Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

RAIS MAGUFULI AWASILISHA FOMU ZAKE ZA TAMKO LA RASILIMALI NA MADENI KWA VIONGOZI WA UMMA KATIKA OFISI ZA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Jengo la Sukari House lenye Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma kwa ajili ya  kuwasilisha Fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma zilizopo katika Mtaa wa Ohio Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni  mara baada ya kuwasili katika Makao makuu ya Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma zilizopo katika Mtaa wa Ohio Jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma kwa Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela katika Makao makuu ya ofisi hizo yaliyopo katika Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaa
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela mara baada ya kuwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela wakati akitoka katika Jengo la Sukari House lenye Ofisi za Sekretarieti ya  Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi walio simama kando ya barabara inayopita mtaa wa Ohio wakati akitoka katika Ofisi za za Sekretarieti ya  Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

WAZIRI MKUU AKUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI KWAKE WILAYANI RUANGWA, MKOANI LINDI

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Nachingwea, kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka ambapo aliamua kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake wilayani Ruangwa, mkoani Lindi, Desemba 28, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mwananchi wa kijiji cha Mibure, Mzee Menrad Kilian, baada ya kukagua ujenzi wa zahanati kijijini hapo, wilayani Ruangwa mkoani Lindi, Desemba 28, 2017. 
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mibure, wakati alipoenda kukagua ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho Desemba 28, 2017. Waziri Mkuu yupo jimboni kwake kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.
 Mkurugenzi Mtendaji wa KALIF Construction, Ally Mohamed Libaba akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) wakati wakijaribu kuvuta maji kutoka kwenye pampu ya mradi wa maji wa kijiji cha Namakuku, Desemba 28, 2017. Wa kwanza kulia ni msimamizi wa mradi huo, Bw. Fadhil Ally Libaba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

CCM mkoa wa Pwani yajipanga kukomboa maeneo mbalimbali yanayoongozwa na vyama vya upinzani

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Pwani Ramadhan Maneno amesema, atahakikisha anakomboa maeneo mbalimbali yanayoongozwa na vyama vya upinzani mkoani humo katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika 2019 na uchaguzi mkuu 2020.
Aidha amewataka wanaccm kuachana na siasa za mazoea ambazo zimekuwa zikikiumiza chama hasa nyakati za uchaguzi ambapo husababisha wanachama kuwapigia kura wapinzani na kukikandamiza chama.
Aliyasema hayo Chalinze wakati wa sherehe za kumpongeza kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo   zilizoandaliwa na CCM kata ya Bwilingu.
Maneno alieleza kwa kushirikiana wanaCCm na kujenga umoja kwa hakika ushindi utapatikana na kurejesha maeneo yaliyopotezwa kwenye uchaguzi uliopita.
Alisema yeye na viongozi waliochaguliwa wana kazi kubwa ya kukiimarisha chama na kuendelea kushika dola.
"Kuna kata, vitongoji, vijiji na mitaa vinashikiliwa na upinzani ambapo waliongoza wakati wa chaguzi zilizopita,ni lazima tuzirudishe "
“Tunaimani tutavirudisha kwenye himaya yetu na kutokana na yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Magufuli kwa sasa wapinzani hawana safari na kata 28, mitaa 11, vitongoji 38 na vijiji 76 ambavyo vinashikiliwa na wapinzani mkoa mzima tutavikomboa,” alisema Maneno.
Alielezea ili kufanikiwa kwenye hilo wataanza mikakati mapema kwa kuhakikisha wanaweka wagombea ambao wana uwezo na si kwa upendeleo na malumbano ambayo yanasababisha kutoelewana.
“Kikubwa ni kuhakikisha tunamsaidia Rais kwani yeye tayari kaanzisha njia tukifuata anavyotaka hatutapata taabu na tusisubiri hadi dakika za mwisho kama kuna mtu anakikwamisha chama ni vema kumsema na si kumficha na tuangalie tulijikwaa wapi ,” alisema Maneno.
Akizungumzia kuhusu siasa za mazoea alisema zimekiharibu chama kwa watu kushindwa kuwakemea wale wanaokwenda kinyume na katiba ya chama na kujiona kuwa wao ni miungu watu .
Alisema siasa za namna hiyo ni za kuumizana kama mtu kakosea asemwe kwenye vikao husika .
Awali akimkaribisha mwenyekiti mwakilishi mkutano mkuu wa mkoa Wakili msomi Imani Madega, aliwataka wanaCCM waondoe makundi na kurekebishana pale penye makosa.
Madega alisema makundi ni moja ya chanzo kinachosababisha kushindwa kwenye chaguzi mbalimbali dhidi ya wapinzani.
Nae mwenyekiti wa halmashauri Saidi Zikatimu alisema  atahakikisha anakaa na madiwani ili kuondoa changamoto zilizopo ambazo zimeonekana baina ya madiwani wa halmashauri hiyo mpya ya Chalinze.
Zikatimu aliomba wawe kitu kimoja pia wao kama madiwani watahakikisha wanaisimamia serikali ili iweze kutekeleza ilani ya chama ambayo ndiyo inayoongoza nchi kwa sasa.
 Mwakilishi mkutano mkuu wa mkoa wa Pwani Wakili Msomi Imani Madega, akizungumza kwenye sherehe za kupongezwa kuchaguliwa kwa uongozi Mpya wa CCM Mkoani hapo ,iliyoandaliwa na CCM kata ya Bwilingu jimbo la Chalinze.(Mwamvua Mwinyi
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM)Mkoani Pwani Ramadhan Maneno ,akizungumza kwenye sherehe za kumpongeza kushika nyadhifa hiyo ,iliyoandaliwa na CCM kata ya Bwilingu jimbo la Chalinze.
Picha na Mwamvua Mwinyi

