Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

RC INJINIA NDIKILO ATAKA KILUVYA UNITED WAIFUNGE RUVU SHOOTING JUMAMOSI

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Pwani Inginia Everist Ndikilo leo ametoa hamasa kwa kuichangia  timu ya Kiluvya United  kiasi cha  Sh. Mil.2.2 ikiwa kwa ajili ya kuweka kambi  kuelekea mechi yao na Ruvu Shooting  itakayopigwa Desemba 30 mwaka huu katika uwanja wa Filbert Bayi uliopo Mkuza  Kibaha Mkoani Pwani ambapo timu hizo zitakutana katika kuwania kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Injinia Ndikilo amewataka wachezaji wa timu ya Kiluvya United kucheza kufa na kupona ili iweze kupanda daraja na kuleta sifa katika mkoa wa Pwani

Injia ndikilo amesema hayo alipozungumza na wachezaji hao ofisini kwake  Kibaha Mkoani Pwani huku akiwasisitiza kuibuka na ushindi kwenye mechi hiyo.

Katika  hamasa  hiyo Mheshimiwa  Ndikilo ametoa Sh. Mil. 2.2  kwa timu hiyo  inayocheza Ligi  Daraja la Kwanza ambayo inawania kupanda  nankuweza kuingia kwenye  mzunguko wa Ligi Kuu Bara katika msimu ujao.

Kiluvya United itashuka dimbani  kukipiga na timu ya Ruvu Shooting  Desemba  30 mwaka huu katika uwanja wa Filbert Bayi  uliopo maeneo ya Mkuza Kibaha Mkoani Pwani.

MAGAZETI YA ALHAMIS LEO DECEMBER 28,2017

TANGAZO LA MNUSO WA KUFUNGA MWAKA WA JUMUIYA YA WATANZANIA LEICESTER

KAMANDA WA POLISI MKOA WA SINGIDA ASHIRIKI IBADA MAALUM YA KULIOMBEA TAIFA ILIYOANDALIWA NA UMOJA WA MAKANISA MKOA WA SINGIDA

$
0
0
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Deborah Magiligimba akizungumza na waumini wa Kikristo(hawapo pichani) kwenye ibada maalum ya kuliombea Taifa iliyoandaliwa na Umoja wa Makanisa Mkoa wa Singida  jana.
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Deborah Magiligimba( wa tano kulia) akifuatilia kwa makini mahubiri wakati wa Ibada maalum ya kuliombea Taifa iliyoandaliwa na Umoja wa Makanisa Mkoa wa Singida jana  wengine pichani ni viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo  Mkoa wa Singida.
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Deborah Magiligimba akizungumza na waumini wa Kikristo kwenye ibada maalum ya kuliombea Taifa iliyoandaliwa na Umoja wa Makanisa Mkoa wa Singida  jana ambapo alisisitiza umuhimu wa wananchi kutii Sheria za nchi bila shuruti.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Deborah Magiligimba akizungumza na waandishi wa habari namna Jeshi la Polisi lilivyojipanga kuimarisha ulinzi katika nyumba za ibada na kumbi za starehe katika kipindi hiki cha sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya.

UKWELI KUHUSU KUTOFANYIKA KWA FAINALI ZA ‘MISS TANZANIA 2017’

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limekua likifuatilia kwa umakini mwenendo wa shindano la Miss Tanzania na waandaji wake kampuni ya LINO Agency katika kuhakikisha taratibu, kanuni na miongozo ya kuendesha matukio ya Sanaa nchini inazingatiwa.

Hivi karibuni LINO wametoa taarifa ya kutokufanyika kwa shindano Miss Tanzania kwa mwaka 2017 ambapo pamoja na sababu ya kukosa wadhamini wametaja kucheleweshewa kibali na BASATA kama sababu ya kutokufanyika kwa shindano hili kwa msimu wa mwaka 2017.

Tunapenda kueleza kwamba sababu inayotolewa na LINO kwamba walicheleweshewa kibali na BASATA si ya kweli na pengine imetengenezwa kuficha uhalisia wa changamoto za shindano hili ambazo mara zote BASATA na hivi karibuni Waziri mwenye dhamana na sekta ya Sanaa Mh. Dkt Harrison Mwakyembe amezieleza na kuzitolea maagizo.

BASATA kama mtoa vibali vya matukio ya Sanaa nchini limeshangazwa na taarifa ya kutokuwepio kwa shindano kwa msimu huu maana tayari lilikwishatoa kibali cha muda kwa kampuni ya LINO ili kufanya maandalizi ya awali ya shindano hili sambamba na kuandaa mshiriki wa shinda la Miss World 2017 lililomalizika hivi karibuni mji wa Sanya nchini China amabapo Tanzania tuliwakilishwa na mshiriki Julitha Kabete aliyekabidhiwa bendera chini ya uangalizi wa Wizara na BASATA.

