Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

KUWAIT YALAANI MAUAJI YA WANAJESHI WA TANZANIA HUKO DRC

$
0
0


Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem (wakwanza kushoto) ameungana na mamia ya viongozi wa Serikali akiwemo Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali katika uwanja wa ndege wa Zanzibar, ameungana nao kupokea na kuaga miili ya wanajeshi wa Tanzania waliopoteza maisha yao huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakilinda amani chini ya muavuli wa umoja wa mataifa. 
Al- Najem amesema kuwa Serikali ya Kuwait inalaani vikali tukio la kushambuliwa wanajeshi wa Tanzania na kupelekea wanajeshi 14 kufariki huku wengine 44 wakijeruhiwa. Ameongeza kuwa' tumefuatulia tukio hili la kushambuliwa wanajeshi wa kulinda amani katika kambi yao huko Kongo kwa huzuni kubwa, ambapo Serikali ya Kuwait inakemea
vikali mashambulizi yanayolenga vikosi vya kulinda amani au mashirika ya kibinadamu'.

Hayo ameyasema wakati wa ziara yake ya kikazi visiwani Zanzibar, Balozi Al-Najem amuomba Mwenyezi Mungu awarehemu wanajeshi waliouwa na kuwaponesha kwa haraka waliojeruhiwa

Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi aongoza mamia kupokea na kuaga miili ya wanajeshi wa Tanzania waliopoteza maisha yao huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakilinda amani chini ya muavuli wa umoja wa mataifa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar,

WALIOACHIA MAENEO KUPISHA MGODI WATAKIWA KULIPWA FIDIA

$
0
0
Serikali imeiagiza Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Shanta Mining Limited inayofanya shughuli zake Mkoani Singida kuharakisha ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha maeneo yao ili shughuli za uchimbaji zianze mara moja. 

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alitoa agizo hilo Desemba 12, 2017 wakati wa ziara yake ya kutembelea migodi ya dhahabu katika wilaya za Ikungi na Manyoni ili kujionea shughuli zinazoendelea pamoja na kuzungumza na wachimbaji wa madini.

“Mchakato wa fidia ufanyike haraka na mgodi uanze shughuli zake za uchimbaji mapema,” aliagiza Naibu Waziri Nyongo. 

Akiwa njiani kuelekea kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Elizabeth Shango uliopo katika Kijiji cha Sambaru, msafara wake ulisimamishwa na wananchi katika Kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi, wilayani Ikungi ambao walilalamika kuzuiwa kuendeleza maeneo yao na kampuni hiyo na huku wakicheleweshewa kulipwa fidia. 

Walisema kuwa tayari wameachia maeneo waliyokuwa wakimiliki kwa kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo kilimo na uchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu ili kupisha shughuli za uchimbaji mkubwa lakini Kampuni hiyo ya Shanta bado haijakamilisha ulipaji wa fidia.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi, wilayani Ikungi waliosimamisha msafara wake (hawapo pichani) 
 Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi, wilayani Ikungi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani). 
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (mbele katikati) akiwa nyumbani kwa Mzee Bastan Mtundwi (mbele kulia) na mkewe Esta Mtundwi ambao walijengewa Nyumba na Kampuni ya Shanta ikiwa ni fidia ya kupisha eneo.
 Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi, wilayani Ikungi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NGORONGORO WAZINDUA KAMPENI YA KUPINGA UKEKETAJI

$
0
0
Wanaharakati wa kupinga ukeketaji wakisikiliza kwa makini mafunzo kabla ya kuanza kampeni ya mwezi mmoja ya kupinga ukeketaji wilayani Ngorongoro. Mafunzo hayo yaliratibiwa na Shrika la UNESCO. Kampeni hiyo inafanywa kwa ushirikiano wa UNESCO, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Baraza la Wazee wa Mila wa Kimaasai (Laigwanan). Kampeni hiyo imeanza Tarehe 5/12/2017 na itaendelea kwa mwezi mzima.
Afisa wa UNESCO anayewakilisha miradi ya Ololoswakan Wilayani Ngorongoro Bwana Hamidun Kweka akiwafundisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Oloirien wilayani Ngorongoro madhara ya ukeketaji katika uzinduzi wa kampeni ya kupinga ukeketaji wilayani humo. Kampeni hizo zilizinduliwa rasmi Tarehe 5 na zitadumu kwa mwezi mmoja.
Ngariba mstaafu akiimba na watoto nyimbo za kupinga ukeketaji baada ya mafunzo ya kuwaelimisha madhara ya ukeketaji katika shule ya msingi Oloirine wilayani Ngorongoro mnamo Tarehe 7, 2017.
Wafanyakazi wa UNESCO na Walimu wa Shule ya Msingi Oloirien wakiwa pamoja baada ya uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Ukeketaji wilayani Ngorongoro.