Jumuiya za Kidini zatakiwa kuzingatia Sheria na masharti ya usajili waliopewa

$
0
0
Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kidini Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi chini ya Sheria ya Jumuiya, Sura ya 337 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002 (Societies Act) inazikumbusha Jumuiya zote zilizosajiliwa chini ya Sheria hii, kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria pamoja na masharti ya usajili waliopewa wakati wa usajili. Miongoni mwa masharti yanayopaswa kuzingatiwa na Jumuiya hizo ni pamoja na kutoa taarifa za mabadiliko ya Katiba zao ambazo pamoja na mambo mengine  hueleza malengo ya Jumuiya husika.


Hata hivyo, baadhi ya Jumuiya  zimekuwa zikifanya shughuli zao kinyume na malengo yaliyomo kwenye Katiba zao bila kuiarifu Ofisi ya Msajili. Mathalani hivi karibuni kumekuwepo na tabia ya baadhi ya viongozi wa Jumuiya kutumia mahubiri yao wakati wa ibada kuchambua masuala ya siasa kinyume na Katiba zao kwani hakuna Jumuiya yoyote iliyosajiliwa chini ya Sheria ya Jumuiya ili kufanya kazi za siasa. Tabia hii ni kwenda kinyume na malengo na ni ukiukaji Kanuni ya 7 ya Kanuni za Jumuiya zilizoundwa chini ya Sheria ya Jumuiya, inayotamka, kati ya mengine  kwamba Jumuiya yoyote hairuhusiwi kufanya mabadiliko ya malengo yake bila ya kibali cha Msajili’’.  

Ofisi ya Msajili inazikumbusha Jumuiya zote zinazofanya kazi kinyume na malengo yaliyoainishwa katika Katiba zao zilizosajiliwa kuacha kufanya hivyo mara moja. Aidha Ofisi ya Msajili inazikumbusha Jumuia zote kwamba ukiukaji wowote wa Sheria ni kosa ambalo linaweza kupelekea Jumuiya husika kufutiwa usajili wake kama ilivyoelezwa kwenye kifungu cha 17 cha Sheria husika.