Kibali hicho cha muda ambacho kilitolewa mapema tarehe 08/09/2017 kinatoa fursa kwa mwandaaji wa tukio la Sanaa kufanya maandalizi yote ya awali ya tukio la Sanaa/Burudani huku akiwa chini ya uangalizi maalum wa kukamilisha taratibu mbalimbali za msingi kwa ajili ya kupewa kibali cha mwisho cha tukio husika hivyo kampuni ya LINO haina sababu yoyote ya kutaja kibali cha BASATA kama kikwazo cha kufanyika kwa shindano la Miss Tanzania mwaka huu maana tayari walikua na kibali hiki cha muda kinachowapa fursa za maandalizi yote ya awali ya shindano

Tunazidi kutoa wito kwa waandaaji wote wa mashindano/matukio ya Sanaa kuzidisha weledi na zaidi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kuendesha matukio ya Sanaa kama zinavyo fafanuliwa katika vikao vya mashauri mara kwa mara. Aidha tunazidi kusisitiza umuhimu wa kujenga taswira chanya kwa matukio ya Sanaa na kuyajengea uendelevu ili kuvutia wawekezaji zaidi na kuyapa mvuto mkubwa wa kibiashara.

BASATA kama msajili na mtoa leseni katika matukio ya Sanaa tutaendelea kuzingatia weledi na kutoa huduma zetu kwa haraka, ubora na kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji matukio ya Sanaa ambazo kwa pamoja wadau wote tumeziridhia.


KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA SANAA LA TAIFA – BASATA

Hatuna tatizo la dawa nchi nzima-Dkt. Ndugulile

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii

Serikali imesema kuwa hakuna tatizo la dawa katika sehemu kutoa huduma za afya katika Hospitali, Vituo vya Afya , Dispensari pamoja na Zahanati.

Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mkanoge Kata ya Nyamato Wilayani Mkuranga.

Dk.Ndugulile amesema kuwa kutokana na kuongezeka kwa bajeti ya Wizara ya afya kumefanya Wizara kujipanga katika kuhakikisha wananchi wanapata dawa pale wanapokwenda kupata huduma za afya katika hospitali vituo vya afya, Zahanati pamoja na Dispensari.

Amesema kuwa licha na jitihada hizo serikali inakuja mpango wa kila mwananchi kuwa na bima ya afya na ni lazima na sio hiari.Dk.Ndugulile katika uzinduzi wa zahanati hiyo ameahidi kuwapelekea jokofu la kuhifadhi dawa za chanjo ili kuwapunguzia wananchi wa kufuata chanjo mbali.

Amesema Tanzania ni nchi inayoongoza katika utoaji wa chanjo duniani kwa asilimia 97.Dkt.Ndugulile ameahidi kutoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili Ujenzi wa nyumba ya Mkunga katika zahanati ya Mkanoge.

Nae Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambae ni Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa jitihada za kuboresha huduma za jamii ni endelevu katika Wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Faustine Ndugulile kwa kushirikiana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga wakizindua Zahanati ya Mkanonge.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii Pwani.

Mkazi wa Kijiji cha Makanonge, Themed Mkale akimkabidhi Zawadi ya Mhogo,pamoja na Mpunga Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , Dk. Faustine Ndugulile.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi wa mkanoge wakati uzinduzi wa zahanati.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza juu ya harakati zilizofanyika za kujenga Zahanati ya Mkanonge.

Sehemu ya wananchi waliofika kwenye uzinduzi huu wa Zahanati ya Kijiji cha Mkanoge

CHAURU YADHAMIRIA KUINUA KILIMO CHA MPUNGA MSIMU UJAO-SADALA

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

CHAMA cha ushirika cha umwagiliaji Ruvu (CHAURU )mkoani Pwani,kimedhamiria kuinua kilimo cha mpunga na kuingia kwenye soko la mchele badala ya mpunga ili kumnufaisha mkulima wa zao hilo katika msimu ujao .

Aidha chama hicho kimenunua trekta lililogharimu sh.mil.77 ,kwa ajili ya kuwasaidia wanachama wa ushirika huo kwa ajili ya kulima kirahisi na kuondokana na gharama za kukodi matrekta .

Akizungumza katika mkutano mkuu wa chama ,;mwenyekiti wa CHAURU ,Sadala Chacha alisema msimu uliopita wa mwaka 2016/2017 walipata changamoto kwa baadhi ya mifereji kukumbwa na mafuriko hali iliyosababisha wakulima wanaolima kwenye mifereji hiyo kushindwa kuvuna.Alisema kutokana na mvua nyingi na mafuriko jumla ya hekari 1,700 ziliathirika.Chacha alieleza ,kwa wakulima waliovuna nao walipata changamoto ya mpunga kuingiliana kwa wakati mmoja na kukosa maeneo ya kuanika .