Mpango wa Malipo kwa Ufanisi waleta Mabadiliko Sekta ya Afya Rufiji

$
0
0

Na.WAMJW-Rufiji.

Utekelezaji wa mpango wa malipo kwa ufanisi(RBF) Wilayani Rufiji umeleta mabadiliko makubwa katika Vituo vya afya na Zahanati kwa uboreshaji wa miundombinu pamoja na upatikanaji wa dawa muhimu

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Ikwiriri na Zahanati ya Nyamwage katika ziara yake ya kuangalia utekelezaji unaofanyika kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi unaotekelezwa katika mikoa nane nchini

Waziri Ummy alisema mabadiliko hayo katika sekta ya afya yamefanyika katika maeneo ya utoaji huduma,Uongozi na Utawala,Rasilimali watu,Mifumo ya usimamizi wa utoaji taarifa za afya,madawa na teknolojia ya afya ambapo mfumo huo umesaidia maboresho, uwajibikaji,ufanisi na usawa kwani dhana hiyo inamfanya mtoa huduma kulipwa kulingana na matokeo ya kazi yake ambayo amehakikiwa na hivyo kufanya vituo hivyo kuongeza hali ya upatikanaji wa dawa na kuboresha miundombinu ya vituo hivyo

"Tumeanza mpango huu katika mikoa 8,tumefanya tathimini kwenye vituo vya afya na zahanati zote za Mkoa wa Pwani ikiwemo Wilaya ya Rufiji,tukabaini vituo vya afya na zahanati hazikuwa na viwango vya ubora unaotakiwa, tukaona tuwapatie  shilingi milioni 10 kila kituo vilivyokidhi kwa ajili ya kuboresha miundombinu"alisema Waziri ummy.

Hata hivvyo aliipongeza kamati ya afya ya kijiji cha Nyamwage kwa kutumia ipasavyo shilingi milioni 10 kwa kuongeza urefu wa paa na kupaua,kuweka malumaru na kuongeza matundu ya choo pamoja na tundu moja la choo kwa ajili ya walemavu"nikupongeze mganga mfawidhi kwa kuboresha zahanati hii kwakweli unapaswa kupongezwa kwani umefanya vizuri ila badilika lugha chafu kwa wananchi haitakiwi,nakupa mwezi mmoja ila kwa upande huu mwingine umenifurahisa,mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni"

Mpango wa Malipo kwa Ufanisi waleta mabadiliko hayo ikiwemo ujenzi na ukarabati wa choo na jengo hilo,kama jengo lionekanavyo pichani juu na chini Waziri Ummy akikagua choo hicho.

Waziri Ummy Mwalimu akipokea mabango kutoka kwa wananchi yenye jumbe mbalimbali kuhusiana na changamoto za Afya, wakati alipokuwa akitembelea Kituo cha Afya cha Ikwiriri na Zahanati ya Nyamwage katika ziara yake ya kuangalia utekelezaji unaofanyika kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi unaotekelezwa katika mikoa nane nchini. 
 Waziri wa Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akimwelekeza mmoja wa Wazee waliopata vitambulisho vya Matibabu bure kwa Wazee wakati wa tukio hilo mapema leo Wilayani Rufiji.
  Waziri wa Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akimkabidhi mmoja wa Wazee kitambulisho cha Matibabu bure kwa Wazee wakati wa tukio hilo mapema leo Wilayani Rufiji.
  Waziri wa Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwakabidhi baadhi ya Wazee vitambulisho vya Matibabu bure kwa Wazee alipokuwa akitembelea Kituo cha Afya cha Ikwiriri na Zahanati ya Nyamwage katika ziara yake ya kuangalia utekelezaji unaofanyika kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi unaotekelezwa katika mikoa nane nchini. 

Mgalu Awataka Wakandarasi Wa REA kuongeza kasi Utekelezaji Wa Miradi

$
0
0
Na Greyson Mwase, Tanga

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka wakandarasi wanaojenga miundombinu ya usambazaji wa umeme vijijini chini ya Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kuongeza kasi ili miradi yote iweze kukamilika ifikapo mwaka 2019.