Imetolewa na:
Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu)
KATIBU MKUU
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Kwa Simu Toka London: Sehemu ya 4 - Mahojiano na Saidi Kanda

$
0
0
Na Freddy Macha
Sehemu ya 4 ya mahojiano na Saidi Kanda - anazungumzia kuhusu bendi yake Mvula Mandondo- na kumhusisha mwimbaji na kiongozi wa bendi hiyo, Fab Moses. Hebu tuwasikilize wakizungumza na kuimba.

The Makaveli Trap song rapper returns again with a new jam "Buku kuwa laki"

$
0
0
The Makaveli Trap song rapper returns again with a new jam. "Buku kuwa laki" here he speaks about the hustle and life after him being under the spot light, the obstacles, and chalenges he faces. This is considered as an extention of his previois releases. Hope you will enjoy and help share this vibrant, emotional, aggresive great work from the new kid on the block.

Introducing "Magufuli Tubebe" By Rose Muhando

Ihanje saafi, ujenzi wa miundombinu ya Afya - Waziri jafo.

$
0
0
Nteghenjwa,Hosseah,Ikungi-Singida.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amepongeza kazi nzuri  ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali inayoendelea kujengwa katika Kituo cha Afya Ihanje kilichopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.
Mhe.Jafo alitoa pongezi hizo wakati wa ziara yake Wilayani humo ya kukagua  miradi ya maendeleo na kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ambapo akiwa kituoni hapo alisema ameridhishwa na usimamizi, ubora na maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ihanje.
Aliongeza kuwa Kituo cha Ihanje ni miongoni mwa Zaidi ya Vituo 200  vitakavyopekea/vilivyopokea Fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Afya ambayo ilikosekana hapo awali na kukifanya kituo hiki kutotoa huduma ipasavyo na agizo langu la awali ilikua kumaliza kazi ya ujenzi mnamo Dec 30,2017 lakini kwa Ikungi walichelewa kuanza utekelezaji kutokana na kupokea maelekezo mengine baadae ila wamefanya kazi nzuri hivyo wao watakamilisha Jengo hili mnamo January 2018.

Nimekagua majengo yote sita yanayojengwa kupitia uboreshaji huu hakika yanavutia na kupendeza, kuanzia Maabara, Wodi ya Kinamama, Chumba cha Upasuaji, Chumba cha kuhifadhia Maiti pamoja na kichomea Taka na ukizingatia ujenzi huu umewahusisha mafundi  kutoka kwenye Vijiji na Kata zetu ambapo kwa kuwatumia wao gharama za ujenzi hupungua ukilinganisha na  wakandarasi; Hii  inanipa faraja kubwa kuona kazi zinaenda vizuri kutoka kwa watalaam walioko kwenye jamii yetu, Alisema Mhe.Jafo.
Awali akitoa taarifa hiyo  Mhandishi wa Ujenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi  Sembua Mrisho amesema Fedha zilizopokelewa ni Tsh. Mil 720 kati ya hizo Mil 220 zimepelekwa bohari ya dawa kwa ajili ya  vifaa Tiba na Dawa mara majengo hayo yatakapokamilika na Tsh Mil 500 ndizo zinazotumika katika Ujenzi wa miundombinu yote sita na hali ya ujenzi mpaka sasa inaonyesha Fedha hizo zitakamilisha kabisa mradi huo kwa ubora unaotakiwa.
“Mara baada ya kupokea Fedha hizo na kupata Muongozo toka OR-TAMISEMI, Fedha zile zililetwa kwenye Kata na zikaundwa kamati Tatu ya Mapokezi, Manunuzi na Ujenzi na kazi yote hii imefanyika kwa kutumia “Local fund” na  inasimamia na Wakandarasi wa Halmashauri kwa kushirikiana na kamati za Ujenzi zilizopo” alisema Mrisho.
Akizungumza wakati wa Ziara hiyo Mbunge wa Ikungi Mhe.Elibariki Kingu amesema Ihanje ni Kata pia ni Makao Makuu ya Tarafa ya Ihanje na mradi huu umejibu shida za wananchi wa Ihanje na Ikungi kwa Ujumla kwa sababu Kituo hicho kinatoa huduma kwa wakinamama wengi wa Kata zaidi ya Tano zinazonguka eneo hili.
Aliongeza kuwa  Kituo cha Afya kilichkuwepo awali kilikuwa hakikidhi  mahitaji kutokana na kutokua na maeneo muhimu kama wodi nzuri na kubwa ya kina mama, maabara, sehemu ya kuhifadhia maiti nk lakini kwa sasa sisi wananchi wa Ikungi tunaishukuru sana Serikali yetu kwa kututatulia hangamoto hii.
Akizungumza kwa furaha Angelina Naaman(Mama Yasinta) amesema “Wakinana mama sasa tutaona raha Zaidi ya kujifungua kwa sababu tumepata mpaka chumba cha Upasuaji wakati awali ilikua ukishindwa kujifungua kawaida inakua mtihani sana kwako na kwa wauguzi wenyewe hivyo sasa zoezi la kujifungua kwetu litakua salama Zaidi kwa masiah yetu nay a mtoto.