";Kutokana na changamoto hizi tunajipanga katika msimu unaokuja kununua maturubai ya kutosha na kuweza kuanika kwa wakati na kuziba mifereji iliyokuwa ikiingiza maji ".Chacha alisema mkakati mwingine waliojiwekea ni kutoka kwenye kuuza mpunga na kuuza mchele ili kupata soko na kujiongezea mapato.Alieleza hatua hiyo inafuatia baada ya kugundua kuwa kuuza mpunga badala ya mchele kumesababisha wakulima kupunjika na kutofaidika na kazi kubwa wanayofanya.

Chacha alisema ,hawawezi kufanikiwa kama hawataboresha kilimo hicho na kuwa cha kisasa na kutumia zana bora ndipo walipoamua kutengeneza kinu na kununua trekta litakalowawezesha kufikia malengo yao.Akizungumzia kuhusiana na mapato na matumizi kwa mwaka 2016 alisema walipata mapato ya zaidi ya milioni.309.234 na matumizi yalikuwa ni milioni .2 .857.

"Tangu kuanzia mwezi februari 2016 tulikuwa na hisa milioni 5.3 ambapo kwasasa tuna hisa ya milioni.20 na faida ni zaidi ya milioni. 33" alifafanua Chacha.Nae mkaguzi msaidizi daraja la pili Samwel Mgeni ,kutoka shirika la ukaguzi na usimamizi wa vyama vya ushirika (COASCO),alisema CHAURU imepiga hatua kwani ni moja ya ushirika unaofanya ukaguzi wa mahesabu yake. 

Aliwashauri kuangalia vyanzo vya mapato,kuwa na elimu ya masuala ya fedha na wapunguze matumizi yasiyo ya lazima."Vyama vingi vya ushirika havifanyi ukaguzi lakini CHAURU ni moja ya ushirika unaojitambua na kusimamia masuala ya ukaguzi ,kuwa na vyanzo vya mapato na hakika watafika mbali" alisema Samwel.

Baadhi ya wanachama wa CHAURU akiwemo William Mserikali na Rogati Chuwa ,waliwataka maafisa ugani kutoka maofisini na kwenda kuwatembelea wakulima hao ili kujua changamoto wanazokabiliana nazo.Afisa tarafa ya Chalinze ,Thomas Mollel alisema ushirikiano na umoja ndio nguzo kwa ushirika huo .

Mollel alisema, ili ushirika ulete manufaa baadhi yao waachane na tabia ya kuwarudisha nyuma viongozi waliopo madarakani.Chama cha ushirika wa wakulima wa umwagiliaji (CHAURU)kilichopo Ruvu,kinajishughulisha na kilimo cha umwagiliaji maji wa zao la mpunga katika mashamba na hadi sasa kina wanachama 894.
Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha umwagiliaji Ruvu (CHAURU)Mkoani Pwani,Sadala Chacha akionekana pichani kuzungumza na wanachama wa chama hicho (hawapo pichani),wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho
Baadhi ya wanachama wa chama cha ushirika cha umwagiliaji Ruvu (CHAURU)Mkoani Pwani wakiwa kwenye mkutano mkuu wa chama hicho.
Picha na Mwamvua Mwinyi)

Wafanyabiashara wadogowadogo Ubungo wamlilia Rais

$
0
0

Na Florah Raphael.

Wafanyabiashara wadogowadogo wanaofanya biashara kwenye stendi ya mabasi yaendayo mikoani wamefanya maandamano madogo wakishinikiza na kupinga manyanyaso dhidi ya wafanyabiashara huku lawama kubwa zikienda kwa meneja wa stendi hiyo Imani E. Kasagala.

Akiongea na wandishi wa habari katika mkusanyiko huo, katibu wa umoja wa wafanyabiashara Ubungo John Shayo amesema kuwa walipewa idhini ya kufanya biashara ndani ya stendi hiyo na meya ikiwa ni kuunga mkono kauli ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya hapa kazi tu pamoja na amri yake ya kuwaacha wafanyabiashara wadogowadogo kufanya biashara kwa uhuru pasipo kubuguziwa.

Pia Shayo ameongeza kuwa pamoja na tamko la Rais imekuwa tofauti kwa meneja huyo kwani amekuwa na manyanyaso yasiyo na sababu za msingi na amekuwa na kauli mbaya pindi wanapomuhitaji kwaajili ya mazungumzo hivyo wanamuomba meya wa jiji kushughulikia tatizo hili ili waijue hatima yao ni ipi.

“Hili tatizo ni la mda mrefu hivyo tunamuomba meya wa jiji aje atoe tamko rasmi ili tujue hatima yetu ni IPI” amesema Shayo.Pia Shayo amesisitiza kuwa lengo lao ni kufanya kazi hivyo hawatayafumbia manyanyaso ya meneja huyo hadi meya atakapokuja kufanya maamuzi tena wakiwa pamoja na meneja huyo ili Haki itendeke.“Lengo letu ni kufanya kazi “hapa kazi tu” hivyo hatutakufumbia macho jambo hili hadi meya atakapokuja kufanya maamuzi tena wakiwa pamoja na meneja huyo ili Haki itendeke” amesema Shayo.