Mgalu aliyasema hayo mapema leo tarehe 15 Desemba, 2017 katika ziara yake aliyoifanya katika kijiji cha Bwitini wilayani Korogwe mkoani Tanga, lengo likiwa ni kukagua hatua ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini iliyopo chini ya REA Awamu ya Tatu na kutorishishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri Mgalu aliambatana na watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Alisema kuwa, Serikali ilikwishawalipa wakandarasi wote malipo ya awali na kuwataka kuanza kazi mara moja lakini wamekuwa wakifanya katika kasi ndogo hususan katika hatua ya upembuzi yakinifu.

“ Wakandarasi wengi wamekuwa wakichukua muda mrefu kutekeleza miradi kwa kisingizio cha kufanya upembuzi yakinifu wakati fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi zimekwishatolewa, nichukue fursa hii kuwatangazia wakandarasi wote nchini kuanza kazi mara moja,” alisema Mgalu
Msimamizi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Pangani kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Mahenda S. Mahenda (kulia) akitoa maelezo kuhusu uzalishaji wa umeme katika kituo hicho kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) katika ziara aliyoifanya mapema leo tarehe 15 Desemba, 2017 katika kituo hicho.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Pangani mapema leo tarehe 15 Desemba, 2017
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ( wa pili kulia) akitoa maelekezo kwa watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika ziara hiyo.


WAZIRI MWIJAGE AZINDUA BODI MPYA YA KAMPUNI YA MBOLEA YA TAIFA (TFC), AITAKA KUTOINGIA MIKATABA YA HASARA

$
0
0

Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, ameitaka Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC) kubadilisha mfumo wa utendaji ikiwa ni pamoja na kutoingia mikataba inayoweza kuisababishia serikali hasara, badala yake kuangalia wabia wanaoweza kuisaidia kujipanua na kupata faida kubwa zaidi.

Waziri Mwijage, aliyasema hayo juzi wakati akiizindua bodi mpya ya Wakurugenzi ya TFC, na kuongeza kwamba serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli, haiko tayari kuona taasisi zake za umma zikiingizwa katika mikataba mibovu na isiyokuwa na tija.

Pia aliagiza kwamba, baada ya kuizindua bodi hiyo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Egid Mbofu na wajumbe wake, waanze kazi mara moja na moja ya majukumu yao ya awali ni kuangalia ama kuipitia upya miokataba ambayo awalo iliingiwa na TFC.

Alisema TFC ikifanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kujielekeza kwenye kazi zenye faida kubwa, itaweza kusaidia kasi ya kuendeleza sekta ya kilimo nchini, na kufikia malengo ya serikali ya awamu ya tano ya Taifa la uchumi wa kati na wa Viwanda.

"Tunatambua sekta ya kilimo ni nguzo muhimu kwa ajili ya uchumi wa TANZANIA, lakini haiwezi kuleta mafanikio makubwa kwa jamii, ikiwa TFC haitaweza kupewa uwezo na kuwafikia wakulima wengi zaidi", alisema Waziri Mwijage.
Waziri wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, akizungumza na wajumbe wa bodi mpya ya Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC), (hawapo pichani), wakati akiizindua bodi hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Wajumbe wa bodi hiyo wakiwa katika hafla ya uzinduzi.
Mwenyekiti wa bodi hiyo, Profesa, Egid Mbofu, akizungumza katika uzinduzi huo. Kulia ni Meneja Mkuu wa TFC, Salum Mkumba.
Wajumbe wa bodi hiyo wakiwa bize kuchukua maagizo ya Waziri Mwijage.

WAZALENDO 47 KUTOKA JWTZ NA KUNDI LA WANAHABARI WALIVYOTUMIA SIKU 5 KUPANDA KILELE CHA UHURU KWA AJILI YA SHEREHE ZA MIAKA 56 YA UHURU

$
0
0
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibok akizungumza katika hafla fupi ya kuagwa kwa wazelendo 47 waliopanda mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya Washiriki katika changamoto ya kupanda Kilimanjaro kwa ajili ya kutangaza Utalii wa Ndani na utunzaji wa Mazingira.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza katika hafla ya kuwaaga washiriki wa changamoto ya upandaji wa mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kutangaza Utalii wa ndani na Utunzaji wa Mazingira.
Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Utalii Tanzania ,Balozi Charles Sanga (kulia) alikua ni miongoni mwa Wazalendo walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimajaro.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara anayeshiriki zoezi la kupanda  Mlima Kilimanjaro kwa mara ya 10 sasa akazungumza na washiriki wa zoezi hilo kabla ya kuianza safari.