Ukarabati sambamba na uboreshaji wa vituo vya Afya vinavyoendelea Nchini Kote utafanyika katika awamu na awamu ya kwanza ilianza Mwezi Sept 2017 na utakamilika January, 2018 na umehusisha vituo 44 wakati awamu ya Pili itaanza mwenzi January 2017 utahusisha Vituo vya Afya 161.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(Tatu kushoto) akimskiliza Mhandisi wa Ujenzi Sembua Mrisho wakati wa ukaguzi wa Jengo la upasuaji linalojengwa katika Kituo cha Afya Ihanje.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Tatu kushoto) akimskiliza Mhandisi wa Ujenzi Sembua Mrisho wakati wa ukaguzi wa Jengo la upasuaji linalojengwa katika Kituo cha Afya Ihanje.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo (mbele) akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu pamoja na Mbunge wa Singida Magharibi Mhe. Elibariki Kingu wakiongozwa na Mhandisi wa Majengo kukagua ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Afya inayojengwa katika Kituo cha Afya Ihanje kilichopo Ikungi.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Kulia) akikagua Ujenzi wa Kichomea Taka katika kituo cha Afya Ihanje.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(katikati) akiwa na Viongozi wa Wilaya ya Ikungi katika picha ya pamoja na watumishi wa Kituo cha Afya Ihanje.

Serikali yazikumbusha Jumuiya zote zinazofanya kazi kinyume na malengo yaliyoainishwa katika Katiba zao zilizosajiliwa kuacha kufanya hivyo mara moja

$
0
0
Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kidini Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi chini ya Sheria ya Jumuiya, Sura ya 337 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002 (Societies Act) inazikumbusha Jumuiya zote zilizosajiliwa chini ya Sheria hii, kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria pamoja na masharti ya usajili waliopewa wakati wa usajili.

 Miongoni mwa masharti yanayopaswa kuzingatiwa na Jumuiya hizo ni pamoja na kutoa taarifa za mabadiliko ya Katiba zao ambazo pamoja na mambo mengine hueleza malengo ya Jumuiya husika.

Hata hivyo, baadhi ya Jumuiya zimekuwa zikifanya shughuli zao kinyume na malengo yaliyomo kwenye Katiba zao bila kuiarifu Ofisi ya Msajili. Mathalani hivi karibuni kumekuwepo na tabia ya baadhi ya viongozi wa Jumuiya kutumia mahubiri yao wakati wa ibada kuchambua masuala ya siasa kinyume na Katiba zao kwani hakuna Jumuiya yoyote iliyosajiliwa chini ya Sheria ya Jumuiya ili kufanya kazi za siasa.

Tabia hii ni kwenda kinyume na malengo na ni ukiukaji Kanuni ya 7 ya Kanuni za Jumuiya zilizoundwa chini ya Sheria ya Jumuiya, inayotamka, kati ya mengine kwamba Jumuiya yoyote hairuhusiwi kufanya mabadiliko ya malengo yake bila ya kibali cha Msajili’’.