Aidha pia mfanyabiashara mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Japhari Hatibu ambaye ni mwenyekiti wa watembeza mikate ndani ya stendi amesema kuwa wafanyabiashara wanapigwa faini bila kosa na hakuna lisiti inayotolewa na anayeshindwa kutoa faini hupelekwa rumande.Pia Hatibu ameongeza kuwa pamoja na kutozwa faini pia Wapo wamama wajane wanaotegemea biashara hiyo ili kulisha familia zao hivyo wanakuwa katika wakati mugumu na itapelekea watu kujihusisha na biashara zisizofaa endapo hali hiyo itaendelea.

Kwa upande wake meneja kasagala aliyetupiwa lawama hizo amejibu tuhuma hizo kwa kusema kuwa kituo kinaendeshwa na sheria ndogo ambayo marekibisho wamefanya mwaka 2009 ambapo sheria hiyo ilikuwa inatumika toka mwaka 2004.

Akifafanua sheria hiyo meneja huyo amesema kuwa biashara zozote zinazotembezwa haziruhusiwi ndani ya kituo na kuongeza kuwa wanaoruhusiwa kuonekana ndani ya kituo ni wanaohusika na mambo ya usafiri pamoja na wafanya biashara wanaotambulika na wale walioko kwenye mfumo maalumu, kama vile wenye maduka na wenye vibali maalum.

“Wanaoruhusiwa kuonekana kwenye kituo ni wanaohusika na mambo ya usafiri pamoja na wafanya biashara wenye vibali maalum na walioko kwenye mfumo maalumu kama wale wenye maduka” amesema Kasagala.


Baadhi ya wafanyabiashara wadogowadogo wanaofanya biashara zao katika eneo la stendi ya mabasi yaendayo mikoani Ubungo, wakiwa wameshikilia mabango yenye kupinga manyanyaso yanayoendelea dhidi yao.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

AMSHA KIPAJI CHAKO NA MASOSO NDANI YA MICHUZI TV.

MAVUNDE AJIBU KERO ZA WANANCHI WA HOMBOLO

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde amefanya ziara kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kata ya Hombolo Bwawani huku akiwahakikishia wananchi wa Mkoyo kuwa wataanza kupata huduma ya maji safi na salama kabla ya mwaka mpya kutokana na mradi huo kukamilika kwa asilimia 95.

Mavunde amefanya ziara hiyo jana ambapo ametembelea kata hiyo na kufanya mikutano ya kusikiliza kero zinazowakabili wananchi, ambapo akiwa kijiji cha Mkoyo miongoni mwa kero walizolalamikia wananchi ni utekelezaji wa mradi ya maji.Kutokana na malalamiko hayo, Mavunde amesema mradi huo umekamilika kwa asilimia 95 lakini bado kuna mapungufu machache ambayo mkandarasi anatakiwa kurekebisha na kuukabidhi kwa wananchi ili waweze kupata maji safi na salama kabla ya mwaka mpya.

Kwa upande wa sekta ya Elimu, Mbunge huyo ameahidi kushirikiana na wananchi katika ujenzi wa shule mbili za msingi kwenye eneo la Ngh’ole na Ndachi kutokana na watoto wa wanatembea umbali mrefu kufuata elimu.“Hivyo kwa kuanza tunaanza na nguvu ya wananchi kwenye ujenzi wa shule ambapo kwa upande wangu nitachangia matofali 1000 na mifuko 100 ya saruji kwa ajili kuanza harakati za ujenzi wa shule hizi,”amesema 

Akiwa katika mtaa wa Hombolo bwawani,Mavunde ameahidi kununua mota yenye thamani ya Tsh 4,000,000 na kuwafungia wananchi ili waanze kupata maji kwenye Mradi wa Maji wa Mtaa wa Bwawani B ambao mota yake imekufa.

Aidha katika Mradi mkubwa wa Maji wa Hombolo ambao ulihujumiwa kwa kuibiwa solar panel,Mavunde amesema wamefanikiwa kuwakamata wezi waliohujumu mradi huo na taratibu za kipolisi zinafanywa ili vifaa hivyo virejeshwe Hombolo na wananchi waanze kupata maji.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kata ya Hombolo Bwawani.
Diwani wa Kata ya Hombolo Bwawani Assedi Ndajilo akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde wa kusikiliza kero za wananchi.
Umati wa watu waliohudhuria mkutano wa hadhara kata ya Hombolo bwawani
Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akisalimiana na wananchi na viongozi wa kata ya Hombolo bwawani.



