakama, Jaji Mkuu amewaomba Wakuu wa mikoa pamoja na Wakuu wa wilaya ambao anawatambua kama walezi wa Mahakama kushirikiana kwa karibu zaidi na Mahakama ili kuhakikisha wanawahudumia wananchi ipasavyo katika suala zima la utoaji wa Haki.
 Kuhusu kusogeza huduma za kimahakama karibu Zaidi na wananchi, Jaji Mkuu amesema Mahakama kwa kushirikiana na Benki ya Dunia inao Mpango wa kuanzisha Mahakama zinazotembea (Mobile Courts) ili kuwafikia wananchi walio mbali na huduma za kimahakama hasa katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora 
 Naye Mkuu wa wilaya ya Tabora na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Uyui, Queen Mlozi   alimweleza Jaji Mkuu kuwa kwa namna wilaya ya Uyui ilivyokaa kijiografia, wananchi hulazimika kufuata huduma za kimahakama umbali wa Zaidi ya kilometa 150 katoka Loya kwenda Kigwa mkoani Tabora.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI KIGWANGALLA AFUNGUA KIKAO CHA WAKUU WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUJADILI KANUNI ZA UANZISHWAJI WA JESHI USU

0
0
  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (aliyesimama), akifungua kikao cha Wakuu wa Vyombo ya Ulinzi na Usalama cha kujadili kanuni za kuanzishwa kwa Jeshi Usu la Uhifadhi wa Wanyama Pori na Misitu Nchini, kilichofanyika leo TANAPA Makao Makuu mkoani Arusha. Picha na Jeshi la Polisi.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (aliyesimama), akitoa hotuba ya ufunguzi mbele ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Venance Mabeyo (Katikati) na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, na wajumbe wengine (hawapo pichani)  kwenye kikao cha kujadili kanuni za kuanzishwa kwa Jeshi Usu la Uhifadhi wa Wanyama Pori na Misitu nchini, kilichofanyika leo TANAPA Makao Makuu mkoani Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla, akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama baada ya kumaliza kikao cha ufunguzi wa kujadili kanuni za kuanzishwa kwa Jeshi Usu la Uhifadhi wa wanyama pori na misitu nchini, kilichofanyika leo TANAPA Makao Makuu mkoani Arusha. Picha na Jeshi la Polisi.

RAIS DKT.MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA RAIS WA BURUNDI, AKUTANA NA MRATIBU WA MAZUNGUMZO YA AMANI YA BURUNDI

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa ambaye ni mratibu wa Mazungumzo ya amani ya Burundi, Kampala nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mratibu wa mazungumzo ya amani ya Burundi Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa, Kampala nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Burundi Gaston Sindimwo kabla ya mazungumzo yao Kampala nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Burundi Gaston Sindimwo, Kampala nchini Uganda.
Makamu wa Rais wa Burundi Gaston Sindimwo akizungumza mara baada ya kikao chake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Kampala nchini Uganda. PICHA NA IKULU

UKAGUZI WA MAGARI MADOGO KUANZA MACHI, WAENDESHA BODABODA KUFUNGIWA KAMERA

0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya Jamii.

BARAZA la Taifa la usalama barabarani  limetangaza kuanza kwa ukaguzi wa magari madogo ya binafsi nchini nzima kuanzia Machi moja mwaka huu, huku likieleza kuwa linatafuta mfadhili atakayesaidia kufunga kamera kwenye baadhi ya makutano ya barabara ili kuwakamata bodaboda watakaofanya makosa.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es saalam na mwenyekiti wa baraza hilo Mhandisi Hamad Masauni ambaye pia ni Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi wakati akielezea tathimini ya utekelezaji wa  mpango mkakati wa kudhibiti ajali za barabarani ambapo inaonesha ajali zimepungua. Akizungumzia kuhusu waendesha bodaboda amesema, baadhi yao wamekuwa wakikiuka sheria za usalama barabarani kwa kufanya makosa mbalimbali na baadhi ya makosa hayo ni kupita katika taa nyekundu, kutovaa kofia ngumu na kubeba abiria zaidi ya mmoja.

Hivyo amesema baraza limepanga kutoa elimu maalumu itakayosaidia kupunguza ajali na kuhakikisha wanaovunja sheria wanachukuliwa hatua.“Hatua hizo zitasaidia kuwajengea uelewa wa usalama barabarani watumiaji wa barabara na madereva wataogopa kufanya makosa barabarani na hivyo na kuwa na utii wa sheria bila shuruti.”