HAKUNA WA KUMPINDUA MUFTI ZUBEIR-BAKWATA

$
0
0

Na Said Mwishehe,Blogu ya Jamii

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA)limesema kwa sasa limeimarika kimfumo na kikatiba huku likiweka wazi hakuna chama zozote za kumuondoa Mufti madarakani.

Akizungumza LEO makao makuu ya muda ya BAKWATA Kinondoni Dar es Salaam ,Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu taifa na Msemaji wa baraza hilo, Sheikh Khamis Mataka amesema kinachoendelea sasa ni kuimarisha mifumo kulingana na mahitaji.

Amesema kutokana na mabadiliko yanayoendelea chini ya usimamizi wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania ,Abubakari Zubeir,kuna watu wanaumizwa na mabadiliko ya mfumo na matokeo yake baadhi yao wanalichafua baraza kwenye mitandao ya kijamii.

Sheikh Mataka amesema wakati baraza likijiimarisha na kufanya mambo makubwa, kuna watu wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kutoa taarifa za kuzusha.Ametumia nafasi hiyo kuwaomba Waislamu nchini kuunga mkono jitihada za Mufti katika kuweka mifumo ambayo italifanya baraza kuwa imara zaidi tofauti na huko nyuma ambako lilingia kwenye matatizo makubwa.

"Kuna mambo mengi yasiyostahili yamefanyika huko nyuma,yakiwamo ya fedha za BAKWATA na mali zake kutumika vibaya.Wapo waliohusika kufanya ubadhirifu huo, wametangulia mbele za haki na hatuna cha kusema zaidi ya kumuachia Mwenyezi Mungu." Tunachoendelea nacho kwa sasa ni kufanya mabadiliko katika maeneo mbalimbali na tunaomba Waislamu kutuunga mkono,tunajua wapo wasiofurahia mabadiliko ya Mufti lakini tutaendelea nayo,"amesema.

Pia amesema kuna taarifa ambazo zinaendelea kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii zikiihusisha BAKWATA.Taarifa hizo ni tishio la kumuondoa Mufti,wafanyakazi walia njaa na mgogoro wa walimu wa shule ya sekondari Bondeni mkoani Arusha inayomilikiwa na baraza hilo.Kuhusu tishio la kumuondoa Mufti ,amesema hazina ukweli wowote na wanafuatilia aliyetoa taarifa.Kuhusu wafanyakazi kudai mishahara ni kweli na hiyo imetokana na malimbikizo ya muda lakini chini Mufti Zubeir wameendelea kulipa.

Amesema malimbikizo yanayodaiwa ni sh Milioni 176 na wanaendelea kulipa.Kuhusu mgogoro haupo kwani ulishaghulikiwa na umepata nafasi kwasababu kuna watu wameondolewa kwa hiyo wanaeneza taarifa mbaya.

Sheikh Mataka amesema BAKWATA ya sasa chini ya uongozi wa Mufti Zubeir ipo imara na kauli mbiu yake yake ya "Jitambue,mabadilika, acha mazoea" imesaidia kuwabadilisha wajumbe mbalimbali wa baraza hilo.Amesema kwa mara ya kwanza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya baraza hilo wameshiriki kwenye vikao bila kulipana posho yoyote na miongoni mwa wajumbe walisafiri kutoka mikoani.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea hatua ya BAKWATA kuamua shule 10 za baraza hilo kupewa watu binafsi kuzisimamia na zilizobaki zinasimamiwa kwa utaratibu wa zamani.Amesema lengo ni kuangalia mfumo upi unafaa katika kusimamia sekondari za BAKWATA ingawa kuna baadhi ya watu wamezusha sekondari hizo kapewa Mufti jambo ambalo si kweli.
 Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu BAKWATA Taifa na Msemaji rasmi wa baraza hilo,Sheikh Khamis Mataka(katikati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) jijini Dar Salaam leo wakati akitolea ufafanuzi wa tuhuma tatu zinazoelekezwa kwa Mufti wa Tanzania ,Sheikh Abubakari Zubeir ambazo ameeleza si za kweli.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Sawa na Tabligh na Msemaji wa Mufti Sheikh Hassan Chizenga na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu BAKWATA Sheikh Salim Abed.
Mkurugenzi wa Dawa na Tabligh na Msemaji wa Mufti wa Tanzania sheikh Abubakari Zubeir, Sheikh Hassan Chizenga akizungumzia nia njema ya Mufti katika kuwaongoza Waislamu kupitia baraza hilo.Pia ameonya tabia ya Watanzania kusema uongo kwani athari zake ni kubwa katika nchi.