UJENZI WA CHUO CHA VETA MKOA WA SIMIYU KUANZA MWEZI MACHI 2018

$
0
0
Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako amesema Serikali inatarajia kuanza ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) cha Mkoa wa Simiyu kuanzia mwezi Machi, 2018.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake ya siku moja Mkoani humo.“Kesho tarehe 28/12/2017 kwenye magazeti kutatoka tangazo la zabuni ya ujenzi wa VETA ya Mkoa wa Simiyu na tunategemea kujenga VETA ya Kisasa itakayohudumia Mkoa na inayoendana na mahitaji ya sasa; tukitangaza zabuni kesho itachukua siku 30 kupokea zabuni unahitajika mwezi mmoja kufanya tathmini, nawaahidi kuwa ujenzi utaanza mwezi Machi” alifafanua Profesa Ndalichako.

Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ambayo inasisitiza juu ya ujenzi wa Uchumi wa Viwanda inatambua umuhimu wa Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi ndiyo maana imejipanga kujenga vyuo hivyo pamoja na kuimarisha Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi.Aidha, Profesa Ndalichako amepongeza ongezeko la wanafunzi walioandikishwa kuanza darasa la kwanza na akasisitiza kuwa Wizara ya Elimu ambayo ndiyo inayotunga Sera itahakikisha inasimamia kikamilifu ili wanafunzi wote wanaoanza darasa la kwanza wamalize masoma yao.

Amesema ongezeko hilo ambalo limesababishwa na mwamko chanya wa wazazi baada ya kuanza kutekelezwa kwa mpango wa elimu bila malipo limepelekea upungufu wa miundombinu shule na ndiyo maana Serikali kuu inashirikiana na Halmashauri pamoja na wananchi katika ujenzi wa miundombinu ili kukabiliana na upungufu kupitia Mradi wa Lipa kulingana na Matokeo(P4R).

“Kupitia mradi wa Lipa kulingana na Matokeo tumeshajenga jumla ya vyumba vya madarasa 1104, matundu ya vyoo 3396, mabweni 261. Tunaendelea pia kuimarisha miundombinu katika sekta ya elimu kwa ujumla, kwa maana ya ukarabati katika vyuo vya Ualimu ambapo tumeshakarabati vyuo 17 na shule kongwe 46 kati ya shule 88 zimeshakarabatiwa” alisema Waziri.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako(kulia) akiweka Jiwe la Msingi katika Mabweni ya Wasichana yaliyojengwa kupitia Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (P4R) katika Shule ya Sekondari Itilima wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu,(kushoto) Mkuu wa Mkoa huo, mhe Anthony Mtaka.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lagangabilili mara baada ya kufungua vyumba vya madarasa vilivyojengwa kupitia Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (P4R) katika Shule ya msingi Lagangabilili wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako( wa tatu kushoto) na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Itilima na Mkoa wa Simiyu wakielekea kukagua vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Lagangabili, wakati wa ziara yake mkoani humo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako(kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi (kulia) wakati akikagua vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Lagangabili, wakati wa ziara yake mkoani Simiyu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako(aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Itilima na Mkoa wa Simiyu mara baada ya kukagua vyumba vya madarasa vilivyojengwa kupitia Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo(P4R) katika Shule ya Sekondari Lagangabilili wilayani Itilima.


UKAGUZI MACHIMBO YA BUHEMBA KUKAMILIKA KABLA JANUARI 10, 2018

$
0
0
Serikali imeagiza kufikia Januari 10, 2018 Ukaguzi wa Usalama kwenye eneo la Machimbo ya Dhahabu ya Buhemba, Wilayani Butiama Mkoani Mara uwe umekamilika ili shughuli za uchimbaji zilizokuwa zimesimamishwa ziruhusiwe.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alitoa agizo hilo Desemba 27, 2017 alipofanya ziara kwenye eneo hilo ili kujionea hali halisi ya machimbo husika pamoja na kuzungumza na wachimbaji waliosimamishwa kuendeleza shughuli zao hadi hapo ukaguzi utakapokamilika. 
“Ninasikitika kuona shughuli za uchumi kwenye eneo hili la Buhemba zimesimama kutokana na shughuli za uchimbaji kusimamishwa baada ya kutokea ajali,” alisema. 
Serikali ilisitisha shughuli za uchimbaji Madini kwenye eneo hilo la Buhemba Februari 2017 baada ya kutokea vifo vya wachimbaji Watatu na wengine wapatao 15 kujeruhiwa kutokana na kufanya shughuli zao bila kuzingatia taratibu na kanuni za uchimbaji salama.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa tatu kutoka kushoto) akikagua moja ya shimo la dhahabu kwenye machimbo ya Buhemba.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi wakati wa ziara yake kwenye eneo la machimbo ya dhahabu la Buhemba, Wilayani Butiama, Mkoani Mara.
 Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi (aliyesimama) akimkaribisha Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) kuzungumza na Wachimbaji (hawapo pichani). Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini (FEMATA), John Bina.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza na baadhi ya Wachimbaji kwenye Machimbo ya Dhahabu ya Buhemba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

JESHI LA POLISI MKOANI NJOMBE LINAMSAKA ASKARI PC ZAKAYO DOTO KWA TUHUMA ZA MAUAJI

$
0
0
Kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe,  Pudensiana Protasi akizungumza na waandishi wa habari 