Pia amesema wamebaini kuwa, pikipiki nyingi zimesajiliwa kwa majina ya kampuni zinazouza pikipiki badala ya majina ya wamiliki wa pikipiki hizo kitendo ambacho ni kinyume na sheria na kimekua kikisababisha usumbufu katika ukamataji wa bodaboda.Hivyo, Masauni amesema pikipiki ambazo zitakamatwa na kubainika zimesajiliwa kwa majina ya kampuni badala ya jina la mmiliki wenye kampuni hizo watakamatwa na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Kuhusu wa magari madogo, Masauni amesema awamu ya pili ya mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani wamefanikiwa kukagua magari makubwa, magari ya abiria, magari ya mizigo na magari yanayobeba wanafunzi ambapo wamefanikiwa kufanya ukaguzi huo kwa asilimia 79.

Amesema hivyo awamu ya tatu ni kwa magari madogo ambapo amehimiza wenye magari kufanya ukaguzi huo ambao utafanyika kwa kipindi cha miezi miwili na baada ya hapo ambao watakabainika kutokuwa na stika zinazoonesha kutokaguliwa kwa magari yao watachukuliwa hatua.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani , Fortunas Musilimu amesema kuwa watu wote wenye magari kuhakikisha magari yao yanakaguliwa katika maeneo maalumu na kueleza wamekuwa makini kwa kuhakikisha gari inayobandikwa stika ni ile ambayo itakuwa imekaguliwa na si vinginevyo.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari(hawapo pichani), ambapo alitangaza kuanza rasmi kwa zoezi la ukaguzi wa magari binafsi mwanzoni mwa mwezi ujao.Wengine ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, SACP Fortunatus Musilimu na Mjumbe wa baraza hilo,Henry Bantu(kushoto).Mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, SACP Fortunatus Musilimu, akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari (hawapo pichani), ambapo ilitangazwa operesheni ya ukaguzi wa magari binafsi unaotarajiwa kuanza mwezi machi mwanzoni.Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, Mkutano huo umefanyika leo latika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Henry Bantu, akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari (hawapo pichani), ambapo ilitangazwa operesheni ya ukaguzi wa magari binafsi unaotarajiwa kuanza mwezi machi mwanzoni.Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, SACP Fortunatus Musilimu(kulia). Mkutano huo umefanyika leo latika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA),Geoffrey Silanda, akijibu baadhi ya maswali yaliyoelekezwa kwake wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari(hawapo pichani).Mkutano huo umefanyika leo latika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

ALICHOKISEMA WAZIRI MWAKYEMBE KWA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS- JAMHURI YA POLAND

CHEKA KUZICHAPA NA MFILIPINO-MTWARA

0
0
Bondia wa Kimataifa Francis Cheka anatarajia kupigana na Bondia Arney Tinampay Kutoka Nchini Ufilipino katika Pambano la raundi 10 litakalofanyika katika Uwanja wa Umoja Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara mwanzoni mwa mwezi wa Nne.

Kwa mara ya Kwanza Bondia Franciss Cheka anapigana Mchezo wa Kimataifa wa Kutetea Ubingwa wa Mkanda wa UBO wa kilogram76 katika Mkoa wa Mtwara,ambapo tayari ameanza Kufanya maandalizi ya Mazoezi tayari kwa Pambano hilo.AKiongea na waandishi wa habari Promota Jay Msangi anasema Bondia Kutoa Ufilipino anatoka katika Historia ya mabondia wakubwa.

“Bondia huyu anahistoria anatokea katika kambi ya Man Pacquiao na anayemfundisha  aliwah pia kumfundisha Pacquiao na ni Bondia mwenye kushika daraja la pili katika Nchi ya Ufilipino kenye uzito wa Kilogram 76 na hivyo unaweza kuona kwa Francis Cheka anakutana na Bondia Mwenye uwezo mkubwa”alisema Promota Jay Msangi.

Naye Fransis Cheka anasema anajiamini licha ya kuwa hamfahamu Bondia huyo Kutoka Ufilipino lakini uwezo wake ni mkubwa kupigana na bondia yeyote wa kiwango chake.