Ofisi ya Msajili inazikumbusha Jumuiya zote zinazofanya kazi kinyume na malengo yaliyoainishwa katika Katiba zao zilizosajiliwa kuacha kufanya hivyo mara moja. Aidha Ofisi ya Msajili inazikumbusha Jumuia zote kwamba ukiukaji wowote wa Sheria ni kosa ambalo linaweza kupelekea Jumuiya husika kufutiwa usajili wake kama ilivyoelezwa kwenye kifungu cha 17 cha Sheria husika.

Imetolewa na:

Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu)
KATIBU MKUU
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MSANI HARMONIZE AGAWA CHAKULA KWA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU MKOANI MTWARA

$
0
0
Msanii wa muziki wakizazi kipya Rajab Abdulkahal au Harmonize amekula chakula cha mchana na watoto wanaishi katika mazingira hatarishi katika kituo cha kulelea Yatima cha kanisa LA EAGT mkoni Mtwara kama moja ya Kuwapa matumaini katika Maisha ya kila Siku.

Harmonize akiongozana na rafiki yake wa kike wa karibu anayejulikana kwa Jina la Sarah amesema kuna watoto waliopoteza wazazi wao wakiwa na umri mdogo huku wakiwa na ndoto kubwa za kimaisha lakini zinaonekana kupotea kutokana hivyo wanahitaji kupewa moya na kuwa na bidii binafsi.

Hata Hivyo Msanii Harmonize amepata fursa ya kubadilishana Mawazo na watoto wenye Ndoto mbalimbali zankimisha na kuwasihi kumshirikisha Mungu kwa kila wanachokifanya.
 Msanii Harmonize akiwa na Rafiki yake Sarah wakigawa chakula kwa Watoto wanaoishi katika Mazingira hatarishi ambao wanalelewa katika kituo cha Kulea Yatima cha EAGT Mtwara.
Harmonize akiongea na Wandishi wa Habari Mara baada ya kumaliza Chakula cha Mchana alichokiandaa kwa ajili ya Watoto Yatima Mtwara

IN LOVING MEMORY

$
0
0
Dear Maxmillian Charles Makwaia... 
It is exactly two years since you were promoted to Glory.

"But those we love don't go away, they walk beside us every day,  unseen, unheard, but always near, still loved, still missed and very dear.

You are loved beyond words and missed beyond measure by your Father ; Charles, Mother; Hilda, Brother Kevin (Mashishi), Sister; Prisca, (Bibi Tillu, Bibi and Babu Urassa), Aunties  and Uncles.

JOHN 3:16
For God so loved the world  that he gave his one and only Son, that  whoever believes in him shall not perish but have eternal life.

MAGAZETI YA IJUMAA LEO DECEMBER 29,2017

KUKITHIRI MASHAMBULIZI DHIDI YA WATOTO 2017

VOA Swahili: Mkimbizi arudi Dadaab miaka miwili baada ya kuondoka

Introducing "SIRI" (Official Video) by Rayvanny ft Nikk wa Pili


INTRODUCING "NITAZOEA" Official Video by Encok Bella

Kwa simu toka London: Mahojiano na Saidi Kanda - Sehemu ya Mwisho

$
0
0
Na Freddy Macha
Kumaliza mwaka 2017 na Sehemu ya 5- ya  mahojiano na Saidi Kanda, tujiulize kwanini vijana wengi siku hizi wanadhani dawa za kulevya (hasa bangi) ndiyo kiini cha usanii - hasa wa muziki. 
Msanii  aliyeshatunukiwa tuzo kem kem za kimataifa, Saidi Tumba Kanda anasisitiza ni mapenzi na fani yake, nidhamu ya kazi na afya ya mwili (kupitia mazoezi) ndiyo nguzo kuu za mafanikio yake.