Na Amiri Kilagalila, Njombe
Jeshi la polisi  mkoani Njombe linamtafuta askari PC Zakayo Doto kwa kosa la kumuua kwa kumpiga risasi askali wa jeshi la wananchi (JWTZ) anayedaiwa kuwa ni mchumba wake kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa majirani wa mtaa wa Jeshini kata ya Makuvani wanasema marehemu Neema Masanja aliyekuwa askari wa Jeshi la Wananchi kikosi cha 514KJ Makambako alipigwa risasi na askari PC Zakayo Doto ambaye anadaiwa kuwa ni mchumba wa marehemu huku sababu zikiwa bado hazijafahamika

Mganga mfawidhi wa hospitali ya mji wa Makambako daktari Kesha Ngunda amekiri kupokea mwili wa marehemu afande Neema Masanja ambao umefikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya uchunguzi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Pudensiana Protasi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

TOCHI ZA TRAFIKI ZIMESAIDIA KUDHIBITI MWENDO KASI BARABARANI, KUPUNGUZA AJALI: SACP MUSILIMU

$
0
0
Na Said Mwishehe, Blogu ya Jamii
JESHI la  Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limesema litaendelea kutumia tochi kwa ajili ya kudhibiti mwendokasi huku likihimiza watuamiaji wa barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani nchini. 

Limetumia nafasi nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo wamefanikiwa kusimamia sheria, hivyo ajali zimepungua ikilinganisha na miaka iliyopita.

Hayo yamesemwa leo, jijini Dar  es  Salaam na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Musilimu wakati akitoa takwimu za kupungua kwa ajali  hasa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka. 

Kamanda Musilimu amesema usimamizi mzuri wa  sheria za usalama baraarani umesaidia kupunguza ajali na kuongeza wataendelea na jukumu lao ili kukomesha ajali. 

Amesema ajali nyingi ambazo zinatokea si  mpango wa  Mungu bali ni uzembe wa madereva na watumiaji wengine wa barabara hizo. 

"Naomba niwaambie wapo wanaosema ajali zinazotokea barabarani na kusababisha vifo na majeruhi ni mpango wa Mungu, si kweli ila zinatokana na uzembe wa madereva. 

"Kwa sasa tunahimiza watumiaji wa barabara kufuata sheria za usalama barabarani.Wapo wanaolalamikia uwepo wa tochi, naomba wafahamu hatutaacha kuzitumia kwani zimetusaidia sana kupunguza ajali,"amesema Kamanda Musilimu. 

Ameongeza uwepo wa tochi umesaidia kuwafanya madereva kutokwenda mwendo kasi ingawa bado wapo wengine wanaenda kasi na wamekuwa wakikamatwa na kuchukuliwa hatua. 

Amesemaa kwa usimamizi mzuri wa sheria na madereva kuwa na uelewa mpana wa matumizi mazuri barabarani, imesaidia kukomesha ajali.

 Kamanda Musilimu amefafanua kwa muda mrefu kumekuwa na utamaduni wa kutokea ajali nyingi kipindi cha mwisho wa mwaka na mwanzoni mwa mwaka lakini wamefanikiwa kudhibiti ajali hizo. 

"Mwishoni mwa mwaka na mwanzoni mwa mwaka havina tofauti na vipindi vingine, hivyo wananchi wasiwe na hofu yoyote, "amesema Kamanda Musilimu. 

Ametaja chanzo cha ajali ni mwendo kasi, ulevi na uzembe, lakini kwa kusimamia sheria wamefanikiwa kupunguza makosa ya barabarani. 

Alipoulizwa uwepo wa trafiki wengi wenye tochi kiasi cha kuonekana kero, jijini Dar  es Salaam Kamanda Musilimu amesema wameamua kuweka tochi hizo baada ya kuona ajali za watu kugongwa zimekuwa nyingi. 

Ametoa mfano wa eneo la Kawe Darajani kulikuwa na matukio ya watu kugongwa lakini baada ya kuweka tochi hakuna matukio ya ajali tena.Pia ameongeza maeneo yote yenye tochi ajali zimepungua. 

Kuhusu kufungiwa leseni 88 kwa madereva waliobainika kufanya makosa barabarani,katika mwezi huu,amesema sheria inamruhusu kufungia leseni kwa kipindi cha miezi sita.

"Madereva ambao tumefungia leseni zao hawataruhusiwa kuendesha mabasi ya abiria wala magari makubwa ila wanaruhusiwa kuendesha magari madogo. 
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani,  Fortunatus Musilimu akizungumza katika makao makuu ya kikosi hicho jijini Dar  es Salaam leo, kuhusu kupungua kwa ajali kipindi hiki cha mwisho wa mwaka huu.