WAWEKEZAJI SEKTA YA UHIFADHI WAKABILIWA NA CHANGAMOTO LUKUKI

$
0
0
Na Wankyo Gati,Arusha

Wawekezaji nchini katika sekta ya utalii na uhifadhi bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uvamizi wa maeneo ,migogoro ya ardhi na kutokuwepo kwa eneo la malisho, hali ambayo imekuwa ikikwamisha jitihada za uwekezaji katika sekta hiyo.

Ambapo wanakijiji wengi bado wanaishi katika maisha ya asilia hali ambayo inapekea kuharibu uhifadhi kwani wamekuwa wakilisha mifugo yao bila kujali kuwa huo ni uharibifu wa mazingira ya utalii nchini .

Hayo yameelezwa leo na Meneja Mkuu kutoka Dhana Investment Company David Laizer katika mafunzo yaliyoandaliwa na Shirikisho la Vyama Vya Utalii Tanzania (TCT) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam kitengo cha sera na utetezi (CPRA) kimefanya mafunzo ya siku mbili ya kuweka na kuendesha mfumo wa mdahalo (PPD) utakaowawezesha jamii katika ngazi za chini kuweza kuendesha mijadala ya maendeleo kati yao na wawekezaji na kushughulikia changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya uwekezaji. yaliyofanyika Mkoani Arusha.

Aidha alisema kuwa kuna haja ya Serikali kuingilia kati katika migogoro hiyo ili kuweza kuwawekea mazingira rafiki kwa wawekezaji uhifadhi na utalii nchini.Kwa upande wake Msemaji wa jumuiya ya Burunge Ramadhani Ismail amesema kuwa Serikali iangalie miundombinu ya uhifadhi ili kuziwezesha hifadhi na jumuiya zake ziweze kujiendesha na wananchi wapate manufaa kupitia jumuiya hizo.

Kwa upande wake mtoa mafunzo wa utetezi kutoka chuo kikuu ,idara ya masoko utafiti utetezi Dkt.Goodluck Urasa amesema kuwa wanatoa mafunzo hayo ili kuweza kuwasaidia jumuiya hizo kujengewa uwezo ili kuwewezesha jumuiya hizo ili kunufauika na uhifadhi.

Mafunzo hayo yatawasaidia katika kujenga jumuiya za uhufadhi zilizo na manuifaa bora.Kwa Upande wake mchambuzi wa sera kutoka tct Mosses ngereza alisema kuwa wameandaa mafunzo hayo ili kuwapa 
mafunzo ya siku mbili ili kuweka na kuendesha mfumo wa mdahalo (PPD) utakaowawezesha jamii katika ngazi za chini kuweza kuendesha mijadala ya maendeleo kati yao na wawekezaji na kushughulikia changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya uwekezaji. 

Aliongeza kuwa mbali na jitihada za kuwapa mafunzo lakini bado kuna changamoto yakutokuwa na wawekezaji wakutosjha katika sekta hiyo.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT JUMA MALEWA AWAAGA MAAFISA MAGEREZA TOKA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WALIOKUWA WAKISHIRIKI MAZOEZI YA ULINZI WA AMANI JIJINI DAR

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa(kushoto) akiteta jambo na Maafisa wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji toka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika Desemba 15, 2017 katika Ukumbi wa Magereza – Recreation, Ukonga Jijini Dares salaam. Maafisa hao walikuwa hapa nchini kushiriki mazoezi ya Kijeshi ya pamoja kuhusu ulinzi wa amani yaliyohusisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yaliyoandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ).
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Charles Novart ambaye pia alikuwa mshiriki kutoka Jeshi la Magereza Tanzania katika mazoezi ya Kijeshi ya pamoja kuhusu ulinzi wa amani akitoa utambulisho kwa Maafisa wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji toka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika Desemba 15, 2017 katika Ukumbi wa Magereza – Recreation, Ukonga Jijini Dares salaam.
Kamishna Msaidizi wa Magereza toka nchini Uganda ambaye pia ni Msemaji wa Jeshi hilo Baine Frank akijitambulisha mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa(hayupo pichani) kwenye hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika katika Ukumbi wa Magereza – Recreation, Ukonga Jijini Dares salaam.
Naibu Kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Magereza toka nchini Kenya James Kodieny(kushoto) akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa(kulia) kama inavyoonekana katika picha katika hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika Desemba 15, 2017 katika Bwalo la Magereza – Recreation, Ukonga Jijini Dares salaam.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini walioshiriki hafla hiyo ya kuwaaga Maafisa wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji toka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliokuwa hapa nchini kushiriki mazoezi ya Kijeshi ya pamoja kuhusu ulinzi wa amani.
Bendi ya Magereza maarufu kwa jina la “MKOTE NGOMA” ikitumbuiza katika hafla hiyo ya kuwaaga Maafisa hao.Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