TANZIA YA SHEIKH AHMED ISLAM NIMJUAE: DKT. DAU

$
0
0
Inaandikwa na Ramadhani K. Dau 

*Ilikuwa siku ya Jumamosi tarehe 23 Disemba 2017, majira ya saa 5 usiku kwa saa za Malaysia nilipopata ujumbe mfupi wa sms kutoka kwa *Sheikh Issa Othman*, maarufu Mufti wa London, Imam wa Masjid Maamur ukiniarifu msiba wa mzee wetu Sheikh Ahmed Islam. Ujumbe wake ulikuwa mfupi sana: “Mzee wetu Ahmed Islam amefariki sasa hivi. Maiti inaletwa msikitini hivi sasa. Maziko kesho In Shaa Allah. Innallillahi Wainnaillahi Raajiuun”.*

Mara tu baada ya kupata taarifa hiyo na baada ya kumtakia maghfira mzee wetu, nikajua kuwa kwa mara nyingine tena umeniangukia wajibu wa kuandika Taazia ya mtu ambaye namfahamu, namheshimu na alikuwa na ukaribu sana na mimi. Nimeshawahi kuandika huko nyuma kuwa kuandika Taazia ni jambo zito na gumu sana.

Kila niandikapo hutamani sana Taazia hiyo iwe ndio ya mwisho. Lakini kwa mipango Yake Mwenyezi Mungu, najikuta nashindwa kukwepa wajibu huo. Hata hivyo, mara hii nilidhani ningeweza kuukwepa wajibu huo kwa kumuomba rafiki yangu na ndugu yangu mwanahistoria maarufu *Sheikh Mohamed Said* aandike Taazia hiyo nami nilikuwa tayari kumpa maelezo yoyote ambayo yangemsaidia katika uandishi wake.

Pamoja ya kuwa alikubali kuifanya kazi hiyo, Mohamed alisisitiza kuwa lazima na mimi niandike. Kwa jinsi ya msisitizo aliouweka Sheikh Mohamed, nimejikuta kwa mara nyingine tena  nalazimika kuandika Taazia hii huku nikiwa na moyo wa huzuni sana kwa kuondokewa na mzee wangu ambaye alikuwa mithili ya baba yangu mzazi.

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI DESEMBA 28, 2017

HARAKISHENI UMEME KUKAMILISHA MRADI WA MAJI NAMAHEMA ‘A’: WAZIRI MKUU MAJALIWA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Meneja wa TANESCO wilaya ya Ruangwa, Bw. Samuel Pyuza ahakikishe umeme unapatikana mapema kwenye pampu ya maji ili kukamilisha mradi wa maji wa Namahema ‘A’.

Ametoa wito huo jana jioni (Alhamisi, Desemba 28, 2017) wakati akizungumza na wakazi wa vijiji vya Namahema ‘A’ na Namahema ‘B’ wilayani Ruangwa, mkoani Lindi waliofika kumsikiliza mara baada ya kukagua mradi wa maji ambao umechukua miezi sita tangu uanze. Mradi huo unatarajiwa kukamilika Januari 15, mwakani.

Mradi huo ambao hadi kukamilika kwake utagharimu sh. milioni 244.52, unatarajiwa kuwahudumia wakazi 2,257 wa vijiji hivyo viwili ambao walikuwa wanasongamana kupata maji kutoka kwenye kisima ambacho kilikuwa kinatumia pampu ya mkono. Kijiji cha Namahema ‘A’ kina watu 1,668 na Namahema ‘B’ kina watu 589.

Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka, ameanza ziara fupi ya siku tatu, kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Jumla ya sh. milioni 189.93 zimeshatumika kwenye mradi huo ambazo ni sawa na asilimia 77.68 ya fedha ziliopangwa kutumika. Fedha za mradi huo zimetolewa na Serikali Kuu kupitia Mfuko wa Uwekezaji wa Maji wa Taifa (National Water Investment Fund).

Kazi ambazo zimekamilika hadi sasa ni ujenzi wa vituo vya kuchotea maji (DP) 32; ujenzi wa mtandao wa mabomba yenye urefu wa mita 6,460; tenki la kuhifadhia maji leye ujazo wa lita 50,000, ujenzi wa nyumba ya mitambo (pump house); ujenzi wa uzio (fence) kwenye nyumba ya mitambo; ujenzi wa uzio (fence) kwenye tenki la kuhifadhia maji; na ununuzi wa pampu na mota.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images