NAIBU WAZIRI NISHATI SUBIRA MGALU AAGIZA REA KUMCHUKULIA HATUA MKANDARASI WA AWAMU YA PILI MKOA WA PWANI

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
NAIBU Waziri wa Nishati Subira Mgalu ameagiza mkandarasi wa mradi wa umeme wa Vijijini REA awamu ya pili Kwa Mkoa wa Pwani ambayo ni kampuni ya MBH kuchukuliwa hatua hatua kali za kisheria.

Hatua hiyo imefikia baada ya mkandarasi huyo Kampuni ya MBH kushindwa kutimiza malengo ya mkataba na kuacha baadhi ya maeneo yakiwa hajaweka miundo mbinu ya umeme kama walivyokubaliana awali.

Akitoa maagizo hayo mbele ya wananchi wa Kata ya Ruauke, Naibu Waziri Nishati Subira amewataka REA kuhakikisha suala la mkandarasi huyo linachukuliwa hatua kwani ameweza kuacha maeneo mengi yakiwa hayajakamilika na tayari mkataba wake ukiwa umeshamalizika.

Subira amesema maeneo mbalimbali ya ikiwemo Mkamba, Kisarawe, Kibaha Vijijini, Mkuranga, Kibiti, Kisiju na hata Rufiji kuacha maeneo mengi yakiwa hayajakilimika na mengine akiacha nguzo za umeme zikiwa zimesimama bila kuwekwa nyaya za umeme.

"REA lazima muhakikishe mkandarasi huyu anachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kushindwa kufikia malengo kwani kuna maeneo mengi ameshindwa kutimiza malengi tuliyokubaliana na tayari mda wake ukiwa umeisha tayari wa kuweka miundi mbinu ya umeme,'amesema Subira.
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Uruma kilichopo Delta ya Kusini wakati wa ziara yake ya katika Wilaya ya Kibiti.
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akikagua miundo mbinu ya shule ya Mtanga Delta akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya Kibiti Shaban Kiffu,Mbunge wa Jimbo la Kibiti Seif Ally Ungando, Mkurugenzi wa Wilaya ya Kibiti Alvera Ndabagoye na Mkuu wa Shule ya Sekondari hiyo Humphrey Mwakyambiki.
  Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Muyuyu kata ya Mtunda wakati wa ziara yake ndani ya Wilaya ya Kibiti. 
 Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Shaban Kiffu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Uruma kichopo Delta ya Kusini wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu.

Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza na wakina mama waliokuwa wamewapeleka watoto wao kupata chanjo katika kituo cha afya kilichopo Kijiji cha Muyuyu wakati wa ziara yake ndani ya Wilaya ya Kibiti.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akikabidhi mifuko ya saruji 50 kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo hilo, Seif Ally Ungando kwa diwani wa kata ya Ruauke, Mwarami Mkopi kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Nyamatanga wakati wa ziara yake ndani ya wilaya ya Kibiti.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAYAGE KUAGWA NA KUZIKWA LEO ALHAMISI DESEMBA 28, 2017; NYUMBANI KWAKE MBWENI, ENEO LA MAPUTO, DAR ES SALAAM.

$
0
0



Ramani ya msiba

Msiba uko nyumbani kwake Mbweni Kijijini, Dar es Salaam, eneo la Mbweni Maputo,siyo mbali na hospitali ya Mbweni Misheni.

Yaani ukiwa unatokea Mwenge unapanda daladala ziendazo Mbweni Kijijini, unashukia kituo cha Mbweni Misheni, kisha hatua chache mbele kuna njia inayokwenda kushoto ifuate barabara hiyo kwa kuongozwa na vibao vinavyoelekeza msiba ulipo mpaka utakapofika nyumbani kwa marehemu, ambaye ni maarufu kama Mzee Magazeti.

Njia nyingine ni kupanda mabasi ya Makumbusho-Bunju/Bagamoyo, shukia  kituo cha Mianzini Bunju.
Hapo chukua bodaboda kwa gharama ya kama 3000/= hadi mbele kidogo ya Mbweni Misheni Hospitali. Ukifika hapo kata kushoto na muelekeze huyo bodaboda afuate vibao vya kuelekeza msiba hadi nyumbani kwa marehemu.

Kwa wenye usafiri binafsi; unaweza kufika kwa njia mbili:

1.Ukitoka Mwenge nenda mpaka Petrol Station ya Lake Oil eneo la Bunju. Hapo kuna barabara ya lami kuelekea Mbweni. Ifuate hadi Mbweni Kijijini,utakapoikuta Hospitali ya Misheni Mbweni. Baada ya hapo kata kushoto.Fuata vibao vya msiba vitakufikisha. 

2.Ukitoka Mwenge nenda hadi njia panda Mbweni Jeshini, fuata njia ya daladala, yapite mageti ya Jeshi hadi Mbweni Kijijini.Endelea mbele hadi Mbweni Misheni Hospitali.Sogea mbele kidogo, halafu kata kushoto na anza kufuata maelekezo ya vibao vya msiba ambavyo vitakufikisha.