“Sifahamu Uwezo wa Mfilipino lakini najifahamu uwezo wangu kwa sababu nimeshakuwa Bingwa wa Dunia na hivyo nawahakikishia Watanzania hususani wakazi wa mkoa wa Mtwara nitafanya vizuri,Simfahamu huyo Bondia lakini nitakapokutana naye Ulingoni tutafahamiana Hapo Hapo”Alisema ChekaCheka.

Wakati huo huo Bondia Francis Cheka amekabidhiwa Ubalozi wa Kuitangaza Eneo la Mikindani ambalo lina majengo ya Kihistoria. 
 Mzee Mohammed Kidume Akimsimika Ubalozi wa Mikindani Bondia Francis Cheka katikati kwa lengo la Kutangaza historia ya Majengo ya Kale ambayo yalitumiwa na Wakoloni.
Bondia Francis Cheka akiwa na wazee wa Mikindani Mara baada ya kukabidhiwa Ubalozi wa kutangaza Hotel ya Old Boma Iliyopo Mkoani Mtwara.

CDMT YABORESHA MIUNDOMBINU YA CHOO HANDENI

0
0
 Uongozi wa Halmashauri ya Wilayaya Handeni umekabidhiwa rasmi mradi wa choo cha matundu sita kilichojengwa na shirika lisilo la Kiserikali CDMT(Community Development Mission of Tanzania) lenye thamani ya Milioni 19 za Kitanzania  kwa lengo la kuboresha huduma ya vyoo kwa wanafunzi wa shule za Msingi. 
 Akipokea mradi huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Aweso Bakari ( Afisa Tarafa Mkumburu) alisema kuwa anashukuru sana CDMT kwa kuona uhitaji wa Shule ya Masatu na kuamua kusaidia ujenzi wa choo chenye  matundu 6 yatakayosaidia kupunguza changamoto ya vyoo shuleni hapo.

Kaimu Mkurugenzi alisema kuwa, Shule ya Masatu kwa mujibu wa ripoti ya Mwalimu Mkuu ilikuwa na upungufu wa matundu 29 ya vyoo, Hivyo kwa mradi wa matundu 6 yaliyojengwa na Shirika la CDMT umepunguza na kufikia matundu 23, hivyo  anashukuru Shirika hilo  kwa jitihada za kuunga Mkono Serikali katika ujenzi wa miundombinu.
 Aidha aliwataka viongozi wa shule na Kijiji kuhakikisha wanatunza mradi huo kwa kuzingatia usafi wa mazingira ili hata waliofadhili mradi huo wakija kuutazama wafarijike na waweze kuisaidia Serikali kutatua changamoto nyingine ambazo bado zinaikabili shule hiyo.

“Naishukuru sana CDMT, Viongozi wa shule na Kijiji msimamie mradi huu vizuri kuhakikisha hauharibiwi kwa michoro ya ajabu na usafi uzingatiwe ili hata wafadhili wakija kutembelea waone thamani yake” alisema Aweso
 Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Segera Mh. Yassin Mtamike alisema kuwa, anaishukuru CDMT na yeye kama Diwani atahakikisha mradi huo unatunzwa na kulindwa ili kuwapa nafasi wafadhili waweze kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali za miundombinu.
 Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali CDMT(Community Development Mission of Tanzania) na Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Emile Philipo alisema kuwa baada ya kufika Handeni aligundua changamoto ya vyoo bora kwa Shule za Msingi na kuamua kuandika andiko la kuomba msaada kwa Serikali ya Marekani yenye fungu la fedha la Rais wa Marekani linalosaidia Afrika kwa lengo la kupunguza changamoto ya vyoo.
 Aliongeza kuwa kwa tafiti zake  za awali aliamua kusaidia shule tatu za msingi ambapo shule  mbili za Msomera na Masatu zipo Hamashauri ya Wilaya ya Handeni na shule moja  1 ya Seuta Halmashauri ya Mji Handeni.

Miradi yote imekamilika kwa jumla ya Milioni 58 za Kitanzania ambapo kila shule imejengewa matundu 6 ikiwa matundu 3 kwa  wanafunzi wa kike na 3 kwa wanafunzi wa kiume.