NGORONGORO WAZINDUA KAMPENI YA KUPINGA UKEKETAJI

$
0
0
Wanaharakati wa kupinga ukeketaji wakisikiliza kwa makini mafunzo kabla ya kuanza kampeni ya mwezi mmoja ya kupinga ukeketaji wilayani Ngorongoro. Mafunzo hayo yaliratibiwa na Shrika la UNESCO. Kampeni hiyo inafanywa kwa ushirikiano wa UNESCO, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Baraza la Wazee wa Mila wa Kimaasai (Laigwanan). Kampeni hiyo imeanza Tarehe 5/12/2017 na itaendelea kwa mwezi mzima. Afisa wa UNESCO anayewakilisha miradi ya Ololoswakan Wilayani Ngorongoro Bwana Hamidun Kweka akiwafundisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Oloirien wilayani Ngorongoro madhara ya ukeketaji katika uzinduzi wa kampeni ya kupinga ukeketaji wilayani humo. Kampeni hizo zilizinduliwa rasmi Tarehe 5 na zitadumu kwa mwezi mmoja. Ngariba mstaafu akiimba na watoto nyimbo za kupinga ukeketaji baada ya mafunzo ya kuwaelimisha madhara ya ukeketaji katika shule ya msingi Oloirine wilayani Ngorongoro mnamo Tarehe 7, 2017. Wafanyakazi wa UNESCO na Walimu wa Shule ya Msingi Oloirien wakiwa pamoja baada ya uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Ukeketaji wilayani Ngorongoro.

NAIBU WAZIRI AFASHASTA AZINDUA MFUMO WA ANUANI ZA MAKAZI ARUSHA

$
0
0
Na Wankyo Gati,Arusha

Naibu waziri wa mawasiliano na uchukuzi Afashasta Nditie amezindua Mkutano mkuu wa kujadili mfumo wa Anuani za makazi uliofanyika mkoani Arusha ambao umewakutanisha wadau mbali mbali wa mawasiliano kutoka nchi za Africa .

Akizungumza na wadu hao Naibu waziri Nditie amesema kuwa mfumo huo kwa hapa nchini upo vizuri na anaamini kuwa mamalaka husika ipo makini katika kukamilisha hatua iliyobaki ambayo itaifanya Tanzania kufika mbali.

Aliongeza kuwa mbali na jitihada mbalimbali zinazofanyika kuweza kufikia kila moja lakini bado kuna changamoto mablimbali za kuwepo na mitaa mingi isiyokuwa na majina ili kuweza kurahisisha huduma ya posta mlangonii.

Kwa upande wake Kaimu Posta mkuu wa shirika la Posta Tanzania Hassani Mwang’ombe amesema kuwa hivi sasa wako katika mpango wa huduma ya posta mlangoni ili kuweza kurahisisha barua zote kumfikia kila mmoja mwananchi mahali anakoishi ili kuweza kupata mawasiliano.

Hata hivyo amesema kuwa watanzania watajiskia vizuri na kuona furaha pindi watakapo ona huduma ya posta inawafikia mpaka milangoni mwao kwani siwananchi wote wanaweza kumudu kwenda mahli paliko huduma ya posta ili kuweza kuwasaidia maelfu ya wakazi walio wengi.

Kwa upande wake katibu mkuu wa Papu Younoss Djibrine alisema kuwa nimwanzo mzuri wa na njia nzuri kwa nchi ya Tanzania kuweza kuanza huduma hii ya anuani na majina ya mtaa ambapo hata united nation nihaki ya kila mmoja kuweza kupata utambuzi wanakoishi lli kuweza kuwafuikia kirahisi zaidi.

Aliongeza kuwa nchi nyingi za afrika zinachangamoto mbalimbali kiwemo kukosa anuiani za makazi yao hali ambayo kuwafikia inakuwa vigumu sana lakini kuna haja za makusudi kuweza nchi husika kuweza kuanzisha utaratibu huo.