Usafiri kwa Wanahabari

Kwa mujibu kamati ya maandalizi kutakuwa na mabasi mawili ya UDA yatakayobeba wanahabari watakaokwenda kumuaga mwenzao.

Basi la kwanza litakuwa Idara ya Habari Maelezo,Mtaa wa Samora, kuanzia saa 1:30 asubuhi ambapo litaondoka saa 2:30 kuelekea msibani Mbweni.

Basi la pili litakuwa Mwenge,maeneo ya kituo cha mafuta cha BP, kuanzia saa mbili asubuhi ambapo litaondoka hapo saa 3 kuelekea msibani.

Poleni sana,

Imetolewa na Kamati ya Maandalizi
Desemba 27, 2017.

Kwa mawasiliano wapigie wanakamati ya Usafiri

Peter Mgongo 0715 765 454
Eric Antony 0755 755 551

BENKI YA CRDB YAANZA MCHAKATO WA KUPATA MRITHI WA DKT. KIMEI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dar es salaam leo, kuhusu Benki hiyo kuanza mchakato wa kumtafuta mrithi wa nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, unaotaraji kuanza mapema mwakani. Huku akiwatoa hofu wateja na wananchi kiujumla kuwa Benki ipo salama. Dkt. Kimei atandelea kuhodhi nafasi hiyo mpaka Mei 2019 atakapostaafu. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Ester Mwambapa na kushoto ni Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya CRDB, James Mabula.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Ester Mwambapa akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari kuhusu Benki hiyo kuanza mchakato wa kumtafuta mrithi wa nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei wakati atoa taarifa ya kuanza mchakato wa kumtafuta mrithi wa nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, unaotaraji kuanza mapema mwakani.
Sehemu ya wanahabari pamoja na wageni wengine.

MWILI WA MAREHEMU MAYAGE WAAGWA LEO NYUMBANI KWAKE MBWENI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Blogu  ya Jamii
TASNIA ya habari imeombwa kuendeleza mapenzi baina yao kama walivyoonyesha katika ugonjwa wa Mayage S. Mayage aliyefariki juzi.

Hayo yamesemwa leo  mchana huu na Padre John kaniki wa Kanisa Katoliki katika ibada ya mazishi ya marehemu Mayage iliyofanyika nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es  Salaam.

Padre Kaniki amesema maumivu aliyokua akipata kitandani Manage wakati anaumwa aliyatoa kwa ajili ya watu anaowapenda ikiwemo wanahabari wenzie.

Alisema msiba ni sehemu ya kutubia kwa wale wanaobaki hivyo ni vema wote kuwa wanyenyekevu kwa Mungu.

Amesema yeye binafsi alimfahamu Mayage  S. Mayage katika kipindi ambacho alikuwa anaunwa kwani alikuwa akimfanyia maombi na alichojifunza ni upendo na uvumilivu. 

"Alikuwa ni mtu mwenye upendo na huruma, ni vema tukaendeleza mema yake na kubwa zaidi ni kumuombea kwa  Mungu, "amesema Padre Kaniki. 
  
Mayage S. Mayage wakati wa uhai wake amesoma katika vyuo mbalimbali vya ndani  na  nje na baada ya kuhitimu amefanya kazi katika maeneo mbalimbali.

Ilipofika mwaka 1995 ndipo alipojiunga na kampuni ya magazeti ya Habari Coparation ambayo sasa ni New Habari na baadae alikwenda gazeti la Raia Tanzania. 

Akizungumza katika maziko ya Mayage S. Mayage, Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absolum Kibanda amemuelezea Mayage kama mwandishi aliyeacha alama ya ujasiri na uthubutu katika taaluma. 

Kibanda amesema mchango wa Mayage katika tasnia ya habari na hasa uchambuzi wa habari za siasa.

"Mimi na Mayage pamoja na wengine tuliojariwa pamoja Habari Coparation, anayeweza kumzungumzia vizuri Mayage ni mhariri na mwalimu wetu kitaalum.
Mchungaji akiongoza misa ya kuombea mwili wa marehemu Mayage S. Mayage aliyewahi kuwa mwandishi wa habari leo nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanafamilia wa marehemu, ndugu na jamaa wakiwa fuatilia ibada ya kuagwa kwa aliyekuwa mwandishi mkongwe Mayage S. Mayage nyumbani kwake Mbweni Kijijini leo.
 Neno la Mungu likisomwa 

Mbunge wa Mtama na Waziri wa zamani wa Habari, Nape Nauye na Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole pamoja na ndugu na jamaa wakiwa kwenye ibada ya mazishi Marehemu Mayage S. Mayage aliyewahi kuwa mwandishi wa habari leo nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakiwa kwenye ibada ya kuagwa kwa mwili wa Marehemu Mayage S. Mayage aliyewahi kuwa mwandishi wa habari leo nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam.

MKUU WA MKOA PWANI AAMRISHA VIONGOZI KUMI WA VYAMA USHIRIKA KUKAMATWA

Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images