DK. KIGWANGALLA AAGIZA MBINU MPYA ITUMIKE KUDHIBITI WANAOCHIMBA MADINI KWENYE CHANZO CHA MAJI YA MTO ZIGI JIJINI TANGA

0
0

Na Hamza Temba, WMU, Muheza Tanga
..........................................................................

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo la chanzo cha maji ya mto zigi kilichopo ndani ya Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani kwa ajili ya kulinda chanzo hicho.


Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari  baada ya kutembelea eneo la chanzo hicho na kukuta uharibifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya wananchi wanaodaiwa kuchimba madini ya dhahabu katika eneo hilo la hifadhi kinyume cha sheria


"Nimeagiza watu wa TFS wajenge kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo hili, na waweke walinzi wetu wa kudumu hapa badala ya kutegemea kufanya patrol (doria) na kuondoka, kwasababu eneo hili wananchi wanaamini lina madini ya dhahabu kwahivo kila siku wataendelea kuja kujaribu kuvuna dhahabu kutoka hapa.


"Kwasababu sisi kazi yetu ni kuhifadhi Maliasili ambayo tumepata kama urithi wa nchi yetu, niwahakikishie kwamba tutaimarisha ulinzi kwa kuanzisha kituo cha ulinzi hapa ili askari wawe wanabadilishana na kudhibiti kabisa uharibu ambao umekuwa ukifanyika, kwasababu maji yanayotoka katika chanzo hiki yanakwenda kunywesha Muheza yenyewe na wilaya wa Tanga, tukiharibu hapa yatakosekana maji safi na salama"  alisema Dk. Kigwangalla.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea zawadi ya pambo la vipepeo kutoka kwa mmoja wa wafugaji Asina Athumani muda mfupi baada ya kukagua shamba la vipepeo katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana ambapo aliwataka wafugaji hao kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa kuandaa maonesho maalum ya kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya shamba la vipepeo katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana ambapo aliwataka wafugaji hao kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa kuandaa maonesho maalum ya kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani tofauti na hivi sasa wanapotegemea soko la kuuza nje ya nchi. Kulia ni Mbunge wa Muheza, Balozi Adadi Rajabu. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho jana Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho jana Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KAMANDA MUSLIMU AZUNGUMZIA BODABODA KUPIGWA BARABARANI

0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii. 

KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslimu amesema hakuna sheria inayoruhusu askari polisi kupiga wanaotumia vyombo vya usafiri barabarani wakiwamo waendesha bodaboda huku akielezea kuwa atafuatilia ili kubaini iwapo kuna askari wenye tabia ya kupiga waendesha bodaboda. 

Muslimu ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akielezea mafanikio yaliyopatikana kwenye kupunguza ajali za barabarani ambapo Baraza la Taifa la Usalama Barabarani limetoa tathmini ya mpango mkakati wa awamu ya kwanza na awamu ya pili unaonesha ajali za barabarani zimepungua kwa kiasi kikubwa nchini. 

Hivyo ameelezea pia umuhimu wa watumiaji wa barabara wakiwamo waendesha pikipiki maarufu bodaboda kuzingatia sheria za usalama na kuelezea kuwa wanapaswa kufuata sheria bila shuruti. Hata hivyo waandishi wa habari waliokuwa kwenye mkutano huo walitaka kufahamu ni kwanini baadhi ya askari polisi hasa maeneo ya makutano ya Tazara, Ubungo, Mwenye na Daraja la Salenda wamekuwa wakiwapiga waendesha bodaboda na kusababisha hali ya sintofahamu. 

MAHAKAMA YAMSOMEA MAELEZO YA AWALI TIDO MHANDO ANAYEKABILIWA NA MASHTAKA MATANO

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii. 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema, Aprili 28 mwaka huu, itamsomea maelezo ya awali aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji uTanzania (TBC), Tido Mhando (Pichani), anayekabiliwa na mashtaka matano. 

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Tido, Ramadhani Maleta kuiomba Mahakama iwapatie muda wa kupitia maelezo ya awali ili aweze kushauriana na mteja wake kabla ya kusomwa. 

Kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya mshtakiwa Mhando kusomewa maelezo ya awali ambapo mwendesha mashtaka wa Takukuru, Leonard Swai alidai wako tayari kumsomea. Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo na wakili Maleta aliomba apewe muda kwa sababu alipatiwa maelezo hayo ya awali na upande wa mashtaka wakati wakiwa mahakamani hapo. 