Article 2

VIJANA WAKUMBUSHWA WAJIBU WA KUTAMBUA NAFASI ZA UONGOZI KATIKA JAMII

$
0
0
VIJANA nchini wametakiwa kutambua wajibu wao katika Taifa kwa kutumia fursa zinazojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi katika jamii ili kutetea maslahi na agenda mbalimbali zinazogusa maendeleo yao.

Hayo yamesemwa leo Jumamosi (Desemba 17, 2017) Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Ushawisihi na Utetezi wa Taasisi ya Vijana ya TYVA, Yusuf Bwango wakati wa mdhahalo wa vijana uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao.

Kwa mujibu wa Bwango alisema tafii mbalimbali zimebaini kuwa Vijana wengi wamekuwa na mtazamo hasi kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi hususani Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, na kubaki nyuma katika nafasi hizo huwaniwa na kushindaniwa na Wazee pekee.

“Tumefanya mdahalo huu kwa malengo ya kuwajengea uwezo vijana kutambua kuwa wao ndio Viongozi wa baadae na hili litaanzia katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika katika ngazi za kijamii ikiwemo chaguzi za Serikali za Mitaa” alisema Bwango.

Bwango alisema umefika wakati kwa Vijana wa Kitanzania kuweza kutumia majukwaa mbalimbali ili kuweza kubadili fikra na mitazamo yao kuhusu mifumo ya kiutawala na kutumia majukwaa hayo kuunda vyombo imara vitakavyoweza kuwasilisha na kupaza sauti zao.
1. Bi. Sumaiya Mahmoud kutoka Taasisi ya Mwanamke na Uongozi akichangia hoja wakati wa mdahalo wa vijana ulioandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao. Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency Park Jijini Dar es Salaam.
1. Baadhi ya Vijana kutoka sehemu mbalimbali za Jijini wakifuatilia mdahalo wa vijana ulioandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao. Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency Park Jijini Dar es Salaam.
1. Bw. Oscar Munga akichangia hoja wakati wa mdahalo wa vijana ulioandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao. Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency Park Jijini Dar es Salaam.
1. Bi. Anna Winstone akichangia hoja wakati wa mdahalo wa vijana ulioandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao. Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency Park Jijini Dar es Salaam.
1. Mmoja wa washiriki wa mdahalo wa vijana ulioandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao. Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency Park Jijini Dar es Salaam.


MWENYEKITI WA UWT TAIFA AKARIBISHWA MKOANI DODOMA

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, DODOMA.

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Taifa, Gaudencia Kabaka amewataka wanawake wa umoja huo kuvunja makundi ya ngazi zote yaliyojengeka wakati wa uchaguzi na badala yake wafanye kazi za kuwatumikia kwa ufanisi wapiga kura waliowapa ridhaa ya kuongoza.

Pia, amesema UWT kupitia uongozi wake mpya ulioingia kwa sasa ni lazima irejeshe heshima yake ya kuwa chombo cha kuwaunganisha wanawake wote wa mijini na vijijini Tanzania ili wapate maendeleo.Wito huo ameutoa katika hafla ya mapokezi ya uongozi huo yalioandaliwa na UWT Mkoa wa Dodoma katika viwanja vya White house Makao Makuu ya CCM Dodoma.

Amesema bila kuvunja makundi Umoja huo hautopata maendeleo na watatumia muda mwingi kulaumiana, kuangaishana na hamaye kukosa muelekeo wa kutekeleza ahadi walizotoa kwa mamilioni ya wanawake wa Tanzania.Kabaka ameeleza kwamba Umoja wa Wanawake Tanzania ni chombo cha CCM kinachotakiwa kuwa nguzo na muhimili mkuu katika kusimamia na kulinda maslahi ya Chama kisiasa, kiuchumi na kijamii.

"Furaha yangu ni kwamba mlituchagua kihalali bila ya kutumia rushwa, hivyo nasi tuna deni la kuwalipa ambalo ni lazima tutimize utumishi bora na uliotukuka kwa miaka mitano ya uongozi wetu.Na nakuombeni tushirikiane kwa pamoja kupinga rushwa na ufisadi ndani ya UWT na Chama kwa ujumla kama tunavyopinga makundi ya kuhatarisha uhai wa Chama cha Mapinduzi", amesema Mama Kabaka.
VIONGOZI Mbali mbali wa UWT walioudhuria katika hafla ya mapokezi ya viongozi wapya UWT ngazi ya Taifa.
MWENYEKITI wa UWT Taifa, Gaudencia Kabaka akihutubia katika hafla ya mapokezi ya viongozi wapya ngazi ya Taifa wa Umoja huo yaliyofanyika katika viwanja vya White House Makao Makuu ya CCM Dodoma.