Swai alipinga hoja hiyo na kudai kwa utaratibu wanapaswa kumsomea mshtakiwa maelezo hayo ya awali na Mahakama imuulize kipi anakubali na kipi anachokikataa na kwamba wanaweza kupitia kwa dakika tano. 
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando (Pichani), anayekabiliwa na mashtaka matano akiwa katika chumba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa kesi yake. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DC Mtanda Kuanzisha Wangabo Cup kupongeza juhudi za Wana Kirando.

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda kuandaa tamasha la michezo ili kuwapongeza wananchi wa Kata ya Kirando kwa kujitokeza kwa wingi katika songambele ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Kirando pamoja na ujenzi wa madarasa manne katika Shule ya Sekondari Kirando.

Ameyasema hayo baada ya kuona umati wa wananchi wa kata hiyo ulipojitokeza wake kwa waume kushambulia ujenzi wa msingi wa kituo cha afya cha kirando, ujenzi ambao unatarajiwa kumalizika baada ya miezi mitatu ukihusisha majengo manne ya maabara, mochwari, jengo la wazazi pamoja na wodi ya kinamama.

“Wanakirando Mmekuwa na mshikamano bila ya kujali Vyama vyenu na itikadi zenu…ninyi mnaongoza kwa kujitokeza katika songambele kuliko mahali kwengine popote, Mh. DC nakutaka unazishe tamasha la michezo ili kupongeza kwa hiki kilichotendeka hapa.” Rc Wanagbo alisema.

Pamoja na hayo Mh. Wangabo aliahidi kutoa mipira ya miguu Minne, ya Netball miwili pamoja na Vikombe viwili vya mashindano hayo.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda baada ya kupokea maelekezo hayo alianzisha harambee kwaajili ya kuanzisha mashindano hayo na hatiame madiwani, na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya Nkasi walichanga fedha na vifaa mbalimbali ili kufanikisha tamasha hilo ambalo Mkuu wa Wilaya alilipa jina la Wangabo Cup.  
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda (jezi ya Njano) akiongea na baadhi ya wananchi waliojitokeza kushiriki Songambele ya Upanuzi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Kirando iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa kwanza Kushoto).

TBA WATUNISHIANA MISULI NA HALMASHAURI YA NYASA

0
0
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) waikatalia halmashauri ya wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma kukatisha mkataba wa ujenzi wa ofisi za halmashauri hiyo,Hii ni baada ya Baraza la madiwani la halmashauri hiyo kukubaliana kwa pamoja na kustisha mkataba. Wasema kama halmashauri itasitisha mkataba itabidi halmashauri iwalipe fidia TBA.

POLAND KUFUNGUA OFISI ZA UBALOZI WAKE NCHINI TANZANIA

0
0
Na Ismail Ngayonga.

SERIKALI ya Jamhuri ya Poland mapema mwezi April mwaka huu inatarajia kufungua upya Ofisi za Ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini ambazo zilifungwa kwa muda, hatua inalenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya Mataifa hayo.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa (Februari 23, 2018) Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipokuwa Salamu za Rais wa Poland kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Dkt. Mwakyembe alisema hatua zote muhimu za ufunguzi wa Ubalozi huo, taratibu zote muhimu kwa ajili ya ufunguzi Ofisi za Ubalozi huo tayari zimekamilika na kuongeza kuwa kufunguliwa kwa ubalozi kutazidi kudumisha ushirikiano na urafiki wa muda mrefu baina ya Tanzania na Poland pamoja na kuimarisha diplomasia ya uchumi baina ya mataifa hayo.

 “Serikali ya Jamhuri ya Poland imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na Tanzania, ambapo matunda ya ushirikiano ni kwa Serikali yetu kupata wa mkopo wa masharti nafuu uliofanikisha uanzishaji wa kiwanda kikubwa cha matrekta kibaha Mkoani Pwani” alisema Dkt. Mwakyekmbe.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Poland Mhe. Krzysztof Szczerski  wakati alipoleta salamu za Rais wa Poland na mwaliko kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokea salamu za Rais wa Poland na mwaliko kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli toka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Poland Mh.Krzysztof Szczerski.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Poland Mh.Krzysztof Szczerski (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe mara baada ya kukabidhi  salamu za Rais wa Poland na mwaliko kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI KAMWELWE AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UHOLANZI

0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe akimkaribisha ofisini mgeni wake, Balozi wa Uholanzi nchini, Jeroen Verheul mara baada ya kuwasili. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Uholanzi nchini, Jeroen Verheul. Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe amekutana na Balozi wa Uholanzi nchini, Jeroen Verheul na kufanya nae mazungumzo kuhusu mpango wa kukamilisha mradi wa maji wa kitaifa wa Handeni (HTM) uliopo katika wilaya za Handeni na Korogwe, mkoani Tanga. 

Mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye ofisi za wizara za Ubungo Maji, Jijini Dar es Salaam, yalilenga katika kutatua changamoto za mradi huo ili uweze kukamilika na kutoa huduma kwa ufanisi kwa wakazi ambao kwa sasa wamefikia 300,000 kulinganisha na 180,000 kama lengo la awali katika vijiji 79 vya wilaya za Handeni na Korogwe. 

Katika kikao hicho Waziri Kamwelwe na Balozi Verheul walikubaliana hatua za haraka zichukuliwe kwa lengo la kuondoa vikwazo vyote na kutekeleza mpango huo mara moja.

AZAM FC, KMC KUSHUKA DIMBANI KESHO

0
0
Na Agness Francis Globu ya jamii 

 MABINGWA wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, wanaendelea vizuri kufanya mazoezi kuelekea mchezo ujao wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) dhidi ya KMC iliyopanda daraja. 

 Katika msimu huu kikosi hicho kimefanikiwa kufika tena hatua ya 16 bora ambapo watashuka katika dimba la Uwanja wa Azam Complex wakiwa wageni dhidi ya timu hiyo siku ya kesho saa moja usiku. Ambapo kikosi hicho kina historia ya kufika mara mbili hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) kwa misimu miwili iliyopita tangu michuano hiyo iliporudishwa tena mwaka 2015. 

 Msimu wa 2015/2016 wakati kikosi hicho kikifika hatua ya fainali na kufungwa na Yanga mabao 3-1, Azam FC ilikutana na Panone ya mjini Moshi kwenye hatua ya 16 bora katika mechi ngumu iliyofanyika Uwanja wa Ushirika, ambapo matajiri hao walitoka nyuma kwa bao moja na kushinda 2-1, mabao yaliyofungwa na wachezaji wa zamani wa timu hiyo, beki Pascal Wawa na mshambuliaji Allan Wanga. 

 Azam FC iliyoishia hatua ya nusu fainali msimu uliopita baada ya kufungwa na Simba bao 1-0, ilifuzu hatua ya robo fainali baada ya kuitoa Mtibwa Sugar kwa kuipa kipigo cha 1-0, kwenye hatua ya 16 bora mchezo ulipofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, bao likifungwa na winga Ramadhan Singano 'Messi'.

MABULA ASHANGAZWA UTATA KATIKA UMILIKI WA HATI ZA ARDHI

0
0
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi mhe. Angelina Mabula ameshangazwa na uwepo wa majalada ya ardhi katika halmashauri za Butiama na Musoma ambayo wamiliki wake hawafahamiki na majalada hayo kujulikana kama ‘’ndugu mhusika’’.

Akiwa katika ziara yake ya siku tatu ya kushughulikia migogoro ya ardhi pamoja na kukagua mfumo wa ulipaji kodi ya ardhi mkoani Mara mhe. Mabula alisema majalada hayo yamekuwa na matatizo ya viwango vya kulipa kodi kwa kuwa yanaonekana kuwa deni huku mmiliki akitaka kumilikishwa upya kwa gharama ndogo.

Kufuatia mkanganyiko huo, naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi aliyakabidhi majalada yenye utata kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kwa uchunguzi zaidi ili kubaini kama suala hilo limefanyika kimakosa ama ni kwa makusudi.‘’Mtu anamilikishwa leo kwa pesa ndogo sana halafu za huko nyuma zinapotea hapa kuna mchezo unafanyika kupunguza mapato ya serikali’’ alisema Mabula.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akizungumza na watumishi wa halmashauri za Mji na Wilaya ya musoma mkoa wa Mara.
Baadhi ya watumishi wa kanda wa Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi wakimsikiliza Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula wakati wa ziara yake mkoani Mara.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dk. Vicent Anney Naano akizungumza wakati wa ziara ya naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi mkoani mara.

Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images