BREAKING NEWZZZZZ: LUKUVI AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU WA NHC

Taarifa kutoka Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

$
0
0
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Edmund Benard Mndolwa akitangaza kutengua ushindi wa Nuru Kassim Bainaga aliyetangazwa kuwa mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya  Wazazi kwenda kwenye Umoja wa Wanawake (UWT) na kumtangaza Zainabu Zubeir Sige kuwa mshindi halali wa nafasi hiyo Picha na Mpiga picha Wetu.

TAARIFA KUTOKA JUMUIA YA WAZAZI YA CCM.

Uongozi wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Mwenyekiti wake Ndg. Dkt. Edmund Mndolwa, leo tarehe 16 Desemba 2017 umekamilisha kuhakiki matokeo ya kura zilizopigwa katika Jumuia hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wajumbe wa Jumuia hiyo walioshiriki katika uchaguzi uliofanyika tarehe 13 Desemba 2017

Katika taarifa yake Ndg. Dkt. Mndolwa amesema matokeo yaliyotangazwa na kumpa ushindi Ndg. Nuru Kassian Bainaga kwa nafasi ya WAZAZI kwenda UWT, yanatenguliwa na badala yake, amemtangaza Ndg. Zainab Zuberi Sige kuwa mjumbe halali wa WAZAZI kwenda UWT.

Huu ni muendelezo wa kuhakikisha kuwa haki inatendekea katika chaguzi mbalimbali za Chama na Jumuia zake.

Imetolewa na,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

WELEDI NA UBORA WA KAZI NDIO MSINGI MZURI WA KUPATA SOKO LA SANAA: DKT. MWAKYEMBE.

$
0
0

Na; Shamimu Nyaki-WHUSM.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka Wasanii wote hapa Nchini kuwa wabunifu na kutumia weledi katika kutengeneza kazi zenye ubora wa hali ya juu kwakua ndio utakaowasaidia kupata soko la uhakika.

Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizindua Kanzi Data ya wasanii iliyoandaliwa na Taasisi ya Muziki hapa nchini (TAMUF) iliyodhaminiwa na Kampuni ya CogsNet Technologies lengo ikiwa ni kusajili wasanii pamoja na kazi zao ili watambulike na wafaidike kupitia kazi hizo, lakini pia kuendelea na harakati za kupambana na wizi wa kazi za wasanii.

“Nawashukuru sana CogsNet pamoja na TAMUF kwa kuja na wazo hili lenye lengo la kulinda kazi za wasanii,naamini Kanzi Data hii italeta mafanikio kwa wasanii endapo watajisajili na kutengeneza kanzi bora zitakazowapatia soko la uhakika ndani na nje ya nchi”Alisema Dkt.Mwakyembe.

Aidha ameipongeza Taasisi hiyo kwa kuwatafutia wasanii Huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo Bima ya Afya inayotolea na mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF lengo ikiwa ni kuwasaidia wasanii kupata huduma ya afya kwa bei nafuu pamoja na mafao mengine yanayotolewa na Mfuko huo lakini pia akiwataka wasanii kuacha tabia ya kuuza Haki Miliki zao.
Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kutunza taarifa za wasanii wa muziki (Kanzi Data) leo Jijini Dar es Salaam. Mfumo huo unatengenezwa kwa ubia baina ya Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) na Kampuni ya CogsNet Technologies ya hapa nchini.
Rais wa Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) Dkt. Donald Kisanga akielezea jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kutunza taarifa za wasanii wa muziki (Kanzi Data) leo Jijini Dar es Salaam. Mfumo huo unatengenezwa kwa ubia baina ya Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) na Kampuni ya CogsNet Technologies ya hapa nchini.Kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa COSOTA Bi. Doreen Sinare, Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mungereza, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea risala ya Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) kutoka kwa Rais wa mfuko huu Dkt. Donald Kisanga wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kutunza taarifa za wasanii wa muziki (Kanzi Data) leo Jijini Dar es Salaam. Mfumo huo unatengenezwa kwa ubia baina ya Mfuko wa Muziki Tanzania (Tamufo) na Kampuni ya CogsNet Technologies ya hapa nchini. Kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa COSOTA Bi. Doreen Sinare na Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mungereza.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

TAARIFA KWA UMMA

WAZIRI WA MAMBO YA NJE, DKT. AUGUSTINE MAHIGA KUZURU CHINA

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images